Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 902 | 903 | (Page 904) | 905 | 906 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Timu nzima ya Kampuni ya Michuzi Media Group (MMG) inawatakiwa Wadau wake wote popote pale mlipo, sikukuu njema ya Idd el Fitr na tuisherehekee kwa amani na mapenzi tele kama ilivyolekezwa katika vitabu vitukufu vya Dini.

  IDD MUBARAK
  MMG TEAM

  0 0


  Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), imekua ikiandaa maonesho haya ya biashara ya kimataifa kila mwaka. Maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yameanza tarehe 28 Juni hadi tarehe 8 Julai, mwaka huu katika uwanja wa maonesho wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam yameendelea kuwa maonesho makubwa na yenye mafanikio katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

  Maonesho haya yanalenga kutekeleza kwa vitendo Sera ya Biashara ya mwaka 2003, ikiwa ni katika jitihada za kukuza biashara. Wigo wa maonesho ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam hutoa fursa mbalimbali.

  Fursa hizo hutolewa kwa wazalishaji, wafanyabiashara na watoa huduma kuonesha bidhaa zao kwa ajili ya kutafuta masoko ya bidhaa hizo, kuweka mazingira ya wafanyabiashara wa nchi mbalimbali kukutana na kufahamiana kwa ajili ya kutengeneza mitandao ya kibiashara.

  Kusaidia waoneshaji wa ndani kupata teknolojia za kisasa za uzalishaji, kujifunza mbinu bora za biashara, ufungashaji, kujilinganisha na wazalishaji wengine wa huduma au bidhaa zinazofanana. Vilevile, husaidia washiriki wa maonesho haya kupata mrejesho wa moja kwa moja kutoka kwa wateja wao kuhusu hisia kwa bidhaa zinazooneshwa. Hali hii humsaidia mzalishaji kujumuisha mapendekezo ya wateja kwenye bidhaa husika katika uzalishaji wa toleo linalofuata, pamoja na kutoa fursa kwa wafanyabiashara kuuza bidhaa zao.  Kila mwaka kumekuwepo na kauli mbiu, kauli mbiu ya mwaka huu inafanana na ya mwaka jana ambayo inasema “Tunaunganisha uzalishaji na masoko”, yenye maana ya kuonesha umuhimu wa mnyororo wa uzalishaji ambao ndio chimbuko la upatikanaji wa bidhaa bora zenye ushindani mkubwa katika soko. Pia kubainisha uhusiano uliopo kati ya uzalishaji na masoko.

  Maonesho haya ya 40 ya biashara ya kimataifa yamekuwa yenye ushiriki mkubwa kutoka mataifa mengi duniani kuliko maonesho yaliyopita. Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade Bw. Edwin Rutageruka anasema kupitia Taasisi inayosimamia maonesho ya Biashara ya Kimataifa Duniani (UFI) ambayo TanTrade ni mwanachama wake imekua ikiyatangaza maonesho haya kwenye tovuti na kuonesha kwamba ni moja ya maonesho yanayotambukila kimataifa. Njia hii husaidia kuyatambulisha, kuyakuza pamoja na kuchangia kuvutia nchi mbalimbali duniani kuomba kushiriki.

  Hali hiyo imechangia nchi nyingi zaidi kuomba kushiriki maonesho ya 40, Bw. Rutegeruka anasema “Nchi 30 kutoka sehemu mbalimbali duniani zinashiriki katika maonesho haya, ikiwa ni ongezeko la nchi tano zaidi ya nchi zilizoshiriki maonesho haya mwaka jana”.

  Kwa kuwa maonesho haya ya kila mwaka yanalenga kutoa fursa ya wafanyabiashara wa ndani kujifunza mambo ya biashara na uzalishaji bora wa bidhaa kulingana na soko la kimataifa, kutengeneza mitandao ya mawasiliano na kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani kuuza bidhaa zao, kampuni za ndani zaidi ya 600 zinashiriki maonesho haya, pamoja na wajasiriamali 2000 kutoka sehemu mbalimbali za nchi.

  Mkurugenzi Mtendaji Msaidizi wa Taasisi ya kuwawezesha wanawake katika masuala ya biashara (TWCC), Bi. Mwanajuma Hamza anasema mwamko wa wanawake wajasiriamali kushiriki katika Maonesho ya Biashara ya 40 umekua mkubwa kwa vile kumekuwepo na uhamasishaji mkubwa zaidi, lakini pia kupitia maonesho haya ya kila mwaka wanawake wengi wamefanikiwa kupata masoko ya nje ya nchi na hivyo uchumi wao umekua.

  Bi. Mwanajuma anasema Taasisi yake inayoshiriki maonesho haya kila mwaka, imekua ikiwasaidia wanawake kuwapatia taarifa za biashara za nje na mfumo kuhusu biashara za kimataifa ikiwa ni pamoja na kuanzisha majukwaa ya wanawake wafanyabiashara za kuvuka mipaka.

  Aidha, anaendelea kusema kuwa kuanzia mwaka 2012 hadi sasa taasisi hiyo imesaidia wanawake wafanyabiashara zaidi ya 7000, ikiwemo vijana wa kike. Na katika maonesho haya ya 40 wameweza kuwaandalia banda maalumu la wafanyabiashara wanawake pamoja na wale wanawake wanaofanyabiashara za kuvuka mipaka ili kuonesha bidhaa zao pamoja na kupata masoko.

  Doreen Chriss na Suzana Mwalongo ni wasichana wenye umri kati ya miaka 17 na 25 wanaomiliki duka la “ African flawles fashion” kutoka jijini Arusha, ambao wanauza bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa kwa kutumia vitenge na khanga kama vile mikoba, nguo na viatu ni washiriki wa maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa, wenye malengo ya kutanua wigo wa biashara zao na kuuza nje ya nchi.

