Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA RAIS WA COMORO PAMOJA NA BALOZI WA JAPAN NCHINI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Rais wa Comoro Mhe.Azali Assouman walipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam ambapo Rais huyo wa Comoro alikuwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari ya kwenda Macca kwenye ibada ya Umrah nchini Saudi Arabia.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Comoro Mhe.Azali Assouman na ujumbe wake walipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam ambapo Rais huyo wa Comoro alikuwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari ya kwenda Macca kwenye ibada ya Umrah nchini Saudi Arabia.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Japan nchini Mhe. Yoshida Masaharu Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo Balozi wa Japan Nchini alisema nchi yake imeridhishwa na kasi ya Serikali ya Rais Mhe. Magufuli na kuahidi kuendelea kuisaidia Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Mhe. Yoshida Masaharu mara baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Comoro AzaliI Assouman amesema serikali yake itaendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Comoro katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya na biashara.

Rais huyo wa Comoro ametoa kauli hiyo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli akiwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari yake ya Mecca – Saudi Arabia kwa ajili ya ibada ya UMRAH.

Rais Azali Assouman pia amepongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tano zinazolenga kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma bora za kijamii na kusisitiza kuwa serikali yake itaendelea kujifunza kutoka Tanzania ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Komoro.

Akitoa ujumbe wa Rais JOHN MAGUFULI kwa Rais wa Comoro Azali assouman, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Rais wa Comoro kuwa Tanzania itadumisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo MBILI hasa kwenye sekta za elimu, afya na biashara kwa ajili ya manufaa ya nchi hizo MBILI.

Makamu wa Rais pia amemtakia Rais wa Comoro kheri katika safari yake ya Mecca– Saudi Arabia kwa ajili ya Ibada ya Umrah.

Wakati huo huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa JAPAN hapa nchini Masaharu Yoshida na kumweleza kuwa serikali itaendelea kuweka na kuboresha mazingira bora kwa ajili ya wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali Duniani ikiwemo wawekezaji kutoka nchini JAPAN.

Makamu wa Rais amesema serikali ya JAPAN imekuwa mshirika mkubwa wa maendeleo kwa Tanzania katika kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo Tanzania Bara na Visiwa hasa kwenye sekta ya elimu, afya na maji na kusema jambo hilo ni zuri na lakuigwa na washirika wengine wa maendeleo.

Kwa upande wake Balozi wa Japan hapa nchini MASAHARU YOSHINDA amemhakikishia Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN kuwa nchi yake itaendelea kufadhili ipasavyo miradi ya maendeleo hapa nchini ili kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma bora za kijamii.

Tatizo la mikopo kupatiwa ufumbuzi

$
0
0


Na: Immaculate Makilika- MAELEZO


SERIKALI kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeandaa mkakati ya kulipatia ufumbuzi tatizo la ukosefu wa mikopo linalowakabili wafanyabiashara wengi nchini ili kusaidia uanzishwaji wa viwanda.


Hayo yamesemwa na Afisa Biashara wa Wizara hiyo Bw. Baruti Mwaigaga wakati akizungumza katika Viwanja vya  Mwl Nyerere wakati wa maonesho ya Sabasaba yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam.


“Kufuatia kuwepo kwa tatizo kubwa la upatikanaji wa mikopo kwa watu wenye nia ya kuanzisha viwanda hapa nchini, Serikali imeandaa utaratibu maalumu wa kutoa taarifa zinazohusu upatikanaji wa mikopo ili kusaidia wananchi, kitu ambacho hakikuwepo awali” alisema Bw. Mwaigaga


Alisema lengo la mkakati huo ni kumrahisishia mwananchi mwenye nia ya kuanzisha kiwanda kupata taarifa sahihi ikiwa ni pamoja na utaratibu mzima wa kupata mkopo ambao unaondoa usumbufu kwa walengwa ikiwa ni utekelezaji wa nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.


Mikakati mingine ya Serikali katika kukuza sekta ya viwanda nchini ni pamoja na kuanzisha programu ya kuendeleza viwanda vidogo vidogo katika mikoa ya Ruvuma, Pwani, Iringa, Tanga na Manyara.


Naye, Afisa Uchumi kutoka Wizara hiyo Bw. Vicent Turuka alisema katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, Wizara inawaunganisha wafanyabiasha wadogo wadogo na wanunuzi wakuu na kuwapatia masoko ya mazao mfano zao la ufuta lina soko kwa kampuni ya Oramu pamoja na Murza Mills.


Aidha, wananchi wamesisitizwa kutembelea banda la Wizara ya Viwanda na Bishara  pamoja na taasisi zake za BRELA, TBS, TFDA , CBE na SIDO lililopo katika viwanja hivyo vya maonesho ili kupata taarifa mbalimbali kuhusu namna za kufanya biashara pamoja na kuanzisha viwanda nchini.

Wananchi mbalimbali wakiingia katika Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa kwa ajili ya kujipatia bidhaa mbalimbali.Maonyesho hayo yameanza leo hii Jijini Dar es salaam.Picha n Daudi Manongi,MAELEZO
Askari wa JKT pamoja na FFU wakihakikisha usalama wakati wananchi wakiingia katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kuangalia bidhaa mbalimbali baada ya maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa kuanza leo jijini Dar es salaam.
Afisa Habari Idara ya Habari,MAELEZO Bi.Immaculate Makilika akizungumza jambo na Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda ,Biashara na Uwekezaji Bw.Baruti Mwaigaga(kushoto) katika banda la Wizara hiyo viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Mwananchi akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na kikundi cha African Flowerless fashion cha Arusha kinachouza bidhaa zake nje ya nchi.Kulia ni Afisa wa kikundi hicho Bi.Suzana Mwalongo.
Mafundi wakiendelea na upakaji rangi katika banda la CRDB katika Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar e Salaam.  

TAARIFA YA UTEUZI wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)

$
0
0
index 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mosses Nnauye amemteua Dkt. Herbert F. Makoye kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).  

Uteuzi huu umefanywa chini ya Kifungu Na. 9 (1) cha Sheria ya Wakala wa Serikali (Executive Agencies Act) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009 ambacho kinampa Waziri mamlaka ya kufanya uteuzi huo.  Uteuzi huu utaanza tarehe 01/07/2016.

