Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 90 | 91 | (Page 92) | 93 | 94 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Saga saga  eneo ambalo kwa sasa limekuwa maarufu sana kwa kuchoma nyama ya mbuzi,wasafiri wengi wanaotumia barabara kuu ya mkoa wa Morogoro kuelekea mikoa ya Iringa kabla ya kufika mbuga ya Mikumi, wamekuwa wakisimama hapo na kupata nyama choma kama inavyoonekanika pichani.
  Mishikaki ya nyama ya mbuzi ikiwa kwenye hatua za mwisho ya kuiva ,mishikaki hiyo inauzwa kwa shilingi 3000 mmoja.Picha na Adam H. Mzee

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakisalimia baadhi ya viongozi, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Iringa asubuhi hii, kwa ajili ya kuanza ziara ya siku saba, mkoani Njombe. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Joyce Msambatavangu.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  akiwa na viongozi wa mkoa wa Iringa. Nyuma ni Nape Nape naye akiwa na wenyeji.
   Kinana akisaini kitabu cha wageni Uwanja wa Ndege wa Iringa baada ya kuwasili uwanjani hapo asubuhi hii. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Joyce Msavatavangu
  Nape akisaini kitabu cha wageni BASHIR NKOROMO

  0 0

  Mama Joshua akipanga vizuri mboga za majani aina ya figili tayari kwa kusubiri wateja,leo katika soko la Mangula,Makambako.

  Soko la Mangula,Makambako mjini Njombe linazidi kuwa maarufu kila kukicha kwa kuuza mboga za majani kwa wingi.  Picha na Adam H. Mzee

  0 0

  Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond na Ney wa Mitego wakitumbuiza jukwaani kwenye uzinduzi wa tamasha la  Epiq Open  Mic 
  =======  ======  ========
  Katika kuelekea msimu wa sita wa shindano la kuimba la Epiq Bongo Star  Search, kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imezindua Epiq Open  Mic ikiwa ni nafasi nyingine kwa vijana wenye vipaji vya muziki kuonyesha  vipaji vyao kabla usaili wa Epiq Bongo Star Serach haujaanza.

  Epiq  Open  Mic  inatarajiwa  kuwapa  nafasi  vijana  kujifunza  misingi  ya  muziki kutoka kwa mmoja wa watayarishaji wa muziki maarufu zaidi nchini,  Marco Chali. Marco  Chali  ambaye  pia  ni  mtunzi  na  mwimbaji,  ametayarisha  nyimbo  nyngi ambazo zimeshinda tuzo ndani na nje ya nchi za wasanii kama Ms. 

  Trinity  kutokea  Jamaica,  A.Y  wa  Tanzania,  Prezzo  wa  Kenya,  J  Martins  kutoka Nigeria na wengine wengi. Tamasha  hilo  la  Epiq  Open  Mic,  ambalo  ni  la  bure  litazinduliwa  rasmi  kwenye  viwanja  vya  Mwembe  Yanga  Temeke  tarehe  26  ya  mwezi  huu  ikisindikizwa  na  wakali  kibao  wa  Bongo  flavor  kama  Diamond  Platnumz,  Madee, Godzila, Ney wa Mitego, Mabeste na Mrap.

  Akizungumza  wakati  wa  kuzindua  matamasha  hayo,  Afsa  Biashara  Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema kampuni ya Zantel inaaminini katika  kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao. ‘Muziki ni ajira kwa vijana wengi, na kuamini hilo ndio maana kampuni ya  Zantel  imeamua  kuwafikia  vijana  wote  wenye  vipaji  na  kuwapa  nafasi  ya  kuonekana’ alisema Khan.

  Baada  ya  uzinduzi  wa  tamasha  la  Epiq  Open  Mic  Mwembe  Yanga  tamasha  hilo  litaendelea  kila  jumamosi  kwenye  makao  makuu  ya  Zantel  likiwapa nafasi vijana kujisajili na kurekod sauti zao.  Vijana watakaorekodi sauti zao watapigiwa simu na timu ya watayarishaji  wa muziki chini ya Marco Chali pamoja na wanamuziki ili kuwapa ushauri   wa namna ya kuboresha muziki wao zaidi. 

  ‘Zantel imejipanga kutumia fursa hii kuwahamasisha vijana kushiriki katika  kukuza  vipaji  vyao,  kuongeza  uelewa  wa  mambo  ya  muziki  pamoja  na  kuchangamkia fursa zilizopo katika muziki’ alisisitiza Khan. Epiq  Open  Mic  pia  inatarajia  kuwapa  fursa  ya  kurekodi  baadhi  ya  vijana  watakaokua na vipaji.

  0 0

  Meneja wa Mawasiliano na Huduma za Jamii wa Benki ya Barclays, Tunu Kavishe (kushoto) akizungumza na waandishi wakati wa kutangaza wadhamini wa Matembezi ya Hisani ya ‘Step Ahead’ ambayo yamelenga kukusanya fedha kwaajili ya kusaidia afya ya mama na mtoto na yanataraji kufanyika Juni 8 mwaka huu jijini Dar es salaam. Pamoja na ni Meneja masoko wa benki hiyo, Sara Munema. Wadhamini hao ni Montage Ltd, ITV/Radio One na Capital TV, Clouds Media Group, Cocacola, Golden Tulip, Mwananchi Communications, Serena Hotels na Ultimate Security.

  *****  ******

  Every year, Barclays Bank Tanzania organises a fund-raising walk christened ‘Step-Ahead’. Barclays Tanzania held its first Step-Ahead event in the year 2008 through which funds were raised and donated towards cancer treatment for children at the Ocean Road Cancer Institute (ORCI). Introduced globally in 2004, Step-Ahead is a signature Barclays initiative which aims to create awareness and resources in support of community needs.  

