Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Tazama hapa Live mechi ya YANGA V/S MEDEAMA


NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, ENG. RAMO MAKANI AZINDUA MIRADI YA TANAPA CHAMWINO, DODOMA.

$
0
0
 Picha ya pamoja.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilangali Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma jana muda mfupi kabla ya kuweka jiwe la msingi katika zahanati ya kijiji hicho. Mradi huo wa zahanati umefadhiliwa kwa ushirikiano wa TANAPA Tsh. Milioni 25, Mbunge wa Jimbo la Mtera (Livingstone Lusinde) Tsh. Milioni 14.3 na Wananchi wa kjiji hicho Tsh. Milioni 12. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akizindua mradi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Maila iliyopo Chamwino, Dodoma jana, mradi huo umefadhiliwa kwa ushirikiano wa TANAPA kupitia Mradi wa Ujirani Mwema, Tsh. Milioni 115.83 na Wananchi wa Kata ya Manda Tsh. Milioni 33.72. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mtera, Lingstone Lusinde.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga (kulia) Hati ya Makabidhiano ya mradi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Maila iliyopo Chamwino, Dodoma jana, mradi huo umefadhiliwa kwa ushirikiano wa TANAPA kupitia Mradi wa Ujirani Mwema,  Tsh. Milioni 115.83 na Wananchi wa Kata ya Manda Tsh. Milioni 33.72. Watano kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Witness Shoo.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Tanzania - TANAPA  ambaye pia Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Shirika hilo, Witness Shoo akitoa taarifa ya juu ya miradi miwili iliyofadhiliwa na Shirika hilo katika vijiji vya Ilangali na Manda. Alisema shirika hilo limechangia Tsh. Milioni 148.3 kupitia mradi wa Ujirani Mwema. 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa pili kulia) akikagua vitanda vya mradi wa bweni la wasichana wa shule ya Sekondari Maila iliyopo Chamwino, Dodoma jana, mradi huo umefadhiliwa kwa ushirikiano wa TANAPA kupitia Mradi wa Ujirani Mwema, Tsh. Milioni 115.83 na Wananchi wa Kata ya Manda Tsh. Milioni 33.72. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mtera, Lingstone Lusinde na Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Samuel Amon (wa tatu kulia).
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa tatu kulia) akiongoza msafara kukagua fensi ya bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Maila muda mfupi kabla ya kuzinduliwa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Witness Shoo na Mbunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde (wanne kulia)
 Taswira ya jengo la Zahanati ya kijiji cha Ilangali lililofadhiliwa na TANAPA
 Taswira ya jengo la Bweni la Wasichana shule ya Sekondari Maila lililofadhiliwa na TANAPA.

Na Hamza Temba - WMU.
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imepanga kulipatia ufumbuzi tatizo la uvamizi wa Wanyamapori kwenye makazi ya watu wanaozunguka Hifadhi zenye Wanyamapori nchini kwa kuwashirikisha wananchi wa vijiji hivyo, kuwapatia mafunzo na silaha maalum za kujilinda na kufukuza wanyamapori hao wakati wa dharua.

Hayo yalibainishwa jana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Eng. Ramo Makani akizungumza na wananchi wa vijiji vya Manda na Ilangali Wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi na uzinduzi wa miradi iliyofadhiliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kupitia Mradi wa Ujirani Mwema katika vijiji hivyo.

Akijibu kero iliyowasilishwa kwake na Mbunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinge katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye vijiji hivyo kuhusu Wanyamapori wanaovamia maeneo ya vijiji vya jirani na Hifadhi ya Ruaha na kuharibu mazao ya wananchi, Eng. Makani alisema, changamoto hiyo inashuulikiwa kwa upana wake na kwamba Serikali inakuja na mpango wa kukabiliana nayo kwa kuwashirikisha wananchi wa vijiji husika.

Akizungumzia mpango huo alisema kuwa Serikali itaanzisha mafunzo maalum ya kujikinga na Wanyamapori kwa baadhi ya wananchi watakaoainishwa kwenye maeneo husika na kupewa silaha maalum kwa ajili ya kuwafukuza kabla ya kuleta madhara. Aliongeza kuwa Askari wa Wanyamapori waliopo pamoja na changamoto za kijiografia za baadhi ya maeneo hawatoshi kulinda maeneo yote ya vijijini hususani wakati wa dharua hivyo kwa kuwapa mafunzo na zana na kujilinda baadhi ya wananchi itasaidia katika kukabilina na tatizo hilo kwa wakati.

Katika hatua za maandalizi ya awali ya mpango huo, aliwaagiza viongozi wa vijiji vya Ilangali na Manda ambavyo vinayozunguka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kuanza kazi ya kutambua vijana wakakamavu, wenye elimu, uadilifu, uaminifu na maadili bora kuanzia watano hadi kumi kwa ajili ya kujiunga na mpango huo pale utakapokuwa tayari kuingia kwenye hatua ya utekelezaji.

Hapo awali akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa zahanati ya kijiji cha Ilangali na baadae kuzindua mradi wa bweni la wasichana shule ya Sekondari Maila  iliyofadhiliwa na TANAPA, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, Naibu Waziri, Eng. Makani alisema kuwa misaada hiyo ni sehemu faida za uhifadhi ambayo wananchi wananufaika nayo kwa kushirikiana na Serikali katika uhifadhi. Aliwataka wananchi hao kuendelea kushirikiana na Serikali katika uhifadhi ili faida kama hizo ziendelee kupatikana kwa wingi kwa kuwa uhifadhi ukiimarika na wanyamapori wakaongezeka na utalii nao utakua na kuongeza mapato zaidi.

"Fedha zilizotumika katika Mradi huu tunaoushuhudia hapa leo ni sehemu ya faida za Uhifadhi, tunawaomba sana wananchi muendelee kuunga mkono juhudi za Serikali za kulinda Wanyamapori na kupiga vita ujangili, tuendelee kulinda chanzo cha fedha hizo, tukipata watalii wengi zaidi na fedha hizo zitaongezeka maradufu. Alisema Makani.

Akizungumzia miradi hiyo miwili, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Shirika hilo, Witness Shoo alisema kuwa shirika hilo limechangia Tsh. Milioni 148.3 katika miradi hiyo ya Ujirani Mwema. Aliongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 1994 - 95 na 2014 - 15 Shirika hilo limechangia jumla ya Tsh. Bilioni 2 kwa vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha katika miradi ya sekta ya  ya elimu, maji, afya na uhifadhi kwa ujumla.

MADUDU KIBAO YABAINIKA MACHINGA COMPLEX - MAKONDA

Uzinduzi wa Rock City Marathon; Serikali yawaasa wadau wa riadha nchini.

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa idara va Michezo Wizara ya  Habari, Sanaa na Michezo  Bw Alex Nkenyenge (alieshika mkasi) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Rock City Marathon wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es jana. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International, Bi Elizabeth Riziki (wa kwanza kushoto)Mkurugenzi Mtendaji wa mashirika ya Freidkin Conservation Fund( FCF) na African Wildlife Trust (AWT), ambao ndio wadhamini wakuu wa mbiohizo Bw Pratik Patel (wa pili kulia), Bi Ombeni Savara katibu Mkuu Msaidizi chama cha Riadha Tanzania (wa kwanza kulia) na Joseph Kahama mwenyekiti wa maandalizi ya mbio hizo.
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Joseph Kahama akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mbio hizo.
 Mwanaridha mkongwe nchini Bw Juma Ikangaa akitoa nasaha zake kwenye hafla ya uzinduzi wa mbio hizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa mashirika ya Freidkin Conservation Fund (FCF) na African Wildlife Trust (AWT), ambae ndio wadhamini wakuu wa mbio
 Kaimu Mkurugenzi wa idara va Michezo Wizara ya  Habari, Sanaa na Michezo  Bw Alex Nkenyenge akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi rock City Marathon.
Baadhi ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo.


Rock City Marathon ilizinduliwa rasmi jana jijini Dar es Salaam huku wito ukitolewa kwa wadau wa mchezo wa riadha kote nchini kuhakikisha wanafanya jitihada za makusudi kuukomboa mchezo huo uliolipa taifa heshima miaka ya nyuma.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa mbio hizo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Bw Nape Nnauye,  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo wa Wizara hiyo Bw Alex Nkenyenge alisema kuna haja ya kuwepo kwa jitihada za makusudi miongoni mwa wadau wa mchezo huo ili kurejesha makali ya taifa katika riadha yaliyoonyeshwa miaka ya 1970 na 1980.

Kupitia mkurugenzi huyo Waziri Nape alitoa wito kwa wadau wa mchezo huo kuhakikisha wanashirikiana na serikali kuhakikisha changamoto zinazokwamisha mchezo huo zinatatuliwa ili kuwezesha uwepo wa maandalizi ya kutosha kwa wanamchezo huo.“Ndio maana nawapongeza waandaaji wa mbio hizi kwa kuwa wanashikiri moja kwa moja kukamilisha adhma yetu hii muhimu…kama serikali pia tunaahidi kuendelea kushirikiana nao,’’ alisema.

