Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

WAFANYAKAZI MKOA WA MANYARA WATAKIWA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA.

$
0
0
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Eliamkim Maswi (kushoto) akipimwa afya yake mjini Babati na mtumishi wa hospitali ya mkoa huo John Martin, kwenye kikao cha kuimarisha afua za ukimwi mahali pakazi.
 
Wafanyakazi wa Mkoa wa Manyara, wametakiwa kupima afya zao mara kwa mara ili kujitambua namna walivyo katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ya kuhudumia jamii ya eneo lao.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Eliakim Maswi aliyasema hayo jana mjini Babati wakati akizungumza kwenye kikao cha kuimarisha afya za ukimwi mahali pakazi iliyotolewa kwa watumishi wa ofisi ya mkuu wa mkoa huo. Maswi alisema kuwa lengo lao ni kuhakikisha mtumishi wa mkoa huo asiingie kwenye hatari ya kuambukizwa virusi vya ukimwi (VVU) na kama amekwisha ambukizwa asinyanyapaliwe na kusiwe na kifo kitokanacho na ukimwi.

Alisema japokuwa hali ya maambukizi ya VVU kwa mkoa wa Manyara ipo chini lakini hivi sasa wanafanya jitihada za kuhakikisha yanapungua na watumishi wanapaswa kujitambua afya zao ili waendelee kujitunza ipasavyo. “Hata mimi nimepima ili kuonyesha njia na sisi kama viongozi tunapaswa kufanya hivyo najiamini nipo salama na nivizuri tuwe na utamaduni wa kupima afya zetu kila mara kwa lengo la kujitambua tulivyo,” alisema Maswi.

Alisema watumishi wa umma wanapaswa kujihadhari na maambukizi mapya ya VVU na kuondokana na athari ya magonjwa sugu yasiyoambukiza kama shinikizo la damu, kisukari, figo, moyo na kupenda kufanya mazoezi.

“Watumishi wa serikali wanapswa kupima afya zao na kutambua namna walivyo kuliko mtu kuendelea kuishi ili hali hautambui afya yako ipo namna gani na kwa njia hiyo tutatambua nguvu kazi tuliyonayo,” alisema Maswi. Mratibu wa kudhibiti ukimwi wa mkoa huo, Anna Fissoo alisema hali ya maambuki ya VVU kwa mkoa huo siyo kubwa kwani hadi hivi sasa ni asilimia 1.5 ndiyo wana maambukizi huku wilaya ya Simanjiro ikiongoza kwa asilimia 3.2.

Fissoo alisema maambukizi ya VVU kwa halmashauri ya Babati mjini ni asilimia 2.3, Kiteto ni asilimia 2.2, Babati vijijini ni asilimia 1.7, Hanang’ ni asilimia 1.0 na halmashauri ya wilaya ya Mbulu ina maambukizi kidogo kwa asilimia 0.7

Serikali yasaidia viwanda vidogo 48,996

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imesaidia jumla ya viwanda vidogo 48,996 kwa kuvipa huduma muhimu zinazowawezesha wajasiriamali kusimama wenyewe ili kuondokana na lindi la umasikini.

Takwimu hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Viwanda Vidogo na vya Kati kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Consolatha Ishebabi alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hii kuhusu mikakati ya Serikali juu ya kuendeleza viwanda vidogo pamoja na umuhimu wa viwanda hivyo.

Dkt. Ishebabi amesema kuwa Viwanda Vidogo vikiendelezwa ndio mwanzo wa kuwa na viwanda vya Kati na Vikubwa na hiyo ndio sababu kubwa inayoifanya Serikali kutilia mkazo na kuzidi kuweka mikakati mingi ya kuviinua viwanda hivyo ili vikue na kufikia viwanda vya kati au vikubwa.

“Kwa mujibu wa Sensa ya Viwanda ya mwaka 2013, Tanzania ina jumla ya viwanda vidogo 48,996 ambavyo vimesaidia kutoa jumla ya ajira 156,476 kwa wananchi, hivyo tunaona umuhimu wa viwanda vidogo katika suala la kutoa ajira na kupunguza umasikini kwa kiasi kikubwa”, alisema Dkt. Ishebabi.

Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa viwanda vidogo sio mali ya Serikali bali Serikali iko pamoja na viwanda hivyo katika kuvisaidia ili viendelee na kuhakikisha vinakuwa kufikia viwanda vya kati au vikubwa hivyo, kazi ya Serikali ni kuwahamasisha wananchi na kuwapa misaada ya elimu, mikopo pamoja na kuwawezesha maeneo ya kufanyia shughuli hizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko na Habari wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Viwanda Vidogo (SIDO), Janeth Minja amesema kuwa Shirika hilo ni kubwa na liko katika Mikoa yote Tanzania, linawasaidia wajasiriamali kwa kuwapa huduma za aina 4 ambazo ni; mafunzo, teknolojia, mikopo pamoja na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao.

“Napenda kutoa rai kwa wananchi hasa vijana na wanawake wasio na ajira kuwa wasijibweteke tu majumbani bali watumie fursa zinazotolewa na SIDO ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini, kama mtu ana wazo la biashara anatakiwa awasiliane na ofisi zetu za SIDO zilizopo kwenye Mkoa husika”, alisema Janeth.

MKUU WA WILAYA MJINI ZANZIBAR AZINDUA MABARAZA YA VIJANA JIMBO LA MAGOMENI.

$
0
0

4 
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Bi. Marina Joel Tomas akizungumza na Vijana wa Jimbo la Magomeni katika uzinduzi wa mabaraza ya Vijana Jimbo la Magomeni kabla yakulizindua rasmin Baraza hilo Julay 16, (kulia) Mbunge wa Jimbo hilo Jamal Kassim Ali na (kushoto) Mwenyekiti wa mabaraza ya Vijana Jimbo la Magomeni Kassim Lila Msoma.
5 
Baadhi ya Vijana wa mabaraza ya vijana Jimbo la Magomeni wakimsikiliza Mgeni rasmin Mkuu wa Wilaya ya Mjini Bi. Marina Joel Tomas hayupo (pichani) wakati wa uzinduzi huo.
6 
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Bi. Marina Joel Tomas na Mbunge wa Jimbo la Magomeni Jamal Kassim Ali wakiwapungia mkono Vijana kuwaaga baada ya uzinduzi wa mabaraza ya Vijana Jimbo la Magomeni.Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
1 
Brasbend ya Chipkizi ikiongoza maandamano ya uzinduzi wa mabaraza ya vijana Jimbo la Magomeni katika shamrashamra za uzinduzi wa mabaraza hayo uliofanyika uwanja wa Magae Meya Mjini Zanzibar.
2 
Sabra Abdalla Amer akisoma risala ya vijana katika uzinduzi wa mabaraza ya vijana Jimbo la Magomeni.
3Mwenyekiti wa mabaraza ya Vijana Jimbo la Magomeni Kassim Lila Msoma akimkaribisha mgeni rasmin katika uzinduzi wa mabaraza ya vijana Jimbo la Magomeni, Mkuu wa Wilaya ya Mjini Bi. Marina  Joel Tomas (hayupo pichani).




Na Maryam Kidiko/Maelezo Zanzibar. 17/07/2016.

Mkuu wa Wilaya ya mjini Marina Joel Tomas amesema lengo la Serikali la kuunda Mabaraza ya Vijana ni kuona Vijana hao wanakaa pamoja ili kujadili mambo muhimu yanayowahusu na kupambana na changamoto zinazowakabili.Ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Baraza la vijana la jimbo la magomeni iliyofanyika katika uwanja wa magae meya wilaya ya mjini unguja.

Mkuu huyo amefahamisha kuwa mabaraza hayo yatasaidia Vijana hao kuandaa Maandiko ya Miradi mbali mbali watakayoanzisha katika mabaraza yao kwa lengo la kujikwamua na maisha.Vile vile amesema kukaa pamoja vijana hao kutaiwezesha Serikali kupata urahisi wa kuwasaidia vijana kuliko kuwasaidia mmoja mmoja .

Amesema kuwa Fursa za kuwapatia ajira Vijana hao Serikalini ni chache sana hivyo vijana hao wanapaswa kujiunga pamoja na kutafuta namna ya kujiajiri wenyewe.Aidha mkuu wa wilaya hiyo aliahidi kuwa serikali itakuwa karibu na Vijana hao sambamba na viongozi wa jimbo hilo ili kuzifanyia kazi changamoto zinazoyakabili mabaraza hayo.

Nae Mbunge wa Jimbo la Magomeni Jamal Kassim Ally alisema atashirikiana na Vijana ili kuleta maendeleo katika jimbo lake na kuungana na Serikali ya wilaya pamoja ili kuweza kuinuwa vipaji walivyokuwa navyo vijana katika jimbo lake .

“Vijana wamejengewa jukwaa lao maalum la mabaraza ya vijana kuweza kujiendesha wenyewe, kujiajiri pamoja na kuweza kufanya shuhuli mbali mbali za kimaendeleo “Alisema Jamal .

Mbunge Jamal alisema baraza hilo halipo kichama hivyo kila kijana anahaki ya kujiunga katika baraza ili asiweze kupoteza haki zake za msingi kama kijana .Hata hivyo amewataka vijana hao kuitumia vizuri nafasi hiyo waliyoipata




BALOZI OMBENI SEFUE ATEMBELEA TAASISI YA WAKALA WA TAIFA WA UTAFITI WA NYUMBA BORA NA VIFAA VYA UJENZI (NHBRA)

$
0
0
Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Menejimenti ya Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) wakati alipofanya ziara katika taasisi hiyo mwishoni mwa wiki ili kujionea shughuli mbali mbali zinazofanywa na taasisi hiyo , Kwa kiwango kikubwa (NHBRA) imeonyesha ni taasisi inayoweza kujenga nyumba za bei nafuu sana hasa vijijini ili watanzania wa maeneo hayo waweze kupata makazi bora ya kuishi kwa bei rahisi zaidi, Kulia katika picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Bw.Matiko Samson Mturi.