  Bi. Doreen anasema, “Kiwango hiki cha kushiriki ni cha kawaida ambacho wengi tunaweza kukimudu, pia malengo yetu ya kushiriki maonesho haya ni kuuza bidhaa zetu ndani na nje ya nchi, kwani tunaamini kuwa kupitia maonesho haya yenye kujumuisha watu wengi utoka sehemu mbalimbali duniani yatatusaidia kufikia malengo yetu.”

  Anaendelea kusema kuwa anafurahi kuona watu wengi wameendelea kutembelea kwenye banda lao kwa ajili ya kuangalia na kununua bidhaa zao ambazo zinadumu kwa muda mrefu na wanaamini watapata mafanikio kupitia maonesho haya.

  Kwa upande wa Taasisi za Serikali, umekuwepo ushiriki mzuri wa taasisi hizo pamoja na Wizara katika kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeongeza uwezo wake wa kushiriki katika maonesho ya mwaka huu kwa kuzishirikisha kwa kiasi kikubwa taasisi zilizo chini yake kama SIDO, TFDA, CBE, TBS na BRELA.

  Wizara imefikia azma hiyo kwa kuona kuwa wananchi hasa wenye nia ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo wamekuwa wakihitaji taarifa zaidi kuhusu masula ya biashara na viwanda.

  Afisa Biashara wa Wizara hiyo Bw. Baruti Mwaigaga, anasema maonesho ya mwaka huu yamekuwa ya tofauti na yenye hamasa kubwa kwa vile wananchi wengi wenye viwanda na wenye nia ya kuanzisha viwanda nchini wamekua wakitembelea banda la Wizara kwa ajili ya kupata maelezo jinsi gani ya kupata mikopo ya kuanzisha viwanda pamoja na kuunganishwa na masoko ya bidhaa za kilimo.

  Aidha, Bw. Mwaigaga anasema Wizara imendaa programu za kuendeleza viwanda vidogo vidogo nchini kwa kuanzia mikoa ya Iringa, Pwani, Tanga, Ruvuma na Manyara, na kusisitiza upatikanaji wa masoko ya ndani kwa zao la ufuta, huku akiwataka wananchi kwa ujumla kutembelea kwa wingi banda hilo ili kupata taarifa zinazoweza kuwasaidia katika masuala ya uzalishaji na masoko.

  Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yamefunguliwa rasmi na Rais wa Serikali ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame tarehe 1 Julai 2016 ambapo ametoa wito kwa washiriki wa maonesho hayo kushirikiana ili kubuni mawazo mapya ya biashara ikiwa ni pamoja na kutambua fursa zilizopo katika soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, katika kukuza biashara zao na kusaidia ukuaji wa uchumi wa pamoja katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.

  Baada ya kufungua maonesho hayo, Rais Kagame alikabidhi tuzo kwa Wizara, taasisi za Serikali, makampuni, nchi washiriki pamoja na mashirika yaliyoshinda katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa, kwa kushinda kwa kuonesha bidhaa bora na kueleza huduma nzuri wanazotoa.

  Ni imani yangu kuwa maandalizi ya maonesho ya 41 yataanza mara tu baada ya kumalizika kwa maonesho haya, lengo likiwa kushirikisha makampuni mengi, wajasiriamali wengi na nchi nyingi zaidi.

  Tafsiri yake ni kwamba hali hiyo itasababisha wafanyabiashara wa ndani kutambulika nje ya mipaka ya nchi kwa kiasi kikubwa, kupata ujuzi wa kutengeneza bidhaa mbalimbali na vile vile kupata soko kubwa kwa ajili ya kuuza bidhaa zao.

  Wito wangu kwa waandaaji wa maonesho haya, ni vyema wakatafuta namna ya kuandaa maonesho kama haya katika ngazi za shule za sekondari na vyuo vikuu nchini, ili kuchochea ubunifu pamoja na kutengeneza mazingira ya kujiajiri kwa vijana wanaomaliza shule na vyuo kila mwaka.

  Jambo hili litasaidia watoto na vijana kupunguza kujiingiza katika makundi na tabia zisizofaa, litakuza vipaji na ubunifu kwa watoto na vijana, kuongeza idadi ya viwanda vidogo nchini ikiwa ni pamoja na kuzalisha ajira na kukuza uchumi wa Taifa letu.

  0 0

  Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu, Mhe, Anne Makinda akimweleza jambo Mkurugenzi wa Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Irene Isaka, alipotembelea Ofisi za mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam leo na kufanya mazungumzo ya kikazi na Mkurunzi Mkuu wa mamlaka hiyo. 
  Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mhe. Spika Mstaafu Anne Makinda akiwana katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi Jamii (SSRA), Bi. Irene Isaka (kushoto), mara baada ya mazungumzo ya kikazi leo, katika Ofisi za mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam.

  KAWAIDA Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Spika mstaafu, Mhe, Anne Makinda akimweleza jambo Mkurugenzi wa Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Irene Isaka, alipotembelea Ofisi za mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam leo na kufanya mazungumzo ya kikazi na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo. 

  Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mhe. Spika Mstaafu Anne Makinda akiwana katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi Jamii (SSRA), Bi. Irene Isaka (kushoto), mara baada ya mazungumzo ya kikazi leo, katika Ofisi za mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Mkurugenzi wa Majanga wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Uphoo Swai, akimkabidhi Kitambulisho Clara Benard, mmoja kati ya wanachama wapya waliojiunga na Mfuko wa PPF kupitia huduma ya Wote Scheme, katika Banda la PPF kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Picha na Mafoto Blog
  Meneja Uhusiano Lulu Mengele na Meneja Masoko Elihuruma Ngowi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiwahudumia baadhi ya wanachama waliojiunga na huduma ya Wote Scheme, katika Banda la PPF.
  Mkurugenzi wa Majanga wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Uphoo Swai, akimkabidhi Kitambulisho Mwita Bony, mwanachama mpya aliyejiunga na Mfuko wa PPF.
  Afisa Uendeshaji wa Kanda ya Temeke, Sosteness Lyimo, akiwahudumia baadhi ya wananchi waliotembelea Banda la PPF leo.


