Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

Twanga Pepeta kufanya shoo kabambe Sikukuu ya Eid Mosi Giraffe Hotel

0
0
BENDI ya muziki wa dansi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, inatarajia kufanya shoo kabambe Sikukuu ya Eid Mosi katika Hoteli ya Giraffe Ocean View iliyopo Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Aset Entertainment, Asha Baraka, alisema kuwa onyesho hilo litakwenda sambamba na utambulisho wa wimbo mpya wa mwanamuziki wao aliyerejea kundini hivi karibuni, Khalid Chokoraa unaokwenda kwa jina la Prison Love.
 
Alisema kwamba onyesho hilo ni maalum kwaajili ya kuwapa burudani mashabiki wao baada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ikiwa ni pamoja na kumkaribisha Chokoraa aliyerejea Twanga Pepeta akitokea Mapacha Watatu.
 
“Onyesho hilo litakuwa ni kwaajili ya kutoa burudani kwa mashabiki wetu baada ya mfungo wa Ramadhani, tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kwani kutakuwa na mambo mazuri ambayo ni ‘surprise’,” alisema Asha anayefahamika pia kwa jina la Iron Lady.
 
Kiongozi huyo alisema wanawasiliana na uongozi wa Giraffe Hoteli ili kuona kama wanaweza kutoa zawadi kwa mashabiki watakaopendeza zaidi na wanamuziki watakaopagawisah zaidi siku hiyo.
 
Wanamuziki wanaounda bendi hiyo kwa sasa wapo katika mazoezi makali kujiandaa na shoo hiyo chini ya uongozi wa wakongwe Ally Choki na Luiza Mbutu.

TAASISI YA NITETEE YAIOMBA SERIKALI KUTOA RUZUKU KWA TAASISI ZINAZOFANYA KAZI VIZURI

0
0

Mkurugenzi wa Taasisi ya Nitetee, Flora Lauwo akipungia mkono alipokuwa akitambulishwa bungeni Dodoma.

Flora Lauwo akitafakari jambo alipokuwa akifuatilia mwenendo wa mijadala ya Bunge mjini Dodoma.

Flora Lauwo (kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula katika viwanja vya Bunge, Dodoma

Serikali imetakiwa kuziangalia kwa jicho la tatu ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuanza kutoa ruzuku kwa taasisi za watu binafsi zinazofanya kazi ya kufuatilia na kubaini matatizo yanayowakumba wananchi kama afanyavyo, Flora Lauwo Mkurugenzi wa Taasisi ya Nitetee.

Licha ya serikali kutambua mchango unaotolewa na taasisi hizo, jamii nayo imeaswa kujitokeza kuwasaidia watu ambao wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia ,maradhi na wale wanaohitaji msaada wa kupata elimu .

Kufatia serikali kutambua mchango huo baadhi ya wadau kutoka sekta binafsi wanajitokeza na kubainisha changamoto zinazowakumba.Yapo malengo yanayowekwa na wadau hao ili kutimiza ndoto za kuwasaidia watanzania.“Lakini wapo Wajanja ambao wamekuwa wakinufaisha na misaada wanayopewa na wafadhili badala ya kuwasaidia walengwa,” alisema Lauwo.

Taasisi ya nitetee inajishughulisha na utatuzi wa matatizo yanayozikumba familia zinazoishi katika mazingira magumu ambapo mpaka sasa imeshazifikia kaya 36 pamoja na kuwapeleka watoto 20 shule.

TASAF YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA.

0
0

 Watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wakiwa katika kilele cha wiki ya Utumishi wa Umma kwenye ukumbi wa Mikutano wa Taasisi hiyo jijini Dar Es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TASAF wakiwa katika Mkutano wa kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma uliojadili namna ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TASAF wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo Bwana Ladislaus Mwamanga, ( hayupo pichani) kujadili uboreshaji wa huduma za mfuko huo katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga ( aliyeshika kipaza sauti) akitoa ufafanuzi juu ya moja ya masuala yaliyoulizwa na wafanyakazi (hawapo pichani) katika kikao cha kufunga wiki ya utumishi wa umma yaliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo jijini Dar esa salaam.
Na Estom Sanga-TASAF.

WAFANYAKAZI wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wameadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa Menejimenti ya taasisi hiyo kukutana nao kwenye ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam na kusikiliza kero zao kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.

Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii unaotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini , unatoa huduma kwa Zaidi ya Kaya Milioni Moja na Lakini Moja nchini kote jukumu iliyopewa na serikali katika jitihada zake za kupambana na Umaskini nchini..

Imearifiwa katika kikao hicho kuwa mafanikio makubwa yameanza kujitokeza kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambapo wengi wao wameanza kujiwekea misingi ya kupunguza umaskini kwa kuwa na uwezo wa kusomesha watoto,kupata huduma za afya,kuwa na uhakika wa lishe na kuongeza uchumi wao.

Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini pia umeanza kusisimua hamasa ya walengwa wa Mpango huo kuboresha maisha yao kwa kiwango cha kuanza kuboresha makazi yao kwa kujinunulia mabati na kuezeka nyumba,kuanzisha miradi midogo midogo kama ufugaji wa kuku wa kienyeji,mbuzi nahata nguruwe.

Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana Ladislaus Mwamanga amesisitiza watumishi wa Mfuko huo kuendeleza jitihada za kuwahudumia wananchi na hususani walengwa wa Mpango kwa kuzingatia taratibu na kanuni za utumishi wa umma kama zinavyoelekeza.

