Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 921 | 922 | (Page 923) | 924 | 925 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na wanamichezo kutoka mabenki mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikagua timu wa wachezaji wa Diamond Trust Bank (DTB) wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mratibu wa mashindano hayo kutoka Barclays Bi. Nasikia Berya
  Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimkabidhi naodha wa timu ya DTB ngao ya hisani kwa kuwafunga mabao matatu kwa moja timu ya Barclays wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Michezo Bw. Rashid Mijuza.
  Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati mwenye koti la bluu) katika picha ya pamoja na wachezaji kutoka Barclays wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam

  Waamuzi wa michezo ya Brazuka kibenki katika picha ya pamoja wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki leo Jijini Dar es Salaam.Picha na Genofeva Matemu – WHUSM

  ………………………………………………………………………………

  Na Lorietha Laurence-WHUSM

  Serikali kupitia sera ya Maendeleo ya Michezo inasisitiza wananchi na jamii kwa ujumla kushiriki katika michezo ili kujenga afya, kuunganisha watu toka makundi mbalimbali bila ubaguzi wa kidini, kisiasa, wala kiuchumi.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Kibenki maarufu kama Brazuka katika viwanja vya Gymkhana leo jijini Dar es Salaam.

  Mhe. Wambura ameeleza kuwa ni muhimu kwa wafanyakazi kujumuika kwa pamoja katika michezo ili kuboresha afya na kuimarisha uhusiano baina yao. “Michezo ni kitu kizuri kwani husaidia katika kuimarisha na kulinda afya zetu hivyo ni vyema kila mmoja wetu kushiriki katika michezo ili kuwa nguvu ya kutekeleza majukumu yetu ya kila siku” alisema Mhe. Wambura.

  Vilevile alitoa shukrani kwa wakuu wote wa mabenki kwa ushirikiano wao wa kuwaleta pamoja wafanyakazi wa benki ili kufahamiana na kuimarisha ushirikiano baina yao . Kwa upande wake Meneja Masoko wa Benki ya Barclays Bw. Aron Luhanga amesema kuwa dhumuni la mashindano hayo ni kuendeleza mahusiano baina ya benki kwa kufahamiana na kuimarisha afya na fikra zao.

  “mashindano haya ni kwa ajili ya kufahamiana na kuimarisha urafiki kwa wafanyakazi wa sekta ya benki kwa kufanya sekta ya kibenki kuwa sehemu bora ya shughuli za kiuchumi nchini” alisema Bw.Luhanga.

  Mashindano hayo ya Brazuka kibenki yanaratibiwa na benki ya Barclays na ni mara ya pili kufanyika nchini ambapo mwaka jana benki ya Diamond Trust (DTB) iliibuka mshindi hivyo kushiriki katika ufunguzi wa michuano hiyo mwaka huu.

  Benki zinazoshiriki mashindano hayo ni 18 ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania, NMB, Stanbic, KCB, Exim, Citi Benki, Commrcial Bank of Africa (BOA),CRDB, Letshego, Eco Bwnki, Akiba, Diamond Trust Benki, Bank of India, Banc ABC,Azania na Twiga Bancorp.

  0 0
  Jengo la Mahakama ya Mwanzo Kigamboni linalojengwa kwa kutumia Teknolojia ya Moladi.
  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Ferdinand Wambali akimsikiliza Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania, Khamadu Kitunzi akimwonyesha Ramani ya jengo la Mahakama ya Mwanzo Kigamboni linaloendelea kujengwa jana jijini Dar es Salaam. Jengo hilo linajengwa kwa kutumia teknolojia ya Moladi.

  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Joseph Emilio Senga na wanahabari wote nchini kufuatia kifo cha aliyekuwa mpiga picha mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima na mwanahabari mkongwe Joseph Emilio Senga kilichotokea tarehe 27 Julai, 2016 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.

  Katika salamu zake Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) amesema tasnia ya habari imempoteza mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya tasnia ya habari nchini.

  “Joseph Senga alikuwa mwanahabari shupavu na hodari, ambaye siku zote alisimama kidete kupigania maendeleo ya tasnia ya habari na kutenda haki katika tasnia hiyo.

  “Napenda kutoa salamu zangu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu” 

  Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) pia amewaombea wote walioguswa na kifo cha Joseph Emilio Senga kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki cha kuondokewa na mpendwa wao.

  RAHA YA MILELE UMPE EHE BWANA, NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE 

  APUMZIKE KWA AMANI

  AMINA.

  0 0

  BUNG1BUNG2

  0 0


  Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambae pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula (katikati), jana amefanya ziara ya kukagua Ukarabati wa Miundombinu ya barabara, mitaro na madaraja katika Kata ya Kirumba Jimboni humo ikiwa ni mwanzo wa ziara zake katika Kata zote za Manispaa ya Ilemela ili kujionea namna ukarabati wa mbiundombinu ya barabara unavyoendelea.

  Kulia ni Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela, Mikidadi Adam, akitoa taarifa ya ukarabati wa miundombinu katika Kata ya Kirumba ambapo alibainisha kwamba zaidi ya Shilingi Milioni 195 zimetengwa kwa ajili ya Kata hiyo ili kukarabati barabara zake ambazo ziliharibika kutokana na mvua ambapo miongoni mwa barabara zinazokarabatiwa katika Kata ya Kirumba ni barabara ya Villa, Kabuhoro, CWT-Sabatho.
  Na BMG

  Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (wa nne kulia), akiwa katika ziara ya kukagua ukarabati wa mbiundo mbinu katika Kata ya Kirumba Jimboni humo.

  Mitaro katika barabara ya Villa inaendelea kukarabatiwa ili kuondoa adha ambayo huwa inajitokeza wakati wa mvua na kusababisha adha kubwa kwa wananchi.

