Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

PPF YAENDELEA KUNG'ARA MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA SABASABA

$
0
0

Afisa Msaidizi wa Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mohamed Siaga akifurahia huku kionyesha tuzo walizokabidhiwa.
Baadhi ya wafanyakazi wa PPF wakiwa na furaha baada ya kukabidhiwa kikombe chao
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, akihojiwa na Waandhi wa habari baada ya Mfuko wake kukabidhiwa Kikombe cha ushindi wa kwanza wa Kundi la Mifuko ya Hifadhi ya jamii na Makampuni ya Bima katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba.
Picha ya pamoja.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni w PPF, Lulu Mengele, akimuongoza Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godious Kahyarara (katikati) walipokuwa wakitembelea Banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya Biashara ya Kimataifa viwanja vya Sabsaba.

Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Saluna Aziz Ally (kulia) na Glory Maboya, wakiendelea kutoa huduma kwa wateja wao waliofika katika Banda la maonesho Sabasaba la mfuko huo.

Sehemu ya Wananchi wakiwa ndani ya Banda la PPF wakipata huduma na maelezo kuhusu namna ya kujiunga na mfuko huo na jinsi wanachama wanavyoweza kufaidika kupitia michango yao.
.

Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Sostenes Lyimo, akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godious Kahyarara, na wasaidizi wake wakati walipotembelea katika Banda la Maonesho la Mfuko huo kwenye Viwanja vya Sabasaba jana. Picha na Mafoto Blog
Afisa Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Janeth Ezekiel, akizungumza na mwananchi aliyefika kwenye Banda lao la Maonesho katika Viwanja vya Sabasaba wakati akimwelekeza jambo kuhusu mafao ya Mfuko huo. 

Afisa Mwandamizi na Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna Shayo, akimfafanulia jambo mmoja kati ya wananchi waliofika katika Banda la Mfuko huo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Mwananchi akitoa maoni yake katika mashine maalum baada ya kupata huduma kwenye Banda la Maonesho la Mfuko wa Pensheni wa PPF, Maonesho ya KImataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mwananchi akitoa maoni yake katika mashine maalum baada ya kupata huduma kwenye Banda la Maonesho la Mfuko wa Pensheni wa PPF, Maonesho ya KImataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mwajuma Msina, akimkabidhi Kitambulisho Mwanachama Mohamed Hassan (23) aliyejiunga na huduma ya ‘Wote Scheme’ wakati alipotembelea kwenye Banda la Maonesho la Mfuko huo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Afisa Michango wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Glory Maboya, akimkabidhi Kitambulisho Mwanachama Hussein Nuru (25) aliyejiunga na huduma ya ‘Wote Scheme’ wakati alipotembelea kwenye Banda la Maonesho la Mfuko huo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya Wananchi wakiwa ndani ya Banda la PPF wakipata huduma na maelezo kuhusu namna ya kujiunga na mfuko huo na jinsi wanachama wanavyoweza kufaidika kupitia michango yao.
Baadhi ya Wananchi wakijaza Fomu za kujiunga na huduma ya Wote Scheme baada ya kupata maelezo ya kutosha nay a kuridhisha kuhusu huduma hiyo, wakati walipotembelea banda ya PPF.

Baadhi ya Wananchi wakijaza Fomu za kujiunga na huduma ya Wote Scheme baada ya kupata maelezo ya kutosha nay a kuridhisha kuhusu huduma hiyo, wakati walipotembelea banda ya PPF.

Sehemu ya Wananchi wakiwa ndani ya Banda la PPF wakipata huduma na maelezo kuhusu namna ya kujiunga na mfuko huo na jinsi wanachama wanavyoweza kufaidika kupitia michango yao.


Sehemu ya Wananchi wakiwa ndani ya Banda la PPF wakipata huduma na maelezo kuhusu namna ya kujiunga na mfuko huo na jinsi wanachama wanavyoweza kufaidika kupitia michango yao.
Sehemu ya Wananchi wakiwa ndani ya Banda la PPF wakipata huduma na maelezo kuhusu namna ya kujiunga na mfuko huo na jinsi wanachama wanavyoweza kufaidika kupitia michango yao.
Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Elihuruma Mgoi, akimkabidhi Kitambulisho Mwanachama Mussa Mzobora (44) aliyejiunga na huduma ya ‘Wote Scheme’ wakati alipotembelea kwenye Banda la Maonesho la Mfuko huo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Afisa Uendeshaji wa PPF Pauline Msanga, akitoa huduma.
Sehemu ya Wananchi wakiwa ndani ya Banda la PPF wakipata huduma na maelezo kuhusu namna ya kujiunga na mfuko huo na jinsi wanachama wanavyoweza kufaidika kupitia michango yao.
Sehemu ya Wananchi wakiwa ndani ya Banda la PPF wakipata huduma na maelezo kuhusu namna ya kujiunga na mfuko huo na jinsi wanachama wanavyoweza kufaidika kupitia michango yao.
Sehemu ya Wananchi wakiwa ndani ya Banda la PPF wakipata huduma na maelezo kuhusu namna ya kujiunga na mfuko huo na jinsi wanachama wanavyoweza kufaidika kupitia michango yao.

WAZIRI WA KAZI ATEMBELEA BANDA LA NSSF KATIKA MAONYESHO YA SABASABA 2016

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (wa pili kulia), akipata maelezo kutoka kwa Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume (kulia), wakati alipotembelea banda la NSSF kwenye maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (katikati), akiwa katika banda la NSSF.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (katikati), akipata maelezo kutoka kwa Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume (kulia), wakati alipotembelea banda la NSSF kwenye maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama akiangalia Kadi ya mwanachama aliyejiunga na NSSF.Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume (kushoto), akitoa maelezo kuhusu huduma za bima zinazotolewa na NSSF kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu, Jenista Mhagama. Kulia ni Mtaalam wa Bima, Peter Isack.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana na Walemavu, Jenista Mhagamaakizungumza na waandishi wa habari.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (kulia) akipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara mara baada ya kuwasili katika banda la Shirika hilo.Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifashi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akisalimiana na Waziri Jenista Mhagama.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama akisalimiana naOfisa Uhusiano wa NSSF, Devota.

