Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

MGAHAWA WA KIPEKEE WA PWEZA WAZINDULIWA JIJINI DAR

$
0
0
Mgahawa huu waleta mapishi mapya ya makange ya pweza, kamba (prawns) na ngisi.

Samaki aina ya pweza amekuwa maarufu sana hapa nchini Tanzania, kutokana na ladha yake tamu na faida zake kiafya. Kutokana na umaarufu huo vijana wa kitanzania wameamua kuwa wabunifu zaidi na kuanzisha mgahawa wa kisasa maalum kwa ajili ya mapishi ya pweza, kamba (prawns) na ngisi unaoitwa Pweza Cafe.

Akiongea na mwanidishi wetu, mmoja wa wamiliki wa mgahawa huo bwana Alfred Kiwuyo alisema, "Sisi wenyewe ni wapenzi wa supu na nyama ya pweza, kamba (prawns) na ngisi lakini mazingira ya awali ya kuuza vyakula hivi kwenye vituo vya daladala na makutano ya barabara kadhaa hapa jijini yalikuwa yanatukatisha tamaa hasa ukizingatia usafi na mapishi yenyewe haukuwa wa kuridhisha sana. 

Sasa tukajiuliza swali je, haiwezekani kuwa na sehemu ya kisasa zaidi ya kuuza pweza, ngisi na kamba (prawns) na kukawa na mapishi zaidi ya haya. Ndipo tukaamua kuanzisha mgahawa huu ambapo tunapika mpaka makange ya pweza, prawns (kamba) na ngisi."
Muonekano wa Pweza Cafe kwa nje.

Vivyo hivyo akiongea na mwandishi wetu mmoja wa wateja waliofika kwenye mgahawa huo wa kipekee nchini alisema, "Mimi nimekula makange ya pweza na ni mara yangu ya kwanza na nimeyapenda kwa kweli, ni matamu. Kwa mara ya kwanza nilivyosikia makange ya pweza nilishtuka kwanza nikasema lazima niyaonje kwa kuwa tumezoea kula makange ya kuku,ng'ombe, na mbuzi lakini sijawahi kuonja makange ya pweza."

Watafiti wa masuala ya kiafya wanasema, gramu 100 za nyama ya pweza ina madini na vitamini za kutosha kwa mahitaji ya mwili wa binadamu kwa siku. Kwa mfano kiwango hiki cha nyama ya pweza kinampatia mwanadamu mahitaji yake ya siku ya madini ya chuma, seleniamu na vitamini B-12. Madini haya na Vitamini hizi ni muhimu katika kuusaidia mwili kupambana na magonjwa,kutengeneza seli hai nyekundu za damu na kuhakikisha ubongo unafanya kazi yake vizuri.

Makange ya Prawns yakiwa tayari kwa ajili ya mteja Pweza Cafe.

Kuanzishwa kwa Pweza Cafe iliyopo nyuma ya jengo la tume ya taifa ya Sayansi na teknolojia, Kijitonyama ni mfano wa kuigwa kwa vijana wabunifu na wenye ndoto za kuwa wajasiriamali nchini hivyo basi ni muhimu kwa vijana wengine kuangalia ni biashara zipi zinaweza kuboreshwa katika jamii yetu na kutengeneza ajira kwa vijana wengine zaidi.

Unaweza kufuatilia zaidi kuhusu mgahawa huu kwa kutembelea tovuti yao: https://www.instagram.com/pwezacafe/
Rosti ya prawns inayopatikana Pweza Cafe.

TRA yazidi kuboresha timu ya kutoa elimu ya kodi, yazindua Jumuiya ya Wanafunzi wa Kodi IFM

$
0
0
Katika kuhakikisha kunakuwa na wasomi ambao wanakuwa na elimu kuhusu kodi, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imefanya uzinduzi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kodi (Student Tax Association) katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambapo wanachama hao watatumika kutoka elimu kwa wananchi wengine kuhusu kodi.

Akizungumza katika uzinduzi wa jumuiya hiyo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alisema malengo ya kuwa na jumuiya za kodi vyuoni ni kuwezesha jamii kupata elimu ya kutosha kuhusu kodi kupitia wanachama wa jumuiya hizo ambao watakuwa wakipatiwa mafunzo kuhusu umuhimu wa kulipa kodi lakini pia kuhudhulia midahalo mbalimbali ambayo itakuwa inazungumzia kodi.

Alisema hatua ya kuanzisha jumuiya hizo imekuja baada ya kuwa na vilabu katika shule za msingi na sekondari nchini na sasa wakaona kuna umuhimu wa kuwa na wanachama kutoka vyuo vya elimu ya juu ili wawe mabalozi wa TRA ili kusaidia utoaji wa taarifa kuhusu kodi lakini pia na wao kutambua umuhimu wa kodi ili hata baada ya masomo yao waweze kuwa walipa kodi wazuri.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wakati wa uzinduzi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa kodi chuoni hapo (Student Tax Association).

"Tulianzisha mfumo wa vilabu mwaka 2008 ambapo tuna vilabu 195 kwa Tanzania Bara na Zanzibar na katika vilabu hivyo tuna wanachama 15,520 hivyo tukaona sasa ni muhimu kuwa na wanachama kutoka vyuoni ili nao waweze kupata elimu kuhusu kodi,

"Wanachama wa jumuiya hizi watakuwa na shughuli ya kutoa elimu kwa watu wengine ambao hawana elimu ya kodi, kuandaa wataalum wa elimu ya kodi kwa miaka ya baadae na hata walipa kodi wa baadae kwani tayari watakuwa wanafahamu umuhimu wa kodi kwa maendeleo ya taifa," alisema Kayombo.
Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kodi IFM (ISTA), Amon Ojode akielezea jinsi ambavyo wanafunzi wa IFM watanufaika na uwepo wa jumuiya hiyo chuoni hapo.

