Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live

Vilainishi aina ya KY Jerry vyakamatwa Mkoani Shinyanga

$
0
0
Sehemu ya Shehena ya Vilainishi aina ya KY Jerry iliyokamatwa Mkoani Shinyanga leo. Shehena ya Vilainishi aina ya KY Jerry imekamatwa Mkoani Shinyanga leo, hivi karibuni Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto kusitisha ugawaji wa Vilainishi miongoni mwa makundi maalumu yaliyo katika hatari ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

RAIS DKT.MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA MFUKO WA BARABARA, DKT. JAMES WANYANZA NA KUMTEUA BW. JOSEPH ODO HAULE KUSHIKA NAFASI HIYO

Dkt. Shein aelekea Nchini Uingereza kwa uchunguzi wa kawaida wa Kiafya.

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali akiagwa na Makamu wa ili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Mjini Dar es salaam akielekea Nchini Uingereza kwa uchunguzi wa kawaida wa Kiafya.
Balozi Seif akimuaga Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar ves salaam Jijini Dar es salaam. Picha na OMPR – ZNZ.

Msajili wa Vyama vya Siasa alaani tamko la CHADEMA

$
0
0
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi amelaani vikali  tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari, kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini la kuazimia kufanya mikutano na maandamano nchi nzima akidai kuwa tamko hilo ni la kichochezi lililolenga kuleta uvunjifu wa Amani.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Msajili wa Vya Siasa na kusainiwa na Jaji Francis Mutungi imebainisha kuwa tamko hilo linaenda kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu 9 (2) (c) inayokataza chama cha siasa kutumia au kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu kama njia ya kufikia malengo yake ya kisiasa.

“Nimepokea kwa masikitiko tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari, kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini. Tamko hilo limejaa lugha ya uchochezi, kashfa, kuudhi na lenye kuhamasisha uvunjifu wa amani. Ili kuepuka kurejea tamko lote, nimeona ni vyema nitoe mfano wa maneno yafuatayo yaliyosemwa, ambayo yanakiuka Sheria ya Vyama vya Siasa”. Ilisema taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo iliongeza kuwa kifungu cha 9(2) (f) kinakataza chama cha siasa kuruhusu viongozi au wanachama wake kutumia lugha ya matusi, kashfa na uchochezi ambayo inaweza kusababisha au ikapelekea kutokea uvunjifu wa amani. Vile vile kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa, Tangazo la Serikali namba 215 la mwaka 2017, zinakataza chama cha siasa kutumia lugha za matusi, kashfa, uongo na uchochezi.

Nakuongeza kuwa kanuni ya 5(1) (d) inakitaka kila chama cha siasa kutotoa maneno yoyote au maandishi ambayo ni uongo. Kuhusu mtu yoyote au chama cha siasa chochote.Katika taarifa yake Jaji Mutungi amesema kutokana na Kanuni hizo tamko la CHADEMA ni ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa.Aidha, hii siyo mara ya kwanza kwa CHADEMA kutumia lugha za namna hii za kuhamasisha uvunjifu wa amani (civil disorder).

Natumia fursa hii kukemea tamko hilo hadharani, kwa mujibu wa kanuni ya 6(2) ya Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa. Pia nawaasa CHADEMA wasiendeleze tabia hii.Jaji Mutungi ametoa rai kwa  Viongozi wa Vyama vya Siasa  waonyeshe ukomavu katika medani za Siasa badala ya kujikita katika vitendo, kauli au matamshi yenye mlengo wa kusababisha uchochezi au kufarakanisha Umma na Serikali yao.

Katika tamko lao CHADEMA wameitangaza siku ya tarehe mosi Septemba kama ni siku maalum kwao kufanya mikutano nchi nzima ikiwamo maandamano ambapo ngazi zote za chama kuanzia ngazi ya msingi hadi Taifa zitahusika.

WAREMBO WANAOWANIA SHINDANO YA MISS TANGA 2016 USIPIME SASA KUFANYIKA IJUMAA MJINI TANGA

$
0
0

Warembo wanaowania Taji la Mrembo wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016) wakiwa kwenye pozi katika hotel ya Tanga Beach Resort kutakapofanyika shindano hilo Ijumaa Kesho.

Warembo hao wakiwa kwenye picha ya pozi .