Zifuatazo ni picha za watumishi wa TASAF wakiwa kwenye ukumbi wa mikutanowa taasisi hiyo maarufu kama “Mlimani City conference hall” ulioko makao makuu ya taasisi hiyo jijini Dar es salaam.

MCHEZAJI BORA WA UMMISETA MUSA SAID KUONDOKA JUMATANO JUNI 28, 2016 KWENDA NCHINI UFARANSA.

0
0
 Meneja Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga, akizungumza na waandishi wa habari kuwaelezea juu ya safari ya mchezaji Musa Said anayetarajia kuondoka Jumatano ya Juni 28, 2016 kwenda nchini Ufaransa kwenye kambi ya kimataifa ya Copa Coca-Cola. Pembeni ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja, Mchezaji Musa Said Bakari na Mwalimu wake wa Kibasila. 
Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. 

 Na Devotha Kihwelo. 
 MCHEZAJI bora wa mashindano ya UMMISETA yaliyofanyika mwaka jana mkoani Mwanza, Said Musa Jumatano ya Juni 28, 2016 kuelekea Ufaransa katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca - Cola ambayo imeandaliwa na kampuni ya kinywaji cha Coca - Cola . Akizungumza jijini Dar es Salaam katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja alisema udhamini wa kampuni ya Coca - Cola imetambua umuhimu wa michezo hivyo kukubali kudhamini michezo kupitia shule za sekondari ili kukuza vipaji vya wanamichezo chipukizi ambao wanamalengo makubwa katika kuitumikia nchini yao kupitia michezo. “Kwetu sisi imekuwa faraja kwa kuibua kipaji kichanga ambacho kitakuwa ni mfano wa kuigwa kama ilivyo kwa Samatta ambaye amekuwa kioo kwa jamii ya wanamichezo na hivyo kuomba makampuni mengine kujitokeza kwa ajili ya kusaidiana na Coca - Cola”, alisema. Kiganja alimtaka Musa kuzingatia nidhamu kipindi chote atakachokuwepo kwenye kambi ili kujijengea heshima katika kukuza kipaji chake kwa kipindi chote ambacho atakuwa chini ya walimu wageni ambao hajawahi kukutana nao na hiyo italeta heshima nchini. Kwa upande wa Meneja msaidizi wa chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga, alisema wamefurahi kupata nafasi ya kudhamini mashindano hayo kwa kuwa ndiyo mara yao ya kwanza na imefanikiwa kufikia malengo ya kupata mchezaji ambaye atakuwa muwakilishi wa Tanzania katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca - Cola iliyopo jijini Paris nchini Ufaransa. Alisema Musa ataondoka kwa kupitia Nairobi kwa kuwa kozi inaanza kesho na kumalizika Julai 4, hivyo aliwataka wanafunzi wengine kujituma ili kufikia malengo kama aliyofikia Mussa. “Sisi kama kampuni imekuwa ni faraja kwani tutakuwa tumeitangaza nchini kwa kupitia Mussa na hii itakuwa ni muendelezo katika michezo inayoendelea,”alisema. Mussa ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Kibasila ambaye alizaliwa Agosti 11, 2000 huku akiwa ni mchezaji tegemeo katika timu ya shule na Mkoa wa Temeke ambapo walitumia jina hilo kwa kupitia michezo.

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA VIWANDA NA MAZINGIRA UNAOENDELEA NCHINI KOREA YA KUSINI

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho la Viwanda Duniani Mr. Li Yong, akimpa zawadi ya picha Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji anayeshughulikia Viwanda Dr. Adelhelm Meru, walipokutana kwa mazungumzo mafupi wakati wa Mkutano wa "Viwanda na Mazingira" unaoendelea Mjini Ulsan, Korea ya Kusini.

Airtel yakabidhi msaada kwa kituo cha Sarnaa Islamic Orphanage Center Mwanza

0
0

Afisa Masoko wa kanda ya ziwa wa Airtel , Emmanuel Raphael akitoa msaada wa chakula kitakachotumika katika msimu huu wa Ramadhani kwa baadhi ya watoto kwaajili ya kituo cha Sarnaa Islamic Ophanage Center kilichoko mwanza. Kwa mwaka huu Airtel ilitenga zaidi ya shilingi milioni 10 kwaajili ya kuwasadidia watoto waishio katika mazingira magumu walioko katika vituo mbalimbali nchini.
Afisa Masoko wa kanda ya ziwa wa Airtel , Emmanuel Raphael akikabidhi msaada wa chakula kwa baadhi ya watoto kwaajili wa kituo cha Sarnaa Islamic Ophanage Center kilichoko mwanza kwa ajili ya kufuturu wakati huu wa mfungo wa Ramadhani. Kwa mwaka huu Airtel ilitenga zaidi ya shilingi milioni 10 kwaajili ya kuwasadidia watoto waishio katika mazingira magumu walioko katika vituo mbalimbali nchini. Akishuhudia Mwalimu mkuu wa kituo cha Sarnaa Islamic Ophanage Center, Hashim Hussein
Afisa Masoko wa kanda ya ziwa wa Airtel , Emmanuel Raphael pamoja na Meneja Mauzo wa Airtel , Joel Laizer wakikabidhi msaada wa chakula kwa baadhi ya watoto wa kituo cha Sarnaa Islamic Ophanage Center kilichoko mwanza ili kuwawezesha kufuturu wakati huu wa mfungo wa Ramadhani. Kwa mwaka huu Airtel ilitenga zaidi ya shilingi milioni 10 kwaajili ya kuwasadidia watoto waishio katika mazingira magumu walioko katika vituo mbalimbali nchini

