Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

VODACOM YAFANIKISHA MAWASILIANO KATIKA SAFARI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA TIMU YA "TRECK4MANDELA " MANDELA KUTOKA AFRIKA KUSINI

$
0
0
 Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini,Henry Tsamburakis akizungumza na wageni raia wa Afrika Kusini wanaopanada Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha za kununua taulo za watoto wa kike wawapo katika siku zao za Hedhi.
 Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini,Henry Tsamburakis akimsaidia mmoja wa wageni hao kubadili lugha ya kiswahili katika simu yake kwenda ya Kiingereza.
 Raia wa Afrika Kusini wanaopanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kunua taulo za watoto wa kike pamoja na kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa baba wa taifa la Afrika Kusini ,Nelson Mandela.
 Baadhi ya wapagazi katika Mlima Kilimanjaro wakishusha mabegi ya wageni hao kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro. 
 
KAMPUNI ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imedhamini safari ya siku sita kwa raia 36 wa Afrika Kusini wakiwemo wafanyakazi wa kampuni hiyo, kupanda Mlima Kilimanjaro yenye lengo la kuchangisha pesa kwa ajili ya Taulo za watoto wa kike.

Kampuni ya Vodacom inadhamini safari hiyo ambayo hufanyika kila mwaka kama sehemu ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muasisi wa Taifa la Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela, ikiwa ni mara ya pili mfululizo kwa Vodacom kufanya hivyo.
 
Akizungumza wakati wa kuanza changamoto ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa kundi hilo la watu 36,Mkuu wa Vodacom kanda ya Kaskazini, Henry Tsamburakis alisema Vodacom imetoa mawasiliano wakati wote wa safari ya kupanda mlima ili wasipate tatizo la kushindwa kuwasiliana na ndugu zao pamoja na kutuma picha za matukio wawapo mlimani.

"Vodacom Tanzania tunajivunia kuweza kuwadhamini watalii na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom kutoka Afrika ya kusini kwa mwaka wa pili mfululizo kwa kudhamini Mfuko wa Mandela ambapo kila mwaka watalii hawa huja nchini mwetu mwezi wa saba kupanda mlima wa Kilimanjaro wakiwa na lengo la kuchangisha pesa kwa ajili ya kusaidia watoto wa kike" alisema Tsamburakis. 

"Kwa upande wetu Vodacom Tanzania tumeamua kuwapatia udhamini wa mawasiliano ili wasipate matatizo ya mawasiliano wakiwa katika harakati za kupanda mlima Kilimanjaro waweze kutuma picha au kuwasiliana na ndugu zao kwa urahisi zaidi kupitia 4G yetu,"aliongeza Tsamburakis. 

Alisema Vodacom imetoa vifaa maalumu (Routers) sita zikiwa zimeunganishiwa katika mtandao wa kasi huku zikiwa zimewekewa bando ya GB 10 watakazoweza kutumia kwa muda wote watakapokuwa mlimani.Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Gerry Elsdon ameishukuru kampuni ya Vodacom kwa kuwezesha mawasiliano hatua itakayochangia safari yao ya kuelekea katika kelele cha Uhuru katika mlima Kilimanjaro kuwa rahisi zaidi. 

"Niishukuru kampuni ya Vodacom kwa niaba ya wenzangu, imewezesha mawasiliano yetu kuwa rahisi sasa,kwa sababu tuliamini kuwa tutakua nje ya mawasiliano kwa zaidi ya siku sita kumbe sasa tutaendelea kuwasiliana na ndugu na jamaa" alisema Elsdon.

Kwa upande wake mratibu wa safari hiyo ambayo hujulikana kama Treck4mandela,Richard Mabaso alisema lengo la safari hiyo ni kuendelea kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua Taulo za kike kwa watoto wa kike wasio na uwezo ili kukitumia pindi wawapo katika siku za hedhi.

""Tunatambua changamoto zinazowakabili watoto wa kike hasa wale walioko mashuleni pindi wanapoingia katika siku zao,kupitia Mfuko wa Mandela tumeendelea kuchangisha pesa kwa ajili ya kuwasaidia angalau kupata Taulo ili waweze kuendelea na masomo bila ya kuwa na kikwazo." alisema Mabaso.

Alisema mbali na zoezi hilo kulenga kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto wa kike pia limekua likitumika kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa baba wa Taifa la Afrika Kusini, Nelson Mandela.
 
 Baadhi ya wageni wakihakiki mabegi yao. 

 Baadhi ya wageni wakiwasili katika lango la Marangu tayari kuanza changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro. 
 Wapagazi katika Mlima Kilimanjaro wakiwa katika foleni ya kupima uzito mizigo yao. 
 Wageni wakijiandikisha kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro. 
 Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini akizungumza na mmoja wa viongozi wa wageni hao ,Gerry Elsdon kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro. 
 Kiongozi wa ugeni kutoka Afrika Kusini ,Richard Mabaso akizungumza kabla ya kuanza safari hiyo.
 Wageni kutoka Afrika Kusini wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini,Henry Tsamburakis muda mchache kabla ya kuanza kupanda mlima Kilimanjaro. 
 Safari ya kuanza kupanda Mlima Kilimnjaro ikaanza. 

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog ,Kanda ya Kaskazini.

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII.

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Wazara ya Maliasili na Utalii kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam Julai 18, 2016 .

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Wazara ya Maliasili na Utalii kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam Julai 18, 2016 .
Baadhi ya Watumishi wa Wizar ya Maliasili na Utalii wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam Julai 18, 2016 .
Baadhi ya Watumishi wa Wizar ya Maliasili na Utalii wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam Julai 18, 2016 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RC MAKONDA AWATOLEA UVIVU WANAOMBEZA MITANDAONI

$
0
0
MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameamua kuwavulia uvivu wale wote wanaosambaza ujumbe wa tofauti juu ya maagizo yake katika mitandao ya kijamii.

Makonda ambaye aliamua kutenga muda na kueleza maswala kadhaa yausuyo jiji la Dar es Salaam kupitia kipindi cha Power Breakfast ya Clouds Fm na 360 ya Clouds Tv juu ya watu ambao wanaotengeneza account feki za mitandao mbalimbali kupitia jina lake.

“Kwanza wanapaswa kujua kuwa sina account ambayo inaanza na cheo changu hivyo account zote zangu zimeandikwa kwa jina langu Paul Makonda na si vinginevyo, hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na hilo” anasema Makonda.

Anasema kuwa juu ya agizo batili lililosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa wasiokuwa na kazi watakwenda jela,sio tamko la account yake bali yeye ameagiza Wenyeviti wa serikali za mtaa kuhakikisha kuwa wanafanya uhakiki wa wakazi wao nyumba kwa nyumba kwa ajili ya usalama wa Maeneo wanayokaa.