Mratibu wa Shindano ya Miss Tanga 2016,Mboni Muya akizungumza na waandishi wa Habari leo kuhusiana na maandalizi ya kuelekea shindano hilo


Warembo wanaowania Taji la Urembo Mkoa wa Tanga(Miss Tanga 2016) ambalo linaandaliwa na Kituo cha Radio cha TK FM cha Mjini Tanga kwa kushirikiana na Hotel ya Tanga Beach Resort wakiwa kwenye picha ya mapozi

Baadhi ya Warembo wakimsikiliza Mdau wa Tasnia ya Urembo hapa nchini Sinza,Beny Kisaka alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kuitembelea kambi ya warembo hao wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers Nassoro Makau
Warembo hao wakimsikiliza Mratibu wa Shindano ya Miss Sinza 2016 ambaye aliitembelea kambi hiyo leo .
Mdau wa Tasnia ya Urembo hapa nchini,Benny Kisaka akitoa nasaha kwa warembo wanaotarajiwa kushiriki kinyang'anyiro cha kumtafuta Mlimbwende wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016 )itakayofanyika Ijumaa kesho kwenye Ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort.
Mdau wa Tasnia ya Urembo hapa nchini,Benny Kisaka akisisitiza jambo wakati akizungumza na warembo wanaotarajiwa kushiriki shindano la kumtafuta Mlimbwende wa Mkoa wa Tanga Ijumaa
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

ZIARA YA WAZIRI MBARAWA MWABEPANDE

$
0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua baadhi ya miundombinu iliyopo katika mradi wa ujenzi wa nyumba za wafanyakazi zilizopo Bunju B jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa nyumba za wafanyakazi eneo la Bunju B jijini Dar es salaam.
Meneja Mradi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania Arch.Humphrey Killo akifafanua mchoro wa ramani ya ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam katika barabara ya Sam Nujoma,wa kwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga .
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Mtendaji Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa nyumba za wafanyakazi eneo la Bunju B jijini Dar es salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga wakati alipokagua ujenzi wa mradi wa nyumba za wafanyakazi eneo la Bunju B jijini Dar es salaam.



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga wakati alipokagua ujenzi wa mradi wa nyumba za wafanyakazi eneo la Bunju B jijini Dar es salaam.






Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na Afisa Uhusiano wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bi. Edna John wakati alipotembelea ujenzi wa mradi wa nyumba za wafanyakazi eneo la Bunju B jijini Dar es salaam



Muonekano wa awali wa ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam.

Muonekano wa nyumba za wafanyakazi nyumba za wafanyakazi eneo la Bunju B jijini Dar es salaam.

PICHA ZOTE NA BENJAMINI SAWE-MAELEZO

KATIBU MKUU AFYA ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE YA KIBIRIZI MKOANI KIGOMA

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongozwa na wafanyakazi wa Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi yaliyopo Mkoani Kigoma kukagua baadhi ya majengo wanayoishi wazee hao ili kuona namna ya kuyaboresha kadiri inavyowezekana wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea Makazi hayo.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongea na wafanyakazi wa Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi yaliyopo Mkoani Kigoma
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akitoa Zawadi ya Sabuni kwa viongozi wa wazee wa Makazi ya Kibirizi Katibu Makazi hayo Bi. Veronica Nyaga na Mwenyekiti Bw.Hamisi Sabuni


Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Mstaafu Emmanuel Maganga mara baada ya kuwasili Mkoani hapo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kutembelea Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Mstaafu Emmanuel Maganga akimueleza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga mara baada ya kuwasili Mkoani hapo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kutembelea Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi, Katikati ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kigoma Bw. Moses Msuluzya.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi yaliyopo Mkoani Kigoma kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Afisa Mfawishi wa Makazi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Kibirizi yaliyopo Mkoani Kigoma Bw. Ladius Mushi akimpa maelezo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga kuhusu Makazi hayo na namna wanavyoshirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha Wazee hao wanakuwa katika mazingira salama.
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

Benki ya TIB Corporate yatoa msaada wa mabati 100 kwa shule za mkoa wa Songwe.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akipokea msaada wa bando za bati kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TIB Corporate Bank, Bwana Frank Nyabundege (wa pili kushoto) kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika Mkoa Mpya wa Songwe.Wa kwanza Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashuri ya Mbozi, Erik Ambakisye akifuatiwa na Mbunge jimbo la Vwawa Josephat Hasunga

Benki ya TIB Corporate leo imetoa msaada wa mabati mia moja kwa mkoa wa Songwe ili kusaidia kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na vyoo mkoani humo.

Mkoa wa Songwe, ambao ni miongoni mwa mikoa mipya, itatumia mabati hayo katika shughulli za ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa wilaya za Mbozi, Mamba, Ileje, Songwe na Tunduma.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya TIB Corporate, Bwana Frank Nyabundege alisema msaada huo umelenga kuonyesha nia na jitihada za benki yake katika kusaidia kukuza elimu na pia kuunga mkono serikali katika jitihada zake za kuboresha elimu nchini.

'Serikali pekee yake haiwezi kukuza sekta ya elimu hivyo basi ni muhimu tuisaidie serikali katika kuboresha sekta ya elimu kwa kuaanda mazingira mazuri kwa vijana wetu kujisomea’ alisema Nyabundege.

Akitoa shukrani zake kwa benki ya TIB Corporate, Mkuu wa mkoa wa Songwe Mheshimiwa Chiku Gallawa alisema mchango huo ni muhimu katika kukuza na kuboresha sekta ya elimu ambayo ndio kichocheo cha ukuaji wa sekta ya uchumi na kijamii kwa taifa la kesho.

