Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli awasihi watanzania kudumisha amani, umoja na utulivu asisitiza serikali kuhamia Dodoma

$
0
0


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma mapema leo asubuhi waliojitokeza kushuhudia maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa iliyofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma.PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasihi watanzania kuwaenzi Mashujaa kwa kudumisha Amani, Umoja na Utulivu uliojengwa na mashujaa hao.Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo tarehe 25 Julai, 2016 wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa, yaliyofanyika katika uwanja wa Mashujaa Mjini Dodoma.

Pamoja na kutoa rai hiyo Rais Magufuli ameahidi kuwa atahakikisha azma ya Serikali kuhamia Dodoma inatekelezwa kabla ya kuisha kwa kipindi chake cha uongozi wa miaka mitano.

"Tunapoadhimisha siku ya Mashujaa hatuwezi kumsahau Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa alisema makao makuu yawe Dodoma, haiwezekani sisi watoto wake, sisi wajukuu wake tupinge kauli ya Mzee huyu.

"Kwa hiyo nilikwishazungumza na leo narudia hili katika siku ya Mashujaa, mlinichagua ndugu zangu wa Dodoma kwa kipindi cha miaka mitano, hadi sasa miezi minane imepita, nimebakiza miaka minne na miezi minne, nataka kuwathibitishia kuwa katika kipindi cha miaka minne na miezi minne iliyobaki nitahakikisha serikali yangu pamoja na mimi tunahamia Dodoma bila kukosa"Amesema Rais Magufuli.

Kufuatia maelekezo hayo ya Mhe. Rais, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza Mawaziri wote waanze mara moja kuhamia Dodoma na kwamba yeye mwenyewe atakuwa amehamia Dodoma ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.

Viongozi wengine waliohudhuria maadhimisho hayo ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid, Mawaziri Wakuu wastaafu Mhe. John Samwel Malecela na Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Mabalozi na wanadiplomasia kutoka nchi mbalimbali, Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, Viongozi wa vyama vya siasa na dini, maafisa na askari waliopigana vita mbalimbali.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma



25 Julai, 2016

NASHUKURU MUNGU KWA KUUTUA MZIGO SALAMA HUKU NIKIIACHA NCHI IKIWA SALAMA TULII KABISA-DKT.JAKAYA KIKWETE

$
0
0
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi na wafuasi wa Chama cha Mapiduzi katika hafla ya kumkaribisha nyumbani mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM,iliyofanyika wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
wananchi na wafuasi wa Chama cha Mapiduzi wakimsikiliza Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete katika hafla ya kumkaribisha nyumbani mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM,iliyofanyika wilaya ya Bagamoyo.

Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akisalimiana na Mke wa Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete,mama Salma Kikwete, katika hafla ya kumkaribisha nyumbani mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM,iliyofanyika wilayani Bagamoyo,wengine ni wabunge wa mkoa huo wakimsalimia Mwenyekiti huyo mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbili wa mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

Na David John Pwani

MWENYEKITI Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete amesema anashukuru Mungu Kwa kuutua mzigo salama huku akiicha nchi ikiwa salama tulii kabisa.

Amesema kuwa safari yake ya urais ilianzia Bagamoyo akitokea wilayani hapo ambapo baada ya hapo alikwenda Kibaha kutangaza nia ya kugombea urasi nakudai kuwa amejisikia flaha kurudi tena Bagamoyo akiwa salama.

Amesema wakati akielekea kutanga nia ya kugombea urais alikuwa na mtoto wake Ridhiwani Kikwete ambapo yeye alikuwa anaandika na Ridhiwani anachapa kwenye Komputa.

Dkt.Kikwete ameyasema hayo leo wilayani Bagamoyo katika hafla ya kumkaribisha Nyumbani baada ya kuitumikia nchi Kwa miaka mingi, ambapo iliandaliwa na Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani.

Alisema.anashukuru Kwa Mara nyingine kurudi mahala alipoazia na kwamba amemaliza salama na ameacha nchi ikiwa salama na imetulia tulii kama Maji kwenye mtungi. Akikumbuka mchakato wa mwakajana wa kumpata Mgombea ulikuwa na mambo mengi lakini mambo yalikwenda salama na hakuna lililokuwa limeharibika .

"Ilikuwa Kazi kubwa si ndogo lakini hatimaye wa kavuka na wakaingia kwenye uchaguzi ambao ulikuwa na vurumayi"amesema Dkt.Kikwete .Aidha amesema kuwa hata hivyo katika uchaguzi huo kulikuwa hakuna mtu ambaye alipatwa na tukio la kumpiga mwezake hali ambayo iliwashangaza hata nchi jirani.

Alisema kuwa katika kipindi chake cha uongozi amefanya kazi kubwa ya kusukuma maendeleo ya wananchi Kwa mikoa yote,wilaya zote bila ubaguzi wowote ule huku akikiri kukabiliana na Changamoto ya kunyoshewa vidole hususani pale alipojalibu kupeleka maendeleo Wilayani Bagamoyo konakamba wananchi wa Bagamoyo walikuwa hawana haki.

Aidha Dkt.Kikwete alisema kuna wakati alisimamisha fedha za ujenzi wa barabara hiyo na kupeleka fedha hizo kujenga barabara ya Geita, Sengerema,usagala ,na kulizuka na Maneno mengi dhidi yake na hadi kufikia wabunge kulumbana.

Amesema hata hivyo anashukuru kwamba amemaliza salama na Kwa Bahati nzuri amepatikana rais ambaye ana ari kubwa ya kuwaletea maendelea watu huku akitaka watanzania kumuunga mkono.
Wanachana

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani leo wamejitokeza Kwa wingi kumkaribisha nyumbani Mwenyekiti Mstaafu wa Chama hicho Dkt.Jakaya Kikwete katika sherehe zilizofanyika wilayani Bagamoyo. Wanachama hao ambao walitoka katika wilaya zote za Mkoa wa Pwani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho mkoa Masikuzi. pamoja na Katibu Joyce Masunga walimuaga na kumkaribisha Kwa nyimbo mbalimbali.

SIMU.tv: Huu ni uchambuzi wa habari za magazeti ya leo July 26, 2016.

TANAPA YAIONGEZEA NGUVU TIMU YA TAIFA YA RIADHA INAYOJIANDAA NA MASHINDANO YA OLIMIPIKI.

$
0
0
Wanariadha wanne watakao iwakilisha Tanzania katika Michuano ya Olyimpiki nchini Brazil wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi pamoja na Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Antony Mtaka ,wengine kutoka kulia ni Mkufunzi wa wanariadha hao,Francis John na anyefuatia ni Mkurugenzi wa Utalii na Masokowa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa.Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akitoa neno la ukaribisho kwa wanahabari na wageni wengine katika hafla fupi ya kukabidhi hundi kwa wanariadha wanaounda timu ya taifa, inayojiandaa na mashindano ya Olimpiki yatakayoafanyika mwezi Agosti  nchini Brazil.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi,akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi hundi ya Shilingi Milioni tano kwa wanariadha wanaounda timu ya taifa inayojiandaa na mashindano ya Olimpiki.
Mkurugenzi Mkuu  wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni tano kwa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia wanariadha wanaounda timu ya taifa wakijiandaa na mashindano ya Olimpiki. 
Mkurugenzi Mkuu  wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akikabidhi "Track Suit "maalumu zenye maandishi na nembo yanayotangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia wanariadha wanaounda timu ya taifa wanaojiandaa na mashindano ya Olimpiki.

Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akizungumza mara baada ya kukabidhiwa hundi pamoja na mavazi maalumu kwa ajili ya wanariadha hao .
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) waliohudhuria hafla hiyo.kutoka kushoto Mkurugenzi wa Utalii na Masoko,Ibtahim Musa,Meneja Utalii Johnson Manase na Mhifadhi Vitalis Uruka.
Wanariadha watakaoiwakilisha nchi katika mashindano ya Olimpiki katika jiji la Reo De Jeneiro nchini Brazil wakiwa katika mavazi maalumu yanaotangaza vivutio vilivyoko nchini.
Mkufunzi wa Wanariadha wanaojiandaa na mashindano ya Olyimpiki ,Francis John akizungumzia matarajio yake juu ya vijana hao.
Mmoja wa Wanariadha hao,Alphonce Felix Simbu akizungumza mara baada ya kupoke msaada kutoka  TANAPA.
Baadhi ya Wanahabari na wageni wengine waliofika katika ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kushuhudia makabidhiano hayo.
Mwanariadha Said Makuka atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Mwanariadha Sara Ramadhan ,mwanadada pekee atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Mwanariadha Alphonce Felix atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Mwanariadha Fabian Joseph atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza  kutumia fursa ya mashindano ya Olyimpiki yanayotarajia kuanza mwezi ujao katika jiji la Rio de Janeiro nchini Brazili kutangaza vivutio vya utalii kupitia wanariadha wa Tanzania.

Hadi sasa ni wanariadha wanne ,wakiume watatu na wa kike mmoja ndio waliofuzu kushiriki mashindano hayo na tayari wako kambini katika hosteli za Chuo cha Misitu cha FITI zilizoko West Kilimanjaro wilayani Siha.

Akiongea mjini Arusha wakati akikabidhi msaada wa fedha na vifaa kwa ajili ya wanariadha hao Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA,Allan Kijazi amesema wameamua kutumia fursa hiyo pia kusaidia wanariadha hao wanaoiwakilisha nchi katika mashindano hayo ili waweze kurejea na medali.

Akishukuru kwa msaada huo Rais wa Shirikisho la Riadha nchini ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu AnthonY Mtaka amesema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuwakatia bima ya Afya mwaka mmoja wanariadha hao pamoja na familia zao ili wanapokua nchini Brazili wasiwe na mawazo mengi kuhusiana na familia zao walizoziacha hapa nchini.

Naye mmoja wa wanariadha waliofuzu kushiriki mashindano hayo Alphonce Felix pamoja na mkufunzi wa timu hiyo ya Riadha Francis John wameushukuru uongozi wa Riadha kwa kuiwezesha timu hiyo kukaa kambini kwa miezi saba na kuahidi safari hii timu hiyo haiendi kushiriki bali kupambania medali.

Wanariadha waliopo katika timu hiyo ya taifa wanaotarajiwa kwenda Brazili ni mwanamke pekee Sara Ramadhani, Fabiani Joseph, Saidi Makuka na Alfonce Felix.

MFUKO WA SAGCOT CTF WATOA SOMO LA KILIMO NA UFUGAJI WAKIBIASHARA KWA WAFUGAJI MKOANI NJOMBE.

$
0
0
 Mratibu wa Biashara wa Mfuko Kichocheo wa Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT CTF), Abdala Msambachi   akitoa elimu  kwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoani Njombe jana ili kufanya ufugaji wa wa kisasa utakaoinua uchumi wakati wa semina ya siku tano ya Kilimo Ufugaji Biashara (FAAB)  iliyoandaliwa na SAGCOT CTF,  Kiwanda cha Maziwa Njombe kwa kushirikiana na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara, (UNCTAD).
 Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT  CTF), John Kyaruzi (kulia), akizungumza na wafugaji wakati wa ufunguzi wa semina ya siku tano ya kilimo ufugaji wa kibiashara (FAAB)  iliyoandaliwa na SAGCOT CTF, Kiwanda cha Maziwa Njombe kwa kushirikiana na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara, (UNCTAD) yenye lengo la kuwafanya wafugaji hao kufuga kibiashara. Semina hiyo ilifanyika mkoani Njombe jana. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya mfuko huo, Dr Rosebud Kurwijila na Mkurugenzi wa Hamashauri ya Mji wa Njombe, Iluminata Mwenda.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya Mfuko Kichocheo wa Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT  CTF), Dk. Rosebud Kurwijila (kushoto), akifungua semina ya siku tano ya Kilimo Ufugaji Biashara (FAAB)  iliyoandaliwa na SAGCOT CTF, Kiwanda cha Maziwa Njombe kwa kushirikiana na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara, (UNCTAD) yenye lengo la kuwafanya wafugaji hao kufuga kibiashara. Semina hiyo ilifanyika mkoani Njombe jana. Kulia ni Katibu Mtendaji wa SAGCOT CTF, John Kyaruzi.

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Iluminata Mwenda (kushoto),  akizungumza na wafugaji wa halmashauri yake waliohudhuria semina ya siku tano kuhusu Kilimo Ufugaji Biashara (FAAB)  iliyoandaliwa na Mfuko Kichocheo wa Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT  CTF), Kiwanda cha Maziwa Njombe kwa kushirikiana na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara, (UNCTAD). Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya SAGCOT CTF, Dk. Rosebud Kurwijila na Katibu Mtendaji wa mfuko, John Kyaruzi.
  Baadhi ya wafugaji wakifanya wakijadiliana wakati wa  semina ya wafugaji inayolenga kuwainua kiuchumi wafugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoani Njombe iliyoandaliwa na  Mfuko wa SAGCOT CTF.

Na Mwandishi wetu Njombe 

WAFUGAJI wa ng’ombe mkoani Njombe wamepewa changamoto kufanya ufugaji kilimo kibiashara ili kuongeza uzalishaji na ubora wa maziwa utakaoweza kuinua kipato chao imeelezwa mkoani humo jana.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya Mfuko Kichocheo wa Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT CTF), Dr Rosebud Kurwijila, wakati akizungumza na baadhi ya wafugaji wa mkoa huo kwenye semina ya siku tano ya Kilimo Ufugaji Biashara (FAAB)  iliyoandaliwa na SAGCOT CTF kwa kushirikiana na Kiwanda cha Maziwa Njombe pamoja na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara, (UNCTAD ikiwa na lengo la kuinua kipato  kutokana na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa kibiashara.  

Alisema hii ni semina ya nne kutolewa nchini Tanzania kwa uratibu wa Mfuko wa SAGCOT CTF  na UNCTAD mara ya kwanza ikiwa ni mkoani Tanga 2015 mafunzo yakitolewa kwa awamu tatu yakiwa na madhumuni ya kuwafanya wafugaji wakulima wanaondokana na kilimo cha kujikimu.  

“Mfuko Kichocheo wa SAGCOT CTF unatoa ufadhili kwa wafugaji hao kupitia kiwanda cha kusindika maziwa cha Njombe ambapo mfuko ulifanya utafiti wa kujua nini mfugaji anahitaji kuinuka kiuchumi,” alisema.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT CTF, John Kyaruzi amesema kuwa sasa ni wakati wa wafugaji kutajirika kutokana na ufugaji na ndio maana ufadhili wa elimu hiyo utasaidia wafugaji kufuga kibiashara ambapo mahitaji makubwa ni kupata  ng’ombe mwenye uwezo wa kutoa maziwa kwa wingi.

“Wafugaji wengi wapo vizuri katika hatua ya kulisha mifugo yao lakini wanachokikosa ni elimu ya uchaguzi wa ng’ombe wazuri wa maziwa na hivyo Mfuko Kichocheo wa SAGCOT CTF  hautatoa mkopo wa pesa pekee kwa wakulima bali kuwawezesha kutoka na kile mfugaji atakacho,” alisema. 


Katibu Mtendaji huyo wa SAGCOT CTF aliongeza kuwa elimu hiyo ni muhimu kwani itasaidia wakulima wafugaji kutambua kuwa kilimo ni biashara huku pia wakipewa mbinu ya kupunguza gharama katika ufugaji wa ngo’mbe wa maziwa kibiashara na kwa matumizi yao hivyo kukuza uchumi wa mkulima mmoja mmoja,  jamii na pia kujenga afya zao kutokana na kutumia maziwa bora. 

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Iluminata Mwenda alisema kuwa wafugaji hao watumie vizuri fursa hiyo kwa kuwa wanaletewa elimu ya kuwa na uchumi mzuri na kuwa wafugaji wakifanya vizuri halmashauri nayo itaongeza kipato chake kwa kuwa na kiwanda cha maziwa kinachozalisha kwa wingi.