PSPF YASAJILI WANACHAMA WAPYA LUKUKI KWENYE MAONYESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA DAR ES SALAAM 2016

$
0
0
Wanafunzi wa chuo Cha Uhasibu (TIA), jijini Dar es Salaam, wakipatiwa maelezo ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF walipotembelea banda la Mfuko huo lililoko jingo la Wizara ya fedha kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, 2016 viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 2, 2016.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, (kulia), akizungumza jambo wakati alipotembelea banda la Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwenye jingo la wizara ya fedha viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 2, 2016 ambako yanafanyika maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam. Hapa waziri akipatiwa maelezo na Afisa Uendeshaji wa PSPF, Hadji Hamisi Jamadari


Afisa Kumbukumbu wa Mfuko Pensheni wa PSPF, Lupakisyo J. Mwaipungu (kushoto), akimsikiliza Mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo na kuamua kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari PSS Julai 2, 2016

BANDA LA BENKI YA CRDB LAVUTIA WENGI MAONYESHO YA 77

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), akishiriki kutoa huduma kwa wateja waliofika katika banda la benki hiyo lililopo kwenye Maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea banda la CRDB na kushiriki kutoa huduma kwa wateja waliofika katika banda hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.
Ofisa Mauzo wa Benki ya CRDB, Robertius Twijuke (kushooto) akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo waliofika kwenye banda la benki hiyo wakati wa maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba.
Banda la CRDB linavyoonekana.
Banda la Benki ya CRDB.
Ofisa Mauzo wa Benki ya CRDB, Robertius Twijuke (katikati) akimuhudumia mteja wa benki hiyo kwenye maonyesho ya Sabasaba.
Wateja wa Benki ya CRDB wakipata maelezo ya huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo.
Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Gerald Mhalanyambu (kushoto), akimsikiliza mteja wa benki hiyo.
Wateja wa benki ya CRDB, wakipata maelezo juu ya huduma za benki hiyo.
Wateja wa Benki ya CRDB wakiwa katika foleni ya kutoa na kuweka fedha katika tawi linalotembea lililopo katika maonyesho ya Sabasaba.
Wateja wa Benki ya CRDB wakipata maelezo katika banda la benki ya CRDB.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (katikati), akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa VETA wakati alipotembelea maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa ya Sabasaba.

SHEIKH MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AUNGA MKONO JUHUDI ZA KUWAKOMBOA WAPALESTINA

$
0
0

Mgeni Rasmi katika semina ya kitaalam iliyofanyika Jijini Dar es salaam leo ambaye ni Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam , Alhadi Mussa Salum, akitoa mada katika semina maalum ya wataalam mbalimbali iliyokuwa na lengo la kujadili kwa pamoja swala la siku ya QUDS Duniani ambayo n i siku maalum ya kuwakumbuka na kupaza sauti kuwatetea wananchi wa Taifa la palestina ambao wamekuwa wakipata mateso makubwa kutoka katika Taifa la israel siku ambayo iliazimishwa Jana Duniani kote huku watu mbalimbali wakifanya matembezi ya kuonyesha kuguswa na swala hilo.

Akizngumza katika semina hiyo ya Wataalam iliyofanyika Jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Karemjee Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum amesema kuwa swala la maisha ya wananchi wa Nchi ya Palestina ni swala la wanadamu wote bila kujali itikadi za kidini hivyo ni Jukumu ya kila mwanadamu kusimama kuwatetea wananchi ambao wanaporwa ardhi yao na Taifa la Israel..

Ameongeza kuwa katika kuazimisha siku ya QUDS Duniani ni siku sio ya wapalestina pekee bali ni siku ya kuazimishwa na dunia nzima kwakuwa mateso wanayopata wanadamu wenzetu ni makubwa na hayavumiliki hata kidogo. Picha zote na EXAUD MTEI Msaka habari.

Balozi wa palestina nchini Tanzania HAZEEM SHABAT akizungumza katika semina hiyo ambapo amesema kuwa hadi kufikia sasa watu zaidi ya 48488 wamepoteza mahali pa kuishi tangu mwaka 1967 jambo ambalo limekuwa hatari sana kwa wanadamu hao ambao hawana hatia.

Balozi huyo amesema kuwa Ni wakati sasa wa mataifa yanayopenda haki likiwemo Taifa la Tanzania kuinuka kwa pamoja na kuungana ili kupigania Haki ya nchi ya palestina ili waweze kuachiwa Ardhi yao ambayo imekuwa inadhulumiwa na Taifa la Israel na kusababisha madhara makubwa likiwemo la maafa na unyanyasaji mkubwa kwenye ardhi yao.

Profesa ABDUL SHARIFU kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam (pichani) akizngumza kuhusu historia ya mgogoro mkubwa baina ya Mataifa ya Palestina na Israel.

Balozi wa Jamhuri ya watu wa IRAN nchini Tanzania MEHDI AGHA JAFAI akitoa mada katika semina hiyo maalumu ya wataalam mbalimbali iliyofanyika kwa lengo la kujadili kwa undani mgogoro wa nchi hizo mbili ikiwa ni jana tu dunia imeadhimisha siku ya QUDS Duniani.

Balozi huyo wa IRAN amesema kuwa kutokana na ukubwa wa tatizo hilo baadhi ya mabalozi waliopo nchini na wadau mbalimbali wa amani wamelazimika kuunda kamati maalum maarufuu kama TANZANIA/PALESTINE SOLIDARITY COMMETTE kamati ambayo ina jukumu la kusimama na kupaza sauti kuwatetea wapalestina ambao wanateseka kwa sasa.