Taasisi hiyo pia imekuwa ikijihusisha na mafunzo teknolojia ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa vikundi mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na kuwafundisha juu ya utengenezaji wa matofali, vigae vya kuezekea nyumba pamoja na ujenzi wa nyumba za zenyewe ambapo taasisi na wananchi mbalimbali wanaweza kufaidika na mpango huo nchini.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Bw.Matiko Samson Mturi akizungmza wakati alipokuwa akimkaribisha Balozi Ombeni Sefue wakati alipotembelea katika taasisi ya Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba na Vifaa vya Ujenzi NHBRA Mwenge jijini Dar es salaam. Bw. Sylivester Shumbusho Fundi kutoka Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba na Vifaa vya Ujenzi NHBRA akimpa maelezo Balozi Ombeni Sefue juu ya utengenezaji wa matofali ya bei rahisi kwa kutumia udongo wakati alipokuwa akitembelea karakana ya taasisi hiyo iliyopo Mwenge jijini Dar es salaamKatikati ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Matiko Samson Mturi. Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Matiko Samson Mturi akimpa maelezo Balozi Ombeni Sefue wakati alipokuwa akitembelea na kukagua shughuli mbalimbali katika taasisi hiyo kulia ni Bw. Sylvester Shumbusho Fundi katika taasisi hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wakiendelea na shughuli za kutengeneza vigae vya kuezekea nyumba katika karakana ya taasisi hiyo.
Balozi Ombeni Sefue akitembezwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Matiku Samson Mturi maeneo mbalimbali ili kujionea shughuli za zinazofanywa na taasisi hiyo. Balozi Ombeni Sefua akishiriki katika shughuli ya kufyatua matofali kazi inayofanywa pia na Taasisi hiyo kwa kutoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali vya ujasiriamali nchini kote. Balozi Ombeni Sefua akiangalia kazi ya kufyatua matofali inayofanywa pia na Taasisi hiyo kwa kutoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali vya ujasiriamali nchini kote.
Balozi Ombeni Sefue akiangalia wafanyakazi wa taasisi hiyo wakati wakitengeneza vigae kwa ajili ya kuezekea nyumba.
Balozi Ombeni Sefue akipiga picha kwa simu yake huku wafanyakazi wa taasisi hiyo wakimuangalia baada ya moja ya nyumba ndogo iliyojengwa katika ghala ya taasisi hiyo kwa ajili ya mfano kumfurahisha. Balozi Ombeni Sefue pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Matiko Samson Mturi wakipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa taasisi hiyo mara baada ya kukamilika kwa ziara hiyo.

LAPF YATOA MSAADA WA MASHUKA 375 KWA HOSPITALI YA WILAYA YA KISARAWE MKOANI PWANI

$
0
0

Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe (katikati), akimkabidhi Mbunge wa Kisarawe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jaffo (wa pili kushoto), msaada wa mashuka 375 yenye thamani ya sh.milioni nane kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe katika hafla iliyofanyika hospitalini hapo juzi. Kutoka kushoto ni Mganga wa hospitali hiyo, Elizabeth Oming'o, Mwenyekiti wa Huduma za Kijamii wa Halmshauri ya Kisarawe, Abel Mudo.


Mganga wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Elizabeth Oming'o (kulia), akitoa historia fupi ya hospitali hiyo kabla ya kumkaribisha Mbunge wa Kisarawe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jaffo (wa pili kulia), kupokea msaada wa mashuka 375 yenye thamani ya sh.milioni nane kutoka Mfuko wa Pensheni wa LAPF katika hafla ya makabidhiano yaliyofanyika juzi hospitalini hapo. Kutoka kushoto ni Katibu wa Madiwani wa Halmshauri hiyo, Jnady Chakachaka na Mwenyekiti wa Huduma za Jamii wa Kisarawe, Abel Mudo.
Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jaffo, akisisitiza jambo. Kutoka kulia ni Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Juma Kanena, aliyemwakilisha OCD katika hafla hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe, Patrick Allute na Mwenyekiti wa Huduma za Kijamii wa Halmshauri hiyo, Abel Mudo.
 


Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe (kushoto), akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo.

 
 
Wafanyakazi wa kada mbalimbali wa hositali hiyo wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa mashuka hayo.


Mwenyekiti wa Huduma za Kijamii wa Halmshauri hiyo, Abel Mudo, akijitambulisha.
Katibu wa Madiwani wa Halmshauri hiyo, Jnady Chaka chaka (kushoto), akijitambulisha.
Katibu wa Waziri Jafo, Eleuter Kihwele (kushoto), akijitambulisha.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jaffo (kushoto), akisisitiza jambo kwenye hafla hiyo..
Waziri Jafo (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa wilaya hiyo.


Na Dotto Mwaibale, Kisarawe

MFUKO wa Pensheni wa LAPF, umetoa msaada wa mashuka 375 yenye thamani ya sh.milioni nane kwa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa mashuka katika hospitali hiyo.

Hafla ya kukabidhiana mashuka hayo ilifanyika juzi katika hospitali hiyo kati ya Mbunge wa Kisarawe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Tamisemi, , Suleiman Jaffo na Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo Mlowe alisema wametoa msaada huo baada ya kutambua wadau wakubwa wa hospitali hiyo ni wateja wao na wananchi wenye kipato cha chini.Alisema wanaofika kupata huduma katika hospitali hiyo ni wadau wao hivyo watashirikiana bega kwa bega kuondoa changamoto wanazokabiliana nazo pindi wanapofuata huduma.

Mlowe alisema walipokea maombi ya kuiwezesha hospitali hiyo kutokana na changamoto zilizopo hivyo wameona ni vyema wakatoa mashuka ambayo yatasaidia kupunguza uhaba uliopo sasa."Suala la afya kwetu sisi ni kipaumbele cha kwanza hivyo ili kupata wanachama bora na wenye afya ni lazima sekta hii iwezeshwe," alisema Mlowe.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (OR Tamisemi), Suleiman Jafo alisema kuimarisha Sekta ya Afya ni pamoja na kuondoa changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

Alisema hospitali ya Kisarawe ina wataalam wengi wa afya japokuwa inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji kutatuliwa.Jafo alisema ni vyema vifaa vilivyopo vikatumika kwa walengwa ambao ni wananchi na kuacha ubaguzi wakati wa utoaji tiba.

Mganga wa Wilaya hiyo, Elizabeth Oming'o alisema wanakabiliwa na changamoto ya vifaa tiba katika hospitali hiyo na vituo vya afya.Alisema hospitali hiyo no ya muda mrefu hivyo miundombinu yake inahitaji pia ukarabati.

Dk.Elizabeth alisema kwa muda mrefu mashine ya Ultra Sound imeharibika bado haijafanyiwa matengenezo jambo linalowalazimu wagonjwa wao kupima nje ya hospitali.Hata hivyo alisema uhaba wa wafanyakazi wa kada mbalimbali katika hospitali hiyo imesababisha huduma kushindwa kutolewa kwa wakati.

"Uhaba wa watumishi wa kada mbalimbali kwetu ni changamoto hivyo tayari tumeomba kibali cha kuajiri watumishi wa kada mbalimbali ili kuweza kufanyakazi kwa ufanisi," alisema Dk.Elizabeth.

Alisema hospitali hiyo ilikuwa ikikabiliwa na uhaba wa mashuka 1200 ambapo hadi sasa wamepokea msaada wa mashuka 475 ambayo kati ya hayo 100 yalitolewa na Mamlaka ya Bandari Tanzania na mengine 375 kutoka LAPF.

UNESCO YAKUTANISHA WADAU KUJADILI USAFI WA MAJI, HALI YA USALAMA BADO SI NZURI

$
0
0
Katika kuhakikisha kunakuwa na usalama wa maji duniani kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya vifo ambavyo vinatokana na uchafu katika maji, Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limefanya kongamano la siku moja ambalo limewakutanisha viongozi wa idara za maji za mikoa mbalimbali nchini na kutoka nje ya nchi.

Katika kongamano hilo mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, George Lugomela alisema sehemu kubwa ya vyanzo vya maji zimekuwa vikichafuliwa kutokana na usafi wa binadamu.

Alisema kuwa takwimu zinaonyesha ni asilimia 24 ya watu Afrika ndiyo wanajisaidia katika maeneo ambayo ni salama na idadi iliyobakia wamekuwa wakijisaidia mazingira ambayo yanahatarisha vyanzo vya maji na wengi wao wakijisaidia maporini.

Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, George Lugomela akitoa hotuba kwa niaba ya serikali katika kongamano hilo. (Picha na Modewjiblog)

"Kongamano hili linaangalia kuhusu vijidudu vilivyo katika maji ambavyo kwa asilimia kubwa yanachafuka kutokana na usafi ambao anaufanya binadamu na ukiangalia kwa nchi zetu inaonyesha bado uhifadhi wa hizo taka kama kinyesi ambacho baadae huathiri vyanzo vya maji ni mdogo," alisema Lugomela.

Aidha alisema pamoja na maeneo mengine kufanya ujenzi wa vyoo lakini jambo hilo bado sio salama kwa asilimia 100 na hivyo inahitajika kufanyika jitihada za ziada ili kuweza kuviweka vyanzo vya maji katika hali ya usalama.
Mshauri Mwandamizi wa UNESCO, Bruno Nguyen, akielezea umuhimu wa kongamano hilo.

Nae Mshauri Mwandamizi wa UNESCO, Bruno Nguyen, alisema kuwa kongamano hilo lina malengo ya kupata suluhisho ili kuhakikisha watu ambao wanaishi bara la Afrika wanapata maji safi na salama.