‘Tunaishukuru benki ya TIB Corporate kwa jitihada zake za kushirikiana na serikali katika kukuza sekta ya elimu kwani hakuna taifa linaloweza kuendelea bila kuwa na raia wasomi ' alisema Mheshimiwa Gallawa.

OLE SENDEKA ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA JANA OFISI NDOGO CCM-LUMUMBA JIJINI DAR

HUDUMA YA UKATAJI TIKETI MABASI YA MIKOANI ZAZINDULIWA

$
0
0
mav2 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde (kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa huduma ya ukataji tiketi za mabasi yaendayo mikoani kwa njia ya simu ya mkononi ijulikanayo kama Tiketi Rafiki mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo inayotoa huduma ya Global Light Company Bw. Raymond Magambo.Picha na Eliphace Marwa – Maelezo
mav1 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma ya ukataji tiketi za mabasi yaendayo mikoani kwa njia ya simu ya mkononi ijulikanayo kama Tiketi Rafiki inayotolewa na kampuni ya Global Light company mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Serikali yazitaka familia zenye uwezo kutokwepa jukumu la kulea wazee na watu wenye ulemavu.

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akimkabidhi moja ya Mzee katika kambi ya wazee ya Sukamahela boksi la sabuni kwa niaba ya wazee katika kituo hicho chenye jumla ya wazee 67.
Viongozi wa Kambi ya kulea Wazee ya Sokamahela wakimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga baadhi ya nyumba wazazoishi wazee ambapo sehemu ya nyumba hizo zipo kwenye hali mbaya za kuhitaji marekebisho.




Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisalimiana na Bi. Theresia Msiwa anayeishi katika kambi ya kulea wazee ya SukaMahela iliyopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida
Baadhi ya Wazee wanaoishi katika kambi ya Sukamahela iliyopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida.


Jengo la Zahanati ya Serikali ya Sukamahela iliyo karibu na kituo hicho ambayo pia inasaidia kutoa kuhuma za matibabu kwa wazee wa kituo hicho.

Muuguzi katika Zahanati ya Sukamahela Bi.Marry Sailale akimpa maelezo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga wa shughuli mbalimbali anazofanya ikiwemo kuwahudumia Wazee wanaoishi katika kambi ya Wazee ya Sukamahela iliyopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida.
Muuguzi katika Zahanati ya Sukamahela Bi.Marry Sailale akimpa maelezo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga wa shughuli mbalimbali anazofanya ikiwemo kuwahudumia Wazee wanaoishi katika kambi ya Wazee ya Sukamahela iliyopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiwaaga Wazee katika kambi ya kulea wazee ya SukaMahela baada ya kutembelea na kuona hali halisi ya Mazingira katika kambi hiyo.
Baadhi ya nyumba zilizo katika kambi ya kulea wazee ya sukamahela iliyopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida.


Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akimpa maelekezo Afisa Mfawidhi wa kambi ya kulea wazee ya Sukamahela iliyopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida Bw. Jeremiah Paul (kushoto)na kumtaka kuwa makini katika kupokea Wazee katika kambi hiyo kwani kumekuwa na tabia ya Vijana wenye uwezo kupeleka wazazi wao kwenye kambi hizi na kukwepa jukumu la kuwalea,Kulia ni Bw. Richard Mallya Mkurugenzi Idara ya Ununuzi na Ugavi kutoka Wizara hiyo. 

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisaini kitabu cha wageni alipotembelea kambi ya kulea wazee ya SukaMahela iliyopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida, Kulia ni Bw. Richard Mallya Mkurugenzi Idara ya Ununuzi na Ugavi kutoka Wizara hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akimueleza jambo Afisa Mfawidhi wa kambi ya kulea wazee ya Sukamahela Bw. Jeremiah Paul
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongea na Wazee wanaoishi katika kambi ya kulea wazee ya Sukamahela na kuwaeleza dhumuni la serikali la kuzisaidia kambi hizo. 
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

MAKAMU WA RAIS AMJULIA HALI SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai alipofika kumsabai nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Spika amerejea nchini hivi karibuni kutoka nchini India ambapo alikwenda kwa ajilia ya uchunguzi pamoja na matibabu ya Afya yake.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai pamoja na Mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga (kulia) alipofika kumsabai nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Spika amerejea nchini hivi karibuni kutoka nchini India ambapo alikwenda kwa ajili ya uchunguzi pamoja na matibabu ya Afya yake.
(Picha na Ofisi ya Bunge)

Airtel yakabidhi vifaa vya michezo vya thamani ya Milioni 200 kwa maendeleo ya soka la vijana

$
0
0
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidhi vifaa vya michezo kwa katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini (TFF) Selestine Mwesigwa tayari kwa msimu wa sita wa Airtel Rising Stars unaotarajiwa kuanza Jumamosi Julai 30.
Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini (TFF) Selestine Mwesigwa akikabidhi vifaa vya michezo kwa katibu wa chama cha soka cha Ilala Daud Kanuti tayari kwa msimu wa sita wa Airtel Rising Stars unaotarajiwa kuanza Jumamosi Julai 30.
Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini (TFF) Selestine Mwesigwa akikabidhi vifaa vya michezo kwa katibu wa chama cha soka cha Kinondoni Isack Mazwile tayari kwa msimu wa sita wa Airtel Rising Stars unaotarajiwa kuanza Jumamosi Julai 30.


