Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 898 | 899 | (Page 900) | 901 | 902 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir na Mgeni Rasmin Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg Ali Khamis, wakijumuika na Wananchi na Wafanyakazi wa PBZ katika futari ilioandaliwa kuadhimisha Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa PBZ mwaka 1966 2016.iliofanyika katika viwanja vya hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar
  Baadhi ya Wafanyakazi wastaaf wa PBZ wakijumuika katika futari Maalum ya kusherehekea Miaka 50 ya PBZ wakipata futari katika viwanja vya hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
  Wafanyakazi wa PBZ wakipata futari katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
  Baadhi ya Wafanyakazi wastaaf wa PBZ wakijumuika katika futari Maalum ya kusherehekea Miaka 50 ya PBZ wakipata futari katika viwanja vya hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
  Wafanyakazi wa PBZ wakipata futari katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
  Wafanyakazi wa PBZ wakipata futari katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
  Iftar Maalim ilioandaliwa na PBZ kwa Wateja wao na Wafanyakazi wa PBZ kusherehekea miaka 50 tangu kuunda kwa Benki hiyo mwaka 1966 -2016  Meneja wa PBZ Tawi la Kariakoo Dar es Salaam Ndg Seif akijumuika na Wafanyakazi wezake katika Iftar hiyo Maalum ya kusherehekea miaka 50 ya PBZ Zanzibar.  Baadhi ya Wafanyakazi wastaaf wa PBZ wakijumuika katika futari Maalum ya kusherehekea Miaka 50 ya PBZ wakipata futari katika viwanja vya hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.  Baadhi ya Wafanyakazi wastaaf wa PBZ wakijumuika katika futari Maalum ya kusherehekea Miaka 50 ya PBZ wakipata futari katika viwanja vya hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
  Maofisa wa PBZ na Wananchi wakipata Iftar ilioandaliwa na PBZ katika viwanja vya hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
  Baadhi ya Wafanyakazi wastaaf wa PBZ wakijumuika katika futari Maalum ya kusherehekea Miaka 50 ya PBZ wakipata futari katika viwanja vya hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.


  Keki Maalum ya miaka 50 ya kuzaliwa kwa Benki ya Watu wa Zanzibar ikiwa ni maalum kwa sherehe hiyo.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar Ali Khamis na Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Ameir wakikata keki wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya PBZ Zanzibar.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Juma Ameir akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Iftar maalum ya kusherehekea miaka 50 ya PBZ na kuzungumzia changamono na mafanikio ya PBZ katika kipindi cha miaka 50 iliopita.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg Ali Khamis akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kuadhimisha miaka 50 ya PBZ katika hafla ya Iftar ilioandaliwa kwa ajili ya kuadhimisha sherehe hiyo iliofanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
  Wafanyakazi wa PBZ wakimsikiliza mgeni rasmin wakati akitowa nasaha zake kwa Uongozi na Wafanyakazi wa PBZ katika Iftar hiyo.

  Mgeni Rasmin wa hafla hiyo ya kuadhimisha miaka 50 ya PBZ Zanzibar akimkabidhi nishani ya Uongozi Mfanyakazi Mstaafu wa PBZ Ndg Chwaya.ni mmoja wa waazilishi wa Benki ya Watu wa Zanzibar
  Mgeni Rasmin wa hafla hiyo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg. Ali Khamis akimkabidhi nishani mfanyakazi Mstaafu wa PBZ.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg Ali Khamis akimkabidhi zawadi ya Mfanyakazi wa PBZ Bi Saada Bakari akipokea kwa niaba ya Mstaafu Bi Maryam Abdurahaman

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar Ali Khamis akimkabidhi mfanyakazi wa PBZ Ndg Mohammed Mussa akipokea zawadi hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Mstaaf wa PBZ Ndg Juma Amour.
  Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya PBZ Ndg Yakout akipokea zawadi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi Mstaaf wa PBZ Ndg Abdrahaman MwinyiMbegu.
  Naibu Katibub Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar Ndi Ali Khamis akimkabidha Mstaaf wa PBZ Mhe Ussi Yahya wakati wa hafla hiyo.  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg Ali Khamis akimkabidhi zawadi Mkuregenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir wakati wa hafla hiyo ya kuadhimisha miaka 50 ya PBZ Zanzibar.  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg Ali Khamis akiwa katika picha ya pamoja na Wastaaf na Wajumbe wa Bodi ya PBZ. baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya kuadhimisha miaka 50 ya PBZ Zanzibar iliofanyika katika viwanja vya hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
  Imetayarishwa na OthmanMapara.Blog.


  Zanzinews.com


  E-mail othmanmaulid@gmail.com.

  0 0


  Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale,Mhifadhi ,Romanus Mkonda akizungumza na kina mama wanaofanya kazi ya kuponda mawe mwambao mwa ziwa Tanganyika kwa lengo la kupata kokoto ambazo TANAPA imekua ikinunua kwao kwa ajili ya ujenzi wa mioundo mbinu.

  Kina mama katika kijiji cha Buhingu wilayni Uvinza mkoani Katavi wakipasua Mawe kwa ajili ya kuponda ili kupata Kokoto ambazo zimekua zikinunuliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano na Hifadhi ya Taifa ya Mahale inayopakana na kijiji hicho.
  Katibu wa waponda Kokoto katika kijiji cha Buhingu Neema Jackson akisoma risala mbele ya viongozi wa Hifadhi Taifa ya Milima ya Mahale na TANAPA walioongozana na wanahabri kutembelea kina mama hao.
  Kazi ya upasuaji wa Mawe katika kijiji vcha Buhingu kimekuwa pia kikifanywa na kina mama ambao umri wao umeenda ili kusaidia familia zao.

  Sehemu ya kokoto zilizokwisha patikana ambazo hata hivyo kina mama hao wamelalamikia bei ndogo wanayolipa Makandarasi wanao pata zabuni ya ujenzi wa miundo mbinu ambapo wamekua wakilipwa sh 500 kwa ndoo tofauti na bei ya Sh 1000 kwa ndoo inayo lipwa na TANAPA pindi inapohitaji malighafi hiyo.

  Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza na kina mama hao mara baada ya kusilikiliza changamoto za kina mama hao.
  Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Pascal Shelutete akimueleza jambo na Katibu wa waponda kokoto Neema Jackson akitizama namna ya kushauri makandarasi wanaopewa dhabuni ya ujenzi na TANAPA kuhakikisha wanatumia malighafi za kina mama hao.
  Menea Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pscal Shelutete akikabidhi kiasi cha Sh 100000 kwa katibu wa kina mama hao mara baada ya kusikiliza changamoto zinazowakabili.
  Baadhi ya Watoto wanaoshiriki kusaidia wazazi wao katika shughuli ya upondaji kokoto katika kijiji hicho.
  Kina mama wanao ponda kokoto wakifurahia na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascla Sheluetete mara baada ya kutoa fedha kwa kina mama hao.Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kigoma.

  0 0

  Muonekano wa Banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), katika Maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa jijini Dar es Salaam.
  Ofisa Masuala ya Bima wa NSSF, Peter Isack akitoa ufafanuzi kwa kuhusu majukumu ya kitengo chake kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kushoto), wakati mkurugenzi huyo alipotembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Sabasaba.
  Ofisa Uwekezaji wa NSSF, Moringe Nyerere akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kushto), juu ya viwanja vinavyouzwa na NSSF vilivyopo eneo la Kiluvya.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kulia), akiangalia michoro ya nyumba ambayo ni sehemu ya miradi ya shirika hilo. Wa pili kulia ni Ofisa Uwekezaji wa NSSF, Moringe Nyerere.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (wa pili kulia), akiangalia mradi wa Mtoni Kijichi.
  Ofisa Mauzo wa NSSF, Abbas Ramadhan akitoa maelezo kuhusu mradi wa nyumba wa Kijichi.
  Ofisa Uhusiano Mwandamizi, Salim Kimaro (kushoto) na Ofisa Uhusiano wa NSSF, Aman Marcel wakimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara kifaa maalum kinachotumiwa na wanachama kutoa maoni yao kuhusu huduma zinazotolewa na shirika hilo.
  Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda la NSSF.
  Ofisa wa Masuala ya Bima wa NSSF, Peter Isaack akitoa maelezo mmoja wa watu waliofika katika banda la NSSF katika viwanja vya Sabasaba.
  Mkurugenzi Mkuu wa NSSF akizungumza na maofisa waandamizi wa NSSF.
  Ofisa Uhusiano wa NSSF, Rehema Urembo akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja wa mfuko huo.

  0 0

  Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha (SSP) Emmanuel Tille akiongea na viongozi wa kata ya Moivaro tarafa ya Suye pamoja na askari wa vikundi vya ulinzi shirikishi wakati wa uzinduzi wa vikundi vinne vya kata hiyo.

  Diwani wa kata ya Moivaro Rick Moiro akiongea na askari wa vikundi vya ulinzi shirikishi toka kwenye baadhi ya mitaa ya kata yake mara baada ya uzinduzi wa vikundi hivyo. Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha (SSP) Emmanuel Tille akiwakagua askari wa vikundi vya ulinzi shirikishi kutoka mitaa ya Ngurumausi, Oldonyommasi, Moivaro Kati na Shangarao. Baadhi ya viongozi wa kata ya Moivaro pamoja na askari wa vikundi vipya vya ulinzi shirikishi wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha (SSP) Emmanuel Tille hayupo pichani. Mmoja wa wahitimu wa askari wa ulinzi shirikishi katika kata ya Moivaro akikabidhiwa kitambulisho cha kazi kutoka kwa Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha (SSP) Emmanuel Tille.

  —————————

  Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

  Ikiwa jeshi la Polisi linaendeleza harakati za kupambana na uhalifu ili kupunguza matukio ya namna hiyo, wananchi wa kata ya Moivaro tarafa ya Suye halmashauri ya jiji la Arusha hawapo mbali na jitihada hizo hivyo kuamua kujitokeza kwa moyo mmoja kupinga uhalifu kwa kuanzisha vikundi vinne vya ulinzi shirikishi kutoka mitaa ya Ngurumausi, Oldonyommasi, Moivaro Kati na Shangarao.

  Akizindua vikundi hivyo ambavyo vimewezeshwa na wadau walioongozwa na Jeff Mligha ambao walijitolea vifaa mbalimbali vya ulinzi zikiwemo tochi, Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Mratibu Mwandamizi wa Polisi Emmanuel Tille kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha alisema kwamba matarajio ya wananchi katika kata hiyo ya Moivaro ni makubwa na ana imani watakuwa wanalala na kuamka salama hivyo kuwataka walinzi hao wawe na nidhamu kwenye kazi yao.

  “Kazi ya ulinzi ina miiko yake; kitu cha kwanza ni nidhamu ya hali ya juu. Mimi mwenyewe mpaka nafikia hatua hii ni kwa sababu ya nidhamu na nawataka ninyi muige mfano wangu, ninachosema hapa ni pamoja na kuwahi kazini, kutunza siri pasipo kuwazunguka wenzako pamoja na kufuata maelekezo ya wakubwa wa vikundi vyenu” Alisisitiza Tille.

  Alisema japokuwa askari hao wapatao 42 wamepewa mafunzo lakini kupitia Wakaguzi wa Polisi wa Tarafa na askari kata wataendelea kuwapa mafunzo mara kwa mara ili waweze kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria, huku akiwaonya wasijichukulie sheria mkononi.

  Aliwataka wananchi wanapopata taarifa watoe kwa viongozi wa Polisi mara moja ili ziweze kufanyiwa kazi kwa haraka na hatimaye kufikia malengo ya kupunguza uhalifu ndani ya jiji la Arusha, huku akiwataka watendaji wa kata na Wakaguzi wa tarafa wahakikishe askari wa kata wanakuwa katika maeneo yao kila siku hali ambayo itawasaidia kubaini maeneo tete.

  Akiongea katika uzinduzi huo Diwani wa kata hiyo Rick Moiro alivitaka vikundi hivyo kufuata taratibu za kazi na kupambana na uhalifu hasa vijana wanaojihusisha na madawa ya kulevya aina ya bangi huku akiomba Jeshi la Polisi litoe ushirikiano wa karibu na vikundi hivyo pindi tu wanapoomba msaada.