Nae Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kodi IFM, Amon Ojode alisema kuwa ni fursa ya kipekee kwa wanafunzi wa chuo hicho kupata nafasi ya kuwa na jumuiya ya kodi na zaidi ni wanafunzi ambao wanajifunza masomo yanayohusiana na kodi hivyo wanaamini watakuwa wawakilishi wazuri wa TRA.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wakati wa uzinduzi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa kodi chuoni hapo (Student Tax Association).
Waziri wa Afya na Mambo Yote kwa Ujumla katika serikali ya wanafunzi wa IFM (IFMSO), Suleiman Kahumbu akizungumza katika uzinduzi huo.
Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Diana Masalla akizungumzia kodi wakati wa uzinduzi wa jumuiya hiyo.
Baadhi ya wanachama wa Jumuiya wa Wanafunzi wa Kodi IFM na wanafunzi wa chuo hicho waliohudhuria uzinduzi wa jumuiya chuoni hapo.



Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ashiriki kampeni ya Media Car Wash mjini Dodoma leo

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma .
 Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson ameshiriki harambee ya kuchangia waandishi wa habari kwa ajili ya kuwakatia Bima ya Afya “Media Car Wash For Health” iliyofanyika leo katika viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma ambapo amechangia jumla ya shilingi milioni 5 ili kuokoa maisha ya waandishi wa habari. 

 “Kuna umuhimu mkubwa wa kuwachangia waandishi wa habari kwani wamekuwa na mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya nchi na kuhamasisha amani ya nchi, kwa kutambua umuhimu wao nitachangia shilingi 5,000,000 ili iweze kuwakatia Bima ya Afya,” alisema Mhe.Dkt. Tulia. 

 Licha ya kuchangia fedha hizo Mhe. Tulia aliosha baadhi ya magari ya waheshimiwa wabunge kwa ajili ya kuchangia harambee hiyo ambapo kila mbunge aliyeoshewa gari yake alichangia shilingi 100,000 ambazo moja kwa moja ziliingia katika mfuko wa kuokoa maisha ya waandishi wa habari kwa kuwakatia Bima ya Afya. 

 Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendelea ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla amechangia shilingi 1,000,000/= ambayo nayo inaenda kusaidia waandishi wa habari ili waweze kukatiwa Bima ya Afya. 

 Lengo la harambee hiyo ni kukusanya zaidi ya shilingi milioni 200 ambazo zitatumika kuwakatia Bima ya afya zaidi ya waandishi wa habari 1000 hapa nchini.  Aidha harambee hii ni ya pili, harambee nyingine kama hii ilifanyika mwaka 2015, viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kukusanya shilingi milioni 30 ambazo zilisaidia kugharamia matibabu kwa waandishi watatu waliokuwa wanaugua kwa kipindi kirefu.​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​
   Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ashiriki kampeni ya Media Car Wash mjini Dodoma leo. Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akiosha gari la Mbunge wa Nanyamba, Abdallah Chikota wakati wa kampeni ya Media Car Wash ya kuchangisha fedha za kusaidia wanahabari kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, kwenye Uwanja wa Jamhuri  mjini Dodoma

Mwenyekiti wa Bunge Sports, William Ngeleja akisalimiana na Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani wakati wa harambee ya kuosha magari kupitia kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. 


Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’, Benjamin Thompson akizungumza na baadhi ya wabunge na wageni mbalim bali kuelezea lengo la kampeni hizo asubuhi njini Dodoma. 


Mwenyekiti wa Bunge Sports, William Ngeleja (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza kuwapongeza waandaaji wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ asubuhi katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani.
 
Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto (kushoto) na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima (kulia) wakishiriki zoezi la kuosha magari kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ Dodoma leo.




Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel na Mkongwe wa Bongo Fleva Inspector Haroun wakiosha moja ya magari yaliofika kuoshwa kwa ajili ya harambee ya kuosha magari kupitia kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. 

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Orodha Ya Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Ufundi Kwa Mwaka 2016 haya hapa

$
0
0

TAMISEMI inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2016.

Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali. Jumla ya wanafunzi 65,720 wakiwemo wasichana 29,457 na wavulana 36,263 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi.

Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 34,064 wakiwemo wasichana 13,466 na wavulana 20,598 sawa na asilimia 52 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi 30,897 wakiwemo wasichana 15,445 na wavulana 15,452 sawa na asilimia 47 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara na wanafunzi 759 wakiwemo wasichana 220 na wavulana 539 sawa na asilimia 1 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Ufundi.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2016 wataanza muhula wa kwanza tarehe 11 Julai, 2016 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule.

Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 24 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.

Imetolewa na Katibu Mkuu,
OR-TAMISEMI

 

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA MPANGO WA KITAIFA WA KITUO CHA MAWASILIANO CHA JESHI LA POLISI (CALL CENTRE) JIJINI DAR LEO

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua kituo cha mawasiliano ya polisi (Call centre) katika kituo cha Kati jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi. .Pamoja naye ni Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Ndani Meja Jenerali Projest Rwegasira, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizindua Kituo kidogo cha Polisi kinachohamishika wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi (Call Centre) katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam.. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizindua Kituo kidogo cha Polisi kinachohamishika wakati wa uuzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi (Call Centre) katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam.. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua kituo cha mawasiliano ya polisi (Call centre) katika kituo cha Kati jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi. .Pamoja naye ni Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Ndani Meja Jenerali Projest Rwegasira, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Maguguli akisimama wakati wa wimbo wa Taifa wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Sehemu ya wananchi na wadau waliohudhuria uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Juni, 2016 amezindua kituo cha mawasiliano cha Jeshi la Polisi ambacho kitarahisisha utoaji wa taarifa za uhalifu na kuharakisha askari polisi kufika katika eneo la tukio.


