Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 897 | 898 | (Page 899) | 900 | 901 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva katika mazungumzo kati yake na wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi yaliyofanyika kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni 30, 2016.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva katika mazungumzo kati yake ya Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi yaliyofanyika kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni 30, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa 2015 kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni30, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Tume ya taifa ya Uchaguzi kwenye Makazi yake mjini Dodoma Juni 30, 2016. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya kuzungumza nao kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni 30, 2016. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damiana Lubuva. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akiwashukuru Watanzania wote walioshiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

  Sweetbert Lukonge na Richard Bukos, DAR HATIMAYE ile safari ya bahati nasibu ya Shinda Nyumba iliyoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers, jana Alhamisi ilifika tamati baada ya kudumu kwa takribani miezi sita, ambapo kulifanyika kwa droo kubwa katika Viwanja wa Zakhem, Mbagala jijini Dar na mshindi kupatikana. Kuponi zote za nchi nzima zikimwagwa sehemu moja ili kumpata mshindi wa nyumba.

  Nelly Mwangosi mkazi wa Mkoa wa Iringa, ambaye ni mama wa nyumbani mwenye watoto wawili ndiye aliibuka mshindi wa nyumba hiyo ya kisasa iliyopo Salasala jijini Dar yenye samani zote za ndani mpya kabisa na mshindi huyo anatarajia kukabidhiwa mali yake hivi karibuni.
  Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global Publishers, Oscar Ndauka akichukua zawadi ya Dinner Set tayari kumkabidhi mshindi.

  Mara baada ya kupigiwa simu kutaarifiwa kuwa yeye ndiye mshindi, mama huyo alisema “Yesu wangu!! Nimefurahi kuona kuwa nimeibuka mshindi, najisikia raha sana, nawaombea Global kwa Mwenyezi Mungu.” Shughuli hiyo ilitarajiwa kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye hata hivyo aliwakilishwa na Meya wa Wilaya ya Temeke, Abdallah Chaurembo ambaye ndiye aliyesoma jina la mshindi huyo.

  Bahati nasibu hiyo ya Shinda Nyumba ilisimamiwa na Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein

  Meya wa Wilaya ya Temeke, Abdallah Chaurembo akisoma jina la mshindi wa nyumba, ambaye ni Nelly Mwangosi kutoka Iringa.
  MC Chaku akimpigia simu mshindi wa nyumba, Nelly Mwangosi kutoka Iringa.
  Meya wa Wilaya ya Temeke, Abdallah Chaurembo akizibwa macho ili akachague kuponi ya mshindi.
  Abdallah Chaurembo akiwa na kuponi ya mshindi wa nyumba.

  Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo akimkabidhi Peter Mihayo zawadi ya Bedsheet.

  Mbali na mshindi wa nyumba, pia kulikuwa na zawadi ndogondogo zilizotolewa kwa washindi wengine. Washindi hao ni Peter Mihayo, Issa Leon Mallya, Frank Ndambo (wote Bed sheets), Mahmoud Mhina alishinda vyombo vya nyumbani (Dinner set) huku Method Kunambi na Halima wakishinda simu ya kisasa (Smartphone).
   
  Mahmoud Mhina akitokomea na zawadi yake ya Dinner Set.

  Wengine ni ving’amuzi vitano vya TING ambapo washindi wake ni Godfrey Mkombo wa Morogoro, Wilbert John mkazi wa Kinondoni, Dar, Baltazar Mrosso kutoka Moshi, Magreth Ndambo wa Tabata, Dar sambamba na Jane Liwinga mkazi wa Dodoma. Pia Hawa Maulidi mkazi wa Mlole, Kigoma alishinda Bed Sheet, huku Helman Haule wa Dodoma akijinyakulia Dinner Set.  Mmoja wa Ma MC wa kilele cha bahati nasibu ya Shinda Nyumba, Kelvin Shayo (kushoto) akiwa na mmoja wa wasomaji wa magazeti ya Global aliyekuwa akisoma jina la mshindi wa zawadi ya Bedsheet.

  Bahati nasibu hiyo ya Shinda Nyumba ilikuwa ikiendeshwa na kampuni hii kupitia kwa magazeti yake ya Risasi, Amani, Uwazi, Championi, Ijumaa Wikienda yanayopatikana kwa shilingi 500 huku lile la Ijumaa linalotoka Ijumaa likiuzwa kwa shilingi 1,000 pekee.  Burudani wakati wa kilele cha bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

  Wakati mchakato wa kuelekea kumpata mshindi huyo jana ukiendelea, wananchi wengi walionekana kufurahishwa na kilichokuwa kikitokea huku wakisema kuwa Global imeweka historia kwa kuwa tukio kama hilo ni nadra kutokea kwa shilingi 500 kumpatia nyumba mtu tena ndani ya Dar es Salaam.
  Mshindi wa simu ya kisasa (Smartphone), Method Kunambi (kulia) akipokea zawadi yake.

  Aidha, kuna wale ambao walionekana kuwa na furaha kupitiliza na kujikuta wakitoa machozi ya furaha kwa kuona nyumba hiyo imeenda kwa mama wa nyumbani ambaye hana kazi. Katika maelezo yake Nelly alisema kwa sasa ana watoto wawili lakini alikuwa nao wanne, wawili walishatangulia mbele ya haki.
  Zoezi la kusoma majina ya washindi wa zawadi ndogondogo likiendelea.