  Hii ni barabara ya CWT-Sabatho, awali ilikuwa haitamaniki kwani ilikuwa ni mashimo tupu. Lakini sasa inapitika vyema na kilichosalia ni ukarabati wa mitaro ili mvua ikinyesha isiweze kusababisha uharibifu wa ukarabati huu.

  Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (wa tatu kulia), akiwa katika ziara ya kukagua ukarabati wa mbiundo mbinu katika Kata ya Kirumba Jimboni humo.

  Namna miundombinu ya barabara na mitaro inavyoendelea kukarabatiwa katika Kata ya Kirumba, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

  Ukaguzi wa miundombinu ya barabara na mitaro inavyoendelea kukarabatiwa katika Kata ya Kirumba, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

  Pia kuna ujenzi wa daraja katika barabara ya Kabuhoro Ziwani ambapo kulikuwa na adha kubwa kwa wananchi ambapo ukarabati huu unaleta ahueni kwa wakazi wa eneo hio pamoja na watumiaji wengine wa barabara.

  Aliagiza ukarabati wa mbiundombinu ya barabara kukamilika haraka kabla msimu wa mvua haujaanza na kwamba Manispaa ya Ilemela imetenga Shilingi Milioni 625 ikiwa ni fedha za mfuko wa dharura na shilingi Milioni 146 ambazo ni fedha za mfuko wa barabara, fedha zote ikiwa ni kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara.

  Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (mwenye miwani) akiteta kidogo na wakazi wa Kata ya Kirumba alipotembelea Kata hiyo ili kujionea ukarabati wa miundombinu ya barabara katika Kata hiyo.

  Katibu wa Mbunge, Heri James (mwenye kofia) ambapo alisema ofisi ya mbunge itahakikisha ahadi zilizotolewa na mbunge wakati wa kampeni zinatekelezwa ikiwemo suala la upatikanaji wa maji na ukarabati wa miundombinu.

  Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela, Mikidadi Adam, akitoa taarifa ya ukarabati wa miundombinu katika Kata ya Kirumba ambapo alibainisha kwamba zaidi ya Shilingi Milioni 195 zimetengwa kwa ajili ya Kata hiyo ili kukarabati barabara zake ambazo ziliharibika kutokana na mvua.

  Diwani wa Kata ya Kirumba, Alex Ngusa, ambapo alibainisha kwamba barabara za Kata hiyo zilikuwa zimeharibika sana kutokana na mvua zilizonyesha mwishoni mwanza mwaka jana.

  Alishukuru ushirikiano baina yake na wananchi wa Kata yake, ofisi ya mbunge pamoja na halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na kwamba juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika kuwafikishia wananchi maendeleo zimepokelewa vyema na wananchi huku akiwasihi kuitunza vyema miundombinu hiyo.

  Mmoja wa wakazi wa Kirumba akieleza adha waliyokuwa wakiipata wakazi wa Kata hiyo kabla ukarabati haujafanyika ambapo aliongeza kwamba ni vyema ukarabati huo ukaendelea kufanyika hususani katika ujenzi wa mitaro ili kuondoa adha ambayo huwa inajitokeza wakati wa mvua ikwemo kuharibu miundombinu ya barabara kutokana na kukosekana kwa mitaro.

  Mkazi wa Kirumba akitoa shukurani zake kwa ukarabati unaofanyika katika barabara za Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

  Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, imeanza ukarabati wa miundombinu ya barabara kwa kiwango cha changarawe pamoja na mikakati ya ujenzi wa baadhi ya barabara kwa kiwango cha lami.

  Akikagua zoezi la ukarabati wa miundombinu ya barabara katika Kata ya kirumba, Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Angelina Mabula, ametaka ukarabati wa miundombinu hiyo ikiwemo mitaro, kukamilika mapema kabla msimu wa mvua haujaanza ili kuepukana na athari za mvua.

  Amesema katika kipindi cha miaka mitano, hali ya miundo mbinu ya barabara katika jimbo  hilo itakuwa katika hali nzuri na hivyo kupunguza kero ya ubovu wa miundombinu
  ambayo imekuwepo kwa muda mrefu katika Manispaa ya Ilemela.

  Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela, Mikidadi Adam, amesema Manispaa hiyo imetenga shilingi Milioni 625 zilizotokana na fedha za mfuko wa dharura na barabara kwa ajili ya
  ukarabati wa miundombinu ya barabara katika manispaa hiyo japo amebainisha
  kwamba bado fedha hizo hazitoshi hivyo ni vyema serikali ikaendelea kutenga
  fedha zaidi kwa ajili ya kutekeleza ukarabari huo.

  Wakati ukarabati huo ukiendelea, diwani wa Kata ya Kirumba, Alex Ngusa, amewataka
  wananchi kutunza vyema mbiundombinu ya barabara inayoendelea kukarabatiwa ikiwa
  ni pamoja na kuacha tabia ya kutupa taka kwenye mitaro.

  Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kirumba, wamepongeza juhudi za ukarabati wa miundombinu ya barabara zinazofanyika katika Manispaa ya Ilemela na kuongeza kwamba ni vyema juhudi hizo zikandelea ili kumaliza kero zilizokuwepo awali.

  Mbunge wa Jimbo la Ilemela, yuko katika mwendelezo wa ziara katika Kata zote 19 za
  Manispaa ya Ilemela ili kujionea ukarabati wa Miundombinu ya barabara ambayo ni
  pamoja na ujenzi wa mitaro na madaraja ambao unaelezwa kuleta ahueni kwa
  wananchi wa Manispaa hiy ikizingatiwa kwamba awali hali ya miundombinu ya
  barabara awali haikuwa ya kuridhisha.

  0 0

   
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 30 Julai, 2016 ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Tabora akitokea Mkoa wa Singida.

