Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

Mh Mwigulu Nchemba alipohutubia leo mkoani Singida kwenye ziara ya Rais Magufuli


JAJI MKUU AMSABAHI SPIKA WA BUNGE NYUMBANI KWAKE.

$
0
0

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai alipofika kumsabai nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mke wa Spika Dkt Fatma Mganga. Spika amerejea nchini hivi karibuni kutoka nchini India ambapo alikwenda kwa ajili ya uchunguzi pamoja na matibabu ya Afya yake.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman aliyefika kumsabai nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Spika amerejea nchini hivi karibuni kutoka India ambapo alikwenda kwa ajili ya uchunguzi pamoja na matibabu ya Afya yake.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akifurahia jambo na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman aliyefika kumsabai nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Spika amerejea nchini hivi karibuni kutoka India alipokwenda kwa ajili ya uchunguzi pamoja na matibabu ya Afya yake.(Picha na Ofisi ya Bunge).

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA JOSEPH SENGA

$
0
0


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Theophil Makunga kutokana na kifo cha Joseph Senga – Mpigapicha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima.

Rais Malinzi amepokea taarifa za kifo cha mwandishi huyo mwandamizi wa habari aliyebobea kuripoti habari za aina mbalimbali ikiwamo za michezo nchini kilichotokea jioni ya Julai 27, 2016 huko India, alikokuwa akipatiwa matibabu ambako habari za kifo chake zilianza kusambaa usiku wa kuamkia jana Julai 28, 2016 kabla ya kuthibitishwa na Mhariri Mtendaji wa Free Media, Neville Meena.

Salamu za rambirambi za Rais wa TFF Malinzi pia zimekwenda kwa familia ya marehemu Joseph Senga, ndugu, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na moyo wa subira wakati huu mgumu wa msiba wa mpendwa wao.

Malinzi alimwelezea Joseph Senga, wakati wa uhai wake alikuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya habari za michezo akitoa mawazo yake hivyo ameacha alama ya ucheshi, kujituma na uwajibikaji katika kufanikisha kazi zake katika gazeti la Tanzania Daima na wakati fulani magazeti ya Kampuni ya New Habari House 2006.

Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu Joseph Senga mahala pema peponi.

Bwana alitoa, Bwana alitoa, jina la Bwana lihimidiwe.

VETA YATOA VIFAA VYA UFUNDI VYA SH.MILIONI 11 KWA ATAMIZI YA OSARIKA JIJINI DAR ES SALAAM leo.

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
MAMLAKA ya Elimu na Ufundi Stadi Kanda ya Dar es Salaam VETA imetoa vifaa vya thamani ya sh.milioni 11 katika atamizi ya Osarika Woodwork ikiwa ni sehemu ya kuendeleza atamizi hiyo kwa ujuzi na kufundisha vijana wengine wanaoenda kufanya mafunzo ya vitendo.

Akizungumza leo wakati hafla ya kukabidhi vifaa katika atamizi ya Osarika Woodwork, Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam wa VETA, Habib Bukko amesema kuwa vifaa hivyo walivyotoa kwa kikundi hicho kuongeza uzalishaji samani mbalimbali ikiwa ni pamoja kutoa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wanaotoka Veta.

Amesema vijana wa Osarika ni zao la VETA ambao wameweza kuunda kukundi na kusajili hivyo wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira lakini wameonyesha njia mpaka kuja kuongeza nguvu ya vifaa.

Bukko amesema vifaa hivyo ni mali kikundi cha Osarika wakivurugana vitu hivyo wanatakiwa kurudisha ili vikaweze kufanya kazi katika atamizi nyingine .

Aidha amesema kuwa VETA kuendeleza ni atamizi ni sehemu yao katika kuhakikisha atamizi zinaendelea katika kuzalisha ajira za vijana kutokana na mafunzo waliopata katika vyuo vya Ufundi.

Naye Mwakilishi wa Diwani wa Kata ya Tandika, Mwenyekiti wa Serikali Mtaa Mabatini ,Sharifu Jumbe amesema kuwa vijana wanatakiwa kujituma katika kufanya kazi na kuwataka wengine waende kupata mafunzo VETA.

 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mabatini-Tandika  ambaye ni Mgeni rasmi, Sharif Jumbe akimkabidhi moja ya kifaa cha Kukatia Mbao na Alminium mwanaatamizi ya Orasika-Tandika, David Mshilili jijini Dar es Salaam leo. Kulia aliyevaa Koti ni Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam, Habibu Bukko.
 Sehemu ya misaada ya iliyotolewa na chuo cha VETA kanda ya Dar es Salaam leo katika kikundi cha Atamizi ya Orasika iliyopo Tandika jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuongeza nguvu kwa vijana ili kupunguza ongezeko la vijana wasio na ajira.
Mtafiti mwandamizi wa Soko la Ajira VETA, Peter Katabi akitambulisha viongozi mbalimbali wa chuo cha VETA kanda ya Dar es Salaam leo.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mabatini-Tandika  ambaye ni Mgeni rasmi, Sharif Jumbe akizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi wanakikundi cha Atamizi ya Osarika vifaa vya ufundi vyenye thamani ya shilingi Milioni 11 kutoka VETA jijini Dar es Salaam leo.
Fundi wa Atamizi ya Osarika kilichopo Mtaa wa Magulue-Tandika jijini Dar es Salaam,Salum Sese akizungumza kwa niaba ya wanakikundi cha atamizi ya Osarika jijini Dar es Salaam leo.