  Speaking at the press conference today, Ms. Tunu Kavishe, the Barclays Tanzania Communications and Community Investment Managersaid “Barclays Bank takes its Citizenship role seriously and recognizes it as one of our key business deliverables.

  Taking on maternal and infant health as our flagship cause in Tanzania springs from our need to play a role in addressing the march towards achieving the 2015 MDG goals on maternal and infant health. 

  We are pleased that our partners CCBRT and AMREF have joined us once again in this initiative. This exciting event will be held on the 8th June, 2013 at the Golden Tulip Hotel and will include a 5km walk in which all members of the public are invited to participate. Step Ahead Walk 2013 welcomes the support of all partners and the community at large.

  Today we are pleased to announce our sponsors for this year’s Event and these are Montage Ltd, ITV/Radio One and Capital TV, Clouds Media Group, Cocacola, Golden Tulip, Mwananchi Communications, Serena Hotels and Ultimate Security she added…

  The funds raised will go towards supporting theCapacity building for midwives, Fistula treatment and Reconstructive surgery for children born with correctible birth defects.

  Tickets cost Tshs 5,000/- each and will be available at any Barclays Bank branch, Montage Limited offices – Ada Estate, Golden Tulip, Serena Hotels and Slipways .

  0 0

  Mwanafunzi wa Chuo Cha Ualimu Kasulu, mkoani kigoma Valerian Nickodemus Kamugisha akinyannyua kwa Furaha sehemu ya fedha Sh 100 Milioni alizoshinda katika droo kuu ya Promosheni ya Vodacom Mehala iliyomalizika hivi karibuni. Kamugisha amekabidhiwa fedha zake hizo leo jijini Dar es salaam na kuamua kuzifungulia akaunti katika benki ya NMB. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB Bw.Abdulmajid Nsekela na Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa.
  Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa akimtambulisha kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) mshindi wa Promosheni kuu ya Mahela iliyomalizika hivi karibuni Valerian Nickodemus Kamugisha (kushoto) wakati wa hafla ya kumkabidhi kitita chake cha zawadi ya sh. 100 Milioni iliyofanyika makao makuu ya NMB. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB Bw.Abdulmajid Nsekela.
  Valerian Nickodemus Kamugisha (katikati) akipokea kitita cha sh. 100 Milioni kutoka kwa Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa alizoshinda katika droo kuu ya Promosheni ya Vodacom MAHELA. Hafla ya makabidhiano imefanyika makao makuu ya benki ya NMB ambako mshindi huyo amechagua kufungua akaunti kuhifadhi fedha hizo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB Bw.Abdulmajid Nsekela.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Mkuu wa jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati alipofika kwa mazungumzo leo Mei 27, 2013. Picha na OMR.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkuu wa jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati alipofika kwa mazungumzo leo Mei 27, 2013
  ========  ======= ======  =======
  MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI NA KUMPA POLE KUFUATIA VIFO VYA ASKARI WALIOFARIKI MTWARA.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amekutana na Mkuu wa jeshi la Polisi Inspekta Jenerali Said Mwema ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Mei 27, 2013. 

  Katika mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais ametumia nafasi hiyo kumpa pole Mkuu wa Polisi kufuatia ajali ya gari la iliyosababisha vifo vya askari wanne wa Jeshi hilo, waliokuwa njiani kutoka Nachingwea kuelekea Mkoani Mtwara kwa kazi maalum ya kudhibiti vurugu zilizojitokeza Mkoani humo juma lililopita.

  Mheshimiwa Makamu wa Rais alisema, askari hao watazidi kukumbukwa kwa kuwa walikuwa mstari wa mbele kuhakikisha majukumu yao kwa Taifa hili yanafanikiwa. Mheshimiwa Makamu wa Rais alisema pia kuwa, serikali inathamini sana mchango wa Jeshi la Polisi sambamba na majeshi mengine kutokana na kufanya kazi kwa kujitolea na kwa kutambua kuwa ulinzi na usalama wa Taifa ni jambo muhimu kwa maendeleo ya nchi.

  Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Mkuu wa Polisi kuwa, kazi inayofanywa na jeshi lake ni kubwa na kwamba Watanzania wanaithamini sana. Pia aliongeza kuwa katika nchi zote wananchi wanaojitolea kufanya kazi katika vyombo vya usalama, ni miongoni mwa wazalendo wakubwa wanaopaswa kuenziwa kwa kuwa wamekubali kuweka maisha yao kwa ajili ya nchi na watu wake.

  Katika mkutano huo, Makamu wa Rais alitumia nafasi hiyo kupata taarifa kuhusu hali ya usalama mkoani Mtwara na pia kubadilishana mawazo kuhusu kuhakikisha maeneo ya nchi yetu kubakia salama wakati wote. 

