Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 915 | 916 | (Page 917) | 918 | 919 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Bi. Sadaka Gandi (mbele) mmoja wa wawasilishaji mada katika semina hiyo akizungumza jambo kwa baadhi ya wanahabari. Semina hiyo kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadhi ya wanachuo iliandaliwa na Kampuni ya Bridge Tanzania Limited kwa kushirikiana na DUFA chini ya udhamini Mkuu wa Banki ya NMB, pamoja na wadhamini wengine wakiwemo PSPF, Crown Cartilage, ACCA na Clouds FM.
   Baadhi ya washiriki wa Semina hiyo kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadhi ya wanachuo iliandaliwa na Kampuni ya Bridge Tanzania Limited kwa kushirikiana na DUFA chini ya udhamini Mkuu wa Banki ya NMB, pamoja na wadhamini wengine wakiwemo PSPF, Crown Cartilage, ACCA na Clouds FM wakifuatilia mada anuani.
   Bi. Sadaka Gandi (mbele) mmoja wa wawasilishaji mada katika semina hiyo akizungumza jambo kwa baadhi ya wanahabari. Semina hiyo kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadhi ya wanachuo iliandaliwa na Kampuni ya Bridge Tanzania Limited kwa kushirikiana na DUFA chini ya udhamini Mkuu wa Banki ya NMB, pamoja na wadhamini wengine wakiwemo PSPF, Crown Cartilage, ACCA na Clouds FM.  Meneja wa Mafunzo na Maendeleo wa Benki ya NMB, Edith Mwiyombela (kulia) akiwasilisha mada kwenye Semina kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadhi ya wanachuo iliandaliwa na Kampuni ya Bridge Tanzania Limited kwa kushirikiana na DUFA chini ya udhamini Mkuu wa Banki ya NMB, pamoja na wadhamini wengine wakiwemo PSPF, Crown Cartilage, ACCA na Clouds FM. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Amina Abdul ambaye pia ni Mratibu wa Semina kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadhi ya wanachuo akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na wanahabari.
   Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB Kitengo cha Wateja Wadogo, Ally Ngingite akiwasilisha mada juu ya Matumizi Mazuri ya Fedha kwa washiriki. Mmoja wa waratibu wa semina hiyo akitoa mwongozo kwa washiriki. Semina hiyo kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadhi ya wanachuo iliandaliwa na Kampuni ya Bridge Tanzania Limited kwa kushirikiana na DUFA chini ya udhamini Mkuu wa Banki ya NMB. Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB Kitengo cha Wateja Wadogo, Ally Ngingite (kushoto) akimkabidhi zawadi mmoja wa wanafunzi baada ya kujibu swali kiufasaha.
   Baadhi ya washiriki wa Semina hiyo kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadhi ya wanachuo iliandaliwa na Kampuni ya Bridge Tanzania Limited kwa kushirikiana na DUFA chini ya udhamini Mkuu wa Banki ya NMB, pamoja na wadhamini wengine wakiwemo PSPF, Crown Cartilage, ACCA na Clouds FM wakifuatilia mada anuani.
   Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB Kitengo cha Wateja Wadogo, Ally Ngingite (kulia mbele) akiwasilisha mada juu ya Matumizi Mazuri ya Fedha kwa washiriki.
   Meneja wa Mafunzo na Maendeleo wa Benki ya NMB, Edith Mwiyombela (kulia) akiwasilisha mada kwenye Semina kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadhi ya wanachuo iliandaliwa na Kampuni ya Bridge Tanzania Limited kwa kushirikiana na DUFA chini ya udhamini Mkuu wa Banki ya NMB, pamoja na wadhamini wengine wakiwemo PSPF, Crown Cartilage, ACCA na Clouds FM.
   Baadhi ya washiriki wa Semina hiyo kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadhi ya wanachuo wakiwa kwenye banda la mdhamini mkuu wa semina hiyo kujifunza shughuli mbalimbali wanazofanya.
   Mmoja wa wasilishaji mada kutoka Kampuni ya Bridge Tanzania Limited akiwaelekeza wanasemina namna nzuri ya kutumia baadhi ya vifaa vya 'printer' na matumizi mazuri ya wino wa mashine hizo. Msanii nyota Nick Wa Pili akiwasilisha mada kwenye Semina kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadhi ya wanachuo iliandaliwa na Kampuni ya Bridge Tanzania Limited kwa kushirikiana na DUFA chini ya udhamini Mkuu wa Banki ya NMB, pamoja na wadhamini wengine wakiwemo PSPF, Crown Cartilage, ACCA na Clouds FM.
   Mmoja wa wasilishaji mada kutoka Kampuni ya Bridge Tanzania Limited akiwaelekeza wanasemina namna nzuri ya kutumia baadhi ya vifaa vya 'printer' na matumizi mazuri ya wino wa mashine hizo.


  0 0

  Mameneja wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza michezo mbalimbali katika Fukwe ya Milenium Bagamoyo Mkoani Pwani.
  Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufika katika ufukwe wa Milenium Bagamoyo Mkoani Pwani mwishoni wa wiki, Wafanyakazi hao ikiwa ni utamaduni wao wa kila mwaka kutembelea sehemu mbalimbali kwaajili ya kufurahi pamoja, kujenga mahusiano mazuri wakati wa kazi pamoja na kunywa na kula pamoja.

  Akizungumza na Globu ya Jamii, Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Killango amesema kuwa  wameamua kupumzika pamoja, kula na kunjwa pamoja mwishoni mwa wiki kwaajili ya kujenga mahusiano mazuri wakati wa kazi ikiwa ni siku mhimu sana kwao ambayo hufanyika kila mwaka.

  Katika Mapumziko hayo ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City walikuwa na michezo mbalimbali ambayo walishiriki kama Mpira wa Mikuu kwa wote, Kuvuta Kamba, kukimbia na ndimu kwenye vijiko, Mpira wa wavu(Voleball) na kukimbia na Magunia.
  Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakiwasili katika ufukwe wa Mileniam Bagamoyo Mkoani Pwani.
  Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakipasha kwaajili ya kuanza kucheza Mpia wa Miguu.
  Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City  mashindano wa timu mili za wafanyakazi hao zilipoanza kufuana katika mchezo uliochezwa mchangani katika fukwe za Milenium Bagamoyo Mkoani Pwani mwishoni mwa wiki.