Afisa Masoko wa kanda ya ziwa wa Airtel , Emmanuel Raphael akimkabidhi Mwalimu mkuu wa kituo cha Sarnaa Islamic Ophanage Center, Hashim Hussein msaada wa chakula kwa ajili ya kufuturu wakati huu wa mfungo wa Ramadhani. Kwa mwaka huu Airtel ilitenga zaidi ya shilingi milioni 10 kwaajili ya kuwasadidia watoto waishio katika mazingira magumu walioko katika vituo mbalimbali nchini

WANAHABARI WATEMBELEA VIJIJI VINAVYO PAKANA NA HIFADHI YA TAIFA YA MILIMA YA MAHALE.

0
0


Baadhi ya Wanahabri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale inayosifika kwa uwepo wa Sokwe Mtu.
Usafiri unaotegemewa katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ni Boti na Mitumbwi .
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ,Pascal Shelutete (Mwenye kofia) akiwa na Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ,Romanus Mkonda wakielekea katika vijiji vinavyopakana na Hifadhi hiyo,Wengine ni wmwandishi wa gazeti la Uhuru,Jackline Massano na kulia ni Mhariri wa gazeti la Jamhuri ,Mkinga Mkinga.
Wanahabari ,Said Mnekano maarufu kama Bonge wa Clouds fm,aliyesimama nyuma.akiwa na Asiraji Mvungi pamoja na muongoza watalii ,Rashid Omary wakiwa katika moja ya boti zinazotumika kama njia ya usafiri katika Hifadhi ya Taifa ya Mahale.

Waandishi ,Beatrice Shayo na Nora Damian wakijaribu kushuka kutoka katika boti.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akionozana na wanahabari kutembelea kijiji cha Nkokwa kinachopakana na Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale.


Ili kuwafikia wananchi maeneo mengine wanahabari walilazimika kuvua viatu na kupita katika maji.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAP A) akizungumza na wananchi katika kijiji cha Nkonkwa wilayani Uvinza.
Baadhi ya wananchi wanaounda vikundi vya wajasilaimali wakimsikiliza Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Pascal Shelutete (hayupo pichani ) alipoongozana a wanahabari kutembelea vijiji vinavypakana na Hifadhi ya Taifa ya Miima ya Mahale.
Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ,MhifadhiRomanus Mkonda akizungungmza katika kikao hicho.
Kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja akijaribu kusukuma chombo chake kwa kutumia kandambili wakati akisafiri katika ziwa Tanganyika.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi blog aliyeko mkoani Kigoma.

GGM YATOA VIFAA TIBA KWA WATOTO KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI.

0
0
WAFANYAKAZI wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) wametoa msaada wa vifaa tiba kwa watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo.

Aizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,  Daktari Mkuu wa Mgodi wa Dhababu wa Geita (GGM), Kiva Mvungi amesema kuwa Msaada uliotolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika kitengo cha watoto ni wadhamani ya shilingi milioni 23.

Pia amesema kuwa msaada huo ni kwaajili ya kusaidia jitihada Serikali katika kuboresha huduma za Afya hasa katika kitendo cha watoto katika hospitali hiyo.
"Lengo la ni kuwa sehemu ya Jamii ambapo uwepo wa Mgodi unaleta manufaa kwa jamii inayozunguka." Alisema Mvungi.

Vifaa vilivyotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita wa GGM katika Hospitali ya Muhimbili leo ni Bp Machine 10, Infrsion Pump 2 Themometers 6110, Standing Weighing Scale 6, Nebulises 3 na Pulse Oxymeter 10.


 Daktari Mkuu wa Mgodi wa Dhababu wa Geita (GGM), Kiva Mvungi akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimili, Mary Charles jijini Dar es Salaam leo.

 Daktari Mkuu wa Mgodi wa Dhababu wa Geita (GGM), Kiva Mvungi (Wapili kulia) akikabidhi msaada wa Vifaa vya matibabu kwa watoto kwa Chama cha madaktari wa watoto Tanzania ukipokelewa na Mkuu Mawasiliano ya Umma na huduma kwa wateja wa Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha.
 Bara baada Mkuu Mawasiliano ya Umma na huduma kwa wateja wa Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha kukabidhiwa msaada wa vifaa tiba kwa watoto naye akakabidhi Msaada huo uliotolewa na Mgodi wa Dhababu wa Geita (GGM) kwa Mkuu wa Idara ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimili, Mary Charles jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Idara ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimili, Mary Charles  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo pamoja na kuwashukuru wafanyakazi wa Mgodi wa Geita wa GGM walipotoa msaada katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika Kitengo cha watoto. 
 Makamu wa Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania na  Daktari Bingwa wa Watoto katika Hopitali ya Tiafa ya Muhimbili, Namala Mkopi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kukabidhiwa Msaada uliotolewa na wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita wa GGM.

NDANI NA NJE YA UWANJA KABLA YA MECHI YA YANGA NA TP MAZEMBE KUANZA UWANJA WA TAIFA JIONI YA LEO

0
0


Mashabiki wafurika kushuhudia mpambano wa kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Tp Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo leo Juni 28,2016.







Wizara ya Michezo yakutana na kampuni ya B.C.E.G yazungumzia maendeleo ya uwekaji wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa.