Anataja kuwa kutokana matatizo yaliyopo kamwe hatoacha  kupambana na mafisadi katika Halmashauri zote tatu,wauza unga , wafanya biashara wa Shisha na Mashoga.Hivyo aliwataka wananchi wa mkoa huu kuwa makini na kufuata maelekezo ya wenyeviti mitaa amabayo nimewapa hili tuweze kuimarisha ulinzi kuanzi ngazi ya chini kabisa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akizungumza ndani ya kipindi cha Power Breakfast ya Clouds Fm

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA 10 WA KIMATAIFA WA MAJI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano Mkuu wa 10 wa African Ministers Council on Water (AMCOW) knew Kituo cha Mimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 18, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Rais Mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki kuingia kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kufungua Mkutano Mkuu wa 10 wa African Ministers Council on Water (AMCOW) Julai 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Rais Mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki kuingia kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kufungua Mkutano Mkuu wa 10 wa African Ministers Council on Water (AMCOW) Julai 18, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa 10 wa African Ministers Council on Water (AMCOW) kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 18, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki katika Mkutano Mkuu wa 10 wa African Ministers Council on Water (AMCOW) kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AMUWAKILISHA RAIS DKT MAGUFULI MKUTANO WA 27 WA AU NCHINI RWANDA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 27 kwa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika AU ulioanza jana katika ukumbi wa KCC mjini Kigali Rwanda. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo.Picha na OMR.

KIGALI, RWANDA.

Tanzania imeuhakikishia Umoja wa Afrika (AU) kwamba itaendelea kufanya kazi kwa karibu na nchi wanachama wa AU katika kujadili changamoto za kiusalama zinazolikabili Bara la Afrika kwa njia ya mazungumzo na upatanishi kama inavyoelekeza Katiba ya umoja huo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati akichangia mada kuhusu Hali ya amani na usalama katika Bara la Afrika katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika hapa Kigali, Rwanda.Mheshimiwa Samia alisema Tanzania inasikitishwa na inalaani vikali matukio ya uvunjifu wa amani yanayoendelea kujitokeza katika baadhi ya nchi za Kiafrika kiasi cha kutishia usalama wa raia.

Alielezea mauaji ya Hafsa Mossi, aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na waziri wa zamani wa Burundi na mapigano ya hivi karibuni Sudan ya Kusini ambapo mamia ya raia wasiokuwa na hatia waliuwawa na wengine maelfu wameachwa bila makazi kwamba ni muendelezo wa uvunjifu wa amani katika nchi hizo.

Aliwataka wadau husika katika nchi za Burundi na Sudan ya Kusini kushiriki kikamilifu katika mazungumzo yanayoendelea kwa kuwa hiyo ndiyo njia muafaka ya kuleta amani, usalama na utulivu wa kudumu  katika nchi zao.Aidha, Makamu wa Rais ambaye alimwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano huo aliiomba Jumuiya ya Kimataifa kuendelea kuisadia Sudan ya Kusini katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu katika mgogoro ulioikumba nchi hiyo.

Akichangia kuhusu mageuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Makamu wa Rais alisema Tanzania kwa ujumla inaunga mkono msimamo wa Afrika wa kuwa na viti viwili katika baraza hilo na kura ya turufu bila ya masharti yoyote.Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo viongozi walisisitiza suala la kuimarisha umoja baina ya nchi wanachama na kusema hiyo ndiyo nguzo muhimu katika kukuza uchumi na ustawi wa wananchi wa Bara la Afrika.

Katika mkutano huo kulikuwa na uzinduzi wa pasi ya kusafiria ya Afrika ambayo ilitolewa kwa Mwenyekiti wa AU, Rais Idris Deby wa Chad na nchi mwenyeji wa mkutano, Rais Paul Kagame wa Rwanda.Mkutano huo ambao ulizungumzia pia gharama za kuendesha umoja huo na masuala ya haki za wanawake ulihudhuriwa na Wakuu wa Nchi zaidi ya 35, Marais wastaafu, wake wa Marais pamoja na viongozi wa serikali.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais

BLESSING KUFAYA UCHANGIAJI WA VIFAA VYA SHULE KWA WANAFUNZI WASIO NA UWEZO.

$
0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa Tasisi ya Blessing.
 Mwanzilishi wa Taasisi ya Blessing, Blessing Mlanga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja wa Taasisi ya Blessing, Zawadi Mlanga.
 Mwanzilishi wa Taasisi ya Blessing, Blessing Mlanga akionesha Tsheti amazo zitavaliwa siku ya 24 ambazo zitauzwa kwaajili ya kuchangi pamoja na kuongeza nguvu za kuwasaidia wanafunzi wa shule ambao hawana nguo nzuri pamoja na wasio na viatu vya shule na mabegi ya shule. Kulia ni Meneja wa Taasisi ya Blessing, Zawadi Mlanga.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mkakati wa  Rais Dk. John Pombe Magufuli  wa elimu bure unatekelezwa kwa vitendo katika kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu ,huku Taasisi ya Blessing  imekuja na mkakati wa kusaidia wanafunzi wasio na vifaa pamoja sare za shule.

Taasisi hiyo inatarajia kufanya uchangishaji kwa ajili ya kupata vifaa pamoja na sare za shule kwa wanafunzi ili waweze kusoma bila changamoto vitu hivyo.

Uchangiaji huo unatarajiwa kufanyika Julai 23 mwaka huu katika ukumbi wa Nkurumah katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Meneja wa Taasisi hiyo, Blessing  Mlanga amesema kuwa baadhi ya wanafunzi wanachangamoto ya vifaa na sare hivyo ikiwa watanzania tunaweza kuchangia sehemu hiyo na kuwa tumeunga mkono jitihada za Rais John Pombe Magufuli.

Zawadi amesema kuwa yeye ni kijana wa kitanzania anayesoma Malaysia ameona kuna sehemu ambayo anaweza kuboresha katika upande wa vifaa pamoja na sare.

Amesema kuwa mradi huo wa sare na vifaa utaanza kwa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Arusha na baada hapo wataendelea na mikoa mingine.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA MAAFISA WA JESHI LA POLISI WALIOPANDISHWA VYEO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM,AWATAKA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA WANAOLETA MATATIZO

$
0
0

Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ahmada Abdalla Khamis akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi la Polisi waliopandishwa vyeo vya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na Naibu Kamishna wa Polisi DCP mara baada ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi la Polisi waliopandishwa cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) mara baada ya kula kiapo cha Maadili ya Watumishi wa umma Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwagaia vitafunwa wageni mbalimbali waliofika Ikulu kwa ajili ya kushuhudia Maafisa wa Polisi walipondishwa vyeo wakati wakila kiapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwagaia vitafunwa baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria tukio hilo Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza viongozi wa Jeshi la Polisi Tanzania kuwaondoa watumishi wote wasiokuwa askari polisi na ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa taratibu na ufujaji wa fedha za umma ili kulinda heshima, nidhamu na uadilifu ndani ya jeshi hilo.