  Naye Afisa Mtendaji wa kata hiyo Bi. Editha Kisangia alisema kwamba mbali na hali ya uhalifu kuwa ya kawaida katika eneo hilo lakini hatarajii kutokea kwa changamoto kutoka kwa baadhi ya wananchi kushindwa kuchangia vikundi hivyo kwani faida wataiona baada ya kuanza kufanya kazi.

  Wakaguzi wa Polisi wanaoongoza tarafa tatu za halmashauri ya jiji la Arusha toka mwaka 2013 ni pamoja na Frimina Massao tarafa ya Suye, Winibrita Moshi tarafa Elerai na Shabani Shabani tarafa ya Themi.

  0 0

  Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mhe.Ummy Mwalimu pamoja na Wajumbe hao na viongozi wa Wizara(Picha na Wizara ya Afya).
  Ujumbe wa wanaharakati wa maendeleo ya jinsia na watoto waliokutana na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa TGNP Liliani Liundi,katikati ni Naemy Sillayo toka LHRC na Janeth Mawinza kutoka WAJIKI ———————————————————-

  Na. Catherine Sungura. WAMJW

  Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa dhamira ya kufikiwa kwa uwakilishi wa 50 kwa 50 katika ngazi mbalimbali za maamuzi inchini inafikiwa.

  Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na ujumbe wa wanaharakati wa maendeleo ya jinsia na watoto waliofika ofisini kwake na kufanya nao mazungumzo

  Mhe.Ummy Mwalimu alisema jitihada zinafanyika kuhakikisha kuwa teuzi mbalimbali zinahusisha jinsia zote, ikiwa ni pamoja na wajumbe wa bodi mbalimbali za uongozi wa Idara na Taasisi za Serikali.

  “Nitoe wito wangu kwa Mashirika mbalimbali ya Serikali na Yasiyo ya Serikali kuzingatia usawa wa jinsia wakati wa teuzi mbalimbali za uongozi wa juu pamoja na wajumbe wa Bodi”.

  Aidha, amewathibitishia wajumbe hao kuwa serikali ina dhamira ya dhati ya kuifanyia marekebisho ya Sheria ya Ndoa, “jitihada za maksudi zinafanyika kuhakikisha marekebisho ya kifungu cha 13 na 17 cha sheria ya ndoa, kinachoruhusu mtoto chini ya miaka 18 kuolewa vinafanyiwa marekebisho kwa kuwasilisha muswada Bungeni kabla ya mwaka kuisha.

  Hata hivyo alisema jitihada hizo za kufanya mabadiliko ya sheria zitahusisha pia sheria ya Mirathi inayomnyima mtoto wa kike na wanawake kurithi mali.

  Akizungumza kwa niaba ya ujumbe huo wa wanaharakati, mkurugenzi wa Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) bi. Liliani Liundi alisema ipo haja ya Serikali kuongeza nguvu zaidi katika kuhakikisha sheria ya Ndoa kifungu cha 13 na 17 inafanyiwa marekebisho, kwakuwa inarudisha nyuma jitihada za kuleta usawa wa jinsia nchini.

  Aidha, alieleza kuwa mabadiliko ya Sheria ya Elimu katika kifungu kinachokataza kuoa / kuoza mtoto wa shule ya Msingi na Sekondari ni jitihada inayohitaji kuungwa mkono.

  “Ipo haja ya kuongeza nguvu zaidi katika kuwalinda watoto walio nje ya shule, kwakuwa mabadiliko haya ya sheria ya Elimu yaliyopitishwa na Bunge la 11 yawewaacha nje pasipo ulinzi wa sheria watoto wengi walio nje ya shule”Alisema.

  Ujumbe wa wanaharakati uliwasilisha maoni yao na changamoto mbalimbali zinazo ikabili nchi katika kuleta maendeleo ya mtoto na usawa wa jinsia nchini, ikiwa ni pamoja na suala la Marekebisho ya Sheria ya Ndoa na Nafasi ya uwakilishi wa mwanamke katika vyombo mbalimbali vya maamuzi. Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Bibi Lilian Liundi na Wanaharakati wa Shirika la LHRC, WAJIKI, TANZANIA Widows Association na shirika la Wanawake katika Jitihada za Kimaendeleo (WAGIC)

  0 0


  Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Zena Kongoi (katikati) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Zena Kongoi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki katika banda la STAMICO kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Joram Kengete (kushoto) akitoa maelezo jinsi umeme unavyozalishwa kwa njia ya maji katika banda la Wizara ya Nishati na Madini, kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
  Baadhi ya washiriki kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika picha ya pamoja katika banda la Wizara kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Mtaalam kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini, Ester Njiwa (kushoto) akielezea sera ya madini kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Mmoja wa watembeleaji katika banda la Wizara ya Nishati na Madini akisaini kitabu cha wageni katika banda la Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) mara baada ya kupata huduma. Kushoto ni Afisa Mawasiliano wa TANESCO, Yasin Silayo
  Afisa Usalama na Mazingira kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Paul Thobias (kulia) akielezea shughuli zinazofanywa na shirika hilo, kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Mtaalam kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini Phillip Mathayo (kushoto) akionesha takwimu za utoaji wa ruzuku kwa wachimbaji wadogo awamu ya pili, kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Petro Marwa (kushoto) akipokea maoni kutoka kwa mmoja wa watembeleaji wa banda la Wizara, kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Nishati na Madini, Asteria Muhozya (kushoto) akibadilishana mawazo na mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Mhandisi Joram Kengete (katikati), kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Theophil Leonard.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wakati wa dhifa ya Kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Rwanda Paul Kagame akizungumza na wageni mbalimbali katika dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu mstaafu Salim Ahmed Salim Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mawaziri wakuu wastaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba na Salim Ahmed Salim Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame, Kulia ni mke wa Rais Mama Janeth Magufuli.
   Kijana Omar Abdalah Ramadhan akimsalimia kwa furaha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika viwanja vya maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Kijana Omar Abdalah Ramadhan akimsalimia kwa furaha mama Janeth Magufuli mara baada ya Rais wa Rwanda Paul Kagame kuondoka kwenye viwanja vya maonesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU  0 0