  Mtanange wa Mchangani ukiendelea kati ya Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City.
  Mpira kati pale.
  Kabumbu mchangani likisongeshwa na Refa Meneja uhusiano wa wateja binafsi, Stephen Makundi(Kulia aliyesimama)
  Mfanyakazi Mlimani City na Kipa akishangilia baada ya Mpira kupigwa juu baada ya kukosa gori la timu Pinzani.
  Mcezo ukiendelea.
  Wakishangilia ushindi.
  Mhhhh mchezo wa mpira ukienda sawia...
  Maandalizi ya Mchezo wa Kamba.
  Mchezo wa Kamba ukiendelea kati ya timu A na B ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City.
  Hapa ni Vuta ni kuvute.
  Hapa ni Kuvuta tuuuuuu.....
  Kazi Kweli kwelii iiiiii........
  Maandalizi ya Mchezo wa Kukimbia huku umevaa gunia.
  Hapa mwendo wa kukimbi huku wenginemwingine akiishiwa pozi la kukimbia na kugusa mchanga kwa viwiko vya mikono.
  Wadada wakiwa tayari  kwa kukimbia na magunia.
  Mashindano ya kukimbia na magunia yakiendelea.
  Maandalizi ya Mchezo wa Kukimbia na mdimu kwenye kijiko.
  Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakikimbia na ndimu kwenye kijiko na kijiko kikiwa mdomoni.
  Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City wa Timu A na B wakicheza mcheo wa Mpira wa wavu katika Fukwe za Milenium Bagamoyo Mkoani Pwani.
  Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya Pmaja mara baada ya kuogelea na wengine kugusa maji ya bahari.

  0 0

  Kiongozi  wa Chama Cha ACT Wazalendo, Ndugu Zitto Kabwe ameondoka  Nchini kuelekea Philadelphia Nchini Marekani Kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democrats (Democratic National Convention) utakaomthibitisha Bi Hillary Clinton Kuwa Mgombea Urais kupitia Chama hicho.

  Wakati Akiwa kwenye Mkutano huo Ndugu Zitto atapata Fursa ya Kufanya Mazungumzo Na Viongozi mbalimbali wa Kisiasa duniani, Kufanya Kikao Cha Maandalizi Juu ya Ufunguzi wa Tawi la Wanachama wa ACT Diaspora la Nchini Marekani pamoja na Kuwa Na Mazungumzo Maalum na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad Juu ya Hali ya Kisiasa ya Zanzibar na Taifa Kwa Ujumla. 

  Zitto na Maalim Seif ndio wanasiasa pekee nchini walioalikwa kwenye shughuli za chaguzi za nchini Marekani.

  Taarifa zaidi zitafuata.

  Abdallah Khamis
  Afisa Habari, ACT Wazalendo

  0 0


  Katika kusherekea Siku ya Merit ambayo huadhimishwa kila Julai, 24 ya kila mwaka, vijana mbalimbali nchini wamekutanishwa kwa pamoja ili kuweza kujadili kuhusu Maendeleo Endelevu (SDGs) pamoja na kuweka mipango jambo gani lifanyike ili kuhakikisha kila raia anapata elimu kuhusu SDGs.

  Akizungumza na Mo Blog kuhusu siku hiyo, Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga alisema kwa Tanzania mwaka huu wamekutanisha vijana kwa pamoja na kujadili jinsi gani wanaweza kusaidia watu wengine kujiunga katika utekelezaji wa Maendeleo Endelevu (SDGs).

  Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga akitoa neno la ufunguzi katika kongamano lililokutanisha vijana ikiwa ni katika kusherekea Siku ya Merit.

  Alisema pamoja na kukutanisha vijana pia wamekutanisha mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi ambayo yataweza kuelezea jinsi gani yanafanya kazi, jinsi ambavyo yanaweza kuwasaidia vijana na jinsi ambavyo wanaweza kusaidiana na Umoja wa Mataifa (UN) ili kutekeleza Mipango ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

  “Kwa mwaka huu tumekutanisha mashirika ambayo yameungana nasi katika kuadhimisha Siku ya Merit lakini pia tuna vijana ambao wameshamaliza vyuo kwa sasa wanatafuta ajira, vijana waliomaliza kidato cha sita na wengine wamemaliza kidato cha nne,” alisema Rose.

  Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga akizungumza katika kongamano lililokutanisha vijana na kupata elimu kuhusu Mipango ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

  Alisema kuwa wameamua kukutanisha vijana wakiamini kuwa bado wana nguvu na wanauelewa mpana hivyo ni rahisi kwa wao kutumika kutoa elimu kwa watu wengine ambao bado hawajawa na uelewa kuhusu SDGs
  Aidha alisema hiyo ni moja ya hatua za awali ambazo wanazifanya kwani wanatambua kuwa kundi kubwa la vijana bado lipo mtaani na hivyo baadhi yao wanataraji kwenda katika mkutano wa kujadili Maendeleo Endelevu (SDGs) utakaofanyika New York, Marekani na baada ya kurejea watarudi na mipango mkakati ambayo wataitumia kufikisha elimu kwa kila mtu ili ajue SDGs ni nini na jinssi gani inaweza mfikia.

  (Na Rabi Hume – MO Blog)

  Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu (SDGs), Nicolaus Mukasa akiwapa elimu washiriki kuhusu SDGs.

  Baadhi ya wawakilishi wa mashirika yaliyoshiriki kongamano hilo wakielezea jinsi mashirika yao yanafanya kazi, jinsi yanavyoweza kuwasaidia vijana na kushirikiana na Umoja wa Mataifa (UN) ili kusaidia kusaidia kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).


  Washiriki kongamano lililokutanisha vijana ikiwa ni katika kusherekea Siku ya Merit.

  Washiriki kongamano lililokutanisha vijana ikiwa ni katika kusherekea Siku ya Merit wakiwa katika picha ya pamoja.

  (Picha zote na Rabi Hume, MO Blog)

  0 0


  Kaimu Mkurgenzi, Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (kulia) akiongea na baadhi ya Viongozi wa Mashirikisho ya Filamu Tanzania (hawapo pichani) kuhusu maendeleo ya sekta ya sanaa nchini wakati alipokutana nao hivi karibuni Wizarani hapo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo.
  Kaimu Mkurgenzi, Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (aliyekaa mbele) akiongea na baadhi ya Viongozi wa Mashirikisho ya Filamu Tanzania (hawapo pichani) kuhusu maendeleo ya sekta ya sanaa nchini wakati alipokutana nao hivi karibuni Wizarani hapo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo.


  Na Benedict Liwenga-WHUSM.