Dkt. Makoye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Juma Bakari aliyestaafu kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma. Dkt. Makoye mwenye Shahada ya Uzamivu (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha Ghana na Shahada ya Umahiri – Sanaa (M. A in Theatre Arts) toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Makoye alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Idara ya Sanaa na Maonesho.

Imetolewa na,
Genofeva Matemu,

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO.
28 Juni,2016

UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA POTOFU JUU YA UTAFITI WA VIASHIRIA NA MATOKEO YA UKIMWI TANZANIA WA MWAKA 2016

PROF. MAKAME MBARAWA ATOA MIEZI MITATU KWA BARABARA YA DODOMA-MAYAMAYA KUKAMILIKA

$
0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akifafanua jambo wakati akizungumza na Mkandarasi SINO HYDRO COMPANY LIMITED anayejenga barabara ya Dodoma-Mayamaya KM 43.6.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kulia), akitoa maelekezo kwa Mkandarasi SINO HYDRO COMPANY LIMITED anayejenga barabara ya Dodoma-Mayamaya KM 43.6, alipokagua maendeleo ya ujenzi huo

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ametoa miezi mitatu kwa Kampuni ya SINO HYDRO COMPANY LIMITED inayojenga Barabara ya Dodoma-Mayamaya kwa kiwango cha Lami kuhakikisha barabara hiyo inakamilika.

Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo yeye urefu wa kilomita 43.6 Prof. Mbarawa amemtaka mkandarasi kuikabidhi barabara kwa Serikali ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.

“Hakikisheni barabara hii ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya Great North Road inakamilika ili kuharakisha mkakati wa Serikali wa kukamilisha barabara hiyo eneo la Tanzania kwa kiwango cha lami, amesema Waziri Prof. Mbarawa.Barabara ya Dodoma-Mayamaya ni sehemu ya Barabara ya Dodoma-Kondoa-Babati yenye urefu wa Kilomita 247.8 ambayo ujenzi wake umegawanywa sehemu tatu ambazo ni Dodoma-Mayamaya KM 43.6, Mayamaya-Mela-Bonga KM 188.15.

‘Kukamilika kwa barabara hii ambayo ni sehemu ya Barabara Kuu ya Great North Road inayoanzia Capetown Afrika Kusini hadi Cairo nchini Misri kutachochea fursa za kibiashara na kiuchumi katika Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na nchi za Kaskazini mwa Afrika’, amesisitiza Prof. Mbarawa

Mpaka sasa takribani shilingi bilioni 43 zimeshalipwa kwa mkadarasi SINO HYDRO COMPANY LIMITED kukamilisha kilimilisha KM 8 zilizobaki katika sehemu ya Dodoma-Mayamaya, barabara ambayo ambayo imejengwa kwa viwango vinavyokubalika.

Barabara ya Great North Road inayopita mikoa ya Iringa, Dodoma na Arusha inaanzia Capetown Afrika Kusini hadi Cairo Misri mbapo kukamilika kwake kutaliunganisha Bara la Afrika kwa Barabara ya Lami.

TAARIFA KWA UMMA:UTEUZI WA BODI YA WADHAMINI WA SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII (NSSF)

$
0
0




JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU




 

UTEUZI WA BODI YA WADHAMINI WA SHIRIKA LA TAIFA LA                                         HIFADHI YA JAMII (NSSF).


Ofisi ya Waziri Mkuu inapenda kuutaarifu umma kwamba Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemteua     Prof. Samwel Mwita Wangwe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuanzia tarehe tarehe 30 Mei, 2016 kwa kipindi cha miaka mitatu.


Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake katika Sheria ya Msimamizi na Mdhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Na.5/2012. (The Social Security Laws (Amendements) Act.2012 jedwali la pili (Second Schedule) kifungu cha 2 (1).


Aidha, kwa mujibu wa Sheria hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista J. Mhagama (Mb.) amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini  wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

1.
Bw. Paul Daud Sangize
-
Mwakilishi wa Wafanyakazi
2.
Bw. Noel Nchimbi
-
Mwakilishi wa Wafanyakazi
3.
Bw. David Magese
-
Mwakilishi wa Waajiri
4.
Bibi Margreth Chacha
-
Mwakilishi wa Waajiri
5.
Bw. Justine Mwandu
-
Mwakilishi wa Sekta Binafsi
6.
Bw. Gabriel Pascal Malata
-
Mwakilishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
7.
Bw. Emmanuel Maduhu Subi
-
Mwakilishi wa Wizara ya Fedha na Mipango
8.
Bw. Ally Ahmed Msaki
-
Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)


Imetolewa na,



Eric F. Shitindi

KATIBU MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

DAR ES SALAAM

28/06/2016

WATEJA WA SIMBA CEMENT KUNUNUA KUNUNUA SARUJI KWA M PESA

$
0
0


Afisa Mkuu Biashara wa Vodacom Tanzania, Gregory Verbond (kulia) na Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart (kushoto) wakiwekea makubaliano ya mteja kunua saruji kwa M PESA bila tozo yoyote popote nchini.

Afisa Mkuu Biashara wa Vodacom Tanzania, Gregory Verbond (kulia) na Mkurugenzi kiwanda cha Saruji cha Simba Cement Tanga (TTCL), Reinhardt (kushoto) wakibadilishana nyaraka za makubaliano ya mteja kununua Saruji kwa M PESA bila tozo yoyote popote nchini.

KIWANDA Cha Saruji cha Simba Cement (TCCL) cha Tanga, kimeinmgia makubaliano na Kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom Tanzania Limited, kwa mteja kununua saruji kwa kutumia M PESA bila tozo yoyote.

Makubaliano hayo yaliyofanyika leo viwanja vya Hotel ya Tanga Beach na kushuhudiwa na viongozi wa pande zote mbili na kutajwa kuwa yatakuwa mkombozi kwa mwananchi wa kipato cha chini kwa kununua Saruji kwa simu badala ya kutumia Taasisi za pesa na kupanga foleni.

Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Mkuu Biashara wa Vodacom Tanzania, Gregory Verbond, alisema kampuni yake imechukua uamuzi huo wa makubaliano na kampuni ya Cement kwa lengo la kumsaidia mwananchi wa kipato cha chini.

Alisema mteja ataweza kununua Saruji (Simba Cement) kwa kutumia M PESA na hakutakuwa na tofati ya mnunuzi wa mifuko mingi na michache ambapo hatotozwa ada yoyote mnunuaji.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kiwanda cha Saruji, Simba Cement, Renhardt Swart, alisema makubaliano hayo ni moja ya sera za kiwanda kumsaidia mwananchi wa chini kuweza kukabiliana na changamoto za maisha.

Alisema Kiwanda cha Simba Cement daima kiko kwa ajili ya wananchi na faida inayopata inairejesha kwa wananchi na kuwataka kuitumia fursa hiyo ambayo iko na unafuu kwa ununuaji.

 

Afisa Mkuu Biashara wa Vodacom Tanzania, Gregory Verbond (kulia) akizungumza mara baada makubaliano na kiwanda cha Saruji cha Simba Cement kwa mteja kununua Saruji kwa M PESA bila tozo popote nchini.










































Mmoja wa wakala wa Simba Cement Tanga, Athuman Ali (kulia) alievaa kibagalashia akiwa mmoja wa watu waliohudhuria makubaliano ya utiaji saini wa Ununuaji wa Saruji kwa M PESA baina ya Kampuni ya Vodacom Tanzania na Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga leo.
William Mgazija wa ITV aliesimama nyuma na kushika MIC ni miongoni mwa wahudhuriaji wa makubaliano ya utilianaji wa saini wa manunuzi ya Saruji kwa M PESSA

Waandishi wa habari nao walikuwa miongoni mwa waalikwa wa ushuhudiaji wa utilianaji saini makubaliano ya ununuzi wa Saruji kwa M PESA. Kutoka kushoto alievaa Ushungi ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania , Betha Mwambellah wa TBC na Maryam Mwandishi wa Jambo leo
Habari kwa Hisani ya Tanga Kumekucha Blog

SEKTA YA MAWASILIANO KUPATA MWEKEZAJI ZAIDI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora akizungumza na ujumbe kutoka Kampuni ya Oracle Afrika (hawapo pichani) walipomtembelea ofisini kwake kwa nia ya ushirikiano katika kulinda miundombinu na mifumo ya TEHAMA. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Oracle Afrika Bw. Cherian Varghese (katikati) akielezea nia ya Kampuni yao katika ushirikiano wa kulinda miundombinu na mifumo ya TEHAMA hapa nchini. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Dkt. Mhandisi Maria Sasabo (wa kwanza kushoto) akizungumza na ujumbe kutoka Kampuni ya Oracle Afrika walipotembelea sekta ya Mawasiliano na kueleza nia yao ya ushirikiano katika kulinda miundombinu na mifumo ya TEHAMA.

…………………………………………………………………………….

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Prof. Faustin Kamuzora amekutana na ujumbe wa Kampuni ya Oracle Sysytem Limited ambayo imeonesha nia na utayari wa kuwekeza kwenye Sekta ya Mawasiliano Tanzania

Kampuni ya Oracle Sytem Limited kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano itakuwa na mkutano wa The Africa Security Summit utakaofanyika hoteli ya Kilimanjaro, Dar es Salaam tarehe 30 Juni, 2016.

Lengo la mkutano huo ni kuwakutanisha wadau na wataalamu mbalimbli wa Taasisi za Serikali na sekta binafsi wapatao 200 kutoka ndani na nje ya nchi iki kuona namna wanavyoweza kuwekeza hapa nchini.

Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oracle system Ltd wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, Afrika Bwana Cherian Varghese, wakati akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora alipokutana na ujumbe wa Kampuni hiyo kuzungumza nae kuhusu maandalizi ya mkutano huo na nia yao ya kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendeleza Sekta ya Mawasiliano

Bwana Varghese amesema kuwa mkutano huo utawawezesha wataalamu wa watanzania na kuwajengea uwezo na kuongeza uelewa wa usalama wa taarifa na umuhimu wake na namna ya kuzitumia ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Taifa la Tanzania. Pia Kampuni yake imetambua na kuona namna ambavyo Tanzania imewekeza na kuthamini Sekta ya Mawasilino kwa kuwa na miundombinu ya kisasa, Sera, sheria na kanuni zinazosimamia Sekta ya Mawasiliano na kutambua mchango wake katika kukuza uchumi.

Prof. Kamuzora aliwaahidi kuwa Wizara itawapatia ushirikiano wa kutosha ili Taifa liweze kunufaika kupitia utaalamu, ujuzi na weledi wa Kampuni ya Oracle ili kuendeleza Sekta ya Mawasiliano nchini

Kampuni hiyo tayari imewekeza na kushirikiana na nchi nyingine za Afrika ikiwemo Zambia, Zimbabwe, Afrika Kusini, Kenya na Uganda kuendeleza Sekta ya Mawasiliano katika maeneo ya usalama wa taarifa na kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa kutumia njia ya kielektroniki

LESOTHO YAKUBALI KUTEKELEZA MASHARTI YA SADC

$
0
0
WAZIRI MKUU wa Lesotho, Dk. Pakalitha Mosisili amekubali kutekeleza masharti yaliyowekwa na Wakuu wa Nchi na Serikali na Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Uchumi na Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC Double Troika Summit), na kuridhia timu ya uchunguzi kwenda nchini humo kufanya uchunguzi wa hali ya kiusalama na kisiasa.

Dk. Mosisili ametoa uamuzi huo leo (Jumanne, 28 Juni, 2016) wakati wa kikao maalum cha Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC Summit) na wakuu wa nchi wanaounda Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ on Politics, Defense and Security Cooperation) kilichofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (GICC), jijini Gaborone, Botswana.

Pia amekubali viongozi waupinzani na baadhi ya maofisa wa kijeshi wanaoishi uhamishoni ambao walikimbia machafuko yaliyotokea nchini humo warejee nchini mwao na kuahidi kwamba atahakikisha wanapatiwa ulinziwa kutosha. 