  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akikabidhi tuzo mbili za ushindi ilizoshinda Wizara yake katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwa viongozi wa Kamati ya Maonesho ya Wizara hiyo jana tarehe 01 Julai, 2016 katika viwanja vya Sabasaba. Tuzo hizo ni Mshindi wa Kwanza katika kundi la Wizara na Taasisi za Serikali na Mshindi wa pili katika kundi la Mshindi wa Jumla wa Maonesho hayo. Tuzo hizo zilikabidhiwa na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame aliyekuwa Mgeni Rasmi akiongozana na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa tano kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waoneshaji wa Wizara yake muda mfupi baada ya kupokea tuzo mbili za ushindi katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam jana tarehe 01 Julai, 2016 katika viwanja vya Sabasaba. Tuzo hizo ni Mshindi wa kwanza katika Kundi la Wizara na Taasisi za Serikali na Mshindi wa Pili katika Kundi la Mshindi wa Jumla.
  Baadhi ya Waoneshaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakifurahia ushindi wa tuzo hizo. Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii ni moja ya mabanda yanayovutia zaidi katika Maonesho ya Sabasaba ya mwaka huu 2016, kwa kuwa na mchanganyiko wa mambo mbali mbali yanayoelimisha kuhusu uhifadhi wa Maliasili, Malikale na Utalii. Katika banda hilo zipo pia fursa za kuwaona wanyama hai kama vile Simba, Nyati, Chui, Mamba, Ndege mbalimbali n.k. Kwa upande wa Utalii wa Ndani zipo fursa za kutembelea hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwa gharama nafuu ya Tsh. 10,000 kwa watoto na Tsh. 20,000 kwa watu Wazima ikiwa ni nauli ya kwenda na kurudi, Aidha kwa wale watakaopenda kulala itawagharimu Tsh. 50,000.
  Baadhi ya Waoneshaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakifurahia tuzo hizo katika banda la Wizara hiyo.
  Taswira ya tuzo hizo.(Picha na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii)

  0 0


  Rais wa Rwanda Paul Kagame, (wapili kulia) akiwa na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli, (wakwanza kulia), akimkabidhi tuzo ya msindi wa kwanza kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na makampuni ya Bima, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 1, 2016. Wapili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.

  Na. Immaculate Makilika, MAELEZO

  RAIS wa Serikali ya Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame amewakabidhi tuzo kwa Wizara, taasisi za Serikali, kampuni, nchi washiriki pamoja na mashirika yaliyoshinda katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa.

  Rais Paul Kagame alikabidhi tuzo hizo jana, wakati alipokuwa akifungua maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya Mwl Nyerere maarufu kama Sabasaba, vilivyopo katika barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.

  Wizara na taasisi za Serikali, kampuni pamoja na mashirika mbalimbali yalishiriki maonesho hayo kwa kushindana katika kuonesha bidhaa bora na kueleza huduma nzuri wanazotoa, ambapo baadae Rais Paul Kagame aliwakabidhi washindi hao tuzo mbalimbali.

  Baadhi ya washindi hao walioganywa katika makundi mbalimbali ni pamoja na, kundi la bidhaa za kilimo nafasi ya mshindi wa tatu ilishikwa na kampuni ya farm equip Tanzania limited, nafasi ya mshindi wa pili ilishikwa na kampuni Asas dairies na nafasi ya mshindi wa kwanza ilishikwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT).

  Katika kundi la usindikaji wa vyakula na huduma za vinywaji, nafasi ya mshindi wa tatu ilishikwa na kampuni ya Bakhresa Group, ikifuatiwa na kampuni ya P&P, na nafasi ya mshindi wa kwanza ilishikwa na kampuni ya Afri tea and coffe blenders limited.

  Kwa upande wa taasisi za kifedha, nafasi ya mshindi wa tatu ilishikwa na benki ya TIB, ikifuatiwa na Benki ya CRDB huku Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ikishika nafasi ya kuwa mshindi wa kwanza. Vilevile katika kundi la Mifuko ya hifadhi ya jamii nafasi ya mshindi wa tatu ilishikwa na mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF, nafasi ya mshindi wa pili ilishikwa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF na nafasi ya mshindi wa kwanza ikiwa ni Mfuko wa Pensheni wa PPF.

  Kwa upande wa nchi za kigeni zilizoshiriki maonesho hayo ya 40 tuzo zilienda kwa nchi za Rwanda iliyoshika nafasi ya mshindi wa tatu, Ujerumani ikishika nafasi ya mshindi wa pili huku nafasi ya mshindi wa kwanza ikiwa ni nchi ya Afrika Kusini. Aidha, washindi wa jumla walioshiriki katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Sabasaba ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kilichoshika nafasi ya mshindi wa tatu , ikifuatia Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja Chuo cha Cha Ufundi Stadi (VETA) kilichoshika nafasi ya mshindi wa kwanza.

  Baada ya kuwakabidhi tuzo hizo na kufungua rasmi maonesho hayo ya 40 ya biashara ya kimataifa Rais Kagame alitoa wito kwa washiriki wa maonesho hayo ya 40, kushirikiana ili kubuni mawazo mapya ya biashara ikiwa ni pamoja na kutambua fursa zilizopo katika soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, katika kukuza biashara zao na kusaidia ukuzaji wa uchumi wa pamoja katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.

  0 0

  Baadhi ya wageni waliotembelea katika banda la VETA wakisaini kitabu cha ushiriki katika maonesho ya 40 ya kimataifa ya mwaka huu katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Wananchi wakiwaangalia Bustani inayohifadhi mazingira hasa kwa wakazi wasio na maeneo makubwa kwaajili ya Kulima Bustani (Vertical Garden) ambayo huoneshwa na banda la VETA jijini Dar es Salaam leo. 
   Baadhi ya wananchi wakipata maelekezo katika banda la VETA kitengo cha vitu vya Samani katika maonesho ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
   Baadhi ya wananchi wakipata maelekezo walipotembelea banda la VETA kitengo cha Umeme katika maonesho ya 40 ya kibiashara ya kimataifa katika viwanja va sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
   Meneja wa Mawasiliano  VETA, Peter Sitta akijadiliana jambo  mtaalaam mamlaka ya VETA leo  katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimatiafa viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Mzazi kulia na mtoto aliyekaa kwenye kiti wakipata maelekezo walipotembelea banda la VETA kitengo cha Vitu vya Samani jijini Dar es Salaam leo.
   Wananchi wakipata maelekezo kutoka kwa mkufunzi wa Viatu vya Ngozi ambavyo hutengenezwa katika chuo cha ufundi stadi cha VETA katika maonesho ya 40 ya kibiashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
   