Kituo hicho cha kwanza kuanzishwa na Jeshi la Polisi hapa nchini kipo katika kituo kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam na kinafanya kazi kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano ya simu na mfumo wa utambuzi wa eneo (GPS) ambapo askari polisi waliopo katika kituo cha mawasiliano watakuwa wakipokea simu kutoka kwa wananchi wanaotoa taarifa za matukio ya uhalifu na kisha kuwaelekeza askari walio jirani ili wafike eneo la tukio na kukabiliana na wahalifu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali (IGP) Ernest Mangu amemueleza Rais Magufuli kuwa kituo hicho kina uwezo wa kupokea simu 18 kwa mpigo kutoka kwa watu wanaopiga simu ya bure namba 111 au 112 kwa ajili ya kutoa taarifa za uhalifu na kwamba lengo la jeshi hilo ni kuhakikisha askari wanafika eneo la tukio ndani ya dakika 15.

IGP Mangu ameongeza kuwa kituo hicho kimeanzishwa kwa msaada kutoka benki ya CRDB iliyotoa shilingi milioni 320, kitaanza kutoa huduma tarehe 01 Julai, 2016 kikianzia katika mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Kanda maalum ya Dar es salaam na polisi imejiwekea malengo ya kuwa na vituo kama hivyo nchi nzima ifikapo mwaka 2019.

Akizungumza katika uzinduzi wa kituo hicho, Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuanzisha mradi huo na ameahidi kuwa serikali itahakikisha inaunga mkono mpango huo ikiwa ni pamoja na kulifanyia kazi ombi la kununuliwa helkopta itakayorahisisha zaidi ufikaji eneo la tukio.

Aidha, Rais Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi kuwanyang’anya silaha wahalifu kabla hawajawadhuru raia na kupora mali zao ama kusababisha mauaji, na amewataka viongozi wa jeshi hilo kuwazawadia askari wanaofanya kazi nzuri ya kupambana na wahalifu.

Dkt. Magufuli pia ametaka jeshi la polisi lisimame imara kuhakikisha serikali inatekeleza ahadi zake kwa wananchi zikiwemo upatikanaji wa maji na huduma nyingine za kijamii na kwamba hatarajii kuona mtu yeyote anafanya vitendo vitakavyosababisha ahadi hizo kutotekelezwa.

Katika hatua nyingine, Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi kubwa anazozifanya katika kuiongoza nchi.

Mufti Mkuu Sheikh Aboubakar Zubeir Ali ametoa pongezi hizo jana jioni tarehe 24 Juni, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam katika futari iliyoandaliwa na Rais Magufuli na akatumia nafasi hiyo kuwasihi Waislamu na watanzania wote kwa ujumla kukataa vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani.

“Niwahusie ndugu zangu watanzania wote, kwamba amani ni kitu muhimu tuitunze amani tuliyokuwa nayo, tuienzi amani tuliyonayo, na hapo tutakuwa tunaisadia serikali na tutakuwa tunamsadia Mhe. Rais katika kuilinda amani” Amesema Mufti Mkuu.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
25 Juni, 2016.
 
Sehemu ya wananchi na wadau waliohudhuria uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph akihutubia uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi tuzo ya ufadhili Mkurugenzi Mtendaji wa TBA Bw. Elius Mwakalinga wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi tuzo ya ufadhili Bi. Edna Rajabu wa kwa niaba ya Shirika la Utangazaji la TBC wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo katika mabanda mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi (Call Centre) katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam.. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.

Rais Dkt MAGUFULI alitaka Jeshi la Polisi Nchini Kuwanyang'anya Silaha Majambazi

Taarifa ya Msiba wa Mwenyekiti wa Bodi ya SUMATRA

$
0
0
index 
MAREHEMU PROF. IDDI S.N. MKILAHA

Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA anasikitika kuufahamisha umma kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SUMATRA Prof. Iddi S.N. Mkilaha amefariki dunia ghafla usiku wa tarehe 24 Juni, 2014 Nyumbani kwake eneo la Boko, Dar es Salaam.

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa Marehemu, Boko, Dar es Salaam. Tunaomba tuungane na Familia ya Marehemu Prof. Mkilaha katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya msiba huu mkubwa.

Mkurugenzi Mkuu

SUMATRA

25 Juni, 2016

MASAUNI AKABIDHI MSAADA WA PAMPU NA KUKAGUA MIRADI JIMBONI KIKWAJUNI

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi wa Operesheni za Kiufundi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar, Maulidi Hassan Khamisi(kulia), bomba za pampu ya maji itakayotumika kuunganisha mtandao wa maji .Mradi huo una umbali wa kilomita 3.5. ukiwa na lengo la kutatua kero ya maji jimboni hapo.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia), akiangalia mafundi wakiweka tuta barabarani wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa barabara katika jimbo hilo ikiwa na lengo la kutimiza ahadi za ujenzi wa barabara kwa wananchi wa jimbo hilo.
Mhandisi wa Mradi wa Uwekaji wa Taa za Barabarani katika Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar, Ephantus Mathi (kushoto)kutoka Kampuni ya Central Electrical, akitoa maelezo juu ya mradi huo kwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia). Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salum Jazeera.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wataalamu wa Mradi wa Uwekaji Taa za Barabarani katika Jimbo la Kikwajuni.
Mafundi kutoka Kampuni ya Central Electrical wakiendelea na uwekaji wa nyaya za umeme katika moja ya nguzo ya taa katika mitaa ya Jimbo la Kikwajuni ikiwa ni ukamilishaji wa ahadi za Mbunge wa Jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni.

