Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

BUHIGWE NA UVINZA ZAANZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA PS3 MKOANI KIGOMA

$
0
0


Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa PS3, Dk Conrad Mbuya (kushoto) akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo bahasha iliyo na majina ya Wilaya mbili zitakaanzo anza utekelezaji wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya seklta za Umma (PS3) Mkoani Kigoma. Mradi huo unafadhiliwa na Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID).
Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo akionesha bahasha hiyo kwa washiriki. Kushoto ni Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa PS3, Dk Conrad Mbuya na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Mrisho Mrisho.
Washiriki wakiwepo wakuu wa Wilaya wakishangilia kwa uteuzi huo.


Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mlindoko akifuatilia mkutano huo.
Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa PS3, Dk Conrad Mbuya (kushoto) akizungumza namna utekelezaji utakavyofanyika. Wengine ni Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo (katikati) na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Mrisho Mrisho.


Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa PS3, Dk Conrad Mbuya alisema mradi utaanza mara moja utekelezaji wake na kwa kuanzia wataanza na mifumo ya tehama kwa kuangalia hali ya miundombinu na kuiboresha.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani kutoka Idara ya Mkaguzi Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Alphonce Muro akijadili jambo na Mkurugenzi Msaidizi Utumishi, Kajura wakati wa mkutano huo.
Washiriki wakiwa katika mkutano huo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Mwakilishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma akiwasilisha majadiliano yao.
Mshiriki wa mkutano akiuliza swali
Mkurugenzi Msaidizi Utawala kutoka Tamisemi, Mrisho Mrisho akifafanua baadhi ya vitu wakati wa mkutano huo na hasa alizungumzia umuhumi wa uboreshaji wa idara ya Masijala ya siri katika Halmashauri.


Washiriki wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallagyo wakati akifunga mkutano huo.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo akihutubia wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.


Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo akitangaza majina ya Halmashauri Mbili za Wilaya ambazo zitaanza katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mradi wa PS3 mkoani Kigoma. Halmashauri za Uvinza na Buhigwe zilipita.

***************

HALMASHAURI mbili za Uvinza na Buhigwe mkoani Kigoma zimefanikiwa kuchaguliwa kuanza utekelezaji wa mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) awamu ya kwanza chini ya ufadhili wa Shirika la Maemdeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).

Halmashauri hizo zimechaguliwa miongoni mwa halamashauri nane za mkoa huo ambazo zipo katika mpango wa utekelezaji wa mradi huo unaotekelezwa katika mikoa 13 na utazinufaisha halmashauri 93 hadi kukamilika kwake.
Mradi huo wa PS3 ulizinduliwa mkoani Kigoma juzi na kufanya jumla ya mikoa 11 kati ya 13 iwe imeshazindua mradi huo ambapo mikoa mingine ambayo inatarajiwa kuzindua Jumanne ijayo ni Kagera na Rukwa na kufanya halmashauri 22 kati ya 93 kuanza utekelezaji wa mradi kwa awamu ya kwanza na utatekelezwa katika kipindi cha miaka mitano kwa gharama ya dola za kimarekani Milioni 62.

Mradi huo wa PS3 utatekelezwa kwa awamu mbili mkoani Kigoma ambapo awamu ya kwanza inaanza mwezi huu na awamu ya pili itaanza Novemba mwaka huu.Awamu ya kwanza ya mradi itatekelezwa katika Halmashauri mbili zenye uhitaji zaidikatika sekta za umma .Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa PS3, Dk Conrad Mbuya alisema alisema mradi utaanza mara moja utekelezaji wake na kwa kuanzia wataanza na mifumo ya tehama kwa kuangalia hali ya miundombinu na kuiboresha.

Dk Mbuya alisema kwa mkoa wa Kigoma Halamsahauri ambazo zitaanza kunufaika na mradi huo ni Halmashauri ya Wilaya Uvinza na Buhigwe ambazo watendaji kutoka halamshauri husika wanaanza mafunzo leo ya siku moja na wiki ijayo madiwani wao nao watapatiwa mafunzo maaluma ya namna ya kushiriki katika utekelezaji wa mradi na yatafayika kwa wiki moja mjini Kigoma.

Mradi huo wa PS3 unalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa na tafiti tendaji Ushirkiano huo wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha.

Aidha Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo aliwataka watendaji katika halmashauri hizo kuufanya mradi huo kuwa endelevu na haitakuwa busara wahisani wakiondoka na kila kitu kinakufa.“Tukahakikishe kuwa mradi huu unakuwa endelevu na hata wahisani wakimaliza muda wao sisi tuweze kuendelea kwa mafanikio ambayo yatazisaidia halmashauri zetu katika utendaji,”alisema Pallangyo.

Awamu ya pili ambayo itatekelezwa mkoani Kigoma kwa halamashauri sita zilizobaki utafanyika kuanzia mwezi Novemba mwaka huu na utahusisha Halmashauri za Wilaya ya Kakonko, Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na Halamashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.

PS3 ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID. Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo ni Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na Urban Institute.
Mradi wa PS3 utatekelezwa katika miakoa 13 ambayo ni Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga.