 Fundi wa Atamizi ya Osarika, Zadoki James akisoma risala kwa niaba ya kikundi cha Atamizi ya Osarika kabla ya kupewa vifaa vya ufundi stadi na Kanda ya Dar es Salaam ya Chuo cha VETA jijini Dar es Salaam leo.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mabatini-Tandika  ambaye ni Mgeni rasmi, Sharif Jumbe akikabidhiwa Risala ya Atamizi ya Orasika-Tandika jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi vijana wa Atamizi ya Orasika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Kanda wa chuo VETA, Habibu Bukko akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vifaa vya ufundi kwa Atamizi ya Orasika-Tandika jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya Vifaa vya ufundi vilivyotolewa na chuo cha VETA kanda ya Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mabatini-Tandika  ambaye ni Mgeni rasmi, Sharif Jumbe akimkabi baadhi ya vifaa vya ujenzi vijana wa atamizi ya Osarika jijini Dar es Salaam leo. 

 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mabatini-Tandika  ambaye ni Mgeni rasmi, Sharif Jumbe, Viongozi wa chuo cha VETA, wanaatamizi ya Osarika wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanachi wa mtaa huo jijini Dar es Salaam leo.

DIAMOND NA SWIZZ BEATS NA MPANGO WA KUINUA MUZIKI WA AFRICA

$
0
0

DIAMOND PLATNUMZ JUZI KATI TAREHE 22 JULY ALIPERFORM KWENYE TAMASHA LA ONE AFRICA MUSIC FESTIVAL AMBAYO ILIFANYIKA BROOKLYN NEWYORK KTK UKUMBI MKUBWA WA Barclay center, NEW SHOW KUBWA KULIKO ZOTE AMBAZO DIAMOND AMEWAHI KU PERFORM NJE YA AFRICA, XXL ILIWAKILISHWA NA B DOZEN AMBAYE ALISHUHUDIA PRODUCER SWIZZ BEATS AKIFIKA KWENYE SHOW HIYO MAALUM KWA AJILI YA KUKUTANA NA DIAMOND PLATNUMZ, SO MUDA MFUPI BAAD AYA MEETING HIYO, DOZEN ALIMVUTA CHAMBER DIAMOND AKAFUNGUKA WALICHOZUNGUMZA NA PRODUCER SWIZZ BEATS AMBAYE ANA TUZO MBILI KUBWA DUNIANI ZA BET, NA GRAMMYS

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MJULIA HALI SPIKA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge , Job Ndugai wakati alipokwenda nyumbani kwa Spika jijini Dar es salaam kumsalimia Julai 29, 2016. Mheshimiwa Spika amerejea nchini hivi karibuni akitoka India kwa matibabu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge , Job Ndugai wakati alipokwenda nyumbani kwa Spika jijini Dar es salaam kumsalimia Julai 29, 2016. Mheshimiwa Spika amerejea nchini hivi karibuni akitoka India kwa matibabu. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Bunge)

WATAKAOLETA VURUGU MIMI NITAWASHUGHULIKIA KIKAMILIFU BILA HURUMA,WANANCHI HAWA WANA SHIDA WANATAKA KUTATULIWA MATATIZO YAO-RAIS MAGUFULI

WATAKAOLETA VURUGU MIMI NITAWASHUGHULIKIA KIKAMILIFU BILA HURUMA,WANANCHI HAWA WANA SHIDA WANATAKA KUTATULIWA MATATIZO YAO-RAIS MAGUFULI


MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA TAASISI YA SARATANI

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza na Katibu wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Saleh Ramadhan Feruzi (katikati) ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimjulia hali Ndugu Said Mohamed mkazi wa Mafia ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Mkazi huyo wa Mafia alimueleza Makamu wa Rais juu ya ugumu wa upatikanaji wa Dawa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimjulia hali Bi. Maria Maliseli Boniface wa Kilosa Morogoro ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimjulia hali Ndugu Calist P. Mushi mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dk. Diwani Msemo (kulia) wakati wa kutembelea Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza na wananchi waliokuja kuwaona ndugu na jamaa zao ambao wamelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Wananchi hao walimueleza Makamu wa Rais haja ya kuongezwa kwa mashine za mionzi suala ambalo Makamu wa Rais aliwajibu kuwa zitafungwa mashine mpya mbili katika mwaka huu wa fedha 2016-2017 ilikurahisisha matibabu.

...................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwa serikali itanunua mashine mbili za kisasa za mionzi kwa ajili ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa utoaji wa matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kupata matibabu katika Taasisi hiyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Sulu Hassan ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara fupi ya kutembelea Taasisi ya Saratani ya Ocean Road pamoja na Kumtembelea na kumpa pole Katibu wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Saleh Ramadhani Feruzi ambaye anapatiwa matibabu kwenye Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa mkakati uliopo wa serikali unalenga kuhakikisha kuwa hali ya utoaji wa huduma za afya na dawa kote nchini unaimarika maradufu ili wananchi waweze kupata huduma hizo kwenye maeneo yao kwa ubora unatakiwa.