Nao baadhi ya wafugaji wameishukuru SAGCOT CTF, UNCTAD pamoja na washirika wengine waliofanikisha semina hiyo kwani kupitia mafunzo hayo wanaweza kuwa ufugaji wenye tija kwa ajili ya kuinua kipato na kuboresha afya zao.

Mfuko wa SAGCOT CTF ulianzishwa Mei 2011 chini ya sheria ya wadhamini ya Mwaka 2002 chini ya Mpango Shirikishi wa Uchumi nchini (PPP), kuchochea maendeleo katika sekta ya kilimo nchini. Katika kufikia malengo mfuko ulitafuta wabia muhimu kufikia azma hiyo hivyo Shirika la UNCTAD ni mshirika wake katika kutoa utaalamu elekezi. (technical assistance).

Abu Dhabi yaendelea kujihimarisha katika kukuza sekta ya utalii, Uarabuni.

$
0
0

Abu Dhabi. Kutokana na utamaduni uliojengeka kwa nchi za Falme za Kiarabu, uwapo wa vivutio na ukarimu kutoka kwa wenyeji ni mambo ambayo yameifanya Abu Dhabi kuwa sehemu muhimu kwa utalii.


Milango imefunguliwa na watalii wanakwenda kujionea vivutio, huku wakiwa na uhakika wa kupata huduma nzuri za malazi, kujionea ukanda wa jangwa na huduma bora za hoteli.

Miaka ya nyuma Abu Dhabi ilikuwa na baadhi ya vivutio na jangwa walikokuwa wanaishi makabila wazawa na nyumba zao za kiasili wakiwa wamezungukwa na vivutio vya kiasili.

Uchumi wao ulitegemea zaidi uvuvi na kilimo cha chikichi. Pia, kulikuwa na nyumba zisizozidi 300 ambazo zilijengwa kiasili.

Hivi sasa Abu Dhabi ambao ndio mji mkuu wa Nchi za Falme za Kiarabu umejiimarisha kwenye ukanda wa Mashariki ya Kati na kuwa mji maarufu kwa utalii. Jambo hilo halikuwa rahisi kutokana na historia ya eneo hilo hususan kwenye utamaduni na vivutio vya asili.

Kukua kwa kasi kwa jiji hilo ni kutokana na kutunza, kuhifadhi na kutangaza utamaduni wake wa kipekee na vivutio vya kale. Kwa maana hiyo imekuwa jambo rahisi kuhimarisha utajiri wa vivutio vya kale na sasa wageni wanaotembelea wameongezeka kujionea vivutio vya kitalii.

Kuwapo kwa uvumbuzi wa mafuta katika eneo hilo, kumewezesha ukuaji wa mji huo kuwa wa kisasa zaidi na kuwavutia wageni kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni wakiwa na shauku ya kuona mambo ya kale na ya kisasa.

Ni juhudi za kipekee za uongozi wa hususan Rais wa Falme za Kiarabu ambaye pia ni kiongozi wa Abu Dhabi, Mtukufu Sheikh Zayed Bin Sultan Al Nahyan kwa kuimarisha maendeleo ya miundombinu.

Kwa kutambua mchango wa sekta ya mafuta, Abu Dhabi imekuwa ikipunguza kiwango cha uchafuzi wa mazingira ili kutoathiri shughuli za kiuchumi kwa wananchi wake.

Mpango wa maendeleo wa Serikali wa mwaka 2030 ni kuwekeza kwenye utalii, usafirishaji, afya na elimu. Sekta ya utalii ndiyo inategemewa kwa kukuza uchumi wa nchi ikiwa ni matarajio ya kuhudumia wageni milioni 2.8 kwa mwaka na matarajio ya mwaka huu ni kuhudumia wageni milioni 2.

Shirika la Maendeleo ya Elimu na Utamaduni Duniani UNESCO) limeitambua Abu Dhabi kuwa sehemu muhimu kwa vivutio vya asili na kiutamaduni kama vile uwapo wa jangwa, miamba, milima mirefu na chemchemi za tranguil, pwani yenye kilometa zaidi ya 400 na vitu ambavyo vimetengenezwa kuwavutia wageni.
​Vivutio.
Mgeni awapo Abu Dhabi anaweza kujifunza mambo mbalimbali ya kiutamaduni na kuelewa mambo ya kale; historia na desturi za wenyeji. Wageni wanaweza kutembelea maeneo ya kale, ngome pamoja na msikiti mkubwa duniani, chemchem za kuvutia, kambi za jangwani, kuona wanyama kama ngamia.

Sekta ya utalii nchini humo inaendeshwa kwa umakini na kusimamiwa na Mamlaka ya Utalii na Utamaduni Abu Dhabi (TCCA Abu Dhabi), ikiwamo kuendesha hoteli zenye hadhi ya juu ulimwenguni na nyumba ambazo zinakidhi matakwa ya wageni. Pia, inahakikisha waongozaji watalii wanafanya kazi yao kwa weledi na ufanisi kwa kila mgeni anavyopenda ahudumiwe.

Abu Dhabi pia imekuwa mwenyeji mikutano mikubwa ya kimataifa kwa kuwa mwandaaji au mwanzilishi ikiratibiwa na TCA Abu Dhabi. Miongoni mwa mikutano hiyo ni iliyohusu watalii, chakula, matembezi ya familia, utamaduni na maonyesho ya sanaa.

Familia ya Kifamle imekuwa madarakani Abu Dhabi tangu 1793, wamewezesha kuifanya jamii kuwa ya kisasa zaidi kwa kuimarisha heshima miongoni mwa jamii jambo ambalo limeweka msingi wa utamaduni waliorithi tangu awali.

Kutokana na kuheshimu utamaduni wake, watu wa Falme za Kiarabu wamekuwa miongoni mwa jamii zenye utamaduni unaofahamika ulimwenguni jambo linalofanya kuwa sehemu muhimu kwa utalii.

Ni mji miongoni mwa miji ya Falme za Kiarabu wenye idadi kubwa ya watu. Ongezeko la watu kwa sasa inakadiriwa kuwa milioni 2.3 na inaweza ikafikiwa watu milioni 3 kwa mwaka 2030.

Hali ya hewa ya Abu Dhabi ni ya kitropiki. Hali ya mawingu na joto kwa kiwango cha juu huwa linajitokeza katika vipindi vya mwaka. Mvua hunyesha hasa kipindi cha baridi kati ya Novemba na Machi ikikadiriwa kipimo cha 12cms kwa mwaka.

Mvua hunyesha hasa katika mji wa Oasis wa Al Ain ukiwa ni mji wa pili kwa ukubwa. Kutokana na mgandamizo wa hali ya hewa kwenye milima ya Hajal joto hukadiriwa kufikia 13c (50F) kipindi cha baridi hasa nyakati za usiku, na kiangazi hufikia 42C (118F) wakati wa usiku hufikia hadi 13C na 56F muda wa usiku.

Wakazi wa Falme za Kiarabu ni takribani asilimia 20 tu ya jumla ya watu wote mjini humo kutokana na uwepo wa watu wengi kutoka mataifa mbalimbali.

Dondoo kuhusu usafiri wa kuelekea Abu Dhabi
​Ndege aina ya Airbus A340-541 ya Shirika la Ndege la Etihad.

Unaposafiri kuelekea Abu Dhabi, Shirika kuu la Ndege linalosifika kwa ubora ni "Etihad Airways" ambalo linatoa huduma bora na za kisasa. Shirika hilo ni la pili kwa ukubwa katika nchi za Falme ya Kiarabu nyuma ya Emirates,lenye makao makuu katika mji wa Khalifa, Abudhabi.

Ni hivi karibuni tu Shirika hilo lilizundua safari za kila siku kati ya Dar es salaam na Abudhabi ambapo Shirika linatoa huduma kupitia ndege zake mbili ambazo ni Airbus A320 yenye nafasi 16 katika daraja la kwanza na daraja la kati nafasi 120. Huduma mpya imelenga kuwapa fursa wasafiri kwa safari za moja kwa moja kati ya Jiji la Dar es Salaam na Abu Dhabi.