Aidha amesema kuwa kumekuwepo na juhudi mbalimbali za mataifa makubwa likiwemo Taifa la Marekani kujaribu kukwamisha Juhudi za kuwasaidia wapalestina ikiwa ni pampja na kutolipa swala hilo kipaumele ila ameuhakikisha ulimwengu kuwa wapalestina wapo imara na hawakati tamaa katika kutetea amani na haki yao ambayo inataka kuporwa na mataifa mengine.
 
 



Meza kuu ikiongozwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum, wakiendelea na semina hiyo Leo Jijini Dar es salaam



BAADHI YA MATUKIO KATIKA SEMINA HIYO.





Baadhi ya picha za matukio ya mateso nchini palestina



BANDA LA PSPF LAVUTIA WENGI, WAMO PROFESA GODIUS KAHYARARA WA NSSF NA MKURUGENZI MKUU WA GEPF DAUD MSANGI

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (kushoto), akizungumza jambo wakati Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara (wapili kushoto), alipotembelea banda la PSPF kwenye jingo la Wizara ya Fedha na Mipango viwanja vya Mwalimu Nyerere kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 1, 2016. (Wapili kulia) ni Meneja Masoko, Mawasiliano na Uenezi, Costantina Martin
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (kushoto), akifurahia jambo na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara, wakati alipotembelea banda la PSPF lililoko jingo la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Julai 1, 2016. Maonyesho hayo yanayoshirikisha nchi 30 kutoka sehemu mbalimbali duniani yalifunguliwa rasmi na Rais wa Rwanda, Paul Kagame

Mwananchi akitazama vipeperushi vyenye maelezo ya kina kuhusu shughukli za Mfuko wa PSPF wakati alipotembelea banda la Mfuko huo

Mwananchi akijaza fomu za kujiunga na Mfuko wa PSPF kupitia mpango wa uchagiaji wa hiari PSS
Mkurugenzi Mkuu wa GEPF Daud Msangi,(kushoto), akipatiwa maelezo na meneja masoko, mawasiliano na uenezi, costantina martin (katikati) na afisa masoko mwandamizi wa mfuko huo, rahma ngassa (kulia)
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu (kushoto) akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Imani Kajula mara baada ya hafla ya uzinduzi wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Julai 1, 2016
Wananchi wakihudumiwa walipotembelea banda la PSPF
Meneja Masoko, Mawasiliano na Uenezi, Costantina Martin(Wanne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na kikosi kazi cha Mfuko huo ambacho kimepiga kambi kwenye banda la Mfuko huo tayari kuwahudumua wanachama na wananchi wanaotembelea banda hilo
Kikosi kazi cha PSPF kinachotoa huduma kwa wanachama na wananchi wanaotembelea banda la Mfuko huo pale Sabasaba
Catherine Salema ,(kushoto), afisa uendeshaji wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, akimpatia maelezo mananchi huyu aliyetembelea banda la PSPF lililoko jingo la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, Julai 1, 2016.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, (wapili kulia), akipeana mikono na afisa Kumbukumbu wa Mfuko huo, Lupakisyo J. Mwaipungu wakati alipofika kwenye banda hilo.
Wafanyakazi wa PSPF wakimsikiliza mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo ili kujua huduma zitolewazo na Mfuko huo
Mfanyakazi wa PSPF, akimpatia maelezo mwananchi huyu aliyetembelea banda hilo

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YANUNUA 620 KWENYE KILELE CHA SHEREHE ZA MIAKA 5 YA KUZALIWA KWA GS1 NA KUADHIMISHA SIKU YA TWCC

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizindua kampeni ya NUNUA 620 (msibomilia) katika ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Bw. Gideon Mazara na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (kushoto) kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye bango la GS1 mara baada ya kuzindua kampeni ya NUNUA 620 kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania Bi. Fatma Kange .

Wanawake kutoka Majukwaa mbali mbali ya Wanawake nchini wakishangilia kwa kujumuika na Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) baada ya kuzindua kampeni ya NUNUA 620 kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa wakati maonyesho ya 40 ya Biashara ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage wakati wa kutembelea maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya jiko lililotengenezwa Tanzania na rafiki wa mazingira wakati alipotembelea mabanda mabali mbali kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kabati lililotengenezwa kwa mbao ya mnazi wakati alipotembelea moja la banda la wajasiriamali kuotoka Zanzibar wakati wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumzana fundi wa kushona nguo mwenye ulemavu wa macho (asiyeona) ambaye anafahamika kama Mtaalamu wa kushona Tanzania Ndugu Abdallah Nyangalio, kulia ni Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage wakati wa maonyesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangali moja ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wanawake wakati wa maonyesho ya kimataifa ya biashara
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ubunifu wa hali ya juu ya gauni la kanga kwenye moja ya mabanda ya wajasiamali wa Kitanzania wakati wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipewa maelezo juu ya bidhaa zinazotengenezwa nchini na Bi. Flaviana Tesha wa Kampuni ya Chai Bora wakati wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiuliza maswali mbali mbali alipotembelea banda la Benki ya Watu wa Zanzibar kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam.

.....................................


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameviagiza viwanda vyote nchini kutumia msibomilia (BARCODES) za Tanzania kama hatua ya kuimarisha masoko na utambulisho wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na ya nje ya nchini.

Makamu wa Rais ametoa agizo hilo kwenye uzinduzi wa kampeni ya “NUNUA 620 Nunua Bidhaa za Tanzania” pamoja na Kusherekea miaka MITANO ya Taasisi ya Global Standard One –GSI-kwenye Viwanja wa Mwalimu Nyerere katika Maonyesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam (SABASABA) mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonyesho.

Makamu wa Rais amesema matumizi ya BARCODES ni muhimu na ni ya lazima kwa sababu yanajumuisha taarifa nyingi ikiwemo asili ya bidhaa,jina la kampuni, kumbukumbu za uzalishaji,utunzaji,usafirishaji na usambazaji wa bidhaa.