  Baadhi ya Wananchi wakipata  maelezo juu ya ufundi umeme walipotembelea banda la VETA katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimatiafa viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
   
  Wananchi wakipata maelekezo juu mitaala ya VETA walipotembelea  banda hilo  katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimatiafa viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

  0 0  0 0

  KIKOSI cha timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17‘Serengeti Boys’

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  KIKOSI cha timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17‘Serengeti Boys’ kimefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa goli 6-0 dhidi ya timu ya Shelisheli  na  Ushindi huo unaifanya Serengeti kuwa na jumla ya goli 9-0 baada ya kushinda mchezo wa awali uliopigwa katika uwanja wa Taifa na baada ya kushinda mchezo huo wa kuwania kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika sasa Serengeti itavaana na timu ya Taifa ya Afrika Kusini mwezi ujao.

  Mchezo ulianza kwa timu zote kushambuliana lakini Serengeti ilionekana kuutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa huku Timu hiyo ambayo ni wawakilishi pekee wa nchi kwenye mashindano ya kimataifa ilipata goli lake la kwanza dakika ya tisa kupitia kwa Ibrahim Abdallah baada ya golikipa kutema shuti lililopigwa na Asadi Ally.

  Serengeti inapata goli la pili lililofungwa na Mohemmed Abdallah dakika ya 43 pale alipoachia shuti kali lililomshinda kipa wa wapinzani wao na kuzama wavuni. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika serengeti walikuwa kifua mbele kwa goli 2 huku wakionekana kuutawala vilivyo mchezo huo wa ugenini.

  Kipindi cha pili kinaanza kwa Serengeti kuingia kwa kasi ambayo inazaa matunda dakika ya 50 pale Asad Juma anapoandika goli la 3 baada ya kupiga faulo inayotumbukia moja kwa moja wavuni.Wageni hao katika uwanja wa Stade Linite  wanapata goli la 4 kwa penati dakika ya 61 inayopigwa na Issa Makamba na Asad Juma anaandika bao la tano dakika ya 70 huku Yohana Mkomola akiandika goli la sita dakika ya 90

  Kikosi cha Serengeti Boys
  Ramadhani Kambwili
  Israel Mwenda
  Nickson Kibabage
  Enrick Nkosi
  Ally Msengi
  Ally Ng'anzi
  Mohameed Abdallah
  Shaban Ada
  Ibrahim Ally
  Rashid Chambo
  Asad Juma

  Kikosi cha Shelisheli.
  Gino Pusureuse
  Juninno Mathiot
  Stan Estner
  Brandon Molle
  Mathew Basset
  Churtill Rose
  Emmanuel Lesperance
  Julius Joseph
  Ryan Henriette
  Aaron Havolock
  Brandon Fanchette

  0 0

  Na Is-haka Omar, Zanzibar.

  CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewataka wananchi wanaoishi katika maeneo yanayomilikiwa na chama hicho kuhakikisha wanafunga mikataba rasmi ili kuepuka usumbufu wakati maeneo hayo yatakapohitajika kwa ajili ya shughuli za kichama.

  Kimesema kuna baadhi ya wananchi waliopewa maeneo ya kuishi kwa muda kwa nia ya kuwasaidia na badala yake wameyageuza kuwa makaazi yao ya kudumu jambo ambalo sio sahihi.Akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ndg. Vuai Ali Vuai kwa nyakati tofauti katika mwendelezo wa ziara ya kuhakiki mali na maeneo mbali mbali yanayomilikiwa na CCM huko Mbweni Mkoa wa Magharibi Kichama.

  Alisema chama kinaendelea na zoezi la kuhakiki mali zake kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu wanaotengeneza hati na mikataba bandia ya kujimilikisha mali za chama hicho kinyume na utaratibu.

  Ndg. Vuai alifafanua kwamba katika hatua za kupunguza kero hizo chama kimeamua watu wote ambao wamepewa kibinadamu sehemu za kuishi ama kufanya biashara kwa muda katika maeneo yanayomilikiwa na CCM wafunge mikataba rasmi ili chama kiweze kunufaika na rasilimali zake.

  “ Watu waliopewa kwa dharura sehemu za kuishi na kufanya biashara kama hatujawapa mikataba rasmi inayotambulikana kisheria, ambayo ni kielelezo cha kumtambulisha nani mmiliki halali wa maeneo hayo baadae inaweza kuwa fursa ya kufanya utapele na kusababisha usumbufu na lawama kwa chama. 

  Tujaalie kwamba mtu anaishi katika kiwanja cha Chama bila mkataba wa kisheria na imetokea ameondoka au amehama watoto, ndugu na jamaa zake hawatokubali mali hizo zirudishwe kwa CCM na kitakachotokea hapo ni ugomvi na kupelekana mahakamani hali ambayo chama hakipo tayari kuona inatokea ”,. Alifafanua Vuai na kuongeza kuwa CCM haitokuwa tayari kuona mali zake zinatumiwa na watu wachache bila ya makubaliano ya kimaandishi ama mikataba ya kisheria.

  Alisisitiza kuwa Chama hicho kitaendelea kuhakiki, kukagua na kuratibu mali zake zote zilizopo nchini kwa lengo la kuziimarisha na endapo patajitokeza vitendo vya udanganyifu na uvamizi vitatafutiwaufumbuzi wa kudumu na taasisi hiyo.

  Alisema bila ya kuwepo na utaratibu maalum na endelevu wa kuhakiki mali za chama hicho baadhi ya watu watakuwa wanajimilikisha na kujinufaisha wenyewe huku chama kikibaki kuwa maskini.Alifahamisha kwamba CCM itaendelea kutekeleza kwa vitendo sera zake zinazoelekeza na kukitaka Chama kutumia rasilimali na vyanzo vyake vya mapato kukuza uchumi wa taasisi hiyo.

