Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 905 | 906 | (Page 907) | 908 | 909 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Nyota wa soka aliyefanya vizuri michezo ya Shule za Sekondari (UMISETTA) Mussa Bakari akiwasili ndani ya uwanja cha ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutokea katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Paris nchini Ufaransa. 
  Meneja Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga (kushoto) akimpokea kwa shangwe nyota wa soka aliyefanya vizuri michezo ya Shule za Sekondari (UMISETTA) Mussa Bakari (katikati) mara baada ya kuwasili ndani ya uwanja cha ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutokea katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Paris nchini Ufaransa. Pembeni ni Pamela Lugenge (kulia) mmoja wa Afisa Masoko. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. 
  Meneja Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga (kushoto) akimkabidhi taji la maua nyota wa soka aliyefanya vizuri michezo ya Shule za Sekondari (UMISETTA) Mussa Bakari mara baada ya kuwasili ndani ya uwanja cha ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutokea katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Paris nchini Ufaransa. Pembeni ni Pamela Lugenge (kulia) mmoja wa Afisa Masoko. 
   Meneja Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na nyota wa soka aliyefanya vizuri michezo ya Shule za Sekondari (UMISETTA) Mussa Bakari (katikati) pamoja na Pamela Lugenge (kulia) mmoja wa Afisa Masoko.

  0 0
  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Mr Sugu' akiwaonesha wabunge wa CCM dole la kati Bungeni Dodoma hivi karibuni, kitendo ambacho kilitafsiliwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwa ni tusi, hivyo kupewa adhabu ya kutohudhuria vikao kumi vya Bunge. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

  0 0

  Baadhi ya akinamama wa Kitanga Green Voices wakiwa wameushikilia muhogo pamoja na viongozi wa kijiji na Kata ya Msimbu wilayani Kisarawe.
  Kijana akiwa amebeba muhogo baada ya kuchimba shambani.

  Kuanzishwa kwa mradi huo wa kusindika muhogo pamoja na bidhaa zake kumeliokoa zao hilo ambalo licha ya kuwa na manufaa makubwa kwa jamii, lakini limekuwa likidorora hata katika soko la vyakula.
  “Tangu tumeanzisha kikundi hiki miezi mitatu iliyopita hivi sasa muhogo hauwezi kuozea shambani na wananchi wanaona umuhimu wa zao hilo,” anasema Mama Abia Magembe, ambaye ni mratibu wa mradi huo.
  Mama Magembe, ambaye yeyé pamoja na akinamama wengine tisa walipatiwa mafunzo nchini Hispania kwa nia ya kuanzisha shughuli za ujasiriamali unaoendana na utunzaji wa mazingira pamoja na kupambana na mabadiliko ya tabianchi, anasema kwamba zao la muhogo sasa limepata thamani kubwa kijijini hapo na wana uhakika wakulima wa wilaya ya Kisarawe wanaweza kugeukia miradi kama hiyo ili kuongeza mnyororo wa thamani.
  Akinamama 10 wanaofanya miradi mbalimbali ya ujasirimali kupitia mradi wa Green Voices wanatoka mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Kigoma, Kilimanjaro, Pwani na Mwanza.Silvera Mujuni, Ofisa Chakula na Lishe wa Wilaya ya Kisarawe, anasema kwamba wilaya hiyo ina fursa kubwa ya kusindika na kuchakata mazao mengi yatokanayo na muhogo kwa kuwa zao hilo ndilo kuu kwa chakula na biashara.
  Anasema kwamba, ardhi katika vijijini vingi vya wilaya hiyo inastawisha muhogo kwa wingi, hivyo ikiwa wananchi watajizatiti na kujifunza namna ya kuchakata bidhaa za muhogo wanaweza kupata faida kubwa kiuchumi.
  “Muhogo ndilo zao kuu katika maeneo mengi ya wilaya hii ambayo haiwezi kustawisha mazao mengine kama mahindi, hivyo ni vyema wananchi wakajifunza utengenezaji wa bidhaa mbalimbali zinazotokana na zao hilo,” anasema Bi. Silvera aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Wilaya hiyo na ambaye ndiye alikuwa akiwafundisha akinamama hao namna ya kutengeneza bidhaa mbalimbali.

  Diwani wa Kata ya Msimbu, Amina Lilomo, akizungumza na akinamama wa kikundi cha Kitanga Green Voices wakati wa uzinduzi wa mradi huo katika Kijiji cha Kitanga hivi karibuni.
  Mshiriki kiongozi wa Kitanga Green Voices Women Group, Mama Abia Magembe, akiwahamasisha wanawake wenzake katika uzinduzi huo.

  Awali Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Wazir Yakoub Wazir, aliwataka akinamama hao wajipange wasajiliwe rasmi ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na serikali na taasisi nyingine za binafsi.
  “Ofisi yangu iko wazi wakati wote, mkitaka kwenda kusajiliwa wilayani hata leo niko tayari kuwasaidia, nawaombeni mje niwasaidie hata namna ya kuandaa katiba ya kikundi pamoja na taratibu nyingine,” alisema.
  Naye Diwani wa Kata ya Msimbu, Anna Lilomo, amesema atajitahidi – kwa kushirikiana na diwani mwenzake wa viti maalum Mossy Sultan Kufurumbaya – kuwapigania akinamama hao kwenye vikao vya Baraza la Madiwani ili waweze kupatiwa misaada na mikopo hata kupitia katika asilimia 10 ya bajeti ya halmashauri ambayo hulenga kuwasaidia wanawake na vijana.
  “Bahati nzuri sisi hapa ni madiwani wanawake, kwa hiyo tutalipeleka suala la akinamama hawa kwenye Baraza la Madiwani na kuelezea umuhimu wa kuongeza thamani kwenye zao letu la muhogo ili limkomboe mkulima,” alisema Diwani Lilomo.Mratibu wa Mradi wa Green Voices nchini Tanzania, Bi. Secelela Balisidya, anasema kwamba anafarijika anapoona wanawake wakihamasika kushiriki shughuli za maendeleo, hasa ujasiriamali unaolenga kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
  “Suala la kuhakikisha uhakika wa chakula, kutokomeza umaskini, kuwawezesha wanawake kiuchumi na mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ni mambo yaliyopewa kipaumbele katika Malengo Endelevu ya Dunia, hivyo wanawake wanaotekeleza miradi ya Green Voices wanayatekeleza malengo hayo kwa wakati mmoja,” anasema Secelela.

  Diwani wa Kata ya Msimbu wilayani Kisarawe, Amina Lilomo (kushoto) na Diwani wa Viti Maalum, Mossy Sultan Kufurumbaya, wakiwa makini kusikiliza maelezo kuhusu namna ya kusindika bidhaa mbalimbali kutokana na zao la muhogo.
  Akinamama wa Kitanga Green Voices wakiwa katika picha ya pamoja na mwandishi Tukuswiga Mwaisumbe (kilemba cha njano).