MKUU WA MKOA WA MBEYA ATEMBELEA PANDAHILL PATAKAPOCHIMBWA MADINI ADIMU DUNIANI KABLA YA KUANZA UCHIMBAJI

$
0
0

Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited ndg Derick ambayo ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ramani itakayotumika katika mradi huo
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza jambo na viongozi wa kisiasa, kamati ya Ulinzi na usalama wilaya ya mbeya, uongozi wa kampuni ya Pandahil limited ambayo ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya
Mwakilishi wa kampuni ya Pandahil limited Mbeya Emanuel Kisasi ambayo ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya adimu aina ya Niobium akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la mradi eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya
Eneo ambalo litahusika kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla mwenye suti ya kaki akitembezwa na mwenyeji wake Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited ndg Derick ambayo ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya .(Picha E.madafa, D.Nyembe)

Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited ndg Derick ambayo ndiyo inahusika na uchimbaji wa madini ya adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer katika eneo la Songwe Gerezani Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla aneo ambalo litachimbwa madini hayo.
Ramani ya mradi

Na Mwandishi wetu,Mbeya

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametembelea eneo la Pandahill kata ya Songwe mahali ambapo patachimbwa madini adimu aina ya Niobium ambayo hutumika kutengeneza Ndege na computer.Mpaka sasa madini hayo huchimbwa bara la Amerika tu na kugundulika kwa madini hayo Tanzania utakuwa mgodi wa nne duniani na wa kwanza Afrika

Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited ndg Derick amesema imewachukua zaidi ya miaka 5 kufanya utafiti na kugundua uwepo wa madini hayo, taratibu zote za kisheria zimekamilika na kampuni hiyo itawekeza zaidi ya shilingi bilioni 500 katika mradi huo na mradi utatengeneza ajira watu 500 na mradi huo utaanza uzalishaji mapema mwaka 2018.

Mkuu wa mkoa ameipongeza kampuni hiyo kwa ugunduzi na uwekezaji huo mkubwa sanjali na kuwataka na kutoa ushirikiano na ushirikishwaji wa kwa viongozi na wananchi kwa kila hatua ili kuweka wazi mradi huo kwa wananchi.Aidha amewataka wananchi na viongozi kutoa ushirikiano kwa kampuni hiyo ili wananchi wanaozunguka eneo hilo uzalishaji utakapoanza wafaidike na ajira, huduma za jamii na kodi mbalimbali kwa hslmashauri na serikali kuu

Pia amewashukuru kwa mchango wa madawati 400 ambayo yatasambazwa kwa shule 7 zilizokuwa na upungufu wa madawati.Hata hivyo Gereza la Songwe mkoani Mbeya linatalaji kuvunjwa na kuhamishiwa sehemu nyingine kupisha uchimbaji wa madini hayo adhimu ya duniani ya niobium baada ya madini hayo kugundulika kuwepo karibu na maeneo ya gereza hilo la songwe.

Kwa mujibu wa taarifa za wataalam zinadai kuwa madini ya mgodi huo huchanganywa na metali zingine na vyuma vyake hutumika kwenye ujenzi bomba la kupitishia mafuta sanjali na metali zake kutumika katika injini za ndege ili kuzuia mitambo yake kutopata joto kali.Hata hivyo

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHUDHURIA BARAZA EID EL FITRI ZANZIBAR

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein baada ya kulihutubia Taifa kwenye Baraza la Eid El Fitry lililofanyika leo Julai 06,2016 katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein Nje ya ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni mjini Zanzibar Baada ya kumalizika kwa Baraza la Eid El Fitry lililofanyika leo Julai 06,2016.
 akamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid Nje ya ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni mjini Zanzibar Baada ya kumalizika kwa Baraza la Eid El Fitry lililofanyika leo Julai 06,2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohamed Nje ya ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni mjini Zanzibar Baada ya kumalizika kwa Baraza la Eid El Fitry lililofanyika leo Julai 06,2016. (Picha na OMR)

HALMASHAURI ZA UVINZA NA BUHIGWE ZAPEWA MAFUNZO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA PS3 MKOANI KIGOMA

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kihoma, Kanali Marco Gaguti akizungumza leo wakati wa mafunzo ya siku moja kwa watendaji wa halamshauri mbili za Buhigwe na Uvinza ambazo zimechaguliwa kuanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika lake la Misaada la Kimataifa (USAID).

Kanali Gaguti aliwataka watumishi hao wa halmashauri hizo mbili kuchukulia fursa hiyo ya kuanza utekelezaji wa ,radi huo kwa umuhimu kubwa kwani kuanza kwao ni kutokana na changamoto zilizipo katika Halmashauri zao.

"Tutumie fursa hii kikamilifu ili kukabiliana na changamoto zilizopo katika halmashauri zetu, tumeona kuwa tuna miradi mingi katika maeneo yetu lakini hatuitumii vizuri kutusaidia hivyo tuanze mradi huu wa PS3 kwa kumbukumbu kwa kupiga hatua nzuri ili tuondoke hapa tulipo katika changamoto,"alisema Kanali Gaguti.


Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, Benard Rusomyo akiwasilisha taarifa ya Wilaya yake.
wakilishi wa Halamashauri ya Buhigwe, ambaye ni Afisa Elimu ya Msingi, Mwl. Freddy Fande akiwasilisha taarifa ya Halmashauri hiyo.
Mshauri wa Masuala ya Fedha wa PS3, Victor Msoma akizungumza jambo baada ya mawasilisho ya Halmashauri.



Washiriki wa kutoka Halmashauri za Uvinza na Buhigwe wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe.
Mwanasheria wa Kigoma Grace Letawo akifuatilia mijada
Mijada katika makundi ilianza kwa ajili ya utambuzi wa wadau mbalimbali wa maendeleo katika Halmashauri. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.




Mshauri wa Masuala ya Utawala Bora wa Mradi wa PS3, Joel Shimba akifafanua jambo alipokuwa na kundi la Halmashauri ya Uvinza.

Washiriki kutoka Halamashauri ya Wilaya ya Buhigwe, wakiwa katika mjadala wa kundi lao.

Mtaalam wa masuala ya uongozi kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI) akifafanua jambo.
Mshauri wa Masuala ya Utawala bora wa mradi wa PS3, Nazar Sola akifuatilia kwa makini mjadala katika moja ya makundi.
Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa PS3, Dk Conrad Mbuya akifuatilia kwa makini mijadala katika makundi ambayo yalikuwa yakifanya utambuzi wa wadau wengine katika Halmashauri na kuangalia namna ambavyo shughuli za wadau zilikuwa zikiratibiwa. Pia makundi yalipaswa kuangalia maeneo ambayo mradi unaweza kushirikiana na sekta binafsi ili kuimarisha mifumo ya sekta za umma.
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Marko Gaguti akifuatilia kwa makini mjadala katika Halamashauri yake.

