Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 904 | 905 | (Page 906) | 907 | 908 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Thursday, 7th July 2016 – Barakah The Prince, formerly known as ‘Barakah Da Prince’, has signed a full rights multi-year worldwide deal with the leading Pan African music entertainment group ROCKSTAR4000, and joins the company’s dynamic Record Label and Management divisions respectively.

  "I am so excited to start this new chapter in my music career with a great record label and management team, there is no doubt that this is the beginning of a very important partnership for me” noted Barakah The Prince.

  Barakah The Prince first priority will be to be to record his highly anticipated debut commercial album set for release in 2017. He has already started creating several singles he’s wanted to pen down and record since his earlier childhood years. Barakah The Prince will be the third artist from Tanzania to sign a full rights multi-year deal with ROCKSTAR4000 alongside East African superstars Alikiba (King Kiba) and Lady Jaydee (Queen Jide) making him the ‘Prince’ to this leading Pan African music entertainment company and ‘royal family’ of some of Africa’s biggest Rockstars.

  In a very short career to date, Barakah The Prince has already achieved stellar success with three ofhis recent singles - “Siachani Nawe”, “Nivumilie” and “Siwezi” - all charting straight to number one in Tanzania across both radio and TV charts making him the fastest rising star of the year in East Africa and the “Artist to Watch” as highlighted by music channel MTV base. Barakah The Prince continues to earn No. 1 singles on media charts and in addition received the accolade of walking away with the coveted trophy at the Kilimanjaro Tanzania Music Award for ‘Best Upcoming Artist in 2015’.

  “We are thrilled to welcome such as multi-talented star as Barakah The Prince to our family of Rockstars and embark on this journey together highly energized for an amazing musical journey” noted Jandre Louw, Founder & CEO, ROCKSTAR4000.

  “Barakah The Prince is without doubt a highly talented major rising star, with several mega hits already behind him, and we are excited to be part of this amazingjourney and partnership with him in taking his music and brand to even greater heights and to the legions of fans across East Africa, Africa and the world!” says Seven Mosha, Director of Talent & Music, ROCKSTAR4000.

  Fans can also follow Barakah The Prince on any of his official social media and digital networks:


  FOLLOW BARAKAH THE PRINCE AT:

  Facebook: www.facebook.com/BarakahThePrince
  Twitter: @BarakahThePrince
  Instagram: @BarakahThePrince

  SnapChat: BarakahThePrince

  For more on BARAKAH THE PRINCE contact:

  ROCKSTAR4000 DIRECTOR OF TALENT & MUSIC: Seven - seven@rockstar4000.com

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa EPZA Canal, Joseph Simbakalia akizungumza na wajumbe pamoja na wawekezaji kutoka jiji la Fuzohou nchini China jijini Dar es Salaam leo (kulia) ni mwakilishi wa ubalozi wa China nchini Tanzania, Sun Chengfeng anaeshughulikia maswala ya baiashara na uchumi ikiwa ni juhudi za uongozi wa EPZA kuunga mkono kauli mbiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Joseph Magufuli kufufua viwanda hapa nchini ili kukuza uchumi wa nchi yetu.

  0 0  Mr ALAF (kulia) akitoa zawadi kwa washindi kwa wa mchezo wa ALAF Wheel of fortune katika maonesho ya kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam waliotembelea banda la ALAF katika Maonesho ya 40 ya kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es salaam.
  Wananchi wakifuatilia maelezo kutoka kwa mhudumu wa ALAF juu ya ubora wa mabati ya ALAF katika maonesho ya 40 ya kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es salaam.