  Mkurugenzi wa Majanga wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Uphoo Swai, akimkabidhi Kitambulisho Mtani Manoko, mwanachama mpya aliyejiunga na Mfuko wa PPF.
  Mkurugenzi wa ukaguzi wa ndani wa PPF, Bw. Hosea Kashimba (kushoto) na Mkurugenzi wa Majanga, Uphoo Swai (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na Mfuko wa PPF leo.
  Maafisa wa Mfuko wa PPF, Mwajuma Msina na Pauline Msanga, wakiwahudumia wateja waliotembelea kwenye Banda hilo, leo.
  Maafisa wa Mfuko wa PPF, wakiwahudumia wateja waliofika kujua michango yao.
  Mkurugenzi wa Majanga wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Uphoo Swai, akimkabidhi Kitambulisho Filipa Sylvester, mwanachama mpya aliyejiunga na Mfuko wa PPF.
  Mkurugenzi wa ukaguzi wa ndani wa PPF, Bw. Hosea Kashimba (wa saba kutoka kulia) na Mkurugenzi wa Majanga, Uphoo Swai (wa saba kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa PPF wakiwa na Tuzo yao waliyokabidhiwa kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa.

  0 0  Wanafunzi wa Madrasatul Ibadul- Rahaman Mwanakwerekwe C Unguja wakisoma Maulidi wakati wa hafla ya Iftar ilioandaliwa na Ubalozi wa Iran Nchini Tanzania katika haotli ya tembo shangani Zanzibar.
  Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayuob Mohammed Mahmoud akiwa na Shekh. Salim Mohammed Hassan Al Qadin Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya Kiserekali ya ZAHCO,akimkaribisha katika hafla hiyo ya Iftar ilioandaliwa na Ubalozi wa Iran Tanzania.
  Wageni waalikwa wakipata iftar ilioandaliwa na Ubalozi wa Iran kwa Wananchi wa Unguja katika hoteli ya tembo shangani Zanzibar
  Wageni waalikwa wakipata iftar ilioandaliwa na Ubalozi wa Iran kwa Wananchi wa Unguja katika hoteli ya tembo shangani Zanzibar
  Wageni waalikwa wakipata iftar ilioandaliwa na Ubalozi wa Iran kwa Wananchi wa Unguja katika hoteli ya tembo shangani Zanzibar
  Wakwanza mwenye koti ni Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran Tanzania Shekh. Ali Baghari na Shekh Maulana Shamsul Hassan wakijumuika na Mgeni rasmin Mufti wa Mkuu wa Zanzibar Shekh. Saleh Omar Kabi katika futari ilioandali kwa Wananchi wa Zanzibar katika Hoteli ya Tembo Shangani Zanzibar.
  Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni Ubalozi wa Iran Tanzania Shekh. Ali Baghari akitowa salamu za Wananchi wa Iran wakati wa Iftari hiyo ilioandaliwa na Ubalozo wa Iran Tanzania katika ukumbi wa hoteli ya Tembo Shangani Zanzibar.
  Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni Ubalozi wa Iran Tanzania Shekh. Ali Baghari akitowa salamu za Wananchi wa Iran wakati wa Iftari hiyo ilioandaliwa na Ubalozo wa Iran Tanzania katika ukumbi wa hoteli ya Tembo Shangani Zanzibar.
  Profesha Shariff akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Iftar ilioandaliwa na Ubalozi wa Iran Tanzania katika ukumbi wa hoteli ya Tembo Shangani Zanzibar.
  Wananchi wa Zanzibar wakiwa katika hafla hiyo ia Iftar ilioandaliwa na Ubalozi wa Iran Tanzania katika Hoteli ya Temba Zangani Zanzibar.
  Katibu wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Fadhil Soraga akitowa mawaidha wakati wa hafla hiyo ya Iftar ilioandaliwa na Ubalozi wa Iran.
  Shekh. Salim Mohammed Hassan Al Qadin Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya Kiserekali ya ZAHCO, Mratibu wa hafla hiyo ya Iftar akitowa shukrani kwa Wageni.

  Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Hassan Othman Ngwali akisoma dua baada ya kumalizika hafla hiyo ya Iftar ilioandaliwa na Ubalozi wa Iran, wapili Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh. Saleh Omar Kabi.
  Wageni waalikwa wakiitikia dua.  Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh. Saleh Omar Kabi akiagana na Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni Ubalozi wa Iran waandaaji wa Iftar hiyo.


  Imetayarishwa na OthmanMapara.


  Zanzinews,Blogspot.Com


  Email. othmanmaulid@gmail.com .

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwatangaza Makatibu Tawala wa Wilaya wateule katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Raisi - Utumishi - jijini Dar es salaam leo jioni. Kulia ni Katibu mkuu wa Utumishi Dkt. Laurian Ndumbalo.

  0 0


  Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Mhandisi Profesa. Ninatubu Lema na Balozi wa Norway hapa nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad wakitia saini makubaliano ya msaada wa Dola za Kimarekani milioni 2 kwa ajili ya kuwawezesha wahitimu wa Kike wa masomo ya Uhandisi nchini kujiendeleza kwa kupata uzoefu na kusajiliwa kuwa Wahandisi kamili. Programu inayoanza 2016 – 2021. Wanaoshuhudia utiwaji wa saini ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani (nyuma kushoto).

