Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

BENKI YA EXIM YAANDAA HAFLA YA FUTARI KWA WATEJA WAKE

$
0
0
 
 Mkuu wa Hazina wa Benki ya Exim Tanzania, Bw George Shumbusho (aliesimama) akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


Baadhi ya wateja wa Benki ya Exim wakishiriki futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

SOBER HOUSE YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KUPIGA VITA MATUMIZI MABAYA YA DAWA ZA KULEVYA.

$
0
0

 Mkuu Wa Kituo  cha Life and Hope Bagamoyo Sober House, Al-Kareem Bhanji aki akizungumza na wananchi (hawapo pichani) waliofika kwenye siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya, jana Mkoa wa Pwani kushoto ni Mkuu Wa Wilaya ya Bagamoyo,Alhaj Majid Hemed Mwanga.
 Mkuu Wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Hemed Mwanga akizungumza na wananchi (hawapo pichani) katika siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya, jana Mkoa wa Pwani kulia ni Mkuu wa Kituo  cha Life and Hope Bagamoyo Sober House,Al-Kareem Bhanji.
 Wananchi wakifatilia mada mbalimbali  kwenye siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya, jana Mkoa wa Pwani.
 Waathirika wa Dawa za Kulevya akiandamana siku ya Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya, jana Mkoa wa Pwani.

 Maandamano yakeendelea.
 Kikundi cha Sana cha Bagamoyo wakiigiza kama Waathirika wa Dawa za Kulevya.
 Mkuu Wa Wilaya ya Bagamoyo,Alhaj Majid Hemed Mwanga akiwa kwenye picha ya  Waathirika wa Dawa za Kulevya.
Mkuu Wa Kituo  cha Life and Hope Bagamoyo Sober House,Al-Kareem Bhanji  akiwa kwenye picha ya  Waathirika wa Dawa za Kulevya
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii
Kituo cha Usaidizi Wa Watu walioathirika na Dawa za Kulevya cha Life and Hope Bagamoyo Sober House leo,June 26,2016 kimeadhimisha siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Matumizi Mabaya ya Dawa za Kulevya.

Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka June 26 lakini kwa Mwaka huu Kituo cha Sober kimeadhimisha siku hiyo Wilayani Bagamoyo.

Akizungumza katika Maadhimisho hayo,Mkuu Wa Wilaya ya Bagamoyo,Alhaj Majid Hemed Mwanga amesema vita vya Mapambano ya Dawa za Kulevya si vya Serikali pekee wala vya mtu mmoja bali ni vita vya kila mtu,ambaye anapaswa kuwajibika katika eneo husika ili kutokomeza kabisa uingizwaji Wa Dawa hizo.

Pia,Mkuu huyo Wa Wilaya ametoa wito kwa Viongozi Wa Dini ,Wananchi pamoja na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kushirikiana kwa pamoja katika kutoa taarifa za kuwafichua waingizaji Wa Dawa hizo ili Serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Amesema,Serikali imeahidi kupatikana kwa eneo kubwa ili kuendeleza kituo hicho na kuwasaidia vijana ambao ndio waathirika wakubwa Wa janga hilo na kuitaka jamii kuwatambua na kuwabaini waathirika wa Dawa hizo.

Kwa upande wake,Mkuu Wa Kituo hicho cha Life and Hope Bagamoyo Sober House,Al-Kareem Bhanji amesema kituo hicho kimesaidia watu zaidi ya 100 mpaka sasa,ambapo ametoa Changamoto za ukosefu wa Majengo kituoni hapo  jambo ambalo limepelekea kwa sasa kulipa kodi kubwa ya pango.

Pia ameiomba Serikali kupatikana Ardhi ya kutosha ili kuweza kuongeza majengo na kukidhi haja ya kupokea Waathirika 200 ikiwa Wanaume 150 na Wanawake 50.