  Kabla ya kuingia Mkoani Tabora, Rais Magufuli amezungumza na wananchi wa Mji wa Misigiri katika Wilaya ya Iramba ambapo amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara katika Mkoa wa Singida kuhakikisha mkandarasi anayejenga daraja la Sibiti anarejea kazini mara moja kukamilisha ujenzi wa daraja hilo.

  Rais Magufuli amesema serikali yake imejipanga kumlipa fedha mkandarasi huyo na hivyo hakuna sababu ya kuendelea kusimamisha ujenzi huo.Mkoani Tabora, Rais Magufuli amezungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika vijiji vya Nanga na Ziba na amefanya mikutano ya hadhara katika miji ya Igunga na Nzega ambako amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake itahakikisha inatekeleza ahadi zilizopo katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2015.

  Katika mkutano wa hadhara uliofanyika Igunga, Rais Magufuli amepokea malalamiko ya wananchi kuhusu kutoanza kutumika kwa kituo cha mabasi na soko na amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha kituo cha mabasi cha Igunga na soko la Igunga vinaanza kutumika kuanzia Jumatatu ijayo ya tarehe 01 Agosti, 2016.

  Kuhusu kero ya maji, Dkt. Magufuli amesema Tanzania imepata mkopo wa dola za kimarekani Milioni 268.35 kutoka nchini India ambazo zitatumika kutekeleza mradi wa kusambaza maji ya ziwa Viktoria katika Miji ya Tabora, Igunga, Nzega, Sikonge na Uyui pamoja na vijiji vilivyopo kandokando mwa bomba kuu kuanzia mwaka huu ambapo watu milioni moja na laki moja (1,100,000) watanufaika.

  Dkt. Magufuli ameongeza kuwa pamoja na juhudi hizo Serikali imefanya usanifu na upembuzi yakinifu kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kusambaza maji ya kutoka mto Malagarasi kwa ajili ya Miji ya Urambo, Kaliua na Nguruka pamoja na vijiji vilivyopo kandokando mwa bomba kuu ambako watu laki sita (600,000) watanufaika.

  Aidha, Rais Magufuli amepiga marufuku wakulima wadogo kutozwa ushuru wa mazao watokapo na mazao mashambani.

  "Ninapenda tukusanye kodi, lakini sio kukusanya kodi kutoka kwa watu masikini, mtu ametoka shambani na magunia yake mawili au hata matano halafu nyinyi mnamtoza kodi."Mimi sipendi kuwanyanyasa hawa watu wanyonge, mtu akiwa na mazao lori zima hapo sawa lakini sio kwa mtu mnyonge mwenye gunia moja" Amesema Rais Magufuli.

  Kuhusu maombi ya Mkoa wa Tabora kutaka kuanzishwa Mkoa mwingine kutokana na ukubwa wa baadhi ya Wilaya Rais Magufuli amesema haioni umuhimu wa kuanzisha Mikoa mipya hapa nchini kwa sasa, na badala yake fedha zitaelekezwa katika huduma kwa wananchi kama vile maji, barabara, miundombinu na huduma za afya.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Nzega
  30 Julai, 2016 


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wakazi wa Igunga mkoani Tabora katika ziara yake ya kikazi katika Mkoa huo wa Tabora.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Igunga mkoani Tabora mara baada ya kuwahutubia Wilayani hapo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Igunga mkoani Tabora mara baada ya kuwahutubia Wilayani hapo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nanga Wilaya ya Igunga Ndugu Masesa Kishiwa Makala kutoka Chadema wakati akiwa safarini kuelekea Nzega Mkoani Tabora.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Ziba Wilayani Igunga mkoani Tabora hawaonekani pichani wakati akielekea Nzega Mkoani Tabora.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na wabunge wa Mkoa wa Singida wakati akiwahutubia wakazi wa Misigiri Mkoani Singida wakati akiwa njiani kuelekea Mkoani Tabora.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wakazi wa Misigiri Mkoani Singida. PICHA NA IKULU

  0 0
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akiongoza viongozi wa Manispaa ya Ilala kuweka vifaa vya usafi barabara ya Kivukoni.DC Mjema na viongozi wengine wa wilaya hiyo wanatekeleza agizo la Rais John Magufuli la kufanya usafi kila ifikapo Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema (katikati akiwa na baadhi ya viongozi wa Manispaa ya Ilala .Pichani kushoto ni Mkurugenzi wilaya ya Ilala Ndugu Msongela Palela pamoja na Katibu Tarafa Ndugu Edward Mpogoro kuweka vifaa vya usafi barabara ya KivukoniDC Sphia Mjea akielekeza jambo wakati wa kuweka vifaa vya usafi barabara ya kivukoni mapema leo,jijini Dar


  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwa, akitoa maelekezo kwa wakazi wa wilaya hiyo waliojitokeza kushiriki kazi za usafi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kufanya usafi kila ifikapo Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
  Mbunge wa Kigamboni Faustine Ndugulile (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya hiyo,Hashim Mgandilwa (wapili kulia) wakishiriki kazi za usafi eneo la Feri Kigamboni jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kufanya usafi kila ifikapo Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

  Mmoja ya watoto waliojitokeza kwenye kazi hiyo ya kufanya usafi.
  Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira Wilaya ya Kigamboni, Fanuel Kipesha akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kazi ya usafi kukamilika.

  Baadhi ya washiriki wa kazi ya usafi walichoma moto takataka laini.

  Baadhi ya askari wa vikosi mbalimbali walishiriki kazi hiyo ya usafi huku wakiwa wamevalia sare tofauti tofauti.  Gari Maalum kwaajili ya kubeba taka ngumu lilikuwepo na kazi hiyo ilifanyika.