Kuhusu uhaba wa wahudumu wa afya katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameuahidi uongozi wa Taasisi hiyo kuwa serikali itahakikisha wahudumu hao wanapatikana katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Baadhi ya wagonjwa na wananchi wamepongeza utoaji wa tiba katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na wameomba serikali iendelee kuipatia taasisi hiyo vifaa vya kisasa vya kutolea tiba kama hatua ya kuboresha utoaji wa matibabu kwa wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu ya saratani.

Rais Magufuli aanza ziara ya siku nne mikoa minne, aonya watakaothubutu kufanya vurugu

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Julai, 2016 ameanza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma, ambapo amezungumza na wananchi kwa lengo la kuwashukuru kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.

Akiwa Mkoani Singida, Rais Magufuli aliyeongozana na mkewe Mama Janeth Magufuli amewasihi watanzania kufanya kazi kwa juhudi na kujiepusha na vitendo vya vurugu vinavyohamasishwa na baadhi ya wanasiasa huku akionya kuwa serikali yake haitamvumilia mtu yeyote ambaye atathubutu kuchochea vurugu ikiwemo maandamano kinyume cha sheria.

"Sitaki nchi hii iwe ya vurugu, watakaoleta vurugu mimi nitawashughulikia kikamilifu bila huruma, na wasije wakanijaribu, mimi ni tofauti sana na kama wapo watu wanaowatumia wakawaeleze vizuri, mimi sijaribiwi na wala sitajaribiwa."Wananchi hawa wana shida, na siasa nzuri ni wananchi washibe, siasa nzuri ni wananchi wetu wapate dawa" Amesema Rais Magufuli.

Kuhusu hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali yake ya awamu ya tano tangu aingie madarakani Rais Magufuli ametaja baadhi ya hatua hizo kuwa ni kufuta ada kwa shule za msingi na sekondari, kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu zaidi ya laki moja na kuongeza fedha za miradi ya maendeleo katika bajeti ya serikali kutoka asilimia 26 ya mwaka 2015/2016 hadi kufikia asilimia 40 katika bajeti ya mwaka huu 2016/2017.


Hatua nyingine ni kuondoa wafanyakazi hewa 12,500 katika orodha ya waliokuwa wanalipwa mshahara na serikali, kudhibiti upotevu wa mapato serikalini, kutenga shilingi Trilioni moja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani Standard gauge na pia akazungumzia hatua zilizochukuliwa dhidi ya wala rushwa na wanaojihusisha na ufisadi kwa kuunda mahakama ya mafisadi huku akiapa kuwa katika kipindi chake hakuna fisadi atakayeendelea kutamba.

Akiwa njiani Rais Magufuli amewasalimu wananchi wa Ikungi na baadaye amefanya mkutano wa hadhara Singida Mjini ambako amesisitiza kuwa serikali yake haiko tayari kumvumilia mtu yeyote atakayekwamisha utekelezaji wa Ahadi na Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Singida
29 Julai, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akimpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Manyoni Mkoani Singida mara baada ya kuwasili katika Wilaya hiyo akiwa njiani kuelekea mkoani Singida. 

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wakazi wa Singida mara baada ya kuwasili. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wakazi wa Manyoni mara baada ya kumaliza kuhutubia katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tambuka Reli Manyoni Mkoani Singida.
Mbunge wa manyoni Magharibi Yahya Masare akicheza ngoma na kikundi cha Ngoma za asili cha Manyoni kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Magufuli kuhutubia mkutano katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tambuka Reli Manyoni Mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Ikungi waliomsimamisha wakati akielekea Mkoani Singida. PICHA NA IKULU

Wasanii waaswa kuzingatia maadili katika utengenezaji wa kazi zao.

$
0
0

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) akikata utepe kuzindua studio mpya ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam wa pili kushoto ni mmoja ya wakurugenzi wa Wanene Entertainment Bw. Darish Pandit.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) akiangalia moja ya vyumba vya kurekodia na kutengengeneza video vilivyopo ndani ya studio ya Wanene Entertainment mara baada ya kuizindua studio hiyo Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia) akipata maelezo kutoka kwa mmoja ya wakurugenzi wa Wanene Entertainment Studio Bw. Darish Pandit(kushoto) kwa kuhusu maeneo mbalimbali ndani ya studio hiyo Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam. Mtayarishaji wa video kutoka kampuni ya Wanene Entertainment Studio Bw. Hanscana akimuonesha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (aliyekaa) naamna kazi za video zinavyotengenezwa mara baada ya kurekodiwa katika maeneo mbalimbali alipotembelea studio hiyo mara baada ya kuizindua rasmi Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wadau waliohudhulia hafla ya uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam.


Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura ( wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa studio za kisasa za Wanene Entertainment na wa tatu kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo.