Akizungumza kwenye hafla Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International, Bi Elizabeth Riziki alisema mbio hizo zinatarajiwa  kufanyika Septemba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza zikihusisha wanariadha kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo baadhi ya nchi za Afrika, Ulaya na Marekani. Alisema mbio hizo zinazofanyika kwa mara ya nane mfululizo tangu zianze mwaka 2009 zinalenga kutambua na kuinua vipaji vya wanariadha nchini na pia kukuza utalii wa ndani kupitia sekta ya michezo.

“Rock City Marathon zitahusisha makundi matano yaani mbio za kilomita 21 kwa wanaume na wanawake, mbio za kilomita 5 kwa ngazi ya ‘corporate’, mbio za kilomita 3 kwa ajili ya walemavu, mbio za kilomita 3 tena kwa ajili ya wazee umri zaidi miaka 55 na kuendelea pamoja na mbio za kilomita 2 kwa ajili ya watoto umri kati ya miaka 7 hadi 19,’’ alitaja.

Alitaja  baadhi ya makampuni yaliyojitokeza kudhamini mbio hizo ikiwa ni pamoja na Freidkin Conservation Fund, African Wildlife Trust, Mwanza Hotel, Nyanza Bottlers Limited na kampuni ya Real PR Solution.

“ Pia mbio za mwaka huu zimeboreshwa zaidi kwa kuwa zitaambatana na uwepo wa majiko ya wachoma nyama ili kutoa fursa kwa washiriki kufurahia aina hiyo ya kitoweo pamoja na vyakula tofauti vyenye asili ya mkoa huo…ifahamike lengo la mbio hizi kukuza utalii wa ndani ,’’

Tunawaalika wadhamini waendelee kujitokeza kwa wingi ili kuzifanya mbio za mwaka huu kuwa bora zaidi,” alisema.Akizungumza kwenye hafla hiyo mdhamini mkuu wa mbio hizo  Bw Pratik Patel ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa mashirika ya Freidkin Conservation Fund( FCF) na African Wildlife Trust (AWT) alisema wameamua kuwa sehemu ya mbio hizo kwa kuwa zinaendana na mkakati wao kukuza utalii kwa kulinda maliasili.

“Tunafurahia kuwa sehemu yam bio hizi kwa kuwa lengo lake linaenda sambamba na agenda yetu ya kulinda maliasili na zaidi linaenda sambamba na kampeni yetu ya kupinga vita ujangili inayofahamika kama ‘Okoa Wanyama Wetu; Kataa Ujangili’. Alisema.

VIJANA WAMETAKIWA KUJIUNGA KWENYE VIKUNDI VYA UJASILIAMALI NAKUACHA KUTUMIA MUDA WAO KUCHEZA BAO.

$
0
0
Wananchi wa kijiji cha Lupondo,kata ya mkamba wakimsikiliza kwa makini mbunge wao Abdallah ulega katika mkutano wake wakuwashuruku wananchi hao kwa kumchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo huku akihaidi kutoawaangusha nakwamba atakuwa karibu na watu wake.
 Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibunguchana,kata ya mkamba ikiwa ni sehemu ya utaratibu ambao ameuweka wa kwenda kushukuru,na kuhimiza utekelezaji wa miradi ya maendeleo leo katiaka kijiji cha kibunguchana  mkoani Pwani.
 Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Kibunguchana, Ahamad Mbonde  akizungumza maneno yaufunguzi kabla ya kumkaribisha mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega kuzungumza na wananchi hao leo mkoani Pwani.

 Mbunge ulega wajimbo la Mkuranga akihesabu fedha.
 Mbunge  wa Mkuranga Abdallah Ulega akikabidhi fedha taslimu shilingi laki tatu kwa  Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Kibunguchana,  Ahamad Mbonde  kwa ajili ya kuazisha msingi wa ujenzi wa shule ya msingi kijijini hapo ambapo pia alifanya harambee ndogo iliyowashirikisha baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo akiwa Mwenyekiti wa halmashauri, Juma abed ambaye alichangia mifuko kumi yacementi na diwani wa kata hiyo Hassan Dunda alichangia pia mifuko kumi ya  cementi leo mkoani Pwani.
 Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Na Mwandishi wetu.
MBUNGE  wa Jimbo la Mkuranga  Abdallah Ulega amewataka vijana wa Wilaya hiyo kujiunga katika vikundi vya vikoba  vinavyoazishwa kwenye maeneo yao  na kwamba wastarajie kuwa ahadi ya rais ya kutoa sh. Milioni50 kila kijijihaitaenda kwa mtu mmoja mmoja bali kwa kukaa katika makundi.

Amesema kuwa kama wananchi wanataka fedha hizo ziwafikie lazima wakae kwenye vikundi na si vinginevyo ,huku akisisitiza akina baba nao kuacha kutumia muda wao mwingi kucheza bao badala yake wajiunge katika vikundi.

Ulega ametoa wito huo  jimbo humo wakati akizungumza na wanachama wa kikundi cha Vikoba cha Tuamke kilichopo katika kijiji cha Lupondo kata ya mkamba.

Alisema kuwa hakuna namna kwani maendeleo yanakuja Kwa kukaa katika vikundi mbalimbali na hata fedha za rais zitaelekezwa katika vikundi hivyo,hivyo kazima watanzania wachangamkie fursa hiyo.

"Binafsi Leo nawachangia sh.laki tatu kwani mmeonesha dhamira ya dhati kupitia risala yenu ambayo mmesoma mbele yangu nami nahaidi nitakuwa pamoja nami kamwe si tawaacha."alisema Ulega.

Aidha alisema kuwa yeye kama mbunge kuna mipango mingi ambayo anayo Kwa ajili ya watu wake ikiwa pamoja na kuleta watu wenye makampuni ya Pikipiki ili kuja katika wilaya hiyo na kukopesha vijana Pikipiki hizo na baadae kulipa kidogokidogo Kwa muda wa miezi 11.

Alisema kuwa lazima vijana,akina baba na akina mama Kwa pamoja wakubali kutengeneza vikundi vya vikoba kwani fursa nyingi zinapitia katika vikoba na si Kwa mtu mmoja mmoja.

Aidha Ulega akiwa katika ziara ya kijiji cha Lupondo alipata fursa ya kufungua jengo la Tuamke Vikoba ambapo pia alitembelea Zahanati ya Kijiji hicho nakuhaidi kutatua tatizo la miundombinu ya Maji.

Alisema kuwa anatambua kuwa Zahanati hiyo inachangamoto kubwa ya Maji hivyo atahakaikisha anasimamia ujenzi wa kisima pamoja na kuona Zahanati hiyo inapata umeme wa Tanesco Kwa ajili ya kurahisisha utoaji huduma.

"Nitajitahidi kadri ya uwezo wangu wote kuleta umeme hapa na kama ule wa tanesco utachelewa basi nitahakikisha naleta solar hapa."alisema Ulega.

Pia mbunge huyo alisema kuwa wananchi watambue kuwa yupo Kwa ajili yao na kwamba watakuwa pamoja katika kipindi chonde cha uongozi wake ikiwa pamoja na kuhakikisha anasukuma huduma jwa wananchi wake.

Naye Diwani wa Kata Dundani ,Hassan Dunda aliwaeleza wananchi hao kuwa uchaguzi umekwisha kilichobaki ni Kazi  huku akisisitiza kuwa watu kukaa katika makundi Kwa ajili kupata mikopo.

Ulega mbali na kufanya ziara katika kijiji cha Kupondo pia alitembelea vijiji vingine mbalimbali ndani ya Kata ya Mkamba ,ambapo pia anaendelea na ziara hizo za kutoa shukrani na kukagua miradi ya maendeleo.

TAARIFA YA AJALI YA KICHWA CHA TRENI KUGONGANA NA BASI LA UDA JANA USIKU

$
0
0
KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)

MTU MMOJA AFARIKI KATIKA AJALI YA KICHWA
TRENI KUGONGANA NA BASI LA UDA JANA USIKU

Mtu mmoja afariki dunia baada ya  basi la UDA kukigonga kichwa cha treni cha Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) katika  makutano ya reli na barabara ya Kamata saa 3:20 usiku jana Julai 26, 2016. Marehemu ametambuliwa  kwa jina la Omari Abdallah Nyumba  mkazi wa Mbagala.Aidha majeruhi 43 wa ajali hiyo walipelekwa hospitali ya Taifa ya Mhimbili ambapo watatu kati yao ni mahututi.
.
Taarifa za awali za Kikosi cha Polisi  Reli zinaeleza kuwa ajali  hiyo ilitokea baada ya dereva Majuto Hamis  wa basi hilo la UDA aina ya Hecher lenye namba za usajili T969 CVP kukaidi amri ya kusimama iliotolewa na Mfanyakazi  wa TRL. Dereva huyo ni mmoja wa majeruhi ambaye amevunjika miguu na yuko chini ya ulinzi wa Polisi wa Reli akiwa wodini baada ya majeruhi wote kupatiwa huduma.