  0 0

   Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo akielezea changamoto za Stendi ya Mbasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabiri wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016. Mkuu huyo wa wilaya ambaye ana mwezi mmoja toka aanze kazi alimweleza Rais kwamba kuanza kwa stendi ya basi kunasubiri kibali kutoka SUMATRA na kwamba soko jipya ambalo limeshamalizika kujengwa halitumiki kwa sababu ya mkanganyiko unaohusu badhi ya wafanyabishara kuhodhi sehemu kubwa ya soko jipya na kutolitumia huku wakiendelea kufanya bishara kwenye soko la zamani ambako nako pia wana sehemu za Biashara.
    Rais  Dkt Magufuli akiendelea kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo wakati akielezea changamoto za Stendi ya Mbasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabili wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016
    Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo akiandika maagizo ya Rais Dkt. Magufuli kuhusiana na  Stendi ya Mbasi ya abiria na Soko ambapo ameamuru huduma hizo zifunguliwe Jumatatu bila kukosa. Rais ameitaka SUMATRA ihakikishe stendi hiyo inaanza kufanya kazi Jumatatu. Pia ameiagiza halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha wafanyabishara waliohodhi sehemu za biashara bila kuzitumia katika soko jipya wathibitiwe mara moja.
   Wananchi wa Igunga wanalipuka kwa furaha na Mzee huyu anatoa  noti ya shilingi 10,000/- akitaka kumtuza  Rais Dkt Magufuli kwa kuweza kutatua changamoto za Stendi ya mabasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabiri wilaya ya Igunga wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016
  Rais Dkt Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipokea zawadi ya mchele wa grade One kutoka uongozi wa wilaya ya Igunga  wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016

  0 0

   Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Joseph Senga likiwa katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri jijini Dar es salaam wakati wakimuaga kwenda Kwimba, Mwanza kwa Maziko. Mwili wa Marehemu Joseph Senga unatarajiwa kuzikwa mara baada ya kufika. 
   Jeneza la Mwili wa Joseph Senga likipewa heshima ya mwisho.
   Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.
   Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.
   Baadhi ya Wapiga Picha wa Vyombo mbalimbali vya Habari nchini, wakibeba Jeneza la Marehemu Joseph Senga wakati wakilipeleka kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda Kwimba, Jijini Mwanza kwa Mazishi.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) akijadiliana jambo na Mbunge wa jimbo la Ubungo Mh.Saed Kubenea mara ya kuaga mwili wa Marehemu Senga,katika viwanja vya Sinza-Uzuro jijini Dar leo,pichani Kati ni aliyewahi kuwa Mgombea Urais wa UKAWA kupitia chama cha CHADEMA (2015) na Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa.


  0 0


  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na jamii wa wavuvi wa Mto Koga, Wilayani Skonge ikiwa na hatua ya kusuluhisha mgogoro kati yao na muwekezaji, Muhsin Abdllah "Shein" ambaye ni Mkurugenzi wa Northern Hunting. Eng. Makani aliwataka viongozi wa Wilaya na Halmashauri kukaa pamoja na muwekezaji huyo na wadau mbaimbali kwa ajili ya kamaliza mgogoro huo. Aliwata viongozi hao kuangaliwa upya vibali vinavyotolewa kwa wavuvi hao ili idadi yake ilingane na ukubwa na mahitaji ya Mto huo.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kulia) akisikiliza malalamiko kutoka kwa muwekezaji ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Northern Hunting, Muhsin Abdallah (kushoto) aliyewekeza katika kitalu cha uwindaji kwenye Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Ipole Wilayani Skonge.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ipembampazi, Wilayani Skonge Tabora. Wananchi hao wameiomba Serikali iwamegee eneo la hifadhi kwa ajili mradi wa kilimo cha umwagiliaji, Uluwa, Hifadhi ya Msitu ambao upo chini ya Halmashauri ya Wilaya Kaliua. Eng. Makani alitoa maelekezo mbalimbali kwa Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya na Mkoa ikiwa ni pamoja kuangalia taratibu za kisheria na kimazingira juu ya uwezekano wa ombi hilo na kuliwasilisha Wizarani kwa ajili ya hatua zaidi. (Picha na Hamza Temba - WMU -


  Naibu Waziri wa Maliasili, Eng. Ramo Makani akizungumza na baadhi ya wananchi waliovamia Msitu wa Hifadhi wa Wembere Wilayani Igunga hivi karibuni. Aliwataka wananchi hao kutii sheria za nchi na kusubiri maelekezo ya Serikali ambapo aliwaagiza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya Igunga na Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) kukusanya taarifa mbalimbali zinazohusu hifadhi hiyo na vijiji jirani ambapo zitatumika kumaliza mgogoro huo.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na wananchi wa waliovamia Msitu wa Wembere na kuweka makazi, Wilayani Igunga hivi karibuni. Alitoa maelekezo mbali kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya na Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania kwa ajili ya kukabili changamoto zilizopo katika hifadhi hiyo.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Igunga pamoja na viongozi wengine kutoka Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA).


  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa pili kushoto) akikagua maeneo ya Hifadhi ya Msitu wa Isawima Wilayani Kaliua hivi karibuni. Hifadhi hiyo ambayo imetengwa na vijiji 11 kwa ajili ya kuanzishwa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Isawima umevamiwa na wananchi kutoka maeneo ya nje ya vijiji hivyo na kuweka makazi, mifugo na kilimo jambo lililoikwamisha jumuiya hiyo kupewa kibali cha kurasimishwa na Wizara ya Maliasili na Utalii. Eng. Makani alitoa maelekezo kwa uongozi wa Wilaya ya Kaliua na Halmashauri kutumia mamlaka ya kisheria waliyo nayo kuwahamisha wavamizi hao ili jumuiya hiyo iweze kuanzishwa.
  Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mtapenda, Wilayani Kaliua wakiwa kwenye Mkutano wa Hadhara wa Naibu Waziri wa Maliasili, Eng. Ramo Makani.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mtapenda, Wilayani Kaliua alipotembelea kuona changamoto wa Uhifadhi na kuweka utaratibu wa kuzikabili.
  Mmoja wa wananchi waliovamia Hifadhi ya Isawima, Kaliua, Charles Msinda (kulia) akiiomba Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Maliasili, Eng. Ramo Makani (wa pili kulia) iwafikirie kuwapa maeneo mbadala baada ya kuondoka katika Hifadhi ya Msitu huo.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (katikati) akizungumza na viongozi wa Chama (CCM) na Serikali Wilayani Skonge. Kulia kwake ni mkuu wa Wilaya hiyo, Peres Boniface.