KITWANGA AKABIDHI RASMI OFISI KWA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA, JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) mara baada ya aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (katikati) kukabidhi ofisi kwa Waziri Mwigulu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba akizungumza na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (kushoto) pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo, kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo, mara baada ya Wizara Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto meza kuu) akimsikiliza aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga alipokuwa anazungumza na Waziri huyo pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo, kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo, mara baada ya Wizara Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano ofisini humo.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa pili kulia) alipokuwa anazungumza kabla ya aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (wa tatu kulia) kukabidhi ofisi kwa Waziri Mwigulu. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto), aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga wakifurahi jambo mara baada ya Waziri Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano katika tukio lililofanyika ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dar es salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (wa pili kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. 
Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

SERIKALI YASISITIZA UMUHIMU WA UTAFITI WA KISAYANSI KWENYE SEKTA YA AFYA.

$
0
0

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto, John Michael akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa chuo cha Muhas pamoja na washiriki wa Mkutano Mkuu wa nne wa mwaka wa utafiti wa kisayansi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi  Muhimbili (MUHAS) uliofanyika jijini Dar es Salam mwishoni 
 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto, John Michael akizungumza wakati akifunga Mkutano Mkuu wa nne wa mwaka wa utafiti wa kisayansi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi  Muhimbili (MUHAS) uliofanyika jijini Dar es Salaam .
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi  Muhimbili (MUHAS) Prof Ephata Kaaya akizungumza wakati wa ufungwaji wa Mkutano Mkuu wa nne wa mwaka wa utafiti wa kisayansi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi  Muhimbili (MUHAS) uliofanyika jijini Dar es Salam .
 Baadhi ya washiriki wa wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SERIKALI imesisitiza utafiti wa kisayansi kwa maendeleo ya taifa na kuhamasisha ushirikishwaji wa vijana wengi zaidi katika eneo hilo , ili kujenga taifa lenye vijana watafiti na wataalam wa kutosha.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kupitia hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  John Michael aliemuwakilisha kwenye ufungaji wa  Mkutano wa nne wa mwaka wa utafiti wa kisayansi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi  Muhimbili (MUHAS) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema utafiti wa kisayansi ni muhimu kwa nchi yeyote ikiwemo  Tanzania katika  kuhakikisha inafikia  malengo yake ya maendeleo  ya utekelezaji wa wa malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGS).

Aliongeza kuwa utafiti wa kisayansi ni kiungo muhimu katika kuweza kufikia malengo ya SDGS  kwa kuwa ndio unatoa muongozo wa kisayansi na mipango ya namna ya kuyafikia malengo hayo.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Ephata Kaaya alisema ni muhimu taifa kuanza kuchukua hatua sasa na kuhakikisha mfumo wa kitaifa wa huduma za afya na uchumi  kwa ujumla  unaweza kukabiliana na mizigo wa magonjwa , kwa njia ya utafiti.

Aidha Prof Kaaya aliwapongeza wanafunzi wa shahada ya uzamili na wahitimu wa MUHAS  waliowasilisha mada takribani  ya 70 kati ya 170  katika mkutano huo na tofauti  na mwaka uliopita ambapo asilimia 30 ya mada ziliwasilishwa na wanafunzi.

WATUMIAJI WA UMEME WA JUA WA MOBISOL WAFIKIA 50,000.

$
0
0
Mkurugenzi wa Mobisol Tanzania Henrik Axelsson (Kushoto) akionyesha vifaa mbalimbali vinavyozalishwa na kampuni hiyo wakati wa ufunguzi wa huduma zake wilayani Bagamoyo hivi karibuni. 

Imefanikiwa kufikisha huduma wa wateja robo milioni kanda Afrika Mashariki Kampuni kutoka nchini Ujerumani inayotoa huduma ya kusambaza umeme wa jua na kuuza vifaa vyake imeweza kubadilisha maisha ya familia robo milioni maeneo ya vijijini kuwa na maisha ya kisasa kutokana na kufikiwa nishati ya umeme katika nchi za Rwanda,Tanzania na Kenya. 