Rais Magufuli ametoa maelekezo hayo leo tarehe 18 Julai, 2016 muda mfupi baada ya Naibu Makamishna wa Polisi 25 na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi 35 kula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Pamoja na kutoa agizo la kutaka wasio askari polisi kuondolewa katika utumishi wa jeshi la polisi, Rais Magufuli pia ameagiza jeshi hilo lichukue hatua dhidi ya wote wanaokabiliwa na tuhuma za wizi wa fedha wakiwemo wanaodaiwa kuiba mabilioni ya shilingi zilizotolewa kwa ajili ya ununuzi wa sare za askari mwaka jana 2015.

"Mnajua kupeleleza, mna vyombo vyote, ofisi ya IGP (Inspekta Jenerali wa Polisi) ipo palepale, ofisi ya DCI (Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai) ipo palepale, Makamishna wote mnazunguka mnakwenda palepale, mwizi mnae palepale, mnashindwa kumshika.

"Kama mnafikiri kuwa na raia katika jeshi la polisi wanawaharibia kazi zenu hamisheni raia wote na wapelekeni utumishi, kwani hakuna mhasibu ambaye ni askari polisi? hakuna mhandisi ambaye ni askari polisi? hakuna afisa tawala ambaye ni askari polisi? Mimi nafikiri kama matatizo ya wizi na wafanyakazi hewa yanaletwa na raia waliomo ndani ya jeshi la polisi na majeshi yetu mengine, IGP kaorodheshe raia wote wanafanya kazi Jeshi la Polisi ili waondolewe na tuwapangie kazi nyingine uraiani" Amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri linayofanya iliyoliwezesha kujenga imani kubwa kwa watanzania na ametaka viongozi wa Jeshi hilo wawaongoze askari walio chini yao vizuri, wawatie moyo na waache vitendo vya kuwakatisha tamaa kwa kuwaadhibu ama kuwatisha pale wanapochukua hatua stahiki dhidi watu wanaovunja sheria.

"Sasa mimi niwaombe nyinyi, wale wadogo mnaowaongoza mkawape mamlaka ya kutimiza wajibu wao, hata kama ameshika gari la IGP liache lishikwe IGP atakwenda kujieleza mwenyewe, hata akishika gari la RPC afanye hivyohivyo, hata akishika gari la Waziri au gari la Rais mwacheni atekeleze wajibu wake, sheria ni msumeno, tunawanyima nguvu hawa wa chini wanapotimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria halafu unamwambia liachie, ukifanya hivyo aliyeshikwa anatoka pale akiwa anatamba kwelikweli na yule askari unamvunja nguvu ya kufanya kazi"Amesisitiza Rais Magufuli. 

Rais Magufuli pia amelitaka jeshi hilo kuungana na vyombo vingine vya serikali katika kutekeleza shughuli zake zikiwemo kusimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali bandarini, katika sekta ya utalii na maeneo mengine, kukabiliana na vitendo vya rushwa na kuondoa watumishi hewa.

Tukio hili la Naibu Makamishna wa Polisi na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi kula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma limeongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda na limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjellah Kairuki, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Yusuf Masauni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju, Makatibu Wakuu na Viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
18 Julai, 2016

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Maafisa wa Jeshi la polisi aliowapandisha vyeo vya Naibu Kamishna wa Polisi DCP na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kedmon Andrew Mnubi akila kiapo cha Ahadi ya uadilifu pamoja na Maafisa wengine wa Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Mwamini Marco Rwantale akila kiapo cha Ahadi ya uadilifu pamoja na Maafisa wengine wa Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ahmada Abdalla Khamis akisaini hati ya kiapo cha Ahadi ya Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Frasser Rweyemamu Kashai akisaini hati hati ya kiapo cha Ahadi ya Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwagaia vitafunwa baadhi ya Maafisa mbalimbali wa Polisi waliokula kiapo cha Maadili Ikulu jijini Dar es Salaam. 


Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Naibu wake Hamadi Masauni mara baada ya Maafisa wa Jeshi la Polisi waliopandishwa vyeo kula Kiapo ahadi ya uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU.
 

MKURUGENZI WA BENKI YA CRDB, DK. CHARLES KIMEI APEWA TUZO YA AMANI TANZANIA

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akipokea tuzo ya Amani kutoka kwa Katibu Mkuu wa Taasisi ya Amani na Maridhiano-Tanzania, mchungaji Osward Mlay,  kutokana na kutambua mchango wake katika kudumisha amani nchini. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sadick Godigodi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Taasisi ya Amani na Maridhiano-Tanzania, mchungaji Osward Mlay,  (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo ya Amani kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei.
Makamu Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sadick Godigodi akifafanua jambo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiishukuru Taasisi ya Amani na Maridhiano-Tanzania kwa kutambua mchango wake katika kudumisha amani nchini. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sadick Godigodi akifafanua jambo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiwa ameshika tuzo ya Amani baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa Taasisi ya Amani na Maridhiano-Tanzania, mchungaji Osward Mlay (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sadick Godigodi.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akiwa ameshika tuzo ya Amani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisalimiana na Katibu Mkuu wa Taasisi ya Amani na Maridhiano-Tanzania, mchungaji Osward Mlay wakati alipofika ofisini kwake kumkabidhi tuzo maalum ya Amani kutokana na kutambua mchango wake katika kudumisha amani nchini.
Makamu Mwenyekiti wa taasisi Taasisi ya Amani na Maridhiano-Tanzania, Sadick Godigodi. (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.

Mwakilishi wa WHO amuaga Waziri wa Afya

$
0
0

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt.Rufaro Chatora akiongea na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu wakati alipoenda kumuaga rasmi ofisini kwake.Dkt.Chatora amemaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Tanzania na hivyo kuhamishiwa nchini Afrika ya Kusini.
Waziri Ummy Mwalimu akifanya mazungumzo na mwakilishi huyo,Dkt.Chatora amesisitiza wizara kujenga uwezo wa ndani katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu kwa kushirikiana na wizara ya maji,mazingira pamoja na elimu.Vile vile alishauri Serikali kuongeza nguvu katika huduma ya mama wajawazito pamoja na kuwekeza katika magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo hivi sasa yanaongezeka kwa kasi na kuathiri jamii
(Picha na Wizara ya Afya)

WAZIRI KAIRUKI AFANYA KIKAO KAZI NA WATUMISHI WA MKOA WA PWANI

$
0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya Mkoa wa Pwani ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo kabla ya kikao kazi na watumishi wa mkoa wa Pwani kilichofanyika tarehe 18/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Baadhi ya Watumishi wa Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika tarehe 18/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiongea na watumishi wa Mkoa wa Pwani (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika tarehe 18/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Afisa Elimu Mkoa wa Pwani, Bw. Yusuph Kipengele akiwasilisha malalamiko yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi wa mkoa wa Pwani kilichofanyika tarehe 18/7/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

