Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 907 | 908 | (Page 909) | 910 | 911 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyopewa amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali, na pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania.
  Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;

  1.   Mhe. Augustino Lyatonga Mrema.
  ·        Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2016.

  ·        Mhe. Augustino Lyatonga Mrema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu Mhe. Eusebia Nicholaus Munuo ambaye muda wake umemalizika.

  2.   Prof. William R. Mahalu
  ·        Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.

  3.   Prof. Mohamed Janabi
  ·        Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

  4.   Prof. Angelo Mtitu Mapunda
  ·        Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

  5.   Bi. Sengiro Mulebya
  ·        Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

  6.   Bw. Oliva Joseph Mhaiki
  ·        Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

  7.   Mwl. Winifrida Gaspar Rutaindurwa
  ·        Ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

  8.   Dkt. Charles Rukiko Majinge
  ·        Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.

  9.   Dkt. Julius David Mwaiselage
  ·        Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.


  Kupandishwa Vyeo

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa 25 wa Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP).

  Waliopandishwa vyeo hivyo ni kama ifuatavyo;

  1.      Essaka Ndege Mugasa
  2.      Adamson Afwilile Mponi
  3.      Charles Ndalahwa Julius Kenyela
  4.      Richard Malika Revocatus
  5.      Geofrey Yesaya Kamwela
  6.      Lucas John Mkondya
  7.      John Mondoka Gudaba
  8.      Matanga Renatus Mbushi
  9.      Frasser Rweyemamu Kashai
  10. Ferdinand Elias Mtui
  11. Germanus Yotham Muhume
  12. Fulgence Clemence Ngonyani
  13. Modestus Gasper Lyimo
  14. Mboje John Shadrack Kanga
  15. Gabriel G.A. Njau
  16. Ahmed Zahor Msangi
  17. Anthony Jonas Rutashubulugukwa
  18. Dhahir Athuman Kidavashari
  19. Ndalo Nicholus Shihango
  20. Shaaban Mrai Hiki
  21. Simon Thomas Chillery
  22. Leonard Lwabuzara Paul
  23. Ahmada Abdalla Khamis
  24. Aziz Juma Mohamed
  25. Juma Yussuf Ally

  Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi wengine 34 kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).


  Waliopandishwa vyeo hivyo ni kama ifuatavyo;

  1.      Fortunatus Media Musilimu
  2.      Goyayi Mabula Goyayi
  3.      Gabriel Joseph Mukungu
  4.      Ally Omary Ally
  5.      Edward Selestine Bukombe
  6.      Sifael Anase Mkonyi
  7.      Naftari J. Mantamba
  8.      Onesmo Manase Lyanga
  9.      Paul Tresphory Kasabago
  10. Dadid Mshahara Hiza
  11. Robert Mayala
  12. Lazaro Benedict Mambosasa
  13. Camilius M. Wambura
  14. Mihayo Kagoro Msikhela
  15. Ramadhani Athumani Mungi
  16. Henry Mwaibambe Sikoki
  17. Renata Michael Mzinga
  18. Suzan Salome Kaganda
  19. Neema M. Mwanga
  20. Mponjoli Lotson
  21. Benedict Michael Wakulyamba
  22. Wilbroad William Mtafungwa
  23. Gemini Sebastian Mushi
  24. Peter Charles Kakamba
  25. Ramadhan Ng'anzi Hassan
  26. Christopher Cyprian Fuime
  27. Charles Philip Ulaya
  28. Gilles Bilabaye Muroto
  29. Mwamini Marco Lwantale
  30. Allute Yusufu Makita
  31. Kheriyangu Mgeni Khamis
  32. Nassor Ali Mohammed
  33. Salehe Mohamed Salehe
  34. Mohamed Sheikhan Mohamed

  Maafisa hawa wa Jeshi la Polisi Tanzania wamepandishwa vyeo kuanzia tarehe 15 Julai, 2016.


  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  16 Julai, 2016

  0 0

  Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla amewaomba wananchi wa Kijiji cha Ipala ambao wamekuwa na mgogoro wa muda mrefu na watu hifadhi ya Msitu wa Ipala kuwa na subira kwa kipindi hiki kwani tatizo lao linashughulikiwa ambapo Waziri mwenye dhamana anatarajiwa kufika kwenye kijiji hicho kwa ajili ya hatua Zaidi za kitatuzi.

  Kijiji hicho cha Ipala chenye Zaidi ya Kaya 700, Wanakijiji wake wamekuwa wakiishi huko kuanzia mwaka 1952 ambapo wameendelea kuishi humo na familia na kufanya shughuli zao za kijamii za kila siku Dk. Kigwangalla amesema kuwa, tayari Serikali suala hilo wanalitambua hivyo wanatumia njia za mazungumzo katika kutatua mgogoro huo kwa sasa wanatarajia ujio wa Waziri Mwenye dhamana kutembelea eneo hilo.

  “Matatizo yenu nayajua na Serikali pia inalifahamu suala hili muda mrefu hivyo nawaomba wananchi muwe na subira kwa kipindi hiki na mimi Mbunge wenu natarajia kurudi hapa na Mh. Waziri wa Maliasili na Utalii na atafika huku kuja kushuhudia mgogoro huu.” Alieleza Dk. Kigwangalla kwa wananchi hao huku akishangiliwa na wanakijiji hao waliofurika kwa wingi katika eneo la uwanja wa kituo cha Ipala.Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasili kwenye kijiji cha Ipala huku akipokelewa na baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo.Msululu wa wananchi wakiwa wamempokea Dk. Kigwangalla wakati akiwasili kwenye kijiji cha Ipala.Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na badhi ya wananchi wa Kijiji cha Ipala. Dk. Kigwangalla amewataka wananchi hao kuendelea kusubiria kwani tatizo hilo analitatua kwa njia ya mazungumzo na tayari Waziri mwenye dhamana amekubali kufika eneo hilo kwa ajili ya kujionea. (Picha zote na Andrew Chale,Nzega-Tabora).