Januari mwaka huu, mkutano wa SADC Double Troika uliagizakwambaifikapo Februari Mosi, mwaka huuSerikali ya Lesotho iwe imetangaza matokeo ya Tume iliyoundwa kuchunguza matatizo ya kisiasa na kiusalama nchini humo hususan mazingira yaliyopelekea kifo cha marehemu Luteni Jenerali Maaparankoe Mahao ambaye alikuwa Mkuuwa Majeshi.

Kwaupande wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa akimwakilisha Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kikao hicho amesema wamepitia ripoti iliyoundwa na timu ya SADC iliyochunguza kuhusu matatizo ya Lethoto ambayo iliwahoji Viongozi wa Serikali, Jeshi, Bunge na familia ya marehemu Luteni Jenerali Mahao.

“Lengo la hatuahiiza SADC ni kuhakikisha inarejesha hali ya amani na utulivu kwenye maeneo ya siasa, ulinzi na usalama katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ili wananchi wake waweze kuishi vizuri,” amesema.

Pia Waziri Mkuu amesema Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa Wakuu wa Nchina Serikali na Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Uchumi na Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC Double Troika Summit), Agosti mwaka huu ambapo kitafanyika kikao kingine nchini Tanzania.

Mkutano huo wa ulifunguliwa na Rais wa Botswana, Mhe. Lt. Jen. Seretse Khama Ian Khama na ulihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa akimwakilisha Rais Dk. John Pombe Magufuli; Rais wa Afrika Kusini, Bw. Jacob Zuma; Rais wa Msumbiji, Bw. Filipe Jacinto Nyusi; Rais wa Zimbabwe, Bw. Robert Mugabe, Mfalme Muswati wa III wa Swazland.

SADC Double Troika ni kikao maalum kinachojumuisha Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC Summit) na wakuu wa nchi wanaounda Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ on Politics, Defense and Security Cooperation).

SADC Double Troika ni mkutano unaohusisha viongozi wakuu watatu wanaoongoza chombo cha ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama na wengine watatu kutoka kwenye Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa SADC. Hawa wanawakilisha mwenyekiti aliyepo madarakani, mwenyekiti aliyemaliza muda wake na mwenyekiti ajaye ambaye huwa ni makamu mwenyekiti.

Chini ya muundo wa SADC, kuna mambo makuu mawili; la kwanza likiwa ni utangamano wa kikanda ambao unasimamiwa na mkutano wa wakuu wa nchi (SADC Summit) na la pili ni la siasa, ulinzi na usalama ambalo linasimamiwa na chombo maalum (SADC Organ).

Wajumbe wa mkutano wa SADC Organ ni Msumbiji (Mwenyekiti); Afrika Kusini (Mwenyekiti aliyemaliza muda wake) na Tanzania inayotarajia kuchukua uenyekiti wa chombo hiki ifikapo Agosti, 2016. Botswana, Zimbabwe na Swaziland ndizo zinaunda SADC Summit.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, JUNI 28, 2016.

SABABU ZA KUNDI LA MUZIKI LA PAYUS & MECRAS KUTOKA JIJINI MWANZA KUBADILI JINA.

$
0
0
Wakali wa wimbo wa Chausiku, Payus na Mecras kutoka Jijini Mwanza, ambao awali walikuwa wanaunda kundi la Muziki la Payus & Pacras, wamebadili jina la kundi lao na sasa wanaitwa WAPANCRAS.

Sikiliza mahojiano ya wasanii hao ambapo msanii Mecras ameanza kwa kueleza sababu za kubadili jina la kundi lao kutoka Payus & Pacras hadi kuwa Wapancras huku msanii Mecras akiweka bayana chimbuko la jina hilo la Wapancras.