  Serikali imekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya Viongozi wa Mashirikisho ya Filamu nchini ikiwa ni sehemu ya kubaini changamoto mbalimbali zinazoyakabili Mashirikisho hayo.Akiongea hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi alisema kwamba, Mashirikisho yanayounda Shirikisho la Filamu nchini hayanabudi kushirikiana kwa karibu na Serikali ili kubaini changamoto na namna ya kuzitatua kwa manufaa ya Wasanii na Taifa kwa ujumla.

  Alieeleza kuwa, Wasanii wanapaswa kuzingatia maadili wakati wanapofanya kazi zao za sanaa ili waweze kujijengea heshima kwao, kwa jamii ambayo ndio mlaji wa kazi zao za kisanaa na kwa Taifa kwa ujumla.“Mnapofanya kazi zenu za sanaa, jitahidini kufuata miiko ya kazi zenu, tumieni vipaji vyenu vizuri kwa kufuata maadili ya Kitanzania, lakini pia jitahidini kuwainua wale wasanii wanaochipukia ama wale wadogo ili waweze kuwa na hamasa ya kuendeleza kazi zao za sanaa”, alisema, Bi. Kihimbi.

  Bi. Kihimbi aligusia suala la fursa ya kazi za sanaa inayodhaminiwa na Taasisi ya British Council Tanzania na kuwataka wasanii kuchangamkia fursa hiyo kwa kuhakikisha kuwa kila msanii au kikundi kinaandika Pendekezo (Proposal) kuhusu fursa hiyo ili kujiwekea nafasi kubwa kwa wasanii wa Tanzania kushinda fursa hiyo na kuweza kupata fedha za kuendesha kazi za sanaa kulingana na wazo lililobuniwa.“Kuweni wabunifu katika hii fursa ili mje na wazo zuri ambalo litawawezesha kushinda hii fursa hasa hii ya nAnA (new Arts new Audiences) kwani inamhusu msanii mmoja mmoja au kikundi”, alisema, Bi. Kihimbi.

  Aliongeza kuwa, Serikali itajitahidi kutatua baadhi ya changamoto ambazo zinaonekana kuwa kero kwa wasanii nchini ikiwemo suala la wizi wa kazi za sanaa (Piracy) ambalo kwa sasa tayari Waziri mwenye dhamana katika Wizara hiyo, Mhe. Nape Nnauye ameonyesha mfano kwa kukamata DVDs feki pamoja na mitambo ikiyotumika kudurufu kazi hizo za sanaa nchini.

  Kwa upande wake, Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo alisema kwamba Bodi yake inashirikiana vema na wasanii nchini kwa kuzingatia Sheria za nchi pasipo kumuonea msanii yeyote na kuwataka wasanii kote kuendeleza uhusiano huo mzuri uliopo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

  Aidha, aliwataka viongozi wa Shirikisho hilo la Sanaa kuendelea na utaratibu wa kupeana taarifa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sanaa na kuwahimiza wasanii kupenda kujiendeleza kielimu ili waweze kumudu soko huku akiwasisitiza kuhakikisha kuwa kazi zao wanazotengeneza zinapata kibali cha Bodi kwa kuwekewa madaraja na zinakuwa na stika halali ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kuepusha uharamia wa kazi zao.

  Naye Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Bw. Simon Mwakifwamba ameiomba Serikali kuendelea kushirikiana na Wasanii kwa karibu kwa kuzifanyia kazi baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo na ikiwemo suala la uharakishaji wa Sera ya Filamu kwani ndiyo kipaumbele chao cha kwanza, elimu ya namna ya kutengeneza filamu bora, usambazaji wa kazi zao pamoja na adui yao mkubwa ambaye ni uharamia wa kazi za sanaa.Ameishukuru Serikali kwa kuunda Sekta mpya ya Sanaa na kusema kuwa, Sekta hiyo itakuwa Mkombozi kwao kwani wanajisikia fahari kutambuliwa na kuwa na kitengo chao cha masuala ya kazi zao huku akiaahidi ushirikiano mzuri kwa sekta hiyo.

  0 0


  …Five year deal across 19 makets focused on driving financial inclusion in Africa

  United Bank Africa (UBA) and MasterCard have announced a partnership which will see UBA act as the issuer for MasterCard in 18 new markets in Africa. The partnership which came into effect in the second quarter of 2016 will see UBA issue MasterCard credit, debit and prepaid cards across these markets.

  The partnership will also focus on increased payments infrastructure across Africa, including the roll out of point-of-sale and mobile-point-of-sale technology, to ensure merchants are able to accept the cards when introduced into these markets.

  MasterCard and UBA are partnering across the 19 African countries in which UBA currently operates: Nigeria, Benin, Burkina Faso, Cameroon, Chad, Cote D’Ivoire, Democratic Republic of Congo, Equatorial Guinea, Ghana, Gabon, Guinea, Guinea-Bissau, Kenya, Liberia, Mozambique, Republic of Congo, Senegal, Sierra Leone, Tanzania, Uganda and Zambia.

  As the needs of our customers change, we are adapting through strategic innovations and partnerships to provide them with excellent and convenient services. Through these strategic partnerships, we are able to accelerate the drive for financial inclusion and economic well-being across the African continent” said Kennedy Uzoka, Group Managing Director-Designate, UBA plc.

  Division President for Sub-Saharan Africa, MasterCard, Daniel Monehin says; “This focus on infrastructure and the roll out of easy-to-access solutions is a key part of driving financial inclusion and a move away from cash in these markets. MasterCard’s continued innovation in the payments space coupled with UBA’s extensive pan-African network will mean the introduction of increased competition and a stronger financial sector in these regions.”

  According to the World Bank there are approximately 2.5 billion people who are financially excluded. Access to financial tools creates economic empowerment and reduces poverty. MasterCard has the tools and resources – including potential partnerships – to drive real change today.

  On June 27, 2016, MasterCard set a goal to connect 40 million micro and small merchants to its electronic payments network within five years. This expands on the company’s Universal Financial Access 2020 commitment made last year.

  To date, financial inclusion has been predominantly centered on providing the underserved and the unbanked with tools and transaction accounts. This remains a critical need with two billion unbanked people, the majority of whom are women, forced to operate in a cash economy. In order for financial inclusion efforts to truly have an impact, there needs to be an equal focus on both access and usage.

  “Collaborating with UBA has allowed for maximum impact when it comes to changing lives and introducing smarter ways for people to pay in Africa. Creating financially inclusive societies is dependent on these kinds of partnerships and we will continue to look for ways to partner in Africa going forward,” Monehin said.

  About United Bank for Africa

  United Bank for Africa is one of Africa’s leading financial institutions, with operations in 19 countries and 3 global financial centres: London, Paris and New York.