Katika ripoti ya mwaka 2014 ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya (WHO) inaonyesha kuwa watu bilioni 1.8 duniani kote wanatumia maji ambayo yana vijidudu.
Mtaalam wa programu wa UNESCO, Alexandros Makarigakis akitoa takwamu za usalama wa maji na jinsi taka mwili za binadamu zinavyoyafanya maji yasiwe salama.

Baadhi ya watu waliohudhuria kongamano hilo la siku moja kutoka mikoa mbalimbali na nchi jirani.





Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

AKINAMAMA MOROGORO WAELIMISHWA JINSI YA KUKAUSHA MBOGA NA MATUNDA

$
0
0


Embe zikiwa zinakaushwa katika kikundi cha Mzinga Green Voives kwenye Kijiji cha Konga, Manispaa ya Morogoro.


Mboga aina ya mnafu ikiwa imestawi vizuri katika shamba la mmoja wa wanakikundi cha Mzinga Green Voices. Mboga hizi ndizo zinazokaushwa na kikundi hicho.

KWA Rahma Masenda (36), mkazi wa Kijiji cha Konga, Mzinga mkoani Morogoro, sasa mboga zake za majani hazitaweza kupotea tena kama ilivyokuwa mwanzo, kwani yeye na wenzake wamepata ufumbuzi wa kudumu.

Rahma anasema kwamba, hivi sasa wanaweza kukausha mboga zote – za bustani na za asili – kwa namna ambayo inawawezesha kuhifadhi muda mrefu pamoja na kuongeza mnyororo wa thamani.

Rahma na wenzake wameunda kikundi chao wanachokiita Mzinga Green Voices Women Group ambacho kinatekeleza mradi wa Green Voices unaolenga kupambana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na uharibifu wa mazingira.

“Tumepata elimu ya kutosha kuhusu namna ya kukausha mboga mboga pamoja na matunda, tunatumia umeme-jua (solar) na kwa hakika tumeweza pia kujifunza jinsi ya kusindika katika ubora unaotakiwa ili tuingie kwenye soko la ushindani,” anasema Rahma, ambaye pia ndiye mwenyekiti wa kikundi hicho chenye wanachama 25.

Rahma anasema kwamba, kabla ya kupatiwa elimu hiyo miezi mitatu iliyopita, mboga zao zilikuwa zimetelekezwa mashambani na kwenye bustani kwa vile hata zinapopelekwa sokoni wanauza kwa bei ndogo.
Banio linalotumia umeme-jua (solar power) ambalo linatumika kukaushia mboga mboga na matunda. Banio hili ndilo linalotumiwa na akinamama wa Mzinga Green Voices katika Manispaa ya Morogoro.

“Hivi sasa msimu wa kilimo umeishia na wengi wanayatumia mashamba hayo kulima bustani, mboga ni nyingi na zinatofautiana ubora, sasa ukipeleka sokoni unauza kwa bei ndogo, hivyo wengi hujikuta wakishindwa kilimo hicho na mboga nyingi kuharibika,” anaongeza mmoja wa wanachama wa kikundi hicho, Mwakaaje Mrisho.

Bi. Mwakaaje anasema kwamba, kwa miaka yote wamekuwa wakikausha mboga za majani kwa njia za asili lakini siyo za aina zote, hata hivyo baada ya kupatiwa elimu kupitia Mradi wa Green Voices wamegundua kwamba kumbe zipo fursa kubwa za kuongeza kipato kwa ukaushaji wa kisasa ambao unaongeza pia thamani.

“Hata maembe yetu ambayo zamani yaligeuzwa mpira na watoto ambao walikuwa wakiyapiga teke kutokana na kukosa walaji sasa tunaweza kuyakausha na kuyasindika kwa kutumia vifungio maalum, na bei yake ni kubwa kuliko kama tungeyauza vivi hivi,” anasema kwa furaha.Kwa ujumla, kila kabila nchini Tanzania lina utamaduni wa kuhifadhi mboga za majani na namna ya kuhifadhi.Ukienda Dodoma, wakazi wa huko wanajua namna ya kukausha na kuhifadhi mboga za asili kama mlenda, mgagani pamoja na majani ya kunde kama ilivyo kwa wakazi wa mikoa mingine.

Hata hivyo, kutokana na kukosa utaalamu, wananchi wengi wamekuwa wakishuhudia mboga za majani zikiharibika mashambani huku hata zile zilizohifadhiwa nazo zikiharibika kutokana na kutohifadhiwa kitaalamu.

Bi. Esther Mfui, mratibu wa mradi huo wa Mzinga Green Voices Women Group, anasema kwamba, wanawake na jamii nzima ya Kijiji cha Konga hivi sasa wameongeza kasi ya kilimo cha mboga mboga na matunda baada ya mradi huo kupelekwa kijijini hapo.

Anasema kwamba, hivi sasa wakulima wengi wa Manispaa ya Morogoro wamekuwa wakifunga safari kutoka maeneo mbalimbali kwenda kujifunza namna ya ukaushaji wa mboga na matunda huku wengi, wakiwemo wanaume, wakitaka kujiunga na kikundi hicho.

“Kuna baba mmoja mkulima kutoka Kingolwira amefunga safari kutoka huko kuja huku ili ajifunze na amesema kwamba anakwenda kuwahamasisha wakulima wenzake wajiunge pamoja ili wapatiwe mafunzo hayo, tutawafundisha kwa sababu lengo ni kutaka kuhakikisha wakulima wanaongeza kipato na kuongeza usalama wa chakula, lakini kwa kuhifadhi chakula bora,” anasema.

Anasema kwamba, siku za nyuma ilikuwa vigumu kwa wananchi kupata mboga za majani nyakati za kiangazi, lakini kwa teknolojia hiyo mpya, wana uhakika wa kutumia mboga za majani mwaka mzima ilimradi tu zikaushwe kitaalamu na kuhifadhiwa.Bi. Esther anasema kwamba, ukaushaji huo unaongeza thamani, kwani wanawake hao wamefundishwa namna ya kuweka katika vifungashio maalum na kuweka alama, ambapo inakuwa rahisi kwao kuuza bidhaa hizo kwa bei ya juu zaidi.

Yeye ni mmoja kati ya akinamama 10 wanaotekeleza mradi wa Green Voices, ambao unafadhiliwa na taasisi ya Foundation for Women of Africa inayojihusisha na maendeleo ya wanawake wa Afrika, ambayo inaongozwa na Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania, María Teresa Fernández de la Vega.

Jumla ya akinamama 10 wanatekeleza miradi mbalimbali ya ujasiriamali nchini Tanzania inayoendana na mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Kigoma, Kilimanjaro, Pwani na Mwanza.

Mboga ni chakula kinachohitajika katika maisha ya kila siku, lakini wananchi wengi wamekuwa wakitumia mboga za majani kwa wingi katika kipindi cha masika tu na kuzikosa wakati wa kiangazi kutokana na kushindwa namna ya kuzikausha na kuzihifadhi.

Kwa teknolojia wanayotumia akinamama wa Mzinga Green Voices, sasa wananchi wanaweza kukausha kila aina ya mboga kuanzia mchicha, spinachi, Chinese, kabichi, kisamvu, nyanya na kadhalika, hivyo kujihakikishia aiba ya kutosha ya chakula.


Mboga za majani pamoja na matunda ni chanzo kikuu cha vitamini zinazohitajika katika mwili wa binadamu ambazo haziwezi kuhifadhiwa mwilini kama vile protini au wanga.Hivyo ili kuuwezesha mwili kupata vitamini hizo ni muhimu kula mboga za majani kila siku, kwani mboga mbichi za majani zina vitamini zote zinazotakiwa na mwili kwa ukamilifu na hupatikana kwa msimu.

Ili ziweze kupatikana baada ya msimu wake, inabidi watumiaji wajue na watumie teknolojia za utayarishaji na uhifadhi wa mboga hizo.Hifadhi ya mboga mbichi ni ngumu na huchukua muda mfupi sana kutokana na uharibifu unaosababishwa na vimelea vinavyosababisha magonjwa na kuoza.

Ili kuwezesha hifadhi ya muda mrefu na upatikanaji wake wakati wote, teknolojia za utayarishaji na ukaushaji wa mboga kama vile mchicha, majani ya mikunde, matembele, kabichi, majani ya muhogo (kisamvu) ni muhimu kuzingatia.Wataalamu wanaeleza kwamba, usafi ni kanuni ya msingi katika ukaushaji wa mboga ambao mtu anayeshughulika na ukaushaji wa mboga na hifadhi, anapaswa kuwa na mwili safi na nguo zenye uwezo wa kuonyesha uchafu.Mboga ni lazima zioshwe vizuri kwa maji safi na salama, vifaa na eneo la kufanyia kazi lazima viwe safi na visivyoshika kutu, na lazima mazingira yanayozunguka eneo la kutayarishia na kukaushia yawe safi.

Jambo jingine muhimu kuzingatiwa ni kwamba, ubora wa mboga zilizokaushwa hutegemea ubora wa mboga mbichi, hivyo malighafi zilizo safi na bora hutoa bidhaa bora baada ya kusindika.Ubora wa mboga zilizokaushwa hutegemea usafi wa mboga mbichi pamoja na utayarishaji bora wa awali lakini pia hutegemea teknolojia iliyotumika kwenye ukaushaji na ufungashaji pamoja na hifadhi.


“Mboga mbichi za majani zilizooshwa vizuri na kukatwa zinapaswa kutayarishwa kabla ya kukaushwa ili kudumisha rangi, harufu na ladha. Utayarishaji wa mboga hizo hufanyika kwa kuziweka kwenye chujio kubwa safi au kitambaa safi cheupe na kuziweka kwenye maji yanayochemka kwa muda usiozidi dakika mbili, kisha hutolewa na kuachwa zipoe. Lengo ni kuzuia kazi ya vimeng’enyo vinavyosababisha mabadiliko yasiyotakiwa kwenye mboga. Utayarishaji huu pia hupunguza upotevu wa vitamini A,” anasema Bi. Esther Mfui.Bi. Mfui anasema kwamba, matunda ya kukausha hutayarishwa kwa kuoshwa vizuri, kumenywa na kukatwa vipande vidogo vilivyolingana vya ukubwa kati ya milimita tatu hadi sita.