Bonyeza HAPA Kusikiliza au Bonyeza Play Hapo Chini




Msanii Payus

Msanii Mecras

Bonyeza Hapa Kujua Zaidi Au wacheck Wapancras 0742 182 836

PBZ Yaadhimisha Sherehe za Miaka 50 kwa Kusaidia Jamii na Kutembelea Hospitali ya Kidongochekundu.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ akizungumza na Maofisa wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar wakati wa kikabidhi msaada wa magodoro kwa ajili ya Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Mafunzo Kilimani Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akimkabidhi msaada wa magodoro 100 Kamishna Msaidizi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Omar Salum Mgaza. hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Mafunzo Kilimani Zanzibar.
Kamishna Msaidizi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Omar Salum Mgaza akitowa shukrani kwa PBZ  kwa msaada wao huo wa magodoro umeletwa wakati muafaka na kuwata taasisin nyengine kujitokeza kutoa misaada.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg.Juma Ameir akisalimiana na Muuguzi Dhamana wa Hospitali ya Kidongochekundu Zanzibar Ndg. Haji Vuai Hilal, wakati walipofika katika hospitali hiyo ya Mental kutowa misaada ya mashuka 200 kwa ajili ya hospitali hiyo. katikatika Afisa Masoko wa PBZ Ndg. Mohammed Nuhu. 
Afisa Masoko wa PBZ Ndg Mohammed Nuhu akisalimiana na Muuguzi Dhamana wa Hospitali ya Mental Kidongochekundu Zanzibar Haji Vuai Hilal. 
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Ameir akizungumza na Uongozi wa Hospital ya Mental Kidongochekundu Zanzibar wakati wa kutembelea hospitali hiyo na kutoa msaada wa mashuka 200 ikiwa ni kusherehekea miaka 50 ya PBZ Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya hospitali hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akikabodhi msaada wa mashuka kwa ajili ya hospitali ya Mental Kidogochekundu Zanzibar akipokea msaada huo Muuguzi Dhamani wa hospitali hiyo Ndg Haji Vuai Hilal. ikiwa ni kusherehekea miaka 50 ya PBZ kushaidia jamii Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akikabodhi msaada wa mashuka kwa ajili ya hospitali ya Mental Kidogochekundu Zanzibar akipokea msaada huo Muuguzi Dhamani wa hospitali hiyo Ndg Haji Vuai Hilal. ikiwa ni kusherehekea miaka 50 ya PBZ kushaidia jamii Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Ameir akimkabidhi mmoja wa mgonjwa katika hospitali hiyo Bi Amina Mwinyi msaada wa tende kwa ajili yao katika kipindi hichi cha mfungo wa mwezi wa ramadhani.
Mmmoja wa mgonjwa katika hospitali Bi Amina Mwinyi, hiyo akitowa shukrani kwa niaba ya wezake kwa uongozi wa PBZ kwa msaada wao huo kwao na kuuthamini na kuwataka na Wananchi wengi kujitokeza kuwasaidia kwa vitu mbalimbali. 
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Ameir akikabidhi msaada wa tenda mmoja wa wagonjwa wa hospitali hiyo Ndg. Mrisho Idrisa Hussein.
Muuguzi Dhamana wa Hospitali ya Mental Kidongochekundu Zanzibar Ndg Omar Vuai Hilal akitowa shukrani kwa Uongozi wa PBZ na Wafanyakazi wao kwa msaada wao huo katika hospitali hiyo.
Afisa wa PBZ Tawi la Mwanakwerekwe Zanzibar Ndg Jaha akitowa huduma za kibenki kwa Wateja wao katika tawi hilo PBZ inatimiza miaka 50 tangu kuazishwa kwake. 
Afisa Manunuzi wa PBZ  Bi Mwanaidi Ramadhani akitowa huduma za Kibenki kwa Wateja wa PBZ Tawi la Mwanakwerekwe Zanzibar, Maofisa wa PBZ wameungana na wafanyakazi wa Matawi la PBZ kutowa Huduma za Kibenki kuadhimisha miaka 50 ya PBZ tangu kuazishwa kwake.  
Meneja wa PBZ Tawi la Mwanakwerekwe Zanzibar akitowa huduma za Kibenki kwa Wateja wa PBZ ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea miaka 50 ya PBZ Zanzibar.
Meneja wa PBZ Tawi la Mwanakwerekwe Zanzibar akizungumza na waandishi wa habari wakati wa shamrashamra za kutimia miaka 50 ya PBZ Zanzibar.
Afisa manunuzi wa PBZ Bi Mwanaidi Ramadhani akitoa zawadi kwa Wateja wa PBZ Tawi la Mwanakwerekwe Zanzibar ikiwa ni kuadhimisha miaka 50 ya PBZ tangu kuazishwa kwake mwaka 1966-2016
Mteja wa PBZ akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma za PBZ ni nzuri na kuwataka kuziboresha zaidi katika kipindi kijacho kwa wateja wao na kuwataka kuongeza huduma na ATM na kuziboresha zaidi huduma hizo kuwafikia hadi wananchi wa vijiji kupata huduma hii ya ATM huko mashamba.


Wafanyakazi wa PBZ wakijumuika na Mkurugenzi Mtenda wa PBZ Ndg Juma Ameir katika kutoa huduma kwa wateja ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 50 ya PBZ tangu kuazishwa kwa benki hiyo wakiwa katika Tawi la Malindi Zanzibar. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Juma Ameir akitowa huduma kwa Wateja wa PBZ katika tawi la PBZ Malindi, Pbz imetimisha miaka 50 tangu kuazishwa kwa kwake Zanzibar. 
Wateja wa PBZ wakipita huduma za Kibenki katika Tawi la PBZ Malindi Zanzibar. 
Meneja wa Benki ya Watu wa Zanzibar Tawi la Malindi akitowa huduma kwa wateja wao akiwa na Afisi wa PBZ wakati wa shamrashamra za kusherehekea miaka 50 ya PBZ Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akitowa zawadi kwa Wateja wa PBZ ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea miaka 50 ya PBZ kuazisha kutowa huduma za Kibenki Zanzibar.
Wateja wa PBZ wakiwa katika Tawi la Malindi Zanzibar wakisubiri kupata huduma za Kibenki katika tawi hilo.  
Wateja wakipatya huduma katika Benki hiyo Tawi la Malindi Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ akitowa zawadi kwa wateja wa PBZ Tawi la Malindi Zanzibar.
Mteja wa PBZ Zanzibar akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma za Kibenki, wakati wa shamrashamra hizo za kusherehekea miaka 50 ya PBZ na kuwataka kuboresha zaidi huduma zao kwa wateja.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ akizungumza na waandishi wa habari malengo na changamoto za PBZ kwa wateja wake na malengo yao kutowa huduma kwa Wateja wao na kuboresha zaidi huduma zao.
Imetayarishwa na OthmanMapara. Zanzinews.com
email othmanmaulid@gmail.com

Airtel FURSA yatoa msaada kwa vituo vya yatima Dar

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso, akimkabidhi mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Irishad Islamic center Juma Kaseja ambaye pia golikipa wa timu ya Mbeya City msaada wa chakula na mahitaji mbalimbali kwa ajili ya mfungo wa Ramadhani . wakishuhudia ni baadhi ya viongozi na watoto kutoka katika vituo vya Irishad Islamic center katika wilaya ya Kinondoni na Huruma Islamic center katika wilaya ya Ilala.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso, pamoja na Meneja Mauzo wa Airtel Bwn James Moilo , wakiwakabidhi watoto kutoka katika vituo vya vituo vya Irishad Islamic center na Huruma Islamic center msaada wa chakula na mahitaji mbalimbali kwa ajili ya mfungo wa Ramadhani . wakishuhudia ni viongozi wa vituo hivyo akishuhudia ni Mkuu wa kituo cha Huruma Islamic center, Bi Hamisa Mwinyipembe.


Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso, pamoja na Meneja Mauzo wa Airtel Bwn James Moilo , wakiwakabidhi watoto kutoka katika vituo vya vituo vya Irishad Islamic center na Huruma Islamic center msaada wa chakula na mahitaji mbalimbali kwa ajili ya mfungo wa Ramadhani . wakishuhudia ni viongozi wa vituo hivyo

Mmoja ya mnufaika wa mradi wa Airtel Fursa anayejihusisha na ufugaji wa kuku wa asili, Bwana Mohamed Kigumi akimkabidhi mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Irishad Islamic center Juma Kaseja ambaye pia golikipa wa timu ya Mbeya City msaada wa chakula na mahitaji mbalimbali kwa ajili ya mfungo wa Ramadhani . wakishuhudia Mwalimu mkuu wa kitu cha Irishad Islamic center Sheikh Maulid Salimu Kidebe na Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde

Dar es salaam, Tanzania: wakati waislam nchini wakiwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kupitia huduma zake za kijamii kupitia Airtel FURSA wametoa msaada wa vyakula mbalimbali kwa vituo viwili vya yatima jijini Dar es Salaam.