Kampuni ya simu za mikononi Airel Tanzania leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu zikaoshiriki michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ngazi ya mkoa ambayo inatarajiwa kuanza Julai 30 mpaka Agosti 30 2016 kwenye mikoa tofauti hapa nchini.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya milioni 200 vimekabidhiwa kwa Wasimamizi wa vituo vyote vya mikoa na Taifa. Vifaa hivyo hivyo ni pamoja na jezi za wachezaji, shin guards, soksi, jezi za marefa, mipira pamoja na glovu.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Katimu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF) Celestine Mwesingwa alisema ‘ Kwa kutoa vifaa hivi vya michezo,mdhamini ametimiza moja kati ya majukumu yake na ni matarajio yangu kwamba mtarudi kwenye vituo vyenu na kuongeza bidii ya kutafuta vipaji vinavyoibuka vya mpira wa miguu’.

‘Tunatarajia kuona mechi zenye ushindani na za kuvutia na natoa wito kwa viongozi wa vyama vya mikoa kuwa makini wakati wa kuchangua timu kombaini ambazo zitakuja kucheza kwenye fainali za taifa ambazo zitafanyika Dar es Salaam tarehe 6 mpaka 11 Septemba mwaka huu.

Kwa upande wake Meneja Mahusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema ‘Airtel Rising Stars inaungana pamoja na promosheni yetu ya Airtel Fursa ambayo ilizinduliwa mwaka jana ikiwa na lengo la kuwasaidia vijana kukuza vipaji vyao. Kwa mwaka, michuano hii inatoa fursa nyingine kwa wavulana pamoja na wasichana kutambua uwezo wao wa kucheza soka na kuweza kufanikisha ndoto zao. Kwa mantiki hiyo, Airtel Tanzania inatumia program hii kuwezesha vijana wenye vipaji vya mpira wa miguu kuvionyesha kwa makocha na hatimaye kufakinisha ndoto zao’.

Airtel Rising Stars ni mpango kabambambe kwa Afrika nzima yenye lengo ya kutoa nafasi kwa vijana kuonyesha vipaji vyao mbele ya makocha, na hatimaye kupata fursa ya kuviendeleza na kuvikuza.

BABATI WATAKIWA KUJIUNG ANA CHF ILIYOBORESHWA

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera amesema atawachukulia hatua kali viongozi wa ngazi ya Vijiji, Kata, na Tarafa za Wilaya ya Babati, watakaozembea zoezi la kuhamasisha kaya zijiunga na mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa (ICHF).

Dk Bendera aliyasema hayo mbele ya mkuu wa Wilaya hiyo Raymond Mushi, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Hamis Malinga, wakati akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Goroa, alipotembelea kuhamasisha kaya kujiunga na mfuko huo.

Hata hivyo, amewaagiza viongozi hao kuhakikisha hadi mwezi Desemba mwaka huu kaya 40,642 zinajiunga na mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa (CHF) hivyo kufikia asilimia 50 ya kaya zilizopo kwenye wilaya hiyo. Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa halmashauri ya wilaya hiyo ya Babati ina kaya 81,284 hivyo viongozi wa wilaya hiyo wahakikishe hadi mwezi Desemba wawe wamefanikisha nusu ya kaya zijiunge na mfuko huo.

“Suala la kupatiwa matibabu pindi mtu akiugua halina mjadala hivyo viongozi wa ngazi tofauti kwenye wilaya hii ya Babati, wanapaswa kufuatilia ili kaya hizo zijiunge na mfuko huo ambao una manufaa kwao,” alisema Dk Bendera. Alisema viongozi wote wa eneo hilo wanapaswa kuhakikisha jamii inajiunga na mfuko huo kwani ni ukombozi wao kwenye sekta ya afya na siku wakistaafu wananchi watawakumbuka kwa kusababisha mabadiliko ya huduma hizo.


Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Goroa Wilayani Babati, juu ya kaya zao kujiunga na mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa (CHF).

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Goroa Wilayani Babati, juu ya kaya zao kujiunga na mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa (CHF).