Mh.January Makamba Ashiriki Mahafali ya 24 ya Chuo cha Biblia mkoani Tanga

$
0
0
Mhe.January Makamba(MB),Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira ) ameitumia Siku ya Tarehe 25 /6/2016 kushiriki katika mahafali ya 24 ya chuo cha biblia Vuga  (VUGA BIBLE )kilichopo katika halmashauri ya Bumbuli mkoani Tanga.  Vilevile Mhe.January Makamba alipata fursa ya kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo inayofanywa na chuo hicho,Pia  aliupongeza uongozi wa chuo kwa kutoa elimu mbali mbali kwa wananchi waishio karibu na chuo na bumbuli kwa ujumla.
 Mhe.January Makamba Akiwasili chuoni hapo huku akisalimiana na wenyeji  
 Mh Makamba akijifunza namna ya utengenezaji wa Mizinga ya nyuki kwa kutumia udongowa mfanyanzi,mizinga hiyo inauwezo wa kudumu miaka 80-100. 
Mh Makamba akielekezwa jambo huku akijifunza  historia ya chuo hicho kwa njia ya picha.
 Akitazama baadhi ya kazi za mikono za kikundi cha wakina mama wa Upendo,kikundi hicho kimepata mafunzo chuoni hapo. 
 Mh Makamba akifuruhia jambo kwa pamoja na Wana kikundi hao. 
Picha zote na Imani Selemani Nsamila

WATUMISHI eGA WAASWA KUBORESHA MIFUMO YA TEHAMA KUONGEZA UKUSANYAJI WA MAPATO NDANI SERIKALI.

$
0
0

k1 
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki akiongea na Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) (hawapo pichani) wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.k2Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabiri Bakari  akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki ili aweze kuzindua Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairukik3Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Long’ida Oltetiai akitoa taarifa ya tawi hilo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki.
k4k6 
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.k7 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) mara baada ya uzinduzi wa baraza hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

——————————————————-
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) wameaswa kuweka vipaumbele na mikakati ya kusimamia mifumo ya TEHAMA inayoboresha utendaji kazi na kutoa huduma ili kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ndani ya Serikali.Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati akizindua baraza la wafanyakazi la Wakala hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

“Nataka mbuni na kutengeneza mifumo tumizi mipya pamoja na kuiboresha mifumo tumizi iliyopo ili kuongeza tija kwenye sekta za kimkakati hususan sekta za afya, kilimo, utalii, elimu, viwanda na biashara” alisema Kairuki.Waziri Kairuki aliyataja maeneo mengine ambayo yanapaswa kuboreshwa katika ukusanyaji na kutiliwa mkazo katika ukusanyaji wa mapato kuwa ni pamoja na sekta za fedha, rasilimaliwatu, ardhi na utambulisho wa taifa.

Hatua hiyo ya eGA ya kuboresha mifumo ya TEHAMA itasaidia Serikali kuimarisha uwezo wake wa kuwa na taarifa juu ya mifumo yake na kukidhi mapato yake na amewataka watumishi hao wazidishe kasi ya utendaji kazi ili kuendana na kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya “Hapa Kazi Tu”.

Aidha, watumishi hao wamesisitizwa kuwa kuundwa kwa baraza hilo la wafanyakazi ni moja ya nyenzo ya kuishauri Serikali katika ngazi ya taasisi katika usimamizi wa kazi na rasilimali, utekelezaji wa majukumu, kulinda haki na wajibu waajiri na wafanyakazi, kutoa ushauri kuhusu kujenga hali bora za kazi na maslahi na kusimamia haki na usatawi katika sehemu za kazi.

Akizungumzia utendaji kazi wa Wakala hiyo, Waziri Kairuki amesema kuwa hatakubali kuona Wakala hiyo kuwa ni sehemu ya tatizo kwenye utendaji kazi wa kila siku bali watumishi wafanye kazi kwa weledi na kuwa na mchango katika kuzipatia suluhisho changamoto zinazoikabili Serikali kwa sasa.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabiri Bakari alipokuwa akimkaribisha Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma alisema kuwa ofisi yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa eneo la ofisi ambapo hadi sasa wanatumia gharama kubwa katika kukodisha jengo ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo.Dkt Bakari alitaja changamoto nyingine kuwa ni ongezeko la tishio la usalama mtandaoni kutokana na ukweli kuwa kadiri Serikali inavyozidi kuhamia mtandaoni, hali ya uhalifu nayo inahamia mtandaoni.

Katika kutimiza majukumu yake, hadi sasa Wakala ya Serkali Mtandao ina wafanyakazi wapatao 94 ambapo inatarajiwa kuwa jumla ya watumishi 126 mara Serikali itakapotoa kibali cha kuajiri watumishi wapya.Wakala hiyo imejenga historia mpya ya kuwa na viongozi wa kwanza wa baraza hilo ambapo Donald Samwel amechaguliwa kuwa Katibu wa Baraza kwa kura 29 zilizopigwa za wajumbe wakati Dianah Mlokozi naye ameingia kwenye historia hiyo kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Msaidizi wa baraza hilo.

Baraza la wafanyakazi la eGA limezinduliwa kwa mujibu wa kutekeleza Sera ya kuwakilisha wafanyakazi mahala pa kazi kkama ilivyoelekezwa kwenye sheria ya majadiliano katika utumishi wa Umma na sheria ya ajira na mahusiano kazini Na. 6 ya mwaka 2004.