 Kichwa cha treni kilichogongwa ni cha kazi za sogeza Namba 7317 kilikuwa  kikitokea  kituo kikuu cha treni cha  Dar es Salaam. 

Kikosi cha Polisi TRL wameahidi kutoa taarifa zaidi baadae hii leo kuhusu maendeleo ya majeruhi wa ajali hiyo.

Tokea uanze mwaka huu kumekuwepo na ukiukwaji mkubwa wa sheria za barabarani kwa watumiaji wa vyombo vya moto hasa madereva wa pikipiki za bodaboda kutokuwa makini katika kuzitii sheria hizo zinazosimamia makutano ya reli na barabara. 

Tokea kuanza kwa mwaka huu wa 2016 ajali nyingi zimeripotiwa hapa jijini Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Manyoni mkoani Singida zikihusisha vyombo hivyo.Wito unatolewa na Uongozi wa TRL kwa watumiaji wa vyombo vya moto boda boda , magari mkubwa na mabasi na wananchi kwa jumla kuzingatia sheria ili kuepuka madhara makubwa  ikiwemo kupoteza maisha, kupata ulemavu wa kudumu na pia upotevu wa rasilimali muhimu ambazo kama zikitumiwa vizuri zitaboresha maisha ya wananchi na Taifa  kwa ujumla.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:
 Kwa niaba ya  Mkurugenzi Mtendaji wa TRL 
Ndugu Masanja Kungu Kadogosa
Julai 27, 2016
DAR ES SALAAM

Tanzania yazidi kupaa matumizi ya simu za mikononi

$
0
0

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbalawa akizungumza kwenye Mkutano wa siku tatu ( Julai 26-28)  unaoendelea jijini Dar es Salaam ukifahamika kama  2016 Mobile 360 Series – Africa  ukihusisha wadau mbalimbali wa mawasiliano ya simu za mikononi.

 Mkurugenzi Mkuu wa GSMA Bw Mats Granryad, akizungumza kwenye mkutano huo.

 Mkurugenzi wa GSMA Afrika Bw Mortimer Hope akizungumza kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo.

 Mkurugenzi wa GSMA Afrika Bw Mortimer Hope akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana nana ripori hiyo.

Tanzania ni miongoni mwa mataifa manane barani Afrika ambayo yana soko kubwa la simu za mikononi, ripoti  mpya ya utafiti  iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam imebainisha.
 
Kwa mujibu wa ripoti hiyo  ijulikanayo;  ‘Uchumi wa simu za mikononi: Afrika 2016’ iliyozinduliwa  kwenye Mkutano wa siku tatu ( Julai 26-28)   unahofahamika kama  2016 Mobile 360 Series – Africa  ukihusisha wadau mbalimbali wa aina hiyo ya mawasiliano, Tanzania  imeungana na mataifa ya Nigeria na Ethiopia ambayo  kwa utatu wao yanachukua zaidi ya theluthi moja  ya soko la aina hiyo ya mawasiliano barani Afrika.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo zaidi ya  watu nusu bilioni barani Afrika kwa sasa wamejiunga  na huduma ya simu za mikononi  huku kukiwa na idadi kubwa ya watumiaji wa aina hiyo ya mawasiliano wanaohamia kwenye huduma ya internet inayopatikana kwenye simu zao, utafiti mpya uliofanywa na na Umoja wa wadau wa Mawasiliano ya simu za mikononi  Duniani  ujulikanao kama GSMA umebaini.
Ripoti hiyo pia iliangazia mchango wa sekta ya mawasiliano ya simu hizo kiuchumi, ikiwemo ajira, ufadhiri kwa umma (Public Funding) pamoja na mchango wa mawasilian hayo katika ukuaji wa digitali na ushirikishwaji wa kifedha.
“Zaidi ya watu nusu bilioni barani Afrika kwa sasa wamejiunga na huduma ya simu za mikononi, hatua ambayo si tu inawaunganisha bali pia inatoa fursa kwao kuweza kupata huduma nyingine kama vile huduma za afya, utambuzi wa kidigitali na huduma za kifedha,’’ alibainisha Mats Granryad, Mkurugenzi Mkuu wa GSMA. “Uhamiaji wa ghafla kwenda kwenye matumizi ya internet ya simu miongoni mwa watumiaji  inatoa fursa mpya kwa watumiaji, biashara, serikali na kukuza mzunguko ambao mwaka jana uliongeza zaidi ya dola bilioni 150 kwenye uchumi wa bara la Afrika,’’
Uwekezaji kwenye mtandao (Network) na simu za kisasa (Smartphones) kunachochea uhamiaji zaidi kwenda kwenye matumizi ya internet ya simu.

 Ripoti hiyo imebaini kuwa kulikuwa na watumiaji milioni 557 wa simu za mikononi kote barani Afrika mwishoni mwa mwaka 2015, sawa na asilimia 46 ya idadi ya watu waliopo kwenye bara hilo na hivyo kufanya bara la Afrika kuwa la pili kwa ukubwa lakini lenye upenyaji hafifu wa aina hiyo ya mawasiliano duniani. Masoko makubwa ya simu za mikononi barani Afrika ni Egypt, Nigeria na Afrika ya Kusini  ambayo kwa pamoja yanachukua takribani theluthi moja ya jumla ya watumiaji wote barani humo. Idadi ya watumiaji inatabiriwa kufikia milioni 725 ifikapo mwaka 2020, ambayo ni sawa na asilimia 54 ya idadi ya watu wanaotarajiwa kuwepo kipindi hicho.
Watumiaji wa simu za mikononi kwasasa wanahamia kwa kasi kwenda kwenye huduma za internet kutokana na ongezeko la mapinduzi ya internet na ongezeko la upatikanaji huduma nafuu za internet. Internet ya 3G/4G ilichukua zaidi ya robo ya watumiaji wa simu mwishoni mwa mwaka 2015, lakini inatarajiwa kuchukua zaidi  ya theluthi mbili ifikapo 2020. Hadi kufikia katikati ya mwaka 2016 kulikuwa na mitandao (networks) ya live 4G ipatayo 72 kwenye mataifa 32 kote barani Afrika, nusu yake imezinduliwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Wakati huo huo idadi ya simu za kisasa barani Afrika inakadiriwa kuwa zaidi ya mara tatu ya sasa miaka mitano ijayo, zikiongezeka kutoka simu milioni 226 mwaka 2015 hadi kufikia milioni 720 ifikapo mwaka 2020.
Mchango wa simu za mikononi kwenye  mapato ya nchi za Afrika (GDP), Ajira na kuongezeka kwa ufadhiri kwa umma (Public Funding)
Matumizi ya teknolojia za simu na huduma zake kote Afrika kulizalisha dola bilioni 153 kwenye uchumi mwaka jana, sawa na asilimia 6.7 ya mapato ya nchi za bara hilo. Mchango huo unatarajiwa kuongezeka hadi kufikia dola bilioni  214 ifikapo 2020 (asilimia 7.6 ya mapato ya nchi (GDP) yanayotarajiwa) wakati mataifa ya Afrika yakiendelea kunufaika kutokana na ongezeko la uzalishaji na ufanisi ulioletwa na kushamiri kwa huduma za simu. Mtandao wa simu za mikononi barani Afrika ulichangia ajira milioni 3.8 mwaka 2015 na kutoa mchango wa dola bilioni 17 kwenye sekta ya umma kupitia jumla ya kodi. Idadi ya ajira zilizozalishwa na sekta hii inakadiriwa kuongezeka hadi kufikia milioni 4.5 ifikapo mwaka 2020 huku mchango wa kodi unakadiriwa kuongezeka hadi kufikia dola bilioni 20.5.
 Ripoti hiyo inaelezea ni kwa namna gani simu za mikononi zinachochea ubunifu kwenye ujasiriamali  barani Afrika. Watoa huduma za simu wamekuwa wakisaidia ujasiriamali kwa kuwezesha uwepo wa huduma kama zile kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu, huduma za malipo kwa njia ya simu na nyingine nyingi.
Teknolojia ya simu pia inachukua nafasi muhimu katika kukabiliana na changamoto za kijamii barani Afrika ikwemo kutoa utambuzi wa kiofisi, upatikanaji wa huduma ya internet pamoja na kutoa huduma za kifedha kwa wanajamii. Idadi ya watu waliojiunga na huduma ya internet kupitia simu barani Afrika imekuwa mara tatu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kufikia milioni 300 mwaka 2015, sawa na robo ya idadi ya watu wote barani Afrika.Ongezeko la watu milioni 250 linatarajiwa kuingia kwenye matumizi ya internet ifikikapo mwaka 2020, na kufanya jumla iwe watu milioni 550 (asilimia 41 ya idadi ya watu inayokadiriwa wakati huo)
 “Athari za mabadiliko chanya kwenye sekta ya simu yanaonekana kwa kina zaidi barani Afrika kuliko sehemu nyingine yoyote barani Afrika; Sekta ya simu za mikononi barani Afrika ipo mstari wa mbele katika kusaidia kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa,’’ aliongeza Granryd. “Tunajikita katika kuandaa baadae nzuri kwa wananchi na biashara kote barani Afrika, kutoa huduma muhimu za mawasiliano, ajira bora,  fursa za kiuchumi, uzalishaji zaidi pamoja na ushindani,’’
 Ripoti mpya ya ‘Uchumi wa simu za mikononi: Afrika 2016’ ipo chini ya idara intelijensia ya GSMA. Ili kupata ripoti kamili pamoja na taarifa nyingine, tafadhari tembelea: http://www.gsma.com/mobileeconomy/africa/.

