Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 906 | 907 | (Page 908) | 909 | 910 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Tulia Akcson amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ulioongozwa na Spika Mhe Zuberi Ali Maulid na kuahidi kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo baina na Vyombo hivyo viwili vya kutunga sheria.

  Akizungumza na ugeni huo uliomtembelea kwa lengo la kufahamiana na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi Naibu Spika amesema ili mahusiano ya Vyombo hivi viwili yaboreke zaidi kuna haja ya kuwa na mafunzo ya pamoja ili kuweza kukabiliana na changamoto zinazojitokeza ambazo nyingi zinafanana.

  Naibu Spika aliongeza pia kuwa Bunge la Jamhuri ya Muuumgano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar ni Vyombo vinavyofanya kazi zinazofanana hivyo kujifunza na kubadilishana uzoefu ni jambo la muhimu katika katika kuboresha utendaji kazi.


  Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson akizungumza na Ugeni kutoka Baraza la Wakilishi Zanzibar walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Ugeni huo uliongozwa na Spika wa Baraza la Wakilishi Zanzibar Mhe Zubeir Ali Maulid.
  Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson akimsikiliza Spika wa Baraza la Wakilishi Zanzibar Mhe Zubeir Ali Maulid wakati alipofanya mazungumzo naye Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam
  . Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson akizungumza na Spika wa Baraza la Wakilishi Zanzibar Mhe Zubeir Ali Maulid( katikati) pamoja na Naibu Spika wa Baraza la Wakilishi Mhe Mgeni Hassan Juma (kulia) walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.( Picha na Ofisi ya Bunge.
  Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson (katikati ya waliokaa) katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Baraza la Wakilishi Zanzibar wakiongozwa Spika wa Baraza la Wakilishi Zanzibar Mhe Zubeir Ali Maulid (wa pili toka kulia).
  “Mahusiano tuliyonayo yanawekewa nguvu tunapokuwa na mafunzo yale ya pamoja kwa sababu fursa inapatikana ya kubadilishana uzoefu lakini pia kujifunza mambo kwa pamoja kuliko kukiwa na uendeshaji ambao ni tofauti sana wakati Vyombo hivi vinafanya kazi inayofanana,” alisema Naibu Spika wakati akizungumza na Ugeni huo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

  Dkt Tulia pia ametumia fursa hiyo kumpongeza Spika na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi kwa kuchaguliwa kushika nyadhifa hizo na kusema kuwa Bunge lipo tayari kutoa ushirikiano wakati wowote utakapohitajika.

  Kwa upande wake Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid amesema Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kitu kimoja hivyo wameona ni muhimu kuja kusalimiana, kufahamiana na kuimarisha mahusiano yaliyopo ili kurahisisha utendaji kazi wa Vyombo hivyo.

  Adiha alisema kuwa Baraza la Wawakilishi litaendelea kujifunza na kuomba ushauri toka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ili hilo lifanikiwe kuna haja ya kuboresha zaidi mahusiano ya mihimili hiyo miwili ya kutunga sheria.

  Pia Mhe. Maulid amempongeza Naibu Spika Dkt Tulia kwa umahiri wake wa kupambana na changamoto zilizojitokeza wakati wa uendeshaji vikao vya Bunge na kusema kuwa kuna mambo mengi wamejifunza kutoka kwake. Pamoja na Watendaji wengine wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Spika wa Baraza hilo aliamabatana pia na Naibu Spika wa Baraza Mhe Mge

  0 0


  Pichani wa kwanza kushoto ni Afisa ustawi wa jamii ambaye pia ni msimamizi wa mahabusu ya watoto mkoa wa Arusha Mussa Mkamate akiwa anabadilishana jambo na baadhi ya wajumbe wa Jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Arusha mara baada yakukabidhi magodoro kama msaada katika mahabusu hiyo.

  Na Woinde Shizza wa globu ya jamii Arusha

  Kamati ya utekeleza ya wazazi wa CCM wilaya ya Arusha leo wamekabidhi jumla ya magodoro 25 katika mahabusu ya watoto iliyopo jijini hapa ikiwa ni ahadi walioiweka ya kusaidia baadhi ya changamoto zilizopo katika mahabusu hiyo.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhi magodoro hayo mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni meneja masoko wa Radio ya Triple A iliopo jijjini Arusha Phidecia Mwakitalima alisema kuwa hii ni mara ya tatu wao kama kamati ya wazazi wa wilaya kukabidhi msaada huo kwani mara ya kwanza walishatoa chakula na mashuka kwa ajili ya watoto hao na sasa hivi wameamua kuwaletea msaada wa magodoro.

  Alisema kuwa magodoro hayo 25 yametokana na msaada ambao wao kama kamati ya wazazi waliuomba kwa wadau mbalimbali ambapo katika wadau hao kampuni ya magodoro ya Tanform iliopo arusha iliwaunga mkono na kuamua kuwapa magodoro hayo kwa ajili ya watoto hao wa mahabusu ya watoto Arusha.

  Aidha Phidecia alimalizia kwa kutoa wito kwa wadau mbalimbali ,wafanyabishara ,viongozi pamoja na wananchi kujijengea tabia ya kutembelea mhabusu mbalimbali za watoto zilizopo hapa nchini ili kuweza kugundua changamoto walizo nazo watoto hao na kuweza kuwasadia kuzitatua ikiwa ni pamoja na kuwapa baadhi ya mahitaji ambayo watoto hao walioko mahabusu hawayapati pamoja na kutatua kero walizo nazo.

  Naye mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Arusha Ally Mtumwa alisema kuwa juhudu za jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Arusha hazitaishia hapo kwani huu ni mwanzo wataendelewa kuwasadia watoto wa mahabusu hii pamoja na watoto wengine wanao ishi katika mazingira magumu na wale yatima waliopo ndani ya mkoa wa Arusha.

  Alisema wao kama wazazi wanaguswa sana na baadhi ya matatizo yanayowapata watoto hao wanaoishi katika mahabusu hii ya watoto pamoja na wale wanaoishi katika mazingira magumu hivyo watajitaidi kwa kila njia kuwasadia .

  “hii sio mara ya kwanza kuwasadia watoto hawa na wala sio watoto hawa tu tunawasaidia na pia atutaishia hapa tutaendelea kuwasaidia watoto hawa sisi kama wazazi adi pale tutakapoona sasa watoto hao wanaishi katika hali nzuri kama wale watoto wana wazazi wanaoishi majumbani kwao.

  Kwa upande wake katibu wa wazazi CCM wilaya Arusha Rehema Mohamed alisema kuwa mara ya kwanza walipotembelea katika mhabusu haya walikuta magodoro yamechakaa ,eneo limechakaa,watoto wanaishi katika mazingira magumu ,vyoo vya mahabusu hiyo vilikuwa vibovu pamoja na mahabusu hiyo kutokuwa na chakula cha kutosha kwa ajili ya watoto hao lakini wao kama jumuiya walishirikiana kutafuta wadau ambao wamejitokeza kusaida kutatua baadhi ya changamoto ikiwa ni pamoja na kupeleka chakula,mashuka ambayo hayakuwepo sasa ivi wamempata huyu ambaye aliwapelekea magodoro na wao wameyachukuwa na kuyakabidhi katika mahabusu hiyo.

  “pia naomba sana serekali ,pamoja na mahakama kwa ujumla kuangalia usikilizaji wa kesi za watoto hawa kwani kuna baadhi ya watoto wameshakaa ndani ya mahabusu hiyo kwa muda mrefu lakini kesi zao azisikilizwi ,na ambazo zinasikilizwa azitolewi ukumu kwa wakati na zikitolewa ukumu watoto hao wanatakiwa kufungwa badala ya kupewa adhabu tunaomba sana serekali hii iangalie sana kwa makini swala hili “alisema Rehema.