Ameleeza kwamba itakuwa ni aibu kubwa kama katika masoko ya ndani ya nchi bado kutakuwa na bidhaa zinazotumia msibomilia (BARCODES) za nje na kusisitiza kuwa matumizi ya Barcodes za Tanzania zitazuia na kupungua upotevu wa ajira kwa wataalamu wa ndani ya nchi.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa serikali ya awamu ya TANO ipo Tayari kufanya kazi na sekta binafsi katika kuleta mapinduzi makubwa yatakayosaidia kukuza uchumi wa Taifa.

Kuhusu uanzishwaji wa Majukwa ya kumwezesha wanawake Kiuchumi nchini, Makamu wa Rais amesema kuwa atahakikisha majukwaa hayo yanaleta matokeo chanya na yenye tija kwa wanawake Wakitanzania mijini na viijijini kwa kuwezeshwa kupata kupata elimu ya ujasiriamali,fursa za masoko,upatikanaji wa mikopo nafuu pamoja na elimu ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakwaza wanawake kiuchumi.



BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MA DC WATANO WALA KIAPO LINDI

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh Godfrey Zambi amewaapisha wakuu wa wilaya tano za mkoa huo na hii ni picha ya pamoja mara baada ya kiapo


Wakuu wa wilaya wakiendelea kula kiapo

Na Mathias Canal, Lindi

Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh Godfrey Zambi amewaapisha wakuu wa wilaya tano za mkoa huo huku kila mmoja akiahidi utendaji uliotukuka katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi husika.

Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa ambapo mkuu huyo amewasisitiza viongozi hao kuhakikisha suala la upatikanaji wa madawati linazaa taswira chanya kwa kuhakikisha madawati yanatimia kama ambavyo agizo la rais lilitolewa hivi karibuni la kuhakikisha wanafunzi wanaketi katika madawati pasipo kuwa na mbanano.

Zambi amewataka wakuu hao wa wilaya kusimamia vyema utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ccm ili kukamilisha ahadi zilizoahidiwa na rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati wa kampeni zilizoanza Agosti na kumalizika Octoba mawaka jana.

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Rukia Akhibu Muwango amesema atasimamia na kudhibiti suala la watumishi hewa na kulifanya kuwa zoezi endelevu ili wilaya hiyo iweze kusonga mbele kwa muktadha wa mafanikio ya ajira kwa vijana na watu wenye elimu lakini nafasi zao zilishikiliwa na watu wasiokuwa halali (watumishi hewa).

Mkuu huyo ameahidi kukutana na makundi mbalimbali Wilayani humo ili kupata picha halisi ya namna hatua zimefikiwa za kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwa ufanisi mkubwa namafanikio zaidi kwa maana ya kufauli na kufikia mpaka chuo kikuu.

Muwango amesema amekuwa mtumishi erikali kwa muda mrefu hivyo kwa kiasi kikubwa anazifahamu changamoto za wananchi hususani matatiuzo ya upatikanaji wa maji, afya, elimu na miundombinu.

Wilaya ya lindi ni moja kati ya wilaya zilizopo mkoani lindi zinazojihusisha zaidi na kilimo kuliko masomo Muwango amesema kuwa atahakikisha anaanzisha kamati ya maendeleo ya Elimu ya wilaya ambapo Kamati hiyo itakuwa na wataalam na watu maarufu wa Wilaya ya Nachingwea na kamati hiyo itajiwekea mikakati ya uboreshaji Elimu, hivyo mkuu wa Wilaya atatashirikiana na wataalamu wa Halmashauri kuona mikakati hiyo inafanikiwa.

Pamoja na hayo mkuu huyo pia amesema kuwa anataraji kuanzishaTuzo ya Mkuu wa wilaya kwa wanafunzi watakaofanya vizuri kila kata ambapo Vigezo watakubaliana na kamati hiyo.

Wakuu wa Wilaya wengine walioapishwa katika hafla hiyo ni pamoja na mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Joseph Joseph Mkirikiti, Mkuu wa Wilaya ya Liwale Sarah Vicent Chiwamba, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Emil Ngumbiagai

TAARIFA KAMILI YA MSIBA WA ALIYEKUWA MBUNGE WA JIMBO LA KILINDI MAREHEMU BEATRICE SHELUKINDO

$
0
0
Familia ya Bwana William H. Shelukindo, inasikitika kutangaza kifo cha Bibi Beatrice Matumbo Shelukindo (pichani) kilichotokea siku ya Jumamosi 2/7/2016 huko Arusha. 

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu 8 Galu Street,Ada Estate, Dar es salaam na huko Arusha.

Mazishi yatafanyika siku ya Jumatano Tarehe 6/07/2016 alasiri Mjini Arusha.
Bwana ametoa. 
Bwana ametwaa.
 Jina la Bwana na lihimidiwe.
AMINA.

MATUKIO KATIKATI YA JIJI LA DAR LEO

$
0
0



Magari mawili aina ya Toyota Rav4 yakiwa yamegongana katika makutano ya barabara ipitayo Benki ya NMB Bank House na Shirika la Bima la Taifa (NIC) mtaa wa Samora 03 July, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Gari la kufagia barabara la Kampuni ya Green Waste Pro. Ltd likisafisha moja ya barabara ipitayo Benki ya NMB Bank House na Shirika la Bima la Taifa (NIC) mtaa wa Samora 03 July, 2016 Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)

KLABU YA GOLF YA JWTZ LUGALO YAPATA UONGOZI MPYA

$
0
0
Na Selemani Semunyu - JWTZ

KLABU ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi  wa Tanzania ya  Lugalo Jijini Dar es Salaam imeahidi  kuendeleza Uwanja na klabu hiyo na kuwa na mafanikio makubwa kimataifa ukilinganisha na klabu zingine za Golf  na kuwa kitovu cha Michezo na Uchumi  kutokana na uwekezaji katika Uwanja huo.