KAMATI YA MASHINDANO NA USAJILI YA COASTAL UNION YAWEKA BAYANA MIKAKATI YAO

$
0
0

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili katika
Klabu ya Coastal Union,Hemed Aurora akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo kujadili masuala ya usajili na mashindano kilichoketijuzi kwenye ukumbi wa makao makuu ya klabu hiyo,kushoto ni mjumbe wa kamati hiyo,Abdallah Zuberi,kulia ni Hussein Chuse na anayefuatia ni
Katibu Mkuu wa Klabu ya Coastal Union Salim Bawaziri,

Mjumbe wa Kamati ya Mashindano na Usajili ya Klabu ya Coastal Union,Steven Mguto akiuliza swali wakati wa kikao cha kamatihiyo kujadili masuala ya usajili na mashindano kilichoketi juzi kwenye ukumbi wa makao makuu ya klabu hiyo

Katibu Mkuu wa Klabu ya Coastal Union,Salim Bawaziri akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kikao hicho

Kamati hiyo inaundwa na wajumbe wengine ambao ni Abdi Masamaki,Salim Bawaziri,Hemed Mbaruku,Hussein Chuse,Abdallah Zuberi “Unenge” na Juma Mgunda ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia mashindano na usajili.

Picha kwa hisani ya kitengo cha Mawasiliano cha timu ya Coastal Union.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWATAKA WAISLAMU NCHINI KUDUMISHA AMANI, UPENDO NA MSHIKAMANO

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa tafrija ya Futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waisalm wa Tanzania (Bakwata) iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Kinondoni Muslim ambapo alimuwakilisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kuwahimiza viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) waendelee kuombea amani katika Taifa na kukemea ipasavyo vitendo vya uhalifu katika jamii ya Kitanzania.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir akizungumza wakati wa tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania ambapo alisema uongozi wa sasa wa BAKWATA umedhamiria kudumisha umoja,upendo na mshikamano baina ya Waislamu wote nchini, Tafrija hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyemuwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania.
Sehemu ya wageni waliohudhuria tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislam katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jopo la Masheikh Sheikh Suleiman Amran Kilemile akitafsiri moja ya aya ya Quran inayojenga na kuimarisha umoja na mshikamano kwa waislam.
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Shekh Alhad Mussa Salum akitoa utambulisho wa wageni wa jumuiya mbali mbali za waislam waliohudhuria tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Viongozi wa Wanawake Waislamu Tanzania wakisikiliza kwa makini nasaha za viongozi mara baada ya kufuturu katika tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania.

======  =====  =======
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JOHN MAGUFULI amewahimiza viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania- BAKWATA- waendelee kuombea amani katika taifa na kukemea ipasavyo vitendo vya uhalifu katika jamii ya Kitanzania.

Kauli hiyo ya Rais imetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN kwa niaba ya Rais katika tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania- BAKWATA- katika uwanja wa shule ya sekondari ya KINONDONI MUSLIM jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema jamii yeyote inayolelewa na kukua katika misingi ya kufuata maandiko ya Mwenyezi Mungu ni vigumu kujiingiza kirahisi katika vitendo vinavyomchukiza Mungu vikiwemo vitendo vya uhalifu.

Rais MAGUFULI pia amewatakia kheri waumini wote wa dini ya kiislamu kote nchini katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa upande wake, Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh ABUBAKAR ZUBEIR ameipongeza serikali kwa hatua inazochukua katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu hapa nchini na kusisisita kuwa Viongozi wa BAKWATA na wataendelea kushirikiana na serikali katika kukemea vitendo viovu katika jamii kama hatua ya kuhakikisha vitendo vya uhalifu vinakoma hapa nchini.

Mufti wa Tanzania pia ametoa rai kwa waislamu wote nchini wadumishe umoja,upendo na mshikamano miongoni mwao katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na hata baada ya mfungo kama kitabu kitukufu cha QUR’AN kinavyoelekeza.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais.
26-Jun-16


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI



GARI ZITAKAZOKAMATWA KWA KUHUSIKA NA USAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA KUFILISIWA-SMZ

$
0
0
Na Miza Kona Maelezo – Zanzibar .

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepanga mikakati maalum ya kuzifilisi gari zitazokatwa au kuhusika uingizaji wa dawa za kulevya kwa lengo la kudhibiti uingizaji, usambazaji na utumiaji wadawa hizo nchini .

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed huko Mnara wa kumbukumbu Kisonge katika Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Usafirishaji na Matumizi ya Dawa za Kulevya Duniani amesema serikali haitamuonea muhali yoyote atakae husika na uingizaji wa biashara ya dawa za kulevya kwa lengo la kutomeza janga hilo linathiri jamii na kupoteza nguvu ya Taifa.

Amesema wafanyabiasha wa bidhaa hiyo hawalitakii mema Taifa kwani wao ni wahujumu wanaorejesha maendeleo ya nchini wanawaumiza vijana na watoto na kupoteza nguvu kazi ya Taifa hivyo wanahitaji kufichuliwa kwa nguvu bila ya kuwaonea muhali.

Ameeleza kuwa tatizo la utumiaji wa dawa za kulevya linamtoa mtu katika hadhi yake ya ubinadamu kwa kutengwa na jamii na kumsababishia madhara makubwa ikiwemo maradhi ya Ini, Figo, Ukimwi na Ugonjwa wa akili pamoja na kupoteza viungo muhimu vya mwili.

Aidha Waziri Aboud amesema kuwa kuna baadhi ya viongozi wa siasa wanawatumia vibaya madaraka yao kwa maslahi yao binafsi kuwatumia vijana kinyume na sheria jambo ambalo linachangia vijana hao kijiingiza katika vikundi viovu na hatimae kujiingiza katika utumiaji wa dawa hizo kwa kuwapotezea malengo na kuiathiri jamii.