  Aidha alitolea mfano mmoja wa mtoto(12) ambaye alishitakiwa kwa kosa la kuiba simu lakini ilifikia sehemu mwenye simu alimsamehe ,na alivyopelekwa mahakamani motto huyo alikiri kosa na kutolewa ukumu afungwe miaka miwili ,kitu ambacho ni sio kizuri kwani sheria inasema mtoto kama huyo anatakiwa kupewa adhabu na sio kufungwa.

  0 0

  Na Mwashungi Tahir -Maryam Kidiko. Maelezo Zanzibar. 

  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanya mageuzi ya vyeti vya kuzaliwa kutoka mfumo uliozoeleka wa kutumia karatasi pekee (PAPER BASED) kwenda katika mfumo wa kisasa unaotumia komputa.

  Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheir wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Michezo huko kikwajuni mjini Zanzibar.

  Amesema jitihada hizi zinalenga kuleta ufanisi katika utoaji wa huduma kwa haraka na utunzaji mzuri wa kumbukumbu za usajili na kufanikisha upatikanaji wa takwimu za uhakika ambazo ni muhimu katika kuiwezesha Serikali kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo.

  Aidha amefahamisha kuwa Serikali hiyo imeamua kuhamisha Ofisi ya Mrajis wa Vizazi , Vifo na Kadi za Utambulisho ambayo ndio yenye mamlaka kisheria kusajili matukio ya kijamii (vizazi , vifo ndoa na talaka) katika ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ kwa madhumuni ya kuunganishwa usajili wa mtoto tangu kuzaliwa mpaka kufariki kwake.

  Hata hivyo ameeleza kuwa vyeti hivyo vinavyotolewa katika mfumo huo mpya vinamuonekano mzuri na ukubwa ukilinganisha na vile vilivyozoeleka ambavyo huchapwa kwa kutumia typewriter. Vile vile alisema kupitia mfumo huo muombaji wa cheti cha kuzaliwa hutakiwa kuwasilisha uthibitisho wa taarifa ya kizazi kutoka Hospitalini au kwa Sheha pamoja na taarifa nyengine ili kuingizwa katika komputa na kuweza kupatikanwa cheti kwa haraka.

  “Napenda kusisitiza kwamba utaratibu huu unafanyika kwa vizazi ambavyo taarifa zake zitakuwa zimeingizwa katika komputa na kwa vizazi ambavyo taarifa zake hazijaingizwa katika komputa utaratibu utakaoendelea kutumika ni uleule wa asili hadi ofisi itakapoweza kuingiza taarifa zote za vizazi katika mfumo mpya wa usajili .”Alisema waziri huyo.

  Sambamba na hayo aliwataka wananchi wote wa mkoa wa Mjini Maghribi Unguja watakapojaaliwa kupata watoto kufika katka ofisi husika iliopo Mazizini wakiwa na taarifa zote zinazohitajika na kusajili vizazi vyao katika mfumo mpya ulioanzishwa .

  Haji omar Kheir amesisitiza kuwa kila mtu ni haki yake kusajili vyeti hivyo kwa kufuata utaratibu maalum uliowekwa na ofisi hizo. Jumla ya Vyeti 480 vitaanza kutolewa rasmin hivi karibuni katika Mkoa mjini Magharibi.

  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman alipomtembelea ofisini kwake mapema leo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman (kulia) akisisitiza jambo, wakati wa mazungumzo kati yake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ofisini kwake mapema leo.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman alipomtembelea ofisini kwake mapema leo.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameridhishwa na maendeleo ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo mpaka sasa ujenzi huo umefikia asilimia 35 ikiwa ni kazi iliyotekelezwa ndani ya siku 18 toka alipotoa agizo hilo mwishoni mwa mwezi juni mwaka huu.

  Ametoa kauli hiyo alipokuwa akikagua ujenzi wa uwanja huo na kumhimiza mkandarasi wa Kampuni ya Chico kuendeleza kasi ya ujenzi huo ili kukamilisha kwa wakati uliopangwa na kutoa msisitizo kwa makandarasi wengine wanaotekeleza miradi mbalimbali nchini kujipanga na kufanya kazi kwa ushirikiano ili kukamilisha miradi hiyo kwa muda mfupi kulingana na makubaliano ya mikataba.

  "Mradi huu umetupa mfano kama tukijipanga vizuri hata kwenye miradi mingine tunaweza kutekeleza kwa haraka na ubora unaotakiwa, kwa upande wetu kama Serikali tutahakikisha uwanja huu unakamilika haraka ili kuruhusu ndege kubwa kuanza kutua", amesisitiza Waziri Mbarawa.

  Aidha ameongeza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa uwanja huo utakuwa chachu kwa Shirika la Ndege Tanzania ATCL kuwaunganisha watanzania kwa kutoa huduma za usafiri anga katika maeneo mbalimbali nchini na hivyo kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi.

  Kuhusu suala la kufufua ATCL Waziri Mbarawa amesema kuwa Serikali imeshalipa kiasi cha sh. Bilion 36 sawa na asilimia 40 katika hatua za ununuzi wa ndege mbili.

  "Kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano tutahakikisha hatua za ununuzi wa ndege mpya zinafanyika kwa haraka ili kuweza kulifufua shirika letu la ndege na kuweza kuanza kutoa huduma za usafiri wa anga ifikapo mwezi septemba mwaka huu", amesisitiza Waziri Mbarawa.

  Kwa upande wake Meneja Mradi wa upanuzi wa uwanja huo kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Eng. Mbila Mdemu amesema kuwa mpaka sasa mita 900 imekamilika kwa kuweka tabaka la kwanza lami katika eneo la kuruka na kutua ndege na kazi ya kuchimba na kusawazisha eneo la kurefusha njia imekamilika.

  "Kasi ya ujenzi wa uwanja huu unaendelea vizuri kwa kushirikiana na mkandarasi wa kampuni ya Chico na kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati kwa kuzingatia viwango na ubora unaotakiwa", amesema Eng. Mbila.

  Upanuzi wa uwanja wa ndege wa Dodoma unahusisha njia ya kuruka na kutua kwa ndege yenye urefu wa Km 2.5 na mita 500 za taa za kuongozea ndege na usalama wa kuruka kwa ndege .

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma, Col. Marco Gaguti.

  ******* 
  MKUU Wa Wilaya ya Buhigwe, Mkoani Kigoma, Col Marco Gaguti amewataka Viongozi wa Serekali na jamii Wilayani Buhigwe kuwatumikia Wanachi kwa nguvu zote na kuhakikisha uundwaji wa mfumo wa nyumba kumi.

  Aidha Viongozi hao wa Serikali na jamii wametakiwa kukamilisha mara moja uundwaji wa mfumo wa kiutawala wa nyumba kumi ambao utasaidia kuimarisha ulinzi na amnani katika wilaya hiyo.

  “Ninatoa siku saba kukamilisha zoezi la kuhuisha daftari la kiusalama pamoja na uundwaji wa mfumo wa kiutawala wa nyumba kumi ambao utasaidia kwa kiwango kikubwa cha ulinzi na usalama wetu,”alisema Col. Gaguti.Col Gaguti alibainisha hayo alipokuwa akiongea na Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na Viongozi wa Serikali ngazi ya Wilaya katika kikao cha kujitambulisha kilichofanyika Julai 11,2016 katika ukumbi Wa Mikutano Wa Wilaya.

  " Nataka kila Kiongozi ajipambambanue kwa kuwapigania na kuwatumikia wanachi,niwakati sasa wa kila mmoja wetu kuainisha kero na changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka," alisema Col Gaguti.