BIA YA ASILI YA NZAGAMBA YAZINDUA PROMOSHENI YA AINA YAKE KANDA YA ZIWA

$
0
0
 Meneja Masoko wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Oscar Shelukindo akionyesha kwa waandishi wa habari Bia hiyo ya Asili inayopatika maeneo ya Kanda ya Ziwa, wakati uzinduzi wa Promosheni yake itakayowawezesha wanywaji wa Bia hiyo kujishindia Ng'ombe kila wiki. Uzinduzi huo umefanyika leo Julai 19, 2016 kwenye Kiwanda cha Nzagamba, Iloganzala Jijini Mwanza. Kulia ni Meneja Mauzo wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Fred Kazindogo.
 Meneja Mauzo wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Fred Kazindogo akionyesha moja ya maboksi yatakayotumika kwa washiriki wa Promosheni ya Bia hiyo ya asili ya Nzagamba itakayowawezesha wanywaji wake wa Kanda ya Ziwa kujishindia Ng'ombe kila wiki, wakati wa uzinduzi wa Promosheni hiyo, uliofanyika kwenye Kiwanda cha Nzagamba, Iloganzala Jijini Mwanza. Kulia ni Meneja Masoko wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Oscar Shelukindo.
Meneja Masoko wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Oscar Shelukindo akionyesha kwa mfano namna ya kushiriki Promosheni hiyo ya Nzagamba. Wengine pichani ni Meneja Mauzo wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Fred Kazindogo (aliebeba boksi), pamoja na Ma Meneja Usambazaji wa Bia ya Asili ya Nzagamba, James Makalla (kulia) na Peter Mwambenja.

MWAKILISHI MKAZI WA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI(WHO), HAPA NCHINI AMALIZA MUDA WAKE, AMUAGA WAZIRI WA AFYA.

$
0
0
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt.Rufaro Chatora akiongea na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipoenda kumuaga rasmi ofisini kwake Dkt.Chatora amemaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Tanzania na hivyo kuhamishiwa nchini Afrika ya Kusini
Waziri Ummy Mwalimu akifanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt.Rufaro Chatora Dkt.Chatora amesisitiza wizara kujenga uwezo wa ndani katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu kwa kushirikiana na wizara ya maji, mazingira pamoja na elimu.

Vile vile alishauri Serikali kuongeza nguvu katika huduma ya mama wajawazito pamoja na kuwekeza katika magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo hivi sasa yanaongezeka kwa kasi na kuathiri jamii

amemshukuru kwa ushirikiano wake katika sekta ya afya tangu awepo nchini na ameahidi kuendelea kutekeleza yale yote aliyoishauri wizara

(Picha na Wizara ya Afya)

MWAKILISHI MKAZI WA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI(WHO), HAPA NCHINI AMALIZA MUDA WAKE, AMUAGA WAZIRI WA AFYA.

$
0
0
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt.Rufaro Chatora akiongea na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipoenda kumuaga rasmi ofisini kwake Dkt.Chatora amemaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Tanzania na hivyo kuhamishiwa nchini Afrika ya Kusini
Waziri Ummy Mwalimu akifanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt.Rufaro Chatora Dkt.Chatora amesisitiza wizara kujenga uwezo wa ndani katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu kwa kushirikiana na wizara ya maji, mazingira pamoja na elimu.

Vile vile alishauri Serikali kuongeza nguvu katika huduma ya mama wajawazito pamoja na kuwekeza katika magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo hivi sasa yanaongezeka kwa kasi na kuathiri jamii

amemshukuru kwa ushirikiano wake katika sekta ya afya tangu awepo nchini na ameahidi kuendelea kutekeleza yale yote aliyoishauri wizara

(Picha na Wizara ya Afya)

DC MTATURU AKUTANA NA WAZEE WA WILAYA YA IKUNGI AWAAHIDI KUFANYA KAZI KWA BIDII

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji J. Mtaturu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wazee waliowawakilisha wazee wengine wilayani humo.

Dc Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa kikao.
Mtaturu akisikiliza kwa makini moja ya ushauri uliopatiwa na wazee baada ya kikao kumalizika

Na Mathias Canal, Singida

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu amekutana na zaidi ya wazee 137 kutoka vijiji 101 vilivyopo katika Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida. Katika mazungumzo ya mkuu huyo wa Wilaya na wazee hao yalijikita zaidi katika kujadili namna ya kukabiliana na umasikini kupitia nguvu Kazi ya Taifa (Vijana) katika kilimo na ufugaji wa kisasa. 
 
Dc Mtaturu amewasilisha dhamira ya serikali ya Hapa Kazi Tu chini ya Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Joseph Pombe Magufulu kwa wazee wa Wilaya ya Ikungi na Taifa kwa ujumla ni kupambana na mafisadi, Rushwa na wahujumu uchumi ili kuboresha huduma za Jamii ikiwemo Afya hususani katika kuboresha huduma za Afya kwa wazee wote nchini sawia na Wanawake wajawazito na watoto. 
 
Katika kuhakikisha kunakuwa na chachu ya maendeleo kwaMapinduzikubwa Wilayani humo Mtaturu alisema kuwa serikali imekusudia kuboresha kilimo na ufugaji ili viwe vya tija na kibiashara na kupelekea kupunguza umasikini wa wananchi mwaka hadi mwaka. Mtaturu anakuwa Mkuu wa Wilaya wa kwanza kukutana na kundi la wazee Siku chache baada ya kuapishwa jambo ambalo halijawahi kutokea kwa kiongozi mwingine yeyote Wilayani humo tangu Mkoa wa Singida ulipoanzishwa. 
Kwa upande wao wazee hao wameonyesha wazi mapenzi yao ya dhati kwa mkuu huyo wa Wilaya na kuahidi ushirikiano uliotukuka katika utendaji wake. 
 
Wakati huo huo wazee hao wamemshukuru Mh Rais Magufuli kwa uteuzi alioufanya kumpeleka Mkuu huyo wa Wilaya kuongoza wananchi hao ambao wameonyesha kukatishwa tamaa na baadhi ya viongozi wa serikali wilayani humo ambao wameshindwa kutatua changamoto za wananchi. Awali Dc Mtaturu alikuwa na kikao cha mapema na watumishi wa Halmashauri na wakuu wa idara ili kukumbushana majukumu ya kila mmoja utendaji wake na kuwasihi kufanya Kazi kwa bidii zaidi kwa kushirikiana na wananchi.
 
Mtaturu amewakumbusha watumishi hao wajibu wao wa kusimamia miradi ya maendeleo kwa kupata thamani halisi ya fedha (Value for Money) kushughulika na kero za wananchi ikiwemo kutafsiri ilani ya Uchaguzi kwa vitendo ya Chama cha Mapinduzi (CCM). Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amewapa muda wa mwezi mmoja watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wanaoishi Singida Mjini takribani kilomita 41 kutoka Wilayani hapo wawe wamehamia Wilayani Ikungi kwani amebaini ni watumishi wanne pekee ndio wanaoishi Wilayani hapa jambo ambalo linapunguza ufanisi wa Kazi. 
 