  Muhogo ni zao linalochukuliwa na wengi kama la ziada hasa kwenye ukame, lakini wengi hulifanya kama mlo wa hamu bila kutambua kwamba zao hilo lina manufaa makubwa kwa lishe na kibiashara.
  Wengi wanauchukulia muhogo kama chakula cha maskini, hawa wale wanaojitiahidi kulima zao hilo, huyapa kipaumbele mazao mengine kuliko muhogo.
  Lakini muhogo ni zao mojawapo ambalo linaweza kuiepusha jamii na baa la njaa huku katika baadhi ya mataifa likitumika kama chanzo cha nishati ili kukabiliana na bei ya mafuta na nishati nyinginezo.
  Baa la njaa ni tatizo kubwa linalozikumba nchi nyingi barani Afrika, Tanzania ikiwa miongoni mwazo, lakini licha ya watu kuhimizwa kulima muhogo, bado wanalipuuza zao hilo na kuliona kama zao fulani la mizizi tu.
  Katika mikoa kama Lindi na Mtwara ambayo kwa miaka mingi inalima kwa wingi muhogo, chakula chao kikuu kilikuwa ugali wa muhogo.
  Licha ya kudharauliwa kwa zao hilo, lakini siyo ajabu ukakuta mlo wa siku hiyo umetokana na muhogo kasoro chumvi na nazi, kwani inawezekana kuni zilizopikia ni matawi ya muhogo, ugali wa muhogo na kisamvu cha muhogo!
  Na wakulima wengi katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara wanakula ugali wa muhogo pale wanapokosa unga wa mahindi, ambapo wanaokula ugali huo wa muhogo (Wazaramo wanasema ‘bada’ na Wamakua wanauita ‘matamba’) huonekana maskini wa kutupa.
  Leo hii wanapohamasishwa kulima muhogo kwa sababu ya kustahimili ukame, bado wengi wanasuasua, lakini watakapoambiwa kwamba unga wa muhogo unatoa bidhaa nyingi zenye faida kubwa, huenda wengi wakaligeukia zao hilo na kulima kibiashara.Inafurahisha sana siku hizi kuona watu wengi wakikimbilia ugali wa muhogo hata hotelini, lakini hiyo bado haijatosha kulirasimisha zao hilo ili liwe na tija kubwa.
  Akinamama wa Kijiji cha Kitanga wanaweza kuwa mabalozi wazuri wa zao hilo, kwa sababu tayari wameanza kutengeneza bidhaa mbalimbali ambazo hata wananchi wa kijiji hicho wameshangazwa nazo baada ya kuzionja na kuona ubora wake.
  Kilimo cha muhogo siyo tu kitasaidia kukuza pato la mkulima, lakini kinaweza pia kuokoa mazingira pamoja na kuisaidia Tanzania kuokoa karibu Dola za Marekani 20 milioni sawa na Shs. 42 bilioni zinazotumika kuagiza chakula nje, jukumu ambalo kikundi cha Kitanga Green Voices kimeamua kulibeba.

  Mashine hizi ndizo zinazotumika kuuponda muhogo na kuucharanga kama chips. Kila kijiji kikiwa nazo kinaweza kutengeneza unga bora wa muhogo ambao utazalisha bidhaa mbalimbali.
  Mihogo ikiwa imeandaliwa tayari kwa kuchakatwa kwenye mashine. 


  Faida za muhogo ni nyingi kama zilivyoelezwa hapo juu, lakini kwa msisitizo ni kwamba, unga wake hutumika kutengeneza vyakula mbalimbali, baadhi ni uji na ugali, vitafunwa kama keki, mikate, skonzi, biskuiti, mandazi, mafuta ya lishe, sabuni ya unga, kuni, mboga, huksi pamoja na bidhaa nyingine nyingi.
   
  Mazao yanayopatikana katika mzizi wenyewe, miti na majani huweza kuzalisha bidhaa anuwai za viwandani kama vifaa vya nguo, karatasi, mafuta, kilevi, dawa za binadamu na plastiki wakati ambapo wanga hutumika kutengeneza dawa za madoa, gundi katika samani, rangi za awali za ukuta na sukari (sugar syrup). 
  Takwimu za kilimo cha muhogo duniani zinaonyesha kuwa, Afrika ni bara la tatu duniani kwa kuzalisha zaidi muhogo ambapo huzalishaji takriban tani milioni 102.6 kila mwaka.
  Tanzania ni nchi ya nne kati ya wazalishaji wakubwa wa muhogo barani Afrika baada ya Nigeria, Ghana na Kongo DRC ambapo inaelezwa kwamba karibu ekari 670,000 za ardhi ya kilimo zinatumika kuzalisha muhogo, zao linalochangia karibu asilimia 15 za chakula kwa nchi nzima ambapo karibu kaya 1,213,958 huzalisha muhogo nchini.
  Mikoa inayozalisha muhogo kwa wingi ni Mwanza, Mtwara, Lindi, Shinyanga, Tanga, Ruvuma, Mara, Kigoma, Pwani na maeneo yote ya Zanzibar. Ukanda wa Ziwa ni wazalishaji wakubwa zaidi ikifuatiwa na ukanda wa kusini. Mkoa wa Ruvuma huzalisha kati ya 5-10% ya uzalishaji wote Tanzania. Muhogo ndilo zao la pili kwa kuchangia pato la taifa kwa asilimia 19 baada ya  mahindi. 
  Taarifa ya Shirika la Utafiti wa Viwanda na Maendeleo ya Mazao ya Chakula Tanzania (TIRDO) inaonyesha kuwa zao la muhogo linastawi kirahisi.
  Hii ni pamoja na kuvumilia ukame na halishambuliwi na magonjwa au wadudu wanaoathiri mazao mengine na pia muhogo unaweza kutoa mazao mengi katika ardhi duni ambayo mazao kama mahindi hayawezi kustawi.
  Kwa mujibu wa TIRDO, muhogo ni zao la pili kuwa na wanga mwingi baada ya viazi vitamu ambavyo vina asilimia 20 hadi 30 ya wanga na kwamba asilimia 84 ya zao hilo hutumika kama chakula cha binadamu.  Baadhi ya bidhaa zinazozalishwa kutokana na unga wa muhogo. Hii ni kazi nzuri ya kikundi cha akinamama wa Kitanga Green Voices katika Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe.
  Mchanganyiko wa mihogo, maharagwe, mboga za majani na nyama. Ni chakula kizuri sana hiki chenye aina nyingi za vitamin, wanga na protini.

  PENGINE unafahamu faida tatu au nne tu za muhogo ambazo ni kuutafuna mbichi, kuuchemsha au kuuchoma; unga wake kwa ajili ya lishe, majani yake kama mboga ya kisamvu na dawa pamoja na miti yake inapokauka kutumika kama kuni.
  Inawezekana hujui kama maganda ya mihogo baada ya kumenywa ni chakula bora cha mifugo yakikaushwa au mabichi.
  Siyo ajabu pia hufahamu kwamba muhogo ukitwangwa mbichi na kuchujwa, maji yake yake yanatoa wanga (starch) ambao hutumika kutengeneza dawa za madoa, gundi katika samani, rangi za awali za ukuta na sukari (sugar syrup) na pia ni lishe nzuri.

  Lakini zao la muhogo ni zaidi ya linavyofikiriwa kwa sababu licha ya faida hizo chache, lakini pia linazalisha bidhaa zaidi ya 300 kama ambavyo akinamama wa Kijiji cha Kitanga, Kata ya Msimbu wilayani Kisarawe wameamua kufanya.
  Akinamama hao kupitia kikundi chao cha Kisanga Green Voices mbali ya kuzalisha unga pamoja na chips, sasa wanatengeneza bidhaa lukuki zenye ubora kama chapati, maandazi, skonzi, biskuti, tambi, cassava chop, na nyinginezo nyingi.
  Hatua hiyo imekuja baada ya kupatiwa mafunzo kupitia mradi wa Green Voices unaofadhiliwa na taasisi ya maendeleo ya wanawake wa Afrika inayojulikana kama Women for Africa Foundation, ambayo iko chini ya Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania, María Teresa Fernández de la Vega.

  0 0  Rais msataafu wa Serikali ya awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kulia akiuliza jambo kwa afisa wa Shirika la maendeleo ya Petroli nchini juu ya utendaji kazi mbalimbali wa shirika hilo.
  Rais msataafu wa Serikali ya awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kulia akiuliza jambo kwa afisa wa Shirika la maendeleo ya Petroli nchini juu ya matumiza ya gesi katika uendeshaji wa mitambo ya magari.
  Rais msataafu wa Serikali ya awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katikati akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wakati alipofanya ziara ya kutembelea maonesho ya kimataifa ya sabasaba.
  Mjasiriamali ambaye hakujulikana jina lake akimueleza jambo Rais Mstaafu Mh. Dkt. Jakaya Kikwete jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali wakati wa maonesho ya biashara ya kimataifa yanayoendelea jijin Dar es Salaam jana


  Rais msataafu wa Serikali ya awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katikati akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wakati alipofanya ziara ya kutembelea maonesho ya kimataifa ya sabasaba.
  Mke wa Rais wa Awamu ya tatu mama Anna Mkapa akimsikiliza Rais Msataafu ya awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete wakati wa maonesho ya kibiashara ya kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

  Kwa hisani ya www.habari360.com

  0 0


  MKUU wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga,Godwin Gondwe amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanawekeza kwenye kilimo kikubwa cha kisasa ambacho kitakuwa na tija kwao ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo na kukuza uchumi.