Anasema, mara nyingi hupitishwa kwenye mvuke wa maji moto au kuwekwa kwenye maji yanayochemka kama inavyofanyika kwa mboga, lakini kwa muda usizidi dakika tano. Mara kwa mara chumvi au sukari au siki au tindikali aina ya sitriki (citric acid) hutumika kwenye utayarishaji wa matunda kabla ya kukausha kutegemea aina ya tunda na matakwa ya walaji.Dhana ya ukaushaji wa mboga na matunda ni kupunguza maji yaliyoko ndani yake kutoka asilimia 90 hadi asilimia 10.

Bi. Mfui anasema, kukausha mboga au vyakula vingine na hifadhi kuna lengo la kuhakikisha chakula kinapatikana hata baada ya msimu. Teknolojia ya kukausha mboga na vyakula vingine inatumika toka zamani, ingawa kwa sasa ipo teknolojia bora zaidi.

“Kimsingi ukaushaji unasababisha vimelea kama bakteria na fangasi kushindwa kukua na kusababisha uharibifu wa vyakula hivyo, tofauti na kuvichemsha vyakula hivyo ambapo vimelea hivyo hufa.

“Wakati unapokausha unapunguza unyevu kiasi ambacho unaobakia kwenye vyakula hivyo hautoshi kusababisha ukuaji na uongezekaji wa vimelea hivyo. Aidha vyakula vilivyokausha vikipata tena maji vimelea hukua kwa kasi na huongezeka na kusababisha uharibifu wa vyakula hivyo,” anasema.

Mwanahabari Tukuswiga Mwaisumbe (kulia) akipiga vigelegele baada ya kumaliza kupanda mti wa ukumbusho wa kikundi cha Mzinga Green Voices.


Uwepo wa teknolojia hiyo utaongeza kasi ya uzalishaji wa mboga mboga, mazao ambayo yanazalishwa kwa wingi nchini China ambapo kwa mwaka 2015 pekee nchi hiyo ilizalisha takriban tani milioni 580, ambapo inauza nchi za nje.

“Ukaushaji na usindikaji wa mboga ni biashara nzuri kwa akinamama na jamii kwa ujumla, unaweza kuongeza pato la taifa kwa sababu ikiwa akinamama hawa watapatiwa nyenzo za kutosha kwa kuongezewa mtaji na kupanua kiwanda, wanaweza wakauza mboga kavu hata nje ya nchi,” anasema Mohammed Omar Mwalimu maarufu kama Chamuzhimu, ambaye ni Ofisa Mifugo na Uvuvi wa Manispaa ya Morogoro.

Chamuzhimu anawashauri akinamama hao kupanua mashamba yao, lakini pia waanzishe na miradi ya ufugaji wa kuku na samaki, kwani mabaki ya mboga mboga ni chakula bora kwa kuku na samaki.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, ambaye muda mfupi baada ya mwandishi wa Makala haya kufanya naye mahojiano akateuliwa na Rais John Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, anasema kwamba ili kupambana na mfumo dume pamoja na kuongeza kipato kupitia ujasiriamali, ni lazima wajifunze.

Anasema Halmashauri ya Manispaa imewajengea jengo maalum akinamama, ambapo watafundishwa ujasiriamali pamoja na kuendesha shughuli zao.

“Nawapongeza akinamama wa Mazinga ambao kwa kweli wanaleta mapinduzi katika suala zima la ukaushaji na uhifadhi wa mboga, lakini naona changamoto kubwa ni usindikaji (packaging), soko lipo kubwa,” anasema.

Katika mahojiano hayo, Bi. Mahongo alisema kwamba serikali imejizatiti katika kuwawezesha wanawake katika shughuli za maendeleo na akawataka wajitokeze kila wakati kushiriki maonyesho mbalimbali ya bidhaa za kilimo.
Ukaushaji wa mboga mboga unakwenda sambamba na ukaushaji pia wa ndizi, ambazo zinaongezeka ubora katika mnyororo wa thamani. Hili ni shamba mojawapo la mwanakijiji wa Konga, Mzinga katika Manispaa ya Morogoro.

MBUNGE WA JIMBO LA MAGOMENI ZANZIBAR ASHIRIKI UJENZI WA TENKI LA MAJI KATIKA JIMBO LAKE

$
0
0

Mbunge wa Magomeni Jamal Kassim Ali akiponda zege katika ujenzi wa ujenzi wa mnara wa Tenki la maji uliopo Maskani ya Kula Jiwe Sogea, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake za upatikanaji wa Maji safai na salama katika Jimbo hilo.

Mbunge wa Jimbo la Magomeni Jamal Kassim Ali (alievaa Shati la kijani) akishiriki ujenzi wa Mnara wa Tenki la maji katika eneo la Sogea Jimbo la Magomeni Zanzibar ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake za upatikanaji wa Maji safai na salama katika Jimbo hilo.

Jioni yake Mbunge wa Jimbo la Magomeni Jamal Kassim Ali alitoa jezi kwa Tim 18 za mpira wa miguu na Netbol katika Jimbo hilo, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake. Picha zote na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

Na Maryam Kidiko –Husna Sheha / Maelezo Zanzibar.

Mbunge wa Jimbo la Magomeni Jamal Kassim Ally amesema changamoto kubwa iliyokuwa inakabili jimbo hilo zimeaanza kupata ufumbuzi katika kila shehia ndani ya jimbo .

Ameyasema hayo katika ujenzi wa mnara wa maji ndani ya shehia ya sogea jimbo la magomeni wilaya ya mjini unguja amesema ujenzi huo ni miongoni mwa ahadi walizozitoa kwa wananchi wakati wa kampeni . Amesema changamoto ya maji ilikuwepo kwa muda mrefu katika shehiya ya sogea jambo ambalo lilikuwa likirejesha nyuma maendeleo ya shehia hiyo.

“Tumechukuwa juhudi kubwa na viongozi wenzangu kuanzia madiwani na muwakilishi ili kuona suala hili linakamilika haraka “ Alisema Jamal. Aidha amesema wameanzisha mradi wa visima vya maji sita katika jimbo hilo ili kuweza kupunguza tatizo la ukosefu wa maji ambalo ni muhimu kwa binaadam kuweza kupata huduma hiyo.

Hata hivyo ametowa fursa kwa wananchi wa shehia hiyo kuweka kamati ya visima ili iweze kusimamia katika mambo mbali mbali yatayovikabili visima hivyo. Vile vile amefahamisha kuwa visima hivyo vya wananchi wote hivyo kila mwananchi anahaki ya kutumia na kuvitunza visima hivyo bila ya kufanya uharibifu .

Pia amewaomba viongozi watakaochaguliwa kusimamia visima hivyo kuwa na hekma pamoja na busara ili kuweza kuepusha migogoro kwa wananchi wataopata huduma hiyo. Sambamba na hayo amewataka wananchi wa jimbo la magomeni mradi huo utapokamilika waweze kutoa michango ili kusaidia umeme ambao ndio utaweza kupatikana kwa huduma hiyo.

Nae Ramadhan Mwadini mzee ambae ni miongoni mwa wa nanchi wa shehia ya sogea jimbo la magomeni amempongeza mbunge wa jimbo hilo kwa kuitimiza ahadi aliyoiahidi wakati wa kampeni. Amewataka viongozi wao wa jimbo kuendelea kutimiza ahadi mbali mbali walizozitoa ili kuweza kuleta maendeleo katika jimbo lao .

Jumla ya visima vinne vimeshachibwa kati ya visima sita katika jimbo hilo na kila kisima kimegharimu shilingi milioni saba na laki tano.

KAMPUNI YA TANZANIA DISTILLERIES YAZINDUA MVINYO WA DODOMA ROSE.

$
0
0


Meneja Bidhaa wa Dodoma Wine Warda Kimaro akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mvinyo mpya wa Dodoma Rose. Uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mtaalam wa kutengeza mvinyo wa Dodoma Rose Erick Schlunz akiwaelezea wageni waalikwa sifa na ladha ya mvinyo huo mpya uliozinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Cheers: Wageni waalikwa wakigonganisha glasi kufurahia uzinduzi wa mvinyo mpya wa Dodoma Rose. Uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meneja Bidhaa wa Dodoma Wine Warda Kimaro (kulia) akipita kugonganisha glasi na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa mvinyo mpya wa Dodoma Rose. Uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Meneja Bidhaa wa Dodoma Wine Warda Kimaro (wa pili kulia) akiwamiminia wageni waalikwa mvinyo mpya wa Dodoma Rose wakati wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


KAMPUNI YA TANZANIA DISTILLERIES YAZINDUA MVINYO WA DODOMA ROSE.

Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) kupitia bidhaa yake ya Dodoma Wine mwishoni mwa wiki imezindua mvinyo mpya uitwao' Dodoma Rose Wine '. Dodoma Rose ni mvinyo wenye rangi ya pink na rahisi kunywa huku ukiwa na harafu ya kuvutia ya ‘candy floss na ‘raspberry. Mvinyo huu ni unakuwa bora pale unapotumika ukiwa kwenye nyuzi 10 na ukitumia chakula chenye mwanga kidogo. Dodoma Rose inapatikana Tanzania nzima katika ujazo wa 750 ml kwa bei ya rejareja ya Tshs 10,000:00. 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja Bidhaa wa Dodoma Wine, Bi Warda Kimaro, alisema, "Dodoma Wine imekuja na kauli mbiu ya Onjeni ladha tofauti! Ladha tofauti si tu ya kile cha kipekee kutoka Dodoma Wine lakini pia ni wito kwa ajili ya walaji kujaribu bidhaa tofauti za Dodoma Wine na kuchangua ipi ambayo ni bora kwao. Dodoma Wine kwa sasa inapatikana katika vinywaji nne tofauti vya kipekee na vya kufurahisha; Dodoma Dry Red Wine, Dodoma Dry White Wine, Dodoma Natural Sweet Wine & leo tumezindua Dodoma Rose Wine. Dodoma Wine si tu mvinyo ambao unakidhi viwango vya Kimataifa pekee, lakini ni mvinyo wa Tanzania kuwa inatambua urithi wake ".