0
0

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge (kushoto) akizungumza na Meneja kampuni ya B.C.E.G Bw. Xiong (Kulia) kuhusu maendeleo ya uwekaji wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Juni 28,2016.

Meneja kampuni ya B.C.E.G Bw. Xiong (Kulia) akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge (kushoto) kuhusu maendeleo ya uwekaji wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Juni 28,2016.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge (kulia) akizungumza na wataalamu kutoka kampuni ya Selcom (Kushoto) kuhusu maendeleo ya uwekaji wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Juni 28,2016.Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM

WAKULIMA WADOGOWADOGO NA WADAU WA KILIMO WAKUTANA KUJADILI BAJETI YA KILIMO NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

0
0
Dar es salaam, Wanawake wakulima wadogowadogo wakiongozwa na waliokuwa washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloratibiwa na shirika la Oxfam, wamekutana pamoja na wadau kutoka taasisi mbalimbali na baadhi ya wanafunzi kutoka elimu ya juu, Tanzania kujadili Bajeti ya Kilimo kwa mwaka 2016/17 na changamoto za mabadiliko ya Tabia Nchi.

Akifungua Mkutano huo wa siku tatu, Meneja utetezi wa Oxfam Tanzania, Bi. Eluka Kibona alisema kuwa lengo la kuwakutanisha wakulima hao na wadau ni kufanya majadiliano juu ya Bajeti ya kilimo na Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa kuwa hali ilivyo sasa ni kwamba wakulima wengi hasa wadogowadogo hawapati nafasi ya kushirikishwa katika masuala ya bajeti hiyo, hivyo mkutano huo utasaidia kuibua changamoto mbalimbali ambazo zitatakiwa kutatuliwa bila kusahau suala la mabadiliko ya Tabia Nchi ambayo yataathiri kwa kiwango kikubwa katika kilimo.

Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi wa Programu Forum CC, Bi. Rebecca Muna alisema mabadiliko ya Tabia Nchi yamekuwa yanaendelea kuathiri zaidi wakulima wadogo wadogo hasa waliopo vijijini, hivyo kupitia mkutano huo wakulima wanapata elimu ili kukabiliana na mabadiliko hayo.

Akieleza kwa undani juu ya Mabadiliko ya tabia nchi mwezeshaji kutoka Forum CC, Faizal Ally alisema kwamba changamoto kubwa zaidi ya mabadiliko ya Tabia nchi ni pamoja na maji chumvi kuingia nchi kavu na kuathiri ukuaji wa mazao, kuongezeka kwa joto, misimu ya mvua zisizotabirika, kupungua kwa kina cha maji katika mito na maziwa, kuongezeka kwa majanga ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na mafuriko, ukame na vimbunga na kuongezeka kwa magonjwa ya mazao.

Alisema kuwa mambo yote hayo yamekuwa yakichochea wakulima na wafugaji kukosa maeneo ya malisho kwa ajili ya mifugo na kuongeza kuwa ili wakulima waweze kukabiliana na changamoto hiyo ya mabadiliko ya Tabia nchi wanatakiwa kujifunza mbinu mbalimbali ikiwemo kuvuna maji ya mvua, kutumia umwagiliaji wa matone, matumizi ya mbegu bora zinazostahimili magonjwa na Ukame, kilimo mchanganyiko/mseto, matumizi ya mbolea asili na kuongeza thamani ya mazao.

Nao wakulima hao kwa nyakati tofautitofauti walizungumzia suala zima la bajeti ambapo walisema kuwa changamoto nyingi wanazozipata kwa kutoshirikishwa kwenye bajeti kuu juu ya kilimo zinasababisha wasifikiwe na elimu na huduma mbalimbali zitakazowasaidia kwenye shughuli zao za kilimo hivyo basi kupitia mkutano huo wameomba kusikilizwa maoni yao hasa wakati wa uandaaji wa bajeti kwa ujumla kwa kuwa wao ndiyo walengwa namba moja kwenye sekta ya kilimo nchini.

Meneja utetezi kutoka Shirika la Kimataifa la OXFAM Tanzania Bi. Eluka Kibona akifungua mafunzo juu ya uelewa wa Bajeti ya Kilimo na Mabadiliko ya Tabianchi yanavyoathiri sekta ya kilimo Tanzania hasa wakulima wadogo wadogo.
Mkurugenzi wa Forum CC Bi. Rebecca Muna akielezea umuhimu wa mafunzo hayo yatakavyoweza kuwasaidia wakulima wadodogo katika kukabiliana na tatizo la Mabadiliko ya tabianchi.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo wakiwa katika kikundi kujadiliana maswala mbalimbali juu ya namna ya kuandaa bajeti.
Baadhi ya wadau waliohudhuria mafunzo hayo wakiwa wanatazama mfano wa jarida linalo onesha jinsi bajeti inavyo andaliwa.

Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Picha na Fredy Njeje .

SHAMO WORLD FOUNDATION YATOA MSAADA KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA MAUNGA JIJINI DAR LEO.

0
0
 Mwakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundtion, Salama akikabidhi baadhi ya Vitu vya msaada kwa  Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre, Zainabu Maunga jijini Dar es Salaam leo wakati walipotembelea katika kituo hicho kilichopo karibu na kituo cha Polisi cha Hananasif jijini Dar  es Salaam.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo mwakilishi wa kampuni ya Shamo World Foundation amesema kuwa wameguswa kutoa msaada katika  kituo hicho kwa kutenda matendo ya huruma wakati wa kipindi hiki cha Mwezi wa Ramadhani kwa watoto kwa kuwa wanamahitiji mengi pia ni kuwapunguzia ugumu wa maisha walezi wa watoto hao.