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani akizungumza wakati wa hafla fupi ya Kutiliana saini baina ya Bodi ya Usajili wa Waandisi (ERB) na Serikali ya Norway kuhusu msaada wa kuwawezesha wahitimu wa Kike wa masomo ya Uhandisi nchini ili waweze kujiendeleza kwa kupata uzoefu na kusajiliwa kuwa Wahandisi kamili leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Balozi wa Norway hapa nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Profesa. Ninatubu Lema.
  Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Profesa. Ninatubu Lema(katikati) akizungumza wakati wa hafla fupi ya Kutiliana saini baina ya Bodi ya Usajili wa Waandisi (ERB) na Serikali ya Norway kuhusu msaada wa kuwawezesha wahitimu wa Kike wa masomo ya Uhandisi nchini ili waweze kujiendeleza kwa kupata uzoefu na kusajiliwa kuwa waandisi kamili leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani na kushoto ni Balozi wa Norway hapa nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad
  Msajili wa Bodi ya Usajili wa Waandisi (ERB) Mhandisi Steven Mlote akifafanua jambo wakati hafla fupi ya Kutiliana saini baina ya Bodi ya Usajili wa Waandisi (ERB) na Serikali ya Norway kuhusu msaada wa kuwawezesha wahitimu wa Kike wa masomo ya Uhandisi nchini ili waweze kujiendeleza kwa kupata uzoefu na kusajiliwa kuwa waandisi kamili leo Jijini Dar es Salaam.
  Msajili wa Bodi ya Usajili wa Waandisi (ERB) Mhandisi Steven Mlote akiwatambulisha baadhi ya wanawake wahitimu wa Vyuo Vikuu katika fani ya Uhandisi (waliosimama kulia) watakao nufaika na msaada wa kuwawezesha wahitimu wa Kike wa masomo ya Uhandisi nchini ili waweze kujiendeleza kwa kupata uzoefu na kuwawezesha kusajiliwa kuwa Wahandisi kamili leo Jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Norway hapa nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad akizungumza wakati wa hafla fupi ya Kutiliana saini baina ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) na Serikali ya Norway kuhusu msaada wa kuwawezesha wahitimu wa Kike wa masomo ya Uhandisi nchini ili waweze kujiendeleza kwa kupata uzoefu na kusajiliwa kuwa Wahandisi kamili leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Profesa. Ninatubu Lema.
   
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia) akifurahia jambo na Balozi wa Norway nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad(katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB),Mhandisi Profesa. Ninatubu Lema. Mara baada ya kutiliana saini baina ya Bodi ya Usajili wa Waandisi (ERB) na Serikali ya Norway kuhusu msaada wa kuwawezesha wahitimu wa Kike wa masomo ya Uhandisi nchini ili waweze kujiendeleza kwa kupata uzoefu na kusajiliwa kuwa Wahandisi kamili leo Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya wanawake wahitimu wa Vyuo Vikuu katika fani ya Uhandisi watakao nufaika na msaada huo leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Esther Kamulali (muhitimu wa UDSM 2014),Balozi wa Norway nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad, Mambazi Godfrey na Tulinyake Lazarus (wahitimu wa chuo cha Mt. Joseph mwaka 2013).

  Picha zote na: MAELEZO

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Ndg. Juma Ameir akizungumza na wakati wa kukabidhi msaada wa Vyakula kwa Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar, ili kusherehekea Sikukuu baada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika katika Nyumba ya Watoto Mazizini Zanzibar.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) akikabidhi msaada wa vyakula kwa Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar kusherehekea vizuri sikuku ya Eid Fitry baada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuungana na Watoto wenzao kusherehekea sikuku hiyo. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Ndg. Juma Ameir akizungumzac wakati wa kukabidhi msaada wa Vyakula kwa Watoto wa Kijiji cha SOS Zanzibar.kushoto baaddhi ya watoto wa kijiji hicho.
  Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akiwakabidhi msaada wa Vyakula Watoto wa Kijiji cha SOS Zanzibar ili kusherehekea vizuri Sikukuu ya Eid Fitry baada ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kijiji hicho huko mombasa Zanzibar.
  Watoto wa Kijiji cha SOS Zanzibar wakimsikiliza Mtoto mwezao akitowa neno la shukrani kwa Uongozi wa PBZ kwa msaada wao huo.
  Mtoto wa Kijiji cha SOS Zanzibar akitowa neno la shukrani kwa Uongozi wa PBZ kwa msaada wao huo.
  Afisa Masoko wa PBZ Ndg Mohammed Nuhu akiwa na Mlezi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Islah Center Bi Zalha Abdalla
  Afisa Masoko wa PBZ Ndg Mohammed Nuhu akitowa maelezo kwa Watoto wa Kituo cha Watoto Yatima cha Islah Center kilichoko mombasa Zanzibar kulia Mlezi Mkuu wa Kituo hicho Bi Zalha Abdalla

  Watoto wa Kituo cha Watoto Yatima cha Islah Center cha Mombasa Zanzibar wakisoma dua kuwaombea Wafanyakazi wa PBZ na Uongozi wao kwa msaada wao huo na kutowa shukrani.


  Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akisalimiana na Watoto wa Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar alipowasili kwa ajili ya kukabidhi misaada ya Vyakula kwa Watoto hao kusherehekea Sikukuu ya Eid Firty.
  Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akisalimiana na Watoto wa Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar alipowasili kwa ajili ya kukabidhi misaada ya Vyakula kwa Watoto hao kusherehekea Sikukuu ya Eid Firty.
  Imetayarishwa na OthmanMapara
  Zanzinews,Blogspot.Com
  Email othmanmaulid@gmail.com

  0 0

  Sheikh Abdulkadir Mohamed akiongoza swala ya Ed- El- Fitr iliyofanyika Viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi.
  Waumini wa dini ya kiislam wakiwa kwenye swala hiyo.


  Mratibu wa swala hiyo ya Ed El-Fitr, Sheikh Othman Abdallah Dishi (kulia), akizungumza katika swala hiyo.
  Watoto wakishiriki swala hiyo.
  Sheikh Zaki akiwasalimia waumini wenzake waliokuwepo kwenye swala hiyo.
  Ibada ikiendelea.
  Swala ikifanyika katika viwanja hivyo vya Mwembe Yanga.
  Sheikh Abdulkadir Mohamed akiongoza swala ya Ed El- Fitr.
  Waumini wa dini ya kiislam wakiswali kuhitimisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan
  Waumini wa dini ya Kiislam wakiswali kwa unyenyekevu mkubwa katika swala hiyo.