 Mobisol,kampuni ya Kijerumani inaoongoza kwa kutoa huduma za umeme wa jua imeweza kufunga umeme wa nishati ya jua kwa familia 50,000 ikiwemo sehemu za biashara katika maeneo wanayoishi wananchi wenye vipato vya chini ambao hawajafikiwa umeme wa gridi ya taifa kwenye nchi za Tanzania,Rwanda na Kenya. Kupitia mpango wake maalumu wa kukopesha unaowawezesha wateja kufanya malipo kwa awamu kupitia simu za mkononi yanaochukua kipindi mpaka kufikia hadi miaka mitatu, wananchi wengi wenye vipato vya chini wameweza kujiunga na kuufurahia mpango huu.Mteja anatakiwa kulipia shilingi 999 kwa siku ambapo akikamilisha malipo atapata umeme wa uhakika wenye nguvu zinazoanzia 80W hadi kufikia 200W kulingana na mahitaji yake kwa matumizi ya vifaa vya nyumbani. 

 Meneja Masoko wa Mobisol Tanzania,Allan Rwechungura amesema jijini Dar es Salaam kuwa mbali na wateja kuunganishiwa umeme wa jua kwa mpango unaoleta unafuu mkubwa pia wanaweza kujipatia vifaa bora vya matumizi kama vile mashine za kukata nywele,vifaa vya muziki (Music system),pasi,feni na vifaa vinavyoweza kuwaongezea wateja vipato mfano chaji maalumu ya kuchajisha simu kibiashara.


 “Mobisol ni mkombozi wa kuondoa tatizo la umeme kwa wateja wasio na uwezo wa kununua vifaa vya kufungiwa umeme wa jua kwa mara moja kwa gharama zinazofikia Dola za Kimarekani 800 ila imewawekea mpango maalumu unaowawezesha kulipia huduma hii kwa awamu.

Dhamira yetu ni kuona huduma hii inaleta mabadiliko kwenye jamii kwa kuboresha maisha ya wananchi na sio kuwasha taa tu ama kuchaji simu”Alisema. Aliongeza kuwa kampuni inatoa ofa ya kufuatilia iwapo wateja wake wanapata huduma ya uhakika kwa kipindi cha miaka mitatu na iwapo kunakuwepo na matatizo yanarekebishwa na wataalamu wake waliobobea katika ufundi wa mitambo inayozalisha umeme wa jua,dhamira kubwa ikiwa ni kubadilisha maisha ya wakazi wa maeneo ambayo hayajafikiwa umeme wa gridi ya taifa hususani maeneo ya vijijini kuwa bora. 

 Rwechungura alisema moja ya malengo ya kampuni pia ni kuwawezesha watoto wanaosoma shule maeneo ya vijini kuweza kujisomea kwa kutumia mwanga wa umeme,kuweza kusikiza redio , kuangalia televisheni na kuperuzi kwenye internet ili wapate taarifa na fursa ya kuelimika “Uwekezaji wetu kwenye sekta hii vilevile umejikita katika utunzaji wa mazingira ikiwemo kuboresha maisha ya wananchi kwa kuwawezesha kufanya shughuli mbalimbali za kuwaongezea vipato kupitia uzalishaji unaofanyika kwa kutumia nishati ya umeme”. 

 Wakati huohuo Rwechungura ameeleza kuwa kwa mara ya kwanza kampuni ya Mobisol itashiriki katika Maonyesho ya kimataifa ya Biashara maarufu kama SabaSaba yanayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.Maonyesho hayo ya biashara yatawawezesha wananchi kujua huduma zinazotolewa na kampuni ya Mobisol nchini ikiwemo kununua bidhaa za kampuni hususani Televisheni bora zenye ukubwa tofauti ambazo zimekuwa zikiwavutia wateja wengi. “Televisheni ni kifaa pekee kinachowawezesha kupatikana taarifa , burudani na kinachounganisha jamii,wakazi wa vijijini kupitia televisheni wanaweza kuunganishwa na dunia nzima,wanahitaji kuishi maisha ya kisasa na sisi tupo kwa ajili ya kubadilisha maisha ao kuwa bora”.