PIL1Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo wakati akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29,2016 Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akisalimiana na mmoja wa wakurugenzi wa Wanene Entertainment Bw. Darish Pandit wakati akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akimsikiliza kwa makini mmoja wa wakurugenzi wa Wanene Entertainment Bw. Bhadresh Pandit (kulia) wakati wa hafla uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam katikati ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo .



Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akizungumza jambo na wakurugenzi wa Wanene Entertainment Bw. Bhadresh Pandit (kushoto) na Bw. Darish Pandit(wa pili kushoto) wakati wa hafla uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam wa pili kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo na kulia ni mtayarishaji wa video kutoka kampuni ya Wanene Entertainment Bw. Hanscana.
(Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM)

…………………………………………………………………………………………..

Na Raymond Mushumbusi WHUSM

Wasanii nchini wameaswa kuzingatia maaadili katika utengenezaji wa kazi zao ili kuenzi na kulinda mila, desturi na tamaduni za mtanzania .

Wito huo umetolewa jana na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakati akizindua studio ya kisasa ya kurekodi kazi za sanaa ya Wenene Entertainment.

Mhe Anastazia Wambura amesema kuwa baadhi ya wasanii wamekuwa hawafati maadili katika utengenezaji wa kazi zao na kuvifanya vyombo vinavyosimamia kazi za sanaa nchini kama Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kutoa adhabu dhidi yao kutokana na ukiukwaji wa maadili katika kazi zao.

“Ninaiomba kampuni ya Wanene Entertainment kuisaidia Serikali kuwaelimisha wasanii watakaoleta kazi zao kutengenezwa kwenu kuzingatia maadili badala ya kutengeneza kazi ambazo haziendani na maadili ya nchi yetu” alisema Mhe Anastazia.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo amehaidi kushirikiana na studio ya Wanene Entertainment kuendeleza sanaa ya Tanzania kufikia katika viwango vya kimataifa na kuongeza pato la wasanii na taifa kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Wanene Entertainment Bw.Darsh Pandit amesema kuwa ufunguzi wa studio hiyo ni muitikio wao kwa Serikali ya awamu ya tano katika suala la kutoa ajira kwa vijana na kuwezesha vijana kujiajiri kwa kutumia vipaji vyao kupitia kazi za sanaa.

“Studio hii ina lengo la kukuza na kuendeleza sanaa ambayo imekuwa ajira kubwa kwa vijana wengi na tunaahidi kuzingatia maadili katika utengenezaji wa kazi zetu na pia tutazingatia ubora ili kuitangaza sanaa ya Tanzania kimataifa” alisema Bw. Pandit.

Aidha mtayarishaji wa video katika kampuni hiyo Bw. Hasacna amesema kuwa ni fursa sasa kwa watayarishaji wa video wanaochipukia nchini kuonesha vipaji vyao kwa kuwa wabunifu katika uandaaji na utengenezaji wa video za muziki na filamu kwa ujumla.

KIWANDA MAARUFU CHA DANGOTE CHATOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 15 KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA.

$
0
0

Naibu Waziri Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ( katikati) Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Khatib Kizinga (kushoto) wakipata maelezo toka kwa Bw. Sultani Pwaga wa kiwanda cha Gesi cha Madiba Mjini Mtwara wakati wa ziara ya Naibu Waziri Mpina kiwandani hapo.
Kushoto Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akipata maelezo kuhusu uchimbaji wa malighafi ya kutengeneza gypsum toka kwa Bwana Hamisi Juma meneja kiwanda cha Dangote.
Eneo ya fukwe ya Mnazibay Mjini Mtwara inavyooneka kuathirika na athari za mabadiliko ya tabia nchi yaliyosababisha sunami mwaka 2015 February..Naibu Waziri Mpina Alitembelea eneo hilo kujionea athari za mabadiliko ya tabia nchi.(Picha na Evelyn Mkokoi)

Serikali kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limekitoza faini ya shilingi milioni 15, Kiwanda maarufu cha kutengeneza simenti cha Dagonte Industry limited kilichopo mjini Mtwara kusini mwa Tanzania, kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.

Katika siku ya Pili ya Ziara ya ziara ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Mkoani Mtwara Imebainika kuwa kiwanda hicho cha Dangote chenye muda wa miezi mitatu tangu kianze kazi ya kutengenza siment, kimefanya uchafuzi wa mazingira kwa kukosa sehemu maalum ya kuhifadhi taka katika kiwanda hicho.
 
Kutokuwa na utaratibu mzuri wa kuhifadhi taka zitokanazo na makaa ya mawe kiwandani hapo, kukosa vyoo kwa ajili ya matumizi ya wateja wao ambao ni madereva na makondakta wanao chukua mzigo wa siment kiwandani hapo, na kusafirisha kwenda sehemu mbali mbali za nchi, pamoja na kutokusakafia sehemu ya nje ya kiwanda hicho ambapo imeelezwa kuwa eneo hilo la nje wakati wa kipindi cha mvua mazingira yake huatarisha afya ya watumiaji wa eneo hilo.

Kwa Mujibu wa Naibu waziri Mpina, adhabu hiyo kwa kiwanda cha Dangote inayotakiwa kulipwa ndani ya wiki mbili, inaenda sambamba na urekebishaji wa kasoro hizo kiwandani hapo pamoja na kuhamsha uongozi wa kiwanda hicho kwa kudharau sheria ya mazingira, na kutaka kiwanda hicho kuajiri afisa mazingira ataeshughulia changamoto hizo.