Dar es Salaam ni eneo ambalo watalii hufika ili kuweza kutembelea maeneo ya kitalii na kihistoria. Watalii wengi wa mataifa mbalimbali hufika kwa lengo la kutembelea maeneo ya kitalii ikiwamo Mlima Kilimanjaro, Mbuga ya Wanyama Serengeti na visiwa vya Zanzibar.

Mji wa Abu Dhabi ni wa kwanza kwa ukubwa katika shirikisho la falme za Kiarabu kwenye rasi ya Uarabuni. Mwaka 2000 kulikuwa na wakazi zaidi ya 1,000,000. Mji huo mkubwa umejengwa kwenye kisiwa karibu na mwambao.

Takriban 80% ya wakazi si wazalendo bali ni wageni. Mwaka 1970 ulikuwa ni mji mdogo uliokuwa umesheheni nyumba za matofali na matope.

Lakini baada ya kupatikana kwa fedha za mafuta mji huo uliendelezwa kwa kasi na nyumba zote zilijengwa upya huku nyingi zikiwa ni za ghorofa.

Maeneo ya Falme za Kiarabu pamoja na Qatar na Bahrain yalikuwa yanamilikiwa na makabila madogo na waliokuwa chini ya machifu wao.

Tangu 1820 walikuwa na mikataba na Uingereza walipoahidi kuachana na uharamia na kushirikiana kiulinzi na Uingereza. Ulinzi huo ulizuia uvamizi wa Saudia katika karne ya 20.

Falme hizo zilikuwa chini ya Uingereza hadi mwaka 1971, ambapo madola hayo madogo yalipata uhuru. Saba kati yake yaliungana kwa jina la Falme za Kiarabu.

PROF. MBARAWA AFUNGUA MKUTANO WA NNE WA WADAU WA SIMU

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akifungua mkutano wa nne wa Chama cha Kampuni za Simu Duniani, GSMA Mobile 360, jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa mkutano wa nne wa Chama cha Kampuni za Simu Duniani, GSMA Mobile 360 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya  wajumbe wa  mkutano wa nne wa Chama cha Kampuni za Simu Duniani, GSMA Mobile 360, wakifatilia mada jijini Dar es Salaam.

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezungumzia umuhimu wa wananchi wa mjini na vijijini kutumia simu ili waweze kunufaika na huduma mbalimbali za kimtandao zinazotumika hapa nchini.

Akizungumza mara baada ya kufungua mkutano wa nne wa kimataifa wa chama cha kampuni za simu duniani GSMA mobile 360, Prof . Mbarawa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha miundombinu ya mawasiliano ya simu inawafikia wananchi wote ili kuwezesha kunufaika na huduma za simu za kisasa.

‘Ili wananchi waweze kupata maendeleo kwa haraka  na kunufaika na fursa za kimtandao katika masuala ya elimu, biashara, kilimo, afya na ustawi wa jamii kwa ujumla kunahitajika uwepo wa simu za kisasa zinazoweza kuruhusu mifumo ya kimawasiliano’, Amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Ameitaja mifumo hiyo kuwa ni Elimu Mtandao, Afya Mtandao, Biashara Mtandao,  Kilimo Mtandao, Serikali Mtandao, Hali ya Hewa Mtandao ambavyo kwa pamoja  vitamhudumia mwananchi kwa ubora na wakati.
Amesisitiza kuwa serikali inashirikiana kwa karibu na kampuni  za mawasiliano ya simu ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha huduma za simu zinakuwa za uhakika na salama.

Serikali inaendelea kuhakikisha kwamba mfuko wa Mawasiliano Vijijini unaendelea kunufaisha watanzania na mkakati wa kuhakikisha umeme unafika vijijini unaimarika sambamba na uwepo wa simu za kisasa za bei nafuu.

Takribani laini za simu milioni 39.9 nchini zinatumika katika huduma mbalimbali na hivyo huchangia uchumi wa nchi.

Waziri Prof. Mbarawa amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji ili kukuza sekta ya mawasiliano hapa nchini ambapo hadi sasa tayari kilomita 18,000/- za mkongo wa taifa wa taifa wa mawasiliano zimejengwa hapa nchini.

 “Serikali itaendelea kudhibiti vifaa vya mawasiliano visivyo na ubora ili visiingie nchini na hivyo kuhakikisha watumiaji wa mitandao ya simu wanakuwa salama na wanaitumia mitandao hiyo kwa wakati wote’. Amesisitiza Prof. Mbarawa.

Mkutano huo wa siku mbili ambao pia umehudhuriwa na Naibu Waziri Mkuu wa Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Bw. Thomas Luhaka ambapo pamoja na mambo mengine utajadili Changamoto mbalimbali na kuja na suluhisho na namna bora ya kuendeleza Sekta ya Mawasiliano duniani.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA MJINI DODOMA LEO.

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Julai, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Frannie Leautier katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma, ambapo ameishukuru benki hiyo kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Tanzania  hususani kutoa mikopo iliyowezesha ujenzi mkubwa wa barabara.

Pamoja na kuishukuru AfDB Rais Magufuli ameiomba benki hiyo kuendelea kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa mipango na miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mpango mkubwa wa uzalishaji wa nishati ya umeme utakaofanikisha ujenzi wa viwanda, ujenzi wa barabara zinazounganisha ndani na nje ya Tanzania na kuunga mkono juhudi za kukabiliana na rushwa.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa AfDB Dkt. Frannie Leautier amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa alizozianza katika kujenga uchumi wa Tanzania, kukabiliana na rushwa na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya serikali na ameahidi kuwa benki hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa kutoa mikopo ya masharti nafuu itakayofanikisha mipango na miradi mbalimbali ya Tanzania.

"Tanzania ni nchi ambayo inapata fedha kuliko nchi zote za Afrika katika mpango wa AfDB kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Afrika,  hizi ni fedha ambazo zinatolewa kwa mkopo nafuu zaidi kuliko mikopo mingine" Amesema Dkt. Frannie Leautier.

Dkt. Frannier Leautier amebainisha kuwa AfDB inatarajia kuwa Tanzania itanufaika kupitia vipaumbele vitano vya benki hiyo ambavyo ni kusaidia uzalishaji wa nishati, utangamano wa bara la Afrika, maendeleo ya viwanda, usalama wa chakula na kuboresha hali ya maisha.

Aidha, Makamu wa Rais huyo wa AfDB amesema kuanzia mwakani benki hiyo imepitisha miradi mikubwa mitatu kwa ajili ya Tanzania ambayo ujenzi wa nyumba ya makazi, utoaji wa mikopo vijijini kwa ajili ya kuendeleza kilimo na maeneo ya uchumi kupitia benki ya CRDB na kukiendeleza Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Nelson Mandela kilichopo Arusha ambapo benki hiyo itatoa Dola za Marekani Milioni 4.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Mwakilishi Mkazi wa AfDB Dkt. Tonia  Kandiero, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
26 Julai, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier aliyemtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016. Kushoto ni ni Mwakilishi wa Benki hio nchini, Bi. Tonia Kandiero
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimewangalia  Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier akisaini kitabu alichotunga kabla ya kumkabidhi Rais alipomtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipokea kitabu kutoka kwa   Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier alipomtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier  na ujumbe wake aliyemtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016. Wa tatu kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, wa tatu kulia ni Mwakilishi wa Benki hio nchini, Bi. Tonia Kandiero, kulia ni Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Fedha za Nje Bw. Johannes Jovin akifuatiwa na Mkrugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara mambo ya Nje Balozi Celestine Mushy. Kushoto ni Mshauri wa Rais Masuala ya Profesa Longinus Rutasitara akifuatiwa na Mshauri wa Rais masuala ya Diplomasia Balozi Zuhura Bundala.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Frannie Leutier aliyemtembele Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Julai 26, 2016. Katikati ni Mwakilishi wa Benki hio nchini, Bi. Tonia Kandiero

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WANADODOMA KUHUSU MIKAKATI YA KUHAMIA MAKAO MAKUU.

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wazee, wafanyabiashara ,  viongozi wa dini na wanachi wa Dodoma kuhusu mikakati ya serikali ya kuhamia Dodoma kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Julai 26, 2016. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Uledi Mussa, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana.