  Imetolewa na Boniphace Makene
             Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais

  0 0

  ZIFF sasa inapokea maombi kutoka kwa watengenezaji filamu Afrika Mashariki wanaotaka kushiriki katika warsha ya utengenezaji filamu wakati wa ZIFF mwaka huu..
  Wanafunzi 5 (mmoja toka kila nchi ya Afrika Mashariki) watalipiwa safari, malazi na chakula ili kushiriki kwenye warsha hiyo. Wanafunzi 5 wengine watajilipia wenyewe.
  Mfumo wa warsha utakuwa ni kufuatilia kikundi cha watengeneza filamu walio tayari mafundi watakaokuwa wanatengeneza filamu fupi wakati wa ZIFF. Utengenezaji huu unaitwa Guerilla Filmmaking (yaani filamu chapchap) na katika siku 6 filamu itapigwa, itahaririwa na kuonyeshwa ZIFF siku ya mwisho.
  Wanaotaka kushiriki kwenye warsha watume maombi yao hivi:
  CV fupi.
  Maelezo kwa nini wachaguliwe (maneno 1000)
  Maombi yatumwe kwa: workshop@ziff.or.tz
  Warsha imedhaminiwa na Goethe Institute na GIZ (Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani) na Jumuia ya Africa Mashariki (EAC)
  Maelezo pia yako www.ziff.or.tz 

  0 0


  HALMASHAURI ya wilaya ya Mufindi kupitia Madiwani wake katika kata
  zote za mufindi  wamekabidhiwa rasmi jengo la wodi ya wazazi na chumba
  cha upasuaji pamoja na chumba cha kuhifadhia watoto ambao hawaja
  timiza muda wa kuzaliwa.

  Wakikabidhiwa jengo hilo baada ya kukamilika na mkandarasi kutoka
  katika kampuni ya SMJ constrution, madiwani hao wameshukuru kupata
  huduma hiyo katika wilaya yao.

  Akizungumza wakati wa kukagua jengo hilo Mganga mkuu wa
  Hospitali ya mufindi ERIC BAKUZA alisema kuwa hospitali hiyo imekuwa
  ikikabiliwa na upungufu wa jengo la kujifungulia na hivyo kusababisha
  wajawazito kujifungua katika chumba kidogo ambacho hakikidhi mahitaji
  ya wagonjwa wote.

  “Hospitali hii chumba cha kujifungulia ni kidogo hivyo kwa siku
  tulikuwa tunahudumia wajawazito watatu lakini kwa sasa tutahudumia
  wapatao sita kutokana na ukubwa wa jengo”alisema BAKUZA

  Hata hivyo kwa sasa jengo hilo jipya linauwezo wa kubeba wajawazito
  sitini na wa kujifungua 12 kwa wakati mmoja katika hospitali hiyo
  tofauti na zamani na limegarimu kiasi cha shilingi 300,642,900.

  Sambamba na hayo hospitali hiyo katika jengo hilo jipya kutakuwa na
  chumba cha upasuaji kwa wajawazito na pia sehemu ya kuhifadhia watoto
  ambao hawaja timiza miezi ya kuzaliwa.

  0 0


   NA BASHIR NKOROMO, IRINGA.  Ni Katika Uchaguzi mdogo wa madiwani ambao kampeni zinaendelea baadhi ya Kata nchini

  CHAMA Cha Mapindizi (CCM) kimesema kimedhamiria kushinda kwenye kata zote 25 katika uchaguzi mdogo wa madiwani ambao kampeni zake zinaendelea katika kata mbalimbali nchini.

  Hayo yamesemwa leo  na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati akizungumza na wananchi katika kata ya Mbalamaziwa, wilayani Mufindi mkoani Iringa, ambako zinaendelea kampeni za udiwani katika kata hiyo. Katika Kata hiyo bendera ya CCM inapeperushwa na  Zuberi Nyamoleo.

  "Kutokana na jeshi kubwa na wafuasi tulio nao na imani inayoendelea kuonyeshwa na wananchi kuiunga mkono CCM, tuna imani dhamira hii itafanikiwa bila shaka yoyote", alisema Kinana na kuongeza;

  "Pale Mbinga katika Kata ya Lokindo CCM imeshapita bila kupigwa, wapinzani wenyewe wametuachia kwa sababu wameridhika kuwa tunafaa kiuwaongoza, na pele Iramba Vijijini, Chadema walijaribu kuchacharika lakini wameambulia matupu vijiji vinane vyote vimeenda CCM".

  Kinana aliwapongeza wagombea wengine waliokuwa katika mhakato na  Nyamoleo kwa kuamua kuuga mkono mgombea wa CCM katika 'vita' hiyo ya kuwania udiwani katika kata ya Mbalamaziwa.

  "Ninyi ni watu wa kuheshimika sana ndani ya CCM, mmefanya uamuzi wa busara kuamua kumsaidia mgombea wa CCM aliyejipita kwenye kura za maoni. Huu ndiyo ustaarabu na moyo wa dhati unaotakiwa kwa kila mwana-CCM", alisema Kinana.

  Kinana alisema, wanachama walio bora ndani ya CCM ni wale wasio na ubinafsi kwa kung'ang'ania kila wanachotaka wapate na wanapokosa inakowa nongwa.

  "Mwanachama lazima uelewe kwamba unapogombea nafasi yoyote inayowaniwa na wengi huwa kuna kushinda au kushindwa, sasa inapotokea umeshindwa ni lazima uendelee kuwa mwaminifu kwa chama ili kuhakikisha kinashinda", alisema.

  Kinana alisema, pamoja na CCM kuwa na uhakika wa kutwaa kata zote, lazima wagombea watakaposhinda wawe watumishi wenye kujinyenyekeza kwa wananchi siyo kujinyayua mabega kana kwamba wao ndiyo bora kuliko wanaowaongoza.

  "Tafadhalini sana, Chama hiki ni cha wananchi, diwani atakayeshinda ahakikishe  ushindi aliopata haugeuzi kuwa utukufu kwake kabla ya utumishi, huyo tutamshughulikia mara moja", alisema Kinana.