  0 0

  Mwanariadha wa zamani aliyewahi kushika nafasi ya pili duniani katika mashindao ya Olimpiki nchini Ugiriki Bw. John Stephen Akhwari (wa kwanza kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (katikati) Mwenge aliyoukimbiza katika viwanjani vya Beijing nchini China wakati wa kufungua mashindano ya Olimpiki mwaka 2008 alipomtembelea nyumbani kwake katika Kijiji cha Khaday, Kata ya Sanu Mjini Mbulu,(wakwanza kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Bw.Chelestino Mofuga.
  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (katikati) akiwa ameshikilia kikombe cha ushindi wa Mwanariadha wa zamani John Stephen Akhwari alichoshinda shinda katika Mashindano yaya Olimpiki yaliyofanyika nchini Ugiriki kwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Bw.Chelestino Mofuga (wa kwanza kushoto) na John Steven Akhwari mwenye (wa kwanza kulia) wakiwa nyumbani kwake katika Kijiji cha Khaday, Kata ya Sanu.
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akisalimiana na Daktari wa Timu ya Jeshi la Wananchi Andrew Panga leo alipotembelea timu hiyo kambini Mjini Mbulu akiwa katika ziara ya kikazi (wakwanza kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Bw.Chelestino Mofuga.
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura(wasita kulia) akiwa katika picha ya pamoja leo na Timu ya wanariadha wa Jeshi la Wananchi waliyoko kambini Wilayani Mbulu alipowatembelea akiwa katika ziara ya kikazi (wasita kushoto) ni mwanariadha wa zamani John Stephen Akhwari pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Bw.Chelestino Mofuga. Mwanariadha wa zamani aliyeweka rekodi ya Kimataifa ya kuonyesha Uzalendo kwa nchi yake katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika Mexico mwaka 1968 kwa kuendelea kukimbia na kushika namba mbili mbali na kwamba alikuwa amevunjika mguu wakati akiwa uwanjani Bw.John Stephen Akhwari akileza changamoto za sekta ya riadha nchini katika Mkutano wa wadau wa kisekta na Naibu Waziri Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (hayupo pichani) ulifofanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara. Mwanariadha wa zamani aliyeiletea Tanzania sifa kwa kushinda mashindano mbalimbali ya Kimataifa na kupata Medali za aina mbalimbali Bw.Alfredo Shahanga akieleza changamoto zilizojitokeza wakati wadau wa kutoka nchini Australia walipokuja Tanzania na kutaka kujenga uwanja wa michezo Wilayani Mbulu kumuenzi mwanariadha mzalendo John Stephen Akhwari kwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (hayupo pichani) leo katika mkutano wa wadau wa kisekta Mkoani Manyara.

  Na Anitha Jonas- MAELEZO,BABATI

  0 0


  Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini mkoani Dodoma, Mhe.Antony Peter Mavunde, akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.

  Kongamano hilo ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya taasisi ya “Tanzania Youth Enterpreneurship Organization-TAYEO) pamoja na Vijana Mwanza Saccos, linafanyika katika viwanja wa Gandh Hall Jijini Mwanza kwa siku mbili, leo Julai 16,2016 hadi kesho Julai 17,2016 ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nhauye. 

  Wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo taasisi ya Desk and Chair Foundation, Mfuko wa Hifadhi ya jamii PPF, Kampuni ya mafuta ya Petro Africa, Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Ofisi ya mbunge wa jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula, Ofisi ya mbunge wa jimbo la Ilemela, Mhe.Angelina Mabula ambae pia ni Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, City Fm na Mhe.Jumanne Kishimba ambae ni mbunge wa jimbo la Kahama Mjini.Na BMG
  .

  Wadau mbalimmbali wakiwa katika Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.

  Wadau mbalimmbali wakiwa katika Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.

  Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe.Antony Mavunde (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Kongamano (kulia), wakifurahia jambo katika kongamano hilo.

  Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kiburwa Kibamba, akizungumza katika kongamano hilo.

  Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kiburwa Kibamba (kulia), wakifuatilia kongamano hilo.

  Flora Magabe, akisoma Risala kwa niaba ya waandaaji wa Kongamano hilo.

  Viongozi pamoja na wadau mbalimbali wakiwa katika kongamano hilo.

  Waandaaji wa Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza

  Mwenyekiti wa Shirika la Machinga mkoani Mwanza (katikati) akiwa pamoja na wadau wengine katika Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.

  Wadau mbalimmbali wakiwa katika Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.

  Wadau mbalimmbali wakiwa katika Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.

  Vijana mkoani Mwanza wameaswa kutambua fursa za kiuchumi zilizopo kwenye maeneo yao na kuzitumia kikamilifu ili kupambana na uhaba wa ajira unaosababisha kukithiri kwa umasikini katika jamii.

  Akifungua hii leo kongamano la siku mbili la vijana kutoka wilaya zote saba za mkoa wa Mwanza, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, amesema mkoa wa Mwanza unazo fursa nyingi za kiuchumi ikiwemo ardhi kwa ajili ya kilimo na Ziwa Victoria kwa ajili ya uvuvi,hivyo vijana wanapaswa kuzitumia ipasavyo fursa hizo.

  Amesema kumejengeka tabia miongoni mwa vijana kulalamikia uhaba wa ajira jambo ambalo amesema linasababishwa na vijana hao kushindwa kujitambua huku wengine hasusani wanaohitimu vyuo vikuu wakichagua
  kazi za kufanya hivyo kuongeza idadi ya vijana wasio na ajira mitaani.