Waganga wa tiba asili watakiwa kujisajili

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
—————————-
Waganga wa tiba asili ambao wamekuwa wakitoa huduma ya tiba pasipo kujisajili wametakiwa kujisajili Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ili waweze kutambulika kisheria.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla ameyasema hayo leo, Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge Viti Maalum Mhe. Zainabu Mussa Bakar juu ya udanganyifu unaofanywa na waganga wa tiba asili wa kutoa dawa feki kwa wagonjwa.

“Waganga wa tiba asili wapo kisheria, ni kweli wapo wanaotoa dawa feki, na wengi wao ni wale ambao hawajasajiliwa, hivyo tumewaagiza kujisajili ili tuweze kuwatumbua na dawa zao ziweze kuhakikiwa na kusajiliwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu,” alifanunua Mhe. Kigwangalla.

Mhe. Kigwangalla amesema kuwa, mganga yoyote atakaye kiuka agizo hilo la kujisajili basi hatua kali zitachukuliwa dhidi yake. Aidha, amesema Wizara iko makini na ufuatiliaji wa dawa feki nchini kwani wanapopata fununu ya uwepo wa dawa feki hutuma kikosi kuchunguza na ikibainika kuwa dawa ni feki basi hatua kali huchukuliwa kwa muhusika.

Aliendelea kwa kusema kuwa, ili kudhibiti uingizwaji wa dawa feki nchini Wizara hiyo hufanya uhakiki wa muda mrefu kuchunguza iwapo dawa inayopendekeza kuingia nchini siyo feki na inafaa kwa matumizi ya binadamu, ikiwa dawa haina madhara yoyote basi inasajiliwa kwa ajili ya kuingia sokoni.

Vilevile Mhe. Kigwangalla amesema kuwa, Wizara imewaagiza waganga wa tiba asili kufunga dawa zao kwa kutumia vifungashio maalum vya madawa ambavyo vitasaidia dawa hizo kuendelea kuwa salama kwa mtumiaji kwa kipindi kilichopangwa kutumika.

MKUTANO WA MASHAURIANO YA KITALAM JUU YA KUANZISHA VITUO BORA VYA UVUVI WAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
Na Mwashungi Tahir- Maelezo Zanzibar

WAZIRI wa Kilimo, Maliaasili Mifugo na Uvuvi Hamad Rshid Muhammed, amesema ipo haja kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika AU kuungana kwa pamoja katika kuangalia soko la ndani katika masuala ya uvuvi ili kukuza uchumi wa nchi hizo.

Akifungua mkutano wa siku mbili wa Nchi wanachama wa Umoja wa Arika AU, wa kujadili namna ya uzalishaji wa samaki, taaluma bora ya uvuvi na namna ya kuwawezesha wavuvi, uliofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Mazizini, Hamad alisema soko la Afrika limekuwa likishuka kutokana na kutokuwa na wataalamu wa kutosha katika sekta hiyo.

Alisema mara nyingi nchi hizo zimekuwa zikijadili suala la kilimo kutokana na kuonekana ndio muhimu kwa jamii, lakini sasa ipo haja kuzungumzia suala la bahari kwa umuhimu wake hasa katika kukuza kipato cha wananchi na taifa kwa ujumla.

Aidha, aliwataka Waafrika kutumia fursa zilizopo katika nchi zao katika kukuza uchumi wa nchi pamoja na kuwapatia wadau husika elimu itakayowajengea uwezo wa kujua nyenzo ziliopo nchini ili waweze kufaidika nazo pamoja kuwashawishi kutumia masoko ya ndani kwanza kabla ya kutumia masoko ya nje.


Meza kuu ikisikiliza utaratibu wa Mkuta kutoka kwa Masta Solomon hayupo (pichani). Mkurugenzi kutoka Umoja wa Africa- Ofisi ya rasilimali wanyama Simplice Noula akitoa tarifa ya ofisi yake katika Mkutano huo uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Mjini Zanzibar.
Waziri wa Kilimo, Maliaasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Hamad Rshid Muhammed akifungua Mkutano wa siku mbili wa mashauriano ya kitaalam juu ya kuanzisha vituo bora vya uvuvi na ufugaji samaki Africa, uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Mjini Zanzibar.