  Gondwe alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wafanyabiashara, viongozi wa dini ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka kuona umuhimu wa kutumia fursa ya uwepo wa rutuba nzuri ya ardhi iliyopo wilayani humo kujikita kulima kisasa ili kuweza kupata mafanikio.

  Alisema kuwa lazima wafanyabiashara watambue kuwa kilimo ndio njia pekee ambayo inaweza kuwainua kiuchumi na kuharakisha kasi ya ukuaji wa maendeleo iwapo watazingati na kukipa kipaumbele kila wakati

  “Niwaombeni suala la kilimo mlipe msukumo mkubwa sana kwani hii ndio njia pekee ambayo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wilaya yetu “Alisema.

  Aidha pia alisisitiza umuhimu wa wananchi wa wilaya hiyo kutilia mkazo kulima mazao yanayostahimili ukame ikiwemo Alizeti, Ufuta,Viazi na Mihogo ili kuweza kukabiliana na tatizo la kutoku patikana mvua za uhakika kwa ajili ya kilimo cha mahindi.

  “ Ninajua katika kipindi hiki tumelima kwa wingi lakini hali ya hewa sio nzuri na mvua nazo zimekuwa hazipatikana kwa uhakika hivyo lazima wakulima tubadilike kwa kuanza kupanda mazao yanayostahimili ukame ili kuweza kuepukana na baa la njaa “Alisema DC Gondwe.

  Sambamba na hayo,Mkuu huyo wa wilaya alizishauri taasisi za kibenki wilayani humo kuhakikisha zinatoa kipaumbele kwa wawekezaji wa kilimo ili waweze kuzalisha kwa wingi mazao ambayo yataweze kuinua kiuchumi lakini pia kuchangia pato la Taifa.

  Hata hivyo ,Mkuu huyo wa wilaya alitumia pia fursa hiyo kuwaasa wakulima waliopata mazao kidogo kuhakikisha wanayatunza na kuacha kuyauza kwani kufanya hivyo kutaweza kusababisha hali ya njaa kwao

  Naye Sherhe wa wilaya ya Handeni, Shabani Mohamed alisema kuwa wao watamuombea dua Mkuu huyo wa wilaya ili mungu amuwezeshe kuweza kutimiza majukumu yake ipasavyo na kusaidia kuchangia juhudi za maendeleo kwa wananchi.

  “Nikuambie Mh Mkuu wa wilaya ujio wako hapa Handeni watu wengi wamefurahi sana kwani uchapakazi wako unafahamika tokea ulipokuwa unafanya kazi kwenye kituo cha ITV na tunaamini uhodari huo pia utasaidia kuinua uchumi wetu “Alisema.

  Alisema kuwa wao watahakisha wanampa ushirikiano wa hali ya juu ili kumuwezesha kutekeleza vema majukumu yake ya kuipa maendeleo wilaya hiyo.

  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0

  Kampuni ya ORIFLAME imezindua bidhaa zake mpya kwenye soko la Afrika Mashariki ambapo vipodozi maalum vitakavyokufanya ngozi yako kuonekana yenye kukaa na safi wakati wote kwa ngozi imeingia dukani kwa sasa.

  Bidhaa hiyo maalum ni ya kusaidia ngozi kung’aa ambapo watumiaji wa bidhaa za ngozi wameshahuriwa kutumia bidhaa hiyo kwani imetengenezwa kwa vitu halisi ikiwemo matunda,mimea na majani ya hasili na kufanya ngozi kuwa katika hali ya afya wakati wote wa matumizi.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Bi. Mary Riung amebainisha kuwa, bidhaa hizo zitasaidia watu wengi kwani zimetengenezwa kwa ubora.

  “Bidhaa hizi ni nzuri kwani zitakufanya kuweka ngozi yako kuwa nzuri ikiwemo kuondoa makunyanzi, kuondoa madoa na kufanya kuwa na rangi moja usoni. Ni bidhaa bora na itapatikana kwetu pekee katika soko la hapa Tanzania na Afrika Mashariki” alieleza Mary Riung.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bwana Piyush Chandra amebainisha kuwa, kampuni hiyo ambayo ilianzishwa tokea 1967 imekuwa ni miongoni mwa makampuni yanayofanya vizuri katika bidhaa zake na watu wengi wametokea kuipenda hivyo kwa bidhaa zao zote wanazotengeneza zimeendelea kuwa na ubora Duniani kote.

  Miongoni mwa bidhaa zao ni pamoja na NovAge ambayo imetengenezwa mahususi kumfanya mtumiaji ambaye ngozi yake imeonekana kuzeeka na endapo ataitumia vipodozi hivyo vitamfanya kumuondolea hali hiyo na kuonekana safi kama kijana kwani inaondoa makunyanzi ndani ya kuanzia wiki 12 huku ikiwa imethibitishwa na wataalamu kwa kuongeza ‘collagen kwa asilimia 200.

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha mshomba, (wapili kulia), akimpatia maelezo mwananchi huyu, Tobist Machenje, (kulia), wakati alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Afoisa Matekelezo wa Mfuko huo Gladness Madembwe, Afisa Uhusiano, Zaria Mmanga, Afisa wa Fedha, Edward Kerenge na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Fulgence Sebera.

  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha mshomba, (pichani katikati), akimpatia maelezo mwananchi huyu  Tobist Machenje, (kulia), wakati alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Fulgence Sebera

  Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakiongozwa na Meneja Masoko na Uhusiano Costantina Martin, (watatu kushoto). Wakwanza kulia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Fulgence Sebera
  .


  Mshomba akizungumza jambo na Suzanne Ndomba-Doran

   
  NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

  MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha Mshomba, ametembelea mabanda ya wadau wa Mfuko huo ili kubadilishana mawazo na kuelewa shughuli za wadau hao, kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

  Sambamba na kutembelea mabanda hayo Mshomba pia aliungana na wafanyakazi wake, katika kutoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la WCF na kuwaeleza shughuli za Mfuko huo ulioanzishwa mwaka mmoja uliopita na ushiriki wa maonyesho hayo ni wa kwanza kwa Mfuko huo.

  Miongoni mwa mabanda aliyotembelea Mkurugenzi huyo ni pamoja na lile la Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Chama cha Waajiri Tanzania, (ATE), Mfuko wa Pensheni wa PSPF, GEPF, na UTT-PID. Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ulianzishwa kwa sheria namba 20 ya mwaka 2008 iliyorejewa mwaka 2015 ya Fidia Kwa Wafanyakazi. Na kazi kubwa ya Mfuko huo ni kutoa Fidia kwa Mfanyakazi aliyeumia au aliyepata magonjwa wakati akitekeleza majukumu yake ya kazi.