Katika sekta ya michezo Mtaturu alisema kuwa ili kuibua vipaji na Mkoa wa Singida kwa muda mrefu umekuwa na Sifa ya kutoa wanariadha hivyo ili kuenzi heshima hiyo anataraji kuanzisha Ikungi Marathon ili kuwapa fursa Vijana wenye vipaji kuibuka na kufika mbali zaidi katika medani za riadha

FAMILIA YA MFANO KUOKOA WATOTO WANAOFANYIWA UKATILI

$
0
0
PRETTY binti mdogo mwenye umri wa kama mwaka mmoja na nusu unapomzungumzisha, kama watoto wengine wenye afya na uhakika wa malezi anatabasamu na kucheka.

Binti huyu mdogo ambaye analelewa na familia iliyomuasili kwa malezi (hajaasiliwa kisheria) ni miongoni mwa watoto kadhaa nchini ambao wanafaidika na mpango mpya wa kusaidia watoto waliokumbwa na ukatili na unyanyasaji.

Pretty (ambaye si jina lake la ukweli-nimempa jina hilo kulinda haki yake) maisha yake mpaka sasa ni kama kitendawili kibaya ambacho ni Mungu tu alitaka kukifumbua.Nasema ni Mungu tu kwa kuwa Pretty aliokolewa kutoka katika shimo la choo alilotumbukizwa akiwa ndani ya mfuko wa rambo uliofungwa vyema.

Sajini taji (Staff Sergeant) Pundensiana Baitu wa Dawati la jinsia wilaya ya Kipolisi Mbalizi, anasema kwamba Pretty wakati alipoopolewa katika choo cha mtu binafsi alikuwa na hali mbaya sana kiafya na juhudi kubwa sana ilifanywa na hospitali ya Meta kumrejeshea afya yake.

Akisimulia tukio hilo la kuhudhunisha alisema kwamba usiku wa Machi Mosi, mwaka jana alipokea simu iliyomtafadhalisha msaada ili kuokoa maisha ya mtoto aliyetupwa katika choo kinachotumika, katika eneo la Mlimareli huko Mbalizi.
Sajini taji Pundensiana Baitu wa Dawati la jinsia wilaya ya Kipolisi Mbalizi akizungumza na mwandishi wahabari wa Modewjiblog (hayupo pichani) hivi karibuni.(Imeandaliwa na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Alisema wakati anajaribu kuwasiliana na askari kwenda kuona kama wanahitaji msaada wa Kikosi cha zimamoto, akapokea simu nyingine kwamba wananchi wamebomoa choo hicho na kumtoa mtoto huyo ambaye alikuwa amefungwa katika mfuko wa rambo na kwamba alishaanza kuliwa na wadudu wa chooni.

Aidha aliambiwa katika simu kwamba mtoto huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa wiki moja alikuwa bado anapumua hali iliyomfanya aelekeze polisi kuitengeneza PF 3 haraka na kumpeleka mtoto huyo katika hospitali ya Ifisu ambao nao kutokana na kukosa vifaa vya watoto wa aina yake katika hali ile, walimkimbiza hospitali ya Meta.

Anasema yeye alifika asubuhi kuona hali ya mtoto huyo akiambatana na Ofisa Ustawi wa Jamii na hakupendezwa na hali aliyomkuta nayo mtoto.

Anasema kwamba juhudi za upelelezi kujua mama wa mtoto huyo hazikufanikiwa kwani mtoto alitupwa katika choo binafsi karibu na klabu ya pombe. Hata hivyo anasema baada ya kushindwa waliwaambia wananchi wa eneo hilo kumtazama mtu ambaye wanamtilia shaka na kumfikisha kwao kwa mahojiano.Mpaka wakati wa kuandika makala haya mtu huyo hajapatikana.

Anasema kutokana na mfumo mpya wa familia ya mfano baada ya wao kama polisi kukamilisha kazi ya usalama na kumkabidhi mtoto huyo kwa Ofisa Ustawi wa Jamii, ofisa huyo alimtafuta mtu ambaye yuko tayari kulea mtoto na kumkakabidhi kwao.

Sajini taji huyo anasema kuwa kuna ongezeko la vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto na kwamba jamii inatakiwa kubadilika na kukubali wajibu wake katika kuhakikisha usalama wa mtoto.
Afisa Ustawi wa Jamii Hospitali ya Kanda ya Nyanda za juu Kusini, Gerald Mwaulesi akielezea tukio la mtoto Pretty mbele ya kamera ya Modewjiblog jijini Mbeya hivi karibuni.

Anasema kabla ya kuanzishwa kwa wilaya mpya wakati bado iko Mbeya amekuwa akishuhudia vurugu nyingi kuhusu ukatili kwa watoto na kwamba dawati lake inachofanya ni kutoa ushauri hasa kwa wadada ambao wanatoa mimba na wengine kutupa watoto wanapopatikana.

Alisema ingawa kuna taratibu ndefu za sheria, mfumo mpya uliokubaliwa na serikali wa kupata familia ya mfano ni mfumo bora wenye kuhakikisha malezi mema na kizazi bora kijacho.

Pretty ambaye kwa sasa anaishi na familia ya mfano yenye watoto sita na yeye akiwa wa saba katika kijiji cha Muvwa kilichopo kata ya Mshewe wilayani Mbalizi ana uhakika na malezi kutokana na mfumo huo mpya.

Na Si ajabu akikua hakuna mtu hata yeye mwenyewe atakayejua kwamba aliokolewa kutoka kwenye shimo la choo alikotupwa na mama katili wiki moja baada ya kuzaliwa kwake na kusaidiwa malezi yake na mfumo wa familia ya mfano.
Dk Sipora Harison Kisanga wa UNICEF kanda ya Iringa akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari wa Modewjiblog (hayupo pichani)

Dk Sipora Harison Kisanga ambaye anafanyakazi na UNICEF kanda ya Iringa anasema kwamba ulinzi na usalama wa mtoto ni eda ya wananchi wote kwa ujumla, lakini kutokana na dosari zilizopo ndio maana UNICEF na Tanzania zimetia saini makubaliano yanayowezesha maandalizi ya watu wa kuwapokea watoto waliotelekezwa na wale wenye mazingira magumu ili nao waweze kuwa sehemu ya familia zilizobora.

Anasema kuufanya mfumo huo uwe na utekelezaji uliobora waliendesha mafunzo na kutambua watu wanaoweza kukaa na mtoto, na baada ya kuwakagua wapo katika orodha wakisubiri mtoto yeyote atakayepatikana.

Anasema kutokana na maandalizi hayo ndio maana hata walipompata mtoto Pretty walijua kwamba watampelaka Muvwa kwa familia ambayo iko tayari kupokea mtoto wa aina yoyote na wa umri wowote.