  0 0

  Rais wa klabu ya Simba,Evans Aveva akizungumza mbele ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),kuwatambulisha katibu mkuu mpya wa klabu ya Simba bwana Patrick Kahemele (mwisho kushoto) na kocha mkuu mpya Joseph Omog (pichani kati) ambae ni raia wa Cameroon.Kocha Omog aliwasili jana usiku hapa jijini..
  Pichani wa tatu kulia ni Katibu mkuu mpya wa Simba Patrick Kahemele akifafanua jambi na kwamba kuanzia sasa ndiye atakaehusika na masuala ya klabu hiyo,kwani kwa kipindi kirefu timu hiyo haikuwa na Mtendaji Mkuu ambaye amekuwa akishugulikia masuala mbalimbali ya kiutendaji kwa ujumla. 
  Kocha Mkuu mpya Joseph Omog,ambae ni raia wa Cameroon akifafanua jambo mbele ya wana habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar.
  Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini  humo .Picha na Michuzi Jr.

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

  KLABU ya Simba imemtambulisha kocha mpya leo na kuingia nae kandarasi ya miaka miwili 2016/2018 huku wakimpa nafasi ya kuchagua benchi lake la ufundi. Raisi wa Simba Evance Aveva amesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya kupitia sifa za Joseph Omog na kuona atakuwa msaada mkubwa sana katika kuisaidia timi ya Simba.

  Akizungumza wakati wa utambulisho wa kocha huyo, Aveva amesema huu ni mwanzo mzuri kwa Simba wana imani ana nafasi kubwa ya kuwasaidia katika namna watakavyobadilisha na kupata mafanikio kwa timu hiyo. " Ni mategemeo yetu kuwa kandarasi hii tuliyoingia na Omog itakuwa na mafanikio na malengo makubwa ya Simba ni kuitoa ilipo na kuirudisha kuwa ya zamani, ". Naye Omog amesema kuwa amekuja Simba kwa ajili ya kuisaidia na kuijenga na atafanya kazi vizuri na kwa ufanisi mkubwa.

  Wakati huo huo Aveva alimtambulisha katibu mkuu mpya wa Simba Patrick Kahemele ambaye kuanzia sasa atahusika na masuala ya klabu hiyo na zaidi kwa kipindi kirefu hakukuwa na mtendaji mkuu ambaye anakuwa anashughulikia suala la utendaji kiujumla. 

  Kahemele amesema kuwa, Simba kuna changamoto kubwa sana na malengo yake ni kuitoa ilipo na kuirudisha ilipokiwa zamani na amewahakikishia wanachama wa Simba wote kuwa atashirkiana vizuri na kamati ya utendaji katika kulitekeleza hilo na ndiyo maana hata viongz walimfuata ili waweze kusaidiana. "Nawaahidi kufanya kaz usiku na mchana na katika.msimu unaoanza nitahakikisha tunakwenda kwa kasi na zaidi wameleta kocha mzuri anayejua majukumu yake na mimi nitajibika kulingana na nafasi yangu,".

  Kahemele amesema Simba wana mtaji mzuri wa wanachama na watatumia nafasi hiyo kuwa faida kwao kwani wanaweza kufanya mambo mengi kwa fedha za wanachama hao hao.

  0 0

  Kufuatia kutimiza agizo la uzimaji wa simu bandia, kutokana na agizo elekezi la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA.

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inapenda kuwajulisha wateja wake walio nunua simu orijino kutoka kwa watoa huduma ndani ya maduka yetu ya Airtel, endapo baadhi ya wateja simu zao zitazima kutokana na agizo hilo. 

  Airtel inawatangazia wateja wote watakaoathirika na zoezi hili kutembelea maduka yetu nchi nzima kwaajili ya kuhudumiwa/kurekebishiwa simu zao wakiwa na simu husika pamoja na risiti za manunuzi ya simu hizo.

  Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na zoezi hili.

  Imetolewa na Idara ya mawasiliano 
  Airtel Tanzania

  0 0


  Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki na mameneja wa vyuo na shule binafsi Tanzania (TAMONGSCO) Mrinde Mzanva akiongea na wamiliki na mameneja wa vyuo na shule binafsi kanda ya Dodoma na kuishukuru Mamlaka ya Elimu Tanzania kwa kuwa tayari kusaidia chama hicho katika kuhakikisha wanachangia katika ukuaji wa sekta ya elimu nchini.Kushoto Mwekahazina Taifa wa Chama hicho Bw.Yona Mapenzi na Kulia Mwenyekiti wa Chama hicho kanda ya Dodoma Bw.Revocatus Majuto
  Meneja Mawasilano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Sylvia Lupembe akiongea na wanachama wa Chama cha Wamiliki na Mameneja wa Vyuo na Shule Binafsi Tanzania (TAMONGSCO) katika kanda ya Dodoma na kuwataka kuendelea kuwa karibu na Mamlaka hiyo hasa pale wanapohitaji misaada na mikopo kwa ajili ya kuendeleza shule na vyuo vyao ili kuweza kusaidiana na serikali katika kukuza na kuendeleza sekta ya elimu nchini.
  Meneja Mawasilano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Sylvia Lupembe akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Chama cha Wamiliki na Mameneja wa Vyuo na Shule Binafsi Tanzania (TAMONGSCO) kanda ya Dodoma Leo Mjini Dodoma.
  Meneja Mawasilano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Sylvia Lupembe akiongea na wanachama wa Chama cha Wamiliki na Mameneja wa Vyuo na Shule Binafsi Tanzania (TAMONGSCO) katika kanda ya Dodoma, alipokuwa akiwaeleza kuhusu Majukumu ya Mamlaka hiyo hasa katika kusaidia kuendeleza sekta ya elimu Nchini.