  Aidha Naibu Waziri Mavunde amezitaka Halmashuri zote nchini kuhakikisha zinatenga asilimia tano ya fedha za mapato mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha vijana huku pia akiwaagiza wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa Halmashuri kutenga maeneo kwa ajili ya vijana na akina mama kufanya biashara zao bila kubughudhiwa.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, amesema Halmashauri ya jiji hilo itahakikisha inatenga asilimia tano ya mapato yake kwa ajili ya vijana na akina mama huku akiwataka vijana kuhamasisha wananchi kulipa kodi ili fedha hizo zipatikane.

  Awali akisoma risala kwa niaba ya waandaali wa kongamano hilo, Flora Magabe, amesema vijana wa mkoa wa Mwanza wamepanga kuwekeza kwenye kilimo na ufugaji wa kuku na kuiomba serikali kuwapatia maeneo kwa ajili ya kuendesha miradi hiyo.

  Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza, limeandaliwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya taasisi ya Vijana Wajasiriamali Tanzania (Tanzania Youth Enterpreneurship Organization-TAYEO) pamoja na Chama cha Akiba na Mikopo cha Vijana Mwanza Saccos, ambapo linafanyika katika viwanja wa Gandh Hall Jijini Mwanza, leo na kesho.

  0 0


  Na Editha Karlo,wa blog ya jamii,Kagera

  WAZIRI wa afya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu ameitaka jamii kujenga tabia ya kusaidia wazee ili na wao waweze kuyamudu maisha yao.

  Ummy ameyasema hayo leo wakati alipotembelea makazi ya kutunzia wazee katika kituo cha kiilima kilichopo katika Wilaya ya Bukoba vijijini.kuwa wazee wametoa mchango mkubwa kwa Taifa na bado wanamchango mkubwa pia katika Taifa hivyo lazima jamii inayoishi nayo kuwatunza na kuwaheshimu.

  "Wazee wangu mimi nipo pamoja na nyie,na matatizo yenu yote nimeyasikia tutaendelea kuyatatua kadri fedha zitakavyo kuwa zinapatikana"alisema.Alisema kuwa ameguswa na matatizo waliyonayo wazee hao kituoni hapo ikiwemo tatizo la huduma ya afya,vyoo,maji pamoja na makazi ya kulala.

  Wazee hao walimuomba Waziri kuwekea mkazo katika suala la huduma za matibabu pamoja na usafiri wa uhakika wa kuwapelekeka hospital pale wanapouugua."Mhe.Waziri tunaomba utufanyie mpango tupate gari hapa kwenye makazi yetu la kutupeleka hospital pale tunapo umwa,hii kwetu ni changamoto kubwa hasa akitokea mgonjwa usiku"alisrma mzee Andrea Lwiza.


  Waziri Ummy Mwalimu akiongea na wazee wanaotunzwa katika kituo cha kulelea wa wazee Kiilima

  Waziri wa afya jinsia maendeleo wazee na watoto akiangalia vyoo wanavyotumia wazee wanaotunzwa katika kituo cha Kiilima kilichopo Wilaya ya Bukoba vijijini.

  Baadhi ya wazee wanaotunzwa katika kituo cha kulelea wazee cha Kiilima wakimsikiliza waziri (hayupo pichani)

  0 0


  Mkuu wa Kituo cha TBC Manyara Bw. Mganga Mwanja (wa kwanza kulia)akimweleza Naibu Waziri wa Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo (katikati) Mhe.Anastazia Wambura changamoto ya mitambo waliyo nayo alipotembelea eneo la mitambo ya kurusha matangazo leo katika Mji wa Babati katika ziara yake ya kikazi.
  Katibu Tawala Mkoa wa Bw.Manyara Eliakim Maswi akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mji wa Manyara Bi. Rena Urio leo kabla ya kuanza kwa ziara ya Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura(wa pili kushoto) kutembelea vivutio vya kiutamaduni vilivyoko katika Wilaya ya Babati.

  Anitha Jonas – MAELEZO,BABATI

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Hassan Sanga akizungumza na watendaji wa kata kuhusu kupeana mikakati ya kazi ,mkutano huo ulioandaliwa na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega leo mkoani Pwani.kushoto ni Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Mkuranga Ulega
  Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na Watendaji wa kata (hawapo pichani) kuhusu kupeana mikakati ya kazi, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, , Filberto Hassan Sanga
  Mwanasheria wa Wilaya ya Mkuranga Salum Papen akisisitiza jambo katika mkutano huo, kulia ni Afisa Utawala na Utumishi wa Wilaya hiyo, Valentine Mbai
  Sehemu ya Watendaji wa kata wakimsiliza Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Hassan Sanga
  Mkuu wa Wilaya ya Mkuraanga, Filberto Hassan Sanga pamoja na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega wakiwa kwenye picha ya pamoja na Watendaji wa kata.

  0 0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua duka la dawa la MSD kwenye hospitali ya Wilaya ya Ruangwa akiwa katka ziara ya jimbo lake la uchaguzi Julai 16, 2016.Kushoto kwake ni mkewe Mary na watano kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Ali Mtopa nakushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kukata utepe wakati akizindua duka la dawa la MSD kwenye hospitali ya wilaya ya Ruangwa Julai 16, 2016. Kulia kwake ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea duka hilo la MSD baada ya kulizindua kwenye hospitali ya wilaya ya Ruangwa akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi Julai 16, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuzindua duka la dawa la MSD kwenye hospitali ya wilaya ya Ruangwa akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi Julai 16, 2016.