  Kinana alipita katika kata hiyo akiwa njiani kwenda wilayani Njombe ambako anaanza ziara ya siku saba akifuatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya walipokutana wakati wa mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) jijini Addis Ababa, Ethiopia.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Marekani Mh Liberata Mulamula walipokutana wakati wa mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) jijini Addis Ababa, Ethiopia.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Misri Mohamed Morsi walipokutana wakati wa mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha Mhe.Bi. Janeth Mbene katika picha ya pamoja na sekretarieti ya maandalizi ya kongamano hilo picha na Ingihedi Mduma na Eva Valerian.
   Naibu Waziri wa Fedha Bi. Janeth Mbene ambaye ni mgeni rasmi katika ufunguzi wa kongamano hilo akiwahutubia wagavi hawapo pichani.
   Kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma Bw. Bunare Daniel, Mkurugenzi Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Wizara ya Elimu Bw. Jacob Kibona, Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala Wizara ya Fedha Bi. Deodatha Makani, Kamishna wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma Dkt. Frederick Mwakibinga akitoa ufafanuzi, Mkurugenzi Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Wizara ya Habari Bi. Anna Chungu na Kamishna Msaidizi Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma Bw. Alex Haraba.
   Watoa mada katika kongamano hilo, kutoka kushoto ni Mtengaji Mkuu wa wakala wa ununuzi na huduma serikalini Bw. Josephat Mwambega, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi Bw. Clemence Tesha, Eng. Ronald Lyatuu kutoka Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Mkurugenzi wa Usimamizi wa mali za Serikali Bw. Ezra Msanya.
   Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma, Mhakikimali mkoa wa Morogoro Bw. Khamis Simba, Meneja Mkoa Morogoro wakala wa Ununuzi na huduma Serikalini Bw. Moses Kitangalala wakisikiliza kwa makini hoja zilizokuwa zinajibiwa.
    Kamishna wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma ambaye ndiye mwenyekiti wa kongamano hilo Dkt. Frederick Mwakibinga akitoa maelekezo kwa wajumbe waliohudhuria.
   Kutoka kushoto ni Bi. Flora Mduma, Revocatus Chuwa, Michael Luzigah na Alex Haraba ambao ni baadhi ya sekretarieti katika kongamano hilo.
   Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi katika Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Samson Akyaoo akichangia mada katika kongamano hilo.
   Afisa Ugavi kutoka Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Bw. Bulley Mwambete akiuliza swali kwa watoa mada.
   Dkt. Mwakibinga akitoa maelekezo kwa Mjumbe wa kongamano huku Eng. Lyatuu akitabasamu.
   Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya maendeleo Zanzibar Bi. Fatma Jaha akiuliza swali kwa watoa mada.
   Dkt. Mwakibinga akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa kongamano hilo.


  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akilakiwa na Mbunge wa Njombe Kaskazini,Mh Deo Sanga a.k.a Jah People mara baada ya kuwasili jioni ya leo mpakani mwa Mkoa wa Iringa na Njombe katika kijiji cha Idofi,kata ya Mlowa,ambapo pia alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Njombe akitokea Mkoani Iringa ambaka aliwasili leo Asubuhi akitokea jijini Dar akiwa ameambatana na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye.

  Ndugu Kinana na ujumbe wake watakuwa na ziara ya siku saba mkoani Njombe ambapo watatembele Wilaya zote za Njombe,Makete, Ludewa na Wanging'ombe  wakiimarisha chama na kusikiliza matatizo ya Wananchi,huku wakikagua miradi ya maendeleo mbalimbali katika kusimamia serikali ili kutekeleza Ilani uchaguzi ya CCM.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akivalishwa skafu .
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Ludewa,Mh.Deo Filikunjombe,kushoto shati la drafti ni Mbunge wa jimbo la Mwibara,Mh Kange Rugora  Pichani kulia ni Mjumbe wa kamati kuu na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Njombe,Pindi Chana akicheza na akina mama wakati wa mapokezi ya katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana 
   Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye  akishirikiana na  mmoja wa wapiga ngoma za asili wakati walipowasili leo jioni wakiongozwa na  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana
   Ndugu Kinana na ujumbe wake wakipokelewa kwa shangwe mapema jionu ya leo,mpakani mwa Mkoa wa Iringa na Njombe katika kijiji cha Idofi,kata ya Mlowa,ambapo pia alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Njombe akitokea Mkoani Iringa ambaka aliwasili leo Asubuhi akitokea jijini Dar akiwa ameambatana na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye .
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitazama moja ya kikundi cha ngoma kilichofika kumlaki,mara baada ya kuwasili jioni ya leo mpakani mwa Mkoa wa Iringa na Njombe katika kijiji cha Idofi,kata ya Mlowa,ambapo pia alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Njombe akitokea Mkoani Iringa ambaka aliwasili leo Asubuhi akitokea jijini Dar akiwa ameambatana na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye.

  Ndugu Kinana na ujumbe wake watakuwa na ziara ya siku saba mkoani Njombe ambapo watatembele Wilaya zote za Njombe,Makete, Ludewa na Wanging'ombe  wakiimarisha chama na kusikiliza matatizo ya Wananchi,huku wakikagua miradi ya maendeleo mbalimbali katika kusimamia serikali ili kutekeleza Ilani uchaguzi ya CCM.

  0 0
 • 05/27/13--10:59: Taharuki ya mabomu makete.


 • NA EDWIN MOSHI, MAKETE.

  Wakazi wa Makete mjini hasa waliokaribu na kituo cha polisi Makete wamekumbwa na taharuki na mshituko wa hapa na pale kufuatia milio ya mabomu iliyokuwa ikisikika tokea kituoni hapo

  Hali hiyo iliyotokea leo hii imewashangaza wengi na kuwaacha na sintofahamu huku wengi wao wakidhani kuwa yale ya liyotokea Arusha yamebisha hodi Makete

  Kutokana na taharuki hiyo, mtandao huu ulibisha hodi kituoni hapo na kukutana na Mkuu wa polisi wilaya ya Makete SP Peter Kaiza (Pichani)ambaye alilitolea ufafanuzi suala hilo na kusema kwamba hali hiyo imetokea kwa kuwa walikuwa wakifanya mazoezi ya kutuliza ghasia ama vurugu, ambapo iliwalazimu kulipua mabomu.