  Meneja Mawasilano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Sylvia Lupembe akiagana na viongozi wa Chama cha wamiliki na mameneja wa vyuo na shule binafsi Tanzania (TAMONGSCO) baada ya kumalizika kwa mkutano huo. PICHA NA HASSAN SILAYO

  0 0


  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (kushoto) akiwapungia wananchi wakati alipomkaribisha Mke wa Rais wa Rwanda Mama Janeth Kagame katika Ofisi zake wakati wa Ziara ya Rais wa Rwanda Mh. Paul Kagame mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Mke wa Rais wa Rwanda Bi. Janeth Kagame (kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Janeth Magufuli mapema hii leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Rais wa Rwanda Paul Kagame hapa nchini .
  Mke wa Rais wa Rwanda Bi. Janeth Kagame (kushoto) akisikiliza kwa makini shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi ya mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakati alipotembelea ofisi hizo ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Rais wa Rwanda Paul Kagame mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Mke wa Rais wa Rwanda Bi. Janeth Kagame (kushoto) mara baada ya Mama Kagame kutembelea ofisi za Mama Magufuli ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Rais wa Rwanda Paul Kagame mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (kulia) akiagana na mgeni wake Mke wa Rais wa Rwanda Bi. Janeth Kagame (kushoto) mara baada ya Mama Kagame kutembelea ofisi za Mama Magufuli ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Rais wa Rwanda Paul Kagame mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Benjamin Sawe - Maelezo

  0 0
 • 07/01/16--05:38: PENUEL CONFERENCE 2016


 • PENUEL Maana yake ni mahala pa Kukutana na Mungu uso kwa uso na nafsi yako ikabaki salama, hii ni kulingana na Mwanzo 32:30 kwa kile kilicho mtokea Yakobo,Kongamano la Penuel linamahanisha mahala pa kukutana na Mungu kupitia Neno lake linalo hubiriwa na watumishi wake mbalimbali kulingana na maelekezo juu ya watu wa Mungu!

  Katika Kongamano hili la PENUEL 2016 litajumuisha wanenaji kutoka nje ya Tanzania na ndani ikiwemo Arusha,Afrika Kusini,Mbeya, DRC, Kenya, Cameroon n.k

  Mwenyeji wa PENUEL 2016 Apostle Onesmo Ndegi na Lilian Ndegi. Pia wanenaji wengine kutoka Tanzania ni Askofu Emmanuel Tumwidike kutoka Mbeya na Bishop Olam Mustapha kutoka Arusha. Kutoka Kenya ni Bishop Tengu Yoka na kutoka Africa Kusini ni Dr.Apostle Peter Muteba pia kutoka Cameroon tunaye Bishop Angela Acha-Morfaw na Apostle Israel Abam kutoka Nigeria.

  Mahali ni Living Water Centre Kawe, Dar es salaam, Tanzania Uzinduzi wa Kongamano ilikuwa ni leo siku ya Jumanne kuanzia saa 8:00 mchana,siku zinazofuata ni kuanzia saa 3:00 asubuhi mpaka saa 12 Jioni.Karibu Ukutane na Mungu kupitia Neno kupitia watumishi wake! Barikiwa!

  Theme: Transformation Romans 12:2


   Source:gospelhabari.blogspot.com

  0 0

  Na Daudi Manongi,MAELEZO

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk Joseph Pombe Magufuli amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) watafungua ofisi nchini Rwanda ili kuraisisha uhakiki wa bidhaa kwa wafanyabiashara wa Rwanda wanaoingia nchini.

  Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa Rwanda Mhe.Paul Kagame anafanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania ikiwemo ufunguzi wa Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

  Aidha amesema kuwa Serikali imetoa eneo la bandari kavu (ICD) kwa ajili ya kuhifadhia Bidhaa kutoka nchi ya Rwanda ili kupunguza urasimu ambao umekuwa kikwazo kwa maendeleo ya biashara hapa nchini na kwa namna hiyo biashara itakua kwani tunategemea uchumi utapanda kutoka asilimia 7 ya sasa mpaka asilimia 7.2.

  Pia amesema kuwa Serikali imepunguza vituo vya ukaguzi barabarani kutoka Tanzania kwenda Rwanda kufikia vitatu na kwa kufanya hivyo itarahisisha safari za magari ya biashara njiani na hivyo kufikisha bidhaa kwa haraka.

  Aidha amesema kuwa serikali iko mbioni kuanzisha kituo kimoja cha kukusanya mapato badala ya kila sehemu kuwa na mfumo wake ambao unapoteza mapato mengi kwa kuwa mifumo hiyo haina uthibiti mmoja na hivyo serikali ya Rwanda itasaidia kwa kuleta wataalamu wa Tehama ambao watasaidia kutoa mafunzo ili kusaidia mapato yetu kuwa katika udhibiti mmoja.

  Kwa upande Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza Uchumi wa nchi izi mbili kwani zina historia ndefu na kwa kuendelea kufanya biashara pamoja nchi izi mbili zimejenga taswira mpya katika mahusiano.

  Awali Mawaziri wa mambo ya Nje wa nchi za Tanzania na Rwanda walitia saini Muhtasari wa Tume ya Ushirikiano wa pamoja baina ya nchi izi mbili.

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haruna Ali Suleiman wakati alipotembelea Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani,Vuga Mjini Unguja ambao unatarajiwa kufanyika kwa Baraza la Eid el Fitri linalofanyika kila mwaka baada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haruna Ali Suleiman (kushoto) na Katibu Mkuu Ofisi ya makamo wa Pili wa Rais Joseph Abdalla Meza(kulia) wakati alipotembelea Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani,Vuga Mjini Unguja ambao unatarajiwa kufanyika kwa Baraza la Eid el Fitri linalofanyika kila mwaka baada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.]

  0 0

  Zoezi la uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili wa Vyama va Siasa kwa upande wa Tanzania Bara linaendelea .Tayari vyama 18 vimekwishakuhakikiwa. Vyama vinne vinatarajiwa kuhakikiwa Julai 4. Zoezi hili ni zoezi la kawaida na endelevu ambalo hufanyika kila mwaka ili kupima endapo vyama vya siasa vinakidhi matakwa ya Sheria ya usajili wa vyama vya Siasa.