  Wafanyakzi wa WCF wakiwa kwenye banda la Mfuko huo, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Edward Kerenge, Zaria Mmanga, na Aly Sheha
  Afisa wa Fedha wa WCF, Edward Kerenge, (kulai), akiwapatia maelezo wananchi waliofika kwenye banda la Mfuko huo
  Mshomba(kulia), akisindikizwa na Meneja Masoko na Uhusiano wa PSPF, Costantina Martin, baada ya kutembelea banda la Mfuko huo
  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, (katikati), akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba, (kushoto) na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Fulgence Sebera, wakati Mshomba kutembelea banda la PSPF
  Mshomba akitembelea banda la UTT-PID
  Mshomba akisalimiana na wafanyakazi wa GEPF alipotembelea banda lao
  Mshomba akipitia jarida la Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), huku akipatiwa ufafanuzi na Meneja wa huduma za Kisheria wa ATE, Suzanne Ndomba-Doran, wakati alipotembeela banda la ATE. Kulia ni Mratibu wa mradi wa NHO, Joyce Nangai
  Mshomba akitembeela banda la OSHA
  Mshomba akiuliza kitu kwa maafisa hawa wa UTT-PID alipotembelea banda la taasisi hiyoEdward Kerenge, akiwapatia maelezo wananchi hawa waliotembelea banda la WCF


  Afisa Uhusiano wa WCF, Zaria Mmanga, (kulia), akimpatia maelezo, mwananchi huyu aliyefika banda la Mfuko huo kujua shughuli zake
  Afisa wa Fedha wa WCF, Grace Tarimo, (kulai), akimpatia amelezo ya shughuli za Mfuko, mwananchi huu aliyetembelea banda la Mfuko kujua kazi zake
  Afisa wa Fedha wa WCF, Grace Tarimo, (kulai), akimpatia amelezo ya shughuli za Mfuko, mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko kujua kazi zake

  0 0


  Watangazaji wa Kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa na Kituo cha redio cha TimesFm ya jijini Dar, Sandra Temu na Raheem wakiongoza mjadala maalumu wa utakaoibua hoja ya kutatua changamoto ya ajira nchini, ambapo mjadala huo umeandaliwa na Kituo cha Timesfm redioni ndani ya kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 kamili usiku. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.


  BAADHI ya wanafunzi wa elimu ya Juu kutoka katika vyuo mbalimbali jijini Dar es Salaam, wakimsikiliza kwa makini Mtangazaji wa kipindi cha Campus Vybez katika mjadala maalumu wa utakaoibua hoja ya kutatua changamoto ya ajira nchini, ambapo mjadala huo umeandaliwa na Kituo cha Timesfm radion ndani ya kipindi cha Campus Vybez kinachorushwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 kamili usiku.

  Mc Pilipili akitoa kibwagizo mara baada ya kukaribishwa.
  Mc Pilipili akijitambulisha kwa vijana, pembeni yake ni Ron Fidanza, Naibu waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Mavunde.  Msimamizi Mkuu wa radio ya TimesFm Ron Fidanza.  Mhadhiri wa Lugha wa Chuo cha Ualimu DUCE, Mhe. Ruben Ndimbo akijitambulisha.  Mmoja wa waalikwa akijitambulisha.  Meza mkuu.
  0 0  Washindi katika picha ya pamoja
  Johari Hamisi akimpokelea bed sheet Hawa Maulid ambaye hakufika kutoka kwa Mhariri wa gazeti la Championi Jumamosi, Elius Kambili .
  Mc aliyeendesha mchakato wa bahati nasibu hiyo tangu ilipoanza miezi 6 iliyopita, mc chaku shemungia naye akifurahia simu aliyokabidhiwa kama shukrani ya kundesha mchakato huo vizuri
  Mc Chaku shemungia akimuhoji Mhariri wa gazeti la Championi Jumamosi, Elius kambili baada ya kumaliza mchakato wa kugawa zawadi
  Mshindi wa king'amuzi, Wilbert Jacob akihojiwa na wanahabari baada ya kukabidhiwa king'amuzi chake

   
  Mwakilish wa Ting, Betty Bonzon akimkabidhi king'amuzi cha Ting, mshindi Wilbert Jacob

   
  Mwalishi wa Ting, Betty Bonzon (kushoto) akimkabidhi kingamuzi na dishi, Edward Mwakapila kwa niaba ya mshindi Baltazari Mrosso


   
  Dadi Tematema akimpokelea dinner set Herman Haule

   
  Dadi Tematema akitoa ushuhuda wa ndugu yake aliyekuja kumpokelea zawadi aitwae Herman Haule jinsi alivyokuwa akiyasoma Magazeti ya Global naye alivyokuwa akimuona anajisumbua

   
  Dadi Tematema akitoka nje ya ofisi za Global na zawadi ya dinner set aliyompokelea ndugu yake, Herman Haule

   
  Ester Josephat akionesha zawadi alizompokelea kaka yake, Godfrey Josephat

   
  Ester Josephat akionesha zawadi alizompokelea kaka yake, Godfrey Josephat.  PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL

  0 0

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi anapenda kuwataarifa wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya walioteuliwa tarehe 07 Julai, 2016 kuwa watakapofika Ikulu Dar es salaam kwa ajili ya kula kiapo cha uadilifu wa uongozi wa umma siku ya Jumanne tarehe 12 Julai, 2016 wahakikishe wanakuja na nakala zao halisi za vyeti vya kitaaluma (Original Academic Certificates).

  Ieleweke kuwa uhakiki wa vyeti halisi vya kitaaluma (Original Academic Certificates) unafanywa kwa lengo la kujiridhisha baada ya mchakato wa kawaida wa uhakiki kufanywa kwa kutumia vyeti visivyokuwa halisi (Photocopies).

  Uhakiki huu wa vyeti utaanza saa mbili asubuhi na wahusika wote mnaombwa kuingia Ikulu kwa kupitia geti kuu la lililopo upande wa mashariki (Upande wa Baharini)

  Tafadhari zingatia maelekezo haya.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  09 Julai, 2016

  0 0


  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Frank Charles Msaki kutokana na makosa ya kufanya malipo hewa yaani kulipa posho ya chakula kwa watu ambao si askari.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizarani hapo ambayo nakala tumeipata, Mhasibu Mkuu huyo Bw. Frank Msaki anasimamishwa kazi kwa kufanya malipo ya kiasi cha sh. 305,820,000 kama posho ya chakula kwa watu ambao sio askari kwa kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014 hadi 2015/2016.

  Meja Jenerali Rwegasira amesema kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Kijeshi anayetakiwa kulipwa posho ya chakula yaani ‘ration allowance’ ni askari peke yake na si mtu mwingine yeyote yule.Meja Jenerali Rwegasira amesema anamsimisha kazi Mhasibu Mkuu huyo tangu leo tarehe 9 Julai, 2016 ili kupisha uchunguzi ufanyike juu ya tuhuma zinazomkabili.

  Katibu Mkuu huyo amesema baada ya jalada la uchunguzi kufunguliwa na Ukaguzi Maalumu kufanywa na Mkaguzi wa Ndani wa Jeshi la Polisi imebainika kuwa mbinu mbalimbali zimetumika ili kufanikisha malipo hayo hewa.

  0 0


  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua rasmi semina ya wadau wa barabara mjini Arusha.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa semina ya wadau wa barabara iliyoanza leo mjini Arusha.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara hiyo sekta ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga kabla ya ufunguzi rasmi wa semina ya wadau wa masuala ya barabara mjini Arusha.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda kushoto akijadiliana jambo na mkuu wa mkoa wa Singida Mathew Mtigumwe kulia walipokutana katika semina ya wadau wa masuala ya barabara.
   Wadau wa masuala ya barabara wakifuatilia kwa makini mijadala katika semina ya mikataba ya muda mrefu ya kupima huduma itolewayo na  barabara na matokeo yake inayoendelea mjini Arusha.

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa wa pili kushoto akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha (AICC), wa pili kulia ni katibu mkuu wizara hiyo sekta ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga na wa kwanza kushoto ni mkuu wa mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda.
  Imetolewa na kitengo cha habari na mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewataka wahandisi na makandarasi nchini kujielimisha vya kutosha kuhusu mfumo mpya wa ujenzi wa barabara wa mikataba inayopima huduma zinazopatikana kwenye barabara hizo.

  Mfumo huo ambao unaotumiwa na nchi zilizoendelea utawawezesha makandarasi nchini kujenga barabara kwa mkataba wa muda mrefu wa kupima huduma ya barabara na mkandarasi atalipwa kulingana na matokeo.

  Akifungua semina ya wadau wa barabara kutoka nchi 19 na taasisi 30 duniani inaofanyika jijini Arusha Prof. Mbarawa amesema utaratibu huo mpya utawawezesha makandarasi kujenga barabara za kiwango cha juu zenye ubora na usalama na kupunguza utaratibu wa ukarabati wa kila wakati unaogharimu serikali fedha nyingi.