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR ATOA SKUKU KWA VIONGOZI WA JIMBO LA KIEMBE SAMAKI

$
0
0
 Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na viongozi wa Jimbo la Kiembe Samaki jana julai 7 kabla ya kuwapa pesa kwaajili ya skukuu hafla hiyo imefanjika katika tawi la CCM Kiembe samaki Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi fedha katibu wa wadi ya Kiembe samaki Bi. Zainab Ali Suleiman.

WAZIRI JANUARY MAKAMBA ASHIRIKI SWALA YA EID EL FITRI JIJINI TANGA

$
0
0


Waziri wa Nnchi ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano, mazingira) Mh.January Makamba  (wanne kushoto) akishiriki swala ya Eidd na Waumini wengine wa Dini ya Kiislam waliojumuika kwenye msikiti wa Ijuma mjini Tanga,ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Waumini wa dini ya Kiislam wakiwa katika swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye msikiti wa Ijumaa,mjini Tanga leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Mh.January Makamba akisilisikiliza Mawaidha mara baada ya Swala



Mh.January Makamba Akepeana mkono wa Iddi na Baadhi ya Wauumini waliokuwepo msikiti baada ya Ibada.
Mh.January Makamba Akipiga picha ya ukumbusho baada ya swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye msikiti wa Ijumaa,mjini Tanga leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

MKUU WA WILAYA YA IKUNGI ATANGAZA SIKU YA JUMATANO KUWA SIKU YA KAZI ZA PAMOJA

$
0
0
Na Mathias Canal, Singida

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu ametangaza rasmi siku ya Jumatano kuwa siku ya kazi za pamoja katika majengo ya Umma katika Vijiji vilivyopo Wilayani humo.

Tangazo hilo amelitoa kwenye halfa iliyofanyika katika ukumbi wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida wakati anakabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye kwa sasa amestaafu Gishuli Charles.

Mtaturu amesema kuwa Uongozi utachagua kama ni Shule, Zahanati au Utengenezaji wa Barabara n.k.ambapo Wananchi wote watapaswa kushiriki kazi hiyo ili warejeshe moyo wa kushiriki shughuli za maendeleo ambapo mkuu huyo amesema yeye atafanya kazi ya kupita katika maeneo tofauti kuungana na Wananchi katika kukamilisha kwa vitendo jambo hilo..

Amewakumbusha wananchi kuwa wakati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na wenzake waliokuwa wanaanza harakati za kudai Uhuru walienda Umoja wa Taifa wakahakikisha tunaweza kujitawala na kujisimamia wenyewe bila mkoloni.

Mwaka 1961 tulipopata Uhuru Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alieleza sasa tumepata uhuru tubadili malengo ya Taifa iwe ni Uhuru na Kazi aliamini kupitia kazi tutapata maendeleo.Awamu ya Tano imekuja na kauli mbiu ya “HAPA KAZI TU”; kwa maana hiyo hiyo kuhimiza Wananchi kufanya kazi na kazi ndio kipimo cha utu.

Mkuu huyo amesema kuwa wananchi wote wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kuboresha maisha ya kila mmoja na familia zetu kwa ujumla.Mkuu huyo amesema kuwa Kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi mwaka 2015 – 2020. Ibara ya 49 imeeleza Serikali kuongeza huduma za Afya, kuongeza Wataalamu wa Afya kwenye Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya n.k.


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwa ofisini mara baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye kwa sasa amestaafu Gishuli Charles.
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye kwa sasa amestaafu Gishuli Charles na baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye kwa sasa amestaafu Gishuli Charles

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu wakikabidhiana nyaraka na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye kwa sasa amestaafu Gishuli Charles.
Amesema Ilani imetambua yaliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Nne katika Sekta ya Afya kama msingi wa kuendeleza juhudi zaidi kupiga vita Malaria, UKIMWI, Vifo vya Mama na Mtoto n.k. Uboreshaji na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.Katika Wilaya ya Ikungi kuna upungufu wa asilimia 62% ya Zahanati hivyo kufanya akina Mama Wajawazito kutembea mwendo mrefu kufuata ushauri wa kitaalamu.

Huduma ya kuzuia maambukizi ya VVU kwenda kwa mtoto (PMTCT) vimeongezeka ila bado havitoshi; Vituo vya tiba vya maangalizi ya wanaoishi na VVU (CTC) bado ni vichache sana.

Ili kutatua changamoto ya huduma duni za afya Mtaturu ameshauri Wananchi kuhamasishwa kujiunga kwenye Mifuko ya Bima ya Afya kama NHIF, CHF n.k. na kusema kuwa Faida ya kujiunga na Bima ya Afya msingi wake ni kuwa ugonjwa hauna taarifa hivyo unaweza kuugua siku hauna fedha Bima ikakusaidia.

Katika sekta ya upatikanaji maji safi na salama amesema kuwa Ni lengo la Serikali kuhakikisha Wananchi wake wanapata Maji Safi na Salama kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo na Wananchi hivyo ameahidi Kuzipa uwezo Kamati za Maji katika Vijiji ili kusimamia Miradi iliyopo iwe endelevu ikiwemo kusoma Mapato na Matumizi kwa Wananchi kwa Mujibu wa Sheria.


Katika swala la Ukusanyaji wa Mapato Mtaturu amesema kuwa Changamoto iliyopatikana kipindi kilichopita ni kuwa chini ya 80% ya lengo la ukusanyaji mapato hivyo Kuanzia tarehe 01Julai, 2016 Serikali imeamua sasa Halmashauri zitakusanya zenyewe mapato badala ya Wazabuni.