  From a single country operation in Nigeria, Africa’s largest economy, UBA has evolved into a pan-African provider of banking and related financial services to more than 11 million customers, through diverse channels globally.


  About MasterCard


  MasterCard (NYSE: MA), www.mastercard.com, is a technology company in the global payments industry. We operate the world’s fastest payments processing network, connecting consumers, financial institutions, merchants, governments and businesses in more than 210 countries and territories. MasterCard’s products and solutions make everyday commerce activities – such as shopping, traveling, running a business and managing finances – easier, more secure and more efficient for everyone. Follow us on Twitter @MasterCardNews, @MasterCardMEA join the discussion on the Cashless Conversations Blog and subscribe for the latest news.


  UBA Media and External Relations Contact


  Charles Aigbe: charles.aigbe@ubagroup.com, + 234 802 5010 901  MasterCard Communications Contact  Geraldine Trennery: geraldine_trennery@mastercard.com, +27 76 301 0264

  0 0


  Msimamizi wa Ushauri na Utafiti (PSPTB), Amos Kazinza akitoa mada LEO katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kulia ni Mkuu wa Idara ya Ugavi, Pindani Nyalile akiwa kwenye semina hiyo. Semina hiyo imelenga kutoa mafunzo kwa watendaji wa MNH ili waweze kuzingatia taratibu na sheria za manunuzi. Wakurugenzi na wakuu wa idara wa MNH wametakiwa kutoa haki wakati wa kutoa zabuni. Pia, wameshauriwa kutonunua bidhaa zilizopo chini ya kiwango.
  Baadhi ya wakurugenzi na wakuu wa idara wakiwa kwenye semina hiyo ya siku tatu iliyoanza LEO katika hospitali hiyo.

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (kulia) akifuatilia mada katika semina hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha, Gerald Jeremia akiwa katika semina hiyo LEO. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminieli Aligaesha akisikiliza jambo kwenye semina hiyo. Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni katika hospitali hiyo, Dk Faraja Chiwanga akifuatilia mada kwenye semina hiyo.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

  0 0

  Mbunge was jimbo la Mkuranga ambaye pia ni katibu wa wabunge wanaotokana na chama cha Mapinduzi CCM Abdallah Ulega akiwa sambamba na katibu wa CCM mkoa wa pwani Joyce Masunga wakijadiliana jambo kabla ya kumpokea mwenyekiti mstaafu wa CCM Dkt.Jakaya Kikwete
  Baadhi ya Wanachama cha CCM wakinogesha sherehe za kumpokea na Kumkaribisha Dkt Jakaya kikwete ambaye amekabidhi kijiti cha Uenyekiti wa chama hicho kwa Mwenyekiti mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli,kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni.
  Maandalizi yaliyoambatana na chereko chereko za hapa na pale za kumpokea na Kumkaribisha Mwenyekiti Mstaafu wa chama hicho,Dkt Jakaya kikwete zikiendelea ukumini humo 
  Wanachana na wafuasi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani wakimsubili kumpokea na kumkaribisha nyumbani Mwenyekiti mstaafu na Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete katika ukumbi wa Kasuba,Msoga-Bagamoyo.PICHA NA EMANUEL MASSAKA-GLOBU YA JAMII-BAGAMOYO.

  0 0


   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu, Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Davis Mwamunyange na Kamishina Jenerali wa Magereza John Minja(kulia)m katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa  mjini Dodoma , Julai 25, 2016.
   Rais John Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa, Julai 25, 2016.
   Rais John Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi,Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa, Julai 25, 2016.  Kulia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubei Ali Maulid na wapili kulia ni Spika wa Bunge, Dkt, Tulia Ackson.
   Wananchi wa Dodoma waliojitokeza kushiriki kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma wakimsikilza Rais John Maguguli wakati alipozungumza kwenye maadhimisho hayo mjini julai 25, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Dodoma katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma , Julai 25, 2016. 
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda  katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma , Julai 25, 2016. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula  na watatu kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu ,John Malecela.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Meya wa manispaa ya Dodoma, Jafari Mwanyembwa  katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma , Julai 25, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali , Davis Mwamunyange katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma , Julai 25, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kamishina Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Minja katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa  mjini Dodoma , Julai 25, 2016. Watatu kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi , Jenerali Davis Mwamunyange na kulia ni Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu.
   (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0  0 0

  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka Sime katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka Ngao katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma leo Julai 25, 2016 .
  Shughuli za maadhimisho hayo ya siku ya Mashujaa zilipokuwa zikiendelea ndani ya uwanja huo wa Mashujaa.
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kuweka silaha za jadi katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma leo Julai 25, 2016.
  Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiongea wakati wa Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016.
   Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiongea wakati wa Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016.
   Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela akiwasalimia wakazi wa Dodoma waliojitokeza kwenye Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016.
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela baada ya kuongea na wananchi kwenye Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016.

  0 0  Meneja Mradi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Celestine Mkama (kushoto) ) akizungumza kwenye Mkutano na waandishi wa habari Dar es salaam, kuhusu mafunzo yatakayotolewa kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kupitia tovuti ya taasisi hiyo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Godfrey Simbeye na Mtaalamu wa ujasiriamali na maendeleo ya kiuchumi, Haji Dachi. Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF),Godfrey Simbeye (katikati) akizungumza kwenye Mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, kuhusu mafunzo yatakayo tolewa kwa wajasiriamali wadogo na wakati kupitia tovuti ya taasisi hiyo. Meneja mradi wa TPSF Celestine Mkama (kushoto) wa mwisho kulia Mtaalamu wa ujasiriamali na maendeleo ya kiuchumi, Haji Dachi.
  Mtaalamu wa ujasiriamali na maendeleo ya kiuchumi, Haji Dachi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam, namna wajasirimali wadogo na wakati watakavyo weza kunufaika na mafunzo yatakayotolewa na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) kupitia tovuti ya Taasisi hiyo . kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Godfrey Simbeye. 

  Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa kushirikiana na Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT) itaendesha mafunzo maalum kwa wajasiriamali nchi nzima kuhusu namna ya kunufaika na tovuti mpya ya habari kwa wajasiriamali. 

   Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa TPSF, Godfrey Simbeye amesema taasisi hiyo imeanzisha vipindi vya redio katika vituo mbalimbali vya redio za kitaifa na vituo vidogo vya redio za jamii katika mikoa ya Dodoma, Geita, Kigoma na Mbeya. Vipindi hivyo vya redio vitaenda sambamba na warsha za mafunzo zitakazowahusisha wajasiriamali na wadau mbalimbali katika mikoa hiyo.