Nae Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre, Zainabu Maunga amewashukuru kampuni ya Shamo World kuwaona kwa jicho la pekee na kwenda kuwapa msaada katika kituo hicho.

Mwakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundation, Salama amesema kampuni hiyo wamekabidhi Kg 50 za Mchele, Kg 50 za unga wa ngano na unga wa ugali, Kg 50 za sukari pamoja na Maboksi 15 ya Tende pamoja na mafuta ya kupikia.
 Wawakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundation, Salama  na Zaituni Ramadhani wakikabidhi mafuta ya kupikia kwa watoto kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga jijini Dar es Salaam leo.
Wawakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundation, Salama  na Zaituni Ramadhani wakiwa katika picha ya pamoja na walezi wa kituo cha kulelea watoto yatima na watoto walio klatika kituo hicho jijini Dar es Salaam leo.

NAIBU KATIBU WAKUU WAAPISHWA LEO ZANZIBAR

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein   akimuapisha Dk.Islam Seif Salum kuwa Naibu Katibu Mkuu ,Mifugo na Uvuvi katika Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi, katika  hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akimkabidhi hati ya kiapo  Dk.Islam Seif Salum  baada ya kumuapisha  kuwa Naibu Katibu Mkuu ,Mifugo na Uvuvi katika Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi, katika  hafla iliyofanyika leo  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein  akimuapisha Nd,Hassan Abdulla Mitawi  kuwa  Naibu Katibu Mkuu Habari katika Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein  akimkabidhi hati ya kiapo Nd,Hassan Abdulla Mitawi  baada ya kumuapisha    kuwa  Naibu Katibu Mkuu Habari katika Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein  akimuapisha Nd, Rafii Haji Makame kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji katika Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein  akimkabidhi hati ya kiapo Nd, Rafii Haji Makame baada ya kumuapisha   kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji katika Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein  akimwapisha  Nd, Rafii Haji Makame baada ya kumuapisha   kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji katika Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
 Viongozi walioshiriki katika hafla ya kuwapishwa Watendaji katika Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika hafila iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,(kutoka kushoto) Mhe,Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Haji Khamis,Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe,Said Hassan Said na Mshauri wa Rais Utamaduni Mhe,Chimbeni Kheir
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe,Zubeir Ali Maulid,(kulia) akifuatiwa na Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi mhe,Hamad Rashid Mohamed,Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo mhe,Rashid Ali Juma,pamoja na Viongozi wengine akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayuob Mohamed Mahmoud wakiwa katika hafla ya kuwapishwa Watendaji katika Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo Ikulu Mjini Unguja, 
[Picha na Ikulu.]{28/06/2016.

Waziri Nape Nnauye akutana na Wanachama wa Shirikisho la kazi za Sanaa za Ufundi Tanzania.

0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akipokea maelezo kuhusu sanamu iliyochongwa toka kwa Mwandamizi na Msemaji wa Chama cha Wasanii na Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA) Bw. Nyunga Joseph Nyunga wakati alipotembela katika eneo lao lililoko Mwenge, jijini Dar es Salaam, 28 Juni, 2016.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (wa tatu kushoto) akiangalia kazi za sanaa ya uchongaji ndani ya moja ya mabadanda ya Wachongaji hao wakati alipotembela katika eneo lao lililoko Mwenge, jijini Dar es Salaam, 28 Juni, 2016.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (katikati) akiwa ameongozana na baadhi ya Viongozi wa Chama cha Wasanii na Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA) wakati alipowasili katika eneo lao lililoko Mwenge, jijini Dar es Salaam, 28 Juni, 2016.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM.


Na Benedict Liwenga-WHUSM.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye ameahidi kuzitataua baadhi ya changamoto mbalimbali zinazoikabili Chama cha Wasanii na Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA) ikiwemo upatikanaji wa Hati Miliki ya Kiwanja kwa ajili ya kazi zao, Ushuru unaotozwa kupitia Idara ya Maliasili nchini pamoja na Sheria ya Tozo katika Viwanja vya Ndege.

Mhe, Nnuaye ametoa ahadi hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Wanachama wa Shirikisho hilo ambapo amesema kuwa, suala la upatikanaji wa Hati Miliki ya eneo kwa ajili ya kazi za Wachongaji hao alishaanza kuifanyia kazi kwa kufanya mawasiliano na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi na amewahakikishia kwamba Hati ya eneo hilo itapatikana ili Wachongaji hao waweze kuwa na eneo lao maalum la kazi zao.

‘’Suala la upatikanaji wa Hati Miliki katika eneo lenu ambalo limekuwa likileta minong’ono niachieni mimi kwani najua katika hili kuna baadhi ya watu wenye fedha wanataka kuwakandamiza watu wasio na uwezo kwa kudai kuwa eneo ni la kwao, hapo awali nilishafanya mazungumzo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na nawahahakikishieni kuwa haki itatendeka, kwani hakuna mtu mwenye mfuko mkubwa wa kuweza kuiingiza Serikali nzima katika suala hili’’, alisema, Mhe. Nnauye.

Kuhusu suala la Ushuru unaotozwa na Maliasili nchini, Mhe. Nnauye amesema kuwa yuko tayari kukaa na watu wa Maliasili na kuona namna gani ushuru huo unavyotozwa hususani kwa Wachonagji hao pasipo kuonewa mtu ambapo pia ameshauri kuwa baadhi ya kodi ambazo zinazoweza kuua biashara za watu wenye vipato vya chini ni vema zikaondolewa ili zisiendelee kuwaumiza.