  Alitoa wito kwa Wana CCM na wananchi kwa ujumla kuunga mkono juhudi za chama hicho za kuhakikisha mali zake zinabaki salama bila ya kuhujumiwa na watu wachache wanaojali maslahi binafsi badala ya Chama na Serikali kwa ujumla.Wakati huo huo Naibu Katibu wa CCM Zanzibar, alitembelea Jumba la kihistoria la Afro-Shiraz Party (ASP) lililopo katika eneo la Kijangwani na kueleza kwamba dhamira ya CCM ni kuhakikisha eneo hilo linaenziwa kwa kujengwa nyumba ya kisasa zinazoendana na hadhi ya Chama.

  Alifafanua kwamba Jengo hilo lilianzishwa na Chama cha Shiraz association ambacho baadae mwaka 1957 iliungana na Chama cha African association na kuunda Chama kimoja kilichoitwa Afro Shiraz Party(ASP) , na hatimaye kuungana na TANU na kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977.

  “ Jengo hili lina historia kubwa ya Chama kwani lilikuwa likitumika na viongozi mbali mbali wa chama kabla na baada ya harakati za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964”, alisema Vuai.Aidha amewataka viongozi wa Mkoa Mjini kuhakikisha wanaadhika historia ya eneo hilo na kuiweka katika kumbukumbu za kudumu za chama ili ziweze kuwanufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.

  Naibu Katibu Mkuu huyo, aliwapongeza wafuasi wa chama hicho na wananchi kwa ujumla kwa kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa marudio ulioiweka madarakani CCM, na kuwasihi kufanya kazi za ujenzi wa Taifa kwa bidii huku wakisubiri Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

  Nao Viongozi wa Mikoa miwili kichama ikiwemo Mkoa wa Magharibi na Mkoa Mjini kwa nyakati tofauti wameipongeza CCM kwa uamuzi wake wa kukagua mali za chama katika maeneo tofauti ya mikoa hiyo, na kuahidi kuendelea kuunga mkono hatua hiyo itakayosaidia Rasilimali za chama kubaki salama.

  Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu huyo ametembelea maeneo mbali mbali yakiwemo Viwanja vya Chama katika eneo la Mbweni, Nyumba ya Chama eneo la Shangani pamoja na Jumba la kihistoria la ASP lililopo Kijangwani Zanzibar, ambapo ziara hiyo itakuwa ni endelevu kwa upande wa Unguja na Pemba.

  0 0  BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU  TAARIFA KWA UMMA

  KUKANUSHA TAARIFA KWAMBA BODI HAINA FEDHA
   
  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa za upotoshaji zinazoenezwa kwa sasa kwamba haina fedha.

  Si kweli kwamba Bodihaina fedha, ila ni kweli kwamba kumekuwa na ucheleweshaji wa kufikisha fedha za wanafunzi vyuoni kutokana na zoezi la kuhakiki wanafunzi wanaonufaika na mikopo linaloendelea vyuoni hivi sasa.

  Hata hivyo, maandalizi ya malipo hayo yameshafanyika na ‘pay sheets’ zimeshapelekwa vyuoni tayari kwa wanafunzi wanaonufaika na mikopo kusaini.

  Bodi inatarajia wakati wowote wiki ijayo baada ya zoezi la uhakiki kukamilika; itapeleka fedha hizo vyuoni.


  IMETOLEWA NA:
  KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO
  BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
  TAREHE 2 JULAI 2016

  0 0

  Rais wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir Mhe,Raza (kushoto) akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia aliyekaa) wakati Jumuiya hiyo ilipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kukabidhi madawati 100 kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar ikiwa ni katika katua za kuimarisha sekta ya Elimu nchini. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia)akikabidhiwa madawati 100 kutoka kwa Viongozi wa jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir na familia ya Rais wa Jumuiya hiyo Mohamed Raza walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,msaada huo kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar, 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir Mhe,Mohamed Raza Daramsi wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na Viongozi na Mashekhe wa jumuiya hiyo kwa ajili ya kukabidhi msaada wa madawati 100 kwa ushirikiano na familia ya Rais wa Jumuiya,msaada huo utaowanufaisha wanafunzi wa Skuli mbali mbali za Zanzibar .
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma akitoa shukurani kwa Uongozi wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir wakati ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kukabidhi madawati 100 kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) ikiwa ni katika kuimarisha sekta ya Elimu hapa Zanzibar .
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mashekhe wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir (kulia) Sheikh Shaaban Hussein,Sheikh Maulana Dhishan Haidar na Rais wa Jumuiya hiyo Mhe, Mohamed Raza (kushoto) wakati walipofika ikulu Mjini Zanzibar kukabidhi msaada wa madawati 100 kawanafunzi wa Zanzibar.
  [Picha na Ikulu.]

  0 0

  AMPUNI ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam imewatahadharisha wanaouza kazi feki za wasanii mbalimbali hapa nchini kuachana na mfumo huo kwa sababu kuanzia mwezi huu watawakamata wanaofanya biashara hiyo ndani ya mwezi mmoja.

  Akizungumza jana, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alisema wametoa siku 30 kwa wanaofanya biashara hiyo kuachana nayo kabla hawajawashukia. “Tunatoa siku 30 kwa wanaofanyabiashara ya kazi feki za i za wasanii, hiyo biashara waachane nayo kwa sababu inapoteza pato la Taifa,” alisema Msama.

  Msama alisema kwa kuanzia watapita nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa na mkoa kwa mkoa ili kusaka computer zinazotumika kuiba kazi za sanaa. Msama alisema ili kufanikisha kazi hiyo wanashirikiana na Jeshi la Polisi, Wizara ya Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo sambamba na Kampuni ya Msama Promotions ili kufanikisha zoezi hilo ambalo litakuwa ni la kusafisha tatizo hilo.

  Aidha Msama alisema ili kukomesha zoezi hilo wakikuta kazi feki kwenye duka wanabeba mzigo mzima wa kazi za sanaa. Naye Inspekta Jenera wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu alisema jamii inatakiwa kutoa ushirikiano na Polisi katika jambo hilo ambalo linaumiza nguvu kazi ya Taifa.

  IGP Mangu alisema wananchi wanatakiwa kutoa taarifa kwa Polisi ili kazi ifanyike inavyotakiwa kwa lengo la maendeleo ya wasanii ambao wanasaka namna ya kuendeleza maisha yao.