Msaada huu wa futari kutoka Airtel ni mwendelezo wa huduma zakujitolea kwa kijamii za Airtel katika kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu wakati huu wa mfungo wa Ramadhan ambapo kwa mwaka huu msaada utafikia vituo 10 katika maeneo mbalimbali nchini. Leo Airtel Fursa imekabidhi msaada kwa kituo cha Irishad Islamic center katika wilaya ya Kinondoni na Huruma Islamic center katika wilaya ya Ilala.

Akiongea wakati wa halfa ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika ofisi za Airtel Makao Makuu, Mkurugenzi Mkuu wa Aritel , Sunil Colaso alisema “ Tunayo furaha kuweza kuwafikia zaidi ya watoto 500 ambao wamenuia kufunga wakati huu wa mfungo wa Ramadhani. dhamira yetu ni kuendelea kugusa maisha ya watoto hawa na kuwafanya wajisikia kuwa sehemu ya familia ya Airtel”.

Akiongea kwa niaba ya vituo vilivyopata msaada, Mkuu wa kituo cha Huruma Islamic center, Bi Hamisa Mwinyipembe Alisema “Tunashukuru sana kwa msaada huu mkubwa tuliopata kutoka Airtel na tunaamini mashirika mengine yatajitokeza kuwasaidia watoto hawa wanaoshi katika mazingira magumu kwa kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani na wakati wote”.

Mwaka huu Airtel imeshirikiana na vijana waliofaidika na mpango wa Airtel FURSA kusaidia vituo mbalimbali ambapo vijana hawa wametoa msaada wa vitu walivyovitengeneza katika biashara zao mara baada ya kuwezeshwa na Airtel

Mathayo Batholomeo Anatafuta Ndugu Zake

$
0
0
 Wafuatao ni ndugu zake ambao wanaweza kumtambua Mathayo Batholomeo ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Dada yake anaitwa Nasemba Matiku Weisiko. Anaishi Mojohe karibu na kwa mzee Wambura. Mama yao alizaliwa Same, mkoani Kilimanjaro. Mtoto wa dada yake anaitwa Mwita Ibarahimu ana duka eneo la Mtoni Kijichi darajani. Pia, amesema mtoto wa dada yake mwingine anaitwa Marwa Makire au Emanuel Makire anauza samaki katika eneo la Ubungo Gereji. Pia dada yake ni Elizabeth Rhoda, Dynaes Batholomeo.

Batholomeo anaishi Kariakoo Msimbazi, karibu na Kituo cha Polisi Msimbazi.

INTRODUCING Rama Dee- kipenda roho new video

Article 19


JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUTOA ELIMU YA KINGA DHIDI YA MOTO.

$
0
0

 Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,  Idd Chanyika (kulia) akitoa maelezo jinsi ya vifaa vya kinga na tahadhari vinavyotumika kwa Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi hilo, Michael Shija (kushoto), Kamishna wa Oparesheni, Rogatius Kipali (wapili kushoto) na Naibu Kamishna wa Utawala naFedha, Billy Mwakatage walipotembelea banda hilo Kituo cha Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.
 Koplo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Amani Hassan (kulia) akimuonyesha mwananchi aliyetembelea Banda la Maonyesho la jeshi hilo jinsi ya kutumia mtungi wa kuzimia moto wa awali, katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.
 Koplo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Amani Hassan (kulia) akimuandikia mmoja ya mwananchi namba ya dharura 114 ambayo hutumika kupokea taarifa ya majanga mbalimbali kutoka kwa jamii.
 Kamishna wa Oparesheni, Rogatius Kipali akisisitiza ufanyaji kazi kwa bidii, nidhamu, uadilifu na weledi kwa askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi waUumma inayofanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala, jijini Dar es Salaam.

NEWZZ ALERT:Mahakama Kuu jijini Arusha yamvua ubunge mbunge wa Longido Onesmo Ole Nangole (CHADEMA),yaamuru uchaguzi urudiwe upya

$
0
0

Aliyekwa Mbunge wa Jimbo la Longido,Mh.Onesmo Nangole

Kesi iliyokuwa ikiunguruma kuanzia  Februari 29 ,2016 katika Mahakam Kuu jijini Arusha imetolewa hukumu leo hii

Katika shauri hilo aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Longido Dkt Kiruswa  alifikisha mahakamni shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi dhidi ya mbunge wa Longido Mh.Onesmo Nangole.

Akisoma hukumu hiyo,Jaji Mwagesi  alisema kuwa mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa na Wakili msomi Dr.Masumbuko Lamwai na Wakili Haraka.Katika shauri hilo,dai la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikua ni:

1.Kutumika kwa lugha ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa mh Onesmo Nangole.
2.Kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mh Nangole

3.kutumika kwa magari ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura

4.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje.

5.Kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo

Kutokana na madai hayo na kwa kuzingatia kanuni,sheria na ushahidi uliotolewa pamoja na vielelezo na mashahidi wa pande zote mbili,Jaji kutoka mahakama kuu Bukoba Mh.Jaji Mwagesi alisema;"Kutokana na kuzingatia viini vyote vya shauri hili kama vilivyosikilizwa na kwa mujibu wa sheria,Natamka kwamba;

Mahakama hii imetengua shauri hili na kwa kujiridhisha kwamba mchakato mzima haukuwa wa haki na huru hivyo mahakama inaamuru uchaguzi urudiwe upya.

Mh. Herman Kapufi aipongeza Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika kuendeleza sekta ya elimu nchini.