  Uhakiki wa Vyama vya siasa ni zoezi muhimu sana kwa sababu ni zoezi ambalo hugusa uhai wa kila chama cha siasa. Kwa upande wa Tanzania Visiwani , uhakiki unatarajiwa kuanza mara baada ya kumalizika Bara kwa tarehe ambazo zitatangazwa baadaye.
  Esther B.Mwanri, Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa akikagua katiba ya Chama cha Wananchi (CUF) wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni Malapa Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Bw. Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa uchumi na Mipango.(Picha zote na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa)
  Msajili Msaidizi wa Vyama Siasa “Gharama za uchaguzi na Elimu kwa Umma “Bi. Piencia Kiurea akimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha United Democratic Party (UDP) Bw. Godluck Ole-Medeye wakati akitoa taarifa muhimu za chama chake katika zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Kisiasa unaoendelea Jijini Dar es Salaam.
  Msajili Msaidizi wa Vyama Siasa “Gharama za uchaguzi na Elimu kwa Umma “Bi. Piencia Kiurea akikagua baadhi ya taarifa za Chama cha Mapinduzi “CCM” jana wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa uliofanyika katika Ofisi ndogo za chama hicho Jijini Dar es salaam
  Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Usajili wa vyama vya Siasa , Bw. Sisty Nyahoza (kushoto) akihakiki daftari lenye orodha ya wanachama wa Chama cha NRA ( National Reconstruction Alliance) wakati wa zoezi la kuhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa Jana Jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party (DP) Bi. Georgia Mtikila (kushoto) akitoa taarifa za chama chake kwa Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini (kulia), Bi. Jacqueline Kilama wakati wa zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam Juni 28 mwaka huu.

  Mhasibu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw.Willium Brown Nyamtiga akisisitiza jambo kwa viongozi wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Jana wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo Jijini Buguruni Dar es salaam .
  Bw.Eugene Kabendera, Katibu Mwenezi Taifa wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) akitoa taarifa wa watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo Jijini Makumbusho Dar es salaam leo
  Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Jahazi Asilia, Bw. Mbwana S. Kibanda akifafanua jambo wakati wa zoezi la uhakiki liliofanyika Leo katika ofisi za chama hicho zilizopo ilala Jijini Dar es salaam . Kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho na kushoto ni watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
   

  0 0


  Mkurugenzi Mkaazi wa Kampuni ya Resolution Insurance Ltd Oscar Osir akipata iftar pamoja na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam Sheikh Alhadi Musa Bin Salum katika iftar kwa ajili ya wateja na wafanyakazi wake iliyoandaliwa na kampuni ya Resolution Insurance LTD jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkaazi wa Kampuni ya Resolution Insurance Ltd Oscar Osir akiongea na wadau mbalimbali(hawapo pichani) kwa ajili ya kuwashukura kwa kuja katika iftar iliyoandaliwa na kampuni ya Resolution Insurance LTD jijini Dar es Salaam.
  Mgeni Rasmi Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam Sheikh Alhadi Musa Bin Salum akiongea na wadau mbalimbali(hawapo pichani) kwa ajili ya kuwakumbusha mambo mema katika mwezi mtukufu wa Ramadhan katika iftar iliyoandaliwa na kampuni ya Resolution Insurance LTD jijini Dar es Salaam.

  Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam Sheikh Alhadi Musa Bin Salum
  Wafanyakizi wa Resolution Insurance

  Wateja wa kampuni ya Resolution Insurance wakipata iftar

  Wadau mbali mbali wakipata iftar
  Wadau mbali mbali wakipata iftar

  Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam Sheikh Alhadi Musa Bin Salum akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkaazi wa Kampuni ya Resolution Insurance Ltd na Mwenyeketi wa Bodi ya Wakurugenzi Bi.Zuhura Muro

  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


  Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na mkewe Jeannette Kagame wakipokea zawadi ya maua mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakifurahia vikundi vya ngoma za asili vilivyokuwa vikiburudisha mara baada ya Rais wa Rwanda kuwasili.

  Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Rwanda Paul Kagame akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JNIA.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo rasmi na Rais wa Rwanda Paul Kagame pamoja na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Rwanda Paul Kagame akizungumza na Wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais Dkt. Magufuli.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais wa Rwanda Paul Kagame.PICHA KWA HISANI YA IKULU NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

  0 0  Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, (Kushoto) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya kilimo mifugo na Uvuvi anayeshuhulikia Mifugo Dkt. Maria Mashingo, kabla ya kukabidhi Ng’ombe bora 42 wa maziwa kwa wafugaji wadogo wa Kibaha Picha ya Ndege na Kibaha Mkuza Mkoa wa Pwani, Ng’ombe hao wamenunuliwa kwa Mkopo kutoka Covenant Bank wana uwezo wa kutoa Maziwa zaidi ya rita 25 kwa siku.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank, Balozi, Salome Sijaona, akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya kilimo mifugo na Uvuvi anayeshuhulikia Mifugo Dkt. Maria Mashingo,( Katikati) kabla ya kukabidhi Ng’ombe bora 42 wa maziwa kwa wafugaji wadogo wa Kibaha Picha ya Ndege na Kibaha Mkuza Mkoa wa Pwani, Ng’ombe hao wamenunuliwa kwa Mkopo kutoka Covenant Bank wana uwezo wa kutoa Maziwa zaidi ya rita 25 kwa siku.Pamoja nao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank Sabetha Mwambenja.