Miraji Mtaruru amezungumzia pia suala la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi SURA YA TANO YA ILANI YA UCHAGUZI MKUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI Ibara ya 56. Imeeleza dhamira ya kuwezesha Wananchi kiuchumi kupitia Ushirika (SACCOS& VICOBA) ikizingatiwa kupitia vikundi ndio mahali pekee unaweza kuwapatia mitaji na kutakuwa na nidhamu ya fedha.


Hivyo amewahimiza Maafisa Ushirika, Maendeleo ya Jamii kuendelea kuwajengea uwezo Wananchi ili kurahisisha Serikali kushusha fedha za mitaji.Katuika swala la Watumishi Hewa Mtaturur amesema kuwa Pamoja na juhudi za Serikali kuboresha masilahi ya Watumishi ila kumejitokeza uzembe mkubwa wa watu kulipwa wasiostahili.

“Natoa muda wa Wiki moja Mkurugenzi na timu yako mnipatie taarifa kamili kuhusu Wafanyakazi hewa na imebainika Idara ya Elimu ndio inayoongoza kuwa na Watumishi hewa, swali la kujiuliza Afisa Utumishi, Mratibu Elimu Kata ambao kazi yao kila siku ni kushughulika na Kada hiyo anakuwa hajui kama kuna watu wanalipwa wasiokuwepo kazini? Hali hii haikubaliki na hakika tutachukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kuingizia Serikali hasara ya aina yeyote.” Amesema Mtaturu

Mkuu huyo amesema kuwa Serikali ya awamu ya Tano imeamua kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Ibara ya 51; imefafanua namna Elimu iliyowekewa msisitizo. Elimu ya Awali; Elimu Msingi na Sekondari hadi Chuo Kikuu ikiwa ni pamoja na Kuboresha masilahi ya Walimu ikiwa pamoja na madai yao ili wapate moyo wa kufanya kazi kwa bidii zaidi, na Ahadi ya Elimu bila kulipa ada Shule ya Msingi hadi Kidato cha Nne imeanza utekelezaji mwaka huu ingawa imekutana na changamoto kwa kupata upungufu wa Madarasa n.k.

Aidha Pamoja na hayo bado kuna baadhi ya watoto wenye sifa za kwenda Shule hawajaandikishwa; kimsingi ni haki ya kila mtoto kupatiwa Elimu, hivyo wazazi wasiowapeleka Watoto Shule wanakiuka Sheria.Mtaturu ametoa maagizo ya Watoto wote waliofikia umri wa kwenda Shule; Maafisa Tarafa, Watendaji Kata na Vijiji wampepe taarifa na hatua walizochukua.

“Kuhusu upungufu wa Nyumba za Walimu, Vyumba vya Madarasa, Maabara zisizokamilika, matundu ya vyoo, vitendea kazi n.k. ni lazima tuweke mpango wa pamoja kuondoa changamoto hizo ili kuhakikisha Watoto waliopo Shuleni wanapata elimu bora” Amesema Mtaturu

Wilaya ya Ikungi ina jumla ya wakazi 272,959 na ongezeko la watu kwa mwaka ni 2.8% hivyo sasa kunakadiriwa kuwa 303,000 kwa mwaka 2015/2016 kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2012

Rais Magufuli ahutubia Baraza la Eid el-Fitr na kumpongeza Mufti wa Tanzania kwa kuwaunganisha waislamu

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika baraza hilo la Eid Elfitri.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ali kwa juhudi zake za kuwaunganisha waislamu wote na kupanua uwigo wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kutoa huduma za kijamii na ameahidi kuwa serikali ya awamu ya tano itaunga mkono juhudi hizo.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo tarehe 06 Julai, 2016 wakati akihutubia Baraza la Eid el-Fitr kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lililofanyika kitaifa katika viwanja vya Karimejee Jijini Dar es salaam.

Dkt. Magufuli amesema kitendo cha kuwaunganisha waislamu wote katika Baraza la Eid el-Fitr kinafungua ukurasa mpya na ni moja ya hatua muhimu za kuimarisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa waislamu wa makundi mbalimbali pamoja na watanzania wengine waisio waislamu.

Aidha Rais Magufuli amezungumzia juhudi zinazofanywa na BAKWATA katika kuimarisha taasisi zake zinazotoa huduma za kijamii na kulinda mali zake akisema serikali itahakikisha mali zote za waislamu zinakuwa salama na kwamba wote waliodhulumu mali za waislamu watazirejesha.

Awali akisoma taarifa, Katibu Mkuu wa BAKWATA Alhaji Suleiman Said Lolila amesema BAKWATA inakusudia kupanua huduma za kijamii kwa lengo la kuwahudumia wananchi ikiwemo kujenga chuo kikuu Mkoani Dodoma na pia amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi zake za kuondoa umasikini huku akimtaka asikatishwe tamaa na wachache watakaoudhika kwa kuguswa na hatua zinazochukuliwa.

Nae Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali pamoja na kumshukuru Rais Magufuli kwa kuongoza bila ubaguzi amewataka watanzania kuungana na juhudi za serikali kupinga matendo maovu ikiwemo rushwa na ufisadi na pia amelaani ndoa za jinsia moja akisema ni kinyume na maadili ya dini.

Baraza la Eid el-Fitr pia limehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, mabalozi na wabunge.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
06 Julai, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mufti Mkuu Sheikh Aboubakar Zubeir.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikhe Aboubakar Zubeir wakati alipowasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya Baraza la Eid El fitri lililofanyika katika viwanja hivyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Sheikhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum mara baada ya kuwasili.


MKURUGENZI WA NHC BW. MEHEMIA MCHECHU AZUNGUMZIA MIRADI YA SHIRIKA HILO KATIKA MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0

Mkurugenzi wa Shirika la Numba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maonyesho ya TANTRADE Sabasaba yanayoendelea katika viwanja hivyo vilivyopo barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam ambapo ameelezea uendelezaji na uuzaji wa nyumba katika maeneo mbalimbali unaoendelea katika miradi yao iliyopo nchi nzima.
Mkurugenzi wa Shirika la Numba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akifafanua jambo kuhusu mipango ya shirika hilo wakati akizungumza na wanahabari katika banda la maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya TANTRADE barabara ya Kirwa.
Clara Lumbanga Ofisa Maendeleo ya Biashara NHC akimuangalia mmoja wa wananchi waliotembelea katika banda hilo wakati alipokuwa akisaini kitabu cha wageni.