Baadhi ya wazee, wafanyabiashara, viongozi wa dini na wananchi wa Dodoma wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu mikakati ya serikali ya kuhamia Dodoma kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Julai 26, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa Dodoma baada ya kuzungumza na wazee, viongozi wa dini, wafanyabiashara na wananchi wa Dodoma  kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Julai 26, 2016.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BENKI YA POSTA YAPATA FAIDA YA SH BILIONI 8.84 KABLA YA KODI KWA NUSU YA KWANZA YA MWAKA 2016

$
0
0

Sabasaba Moshingi akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye picha) juu ya Utendaji kazi wa Benki ya Posta kwa Nusu mwaka. Katikati ni Mkurugenzi wa Fedha Regina Semakafu na Mkurugenzi wa Sheria, Mystica Mapunda Ngongi. Benki ya Posta imepata faida ya shilingi bilioni 8.84 kabla ya kodi kwa nusu mwaka wa 2016.
Sabasaba Moshingi akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye picha) juu ya Utendaji kazi wa Benki ya Posta kwa Nusu mwaka. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha Regina Semakafu. Benki ya Posta imepata faida ya shilingi bilioni 8.84 kabla ya kodi kwa nusu mwaka wa 2016.


***********

NUSU ya kwanza ya Mwaka 2016 iliyoisha mwezi Juni, imekuwa yenye mafanikio makubwa sana kwa Benki ya Posta Tanzania (TPB). Pamoja na changamoto mbalimbali ambazo bado zinaikabili benki yetu, kwa kipindi kirefu sasa, lakini Benki imefanikiwa kupata faida kabla ya kodi ya shilling bilioni 8.84 ukilinganisha shillingi bilioni 5.48 zilizopatikana kipindi kama hicho mwaka 2015,ambayo ni sawasawa na ukuaji wa asilimia 61.47%.


Ukuaji huu wa faida katika kipindi hiki cha nusu mwaka wa 2016 umewezesha kukua kwa mtaji wa wawekezaji hadi kufikia shillingi billioni 48 kutoka shillingi bilioni 37 mwezi Juni mwaka 2015.

Mapato ya Benki kwa nusu mwaka 2016 yaliongezeka hadi kufikia shilling bilioni 42.5 kutoka bilion 34 iliyofikiwa nusu ya mwaka 2015, huu ni ukuaji wa asilimia 38%. Vilevile katika kipindi hichohicho amana za wateja ziliongezeka na kufikia shilingi bilioni 294.64 kutoka shilingi bilioni 263.68 June mwaka 2015, ukuaji wa asilimia 11.74%.


Mikopo imeongezeka hadi kufikia shillingi billioni 278 kutoka shilingi billioni 241.51 Juni mwaka 2015, ongezeko la asilimia 15.22%. Sehemu kubwa ya mikopo hii imetolewa kwa wafanyabiashara wadogowadogo pamoja na wafanyakazi wa sekta ya umma na serikali kuu.BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Rasilimali za benki zilikuwa hadi kufikia shilling 390.8 bilioni mwezi Juni mwaka huu 2016 kutoka shillingi billioni 333.96 Juni mwaka 2015 ongezeko la asilimia 17.16%.






Benki ya Posta kwa mwaka 2016, iliendelea na jitihada zake za kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi, mwanzoni mwa mwaka huu benki ilifungua tawi lake jipya la Songea, Mkoani Ruvuma, ambapo Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, pamoja na tawi la Babati Mkoani Manyara, ambapo mgeni rasmi alikuwa Msajili wa Hazina Bw.Lawrence Mafuru. 

Matawi hayo mawili yamejengwa kwenye viwanja vinavyomilikiwa na TPB. Benki ilihamishia Makao yake Makuu kutoka jengo la Extelecoms lililopo mtaa wa Samora na kuhamia kwenye Jengo la Millenium Towers, Kijitonyama.

Pia, benki imehamisha tawi lake la Moshi kwenda kwenye jengo jipya la NSSF, na hivi karibuni itahamisha matawi yake yaliyoko Kahama na Tanga kwenda kwenye majengo mapya na ya kisasa. Hizi zote ni jitihada za benki za kuongeza ufanisi na pia kutoa huduma zake kwenye mandhari bora naya kisasa zaidi.

Hadi hivi sasa TPB inayo matawi 30 na madogo (min branches) 30, Mashine za kutolea pesa (ATM) zinazo milikiwa na benki ya posta ni 38 na 200 za umoja wamabenki (Umoja switch), hivyo kuwawezesha wateja wetu kupata huduma ya pesa nchi nzima.

Pia benki inao mawakala wa benki 133 kupitia TPC,na vituo vya huduma 200 kupitia mawakala binafsi.Benki ya posta inaendelea na jitihada zake za kuongeza wigo wa biashara kwa njia mbalimbali, zikiwemo:

kutoa mikopo kwa vikundi vidogo vidogo (group lending), ambapo hadi sasa tumetoa mikopo ya kiasi cha shilingi 6.5 bilioni na huduma ya kuwakopesha wazee (wastaafu loan) kupitia mifuko ya jamii kama vile PSPF,NSSF na ZFF, ambapo hadi sasa tumetoa mikopo ya kiasi cha shilingi 56 bilioni.

Kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), enki imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi Milioni 541 ili kuviinua kiuchumi vikundi vilivyo chini ya Baraza hilo.Kufungua account za vikundi visivyo rasmi(VICOBA informal groups) ambapo hadi sasa akaunti 30 elfu zimefunguliwa.

Huduma za kibenki kupitia simu za kiganjani,ambapo kwa kipindi cha nusu ya mwaka huu akaunti 271,427 zilifunguliwa, kulinganisha na akaunti 236,981 zilizofunguliwa hadi mwishoni mwa mwaka jana. Hili ni ongezeko la akaunti 34,446, sawasawa na asilimia 15.

Benki ya Posta imejidhatiti kuendelea kutoa huduma bora, nafuu na za kisasa kwa maana ya kutumia teknolojia zaidi katika kipindi hiki. Tunaamini kwamba bado kwa kutumia teknolojia ya TPB POPOTE tutaweza kuwafikia Watanzania walio wengi hasa vijijini ambao bado hawajaingia kwenye mfumo wa kifedha.Pia benki itaendeleza na kuboresha mahusiano yake na makampuni za simu ili kuweza kupeleka huduma zake karibu zaidi na wananchi, na pia ushirikano wake na Saccos pamoja na Vicoba.

Benki ya Posta inapenda kuwashukuru wateja wake na Watanzania wote kwa ujumla kwa kutuamini na kuendelea kutumia huduma zetu. Tunaahidi hatutawaangusha, na tutaendelea kuboresha huduma zetu zenye gharama nafuu.

Pia shukrani za pekee ziende kwa Bodi ya Wakurugenzi kwa uongozi wao thabiti na usimamizi imara, unaoendelea kuhakikisha kuwa benki inakuwa miongoni mwa taasisi bora za kifedha hapa nchini.