Sehem ya wajumbe wa Mkutano wakimsikiliza mgeni rasmin Waziri wa Kilimo, Maliaasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Hamad Rshid hayupo (pichani) alipokuwa akifungua Mkutano huo.

Afisa Mkuu kiongozi wa Uvuvi kutoka Umoja wa Africa Dk. Mohamed Seisay akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Mkutano wa mashauriano ya kitaalam juu ya kuanzisha vituo bora vya uvuvi na ufugaji samaki Africa.



Picha ya pamoja ya wajumbe wa Mkutano wa mashauriano ya kitaalam juu ya kuanzisha vituo bora vya uvuvi na ufugaji samaki Africa.

Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

————————————————
“Tunalo tatizo wenyewe sisi wa Afrika hatulitumii ipasavyo soko la ndani,tunahangaika masoko ya nje wakati uchumi wetu wenyewe bado haujakuwa, hivyo ipo haja kuungana wa nje na wa ndani ili tuweze kupanua soko letu kwa matumizi yetu” alisema.

Nae Mkuu wa Huduma za Wanyama na Mratibu wa Umoja wa Afrika, Simplece Novala alisema madhumuni ya kufanya mkutano huo ni baada ya kuona tatizo la soko katika samaki, ili kuweza kubuni njia zitakazosaidia kukuza soko hilo na kujipatia ajira kwa wananchi katika nchi husika.

Kwa upande wake Mkurugenzi Maendeleo ya Uvuvi kutoka Tanzania bara,Fatma Sobo alisema Tanzania bado ina tatizo kubwa katika masuala ya biashara ya samaki, inatokana na kutokuwa na wataalamu wa kutosha, wavuvi waliopo ni wadogo wadogo, vifaa duni walivyonavyo ambavyo wanachangiwa na mabenki kuwanyima mikopo ya kuweza kujinunulia vifaa ili waweze kuvua samaki wakubwa na kuongeza kipato kwa taifa.

Hivyo, alisema kufanyika kwa mkutano huo hapa Zanzibar, utawasaidia kupata elimu ya kutosha na kuwajengea uwezo wa namna gani wataweza kuboresha huduma za msingi katika masuala mazima ya uvuvi.

Akizungumzia biashara ya samaki ya ndani ya Afrika, Fatma alisema, bado Tanzania ina tatizo la kuangalia zaidi kiwango cha samaki wanachopeleka nchi za nje badala ya kuangalia samaki wa ndani, kwani jambo hilo linapelekea kuonekana samaki wa ndani hawana ubora.

mkutano wa kikao kazi cha wafanyakazi, maendeleo ya jamii CHAFANYIKA DAR ES SALAAM

$
0
0


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Bibi Sihaba Nkinga akifungua Mkutano wa watumishi wa Wizara (hawapo pichani) walioshiriki kikao kazi cha watumishi wote katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam, ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha Wiki ya Utumishi wa Umma katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii. Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Raslimaliwatu Erasmus T. Rugarabamu na kushoto ni Mwenyekiti wa TUGHE wa Tawi Edwin B. Mtembei. Pcha na Mpiga Picha Wetu

Mashine za tiketi za kieletroniki kuanza kutumika Uwanja wa Taifa hivi karibuni.

$
0
0

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akisisitiza jambo wakati alipotembelea kuangalia maendeleo ya uwekaji wa mashine za tiketi zakieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Juni 27,2016.
Mhandisi kutoka kampuni ya B.C.E.G ya China Bw. Xiong (kushoto) akifafanua jambo kwa Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge(kulia) kuhusu mashine za tiketi za kieletroniki zinazotarajiwa kutumika kuingia katika Uwanja wa Taifa leo Juni 27,2016.
Mtaalamu wa Mashine za tiketi za kieletroniki kutoka kampuni ya Selcom Bw. Adrew Emmanuel (kushoto) akimuelekeza jinsi ya kutumia moja ya mashine hizo Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge alipotembelea kuangalia maendeleo ya uwekaji wa mashine hizo uwanjani hapo Leo Juni 27,2016.
Mtaalamu kutoka kampuni ya Selcom Bw. Adrew Emmanuel akirekebisha moja ya mashine za tiketi za kieletroniki zinazotarajiwa kuanza kutumika kuingia katika Uwanja wa Taifa hivi karibuni.