Kwa upande wake Meneja utumishi na utawala wa kiwanda hicho Bw. James Kajeli aliomba serikali kusamehe adhabu hiyo kwani kiwanda kilikuwa kwenye mpango wa kufanya marekebisho hayo na kuongeza kuwa kutokufanya hivyo kwa wakati ni kujisahau kwa kibinadamu, na kuwa utengenezaji wa baadhi ya miundombimu kiwandani hapo ulicheleweshwa na upatikani wa baadhi ya vibali kutoka katika taasisi za serikali na si kudharau sheria ya mazingira.

Naibu waziri Mpina Pia alitembelea kiwanda cha kutengeneza gas cha Madiba na kukisifu kwa utekelezaji wa sheria za mazingira na kuviasa viwanda vya serikali, kuwa mfano katika kutii sheria za mazingira.Ziara ya Mhe. Mpina pia ilihisisha ukaguzi wa kiwanda cha kubangua korosho cha micro mix cha mjini Mtwara, kiwanda cha gas cha Solvochemi pamoja na fukwe ya mnazi bay iliyoathiriwa na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

Mahumi Mdogo - Tanzania (Official Video )

Wafanyakazi Muhimbili Waongeza Mapato Hadi Kufikia Sh 4.8 Bilioni

$
0
0

Na John Stephen, MNH .

Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imefanikiwa kuongeza mapato kutoka Sh 2.3 bilioni yaliyokuwa yakikusanywa Desemba mwaka jana hadi kufikia Sh 4.8 bilioni Mei mwaka huu. 

Hayo yamesemwa LEO na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru wakati hafla ya kutunuku vyeti kwa wafanyakazi bora wa hospitali hiyo.
Hospitali hiyo imefanikiwa kuongeza mapato kutokana na juhudi za wafanyakazi ambao wanafanya kazi kwa ari kubwa ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa. 
 
Pia, wafanyakazi wamehamasika kutokana na mkurugenzi huyo kuwajali wafanyakazi na kusikiliza kero na kuzitatua kwa wakati kwa mfano hivi karibuni alilipa malimbikizo ya wafanyakazi. Profesa Museru amesema mapato hayo yameongezeka kutokana na juhudi za wafanyakazi ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii na hivyo kusababisha mapato hayo kufikia Sh 4.8 bilioni. 

“Mafanikio haya yametokana na juhudi za wafanyakazi. Mwaka jana niliwaomba wafanyakazi wafanye kazi kwa bidii, na wao walikubali. Imani yangu ni kwamba posho kwa wafanyakazi wangu zitaanza kulipwa baada ya bodi kupitisha ombi la kuwaongezea. Nafikiri tukiwaeleza vizuri bodi watatuelewa na hivyo wafanyakazi watapata kile tulichowaahidi,” amesema Profesa Museru. 

Mkurugenzi huyo amesema kwamba hospitali imepata mafanikio makubwa yakiwamo kuongeza huduma za afya kwa mfano kuanzishwa kwa huduma ya kusafisha figo, kuongeza wodi kwa wagonjwa wanaohitaji uangali maalumu, huduma za matumbo na kuboreshwa kwa mazingira ya kutolea huduma. 

Amesema hospitali hiyo inajitahidi kuongeza mapato zaidi ili iweze kulipia huduma za umeme, huduma za simu, ankra za maji pamoja na kudi za majengo.
“Sisi hatufanyi biashara bali tunatoa huduma kwa wagonjwa, tunapaswa kuongeza mapato ili kulipia huduma kutoka kwa washirika wetu akiwamo Tanesco, kulipia maji na huduma za simu,” amesema Kaimu Mkurugenzi huyo. 

Akizungumzia changamoto, Profesa Museru amesema sehemu zinazotumika kutoa huduma zinatakiwa kukarabatiwa. Amesema miundombinu inapaswa kukarabatiwa kwa kuwa imekuwa ikichakaa kutokana na kuongezeka kwa wagonjwa hospitali hapo.
“ Majengo ya hospitali hayajakarabatiwa karibu miaka 20, hivyo tunapaswa kukarabati sasa,” amesema. 

Pia Profesa Museru amewapongeza wafanyakazi bora ambao wametunukiwa vyeti baada ya kuibuka kuwa wafanyakazi bora. 

Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza katika hafla ya kuwatunukia vyeti wafanyakazi bora 54. Hafla hiyo imefanyika katika hospitali hiyo. Wafanyakazi wa hospitali hiyo wakiwamo madaktari na wauguzi wakimsikiliza Profesa Museru Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Muhimbili, Mziwanda Chimwege akisoma risala kwa mgeni rasmi, Profesa Museru katika hafla ya kuwakabidhi vyeti wafanyakazi bora Wafanyakazi wa hospitali hiyo wakimsikiliza Mwenyekiti wa TUGHE, Mziwanda Chimwege.
William Chimwege wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Hospitali hiyo, akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Uuguzi, Agness Mtawa baada ya kuchaguliwa kuwa mfanyakazi bora. Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru akimkabidhi cheti mfanyakazi wa Idara ya Ajira na Mafunzo, Farisha Jumanne baada ya kuchaguliwa kuwa mfanyakazi bora. Wafanyakazi wa Muhimbili wakiserebuka baada ya wafanyakazi bora kutunukiwa vyeti. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)  

Mtanzania mkazi wa UK Karrima Carter na wahisani wenzie kutoka Norwich watoa misaada Tanzania

$
0
0


Kundi la watoto yatima wanaotunzwa na Karrima na wahisani wenzake Waingereza kutoka Norwich hapa Uingereza
Baadhi ya wahisani kutoka Norwich wakiwa katika halfa ya utoaji misaada kwa kituo cha kulea yatima, Bagamoyo


Mwanadada wa Kitanzania, Karrima Carter, mwenye makazi yake Norwich, hapa Uingereza, wiki hii ameshirikiana na wahisani wenzake kutoka Uingereza kutoa misaada kwenye kituo cha kulelea watoto yatima huko Bagamoyo na uzinduzi wa vyoo vilivyokarabatiwa kwa uhisani wa dada huyo na wahisani wenzake kutoka Uingereza.

Tukio la kwanza lilifanyika Jumapili iliyopita na kuhudhuriwa na baadhi ya wasanii mbalimbali kama vile Gabo na Faiza Ally (ambao walialikwa rasmi kwa minajili ya kuwapa tabasamu watoto yatima), na tukio la pili lilifanyika Jumatatu iliyopita.

Picha na maelezo ya tukio la tatu la kukabidhi madawati zitawajia kesho. Awali, Karrima alisita kuhusu wazo la ku-blogu kuhusu matukio haya akisema kwamba asingependa 'publicity' lakini mie binafsi nilimshauri kuwa kuweka hadharani habari hizi kunaweza kusaidia kuwahamasisha Watanzania kuhusu utamaduni wa kutoa misaada kwa wenzetu wenye uhitaji, eneo ambalo ni maarufu hapa Uingereza lakini ni geni kwa nchi nyingi za Afrika.

Karrima amekuwa akijibidiisha katika sekta hiyo ya misaada kwa wenye uhitaji kwa kitambo sasa. na amekuwa akipata ushirikiano mkubwa kwa wakazi wenzie wa Norwich.

Karrima n wahisani wenzake kutoka Norwich, uingereza, mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwa hafla mbalimbali za utoaji misaada

Hafla ya kuzindua vyoo katika Shule ya Msingi Ilala, ambavyo vilifanyiwa ukarabati kwa uhisani wa Karrima na wenzie kutoka Norwich, Uingereza

Karrima na wahisani wenzie kutoka Norwich wakiwa shuleni Ilala
Mmoja wa wahisani kutoka Norwich akisaini kitabu cha wageni
Karrima akisalimiana na mmoja wa wadau
Karrima akisalimiana na walimu
Moja ya vyoo vilivyofanyiwa ukarabati
Ukitoa 'viboko' na ugumu wa masomo, moja ya vitu vinavyowafanya wanafunzi wengi wachukie shule, hasa za msingi, ni vyoo visivyofaa kwa matumizi ya binadamu. Bila shaka jitihada hizi za Karrima zitahamasisha Watanzania wengi zaidi kujitokeza katika ufadhili wa taasisi zetu.

Hafla ya utoaji misaada kwa kituo cha kulea yatima huo Bagamoyo
Karrima, Gabo, Faiza na mmoja wa wahusika wa kituo cha kulea yatima Bagamoyo

Faiza, mmoja wa walioshiriki katika maandalizi ya hafla hiyo huko Bagamoyo
Msanii maarufu wa Bongo Movies, Gabo, naye allijumuika katika hafla hiyo. Pembeni yake ni mmoja wa wahisani kutoka Norwich.
Gabo akiwaburudisha watoto yatima
Karimma akitoa hutuba katika hafla hiyo
Nathani Mpangala, mmoja wa walioshiriki katika maandalizi ya hafla hiyo
Mmoja wa wahisani kutoka Norwich akijiandaa kupata msosi

WAKURUGENZI MKOANI SIMIYU WAAGIZWA KUTENGA BAJETI ZA MAAFISA KILIMO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka akizungumza na Viongozi  na Maafisa Kilimo wa mkoa huo(hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu, (kushoto) Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Bw. Donatus A. Weginah .
Wakuu wa Wilaya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa(hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu, (kutoka  kushoto), Mhe. Tano Mwera (Busega),Mhe. Joseph Chilongani(Meatu), Mhe. Benson Kilangi (Itilima ) na Mhe. Seif Shekalaghe.Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa waSimiyu, Ndg. Jeremia Shigala akichangia katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu .
Viongozi na Maafisa kilimo wa Mkoa wa Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Anthony J. Mtaka (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu.

Na Stella Kalinga (Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu)

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kutenga bajeti kwa ajili ya kuwawezesha  Maafisa kilimo wa Vijiji,Kata na Wilaya kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Mtaka ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi na Maafisa Kilimo katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ambacho kilihudhuriwa na Wakuu wa wilaya,Wenyeviti wa Halmashauri,Wakurugenzi na Makatibu Tawala Wilaya kutoka katika wilaya zote tano za mkoa huo.