Hayo yamesemwa  leo na Mwenyekiti Mpya wa klabu hiyo Brigedia Jenerali  Michael Luwongo wakati akikagua Uwanja wa Klabu hiyo ikiwa ni mara ya Kwanza tangu kuteuliwa na kushika nafasi hiyo Jijini Dar es Salaam.
“Uwanja wa Klabu ya Golf ya Lugalo ndio uwanja wa Kwanza uliojengwa na Wazalendo hivyo tunataka kuhakikisha unakuwa na hadhi ya kimataifa na kuzalisha wachezaji watakaoletea taifa Ushindi” AlIsema Brigedia Jenerali Luwongo.
Brigedia Jenerali Luwongo alisema uwekezaji wenye lengo la kuwa kitovu cha Michezo yote kwa kuwa viwanja bora licha ya kuendeleza michezo lakini inaweza kuwa kitovu cha kiuchumi kutokana na wageni na wazawa kutumia viwanja hivyo vitakavyokuwa na ubora wa Kimataifa.

Mwenyekiti huyo alisema mbali na Uboreshaji Miundombinu  kazi kubwa iliyoko mbele yake ni kuhakikisha Mchezo wa golf unachezwa na watu wa rika zote lakini hasa vijana na Watoto ambao watakuwa tegemeo na hazina kubwa kwa Taifa.

Alisema kumekuwa na dhana isiyosahihi kuwa mchezo wa golf ni kwa matajiri dhana ambayo ameipinga na kutaka watu wajitokeze katika Uwanja huo unaomilikiwa na JWTZ ambao gharama za uchezaji wake ni ndogo ukilinganisha na klabu zingine.

“Uwanja ni wa Jeshi lakini sio kwamba Wanajeshi pekee ndio wa naruhusiwa kuja kucheza hata ukiangalia wanajeshi wanaotumia uwanja huo ni ndogo ukilinganisha na raia na wageni toka nje ya Nchi” Alisema  Mwenyekiti.

Aidha alitoa Wito kwa Maofisa na Askari wa JWTZ kujitokeza kuwa wanachama katika Klabu hiyo lakjini pia kushiriki mchezo wa Golf.

Kwa upande wake Msimamizi wa Miundombinu wa Klabu hiyo Kanali Mstaafu   Jackson Nsigaye amesema sasa wana viwanja 18 ambavyo ndio sahihi vya Golf toka Viwanja Tisa walivyokuwa navyo awali na muelekeo ni kuwa na Viwanja vya michezo mingine pia ili kiwe kituo cha michezo.

Naye Meneja wa Uwanja huo Kanali Omary alisema mpaka sasa ndio uwanja pekee wenye mashindano mengi kuliko vilabu vyote na wataendeleza mafanikio hayo katika mwaka huu.

Brigedia Jenerali Luwongo ameteuliwa kushika wadhifa huo  na  Mlezi wa Klabu hiyo ambaye ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kuziba nafasi  iliyoachwa wazi na Marehemu Brigedia Jenerali  Mstaafu Ernest Galinoma.

TZUK-DTF June Newsletter: TUJUMUIKE UK

PSPF YADHIHIRISHA NI MFUKO CHAGUO NAMBA MOJA, WENGI WAJIUNGA NA MPANGO WA PSS MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0

Julita N Mongi, mwanachama mpya wa PSPF kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari, PSS, akionyesha kitambulisho chake cha uanachama alichokabidhiwa dakika 5 tu baada ya kujaza fomu. Huduma hiyo inatolewa kwenye banda la PSPF lililoko jengo la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa, viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Julai 3, 2016. Wananchi wengi wamejitokeza kujiunga na Mfuko huo na kudhihirisha kuwa ni chaguo la wengi. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Julita akikabidhiwa kadi yake na Afisa Masoko wa PSPF, Magira Werema
Mstaafu ambaye kwa sasa ni Mkulima wa Turian, Mzee Gabriel E. Kiogwe (84), akijaza za kujiunga na mpango wa PSS
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, akimkabidhi kadi ya uanachama, Mwanachama mpya, Mzee Gabriel E. Kiogwe (84) dakika 5 baada ya kujaza fomu za kujiunga

Wananchi wa kila kada wakipatiwa maelezo na maafisa wa PSPF kwenye banda la Mfuko huo
 


Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, akimpiga picha Mwanachama mpya Scola Malinga




Njaidi akimkabidhi kadi Scola Malinga, baada ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari, PSS




Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi akiwapatia maelezo ya kina ya faida za kujiunga na uanachama kwenye Mfuko huo, wafanyakazi wa wizara ya Fedha, ambapo baada ya maelezo hayo walijiunga na kuwa wanachama kupitia mpangio wa uchangiaji wa hiari, PSS.




Joyce Kakore, akijaza fomu za kujiunga na mpango huo




Joyce Kakore, wa wizara ya Fedha, (kulia), akikabidhiwa kadi ya kujiunga na uanachama PSPF, kupitia mpango wa PSS. Anayemkabidhi ni Afisa Uhusiano Mwandamizi, wa Mfuko huo, Abdul Njaidi




Afisa Matekelezo wa PSPF, Penzila Kaisi, (kulia), akimpatia maelezo Mwanachama wa Mfuko huo aliyefika kwenye banda la PSPF, ili kujua hali ya michango yake




Afisa wa PSS wa PSPF, SophiaMbilikira, (kushoto), akimsikiliza mwanachama wa PSPF aliyetembelea banda la Mfuko huo




Mwanachama mpya wa PSPF, kupitia PSS, Lillingani S. Juma akionyesha kadi yake




Julita N Mongi akijaza fomu


Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, (kulia) na Afisa Uwekezaji wa Mfuko huo Hawa Kivina, (wapili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wanachama wapya wa Mfuko huo dakika chache baada ya kukabidhiwa kadi zao
Afisa Masoko wa PSPF, Magire Werema, (kushoto), akimkabidhi kadi ya uanachama wa PSPF, mwanachama mpya, Grace M Malya
Grace M Malya akiwa amembeba mtoto wake, akionyesha kadi yake ya uanachama baada ya kukabidhiwa