MSANII NAY WA MITEGO ATOZWA FAINI YA TSH. MILIONI 1, AFUNGIWA.

$
0
0
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki (Ney wa Mitego).
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia kwa kipindi kisichojulikana Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kwa jina la Nay wa Mitego hadi hapo litakapojiridhisha kwamba ametekeleza maagizo yote aliyopewa na Baraza sambamba na yeye kubadilika katika kubuni kazi zenye maadili na zisizo dhalilisha watu wa kada mbalimbali.

Maagizo aliyopewa Msanii Nay ni pamoja na kulipa faini (adhabu) ya kiasi cha Shilingi milioni 1, kufanya marekebisho ya mashairi ya wimbo wake wa ‘Pale Kati’, kufuata sheria, kanuni na taratibu za urasmishaji sekta ya Sanaa kwa maana ya kusajiliwa na BASATA na kuhakikisha wimbo wake umefuata taratibu zote. 

Aidha, Msanii Nay ameagizwa kuwaomba radhi watanzania kwa kutoa kazi ya muziki yenye kuvunja maadili na kudhalilisha watu wa kada mbalimbali hususan wanawake.

Maamuzi haya yamefanyika kwa mujibu wa kifungu cha 4(2) cha sheria nambari 23 ya mwaka 1984, ikisomwa pamoja na kifungu cha 30(1)(2) na waraka wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo wa tarehe 16/7/2009 ambayo kwa sasa inafahamika kama Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Adhabu hizi zimetolewa kufuatia BASATA kufanya kikao cha pamoja na Msanii huyu jana siku ya Jumanne tarehe 26/07/2016 kwenye Ukumbi wa Baraza na yeye kukiri makosa na kuahidi kubadilika.

Makosa aliyosomewa na yeye kuyakiri kwa maandishi ni pamoja na;
1. Kujihusisha na shughuli za Sanaa pasipo kusajiliwa na BASATA.
2. Kutoa wimbo wa “Pale Kati” na kuupakia katika mitandao ya kijamii bila kuuleta kufanyiwa uhakiki wa maudhui yake.

3.Maudhui ya wimbo wa ‘Pale Kati’ kwa sehemu kubwa hayafai kwa matumizi ya wazi na ni kinyume cha sheria za nchi na maadili ya mtanzania.
Ikumbukwe kwamba mnamo tarehe 16/07/2016 BASATA lilitoa taarifa kwa umma ya kuufungia wimbo wa Pale Kati kufuatia kubeba maudhui yenye uvunjifu mkubwa wa maadili na kupambwa na picha dhalilishi kwa wanawake. 

Aidha, tarehe 12/02/2016 BASATA liliufungia wimbo wa Shika Adabu Yako wa Msanii huyuhuyu kwa makosa yanayofanana na haya. Hivyo adhabu hii imetolewa ili kumpa muda wa kujifunza, kujitathimi na kujirekebisha kama kweli ana nia ya kuendelea kufanya kazi ya muziki 
SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI
Godfrey L. Mngereza 
KATIBU MTENDAJI, BASATA.

JAJI MKUU ATEMBELEA JENGO LA MAHAKAMA YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI LEO.

$
0
0

 Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman (Katikati) akimsikiliza Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania, Khamadi Kitunzi akimuelezea jambo alipotembelea jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililoko kwenye Shule ya Sheria (Law School) Sinza jijini Dar es salaam. Kulia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Ferdinand Wambali.
  Hili ni jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililopo kwenye Shule ya Sheria (Law School) Sinza jijini Dar es salaam.
  Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman (Katikati) akimuelezea jambo Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga alipotembelea  jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililoko kwenye Shule ya Sheria (Law School) Sinza jijini Dar es salaam. Kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Ferdinand Wambali.  

Leaders to convene in Dar on enabling African businesses

$
0
0
Although recent growth rates in Africa are celebrated in policy and development circles, significant challenges remain with regard to realising the potential of the private sector in Africa. Enabling businesses to enhance the competitiveness of the continent, create employment opportunities and enhance Africa’s economic growth and sustainable development will be the focus of the African Leadership Forum this year. 

The Forum, which will take place on the 28th-29th July, is the third in a series of annual high-level meetings convened by H.E. Benjamin W. Mkapa, former President of Tanzania, with the support of UONGOZI Institute.

According to a statement released by UONGOZI Institute, the African Leadership Forum 2015, with the theme of ‘Enabling African Businesses to Transform the Continent’, will bring together more than 100 key influential leaders and thinkers across the continent, including former Heads of State and leaders from business, government, civil society and academia.

Former Presidents H.E. Joaquim Chissano and H.E. Armando Guebuza of Mozambique, H.E. Thabo Mbeki of South Africa, H.E. Hifikepunye Pohamba of Namibia and H.E. Bakili Muluzi of Malawi are also set to attend the Forum.

“The forum builds on the success of the inaugural dialogue in 2014 on Meeting the challenges of Africa’s transformation and the dialogue in 2015 on Moving towards an integrated Africa”, said the statement, “this year’s event will provide a platform to deliberate on the obstacles preventing African business from flourishing, and what needs to be done about them.”

The African Leadership Forum 2016 will begin with a public plenary on the 28th of July where Mr. Sipho Nkosi, former President of the Chamber of Mines of South Africa will deliver the Keynote Address.

At the end of this one-day event, it is expected that an official statement from participants will be produced, with recommendations on the way forward.

ASKARI ALIYEMUUA MWANAHABARI DAUDI MWANGOSI AFUNGWA JELA MIAKA 15

$
0
0

Na MatukiodaimaBlog , Iringa

MAHAKAMA kuu kanda ya Tanzania kanda ya Iringa imemhukumu kwenda jela miaka 15 askari Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia ( FFU )Iringa namba G 58 Pacificius Cleophace Simon (27) kwa kosa la kumuua bila kukusudia mwaahabari Daudi Mwangosi mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi. wakati akiwa katika majukumu yake ya kuchukua habari huku mke wa marehemu Mwangosi Itika Mwangosi akipongeza vyombo vya habari nchini kwa ushirikiano mkubwa katika kufuatilia kesi hiyo. 


"Mahakama inatambua uchungu wa familia iliyoupata kwa kifo cha marehemu Daudi Mwangosi ambaye aliuwawa pia marehemu aliuwawa kikatili ....siku zote adhabu inapaswa kulingana na kosa husika mahakama haiafiki maombi ya wakili wa upande wa utetezi kuomba mshtakiwa apewe adhabu ya kuachiwa huru kwa kuwa ni yatima ....mgongano wa hisia umeonekana katika kesi hii ila mahakama inampa adhabu ya kwenda jela miaka 15" alisema jaji Dkt Paul Kiwelo.

Akisoma shauri ya kesi hiyo kabla ya kutoa adhabu leo mahakamani hapo jaji Dkt Kiwelo aliwashukuru wazee wa baraza la mahakama kwa michango yao mkubwa mchango ulioisaidia mahakama hadi kufikia siku hiyo ya hukumu pia mawakili wote walioshiriki katika kesi hiyo.

" Suala la aina gani ya adhabu inafaa halikuwa rahisi sana kwani shauri hili upande wa jamhuri uliomba adhabu ya kufungwa maisha jela huku upande wa utetezi ukiomba mshitakiwa aachiwe huru kwa masharti ambayo mahakama ingeona yanafaa kutokana na kuwa na majukumu ya kulea wadogo zake na yeye kuwa yatima .....mahakama imetazama ukubwa wa kosa husika pia jamii ina mtazamo gani katika kesi hiyo lakini mahakama haitoi hukumu kwa mitazamo mbali mbali inatumia vifungu vya sheria suala la kutoa adhabu ni la kisheria si vinginevyo".

Jaji Dkt Kiwelo alisema kuwa adhabu haitolewi kwa ajili ya kulipiza kisasi ila inatolewa kama sehemu ya onyo na kuifanya jamii kutambua kuishi kwa kuheshimu misingi ya sheria kwani kuna mambo manne katika kesi yanatazamwa likiwemo la medhania ya kosa alilotenda na aina ya kosa pia maslahi ya jamii katika kosa husika.

Mjane wa marehemu Daudi Mwangosi akizungumza na wanahabari ikiwa ni pamoja na kuwashukuru kwa umoja wao .


Rais wa umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania Bw Deo Nsokolo akizungumza na wanahabari baada ya hukumu ya kesi ya mauwaji ya Mwangosi .

Wanahabari mkoa wa Iringa wakimsikiliza Bw Nsokolo leo





Wanahabari wakiwa nje ya viwanja vya mahakama baada ya kesi kumalizika .