  Waziri Mkuu, Kassim Majakipokea miguu miwili ya bandia kabla ya kuzindua duka la dawa la MSD lililokwenye hospitali ya wilaya ya Ruangwa Julai 16, 2016. Miguu hiyo imetengeezwa na kutolewa msaada Kampuni ya Kamal Steel kwa wananchi wawili wa wilaya ya Ruangwa. Watatu kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majliwa na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Ali Mtopa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  ……………….  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua duka la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika Hospitali ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi ambalo litakuwa na uwezo wa kuhudumia hospitali 524 katika mikoa ya Lindi, Mtwara na wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

  Akizindua duka hilo leo (Jumamosi, Julai 16, 2016) Waziri Mkuu amesema duka hilo litaendelea kuboresha huduma za upatikanaji wa dawa kwa gharama nafuu katika hospitali, vituo vya afya na zahanati katika wilaya ya Ruangwa pamoja na mikoa na wilaya za jirani.

  Duka hilo ni la sita kufunguliwa tangu Mhe. Rais Dk. John Magufuli alipotoa agizo kwa MSD kufungua duka la dawa ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambapo mengine yako katika mikoa ya Mwanza (Sekou Toure), Arusha (Mount Meru), Mbeya (karibu na hospitali ya mkoa) na Geita (hospitali ya wilaya ya Chato).

  “Duka hili litasaidia kufikiwa kwa malengo ya Serikali ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa wakati na kwa gharama nafuu, hivyo nawaomba mlitumie duka hili,” amesema.

  Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuushukuru uongozi wa benki ya NMB, kikosi cha SUMA JKT na MSD kwa kufanikisha ujenzi wa duka hilo ambalo litaimarisha upatikanaji wa dawa kwa uharaka.

  Awali Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema kuanzishwa kwa duka hilo kutaongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa gharama nafuu , hivyo kuondoa usumbufu kwa wagonjwa wa kwenda kuzitafuta katika ya mbali na kwa bei kubwa.

  “Nitoe mfano wa tofauti wa bei za dawa kati ya maduka yetu na mengine, dawa ya sindano ya diclofenac tunauza sh. 250 huku mitaani ni sh. 1,000 hadi 1,500 , ampliclox dozi moja MSD sh. 1,500 mtaani sh. 3,500 na Ciprofloxacin MSD sh. 100 na mtaani sh. 500 hadi 1,000,” amesema.

  Mkurugenzi huyo amesema lengo la maduka hayo si kuuza dawa reja reja, nia yao ni kuziuzia hospitali, vituo vya afya na Zahanati ili wagonjwa wanapokwenda huko kupatiwa huduma wasikose dawa kwa wakati.

  Akizungumzia kuhusu gharama za ujenzi wa duka hilo Bwanakunu mesema umegharimu sh.milioni 59 ambapo kati yake MSD imetoa sh. milioni 29 na benki ya NMB imetoa sh. milioni 30.“Mbali na gharama za ujenzi MSD tumenunua na kufunga vifaa vya TEHAMA kwa sh milioni 17 na mtaji wa dawa wa sh. milioni 37, ambapo imetenga sh. milioni 100 kwa ajili ya dawa za duka hilo.

  Amesema duka hili litaendeshwa na kusimamiwa na MSD kwa muda wa mwaka mmoja na kisha wataikabidhi Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa ajili ya kuliendeleza ambapo litaisaidia katika kuiongezea mapato.

  0 0

  LIO1 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee wa Ruangwa  ambao walimshukuru kwa jitihada kubwa anazofanya  za kuboresha maisha ya Wanachi wa jimbo lake la uchaguzi.  Alikuwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi Julai 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  LIO2 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee wa Ruangwa  ambao walimshukuru kwa jitihada kubwa anazofanya  za kuboresha maisha ya Wanachi wa jimbo lake la uchaguzi.  Alikuwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi Julai 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  LIO3 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi Ruangwa kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara  kwenye uwanja uliopo kwenye kata ya  Nachingwea mjini Ruangwa Julai 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  LIO4 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Lindi  , Renather Mzinga ambaye amepandishwa cheo na kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi. Alikuwa  katika ziara ya mkoa wa Lindi Julai 16,2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  LIO5 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi, viongozi na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Julai 16, 2016.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendego na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  LIO6 
  Baadhi ya Watumishi , Viongozi na wananchi wa mkoa wa Mtwara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa huo Julai 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  LIO7 
   Baadhi ya Watumishi , Viongozi na wananchi wa mkoa wa Mtwara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa huo Julai 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  ……………………………………………………………………………………………….
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Serikali wa kufuta tozo tano kati ya tisa alizokuwa anakatwa mkulima wa zao la korosho uko pale pale na unatarajiwa kuanza kutumika katika msimu mwaka huu hivyo ameitaka Bodi ya Korosho kusimamia uamuzi huo.

  “Watendaji wa Serikali katika ngazi mbalimbali mnatakiwa kuhakikisha kwamba maelekezo haya yanafuatwa. Malengo yetu ni kumpunguzia mkulima mzigo wa tozo nyingi alizokuwa anakatwa,” alisema.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumamosi, Julai 16, 2016) wakati akipokea taarifa ya maendeleo ya mkoa Mtwara pamoja na taarifa ya kuondolewa kwa baadhi ya tozo katika zao la korosho zilizowasilishwa na Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendego.Alisema Serikali iliamua kuzifuta tozo hizo baada ya kubainika kuwa zilikuwa zikiwanyonya wakulima hali iliyosababisha wauchukie mfumo wa stakabadhi ghalani.