  0 0

  Madawati  yaliyotengenezwa kwa  pesa  za  mfuko  wa   jimbo la  Kilolo ambayo mbunge  wake Mhe. Venance Mwamoto ameyakataa kutokana na  kukosa  ubora  ukilinganisha na thamani ya  pesa iliyotumika  
  Mbunge  Mwamoto  katikati  akikimbia  kwenda  kukagua  madawati  katika   kijiji  cha Nyanzwa  leo
  Mbunge wa  Kilolo Mhe. Venance  Mwamoto akikagua madawati  yaliyotengenezwa kwa  pesa za mfuko wa  jimbo.
  Mhe. Venance  Mwamoto  akikagua na kuyakataa katakata   madawati yaliyotengenezwa chini ya  kiwango

  0 0


  Meneja wa Benki ya Azania tawi la Moshi Hajira Mmambe akiwakaribisha wageni kupatra futari iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa wateja wake.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadick na Mkuu mpya wa wilaya ya Moshi,Kipi Warioba pia walikua ni miongoni mwa wageni waalikwa.

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akizungumza wakati wa Futuru iliyoandaliwa na Benki ya Azania tawi la Moshi .\Baadhi ya wageni wakifuatilia hotuba iliyoyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadick (hayupo pichani) wakati wa Futuru iliyoandaliwa na Benki ya Azania tawi la Moshi.
  Meneja wa Azania Benk tawi la Moshi ,Hajira Mmambe akiwakaribisha wageni katika Futuru iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo,hafla fupi iliyofanykika katika uwanja wa gofu wa Moshi maarufu kama Moshii Club.
  Viongozi mbalimbali wa serikali wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadick walijumuika katika hafla hiyo.  Baadhi ya wageni waalikwa wakipata Futari.
  Mkuu mpya wa wilaya ya Moshi ,Kipi Warioba akisalimiana na baadhi ya wageni walioshiriki hafla hiyo.Na Dixon Busagaga wa Michuzi blog.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela usiku wa kuamkia leo alishiriki katika kuzima moto uliounguza bweni wanaloishi watoto yatima katika kituo cha Mgongo mjini Iringa. Moto huo ilioanza kwa hitalafu ya umeme umeteketeza mabweni matatu na kuunguza mali za watoto hao ikiwemo nguo, amadaftari ba magodoro. 

  Kikosi cha zimamoto chini ya Mrakibu Komba kilifanya kazi ya ziada kuzuia moto huo usieneee majengo mengine. Wananchi wa eneo la Mgongo wamefanya kazi kubwa wakisaidiana na jeshi la zima moto.
  Akizungumza na wananchi Mh Kasesela ameahidi kuomba wahisani pia kuangalia uwezekano wa kuwasaidia waathirika wa janga hili la moto. Inakadiriwa watoto zaidi ya 45 wameathirika na moto huu ingawaje hamna majeruhi hata mmoja.

  "Nilipata taarifa nikiwa kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB ikabidi niache nije mara moja nafurahi kuona tumefanikiwa kuzima moto ingawaje umeleta madhara makubwa."Pongezi ziwandee jeshi la Zimamoto pamoja na changamoto walifanikiwa kuzima moto huo" aliesema Mkuu wa Wilaya.

  Mkuu wawilaya huyo alikutana na watoto na kuwapa matumaini serikali ipo pamoja nao. Serikali ya Wilaya ya irnga inawaomba wadau wajitokeze kusaidia watoto hawa mahitaji makubwa ikiwa ni magodoro, blanketi na nguo hasa kipindi hiki cha baridi.
  Mkuu wa wilaya akishirikiana na zimamot kuwapanga wananchi
  DC Kasesela  akishirikiana na zimamoto  kuwapanga wananchi
  DC Kasesela  akishirikiana na zimamoto kuzima moto huo
  DC Kasesela akizungumza na watoto ambao vitu vyao vimeungua .


  0 0

  BANKI ya 'AccessBank' inayoshiriki Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam imeendelea kutambulisha akaunti yake ya 'RAHISI' yenye mvuto mkubwa kwa wajasiliamali mbalimbali. Akizungumza leo kwenye Banda la AccessBank kwenye maonesho ya Sabasaba, Ofisa Masoko wa banki hiyo, Sijaona Simon alisema Rahisi akaunti ni miongoni mwa bidhaa zinazowavutia wajasiliamali wengi kutokana na muundo rahisi wa uendeshaji wa akaunti hiyo kwa wajasiliamali wa kawaida. 
   
  Alisema akaunti hiyo inafunguliwa papo hapo tena bila gharama zozote kwa mteja mjasiliamali anayeitaji na hakuna gharama za uendeshaji huku ikiunganishwa na huduma za kibenki kwa kutumia simu ya mkononi ya mteja (AccessMobile). Alisema faida zingine za akaunti hiyo ni kwamba mteja anaweza kuweka na kununua muda wa maongezi bila makato na hata kuhamisha fedha zake. 
   