   “Kampeni hii imelenga kuongeza uelewa wa wajasiriamali juu ya tovuti hiyo ambayo ina mifumo ya mafunzo kwa wajasiriamali, namna ya kuanzisha na kukuza biashara, upatikanaji wa mitaji, mbinu sahihi za kuendesha biashara, namna ya kutafuta na kuuza bidhaa katika masoko, vilevile kampeni itatoa jukwaa la majadiliano kuhusu mada mbalimbali zinazowahusu wajasiriamali wadogo nchini.” alisema Simbeye.

   Mafunzo yatatolewa nchi nzima na wataalamu waliobobea katika biashara na ujasiriamali kwa kipindi cha miezi nane ili kuwajengea uwezo wajasiriamali waweze kunufaika ipasavyo na tovuti hiyo iliyozinduliwa mapema mwaka huu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage mapema mwaka huu. Tovuti hiyo inayopatikana kupitia www.entrepreneurs.or.tz, www.wajasiriamalitz.or.tz au kwa kupiga namba *148*99*06# ni kituo maalum chenye taarifa zote sahihi zinazomtosheleza mjasiriamali kuendesha biashara kwa mafanikio. 

   “Huduma hii imetolewa ili kuwasaidia wajasiriamali ili waweze kupata nyenzo muhimu za kuendesha biashara, vyanzo vya fedha, kuingia kwenye masoko ya hapa nchini na kimataifa, na taarifa nyingi za kuweza kumsaidia mtu anayetaka kuanzisha biashara na kuwawezesha wale ambao tayari wanafanya biashara kujiongezea ujuzi na uzoefu,” alisema Simbeye.

   Meneja Mradi wa Tovuti hiyo, Celestine Mkama alisema “Tumeona umuhimu wa kuendesha kampeni ya kuongeza uelewa wa tangu wakati tunatengeneza mfumo huu wa habari. Tunatarajia kupitia kampeni hii kuweza kuwafikia wajasiriamali moja kwa moja kupitia vipindi vya redio na warsha na kuweza kutatua matatizo yao kwa kuwapatia ujuzi”. 


  Hivi sasa kuna wajasiriamali zaidi ya milioni tatu nchini na tunajua kwamba ujuzi hafifu ni kikwazo kikubwa katika ukuaji wa biashara ndogo ndogo ambazo ni muhimu sana katika ukuaji uchumi,” alisema Mkama. “Tunataka kuhamasisha matumizi ya tovuti hii na kutoa mafunzo wakati huo huo. Tunaamini jambo hili litawajengea uwezo na kuwapa wajasiriamali ujuzi muhimu wa kuendesha biashara endelevu.”

  0 0


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  alipokuwa akiwasalimia na kuwashukuru mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma mapema leo asubuhi  waliojitokeza kushuhudia maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma.PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA


  *Asema akishahamia, Mawaziri na Naibu Mawaziri wote wafuatie mara moja

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atahamia Dodoma ifikapo Septemba, mwaka huu kuonyesha kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza ahadi ilizotoa kwa wananchi.

  Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumatatu, Julai 25, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma na kuwashukuru kwa ushiriki wao kwenye maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma.

  “Jana nilimwita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na kumwambia akamilishe matengenezo kwenye nyumba yangu kwa sababu ninataka kuhamia Dodoma ifikapo Septemba,” amesema na kushangiliwa na mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma waliohudhuria maadhimisho hayo.

  Amesema tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, kazi nyingi zimefanyika na wananchi wameziona na kwamba sasa hivi kazi iliyobakia ni utekelezaji wa ahadi alizotoa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.“Wananchi kazi mmeziona na sasa tunaenda kwenye utekelezaji. Ninatoa agizo kuwa mawaziri na manaibu wote wahame mara moja kutoka Dar es Salaam na kuja Dodoma. Wana ofisi ndogo Dodoma na kwa kuwa wamekuwa wakiishi wakati wote wa Bunge, wahamie mara moja. Mimi nahamia Septemba, na utekelezaji wake nitausimamia kwa juhudi zote,” alisisitiza.

  Amewataka wakazi wa Dodoma watumie fursa hiyo kutunza amani ya nchi na kudumisha umoja uliopo na pia akataka watumie fursa hiyo kujenga nyumba za kuishi za kutosha, nyumba za kulala wageni na hoteli za kitalii ili watu watumishi na wageni wanapokuja wasipate taabu mahali pa kuishi.

  Wakati huo huo, mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli katika muda wa siku tatu amerudia kusisitiza nia ya Serikali kuhamia Dodoma katika kipindi chake cha uongozi ili kutekeleza ndoto ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kutaka makao makuu ya nchi yawe Dodoma.

  Akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma kwenye uwanja wa mashujaa huku akishangiliwa, Rais Magufuli amesema atahakikisha Dodoma inakuwa makao makuu ndani ya miaka minne na miezi minne iliyobakia kwenye awamu ya kwnza ya uongozi wake.“Kama wabunge karibu 300 na mawaziri na manaibu wao ambao hawafiki 30 wanakaa hapa kwa miezi mitatu na maisha yanakwenda, kama makao makuu ya chama kinachotawala nchi yako hapa sioni sababu ni kwa nini Serikali ninayoiongoza iendelee kubakia Dar es Salaam,” amesema.

  Mara kwanza kutoa kauli hiyo, ilikuwa ni Jumamosi iliyopita, Julai 23, 2016 wakati akitoa hotuba yake ya kwanza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mkutano Mkuu maalum wa chama hicho.Rais Magufuli amesisitiza wananchi na wanasiasa kutunza amani na kudumisha amani iliyokuwepo nchini. Pia amewataka Watanzania wote kuendelea kuwaenzi mashujaa walioipigania nchi hii.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  JUMATATU, JULAI 25, 2016.