   “Kuanzia mwaka huu Serikali imeamua mfanyabiashara yeyote wa korosho hana budi kuanza kulipa malipo ya awali kabla ya kuingia kwenye mnada ili tuwe na uhakika wa kununua korosho hizo na kuwalipa wakulima kwa wakati,” alisema.Akizungumzia kuhusu changamoto ya kushuka kwa uzalishaji wa korosho Waziri Mkuu aliutaka mfuko wa wakfu wa kuendeleza zao hilo ufanye utafiti wa kubaini sababu ili waweze kutafuta namna ya kuipatia ufumbuzi.

  “Nitakuja kukutana na viongozi wa mfuko waniambie wanafanya nini na wamefanya nini miaka mitatu iliyopita na wana mpango gani huko mbele tunakokwenda kama hakuna mpango tutauangalia mara mbili mbili kwani wana fedha nyingi lakini hata mbegu hawapeleki kwa wakulima,” alisema.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliitaka Bodi ya Korosho kuhakikisha kila msimu wakulima wanapata pembejeo bora na zinawafikia kwa wakati ili waweze kupata mazao ya kutosha

  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Spika Mstaafu, Anne Makinda akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) juu ya maboresho ya muundo wa safu ya wakurugenzi leo jijini, Dar es Salaa,Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernald Konga.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernald Konga akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) juu ya hatua ya bodi waliochukua katika shirika hilo katika kubadili muundo wa wakurugenzi, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Spika Mstaafu, Anne Makinda.
  Wajumbe wa bodi na waandishi habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Spika Mstaafu, Anne Makinda.( picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii’)

  ………………………………………………………………………………

  Na Chalila Kibbuda, Globu ya Jamii.

  BODI ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imefanya maboresho kwa kupunguza idadi ya wakurugenzi kutoka tisa hadi watano ili kuweza kufanya kazi kwa kasi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

  Akizungumza na waandishi habari Makao Makuu NHIF leo Mwenyekiti bodi hiyo Spika Mstaafu, Anne Makinda amesema kuwa utaratibu wa awali wakurugenzi walikuwa wanaajiliwa kwa mikataba ya miaka mitatu mitatu.Amesema kuwa wakurugenzi waliokuwa wanafanya wengine kwa mikataba wengine wamemaliza na ambao walikuwa wanaendelea wamesitisha mikataba yao.

  Makinda amesema kuwa NHIF imekaa kwa muda ikiwa haina bodi kwa mwaka mmoja na nusu hivyo baadhi ya vitu havikuwa sawa.Amesema kuwa watu ambao wamemaliza mikataba na weengine kusitisha mikataba yao wanaweza wakaomba tena kama wana sifa ya kazi watazoomba na kuangalia weledi wao.

  0 0


  Kipa wa Yanga, Dennis Munishi “Dida” akiiunyaka mpira kwa umaridadi kabisa.

  Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa akichuana vikali kuwania mpira na Beki wa Medeama, Samuel Adade.

  Mwamuzi wa Mchezo huo, Ibrahim Nour El Din akimzawadia kadi ya njano, beki wa Timu ya Medeama.

  Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akijiandaa kuachia shuti kuelekea langoni mwa Timu ya Medeama, wakati wa Mtanange wa Kombe la Shirikisho, uliopigwa Uwanja wa Taifa leo. timu hizo zimetoka sare ya kufungana 1-1.

  Waamuzi wa Mchezo wa leo kati ya Yanga ya Tanzania na Medeama ya nchini Ghana, wakiziongoza timu kuingia uwanjani tayari kwa kuanza kwa mchezo huo wa Kombe la Shirikisho, uliopigwa kwenye Dimba la Taifa jijini Dar es salaam. Mchezo huo umemalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa kufungana Bao 1-1. ambapo Goli la Yanga liliwekwa kimyani na Mshambuliaji Donald Ngoma dakika ya pili tu ya Mchezo kipindi cha kwanza huku Medeama wakisawazisha dakika 17 baadae kupitia mwa Mshambuliaji wake Benard Danso.

  Kikosi cha Medeama.

  Kikosi cha Yanga.

  Wachezaji wa timu ya Yanga, wakishangilia ushindi wao pamoja na Washabiki wao, baada ya Mshambuliaji wake Donald Ngoma kuipatia timu yake goli la kuongoza ikiwa ni dakika ya pili tu Mchezo dhidi ya Medeama ikiwa ni Mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

  Washabiki wa Yanga wakiishangilia timu yao. 

  0 0

  Anitha Jonas – MAELEZO,Kahama.

  Kahama.

  Halmashauri ya Kahama ya imeelezwa kuacha kuchukua tozo zisizo na umuhimu katika kipindi michezo yakunufaisha jamii.

  Kauli hiyo imetolewa jana Mjini Kahama na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokuwa akifunga mashindano ya Mbio za Baiskeli ya Tushikamane yaliyohusisha Mikoa ya Kanda ya Ziwa na yamekuwa yakidhaminiwa na Kampuni ya Madini ya Acacia Buzwagi.

  “Ombi langu kwenu Kampuni ya Acacia Buzwagi muongeze mkataba wenu wa kuwezesha mashindano haya kwa kuwa kupitia msaada wenu vijana hawa wa Kanda ya Ziwa wanapata kipato ambacho kinawasaidia katika maisha yao ya kiuchumi”,alisema Naibu Waziri Wambura.

  Pamoja na hayo Naibu Waziri huyo alitoa rai kwa taasisi nyingine kujitokeza kusaidia mashindano hayo ya ili kuweza kuwafikisha mbali wanamichezo hao wenye uwezo mkubwa wa kufanya mchezo huo kufikia hata kiwango cha Kimataifa.

  Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Baiskeli Bw.Godfrey Mhagama alisema kwa mwaka huu kuna zaidi ya wachezaji 200 waliyoshiriki mshindano haya ombi langu kwa serikali ifatafute wadau watakao weza kusaidia kuendeleza vipaji vya vijana hawa kanda ya ziwa iliwaweze kuufanya mchezo huu kuwa ajira na kupata mafanikiwa makubwa kama wachezaji wa ulaya.