  "Akaunti ya Rahisi ni nzuri sana kwa Wajasiliamali wote maana inafaida lukuki waje katika banda letu lililopo ndani ya Sabasaba Hall namba 9 na 10 mkabala na Banda la Bodi ya Kahawa...kuna mambo mengi na mazuri tumewaletea Watanzania hivyo waje kushughudia," alisema Simon.
  Mmoja wa wafanyakazi wa AccessBank (kulia) akitoa maelezo kwa baadhi ya wateja na wananchi mbalimbali wanaotembelea banda la banki hiyo katika Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wafanyakazi wa AccessBank (kulia) wakitoa maelezo kwa baadhi ya wateja na wananchi mbalimbali wanaotembelea banda la banki hiyo katika Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wananchi wanaotembelea banda la AccessBank (kulia) wakihudumiwa ndani ya banda la banki hiyo katika Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Mmoja wa wafanyakazi wa AccessBank (katikati) akitoa maelezo kwa baadhi ya wateja na wananchi mbalimbali wanaotembelea banda la banki hiyo katika Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wananchi wanaotembelea banda la AccessBank (kulia) wakihudumiwa ndani ya banda la banki hiyo katika Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wafanyakazi wa AccessBank (kulia) wakitoa maelezo kwa baadhi ya wateja na wananchi mbalimbali wanaotembelea banda la banki hiyo katika Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wafanyakazi wa AccessBank wanaotoa huduma katika banda la banki hiyo kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja Ofisa Masoko wa AccessBank, Sijaona Simon (kulia) akizungumza na mmoja wa wageni waliotembelea Banda la AccessBank kwenye maonesho ya Sabasaba. Baadhi ya wafanyakazi wa AccessBank wanaotoa huduma katika banda la banki hiyo kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja.[/caption]
   

  0 0

   JUMUIYA ya serikali za mitaa nchini (ALAT) imepongeza kazi wanayoifanya waandishi wa Habari mkoani Shinyanga kwa kuuhabarisha umma kuhusu shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na serikali na kuibua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii. Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambaye pia ni Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gullam Hafeez Mukadam ametoa pongezi hizo jana alipotembelea ofisi za Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC). 
   
  Mukakadam alisema maendeleo yanayoonekana mkoani humo yametokana na mchango wao mkubwa wa kuandika,kuchapisha na kutangaza habari zinazotokea katika jamii. Alisema kazi inayofanywa na waandishi wa habari mkoani humo haiwezi kubezwa na mpenda maendeleo yoyote kwa kuwa matunda yake yanaonekana huku akitolea mfano uharakishwaji wa ujenzi wa barabara za lami katikati ya manispaa ya Shinyanga. 
   
  “Ndugu zangu mimi nawapongeza sana kwa juhudi mlizo nazo za kuuhabarisha umma wa Watanzania juu ya shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali yao lakini pia kwa kutoficha uovu unaofanywa na watu wachache ndani ya serikali na jamii kwa ujumla” ,alisema Mukadam. “Mmeibua mengi kwa faida ya taifa lenu na wananchi wake, ikiwemo ubadhirifu wa mali za umma, wizi wa fedha kwenye halmashauri zetu, matumizi mabaya ya madaraka na ofisi za umma”,aliongeza. 
  Katika hatua nyingine aliupongeza uongozi wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kwa kuimarisha mshikamano miongoni mwa waandishi wa habari na wadau wa habari.
   
   Akiwa katika ofisi hizo za waandishi wa habari Mukadam alitoa msaada wa shilingi 300,000/= kwa ajili ya kusaidia uendeshaji wa ofisi hiyo na kusisitiza kuwa ataendelea kushirikiana na waandishi wa habari huku akiahidi kutoa viti vya kisasa kwa ajili ya ofisi hiyo. Kwa upande wake mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga Kadama Malunde alishukuru kwa msaada uliotolewa na mstahiki meya na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuisaidia SPC kwa ajili ya maendeleo ya waandishi wa habari.
   
  Malunde alisema waandishi wa habari mkoani Shinyanga watatekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya mheshimiwa Rais Magufuli ya Hapa Kazi tu kwa kuhakikisha kuwa wanaandika mazuri na mabaya yote yanayofanyika katika jamii. 
   
  “Nawapongeza waandishi wa habari kwa kazi nzuri wanayofanya tena kwa kujitolea zaidi kwa hali na mali japo kuna vikwazo vingi wanavyokutana navyo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo baadhi ya halmashauri kuwaona kama maadui hasa pale wanapofuatilia vitendo vya ubadhirifu wa mali za umma na uwajibikaji mbovu wa viongozi”,alieleza Malunde. 
  Mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam akikabidhi mchango/msaada wa shilingi 300,000/- kwa mwenyekiti wa SPC bwana Kadama Malunde kwa ajili ya maendeleo ya ofisi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga 
  Kushoto ni mwenyekiti wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini Tanzania,ambaye ni mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam akiwa katika ofisi ya klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club -SPC) zilizopo mjini Shinyanga alipotembelea ofisi hiyo jana.Kulia ni mwenyekiti wa SPC bwana Kadama Malunde-picha kwa hisani ya SPC .
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini Tanzania,ambaye ni mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga zilizopo mjini Shinyanga .
  Mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam akiwa katika ofisi za SPC Mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam akizungumza katika ofisi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga -SPC bwana Kadama Malunde akimkaribisha mwenyekiti wa ALAT na meya wa manispaa ya Shinyanga mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam Bwana Malunde akisizungumza wakati wa ugeni huo Mwenyekiti wa SPC bwana Kadama Malunde akishikana mkono na mwenyekiti wa ALAT mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam Mwenyekiti wa SPC bwana Kadama Malunde akishikana mkono na mwenyekiti wa ALAT mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam Mwenyekiti wa SPC bwana Kadama Malunde akihesabu kiasi cha fedha zilizotolewa na mwenyekiti wa ALAT mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam Mheshimiwa Gulam Hafeez akizungumza katika ofisi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza katika ofisi ya waandishi wa habari ambapo aliwataka kuandika habari bila uoga kuhusu mambo mbalimbali yanayofanywa na halmashauri za wilaya,mkoa na nchi kwa ujumla Mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam akisitiza jambo ambapo pamoja na mambo mengine alitumia fursa hiyo kuwaomba watanzania kumuunga mkono rais John Magufuli katika jitihada mbalimbali anazofanya kuwaletea maendeleo wananchi.  Msikilize hapa Mheshimiwa Gulam Hafeez Akizungumza kuhusu rais Magufuli


  Msikilize mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga bwana Kadama Malunde akizungumzia waandishi wa habari na changamoto wanazopitia  0 0


  Mfano wa nyumba iliyoezekwa kwa kutumia mabati ya Versatile yanayopatikana ALAF Tanzania ambapo imekuwa kivutio cha watu wengi katika maonesho ya Sabasaba2016 .
  Wahudumu wakionesha mabati Versatile yanayopatikana ALAF Tanzania katika maonesho ya Sabasaba 2016 ambapo bei zake zikiwa na punguzo la asilimia tano katika maeneosho hayo
  Wananchi na baadhi ya wafanyakazi wa ALAF wakiwa katika banda lililoezekwa na mabati ya Versatile yanayopatikana ALAF Tanzania ambapo imekuwa kivutio cha watu wengi katika maonesho ya Sabasaba2016.