Anasema ni lengo la UNICEF kuhakikisha kwamba haki za watoto zinatekelezwa ikiwamo ya ulinzi na usalama dhidi ya vitu na watu wabaya, huduma za afya, huduma za elimu, haki ya kucheza na haki ya kufundishwa yaliyo mema kutoka kwa wakubwa wao.
Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Mbeya, Lilian Kilongumtwa akielezea tukio la mtoto Pretty aliyetupwa kwenye shimo la choo jijini Mbeya kwa mwandishi wa habari wa mtandao wa Modewjiblog.

Anasema Ofisa huyo wa UNICEF kwamba Mradi wa familia ya mfano ulianzia Temeke na sasa upo Mbeya, Mbarali, na Mbalizi kwa lengo lile lile kuwawezesha watoto hawa kuwa na familia na kuwa salama kuliko kuwapeleka katika vituo vya kulelea yatima.

Mama anayemtunza mtoto huyo pamoja na mumewe, Mama Christer Eliston Mwashusa anasema amefurahi sana kupata mtoto huyo kwani alikuwa tayari kumsaidia kutokana na hofu ya Mungu aliyonayo.

Anasema yeye angelifurahi kama mtoto angemuasili kisheria kwani hali ya sasa ya ulezi pekee anaiona kama haimpi nafasi ya kufanyakazi yake vyema ya kumtunza. Anataka awe mali yake moja kwa moja.

Anasema amepata changamoto nyingi tangu alipomkuta mtoto Pretty hospitali ya Meta, changamoto ambazo zilimuumiza kwanza kama mzazi kwa kutambua kwamba mtoto yule hana wazazi na pia kwa kutambua kwamba ametelekezwa kikatili.
Familia Bw. Juma Mbuza (48) na Bi. Christer Mwashusha (43) inayomlea mtoto Pretty wakifurahi jambo na binti yao baada ya mahojiano na mwandishi wa habari wa Modewjiblog (hayupo pichani).

Pia changamoto ambayo alikumbana nayo ni kule kutambua kwamba mtoto yule kwa sababu ya kuwekwa chooni alikuwa na dhiki kubwa ya afya na hivyo kumfanya kuwa dhaifu.

Anasema hata wakati alipoanza kumtunza changamoto za afya yake zilikuwa kubwa na hasa alipoambiwa kwamba ana ugonjwa ambao ameurithi kwa mama yake, ugonjwa ambao ni upungufu wa kinga na kuanza kumlisha dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI kuanzia alipokuwa na miezi miwili hadi minne.

Hata hivyo katika mahojiano na Ofisa Ustawi wa Jamii kutoka hospitali ya kanda ya rufaa Mbeya (Meta) aliyempokea mtoto huyo Gerald Godfrey Mwambesi alisema kwamba Pretty hakuwa na virusi tangu awali walipompima na kusema kwamba hata vipimo vya hospitali nyingine vilivyosema kwamba ana virusi havikuwa sahihi.

Anasema Pretty alipoteza nguvu ya kinga ya mwili kutokana na kukaa chooni kwa muda na hivyo siku zilivyozidi ndivyo alivyokuwa akiongeza kinga.

Anasema baada ya siku tatu ya kukabiliana na vidonda vyake vilivyotokana na kutafunwa na wadudu chooni na baada ya wiki tatu alionekana kuwa nafuu sana na ingawa mlezi alipata changamoto kiukweli mtoto huyo hakuwa na virusi zaidi ya kupoteza kinga za kawaida ambazo zilitakiwa kurudishwa taratibu.
Dada na kaka wa kufikia mtoto Pretty wakifurahi na mdogo wao mara baada ya kutoka shule.

Anasema mtaalamu huyo kwamba waliongea na wataalamu wa watoto kuhusiana na shida hiyo ya hospitali Mbalizi kumuona mtoto na virusi wakati wao walimpima mara mbili bila kuviona na kusema kwamba hali hiyo inatokana na maambukizi yaliyosababishwa na kutupwa ndani ya choo ambayo yalihitaji tiba ya muda mrefu.

Mlezi anasema kwamba baada ya miezi miwili ya kukaa na mtoto huyo kwa uzuri aliona afya yake inadorora kiasi cha kuhitaji msaada wa tiba na kuanza kwenda hospitali kupata msaada.

Anasema hospitali aliyoenda ilisema mtoto ana maambukizi kutoka kwa mama na kushauri tiba hivyo alipelekwa katika kiliniki ya Beira ambako walimpima na kumwanzishia dozi waliyokuja kuikatisha baada ya kumpima tena kutokana na ufuatiliaji wa hospitali ya Meta na kugundua kwamba hana tatizo la maambukizi ya UKIMWI.

Mlezi wa mtoto huyo alishukuru sana watendaji wa taasisi ya Kihumbe ambao walimsaidia fedha za nauli kwenda katika hospitali kutetea afya ya Pretty na kwamba baada ya matumizi ya dawa na dawa lishe mtoto huyo mwezi uliopita (Juni 16,2016) aliambiwa kwamba mtoto wake hana maambukizi tena.

KIHUMBE, ni taasisi inayofundisha wawezeshaji namna ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hasa familia zao ili waweze kujimudu wenyewe na kuondokana na matatizo hayo.

Baba mlezi katika familia hiyo yenye watu saba akiwamo Pretty, Juma Mbuza amesifu juhudi za mke wake katika kuhakikisha kwamba Pretty anapata mapenzi yote ya kimama na kuendelea kustawi akiwa katika familia hiyo.

Anasema familia yake inawiwa.kulea mtoto huyo kwa kuwa ndiyo ilikuwa nia yao tangu awali na kwamba awali walitaka kuwachukua watoto waliotelekezwa katika kijiji jirani kwenye tarafa yao. Kuendelea kusoma makala hii bofya hapa

DC MUHEZA AWATAKA WAFANYABIASHARA WA SOKO LA SAMAKI KUHAMIA ENEO LA SOKO LA MICHUNGWANI

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akisisitiza jambo kwa wafanyabiashara wa soko la samaki wabichi na wakavu kuhusu kuondoka eneo hilo na kuhamia soko la michungwani ambalo limejengwa kwa ubora mzuri kwa ajili ya kufanyia biashara zao

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akimsikiliza mmoja wa wafanyabiashara ya samaki katika soko la kuuzia samaki wilayani humo ambao waliamuriwa kuhamia kwenye soko la Michungwani ambalo limejengwa kwa ubora kwa ajili ya shughuli zao.


Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akizungumza na wafanyabiashara wa samaki katika soko la kuuzia samaki wabichi na wakavu ambalo limevunjwa na kutakiwa kuhamia kwenye soko la michungwani ambalo limejengwa kwa ubora kwa ajili ya kufanya shughuli zao

Mfanyabiashara wa soko la samaki la kulia akimuonyesha mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo kitu wakati alipotembelea soko la kuuzia samaki wabichi na wakavu ambapo aliwataka wafanyabiashara hao kuondoka eneo hilo kuhamia eneo la michungwani.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

WASHINDI WA MBIO ZA BAISKELI ZA KANDA YA ZIWA ,WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO.