  Amewataka kuweka kipaumbele katika kukamilisha zoezi la upatikanaji wa madawati ya kushughulikia kero za wananchi.Col Gaguti alisema watendaji wa serikali kila ngazi wasimamie vyema shughuli za serikali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha lego la Serekali kutoa elimu bure yenye ubora lifikiwa mapema kwa kukamilisha mahitaji yote muhimu na kusimamia huduma bora za Afya .
  Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Col. Marco Gaguti akisalimia baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo alipowasili katika Ukumbi wa Hlamashauri kwaajil;i ya kikao cha kujitambulisha.
  Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Col. Marco Gaguti akisalimiana na  baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo alipowasili katika Ukumbi wa Halmashauri kwa ajili ya kikao cha kujitambulisha.
  Akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya ulinzi na Usalama ya Wilayawatumishi wakimsikiliza mkuu huyo wa Wilaya. Source:Father Kidevu Blog


  0 0


  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula (kushoto), akihutubia wakati akifungua mkutano wa wadau wa uendelezaji milki uliofanyika Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Usimamizi Milki, Hamad Abdallah, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu, Mkurugenzi wa Nyumba wa wizara hiyo, Charles Mafuru na Mkurugenzi wa Fedha wa NHC, Felix Maaly. Mkutano huo uliandaliwa na NHC.
  Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu, akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula kuufungua.
  Mwonekano wa meza kuu wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
  Wadau wa uendelezaji milki wakiwa kwenye mkutano huo.

  Wadau wa uendelezaji milki wakiwa kwenye mkutano huo.


  Taswira ya chumba cha mkutano huo.
  Mwonekano wa chumba cha mkutano katika ufunguzi wa mkutano huo.


  (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

  0 0

  Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,luhaga Mpina (katikati)na Meneja mazingira kiwandani hapo bw. Richard Magoda akitembezwa ndani ya kiwanda baada ya kupata malalamiko ya uchafuzi wa mazingira kutoka kwa wananchi.

  Baadhi ya Sehemu za Uzalishaji ndani kiwanda hicho ambayo yanalalamikiwa na Wanachi kwa Uzalishji vumbi linalowaathiri wananchi.

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akizungumza na Uongozi wa kiwanda cha twiga cement,pamoja na Maafisa kutoka Baraza la Usimamizi wa Mazingira(NEMC)alipofanya ziara mapema hii leo.

  EVELYN MKOKOI

  Kiwanda cha kutengeneza cement cha Twiga cement cha wazo jijini dare s Saalaam kimepewa muda wa mwezi mmoja kurekebisha mfumo wao wa utoaji taka ili kunusuru uharibifu wa mazingira na maisha viumbe hai.

  Hayo yamesemwa Leo jijini Dar es Salaamna waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina katika ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho.Mhe. Mpina amekitaka kiwanda hicho kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kupima vumbi litokanalo na uzalishaji kiwandani.. ili kuona kama ni la kiwango ambacho si hatarishi kwa mazingira na viumbe hai vinavyozunguka maeneo hayo.

  Maagizo hayo ya Naibu waziri Mpina yametokana na malalamiko ya wananchi wa maeneo jirani na kiwanda hicho yanayoeleza kuwa kiwanda hakina mahusiano mazuri na wakazi au majirani wa maeneo hayo hivyo, amemtaka muwekezaji huyo kuimarisha mahusiano baina ya kiwanda hicho na wananchi na kufanyia marekebisho kasoro zilizoonekana kujitokeza kiwandani hapo na kuwaasa wawekezaji wa kiwanda hicho kufanya kazi pamoja na kuheshimu sheria hususan za mazingira.

  Kwa upande wa Baraza la Taifa na Usimamizi wa Mazingira Nemc kumeonekana kuwa na uzembe katika ufuatiliazi wa utekelezaji wa sheria za mazingira hasa kiwandani hapo, baada ya mkurugenzi wa uzingatiaji na utekelezaji wa baraza hilo bi Ruth Lugwisha kushindwa kujibu swali aliloulizwa na Naibu waziri Mpina kuwa ni lini Mara ya mwisho baraza hilo lilijiridhisha kwa kuchukua vumbi kiwandani hapo na kulipima ili kujua lina athari kwa kiasi gani kwa mazingira na viumbe hai.

  Kwa upande wake Meneja wa Mazingira wa kiwanda hicho Bw. Bw. Richard Magoda amejitetea kuwa kiwanda kina mahusiano mazuri na wanachi kwani kimeweza kutoa misaada katika baadhi ya maeneo ikiwa ni pamoja na vyandarua na kuchonga barabara za baadhi ya mitaa.

  Wakati huo huo viongozi wa serikali za mitaa Bw. Gration Mbelwa (mwenyekiti wa kata ya madale) na Atilio Maginga mwenyetiki wa serikali ya mtaa wa mivumoni..wametofatofautiana kwa kusema kwamba kiwanda kina mashirikiano mazuri na wananchi, wakati mwenyekiti wa kata ya madale akiwakilisha wanachi kwa kulalamika kuwa kiwanda hakina mahusiano mazuri na wananchi.

  0 0
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw.Enterberth Nyoni(kushoto) akisisitiza jambo wakati wa Kikao Kazi cha Wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii mjini Dodoma.Katikati ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Erasimus Rugarabamu na Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vilivyo chini ya Wizara hiyo Bw.Paschal Mahinyila.

  Na.Aron Msigwa - DODOMA

  Wito umetolewa kwa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo Jamii kote nchini kushirikiana na wataalam walio katika vyuo hivyo kubuni vyanzo vipya vya mapato kupitia uanzishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuviwezesha vyuo hivyo kumudu baadhi ya gharama za uendeshaji zikiwemo za ukarabati wa miundombinu.

  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Enterberth Nyoni ametoa wito huo mjini Dodoma wakati aizungumza na wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vilivyo chini ya wizara hiyo kuhusu namna vinavyoweza kumudu baadhi ya gharama za uendeshaji kupitia miradi mbalimbali.

  "Tuna vyuo vina maeneo makubwa ya wazi ya ardhi ambayo yangeweza kutumika kuongeza kipato kwa shughuli za kilimo na ufugaji, maeneo haya hayatumiki ipasavyo jambo linalosababisha wananchi wayavamie na kuanza kulima jambo ambalo limekuwa chanzo cha migogoro baina ya vyuo husika na wananchi" Amesisitiza Bw. Enterberth.

  Amesema kuwa licha ya vyuo hivyo kubuni miradi kujiongezea kipato, lengo la Serikali ni kuhakikisha inaendelea kuviwezesha vyuo hivyo kwa majengo mapya yanayoendana na hali halisi na hadhi ya vyuo husika ili kwenda na kasi ya mabadiliko ya elimu na mahitaji ya vyuo hivyo.

  Aidha, amefafanua kuwa ipo haja ya kuangalia namna bora ya kuendelea kuiboresha miundombinu ya vyuo vya Maendeleo ya Jamii vilivyopo nchini ili viendelee kuwavutia wanafunzi wanaodahiliwa kusoma katika mazingira bora.

  Amesisitiza kuwa ni vyema vyuo hivyo kuwa na mkakati mkakati wa kujenga majengo mapya ikiwemo madarasa ya kufundishia ili kukidhi mahitaji ya majengo, kuhimili ushindani pia mahitaji ya makundi maalumu.

  Ametoa rai kwa wakuu hao kuangalia upya namna ya kupata fedha nje ya utaratibu wa Bajeti ya Serikali na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kuvijengea uwezo vyuo hivyo kulingana na Bajeti inayopangwa ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali imetenga shilingi Bilioni 5.6 kwa ajili ya uendeshaji wa vyuo hivyo.