  0 0

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati mwenye suti ya bluu) akiwa katika jengo la kisasa linalojengwa kwa ajili ya Hospitali ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Jijini Mwanza.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo namna ya miundo ya Hospitali na viwango vyake.

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za watu binafsi zikiwemo zile za kidini na kijamii katika kufanikisha maendeleo ambapo amelipongeza Kanisa la Waadventista wa Sabato la Ilemela Jijini Mwanza kwa hatua yake kujenga Hospitali ya Kisasa ambayo itakuwa msaada katika Wilaya hiyo.

  Dk. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo la ufungaji wa sherehe za miaka 50 ya Jubilee ya kuanzishwa Utume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato katika jiji la Mwanza tukio lililofanyika siku ya Julai 3.2016 kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

  Akitoa hotuba za kufunga sherehe hizo, Dk. Kigwangalla amelipongeza kanisa la Kirumba kuwa na jubilee ya miaka 50 Lakini pia amelipongeza kwa huduma ya malezi ya vijana wa kanisa hilo wakingali wadogo na kwamba kwa kufanya hivo ni kuliandaa kanisa na Taifa kwa ujumla kuwa na viongozi waadilifu.Dk. Kigwangalla ameyataka madhehebu ya dini yawe mstari wa mbele katika kukemea maovu ili Taifa lidumu kuwa na Amani.

  “Uwepo wenu tunaupongeza kwani naamini mumekuwa mstari wa mbele katika kuliombea Amani Taifa hili na pia kuwaombea ulinzi watu mbalimbali pamoja na kutoa misaada, huduma za Afya na mambo mengine mbalimbali. Hii ni faraja sana na Serikali tutaendelea kuwaunga mkono.Aidha, katika hutuba hiyo, Dk. Kigwangalla aliwahakikishia uongozi wa kanisa hilo kuwa Hospitali yao mpya inayojengwa Serikali itakuwa nao bega kwa bega na kuaahidi kutoa ushirikiano katika suala hilo la ujenzi pamoja na uendeshaji wa Hospitali hiyo kwa lengo la kuboresha afya za Wananchi wote.

  Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla alikemea vitendo vilivyoanza kushamili ikiwemo baadhi ya watu kushabikia masuala ya mapenzi ya jinsia moja ambapo ikiwemo suala la ushoga.

  “Serikali haipo tayari kuona vitendo vya ushoga vinafanyika kwa wananchi wake lakini pia kuzitangaza kwa jamii. Wizara yangu itakutana na NGOs, zote za Kijamii na taasisi zilizosajiliwa ambazo pia zingine zipo chini ya Wizara yetu kukaa nazo na kujua ni zipi zinajihusisha na masuala haya iwe kwa kutetea ushoga ama kubariki vitendo hivi, tutawachukulia hatua kali za kisheria na hata kuzifuta kabisa” alimalizia Dk. Kigwangalla.

  Aidha, katika tukio hilo, Dk. Kigwangalla alipata kutembelea ujenzi wa Hospitali hiyo mpya na ya kisasa inayotarajiwa kukamilika kwake hapo baadae na kisha kuwasili kwenye viwanja vya CCM Kirumba ambapo pia alipata kukagua gwaride la vijana wadogo, wa kati na wa kanisa hilo ambao ni pamoja na vijana waliopatiwa mafunzo ya Kiroho, Kimwili na Kikakamavu wakiwemo Wavumbuzi (adventure) Watafuta njia (path finder-Pf), Mabalozi na Kiongozi Mkuu (Master Guide)
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kanisa hilo
  Kituo cha Afya kilichopo kwa sasa kikiendelea na huduma
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakitoka walipotembelea jengo hilo la Hospitali linalojengwa..
  Picha ya jengo hilo la Hospitali pindi litakapokamilikaMuonekano wa mbali katika jengo hilo la kanisa
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akivikwa skafu maalum wakati alipowasili kwenye uwanja wa CCM Kilumba katika sherehe za kufunga Jubilee ya miaka 50 ya kanisa hilo Jijini Mwanza.
  Heshima zikitolewa kwa mgeni rasmi
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakishuhudia matembezi ya sherehe hizo
  Matembezi ya sherehe hiyo yakiendelea
  Sehemu ya umati wa watu katika tukio hilo la Jubilee ya Miaka 50
  Vikundi vya matembezi yakiendelea
  Jukwaa kuu wakishuhudia matembezi hayo
  Vijana wadogo wa Path Finde-(PF) wakipita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima zao. 
  Vijana wadogo wa Path Finde-(PF) wakipita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima zao
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akielekea kukagua gwaride la vijana hao
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua gwaride hilo
  Sehemu ya wananchi wakishuhudia tukio hilo
  Vijana PF wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya mgeni rasmi (Hayupo pichani)
  Jukwaa kuu wakishuhudia matembezi hayo

  Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula akitoa salamu katika tukio hilo
  Vijana wakiwa katika hali ya ukakamavu katika tukio hilo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihutubia katika tukio hilo
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipokea vitabu kama kutoka kwa uongozi wa kanisa hilo vyenye mafunzo mbalimbali 
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishuka katika jukwaa kuu mara baada ya kumalizika kwa tukio hilo.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mzee Mark Boman.  Mzee Boman ni miongoni mwa Wazee waanzilishi wa kanisa hilo ambalo kwa sasa limetimiza Jubilee ya Miaka 50.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla ateta jambo na Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mzee Mark Boman ambaye ni Mzee wa kanisa hilo. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Mwanza).