Aidha, Mhe, Nnauye ameahidi kutembelea maeneo ya Viwanja vya ndege ili kuweza kujua baadhi ya bidhaa za kazi za Uchongaji ambazo zimekuwa zikikamatwa na Watendaji viwanjani hapo zimekuwa zikiishia wapi ili kuondoa malalamiko yanayoelekezwa katika viwanja hivyo.


‘’Niwahakikishieni kwamba nitakwenda mwenyewe katika viwanja vya ndege ili nijue ukweli wa malalamiko yenu kwamba kumekuwa na baadhi ya kazi zenu za sanaa kama vile Uchongaji ambazo zimekuwa zikikamatwa katika baadhi ya viwanja vyetu vya ndege lakini mwisho wa siku hazijulikani zinaishia wapi’’, Alisema, Mhe. Nnauye.

Mhe. Nnauye ameahidi pia kujenga utaratibu wa kutembelea maeneo ya kazi za sanaa mara kwa mara na kwa namna nyingine amewaasa Kampuni ya Quality Group kusaidia kuzitangaza kazi za sanaa za Wachongaji hao kwani wao wameshafungua Duka Maalum ambalo linarahisisha upatikanaji wa bidhaa za sanaa kwa wageni na wenyeji ili kuwasaidia Wachongaji hao nchini.

Sambamba na hayo, Mhe. Nnauye amewashauri Wanachama hao kuunda SACCOS imara ambayo itawasaidia katika kujikwamua kiuchumi kutokana na kazi zao na kuwaahidi kuwatafutia mitaji kwa makubaliano ya kwamba, wanapaswa kuwachagua viongozi waaminifu ambao wanaweza kuongoza vema Saccos hiyo kwa manufaa ya wanachama wote.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wasanii na Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA), Bw. Adrian Nyangamalle amepongeza juhudi za Serikali katika kuwasimamia Wasanii kote nchini ambapo ameiomba Serikali pia kuharakisha suala la upatikanaji wa Sera ya Sanaa pamoja na Mfuko wa Sanaa kwa ajili ya Wasanii hao.

‘’Nikuombe Mhe. Waziri kutusaidia kuzishawishi baadhi ya Taasisi na Makampuni nchini kujenga utarataibu wa kuwatembeza wageni wanaokuja nchini katika maeneo ya sanaa ili soko la bidhaa zetu liweze kukukua ndani na nje ya nchi yetu’’, alisema Bw. Nyangamalle.

Chama cha Wasanii na Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA) kilianzishwa mnamo mwaka 1984 na kimesajiliwa kihalali na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ambapo mbali na majukumu yake kimeweza kuwaandaa na kuwashirikisha Wasanii wa ndani na nje ya nchi pamoja na kutetea Wasanii katika kupata haki zao.

TAARIFA YA UTEUZI KWA UMMA

0
0


Wafanyabiashara wahimizwa kuchukua mashine za EFD.

0
0
Na: Lilian Lundo - MAELEZO - Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza kugawa Mashine za Kutunza Hesabu za Kodi za Kielektroniki (EFD) bila malipo kwa wafanyabiashara wa kati na wadogo.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kachwamba alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Neema William Mgaya juu ya mpango wa serikali kugawa mashine hizo Nchi nzima.

“Nia ya Serikali ni kusambaza mashine za EFD Nchi nzima lakini tumeanza na Mkoa wa Dar es Salaam ambapo jumla ya mashine 5,703 zinaendelea kugawiwa kwa wafanyabiashara wa kati na wale wadogo ambao mauzo ghafi yao ni kati ya shilingi milioni 14 mpaka milioni 20 kwa mwaka,” alifanunua Mhe. Ashatu.

Aliendelea kwa kusema kuwa, japo mashine hizo zimekuwa zikitolewa bure lakini wafanyabiashara hawafiki katika ofisi za TRA kuzichukua. Hivyo amewataka kundi hilo la wafanyabiashara kufika katika ofisi za TRA wanazolipia kodi katika Mikoa ya Ilala, Kinondoni au Temeke kuchukua mashine hizo, kwani ni wajibu wa kila mfanyabiashara kutumia mashine hizo katika mauzo ya kila siku.

Aidha Mhe. Ashatu amesema kuwa utaratibu wa matumizi ya mashine hizo ulianzishwa kwa lengo la kurahisisha na kuboresha utunzaji wa kumbukumbu za biashara za walipa kodi. Aliongeza kuwa mfumo huo ulianzishwa ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya utunzaji kumbukumbu za mauzo na utoaji wa risiti za mauzo zinazoandikwa kwa mkono.

Vile vile mfumo huo umerahisisha usimamizi na ukadiriaji wa kodi kwa kuwa kumbukumbu zote za mauzo na manunuzi huhifadhiwa na kutunzwa kirahisi kwenye mashine za EFD na taarifa za mauzo ya mlipa kodi hutumwa kwenye seva ya TRA kwa njia ya mtandao kupitia mashine hizo.

RC MAKALLA AIOMBA BENKI KUU IFANYE UTAFITI KUHUSU UNUNUZI WA MAZAO YAKIWA SHAMBANI.