Mtaka amesema Maafisa Kilimo wanapaswa kuwezeshwa kwa kupewa vyombo vya usafiri kama pikipiki na magari pamoja na mafuta, ili waweze kuwafikia wakulima katika maeneo yao kwa ajili ya kuwapa ushauri wa kitaalam kila wanapowahitaji katika kuendeleza kilimo bora na chenye tija.

“Mwaka huu kilimo kwa mkoa wetu ni kipaumbele cha pili na Halmashauri za Mkoa huu zinategemea kilimo kwa takribani asilimia 90 ya mapato yake ya ndani, ipo haja kuwawezesha maafisa kilimo kwa kuwa wana mchango kubwa katika mapato ya Halmashauri. Ningependa kuona mwaka 2016/2017 hadhi ya Maafisa Kilimo inapanda, Wakurugenzi muwathamini hawa wataalam ndiyo wanaowasaidia kupata hayo mapato katika pamba, choroko, dengu, mpunga na mazao mengine”, alisema Mtaka.

Aidha, kufuatia makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na India yaliyofanywa hivi karibuni kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa India juu ya biashara ya mazao ya jamii ya mikunde kama choroko, dengu na mbaazi takribani tani milioni sita, Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu unayo fursa kubwa ya kuzalisha mazao haya kwa takribani asilimia 60 kama ilivyo katika zao la pamba, kwa kuwa kuna ardhi yenye rutuba na wananchi wanalima mazao hayo.

AfDB YAAHIDI KUENDELEA KUIPIGA JEKI TANZANIA KUKUZA UCHUMI WAKE

$
0
0
Na Benny Mwaipaja,MoFP 

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Frannie Leautier, ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ambapo ameishukuru Benki hiyo kuwa mojawapo ya mashirika ya kimataifa yanayoisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali za maendeleo. 

Benki hiyo imewekeza hapa nchini kiasi cha dola Bilioni 2 sawa na zaidi ya shilingi Trilioni 4.4 kama ruzuku na mikopo yenye riba nafuu ili kuendeleza sekta mbalimbali ikiwemo barabara, elimu, kilimo, nishati ya umeme, na viwanda. 

Katika mazungumzo hayo Mhe. Dkt. Mpango, ameelezea kufurahishwa kwake na Dira ya AfDB ambayo inafanana na vipaumbele vya serikali, kupitia Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano ambao umelenga kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2025. 

Dira ya Benki hiyo imejikita katika malengo matano ambayo ni kuwekeza katika nishati ya umeme, uzalishaji wa chakula, kuendeleza viwanda, kuiunganisha Afrika kwa mtandao wa barabara na kuboresha maisha ya watu. 

Mhe. Dkt. Mpango, amesema kuwa uwekezaji katika sekta hizo utasaidia mpango mkubwa wa uboreshaji wa miundombinu kama vile kujenga viwanda kwa kuhusisha sekta ya umma na binafsi-PPP, umeme wa kutosha kuendesha viwanda, barabara ambazo zitaunganisha nchi zote za Afrika. 

“AfDB wametusaidia sana katika ujenzi wa barabara nyingi nchini Tanzania ikiwemo barabara ya kutoka Tanga kwenda Horohoro, ambayo imerahisisha usafiri wa kwenda nchini Kenya. Barabara nyingine zitajengwa kutoka mpakani Kagera kupitia Kigoma kwenda Katavi, Dodoma hadi Iringa. Hili ni jambo kubwa” Alisema Dkt. Mpango 
.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na Mwakilishi mkazi wa Benki hiyo Bi. Tonia Kandiero.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (kulia) akiwa kwenye majadiliano na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Frannie Leutier (katikati) na Mwakilishi mkazi wa Benki hiyo Bi. Tonia Kandiero.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akifafanua jambo mbele ya Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB ) Dkt. Frannie Leutier, kulia kwa Dkt. Leutier, ni Mwakilishi mkazi wa Benki hiyo Bi. Tonia Kandiero na watendaji wa Wizara.
Mwakilishi mkazi wa Benki hiyo Bi. Tonia Kandiero (wa kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango. Kutoka kushoto kwake ni Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB ) Dkt. Frannie Leutier, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja (anayeandika).

SIA PIUS AIBUKA NA TAJI LA MISS SINZA 2016

$
0
0

Windhoek Draught Miss Sinza 2016, Sia Pius (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Catherine Listoni (kushoto) na mshindi wa tatu Hafsa Mahamood baada ya kutangazwa mshindi Hoteli ya Defrance lilikofanyika shindano hilo jana usiku kwa udhamini wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd kupitia kinywaji wa Windhoek.

Warembo walioingia tano bora. Kutoka kulia ni Catherine Listone, Sia Pius, Hafsa Mahamood, Saida Khalifa na Faith Msuya.