Mjane wa Mwangosi Itika Mwangosi mwenye kilemba akitoka mahakamani hapo huku akiwa na uso wa furaha baada ya hukumu kutolewa kwa muuaji kufungwa miaka 15 jela .

Mjane wa Mwangosi akiwa katika viwanja vya mahakama kuu kanda ya Iringa
Rais wa UTPC Deo Nsokolo akiwa na mtaalam wa IT Lukelo Mwaipopo leo nje ya mahakama kuu kanda ya Iringa
"Naomba kusema mgongano wa hisia umeonekana katika kesi hii pamoja na kuwepo kwa changamoto hizo bado mahakama haijayumbishwa na migogano hiyo .....mahakama haiitoi hukumu kwa kutazama ni kosa la kwanza wala mhusika hana rekodi mbaya ya makosa mahakama inaendeshwa kwa sheria ndugu wangefurahi kuona mtuhumiwa anafungwa hivyo siafiki maombi ya upande wa utetezi juu ya mkosaji naamini kabisa kwa kosa hili kumwachia kwa Masharti haki haitakuwa imetendeka"




Ndugu wa Marehemu Daudi Mwangosi mama Mfugale kushoto akitoka mahakama kuu kanda ya Iringa akiwa na furaha baada ya hukumu ya kesi hiyo kutolewa leo kwa askari aliyeuwa kufungwa jela miaka 15 Picha zote na MatukiodaimaBlog .

Mjane wa marehemu Daudi Mwangosi Itika Mwangosi mwenye kilemba cheusi akiwa katika foleni ya ukaguzi wa polisi ili kuingia mahakama kuu kanda ya Iringa leo .
Mjane wa marehemu Daudi Mwangosi Itika Mwangosi mwenye kilemba cheusi akiwa katika foleni ya ukaguzi wa polisi .

Mjane wa marehemu Daudi Mwangosi Itika Mwangosi mwenye kilemba cheusi akifurahi jambo na ndugu yake mzee Marko Mfugale mahakamani hapo leo .
Mdogo na marehemu Mwangosi Bw Mecky Mwangosi kulia akisalimiana na Rais wa UTPC Deo Nsokolo kabla ya mahakama kuanza leo

Kwa mujibu wa sheria kuua bila kukusudia ni kosa kubwa sana ambapo adhabu yake huwa ni kufungwa jela maisha japo kila kosa huamuliwa kutokana na mazingira yake hivyo lazima upewe adhabu ambayo itakuwa funzo kwa wengine." Kuua si jambo dogo na mahakama hii kwa kuzingata vifungu vya sheria na pia mtuhumiwa umekaa mahabusu miaka minne inakuhukumu kwenda jela miaka 15 rufaa ipo wazi kwa asiyeridhika".

Akizungumza na wanahabari mara baada ya hukumu hiyo aliyekuwa wakili wa utetezi Lwezaula Kaijage alisema kuwa alisema kuwa yeye alikuwa ni wakili wake na kuwa kwa sasa hawezi kusema ni uamuzi gani ambao mteja wake anaweza kuchukua hadi hapo atakapowasiliana nae .


" Nafikiri wote mlikuwepo mahakamani mmesikia kuwa amefungwa miaka 15 itabidi sasa mimi niende magereza kuzungumza nae ili nichukue sheria nione zinasemaje pia kuomba mwenendo mzima wa sheria kuona jinsi ulivyokwenda ili nione ni kitu gani ambacho labda mahakama ilielekezwa vibaya kabla ya kutoa hukumu hiyo kama nitaona kuna jipya basi tutakwenda kwenye rufaa".

Wakili wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu ((THRDC)Benedict Ishabakaki alisema kuwa katika hukumu hiyo mahakama kuu kanda ya Tanzania kanda ya Iringa imetenda haki pasipo kuegemea upande wowote na kuwa pamoja na nguvu kubwa ya polisi na jinsi ambavyo ushahidi uliokuwa umepelekwa kulenga kumnasua mwenzao ila mahakama hiyo imetumia ushahidi wa ungamo la mlinzi wa amani kutoa hukumu ambayo kimsingi haijaacha maswali kwa wananchi .

Wakili Shabakaki alisema kuwa kesi hiyo polisi waliifanya kama kesi ya nyani kumhukumu ngedele kwa kula mahindi kwani alisema aliyetenda kosa alikuwa ni askari ,mchunguzaji wa kesi hiyo ni askari hivyo katika mazingira hayo haikuwa rahisi kesi hiyo kufikia hukumu hiyo ila mahakama imetenda haki na kuwa wao kama watetezi wa haki za binadamu wataona ni hatua zipi za kuchukua baada ya mahakama kutenda haki .


Alisema pamoja na jukumu la polisi la ulinzi wa jamii ila polisi baadhi yao wameendelea kukiuka wajibu wao na kuogopwa zaidi na raia jambo ambalo si jema na kuwa nguvu kubwa iliyotumika siku zote wakati wa kesi hiyo ni kielelezo tosha kuwa polisi walikuwa wakitegemea mwisho wa siku mwenzao huyo kuachiwa huru . 


Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deo Nsokolo alisema kuwa wao kama UTPC wanapongeza mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Iringa kwa kutenda haki katika kesi hiyo kwani alisema kuwa jeshi la polisi walipanda kuharibu kesi hiyo ila jaji kwa umakini wake ametoa adhabu .


" Sisi kama wanahabari tunajipongeza pia kwa hukumu hii kwanza kutiwa hatiani kwa mtuhumiwa na pili kufungwa jela miaka 15....... na ifahamike kuwa kesi hiyo ilikuwa ikiihusu serikali hivyo hukumu ya kesi hiyo imeingia katika rekodi ya dunia kuwa mwandishi aliuwawa na muuaji amefungwa miaka 15 jeshi la polisi Iringa kwa muda wote limekuwa likiwanyanyasa waandishi hivyo sisi kama viongozi wa wanahabari tutakwenda kuonana na viongozi wao wa juu".

Alisema kuwa yapo mambo ya msingi ambayo jeshi la polisi linapaswa kufanya ila si kwa kutumia nguvu kubwa kunyima uhuru wa vyombo vya habari hasa katika kesi hiyo ya Mwangosi .

" Polisi katika kesi nyingine wamekuwa wakiwasaidia wanahabari kupata picha kirahisi kwa watuhumiwa pindi wanapofikishwa mahakamani ila katika kesi hiyo wamekuwa wakimfunika mwenzao na kuzuia waandishi kupiga picha ila pamoja na yote hayo adhabu imetolewa pale pale"

Makamu Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile alisema kuwa polisi Iringa walitamani kuona kesi hiyo inaharibika na kama lisingelikuwa ungamo la mlinzi wa amani mtuhumiwa huyo alikuwa anaachiwa huru na ungamo chini ya mlinzi wa amani ni mahakama yenyewe hivyo ni wazi mahakama imeweza kutenda haki zaidi .


" Adhabu ni kumfanya mtu ajirekebisha na wapo waliotegemea kuwa muuaji wa Mwangosi nae ana hukumiwa kufa ila si haki binadamu ....lakini mtuhumiwa huyo wakati wote wa kesi hiyo hakupaswa kufikishwa mahakamani na polisi wenzake badala ya askari wa magareza ambao ndio wanawajibu wa kumpeleka mahakamani na mahabusu ila .....hata leo baada ya hukumu hatujui amepelekwa wapi maana wameondoka nae wao wenyewe ambao walitaka kesi ivurugike sasa sijui wanampeleka rumande ama gerezani au wamempeleka nyumbani kwanza kula chakula lakini naomba hili kuliacha hapo"

Bw Balile alisema kuwa kwa sasa wanaanzisha mchakato wa kufungua kesi ya madai kwa ajili ya familia ya Mwangosi na kuwa kujua ni mahakama ya ndani ama ya Afrika ambayo kesi hiyo itafunguliwa itajulikana baada ya kwenda kukaa na viongozi wenzake japo alisema haki yote itafikishwa kwa familia ya Mwangosi .

Juzi Julai 25 mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Iringa ilimkuta na hatia askari Simon katika kesi hiyo namba 45 ya mwaka 2013 ya mauaji ya bila kukusudia ya mwahabari Mwangosi aliyeuwawa kinyama Septemba 2 mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi wakati chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) wakifanya uzinduzi wa matawi huku kukiwa na katazo la matukio ya mikutano ama mikusanyiko ya kisiasa kutokana na serikali kuongeza muda wa kuendelea na zoezi la senza ya watu na makazi.

Mjane wa marehemu Mwangosi Bi Itika Daudi Mwangosi alitoa pongezi nyingi kwa wanahabari kwa ushirikiano wao wakati wote wa kesi hiyo hadi ilipofikia mwisho .

" Napenda kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutufikisha salama siku hii ya leo .....na niishukuru mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Iringa kwa kuweza kutenda haki pili ninawashukuru sana ninyi waandishi wa habari kwa umoja wenu ...nawashukuru sana tena sana zaidi ya sana hata kama mtu amekutendea wema gani Mungu alitupa neno moja tu la ahsante pia napenda kuwatia moyo msiogope songeni mbele Mungu yu paoja nanyi kama alivyowapigania hadi kufika leo atazidi kuwapigania zaidi teteeni kazi zenu elimisheni jamii vile mnavyoendelea kusaidia jamii ndivyo Mungu anavyowabariki daima sina neno la zaidi zaidi ya ahsante ".