Bi Warda alielezea zaidi kuwa, mbali na Dodoma kuwa mji mkuu wa nchi yetu; lakini pia ndio nyumbani kwa mivinyo ya Tanzania kwa kuzalisha mvinyo wa pili mkubwa katika Afrika kusini mwa Sahara, kwa hivyo kanda hii inastahili kuwa na mvinyo wenye jina lake na ndio sababu ikaitwa Dodoma Wine kuonyesha mizizi yake na kutambua urithi wetu. Dodoma Wine ilizinduliwa 2010 Na inatengezwa kutoka kwa zabibu bora kabisa zinazolimwa na wakulima wetu wa Tanzania na hivyo kufanya kuwa kinywaji laini na tamu.

Akiongea zaidi jinsi kampuni ya TDL inavyounga mkono wakulima wa zabibu, Mkurungenzi Mtendaji wa TDL Devis Deogratius alisema, ‘Wakulima wa zabibu walikuwa na hali ngumu hapo zamani lakini kupitia miradi tumeweza kuwainua wakulima sio tu kuwapa soko la uhakika pekee, lakini pia kwa kuwapa ujuzi wa kulima zabibu kupitia mtaalamu wetu wa kutengeneza kinywaji cha Dodoma Wine Erik Schlunz, ambaye leo tuko naye hapa’.

Mtengenezaji wa kinywaji cha Dodoma Wine Erik Schlunz alipata nafasi ya kuwatembeza wangeni waalikwa na kuwapa uzoefu wa kuonja mvinyo mbali mbali ya Dodoma Wine.

Devis alimalizia kwa kuwaomba wateja kuijaribu mvinyo wa Dodoma Wine, na sana sana wakati kampeni ambazo zitakuwa zikifanyika kwenye baadhi ya bar na supermarket jijini Dar es Salaam ili kuweza kutambua ni mvinyo ngani unaowafaa. Aliongezea kuwa uzinduzi huu wa Dodoma Rose Wine ni uthibitisho wa Mafanikio yanayotokana na mvinyo wa Tanzania pamoja na wakulima wa zabibu.

RC MAKONDA AZINDUA KAMPUNI YA NAS-DAR AIRCO JIJINI DAR

$
0
0

Katika kipindi ambacho Tanzania inaendelea kukua kwa kasi kiuchumi na hivyo kuwepo kwa wageni wengi ambao wamekuwa wakiwasili nchini, kampuni ya Mwanza Ground Handling Company (AIRCO) imeungana na kampuni nyingine ya National Aviation Services (NAS) ili kutoa huduma katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere kwa kuboresha huduma zinazotumia usafiri wa anga kwa kuhudumia abiria, ndege na shughuli za mizigo.

Akizungumzia ushirikiano huo ambao umewezesha kupatikana kampuni ya NAS-DAR AIRCO, Mwenyekiti wa NAS-DAR AIRCO, Salim Ajib alisema NAS na AIRCO zimeungana kwa pamoja ili kuboresha huduma ambazo zinatolewa kwa abiria ambao wanatumia usafiri wa ndege.

Alisema wamejipanga kutoa huduma bora ambazo zitaisaidia Tanzania kupokea wageni wengi zaidi ambao kwa namna moja au nyingine itasaidia kukuza uchumi wa nchi lakini pamoja na hilo ushirikiano huo umekuja na neema kwa watanzania kwa kupata ajira na ambapo kwa kuanza wameajiri wafanyakazi 60.
Mwenyekiti wa NAS-DAR AIRCO, Salim Ajib akizungumza kuhusu kampuni ya NAS-DAR AIRCO ambayo itakuwa ikifanya kazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere. (Picha zote na Rabi Hume, Mo Blog)

"Tunajua kuna changamoto na sisi tupo tayari kuingia katika ushindani huo kwa kuwapa wateja huduma bora ... tunafahamu Tanzania inakua kwa sasa na huduma zetu tunatumai kusaidia ukuaji wa uchumi kupitia huduma zetu wa abiria wanaotumia uwanja wa Mwalimu Nyerere,

"Tumetoa nafasi za kazi kwa watu 60 na tumewapa mafunzo kwa ajili ya kuanza kazi hivi karibuni na baadae tutaongeza wengine sababu tutakuwa na huduma nyingi ambazo tutakuwa tunazitoa," alisema Ajib.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampuni ya NAS-DAR AIRCO, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiikaribisha kampuni hiyo katika mkoa wake kwa ajili ya kutoa huduma kwa abiria wa usafiri wa anga.

Kwa upande wa mgeni rasmi katika halfa hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliwakaribisha NAS-DAR AIRCO kutoa huduma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere na kutoa angalizo kwa kampuni ya Swissport kuwa iwe makini kwa sababu sasa wamepata mshindani.

"Mji wetu bado unakua na tunazidi kuongezeka kama nyie mkitoa huduma nzuri hata wageni wataongezeka na wengine watakuja hata kuwekeza kabisa niwakaribishe nchini lakini pia nitume salamu kwa Swissport kama walikuwa wanafanya kazi na kuna sehemu wanajikwaa sasa wamepata jirani," alisema Makonda.

Makonda alisema ujio wao wa kufanyakazi nchi uwe na mfumo mpya ili kuboresha huduma kwani kwa sasa kumekuwepo na taarifa za abiria wengine wanaofika nchini kupoteza mizigo yao na hivyo kuanza kupoteza imani kama kiwanja hicho kinakuwa salama kwa kukitumia pindi wanapowasili au kuondoka nchini.


Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Kampuni ya NAS-DAR AIRCO, David Handerson akielezea jinsi ambavyo kampuni yao imejipanga kutoa huduma bora nchini.






Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya NAS-DAR AIRCO wakionyesha mavazi ambayo watakuwa wakiyatumia muda wa kazi.

























Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mwenyekiti wa NAS-DAR AIRCO wakifanya uzinduzi wa NAS-DAR AIRCO nchini.













Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mwenyekiti wa NAS-DAR AIRCO wakipongezana baada ya kufanya uzinduzi.



Mgeni rasmi,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa NAS-DAR AIRCO.



Baadhi ya watu waliohudhuria halfa ya uzinduzi wa NAS-DAR AIRCO.


















Bendi ikitoa burudani baada ya uzinduzi kufanyika.

WANAHABARI JIJINI MWANZA WAMLILIA MAREHEMU MWALIMU SOKORO, ALIEKUWA MHARIRI WA BARMEDAS TV.

$
0
0
Aliekuwa Mhariri wa miaka mingi wa Barmedas Tv ya Jijini Mwanza, Mwalimu Charles Sokoro, enzi za uhai wake. Marehemu Sokoro alifariki dunia jumamosi julai 16,2016 majira ya saa mbili usiku katika hospitali ya Rufaa Bugando alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.

Kifo chake kimesababisha majonzi makubwa kwa ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo waandishi wa habari Jijini Mwanza ambao baadhi yao walipitia mikono ya Sokoro aliefahamika kwa jina maarufu la Mwalimu kutokana na ujuzi wake katika kufundisha nyimbo za Injili na ubobeaji wake katika taaluma ya habari.

Enzi za uhai wake alikuwa Mwalimu wa kwanza wa Kwaya ya AICT Makongoro waliowahi kutamba na wimbo wa Kekundu huku pia akiwa miongoni mwa wafanyakazi wa kwanza katika kituo cha luninga cha Barmedas Tv Cable ambayo awali ilikuwa ikipatikana kwa njia ya cable tu kabla ya hivi karibuni kupatikana katika ving'amuzi mbalimbali.

Mwalimu Charles Sokoro alizaliwa mwaka 1965 na mauti yamemfika mwaka huu 2016 akiwa na miaka 51. Ratiba ya Mazishi ni kama ifuatavyo;

1.Siku ya Jumatatu (18/7/2016 ) saa 10:00 jioni, Mwili wa Marehemu kuwasili kutoka hospitalini Bugando kuelekea Kanisa La AICT Makongoro


2.Siku ya Jumanne (19/7/2016) Kanisa La AICT Makongororo
~Saa 6:00 mchana IBADA ya Kumuaga Mareemu
~Saa 7:30 mchana Safari ya kuelekea Malaloni (Makaburini Kitangiri)
~Saa 8:30 Chakula na baadaye kuhitimisho.
Wanahabari Jijini Mwanza wakieleza namna walivyomfahamu Mwalimu Sokoro enzi za uhai wake.

Ni juzi tu Tasnia ya Habari ilipata pigo kwa kumpoteza Mwandishi mbobezi kwenye dimba la michenzo Dada yetu mpendwa Elizabert, na leo tasnia hiyo hiyo imekubwa na msiba mwingine wa kaka yetu sokoro. HAKIKA msiba wa ndugu yetu Sokoro umetuacha midomo wazi tunahisi km ni ndoto ya usiku lakini ndio ukweli.

Nani asiye mjua sokoro kwa ukarimu wake kwa kila mtu ? Kiukweli alikuwa mcheshi asiye na makuu.

Aliipenda taaluma yake kwa dhati na kila penye kusanyiko la wanahabari naye alimuwepo.

Hakuonyesha umahiri pekee kwenye tasnia ya habari bali hata kwenye mambo mengine. Nani asiyejua uwezo wake.kwenye kupiga kinanda?.