Waziri huyo ameeleza kuwa takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya watu milioni 200 Duniani wameathitika na utumiaji wa dawa za Kulevya ambapo Zanzibar watu 10000 wameathirika na utumiaji wa dawa hizo kati ya 3200 wanatumia niia ya kujidunga sindano .

Hata hivyo Waziri huyo amewata wazee na walezi kuwalea vyema watoto wao kwa kuwafunza maaadili mema ili kuweza kujiepusha na kujiingiza katika vikundi viovu sambamba na kuwapokea walioathirika na utumiaji wa dawa za kulevya kwa kuwajali , kuwakubali, kuwasidiana pamoja na kuwapa ushauri kwa lengo la kuwaondolea matatizo yao ili wasirejee tena katika janga hilo.

Nae Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Moh’d Mahmoud ameitaka jamii kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kuwadhiti janga hilo kupitia njia zote zinatumika kupitishia dawa hizo kwa kukata minyororo iliomo katika sehemu husika kwa lengo la kutokomeza uingizaji wa bidhaa haramu nchini.

Akitoa taarifa ya Jeshi la Polisi Mngwali Ussi amesema jumla ya kesi 79 zimeripotiwa kati ya kesi saba zinahusiana na dawa za kulevya ambazo zinaendelea mahakani na kesi 72 za makosa tofauti ambazo ziko chini ya upelele wa polisi.

Wakitoa ushahidi vijana waliopata nafuu wameionya jamii wasiwaachie watoto wao kukaa katika vikundi na kujiepusha na marafiki waovu kwani ndio kishawishi kikubwa kinachopelekea watoto hao kujiingiza katika dimbwi la dawa hizo

Siku ya Kupambana na Usafirishaji na Utumiaji wa Dawa za Kulevya Duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 26 Juni ambapo Ujumbe wa Mwaka huu Tuwajali, Tuwasikilize Watoto na Vijana.

SERENGETI BOYS YAONGOZA GOLI 3-0 DHIDI YA SECHELLES UWANJA WA TAIFA,MPIRA UNAENDELEA.

$
0
0
 Mpira umeanza kwa kasi na katika dakika 10 za mwanzo Serengeti Boys wanaonekana kutawala mpira na katika dakika ya 15 Nickson Kibabage anaiandikia Serengeti goli la kwanza akitumia maridadi mguu wake kushoto na kutinga nyavuni.

Dakika ya 22, Ibrahim Ally anaiandikia Stars goli la pili ikiwa ni shambulizi lililoanzia katikati ya uwanja.Mpira umeonekana kuchezwa upande mmoja na Serengeti kukosa nafasi nyingi za wazi.Mpira ni mapumziko na Serengeti wanatoka wakiwa mbele kwa goli 2.

Kipindi cha pil kimeanza na timu zote kuwa makini ambapo dakika ya 60, Ally Msengi anaiandikia Serengeti goli la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Shelisheli kuushika ndani ya 18 na mwamuzi kuamuru penati.
   
Mchezo kati ya Serengeti Boys na Sechelles unaopigwa hivi sasa uwanja wa Taifa, hadi sasa Serengeti Boys inaongoza kwa bao 3-0. 
 Wachezaji wa timu ya Serengeti Boys wakishangilia mara baada ya kupata goli. 
Mchezaji wa timu ya Serengeti Boys Rashid Mohamed Chambo akimchomoka  mchezaji wa timu ya Sechelles,katika mchezo wao unaopigwa hivi sasa uwanja wa Taifa, hadi sasa Serengeti Boys inaongoza kwa bao 3-0.
 Wachezaaji wa timu ya Serengeti Boys wakionesha umahiri wao dhidi ya timu ya Sechelles
Mchezaji wa timu ya  Sechelles akiwa amelelala chini katika nginja ngija ya kusaka magoli dhidi ya timu ya Serengeti Boys ,katika mchezo wao unaofanyika hivi sasa uwanja wa Taifa, hadi sasa Serengeti Boys inaongoza kwa bao 3-0.

RAIS WA VoWET MAIDA WAZIRI AZINDUA UMOJA WA WANAFUNZI WA BIASHARA(BAA) ATOA SEMINA YA UJASILIAMALI, (TIA) DAR ES SALAAAM

$
0
0

Rais wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction Limited Bi. Maida Waziri akiongea na wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu TIA wakati wa uzunduzi rasmi wa umoja wa wanafunzi wa Biashara (BAA), ambapo aliwahimiza elimu wanayoipata wasiitumie kwenda kuombea kazi tuu lakini pia waitumie kwa ajili ya kufanya ujasiliamali kwa kujiajili wao wenyewe.

Rais wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction Limited Bi. Maida Waziri akikata keki ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa umoja huo.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa BAA Gwamaka Andrew (Kushoto) akimmkabidhi Cheti cha Shukurani Mgeni rasmi Bi. Maida Waziri (Kulia).


Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu (TIA) wakiwa katika uzinduzi wa BAA.Picha zote na Fredy Njeje

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHITIMISHA MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR'AN TUKUFU YA KIMATAIFA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Juni 26, 2016 kuhitimisha Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya kimataifa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es slaam 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubery bin Ally baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam kuhitimisha Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa Juni 26, 2016. Katikati ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhadi Mussa Salum.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na baadhi ya wageni  kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Juni 26, 2016 kuhitimisha Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya kimataifa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es slaam.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipohitimisha Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Juni 26, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na watoto wadogo kuliko wote walioshiriki katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam Juni 26, 2016.Watoto hao ni Abuzar Kholidi wa Tajikistan (Kulia) na Ahmad Abdullah Al-Azhar wa wa Bangladesh. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Mkubwa na Wanawe watoa msaada Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke

$
0
0
Baadhi ya vijana wanaounda kundi la Mkubwa na Wanawe Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke wakati wa tukio hilo lililofanyika leo Juni 26.2016.Kiongoni wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella, akielezea namna vijana wake walivyoguswa na kuamua kujitolea kwa ajili ya watu wenye kuhitaji wakiwemo wa Hospitali hiyo ya Temeke.Kiongoni wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella, akimkabidhi baadhi ya vifaa Daktari wa hospitali hiyo, Rashid Nyumbiage Baadhi ya wasanii wa kundi la Yamoto Band ambao pia wanatoka Mkubwa na Wanawe wakitoa vionjo kadhaa wakati wa tukio hilo.

Kiongoni wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella akishukuru kwa hatua hiyo ya kurudisha fedhila kwa JamiiMsanii Kiongozi wa Kundi la Yamoto Band,"Aslay Isihaka"-Dogo Aslay akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake wa Yamoto pamoja na kundi hilo la Mkubwa na Wanawe.
Kituo cha kuvumbua na kuendeleza vipaji vya muziki cha Mkubwa na Wanawe, kimetoa msaada ya vifaa vya tiba na vifaa mbalimbali vikiwe vile vya usafi, dawa za meno, sabuni, maji na juisi kwa wodi ya Watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Jijini Dar es Salaam.

Awali akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, kiongoni wa kituo hicho, Said Fella, amesema wameamua kufanya hivyo kutokana na kuguswa na changamoto zinazoikabili hospitali hiyo ya Temeke ambayo pia ni majirani zao ambapo pia amebainisha kuwa kundi hilo limekuwa likifika Hospitalini hapo kuchangia misaada mbalimbali.

Said Fella ameongeza kuwa, alishauriwa na vijana wake waliopo katika kituo chake kuona ni vipi wanaweza kushiriki katika shughuli yoyote ya kijamii kwa kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na wote kwa pamoja kukubaliana kutoa msaada huo.

“Nasi pia ni kama wagonjwa watarajiwa, hivyo tumeona ni vema kuja kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba kama tulivyoshauriwa na wenyeji wetu, tukiwa pamoja na mabalozi wetu. Msaada tuliotoa una thamani ya Sh milioni tatu,” alisema Fella.

Akipokea msaada huo, mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo, Rashid Nyumbiage, alikishukuru kituo hicho kwa kuwakumbuka akiwataka wasanii na viongozi wake pamoja na wengineo wenye nafasi kuendelea kuwakumbuka.

“Vifaa tulivyoletewa ni Paso-Oximeter cha kupimia kiwango cha oksijeni mwilini, HB Culvate cha kupima kiwango cha damu, mashine ya BP ambayo kazi yake ni kufahamu kama presha ya damu (BP) imeshuka au la na Mashine ya Nebulizer yenye kazi ya kuwapimia dawa wagonjwa wa pumu,” alisema Nyumbiage.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake takribani 50 alioambatana nao hospitalini hapo, msanii anayeunda kundi la Yamoto, Dog Aslay, alisema kuwa wamefarijika kuwasaidia wagonjwa akiahidi kufanya hivyo wakati mwingine watakapopata nafasi.

Tukio hilo la aina yake kwa kundi hilo ambalo ufanya mara kwa mara katika kutembelea jamii na kusaidia misaada, limeweza kupongezwa na baadhi ya ndugu wa wagonjwa na wagonjwa wenyewe kwa kueleza kuwa ni tendo la kuigwa na kila mmoja wetu hasa wasanii ambao ni kioo cha jamii.


Kiongoni wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella akionyesha moja ya vifaa hivyo vya tiba
Daktari wa hospitali hiyo, Rashid Nyumbiage akionyesha moja ya kifaa huku akielezea namna kinavyofanya kaziMakabidhiano yakiendelea..
Vijana na Mabalozi wa kundi la Mkubwa na Wanawe wakibeba baadhi ya vifaa walivyotoa msaada hospitalini hapo.
Wakielekea wodini...
Amani James a.k.a Chiba wa kundi la Yamoto Band akitoa msaada katika tukio hiloMsanii Kiongozi wa Kundi la Yamoto Band,"Aslay Isihaka"-Dogo Aslay akimfariji mmoja wa Watoto wanaopatiwa matibabu katika hospitali hiyo ya Temeke
Said Fella (kulia) na Mh. Temba (kushoto) wakielezea jambo wakati wa tukio hilo leo Juni 26
Enock Deogratius 'Enock Bella' akimfariji mtoto
Amani James a.k.a Chiba wa kundi la Yamoto Band aliweza kuwafariji watoto na ndugu wanaouguza watoto wao pale walipomuomba awachezee kidogo kwani imekuwa faraja kwa kumuona kwa mara ya kwanza
Mkubwa na Wanawe..
Mkubwa na Wanawe Baadhi ya vijana wanaounda kundi hilo la Mkubwa na Wanawe wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa tukio hilo la kutoa msaada hospitali ya Temeke. leo Juni 26.2016. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