  0 0


  Mtaalam na Mkufunzi wa masuala ya Afya kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva - Switzarland, Olau Poppe akitoa mafunzo kwa Timu ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika kuhusu mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kwa lengo kuwajengea uwezo watalaam kuhusu ujazaji wa taarifa kuhusu sababu ya kifo cha mgonjwa pindi wanapojaza cheti cha kifo (Death Certificate).Washiriki wa Mafunzo hayo ya Siku mbili watakua na jukumu la kutoa mafunzo kwa wataalam wengine kwenye nchi wanazotoka kuhusu mfumo huo.
  Mtaalam na Mkufunzi wa masuala ya Afya kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva, Olau Poppe akifuatilia majadiliano ya washiriki wa mafunzo ya siku 2 ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika kuhusu mfumo unaotumika kutambua sababu ya kifo cha mgonjwa utakaowasaidia watalaam hao kujaza taarifa sahihi kwenye cheti cha kifo.
  Mtakwimu kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva,Switzarland Doris MA FAT (Kulia) akigawa machapisho yenye mwongozo kuhusu namna ya kujaza taarifa mbalimbali zinazosababisha vifo wakati wa mafunzo ya siku 2 ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika leo jijini Dar es salaam.

  Baadhi ya Washiriki wa mafunzo kwa Timu ya wataalam wa Afya kutoka Tanzania, Zambia na Cameroon wakifuatilia miongozo mbalimbali iliyokuwa inatolewa na watalaam kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) wakati wa Mafunzo kuhusu mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kuwawezesha watalaam hao kujaza taarifa sahihi juu ya sababu ya kifo cha mgonjwa leo jijini Dar es salaam.
  Sehemu ya Washiriki wa mafunzo kwa Timu ya wataalam wa Afya kutoka Tanzania na Malawi wakifuatilia miongozo mbalimbali iliyokuwa inatolewa na watalaam kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) wakati wa Mafunzo kuhusu mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kuwawezesha watalaam hao kujaza taarifa sahihi juu ya sababu ya mwisho ya kifo cha mgonjwa leo jijini Dar es salaam. Picha/Aron Msigwa.

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Said Bakar Jecha kuwa Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bibi Septuu Mohamed Nassor kuwa Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo,
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Dk.Juma Yakout Juma kuwa Naibu Katibu Msaidizi wa Baraza la Mapinduzi (Sera,Ufuatiliaji na Tathmini) katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Ndg.Tahir Mohamed Khamis Abdulla kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (Gavu) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba Sheria,utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haroun Ali Suleiman wakiwa ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika kuapishwa Viongozi mbali mbali leo Ikulu Mjini Zanzibar.

  [Picha na Ikulu.] 25/07/2016.

  0 0

  Muandishi wa ‘script’ ya igizo la Kumekucha, Priscilla Mlay (kulia) akizungumza wakati wa utambulisho wa igizo la Kumekucha ambalo limeandaliwa na taasisi ya Africa Lead kwa kushirikiana na Media For Development International (MFDI) chini ya udhamini wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (Usaid). 
  Muigizaji nyota wa filamu nchini, Jacob Steven (JB) akiizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na igizo jipya lilijulikanalo kwa jina la Kumekucha ambalo imeandaliwa na taasisi ya Africa Lead kwa kushirikiana na Media For Development International (MFDI) chini ya udhamini wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (Usaid). Katika igizo hilo, JB ametumia jina la Mzee Kidevu. 
  Mkurugenzi wa masuala ya Uchumi wa USAID, Randy Chester (wa kwanza kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa igizo hilo la Kumekucha utawaamsha na kupata maendeleo.
  Mwanamuziki mkongwe nchini, John Kitime (wa kwanza kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa igizo la Kumekucha ambalo limeandaliwa na taasisi ya Africa Lead kwa kushirikiana na Media For Development International (MFDI) chini ya udhamini wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (Usaid). Kitime ndiye aliyeingiza muziki katika igizo hilo. waigizaji wa igizo hilo.

  Msanii nyota nchini wa filamu, Jacob ‘JB’ Steven ni miongoni mwa waigizaji mbalimbali walioshiriki katika igizo la Kumekucha ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kuhamasisha vijana kujishughulisha na kilimo kutokana na uhaba wa soko la ajira.

  Igizo hilo ambali pia ni mchezo wa redio (radio plays) limeandaliwa na taasisi ya Africa Lead kwa kushirikiana na Media For Development International (MFDI) chini ya udhamini wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (Usaid) ya ushauri wa Taasisi ya chakula na lishe (TFNC), Taasisi ya TAHA, ACDI VOCA – NAFAKA, Land O Lakes, Rudi, Mwanzo Bora, The Rice Council of Tanzania, Technoserve, ANSAF (Non State Action Forum) na taasisi ya AMSHA.

  Katika filamu hiyo, JB anatumia jina la Mzee Kidevu ambaye kazi yake kubwa ni kununua mazao kwa wakulima kwa bei ya ukandamizaji na kuwafanya wakulima hao kuendelea kuwa na maisha duni huku yeye akijinufaisha.

  Akizungumza katika uzinduzi huo, JB alisema kuwa amefurahi sana kushiriki katika filamu hiyo ambayo inafundisha na kuhamasisha vijana kujihusisha zaidi na masuala ya kilimo na kuacha tabia ya kukimbilia mijini kama suluhisho lao la kutatua matatizo yao. “Nimepanda kushiriki katika filamu na mchezo huu wa redio, umenipa mwanga mkubwa na kupanua wigo wa kazi yangu ya kuigiza, kabla ya kuingia kwenye kuigiza, nilikuwa mnunuzi wa mazao hasa mahindi kule Kibaigwa na kusaga na kuuza unga wa chakula, hii ilikuwa fursa kwangu na nimeipenda, nawashukuru wahusika wote waliofanikisha filamu hii,” alisema JB.

  Mkurugenzi wa masuala ya Uchumi wa USAID, Randy Chester alisema kuwa wamefurahi kujihusisha na masuala mbalimbali yaa maendeleo hapa nchini na kuamua kusaidia mradi huo ambao unahusika zaidi maeneo ya vijini. “USAID imejihusisha katika miradi mingi ya maendeleo nchini, kama unajua, zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wanajihusisha na masuala ya kilimo, waahitaji kuendelezwa ili kufikia hatua kubwa ya maendeleo, mchezo wa Kumekucha utawaamsha na kupata maendeleo,” alisema Chester.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa mashujaa waliojitoa kwa uzalendo kupigania Tanzania hawana budi kukumbukwa kutokana na kujitoa kwao ili Tanzania isitawaliwe na wakoloni.

  Makonda ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa katika Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, amesema kuwa mashujaa hao walifanya ukombozi kwa uzalendo bila kuangalia dini zao na makabila yao.

  Makonda amesema kuwa kila mtu lazima ajiulize juu ya mashujaa katika kufanya kazi katika kungalia kutenda haki pamoja na uzalendo kwa masilahi ya taifa.