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya  Amosi Makalla akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya mara baada ya kufanya ziara katika kwa engo la kujitabulisha .
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala (Katikati)akizungumza na viongozi wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya,kulia Mkurugenzi wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya Jovent Rushaka na Meneja Utawala na fedha Bakali Ally kushoto katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya ,June 28 -2016.
Baadhi ya viongozi wa benki hiyo wakimsikiliza kwa makini Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla mara baada ya kufanya ziara katika benki hiyo June 28 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla (kulia)akimsikiliza kwa makini Meneja utwala na fedha wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya ,Ally Bakari wakati akizungumza mambo mbalimbali yahusuyo benki hiyo.
Baadhi ya viongozi wa benki hiyo wakiwa makini katika mkutano huo.
Mgeni rasmi katika picha ya Pamoja na viongozi na wafanyakazi wa benki hiyo.



Na EmanuelMadafa, JamiiMojablogu Mbeya
SERIKALI MKOANI Mbeya imeitaka benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya  kufanya utatifi juu ya kuwepo kwa ununuzi wa mazao kwa wakulima mapema kabla ya kuanza kukomaa hususani mazao ya ndinzi hasa katika halmsahuri ya wilaya ya Rungwe Mkoani humo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla wakati akizungumza na  wafanyakazi wa benki Kuu Tanzania (BOT)tawi la Mbeya mara baada ya kufanya ziara katika benki hiyo yenye lengo la kujitambulisha.

Amesema kwa muda mrefu sasa  wakulima wa mkoa huo wamekuwa wakinyonywa na baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakinunua mazao mapema yakiwa shambani na kupangia bei ya chini ambayo haiendani na bei hali ya sokoni .

 Amesema nivema benki hiyo ikajaribu kulifanyia utatiti suala hilo  ili kuona kama mfumo huo unaweza kuleta tija  kwa mkulima  kwani  benki hiyo inanafasi nzuri ya kuisaidia serikali katika uchocheaji wa  ukuaji wa uchumi.
Amesema lengo la serikali ni kuwalinda wananchi wake sanjali na kuwaondolea umaskini hivyo lazima ifanyike kila aina ya jitihada katika kufanikisha suala hilo.

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa wa mbeya Amosi Makalla ameipongeza benki hiyo kwa kuweka jitihada za  makusudi katika  kudhibiti mfumuko wa bei nchini.

Amesema kama mfumuko wa bei utashindwa kudhibitiwa tafsiri halisi ya kukua kwa uchumi haitakuwa na maana yeyote kwa mwananchi wa kawaida hivyo lazima benki hiyo ikaongeza jitihada zaidi katika kudhibiti hali hiyo.

Kwa upande Mkurugenzi wa benki  kuu ya Tanzania( BOT)tawi la Mbeya Ndugu Juvent Rushaka amesema benki hiyo iko tayari kufanya utafiti suala lolote la kiuchumi.

Aidha Mkurugenzi huyo ameelezea changamoto mbalimbali ambazo tawi hilo linakutana nazo  likiwemo suala la kutopata takwimu mbalimbali kwa usahihi na kwa wakati.

Amesema changamoto nyingine ni miundombinu ya kiusalama ya majanga ya moto kwa kipindi kirefu sasa kwa ukosefu wa maji katika bomba la kuzimia moto hali ambayo ni hatarishi endapo litatokea janga la moto katika twi hilo.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS DKT MAGUFULI MKUTANO WA SADC NCHINI BOTSWANA

0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma (wapili kulia) kuingia kwenye ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Grand Palm mjini Gaborone kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi na serikali wa Jumuiya yaMaendeleo kusini mwa Afrika ( SADC ) kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli Juni 28, 2016. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki akatika Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC) uliofanyika kwenye hoteli ya Grand Palm mjini Gaborone Botswana Juni 28. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).



WAZIRI MKUU wa Lesotho, Dk. Pakalitha Mosisili amekubali kutekeleza masharti yaliyowekwa na Wakuu wa Nchi na Serikali na Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Uchumi na Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC Double Troika Summit), na kuridhia timu ya uchunguzi kwenda nchini humo kufanya uchunguzi wa hali ya kiusalama na kisiasa.

Dk. Mosisili ametoa uamuzi huo leo (Jumanne, 28 Juni, 2016) wakati wa kikao maalum cha Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC Summit) na wakuu wa nchi wanaounda Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ on Politics, Defense and Security Cooperation) kilichofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (GICC), jijini Gaborone, Botswana.

Pia amekubali viongozi waupinzani na baadhi ya maofisa wa kijeshi wanaoishi uhamishoni ambao walikimbia machafuko yaliyotokea nchini humo warejee nchini mwao na kuahidi kwamba atahakikisha wanapatiwa ulinziwa kutosha.

Januari mwaka huu, mkutano wa SADC Double Troika uliagizakwambaifikapo Februari Mosi, mwaka huuSerikali ya Lesotho iwe imetangaza matokeo ya Tume iliyoundwa kuchunguza matatizo ya kisiasa na kiusalama nchini humo hususan mazingira yaliyopelekea kifo cha marehemu Luteni Jenerali Maaparankoe Mahao ambaye alikuwa Mkuuwa Majeshi.

Kwaupande wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa akimwakilisha Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kikao hicho amesema wamepitia ripoti iliyoundwa na timu ya SADC iliyochunguza kuhusu matatizo ya Lethoto ambayo iliwahoji Viongozi wa Serikali, Jeshi, Bunge na familia ya marehemu Luteni Jenerali Mahao.