  Katibu Mkuu Wizara ya kilimo mifugo na Uvuvi anayeshuhulikia Mifugo Dkt. Maria Mashingo (Katikati) akikagua moja ya kati ya Ngombe 42 wa Maziwa waliotolewa kwa wafugaji wa wadogo wa Kibaha Picha ya Ndege na Kibaha Mkuza Mkoa wa Pwani, Ng’ombe hao wamenunuliwa kwa Mkopo kutoka Covenant Bank wana uwezo wa kutoa Maziwa zaidi ya rita 25 kwa siku. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank Sabetha Mwambenja (kulia). Na Mwenyekiti wa Kikundi cha Wafugaji Picha ya Ndege Anna Rose Ndashau.
  Katibu Mkuu Wizara ya kilimo mifugo na Uvuvi anayeshuhulikia Mifugo Dkt. Maria Mashingo, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, (Katikati) wakimhudumia moja ya kati ya Ngombe 42 wa Maziwa waliotolewa kwa wafugaji wa wadogo wa Kibaha Picha ya Ndege na Kibaha Mkuza Mkoa wa Pwani, Ng’ombe hao wamenunuliwa kwa Mkopo kutoka Covenant Bank wana uwezo wa kutoa Maziwa zaidi ya rita 25 kwa siku. Pamoja nao katika Picha ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Wafugaji Picha ya Ndege Anna Rose Ndashau.


  · Ni katika kuboresha uzalishaji wa Maziwa na kipato kwa Wafugaji

  PWANI, Kibaha Katibu Mkuu wa Mifugo, Katika wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, anayeshuhulikia Mifugo, Dkt. Maria Mashingo, amekabidhi Ng’ombe bora wa maziwa arobaini na mbili ( 42) kwa vikundi vya Wafugaji wadogo walioko kibaha picha ya ndege na kibaha Mkuza, mkoa wa Pwani.

  Ng’ombe hao ambao wametolewa kwa mkopo kutoka Covenant Bank wana uwezo wa kuzalisha maziwa zaidi ya Lita 25 kwa siku. Akizungumza na wakazi wa eneo hilo kwa niaba ya Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mama Mashingo, amebainisha kuwa mikopo ya aina hiyo italeta mapinduzi makubwa katika sekta ya mifugo, katika wakati ambao nchi inaelekea katika mapinduzi ya viwanda.

  “Sasa nchi yetu inaelekea katika mapinduzi makubwa ya Viwanda hivyo tukiweza kuzalisha Maziwa kwa wingi tutaweza kuhudumia viwanda vyetu vya ndani ikiwa ni pamoja na kuepukana na kuagiza Maziwa kutoka nje ya nchi, na hili litawezekana endapo tu taasisi za fedha kama Covenant Bank, zitajitokeza kuwawezesha wafugaji wadogo”

  “Kitendo cha kukabidhiwa Ng’ombe kwa vikundi vya wafugaji wadogo wa Kibaha ni hatua kubwa sana katika kuleta maendeleo na mapinduzi makubwa katika sekta ya mifugo. Mikopo ya aina hii imekuwa ikitolewa kwa ranchi za Taifa lakini haikuwahi kutolewa kwa wafugaji wadogo wadogo” alisema Dkt. Mashingo na kuongeza kuwa,.

  “Hatua hii ni ya kupongezwa sana hasa kutokana na Uhitaji mkubwa wa Maziwa uliopo nchini kwa sasa, ambapo kama nchi tunatakiwa kuzalisha lita bilioni 9 za maziwa kwa siku ili kuwatosheleza watu wetu lakini kwa sasa tuna uwezo wa kuzalisha lita bilioni mbili tu. Hivyo ninaomba Covenant benki kwa kushirikiana na wadau wengine waendelee kutoa mikopo hii kwa vikundi vingine ili kuongeza uzalishaji”. Alisema.

  Aidha, Dkt. Mashingo aliwataka wana kikundi hao kuhakikisha wanawatunza vizuri ng’ombe hao ili kujipatia kipato na kurudisha mikopo hiyo kwa wakati, kuwezesha vikundi vingine kukopa kupitia marejesho hayo.

  Awali, Akitoa maelezo yake kwa Katibu Mkuu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Covenant Bank, Balozi, Salome Sijaona alisema kuwa Mradi huu wa kuwawezesha Wafugaji wadogo wadogo, utaendelea katika maeneo mengine ya nchi hasa vijijini ili kuwawezesha Wafugaji kupata tija katika ufugaji, unaoenda sambamba na kuunganishwa na masoko ya Maziwa moja kwa moja.

  “Mpango huu, utaendelea katika maeneo mengine, kama Songea, Tanga, Mwanza, Iringa, Mbeya na maeneo mengine katika kanda ya SAGCOT. Covenant Bank hatuishii tu kutoa mikopo, pia tunawaunganisha wafugaji na masoko ya uhakika ya mazao yatokanayo na Ng’ombe hawa”.

  Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bibi Sabetha Mwambenja alisema ng’ombe hao 42 wamekatiwa bima hivyo endapo watakufa au kupatwa na tatizo lolote kampuni ya bima itachukua jukumu la kumlipia ng’ombe mwingine mfugaji aliyeathirika. Pia kila mfugaji aliyepata mkopo amekatiwa Bima ya Matibabu ya AAR kwa ajili yake na familia yake.

  “Licha ya kutoa mikopo ya ng’ombe kwa hawa wakulima, Covenant Bank, tumekwenda mbali zaidi kwa kuwawezesha Wafugaji hawa kupata mafunzo ya ufugaji wa kisasa wa Ng’ombe wa Maziwa kupitia kwa wataalam wa bodi ya maziwa na tayari mabanda yamekaguliwa na kujiridhisha kuwa sasa watakuwa mahali salama’’, Alisema.