  0 0


  0 0


  Mtaalam kutoka Kampuni ya Kuendeleza Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Nyaso Makwaya (kulia) akielezea shughuli za kampuni hiyo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (wa pili kutoka kushoto) mara alipotembelea banda la TGDC.
  Mtaalam kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini Philip Mathayo (kushoto) akitoa maelezo juu ya sera ya madini kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (wa pili kutoka kulia) mara baada ya kuwasili kwenye banda la Wizara kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini Tanzania (STAMICO) Zena Kongoi (kulia) akielezea mikakati ya shirika hilo katika kuwasaidia wachimbaji wadogo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (kushoto)
  Meneja Uendelezaji Masoko na Teknolojia kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Advera Mwijage (kulia) akimwonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (katikati) matumizi ya majiko sanifu katika kupikia mara alipotembelea banda la REA. Kushoto kabisa ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Asteria Muhozya.
  Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Ally Mluge (kulia) akielezea muundo wa shirika hilo kwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (kushoto) mara alipotembelea banda la TPDC.


  Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe amekitaka Kitengo cha Dharura cha Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kufanya kazi kwa ubunifu ili kukabiliana na malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na wananchi mara kwa mara.

  Profesa Mdoe aliyasema hayo mara baada ya kufanya ziara katika banda la Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

  Alisema kuwa malalamiko ya wananchi juu ya ucheleweshaji wa huduma unaofanywa na kituo cha dharura cha TANESCO yamepelekea wananchi kuwa na taswira hasi juu ya shirika hilo. “Ninawataka kuwa wabunifu katika utendaji kazi wenu, kwa kutoa huduma kwa haraka kwa kuwa nyinyi ndio mliobeba taswira ya shirika,”alisema Profesa Mdoe.

  Wakati huo huo akizungumzia sekta ya madini nchini, Profesa Mdoe alisema kuwa Serikali imejipanga katika kuwawezesha wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwa wana mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

  Alisema kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Madini (SMMRP), Serikali imekuwa ikitoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo wa madini wanaokidhi vigezo. Alitaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na kuwa na leseni za uchimbaji madini, kuonesha kuwa wanaendesha shughuli za uchimbaji madini pamoja na ulipaji wa kodi serikalini.

  Alisisitiza kuwa Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), ipo tayari kuwasaidia wachimbaji wadogo kwa kuwapatia vifaa na mafunzo ili kukuza uzalishaji wa madini nchini na hivyo sekta hiyo kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi .

  0 0

  Ili kupambana na changamoto za ajira Nchini kama kijana hususani mwanafunzi wa elimu ya juu, unaitaji mbinu mbadala za kujikwamua kimaisha. #CampusVybez ya #TimeFm @timesfmtz @sandytemu @djj_one @ inakukutanisha wewe kijana na Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu kazi ajira na vijana Antony Mavunde, kuzungumzia mbinu za kujikwamua kwenye ajira @anthonymavunde Jumamosi hii Protea Hotel, saa mbili kamili asubuhi.

  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesitisha utoaji wa vibali vya uvunaji wa mbao kutoka katika mashamba nane ya miti ya kupandwa yanayosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

  Serikali  kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii inamiliki mashamba ya miti ya kupandwa 18, na kati ya hayo uvunaji umekuwa ukifanyika katika mashamba nane ambayo ni Sao Hill (Mufindi), Buhindi (Sengerema), Meru/Usa (Arumeru), West Kilimanjaro (Hai), Shume (Lushoto), North Kilimanjaro (Rombo), Kiwira (Rungwe) na Kawetire (Mbeya Vijijini).

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Julai 8, 2016) na kufafanua kwamba usitishaji huo unalenga kutathmini taratibu, kanuni na vigezo sahihi vinavyotakiwa kutumika katika kugawa malighafi kutoka kwenye mashamba hayo.

  Amesema wadau wote wa viwanda vinavyojikita katika malighafi ya misitu na hususan wamiliki wa viwanda vya kupasua mbao wanashauriwa kuwa watulivu wakati utaratibu huu ukifanyiwa mapitio na umma utatangaziwa rasmi pindi uboreshaji huo utakapokamilika.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  IJUMAA, JULAI 8, 2016.