Nani asiyejua umahiri wake kwenye kuenzi utamaduni wa kiafrika?

Kipindi chake cha ngoma asilia pale Barmedas kilileta uhalisia wa utamaduni wetu. Sokoro waandishi wenzako tunakulilia umetuacha kwenye wakati mgumu.

Tutakukumbuka daima tulikuoenda lakini Mungu kakupenda zaidi na alikuita na umeitika leo haupo nasi. Huu ni wakati mgumu sana kwa tasnia ya habari. Mungu tupe nguvu tumpumzishe mwenzetu kwa mikono yetu miwili.
AMINA!
NAEDWIN SOKO;

MRATIBU, CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MWANZA (MPC).

HIVI NDIVYO MAHARAMIA WA KAZI FEKI ZA WASANII WANAVYOIKOSESHA SERIKALI MAPATO KWA KUSHIRIKIANA NA BAADHI YA MAOFISA WA TRA WASIO WAAMINIFU

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama Action Mart ,Alex Msama pichani kushoto akionesha stika halisi za TRA zinazotumika kuwekwa kwenye bidhaa mbalimbali zikiwemo kazi za wasanii wa Filamu na muziki na kulia akionesha CD ya Muimbaji wa nyimbo za injili Boniphace Mwaitege ambayo ni "FEKI" lakini imebandikwa stika halisi za TRA.
Kufuatia kadhia hiyo,Msama ameeleza kuwa kumekuwepo na baadhi ya Maofisa wa TRA wasio waaminifu wakitumika kuhujumua Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuzitoa stika hizo halisi za mamlaka hiyo na kuwauzia maharamia wanaouza kazi feki za Wasanii zikiwemo pia na bidhaa mbalimbali hapa nchini,hali inayopelekea Maharamia hao kukwepa kodi ya Serikali sambamba na Wasanii wetu wakiendelea kuwa masikini wa kutupwa.
Msama amebainisha kuwa kufuatia uchunguzi wao walioufanya na kubaini hujuma hizo za kuidhoofisha Serikali kwa kukosa mapato yake, watachukua hatua ya kuufikisha uchunguzi huo kwa mamlaka husika,ili waliohusika kwa namna moja ama nyingine wachukuliwe hatua kali .

Msama amempongeza Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye kwa kazi aliyoifanya kutoka ofisini kwake na kuenda kwenye maduka mbalimbali yaliyopo katikati ya jiji Kariakoo kwa ajili ya kusaka na kubaini wezi wa kazi feki za wasanii,ambapo katika operesheni hiyo Mh Nape alifanikiwa kuyafunga maduka zaidi ya 40 yaliyokuwa yakidaiwa kuuza kazi feki ikiwemo na suala zima la kukwepa kopi.

Amesema Jambo hilo limemtia moyo kama mpigania haki wa kazi za wasanii ambaye amekuwa akipambana kila siku ili wasanii waweze kufaidika na jasho lao na ataendelea na kazi ya kuhakikisha wezi wote wa kazi za sanaa wanashughulikiwa kisheria na kuwafanya wasanii nao wanafaidi jasho la mikono yao.
Baadhi ya Vielelezo hivyo zikiwemo stika halisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),pamoja na CD Feki lakini imebandikwa stika za mamlaka hiyo.

WAZIRI MBARAWA AKAGUA MRADI WA BARABARA YA MBINGA-MBAMBABAY KM 66 NA BANDARI YA MBAMBABAY

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kuanza ujenzi wa maegesho ya meli katika bandari ambazo meli mbili mpya zinazojengwa na Mamlaka hiyo katika bandari ya Itungi Wilayani Kyela, zitatoa huduma ya usafiri baada ya kukamilika.

Waziri Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo alipokagua bandari ya Mbambabay iliyopo Wilayani Nyasa ambayo ni miongoni mwa bandari ambazo meli hizo zitatoa huduma na kubaini kuwa bado bandari hiyo haina maegesho kwa ajili ya meli hizo.“Nataka kuona maegesho ya meli yanakamilika haraka ili kuwezesha meli mpya kupakua na kupakia mizigo katika bandari hii”, amesema Waziri Prof Mbarawa.

Ameeleza kuwa meli hizo mbili za mizigo ambazo zinatarajiwa kukamilika mwezi Agosti na Oktoba zitaongeza kasi ya utoaji wa huduma katika bandari hiyo na kuwa chachu ya maendeleo hususan katika shughuli za biashara na kiuchumi katika mkoa wa Ruvuma na nchi jirani.

Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amemtaka Meneja wa Bandari ya Kyela kuisimamia kampuni ya M/s Songoro Marine Transport Boart Yard inayojenga meli hizo ili zijengwe kwa ubora na viwango vinavyotakiwa kulingana na thamani ya fedha ambazo zinatokana na kodi za wananchi.Katika Hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua barabara ya Mbinga-Mbambabay yenye urefu wa Km 66 ambayo Serikali iko katika hatua ya kumtafuta mkandarasi atakayejenga kwa kiwango cha lami.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) akiongea jambo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Binilith Mahenge (wa pili kushoto) wakati alipokagua uwanja wa Songea Mkoani Ruvuma. Muonekano wa uwanja wa ndege wa Songea Mkoa ni Ruvuma, ambao uko kwenye mradi wa upanuzi wa viwanja kumi na moja.
Waziri wa Ujenzi, Uchuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tano kushoto) akitoa maelekezo kwa Meneja wa kiwanja cha ndege cha Songea, Valentine Fasha (wan ne kulia) wakati alipokagua barabara ya kutua na kuruka ndege katika uwanja huo Mkoani Ruvuma. Muonekano wa Barabara ya Mbinga-Mbambabay KM 66 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha Lami unatarajiwa kuanza hivi karibuni. Kukamilika kwa barabara hiyo kutachochea uchumi wa Mkoa wa Ruvuma kupitia bandari ya Mbambabay.
Waziri wa Ujenzi, Uchuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa(kulia) akiteta Jambo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakati alipomtembelea ofisini kwake.
Meneja wa Bandari ya Kyela, Percival Salama (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) ya namna shughuli za biashara ya makaa ya Mawe zinavyoweza kuongeza pato kwa bandari ya Bambabay Mkoani Ruvuma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kulia) akisalimiana na baadhi ya Madereva wa Malori wanaosafirisha makaa ya mawe Mkoani Ruvuma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na watendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo, Mkoani Ruvuma.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutaimarisha huduma ya bandari ya Mbambabay na kupunguza adha ya usafiri kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa Ruvuma Eng. Lazeck Alinanuswe amesema kuwa kwa sasa wakala unakamilisha zoezi la kulipa fidia kwa wananchi waliopo katika hifadhi ya barabara wakati hatua za mwisho za kuanza ujenzi wa zinakamilishwa.

Naye Meneja wa Bandari ya Kyela Percival Salama amemueleza Waziri kuwa pamoja na changamoto ya kukosa wa chombo cha usafiri majini kinachotoa huduma katika bandari hiyo pia ameomba kuboresha huduma za miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami ili kuwezesha ufanisi wa bandari.“Kuimarika kwa barabara ya mbinga-mbambabay na barabara nyingine za maingiliano katika bandari hii kutaongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuongeza fursa za uwekezaji na biashara na Mkoa na nchi jirani”,

Waziri Prof. akame Mbarawa, yuko katika ziara ya Kikazi Mkoani Ruvuma kukagua miradi ya Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

KILIMO CHA UYOGA DAR CHAWAVUTIA WAHISPANIA

$
0
0

Bi. Sophia Chove, Mwenyekiti wa kikundi cha Tunza Women cha Bunju jijini Dar es Salaam, akiwaelekeza wageni namna ya kuandaa mahitaji mbalimbali ya kilimo cha uyoga.

“SIJAWAHI kuvuna uyoga katika maisha yangu, achilia mbali kushuhudia namna unavyolimwa,” anasema Anna Salado, Mkurugenzi wa taasisi ya Mfuko wa Wanawake wa Afrika (WAF) kutoka Hispania, wakati akikwanyua kikonyo cha uyoga katika shamba la akinamama wa kikundi cha Tunza Women Group, Bunju jijini Dar es Salaam.

Anaongeza: “Kwa hakika ninyi wanawake mmefanya jambo kubwa na muhimu katika jamii, kwa sababu mbali ya kufanikiwa kulisha familia zenu, lakini sasa mtaweza kuongeza kipato kwa kuwauzia wengine zao hili.”Akiwa ameongozana na maofisa wengine wa taasisi hiyo Alicia ambaye ni mratibu na Noelia ambaye ni mkurugenzi wa miradi, Anna Salado anasema kwamba, wamehamasika sana na kilimo hicho na katika kuunga mkono juhudi za akinamama hao watawasaidia kutatua changamoto zinazowakabili pamoja na kuwawezesha kupanua mradi wao.

Mradi huo wa kilimo cha uyoga ni sehemu ya utekelezaji wa mradi mama wa Green Voices nchini Tanzania unaofadhiliwa na taasisi ya Mfuko wa Wanawake wa Afrika, ambayo rais wake ni Mama Maria Teresa Fernandez de la Vega Sanz ambaye ni Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania.

Anna na wenzake wamekuwa wakitembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Green Voices nchini Tanzania tangu mradi huo ulipozinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Julai 11, 2016 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Uyoga ukiwa umeota vizuri ndani ya banda.

Wakati wa ziara yao kwenye mradi wa kilimo cha uyoga, viongozi hao walioambatana na Mratibu wa Green Voices Tanzania, Bi. Secelela Balisidya, walijifunza mambo mbalimbali kuanzia utaarishaji wa shamba, upandaji, uvunaji pamoja na namna ya kufungasha huku pia wakielekezwa mapishi ya uyoga.“Tunakunywa supu kwenye mahoteli, tunauona tu kwenye picha, lakini leo tumeweza kuuona namna unavyolimwa, tena tumeonja mapishi mengine tofauti,” alisema Anna Salado baada ya kula uyoga ulioungwa kwa nazi.