  Akitoa Shukurani zake kwa Katibu Mkuu na Covenant Bank, Mwakilishi wa Compassion International, Audax Kisato, aliishukuru Covenant Benki huku akitoa wito kwa Serikali kuboresha miundombinu kwa wafugaji wadogo kwa kuwapatia wataalam wa kutosha na kuwasisitizia Wafugaji hao waliopata mikopo kuwa waaminifu kwa kuhakikisha wanarejesha mikopo hiyo,katika muda waliyopangiwa.

  0 0


  TIMU 20 kutoka ndani ya nchi na Nje ya nchi Tatu zilizothibitisha kushiriki mashindano ya Rolling stone zimeanza kuwasili mkoani Arusha kwa ajili ya mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, Iilboru sekondari na Arusha Meru.

  Mikoa hiyo ni Simiyu, Mara, Singida, Dodoma, Lindi, Pwani, tanga, Kigoma, Geita, Mwanza, Manyara, Kilimanjaro, Iringa, Dar es Salaam na Arusha ikiwa ni wenyeji na nchi za nje ni Burundi, Kenya Congo na Zanzibar kama nchi.

  Akizungumza mjini hapa Mwenyekiti wa Rolling stone Ally Mtumwa alisema maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika na wageni kutoka mikoa mbalimbali wameanza kuwasili. Alisema mpaka sasa kuna mikoa imeanza kuwasili kwa ajili ya mashindano hayo ingawa idadi tuliyoitarajia kwenye mashindano hayo imekuwa pungufu tofauti na mialiko tuliyoitoa.

  “ Tulialika mikoa yote ya Tanzania na nchi zote za Afrika masharika lakini nchi zilizotoa majibu kwa njia ya barua ni hizo tatu tu huku zilizotoa majibu kwa njia simu ni nying lakini hatuna uhakika nazo kwani mpaka leo hii ambapo timu nyingine zimeanza kuwasili lakini nchi hizo hazijathibitisha kwa maandisha” alisema Mtumwa.

  Mtumwa alisema wametoa nembo itakayowakilisha mashindano hayo ya Rollingstone kuwa ni Tembo kwani mnyama huyo ni wa bahati ambae kwa sasa serikali inapinga ujangili wa mnyama huyo.

  “Tumemtumia mnyama tembo kwasababu kwenye mashindano haya tunataka kutoa elimu ya kupinga ujangili unaoendelea nchini na kwa nchi jirani hivyo kupitia mashindano haya najua elimu itafika kwa wakati”alisema Mtumwa.

  habari picha na woinde shizza globu ya jamii Arusha

  0 0


  Mkuu mpya wa wilaya ya Arusha Mrisho Gambo akiongea na wadau mbalimbali waliouthuria katika sherehe za kuapishwa kwa wakuu wa wilaya wapya wa wilaya tano zilizopo mkoa ndani ya mkoa wa Arusha ,ambapo mkuu huyu wa wilaya aliwataka wadau mbalimbali pamoja na wananchi kumpa ushirikiano katika kufanya kazi ,huku akisisitiza kuwa swala ya siasa pamoja na mambo ya kisiasa yameisha sasa ivi ni muda wa kufanya kazi tu9(habari picha na Woinde Shizza,Arusha ).
  Wakuu wa wilaya za mkoa wa Arusha walioapishwa leo wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Felexs Ntebenda pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Adolfu Mapunda nje ya jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa
  Mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Geofrey Chongolo akikaribishwa rasmi na mmoja wa kiongozi wa chama cha mapinduzi wilayani humo ,kwa kupewa shuka la kimasai hii ikionyesha ishara ya kuwa wilaya yake ina wananchi wengi wa kabila la kimasai na kiarusha ambao ni wafugaji


  Aliekuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru Wilson Nkambaku. akiwa akiwa anaongea na wananchi wa mkoa wa arusha pamoja na baadhi ya viongozi wakati wa sherehe za kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya ambao wameteuliwa na rais Magufuli,ambapo mkuu huyu wa wilaya aliwaomba wananchi pamoja na wafanyakazi wa serekali kuwapa ushirikiano wa kutosha viongozi walioteuliwa huku akimshukuru rais magufuli kwa kumpa ushirikiano katika kipindi cha miezi nane aliyefanya nae kazi huku akimuaidi kuendelea kutoa ushirikiano katika serekali yake pamoja na chama kwa ujumla
  Baadhi ya wananchi waliouthuria sherehe izo za kuapishwa wakuu wapya wa wilaya


  mkuu wa wilaya ya Monduli nne Idd Hassan Kimanta kushoto kulia kwake ni mkuu wa mkoa wa Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya monduli mara baada ya kuapishwa

  wa tatu kushoto ni mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Geofrey Chongolo akiwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Felexs Ntebenda pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Adolfu Mapunda katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya ya longido

  mkuu wa wilaya ya Arusha Mrigo gambo wa kwanza kushoto akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexander Pastory Mnyeti wa pili ,watatu ni mkuu wa wilaya ya ngorongoro Rashid Mfaume Taka watatu kutoka kushoto akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya longido Daniel Geofrey Chongolo,wa kwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Karatu Therezia Jonathan Mahongo


  huku wa pili akiwa ni mkuu wa wilaya ya monduli Idd Hassan Kimanta mara wakiwa wameketi wakisiliza hutuba ya mkuu wa mkoa wa Arusha (hayupo pichani )mara baada ya kuapishwa rasmi hii leo
  baadhi ya wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara ,viongozi wa dini na wananchi waliouthuthiria katika sherehe za kuapishwa wakuu wa wilaya wapya wa mkoa wa Arusha
  mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexander Pastory Mnyeti akiwa anakula kiapo cha utiii mbele ya mkuu wa mkoa wa Arusha hii leo

  0 0

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipokea mfano wa hundi ya sh.miliioni 250, kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas Rubaratuka .Fedha hizo ni kwaajili ya mchango wa madawati, Dar es Salaa, jana. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu TPA, Mhandisi Deusdetit Kakoko. (Picha na Christopher Lissa).
   