  0 0


  Na Daudi Manongi,MAELEZO.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk John Pombe Magufuli amewaagiza makatibu wakuu wote wa wizara kutumia mashine za kietroniki (EFD) katika kukusanya mapato serikalini.

  Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akizungumza na wakurugenzi wateule wa Halmashauri,Wilaya,Majiji na Manispaa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi hao wa umma.

  “Vyombo vya Serikali lazima vianze kutumia mashine za EFD,haiwezekani wafanyabiashara wawe na mashine za EFD alafu maafisa wa serikali hawana,kama tumeamua kwenda kwa elektroniki lazima twende hivyo”Alisema Rais Magufuli.

  Aidha amewataka wakurugenzi wote kuchukua mashine hizi na kwenda nazo katika maeneo yao ya kazi ili ziwasaidie katika ukusanyaji wa mapato ya serikali katika halmshauri zao.

  Pia amewaagiza wakurugenzi hao kukusanya kodi na kutatua kero za wananchi wa chini zisizokuwa na lazima na kuongezea kuwa kama watakuta watendaji wa chini yao wasioendana na kasi ya awamu ya tano basi watumie madaraka yao kuwaweka sawa.

  Rais magufuli pia amewaagiza wakurugenzi hao kusimamia ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi kwakuwa waliahidi kutatua kero za wananchi na wahakikishe wanazitatua ili wananchi waishi vizuri kwa amani ndani ya nchi yao na kuongezea kuwa viongozi wa juu wana imani kubwa sana nao ndio maana hata wakachaguliwa kutoka katika watanzania hawa milioni 50.

  Aidha Rais magufuli amewataka wakurugenzi hao kusimamia kuanzishwa kwa viwanda vidogo vidogo katika maeneo yao ili kukamilisha azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa na viwanda.

  Mbali na hayo pia amewataka wakurugenzi hao kubadilika kifikra na kuachana na kuongoza kwa historia kwani wananchi wa sasa wamebadilika na hivyo wafanye kazi kwa bidii ili kuwatimizia wananchi yale wanayotaka na hivyo nchi itasonga mbele.

  0 0

  MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeitisha mkutano Jumamosi Julai 16,2016 kwa wanachama wake waliokamilisha nyumba zao, waliochangia ujenzi na waliogaiwa mashamba ili kujadili umuliki na maendeleo ya maeneo ya makazi na kilimo.

  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa mkutano huo utakaofanyika ukumbi la Chuo cha Splendid, Ilala \Bungoni utaanza saa tatu asubuhi ili kujipanga kuhamia kijijini kwao Mwanzega Mkuranga ambapo mpaka sasa kuna nyumba 185 ambazo tayari zimejengwa na wanachama hao kwa njia ya kuchangishana.

  Alisema wanachama ambao watahamia katijka nyumba zao watapewa ekari moja bure kwa ajili ya kulima na ufugaji kwa ajili ya kuwaendeleza wajasiriamali wa SHIWATA.

  Taalib alisema SHIWATA inakusudia kuwapokea wadau na wajasiriamali mbalimbali wa sanaa na michezo ambao watapatiwa fursa ya kujiunga na mtandao huo kwa gharama ya sh. 100,000 kuanzia Julai 18, 2016 hadi Septemba 30,2016 itawafaidisha wajasiriamali na wadau hao kupata eneo la makazi lenye ukumbwa wa mita 35 kwa 35 pamoja na ekari moja bure kwa wale ambao wamejenga na kuhamia.

  Alisema kwa upande wa shamba, SHIWATA inampango maalum wa kuendesha kilimo cha pamoja kutumia wataalamu wa kilimo wawilaya ya Mkuranga ili kufanikisha mradi wa kilimo kwa njia ya kuchangiana.

  Pia SHIWATA inakaribisha wawekezaji kwa ajili ya kujenga shule, hospitali pamoja na maduka ya kuuza bidhaa mbalimbali ambapo baada ya kujiunga na mtandao huo watapewa maeneo bure.

  Mwenyekiti Taalib alisema Ujenzi wa awamu ya sita unatarajiwa kuanza Julai 30 mwaka huu na nyumba zitagaiwa kwa wanachama watakaokuwa wamekamilisha michango ya ujenzi wa nyumba zao.

  0 0

  Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa huduma za kitabu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki iliyopo Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka maarufu kama Dkt. Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabu za tiba asili huku akiwa ameonywa na kushindwa kubadilika.

  Akizungumza jijini Dar es salaam leo katika Mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk. Edmund Kayombo amesema kuwa kufutiwa kibali cha Dk. Mwaka kunatokana na sababu nyingi ambazo amekuwa akikiuka licha ya kupewa maonyo na barua juu ya utoaji huduma zake.

  Amesema sababu nyingine ni kuwa katika matangazo yake amesema anatoa tiba za kisasa wakati hiyo elimu hana ya kufanya hivyo.
  Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala , Dk. Edmund Kayombo akizungumza na waandishi habari juu hatua walizozichukua kwa watoaji huuduma tiba asili na tiba mbadala leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Msajili Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Ruth Suza kushoto ni Kaimu Mkurugenz Msaidizi wa Huduma na Tiba Mbadala, Paulo Muhame.

  Wengine waliofutiwa usajili ni Fadhaget Sanitarium kinachoendeshwa na Tabibu Fadhili Kabujanja pamoja na Mandai Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Abdallah Mandai

  Hata hivyo limetoa adhabu mbalimbali kwa kituo cha Aman Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Esbon Baroshigwa, na Tabibu Castory Ndulu wa Kituo cha Ndulu Herbal Clinic wamepewa barua ya onyo.

  Aidha wengine wamesimashwa kwa miezi sita ambao ni Tabibu John Lupimo wa Lupimo Suntarium Herbal Clinic pamoja na Tabibu Simon Rusigwa wa Sigwa Herbal Clinic.
  Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma na Tiba Mbadala, Paulo Muhame akizungumza na waandishi habari juu ya utekelezaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa wanaokiuka taratibu za utoaji huduma wa tiba asili na tiba mbadala katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala , Dk. Edmund Kayombo kulia ni Msajili Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Ruth Suza.

  Dk. Kayombo amesema kuwa wale wote ambao wamepewa onyo pamoja na kusimamishwa wametakiwa wasiingie mikataba na vyombo vya habari kwa ajili ya Matangazo

  Amesema kuwa waliofutiwa walifuata taratibu zote ikiwa kuwahoji na kujiridhisha kuwafutia kibali cha utoaji wa huduma za tiba asili na tiba mbadala.Imeandikwa na Chalila Kibuda.

  0 0

  Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeweka wazi msimamo wake kuwa haitauza meno yake ya Tembo yaliyohifadhiwa kwa kuwa kufanya hivyo ni kuongeza upatikani wa meno hayo kwenye soko hivyo kuchochea biashara haramu ya ujangili.

  Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alipokuwa kwenye mazungumzo ya na Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Egon Konchanke ofisini kwake Mpingo House, Jijini Dar es Salaam.

  Balozi Konchanke alimueleza Prof. Maghembe kuwa, mwezi Septemba mwaka huu (2016), Wanachama wa Mkataba wa Kimataifa unaosimamia biashara ya Viumbe vilivyo hatarini kutoweka vya wanyama na mimea (CITES) watakutana nchini Afrika ya Kusini kujadili mambo mbali mbali ikiwemo baadhi ya nchi wanachama ikiwemo Namibia kutaka kuuza Meno yake ya Tembo yaliyohifadhiwa ili kujipatia kipato.