  0 0


  0 0


  Ofisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano wa UTT-AMISMfaume Kimario (kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, James Doto alipotembelea Banda la Kampuni ya Uwekezaji Tanzania (UTT-AMIS) kwenye Maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Ofisa wa UTT AMIS kutoka Idara ya Uendeshaji, Said Mkomwa akitoa maelezo kuhusu faida ya uwekezaji wa pamoja.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PPF, William Erio akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Kampuni ya Uwekezaji (UTT-AMIS) katika maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Masoko na Uhusiano wa UTT-AMIS, Waziri Ramadhani na Ligwa Temela kutoka Idara ya Fedha na Utawala.
  Msajili wa Hazina Lawrence Mafuru akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la UTT-AMIS kwenye maonesho Biashara ya 40 ya Kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mwandamizi Idara ya Masoko na Uhusiano wa UTT-AMIS, Mather Mashiku.

  Baadhi ya watu wakiwa katika banda la UTT-AMIS.
  Ofisa Uendeshaji wa Kampuni ya Uwekezaji Tanzania UTT-AMIS, Lauren Chokola akitoa maelezo kwa watu waliofika katika banda la kampuni hiyo.

  0 0


  Dk. Charles Kimei akifurahia huduma za Mfuko wa Pensheni wa LAPF.
  Ofisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Habiba Kisaka akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB juu ya huduma wanazotoa.
  Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB pamoja na maofisa wa benki hiyo.  Ofisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Habiba Kisaka akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei alipotembela banda hilo.
  Dk. Kimei akisaini kitabu cha wageni katika banda la LAPF.
  Ofisa wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Lucia Chuwa akimkaribisha Dk. Kimei.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiangalia aina mbalimbali za simu katika banda la Halotel.
  Dk. Kimei akipata maelezo kuhusu mtandao wa Halotel unavyofanya kazi.
  Dk. Kimei akilipa fedha kwa ajili ya kununua simu ya Halotel.


  Mkurugenzi wa Kanda wa Kampuni ya Simu ya Halotel, Alex Thiem akimpa maelekezo Dk. Kimei kuhusu mtandao wa simu ya Halote.
  DK. kimei akipata maelezo alipotembelea Kampuni ya Total.
  DK. kimei akisaini kitabu cha wagei katika banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  Dk. Kimei na ujumbe wake wakiwa katika banda la Chuo Kikuu.
  Dk. Anold Towo kutoka Kurugenzi ya Huduma za Jamii Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.

  Dk. Kimei akiangalia saa yake wakati akitoka katika banda la Chuo Kikuu.
  Dk. Kimei akipokea zawadi.
  Dk. Kimeia akisaini kitabu katika banda la Kampuni ya Property.
  Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Property, Saleh Omary akimuonesha Dk. Kimei picha mbalimbali za viongozi waliotembelea banda hilo.
  Dk. Kimeia akiangali Pampu ya kisima.
  Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma za kifedha katika tawi linalotembea lililopo katika viwanja vya Sabasaba. 

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiwasili katika banda la CRDB kwenye Maonesho ya Sabasabasa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisalimiana na wafanyakazi wa benki hiyo alipofika katika banda la CRDB kwenye Maonesho ya Sabasabasa.
  Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei alipotembelea banda la CRDB katika Maonesho ya Sabasaba.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiwa katika banda la CRDB.
  Dk. Kimei akishuhudia wateja wakihudumiwa.
  Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya benki hiyo yaliyopelekea benki ya CRDB kupata tuzo ya mshindi katika sekta ya mabenki wakati alipotembelea maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya benki hiyo yaliyopelekea benki ya CRDB kupata tuzo ya mshindi katika sekta ya mabenki wakati alipotembelea maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

  Wateja wakipata huduma.