  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  MAMLAKA ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa
  Sh milioni 250 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwaajili
  ya kuchangia kampeni ya madawati Mkoa wa Dar es Salaam ili kuondokana na tatizo la kukaa chini wanafunzi.

  Licha ya kukabidhi msaada huo mamlaka hiyo pia imechangia kiasi cha Sh
  milioni 165 katika Halmashauri 11 nchini zenye uhaba wa madawati ambazo walizianisha katika uhitaji wa msaada huo.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi (TPA) Profesa Ignas Rubaratuka alisema, msaad huo ni kutekeleza jukumu katika kuunga mkono kampeni ya Rais katika kuhakikisha wanatatua tatizo la ukosefu wa madawati katika Wilaya za
  Mkoa huo ili watoto wa kitanzanbia wwasome katika mazingira bora.

  “Pamoja na shughuli zake za kupakua na kupatia mizigo pia mamlaka imekuwa mstari wa mbele kuchangia masuala ya kijamii kupitia sera yake  ya msaada kwa jamii (CSR) ambapo inashiriki kikamilifu kurudisha  faida yake kwa jamii,” alisema. Akizungumza baada ya kupokea hundi hiyo Makonda ameishukuru mamlaka hiyo  kwa kuona umuhimu wa kuchangia sekta ya elimu ambayo imekuwa ikukabiliwa na changamoto kubwa hasa ya uhaba wa madawati.

  Amesema msaada uliotolewa na TPA utasaidia kupunguza uhaba wa madawati zaidi ya laki nane unaolikumba jiji la Dar es Salaam ambao utasaidia kupunguza adha wanayoipata wanafunzi. “Tunachangamoto kubwa ya madawati na tumeambiwa mpaka ifikapo juzi tuwe tumekamilisha kampeni ya madawati najua Mkoa wangu ni miongoni mwa mikoa yenye uhaba mkubwa lakini ninyi bado mmenipa nguvu ya kuamini tutafanikiwa na kibarua changu kitaendelea kuwa salaama,” alisema Makonda.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu TPA Deusdedit Kakoko alisema wameamua kutoa msaada lengo ni kurudisha kiasi kwa jamii na msaada uliotolewa umetolewa kwa makubaliano yao pamoja na wafanyakazi wa TPA ili kuondoa uhaba wa madawati katika Mkoa wa Dar es Salaam na Mikoa mingine . “Kampeni ya madawati mnayoifanya tunaiona na ndio maana tumeamua kutoa msaada huu kama mchango wa kampeni fedha zote tayati tumeshaweka katika akaunti za Mkoa naamini zitakwenda kufanya yale yaliyokusudiwa,” amesema

  0 0

  Na Lydia Churi, Mahakama ya Tanzania

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman amewakubali na kuwaapisha Mawakili wapya 624 na kuifanya Tanzania kuwa na jumla ya Mawakili 5800.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa sherehe za kuwaapisha Mawakili leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Jaji Mkuu wa Tanzania alisema mawakili walioapishwa wanatoka katika maeneo mbalimbali ikiwemo Serikalini, sekta binafsi, mashirika ya Umma na halmashari mbalimbali nchini.

  Alisema hivi idadi ya Mawakili inaendelea kuongezeka ambapo mwezi Desemba mwaka huu Mahakama inatarajia kuwaapisha mawakili wengine zaidi ya 300. Aliongeza kuwa kwa upande wa Afrika Mashariki, Kenya inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya mawakili ambapo ina zaidi ya Mawakili 14,000. Uganda kwa upande wake inayo mawakili 2500.

  Aidha, Jaji Mkuu aliwataka mawakili walioapishwa leo kutekeleza wajibu wao katika maeneo matatu ambayo ni kuwajibika kwa wateja wao kwa kuhakikisha wanatoa huduma kwa viwango vya kuridhisha.

  Aliyataja maeneo mengine mawakili hao wanayopaswa kutekeleza wajibu wao kwa ni kwa mahakama ya Tanzania pamoja na kuwajibika kwa taaluma yao kwa kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma hiyo.

  Akizungumzia hatua ya mawakili wengi kufanya kazi zao maeneo ya mijini zaidi kuliko maeneo mengine, Jaji Mkuu alisema hatua hiyo inatokana na sababu za kiuchumi zaidi ingawa baadhi ya mawakili walioapishwa leo wanatarajia kwenda kufanya kazi ya kutoa msaada wa kisheria katika mikoa mbalimbali nchini na wengine ni wale walioajiriwa na halmashari mbalimbali nchini.

  Sherehe za kuwakubali na kuwaapisha Mawakili leo zimefanyika kwa mara ya 54 tangu kuanzishwa kwa sherehe hizo mwaka 1986 hapa nchini.

  0 0


  Kamishina Mkuu wa Mamalaka ya Mapato Nchini (TRA ), Alphayo Kidata akizungumza na waandishi habari juu zuio la taasisi za fedha na kampuni za simu kukata miamala ya kodi ya ongezeko la thamani VAT leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kamishina wa Mapato ya Ndani wa TRA, Elijah Mwandumbya .

  Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishina Mkuu wa Mamalaka ya Mapato Nchini (TRA ), Alphayo Kidata leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  SERIKALI imezuia taasisi za fedha (Benki) pamoja na kampuni za simu za mikononi kutoza ongezeko la thamani (VAT )kwa walaji (wananchi).

  Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Alphayo Kidatta amesema kuwa fedha ambayo walikuwa wanakata haina ongezeko la thamani hivyo taasisi za fedha (Benki) kampuni za simu zimetakiwa zisiongeze miamala kwa wateja kwa kizingizio cha ongezeko la thamani.