$
0
0
Mgeni rasmi katika Mashindano hayo,Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi pamoja na waendesha Baiskeli. Mgeni rasmi katika Mashindano hayo,Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akiwa meza kuu kwa ajili ya zoezi la utoaji wa zawadi kwa washindi wa mashindano hayo.kulia kwake ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi ,Asa Mwaipopo.
Mshindi wa kwanza katika Mashindano ya Mbio za Baiskeli ya Kanda ya ziwa yajulikanayo kama Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016 ,Seni Konda akifurahia zawadi ya kikombe mara baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura.



Mshindi wa pili katika Mashindano ya Mbio za Baiskeli ya Kanda ya ziwa yajulikanayo kama Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016 ,Makoja Hamis akionesha zawadi ya kikombe mara baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura.



Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akikabidhi kikombe kwa mshindi wa tatu wa Mashindano hayo ya baiskeli, Hamis Clement.Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akimvisha medali mshindi wa kwanza kwa upande wanawake wa mbio za baiskeli za Acacia tufanikiwe pamoja cycle Challange 2016,Martha Anthony.
Mshindi wa kwanza kwa upande wanawake wa mbio za baiskeli za Acacia tufanikiwe pamoja cycle Challange 2016,Martha Anthony akiwa amenyanyua juu kikombe mara baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi. Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akikabidhi kitita cha fedha kwa mshindi wa pili wa mashindano ya baiskeli ,Salma William . Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akikabidhi zawadi ya kikombe na fedha kwa mshindi wa tatu wa mbio za baiskeli,Elizabeth Clement. Washindi wa Mbio za Baiskeli kwa upande wa wanawake na wanaume katika mashindano ya Acacia tufanikiwe pamoja Cycle Challange 2016 wakifurahi mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao. Washindi kwa upande wa wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi. Washindi kwa upande wa wananume wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi. Bingwa mara mbili wa mashindano ya Mbio hizo, Masunga Duba akipeana mkono na mgeni rasmi mara baada ya kuhitimisha mbio hizo akishika nafasi ya nne.
Mkuu wa kitengo cha biashara katika Mgodi wa Buzwagi,Jackson Kanumba akikabidhi zawadi kwa mshiriki wa mbio hizo Ashiraf.
Mshiriki Ashraf ambaye amekua akishiriki mashindano mbalimbali ya baiskeli ,akipongezwa na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Asa Mwaipopo.Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano kwa umma wa kampuni ya Madini ya Acacia,Necta Foya akikabidhi zawadi kwa mmoja wa washindi waliofanikiwa kuwa kati ya washiriki 30 bora. Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano kwa umma wa kampuni ya Madini ya Acacia,Necta Foya (katikati) pamoja na Afisa Mawasiliano wa Mgodi wa Buzwagi,Magesa Magesa wakitoa maelekzo kwa mshereheshaji wa shughuli hiyo,Mc Kalinga. Wasanii wa kikundi cha Ngoma wakitumbuiza katika hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa mbio za baiskeli. Msanii Marry Banyukwa akitumbuiza katika hafla hiyo. Viongozi wa mgodi wa Buzwagi wakisakata Rhumba pamoja na Washiriki wa mbio za baiskeli .


Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog.

FAINALI ya mashindano ya mbio za baiskeli zijulikanazo kama “Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle challange 2016 zinazoandaliwa na chama cha mchezo wa mbio za baiskeli (CHABATA) na kudhaminiwa na kampuni ya kuchimba Madini ya Acacia zimemalizika mjini Kahama huku mwendesha baiskeli Seni Konda akiweka rekodi ya kushinda mbio hizo kwa kutumia saa 4:15:07 .

Konda mkazi wa mkoa wa Shinyanga amefanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kuwashinda wapinzani wake Makoja Hamis aliyemaliza nafasi ya pili na Hamis Clement aliyemaliza nafasi ya tatu huku wakifuatiwa na waendesha baiskeli zaidi ya 150 walioshiriki mbio hizo kutoka mikoa sita ya kanda ya ziwa.

Kwa upande wa wanawake ,mwendesha baiskeli,Martha Anthony kutoka mkoani Mwanza amefanikiwa kutetea ubingwa wake akimaliza wa kwanza huku akiwashinda washindani wake,Salma William aliyeshika nafasi ya pili na Elizabeth Clement aliyeshika nafasi ya tatu.

Mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume ,Seni Konda amejinyakulia kitita cha sh Mil 1.5 ,mshindi wa pili Makoja Hamis akijinyakulia kiasi cha sh Mil moja huku mshindi wa tatu ,Hamis Clement akiambulia kiasi cha sh 700,000.

Upande wan wanawake mshindi wa kwanza Martha Anhtony amejinyakulia kiasi cha sh Mil 1.2,mshindi wa pili Salma William akipata sh 800,000 huku mshindi wa tatu ,Elizabeth Clement akipata sh 600,000.

Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mbio hizo mgeni rasmi naibu waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo Anastazia Wambura amesema michezo ni ajira na afya ambapo pia amewataka wachezaji kutotumia madawa ya kusisimua misuri kwa kuwa kitendo hicho ni kinyume cha taratibu za michezo na atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Baiskeli cha Tanzania (CHABATA) Jacx Mhagama alisema CHABATA na kampuni ya madini ya ACACIA wamesaini mkataba wa udhamini wa mashindano hayo kwa muda wa miaka mitatu kuanzia 2014 mpaka 2016.

“Kipindi hiki cha miaka mitatu kimekuwa na mengi kiutendaji na kimahusiano kwetu sote CHABATA na ACACIA. lakini kwetu imekuwa ni kipindi chenye chenye changamoto zenye kutukomaza na kutujenga. Hivyo tumevuna tuliyoyategemea na ziada pia.”alisema Mhagama.

“ACACIA ni kampuni yenye machimbo ya madini kwenye eneo hili la kanda ya Ziwa, lakini wameonyesha upendo na uzalendo mkubwa hata kwa Taifa. Pamoja na kujishughulisha na michezo kwenye eneo hili la kanda ya ziwa, wameenda juu Zaidi kufikia taifa kwa kuifadhili timu yetu ya Taifa ya Baiskeli kwenye mashindano ya Ubingwa wa Afrika mwaka jana 2015, yaliyofanyika huko Petermarizburg nchini Afrika ya Kusinu.”aliongeza Mhagama.