  “Huo ni utaratibu wa jeshi kutokana na kufanya mazoezi mbalimbali, mara ya mwisho tulilipua mabomu mwaka 2010 mwezi januari, tumekuwa tukiwa katika mazoezi tunafanya hivyo na hii pia inasaidia kuweka askari wetu tayari, na pia wananchi kufahamu kama hali hiyo ikitokea hali inakuwaje” alisema Kaiza.

  Akizungumzia kuhusu kutoa taarifa kwa wananchi, SP Kaiza amesema wangeweza kutoa taarifa kwa wananchi ingawa walitoa taarifa kwa uongozi wa wilaya, lakini wakati mwingine mabomu hulipuka eneo lolote bila taarifa na kwa kufanya hivyo kunasaidia kuwaweka tayari wananchi.

  Amesema mabomu hayo hayana madhara na hakuna tukio baya lililotokea, hivyo kuwataka wananchi kuondoa hofu na kuendelea na shughuli zao kama kawaida

  0 0

  Idda Shizza akiwa na swaiba yake Farida Nyamsogoro wakiwa na furaha mara baada ya kuhitimu  diploma ya ualimu wa sekondari.
   Familia ya Idda Shizza,Pamoja na familia ya Farida Nyamsogoro wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya wanafunzi hawa kuitimu ualimu wa sekondari ngazi ya diploma katika chuo cha kigurunyembe
   Mdada wa libeneke la kaskazini kati kati akiwa na walimu wapya  mara baada ya kugradueti katika chuo cha ualimu wa sekondari kigurunyembe kilichopo Morogoro


  0 0

   Wanenguaji wa bendi ya Akudo wakifanya vitu vyao ndani ya ukumbi wa world  garden.
   warembo walikua kibao waliokuja kucheki shoo ya Akudo
   Kamafa wa Radio 5 nae alikuwepo katika shoo hiyo.
   hii meza ilikuwa imetawaliwa na kinywaji cha K-vant iliongozwa na meneja wa kanda wa kinywaji hicho Godluck
   Watangazaji wa Radio 5 107:5 fm Arusha wa kwanza kulia ni Deo  G katikati mdada wa libeneke pamoja na mkaka Matungilo wakisakata rumba
   watu waliyarudi balaa yote haya ni chini ya uthamini kampuni ya Tan Media Comunication kupitia kituo chao kikubwa cha   Radio ya watu Radio 5 Arusha.


   Full mzuka kampani nzima ya Radio 5 ikiongozwa na kamafa
   Mwanadada Ashura Muhamedi Alikuwepo kwenye shoo hiyo
   Ulikua ukiingia tu unakutana na meza iliyopendeza vinywaji vya k-vant gin


  0 0

  Katibu mkuu wa chama cha Riadha Taifa,Suleyman Nyambui (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza kufunguliwa rasmi milango kwa makampuni, mashirika na taasisi mbalimbali zitakazopenda kudhamini mbio za Uhuru Marathon ambazo ni za aina yake nchini zitakazokuwa zikifanyika kila mwezi Desemba zikiambatana na maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa Tanzania.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Intellectuals Ltd ambao ndio Waratibu wa Mbio hizo,Innocent Melleck.
  Mkurugenzi Mkuu wa Intellectuals Ltd ambao ndio Waratibu wa Mbio hizo,Innocent Melleck akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza kufunguliwa rasmi milango kwa makampuni, mashirika na taasisi mbalimbali zitakazopenda kudhamini mbio za Uhuru Marathon ambazo ni za aina yake nchini zitakazokuwa zikifanyika kila mwezi Desemba zikiambatana na maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa Tanzania.Kushoto ni Katibu Mkuu wa chama cha Riadha Taifa,Suleyman Nyambui.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukua tukio hilo.

  Kampuni ya Intellectuals Limited, ambao ndio waasisi na waratibu wa mbio za Uhuru zijulikanazo kama “Uhuru Marathon” leo wametangaza kufungua rasmi milango kwa makampuni, mashirika na taasisi mbalimbali zitakazopenda kudhamini mbio hizi za aina yake nchini zitakazokuwa zikifanyika kila mwezi Desemba zikiambatana na maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa Tanzania.

  Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam, mkurugenzi mkuu wa Intellectuals Ltd Bw. Innocent Melleck, alisema; Nadhani wote mnakumbuka uzinduzi wa mbio hizi za Uhuru, uliofanyika mwezi Desemba mwaka Jana, ukiwa unaashiria kuanza kwa mchakato wa maandalizi ya mbio zenyewe ambazo zitaanza kufanyika mwezi desemba mwaka huu 2013. 

  Mbio hizi za Uhuru, kama lilivyo jina lake ni mbio zilizoanzishwa ili kuongeza chachu za watanzania kuwa na moyo wa kulinda Amani, Umoja na Mshikamano wetu, wakati tunaposherehekea sikikuu za Uhuru wa Taifa letu. Tangu tulipofanya uzinduzi mwezi desemba mwaka jana, sisi waratibu  na viongozi wa chama cha riadha Tanzania (RT), tulianza mchakato wa maandalizi ya awali ya kufanikisha mbio hizi, ikihusisha kupanga mzunguko utakaotumika kwa mbio hizo n.k.