  Katika maelezo yake Balozi Konchanke alimuomba Prof. Maghembe kutoa msimamo wa Serikali ya Tanzania kuhusu hoja hiyo ya kuuza meno ya tembo yaliyohifadhiwa kutokana na matukio ya Ujangili na vifo asilia vya wanyama. “Ni upi msimamo wa Tanzania katika kuelekea mkutano huo kuhusiana na uamuzi wa nchi kama Namibia wa kuuza meno yake ya tembo yaliyohifdhiwa?” aliuliza Balozi Konchanke.

  Katika majibu yake Prof. Maghembe alisema “Tanzania tunaungana na mataifa mengine ambayo yanapinga uuzwaji wa meno ya tembo, Kama tukiuza meno haya tutaongeza upatikanaje wake kwenye masoko, hivyo kuchochea zaidi biashara hii haramu, hatuna sababu ya kuyauza wala kuyachoma moto, ukiyachoma moto unakuwa umechoma kila kitu ikiwemo sampuli ambazo zingeweza kutumika kwenye tafiti mbalimbali zikiwemo za kutengeneza madawa ya kutibu maradhi ya wanyama hao”. Aliongeza kuwa nchi zitakazofanya hivyo zitakuwa hazijafanya jambo la busara zaidi ya kuleta maafa kwa nchi jirani ya kuongezeka kwa vitendo vya ujangili.


  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimkaribisha Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Mhe. Egon Konchanke alipomtembelea jana tarehe 11 Julai, 2016 ofisini kwake, Mpingo House, Jijini Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya Maliasili nchini.

  Waziri Maghembe (kulia) akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Balozi Konchanke (kushoto).

  Waziri Maghembe (kulia) akizungumza katika kikao hicho.

  Balozi Konchanke (kushoto) akimueleza jambo Prof. Maghembe (kulia) katika mazungumzo hayo.
  Balozi Konchanke (kushoto) akimuonesha Waziri Maghembe (kulia) ramani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi ambayo Balozi huyo ameahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuendeleza utalii wake kwa pamoja na ule wa Mkoa wa Kigoma (Hifadhi ya Mahale)
  ______________________________________
   
  Wakati huo huo, Waziri Maghembe alimuomba Balozi Konchanke kuleta wawekezaji kutoka Ujerumani kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya Utalii na Uhifadhi hapa nchini. Balozi huyo aliahidi ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania ambapo alisema mwishoni mwa mwezi huu wa Julai Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Serikali ya Ujerumani Dkt. Gerd Muller atakuja nchini na wafanyabiashara kutoka nchini humo wenye nia ya kuwekeza katika sekta ya Uhifadhi na Kilimo.

  Balozi Konchanke ameahidi pia kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuendeleza Utalii kwenye Mikoa ya Kigoma na Katavi kwa kuunganisha utalii wa Hifadhi ya Mahale na Hifadhi ya Katavi. Amesema kuwa eneo hilo linahitajika kuwekewa miundombinu mizuri ya barabara ili liweze kufikika kirahisi.

  Kwa upande wake Waziri Maghembe amesema kuwa utalii katika Mikoa hiyo unapewa nafasi kubwa ili uweze kukua na kuliingizia zaidi taifa mapato. Ameeleza kuwa katika kukabiliana na changamoto ya usafiri zitaansishwa safari za ndege za bei nafuu mara tatu kwa wiki kutoka Dar es Salaam kwenda Mikoa ya Kigoma na Katavi kwa bei ya dola za kimarekani 150.

  Akizungumzia kuhusu kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye huduma za Utalii wakati akijibu hoja ya Balozi Konchanke juu ya malalamiko ya watoa huduma hizo kuwa sheria hiyo imekuja ghafla na inapunguza ujio wa watalii nchini, Waziri Maghembe alisema sheria hiyo imepitishwa na bunge na watoa huduma hao walishataarifiwa toka mwaka jana (2015) juu ya mabadiliko ya sheria hiyo kwa ajili ya kufanya maandalizi ya mabadiliko yake. Aliongeza kuwa ili Serikali ijiendeshe inahitaji mapato na kwamba watalii wanalipa kodi hivyo na watoa huduma nao wanahitajika kulipa kodi.

  Katika hatua nyingine Balozi Konchanke aliomba ufafanuzi kwa Waziri Maghembe juu utaratibu mpya wa mashirika ya umma kupeleka fedha zote za makusanyo hazina na kwamba kama wahisani wakichangia kuendeleza mashirika hayo ikiwepo TANAPA na TAWA, pengine lengo lao litakuwa halijafikiwa na hivyo kuwa vigumu kujiendesha. Akijibu hoja hiyo Waziri Maghembe alisema kumekuepo na uelewa hafifu juu ya utaratibu huo ambao kimsingi Mamlaka hizo ikiwemo TANAPA na TAWA zitapelekea fedha zao hazina na kuzitumia pale itakapohitajikwa kwa mujibu wa mpango kazi wao.

  (Na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii #www.wizarayamaliasilinautalii.blogspot.com#)

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali (Mstaafu), Salum Kijuu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Uimarishaji wa mifumo ya sekta za Umma (PS3) unaotekelzwa katika mikoa 13 ya Tanzania bara kwa ushirikiano wa baina ya Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID) na Serikali ya Tanzania. Mradi huo utazihusisha Halmashauri 93 katika mikoa hiyo.
  Mtaalam wa fedha wa mreadi wa PS3 ambaye ndie msimamizi wa uzinduzi huo Mkoani Kagera, Abdul Kitula akielezea maeneo mbalimbali ambayo mradi huo utahusika na kufanya kazi. Kitula alisema PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji.
  Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Kagera wakifuatilia uzinduzi huo.
  Mratibu wa Mradi wa PS3 kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bertha Swai akijibu na kutolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyoulizwa na washiriki.
  Mtaalam wa masuala ya Rasilimali watu kutoka Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Remmy Moshi akiwasilisha mada.


  washiriki wakifuatilia mada katika mkutano huo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  Maofisa wa mradi wa PS3 waliobobea katika masuala ya utawala bora wakiwa katika mkutano huo.
  Mtaalam wa Mawasiliano na Takwimu wa Mradi wa PS3, Desideri Wengaa akitoa mada juu ya mawasiliano na utoaji takwimu sahihi.
  Maofisa kutoka Wizarani wakiwa katika mkutano huo.
  Mshiriki akifuatilia mada kwa umakini.
  Waandishi wa habari wakifuatilia matukio.
  Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawiro (kushoto) akijadili jambo na Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Ruyango.
  Mratibu wa Mafunzo ya muda Mfupi kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo ambao ni moja wa wadau wa utekelezaji wa mradi huo wa PS3, Benjamin Magori akifafanua baadhi ya mambo.  Picha ya pamoja ya makundi mbalimbali.
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu), Salum Kijuu (katikati) akiwa na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa huo.
  Picha ya pamoja katika ya Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya na Maofisa wa PS3.

  *********

  UZINDUZI wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Bukoba mkoani Kagera siku ya Jumanne na Jumatano, leo Julai 12-13, 2016. Mradi huo ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening (PS3) ni wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 93 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.

  PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji. Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha.

  Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja.Jenerali (Mstaafu), Salum Kijuu na unawashirikisha watemdaji takribani 200. Washiriki wa uzinduzi huo walikuwa ni: Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Wakuu wa Wilaya za Kagera, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa, na Wajumbe wa Timu ya Mejenimenti kutoka kwenye Halmashauri.

  Mkoa wa Kagera una Halmashauri nane, ambazo ni: Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo, Halmashauri ya Mji wa Karagwe, Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi.PS3 ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID.

  Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo ni: Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ambao ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzi ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na Urban Institute. Mikoa 13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni: Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga.PS3 itaimarisha mifumo katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri.