Mkurugenzi wa Shirika la Numba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akifurahia jambo na baadhi ya wateja waliotembelea katika banda hilo.
Clara Lumbanga Ofisa Maeneleo ya Biashara NHC akitoa maelezo kwa wananchi mbalimbali waliotembelea katika banda la Shirika la Nyumba la Taifa NHC.

Clara Lumbanga Ofisa Maeneleo ya Biashara NHC akipokea wageni mbalimbali waliofika katika banda hilo ili kujionea shughuli mbalimbali za shirika hilo.
Bw. Emmanuel Lyimo Ofisa Utafiti wa Masoko akizungumza na Mkurugenzi wa Blogu ya Fullshangweblog Bw. John Bukuku wakati alipotembelea katika banda la NHC.

Clara Lumbanga Ofisa Maeneleo ya Biashara NHC akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika la NHC wanaoshiriki katika maonyesho ya TANTRADE yanayofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba jijini Dar es salaam katika barabara ya Kirwa.

RAIS DKT MAGUFULI ASALIMIA WANANCHI BAADA YA KUHUTUBIA BARAZA LA IDDI VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria  Baraza la Iddi alilolihutubia kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Julai
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na mtoto Asma Maulid baada ya kuhubia Baraza la Iddi kwenye  ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam. Picha na PMO

WANANCHI WAENDELEA KUFURAHIA HUDUMA ZA PPF MAONESHO YA SABASABA

$
0
0

Msajili wa Hazina Lawrence Mafuru (katikati) Mkurugenzi wa Sheria wa Mfuko wa Pensheni PPF, Vupe Ligate (wa tano kutoka kushoto) Mke wa Msajili, Noela Mafuru (wa tano kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Fedha na Mipango, Benny Mwaipaja, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa PPF nje ya Banda lao kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba.

Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa PPF, Pauline Msanga, akiwahudumia wateja , waliofika katika Banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Mafoto Blog
Afisa Michango wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Glory Maboya (kulia) akimhudumia mmoja kati ya wateja waliofika katika Banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Maafisa Michango wa Mfuko wa PPF, wakiwahudumia wateja , waliofika katika Banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.


Afisa Michango wa Mfuko wa PPF, Tula Mwigune, akitoa elimu kwa wateja , waliofika katika Banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Msajili wa Hazina Lawrence Mafuru (kushoto) akisaini Kitabu cha Wageni wakati alipowasili kutembelea Banda la Mfuko wa PPF, leo. Kulia ni mkewe, Noela Mafuru.

Afisa Huduma kwa Wateja wa PPF, Mwajuma Msina, akiwahudumia wateja , waliofika katika Banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Afisa Uwekezaji wa PPF, Jonas Mbwambo, akifafanua jambo kwa baadhi ya wananchi waliofika katika Banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa Uendeshaji wa PPF, Pauline Msanga (kulia) akimkabidhi Kitambulisho Kwangu Jessey, mmoja kati ya wateja waliojiunga na Mfuko huo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa PPF, Elihuruma Ngowi (kulia) akiwaelekeza jambo wateja waliokuwa wakijaza fomu ya kujiunga na huduma ya Wote Scheme kwenye Banda la PPF Sabasaba.

Vijana Dar wajiandikisha na masomo ya VETA kupitia simu za Airtel yajulikanayo Kama VSOMO

$
0
0
 Mabalozi wa Airtel Tanzania wakitoa maelezo kwa wateja waliotembelea banda la Airtel, juu ya mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mikononi ujulikanayo kama VSOMO unaotolewa na VETA kwa kushirikiana na Airtel kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Ikiwa ni takribani mwezi moja tangu kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na VETA kuzindua application ijulikanayo Kama VSOMO na kuwawezesha watanzania kusoma masomo ya ufundi kupitia simu zao za Mkononi.

Airtel na VETA imeendelea kutoa elimu kwa vijana na wakazi wa Dar katika maonyesho ya sabasaba ili kuhakikisha Taarifa taarifa muhimu kuhusu mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu zinawafikia watanzania wengi na kuwanufaisha vijana nchini  kujisomea na kuongeza ujuzi.
Mpaka sasa zaidi ya vijana 700 mkoani Dar Es saalam wameshajiandikisha na Kati yao wameshaanza  kusoma kozi mbalimbali.
 Mabalozi wa Airtel Tanzania wakitoa maelezo kwa wateja waliotembelea banda la Airtel, juu ya mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mikononi ujulikanayo kama VSOMO unaotolewa na VETA kwa kushirikiana na Airtel kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
 Balozi wa Airtel Tanzania, Emmanuel Alfred akitoa maelezo juu ya mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mikononi ujulikanayo kama VSOMO unaotolewa na VETA kwa kushirikiana na Airtel kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

 Mhitimu wa Kozi ya umeme Salehe Shomari, akitoa maelezo kwa waliotembelea banda la VETA juu ya mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mikononi ujulikanayo kama VSOMO unaotolewa na VETA kwa kushirikiana na Airtel kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Veta Kilichopo Kipawa Jijini Dar es salaam,Mhandisi Lucius Lutenganya akitoa maelezo kwa waliotembelea banda la VETA juu ya mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mikononi ujulikanayo kama VSOMO unaotolewa na VETA kwa kushirikiana na Airtel kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

WAGENI WAENDELEA KUFURIKA MALI ASILI NA UTALII KATIKA MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0

SEHEMU ya wageni mbalimbali wakiingia na wengine wakitoka kutembelea mabanda ya mali asili na Utalii kwenye viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere Dar es Salaam leo.
Maofisa wa Mali Asili na Utalii wakiwahudumia wageni waliofurika kwenye mabanda yao.
Afisa Mkuu wa Misitu Charles Ng'atingwa akiwafafanulia jambo wageni waliotembelea moja ya banda kwenye maonesho hayo.
Wageni waliotembelea moja ya banda kwenye maonesho hayo.
Afisa wa Maliasili na Utalii, Munir Shellimoh akiwafafanulia jambo wageni waliotembelea moja ya banda kwenye maonesho hayo.