  “Wakazi wa Kanda ya Ziwa wa wanauwezo mkubwa katika uendeshaji wa baiskeli hii ni kutokana na utamaduni wao wa kutumia Baiskeli kama chombo cha usafiri”,alisema Bw.Mhagama.

  Naye Meneja wa Mgodi wa Acacia Buzwagi Bw.Asa Mwaipopo alisema katika mashindano hayo ya mwaka huu watatoa zawadi kuanzia mtu wa kwanza mpaka wa 30 na katika mashindano hayo wanaume watakimbia kilomita 156 na wanawake kilomita 80 na zawadi ya mshindi kwanza kwa mwanaume ni milioni moja na nusu na kwa wanawake ni milioni moja.

  Pamoja na hayo wanamichezo hao wameaswa kufanya juhudi katika mchezo huu pia kutojaribu kutumia madawa ya kuongeza nguvu wakati wa michezo.

  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Serikali wa kufuta tozo tano kati ya tisa alizokuwa anakatwa mkulima wa zao la korosho uko pale pale na unatarajiwa kuanza kutumika katika msimu mwaka huu hivyo ameitaka Bodi ya Korosho kusimamia uamuzi huo.

  “Watendaji wa Serikali katika ngazi mbalimbali mnatakiwa kuhakikisha kwamba maelekezo haya yanafuatwa. Malengo yetu ni kumpunguzia mkulima mzigo wa tozo nyingi alizokuwa anakatwa,” alisema.Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumamosi, Julai 16, 2016) wakati akipokea taarifa ya maendeleo ya mkoa Mtwara pamoja na taarifa ya kuondolewa kwa baadhi ya tozo katika zao la korosho zilizowasilishwa na Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendego.

  Alisema Serikali iliamua kuzifuta tozo hizo baada ya kubainika kuwa zilikuwa zikiwanyonya wakulima hali iliyosababisha wauchukie mfumo wa stakabadhi ghalani. “Kuanzia mwaka huu Serikali imeamua mfanyabiashara yeyote wa korosho hana budi kuanza kulipa malipo ya awali kabla ya kuingia kwenye mnada ili tuwe na uhakika wa kununua korosho hizo na kuwalipa wakulima kwa wakati,” alisema.

  Akizungumzia kuhusu changamoto ya kushuka kwa uzalishaji wa korosho Waziri Mkuu aliutaka mfuko wa wakfu wa kuendeleza zao hilo ufanye utafiti wa kubaini sababu ili waweze kutafuta namna ya kuipatia ufumbuzi.

  “Nitakuja kukutana na viongozi wa mfuko waniambie wanafanya nini na wamefanya nini miaka mitatu iliyopita na wana mpango gani huko mbele tunakokwenda kama hakuna mpango tutauangalia mara mbili mbili kwani wana fedha nyingi lakini hata mbegu hawapeleki kwa wakulima,” alisema.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliitaka Bodi ya Korosho kuhakikisha kila msimu wakulima wanapata pembejeo bora na zinawafikia kwa wakati ili waweze kupata mazao ya kutosha.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU, JUMAPILI, JULAI 17, 2016

  0 0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda, Francis Gatare alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kigali, Rwanda kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Makamu wa Rais anamwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano huo picha na (OMR).
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda ,Francis Gatare mara alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na SerIkali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Makamu wa rais anamwakilisha Rais Dkt John Magufuli Katika Mkutano huo .
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda,Francis Gatare kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kigali, Rwanda mara baada ya Kuwasili nchini humo kwa ajili ya Kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Makamu wa Rais anamwakilisha Rais Dkt John Magufuli katika Mkutano huo. (Picha na OMR)

  0 0  0 0  logo
  TaSUBA has been established by The Executive Agency Act No. 30 of the year 1997. In the year 2012, TaSUBA has been pronounced a Centre of Excellence in East Africa Region in the category of training Institutions. It now wishes to invite suitably qualified Tanzanians to apply for appointment to fill the positions of the Chairperson and Members of the TaSUBA Board of Directors. The Board plays a key advisory role and it is the supreme administrative organ of the Organisation.
   
  QUALIFICATIONS:The following are the minimum qualifications for appointment to the Board:1. Should be a graduate (at least first degree or equivalent) from a recognized University in one of the following fields of Study: Arts/Culture, Accountancy (CPA), Economics, Law or Human Resource Management.
   2. Have at least 5 years working experience in at least on one of the said fields above.3. Should satisfy the Nomination Committee that he/she is unlikely to have a conflict of interest with the roles of the Board;4. Be willing to serve as Chairperson or member to the Board.
   
  APPLICATION INSTRUCTIONS:
  All applications including detailed Curriculum Vitae, photocopies of relevant genuine certificates and names and addresses of three easily contactable referees (including current or last employer) should be sent by post, courier, E-mail or delivered by hand so as to reach the Chairman of the Nomination Committee by 15:30Hrs, Monday 01August, 2016.
  The Chairman of TaSUBA Nomination Committee,Ministry of Information, Culture, Arts and Sports,
  Golden Jubilee Towers: 8th Floor,
  Ohio Street,
  P.O. BOX 8031,
  DAR ES SALAAM
  Email: chairman.nomination@habari.go.tzPlease Note:
   
  On the envelop/Email mark the position of application and your area ofspecialization. REMEMBER; Apply by 01/08/2016. !This advert is also available on: www.habari.go.tz
  Contact Help Desk, Mobile: 0719-349825 or 0719-355770.