Wananchi wa Kata ya Duru Tarafa ya Goroa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakimsikilimza Mkuu wa Mkoa huo Dk Joel Bendera wakati wakiwaeleza umuhimu wa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Hamis Malimba akizungumza kwenye mkutano wa ndani juu ya mikakati yake ya kuhakikisha kaya za wilaya yake zinajiunga na mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa (CHF).
Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Raymond Mushi akizungumza na viongozi wa Tarafa ya Goroa juu ya mikakati yake ya kuhakikisha jamii inajiunga na CHF iliyoboreshwa.
Hata hivyo, Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya nchini (NHIF) mkoani humo, Isaya Shekifu alisema mpango wa CHF ulioboreshwa utawawezesha kila kaya ya watu sita baba, mama na watoto wanne ambao hawajafikisha miaka 18 kupata matibabu kwa gharama ya sh30,000 katika mwaka mzima.

Shekifu alisema bima ya afya ni muhimu kwa sababu siyo kila mtu anapopata ugonjwa ana uwezo wa kugharamia matibabu na nchi zilizoendelea zimefanikiwa kupunguza vifo visivyo na lazima kwa kuhakikisha watu wanajiunga na mfuko. Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati Hamis Malinga akizungumza mbele ya Dk Bendera, alisema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa wananchi wa eneo hilo wanajiunga kwa wingi na mfuko huo.

Malinga alisema kupitia timu waliyonayo kuanzia ngazi ya vijiji, kata na tarafa, watatimiza majukumu yao kwa kupeana mrejesho kila mwezi ili kutambua wamefikia hatua gani na wanatarajia hadi mwezi Desemba watafanikisha suala hilo.

MBUNGE MWAMOTO NA RC IRINGA HATMAYE WAPOKEA MADAWATI YA MFUKO WA JIMBO LA KILOLO

$
0
0

Mbunge wa Kilolo Bw Venance Mwamoto akikabidhiwa madawati leo la Bi Malidadi kwa niaba ya mkurugenzi wa Kilolo ,madawati hayo yametengenezwa kwa mfuko wa jimbo la Kilolo kwa kiasi cha Tsh milioni 30 awali madawati hayo yalikataliwa kutokana na kutengenezwa chini ya kiwango ila sasa yametengenezwa kwa kiwango
Dc Kilolo Asia Abdalah na timu ya wataalam wakijiridhisha na ubora wa madawati hayo ambayo sasa yapo safi
Mbunge Mwamoto akifurahia ubora wa madawati ya mfuko wa jimbo la Kilolo
Na MatukiodaimaBlog

MADAWATI 745 ambayo yalitengenezwa na mfuko wa jimbo la Kilolo kwa gharama ya Tsh milioni 30 zilizotolewa na mbunge wa jimbo hilo Venance Mwamoto ambayo yalikataliwa na mbunge huyo na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza yamekamilika kutengenezwa kwa ubora .

Akizungumza baada ya kukabidhiwa madawati hayo leo mbunge Mwamoto alisema kuwa amekubali kupokea madawati hayo baada ya kufurahishwa na ubora wake na hivyo imani yake kuona walimu wanasimamia utunzaji wa madawati hayo ili kuondokana na kero tena ya madawati katika shule zote za wilaya ya Kilolo.

Mbunge Mwamoto alisema kuwa kufuatia uhaba wa madawati uliyokuwa ukiikumba wilaya ya Kilolo na kama sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dr John Magufuli alilazimika kuidhinisha pesa kiasi cha Tsh milioni 30 kutoka mfuko wa jimbo la Kilolo ili kuweza kusaidia utengenezaji wa madawati 300 japo Halmashauri ya Kilolo kupitia wadau wake wa ndani na makusanyo ya ndani waliweza kuongeza kiasi cha Tsh milioni 19 na kufanya kuwepo kwa kiasi cha pesa cha Tsh milioni 49 ambazo zilifanikisha kutengeneza madawati zaidi ya 1000 .

Alisema kuwa pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na Halmashauri hiyo katika kushughulikia kero ya madawati katika wilaya hiyo ya Kilolo ila mafundi ambao walipewa kazi ya kutengeneza madawati hayo hawakuwa wazuri kutokana na kushindwa kuifanya kazi hiyo kwa ubora uliotakiwa hivyo kupelekea kufanya kazi hiyo kwa kiwango cha chini zaidi.

"Nililazimika kukataa madawati 40 ambayo yalipelekwa shule ya Msingi Nyanzwa na Igunda baada ya kuyaona hayana ubora na wananchi kulalamika kuwa ni mabovu ukilinganisha na madawati ambayo yalitengenezwa kwa nguvu ya wananchi katika vijiji hivyo ......hivyo sikuwa tayari kupokea madawati hayo hali iliyopelekea mkuu wa mkoa wa Iringa kufika kuona madawati hayo na kulazimika kuyakataa madawati yote 745 kwa kutaka yatengenezwe kwa ubora"

Mwamoto alisema kuwa amefurahishwa na usimamizi mzuri wa mkuu wa wilaya ya Kilolo na timu yake ya mkurugenzi wa wataalam wengine ambao wameweza kuifanya kazi hiyo ya kusimamia ubora kwa muda mfupi wa wiki tatu kinyume na muda ule wa mwezi mmoja uliotolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa .

Hata hivyo Mwamoto alisema kuwa yawezekana wapo watendaji ambao walimchukia kwa yeye kukataa madawati hayo ila ukweli alifanya hivyo kusaidia watoto wa wana Kilolo kutoendelea kukaa chini na kuwa iwapo madawati hayo yangepelekwa shuleni bado wananchi wangebeba dhamana ya kuendelea kuchangishana kwa ajili ya kuchonga madawati.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah alisema kuwa baada ya mkuu wa mkoa wa Iringa kumpa agizo la kusimamia zoezi hilo ndani ya mwezi mmoja alilazimika kuifanya kazi hiyo kwa haraka zaidi ndani ya wiki tatu ili kuona wanafunzi wote wanakaa kwenye madawati .

Alisema kuwa timu ya wakuu wa idaraka katika wilaya ya Kilolo wameonyesha ushirikiano mkubwa katika kutekeleza agizo hilo na kuwa baadhi yao walikuwa wanalala kwenye karakana zilizopewa kazi ya kutengeneza madawati hayo mapema kabla ya muda waliopewa na mkuu wa mkoa wa Iringa .

Wakati mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Masenza pamoja na kumpongeza mkuu wa wilaya ya Kilolo na timu yake kwa kutekeleza zoezi la usimamiaji wa ubora wa madawati hayo bado alimpongeza mbunge wa Kilolo Bw Mwamoto kwa kubaini suala hilo huku akiwataka walimu katika shule zote kuhakikisha wanatunza madawati hayo ili kuondokana na adha ya kuchangia madawati mara kwa mara .

 Nimeridhishwa na ubora wa madawati hayo na yale machache ambayo yalipelekwa mashuleni wanaendelea kuyarekebisha ili yaweze kufanana na haya ambayo kweli yapo katika ubora mzuri "

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki watekeleza agizo la Rais kwa kuchangia Madawati.

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akimkabidhi hundi Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya makabidhiano madawati ikiwa ni fedha zilizochangwa na watumishi wa wizara hiyo ikiwa sehemu ya kutekeleza agizo la Rais Mhe. John Magufuli mapema hii leo katika shule ya Msingi Chamanzi iliyopo wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam . Picha na Beatrice Lyimo-MAELEZO

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wamechangia kiasi cha Tsh. Milioni 100 ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha umma kuhusu zoezi la upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na Sekondari nchini.

Akikabidhi mchango huo kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kwa niaba ya watumishi wa wizara hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi  Augustine Mahiga amesema kuwa watumishi hao wametoa fedha hizo kwa shule ya msingi Chamazi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais la upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na sekondari nchini.

Balozi Mahiga amesema Wizara yake iliwahamasisha watumishi wake walio makao makuu na wale walio kwenye balozi mbalimbali nje ya nchi kuchangia zoezi hilo la upatikanaji wa madawati.

“Ili kufanisha upatikanaji wa fedha hizi Wizara yangu iliwahamasisha watumishi wake wote walio Makao makuu na wale walio katika balozi zetu duniani kote,  wito huu uliitikiwa kwa ari na hamasa kubwa na kufanikisha kukusanya kiasi cha Shilingi 100,176,825.52 za kitanzania”alisisitiza Balozi Mahiga

Waziri Mahiga aliongeza kuwa mara baada ya kukusanya fedha hizo watumishi wa Wizara hiyo waliamua kumpatia aliyekuwa Mtumishi wa Wizara ambaye sasa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni kiasi cha shilingi Milioni 15 kwa ajili ya ununuzi wa madawati katika Wilaya yake.

Aidha, amesema kiasi fedha zilizobaki zaidi ya shilingi milioni 85 zilikabidhiwa kwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa  kwa ajili ya mchango wa utengenezaji wa madawati ya shule ya Msingi Chamazi iliyoko Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mahiga aliongeza kuwa mbali na wizara yake kuwa na majukumu mbalimbali bado inalo jukumu la kuhakikisha inaitangaza Tanzania ili kuvutia wawekezaji na kukuza uchumi wa nchi, na kuongeza kuwa elimu bora ni msingi imara katika kufanikisha hilo.

Marufuku kufanya kazi za mipangomiji bila kusajiliwa – TPRB

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Bodi ya Usajili ya Wataalam wa Mipangomiji (TPRB) imewapiga marufuku wanaofanya kazi za Mipangomiji bila kusajiliwa ili kuondoa usumbufu na kupunguza udanganyifu kwa wananchi wanaohitaji huduma hiyo.

Onyo hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Msajili wa Bodi hiyo, Helena Mtutwa katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari kuhusu majukumu ya Bodi hiyo.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 23(4) cha Sheria ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji ya 2007 inasema kuwa ,ni kosa la jinai kufanya kazi hizi bila kusajiliwa kwa hiyo, nawashauri wafanyao shughuli hizo kuacha mara moja”, alisema Mtutwa.