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd, Benedicta Rugemalira (kushoto), akimkabidhi mshindi wa kwanza wa shindano hilo kitita cha sh.500,000.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd, Benedicta Rugemalira (kushoto), akimkabishi mshindi huyo moja ya katoni ya windhoek kati ya tano zilizotolewa na kampuni hiyo kwa mshindi huyo ambapo pia mshindi wa pili na watatu walikabidhiwa.

Na Dotto Mwaibale

KAMATI ya maandalizi ya shindano la Miss Sinza 2016 imemtangaza Sia Pius kuwa mshindi wa Windhoek Draught Miss Sinza 2016 baada ya kuibuka mshindi katika shindano lililofanyika Hoteli ya Defrance iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam jana usiku.

Pius aliibuka mshindi baada ya kuwabwaga washiriki wenzake tisa waliokuwa wakiwania taji hilo ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na Catherine Listoni huku ya tatu ikichukuliwa na Hafsa Mahamood.

Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spiritis kupitia bia ya Windhoek pamoja na wadhamini wengine.Mshindi wa kwanza wa shindano hilo alizawadiwa sh.500,000 wakati wa pili akijipatia sh.300,000 na watatu akiondoka na kitita cha sh.200,000 huku washiriki wengine wakiondoka na kifuta jasho cha sh.100,000 kila mmoja.

Washindi hao watatu wataingia moja kwa moja katika shindano la kumsaka Miss Kinondoni 2016 litakalofanyika mwezi ujao.

MWILI WA MAREHEMU JOSEPH SENGA WAWASILI DAR, KUAGWA KESHO VIWANJA VYA SINZA-UZURI

$
0
0

Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu tayari kwa safari ya kutoka uwanjani hapo kuelekea Muhimbili kuhifadhiwa.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, (watatu kushoto), mbunge wa Nsumve Richard Ndasa, (wanne kushoto) nabaadhi ya waaandishi na wapiga picha, wakilitama jeneza lenye mwikli wa hayati Joseph Senga, aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa gazetila Tanzania Daima, wakati wafanyakazi wa Swissport wakilitoa jeenza hilo kwenye uwanjawa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 30, 2016 ulipowasili kutoka nchini India. 
 
MarehemuSenga alifariki katikati ya wiki hii nchini India, alikokwenda kwa matibabu. Taarifaza ndugu wa marehemu kuhusu taratibu za mazishi zinasema, Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo Jumapili asubuhi utapelekwa nyumbani kwake Sinza, kwa ajili ya ibada fupi na kisha utapelekwa viwanja vya Sinza-Uzuri kwa wananchi ndugu jamaa na marafiki kuuuaga. Taarifa hiyo pia inasema, Mwili wa Marehemu utasafirishwa baada ya zoezi la kuuaga Jumapili Julai 31, 2016. (PICHA NA K0-VIS MEDIA/Khalfan Said) .

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kulia), akiteta jambona Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena, wakati wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu Joseph Senga, aliyekuwa mpiga picha mkuu wa gazeti hilo.

Waombolezaji wakisubiri mwaili kuwasili kutoka nchini India, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
 
Baadhi ya wapiga picha na waombolezaji wengine wakiondoka baada ya mwili kuwasili.

JUMUIYA YA KANGA MATERNITY TRUST YA ZANZIBAR YAFANYA SEMINA KWA WATAFITI WAZALENDO

$
0
0

Dkt. Mdhamin wa Kijiji cha Watoto (S.O.S) Zanzibar Abdulla Mohammed Hassan akimkabidhi Certificate Dkt. Natasha Hussein kwa niaba ya Jumuiya ya Kanga Maternity Trust kwa kazi nzuri waliyoifanya.
Baadhi ya walikwa katika Semina ya Jumuiya ya Kanga Maternity Trust. Picha na Makame Mshenga /Maelezo Zanzibar.

Daktari bingwa. Tarek Meguid wa wodi ya Wazazi Mnazimmoja Hospitali akitoa tarifa ya pili ya watafiti wazalendo kuhusu wajawazito na watoto katika Semina ya Jumuiya ya Kanga Maternity Trust iliyofanyika Tembo Hotel Mjini Zanzibar.
Dkt. wa Maradhi ya Saratani Mnazimmoja Hospital Salama Uledi Mwita akitoa taarifa ya hali yaugonjwa wa Saratani ulivyo sasa Zanzibar katika Semina ya Jumuiya ya Kanga Maternity Trust.
Madaktari bingwa wa Hospitali ya Mnazimmoja, (kulia) Dkt. Tarek Meguid na (kushoto) Dkt. Msafiri Marijani wakiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kanga Maternity Trust (KMT) wakatikati Dk. Mohammed Hafidh wakifuatilia uwasilishwaji wa Tafiti za ndani kwa madaktari wazalendo.
Dkt. Sanaa S. Said Phisician (Internal medicine) Mnazimmoja Hospital akiuliza swaali kwa watafiti wazalendo (hawapo pichani) katika Semina iliyofanyika Tembo Hotel Mjini Zanzibar.
Dkt. Msafiri Marijani akitoa ufafanuzi wa maswali yaliyoulizwa kuhusu ugonjwa wa Saratani (kushoto) Dkt. Salama Uledi Mwita ambae amewasilisha tafiti ya ugonjwa wa Saratani ulivyo Zanzibar. 
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images