$
0
0
 -Watendaji kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Wakifanya ukaguzi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa ukarabati wa miundo mbinu mbalimbali ikiwemo madarasa, vyoo, maabara, mabweni na mifumo ya umeme katika shule kongwe 11 katika mikoa ya Bukoba, Mwanza, Tabora, Singida, Same, Arusha, Dodoma, Morogoro na Pwani kwa kuzifanyia. 

 Na Hassan Silayo

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Same Mh. Herman Kapufi ameshukuru Jitihada zinazofanywa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika kutekeleza miradi inayosaidia kuongeza ubora wa elimu nchini ikiwemo utekelezaji wa mradi kukarabati shule kongwe nchini utakaoboresha mazingira ya kufundishia na kusaidia kuinua kiwango cha elimu katika shule hizo.

Mh. Kapufi amesema kuwa mpango huo umekuja wakati muafaka wakati uongozi wa wilaya hiyo ukipambana kutatua changamoto za elimu na kuwataka wadau kuipa ushirikiano Mamlaka hiyo.

“Kwa kweli napenda kuishukuru Mamlaka ya elimu Tanzania kwa jitihada zake hizi za kuboresha sekta ya elimu nchini, kwa kweli wamefanya kazi kubwa sana katika wilaya hii kwa kipindi chote nilichokuwa hapa kama mkuu wa wilaya, shule zetu kongwe zimechoka sana na zinahitaji ukarabati ili kuweza kuzirudisha katika hali yake ya kawaida kwa utekelezaji wa mpango huu” Alisema Mh.Kapufi.

Naye Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bibi. Sylvia Lupembe amesema kuwa kupitia TEA mpango huo utatekelezwa katika shule kongwe 11 katika mikoa ya Bukoba, Mwanza, Tabora, Singida, Same, Arusha, Dodoma, Morogoro na Pwani kwa kuzifanyia ukarabati wa miundo mbinu mbalimbali ikiwemo madarasa, vyoo, maabara, mabweni na mifumo ya umeme.

“hali ya shule zetu kongwe kwa kweli sio nzuri tumetembea kwenye mikoa takribani Mikoa sita tumejionea halihalisi ya miundombinu ya shule zetu kongwe hazipo katika mazingira mazuri ya kujifunzia kutokana na kuwa na miundombinu chakavu na kwa mradi huu tunataka kuweka mazingira mazuri ya watoto wetu hawa kujifunzia hasa kwa kuanza na shule hizi kongwe” Alisema Sylvia.

Wakizungumzia ukarabati huo Mwalimu Mkuu wa shule wa Shule ya Sekondari Nganza Bi. Yacinta Lyimo aliishukuru Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa Utekelezaji wa mpango huo kwani utasaidia kuboresha mazingira ya kufundishia na hata kusaidia kuinua kiwango cha elimu na ufaulu katika shule hizo.

Aidha, Afisa Elimu wa Manispaa ya Singida Bw. Omari Kisuda Mpango huu wa maboresho ya shule kongwe ni mkombozi katika sekta ya elimu na umekuja wakati uhitaji wa maboresho ya shule hizo unahitajika hasa kutokana na baadhi ya shule kushindwa kufanya ukarabati wa mara kwa mara kutokana na ufinyu wa bajeti.



 

SMZ YAAHIDI KUENDELEZA MIPANGO YA UCHUMI INAYOCHAGIZWA KIMATAIFA

$
0
0
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuhakikisha mipango yote ya kimaendeleo inayochagizwa na malengo endelevu ya kimataifa inatekelezwa kwa vitendo ili wananchi waweze kunufaika.

Imesema katika malengo ya milennia ya 2015 serikali ilifanikiwa katika baadhi ya sekta zikiwemo sekta za elimu, afya na miundo mbinu hatua zinazotakiwa kuendelea kupewa kipaumbele na wadau wa maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Juma Reli katika Mkutano wa wadau wa sekta za maendeleo nchini wanaojadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani humo. Mkutano huo ulifanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View.

Alisema licha ya kuwepo na changamoto mbali mbali za kiutendaji katika utekelezaji wa mipango hiyo ikiwemo suala la wananchi kutokuwa na uelewa mzuri wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya dunia bado mamlaka husika zinaendelea kutoa elimu hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho katika Mkutano wa wadau wa sekta za maendeleo nchini wanaojadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar ambao umeandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Tume ya Mipango Zanzibar chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini.


Mgeni rasmi Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Juma Reli akitoa nasha wakati akifungua mkutano wa siku moja wa wadau wa sekta za maendeleo nchini wa kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar ambao umefanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View.
 
Reli alieleza kwamba malengo na mipango mbalimbali ya maendeleo ni kuwasaidia wananchi wa Zanzibar waweze kuondokana na tatizo sugu la umaskini, magonjwa na changamoto za kiusalama.

“Katika MDG tumeweza kufanikiwa kwa baadhi ya malengo ikiwemo suala la elimu na afya lakini kuna mengine bado hatukuweza kufanikiwa kuyafikia na kwa sasa tunaendelea na malengo mapya ya SDG’s ambayo tunatakiwa kuyafanyia kazi ili yaende sambamba na mipango ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar." alisema Reli.Aidha alisema bado wanajadiliana ni kwa namna gani mipango ya kimataifa tutaiingiza katika sera na mipango yetu ya kimaendeleo ili wananchi waweze kunufaika na fursa hizo za kimaendeleo na kiuchumi kwa ufanisi zaidi.

Alisema utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu SDG’s ambayo ni 17 yanatakiwa kupewa kipaumbele kwani yanagusa nyanja mbalimbali za kijamii yakiwemo maisha halisi ya wananchi wanaostahiki kunufaika na fursa na mahitaji muhimu ya kibinadamu.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN) Ofisi ya Zanzibar, Anna Senga akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez katika mkutano wa wadau wa sekta za maendeleo nchini kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar.

Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafti, Uchumi na Kijamii nchini ( ESRF), Dkt.Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho alisema, ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika SDG’s ni vyema sera na mipango endelevu ya nchi husika iweke vipaumbele vya kukuza uchumi kuanzia ngazi za chini

Kida alieleza kwamba katika utekelezaji wa SDG’s lazima kuwepo na mpango endelevu wa ufuatiliaji kuanzia ngazi za chini hadi taifa kwa lengo la kuhakikisha malengo hayo yanatekelezwa kwa mujibu wa matakwa ya malengo ya kimataifa.Naye Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN), Ofisi ya Zanzibar, Anna Senga alisema endapo malengo ya dunia yataweza kutekelezwa ipasavyo Zanzibar itaweza kupunguza changamoto mbali mbali zinazokabili sekta za kijamii na kiuchumi.