DC MUHEZA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA TEULE MUHEZA,AWATAKA WATUMISHI KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA

$
0
0

MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akipofanya ziara ya kuitembelea hospitali ya Teule kuangalia changamoto zinazoikabili kulia ni Mganga Mfawizi wa Hospitali hiyo,Malahiyo Rajabu katikati ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza
Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyekaa kulia kuzungumza na watumishi wa Hospitali Teule ya Muheza
Mganga Mfawizi wa Hospitali Teule ya Muheza Malahiyo Rajabu akizungumza jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye hayupo pichani wakati alipofanya ziara ya kuitembelea hospitali hiyo

Mganga Mfawizi wa Hospitali Teule ya Muheza Malahiyo Rajabu kulia akitoa ufafunuzi kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto katikati ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza wakati mkuu huyo wa wilaya alipofanya ziara kwenye hospitali hiyo
kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Mhandisi,Hajat Mwanasha Tumbo akisisitiza jambo kwa DMO wa wilaya ya Muheza wa pili kutoka kushoto Dkt Elias Mayala wakati alipofanya ziara ya kuitembelea hospitali Teule ya Muheza
Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyevaa hijabu akiwa na baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Teule ya Muheza wakati alipofanya ziara kulia ni Mganga Mfawizi wa Hospitali hiyo Malahiyo Rajabu na anayefuata ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza .
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kutoka kulia aliyevaa hijabu akipata maelezo kutoka kwa mhudumu wa zama katika hospitali Teule ya Muheza kushoto mara baada ya kufanya ziara ya kuitembelea anayefuatia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Teule Muheza Mkoani Tanga,Malahiyo Rajabu kushoto akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo kabla ya kuingia kwenye chumba cha maabara wakati alipofanya ziara ya kuitembelea hospitali hiyo
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akitembea hospitali ya Teule wilayani humo kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo,Malahiyo Rajabu kushoto ni DMO wa wilaya ya Muheza,Daktari Elius Mayala

Kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Muheza,Malahiyo Rajabu akimueleza jambo Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo kuhusua namna wanavyofanya kazi kwenye maeneo mbalimbali ambaye alifanya ziara ya kushtukiza ya kuitembelea hospitali hiyo Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

WATEJA WAFURAHIA MICHUANO YA ICC INAYOONEKANA KUPITIA STARTIMES

$
0
0

Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka akizungumza na timu ya StarTimes na maveterani wa uwanja wa Mwembe Yanga – Temeke kabla ya mchezo wa kirafiki uwanjani hapo. StarTimes iliweka kambi uwanjani hapo ikiwa ni uzinduzi wa michuano ya ICC mwaka 2016 iliyokwishaanza kutimua vumbi Julai 22 wiki iliyopita ambapo ilidhamiria kuonyesha mchuano mkali wa ‘Manchester Derby’ uliopaswa kuchezwa jijini Beijing, China lakini kwa bahati mbaya ukaahirisha kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya na hivyo wateja wakapewa kutazama marudiano ya mchezo baina ya Manchester United na Borrusia Dortmund ambapo Dortmund waliibamiza United kwa magoli 4 - 1.

Baadhi ya wateja na mashabiki wa soka waliojitokeza kutazama mchezo wa ‘Manchester Derby’ uliopaswa kuchezwa jijini Beijing, China lakini kwa bahati mbaya ukaahirisha kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya na hivyo wateja wakapewa kutazama marudiano ya mchezo baina ya Manchester United na Borrusia Dortmund ambapo Dortmund waliibamiza United kwa magoli 4 - 1.

Mmoja wa wateja waliofika katika viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, akipata maelekezo juu ya huduma za StarTimes kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Na Dotto Mwaibale

Wateja wa StarTimes na watanzania kwa ujumla wameipongeza kampuni inayouza na kusambaza visimbuzi vya matangazo ya dijitali, Starimes, kwa kuwaletea michuano ya kombe la mabingwa kimataifa au ICC mwaka 2016 moja kwa moja kupitia chaneli yake ya ST WORLD FOOTBALL.

Hayo yalisemwa na wateja mbalimbali waliohudhuria tamasha la uzinduzi wa michuano hiyo iliyoanza katika viwanja vya Temeke, Mwembe Yanga.

Katika tamasha hilo StarTimes walitinga viwanjani hapo na timu kamili ya wafanyakazi wake wa vitengo mbalimbali ambapo pia walifunga luninga uwanjani ili kuonyesha moja kwa moja mtanange wa watani wa jadi kutoka jiji la Manchester unaojulikana kama ‘Manchester Derby’ uliopangwa kufanyika jijini Beijing China lakini kutokana na hali ya hewa mbaya ikabidi uahirishwe.
 
Akizungumza katika viwanja hivyo Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka alibainisha kuwa, “Siku ya leo tumefika viwanjani hapa kwa lengo kubwa la kutaka kuwapa fursa wateja wetu kujionea uhondo wa michuano ya ICC inayonekana moja kwa moja kwenye visimbuzi vyetu. Michuano hii inayofanyika katika nchi ya Marekani, Ulaya, Australia na China inazishirikisha timu kubwa duniani kama vile Real Madrid, Barcelona, Manchester United na City, Juventus, Chelsea, Liverpool na nyiginezo.”

“Michuano hiyo imekwishaanza tangu Ijumaa ya wiki iliyoishia ambapo tumekwishashuhudia tayari timu kama Manchester United, Borussia Dortmund, Celtic, Leicester City, Inter Milan na PSG zimekwishatinga uwanjani. Siku ya leo tumekuja hapa kwa lengo la kuonyesha Manchester Derby lakini tunasikikita kuwa mchezo huo umeahirishwa kutokana na hali ya hewa mbaya kulikumba jiji la Beijing ambamo mchezo huo ulipangwa kuchezwa. Lakini badala yake tunaonyesha mchezo wa marudio baina ya Manchester United na Borussia Dortmund.” Aliongezea Bw. Kisaka

Meneja huyo wa Mauzo alimalizia kwa kusema, “Ningependa kuchukua fursa hii kwa kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kufurahiamichuano hii mikubwa zaidi ambayo ni ya awali au maandalizi kabla ya ligi kuu mbalimbali kuanza mwishoni mwa mwezi wa Agosti.

StarTimes pia tunaonyesha ligi hizo ambapo wateja watafurahia mechi zote za ligi za Bundesliga na Serie A kupitia chaneli zetu za michezo za SPORT ARENA, SPORTS FOCUS, WORLD FOOTBALL, SPORT LIFE NA SPORT PREMIUM na bila kusahau ligi za Ufaransa na Ubelgiji kupita chaneli ya FOX SPORTS.

Ili kufaidi michuano hii ya ICC mwaka 2016 wateja itawabidi kulipia malipo kiduchu ya kifurushi cha Mambo kwa shilingi 12,000/- tu na kuweza kutazama mechi zote moja kwa moja ambazo zitarajiwa kuisha Agosti 13.”

Michuano ya ICC mwaka 2016 imekwishaanza Julai 22 ambapo mechi ya kwanza iliyofungua pazia ilikuwa ni kati ya Machester United na Borrusia Dortmund ambapo Dortmund iliibamiza United kwa mabao 4 – 1. Michezo mingine iliyokwishachezwa ni pamoja na PSG kuitandika 3 -1 Inter Milan na Leicester City kuwashinda Celtic kwa mikwaju 6 – 5 ya penati baada ya kutoshana nguvu kwa kufungana magoli 1 – 1 ndani ya dakika 90.

Siku ya leo Jumanne kutakuwa na mechi nyingine ambapo mabingwa wa Italia, Juventus watashuka dimbani kuwakabili timu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza katika mishale ya saa 7 mchana kwa muda wa hapa nyumbani Tanzania kupitia chaneli ya WORLD FOOTBALL ndani ya ya StarTimes pekee.






(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

KAMPUNI YA MGODI WA GEITA GOLD MINING (GGM) YAFANIKISHA ZOEZI LA KUKUSANYA PESA KWA AJILI YA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI.

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Moshi Kipi Warioba akiongozana na kundi la wapanda mlima Kilimanjaro kutoka kampuni ya Mgodi ya Geita Gold Mining (GGM) waliopanda kwa lengo la kuchangisha fedha za kusaidia taasisi mbalimbali zinazo shughulika na mapambano dhidi ya Ukimwi. Makamu wa Rais wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM) ,Simon Shayo akizungumza wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya kundi la wapanda mlima wakiwemo wafanyakazi wa mgodi huo waliopanda kwa leongo la kuchangisha fedha za kusaidia taasisi mbalimbali zinazo shughulika na mapambano dhidi ya Ukimwi. Kiongozi wa kundi la wafanyakazi wa kampuuni ya Mgodi ya Geita Gold Mining ,Kelvin Yasiwa akizungumza kwa niaba ya wenzake mara baada ya kuwasili wakitokea katika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro. Balozi wa Tume ya kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) Msanii Mrisho Mpoto akizungumza mara baada ya kurejea salama kutoka katika kilele cha Mlima Kilimanjaro. Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Kipi Warioba akikabidhi cheti kwa mtoto Lucy Mashauri(15)baada ya kufanikiwa kufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro. Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Kipi Warioba akikabidhi cheti kwa mtoto Jacob Musa (16) baada ya kufanikiwa kufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Balozi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) Msanii Mrisho Mpoto akifurahia baada ya kukabidhiwa cheti kwa kufanikiwa kufika katika moja ya vilele vya Mlima Kilimanjaro,kilele cha Stela .







Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kipi Warioba akikabidhi vyeti kwa washiriki wengine wa changamoto hiyo ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya Ukimwi.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kipi Warioba aliyekua mgeni rasmi katika hafla hiyo Kipi Warioba akizungumza mara baada ya kuwapokea wapandaji wa Mlima Kilimanjaro kutoka kampuni ya Mgodi ya Geita Gold Mining.



Washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengoo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia taasisi mablimbali zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya Ukimwi wakifungua "champagne" kuonesha furaha mara baada ya kurejea salama kutoka katika kilele cha Mlima Kilimannjaro.



Washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia taasisi mbalimbali zinazojihusisha na mapambano dhidi ya Ukimwi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa hafla ya mapokezi yao,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Kipi Warioba.

Watoto Yatima ambao ndio pekee walioshiriki katika changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro na kufika Kileleni wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kipi Warioba pamoja na viongozi wengine akiwemo Makamu wa Raisi wa kampuni ya Mgodi wa Geita Gold Mining,(GGM).

Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mgodi wa Geita Gold Mining (GGM) Simon Shayo akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mapokezi ya washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi.




Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.

NEWZ ALERT:KOFFI OLOMIDE AHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI 18 BAADA YA KUKUTWA NA HATIA YA KUMDHALILISHA DANSA WAKE

$
0
0
Mwanamuziki wa Kimataifa wa Miondoko ya Dansi kutoka Nchini Congo, Antoine Christophe Agbepa Mumba maarufu kama "Koffi Olomide" amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela baada ya kuonekana na hatia ya kumdhalilisha kwa kumpiga dansa wake wakati wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nchini Kenya hivi karibini.

Mwanamuziki huyo alikamatwa mapema leo akiwa nyumbani kwake katika mji wa Kinshasa na kupelekwa Mahakamani moja kwa moja na kukutwa na hatia hiyo.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya ushahidi huo kuonekana akimpiga dansa wake na atatakiwa kuitumikia adhabu hiyo kwani hajapewa nafasi ya kulipa faini ya aina yoyote ile.

hatua ya kumkamata Mwanamuziki huyo ilifikiwa baada ya kuanzishwa kwa kampeni ya baadhi ya wadau wa maswala ya kijamii wakiongozwa na Zakarie Bababaswe aliyefungua kesi kwa niaba ya Serikali ikiwa ni madai ya udhalilishaji kwa dansa wake, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Kongo, kuamua kukamatwa kwake na kusema anataka haki itendeke.

CHINI NI VIDEO INAYOONYESHA TUKIO HILO.

WASANII WA FILAMU KUNUFAIKA NA MFUMO MPYA

$
0
0

Na Beatrice Lyimo -MAELEZO

WASANII wa Filamu nchini wanatarajia kunufaika na kazi zao kufutia makubiliano ya Kampuni ya Star Media Tanzania Ltd (Startimes), pamoja na Steps Entertainment za kutumia kazi zao kwenye vituo vya televisheni nchini.

Akizungumza waandishi wa habari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Sibuka Media, Dkt. George Nangale alisema kazi hiyo itafanywa kwa ushirikiano na taasisi hizo ili kuweza kuwasaidia wasanii kunufaika na kazi zao kupitia luninga badala ya kuwasubiri wateja wao kuzinunua katika santuri (DvD).

“Tumefikia uamuzi huu baada ya kuona ombwe lililopo sasa katika kuzifikisha filamu zetu kwa walio wengi pamoja na kwamba Watanzania wana mwamko mkubwa wa kuzitazama filamu hizi zenye mafunzo ya maisha na burudani” alisisitiza Mkurugenzi huyo.

Kwa upande wake Msanii wa Bongo Movie, Mwanaheri Hamad alisema uonyeshaji wa kazi zao katika vituo vya televisheni utawanufaisha wasanii chipukizi ambao kazi zao bado hazijaonekana.Amesema kuwa kutokana na mkataba huo wa kurusha filamu hzo umerahisisha soko za kazi hizo katika mfumo DvD ambapo ulikuwa unatumiwa hapo awali.

Filamu hizo zitaonyeshwa kupitia king’amuzi cha StarTimes chaneli 111 ikijulikana kama Sibuka Maisha Steps chaneli kila siku na itaanza kuonyeshwa Ijumaa hii tarehe 29 Julai, 2016.

Msemaji kutoka kituo cha Sibuka Televisheni wa kwanza kulia Bw. George Nangale akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa kipindi cha INABAMBA “Ni bongo movie bandika bandua” kitachokuwa kinaonyeshwa katika kituo hiko cha matangazo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, kushoto ni Afisa habari wa kampuni ya Step Entertainment Bw. Moses Mwanyilu
Mkurugenzi wa matamasha kutoka kampuni ya usambazaji filamu nchini Steps Entertainment katikati Bw. Jonas Sabuni akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa kipindi cha INABAMBA “Ni bongo movie bandika bandua” ambao uliofanyika leo jijini Dar es salaam, kushoto ni Afisa habari wa kampuni hiyo Bw. Moses Mwanyilu na kulia ni mwigizaji wa bongo movie Jimmy Mafufu.
Afisa habari wa kampuni ya Step Entertainment Bw. Moses Mwanyilu wa kwanza kushoto akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa kipindi cha INABAMBA “Ni bongo movie bandika bandua” kitachokuwa kinaonyeshwa katika kituo cha matangazo Sibuka Televisheni uliofanyika leo jijini Dar es salaam,katikati ni , Msemaji kutoka kituo cha Sibuka Televisheni Bw. George Nangale na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Masoko kutoka Startimes Bw. Awino Felia .
Meneja Masoko kutoka Startimes Bw. Awino Felia wa kwanza kushoto akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa kipindi cha INABAMBA “Ni bongo movie bandika bandua” kitachokuwa kinaonyeshwa katika kituo cha matangazo Sibuka Televisheni kupitia king’amuzi cha Startimes uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

PICHA ZOTE NA ALLY DAUD-MAELEZO. 

TUZO ZA UBORA KIMATAIFA YA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA (TCAA)

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari (katikati) baada ya kukabidhiwa  tuzo ya kimataifa ya utoaji wa huduma za viwango vinavyokidhi  ubora wa kimataifa na Raisi wa kampuni ya Otherways, Charbel Tabet inayoendesha mashindano hayo, jijini Rome Italy.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imepokea tuzo ya kimataifa ya utoaji wa huduma za viwango vinavyokidhi ubora wa kimataifa, jijini Rome Italy Julai 25, 2016.

Kutolewa kwa tuzo hiyo kunafuatia mashindano yaliyohusisha zaidi ya makampuni 300 duniani ambayo yamesajiliwa na Shirika la Viwango la Kimataifa(ISO) na kupitia mchakato wa kupigiwa kura na hatimaye kupata washindi.

Meneja wa udhibiti wa viwangoTCAA, Magesa Sarota akielezea kuhusu tuzo hiyo alisema pamoja na mambo mengine mashindano hayo yanaangalia kampuni husika ni kwa namna gani inahakikisha inaendelea kutoa huduma zenye viwango katika masuala ya Uongozi pamoja na kuwa na mifumo inayohakikisha huduma wanazozitoa zinakidhi viwango.

Tuzo hiyo ya TCAA ilipokelewa na Mkurugenzi Mkuu Hamza Johari kwa niaba ya Mamlaka. Kupokelewa kwa tuzo hiyo ni heshima kwa Mamlaka na ni motisha ya kuendelea kutoa huduma zenye viwango vya wa kimataifa.

SIMBA APIGWA 2-0 NA JKT RUVU KATIKA FAINALI ZA FASDO FOOTBALL CUP JIJINI DAR.