  Amesema kuwa fedha iliyokuwa ikikatwa imekuwa haikatwi hivyo kwa sheria hiyo inataka miamala hiyo iliyokuwa ikikatwa ikatwe asilimia 18 ya thamani ya ongezeko.

  Aidha amesema TRA haijaweka muongozo wa juu ongezeko hilo kwa taasisi za fedha na kampuni za simu, hivyo kwa watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua.

  Kidata amesema kuwa wananchi wametakiwa wasiguswe kabisa katika ongezeko hilo kutokana na kutohusika na kufanya hivyo ni makosa.

  0 0


  Rais wa Rwanda Paul Kagame, (wapili kulia) akiwa na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli, (wakwanza kulia), akimkabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na makampuni ya Bima, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 1, 2016. Wapili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.

  Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele (wakwanza kulia) akiungana na wafanyakazi enzake kusherehekea tuzo ambayo Mfuko umepata wakati wa uzinduzi wa maonyesho hayo ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

  Afisa wa PPF anayeshughulikia huduma kwa Wanachama Mohammed Siaga,akionyesha tuzo hiyo.

  Wafanyakazi wa PPF wakishangilia ushindi huo mbele ya banda lao

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu ala kiapo cha kuitumikia Wilaya hiyo kwa uadilifu, ubunifu na utu kwa kila mwananchiMkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng Methew Mtigumwe akiwa na wakuu wa wilaya wapya wa mkoa huu baada ya kuapishwa.

  Na Matias Cana,Singida 

  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu ala kiapo cha kuitumikia Wilaya hiyo kwa uadilifu, ubunifu na utu kwa kila mwananchi, Kiapo hicho kimejidhihirisha mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng Methew Mtigumwe. Muda mchache baada ya kiapo hicho mkuu huyo ameshiriki hafla fupi ya kukaribishwa na Chama Cha Mapinduzi katika ofisi za Chama hicho katikati ya mji wa Singida.

  Mtaturu amesema kuwa ana dhamira ya dhati kuhakikisha wananchi wanapata maendelea shirikishwa hususani katika kuimarisha sekta ya elimu, afya, miundombinu na kukemea Rushwa ambayo inarudisha nyuma Taifa.

  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa Mtaturu amesema kuwa ushirikiano baina ya serikali na wananchi wa Ikungi itakuwa turufu kubwa katika kuhakikisha wilaya inakomaa zaidi kimaendeleo.

  "Naenda kusaidiana nao ili kuhakikisha wilaya ina komaa zaidi kimaendeleo na watu wake kuondokana na uduni wa kipato walionao wananchi, wananchi wana uwezo wa kufuga na kulima vizuri jambo ambalo linaashiria kuwaondoa wananchi kwenye wimbi la umasikini".

  Amesema Mtaturu Kuhusu wananchi wa Ikungi kukataa kuchangia shughuli za maendeleo kufuatia pingamizi lilichagizwa na mbunge wa jimbo hilo Mtaturu amesema kuwa Utaratibu wa kuchangia maendeleo upo katika dunia nzima nchi mbalimbali za ulaya na kwingineko zimekuwa zikichangia shughuli za maendeleo nchini Tanzania kwa ajili ya wananchi masikini lakini wananchi tunaosaididiwa kuondokana na wimbi hilo tunapaswa pia kuchangia shughuli za maendeleo.

  Amesema wananchi wa Ikungi hawapaswi kutumika kisiasa huu ni muda wa kufanya kazi ili tusikubali maendeleo yetu kurudishwa nyuma na wanasiasa au watu wachache wenye mtazamo wa kisiasa zaidi kuliko maendeleo.

  "Huko nyuma kulikuwa na watu wanajitolea kufanya shughuli za mikono kwa kuchangia mawe, tofali au mchanga hivyo mchango huo ulikuwa muhimu zaidi japo asilimia kubwa ya watanzania wanadhani mchango ni pesa pekee"

  Ameongeza Mtaturu Katika halfa hiyo pia Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng Methew Mtigumwe amemuapisha mkuu wa Wilaya ya Mkalama Bw Jackson Jonas Masaka, Mkuu wa Wilaya ya Singida Bw Elius Chollo John Tarimo, na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Bw Emmanuely Jumanne Luhahula.

  Aidha mkuu wa Wilaya ya Manyoni hakuapishwa kutokana na kuwa nje ya nchi kikazi tangu alipoteuliwa. Katika hotuba yake Mkuu wa Mkoa wa Singida amewataka wakuu wote wa Wilaya walioapishwa kuhakikisha wanasimamia vizuri katiba na sheriaza nchi sawia na kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015-2020.

  "Nawaomba mkasimamie uadiligu, uaminifu, kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha wanapinga rushwa kwa nguvu zote, lakini nataka niwakumbushe hadi kufikia jana tarehe 30 Hakuna Halmasahauri ambayo imefanikiwa kukusanya mapato na kufikia asilimia 80 hivyo nendeni mkahakikishe watu wanalipa kodi stahiki ili kukuza pato la kila wilaya na kunusuru Halmashauri zetu kufutwa"

  Amesema Mtigumwe Mkuu huyo Amewapongeza wadau mbalimbali katika Wilaya hiyo kwa kujitolea kuchangia madawati elfu arobaini mpaka sasa na kuubakisha mkoa huo ukiwa na upungufu wa madawati kati ya 1500 katika mkoa huo. Imetolewa na Ofisi ya muda ya Mkuu wa Wilaya (Ikungi) Julai 1, 2016

older | 1 | .... | 897 | 898 | (Page 899) | 900 | 901 | .... | 1898 | newer