Afia Uhusiano Mwandamizi, wa PSPF, Abdul Njaidi akimkabidhi kadi ya uanachama mwanachama mpya Catherine D Mhina





Afisa uwekezaji wa PSPF, Hawa Kivina, (kushoto), akimpatia maelezo Mwanachama wa Mfuko huo, Meneja Mawasiliano, Mamlaka ya Udhibiti Makampuni ya Bima Tanzania, Eliezer Rweikiza, juu ya mikopo ya nyumba




Hadji Jamadari, Afisa Mwendeshaji Mkuu wa PSPF, akichapisha vitambulisho vya wanachama wapya papo hapo na kuwakabidhi




Catherine D Mhina, akionyesha kadi yake

KAPUMZIKE KWA AMANI MPIGANAJI MWENZETU OMAR MASOUD

$
0
0

Sehemu ya Waombolezaji waliojitokeza kumsindikiza Mpiganaji mwenzetu aliekuwa Mpiga picha wa Kampuni ya Azam Tv, Marehemu Omar Masoud aliefariki Dunia jana kwa ajali ya pikipiki aliyoipata eneo la Makongo Jijini Dar es salaam wakati akielekea kazini. Mazishi yamefanyika mchana huu kwenye Makaburi ya Boko, jijini Dar.
Marehemu Omar Masoud enzi za uhai wake.
Ibada ya mazishi ya ndugu yetu Omar Masoud ikiendelea kwenye Makaburi ya Boko, Jijini Dar es salaam mchana huu.
Waombolezaji.
Waumini wa Kiislam wakiuswalia Mwili wa Marehemu kabla ya kwenda kuuhifadhi kwenye nyumba yake ya Milele kwenye Makaburi ya Boko, Jijini Dar es salaam.

Innalilahi wa inna ilaihi rajiun

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mhe. Beatrice Shelukindo

$
0
0



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Kilindi Mkoani Tanga Mhe. Beatrice Shelukindo kilichotokea jana tarehe 02 Julai, 2016.


Mhe. Beatrice Shelukindo ambaye amewahi kuwa Mbunge Bunge la Afrika Mashariki na baadaye kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vipindi viwili mfurulizo hadi alipostaafu mwaka jana 2015, amefariki dunia akiwa nyumbani kwao Njiro Mkoani Arusha.


Katika salamu zake Rais Magufuli amesema taifa limempoteza mtu aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo hususani alipokuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwawakilisha wananchi wa Jimbo la Kilindi na Mkoa wa Tanga.


“Mhe. Beatrice Shelukindo alikuwa kiongozi shupavu, ambaye siku zote alisimama kidete kupigania maendeleo ya wananchi na kutetea rasimali za taifa.“Kupitia kwako Mhe. Spika Job Ndugai naomba unifikishie salamu zangu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu na pia kwa wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” Amesema Rais Magufuli.


Dkt. John Pombe Magufuli pia amewaombea wote walioguswa na kifo cha Mhe. Beatrice Shelukindo kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki cha kuondokewa na mpendwa wao na amemuombea marehemu apumzishwe mahali pema peponi, amina.



Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam
03 Julai, 201

SHRIKA LA TAIFA LA BIMA (NIC ) KUANZISHA BIMA YA KILIMO

$
0
0

Naibu katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango- Hazina Ndugu Dotto Mgosha James akipokea zawadi toka NIC iliyokabidhiwa na Mkuu wa kitengo cha Mahusiano , Mwanaidi Shemweta. NIC ilishiriki maonyesho ya 40 katika viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere maarufu kama sabasaba kama ilivyo desturi ili kutoa elimu kwa umma kuhusiana na maswala ya Bima. Pamoja na kutoa Elimu NIC imepata fursa ya kuelezea bidhaa mpya zilizokwishaanzishwa pamoja na zile mpya zinazotarajia kuanzishwa hususani Bima za KILIMO. Wananchi wanakaribishwa kuja kupata elimu hizo.
Naibu katibu mkuu Wizara ya Fedha na Mipango-Hazina Ndugu Dotto Mgosha James akitia saini kitabu cha wageni ndani ya banda la NIC baada ya kupata maelezo kutoka kwa wataalamu wa maswala ya Bima NIC.
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na wenye ulemavu Mheshimiwa Jenista Mhagama akipokea zawadi toka NIC iliyokabidhiwa na Bw. Elisante Maleko Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa wateja baada ya kutembelea na kupata maelezo yahusuyo maswala ya Bima ndani ya banda la NIC. Wakuu hawa wameona umuhimu wa Bima zitolewazo na NIC na wamesisitiza swala la Elimu liwe endelevu ili jamii ya kitanzania ipate uelewa na hatimaye kukatia bima hizo kwa manufaa ya familia zao.

AMEPOTEA ! ANATAFUTWA NA FAMILIA YAKE

$
0
0
Bwana Philemon Anamwikira Ikaa Munuo,
Anayeoneka Kwenye Picha Hapo juu anaitwa Philemon Anamwikira Ikaa Munuo, umri miaka (61) ametoweka kuuanzia siku ya juma tano tar.29.06.2016 Nyumbani kwake Bunju B Dsm, Tafadhali yeyote atakaemuona apige simu Police au Kwenye number zifuatazao..0713449666 (Rich) 0754226760 (Tumsifu) 0713552828(Rodrick) 0718555909 (lucas) 0713481648 (Tumaini)..Tafadhali sambaza ujumbe huu.