  0 0


  Meneja mahusiano Kituo cha Uwekezaji (TIC) Daud Riganda akizungumza leo jijini Dar na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la kibiashara kati ya Tanzania na India linalotarajiwa kufanyika julai 10 mwaka huu, ambalo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. Kulia ni Meneja Uhamasishaji Uwekezaji wa Nje Zacharia Kingu


  WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la kibiashara kati ya Tanzania na India linalotarajiwa kufanyika julai 10 mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja mahusiano wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Daud Riganda amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuwaleta pamoja wafanyabiashara wa nchi hizo mbili kwa ajili ya kujadiliana na kubadilishana uzoefu katika masuala ya biashara na uwekezaji.

  Amesema Tanzania na India ni nchi zenye ushirikiano wa muda mrefu katika masuala ya kisiasa, kijamii na kibiashara hivyo ujumbe wa wafanyabiashara kutoka India utajumuisha sekta za kilimo, viwanda, miundombinu, elimu, afya, nishati na maji.

  Riganda amesema kati ya mwaka 1990 na Juni 2016 TIC imeweza kusajili jumla ya miradi 442 ya uwekezaji kutoka India yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 2.12.

  Alisema miradi hiyo inayoongoza katika kusajiliwa ni ile iliyopo katika sekta ya viwanda na usindikaji ambapo takribani asilimia 53 ni miradi ya kutoka sekta hiyo.Pia alisema kongamano hilo limeandaliwa na TIC kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi nchini(TPSF), Jukwaa la Biashara la India(IBF) na Shrikisho la Biashara na Viwanda la India(FICCI).

  Alisema makampuni kutoka India ni miongoni mwa mataifa yanayoshika nafasi ya tano za juu kiuwekezaji hapa nchini kwa kuzingatia thamani katika uwekezaji.Hata hivyo aliwataka wafanyabiashara kushiriki kikamilifu katika kongamano hilo ili kujijengea uwezo na kuweza kufikia malengo ya sekta ya uwekezaji kupitia viwanda.

  0 0


  Na Daudi Manongi, MAELEZO

  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa sikukuu za Eid al Fitr na Sabasaba zilisababisha ukosefu wa nishati ya Petroli Mkoa wa Mtwara na kuathiri wa baadhi ya shughuli za maendeleo.

  Hatua hii ilitokana na wamiliki wengi wa ‘deport’ za mafuta kufunga kwa ajili ya kushiriki sikukuu hizo.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja Mawasiliano na Uhusiano (EWURA) Bw.Titus Kaguo wakati wa mahojiano na Idara ya Habari(MAELEZO) wakati akitoa ufafanuzi juu ya uhaba wa tatizo hilo katika Mkoa wa Mtwara lililoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

  Alisema kuwa hivi sasa hali ya upatikanaji wa nishati hiyo imerejea kwani vituo vingi vimeanza kuuza nishati hiyo baada ya sikukuu hizo kumalizika.

  Bw.Kaguo alisema kuwa kutokana na biashara hiyo kuendeshwa na watu binafsi na wahusika hao kushiriki sikukuu hiyo ilisababisha kusimama kwa shuguli hiyo, hatua ilivifanya baadhi ya vituo kukosa nishati ya mafuta na kushindwa kufanya kazi katika kipindi hiki cha sikukuu.

  Aidha amewahakikishia wananchi kuwa kwa sasa nishati ya Petroli na Dizeli ipo kwa wingi kwani kwa siku ya jumanne dizeli lita milioni (5) tano ziliuzwa ukilinganisha na matumizi ya nchini ya siku ambayo ni lita milioni 4.8 na kwa Petroli lita zilizouzwa ni milioni 3.6 ukilinganisha na matumizi ya nchi nzima ya petroli ya lita milioni 2.8. kwa siku.

  Aliongeza kuwa toka jumanne vituo kama Lake Oil,Tsn na Central belt vimeendelea kutoa huduma kama kawaida kwa wananchi wa Mkoa wa Mtwara.