  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambapo alifanya ziara ya kikazi ya siku nne na kutembelea maeneo mbalimbali ya hifadhi ya Hifadhi ya Misitu na Wanyamapori yenye migogoro. Maeneo hayo ni Hifadhi ya Msitu wa Wembere (Wilaya ya Igunga), Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Isawima (Wilaya ya Kaliua), Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Ipole (Wilaya ya Skonge), Msitu wa Hifadhi wa Ipembampazi (Wilaya ya Skonge) na Msitu wa hifadhi wa Ilomero (Wilaya ya Nzega).

  0 0


  Mgeni rasmi kutoka Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania, Bishop Dr Kameta (katikati) akizungumza na wanachama wa Shirika la kidini linalotoa huduma kwa makanisa na mashirika yanayofanya kazi ya kueneza injili ulimwenguni lijulikanalo kama SINAI MISSIONS INTERNATIONAL(SMI) wakati wa mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika jijini Dar es Salaam Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kupeana taarifa za utendaji wa SMI na kila huduma chini ya mwavuli wa SMI. kulia ni Rais wa shirika hilo Ing.Bishop Piter M.Sanga.na kushoto Katibu Mkuu anaemaliza muda wake Bishop Pite W.Chinyama kutoka Zambia.na Mweka Hazina anayemaliza muda wake Msh Raphael Muhagama kutoka Tanzania.
  Viongozi wakimtukuza Mungu kwa wimbo wa pambio wakati wa mkutano mkuu wa mwaka kupeana taarifa za utendaji wa SMI na kila huduma chini ya mwavuli wa SMI.
  Wajumbe wa mkutano wakimtukuza Mungu kwa wimbo wa pambio.
  Wajumbe wa mkutano mkuu wakimtukuza Mungu kwa wimbo wa pambio wakati wa mkutano mkuu wa mwaka kupeana taarifa za utendaji wa SMI na kila huduma chini ya mwavuli wa SMI.
  Mgeni Rasmi kutoka Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Bishop Dr Kameta (kushoto), pamoja na Mtafisiri ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Shirika la MSI, Bishop Gilibert Biyengo.wakihutubia Mkutano Mkuu wa Mwaka.
  Mgeni rasmi kutoka Baraza la Makanisa ya Kipentekosite, Bishop Dr Kameta (kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa SINAI MISSIONS INTERNATIONAL(SMI) uliofanyika jijini Dar es Salaam kwaajili ya kupeana taarifa za utendaji wa SMI na kila huduma chini ya mwavuli wa SMI.

  Wajumbe wa Mkutano.
  Mkutano ukiendelea.
  Wajumbe wa mkutano mkuu wa mwaka wakifuatilia mada mbalimbali.

  PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG

  0 0


  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb) amezitaka Radio za jamii kuhamasisha usafiri wa mazingira nchini. Naibu Waziri Mpina ametoa kauli hiyo alipokuwa akishiriki siku ya usafi kitaifa, mwishoni mwa wiki wilayani Masasi Mkoani Mtwara.

  Akitolea Mfano wa Radio Pride FM ya Mjini Mtwara yenye kupatikana katika frequencies 87.8 mjini Mtwara, ambayo imeanzisha kampeni ya usafi katika mkoa wa mtwara na wilaya zake kwa kufanya vipindi vya moja kwa moja na kutembelea wilaya za mkoa huo kufanya usafi wa mazingira kwa vitendo.

  Kwa Upande wake Bw. JUma Andrea Manager uzalishaji wa kituo hicho cha Radio, alisema kuwa lengo kubwa la kituo hicho kuhamasiha usafi ni kuunga mkono agizo la Mhe. Rais kwa kuwaweka pamoja wananchi, kuweka muamko na hamasa ili kujenga tabia ya kupenda usafi na kuepukana na magonjwa yatokanayo na uchafu akitolea mfano ugonjwa wa homa ya matumbo na kipindipindu.


  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (katikati) akiangalia samaki katika soko ya wilaya ya Masasi akiwa katika ziara yake ya usafi na ukaguzi wa mazingira mjini Masasi, (kilia) ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bw. Selemani Mzee.
  Aliyeinama katikati akikusanya uchafu ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akishiriki katika zoezi la usafi wa mazingira Wilayani Masasi mwishoni mwa wiki.
  Bw. Benjamini Elias (kulia) Afisa Afya wa Halmashauri ya Mji wa Masasi akitoa taarifa na maelezo ya hali ya usafi wa soko la mji wa Masasi kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina (kushoto), wakati wa ukaguzi wa usafi wa mazingira mjini Masasi. (PICHA NA EVELYN MKOKOI)   Akiongea na Uongozi wa Mkoa wa Mtwara katika majumuisho ya ziara yake Wilayani Masasi, Naibu Waziri Mpina aliwataka viongozi wa mkoa huo kuunda sheria ndogondogo za mazingira zitakazo watoza faini wananchi waharibifu wa mazingira mkoani humo, na kuwachukulia hatua za kisheria kulingana na hali ya wananchi ili waweze kujifunza na kujijengea tabia ya usafi.