  0 0


  Bw.Amil Shivji akitangazwa kuwa mshindi tuzo kwenye tamasha la ZIFF baada ya filamu AISHA kutangazwa filamu bora
  Bw.Amil Shivji akipokea tuzo kwenye tamasha la ZIFF baada ya filamu AISHA kutangazwa filamu bora
  ………………….

  Usiku wa jana ulikuwa ni wa furaha ya aina yake kwa wadau mbalimbali waliokuwa wakiwania tuzo kwenye tamasha la kimataifa la filamu la ZIFF lililofanyika Zanzibar na miongoni mwa washindi hao ni Amil Shivji,ambaye pia ni mwalimu wa masuala ya uandaaji filamu kwenye idara ya sanaa ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.

  Bw.Amil kupitia filamu ya AISHA iliyotengenezwa na kampuni ya Kijiweni Production kwa ushirikiano na shirika la Uzima kwa Sanaa(UZIKWASA) lilipo Tanga,kwa ujumla ilijishindia tuzo takriban nne katika kipengele kilichoshindanisha filamu za kiswahili, maarufu kama “bongo movie”.

  Filamu ya AISHA iliyotengenezwa Pangani-Tanga, imekwishachezwa kwenye zaidi ya matamasha thelathini(30) duniani, iliweza kuibuka kinara kwenye ZIFF kwa kutoa muongozaji bora(Omar Chande), muigizaji bora wa kike(Godliver Gordian), filamu bora(AISHA) na mhariri bora wa filamu(Momose Cheyo).

  Mtengenezaji huyo wa filamu aliyewahi kujinyakulia tuzo kadhaa kupitia filamu za SHOESHINE pamoja na SAMAKI MCHANGANI, akitoa ushauri kwa vijana, wasanii chipukizi na pia wasanii wakongwe aliwasihi wasidharau umuhimu wa kuingia darasani kujinoa zaidi na kupata maarifa.

  Bw.Amil aliongeza,”hata kama chuo si chaguo la kwanza ama hauchukulii kwa uzito, kuna warsha nyingi sana ambazo zinasaidia kukuza kipaji na uzoefu katika utengenezaji wa filamu. Tafadhalini endeleni kusoma, kudadisi mambo mbalimbali yanayoendelea ulimwenguni, na daima ujiulize filamu zako zitaongelea kuhusu nini”.

  Akiwashukuru wadau wa filamu alisiwasisitiza wajue tu kwamba Kijiweni productions ipo, na itaendelea kupambana na mifumo inayokandamiza na kunyanyasa watanzania na watu wote bila kujali rika, rangi au jinsia ya mtu.Tamasha hilo la filamu huandaliwa kila mwaka na kushirikisha maonesho ya filamu na sanaa mbalimbali, utoaji tuzo na mafunzo kwa watengenezaji wa filamu

  0 0
 • 07/17/16--06:12: Article 4


 • THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  MINISTRY OF INFORMATION, CULTURE, ARTS AND SPORTS    APPOINTMENT OF THE CHAIRPERSON AND MEMBERS OF THE BOARD OF TANZANIA STANDARD (NEWSPAPERS) LIMITED (TSN)

  Pursuant to Articles 75 and 76 of the companys MEMARTS, TSN wishes to invite suitably qualified Tanzanians to apply for appointment to fill the positions of the Chairperson and Members of the Board of Directors. The Board plays a key advisory role and it is the supreme administrative organ of the Organisation.

  QUALIFICATIONS:
  The following are the minimum qualifications for appointment to the TSN Board:
  1.    Should be a graduate (at least first degree or equivalent) from a recognized University in one of the following fields of study:  Media, Accounts (CPA), Economics, Law or Human Resource Management.
  2.    Have at least 5 years working experience in at least one of the said fields above. 
  3.    Should satisfy the Nomination Committee that he/she is unlikely to have a conflict of interest with the roles of the Board;
  4.    Be willing to serve as Chairperson or member to the Board.

  APPLICATION INSTRUCTIONS:
  All applications including detailed Curriculum Vitae, photocopies of relevant genuine certificates and names and addresses of three easily contactable referees (including current or last employer) should be sent by post, courier, E-mail or delivered by hand so as to reach the Chairman of the Nomination Committee by 15:30Hrs, Monday 01 August, 2016.

  The Chairman of TSN Nomination Committee,
  Ministry of Information, Culture, Arts and Sports,
  Golden Jubilee Towers: 8thFloor,
  Ohio Street,
  P.O. BOX 8031,
  DAR ES SALAAM
  Email: chairman.nomination@habari.go.tz

  Please Note:
  On the envelop/Email mark the position of application and your area of specialization. REMEMBER; Apply by 01/08/2016.
  This advert is also available on: www.habari.go.tz
  Contact Help Desk, Mobile: 0719-349825 or 0719-355770.  0 0  Mkuu wa mafunzo na Utendaji Kivita Meja Jenerali Issa Nassoro akizungumza na Wanamichezo (hawapo pichani) katika Kambi ya Bavuai ikiwa ni maandalizi kuelekea Michuano ya Afrika mashariki kwa majeshi ya nchi za Afrika Mashariki yatakayofanyika Kigali Rwanda Agosti mwaka Huu. (Picha na Selemani Semunyu).
  Baadhi ya wachezaji wa Timu teule wa JWTZ wakimsikiliza mkuu wa mafunzo na Utendaji kivita Meja Jenerali Issa Nassor aliyetembelea kambi ya Timu hizo Mjini Zanzibar zinazotarajiwa Kushiriki mashindano ya majeshi kwa nchi za Afrika mashariki Agosti mwaka huu Rwanda(picha Na Selemani Semunyu).

  Na Selemani Semunyu, JWTZ.