Marehemu Daudi Mwangosi aliuwawa kinyama Septemba 2 mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wakati wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kilipokuwa kikifanya mikutano ya ufunguzi wa matawi wakati kukiwa na zuio la mikutano hiyo kutokana na kuongezwa kwa muda wa senza ya watu na makazi .

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA APOKEA SALAAM MAALUM KUTOKA SUDAN YA KUSINI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia)akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Sudan ya Kusini Mhe. Stephen Dhieu Dau Ayik aliyeleta ujumbe maalum wa Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na kupokelewa na Makamu wa Rais ,Ikulu jijini Dar es Salaam 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia)akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Sudan ya Kusini Mhe. Stephen Dhieu Dau Ayik pamoja na ujumbe wake walioleta ujumbe maalum wa Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na kupokelewa na Makamu wa Rais ,Ikulu jijini Dar es Salaam 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Sudan ya Kusini Mhe. Stephen Dhieu Dau Ayik pamoja na ujumbe wake ambao walileta ujumbe maalum wa Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na kupokelewa na Makamu wa Rais ,Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemtumia ujumbe maalum Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru kwa jitihada za serikali ya Tanzania za kusaidia kupatikana kwa amani katika nchi hiyo.

Ujumbe huo wa Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir umewasilishwa nchini na Waziri wa Biashara na Viwanda wa nchi hiyo Stephen Dhieu Dau Ayik kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ikulu jijini Dar es Salaam Tarehe 27-Jul-16.

Waziri huyo wa Serikali ya Sudan Kusini Stephen Ayik amesema hali ya usalama kwa sasa imeendelea kuimarika kufuatia kusitishwa kwa mapigano kati ya wanajeshi watiifu wa Rais Salva Kiir na wanajeshi wa watiifu wa Aliyekuwa Makamu wa Rais Riek Machar.

Akipokea ujumbe maalum wa Serikali ya Sudan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali ya Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha amani inapatikana katika Taifa hilo changa barani Afrika ambayo itawezesha wananchi wa taifa hilo kufanya kazi za maendeleo kwa amani na utulivu. 

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pia amezitaka pande hizo MBILI zinazohasimiana kuzingatia na kuheshimu mkataba wa amani waliosaini jijini Arusha mwaka 2015 uliolenga kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe na kurejesha amani katika Taifa hilo. 

Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa kufanyika kwa mazungumzo ya amani ya kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huo ili kukomesha vita ambavyo vimekuwa vikigharimu mali na maisha ya mamia ya wananchi wa Sudan Kusini.

TAMASHA KUBWA LA MUZIKI WA DANSI KUFANYIKA JUMAMOSI KATIKA VIWANJA VYA LEADERS JIJINI DAR

$
0
0


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wanamuziki hao kuhusu tamasha hilo la muziki wa dansi nchini. Picha na Geofrey Adroph.
Mdau wa muziki wa dansi, Asha Baraka akizungumza katika mkutano huo kuhusu tamasha hilo la kukata na shoka ambalo alijawahi kufanyika hapa nchini.
Mwanamuzi wa mziki wa dansi, Ali Choki akiwaongoza wenzake kutoa burudani mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda walipofika ofisini kwake leo, kuzungumzia Tamasha la muziki huo litakalofanyika Jumamosi Viwanja vya Leaders ambalo litashirikisha bendi 10 maarufu za hapa nchini.
Baadhi ya waandishi wakiwa kazini.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wanamuziki wa dansi baada ya kuzungumza nao ofisi kwake.

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI, DK ANGELINA MABULA AAGIZA HALMASHAURI YA UYUI KUKAMILISHA UNUNUZI WA NYUMBA ZA NHC UYUI

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akitembelea nyumba za gharama nafuu Uyui zilizopo Isikizya wilayani Uyui, Tabora ambapo ameiagiza Halmashauri ya Uyui kulipia nyumba zilizojengwa na NHC ili watumishi wake waweze kuhamia. Kushoto kwake ni Meneja wa NHC mkoani Tabora, Dickson Ngonde.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tabora muda mfupi baada ya kutembelea nyumba za gharama nafuu Uyui ambapo ameiagiza Halmashauri ya Uyui kulipia nyumba zilizojengwa na NHC ili watumishi wake waweze kuhamia. PICHA ZOTE ZA KITENGO CHA MAWASILIANO KWA UMMA NA HUDUMA KWA JAMII CHA NHC.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akisikiliza taarifa kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Ardhi Tabora, Bw. Biseko Musiba wakati Waziri huyo alipofanya ziara katika mkoa wa Tabora na kujione hali ya maendeleo ya sekta ya ardhi mkoani humo pamoja na kutembelea miradi ya maendeleo ya taasisi zake.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akimsikiliza Kamishna Msaidzi wa Kanda ya Magharibi, Dorothy Wanzala wakati akikagua masjala ya ardhi ya Tabora.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akisoma mojawapo ya mafaili yaliyopo katika masjala ya Ardhi huku Kamishna Msaidizi wa Kanda ya Magharibi, Dorothy Wanzala akishuhudia.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Tabora muda mfupi baada ya kufika katika ofisi hizo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akizungumza na watumishi mbalimbali wa sekta ya ardhi mkoani Tabora.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Tabora muda mfupi baada ya kufika katika ofisi hizo.

SERIKALI ZA TANZANIA NA KOREA, ZIMETILIANA SAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Hamis Shaban na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo wakibadilishana Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo baada ya kusainiwa. Hati hiyo ina thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 650.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Hamis Shaban na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo wakisaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo, yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 650.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Hamis Shaban na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo wakipeana mikono baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo, yenye thmani ya zaidi ya dola za Marekani milioni 300, katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Wizara ya Fedha ya Korea Weon-Kyoung Jo (kushoto) akizungumza wakati wa mjadala wa Ushirikiano katika misaada ya maendeleo ya kiuchumi kabla ya kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Korea, yenye thamani ya dola Milioni 300, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dar es salaam.


Na Benny Mwaipaja,MoFP 

SERIKALI za Tanzania na Korea Kusini, zimetiliana saini Hati ya Makubaliano (Aide Memoire) kwa ajili ya Ushirikiano wa utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo wa Maji, Nishati, Kilimo, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano-TEHAMA na Viwanda itakayogharimu Dola za Marekani Milioni 300, sawa na TSh.Bilioni 650, katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka 2016 hadi 2020.

Fedha hizo ni sawa na ongezeko la Dola Milioni 100 ikilinganishwa na kiasi cha Dola Milioni 200 ambazo nchi hiyo ya Korea iliipatia Tanzania kama mkopo wenye masharti nafuu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita (2014 hadi 2016). 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaaban, ametia saini makubaliano hayo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, huku upande wa Korea Kusini ukiwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Fedha ya Korea Bw. Weon-Kyoung Jo. 

Kusainiwa kwa makubaliano hayo ni mwanzo wa matayarisho ya kuandaa Mpango kazi wa namna ya kutekeleza miradi hiyo ili iende sambamba na Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa miaka 5 uliozinduliwa hivi karibuni mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Mkakati Mbadala wa Kupunguza Umaskini Zanzibar (MKUZA Successor Strategy). 

Akizungumza mara baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaaban, amesema kuwa miradi hiyo ya maendeleo iliyochaguliwa kutekelezwa katika sekta zilizotajwa zitachochea ukuaji wa uchumi wa Taifa na kupunguza umasikini kwa wananchi. 

Bi. Amina Shaaban alisema kwamba Hati hiyo ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Korea Kusini, yamejikita zaidi katika uboreshaji wa mifumo ya Tehama, kuimarisha sekta ya kilimo pamoja na kuboresha miundombinu inayosaidia ukuaji wa viwanda hususan ya nishati ya umeme katika kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2016/17 hadi 2020/21. 

“Ushirikiano wa Tanzania na Korea Kusini umeanza tangu mwaka 2000, kwa kuhusisha taasisi zake mbili ambazo ni Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA) ambalo limeipatia Tanzania kiasi cha zaidi ya dola za Marekani 30.9 na Benki ya Exim-Korea ambayo imetoa Dola za Marekani zaidi ya Milioni 455 sawa na zaidi ya Tsh 900 bilioni kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii katika kipindi cha miaka 10 iliyopita” alisema Bi. Amina Shaaban

TANZANIA YAENDELEA KUPATA MAFANIKIO KATIKA KUKABILIANA NA UGONJWA WA VIKOPE (TRACHOMA)

$
0
0
Na. Aron Msigwa – Dar es salaam.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeeleza kuwa licha ya Tanzania kuendelea kupata mafanikio katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Vikope (Trachoma) jamii bado inalojukumu la kuendelea kuzingatia na kufuata kanuni za afya kwa kufanya usafi wa mwili na mazingira ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo. 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa Wadau wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele wenye lengo la kuutokomeza ugonjwa wa Vikope, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Neema Rusibamayila amesema kuwa Tanzania imepiga hatua katika kupunguza ugonjwa huo ikishirikiana na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Amesema kupitia idadi ya wagonjwa wanaougua vikope imeendelea kupungua mwaka hadi mwaka kupitia afua mbalimbali chini mpango ujulikanao kama “SAFE” ambao unahusisha huduma za Upasuaji,utoaji wa dawa za Antibayotiki, kuosha uso pamoja na usafi wa mazingira.