  0 0

  Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkaribisha kwa mazungumzo Ofisini kwake katika Jengo la SMZ Magogoni Jijiji Dar es salaam Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Lu Youqing.
  Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Lu Youqing kati kati akielezea mikakati atakayoitekeleza katika kuratibu usimamizi wa miradi ya Zanzibar iliyopata ufadhili wa Nchi yake ya China.
  Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Lu Youqing mara baada ya mazungumzo yao ya kuimarisha ushirikiano kati ya Zanzibar na China.Picha na – OMPR – ZNZ.

  Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa China Nchini Tanzania Bwana Lu Youqing ameahidi kufanya jitihada za makusudi katika kufuatilia taratibu za Mikataba ya makubaliano kwa upande wa Nchi yake ili kuona kwamba miradi yote ya Zanzibar iliyopata ufadhili wa Nchi hiyo inaanza, inaendelea na kukamilika kwa wakati uliopangwa.

  Akizungumza na Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipomtembelea Ofisini kwake katika Jengo la SMZ Magogoni Jijiji Dar es salaam Balozi Lu Youqing aliitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa Bandari ya Mpiga Duri, ukamilishaji wa ujenzi wa eneo la maegesho ya Ndege kwenye uwanja wa ndege wa Zanzibar pamoja na Mradi wa Kisasa wa mawasiliano kwenye ofisi zote za SMZ { E government }.

  Balozi Lu Youqing. alisema zipo taratibu za ukamilishaji wa Miradi iliyoanzishwa kwa pamoja kati ya pande hizo mbili ambayo imeonekana kuchelewa kiasi kutokana na mabadiliko makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Jamuhuri ya China kwa Uongozi wa Benki ya Taifa ya China { Exim Bank }.

  Alisema jukumu alilonalo kwa sasa ni kuzungumza moja kwa moja na Uongozi wa Benki hiyo kupitia Wizara ya mambo ya Nje ya China ili kupata uelewa wa masuala hayo katika azma ya kuangalia mapungufu yaliyojitokeza ya miradi hiyo na kutafuta mbinu za pamoja za kuyakamilisha.

  Balozi Youqing Alieleza kwamba hatua hiyo inafuatia kuheshimu Vikao na mazungumzo ya pamoja kati ya Viongozi Wakuu Rais Shii Jinping wa Jamuhuri ya Watu wa China na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein kuhusu Miradi hiyo ya Kiuchumi na Maendeleo.

  Alifahamisha kwamba Historia inaonyesha wazi kwamba Visiwa vya Zanzibar vina kumbukumbu ndefu ya kuwa Kituo cha Kibiashara Duniani kwa karne nyingi zilizopita kikitumiwa pia na wafanyabiashara wa Bara la Asia wakiwemo wale wa Jamuhuri ya Watu wa China.

  Balozi Youqing aliahidi kwamba kwa kutumia uwezo wake wa Kidiplomasia atahakikisha kwamba Nchi yake inaendelea kufanyakazi pamoja na Tanzania na Zanzibar kwa ujumla katika kuimarisha miundombinu itakayosaidia kukuza kwa uchumi wa Tanzania hasa sekta ya Kibiashara itakayosaidia kustawisha wananchi walio wengi.

  “ Nitafanya juhudi za makusudi kwa kuuhimiza Uongozi wa Exim Benki ya China inayoratibu uwezeshaji wa miradi ya Kiuchumi na Maendeleo katika Mataifa rafiki hasa yale ya Bara la Afrika kukamilisha taratibu ili kutoa fursa ya kukamilisha miradi yote iliyoanzishwa ”. Alisema Balozi Youqing

  Alisema Benki hiyo ya Exim imekuwa na mpango Maalum kwa uratibu wa Nchi hiyo kuunga mkono ufadhili wa Uwezeshaji wa Miradi mikubwa iliyoanzishwa na Mataifa Rafiki na Nchi hiyo katika kipindi cha Miaka Kumi.

  Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa China Nchini Tanzania amwapongeza Wananchi wa Zanzibar kwa jitihada zao za kukamilisha zoezi la Pili la Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Machi mwaka huu kwa misingi ya amani na utulivu.

  Alisema China imeguswa na hali hiyo kiasi kinachoonyesha kuridhika kwake na kuwa na shauku ya kuzidi kuunga mkono maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar katika kujikwamua Kiuchumi.

  Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kupitia Balozi Zake za Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika kusaidia miradi ya Maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar.

  Balozi Seif alisema China imeonyesha wazi imani yake kwa Zanzibar katika kusaidia kuunga mkono miradi ya ujenzi wa Gati ya Kwampigaduri Maruhubi, Maegesho ya Ndege katika uwanja wa Ndege wa Zanzibar pamoja na ukamilishaji wa Mradi wa Kisasa wa mawasiliano kwenye Ofisi za SMZ { E. government }.

  Alisema muendelezo wa Serikali ya China katika kuiunga mkono Zanzibar unaleta faraja na matumaini makubwa kwa Wananchi waliowengi wa Visiwa vya Zanzibar katika kukomboka kiuchumi.

  Balozi Seif alitolea mfano ukombozi huo ni ule ujenzi wa Gati ya Kisasa ya Mpigaduri ambao utasaidia kukwamua msongamano mkubwa uliopo hivi sasa katika Bandari Kuu ya Malindi hasa uhifadhi wa Makontena yanayoshushwa na kuingia kwa kasi kubwa.

  Alimfahamisha Balozi huyo wa Jamuhuri ya Watu wa China kwamba hivi karibuni alijionea hali halisi ya mrundikano wa Makontena yanayozagaa na kushindwa hifadhi ndani ya Bandari ya Malindi hali ambayo imeleta wasi wasi mkubwa kwa wafanyabiashara wengi walioagiza bidhaa zao kwa ajili ya Siku Kuu ya Iddi el-Fitri.

  Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  2/7/2016.

  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, ajira, vijana na wenye ulemavu), Jenista Mhagama, (kulia), akizungumza jambo wakati alipotembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 2, 2016. Kulia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Fulgence Sebera.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, (katikati), akizungumza jambo wakati alipotembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 2, 2016. Kulia ni Afisa Uhusiano wa WCF, Zaria Mmanga, na kushoto ni Mhasibu wa Mfuko huo, Grace Tarimo

  NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID

  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, ameutaka Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), kujiweka tayari kulipa mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi kama ambavyo Sheria ilivyoelekeza.Waziri Mhagama aliyasema hayo leo Julai 2, 2016 wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inayoshiriki kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iko chini ya Ofisi yake.