Mmoja wa wageni akiangalia kumbukumbu za historia ya mawaziri waliwahi kuhudumu katika wizara ya Mailiasili na Utalii.









Afisa wa Maliasili na Utalii, Deogratius Kahwa akiwafafanulia jambo wageni waliotembelea moja ya banda kwenye maonesho hayo.













Afisa wa Maliasili na Utalii, Deogratius Kahwa akiwafafanulia jambo wageni waliotembelea moja ya banda kwenye maonesho hayo.







Mhandisi Righton John na Afisa Masoko wa Air Tanzania, Lily Fungamtama wakiwawapa maelezo wageni waliotembelea banda la Maliasili na Utalii, kwenye maonesho hayo.



















Afisa wa Maliasili na Utalii, Abdallah Mnongwa akiwafafanulia jambo wageni waliotembelea moja ya banda kwenye maonesho hayo.







(Imeandaliwa na Robert Okanda www.robertokanda.blogspot.com)

AKINAMAMA DAKAWA WAFUGA NYUKI KUPAMBANA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

$
0
0
TAKRIBAN kilometa 10 kutoka Kijiji cha Dakawa kuna kitongoji cha Magogo kilichoko msituni kabisa ambako pia kuna mashamba ya mpunga.

Msitu huu ambao bado ungali na miti mingi ya asili ambayo imenusurika kucharangwa na wachoma mkaa na wanaotafuta ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo, ndiko akinamama wapatao 30 wameamua kutundika mizinga kwa ajili ya ufugaji wa nyuki katika shamba lenye ukubwa wa ekari nne.


Licha ya kujikwatua vilivyo, lakini wanapoingia katika msitu huu akinamama hawa hawana mchezo kabisa, baadhi yao wanavaa mavazi maalum ya kujikinga na nyuki na kuanza kukagua mizinga yao kama tayari nyuki wamekwishaingia.
Ofisa Nyuki wa Wilaya ya Mvomero, Oscar Kunambi (aliyechuchumaa kushoto) akisaidiana na mwanakikundi cha Dakawa Green Voices, Neema Obeid, kuweka vizuri mzinga.


“Kujipamba ni jambo la kawaida, lakini tunapokuja huku tuko kikazi zaidi,” anasema Neema Obeid huku akipenya kwenye vichaka kuiendea mizinga ambayo iko juu ya miti mikubwa.


Akina mama hao wa kikundi cha Dakawa Green Voices Women Group wameamua kuingia kwenye ujasiriamali wa ufugaji wa nyuki kwa malengo makubwa mawili – kupata fedha kutokana na mazao ya nyuki pamoja na kupambana na mabadiliko ya tabinchi.

“Misitu inateketea, watu wanaendelea kuchoma mkaa na wengine wanafyeka miti ili wapate mashamba, lakini kwa kuanzisha ufugaji huu wa nyuki, kamwe hatutakubali kuona yeyote akikata hata fimbo, achilia mbali miti mikubwa,” anasema Bi. Mariam Bigambo, mshiriki kiongozi wa mradi huo.
Mwanahabari Judica Losai (wa pili kushoto) akimuuliza maswali Ofisa Nyuki wa Wilaya ya Mvomero, Oscar Kunambi, wakati wakiwa kwenye eneo la ufugaji wa nyuki. 

Mariam Bigambo ni miongoni mwa akinamama 10 waliopatiwa mafunzo nchini Hispania mapema mwaka huu na wanatekeleza kwa vitendo mradi wa Green Voices, ambao unafadhiliwa na taasisi inayojihusisha na maendeleo ya wanawake wa Afrika, ijulikanayo kama Women for Africa Foundation inayoongozwa na Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania, María Teresa Fernández de la Vega. Hapa nchini, mradi huo unasimamiwa na asasi ya Environment Media Agenda (EMA) chini ya uratibu wa Bi. Secelela Balisidya.

UTEUZI WA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZA MAJIJI 5, MANISAPAA 21, MIJI 22 NA WILAYA 137 ZA TANZANIA BARA


Shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika kuonyeshwa leo kupitia chaneli ya Trace

$
0
0
Shindano la Airtel Trace Music Stars la Afrika lililofanyika nchini Nigeria linategemea kuonyeshwa live leo kupitia kituo cha television cha Trace chanel 325 saa tatu kamili usiku, katika shindano hilo tutashuhuhia washiriki kutoka nchi 10 barani Afrika wakichuana vikali kila mmoja akionyesha kipaji chake cha kuimba ikiwemo mshiriki kutoka Tanzania Bi Melisa  John

ili kupata burdani na kushuhudia ni jinsi gani washiriki hawa walivyoonyesha vipaji leo saa 3 kamili usiku fungua kituo cha TRACE Urban namba 325 kinachopatikana kupitia kingamuzi cha DSTV.

marudio ya kipindi hiki ni siku yatakuwa siku ya ijumaa saa 8 mchana katika kitu hicho hicho cha TRACE 
Mwanamuziki nguli kutoka nchini marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars Keri Hilson (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki waliongia tatu bora ambao wametoka nchi ya Zambia, Tanzania na Madagascar.