Wabunge wapewa semina juu ya uanzishwaji wa masoko ya bidhaa

$
0
0

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bibi Nasama Massinda akiwasilisha mada leo Mjini Dodoma kwa Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Biashara, Viwanda na Mazingira na Kamati ya Bunge ya Uwekezaji( hawapo pichani)kuhusu uanzishwaji wa Masoko ya Bidhaa hapa nchini ili kuwainua wakulima.
Mkurugenzi wa Usimamizi na Uendelezaji wa Masoko Kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Bw. Godfrey Malekano akijibu hoja za Wabunge (hawapo pichani) kuhusu hatua zinazochukuliwa katika kuwasaidia wakulima kupitia Masoko ya Bidhaa ili waweze kunufaika na bidhaa wanazozalisha.
Mbunge wa Newala Mjini Mhe. George Mkuchika akichangia mada juu ya namna bora ya kuwainua wakulima hapa nchini hasa wanaozalisha Korosho na mazao mengine ya biashara wakati wa semina kuhusu Masoko ya Mitaji na Dhamana iliyofanyika Mjini Dodoma leo.
Baadhi ya Wabunge wakifuatilia mada kuhusu Masoko ya Bidhaa iliyowasilishwa wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo Wabunge wa Kamati ya Biashara Viwanda na Mazingira na Kamati ya Bunge ya Uwekezaji kuhusu mikakati ya mamlaka hiyo kuwainua wakulima hapa nchini.
Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania Bw. Mfaume Juma akijibu hoja za Wabunge kuhusu mikakati ya Bodi hiyo kuimarisha zao la korosho ili liweze kuwainua wananchi kiuchumi wakati wa semina kuhusu Masoko ya Mitaji na Dhamana iliyofanyika Mjini Dodoma leo. (Picha Zote Na: Frank Mvungi – MAELEZO – Dodoma)


Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

Kilimo kinachangia asilimia 26 ya pato la Taifa na kuchangia zaidi ya asilimia 75 ya kipato kwa wananchi waishio vijijijini, pamoja na mchango mkubwa wa kilimo kwenye uchumi wa nchi, wakulima wamekuwa wakipata matatizo mbalimbali ya masoko yenye bei zenye ushindani.

Kwa kuliona hilo Serikali ilipitisha sera ya masoko ya bidhaa mwaka 2014 kwa kuanza na mazao manne ya majaribio ambayo ni, Korosho, Ufuta, Alizeti na Mchele.

Hayo yamesemwa leo, mjini Dodoma na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bibi. Nasama Massinda wakati wa semina kwa Wabunge juu ya uanzishwaji wa masoko ya bidhaa nchini iliyoandaliwa na mamlaka hiyo.

Akieleza kazi kuu za soko la bidhaa Massinda amesema kuwa soko la bidhaa linaleta uwazi wa bei za mazao na mwenendo wa soko, kila mtu ataweza kujua bei ya mazao sokoni ambapo bei zitatolewa kwa vyombo vya habari pamoja na kuondoa ulazima wa wakulima kusafirisha mazao yao toka eneo moja kwenda lingine kutafuta wanunuzi.

“Vile vile soko la bidhaa litasaidia kutoa bei zenye ushindani kwa kuzingatia upatikanaji wa bidhaa na mahitaji ya bidhaa, litaboresha bei ya mazao vijijini kwa kuwa na soko la bidhaa litakalo toa taarifa kwa wakulima wote kuhusu soko, bei na mwenendo wa soko,” alifafanua Massinda.

Kwa upande wake Mbunge wa Nanyamba, Mhe. Abdallah Chikota alilitaka soko hilo kupanua wigo wa uelimishaji kwa kushuka mpaka kwa wakulima na watendaji wa Serikali katika ngazi ya chini kuliko kuishia kwa mawakala ambao wanaweza wasitoe elimu hiyo kama ilivyotarajiwa.

Soko hilo la Bidhaa linalotarajia kuanza Septemba mwaka huu linategemea kumnufaisha mkulima mdogo, wakulima wakubwa, wenye viwanda, wakusanya mazao (ushirika), wauzaji mazao nje, wakopeshaji na vyombo vya fedha pamoja na Serikali kupata mapato kupitia tozo kutokana na uwepo wa takwimu na uwazi.

BREAKING NEWZZZ: Rais Magufuli afanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya na afanya mabadiliko madogo ya Wakuu wa Mikoa

$
0
0




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.

Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 139.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60 ameamua wastaafu.

Mhe. Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.

Katika uteuzi huo, Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya kutokana na utendaji wao mzuri.

Aidha, nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali.

Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa).

BENKI YA CRDB YAFADHILI UJENZI WA KITUO CHA MAWASILIANO CHA JESHI LA POLISI

$
0
0

 Rais John Magufuli akizindua rasmi Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi Dar es Salaam.
 Rais Magufuli akipata maelezo ya namna kituo hicho kinavyofanyakazi.
  Rais Magufuli akipata maelezo ya namna kituo hicho kinavyofanyakazi.Jiwe la Msingi la Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi lililowekwa na Rais Dk. John Magufuli. Kituo hicho kimefadhiliwa na Benki ya CRDB kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 300. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akiteta jambo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Esther Kitoka.
Brass Band ya Polisi ikitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akisalimia na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (wa kili kulia) akifurahia jambo na Naibu wake (kulia), IGP,Ernest Mangu, wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisalimia na Rais John Magufuli.
 Rais John Magufuli akisalimia na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa.
 Mkurugenzi wa Utawala wa Benki ya CRDB, Beatus Segeja akisalimiana na Rais Dk. John Magufuli
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Esther Kitoka akisalimiana na Rais Dk. John Magufuli.
 Wakurugenizi wa Benki ya CRDB wakifuatilia uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei akitoa hotuba yake.
Rais John Magufuli akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei baada ya kutoa hotuba yake. 
 Rais John Magufuli akifurahia jambo wakati akimkabidhi Tuzo ya Ufadhili Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi, uliofanyika katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. ambapo benki hiyo imetoa zaidi ya shs. milioni 300. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba. 
 Rais John Magufulia (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikli. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images