  Mradi utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa kupitia kitita cha afua zilizoundwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania. Mafanikio yanayotarajiwa ni pamoja na:

  Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Raia: Uimarishaji wa utawala katika ngazi ya kitaifa na ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, ili kuweza kutumia rasilimali kwa uwazi, kuwezesha ushiriki wa wananchi katika kupanga, kufuatilia, na kutoa matokeo katika kila sekta.Rasilimali Watu: Kuongezeka kwa usawa katika mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili ya utoaji wa huduma bora kwenye maeneo yenye uhitaji zaidi. Kuimarisha mfumo wa ajira pamoja na kudumu kwa watumishi katika ajira serikalini.

  Fedha: Ongezeko la pato la ndani kwa ajili ya huduma za umma, kuongeza ufanisi katika matumizi ya fedha za umma, na pia kuongeza uwiano kati ya kiasi cha fedha kilichotumika na mali iliyonunuliwa.Mifumo ya Mawasiliano: Kuimarisha mifumo ya utoaji taarifa iliyopo nchini, pamoja na matumizi ya takwimu kwa wadau.Utafiti Tendaji: Tafiti Tendaji muhimu zitakazosaidia mradi kujua changamoto na mikakati ya kuzishughulikia changamoto hizo.

  Tafiti hizi zitasaidia kugundua fursa zilizopo na kuzitumia kuweza kupata matokeo yanayotarajiwa.Pia tafiti hizo zitasaidia kuboresha maamuzi serikalini.

  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, Miji, Manidpaa na Majiji 185 kabla ya hawajakula kiapo cha maadili ya viongozi leo Ikulu jijini Dar es salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya hapa nchini kufanya kazi za kuwaletea maendeleo wananchi na kuondoa kero zinazowakabili kwa kujiamini, uadilifu na uaminifu.

  Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo tarehe 12 Julai, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya wakurugenzi hao wa halmashauri kula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma, zoezi ambalo limeendeshwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

  Mhe. Rais Magufuli amesema katika kutekeleza jukumu hilo la kuwaletea wananchi maendeleo na kuondoa kero zinazowakabili, wakurugenzi hao hawana budi kuhakikisha wanatekeleza kwa vitendo ahadi ambazo serikali ya awamu ya tano imezitoa, wakiongozwa na Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 - 2020.

  Aidha, amesema wakurugenzi wote wa halmashauri wana wajibu wa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na amewataka kutosita kuchukua hatua dhidi ya watendaji ambao wamejigeuza kuwa miungu watu na wanawanyanyasa wananchi.

  "Wapo watendaji wa kata ambao ni miungu watu, wanachonganisha wananchi na serikali, katumieni madaraka mliyonayo kuwaondoa kazini" Amesema Rais Magufuli

  Mhe. Rais Magufuli pia amewataka wakurugenzi hao kusimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato ya serikali na ametumia nafasi hiyo kuagiza wizara zote kuanza kutumia mashine za kielektroniki (EFD) katika ukusanyaji wa mapato kwenye taasisi zote ambazo zinakusanya maduhuli.

  Dkt. Magufuli amewasisitiza wakurugenzi hao kuhakikisha wanasimamia vizuri fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya utoaji wa elimu ya msingi na sekondari bila malipo, ambapo kila mwezi serikali hutoa shilingi bilioni 18.777 na ametaka tabia ya wakurugenzi wa halmashauri kushirikiana na wafanyabiashara ama wanasiasa kujinufaisha kupitia zabuni za serikali ikome.

  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambao walikuwepo wamewataka wakurugenzi hao wa halmashauri kuwa watumishi bora, kusimamia vizuri rasilimali za halmashauri na kushirikiana na viongozi wa mkoa na wilaya katika halmashauri zao.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  12 Julai, 2016

  0 0

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akipokea bahasha yenye mafanikio ya Tanzania Media Foundation ambayo yamefanywa nchini katika kuwajengea uwezo Waandishi wa habari toka kwa Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation, Bw. Ernest Sungura 12 Julai, 2016 jjijjini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akipokea zawadi ya bango la picha zilizopigwa na baadhi ya Waandishi wa Habari waliowahi kujengewa uwezo na Tanzania Media Foundation 12 Julai, 2016 jijini Dar es Salaam.

  Na Benedict Liwenga, WHUSM.

  Serikali kwa kushirikiana na Uongozi wa Tanzania Media Foundation itaendelea kushirikiana bega kwa bega katika kuwawezesha Waandishi wa Habari nchini kupenda kutembelea maeneo ya vijijini na kuandika habari mbalimbali kuhusu changamoto za maeneo hayo.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye wakati akizindua Miradi Nane ambayo inafadhiliwa na Taasisi hiyo ambayo unahusisha Waaandishi wa Habari kutembelea maeneo ya vijijini na kuandika habari mbalimbali kwa lengo la kuelimisha Umma.

  Mhe. Nnauye amesema kuwa, Serikali inatambua mchango mkubwa unaofanywa na Taasisi hiyo ya kuwajengea uwezo Waandishi wa habari na kuwawezesha kifedha kwa ajili ya kwenda kutafuta habari mbalimbali katika maeneo ya vijijini.

  ‘’Ni muhimu kwa waandishi wa habari kufika maeneo ya vijijini na kuapata habari mbalimbali kwa jili ya kuhabarisha umma, hivyo Serikali bado iko na nyie na itaendelea kuwaunga mkono na endeleeni na kazi hiyo nzuri’’, alisema Mhe. Nnauye.

  Ameongeza kuwa, kuna haja ya Taasisi hiyo kuendelea kujenga uwezo wa kusaidia kupata umakini katika kazi za habari ili jamii iweze kuwa na imani na Serikali pamoja na Vyombo vya habari na pia kuonyesha juhudi ya kuendelea kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kuwafikia watu wenye mahitaji makubwa ya habari ambao ni watu wa vijijjini ambao wakati mwingi wamekuwa wakichelewa kupata habari.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation, Bw. Ernest Sungura ameyataja baadhi ya mafanikio yaliyofikiwa na Taasisi hiyo katika kuwajengea uwezo wanahabari nchini ambapo amesema kuwa, mpaka sasa wameweza kuwajengea uwezo jumla ya Waandishi wa habari wapatao 700 pamoja na Vyombo vya Habari 135.

  Mbali na kuanza na miradi ya mwandishi mmoja mmoja, kwa sasa wanatarajia kuanza na miradi mingine inayoanza mwishoni mwa mwezi huu na itakuwa ni ya Awamu ya Pili ambapo itahusisha jumla ya Waandishi wa habari wapatao 30 kwenda vijijini kufanya kazi za kihabari na kupewa mafunzo ya namna ya kuandika habari za vijijini.

  ‘’Kwa sasa tumeanza mradi wa watu kubobea katika eneo maalum na safari hii tutajikita katika masuala ya Viwanda yaani kuwaandaa waandishi wa habari watakaobobea katika masuala ya viwanda na tayari tumeshamdokeza Waziri wa Viwanda kuhusu taarifa hizo kwa ajili ya kuizindua miradi hiyo’’, alisema Sungura.

  Ameongeza kuwa katika kuandika masuala ya viwanda, tayari kuna waandishi wa habari wapatao 10 ambao hivi sasa wanajengewa uwezo ili waweze kuendana na kasi ya Serikali na katika suala la kuwandaa waandishi hao wanatumia Waandishi wa habari wazoefu pamoja na wadau wengine.

  Amefafanua kuwa, lengo kubwa la kazi hizo zote ni kuwawezesha waandishi nchini kuweza kuyafikia maeneo ambayo yamekuwa hayafikiki, hivyo wanatoa rasimali fedha kwa waandshi hao ili kuweza kutembelea maeneo hayo na kuhabarisha umma.