Ameeleza kuwa wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeweza kufanikisha upunguzaji wa ugonjwa huo kwa kutoa dawa/tiba kinga kwa wananchi katika maeneo yaliyoathirika ambapo amesema kufuatia utafiti uliofanyika mpaka sasa wilaya 22 ugonjwa huo umepungua sana kiasi cha wananchi wa maeneo hayo kutohitaji dawa za tiba kinga.

Aidha, amesema kuwa juhudi za sasa ni kuendelea kuwaelimisha wananchi kuendelea kuchukua hatua kwa kufanya usafi ikiwemo unawaji wa uso pamoja pia kuwaangalia wale waliokwisha kuugua ugonjwa wa Vikope (Trachoma) ili waweze kufanyiwa upasuaji.

“Baada ya mtu kupata ugonjwa huu kope za mgonjwa huingia ndani , kope za mtu ambaye hana ugonjwa huu hutoka nje, zikiingia ndani zinakwaruza jicho na mtu asipofanyiwa upasuaji kope zake mapema na kuziacha zikaendelea kukwaruza jicho mwisho mgonjwa huyu hupata upofu” Amesisitiza Rusibamayila.



Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Neema Rusibamayila akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano uliowahusiaha Wadau wa Wizara hiyo na washirika wa maendeleo Maendeleo kutoka Mfuko wa Malkia Elizabeth unaojihusisha na utokomezaji wa Ugonjwa wa Vikope na wale wa Idara ya Kimataifa ya Maendeleo (DFID).
Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Malkia wa Uingereza unaojihusisha na utokomezaji wa ugonjwa wa Vikope katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania (The Queen Elizabeth Diamond Jubilee Trust Trachoma Initiative) Dk. Aristid Bonifield akieleza namna Mfuko huo utavyoendelea kuisaidia Tanzania kwa kuwa inafanya vizuri katika kuhakikisha ugonjwa huo unatokomezwa nchini leo jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Idara ya Kimataifa ya Maendeleo nchini Tanzania (DFID) Vel Gnanendra akifafanua namna wadau wa maendeleo walivyojipanga kuiunga mkono Tanzania kwa kuhakikisha ugonjwa wa vikope (Trachoma) unatokomezwa nchini.
Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele, Upendo John Mwingira akizungumza wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Sightsavers kutoka Uingereza Dk. Caroline Harper akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa kutokomeza ugonjwa wa Vikope leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Sightsavers kutoka Uingereza Dk. Caroline Harper akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa kutokomeza ugonjwa wa Vikope leo jijini Dar es salaam.
Washiriki wa Mkutano wa Kutokomeza Ugonjwa wa Vikope kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto na Wale wa Mashirika ya Kimataifa wakiwa katika picha ya Pamoja leo jijini Dar es salaam.Picha/Aron Msigwa – MAELEZO.
Amefafanua kuwa mashirika mbalimbali yamekuwa mstari wa mbele katika kufanikisha zoezi hilo ikiwemo Shirika na la Msaada la Kimataifa la Uingereza (DFID) pamoja na Mfuko wa Malkia ya Uingereza (The Queen Elizabeth Diamond Jubilee Trust) ambao umekua ukitoa fedha kutokomeza ugonjwa wa Trakoma , shirika la Sightsavers, Shirika la Helen Keller International (HIK) Tanzania pamoja na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali ambayo mengine yapo Kongwa mkoani Dodoma na Kilimanjaro ambao hushirikiana na wizara kuwatafuta wagonjwa kwa lengo la kutoa matibabu.

Amesema mpaka sasa kuna wilaya 18 ambazo zinakabiliwa na ugonjwa huo na kufafanua kuwa juhudi za kuwapata walioathirika zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuwapata wale walioathirika kwa lengo la kuwafanyia upasuaji na kuwapatia dawa ya tiba kinga pia kuwaelimisha ili waweze kubadili tabia kwa kuwa wasafi.

“Tunaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo uelimishaji wa wananchi wa maeneo husika wachukue hatua, tunajua ugonjwa huu unaletwa na nzi, tunawahimiza wananchi wanawe uso kuondoa uchafu na kuzuia nzi wanaosambaza ugonjwa huo kutua kwenye macho yao” Amesisitiza Dk. Dk.Neema Rusibamayila.

Aidha, amewashukuru wadau hao wa maendeleo kwa kuendelea kutambua mchango wa Tanzania katika mapambano dhidi ya magonjwa hayo na pia kuendelea kutimiza malengo ya kidunia ambayo yanaeleza kwamba ifikapo mwaka 2020 Tanzania iwe imeondoa ugonjwa wa vikope nchini.

Akizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili kampeni ya kuwafikia wale walioathirika katika maeneo yaliyo na ugonjwa huo hasa kwenye jamii za wafugaji amesema ni pamoja na hali ya wananchi hao huishi kwa kuhamahama pia sababu za mazingira hasa miundombinu ya barabara ambayo imekua kikwazo cha kuzifikia jamii hizo hasa wakati wa kipindi cha mvua.

Kwa upande wake Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Upendo John Mwingira akizungumza wakati wa mkutano huo amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi za Bara la Afrika ambazo zimekuwa zikinufaika na fedha kutoka Shirika la Kimataifa la Uingereza na DFID na mfuko wa ulioanzishwa wa kumuenzi Malkia wa Uingereza kwa miaka 60 ya Utawala wake unaojihusisha na utokomezaji wa ugonjwa wa Trakoma katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika Tanzania ikiwemo.

Amesema ugonjwa wa Vikope nchini Tanzania kwa mujibu wa Takwimu uko katika wilaya 56 na kueleza kuwa kutokana na juhudi ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Serikali kuanzia mwaka 1990 hali inaonesha kuwa maabukizi yameshuka hasa katika wilaya 22 ambako wananchi hawahitaji tena ugawaji wa dawa.

Amesema kuwa hali ya maambukizi katika maeneo hayo imekuwa zaidi kwa watoto na wanawake kwenye maeneo yenye ukame na shida ya maji ikiwemo mkoa wa Manyara na Dodoma na kubainisha kuwa mpaka sasa ni wilaya 18 ambazo zinahitaji huduma ya dawa katika mkoa wa Arusha , Manyara, Dodoma katika wilaya ya Kongwa, Chemba na Chamwino.

“Naweza kusema jitihada tunazofanya ni kubwa na kazi bado ipo hasa maeneo ya wafugaji ambao baadhi yao wamekuwa wakitumia kifaa Fulani ambacho kinaweza kunyofoa zile kope zinazowasumbua ili kuondoa usumbufu bila kujua hali hiyo inatengeneza tatizo zaidi, ni changamoto kwetu, tunahitaji kuendelea kuwaelimisha” Amesisitiza.

Ameeleza kuwa kupitia juhudi mbalimbali zilizofanyika wanajiandaa kufanya tathmini katika wilaya zipatazo 10 katika kipindi cha mwaka huu kuangalia maambukizi yamefikia wapi kwa lengo la kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Trakoma na kupunguza hali ya maabukizi katika wilaya hizo.

Akizungumzia idadi ya wagonjwa katika wilaya 56 ambazo maambukizi ya ugonjwa huo yapo ilikadiliwa kwamba kuna maambukizi ya watu takribani 160,000 ambao wameambukizwa tayari Vikope na kubainisha kwamba kuna mikakati mbalimbali ilifanywa na Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuendesha upasuaji kwa wagonjwa wenye tatizo hilo hali iliyoshusha kiwango hicho hadi kufikia wagonjwa 80,000 mwaka huu.

Amesema chini ya ufadhili wa wadau hao wa miaka 5 wagonjwa takribani 50,000 wenye tatizo la vikope watafanyiwa upasuaji, huku Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine ikiendelea kutafuta fedha za kuwafikia wagonjwa 30,000 watakaobaki.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Kimataifa ya Maendeleo nchini Tanzania (DFID) Vel Gnanendra amesema kuwa wao kama wadau wa maendeleo wataendelea kuiunga mkono Tanzania kwa kuhakikisha ugonjwa wa vikope (Trachoma) unatokomezwa nchini.