  “Ukijenga barabara kwa viwango vya juu na ukiisimamia mwenyewe kwa muda mrefu itapunguza gharama za ukarabati wa kila mwaka zinazotolewa na serikali” amesema Prof. Mbarawa
  Profesa Mbarawa amekiri uwepo wa changamoto kubwa kwenye ujenzi na ukarabati wa barabara za wilaya na kusisitiza kwamba barabara nyingi zinajengwa chini ya kiwango na hazina uwiano na thamani ya fedha zilizotumika.

  “Serikali inajipanga kuanzisha wakala wa barabara za wilaya utakaohakikisha unafanya kazi kama ilivyo kwa wakala wa barabara kuu na za mikoa ili kuongeza ufanisi” amesema Prof. Mbarawa
  Profesa Mbarawa amepongeza Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) kwa kazi nzuri ya kusambaza fedha za ujenzi wa barabara katika halmashauri zote kwa wakati na kuwataka viongozi wa halmashauri hizo wazitumie fedha hizo kwa kazi zilizokusudiwa.

  “Atakayecheza na fedha za mfuko wa barabara hatutakuwa na uvumilivu naye, tunataka fedha hizo zifanye kazi iliyokusudiwa ili adhma ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 kwa kuwa na miundombinu bora ifanikiwe” amefafanua Prof. Mbarawa.

  Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, sekta ya ujenzi Eng. JOSEPH NYAMHANGA amesema semina hiyo ya siku tano inawaleta wataalam wa barabara nchini kujadili changamoto na mafanikio ya mfumo mpya ya ujenzi wa barabara na mfumo huo utakapoanza utapunguza gharama za ujenzi na kuwaongezea nguvu makandarasi wazawa.   

  Amesema Tanzania ina takribani ya km 87,481 za mtandao wa barabara ambapo km 35,000 ni barabara kuu na za mikoa, km 52, 581 ni barabara za wilaya ambapo zote zitanufaika na mfumo huo utakapoanza.

  Naye meneja wa bodi ya mfuko wa barabara Joseph Haule amesema utaratibu huu mpya utakapoanza nchini utapunguza gharama za ujenzi wa barabara kwa asilimia 30 na utanufaisha wahandisi na makandarasi wengi nchini kutokana na sera nzuri ya kuwalinda makandarasi wazawa.

  Takribani wataalam 200 wa masuala ya barabara kutoka nchi za Afrika, Ulaya na Amerika wanashiriki katika semina hiyo inayoongozwa na mwenyekiti wa shirikisho la masuala ya barabara Bw. Kiran Kapila lengo likiwa ni kubadilishana uzoefu katika masuala ya ujenzi wa barabara bora kwa gharama nafuu.

  Imetolewa na kitengo cha habari na mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0

  MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imetoa hukumu ya shauri la kikatiba la kupinga vifungu vya sheria ya ndoa, 1971 vilivyokua vinaruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa chini ya miaka 18. 

  Mahakama Kuu ya Dar es Salaam, Julai 8 mwaka huu kupitia shauri la Rebeca Z Gyumi vs A.G Miscellaneous case No. 5 of 2016, ilitamka kuwa vifungu vya sheria ya ndoa namba 13 na 17 vya sheria ya ndoa vinakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 na kuweka umri wa miaka 18 kama umri wa chini wa kuoa/kuolewa. Vifungu hivyo vilikua vinaruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa ridhaa ya mahakama na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi wake, na hivyo kukinzana na sheria mbalimbali ambazo zinamlinda mtoto. 

  Mahakama Kuu pia imeipa serikali maagizo chini ya mwanasheria mkuu wa serikali, kuwa imeshabadili sheria hii ndani ya mwaka mmoja na kuweka umri wa miaka 18 kama umri wa chini kwa msichana na mvulana kuindia kwenye ndoa.

  Kesi hii ya Kikatiba ilifunguliwa na Rebeca Gyumi, Mkurugenzi wa shirika la Msichana Initiative, linalofanya kazi ya kutetea haki ya mtoto wa kike kupata elimu na kujiendeleza, kupitia kwa wakili Jebra Kambole wa Law Guards Advocate.

  Rebeca alikua akidai vifungu hivi vinamnyima msichana haki yake ya kusoma na ni kinyume na ibara ya 12, 13 na 18 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zinatoa haki ya usawa mbele ya sheria, kutobaguliwa , kuheshimu utu wa mtu na haki ya uhuru wa kujieleza. 

  Hukumu hii imesomwa na Jaji Ataulwa Munisi kwa niaba ya jopo la majaji watatu waliokua wanasikiliza kesi hii. Wengine ni Jaji Kiongozi Shaban Lila na Sakiet Kihiyo.

  Jaji Munisi alisema vifungu hivyo ni batili na kwamba vinaenda kinyume na Katiba kwa kuwa mtoto wa miaka 14 hawezi kuingia katika ndoa na hana ufahamu wa kujihusisha na mambo ya ndoa. Jaji pia aliongeza kuwa vifungu hivyo vimepoteza thamani yake na havitimizi tena lengo  lilikosudiwa wakati vinawekwa. Hivyo kuamuru umri wa kuolewa uwe kuanzia miaka 18 na kuendelea. 

  Tanzania ni moja ya nchi zenye idadi kubwa ya ndoa za utotoni duniani. UNFPA wanasema kwa wastani wasichana wawili kati ya watano nchini Tanzania huolewa kabla hawajatimiza miaka 18. Pia wanasema zaidi ya asilimia 37 ya wasichana wenye kati ya umri wa miaka 20 na 24 waliolewa au kuingia kwenye mahusiano ya kindoa kabla ya kutimiza miaka 18. 

  Ndoa  za utotoni nchini Tanzania huathiri zaidi wasichana. Kwa wastani wanawake wa  Tanzania huolewa zaidi ya miaka 5 mapema zaidi kuliko wanaume. Sheria ya ndoa, 1971 ilikua inaruhusu mwanaume kuoa kuanzia miaka 18 na wasichana waliruhusiwa kuolewa kuanzia miaka 14. 