  Kwa sasa maandalizi ya awali yanaendelea vizuri, nasi tumeona kuwa huu ni muda muafaka kufungua milango ya Udhamini kwa makampuni, mashirika na Taasisi mbalimbali ambazo zitahitaji kushirikiana nasi katika kufanikisha mbio hizi wajitokeze na kupata taratibu za udhamini. Tuna imani kubwa kuwa wapo wadau wengi wenye lengo la kufanikisha ajenda hii muhimu ya kuenzi Amani, Umoja na mshikamano wa Taifa letu. Mbio hizi zina vipengele vikuu vitatu; 
  i.                     Mbio Ndefu (Full Marathon 42 km)
  ii.                   Mbio za Kati (Half Marathon 21 km) na
  iii.                  Mbio za kujifurahisha (Fun run 5km)
  Mdhamini atakayedhamini mbio ndefu (full marathon), ndie atakaebeba jina la Mashindano haya. Hivyo nawasihi wale wote wenye nia ya kudhamini kuanza kujitokeza sasa na kuchagua mbio zipi wanataka kudhamini ili taratibu nyingine zifuatie. Alisema Innocent.

  Akizungumzia kuhusu upande wa ufundi, Katibu mkuu wa chama cha Riadha Taifa Bw. Suleyman Nyambui alisema; kwa upande wetu sisi RT, maandalizi ya awali yameshaanza kufanyika ikiwemo kupendekeza mzunguko wa mbio hizo na kuangalia mambo yote ya kiufundi yanayohusiana na mbio hizi. 

  Tunawaomba wadhamini wajitokeze ili kwa pamoja tuweze kufanikisha mbio hizi zenye malengo mazuri kwa Taifa letu kwa ujumla. Mbio hizi tutazisimamia na kuziendesha katika hadhi ya kimataifa ili kuhakikisha kuwa zaidi ya kulinda Amani na Umoja wetu, pia tunalitangaza Taifa letu kote ulimwenguni. 

  Kwa kuwa mimi ninaangalia zaidi upande wa ufundi, nichukue nafasi hii pia kuwasihi wanariadha wa hapa nchini kuanza maandalizi ya mbio hizi, maana mwezi desemba si mbali, japo najua kuwa wapo ambao walishaanza maandalizi tangu tulipozindua rasmi mwaka jana. Itakuwa si vyema nafasi za juu zikichukuliwa na wageni, wakati sisi tunao wana riadha wazuri hapa nyumbani.

  0 0  28 housemates, 91 days and USD300 000 - Big Brother Africa is back!
  The eighth season of the continent's biggest reality show blasted off
  on Sunday night (26 May at 19:00 CAT on DStv Channel 197 & 198) with
  one thing in mind - The Chase!

  Produced by Endemol SA and headline sponsored by Airtel, Sunday
  night's blazing live show saw 28 housemates from 14 countries pair up
  to share two houses. But the heat is on as they'll have their first
  nomination sessions less than 24 hours after meeting each other for
  the first time. Two housemates WILL leave the show next Sunday!

  Managing Director, Airtel Tanzania, Sunil Colaso commented: "Airtel is
  proud to be associated with Big Brother - Season 8. We identify with
  the diverse audiences watching this remarkable programme in over 50
  African countries and the unique opportunity to create awareness of
  some of our ground breaking services to the audience. The reality show
  is also a perfect match with Airtel's goal of not only offering
  entertainment but also connecting millions of people through music."

  The show kicked off with South African supergroup Mafikizolo
  performing 'Khona', backed by magnificent dancers from the Mzansi
  Ballet Theatre.  Presenter IK rolled up in style on a motorcycle and
  promised viewers an exciting three months of television, which will
  see the housemates playing the game with their eyes firmly on the
  USD300 000 prize.

  After a touching tribute to Nigerian star Goldie, who passed away
  earlier this year, comedians Tumi Morake (South Africa) and Churchill
  (Kenya) got the chance to explore the two houses which will host the
  housemates this year - called Diamond and Ruby. Two houses, of course,
  mean two 24/7 channels, with viewers able to follow the action in
  either house via DStv Channel 197 or 198.

  Boity Thulo was on hand to show viewers how they can interact with Big
  Brother: The Chase this year. Last year, Big Brother StarGame
  captivated the market with 2.3 million website visitors, 140 million
  page views, over 1 million Facebook likes and 2.3 million TV messages.
  is tailored to whichever device you view it on, to deliver the best
  possible user experience. Signing up as a VIP Member will deliver a
  host of exclusive content that you won't want to miss out on. Viewers
  will also be able to use the website or their mobile devices to vote
  to keep their favourite housemate in The Chase.

  It was time to meet the housemates, with IK explaining that the ladies
  would be given the choice of their male counterparts. After being
  called on stage, they would select a male housemate to join them in
  the house, based on a picture of their smile, alone. Each of the men
  would be wearing an element with a particular colour to denote which
  house the duo would then head into - red for Ruby or yellow for
  Diamond.

  Zimbabwe's Pokello was the first housemate to be introduced to Africa.
  Asked to select a pic from IK's tablet, she chose LK4 from Uganda.
  Ghana's Selly was up next and selected a pic of Bassey from Sierra
  Leone. Dellish (Namibia) was the third lady to take the stage,
  selecting South Africa's Angelo, based on the image of his smile on
  IK's tablet. Malawi's Fatima was up next, selecting Tanzania's Nando
  to join her.