  ‘’Ziko takwimu nyingi kila mahali kama vile za maji, afya, alimu lakini baadhi ya waandishi wetu hawafanyi ule uandishi wa kuzifanya takwimu hizo zieleweke na ziwe na manufaa kwa walaji, hivyo sisi tumeamua kuwajengea waandishi katika maeneo hayo’’, alisema Sungura.

  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni na kuwataka kuwatumikia wananchi ikiwemo kuondoa kero zinazowakili wananchi katika maeneo yao kama utitiri wa kodi hasa kwenye bidhaa wanazozalisha.Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angella Kairuku na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan. wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akiongea na wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya (Hawapo pichani) walioteuliwa hivi karibuni na kusisitiza kwenye matumizi ya Kanuni, Sheria na Taratibu katika kutimiza majukumu yao. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angella Kairuku. wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim akiongea na Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni na kuwataka kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa dhumuni la kuwaletea wananchi maendeleo.Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angella Kairuku, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angella Kairuku akiongea na wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni na kuwataka kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma na kuwataka kuepuka vishawishi ikiwemo kupokea rushwa. Wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.


  Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni wakila kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma. Wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Luhende Pius akionesha cheti chake cha taalum kwa waandishi wa habari baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na uwepo wa taarifa potofu juu ya taaluma yake. wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. 


  Kamishna wa Maadili Kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mhe. Jaji (Mst.) Salome Kaganda akiongea akiongea na wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni na kusisitiza kuzingatia maadili katika kipindi chao cha uongozi wakati wa hafla ya uapishwa wa kiapo cha Ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa wakurugenzi hao.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  Kamishna wa Maadili Kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mhe. Jaji (Mst.) Salome Kaganda akiongea akiongea na wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni na kusisitiza kuzingatia maadili katika kipindi chao cha uongozi wakati wa hafla ya uapishwa wa kiapo cha Ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa wakurugenzi hao.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya aliowateua hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Bw. Elias Nawela. Wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni. Wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  Picha na Hassan Silayo

  0 0


  Bi. Anna Salado, Mkurugenzi wa taasisi ya Women for Africa Foundation ya Hispania, akizungumza na akinamama wa kikundi cha Green Voices katika Kijiji cha Kitanga (hawako pichani) na kueleza jinsi alivyofurahishwa na mafanikio yao kwenye usindikaji wa zao la muhogo.

  Bi. Anna Salado akicheza wakati akinamama wa Kitanga wakiimba.


  Mratibu wa Mradi wa Green Voices nchini Tanzania, Secelela Balisidya, akizungumza na akimama wa Green Voices katika Kijiji cha Kitanga, Kisarawe.
  NAIBU Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo, ameunga mkono jitihada za wanawake wa Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe kusindika zao la muhogo.

  Jaffo, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe (CCM), amesema yuko tayari kushirikiana na wanawake wa kijiji hicho pamoja na wilaya nzima ya Kisarawe kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi kutokana na zao hilo.

  Akizungumza kwa njia ya simu na mshiriki kiongozi wa kikundi cha Kitanga Green Voices, Bi. Abia Magembe, mara baada ya ziara ya ujumbe wa taasisi ya Mfuko wa Wanawake Afrika (WAF) kijijini hapo Julai 13, 2016, Mhe. Jaffo alimtaka kiongozi huyo kuwasiliana naye mara moja ili kuona ni namna gani anaweza kusaidia mradi huo ambao umeanza kuonyesha matunda mazuri kwa wanawake na jamii kwa ujumla.

  Wakati wa ziara ya ujumbe wa taasisi ya WAF kutoka Hispania, Mhe. Jaffo hakuwepo kutokana na kutingwa na majukumu ya kazi, lakini kwa mujibu wa Bi. Magembe, amemtaka kuwasiliana naye haraka ili kuhakikisha jitihada za wanawake hao zinaendelezwa.

  Ujumbe wa WAF ulioongozwa na Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Anna Salado kutoka Hispania, pamoja na mratibu wa mradi wa Green Voices nchini Tanzania, Secelela Balisidya, ulijionea namna akinamama hao wanavyosindika bidhaa mbalimbali zinazotokana na zao la muhogo kijijini hapo.Aidha, ujumbe huo ulielezwa kwamba, mpango wa akinamama hao kwa sasa ni kujenga viwanda vidogo kijijini hapo ili kusindika zao la muhogo ikiwa ni hatua mojawapo ya kuunga mkono kauli ya serikali ya kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda.  “Kwa kuwa serikali imekwishaahidi kwamba inataka kuona Tanzania ya viwanda ili kuongeza ubora wa thamani ya mazao yetu pamoja na kuzalisha ajira, sisi tumedhamiria kujenga viwanda vidogo hapa hapa kijijini ili iwe rahisi kwa akinamama kupata malighafi na kuwasaidia wengine kujifunza,” alisema Mama Magembe.

  Mama Magembe, ambaye ni miongoni mwa akinamama 15 waliokwenda Hispania mapema mwaka huu kujifunza miradi mbalimbali inayolenga kutunza mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabianchi, alisema kwamba kujengwa kwa viwanda vidogo kijijini hapo kutakuwa ukombozi wa jamii nzima hasa kwa vile wilaya ya Kisarawe inalima sana muhogo, lakini wananchi wanapunjwa na walanguzi, hivyo zao hilo kuonekana kutowakwamua kiuchumi.

  Kwa upande wake, Bi. Anna Salado, ambaye alimwakilisha Rais wa taasisi hiyo, Maria Tereza Fernandez de la Vega, alieleza kufurahishwa na jitihada za wanawake hao na akaahidi kwamba, mradi huo ni miongoni mwa miradi itakayopewa kipaumbele katika awamu ya pili.

  Alisema kwamba, imekuwa vizuri kwa wananchi wenyewe kubuni miradi inayotekelezeka na yenye tija, na kwa namna walivyoweza kufanikiwa katika kipindi kifupi, wana matumaini makubwa wanawake hao na wanawake wengine nchini watafanya vizuri ikiwa watajifunza.

  Aidha, Mratibu wa Mradi wa Green Voices kutoka Hispania, Alicia, alisema kwamba mradi wa kusindika muhogo utaikwamua jamii katika suala zima la kukabiliana na njaa, lakini pia utawasaidia wanawake kuongeza kipato kutokana na kuongeza mnyororo wa thamani.

  “Mmefanya vizuri sana, tunawaongeza na tunaamini kwamba, katika awamu inayofuata mtafanya vizuri zaidi,” alisema.

  Hata hivyo, aliwataka wanawake wa kikundi hicho kuwa waalimu kwa wanawake wengine kwa kuwa lengo ni kuhakikisha wanawake wote wanapata elimu na ujuzi na wanatekeleza miradi inayoweza kuwakwamua kiuchumi na kuwaletea maendeleo.

  Bi. Secelela Balisidya, ambaye ni mratibu wa Green Voices Tanzania, aliwapongeza akinamama hao na kuwataka wasikate tamaa kwa kuwa mwanzo umeonekana.Aliwaasa kudumisha umoja ili kikundi hicho kiwe cha mfano na kuwahimiza kukisajili haraka ili serikali iweze kukitambua.


  “Dumisheni umoja, vikundi vingi huanza vizuri halafu vinasambaratika, tusingependa kuona hilo linatokea kwa sababu bado kuna fursa nyingi za kuwawezesha wanawake na umoja ndiyo nguzo muhimu,” alisema.
  Bidhaa mbalimbali zinazotokana na zao la muhogo ambazo zinazalishwa na akinamama wa Green Voices katika Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe.