  Mji wa Mtwara siku ya Jumatano ulikumbwa na uhaba wa mafuta ya Petroli na hivyo kufanya wakazi wa mji huo kununua nishati hiyo kwa bei ya ulanguzi toka lita shilingi 1950 hadi kufikia shilingi 2500 kwa lita jambo liloathiri shughuli za maendeleo ya wananchi.

  0 0  Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena (wa pili kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani moja ya majarida ya utalii ya TTB yaliyopo katika Banda la TTB.

  Geofrey Meena, Meneja Masoko wa TTB akimwelezea Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Eng. Makani amna ambavyo TTB inavyotumia mbinu mbalimbali katika kutangaza vivutio vya Utalii vya Tanzania ndani na nje ya nchi.
  Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa TTB Bw. Philip Chitaunga(wa pili kulia ) akitoa maelezo kuhusu namna tuvuti maalumu ya Utalii (Online Tourism Portal) inavyofanya kazi na inavyoweza kutumiwa na wadau wa utalii kwa Naibu Waziri Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani huku afisa wa TTB Bw. Francis Malugu akisaidia kuonyesha kurasa za tovuti hiyo .

  Naibu Waziri Eng. Ramo Makani akisisitiza jambo kuhusu tovuti maalumu ya Utalii baada ya kupata maelezo kuhusu tovuti hiyo kutoka kwa maafisa wa TTB.


  Na: Geofrey Tengeneza

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani ameipongeza Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kazi nzuri inayoifanya katika kuitangaza Tanzania kama eneo bora la Utalii Duniani kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo tovuti maalumu ya utalii (Online Tourism Portal) na Nyenzo maalumu ya kutangaza utalii wa tanzania kupitia simu za mkononi ( Tanzania Tourism App).

  Naibu Waziri huyo ametoa pongezi hizo alipotembelea Banda la Bodi ya Utalii Tanzania lililopo ndani ya jingo la Wizara ya Maliasili na Utalii katika viwanja vya Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.

  “ Kwa hakika mnafanya kazi nzuri sana katika kutangaza vivutio vyetu vya utalii, endeleeni na juhudi hizo” alisema Naibu Waziri mara baada ya kupata maelezo mafupi kuhusu mbinu zinazotumiwa na TTB katika kuitangaza Tanzania kama eneo Bora la Utalii Duniani.

  0 0
 • 07/08/16--07:04: MILIMA YA RORYA MKOANI MARA


 • Na BMG

  Ni muonekano wa milima ambayo inapatikana katika Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Mita chache Kutoka Mto Mara ukiwa unatoka au unaelekea wilayani Tarime, ukitokea maeneo mbalimbali katika barabara ya Musoma-Tarime.

  Maajabu ya milima ambayo iko pande zote mbili za barabara si kwamba yanatisha, la hasha. Ni maajabu ambayo ni ya kufurahisha kiukweli hususani ukiwa safarini ambapo ukiitazama utaona namna inavyorudi nyumba na kufanya abiria kuhisi uumbaji wa Mungu uliotukuka katika hii dunia.

  Ujenzi wa barabara iliyopinda mithiri ya nyoka katikakati ya milima hii huifanya kuwa kivutio kingine japo kwa abiria waoga wakifika katika milima hii sara huwa inaongezeka maana si mchezo hususani likija suala la mpando huwa ni mpando kweli, na likija suala la mtelemko huwa ni mtelemko kweli kwani ikiwa wewe ni muoga basi huweza hata chungulia nje japo ukweli ni kwamba ukichungulia nje utaona uzuri wa kipekee katika milima hiyo.

  Kikubwa tunaomba shughuli za kibidanamu zisiiathiri milima hii (mfano katika picha) maana ni tegemeo kwa wanamara na sote twajua umuhimu wa milima kama hii ambayo ina uwepo mkubwa wa mistu ya asili.

  Tazama HAPA Picha Zaidi

  0 0


  Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akigawa chakula kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Maunga kilichopo Kinondoni Hananasifu Jijini Dar es salaam katika kusherekea sikukuu ya Iddi.
  Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akijumuika pamoja katika chakula cha pamoja na watoto hao wanaolelewa katika kituo cha Maunga kilichopo Kinondoni Hananasifu Jijini Dar es salaam .