  Kenyan Huddah's photo selection drew Ethiopia's Bimp to the stage,
  before Motamma from Botswana chose Angola's Neyll. Beverly (Nigeria)
  picked Sulu from Zambia, followed by Zambia's Cleo who chose
  Botswana's Oneal. Namibian Maria was the next housemate to join IK on
  stage, joined shortly afterwards by Nigeria's Melvin. IK introduced
  Natasha from Malawi next, with Angola's Biguesas, her choice.

  Tanzanian Feza was the next housemate to join IK on stage, choosing
  Ghana's Elikem to join her. Betty from Ethiopia followed, with Bolt
  from Sierra Leone joining her shortly after. Annabel from Kenya was
  next up, with her photo selection giving IK the chance to introduce
  Uganda's Denzel to the continent. South Africa's Koketso was the final
  housemate IK summoned to the stage to make her choice, bringing
  Zimbabwe's Hakeem up to join her.

  IK then revealed a few changes to the game this year, with the news
  that Big Brother was on the hunt for housemates who would be making
  romantic gestures, with a special prize up for grabs for the housemate
  who brought the most romance into the house. The Head of House also
  gains new powers. Along with the ability to 'save & replace' nominees,
  the HoH will also have the power to switch housemates between houses
  each Friday during the Airtel Showdown arena games. There's also a new
  '3 Strike Rule' for housemates. Those who commit serious infringements
  of rules which don't lead to immediate disqualification, will pick up
  'strikes'. Three strikes will see them disqualified from the game, and
  leaving the house.

  South African comedian Tumi Morake will also be hosting a special show
  on AfricaMagic after each Sunday's show called Big Brother Hot Room,
  starting 2 June at 21:00 CAT. She'll put a satirical spin on the week
  that was, take comic pot shots at the most talked-about events of the
  week and re-enact parody scenes with housemates.

  Kenyan singer, songwriter and rapper STL delivered an unforgettable
  performance of 'Stella Stella Stella' in her distinctive style during
  the show, which was closed out by performances from D'Prince, who
  dazzled the continent with 'Goody Bag' and Don Jazzy & Wande Coal, who
  took the roof off the studio with 'The Kick'.

  Commenting on the launch The Chase, M-Net Africa MD Biola Alabi says,
  " AfricaMagic is excited that Africa's biggest reality show is now
  underway. Audiences can expect the addition of interesting and
  engaging new elements to the show. Big Brother has displayed
  remarkable growth over the years and we hope that this year will be no
  different. The launch of Hot Room will certainly bring fun, laughter
  and witty commentary in an amusing and comical way. Shock, drama,
  emotions and surprises have always been synonymous with the show but
  audience must keep watching because anything is possible over the next
  91 days. There will also be great prizes up for grabs weekly so keep
  watching the show and AfricaMagic channels for details!"

  As the housemates congregated in their respective lounges to get their
  first message from IK, Boity reminded viewers of the ways to stay up
  to date with Big Brother Africa: The Chase. Viewers can press 'OK' on
  DStv Channels 197 or 198 to read up on the latest news, send messages
  to TV by tweeting and using #bigbroafrica or #bbathechase, using
  Facebook to log into the 'message to TV' application on their computer
  or phone or send a text message via the shortcode for their country.

  The winner of Big Brother: The Chase will be named after 91 days of
  head-to-head competition - and the power to award to USD 300 000 prize
  rests completely in the hands of the viewers.

  0 0


  Jana usiku tumeona nusu fainali ya kwanza ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLEGE™ ambapo timu ya Ghana walionesha kuwa wao ni timu bora baada ya kushinda na kuwa timu iliyoshinda kiasi kikubwa zaidi cha pesa.

  Jonathan Nabb and Desmond Odaano showed that they have the confidence to live bold sensationally knocking out their rivals and going on to hit target four on the GUINNESS Money Wall taking their winnings from the episode to over $12,000 to add to their $8,500 from previous rounds.

  Jonathan Nabb na Desmond Odaano walionesha kuwa wana uwezo na ni majasiri walipowashinda adui zao na mwisho kushinda hadi $12,000 USD baada ya kulenga lengo namba nne katika hatua ya pesa ukutani.


  Going home, but not empty handed with their $ 5,500 USD winnings from their National episodes and Quarter Finals were Daniel Msekwa and Mwalimu Akida Hamad from Dar Es Salaam.  The pressure will now be on the final two teams from Kenya in the next Semi-Final as they will be flying the flag for the whole of East Africa. 

  Watakaorudi nyumbani ni Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad kutoka Dar-es-Salaam wakiwa na $5,500 USD walizojipatia katika hatua za kitaifa.Sasa kazi itakuwa kwa timu mbili za Kenya katika nusu fainalli ijayo watakapokuwa wakiiwakilisha Afrika mashariki.

  Winners, Jonathan and Desmond, were also awarded $4,000 in recognition of the amazing effort they put in through the first two rounds, which saw a completely flawless performance.  They showed how to live bold, not faltering on any question or missing any opportunity with the ball.  They have now secured a spot on the first Pan-African Final and are in with a chance of raising their country’s flag as champions.  

  Washindi,Jonathan na Desmond,walizawadiwa pia $4,000 USD baada ya kuonesha mchezo mzuri sana katika mizunguko miwili ya mwanzo ya mchezo ambapo hawakukosa hata swali moja.Sasa wamefanikiwa kujihakikishia nafasi katika fainali ya Pan-african na hata kuwa washindi wa mashindano hayo.


  Joining Jonathan and Desmond in the final will be the show’s runners-up Francis Ngigi and Kepha Kimani from Nairobi who narrowly missed out on the GUINNESS Money Wall but will still have a chance of becoming champions.  Their fellow countrymen Kenneth Kamau and Willis Ogutu didn’t make it to the final stages of the episode and will be leaving the pride of East Africa in Francis’ and Kepha’s hands. 