  0 0

  Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, Evelyne Mushi (kushoto) akimkabidhi baba wa watoto pacha wanee, Abednego Andrew Mafuluka mkazi wa Kimara Mwisho, Dar es Salaam mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 ikiwa ni msaada kwa mapacha hao wanne. Benki ya NMB imewafungulia akaunti za watoto kwa kila mtoto na kuwawekea shilingi cha shilingi milioni 10, kuwasaidia wazazi na watoto hao hapo baadaye. Wa pili kulia ni mama mzazi wa mapacha hao, Sara Dimosso akiwa kabeba watoto wake huku akisaidiwa na nduguye. Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, Evelyne Mushi (kushoto) akimkabidhi baba wa watoto pacha wanee, Abednego Andrew Mafuluka mkazi wa Kimara Mwisho, Dar es Salaam mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 ikiwa ni msaada kwa mapacha hao wanne. Benki ya NMB imewafungulia akaunti za watoto kwa kila mtoto na kuwawekea shilingi cha shilingi milioni 10, kuwasaidia wazazi na watoto hao hapo baadaye. Wa pili kulia ni mama mzazi wa mapacha hao, Sara Dimosso akiwa kabeba watoto wake huku akisaidiwa na nduguye.Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, Evelyne Mushi (kushoto) akimkabidhi mama mzazi wa watoto wanne mapacha, Sara Dimosso (kulia) mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 ikiwa ni msaada kwa watoto mapacha wanne aliojifungua hivi karibuni. Benki ya NMB imewafungulia akaunti za watoto kwa kila mtoto na kuwawekea shilingi milioni 10 ikiwa ni kuwasaidia wazazi na watoto hao hapo baadaye. Katikati ni baba wa watoto pacha wanee, Abednego Andrew Mafuluka akishiriki kupokea msaada huo. Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, Evelyne Mushi (kushoto) akimkabidhi mama mzazi wa watoto wanne mapacha, Sara Dimosso (kulia) mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 ikiwa ni msaada kwa watoto mapacha wanne aliojifungua hivi karibuni. Benki ya NMB imewafungulia akaunti za watoto kwa kila mtoto na kuwawekea shilingi milioni 10 ikiwa ni kuwasaidia wazazi na watoto hao hapo baadaye. Katikati ni baba wa watoto pacha wanee, Abednego Andrew Mafuluka akishiriki kupokea msaada huo.Mama mzazi wa watoto mapacha wanne, Sara Dimosso (kulia) pamoja na mume wake, Abednego Andrew Mafuluka (katikati) wakipiga picha ya pamoja na mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 iliyokabidhiwa na Benki ya NMB ikiwa ni msaada kwa watoto mapacha wanne aliojifungua hivi karibuni. Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, Evelyne Mushi mara baada ya kuwakabidhi, Benki ya NMB imewafungulia akaunti za watoto kwa kila mtoto na kuwawekea shilingi milioni 10 ikiwa ni kuwasaidia wazazi na watoto hao hapo baadaye.  Mama mzazi wa watoto mapacha wanne, Sara Dimosso (kulia) pamoja na mume wake, Abednego Andrew Mafuluka (katikati) wakipiga picha ya pamoja na mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 iliyokabidhiwa na Benki ya NMB ikiwa ni msaada kwa watoto mapacha wanne aliojifungua hivi karibuni. Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, Evelyne Mushi mara baada ya kuwakabidhi, Benki ya NMB imewafungulia akaunti za watoto kwa kila mtoto na kuwawekea shilingi milioni 10 ikiwa ni kuwasaidia wazazi na watoto hao hapo baadaye.Baadhi ya maofisa wa Benki ya NMB wakiwa katika picha na familia ya Bwana na Bibi Abednego Andrew Mafuluka pamoja na watoto wao mapacha wanne mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya msaada.  Baadhi ya maofisa wa Benki ya NMB wakiwa katika picha na familia ya Bwana na Bibi Abednego Andrew Mafuluka pamoja na watoto wao mapacha wanne mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya msaada.
  Bwana Abednego Andrew Mafuluka (katikati) akizungumza kuishukuru Benki ya NMB baada ya kuguswa na kuamua kuwasaidia watoto wao mapacha wanne.  Bwana Abednego Andrew Mafuluka (katikati) akizungumza kuishukuru Benki ya NMB baada ya kuguswa na kuamua kuwasaidia watoto wao mapacha wanne.Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, Evelyne Mushi (kushoto) akizungumza kuelezea namna Benki ya NMB ilivyoguswa na kuamua kuwasaidia watoto hao mapacha wanne waliozaliwa pamoja. Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ubungo, Evelyne Mushi (kushoto) akizungumza kuelezea namna Benki ya NMB ilivyoguswa na kuamua kuwasaidia watoto hao mapacha wanne waliozaliwa pamoja.Mama mzazi wa watoto mapacha wanne, Sara Dimosso (kulia) pamoja na mume wake, Abednego Andrew Mafuluka akizungumza kuishukuru Benki ya NMB kwa kuwasaidia shilingi milioni 10 iwawezeshe katika malezi ya watoto hao. Mama mzazi wa watoto mapacha wanne, Sara Dimosso (kulia) pamoja na mume wake, Abednego Andrew Mafuluka akizungumza kuishukuru Benki ya NMB kwa kuwasaidia shilingi milioni 10 iwawezeshe katika malezi ya watoto hao.Baadhi ya maofisa wa Benki ya NMB wakiwa katika picha na familia ya Bwana na Bibi Abednego Andrew Mafuluka pamoja na watoto wao mapacha wanne mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya msaada.  Baadhi ya maofisa wa Benki ya NMB wakiwa katika picha na familia ya Bwana na Bibi Abednego Andrew Mafuluka pamoja na watoto wao mapacha wanne mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya msaada.


  0 0
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Enterberth Nyoni akitoa ufafanuzi kwa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kuhusu uboreshaji wa vyuo kwa kujitegemea wakati wa kikao kazi cha wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii mjini Dodoma.

  Baadhi ya Wakuu wa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii waliohudhuria Kikao Kazi mjini Dodoma wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kikao hicho leo mjini Dodoma.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw.Dickson Rusage akitoa ufafanuzi kwa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kuhusu matumizi mazuri ya rasilimali fedha, watu, utunzaji wa mali za Serikali na Utekelezaji wa dhana ya Utawala Bora katika Taasisi za Maendeleo ya Jamii leo mjini Dodoma.

  Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Eliasifu Mlay akitoa ufafanuzi kuhusu uzingatiaji wa Maadili katika Utumishi wa Umma wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii leo mjini Dodoma.

  Na.Aron Msigwa - Dodoma.

  Maafisa Maendeleo ya Jamii wanaohitimu mafunzo katika vyuo mbalimbali nchini na wale waliko kazini wametakiwa kuwa tayari kufanya kazi vijijini ili kuwawezesha wananchi kuzitumia fursa za maendeleo zilizoko katika maeneo wanayoishi kukabiliana na changamoto mbalimbali.

  Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Enterberth Nyoni wakati akitoa ufafanuzi kuhusu Utendaji Kazi wa Maafisa hao wakati wa kikao kazi cha wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii mjini Dodoma.

  Amesema Maafisa Maendeleo popote walipo lazima watambue kuwa wao ni dira na chachu ya mabadiliko ya kuwafanya wananchi kubadilika kwa kufanya kazi kulingana na mabadiliko na rasilimali zilizopo katika maeneo yao.

  Amesema kuwa dhana ya Maendeleo ya Jamii ni pana na ikilenga kuwafanya wananchi kutumia rasimali zinazopatikana katika mazingira yao kujiletea maendeleo akibainisha kuwa maafisa Maendeleo wanaozalishwa katika vyuo mbalimbali lazima washiriki kikamilifu katika katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu kwa kuwapatia elimu, ushauri na mbinu mbalimbali za kuondoa umaskini.

  Kuhusu ubora wa kiwango cha taaluma ya maendeleo ya Jamii inayotolewa katika vyuo mbalimbali amesema kuwa ipo haja ya kuendelea kujenga msingi imara vyuoni na kuandaa vigezo vya kuwapima maafisa maendeleo ya Jamii kwa kuangalia ufanisi wa utendaji kazi wao wa kila siku.

  Amefafanua kuwa jukumu kubwa la vyuo hivyo pamoja na mambo mengine ni kubadilisha mitazamo ya wanafunzi walioko vyuoni kwa lengo la kuwafanya kuwa chachu ya mabadiliko na kuwa msaada kwa wananchi wanaowatumikia.

  Kuhusu mafunzo kwa vitendo Bw.Enterberth amesema kuwa ipo haja kwa wanafunzi walio katika mafunzo kupangiwa mazoezi kwa vitendo katika maeneo ya vijijini kwa kuwa ndiko liliko chimbuko la shughuli Maendeleo ya jamii na kutoa wito kwa wahitimu hao kuwa tayari kufanya kazi katika mazingira ya vijijini.

  Aidha,amesema kuwa katika kufanya mabadiliko katika taaluma ya maendeleo ya jamii kitaanzishwa Chama au Bodi ya kitaaluma kusimamia wahitimu wanaomaliza katika vyuo mbalimbali kwa lengo la kupima uelewa, ubora na viwango kabla ya kuruhusiwa kuitumikia jamii.

  Akitoa ufafanuzi kuhusu mafunzo kwa maafisa maendeleo ya Jamii walioko kazini amesema kuwa Serikali inaendelea kulifanyia kazi jambo hilo kwa kuhakikisha kuwa mafunzo rejea kwa maafisa maendeleo ya jamii walioajiliwa yanatolewa ili maafisa hao waweze kwenda na kasi ya maendeleo na mabadiliko yanayotokea katika jamii.