  “Nimeona kuwa uchomaji moto misitu ovyo hapa kwenu umekithiri, uchomaji moto taka nao siyo njia nzuri ya uondoshwaji wa taka,hiyo kuwe na miondombinu rafiki kwa uondoshwaji wa taka, na kiongozi wa mkoa ambae hatakuwa tayari kushughulikia usafi wa mazingira na yeye awe tayari kushughulikiwa alisisitiza.”

  Ziara ya Naibu Waziri Mpina Mkoani Mtwara ni muendelezo wa Ziara zake nchini za ukaguzi wa viwanda na usafi wa mazingira iliyohusisha pia ukaguzi wa machinjio ya mji wa Masasi.

  0 0

  J1 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Mkoani Tabora Mhashamu Paulo Ruzoka  mara baada ya Kuwasili Nzega mkoani Tabora jana kwa ajili ya ziara ya kikazi.
  J2 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Tabora Al-Haji Ramadhani Rashid katika viwanja vya  Stendi ya Nzega kabla ya kuhutubia mamia ya wakazi wa Nzega.
  J3J4 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia  mamia ya wananchi katika viwanja vya Stendi ya Nzega wa mkoani Tabora jana.
  PICHA NA IKULU

  0 0

  Na. Benedict Liwenga-WHUSM.

  Wadau wanaojishughulisha na masuala ya Sanaa nchini wamehamishwa kujitokeza kwa wingi katika kusaidia maendeleo ya Sanaa kwa kudhamini na kufadhili mashindano ya urembo bila kubagua.

  Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Francis Songoro wakati alipokuwa akiwasilisha hotuba ya Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Anastazia Wambura ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika Mashindano ya Miss Tanzania Indian Ocean 2016 yaliyofanyika katika Ukumbi wa MRC uliopo Mikocheni jijini hapa.

  Akiwasilisha hotuba hiyo, Songoro amesema kwamba kazi inayofanywa na wadau wa sanaa ni hatua ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Utamaduni ambayo inasisitiza jamii na wakuzaji sanaa kuendeleza ubunifu katika kazi za kiutamaduni.

  Ameeleza kuwa, Serikali kupitia Wizara yake inathamini na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wadau hao hasa katika kukuza na kuviendeleza vipaji vya vijana nchini, hivyo amewapongeza wadau hao kwa moyo wao wa kujitoa na kuwataka kuendeleza kwa vitendo Sera ya Taifa ya Utamaduni ya mwaka 1997 katika Sura ya 9 kifungu cha 9:5:8 ambacho kinasisitiza na kuhimiza watu binafsi pamoja na Mashirika kuwekeza rasilimali katika sekta ya utamaduni.


  Miss Dar Indian Ocean aliyemaliza muda wake, Camilla John (katikati) akimvisha skafu Mshindi wa Mashindano ya Miss Tanzania Indian Ocean 2016 Jackline Kimambo (kushoto) mara baada ya kuibuka mshindi katika mashindano hayo yaliyofanyika 30 Julai, 2016 katika Ukumbi wa MRC Ulioko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
  Miss Tanzania Indian Ocean 2016 Jackline Kimambo (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na warembo wenzie ambaye ni Mshindi wa pili na wa tatu mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yaliyofanyika 30 Julai, 2016 katika Ukumbi wa MRC Ulioko Mikocheni jijini Dar es Salaam.

  Kaimu Mkuregenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Francis Songoro (kulia) akimpongeza Miss Tanzania Indian Ocean 2016 Jackline Kimambo kwa kuibuka mshindi wa mashindano hayo baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yaliyofanyika 30 Julai, 2016 katika Ukumbi wa MRC Ulioko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
  Miss Tanzania Indian Ocean 2016 Jackline Kimambo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yaliyofanyika 30 Julai, 2016 katika Ukumbi wa MRC Ulioko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
  ‘’Maonyesho haya ni ishara tosha kuwa sanaa ni kazi, ajira, biashara na burudani, hivyo kipekee nawapongeza sana’’, alisema Songoro.

  Aliongeza kuwa, Warembo ambao wameshiriki katika mashindano hayo wanautangaza utalii wa ndani na nje ya nchi na kwa kufanya hivyo wanaiwakilisha vyema Tanzania Duniani katika mashindano ya Miss World na pia kukuza uchumi wa nchi.

  Aidha, amewataka warembo ambao hawakubahatika kuibuka washindi katika mashindano hayo kutokata tamaa, bali waitumie fursa hiyo hususani ya elimu waliyoipata wakiwa kambini kwa kuisadia jamii inayowazunguka na kuwa wanawake wa mfano wa kuigwa katika kujitambua na kujiamini.

  ‘’Mtambue kwamba, siyo wote mtakaoibuka washindi na kuendelea mbele katika mashindano haya, niwaombe wale ambao hamtashinda msivunjike moyo, bali mkaitumie elimu mliyoipata na yale ambayo mmejifunza mkiwa kambini kwa kuisaidia jamii inayowazunguka na muwe wanawake wa mfano wa kuigwa’’, alisema Songoro.

  Katika mashindano hayo, Mshindi wa Kwanza aliyeibuka na kunyakua taji hilo ni Jackline Kimambo ambaye alipatikana kati ya tano bora na kuvikwa taji la Miss Tanzania Indian Ocean 2016 na Mshindi wa pili ni Regina Ndimbo huku wengine waliobaki kwenye tano bora wamepata fursa ya kuingia katika mashindano ya Miss Kinondoni.

  Shindano hilo lilihusisha jumla ya washiriki wapatao 20 ambapo mmoja kati yao ndiyo aliyeibuka mshindi na lilidhaminiwa na wadau mbalimbali wakiwemo Mikocheni Resort Centre, Mlimani TV, Channel Ten, Darling, Helmic, Tanzania Breast Cancer Foundation, Magic FM, Jozi Lounge, Kiss Printers pamoja na NTS.