Kamati ya Maadili TFF Yampia pini Jerry Muro, Kutojishughulisha na maswala ya soka kwa Mwaka Mmoja

$
0
0
MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro (pichani) amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka pamoja na kutozwa faini ya Sh. Milioni 3, baada ya kikao cha Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kilichokaa leo kwenye Makao Makuu ya Shirikisho hilo, chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Wilson Ogunde 

Muro amefungiwa baada ya kukutwa na hatia katika mashitaka mawili kati ya matatu yaliyowasilishwa na TFF mbele ya Kamati ya hiyo, ambayo ni kudharau maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF mwaka 2015 alipotakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 5 baada ya kufanya makosa, lakini amekaidi kulipa hadi leo, akahukumiwa kutengana na kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja, wakati shitaka lingine ni kuchochea vurugu na kuhatarisha amani kuelekea mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na TP Mazembe ya DRC.

Katika shitaka hilo, Jerry alidaiwa kuwashawishi mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao na kutowapa nafasi watani wao wa jadi (Simba) kuingia kwenye mchezo huo ambao timu yake ilifungwa bao 1-0 na Mazembe Juni 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Hata hivyo, Jerry Muro alifanikiwa kuishinda TFF katika shitaka la kupingana na maamuzi ya shirikisho hilo juu ya masuala ya utoaji wa haki za matangazo ya Televisheni.

“Kamati ilisikiliza kwa makini taarifa zake alipokuwa anazungumza na vituo vya Redio na kugundua alikuwa sahihi, hivyo hapa hana hatia,”kimesema chanzo.Hata hivyo, Jerry Muro amehukumiwa wakati mwenyewe hakuwepo kwenye kikao na inadaiwa hakutoa taarifa ya maandishi juu ya kutohudhuria kwake.

Badala yake, imeelezwa Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit alifika mapema leo kabla ya kikao kwa ajili ya kutoa taarifa ya mdomo kwamba Muro amekwenda kwao Kilimanjaro kusafisha makaburi ya wazee wake. 

Lakini Kamati ikaamua kuendelea na kikao kwa mujibu wa kanuni na hatimaye kuchukua hatua ilizochukua. Hata hivyo, Muro ana haki ya kukata rufaa Kamati ya Rufaa ya TFF.

RAIS DKT MAGUFULI AMTEUA DEOGRATIUS NDEJEMBI KUWA MKUU WA WILAYA YA KONGWA MKOANI DODOMA

$
0
0


Bw. Deogratius John Ndejembi




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Julai, 2016 amemteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema Bw. Deogratius John Ndejembi anachukua nafasi iliyoachwa na aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. John Ernest Palingo ambaye amehamishiwa Wilaya ya Mbozi katika Mkoa wa Songwe.


Uhamisho wa Bw. John Ernest Palingo kwenda Wilaya ya Mbozi, umefanywa baada ya Mhe. Rais Magufuli kuridhia maombi ya Bw. Ally Masoud Maswanya aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, kuomba uteuzi wake utenguliwe kutokana na sababu binafsi.

Bw. Deogratius John Ndejembi atakula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma siku ya Jumanne tarehe 12 Julai, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.





Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

07 Julai, 2016

WASHINDI WANNE WANYAKUA ZAWADI KATIKA KAMPENI YA FAIDIKA NA AMANA BANK

$
0
0
Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akimkabidhi zawadi ya Television mshindi wa kwanza wa kampeni ya Faidika na Amana Bank Bi PIKIRA NLONGANE wakati wa Hitimisho la kampeni hiyo iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo watanzania wa kuwekeza zaidi,Hitimisho la Kampeni hiyo limefanyika wakati wa siku ya maonyesho ya kimataifa ya biashara saba saba Jijini Dar es salaam ambayo Bank ya amana ni moja kati ya wafanyabiashara waliokuwa na Banda katika Maonyesho hayo .
Zawadi ya JOKOFU kwenda kwa mshindi wa pili ambaye ni SHAKIRA IBRAHIMU imekabidhiwa na kupokelewa na mwakilishi wake ambaye ni AHMED SANDE (Pichani) akikabidhiwa zawadi hiyo na Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD wakati wa utoaji wa zawadi hizo. 
Mshindi wa nne amepata zawadi ya Table Feni ya kisasa yenye AC pia.Pichani ni Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akimkabidhi zawadi Bwana HEMED SULEIMAN ambaye ameibuka mshindi wa nne katika kampeni ya Faidika na Amana Bank iliyochezeshwa ndani ya banda la Bank hiyo katika maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya saba saba Jijini Dar es salaam ambapo washindi wanne wamejinyakulia zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi za kitanzania Million Tano 

Katika kuadhimisha kilele cha kampeni ya FAIDIKA NA AMANA BANK,Bank imezawadiwa wateja wake waliobahatiika kushinda zawadi mbalimbali kutokana na kujiwekea akiba zao na Benk hiyo leo siku ya kilele cha maonyesho ya saba saba Tarehe 7/7/2016.

Wateja hao walichaguliwa kitaalam katika droo iliyochezeshwa ndani ya viwanja vya saba saba katika banda la amana bank na kupewa taarifa ya kufika kupokea zawadi zao kutoka uongozi mkuu wa bank hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji DR MUHSIN SALIM MASOUD.

Kampeni hiyo iliyojumuisha wateja wa akaunti za akiba binafsi kujiwekea akiba katika akaunti zao kuanzia kiasi cha shilingi 500,000 na kuendelea kwa muda wa miezi mitatu na kuweza kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali za vifaa vya matumizi ya nyumbani kama Luninga,Jokofu,Microwevu,Pamoja na Table Feni yenye AC Pia.
Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akizungumza na wanahabari wakati wa Utoaji wa zawadi hizo kwa washindi wanne wa Kampeni ya Faidika na Amana Bank ambapo amewataka watanzania kuwa na utamaduni wa kuwekeza kwani ni utamaduni mzuri na unaofaa kuendelezwa 

Akizungumza na wanahabari mapema leo wakati wa utoaji wa zawadi hizo kwa washindi hao meneja masoko wa Bank hiyo Ndugu DASSU MUSSA amesema kuwa bank ya amana imejipanga kuendelea kuwafikia na kuwapatia watanzania wote huduma bora zenye ubunifu na zenye tija kufuatana na mahitaji yao mbalimbali,huDuma pia ambazo zinafwata misingi ya sheria ya kiislamili kuwapatia faida iliyo halali na kuwaondoa katika mzigo wa riba.