  Kwa upande wao baadhi ya Wakuu wa vyuo hivyo wakizungumza kwa nyakati tofauti kuhusu namna bora ya kuboresha maslahi ya vyuo hivyo hususan kiwango cha taaluma inayotolewa wameiomba Serikali kwa kushirikiana na wanataaluma husika kuanzisha Bodi itakayosimamia suala la viwango na uhakiki wa wataalam wanaohitimu.

  Aidha, wamebainisha kuwa katika miaka ya hivi karibuni idadi ya wahitimu wa fani ya Maendeleo ya Jamii imeongezeka jambo linalotoa matumaini ya kukua kwa taaluma hiyo na kuiomba Serikali kuendelea kuweka vigezo vya udhibiti ili kulinda viwango vya huduma zinazotolewa.

  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, Miji, Manidpaa na Majiji 185 kabla ya hawajakula kiapo cha maadili ya viongozi leo Ikulu jijini Dar es salaam.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mkutano ulioitishwa  na Rais John Magufuli kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote za wilaya na baadhi ya Wakuu wa  wilaya  ikulu jijini Dar es salaam Julai 12, 2016.
  Wakuu wa wilaya za Kongwa Mhe deo Ndejembi (kushoto), Siriel Shaidi Mchembe (DC Gairo) na Mhe. Geoffrey Idelphonce Mwambe (DC Manyoni) wa kila kiapo cha maadili ya viongozi leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukosa kufanya hivyo na wenzao wiki iliyopita. 

  Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, Miji, Manispaa na Majiji 185 wakila kiapo cha maadili ya viongozi leo Ikulu jijini Dar es salaam.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa Tanga Martine Shigela akitoa taarifa ya changamoto za kisekta zinazoukabili Mkoa ikiwemo uhaba wa Maafisa Habari na Maafisa Michezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura (wakwanza kushoto)alipowatembelea katika ziara ya kikazi kwa lengo la kujua utekelezaji wa shughuli za kisekta katika mkoa huo,(wa kwanza kulia) Afisa Michezo Mkoa Bi. Digna Tesha.
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (Katikati) akizungumza wadau wa kisekta (hawapo pichani) leo Jijini Tanga katika ziara ya kikazi iliyokuwa na lengo la kujua utekelezaji wa shughuli kisekta katika Mkoa huo,(Kushoto)Mkuu wa Wilaya ya Tanga Bw.Thobias Mwilapwa na (kulia) Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe. Mustapha Selemani.
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akitoa maagizo ya kuanzishwa kwa Kamati za Michezo kuanzia ngazi ya Halmashauri kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga (hayupo pichani) leo Jijini Tanga alipokuwa katika ziara ya kikazi Mkoani hapo kufuatilia utekelezaji wa shughuli za kisekta ,(Katikati) Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe. Mustapha Selemani.


  Na Anitha Jonas – MAELEZO, Tanga.

  Serikali imeagiza Maafisa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mikoani kuanza kushirikishwa katika vikao vya maamuzi ili wapate kujua mikakati ya maendeleo kwa sekta zao.

  Agizo hilo limetolewa na Mheshimiwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Annastazia Wambura alipokuwa katika ziara ya kikazi Jijini Tanga kwa ambapo lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kufuatilia utekelezaji wa shughuli za kisekta kwa Wizara yake katika Mkoa huo.Mheshiwa Naibu Waziri Wambura alisema kushirikishwa katika vikao vya maamuzi kwa watendaji wa Kada hizo kutasaidia kuongeza chachu ya ukua wa sekta hizo katika mikoa pamoja na kutoa maoni ya kitaalum kwa sekta hizo kutoka kwao.

  “Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 mtenge bajeti ya Kitengo cha Habari na pia mfanye utaratibu wa kupata Maafisa Habari kwa kuanzia ngazi ya Mkoa,Wilaya ,Halmashauri,pamoja na Jiji kwani kada hii ni muhimu kuwepo kwa lengo lakusaidia kutangaza maendeleo na fursa zilizopo katika Mkoa wenu”,alisema Mhe .Wambura.

  Pamoja na hayo Mhe. Naibu Waziri Wambura aliendelea kusema Serikali inataka wananchi wapate kujua shughuli zote za maendeleo katika Mkoa wao zinafanyika vipi na mikakati ya maendeleo iko vipo,hivyo ni muhimu kupata Maafisa Habari watakao wasaidia kufanikisha hilo kazi ya kutoa habari hizo kwa umma.

  Aidha, Naibu Waziri huyo alisisitiza kuwa Wizara kwa sasa ipo katika mazungumzo na TAMISEMI kwa jili ya kubadili mfumo na kuanzisha Kurugenzi za kisekta kwa Maafisa Habari,Maafisa Utamaduni,Maafisa Sanaa na Maafisa Michezo katika ngazi za Mikoa lengo ikiwa ni kuimarisha sekta hizo.

  Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martin Shigela alisema Mkoa huo unakabiliwa pia na uhaba wa Maafisa Michezo ,Maafisa Utamaduni na Maafisa Sanaa katika Mkoa na Halmashauri lakini suala hilo tayari wameanza kulifanyia kazi kwa kufanya utaratibu wa kupata Maafisa hao.

  Halikadhalika naye Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini Bw. Thobias Mwilapwa alimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa ziara yake kwa kuwa ametoa somo zuri la utendaji na pia anaamini atafanyia kazi kilio cha wadau wa michezo wa mkoa huo kwani ni mmoja wapo katika historia ya Michezo ,pamoja na Muziki wa Mwambao (Taarabu) pamoja na Mchezo wa Mbio za Baiskeli.

  Pamoja na hayo naibu waziri huyo alitoa wito kwa wakazi wa Tanga katika kipindi wanapokuwa wakifanya shughuli za kimila na desturi kama za Jando na Unyago basi wawashirikishe wataalam wa Afya pamoja na wa Elimu kwa lengo la kutoa elimu ya afya ya uzazi halikadhalika kuelezewa umuhimu wa elimu katika maisha ya vijana wanaofanyiwa shughuli hizo.

  Hata hivyo wakazi wote wa mkoa wa Tanga wametakiwa kuongeza juhudi za kusimamia muenendo mzuri wa maadili ya kitanzania ikiwa ni jukumu la kila mtu pamoja na kufanya kazi kwa kujituma zaidi kama kauli mbiu ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya HAPAKAZI TU!

  0 0

  Hapa sasa ni Kazi Tu: Kocha wa Dar Swim Club, Michael  Livingstone akiwafanyika mazoezi ya kuchumpa (ku-dive) waogeleaji wa klabu hiyo. Waogeleaji hao walifanya tendo hilo kwa staili mbalimbali baada ya kupokea mafunzo kutoka kwa makocha wa klabu maarufu ya Hamilton Aquatics, Nebojsa Durkin na Katy Morris. 
   
   Mafunzo ya kuogelea siyo lazima yafanyikie kwenye maji. Hapa mkufunzi wa kimataifa wa mchezo wa kuogelea kutoka klabu ya Hamilton Aquatics, Nebojsa Durkin aionyesha kwa vitengo waogeleaji wa Dar Swim Club jinsi ya kuchumpa kwenye maji (ku-dive) katika mafunzo yaliyomalizika hivi karibuni kwenye shule ya Kimataifa ya DIA, Masaki.
   Mkufunzi wa kimataifa wa mchezo wa kuogelea kutoka klabu ya Hamilton Aquatics ya Dubai, Nebojsa Durkin aionyesha kwa vitengo waogeleaji wa Dar Swim Club jinsi ya kugeuka kwa kasi kwa kutumia  nguvu ya miguu katika mafunzo yaliyomalizika hivi karibuni kwenye  shule ya Kimataifa ya DIA, Masaki.
   
  Chama cha mchezo wa kuogelea nchini (TSA) kimeipongeza klabu ya Dar Swim Club (DSC) kwa kufanya semina ya kuendeleza mchezo huo kwa wachezaji na makocha iliyokuwa chini ya wakufunzi kutoka klabu ya Hamilton Aquatics ya Dubai. 

  Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa TSA, Ramadhan Namkoveka mara baada ya kutembelea mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la shule ya kimataifa ya DIA iliyopo Masaki jijini. 