  “Najua mnatakiwa kuanza kulipa fidia mwezi huu wa Julai, vipi mko tayari na kama bado basi mjiweke tayari kufanya hivyo.” Alisema Waziri.

  Akimjibu Waziri Mhagama ambaye alifuatana na maafisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), wakiongozwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka hiyo, Sarah Kibonde Msika, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Fulgence Sebera alimwambia Waziri kuwa Mfuko umejiandaa kikamilifu kutoa fidia kwa wafanyakazi ambapo elimu ilitolewa kwa wadau wengi wakiwemo madaktari kote nchini watakaowafanyia tathmini wafanyakazi waliopata madhara mahala pa kazi.

  Sebera pia alitoa wito kwa wadau kutembelea banda la WCF ili kujipatia maelezo ya kina ,kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko huo ikiwemo Fidia kwa Wafanyaakzi ambayo inaanza kutolea Julai mosi mwaka huu wa 2016.Banda la WCF liko kwenye ukumbi wa Sabasaba kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere.
  Waziri akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakzi wa WCF, na maafisa wa SSRA.

  Waziri akiagana na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha na Mipango, Ben Mwaipaja, baada ya kutembelea Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwenye Jengo la Wizarabya Fedha, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 2, 2016. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha SSRA, Sarah Kibonde Msika.

  Afisa Uhusiano wa WCF, Zaria Mmanga, (Kushoto), akimpatia maelezo mwananchi huyu aliyetembelea banda la WCF
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha Mshomba, (kulia), akijadiliana jambo na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Fulgence Sebera, nje ya banda la WCF kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam jijini Dar es Salaam.

  Grace Tarimo, (kulia), Afisa wa fedha wa WCF, akimpatia maelezo mwananchi aliyetembelea banda la Mfuko huo.
  Zaria akimpatia maelezo mwananchi aliyetembelea banda la WCF

  0 0


  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akifungua Kikao cha Uongozi cha Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika kilichofanyika jijini Dar es Salaam, 02 July, 2016.
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa tatu toka kushoto) akiongea na Viongozi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika wakati wa Kikao cha Uongozi kilichofanyika jijini Dar es Salaam, 02 July, 2016.
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akimweleza jambo Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya Afrika, Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) (kushoto) kutoka Afrika Kusini wakati wa Kikao Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika wakati wa Kikao cha Uongozi cha Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika kilichofanyika jijini Dar es Salaam, 02 July, 2016.

  Baadhi ya Wajumbe na Sekretarieti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika wakifuatilia agenda za kikao kilichokuwa kikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya Afrika, Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) wakati wa Kikao cha Uongozi cha Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika kilichofanyika jijini Dar es Salaam, 02 July, 2016.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya Afrika, Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) (aliyekaa mbele) akiongea Viongozi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika wakati wa Kikao cha Uongozi kilichofanyika jijini Dar es Salaam, 02 July, 2016.

  Sekretarieti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika wakifuatilia agenda za kikao kilichokuwa kikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya Afrika, Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) wakati wa Kikao cha Uongozi cha Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika kilichofanyika jijini Dar es Salaam, 02 July, 2016.

  Baadhi ya Wajumbe walioshiriki katika Kikao cha Kikao cha Uongozi cha Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika wakifuatilia agenda ya kikao hico kilichofanyika jijini Dar es Salaam, 02 July, 2016.

  Wajiumbe wa Kikao cha Uongozi wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa tatu kulia waliokaa mbele) mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam, 02 July, 2016. Picha na Ofisi ya Bunge)

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN ameviagiza viwanda vyote nchini kutumia msibomilia (BARCODES) za Tanzania kama hatua ya kuimarisha masoko na utambulisho wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na ya nje ya nchini.

  Makamu wa Rais ametoa agizo hilo kwenye uzinduzi wa kampeni ya “NUNUA 620 Nunua Bidhaa za Tanzania” pamoja na Kusherekea miaka MITANO ya Taasisi ya Global Standard One –GSI-kwenye Viwanja wa Mwalimu Nyerere katika Maonyesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam (SABASABA) mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonyesho.

  Makamu wa Rais amesema matumizi ya BARCODES ni muhimu na ni ya lazima kwa sababu yanajumuisha taarifa nyingi ikiwemo asili ya bidhaa,jina la kampuni, kumbukumbu za uzalishaji,utunzaji,usafirishaji na usambazaji wa bidhaa.

  Ameleeza kwamba itakuwa ni aibu kubwa kama katika masoko ya ndani ya nchi bado kutakuwa na bidhaa zinazotumia msibomilia (BARCODES) za nje na kusisitiza kuwa matumizi ya Barcodes za Tanzania zitazuia na kupungua upotevu wa ajira kwa wataalamu wa ndani ya nchi.

  Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amesema kuwa serikali ya awamu ya TANO ipo Tayari kufanya kazi na sekta binafsi katika kuleta mapinduzi makubwa yatakayosaidia kukuza uchumi wa taifa.

  Kuhusu uanzishwaji wa Majukwa ya kumwezesha wanawake Kiuchumi nchini, Makamu wa Rais amesema kuwa atahakikisha majukwaa hayo yanaleta matokeo chanya na yenye tija kwa wanawake Wakitanzania mijini na viijijini kwa kuwezeshwa kupata kupata elimu ya ujasiriamali,fursa za masoko,upatikanaji wa mikopo nafuu pamoja na elimu ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakwaza wanawake kiuchumi.

  Makamu wa Rais pia ametoa wito maalum kwa wanawake kote nchini kujiunga na majukwaa hayo pindi yatakapoanzishwa kwenye maeneo yao kwa sababu yatakuwa na faida kubwa kwao kwa kuunganisha nguvukazi zao na kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu.

  Imetolewa na
  Ofisi ya Makumu wa Rais
  2-Jul-16

older | 1 | .... | 898 | 899 | (Page 900) | 901 | 902 | .... | 1897 | newer