  ILI watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu waweze kutimiza ndoto zao za kimaisha , Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda ameiasa jamii kujenga utamaduni wa kutembelea vituo vinavyowalea watoto hao sanjari na kutatua changamoto wanazokabiliana nazo hatua itakayowasaidia kufikia malengo hao.

  Ametoa rai hiyo juzi mara baada ya kujumuika pamoja katika chakula cha pamoja na watoto hao wanaolelewa katika kituo cha Maunga kilichopo Kinondoni Hananasifu Jijini Dar es salaam ambapo pia alitoa misaada mbalimbali ya yakiwemo madaftari, kalamu, sabuni,vyakula na fedha kwa ajili ya kusaidia mahitaji ya kituo hicho.

  Alisema watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu wanapaswa kupata elimu kama ilivyo kwa watoto wengine wanaoishi na wazazi wao hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuona umuhimu wa kutoa chochote alichonacho ili kuwawezesha watoto hao kuipata elimu hiyo kwa ukamilifu.

  “Tunashukuru kwa sasa Rais John Magufuli ametoa unafuu wa elimu bure kwa watoto katika ngazi ya msingi na Sekondari kwa hiyo kilichopo hapo ni mahitaji madogo madogo ili kumfanya mtoto aweze kufika shuleni na kuudhuria masomo, kama jamii hili ni jambo linalowezekana kabisa tukalitatua kama kila mmoja wetu atakuwa na nia” alisema Mwenda

  Aidha katika hatua nyingine Mwenda ameahidi kutoa huduma ya mahitaji ya shule kwa watoto wanaosoma darasa la sita hadi sekondari waliopo katika kituo hicho ili kukipunguzia mzigo kituo hicho katika suala linalohusiana na masomo Mbali na hilo pia ameahidi kununua vitanda kwa ajili ya watoto hao na kuvifanyia ukarabati vitanda vilivyoharibika baada ya kuombwa na uongozi wa kituo hicho kutatua tatizo hilo lililodumu kwa muda mrefu kituoni hapo.

  Kwa upande wake Mlezi wa kituo hicho Zainabu Maunga alisema dhumuni la kuanzishwa kwa kituo hicho chenye jumla ya watoto 50, lilikuwa kutoa msaada wa malezi kwa watoto hao waliopatikana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya vifo vya wazazi wao.

  Alisema kituo hicho kinalea watoto hao wakiwemo wavulana 26 na wasichana 24 kwa kutegemea misaada ya watu mbalimbali wanaofika kituoni hapo huku akitaja changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika malezi ya watoto hao.

  Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ufinyu wa eneo la kituo, mavazi kwa watoto, chakula pamoja na huduma za afya pale inapotokea mtoto kaugua hatua inayomfanya kupaza sauti yake kwa jamii kila siku akiomba imsaidie kutatua changamoto hiyo.

  MWISHO

  0 0  Meneja wa banda la Benki ya NMB katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2016, Josephiner Kulwa (kushoto), akimkaribisha Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete alipotembelea banda hilo Dar es Salaam leo asubuhi.
  Hapa Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
  Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo.
  Meneja wa banda la Benki ya NMB katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2016, Josephiner Kulwa (kushoto), akitoa maelezo kwa Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.
  Rais mstaafu Jakaya Kikwete (katikati), akitoka katika banda la Benki ya NMB alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2016 yanayoendelea katika viwanja vya Biashara vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo . Kulia ni Meneja wa banda hilo, Josephiner Kulwa na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka. Maonesho hayo yatafikia tamati kesho kutwa.