Dkt. Kigwangalla asimikwa Uchifu wa Wanyamwezi wa Tanzania, aahidi makubwa

$
0
0

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akivishwa shuka katika hatua ya kusimikwa uchifu huo
 

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipata picha ya pamoja na wazee wa mila pamoja na wanakijiji
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwaaga wazee wa mila
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga picha pamoja na vijana wa kijiji hicho. (Picha zote na Andrew Chale,Nzega-Tabora).
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla amepewa heshima ya Uchifu wa Watanzania wa Kabila la Wanyamwezi na Wazee wa Kijiji cha Isalalo katika Kata ya Utwigu iliyopo katika Jimbo hilo la Nzega Vijijini Mkoani Tabora.

Dk. Kigwangalla ambaye yupo ziarani katika maeneo mbalimbali ya Jimbo hilo kwa lengo la kushukuru Wananchi hao kwa kumpigia kura nyingi za zilizomwezesha kuingia Bungeni, ambapo katika tukio hilo lililoshuhudiwa na umati mkubwa wa wanakijiji wa Kijiji hicho,

Wazee hao wa Mila walieleza kuwa, hatua hiyo ya kusimikwa Uchifu wa heshima wa kabila la Wanyamwezi ni ishara kubwa kuwa Kijana mashuhuri na kijana mpiganaji sawasawa hivyo kwa ushindi wake kuchaguliwa nahata kupewa Uwaziri (Naibu Waziri), ni ishara kubwa ya kufikia malengo yake aliyokusudia katika Taifa hili.

Wazee hao wa Mila waliweza kumkabidhi mishale, Mkuki, upinde na kumtakia kila lakheri katika safari yake hiyo ya kiutawala.

Akitoa shukrani zake katika tukio hilo, Dk. Kigwangalla amesema kuwa, Wananchi wake wategemee neema kubwa kwani kwa sasa yupo katika hatua ya utendaji kazi Zaidi na kuwataka wawe na Imani naye pamoja Serikali iliyopo madarakani kwani imejipanga kuleta maendeleo makubwa.

“Nawashukuru nyie kwa kuniwezesha kunipigia kura nyingi sana ambazo zimeniwezesha mimi kupata nafasi ya kuingia Buangeni. Nawaahidi kuwatumikia kwa nguvu zangu zote. Nguvu nilizozianza tokea awali na kwa sasa zitakuwa kubwa Zaidi, muendelee kuniombea.

Nafahamu kuna kero nyingi sana, shida za barabara za kuingia na kutoka huku Vijijini, Suala la Umeme na mengine mengi haya yote yanafanyiwa kazi na taratibu zote zinaenda vizuri.” Alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa kuwashukuru wananchi wa kijiji hicho cha Isalalo.

Ziara hiyo iliyoanza tokea Julai 13 mwaka huu, Mbunge huyo ambaye Jimbo lake hilo lenye jumla ya Kata 19, zikiwemo Kata ya Puge, Ndala, Nata,, Sanzu, Lusu, Milambo Itobo, Magengati, Budushi, Nkiniziwa, Mbagwa, Mizibaziba, Utwigu, Muhugi, Mwantundu, Wela, Mwasala, Tongi, Ugembe.

Ambapo katika Vijiji vya Kata hizo amewafikia wananchi na kuwashukuru kwa hatua yao ya kumchagua ambapo pia ameweza kutekeleza ahadi aliyoitoa yeye mwenyewe ikiwemo vifaa vya michezo kwa timu za vijana, pamoja na kutimiza ahadi za michango mbalimbali ikiwemo ya kuchangia ujenzi wa shule, makanisa, misikiti, Zahanati na mambo mbalimbali huku pia akipokea maoni na uashahuri kutoka kwa wapiga kura wake hao.
DSC_2015DSC_2023DSC_2030

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Wanakijiji cha Isalalo



Wazee wa Mila



Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni



Wazee wa Mila wakiwa upande wa wageni maalum


Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akikabidhiwa mkoba wa mishale



Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipewa baraka na wazee hao



Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akirejea kukaa baada ya kukabidhiwa Uchifu wa Wanyamwezi



Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akinyanyua juu mkuki ishara ya Kijana shujaa wa Wanyamwezi..



Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Diwani wa Kata Utwigu



Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa shukrani zake kwa wananchi



Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Kijiji



Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea salamu kutoka kwa watoto


Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipata picha ya pamoja na wazee wa mila pamoja na wanakijiji
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwaaga wazee wa mila
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga picha pamoja na vijana wa kijiji hicho. (Picha zote na Andrew Chale,Nzega-Tabora).

WAZIRI MKUU MAJALIWA: BARA LA AFRIKA BADO LINAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA MAJI

$
0
0


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Bara la Afrika bado linakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama hasa vijijini kwa sababu nchi zake bado hazijamudu kuunganisha huduma hiyo katika maeneo hayo.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu amewataka wataalamu wa masuala ya maji watafute njia sahihi itakayowezesha kutatua tatizo hilo kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya maji vilivyoko.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Julai 18, 2016) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano wa 10 wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Afrika (AMCOW) ambao unaokwenda sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Maji Afrika.

“Tunategemea baada ya kumazika kwa mkutano huu wataalamu wetu wataondoka na maazimio mazuri ya kumaliza tatizo la maji katika Bara letu kwa kutumia mito na maziwa ili kufikisha maji kwa wananchi,” alisema.

Akizungumzia kwa upande wa Tanzania alisema, suala la maji limepewa kipaumbele hata katika bajeti ya mwaka huu na kwamba Serikali itahakikisha maji yanapatikana katika maeneo yote ili kutimiza sera yake ya kila mwananchi kupata maji umbali usiozidi mita 400.

Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki ambaye ni Mjumbe Maalumu wa UNESCO kwa ajili ya masuala ya maji Barani Afrika alisema maji ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi, hivyo wataalamu wanatakiwa kuhakikisha huduma hiyo inapatika katika maeneo yote.

Mkutano huo wa siku tano unahudhuriwa Mawaziri wa Maji kutoka nchi 45 za Afrika na unaongozwa na Waziri wa Maji na Mazingira wa Senegal Amadou Mansour Faye ambaye ni Rais wa AMCOW.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
JUMANNE, JULAI 19, 2016
 

SOUTH AFRICAN RALLY DRIVER DIED IN TANZANIA AND NOT KENYA

$
0
0
 Tanzania Tourist Board (TTB) wishes to refute claim made by Cara Anna, an Associate Press for Miami Herald, a US based media house who on July 18th , 2016 wrote an article claiming that Mr. Guguleth Zulu, a renowned South African rally driver, died while trying to summit ‘Kenya’s Mt Kilimanjaro’.

We would like to correct this misleading information issued by Miami Herald, that Mt. Kilimanjaro is in TANZANIA and not in KENYA.
TTB has contacted Miami Herald and has demanded that they issue a correct statement via the same media channel they used to issue the misleading information about the location of Mt. Kilimanjaro, so as to put it clear to the International community that MT. KILIMANJARO IS IN TANZANIA.

Issued by:
MANAGING DIRECTOR
TANZANIA TOURIST BOARD
July 19 th , 2016
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>