  Watakaowaunga washindi ni Francis Ngigi na Kepha Kimani kutoka Nairobi  waliokuwa washindi wa pili.Japokuwa hawakufanikiwa kufikia hatua ya pesa ujutani lakini wamefuzu fainali.Wenzao kutika Kenya Kenneth Kumau na Wills Ogutu hawakufanikiwa kufuzu hivyo Francis na Kepha ndio watakaowakilisha Afrika mashariki.  

  Guinness Brand Manager, Davis Kambi from Serengeti Breweries said: “Everyone at GUINNESS and the whole of Tanzania are extremely proud of Daniel and Mwalimu – even though they didn’t make it through they won a great amount of money and really showed that they have what it takes to be real players in life.  All of our footballing pairs did incredibly well to get to our first ever Semi-Final and congratulations to Jonathan and Desmond from Ghana!  We are now looking forward to the next Semi-Final and cheering on the Kenyan teams who will be playing for East Africa!”

  Mkurugenzi wa GUINNESS alisema,”Sote Tanzania tunawapongeza Daniel na Mwalimu-japokuwa hawakufanikiwa kufuzu fainali lakini wamejishindia kiasi kikubwa cha pesa.Kila timu ilijitahidi kufikia nusu fainali na hongera kwa Desmond na Jonathan kutoka Ghana kwa ushindi wao.Sasa tunasubiri nusu fainali ijayo kila la heri kwa wote pamoja na timu za Kenya zitakazowakilisha Afrika mashariki.

  Vying for their chance in the Finals in the second Semi-Final are the following football fanatics:  EAST AFRICA
  ·         IN BLACK - Ephantus Nyambura, 24, and Samuel Papa, 23, from Nairobi will be hoping to do better than the $3,000 they won in their National and Quarter Final episodes. Ephantus will be the Brain of the pair whilst Samuel, who plays football for Nakuru Allstars FC, will take on the skills round

  ·         JEZI NYEUSI – Ephatus Nyambura,24 na Samuel Papa,23 kutoka Nairobi watatarajia kushinda zaidi ya $3,000 USD walizopata katika hatua za kitaifa na robo fainali.Ephatus atajibu maswali wakati Samuel anayechezea Nakuru Allstars atakuwa mchezaji.

  ·         IN RED - Kenneth Mukuri , 26, and Chris Mwamgi, 19, are from Nairobi.   They will be hoping to go all the way after struggling to win more than $1,500 on the GUINNESS Money Wall in their National episode.  Kenneth will be the teams Brain while Chris will be the Brawn. 

  ·         JEZI NYEKUNDU – Kenneth Mukuri,26 na Chris Mwamgi,19 kutoka Nairobi watakuwa wakitarajia kushinda zaidi ya $1,500 USD walizopata katika hatua za kitaifa.Kenneth atakuwa kichwa cha timu wakati Chris atakuwa mchezaji.

  CAMEROUN:
  ·         IN GREEN - Emerand Tchouta, 24 and Abdul Salam, 25 have a total prize fund of $6,500 after hitting target 4 on the GUINNESS Money Wall in their Quarter-Final.  Brain Emerand and Brawn Abdul will now be hoping to captalise on their winnings and make it all the way to the final

  ·         JEZI ZA KIJANI – Emerald Tchouta,24 na Abdul Sam,25 ambao wana jumla ya $6,500 baada ya kulenga lengo namba nne katika robbo fainali.Sasa Emerald na Abdul watacheza kuwania nafasi ya kufuzu fainali.

  GHANA:
  ·         IN BLUE - Emmanuel Kofi Okarku, 27 and Isaac Aryee, 25 from Accra in Ghana will be playing for their West African nation as they hope to win the episode and become Pan-African champions.  They already have $3,000 USD and pro footballer Isaac will need to once again put his skills to good use while Emmanuel tackles the knowledge questions 

  ·         JEZI ZA BLU – Emanuel Kofi Okarku,27 na Isaac Aryee,25 kutoka Accra Ghana wataichezea nchi yao kutoka Afrika magharibi ili kufuzu fainali.Tayari wana $3,000 USD hivyo Isaac atahitajika kuonesha kipaji chake cha kucheza wakati Emanuel atajibu maswali.

  Fans of the show can test their own football knowledge via the GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE mobile phone game which is available on the exciting GUINNESS mobile social community for football lovers, GUINNESS® VIP™.   Sign up for free and test your knowledge to see where you stand on the all new Pan-African leader board at m.guinnessvip.com on your phone.  

  Mashabiki wa mashindano haya wanaweza kupima maarifa yao kupitia mchezo wa simu za mkononi wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE unaopatikana katika simu za kijamii za GUINNESS kwa ajili ya wapenzi wa mpira wa miguu, GUINNESS® VIP™. Jiunge bure sasa upime maarifa yako katika michezo,tembelea m.guinnessvip.com sasa.

  Make sure to like to GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE Facebook page for all the latest details – www.facebook.com/[insert]

  The second Semi-Final, produced by Endemol, is broadcast on ITV every Wednesday at 21:15hours, so make sure you grab a bottle of ice cold GUINNESS and get behind East Africa.
  Nusu fainali ya pili ya mashindano haya itaoneshwa ITV jumatano saa 3:15 usiku, usiikose huku ukiburudika na Guinness.
  Please drink responsibly – strictly 18+.
  Tafadhali kunywa kistaarabu-kwa wenye miaka 18 na kuendelea tu.

  0 0


older | 1 | .... | 90 | 91 | (Page 92) | 93 | 94 | .... | 1898 | newer