“Lengo la hatuahiiza SADC ni kuhakikisha inarejesha hali ya amani na utulivu kwenye maeneo ya siasa, ulinzi na usalama katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ili wananchi wake waweze kuishi vizuri,” amesema

Pia Waziri Mkuu amesema Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa Wakuu wa Nchina Serikali na Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Uchumi na Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC Double Troika Summit), Agosti mwaka huu ambapo kitafanyika kikao kingine nchini Tanzania.

Mkutano huo wa ulifunguliwa na Rais wa Botswana, Mhe. Lt. Jen. Seretse Khama Ian Khama na ulihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa akimwakilisha Rais Dk. John Pombe Magufuli; Rais wa Afrika Kusini, Bw. Jacob Zuma; Rais wa Msumbiji, Bw. Filipe Jacinto Nyusi; Rais wa Zimbabwe, Bw. Robert Mugabe, Mfalme Muswati wa III wa Swazland.

SADC Double Troika ni kikao maalum kinachojumuisha Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC Summit) na wakuu wa nchi wanaounda Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ on Politics, Defense and Security Cooperation).

SADC Double Troika ni mkutano unaohusisha viongozi wakuu watatu wanaoongoza chombo cha ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama na wengine watatu kutoka kwenye Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa SADC. Hawa wanawakilisha mwenyekiti aliyepo madarakani, mwenyekiti aliyemaliza muda wake na mwenyekiti ajaye ambaye huwa ni makamu mwenyekiti.

Chini ya muundo wa SADC, kuna mambo makuu mawili; la kwanza likiwa ni utangamano wa kikanda ambao unasimamiwa na mkutano wa wakuu wa nchi (SADC Summit) na la pili ni la siasa, ulinzi na usalama ambalo linasimamiwa na chombo maalum (SADC Organ).

Wajumbe wa mkutano wa SADC Organ ni Msumbiji (Mwenyekiti); Afrika Kusini (Mwenyekiti aliyemaliza muda wake) na Tanzania inayotarajia kuchukua uenyekiti wa chombo hiki ifikapo Agosti, 2016. Botswana, Zimbabwe na Swaziland ndizo zinaunda SADC Summit.

MATUKIO YA UNGENI LEO.

0
0

 Mwenyekiti wa Kamati maalum ya maandalizi ya mechi ya kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu yaSimba na wapenzi wa timu ya Yanga Mhe. John Kadutu akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo mjini Dodoma uliolenga kuhamasisha wadau mbalimbali kujitokeza kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua tatizo la madawati ambapo kamati hiyo inaratibu maandalizi ya mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu hizo itakayofanyika mwezi Agosti 2016 kwa lengo la kukusanya madawati yatakayo pelekwa katika Halmashauri zote nchini, kushoto ni Mwenyekiti wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club) Mhe. William Ngeleja.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasilisha  Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa Mwaka 2016 (The Public Procurement Amendment Bill 2016) Leo Bungeni Mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (Kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Dkt. Angella Kairuki Bungeni Mjini Dodoma leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
 Mwenyekiti waTimu ya Bunge (Bunge Sports Club) Mhe. William Ngeleja akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu ya Simba na wapenzi wa timu ya Yanga itakayofanyika mwezi Agosti 2016 kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua tatizo la madawati hapa nchini kwa kuhamasisha wadau kuchangia madawati yatakayo gawanywa katika Halmashauri zote nchini.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati maalum ya maandalizi ya mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu ya Simba na wapenzi wa timu ya Yanga itakayofanyika mwezi Agosti 2016 Mhe. Mussa Azzan Zungu akitoa ufafanuzi juu ya umuhimu wa mechi hiyo yenye lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua tatizo la madawati nchini, kulia ni Mwenyekiti wa (Bunge Sports Club) Mhe. William Ngeleja.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Tulia Ackson akitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya Kuahirisha shughuli za Bunge mapema leo.
( Pichazote na Frank Mvungi-Dodoma)

BALOZI SEIF AFUNGUA SEMINA YA UTAFUTAJI NA UCHIMBAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA ZANZIBAR

0
0

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifungua Semina juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi iliyofanyika katika ukumbi wa juu wa Baraza la Wawakilishi uliopo Mbweni.Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib na wa Pili kutoka Kulia ni Mwakilishi wa Kampuni ya Utafiti wa Mafuta na Gesi asilia ya Rakgas kutoka Nchini Ras Al – Khaimah Bwana Kamal Ataya.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia mada mbali mbali zilizotolewa kwenye Semina juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia.

Mtaalamu wa utafiti na uchimbaji mafuta na gesi kutoka Kampuni ya Rakgas ya Nchini Ras Al – Khaimah Bwana Osama Abdel akityoa mada kwenye semina ya mafuta na gesi ilitotolewa kwa wawakilishi wa Zanzibar.
Mrakibu Msaidizi wa Mafunzo { ASP } Juma Makame wa Pili kutoka kulia mwenye shati la drafti akimpatia maelezo Balozi Seif aliyepo kati kati juu ya harakati za kukamilika kwa matengenezo makubwa ya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi hapo Kikwajuni Mjini Zanzibar.Wa kwanza kutoka Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza, wa kwanza kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Nd. Omar Hassan na nyuma ya ASP Juma Makame ni Msimamizi wa ujenzi kutoka KMKM LCDR Hamad Masoud Khamis.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais w Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza akimueleza Balozi Seif hatua zinazofanywa za kuimarisha eneo la nje ya Ukumbi huo.Picha na – OMPR – ZNZ.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images