Mtutwa amewataka wananchi wenye sifa zinazowawezesha kusajiliwa na TPRB wafike katika ofisi zao kwa ajili ya kusajiliwa ili kuepusha usumbufu utakaojitokeza kwao na kwa Bodi hiyo.

Aidha, Msajili huyo amesisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mwananchi yeyote atakayebainika kukiuka agizo hilo.

Bodi ya Usajili ya Wataalam wa Mipangomiji ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa chini ya Sheria namba 7 ya mwaka 2007 ambapo moja ya majukumu yake ni kusajili wataalam wa Mipangomiji na kusimamia maadili.

Ratiba ya Usaili Maisha Plus East Africa 2016

$
0
0
Baada ya Usaili kufanyika kwa kishindo katika mikoa ya Mtwara na Dar es salaam usaili wa Maisha Plus unaendelea katika mikoa mingine ndani ya Tanzania. 
30/07/2016 - MBEYA - Ukumbi wa City Pub 
31/07/2016 - IRINGA - Savanna Garden 
02/08/2016 - DODOMA - Matei Lounge 
04/08/2016 - MWANZA - Rock Garden 
06/08/2016 - ARUSHA - Via Via
 13/08/2016 - ZANZIBAR - Ngome Kongwe 


Vijana wote wenye umri wa miaka 18 - 26 wanakaribishwa kujitokeza kwa wingi. Elimu na ujuzi ni kiwango chochote. Zawadi kwa mshindi ni Tzshs. Milioni 30. Fomu zinapatikana BURE kabisa kupitia www.maishaplus.tv na katika maeneo tajwa hapo juu. 

 Maisha Plus East Africa 2016 | #VijanaNdioNgazi #HapaKaziTu
   
 Bofya hapa chini kuona video 33 fupi za usaili wa Maisha Plus Dar.

MAHAKAMA KUU KANDA YA TANGA YATUPILIA MBALI SHAURI LA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI JIMBO LA PANGANI

$
0
0
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tanga jana imetupilia mbali shauri la kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Pangani lililofunguliwa na aliyekuwa mgombea kupitia tiketi ya CUF Amina Mwindau dhidi ya Mbunge wa Jimbo hilo Jumaa Hamidu Aweso CCM na kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo. 

Akizungumza wakati akitoa huduma ya Shauri hilo,Jaji Patricia Fikirini alisema mlalamikaji Amina Mwindau CUF ameonekana kushindwa katika shauri hilo dhidi ya mlalamikiwa Jumaa Aweso katika upingaji wa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika oct 25 mwaka jana. 

Alisema miongoni mwa malalamiko yalioambatanishwa kutoka kwa
mlalamikaji katika zoezi zima la kupinga matokeo hayo ni pamoja na kuwa mlalamikiwa ambae ni Jumaa Aweso katika kampeni zake alikiuka taratibu za uchaguzi,ubaguzi wa mgombea wa jinsia ya kike na kutumia lugha ya siziokuwa za kiungwana jambo ambalo mlalamikaji alidai lilimgharimu kupata matokeo mazuri katika uchaguzi huo. 

Alisema sambamba na vielelezo vilivyoletwa mahakamani hapo pamoja na ushahidi uliotolewa kwa upande wa mlalamikaji havikuwa na ushawishi wa kuweza kutengua matokeo ya uchaguzi huo. Jaji Fikirini alisema amezingatia hoja zote kutoka pande mbili na kujiridhisha Jumaa Aweso ambae ni mbunge hivi sasa kuwa ni mbunge aliyepita kihalali na hakukuwa na vigezo vya upingwaji wa matokeo aliyopata katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana. 

Alisema haki zote za kisheria zipo wazi kwa pande zote mbili
mlalamikiwa na mlalamikaji ikiwa pamoja na kukata rufaa kwa maamuzi yaliyochukuliwa na Mahakam hiyo ikiwa kama kuna upande hauta ridhika na hukumu iliyotolewa.


Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso katika akipongezwa na wananchi wa Jimbo la Pangani mara baada ya kutangazwa na Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kuwa mshindi halali katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba mwaka jana mara baada ya kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo katika kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CUF Amina Mwidau

Mbunge Aweso Jumaa akiwa amebebwa juu juu na wananchi wa Jimbo la Pangani mara baada ya kesi iliyofunguliwa dhidi ya mpinzania wake wa CUF Amina Mwidau ya kupinga matokeo ya uchaguzi kutupiliwa mbali na mahakama kuu kanda ya Tanga .

Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso wa pili kutoka kulia akiwa na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini,Stephen Ngonyani "Proffesa Maji Marefu " wakiwa ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Tanga wakisuburia kuanzwa kwa kesi hiyo hata hivyo hukumu hiyo ilimpa ushindi halali Mbunge Aweso katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba mwaka jana mara baada ya kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo katika kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CUF Amina Mwidau
Kwa upande wake Wakili wa kujitegemea na mahakama kuu Warehema Kibaha alisema Jaji Patisia Fikirini amefanya maamuzi sahihi ya kutenda haki kwa mteja wake katika shauri hilo lililo dumu kwa takriban miezi 7. 