Mratibu wa mradi wa Green Voices kutoka Hispania, Bi. Alicia akizungumza na washiriki wa mradi huo, alisema kwamba mradi huo ulikuwa wa majaribio, lakini sasa umewahamasisha na wako tayari kusaidia awamu ya pili ili kuwawezesha wanawake wengi wajikite kwenye kilimo hicho cha uyoga.

“Tumefarijika sana, kwa sababu ni kipindi kifupi tu tangu tulipowapa mafunzo wanawake 15 kule Madrid, lakini leo hii mmeweza kufanya mambo makubwa kama haya, hakika tuko nanyi bega kwa bega,” alisema Alicia.Mshiriki kiongozi wa mradi wa kilimo cha uyoga, Magdalena Bukuku, alisema kwamba tangu walipoanza kilimo hicho mwezi Machi, tayari wamekwishaona faida yake baada ya kuvuna na kuuza sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam.

Magdalena, ambaye yeyé na wanawake wengine 14 walipatiwa mafunzo Hispania mapema mwaka huu, amesema kwamba kutokana na wingi wa akinamama waliojitokeza, amewagawa katika makundi mawili, ambapo kimoja kipo Mtaa wa Kilungule, Bunju na kingine kipo Boko, vyote vikiwa na wanachama 10 kila kimoja.

Hata hivyo, amesema kuwagawa tu hakukuwazuia wanawake wengine kwenda kujifunza, kwani tayari wanajamii katika maeneo hayo wamekuwa wakimiminika kujifunza namna ya kuanzisha mashamba ya uyoga majumbani mwao.“Mpaka sasa nimekwishawafundisha wanawake wengine zaidi ya 50, wengine wanatoka Zanzibar, Kibaha na Bagamoyo,” alisema.

Mwenyekiti wa kikundi cha Tunza cha Bunju, Sophia Chove, anasema hivi sasa wanafikiria kuongeza shamba jingine la uyoga, ingawa changamoto ya mtaji ndiyo inayowapa shida.Anasema ili kuweza kupata faida ni muhimu kuongeza shamba hasa ikizingatiwa kwamba mahitaji ya uyoga yameongezeka katika jamii.“Wateja ni wengi sana kuliko tunachozalisha, hivyo tunaona ni vyema tukaongeza banda jingine, lakini changamoto hapa ni mtaji, tukiwezeshwa tunaweza,” anasema.

Anasema kwamba, tayari wamepata wateja wa maduka makubwa ya bidhaa (super markets) pamoja na jamii inayowazunguka, mahitaji ambayo ni makubwa kuliko uwezo wa kuzalisha.“Uyoga una faida kubwa, fikiria robo kilo ya uyoga inauzwa Shs. 2,500 wakati kilo moja ni Shs. 10,000,” anaongeza Sophia.
Mratibu wa Green Voices kutoka Hispania, Alicia, akizungumza na wanawake wakulima wa uyoga wa Bunju na Boko (hawapo pichani).

Mhazini wa kikundi hicho ambaye pia ndiye mwalimu wa ukulima wa uyoga na Ofisa Kilimo Msaidizi Mwandamizi wa Manispaa ya Kinondoni, Esther Chiombola, anasema kwamba kila wiki wamekuwa wakiwafundisha akinamama kati ya watano hadi 10 kutoka maeneo mbalimbali.

“Hapa pamekuwa kama kituo cha mafunzo, wanawake wengi wamehamasika na tunawafundisha namna ya kuanzisha kilimo hiki ambacho ni rafiki wa mazingira na kina tija kubwa kwa uchumi,” anasema Mama Chiombola.Anaongeza: “Ni mradi unaotumia gharama kidogo huku mavuno yake yakiwa endelevu, hapa Bunju tayari akinamama wameanza kuvuna.”

Miradi mingine ya Green Voices inatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Mwanza, Kigoma na Kilimanjaro ambayo yote inaendana na mkakati wa mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, miradi hiyo ya Green Voices nchini inalenga pia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 pamoja na Malengo Endelevu ya Dunia katika kuondoa umaskini, kuongeza ajira, kuwawezesha wanawake kiuchumi, kuhakikisha usalama wa chakula pamoja na kupambana na uharibifu wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mambo ya msosi, na kuna rosti la uyoga hapo.
Noellia (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa mwakilishi wa wakulima wa uyoga wa Bunju na Boko jijini Dar es Salaam.


Anna Salado, Mkurugenzi wa taasisi ya Women for Africa Foundation kutoka Hispania, akiwa na uyoga aliouvuna. 

Bayport Financial Services yachangia ujenzi shule ya sekondari Lindi

$
0
0

Meneja wa Bayport Financial Services, Tawi la Lindi, Lovin Mapunda, mwenye fulana juu ya jukwa, akitoa msaada wa Sh Milioni mbili katika harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari Lindi iliyoungua, ambapo harambee hiyo iliongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, wa pili kutoka kushoto mstari wa mbele, akifuatilia jambo wakati Meneja wa Bayport Financial Services, taasisi inayojihusisha na mikopo, tawi la Lindi, Lovin Mapunda, hayupo pichani wakati anatoa jumla ya sh Milioni mbili kwa ajili ya mchango wa taasisi yake kwa shule ya Sekondari Lindi, iliyopata balaa la kuungua kwa baadhi ya majengo yake. Picha na Mpiga Picha Wetu, Lindi.

WATANZANIA WAENDELEA KUTOA USHUHUDA JINSI PROMOSHENI YA TUSKER ILIVYOBADILI MAISHA YAO

$
0
0

Mmoja wa washindi wa Tusker milionea Albert Tarimo (kulia) akijadiliana jambo na fundi wa matofali Emmanuel Mboya (kushoto) ambayo aliyonunua kwa kutumia Milioni moja aliyoipata kutoka promosheni Tusker .
Meneja wa Bia ya Tusker Jasper Migambile(kushoto) akiongea kwa njia ya simu na mmoja wa washindi walioshinda katika droo ya nane ya promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini, kushoto kwake ni afisa kutoka Bodi ya michezo ya kubahatishanchini Mrisho Millao akihakiki taarifa za mshindi.

Ikiwa imebaki wiki moja tu kukamilisha wiki kumi za promosheni ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini, mwishoni mwa wiki ilichezeshwa droo ya nane ya promosheni hiyo huku washindi wengine kumi kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wakitangazwa kujishindia vitita vya shilingi Milioni moja kila mmoja. 


Hii inafanya idadi ya washindi kufikia 90 tangu promosheni hiyo ianze wiki tisa zilizopita. Droo hiyo iliyofanyika katika studio za ITV na kushuhudiwa na wakaguzi wa wahesabu na Maofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini kuhakikisha droo imechezeshwa kwa kufata taratibu na masharti elekezi yaliyowekwa.

Washindi wa droo ya 8 ya Tusker Fanya Kweli Uwini ni :- God Muingi na Yohana Shirima kutoka Morogoro, Boniface Masanja na Selestin Simon kutoka Mwanza, Evarist Simwita kutoka Kilimanjaro, Obwor Nyambade kutoka Arusha, Rose Moses, Juliana Petro, Innocent Kiwango na Ally Mkemi kutoka Dar es Salaam.

“Tayari tumeshatoa 90,000,000 kwa watanzania na watumiaji wa bia ya Tusker, ni Milioni kumi tu ndo imebaki kwaajili yako wewe mteja wetu ili kukamilisha Milioni 100 tulizokusudia kutoa kwa wateja wetu. Ni furaha kubwa kwetu kuona wateja wengi wakiendelea kuwa na shauku ya kushiriki lakini wasife moyokwani bado tutaendelea kuwapa zawadi kibao zikiwemo bia za bure. Je ni kina nani watatukamilishia kumi ya mwisho?” alieleza kwa msisitizo Meneja wa Bia ya Tusker Jasper Migambile 

Pia aliongeza kuwa Kampuni ya Bia ya Serengeti bado ina vitu viruri zaidi vinakuja kwa wateja wake kwani kuelekea ukingoni mwa mwa promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini ni maandalizi ya kitu kinginekizuri zaidi. “Kila wakati tunawaza mambo mazuri kwa wateja wetu siku zote make mkao wa kula.” Aliongeza Jasper.Alisisitiza kuwa watanzania kuendelea kushiriki katika wiki hii ya mwisho mara nyingi kadiri wawezavyo ili waweze kuwa na nafasi za kushinda zaidi. 

Promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwili ipo katika mfumo wa kuwazawadia wateja na watumiaji wa bia ya Tusker yenye lengo la kubadilisha maisha ya wateja wa Tusker katika njia tofauti. Wiki chache zilizopita Albert Tarimo alishinda Tsh 1,00,000 ambayo aliitumia kununulia tofalikwaajili ya kujengea nyumba yake katika kiwanja alichokua nacho muda mrefu lakini hakuweza kukiendeleza. Albert ambaye ni meneja wa baa amekiri kuwa maisha yake yamebadilika kupitia promosheni hiyo.

“Niliposhinda Milioni moja, moja kwa moja niliwaza kufanya kitu ambacho kitakua kinamanufaa kwangu na familia yangu. Tayari nilikua na kijisehemu changu nikaona chamsingi ninunue matofali ili nianze ujenzi taratibu. Mwanzo sikujua wapi naweza pata pesa za kununulia vifaa vya ujenzi wala hata namna ya kuanza msingi wa nyumba, lakini leo Tusker imeniwezesha nimenunua tofali 1000 ntakazotumia kuanza ujenzi hivi karibuni.

‘Tusker Fanya Kweli Uwini’ ni promosheni iliyoanza takribani wiki nane zilizopita mikoa yote nchini. Wiki moja tu imesalia kukamilisha washindi 100 wa promosheni hiyo.

KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI AIPONGEZA TIMU YA UCHUKUZI KWA KUIBUKA MSHINDI MASHINDANO YA MEI MOSI

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leornard Chamuriho kulia akopokea moja baadhi ya vikombe 11 ambavyo timu ya uchukuzi imeshinda katika mashindano ya mei mosi yaliyofanyika mapema mwezi mei mkoani Dodoma, anayemkabidhi ni Katibu wa Uchukuzi Sports Club Bw. Alex Temba.(Picha na Benjamin Sawe- Maelezo)
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leornard Chamuriho kulia akipokea cheti cha ushiriki wa mashindano ya mei mosi yaliyofanyika mpema mwezi mei mkoani Dodoma, anayemkabidhi ni Katibu wa Uchukuzi Sports Club Bw. Alex Temba
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leornard Chamuriho kulia akipokea zawadi ya jezi kutoka kwa Katibu wa Uchukuzi Sports Club Bw. Bw. Alex Temba mara baada ya kupokea vikombe 11 ambavyo timu ya uchukuzi imeshinda katika mashindano ya mei mosi yaliyofanyika mpema mwezi mei mkoani Dodoma, kati ya hivyo vikombe 5 vilitolewa na Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli vikiwa ni ushindi wa kwanza katika netball Kamba,Baiskeli na Bao
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leornard Chamuriho aliyeshika Kikombe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wachezaji wa timu ya Uchukuzi Sports Club mara ya kupokea vikombe na vyeti vya ushindi wa timu hiyo katika mashindano ya mei mosi yaliyofanyika mapema mwezi mei mkoani Dodoma.

SERIKALI YATOA MSIMAMO WAKE KUHUSU BENKI YA TWIGA BANCORP

$
0
0
 Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu msimamo wa Serikali kuhusu Benki ya Twiga Bancorp. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Cosmas Kimario na Mkurugenzi  Rasilimali Watu na Utawala, Amina Lumuli.
 Maofisa wa Benki hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.

MSAJILI wa Hazina Ndugu Lawrence Mafuru ametolea ufafanuzi taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari kuhusu msimamo wa Serikali kwa Benki ya Twigabancorp.

Taarifa hiyo ilieleweka vibaya kuhusu msimamo wa Serikali kwa benki hii ya  Twiga Bancorp. Naomba nieleze kwamba kwa hivi sasa Serikali inasubiri mapendekezo ya kitaalamu yatakayowezesha kutatua changamoto za kimtaji za Twiga Bancorp. 

Ninaposema changamoto za kimtaji sijasema kwamba benki hiyi ipo kwenye hali mbaya ya kushindwa kujiendesha, ila inahitaji nyongeza ya mtaji kwa ajili ya kutekeleza matakwa ya kisheria na vilevile kuimarisha na kusambaza  huduma mbalimbali katika maeneo ya nchi. Hatua hizo zinafuatia agizo la Mheshimiwa Rais kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipangokufuatilia utendaji wa benki ya Twiga Bancorp na kuhakikisha kasoro zilizopo zinatatuliwa.

“Kuna njia mbalilimbali za kuiwezesha benki kupata mtaji ikiwemo nje ya utaratibu wa Serikali, ndiyo maanaWizara na Ofisi ya Msajili wa Hazina ikishirikiana na Manejiment ya Twiga Bancorp zinaandaa mapendekezo yatakayoiwezesha Benki hii kupata mtaji ili kuiwezeshakutimiza malengo yake ya kiukuaji na kujiendesha kwa faida.”

Hatua mbalimbali zilianza kuchukuliwa na Wizara ya Fedhana Mipango na ofisi ya Msajili wa Hazina kwa ajili ya kuboresha utendaji wa Benki ya Twiga Bancorp. Kwa mfano, mnamo mwaka 2015, Muundo wa Shirika ulibadilishwa ambao pamoja na mambo mengine ulipelekea kuteuliwa kwa Menejimenti mpya, kwa kupitia Menejimenti hiyo mpya  umetengenezwa Mpango Mkakati wa miaka mitano ambao umeanza kutumika Januari 2016, serikali pia ilifanya mabadiliko katika bodi ya wakurugenzi kwa kuteuaBodi mpya ya Wakurugenzi. 

Kwa ujumla kuna mabadiliko makubwa ya kiutendaji baada ya hatua hizo kuchukuliwa. Kwa mfano benki imeweza kupata Hati Safi ya Mahesabu (Unqualified Opinion) kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Heasabu za  Serikali kwa mara ya kwanza kwenye hesabu zake za mwaka 2015 jambo ambalo halikuwezekana toka Mwaka 2011. 

“Hizi taarifa zinazosambaa kuwa benki inafungwa sio za kweli. Kwenye benki kuna pesa za wananchi, kuna mikopo iliyotolewa kwa watu mbalimbali, kuna rasilimali za benki ikiwemo rasilimmali watu. Yote hayo yana Utaratibu wake wa kuyasimamia.. Hata ukisikiliza hotuba ya Rais hakusema funga benki ya Twiga Bancorp aliagiza hatua zichukuliwe na kwamba Katibu Mkuu asimamie.” 

Hivyo tuna wahakikishia kuwa fedha za wananchi zilizo katika benki ya Twiga Bancorp zipo salama na kwamba uongozi uliopo hivi sasa unaendelea kushughulikia changamoto za kiutendaji zilizokuwepo na kama yalivyokuwa  maagizo ya Rais hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa kwa ajili ya kuhakikisha mambo yote yanakuwa sawa. Pia benki hii inaendelea kutoa huduma zake kwa wateja kama kawaida.”

Mwisho, Serikali itaendelea kutoa msukumo kwa benki hiiili kuhakikisha tatizo lililopo sasa la mtaji linatatuliwa na kuhakikisha inajiendesha kwa faida.

Waziri Mkuu Mgeni Rasmi Kongamano la ushiriki wa watanzania katika uwekezaji.

$
0
0
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Dk.Hamis Mwinyimvua (kulia) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la siku mbili la ushiriki wa watanzania katika uwekezaji ili kuiwezesha serikali kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha waanchi wake wanashiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi yao.Kulia kwake ni Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Bengi Issa.
Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Bengi Issa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari na kuwahimiza watanzania kushiriki kikamilifu katika kongamano la siku mbili la ushiriki wa watanzania katika uwekezaji ili kuiwezesha serikali kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha waanchi wake wanashiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi yao.Picha na Daudi Manongi,MAELEZO.


Na Daudi Manongi-MAELEZO

SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeandaa kongamano kongamano la siku mbili la uwekezaji litakalojadili mipango madhubuti ya kuhakikisha Watanzania wanashiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao.

Kongamano hilo linatarajia kufanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 -22 Julai mwaka huu. Hayo yamesemwa leo Jijiji Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt.Hamis Issa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu kongamano hilo.

Dkt. Issa alisema Serikali imepitisha Sera ya ushiriki wa watanzania katika sekta ya Mafuta na Gesi asilia, hatua ambayo itasadia wananchi wazawa kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao.

“Msukumo mkubwa wa serikali kwa sasa ni kuongeza ushiriki katika uwekezaji unaochochewa na ugunduzi mkubwa wa gesi asilia katika kina kirefu cha bahari ambao utaweza kuwanufasha Watanzania” alisema Dkt. Issa.

Aidha alisema kuwa kutokana ushiriki huo wa Watanzania kuwa suala mtambuka na agenda endelevu, Serikali iliiagiza Baraza la Taifa la Uwezeshaji kuanzisha Idara ya ushiriki wa watanzania katika uwekezaji ambayo imeanza kutekeleza majukumu yake mwezi Novemba mwaka 2015.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Beng’i Issa alisema kuwa katika kongamano hilo linatarajia kushirikisha jumla ya wajumbe 350 wakiwemo wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, Watendaji wa Serikali Kuu na halmashauri za Miji na Majiji.

Akizungumzia kuhusu manufaa ya kongamano hilo, Beng’i alisema Watanzania watanufaika zaidi kwa kuwa wataongeza ujuzi na uzoefu katika kushirikiana na wafanyabiashara wakubwa waliopo nje ya nchi wanaojihusisha na sekta za mafuta, gesi, kilimo, fedha, bima, ujenzi na manunuzi ya umma.

MADIWANI WA HALMASHAURI ZA KYERWA NA BIHARAMULO WAANZA MAFUNZO YA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA PS3 MKOANI KAGERA

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Deusdedith Kinawiro akifuyngua mafunzo ya siku nne ya Madiwani kutoka Hlamashauri mbii za Kyerwa na Biharamuo juu ya namna ya utekelezaji wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za umma (PS3) chini ya ufadhili wa Serikali ya Marekali kupitia shirika ake la misaada la Kimataifa (USAID) ikishirikiana na serikali kuu.

Mradi huo ulizinduliwa Julai 12 mwaka huu ambapo Halmashauri hizo mbii ndio zitatekeeza mradi huo mkoani Kagera kwa awamu ya kwanza.Kinawiro alisema anatarajio kuona mafunzo haya elekezi yanatumika kama ilivyokusudiwa, na waheshimiwa madiwani wanapata uelewa na maarifa kuhusu uendeshaji wa Serikali za Mitaa, pamoja na wajibu na majukumu yao katika kusimamia uendeshaji wa Mamlaka hizi. 
Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Kanali (Mstaafu), Shabaan Lissu akiwa na Mkuu wa Wiaya ya Biharamulo, Saada Malunde wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya madiwani yaliyofanyika mjini Bukoba leo. 
Mwenyekiti wa Hlamashauri ya Kyerwa, Kashunju Runyogote (kushoto) akiwa na madiwani wenzake wa Kyerwa wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.

Baadhi ya Madiwani na Watendaji wa Hamashauri za Kyerwa na Biharamuo mkoani Kagera wakifuatilia ufunguzi huo.

Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images