  (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com

  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(Katikati) akiongea na wadau wa utamaduni kutoka UNESCO  pamoja na Idara ya Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni katika  kikao cha kujadili mpango mkakati wa miaka mitano wa  maendeleo ya Utamaduni nchini,leo jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kulia) akimsikiliza Afisa Utamaduni kutoka UNESCO Bw.Louise Crayssac katika kikao cha kujadili mpango mkakati wa miaka mitano wa  maendeleo ya Utamaduni nchini,leo jijini Dar es Salaam.
    Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kulia) akimsikiliza Afisa Utamaduni kutoka UNESCO Bw.Halvor Storrusten katika kikao cha kujadili mpango mkakati wa miaka mitano wa  maendeleo ya Utamaduni nchini, jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kulia) akimsikiliza Afisa Utamaduni kutoka UNESCO Bi.Halvor Rehema Sudi katika kikao cha kujadili mpango mkakati wa miaka mitano wa  maendeleo ya Utamaduni nchini, jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kulia) akiwa katika picha na wageni kutoka UNESCO na Idara ya Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa baada ya kumalizika kikao kilichokuwa kikijadili mpango mkakati wa miaka mitano wa  maendeleo ya Utamaduni nchini,leo jinini Dar es Salaam.

  0 0  Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ephraim Kwesigabo (kulia) akitoa taarifa ya mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Julai, 2016 mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es salaam ambapo mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 5.5 kutoka asilimia 5.2 mwezi uliopita kushoto ni Mtakwimu Bw. Opiyo mamu.
  Waandishi wa Habari wakifatilia kwa makini maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ephraim Kwesigabo hayupo pichani akitoa taarifa ya mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Julai, 2016 leo Jijini Dar es salaam.PICHA NA ALLY DAUD-MAELEZO.

  Na Ally Daud-Maelezo

  Mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Juni, 2016 umeongezeka hadi asilimia 5.5 kutoka asilimia 5.2 mwezi uliopita kutokana na kuongezeka kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephaim Kwesigabo amesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei kumesababishwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi.

  “Mfumuko wa bei umesababishwa na kuongezeka kwa bei za vyakula kama vile mahindi ambayo yameongezeka kwa asilimia 3.2, unga wa muhogo kwa asilimia 2.4, samaki wabichi kwa asilimia 3.8, maziwa mgando kwa asilimia 4.3, maharage mabichi yaliyomenywa kwa asilimia 6.1, kitunguu swaumu kwa asilimia 12.5, njegere kwa asilimia 6.2, viazi mviringo kwa asilimia 2.5, mihogo mibichi kwa asilimia 6.7, magimbi kwa asilimia 4.5, na ndizi za kupika kwa asilimia 2.7,” amesema Kwesigabo.

  Amesema bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na huduma ya kinywa na meno ambayo imeongezeka kwa asilimia 13.8, mafuta ya dizeli kwa asilimia 2.4 na mafuta ya petroli kwa asilimia 4.3. Kwesigabo amesema mfumuko wa bei wa mwezi Juni, 2016 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.5 ongezeko sawa na mwezi uliopita.

  Aidha amesema mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka wa bidhaa za vyakula majumbani na migahawani umeongezeka hadi asilimia 8.3 mwezi Juni, 2016 kutoka asilimia 7.2 mwezi Mei, 2016. Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 103.47 mwezi Juni, 2016 kutoka 103.00 mwezi uliopita.

  Kwesigabo amesema uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia Shilingi 96 na senti 65 mwezi Juni, 2016 kutoka mwezi Disemba, 2015.

  0 0


  Waziri wa Habari, sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnaye akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya magari jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Habari, sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnaye akiwa amenyanyua bendera ya Taifa juu kuashiria uzinduzi wa Mashindano ya Mbio za Magari ya 2016 jijini Dar es Salaam leo .Kulia kwa Nape ni Katibu wa Balaza la Michezo Tanzania(BMT), Mohamed Kiganja. 