  Mafunzo hayo yalikuwa chini ya wakufunzi wa kimataifa wa mchezo wa kuogelea wa klabu bingwa ya Mashariki ya Kati (Middle East) ijulikanayo kwa jina la Hamilton Aquatics ya Dubai, Nebojsa Durkin na Katy Morris.
  Mafunzo hayo yalidhaminiwa na kampuni za Alios Finance Tanzania, Europcar, DSC, DIA na kampuni ya utafiti na uchimbaji wa mafuta ya Maurel & Prom. 

  Wakufunzi hao walifuraishwa na viwango vya waogeleaji wa klabu hiyo pamoja na kukabiliana na changamoto mbalimbali za mchezo huo ikiwa pamoja na kukosa bwawa la mita 50 linalotambuliwa kimataifa.
  Namkoveka alisema kuwa wamefuraishwa na mafunzo hayo ambayo yaliwahusisha waogeleaji chipukizi (yoso) na wakubwa pia na makocha wa timu hiyo. Alisema kuwa wamevutiwa na jinsi mafunzo hayo yalivyokuwa yanaendeshwa na anaamini Tanzania itapata waogeleaji nyota kama wadau wa mchezo huo wataiga mfano wa DSC. 

  “Nimefuraishwa na jinsi mafunzo yalivyoendeshwa, kwa kweli nimevutiwa sana kwani nimeona jinsi waogeleaji chipukizi waliokuwa wanaanza kujifunza mchezo, waogeleaji wenye uelewa wa mchezo na makocha walivyokuwa wanapewa mafunzo, hii ndiyo njia sahihi ya kuendeleza mchezo huu,” 

  “Naamini, kama juhudi hizi zitaendelezwa, Tanzania itakuwa na waogeleaji wengi wenye ubora wa kimataifa katika miaka ijayo, mchezo wetu unahitaji sapoti kubwa sana ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea,” alisema Namkoveka. 

  Kocha wa Dar Swim Club, Michael Livingstone alisema kuwa wamepata mwanga mkubwa katika mafunzo hayo ambayo watayatumia katika kuendeleza mchezo katika klabu yao na kwa Taifa kwa ujumla.
  “Tumejifunza mbinu, ujuzi na mambo kadha wa kadha kuhusiana na mchezo wa kuogelea, kwa kifupi tumepata mwanga wa hali ya juu kwa ajili ya ufundishaji kwa waogeleaji yoso na wakubwa,” alisema. 

  Katibu Mkuu wa DSC, Inviolata Itatiro amesema kuwa wamepania kuweka historia nchini kwa kutoa waogeleaji bora na ndiyo maana waliamua kuendesha mafunzo hayo yaliyokuwa yanafanyika kwa mara ya pili. 

  “Tunahitaji sapoti katika mchezo huu, lengo ni kuona waogeleaji wanapata maendeleo makubwa kwa kufikia viwango, nawaopongeza wadhamini Alios Finance Tanzania, Europcar, DSC, DIA na kampuni ya utafiti na uchimbaji wa mafuta ya Maurel & Prom kwa kutuunga mkono, gharama za kuwaleta walimu kutoka nje ni kubwa sana,” alisema Inviolata.

  0 0


  Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Nchini Kenya, SJAK, Mbais Criss, akimkabidhi zawadi ya Kombe la mchezaji bora Nahodha wa timu ya TASWA QUEENS, Lightness Sirikwa Mayeye, baada ya kutangazwa mchezaji bora aliyejituma katika mchezo wao dhidi ya timu ya SJAK ya Kenya.

  Timu hizo zilizoshiriki katika Bonanza maalumu la Maadhimisho ya Siku ya Waandishi wa Habari Duniani, lililofanyika kwenye Uwanja wa Luna Park Jijini Nairobi Kenya Leo Julai 9, 2016, zilitoka sare ya 0-0 katika muda wa kawaida na kupigiana penati ambapo Taswa Queens waliibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 4-3. Picha na Mafoto Blog

  Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Nchini Kenya, SJAK, Mbais Criss, akimkabidhi Kombe la ushindi Kipa wa timu ya TASWA QUEENS, Somoe Ng'itu, baada ya timu hiyo kuifunga timu ya SJAK ya Kenya kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya timu hizo kutoka sare ya 0-0 katika muda wa kawaida.

  Timu hizo zilishiriki kwa pamoja katika Bonanza maalumu la Maadhimisho ya Siku ya Waandishi wa Habari Duniani, lililofanyika kwenye Uwanja wa Luna Park Jijini Nairobi Kenya Leo Julai 9, 2016.
  Kiungo wa timu ya Taswa Queens, Ester Zelamula (kulia) akimtoka mchezaji wa Sjak ya Kenya, Mercy Njue, wakati wa mchezo wa kirafiki katika Maadhimisho ya Siku ya Waandishi wa Habari Duniani, uliochezwa kwenye Uwanja wa Luna Park Jijini Nairobi Kenya Leo Julai 9, 2016. Katikati ni Lightness Sirikwa wa Taswa Queens akijiandaa kutoa msaada.
  Kiungo wa timu ya Taswa Queens, Ester Zelamula (kulia) akimtoka mchezaji wa Sjak ya Kenya, Mercy Njue, (katikati) Kushoto ni Lightness Sirikwa wa Taswa Queens akijiandaa kutoa msaada.
  Zelamula akiambaa na mpira baada ya mtoka Mercy Njue..
  Winga wa Taswa Queens, Angela Msangi (kulia) akipiga shuti huku beki wa Sjak ya Kenya, Rebecca Magoma, akijaribu kumdhibiti bila mafanikio.
  Lightness (kulia) akichuana kuwania mpira na Mercy

  Kipa wa Tswa Queens, Somoe Ng'itu akituliza mpira wakati wa mechi hiyo


  Lightness akiambaa na mpira

  Mtanange wa Taswa Fc dhidi ya Sjak ya Kenya ukiendelea. Katika mchezo huo Sjak waliibuka na ushindi.
  Mshike mshike langoni mwa Sjak....
  Julius Kihampa (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Sjak.

  Khadija Kalili wa Taswa Queens (katikati) akimdhibiti Eveline wa Sjak.

  Angela Msangi akipiga shuti.

  Angela Msangi akichuana kuwania mpira na beki wa Sjak Rebecca Magoma
  Ester Zeamula akifunga penati.

  Kipa wa Taswa Queens Somoe Ng'itu akiokoa penati ya Eveline

  Kipa wa Taswa akibebwa juu kwa furaha baada ya kuokoa penati moja iliyowawezesha kuibuka kidedea.
  Picha ya pamoja kabla ya kuanza mechi hizo..
  Mazoezi ya kupiga danadana kabla ya mchezo wao...
  Katibu wa Chama cha Waandoshi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa) Amir Mhando akizungumza na wachezaji wa Taswa kabla ya kuanza kwa michezo hiyo.
  Picha ya pamoja
  Picha ya pamoja

  Lightenss mazoezini

  Winga wa Sjak, Consolata Makokha (kushoto) akiambaa na mpira....
  Taswa Queens wakinyoosa misuri kabla ya mechi
  Muda wa mapumziko
  Kikosi cha Taswa Queens
  Muda wa mapumziko
  Picha ya pamoja na viongozi...

  Picha ya pamoja na wapinzani wao
  Wachezaji wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mtanange huo.
  Kikosi cha Taswa Fc
  Wachezaji wakisalimiana


  Taswa Queens wakishangilia baada ya kukabidhiwa kikombe chao
  Wakipozi kwa picha na Kombe lao baada ya kukabidhiwa.
  Afisa kutoka Kampuni ya Bia TUSKER, Samuel Nzau, akimkabidhi Kikombe cha ushindi, Naohidha wa Sjak ya Kenya, Alex Boke baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Wazee wa Taswa. Katikati ni Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) Amir Mhando.

older | 1 | .... | 905 | 906 | (Page 907) | 908 | 909 | .... | 1897 | newer