Aidha amewahamasisha watanzania wote kujijiengea na kudumisha utamaduni wa kujiwekea akiba ya pesa kwa ajili ya malengo mbalimbali katika benk ya amana ili wapate kufurahia huduma bora zitowelewazo kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu.
Meneja masoko wa Bank ya Amana Ndugu DASSU MUSSA akifafanua jambo kwa wanahabari ambao walifika kushughudia Utoaji wa zawadi hizo katika Banda lao lililopo katika maonyesho ya saba saba ambayo ndiyo yanaelekea ukingoni 

Ameongeza kuwa kampeni ya faidika na amana bank ni mwanzo tu wa kampeni za bank hiyo zitakazohusisha wateja kuweka fedha na kujishindia zawadi mbalimbali kutoka amana bank ukiachia faida nyingine zipatikanazo kwa wateja kujiwekea akiba huku akisema kuwa wanatarajia kutangaza kampeni nyingine kubwa itakayowezesha wateja wengiine Zaidi kujishindia zawadi lukuki kutokana na kujiwekea utaratibu wa kuweka akiba zao amana Bank Bank ambayo inafwata misingi ya kiislam kikamilifu.
Zawadi ambazo zimetolea kwa washindina Bank ya Amana ambazo jumla zimegharimu kiasi cha shilingi million Tano 


Aidha akiwahamasisha watanzania kujiunga na Bank hiyo amesema kuwa watanzania wengi wamekuwa wakidhani Bank hiyo ni kwa ajili ya waislam jambo ambalo sio kweli huku akitanabaisha kuwa Bank hiyo inahusisha wateja wa Dini zote bila kubagua hivyo watanzania wajiunge kwa wingi katika Bank hiyo,

Washindi waliojishindia zawadi mbalimbali katika hitimisho la Kampeni hiyo ya Faidika na Amana Bank ni pamoja na Pikira Nlongane aliyejishindia zawadi ya Televission kwa kuwa mshindi wa kwanza,Shakira Ibrahim aliyeshika nafasi ya pili na kujishindia zawadi ya Friji kubwa,Khamis Said aliyejishindia Microwave huku mshindi wa nne akiwa ni Hemed Suleiman aliyejishindia Table Feni katika droo hiyo.
Picha ya Pamoja maafisa wa Bank ya amana wakiwa na washindi wa Zawadi mbalimbali za kampeni ya Faidika na Amana Bank mara baada ya utoaji wa zawadi hizo katika maonyesho ya Saba saba 

Bank ya amana ni bank inayoongozwa kwa ustadi mkubwa na misingi ya Dini ya kiislam huku ikiwahudumia watanzania wapatao Elfu 34 katika matawi yake saba nchi nzima hadi sasa.


PICHA NYINGINE ZAIDI WATEJA WAKIMIMINIKA KATIKA BANDA LA AMANA BANK KATIKA MAONYESHO HAYO





















BODI YA FILAMU YATOA MSAADA KWA WAKONTA

$
0
0

Na Shamimu Nyaki WHUSM

Serikali imewataka wadau wa kazi za sanaa kuwasaidia wasanii wachanga katika kazi zao ili waweze kufanikiwa na kutangaza kazi zao kimataifa.

Wito huo umetolewa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi.Joyce Fissoo jijini Dar es Salaam wakati akimkabidhi Bi Wakonta Kapunda Shilingi laki tano kwa ajili ya Safari ya kwenda Zanzibar kushiriki mashindano ya uandishi wa Muswada (Script).“ Napenda kutoa wito kwa wadau wa sanaa kusaidia wasanii wanaochipukia kwani ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya sanaa nchini” Alisema Bi Joyce.

Kwa upande wake Bi Wakonta Kapunda ametoa shukrani kwa watanzania wote ambao wamejitoa kwa ajili ya kufanikisha safari yake na bado wamekuwa watu wa karibu kwake katika kufanikisha ndoto yake ya kuwa mwandishi bora wa Muswada.“Naweza kusema kuwa mimi ni mtu mwenye bahati kwani nimekuwa nikipata msaada kutoka kwa watu mbalimbali wananipigia simu na kunipa faraja lakini najua kuna wengi wapo kama mimi na wamesahaurika hawana msaada “Alisema Bi Wakonta.

Naye Bw. Bazilio Kapunda baba wa Wakonta ameishukuru Bodi ya Filamu Tanzania na wadau wa Filamu nchini kwa msaada mkubwa kwa mtoto wake na kuwaasa wadau wa sanaa nchini kuendelea kusaidia wasanii wanaochipukia.

Wankota Kapunda ni mwandishi wa muswada wa filamu anayechipukia ambaye alipata ajali ya gari mwaka 2012 akiwa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wasichana Korogwe na kupooza mwili mzima, yupo Zanzibar kushiriki katika warsha ya uandishi wa Muswada (Script) iliyoandaliwa na Maisha Film Lab baada ya kuibuka mshindi kati ya washindi wa Muswada (script) 15 baada ya script yake kuibuka mshindi Julai 5, 2016.

Wakonta Kapunda akimshukuru Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo kwa msaada wa shillingi laki 5 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akikabidhi msaada wa shillingi laki 5 kwa Wakonta Kapunda Jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Shamimu Nyaki WHUSM).



Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akisalimiana na Bw. Bazilio Kapunda baba wa Wakonta wakati wa kukabidhi msaada wa shillingi laki 5 kwa Wakonta Kapunda Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (kulia) akizungumza na familia ya Wakonta wakati wa kukabidhi msaada kwa wa shillingi laki 5 kwa Wakonta Kapunda Jijini Dar es Salaam.
 
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images