Alisema UN itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika utekelezaji wa SDG’s kama ilivyokuwa katika utekelezaji wa malengo ya dunia MDG’s yaliyopita ili serikali iweze kufikia ngazi za chini kwa kuinua kipato cha wananchi kiendane na ukuaji wa uchumi wa nchi.

Senga aliishauri serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuendelea kuwashirikisha wananchi wa ngazi za chini katika kupanga na kutekeleza maendeleo yao katika maeneo husika ya wananchi.“Changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya kimataifa ili yaendane na mipango ya maendeleo ya serikali ni upungufu wa ushirikishwaji wa wananchi ama jamii husika na wengine hawafikiwi kabisa katika maeneo yao jambo linalotakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka katika kutekeleza kwa vitendo Malengo ya Maendeleo Endelevu ya SDG’s”, alifafanua Senga.

Naye Mshauri wa Masuala ya Uchumi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, Rogers Dhliwayo alisema Malengo ya Maendeleo Endelevu SDG’s yanatakiwa yawekewe vipaumbele mbalimbali vya takwimu na tafti za kiuchumi katika maeneo tofauti ya jamii ili malengo endelevu yaweze kuwafikia walengwa.

Kwa upade wa washiriki wa mkutano huo kwa nyakati tofauti walisema kwamba mipango mbalimbali ya kimaendeleo inayopangwa na serikali inatakiwa kuwekewa vipaumbele kwa wananchi badala ya utekelezaji na tathimini kubakia ngazi za serikali kuu pekee.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto) na Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha wakinakili mambo muhimu wakati mgeni rasmi (hayupo piichani) akitoa nasaha zake.

Walisema kwamba katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu SDG’s ni lazima kutengeneza mpango mkakati wa mawasiliano wa masuala ya utamaduni, mila na desturi za jamii husika ambapo mipango hiyo inatakiwa kutekelezwa ili iwe rahisi wananchi kufahamu vizuri umuhimu wa mipango hiyo.

Washiriki hao walisema katika utekelezaji wa mipango hiyo ni lazima kuwepo na mikakati ya makusudi ya kuhakikisha changamoto ya umasikini uliokithiri unapungua kulingana na mikakati mbalimbali inayowekwa na vipaumbele vya kimataifa ili viweze kutekelezwa kwa vitendo na nchi husika.

Aidha wameshauri kwamba katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu SDG’s ni lazima kuzingatia suala la serikali za mitaa, kutumia lugha nyepesi katika mawasiliano, kufanya marejeo katika maandiko ya baadhi ya waasisi wa kitaifa akiwemo Mwalimu Nyerere na kufanya utafiti juu ya matumizi sahihi ya Rasilimali.

Pichani juu na chini ni wadau wa sekta za maendeleo visiwani Zanzibar walioshiriki katika mkutano wa kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani humo ambao umefanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View.

Sambamba na hayo wamesema katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) ni lazima kuweka kipaumbele kwa makundi maalum ya watu wenye mahitaji maalum wakiwemo Watu wenye Ulemavu.

Warsha hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) ambapo imewakutanisha wadau mbalimbali kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Mshauri wa Masuala ya Uchumi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, Rogers Dhliwayo akiwasilisha mada katika mkutano wa wadau wa sekta za maendeleo nchini wa kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar.
Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN) Ofisi ya Zanzibar, Anna Senga, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy, mgeni rasmi Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Juma Reli, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha wakiwa meza kuu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto ya visiwani Zanzibar, Mauwa Makame Rajab akitoa maoni katika mkutano wa wadau wa sekta za maendeleo nchini wa kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View.

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Juma Reli wakisikiliza maoni ya wadau yaliyokuwa yakiwasishwa kwenye mkutano kuelekea utekelezaji wa SDGs.

Bw. Sefu Mwinyi kutoka Tume ya Mipango Zanzibar akiwasilisha maoni yake katika mkutano huo uliowakutanisha wadau wa sekta za maendeleo visiwani Zanzibar.

Katibu Mkuu Wizara ya ya Elimu na Mafunzo ya Amali visiwani Zanzibar, Khadija Juma (kushoto) akichangia hoja katika mkutano huo. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora visiwani Zanzibar, Asha Abdallah Ali.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo.

RE A TANZANIAN WINS HER MAJESTY THE QUEEN’S YOUNG LEADERS AWARD

$
0
0



A TANZANIAN WINS HER MAJESTY THE QUEEN’S YOUNG LEADERS AWARD By Ayoub Mzee-London Her Majesty The Queen, Head of the Commonwealth, accompanied by Prince Harry, has hosted a special ceremony in the Ballroom at Buckingham Palace to present medals to the 60 winners of The Queen's Young Leaders Awards for 2016.

Among them was Rachel Nungu from Tanzania a doctor and the national co-ordinator of a medical programme to help children who are born with clubfoot. The programme uses a non-surgical method called the Ponseti method to treat patients. Children born with clubfoot are often hidden away, so Rachel has built good relationships with community leaders to spread awareness of the condition and its treatment.

 She has contributed to the establishment of partnerships with clinics in different regions and has trained staff. So far, more than 100 children have been treated, and in the future the group hopes to help more of the 3,000 children who are born with the condition each year. Chairman of The Queen Elizabeth Diamond Jubilee Trust, Sir John Major, David Beckham and Sir Lenny Henry were also in attendance. 

The Queen’s Young Leaders Award is a prestigious Commonwealth project which recognises and celebrates exceptional young people from across the Commonwealth who are taking the lead in their communities and using their skills to transform lives. The Queen’s Young Leaders programme aims to discover, celebrate and support young people from every Commonwealth nation. The awardees are chosen for having transformed their own lives and the lives of those around them, despite challenges they may have faced along the way.
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images