  Zao la muhogo lina manufaa mengi kwani mbali ya kuutafuna mbichi, kuuchemsha au kuuchoma, kutengeneza mchanyato; unga wake hutumika kwa ajili ya lishe, majani yake kama mboga ya kisamvu na dawa pamoja na miti yake inapokauka hutumika kama kuni.


  Lakini pia unga wa muhogo unatumika kutengeneza bidhaa nyingine kama keki, mikate, skonzi, biskuiti, sambusa, maandazi, chapati, tambi, mafuta ya lishe, sabuni ya unga, huku maganda ya mihogo hutumika kama chakula bora cha mifugo.


  Aidha, muhogo ukitwangwa mbichi na kuchujwa, maji yake yake yanatoa wanga (starch) ambao hutumika kutengeneza dawa za madoa, gundi katika samani, rangi za awali za ukuta na sukari (sugar syrup) na pia ni lishe nzuri.


  Kilimo cha muhogo siyo tu kitasaidia kukuza pato la mkulima, lakini kinaweza pia kuokoa mazingira pamoja na kuisaidia Tanzania kuokoa karibu Dola za Marekani 20 milioni sawa na Shs. 42 bilioni zinazotumika kuagiza chakula nje, jukumu ambalo kikundi cha Kitanga Green Voices kimeamua kulibeba.


  Takwimu za kilimo cha muhogo duniani zinaonyesha kuwa, Afrika ni bara la tatu duniani kwa kuzalisha zaidi muhogo ambapo huzalishaji takriban tani milioni 102.6 kila mwaka.


  Tanzania ni nchi ya nne kati ya wazalishaji wakubwa wa muhogo barani Afrika baada ya Nigeria, Ghana na Kongo DRC ambapo inaelezwa kwamba karibu ekari 670,000 za ardhi ya kilimo zinatumika kuzalisha muhogo, zao linalochangia karibu asilimia 15 za chakula kwa nchi nzima ambapo karibu kaya 1,213,958 huzalisha muhogo nchini.


  Mikoa inayozalisha muhogo kwa wingi ni Mwanza, Mtwara, Lindi, Shinyanga, Tanga, Ruvuma, Mara, Kigoma, Pwani na maeneo yote ya Zanzibar. Ukanda wa Ziwa ni wazalishaji wakubwa zaidi ikifuatiwa na ukanda wa kusini. Mkoa wa Ruvuma huzalisha kati ya 5-10% ya uzalishaji wote Tanzania.


  Muhogo ndilo zao la pili kwa kuchangia pato la taifa kwa asilimia 19 baada ya mahindi.


  Taarifa ya Shirika la Utafiti wa Viwanda na Maendeleo ya Mazao ya Chakula Tanzania (TIRDO) inaonyesha kuwa zao la muhogo linastawi kirahisi.


  Hii ni pamoja na kuvumilia ukame na halishambuliwi na magonjwa au wadudu wanaoathiri mazao mengine na pia muhogo unaweza kutoa mazao mengi katika ardhi duni ambayo mazao kama mahindi hayawezi kustawi.

  Kwa mujibu wa TIRDO, muhogo ni zao la pili kuwa na wanga mwingi baada ya viazi vitamu ambavyo vina asilimia 20 hadi 30 ya wanga na kwamba asilimia 84 ya zao hilo hutumika kama chakula cha binadamu.
  Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kitanga, Wazir Yakoub Wazir, akisalimiana na Mkurugenzi wa taasisi ya Wanawake wa Afrika, Anna Salado.
  Mratibu wa Mradi wa Green Voices kutoka Hispania, Alicia (kushoto) na Anna Salado wakipata msosi huku wakiwa na madafu yao wakati walipotembelea mradi wa kusindika muhogo katika Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe Julai 13, 2016.

  0 0

  VIONGOZI wa Chuo cha Acharya cha Nchini India wawakutanisha watanzania waliosoma katika chuo Acharya jijini Dar es Salaam leo.
  Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa Chuo Acharya huko nchini India, Premnath Reddy amesema kuwa wapo tayari kuwasaidia wanafunzi waliosoma katika chuo cha Acharya watakaoanzisha wazo zuri la biashara."Tupo tayari kusaidia wanafunzi watakao kuwa na wazo zuri la kibiashara kwa wanafunzi waliosoma nchini India katika chuo cha Acharya " Amesema Reddy. Hayo amesema kwa wanafunzi hao ili kutokuteemea kuajiliwa tuu na waweze kujiajili wenyewe kutokana na elimu waliyoipata wakiwa chuoni.
  Mwenyekiti wa Chuo Acharya huko nchini India, Premnath Reddy akizungumza na wanafunzi wa hapa nchini waliosoma chuo cha Acharya kwanzia mwaka 2009 hadi mwaka huu katika hafla fupi iliyowakutanisha jijini Dar es Salaam na kula na kunywa pamoja.
  Mwananfunzi aliyesoma kuchu cha Acharya nchini India, Zakina Naushad Karmali akizunguma jijini Dar es Salaam na wanafunzi waliosoma katika chuo cha Acharya
  Mkurugenzi wa chuo cha Acharya cha nchini India, Vishesh Chanrashelear akizungumza na wanafunzi wa kitanzania waliosoma katika chuo cha Acharya katika hafla iliyowakusanya jijini Dar es Salaam.
   Watanzania waliosoma India chuo cha Acharya wakiwa wamesimama na kuimba wimbo wa Taifa wakati wa hafla iliyowakutanisha wanafunzi waliosoma chuo kimoja.
   Muunguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Mwanafunzi aliyewahi kusoma katika chuo cha Acharya, Christina Mwandalima akizungumza na wanafunzi wenzie pamoja na viongozi wa Chuo chao  waliofika kujumuika pamoja na kula na kunywa pamoja.
  Mwanafunzi wa chuo cha Acharya akizungumza katika mjumuiko wa wanafunzi wa chuo chao jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa ‘pale kati patamu’ ulioimbwa na Msanii Ney wa Mitengo kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili.
  Msanii huyu amekuwa na tabia na mienendo yenye kuchafua Sekta ya Sanaa yeye binafsi kupitia kutoa kazi chafu na kufanya maonesho yenye kukiuka maadili. Kazi zake zikikiuka maadili na kudhalilisha utu wa mwanamke sambamba na kutoa lugha za matusi na za kudhalilisha watu wa kada mbalimbali.

  Ieleweke kwamba kwa mujibu wa kifungu namba 4(L) cha Sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepewa jukumu la kuhakikisha linalinda maadili miongoni mwa wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi yoyote ya sanaa.

  ikumbukwe kwamba BASATA limeshamuita na kumuonya msanii huyu mara kadhaa kutokana na tabia yake ya kutoa kazi zisizokuwa na maadili na aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio haya kwa makusudi ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha Sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu kazi ya sanaa kama kazi nyingine. Kwa sasa Msanii huyu ametoa wimbo mwingine wa Pale Kati patamu ambao uko mitandaoni ukipambwa na picha chafu zinazoonesha mwanamke akiwa mtupu yaani uchi wa mnyama.

  Kwa mantiki hii BASATA halitavumilia wasanii wachache ambao wanataka kuigeuza tasnia ya sanaa na wasanii genge la wahuni wasio na staha na wanaojipanga kuibomoa jamii. BASATA linapenda kueleza ya kufuatayo
  BASATA linatamka kuwa limeufungia wimbo huu rasmi kutumika kwa namna yoyote ile.
  Aidha pamoja na adhabu ya kufungia wimbo huu hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
  Aidha, BASATA linawataka Wasanii wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu mara wanapotengeneza kazi zao.
  SANAA NI KAZI, TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI

  Godfrey Mngereza
  KATIBU MTENDAJI.

older | 1 | .... | 906 | 907 | (Page 908) | 909 | 910 | .... | 1898 | newer