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
  WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amezindua mashindano ya magari ya hapa nchini  ya 2016 na kuwataka watazania kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye mchezo huo ambapo amewataka kuacha kujiweka nyuma na kuitwa kichwa cha mwendawazimu kila siku. Hayo ameyasema wakati akizindua mashindano hayo ya magari yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho wilaya ya Bagamoyo ikihusisha magari 25.

  Nape amesema kuwa wanachotaka kuona ni kuwa Tanzania inafanya vizuri kwenye mashindano hayo na zaidi wanataka kuona wanazidi kuwavutia wageni kwenye mashindano hayo ili kuongeza utalii wandani na kuongeza pato kwa serikali pale watakapoamua kutembelea mbuga za wanyama. 

  “Nawataka watanzania kuzidi kufanya vizuri kwenye mashindano na zaidi wawavutie wageni kwani watakapokuja kwa wingi wataongeza pato la taifa pale watakapotembelea hifadhi za taifa,”amesema. 

  Naye  Rais wa chama cha Magari Tanzania (AAT), Bwana Nizar Jivani amesema kuwa mwaka jana waliweza kuondoa kauli ya kichwa cha mwendawazimu na walilitekeleza kama walivyomuahidi Raisi mstaafu wa awamu ya Pili Ally Hassan Mwinyi na mwaka huu watazidi kufanya vizuri na watabakisha ushindi nyumbani. Mashindano hayo yamezingatia viwango vyote ambapo jumla ya magari 25 yatashiriki ambapo kati  ya magari hayo, Magari 4 yatatoka Uganda, 2- Zambia, Kenya (1), Falme za Kiarabu (1). Na kwa magari ya kutoka Tanzannia ni  17.

  Magari hayo  17  ya Tanzania ambapo  Dar es Salaam  magari 10, Arusha (3), Moshi (3), na Tanga (1). Aidha, magari hayo yanatarajiwa kushindana katika umbali wa kilometa 246 kwa siku ya kwanza na yatakuwa kwa muda wa siku mbili.

  0 0


  Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati mkutano wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) juu ya utekelezaji wa agizo la kusitisha usajili bodi za wadhamini, Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RITA, Emmy Hudson (Kulia) akitoa taarifa ya utekelezaji wa agizo la Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Harrison Mwakyembe la kusitisha usajili wa bodi za wadhamini leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome.
  Sehemu ya wajumbe wa bodi wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam.
  (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwa wakati wa uchguzi mkuu kumekuwa na utitiri wa vikundi ambavyo havionekani kazi zake na mwisho wa siku vinaomba msamaha wa kodi.

  Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwakyembe amesema kutokana na utitiri wa vikundi hivyo aliagiza Wakala wa Usajili ,Ufilisi na Udhamini (RITA), kusitisha usajili wa vikundi hivyo na kufanya uchambuzi ni vikundi ambavyo viko hai na vina vigezo kwa mujibu wa sheria.

  Amesema kufanya usajili wa vikundi ambavyo kimsingi hafifanyi kazi iliyokusudiwa mwisho wa siku kuna uwezekano wa kusajili vikundi ambavyo ni hatarishi kwa taifa.

  Aidha amesema kuwa kutokana na uchambuzi ambao umefanywa na kubainika kuwepo kwa vikundi 180 ambavyo vinatakiwa kufutwa kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya bodi za udhamini.

  Mwakyembe baada uchambuzi huo ameitaka RITA kuendelea na kazi usajili bodi za wadhamini kwa kufuata taratibu zote na kuwa na taarifa zao.

  Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (RITA), Emmy Hudson amesekuwa katika uchambuzi huo kuna changamoto ambazo zilijitokeza ikiwa baadhi bodi za wadhamini kubadili ofisi pamoja na kubadili majina bila kufuata sharia.

  Amesema kuwa bodi za wadhamini wengine wanamiliki mali bila kufuata sheria kwa mujibu sheria za RITA.

older | 1 | .... | 904 | 905 | (Page 906) | 907 | 908 | .... | 1896 | newer