“Tunafurahia ushirikiano huu kutoa mchango wetu kuisaidia Tanzania kutokomeza ugonjwa wa Vikope (Trachoma), kuzuia maumivu na mateso yanayosababishwa na ugonjwa huu yanayowafanya watu kuangukia katika lindi la umasikini, Tunaiahidi Serikali ya Tanzania kuwa kupitia ushirikiano huu tutautokomeza ugonjwa huu na kubadili maisha ya wengi miaka ijayo” Amesisitiza Gnanendra.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Malkia wa Uingereza unaojihusisha na utokomezaji wa ugonjwa wa Vikope katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania Dk. Astrid Bonfield CBE amesema kuwa Mfuko huo utaendelea kuisaidia Tanzania kwa kuwa inafanya vizuri katika kuhakikisha ugonjwa huo unatokomezwa nchini.

Amesema Mfuko wa Malkia Elizabeth utafanya kazi bega kwa bega na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuhakikisha kuwa hakuna mtanzania anayepoteza haki ya kuonakutokana na ugonjwa wa vikope.

" Kwa pamoja tutahakikisha hakuna mtanzania anayepata shida na madhara yanayotokana na ugonjwa wa Vikope, tutafanya kazi na Serikali ya Tanzania tukishirikiana na wadau wengine wa Maendeleo na mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali kutokomeza ugonjwa huu" Amesisiza Dk. Astrid.

JAJI MKUU ATEMBELEA JENGO LA MAHAKAMA YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI LEO.

$
0
0
  Hili ni jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililopo kwenye Shule ya Sheria (Law School) Sinza jijini Dar es salaam.
 Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman (Katikati) akimsikiliza Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania, Khamadi Kitunzi akimuelezea jambo alipotembelea jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililoko kwenye Shule ya Sheria (Law School) Sinza jijini Dar es salaam. Kulia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Ferdinand Wambali.
  Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman (Katikati) akimuelezea jambo Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga alipotembelea  jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililoko kwenye Shule ya Sheria (Law School) Sinza jijini Dar es salaam. Kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Ferdinand Wambali. 

MKATABA KATI YA TTCL NA BHART AIRTEL WAISHA RASMI

$
0
0
Serikali imehitimisha ubia kati ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), na Kampuni ya Bhart Airtel ya India kwa kuilipa kampuni hiyo Shilingi Bilioni 14.9 na hivyo kuirudisha TTCL mikononi mwa Serikali kwa asilimia miamoja.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hatua hiyo ni mkakati wa Serikali wa kuiwezesha TTCL kujitegemea ili kuzalisha faida, Kuimarisha Miundombinu yake, na kutoa gawio Serikalini. “Tunawataka TTCL mjipange vizuri mjitangaze ili muwe kampuni kubwa na bora ya mawasiliano hapa nchini”, amesema Prof. Mbarawa.

Waziri Prof. Mbarawa amesema katika kuiongezea nguvu TTCL Serikali itawapa kituo cha Kutunza Taarifa cha Kijitonyama (Internet Data Center) ili ikisimamie na hivyo kujipatia mapato kupitia gharama za uendeshaji na usimamizi wa kituo hicho. Amewataka wafanyakazi wa TTCL kufanya kazi kwa bidii, kasi, uaminifu, ubunifu na kuulinda Mkongo wa Taifa ili uwawezeshe kuwa na huduma bora na za uhakika wakati wote.

“Tumetumia fedha za mkongo wa taifa kumlipa mbia mwenzenu bhart airtel ili kuiwezesha TTCL kumilikiwa na Serikali kwa asilimia miamoja hivyo changamoto inayowakabili sasa ni kufanya mabadiliko makubwa katika upande wa kutafuta masoko ili kuweza kuongeza idadi ya wateja na kufanya kazi kwa faida”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Aidha Prof Mbarawa amesema katika kuijali TTCL, Serikali imeipa masafa ya 1800 na masafa ya 2100 na itawaongezea masafa ya 800 yatakayowawezesha kuwa na huduma ya 4G LTE yenye mtandao wenye kasi na hivyo kuiongezea wateja hususani katika huduma za data.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Profesa Tolly Mbwete amesema TTCL imejipanga kutoa huduma zake katika maduka makubwa, hospitali, stesheni za treni, mabasi ya mwendokasi na viwanja vya ndege katika jiji la Dar es salaam na Miji mikubwa ili kuwawezesha wananchi kunufaika na huduma za mtandao na data wakati wote.

Naye, Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura, ameishukuru Serikali kwa fursa mbalimbali inazoipa kampuni hiyo na kumhakikishia Waziri Prof Mbarawa kuwa katika kipindi cha miezi mitatu ijayo matokeo ya mkakati wa mabadiliko ya kibiashara yataanza kuonekana.

Dkt. Kazaura amesema kuwa tayari watumishi wenye mtazamo wa mabadiliko ya kiteknolojia wameajiriwa na wengine watapewa mafunzo ili kuhimili soko la kibiashara na kuiwezesha TTCL kunufaika na miundombinu yake iliyopo nchi nzima.  Waziri Prof. Mbarawa alikuwa akizungumza na Menejimenti na wafanyakazi wa TTCL ikiwa ni utaratibu aliojiwekea kuzungumza na wafanyakazi na taasisi zilizopo chini ya Wizara yake.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na Uongozi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakati alipotembelea kampuni hiyo, Jijini Dar es salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Dkt . Kamugisha Kazaura akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipofanya mazungumzo na wafanyakazi wa kampuni hiyo,jijini Dar es salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu Tanzania (TTCL), jinsi ya mfumo wa kutoa taarifa kwa wafanyakazi unavyofanya kazi wakati alipotembelea ofisini hiyo jijini Dar es salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Dkt . Kamugisha Kazaura akisoma taarifa ya utendaji kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Hayupo pichani) wakati alipoongea na uongozi wa kampuni hiyo, jijini Dar es salaam. Mwenyekiti wa bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Profesa Tolly Mbwete akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati Waziri alipotembelea ofisi hiyo, jijini Dar es salaam. 

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),Jijini Dar es salaam. PICHA ZOTE NA BENJAMINI SAWE -MAELEZO 

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MWENYEKITI PAMOJA NA KATIBU WA TUME YA UTUMISHI WA WALIMU (TSC) IKULU CHAMWINO MKOANI DODOMA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Oliva Joseph Mhaiki kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Winfrida Gaspa Rutaindurwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Oliva Joseph Mhaiki (kushoto) pamoja na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Winfrida Gaspa Rutaindurwa (kulia) mara baada ya kuwaapisha ) katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Oliva Joseph Mhaiki (watatu kutoka kushoto) pamoja na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Winfrida Gaspa Rutaindurwa (watatu kutoka kulia) mara baada ya kuwaapisha. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa , Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo.
Rais Dkt. John Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo mara baada ya tukio la uapisho katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma. Katikati ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpongeza Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Oliva Joseph Mhaiki mara baada ya tukio la uapisho wa Mwenyekiti huyo pamoja na Katibu wa Tume hiyo katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma. Picha na IKULU

Mshindi wa Nyumba Atua Global Tayari Kukabidhiwa Nyumba Yake

$
0
0
MWANAMAMA Nelly Mwangosi, aliyeibuka mshindi wa droo kubwa ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba, iliyoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd kwa muda wa miezi sita, leo ametembelea ofisi za kampuni hiyo zilizopo Mwenge, Bamaga tayari kwenda kukabidhiwa mjengo wake uliopo Salasala.

Nelly ambaye ni mama wa watoto wawili mwenyeji wa mkoani Iringa, aliibuka kidedea katika droo ya mwisho iliyochezeshwa Mbagala Zakhem, jijini Dar es Salaam Juni 30, mwaka huu na kuhudhuriwa na mamia ya wasomaji wa magazeti ya Global Publishers, ambayo ni Championi, Ijumaa, Risasi, Amani, Uwazi na Ijumaa Wikienda. Nelly ametua Global akiwa ameambatana na mumewe aitwaye Karolo Stephen Magani, mwanaye Emmanuel Karolo, dada zake wawili Sofia Mwangosi na Lusia Mwangosi pamoja na baadhi ya ndugu jamaa na marafiki tayari kwa zoezi la kukabidhiwa nyumba yake iliyogharimu mamilioni ya shilingi.

Mshindi wa nyumba ya Global, Nelly Mwangosi (katikati) akiwa katika studio za Global TV Online kabla ya kwenda kukabidhiwa nyumba yake. Kulia ni mumewe Karolo Stephen Magani na kushoto na kijana wao, Emmanuel Karolo.
Nelly Mwangosi akielezea furaha yake akiwa katika studio za Global TV Online.

Mume wa Nelly Mwangosi, Karolo Stephen Magani naye akielezea alivyojisikia baada ya mkewe kutangazwa kuwa mshindi wa nyumba.



Baadhi ya wafanyakazi wa Global wakimsikiliza mshindi wa nyumba.



Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia) akimpongeza mshindi wa nyumba Nelly Mwangosi (wa kwanza kushoto). Katikati ni Karolo Stephen Magani.



Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo James akimpongeza mshindi wa nyumba Nelly Mwangosi.



Shigongo akiwasihi Watanzania kuendelea kusoma magazeti ya Global na kujishindia zawadi mbalimbali zinazotangazwa kama alivyofanya Nelly Mwangosi.


Shigongo akiongea na mtoto wa mshindi wa nyumba, Emmanuel Karolo.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images