  0 0

  SERIKALI imeanza kupima viwanja zaidi ya 25,000 kwa wakazi wa kata za Kimara na Saranga zilizopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kurasimisha makazi holela.

  Akizungumza kwa nyakati tofauti Kaimu mkurugenzi wa Urasimishaji Makazi Holela Bi. Bertha Mlonda amesema, Uendelezaji Miji ni kwa mujibu wa Sheria ya MipangoMiji na una faida nyingi kwa wanachi. Alisisitiza kwamba, Maendeleo ya sehemu yeyote hutokana na miundombinu ya sehemu husika pamoja na huduma za kijamii zinazopatika.

  Mlonda amewaasa wananchi haswa wa Kata za Kimara na Saranga kutoa ushirikiano kwa wataalam ambao wameanza kupima maeneo yao ili kuondokana na tatizo la Makazi Holela kwa wakazi hao kwani upimaji huo utabadilisha taswira na hadhi ya maeneo yao.

  Kwa sasa Urasimishaji umeanzia katika Kata za Kimara na Saranga, baada ya hapo yatafuata maeneo yote yenye sifa za urasimishaji katika jiji la Dar es Salaam, na mikoa yote ya Tanzania. Zoezi hili litakuwa likitekelezwa kwa awamu kulingana na maeneo yatakavyobainishwa.

  Diwani Kata ya Kimara Mhe. Pascal Manota akihamasisha wananchi wa Mtaa wa Mavurunza Kata ya Kimara kushirikiana na Wataalam wa masuala ya Ardhi ili kuruhu upimaji wa maeneo yao walipofanya mkutano wa uhamasishaji juu ya Urasimishaji wa Makazi holela.
  Kaimu Mkurugenzi Urasimishaji Makazi holela Bi. Bertha Mlonda akielezea faida za urasimishaji katika mkutano wa Uhamasishaji kwa wanachi wa Kata ya kimara mtaa wa Mavurunza.

  Badhi ya wakazi wa Mtaa wa Mavurunza waliohudhuria mkutano wa Uhamasishaji kuhusiana na Urasimishaji Makazi holela, wakiwasikiliza viongozi wa Serikali za Mitaa (Hawako pichani) pamoja na wataalam kutoka Sekta ya Ardhi walipokuwa wakitoa elimu kwa wakazi hao.
  Hamza Khatibu, Mkazi wa Mtaa wa Mavurunza akiuliza swali kwa viongozi wa Serikali za Mitaa na wataalam wa Sekta ya Ardhi walipokuwa katika mkutano kuhusiana na Urasimishaji Makazi holela.
  Alama inayotenganisha kiwanja kimoja na kingine inayowekwa na wataalam wa upimaji kutoka Wizara ya Ardhi, wakishirikia na wataalam kutoka Manispaa ya Kinondoni.
  Wataalam kutoka Wizara ya Ardhi na Manispaa ya Kinondoni wakiandaa ramani za maeneo ambayo tayari yamefikiwa kwa ajili ya kupimwa na kurasimisha makazi holela katika Kata ya Kimara, Mtaa wa Kilungule B. 

  0 0  Dk Edmund Mndolwa mshindi wa Jumla kwa mwezi July baada ya kuibuka na Ushindi wa Mikwaju ya Jumla (Gross) 87 katika mashindano yaliyofanyika jana katika Viwanja vya Golf Lugalo Jijini Dar es salaam.
  Dk Edmund Mndolwa mshindi wa Jumla kwa mwezi July baada ya kuibuka na Ushindi wa Mikwaju ya Jumla (Gross) 87 akipiga mkwaju wa mwisho katika mashindano yaliyofanyika jana katika Viwanja vya Golf Lugalo Jijini Dar es salaam.
  Mshindi wa kwanza kwa Wanawake Victoria Elias Akijiweka sawa huku Mwezie Chiku Elias akimshuhudia wakati wakimenyana katika mashindano ya Kila mwisho wa mwezi katika Klabu ya Lugalo ya Nmb Monthly Mug.


  Mshindi wa kwanza kwa Wanawake Victoria Elias Akijiweka sawa kupiga mpira wa Mwisho wakati wakimenyana katika mashindano ya Kila mwisho wa mwezi katika Klabu ya Lugalo ya Nmb Monthly Mug.
  Afisa wa Habari kutoka JWTZ Luteni Selemani Semunyu akitoa Zawadi kwa Mshindi wa Kwanza kwa Watoto (Junior) Zuwena Hamisi mara baada ya Kumalizika mashindano ya mwezi July (Monthly Mug )yaliyofanyika jana katika Viwanja vya Golf Lugalo Jijini Dar es salaam.

  Wachezaji Golf Chipukizi wakijiweka sawa wakati wa mashindano ya kila mwisho wa Mwezi ambapoi kwa mwezi July yalifanyika jana katika Viwanja vya Golf Lugalo Jijini Dar es salaam.(Picha na Selemani Semunyu).

  0 0


  Picha na Fredy Njeje/Blogs za mikoa.