CUF YAZINDUA TAWI LA WANAFUNZI WANACHAMA WA CUF LA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (JIVICUF UDSM)

$
0
0
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimezindua Tawi la Wanafunzi wanachama wa CUF la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Jivicuf UDSM), ikiwa ni moja ya mikakati ya kujitanua kisiasa kwa chama hicho.

Uzinduzi huo umefanywa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa , Juvicuf, ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga Hamidu Bobal, Dar es Salaam jana ambapo aliwataka vijana kutumia ujana kupigania haki na demokrasia nchini.Alisema pamoja na kupigiani haki hasa za wanyonge vijana pia wanapaswa kushika nafasi mbalimbali za uongozi ili kusimamia rasilimali za nchini na wananchi.

"Nimezindua tawi hili la Juvicuf UDSM, nawataka mfanye siasa za nidhamu lakini msiwe waoga kwani sisi tumechelewa katika hizi harakati naamini mtaendana na kasi ambayo tunataka ya kuitanga CUF kila mahali." alisema

Alisema atawapigania vijana wote ambao watashiriki katika nafasi za uongozi kuanzia ngazi ya mitaa, vijiji, kata, wilaya, jimbo, mkoa na taifa ili kuendeleza chama chao.Bobal aliwapa tahadhari vijana hao kuwa siasa si jambo la lelemama wanahitajika kujituma ili kuweza kufikia mafanikio kwani yeye mwenyewe amepitia changamoto nyingi hadi kufikia hapo alipo.

Mbunge huyo alisema historia yake alikuwa mwalimu wa Sekondari ambapo alipotangaza kujihusisha na siasa alipata changamoto kutoka kwa walimu wenzake ila leo amefanikiwab kuwa mbunge na kutumikia wananchi wa Mchinga.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mbunge wa Kilwa Kusini Seleman Bungara maarufu Bwege CUF, aliwataka vijana hao kujikita katika kutetea wanyonge kwani ndio njia ambayo itawasaidia kuchaguliwa na wananchi."Mimi nilifanikiwa kushinda ubunge kwa sababu nilikuwa natetea watu wanyonge nilipambana na watu matajiri lakini niliwashinda kwa sababu wananchi waliangalia mtu sahihi na si fedha," alisema.

Mbunge wa Liwale Zubeir Kuchauka CUF, alisema siasa ndio kila kitu katika maisha hivyo ni vigumu kutenganisha siasa na wananchi.Kuchauka aliwataka vijana hao kuwa wavumilivu katika kupigania maslahi ya nchi kwa kuweka uzalendo mbele na haki.

Mwenyekiti wa Juvicuf UDSM, Jidawi Chande, alisema, tawi hilo kwa sasa lina vijana wanachama wa CUF zaidi ya 100.Alisema changamoto walizonazo ni ukosefu wa ofisi hivyo kuwaomba wabunge hao kuwasaidia kupata ofisi ili waweze kufanya kazi cha chama kwa uhuru.
 Hapa ni wanafunzi hao wakiwa na furaha baada ya kukabidhiwa kadi
 Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa , Juvicuf, ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga Hamidu Bobal (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi hao baada ya kuzindua tawi hilo.
 Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa , Juvicuf, ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga Hamidu Bobal (kushoto), akizungumza na wanafunzi wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (JIVICUF UDSM), Dar es Salaam jana wakati akizindua tawi la wanafunzi hao katika chuoni hapo.
 Mbunge wa Kilwa Kusini Seleman Bungara maarufu Bwege (CUF), akizungumza na wanafunzi hao katika uzinduzi huo.
 Mbunge wa Liwale Zubeir Kuchauka (CUF), akichangia jambo kwenye mkutano huo wa uzinduzi.
Mwongozaji wa uzinduzi wa tawi hilo, akiwa kazini.
 Mbunge wa Viti Maalumu (CUF) kutoka Pangani akichangia jambo.
 Taswira meza kuu katika uzinduzi huo.
 Wanafunzi hao wakiwa katika hafla hiyo ya uzinduzi.
 Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa , Juvicuf, ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga Hamidu Bobal (kushoto), akikabidhi kadi kwa wanafunzi hao.
 Kadi zikitolewa.
 Kadi zikiendelea kutolewa.


Picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa kadi za kujiunga na umoja huo.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUTURU KATIKA MSIKITI WA KHOJA SHIAITHNA-ASHERI -DAR ES SALAAM.

$
0
0

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakizungumza katika futari iliyoandaliwa kwenye  Msikiti wa   Khoja Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam Julai 3, 2016. Kushoto ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakary Zubery bin Ally na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa  Khoja Shia Ithna-Asheri,  Azim Dewji
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi  akisalimiana na viongozi wa Msikiti wa  Khoja Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam wakati alipowasili msikitini hapo kushiriki katika fuatari ambayo mgeni Rasmi alikuwa Waziri mkuu, kassim Majaliwa Julai 3, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na viongozi wa Msikiti wa  Khoja Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam wakati alipowasili msikitini hapo kushiriki katika fuatari Julai 3, 2016.  Kushoto  ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhaji Mussa Salum na  kushoto kwa Waziri Mkuu  ni Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Mfanyabiashara Maarufu nchini, Mohsin Abdalah  wakati alipowasili kwenye  Msikiti wa  Khoja Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam  kushiriki katika futari iliyoandaliwa msikitini hapo Julai 3, 2016. Katikati ni Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri, Azim Dewji.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na  Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakary Zubery bin Ally baada ya kuwasili kwenye msikiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri jijini Dar es salaam kushiriki kwenye futari iliyoandaliwa msikitini hapo Julai 3, 2016. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es salaam, Ramadhan Madabida.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi wakishiriki  katika swala  kabla ya kufuturu kwenye Msikiti wa  Khona Shia Ithna-Asheri  wa jijini Dar es salaam  Julai 3, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi alipozungumza katika futari iliyoandaliwa katika  Msikiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam Julai 3, 2016. Wanne kushoto ni  ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Abukakary Zubery bin Ally  na watano kushoto ni Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri,  Azim Dewji.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Rais wa Awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi wakimsikiliza Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakary Zubery bin Ally wakati alipozungumza  katika futari iliyoandaliwa  katika Msikiti wa  Khoja Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam Julai 3, 2016. Kushoto ni Sheikh  wa mkoa wa Dar es salaam,  Alhaji Mussa Salum. 