  Amesema kuwa amani iliyopo nchini imetokana na watu kuwa wazalendo katika kupigania nchi yao na hawakuangalia kupoteza maisha au familia zao.Aidha amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuwa wazalendo na nchi bila kuangalia vyama wanavyotoka au kabila kutokana na umoja uliojengwa na mashujaa.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiweka Ngao kwenye Mnara uliopo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuwakumbuka Mashujaa waliopigana vita hapa nchini. Siku ya Mashujaa hufanyika Julai 25 kila mwaka.
   Askali wakitoa heshima wakati wa sherehe za kumbukumbu ya mashujaa ambayo imefanyika katika viwanja vya mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali jijini Dar es Salaam leo wakati wa sherehe za kuwakumbuka mashujaa waliopigana vita hapa nchini.

  0 0

   
  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

  SERIKALI imesema sekta ya kilimo inaendelea kuwa sekta muhimu katika uchumi wa Tanzania kwa asilimia 25% ya pato la taifa na kuajiri asilimia 75% ya watanzania wakiwemo wanawake na vijana.

  Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Richard Kasuga wakati wa uzinduzi wa mchezo wa redio uitwao KUMEKUCHA unaotarajia kuonyesha mchango wa wanawake na vijana katika kutokomeza tatizo la uhaba wa chakula nchini.

  Kasuga amesema kuwa igizo hilo la mchezo wa redio, litaakisi umuhimu wa ushirikishwaji wa wanawake na vijana katika kukuza sekta ya kilimo na kutoa ujumbe kwa vijana kuona umuhimu wa kilimo hasa kilimo cha biashara.

  “Sheria na tamaduni zilizopo zinakwaza juhudi za mwanamke kupata fursa za kiuchumi kwa sababu hawana haki ya kumiliki ardhi au vifaa vya kilimo, vyanzo endelevu vya maji, ukosefu wa mikopo ambayo wanahitaji ili kufanikisha juhudi zao”alisema Kasuga.

  Kwa upande wake mwakilishi kutoka shirika la msaada la Marekani (USAID) Randy Chester alisema kuwa mchezo wa KUMEKUCHA umeandaliwa na taasisi ya Africa Lead kwa kushirikiana na Media for Development International (MFDI) na kufadhiliwa na USAID kwa lengo la kupunguza uhaba wa vyakula vyenye virutubisho hapa Tanzania.

  Mchezo wa KUMEKUCHA ni mchezo wa redio wa kila wiki ambao unaangazia maisha, vikwazo na fursa za wakulima Tanzania na utaanza kurushwa hewani kuanzia Julai 25, 2016 kupitia Redio Free Afrika, Redio Abood FM, Redio Ebony FM na Redio Bomba FM.

  0 0


  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Bi. Joyce Fissoo akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Wawakilishi wa Wasambazaji wa kazi za Filamu nchini (hawapo pichani) waliotembelea kujua Urasimishaji wa kazi hizo katika ofisi ya Bodi hiyo 25 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.

  Afisa Utamaduni Bodi ya Filamu, Bw. Romanus Tairo akielezea jambo wakati wa mazungumzo na Wawakilishi wa Wasambazaji wa filamu nchini walioitembelea Bodi ya Filamu kujua Urasimishaji wa kazi zao, 25 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.

  Mwakilishi wa Wahifadhi kazi za Sanaa, Bw. Frank Pangoni (kushoto) akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu yaliyofanyika leo 25 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi Kampuni ya Salt Inc, Bw. Edwin Musiba (kulia) akifafanua jambo mbele ya Wasambazaji wa filamu wakati wa mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu yaliyofanyika leo 25 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.

  Mwakilishi wa Wauzaji DVDs Mikononi, Bw. Jumanne China (kulia) akieleza jambo mbele ya Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo 25 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam katika ofisi hiyo.

  Mwakilishi wa Wauzaji wa Jumla wa kazi za Sanaa, Bw. Augustino Karia (aliyekaa katikati upande wa kushoto) akimweleza jambo Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu (wa pili) wakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo 25 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam katika ofisi hiyo. (Picha zote na Benedict Liwenga)

  0 0

   
  Msafala wa gari za FFU zilizomsindikiz askari mwenzao anayekutwa na kosa la kuua bila kukusudia leo
  Askari wa FFU wakitoka mbio mahakamani hapo
  Wananchi na wanahabari wakitoka mahakamani hapo
  wakili kutoka mtandao wa watetezi wa haki za binadamu ((THRDC)Benedict Ishabakaki akizungumza na wanahabari nje ya viwanja vya mahakamani leo. 
   
  Na MatukiodaimaBlog Iringa

  MAHAKAMA kuu kanda ya Iringa imemtia hatiani kwa kosa la kuua bila kukusudia askari Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia ( FFU )Iringa G 58 Pacificius Cleophace Simon (27) anayetuhumiwa kumuua mwanahabari Daudi Mwangosi mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi.

  Huku wakili upande wa jamhuri katika kesi hiyo Adolph Mwaganda akiiomba mahakama hiyo kutoa hukumu ya kifungo cha maisha jela kwa askari huyo ambae hata hivyo alisema upande wa jamhuri hauna taarifa za makosa yoyote aliyopata kuyafanya.

  Hata hivyo mahakamani hiyo imesema adhabu kwa mtuhumiwa huyo kutokana na kupatikana na kosa hilo la kuua bila kukusudia itatolewa Julai 27 majira ya saa 4 asubuhi mwaka huu.

  Jaji Dkt Paul Kiwelo ambaye anayesikiliza kesi hiyo alisema mahakakamani hapo leo kuwa kati ya vielelezo vitano vyote vilivyoleta kama ushahidi mahakamani hapo kwa ajili ya kesi hiyo namba 54 ya mwaka 2013 ni kielelezo kimoja pekee cha ungamo kwa mlinzi wa amani ambacho ndicho hakukuwa na shaka na ungamo hilo ndilo lililomtia hatiani asikari huyo.

  Alivitaja vielelezo vilivyopelekwa kama ushahidi kuwa ni Ramani ya eneo la tukio,ripoti ya tabibu ,ungamo la mlinzi wa amani ,silaha aliyoitumia na rejista ya silaha .

  Hata hivyo alisema kuwa idadi ya mashahidi katika kesi sio inayowezesha kumtia hatiani mtuhumiwa ila kinachomtia hatiani ni aina ya ushahidi wenye uhakika ambao unatolewa na kuongeza kuwa katika kesi hiyo upande wa jamhuri ulishindwa kuleta mashahidi stahiki zaidi ya kuwa na mashahidi ambao ukiacha mlinzi wa amani mashahidi wote ushahidi wao una masahaka na haoonyeshi kama mtuhumiwa huyo ndio aliyehusika na mauwaji .