Wakili Kibaha alisema katika shauri hilo walijiandaa kwa ushahidi na mashahidi wazuri ili kuweza kukabiliana na kesi hiyo jambo ambaloliliwawezesha kupata ushindi wa kihalali na kuweza kumpa nafasi mteja wake kuendelea na majukumu yake ya Kibunge. 

Nae Wakili Mashaka Ngole aliyemsimamia Mlalamikaji Amina Mwindau alisema hana pingamizi lolote na atamsikiliza mteja wake ikiwa ataamua kukata rufaa wataangalia vigezo muhimu vitakavyo wasaidia katika awamu ya pili pindi watakapo kata rufaa hiyo .

Mbunge wa Jimbo la Pangani Jumaa Aweso ambaye alikuwa anakabiliwa katika shauri hilo alisema kipindi chote alichokuwa anakabiliana na kesi hiyo kulimpotezea umakinifu wa kufanya majukumu yake ya kibunge na kuweza kuangalia shida za wananchi wa Pangani kwa umakini zaidi.
Aweso alisema kesi imekwisha na sasa kilichombele yake ni kupambana na kero za wananchi wa Wilaya hiyo ili kuweza kuwaletea maendelo kama alivyowaahidi kipindi cha kampeni.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

MAKAMU WA RAIS, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ATEMBELEA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali, Swalehe Mohamed (mwenye fulana nyeupe) aliyelazwa katika taasisi ya saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake aliyoifanya katika hospitali hiyo leo Ijumaa (Julai 29, 2016).
Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwajulia hali, Said Mohamed (kushoto) na Balitiamo Damian waliolazwa katika taasisi ya saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake aliyoifanya katika hospitali hiyo leo Ijumaa (Julai 29, 2016).
Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwajulia hali, Isaya Sanga (katikati) na Abasi Bushole waliolazwa katika taasisi ya saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake aliyoifanya katika hospitali hiyo leo Ijumaa (Julai 29, 2016). Kulia ni Mganga Mkuu wa Taasisi hiyo, Dkt. Damian Msemo.
Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na ndugu za wagongwa waliolalazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake aliyoifanya katika hospitali hiyo leo Ijumaa (Julai 29, 2016).
Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika taasisi ya saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake aliyoifanya katika hospitali hiyo leo Ijumaa (Julai 29, 2016).






Na Beatrice Lyimo- MAELEZO

MAKAMU wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya ziara yake ya kwanza katika Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuona wagonjwa sambamba na kuangalia maendeleo ya hospital hiyo.

Akiwa katika ziara hiyo Mhe. Samia amebaini baadhi ya changamoto zinazoikabili hospitali hiyo ikiwemo ya upungufu wa wauguzi na madaktari, uhaba wa mashine za mionzi, upungufu wa vifaa tiba pamoja na upatikanaji wa dawa za Saratani kwa wagonjwa hao.

Amesema kuwa Serikali itahakikisha inaongeza mashine mbili mpya za mionzi kwa ajili ya kupimia wagonjwa wanaosumbuliwa na matatizo ya Saratani na kuahidi kupunguza deni la MSD wanaloidai hospital hiyo ili wagonjwa waweze kupata dawa kwa gharama nafuu.

Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Damian Msemo ameiomba Serikali kuwekeza bajeti ya kutoshakatika hospital hiyo kwani inatoa huduma bure kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na matatizo hayo ambapo matibabu yake haa kwa upande wa mashine ya mionzi hutumia gharama kubwa

Akifafanua utaratibu wa kutibu wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kutibiwa amesema kuwa hospitali hiyo imeweka utaratibu mzuri wa kuwahudumia wagonjwa hao ambapo mgonjwa anayefika mapema ndiye anayehudumiwa na kuongeza kuwa huwa wanatimu wagonjwa 160 kwa siku kuanzia asubuhi hadi usiku licha ya uhaba wa vifaa tiba walionao”

“Hospitali hii tumeweka utaratibu mzuri wa kuwahudumia wagonjwa wanaofika, mgonjwa anayefika mapema ndiye anayehudumiwa kwanza
ukiacha wagonjwa wa dharula” Amesema Dk. Msemo.

Amesema wagonjwa wanaowafikia kutibiwa hospitalini hapo ni wengi ikilinganishwa na vifaa tiba walivyonanvyo na kuwataka wananchi kuwa wavumilivu pale wanapokumbana na changamoto mbalimbali.
Kwa upende wao baadhi ya wagonjwa waliofika hospitalini hapo kupata matibabu wameushukuru uongozi wa Hospitali ya Taasisi hiyo kwa kujituma mbali na uhaba wa waauguzi na changamoto za upatikanaji wa mashine za mionzi na dawa kwa ajili ya kutibu matatizo hayo
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live




Latest Images