 Mwenyekiti wa  Khoja Shia Ithna-Asheri,  Azim Dewji akizungumza katika futari iliyoandaliwa kwenye  Msikiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam Julai 3, 2016. Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Mwenyekiti wa MOHAMMED ENTERPRISES   GROUP, Gulam Dewji ambaye alitoa mchango wa madawati 500 katika futari iliyoandaliwa kwenye  Msikiti wa  Khoja Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam Julai 3, 2016. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakizungumza katika futari iliyoandaliwa kwenye  Msikiti wa   Khoja Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam Julai 3, 2016.

Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa kwenye  Msikiti wa  Khoja Shia Ithna-Asheri  jijini Dar es salaam wakimsikiliza mgeni rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza Julai 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Airtel na VETA wawafikishia vijana katika mkoa wa Mwanza VSOMO

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella akimpatia vipeperushi mmoja wa kijana katika kijiwe cha Bodaboda mkoani Mwanza wakati alipokwenda kuzindua mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mkononi yajulikanayo kama VSOMO yanayoletwa na VETA kwa kushirikiana na Airtel kwa wakazi wa Mwanza
Meneja huduma kwa jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella mara baada ya kumtembelea ofisini kwakwe na kutambulisha fursa zinazopatikana kwa wakazi wa mwanza kupitia mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mkononi ujulikanayo kama VSOMO unayoletwa na VETA kwa kushirikiana na Airtel.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakazi wa Mwanza katika kijiwe cha waendesha bondabonda wakati alipokwenda kuzindua mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mkononi yajulikanayo kama VSOMO yanayoletwa na VETA kwa kushirikiana na Airtel kwa wakazi wa Mwanza. Pichani ni wafanyakazi wa Airtel na VETA
 
Mpango maalumu wa VSOMO unaotolewa kwa ushirikiano kati ya Airtel na VETA unalenga kuwafikia vijana wengi zaidi katika kila kona ya nchi kupitia simu za mkononi hivyo kuwapa urahisi wakazi wa mwanza na maeneo mengine kupata nyenzo na mbinu muhimu katika biashara zao na kuwaandaa vyema katika ushindani wa ajira ili kuinua uchumi wa viwanda wa Tanzania

Akiongea na wakazi wa Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella aliwapongeza VETA na Airtel kwa kuanziasha mpango huu wa VSOMO kwa wakati muafaka. Alisema “mpango huu ni wakibunifu na umekuja wakati muafaka kwani utawawezesha vijana kupata masomo ya kiufundi ambayo yachochea kukua kwa uchumi wao. Hivyo nawaomba VETA na Airtel wahakikishe VSOMO inaendelea kuwa mpango bora utakaosaidia watanzania kupata vijana wengi wenye taaluma kwaajili ya kuendesha uchumi wa viwanda na kunufaika na ajira zitakazotokana na kufanya vizuri kwa viwanda hivyo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza alitoa wito kwa vijana wa mkoa huo kutumia fursa hii kwa kujiunga na masomo ya VETA kupitia VSOMO. Alitoa shukrani zake na kusema “ Tunafurahi kwa Mwanza kuwa kati ya mikoa iliyopata nafasi ya kushuhudia uzinduzi huu kati ya VETA na Airtel. Nawapongeza kwa kushirikiana na serikali katika kuhakikisha tunawawezesha watanzania kupata elimu bora na ujuzi zaidi kupitia VSOMO.

Kwa upande wake, Meneja huduma kwa jamii wa Airtel , Bi Hawa Bayumi alisema “ katika kutekelea za huduma zetu za jamii kwa nchini Airtel imedhamiria kuwawezesha na kuwaendeleza vijana kujikwamua kiuchumi kupitia program zetu. Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kutengeneza suluhisho la kibunifu kupitia simu za mkononi ambalo limeleta tija kwa jamiii kama vile VSOMO kwaupande wa msomo ya ufundi kwani VSOMO inawawezesha wateja wa Airtel kupata ujuzi na maarifa kupitia viganja vyao”

Akiongea kuhusu VSOMO, Mkuu wa chuo cha VETA kipawa Eng. Lucius Luteganya, alisema “ kuanzishwa kwa mfumo huu wa VSOMO kutachochea mabadiliko makubwa yatakayotoa nafasi kwa watanzania kutumia mpango huu wa kipekee kupata mafunzo ya ufundi kwa urahisi na kwa gharama nafuu mahali popote kwa kutumia simu zao.
 
 Huu ni mpango wa kipekee Afrika mashariki na kati kwa kuwa hakuna taarifa zinazoonyesha mfumo kama kuna application yenye kutoa mafunzo ya ufundi duniani. wazi kabisa kukuwa kwa uchumi wa viwanda kutazidi kukua kutokana na upatikanaji wa elimu za ufundi kwa uhakika na urahisi na hivyo kushukuru kwa ushirikiano ulianzishwa kati ya VETA na Airtel unakaosaidia utekelezaji wa mpango wa viwanda wa serikali ya awamu ya 5

Kozi vinazotolea kupitia application ya VSOMO kwa sasa ni pamoja Misingi Ya Ufundi Wa Pikipiki, Kuweka Umeme, Ufundi Wa Simu, Kuchomelea Na Kuunda Vyuma na Urembo Kozi hizi zinatolewa kwa gharama ya shilingi 120,000, muda wa kufanya mafunzo ya vitendo baada ya kufaulu masomo kwa njia ya mtandao ni masaa 60. Hii inamaanisha kwa aliyedhamiria kushoma itamchukua mwenzi moja kumaliza masomo yake kupitia VSOMO.

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images