  Askari hao wakimtoa mahakamani hapo leo mtuhumiwa wa mauwaji ya Mwangosi
  Marehemu Mwangosi enzi za uhai wake
  “ Niseme baada ya kusikiliza ushahidi wote …..mtuhumiwa kaonekana na kosa la kuua ila kujua kama alikuwa na nia ovu ama bila kukusudia ni jukumu la Jamhuri ambayo ilipaswa kuleta ushahidi ….. maelezo ya ungamo ambayo hata hivyo hayaonyeshi alipanga ila ni uzembe wa hali ya juu …..haijathibitika kuwa alikusudia mahakama inaamini hakukusudia”

  Hivyo alisema kuwa mahakama yake imelifuta kosa la kuua kwa kukusudia na kumtia hatiani kwa kosa la kuua bila kukusudia alisema jaji Kiwele kuwa hamakama yake inashangazwa na RCO kwa kuleta mahakamani kesi ambayo ushahidi wake haukukamilika .

  “ Ushahidi pekee ambao ni ule wa mlizi wa amani hakimu Flora Mhelela ambae kweli alitoa ushahidi usio na shaka hata kidogo ila ushahidi mwingine wote ulikuwa na mashaka mengi mfano ushahidi namba moja , mbili na nne ni ushahidi ambao haukuwa halisi “

  Alisema mfano jambo la kujiuliuza katika ungamo lake mtuhumiwa lisema kuwa silaha aliyokuwa akitumika wakati amemzingira mwanahabari huyo ilifyatuka bahati mbaya hivyo ilikuwa ni mbovu ila cha kushangaza hakuna hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa silaha hiyo ilikuwa mbovu ama nzima.

  Alisema kuwa si salama sana kumtia hatiani mtuhumiwa huyo kwa kosa la mauwaji ya kukusudia wakati upande wa jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi kamili unaoonyesha kuwa mtuhumiwa huyo alikusudia kufanya mauwaji hayo.

  Aidha alisema mbali ya upande wa utetezi pamoja na mtuhumiwa kukana ungamo alilolitoa Septemba 5 mwaka 2012 kwa mlinzi wa amani kuwa hakulitoa kwa uhuru na amani ila bado haisaidii kulikataa sasa maana kama si kweli alipaswa kielelezo hicho kukataliwa siku ya kwanza kilipofikishwa mahakamani hapo kama ushahidi hivyo mahakama hainashaka na kieelezo hicho amacho ni ungamo kwa mlinzi wa amani.

  Simon ambae anatetewa na wakili wake Lwezaula Kaijage aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu sahihi yenye jicho la huruma kwa mteja wake huyo kwani hana wazazi na yeye ndio anategemewa na wadogo zake watano pia ana mtoto wa miaka mitano anayehitaji zaidi malezi yake katika makuzi yake.

  “Mheshimiwa jaji huyu mshitakiwa ni kijana mdogo mwenye miaka 27 na ni nguvu kazi ya Taifa pia katika oparesheni hiyo ya Septemba 2 mwaka 2012 alikuwa katika kazi hiyo ambayo ilikuwa ni amri ya jeshi na kuwa slaha ililipuka bahati mbaya basi ijulikane hivyo pia amekuwa mahabusi miaka minne na kwa kipindi chote amekuwa akijutia kosa lake hilo…. Naomba anachiwe huru kwa masharti ambayo mahakama inaona yanafaa”

  Huku wakili upande wa jamhuri katika kesi hiyo Adolph Mwaganda akiiomba mahakama hiyo kutoa hukumu ya kifungo cha maisha jela kwa askari huyo ambae hata hivyo alisema upande wa jamhuri hauna taarifa za makosa yoyote aliyopata kuyafanya.

  “ Hatuna kumbukumbu ya kosa lolote ila kwa kuwa mahakama imemtia hatiani kwa kosa dogo la kuua bila kukusudia tunaomba mahakama yako kutoa adhabu kwa mujibu wa kifungu namba 198cha kanuni ya adhabu sura namba 16 mapitio ya mwaka 2002 kwamba mtu yeyote aliyetiwa hatiani kwa kosa la mauwaji ya bila kukusudia afungwe jela maisha “

  Kesi hiyo ambayo ilijaza umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Iringa huku polisi wa FFU na wale wa kawaida wakitanda nje ya mahakama hiyo na ndani ya chumba cha mahakama kabla ya msajili wa mahakama hiyo kutoa onyo kwa jeshi la polisi kufuatia vurugu mbali mbali wanazozifanya mara kwa mara katika kesi hiyo , wakili kutoka mtandao wa watetezi wa haki za binadamu ((THRDC)Benedict Ishabakaki alisema kuwa hajapendezwa na nguvu kubwa ya jeshi la polisi ambayo wanaitumika katika kasi hiyo ndani na nje ya mahakama kuwa kinachofanyika ni kuingilia uhuru wa mahakama.

  Kwani alisema mahakama haipaswi kuingiliwa na chombo kingine chochote na kuwa kitendo cha polisi kuzuia wanahabari ndani ya mahakama kufanya kazi zao kabla ya kesi kuanza ama baada ya kesi kumalizika si haki .

  Lakini pia wakili msom I Ishabakaki, alisema kwa maoni yake anaona kulikuwa na mapungufu kwanzia kweye uchugunzi wa kesi ya mpaka uendeshaji wa kesi hiyo. Wakili msomi alisema anaunga mkono maswali ambayo mahakama ilijiuliza kwa nini RPC na RCO hawakuitwa kutoa ushaidi.

  Wakili anasema kutkana na mwenendo wa kesi kwa kitendo cha viongozi wa juu kutokuita mahaakamani kuisaidia mahakama kunaweza kukawa kumepindisha haki sit u kwa marehumu mwangosi lakini hata kwa askari aliyehukuiwa.

  Hii ni kutkana na kwamba mahakma iisema imepata kazi sana kutambua siku hiyo oda ilitoka kwa nani. 

  Ulinzi wa polisi viwanja vya mahakama kuu kanda ya Iringa leo kabla ya mtuhumiwa wa mauwaji kufikishwa
  Wananchi wakiwa foleni kukaguliwa kabla ya kuingia mahakamani leo
  Mtuhumiwa wa mauwaji ya Mwangosi akipakiwa kwenye gari za FFU 

older | 1 | .... | 915 | 916 | (Page 917) | 918 | 919 | .... | 1898 | newer