  Bohari moja ambalo lilikuwa la kuhifadhia mataili pamoja na vifaa venginevyo vya magari lililopo Sinza Lego ambalo mmiliki wake hakufahamika kwa mara moja, limeteketea kwa moto ambapo kwa mujibu ya wenyeji wa eneo hilo wamedai kuwa chanzo cha moto huo ni mataili. Pia katika eneo hilo kuna Gereji ambayo haikuathirika na moto huo mkubwa, mpaka jioni hii kikosi cha kuzima moto kilikuwa eneo la tukio kuendelea kusaidiana na wananchi kuhakikisha moto huo unazimika. Taarifa kamili itatolewa na Jeshi la Polisi.
  Bohari linalosadikiwa kuhifadhi vipuri vya magari likiwa linateketea kwa moto jioni hii Sinza Lego jijini Dar es salaam ambapo juhudi za kuzima moto zinaendelea japokuwa kazi ya kuzima imekuwa ngumu kutokana na aina ya vipuri vinavyohifadhiwa katika ghala hilo kuwa aina ya mipira na mafuta ya vilainishi vya vipuri.
  Mmoja wa kijana ambaye alifika kushuhudia tukio hilo akipanda juu ya Ghorofa baada ya kunusurika kudondokea katika moto huo


  Moto ukiendelea kuwaka huku juhudi za kuzima zikiendelea

  Mbele ni Gari la zima moto likiwa limefanya juhudi za kuzima moto , hapa wakiondoka kufuata maji mengine ili kuendelea na zoezi la kuzima moto huo

  Moto ukiendelea kuwaka katika Bohari hilo  Baadhi ya Mashuhuda wakishuhudia tukio hilo la kuwaka kwa Bohari

  Magari yakiwa yameruhusiwa kuendelea na safari baada ya moto huo na moshi mkubwa kupungua

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na Mbunge wa zamani wa Kahama James Lembeli ambaye ni mwanachama wa Chadema mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano mjini Kahama mkoani Shinyanga. 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia wa wakazi wa Kahama mara baada ya kuwasili akitokea Nzega mkoa Tabora.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akicheza jukwaani wimbo wa kwaya ya Haleluya Kuu kutoka Kanisa la KKKT-Usharika wa Yeru Ndala Shinyanga kabla ya Kuhutubia mamia ya wakazi Kahama mkoani Shinyanga.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mbunge wa zamani wa Kahama James Lembeli mara baada ya kuwasalimia wananchi waliofika kwa ajili ya kumsikiliza Rais katika viwanja hivyo vya Kahama.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia wa wakazi wa Isaka mkoani Shinyanga. 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akicheza pamoja na Wanakwaya wa Haleluya Kuu kutoka Kanisa la KKKT-Usharika wa Yeru Ndala Shinyanga mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano Kahama mjini mkoani Shinyanga.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia mara baada ya kuoneshwa picha na kijana mmoja aliyeishika picha hiyo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Tinde mkoani Sinyanga.

  PICHA NA IKULU.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali yake haitagawa chakula cha bure kwa wananchi wanaopatwa na tatizo la njaa pasipo kuwa na sababu za msingi na badala yake amewataka watanzania wajikite kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ikiwa ni pamoja na kuzalisha chakula cha kutosha.

  Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 31 Julai, 2016 wakati akihutubia mikutano ya hadhara na kuzungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake akiwa njiani kutoka Mkoani Tabora kuelekea Shinyanga na baadaye Geita anakoendelea na ziara yake.

  Pamoja na kuwahimiza wananchi kuzalisha chakula cha kutosha ili kuondokana na njaa Rais Magufuli amesema serikali yake itajikita kuhakikisha inashughulikia tatizo la uhaba wa maji, ujenzi wa miundombinu hususani barabara na reli, kuimarisha huduma za matibabu, elimu na kutengeneza ajira.  

  Akiwa Isaka Mkoani Shinyanga Rais Magufuli amesema serikali haitalipa fidia kwa wananchi waliopatwa na maafa ya mafuriko yaliyobomoa nyumba zao mwezi Machi mwaka 2015 na badala yake itajielekeza kutatua tatizo kubwa la uhaba wa maji katika mji huo ambao una makutano ya reli ya kati ya kutoka Dar es Salaam kwenda nchi za Burundi na Rwanda.

  Katika Mji wa Kagongwa Rais Magufuli amepokea kilio cha wananchi dhidi ya vitendo vya ujambazi na ametoa siku tano kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha watu wanaojihusisha na ujambazi wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

  Mjini Kahama, Dkt. Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini kushirikiana na Mbunge wa Kahama Mhe. Jumanne Kishimba kukokotoa mahesabu vizuri na kubaini kodi ambayo Serikali inastahili kulipwa baada ya Mbunge huyo kudai kuna kiasi kikubwa cha kodi hakijakusanywa kama ambavyo sheria inaelekeza.


  Aidha, Rais Magufuli amesema serikali itahakikisha wawekezaji wanaochimba madini wanaacha kusafirisha mchanga wenye madini kwa lengo la kwenda kuchakata nje ya nchi na badala yake ametaka uchakataji huo ufanyike hapa hapa nchini.Dkt. Magufuli amezungumza na wananchi vijiji vya Segese na Bukoli na kuwahakikishia kuwa Barabara ya Kahama, Segese, Kakola hadi Geita yenye urefu wa kilometa 146 itajengwa kwa kiwango cha lami kama alivyoahidi.

  Mjini Geita, Rais Magufuli amepokea kilio cha wananchi wanaodai kuwekewa zuio la kutumia mawe yenye mabaki ya madini ya dhahabu (Magwangala) kwa lengo la kusaga na kuchenjua ili kupata dhahabu, na ametoa wiki tatu kwa Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanya tathimini na kuwaruhusu wachimbaji wadogo kutumia Magwangala.

  Rais Magufuli pia ameiagiza Bodi ya Pamba hapa nchini kuhamisha ofisi zake zilizopo Jijini Dar es salaam na kuzileta katika Mikoa ya kanda ya ziwa ambako uzalishaji wa zao la pamba unafanyika.

  Dkt. Magufuli amewaonya viongozi na watendaji wa bodi hiyo dhidi ya vitendo vya usambazaji wa mbegu za pamba zisizoota na amesema ikitokea tena watachukuliwa hatua.
  Kesho tarehe 01 Agosti, 2016 Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli anatarajia kukamilisha ziara yake ya siku nne katika Mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita.


  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Geita
  31 Julai, 2016

older | 1 | .... | 921 | 922 | (Page 923) | 924 | 925 | .... | 1897 | newer