  0 0

  Familia ya William H. Shelukindo inapenda kuwataarifu kuwa mazishi huko Arusha ya Mpendwa wao Beatrice Matumbo Shelukindo Mbunge wa zamani wa Kilindi sasa yatafanyika kesho siku ya Alhamisi tarehe 7/7/2016 na sio leo Jumatano tarehe 6/7/2016 kama ilivyotangazwa awali.

  Mazishi yatafanyika kesho saa tisa alasiri pale pale eneo la  Oloirien jijini Arusha.

  Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa.
  Jina la Bwana Lihimidiwe.
  AMEN


  0 0  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF Prof. Samwel Chacha Wangwe mara baada ya uzinduzi wa bodi hiyo Julai 5, 2016.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF Prof. Samwel Chacha Wangwe akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) mara baada ya uzinduzi wa Bodi hiyo Julai 05, 2016 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (mb) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Julai, 05, 2016.

  Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Julai 5, 16 Dar es Salaam.


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Hifadhi wa Jamii (NSSF) mara baada ya kuuzindua rasmi katika Ofisi yake Jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama ameizindua rasmi Bodi ya Wadhamini wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF Julai 5, 2016 Dar es Salaam.

  Bodi hiyo imezinduliwa rasmi na kujadili mambo muhimu ikiwa ni kufikia malengo ya mfuko huo kwa kuzingatia masuala ya Utawala bora na ushirikiano ili kuchangia kukua kwa uchumi wa wananchi na kusaidia mahitaji ya wanachama wa mfuko huo.

  Mhe.Mhagama aliahidi kutoa ushirikiano wake kwa Bodi hii mpya ili kusaidia majukumu yote na kuhakikisha mafanikio yaliyopo yanakuwa ni chachu ya kuongeza kasi ya kufanya vizuri zaidi ili kuifikisha mahali pazuri zaidi.

  “Ninawaahidi kuwapa ushirikiano wa hali na mali na kuamini kuwa Prof.Wangwe ameaminiwa na kupewa dhamana ya kutufikisha mahali fulani kwa kuisaidia bodi hii iliyozinduliwa rasmi leo.”Alisisitiza Mhe.Mhagama.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof.Samwel Chacha Wangwe alieleza kuwa, watajikita kwa kusaidia maeneo muhimu yenye changamoto kwa kuhakikisha wanaboresha na kuongeza wanachama wa Mfuko huo.

  “eneo la Utawala bora utakuwa msingi wa kusaidia mfuko uwe imara kwa kuzingatia kuwapa kipaumbele wanachama ili kuendana na kasi ya kukuza uchumi kwa kuzingatia kaulimbiu ya hapa kazi tu” Alisema Prof.Wangwe.

  Mhe.Mhagama alimalizia kwa kuwashukuru wajumbe wote kwa kufika na kushiriki katika uzinduzi huo, “nitoe shukrani zangu za dhati kwa wajumbe wote na kuwaomba tuwe kitu kimoja ili kuhakikisha shirika linatumia rasilimali zake ipasavyo ili kuwa na mapato ya kutosha.” Alisisitiza Mhe. Mhagama.

  0 0  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma hotuba fupi mbele ya Waumini wa Dini ya Kiislam (hawapo pichani) waliojitokeza kwa wingi katika swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

  Mufti wa Tanzania, Alhaj Sheikh Abubakary Zubeir akitoa neno mbele ya Waumini wa Dini ya Kiislam (hawapo pichani) waliojitokeza kwa wingi katika swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.  Waumini wa dini ya Kiislam wakiswali swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijumuika pamoja na Waumini wengine wa Dini ya Kiislam, akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa pili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Ally Hapi,katika swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijumuika pamoja na Waumini wengine wa Dini ya Kiislam, akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa pili kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhaj Mussa Salum pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Ally Hapi,katika swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijumuika pamoja na Waumini wengine wa Dini ya Kiislam, akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa pili kulia), Mufti wa Tanzania, Alhaj Sheikh Abubakary Zubeir (katikati), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhaj Mussa Salum pamoja na Naibu Mufti, Sheikh Hamid Jongo katika swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwaaga waumini wa dini ya Kiislam wakati akiondoka viwanjani hapo mara baada ya kuisha kwa swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.


  Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akipokelewa na baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislam akiwepo na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhaj Mussa Salum alipokuwa akiwasili katika viwanja vya mnazi mmoja mapema leo jijini Dar kuhudhuria swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokelewa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhaj Mussa Salum alipokuwa akiwasili katika viwanja vya mnazi mmoja mapema leo jijini Dar kuhudhuria swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini ya Kiislam mara baada ya kuwasili katika viwanja vya mnazi mmoja mapema leo jijini Dar kwa ajili ya kuhudhuria swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. PICHA NA MICHUZI JR

  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Longido Bw. Daniel Chongolo (wa tatu kulia) akikabidhi zawadi za Idd kwa Masheikh wa misikiti ya mji wa Namanga na Longido mjini wilayani Longido leo,mkoani Arusha. Mh Chongo amekabidhi  zawadi hizo kwa misikiti 6 iliyopo wilayani Longido mapema Leo.
   Mkuu wa wilaya ya Longido mkoani Arusha Bw. Daniel Chongolo akikabidhi zawadi za sikukuu ya Idd kwa Masheikh wa Misikiti ya Namanga na Longido mjini leo. Mkuu huyo wa wilaya pia ametumia nafasi hiyo kujitambulisha kwao.


older | 1 | .... | 902 | 903 | (Page 904) | 905 | 906 | .... | 1897 | newer