  Mkuu wa mafunzo na Utendaji Kivita wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Meja Jenerali Issa Nassoro amezitaka Timu teule za Jeshi kutobweteka na Ushindi wanaoupata katika mechi za majaribio wanazocheza.

  Kauli hiyo imekuja Mwisho mwa wiki wakati Timu ya Mpira wa Pete (Netball) Wanawake ya jeshi la Wananchi wa Tanzania kudhihirisha ubabe wake baada ya kuifunga Timu ya Mpira wa pete ya Wananume ya kikosi cha Valentia Zanzibar -KVZ kwa Magoli 36 kwa 24 katika mchezo uliofanyika Mwishoni mwa wiki Visiwani Zanzibar.

  Mchezo huo uliofanyika Katika katika uwanja wa Polisi Bwawani Ulikuwa kivutio kikubwa kutokana na kuhusisha jinsi mbili tofauti kwa maana ya Wanaume na Wanawawake lakini pia ukiwa na wachezaji mahiri kutoka katika Timu zote mbili ambao wamekuwa na majina makubwa katika mchezo huo.

  Meja Jenerali Nassoro aliyekuwa katika Ziara ya kutembelea kambi ya Timu teule za jeshi za mpira wa Miguu,Pete,Kikapu na Mpira wa Mikono zilizoweka kambi katika Visiwa vya Unguja Mjini Zanzibar alisema ameridhishwa na kambi licha ya Jitihada zaidi kuongezwa ili kujihakikishia ushindi.

  Alisema anamatumaini Makubwa historia ya kuweka kambi Zanzibar kutazibeba Timu za Jeshi kwani Timu mbalimbali zilizowahi kuweka kambi Zanzibar zilipata Mafanikio hivyo Jeshi na Taifa tunategemea hilo kama eneo zuri kwa kambi ili kujiandaa vizuri.“Niliamua kwa Makusudi kupendekeza kambi kuwa Zanzibar nimekuwa Mchezaji na Mwanamichezo muda mrefu najua faida za kuweka kambi Zanzibar ukilinganisha na maeneo mengine kama Dar es Salaam” Alisema Meja Jenerali Nassoro.

  Katika michezo ya majaribio za Timu hizo Teule za jeshi Katika Mchezo wa mpira wa Kikapu Timu ya Jeshi wameifunga Timu ya Mbuyuni kwa Vikapu 104 kwa 58 na kuifanya Timu hiyo kuendeleza ubabe ikiwa ni mchezo baada ya michezo yake ya Awali kuzifunga Timu mabingwa wa Mchezo huo kwa Zanzibar.Timu hizo zilizochezea kichapo katika Mpira wa Kikapu JWTZ iliifunga Stone Town kwa Vikapu 69 kwa 48 wakati mchezo uliochezwa kabla JWTZ waliifunga polisi kwa Vikapu 68 kwa 49 michezo iliyochezwa katika Viwanja Vya Maisara.

  Katika hatua Nyingine Timu ya Soka ya JWTZ inakumbukumbu ya kuifunga Mafunzo kwa mabao Mawili kwa moja ikiwa ni mchezo wa marudiano huku mchezo wa Kwanza Timu ya Jeshi ikiwa imeibuka kwa Ushindi wa mabao Mawili kwa Moja, Katika mchezo Mwingine JWTZ wameifunga jeshi la Kujenga Uchumi JKU kwa Magoli Mawili kwa Moja.Katika Mpira wa Mikono JWTZ wameifunga Vijana Combine kwa Magoli 37 kwa 16 wakati katika Mchezo mwingine JWTZ waliifunga Zanzibar Warriors kwa Magoli 36 kwa 16.

  0 0
 • 07/17/16--06:30: Article 2
 • THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  MINISTRY OF INFORMATION, CULTURE, ARTS AND SPORTS 


  APPOINTMENT OF THE CHAIRPERSON AND MEMBERS OF THE BOARD OF BARAZA LA SANAA LA TAIFA
  (BASATA)

  BASATA is established by Act No. 23 of 1984. BASATA coordinates all programmes and operations related to the four sections of arts (Music, Performing Arts, creative arts and Film). It now wishes to invite suitably qualified Tanzanians to apply for appointment to fill the positions of Chairperson and Members of Board of Directors. The Board plays a key advisory role and it is the supreme administrative organ of the Organisation.

  QUALIFICATIONS:

  The following are the minimum qualifications for appointment to the Board:

  1. Should be a graduate (at least first degree or equivalent) from a recognized university in one of the following fields of Study: Arts, Accountancy (CPA), Economics, Law or Human Resource Management.
  2. Have at least 5 years working experience in at least one of the said fields above.
  3. Should satisfy the Nomination Committee that he/she is unlikely to have a conflict of interest with the roles of the Board;
  4. Be willing to serve as Chairperson or member to the Board.


  APPLICATION INSTRUCTIONS:

  All applications including detailed Curriculum Vitae, photocopies of relevant genuine certificates and names and addresses of three easily contactable referees (including current or last employer) should be sent by post, courier, E-mail or delivered by hand so as to reach the Chairman of the Nomination Committee by 15:30Hrs, Monday 01 August, 2016.

  The Chairman of BASATA Nomination Committee,
  Ministry of Information, Culture, Arts and Sports,
  Golden Jubilee Towers: 8th Floor,

  Ohio Street,
  P.O. BOX 8031,
  DAR ES SALAAM
  Email: chairman.nomination@habari.go.tz

  Please Note:

  On the envelop/Email mark the position of application and your area of specialization. REMEMBER; Apply by 01/08/2016.

  This advert is also available on: www.habari.go.tz
  Contact Help Desk, Mobile: 0719-349825 or 0719-355770.


older | 1 | .... | 907 | 908 | (Page 909) | 910 | 911 | .... | 1897 | newer