$
0
0

Wakiwa wanalipokea rasmi kombe lao baada ya ushindi
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Humphrey Polepole (Kulia) akikabidhiwa zawadi ya picha kutoka taasisi isiyo ya kiserikali ya FASDO
Timu ya JKT Ruvu wakifurahi baada ya kuibuka washindi.
Mgeni rasmi katika fainali hizo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Humphrey Polepole akikabidhi kitita cha Tsh 2,000,000 kwa nahodha wa timu ya JKT Ruvu ambao ndio waliibuka kidedea.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Humphrey Polepole akikabidhi Kombe kwa timu ya JKT Ruvu baada ya kuibuka washindi.


Refa Bora katika mashindano ya mpira wa miguu ya FASDO akikabidhiwa zawadi ya Kitita chake cha Laki moja
Washindi wa pili katika Mchezo huo timu ya Simba wakiwa wanapokea zawadi yao ya Tsh 1,000,000





Timu ya Simba chini ya Umri wa Miaka 20 wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mpira kuanza dhidi ya JKT Ruvu




Timu ya JKT Ruvu chini ya umri wa miaka 20 wakiwa katika picha ya pamoja kabla mechi haijaanza dhidi ya Simba




Mkurugenzi mtendaji wa Faru Arts and Sport Development Organization (FASDO) Tedvan Chande Nabora akikagua timu zote mbili kabla ya mpira haujaanza








Mpira ukiwa unaendelea huku ikiwa ni vuta nikuvute ambapo JKT Ruvu waliibuka washindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba, pia simba walikosa penalti.




Mgeni Rasmi katika Mashindano ya mpira wa Miguu wa FASDO, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Humphrey Polepole akiwa anafuatilia Mchezo huo




Mashabiki wa upande wa Simba wakifuatilia kwa makini Mchezo huo




Mashabiki upande wa JKT Ruvu wakiwa wanafuatilia kwa makini mchuano huo






Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Humphrey Polepole akionesha kombe pamoja na zawadi ya mshindi wa kwanza kiasi cha Tsh 2,000,000 wakati wa fainali hizo, zilizofanyika katika viwanja vya JMK jijini Dar
 

Serikali yatenga bilioni 1.6 kwa ajili ya uanzishwaji wa mfumo wa kielekroniki wa kusajili wakazi.

$
0
0


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI Injinia Mussa Iyombe akiongea na wanahabari wakati wa kupokea maendeleo ya mfumo wa kuboresha upatikanaji wa taarifa sahihi katika serikali za mitaa, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Kata ya Mapinga Wilaya ya Bagamoyo Ibrahimu Mbonde akiongea jambo wakati wa kupokea maendeleo ya mfumo wa kuboresha upatikanaji wa taarifa sahihi katika serikali za mitaa, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Sensa ya Watu na Mkazi Hajjat Amina Mrisho Said akiongea jambo wakati wa kupokea maendeleo ya mfumo wa kuboresha upatikanaji wa taarifa sahihi katika serikali za mitaa, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Benjamin Sawe- Maelezo)
Benjamin Sawe -Maelezo Dar es Salaam.

Serikali imetenga Jumla ya shilingi bilioni 1.6 kupitia ofisi ya Taifa ya Takwimu na wafadhili wametoa shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya uanzishwaji wa mfumo wa kielekroniki wa kusajili wakazi Tanzania .Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- TAMISEMI Injinia Mussa Iyombe wakati wa kupokea maendeleo ya mfumo wa kuboresha upatikanaji wa taarifa sahihi katika serikali za mitaa.

Injinia Iyombe alisema mfumo huo unalenga kuwa na kanzi data ya watu wote nchini kiumri, uraia, jinsia, hali ya ulemavu, hali ya elimu, shughuli za kiuchumi, uhamaji na uhamiaji ikiwa ni pamoja ikiwa na vizazi na vifo.

“Taarifa hizi zitaisaidia serikali na wadau wengine kujibu maswali ambayo wengine tumekuwa tukijiuliza kila siku”.Alsema Injini Iyombe. Alisema katika kutekeleza malengo Endelevu ya Maendeleo ya Mwaka 2030 serikal;I haina budi kuhakikisha wananchi wanaandikishwa katika rejesta ya wakazi ili iweze kuwafahamu mahitaji yake.

Aliongezea kuwa mfumo huo utasaidia upatikanaji wa idadi kamili ya wanafunzi waliopo mashuleni na kiasi gani cha fedha kinachotitajika kupelekwa shuleni, upatikanaji wa hali halisi ya uandikishaji wa watoto katika shule za msingi, mahudhurio shuleni na idadi ya walimu na taarifa nyingine.

Alisema kwa upande wa TAMISEMI mfumo huo utasaidia kuwagundua wazazi ambao hawana nia nzuri ya kuwapeleka watoto kuandikishwa kupitia katika kata zao kwa kutumia Global Positioning System za kaya zao katika ramani.

Akielezea faida za mfumo huo Injinia Iyombe alisema utaiwezesha serikali kufahamu idadi kamili ya watu wake kiumri na kijinsia kwa kuwa kazi hiyo itakuwa endelevu na itafanyiwa kazi kila siku na maafisa watendaji wa vijiji na mitaa kwa Tanzania nzima kwa kutumia teknolojia ya simu.

Aidha mfumo huo utaipa fursa Ofisi ya Takwimu ya kuwa na takwimu bora ambazo zitaipunguzia gharama ya kufanya tafiti za kila baada ya miaka mitatu, mitano hata kumi ikiwa ni pamoja na kupunguza maswali mengi ambayo huulizwa wakati wa sensa wa watu na makazi ambayo itafanyika tena hapa nchini mwaka 2022.

Diwani wa Ilala atoa wito kwa Serikali kuisaidia Dar Festival

$
0
0

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Diwani wa Kata ya Ilala, Saady Khimji ametoa wito kwa Serikali na Mashirika binafsi kuisaidia Kampuni ya Dar Festival ili Iweze kufanya tamasha la kutangaza utamaduni wa nchi ya Tanzania.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Diwani huyo ambaye pia ni Mlezi wa Kampuni hiyo alipokuwa akilitangaza rasmi tamasha hilo mbele ya waandishi wa habari. Khimji amesema kuwa ni jambo jema kuona vijana wanazungumzia suala la utamaduni kwani hali hii inaonyesha dhahiri kuwa wameamua kuirudisha nchi kwenye mstari wa kujali utamaduni wetu.

“Mataifa yote makubwa yanajali tamaduni zao hivyo ni vema na sisi kama watanzania kuamua kwa dhati kuhakikisha tunarudisha utamaduni wetu, jambo hili sio dogo linahitaji fedha nyingi kwahiyo, tunaomba msaada kutoka kwa Serikali na Mashirika binafsi ili kufanikisha tamasha hili”, alisema Khimji.

Diwani huyo ameongeza kuwa vijana hao wamejitahidi hadi hapo walipofika lakini kama wakikosa misaada kutoka kwa wadhamini mbalimbali basi tamasha hilo halitoweza kufanikiwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Faridi Faradji amesema kuwa wameamua kuisaidia Serikali kwa kuangalia njia mbadala ya kukusanya mapato kwa kutangaza utamaduni wa Tanzania kupitia tamasha hilo. “Kwa namna moja au nyingine,tuna kila sababu ya kuisaidia nchi yetu kukusanya mapato ili iweze kuendelea kwasababu baadhi ya nchi zingine zimeweza kuendelea kupitia matamasha kama haya”, alisema Faradji.

Naye Katibu wa Kampuni hiyo, Amini Kingazi amesema kuwa tamasha hilo ni la asili kwahiyo wameamua kulifanyia katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kwa sababu ni eneo lenye vitu vingi vinavyoonyesha utamaduni wa kitanzania.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika kila mwaka, Kwa mara ya kwanza litafanyika mwezi Septemba mwaka huu likijumuisha vitu vyenye asili ya kitanzania kama vyakula vya kitanzania, mashindano ya michezo ya kiasili pamoja na wanamuziki wa kitanzania.

Kipindi maalum cha Rais wakati akihutubia siku ya Mashujaa dodoma Julai 25, 2016

Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images