Baadhi ya wananchi wakijaribu kutumia mashine ya tiketi za kieletroniki zinazotarajiwa kuanza kutumika kuingia katika Uwanja wa Taifa hivi karibuni.Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM

BUNGE LIMEPITISHA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA ELIMU.

$
0
0
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akijibu hoja za Wabunge mapema leo Bungeni  Mjini Dodoma wakati akihitimisha hoja kuhusu muswaada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali  wa mwaka 2016.
 Naibu Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Injinia Stella Manyanya akitoa ufafanuzi leo Bungeni Mjini Dodoma kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wenye ulemavu wanapata elimu sawa na wale wasio na ulemavu kwa kuweka miundo mbinu rafiki katika shule na vyuo vyote nchini.
 Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Amina Mollel  akiuliza swali Bungeni leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali kuwawezesha wanafunzi wenye Ulemavu sawa na wale wasio na ulemavu hasa kwa kuangalia miundombinu iliyopo ili iwe rafiki kwa kundi hilo na kuleta usawa katika kupata elimu.
 Naibu Spika,Dkt. Tulia Ackson akiteta jambo na Mbunge Viti Maalum Mhe. Kiteto Zawadi Koshuma katika viwanja vya Bunge, mjini Dodoma.
(Picha zote na Frank Mvungi – MAELEZO - Dodoma)


Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma. 
Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania leo, Mjini Dodoma limepitisha muswada wa marekebisho ya sheria ya Elimu kifungu kinachoeleza kuwa mtu anayempatia ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari kuwa adhabu yake ni faini isiyozidi shilingi laki tano au kifungo kisichozidi  miaka mitatu.

“Muswada unapendekeza kuwa kifungu hicho kifutwe na badala yake kitungwe kifungu kipya cha 60A ili kuweka masharti yanayojitosheleza kuhusu zuio la kuoa au kumpatia ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari, kinapendekeza adhabu yake iwe kifungo cha miaka 30 gerezani,” alifafanua Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju.

Vile vile mtu atakayebainika kusaidia, kushawishi au kuacha mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari kuolewa au kuoa anatenda kosa la jinai ambalo adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi milioni tano au kifungo cha miaka mitano gerezani au vyote kwa pamoja.

Mhe. Masaju aliendelea kwa kufafanua kuwa, sheria hiyo imependekeza kuwa pale ambapo kosa hilo litafanywa na mtoto basi adhabu yake itakuwa kwa mujibu wa masharti ya sheria ya mtoto. Hii ni kwa sababu sheria ya mtoto inakataza mtoto anayetiwa hatiani kufungwa gerezani.

Aidha marekebisho hayo katika sheria ya Elimu yanalenga kumjengea mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari mazingira mazuri ya kumaliza ipasavyo elimu yake kwa ngazi hiyo.Hivyo basi kila Mkuu wa shule au Mwalimu Mkuu atawasilisha kwa Kamishna wa Elimu taarifa ya robo mwaka kuhusu matukio ya ndoa na mimba kwa wanafunzi katika shule yake na hatua zilizochukuliwa.

Sheria ya Elimu inamruhusu mwanafunzi aliyepewa ujauzito kuendelea na masomo mara tu anapojifungua. Sheria hiyo inasubiri kuwekwa saini na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ili ianze kutumika.

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUSHIRIKI MAONESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA SABASABA.

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII



Wizara ya Maliasili na Utalii itashiriki katikaMaonesho ya40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(SABASABA)kuanzia tarehe 28 Juni hadi tarehe 8 Julai, 2016 katika viwanja vya Mwalimu Julius.K.Nyerere, Dar es Salaam.

Wizara itakuwa na washiriki kumi na sita (16) ambao ni Idara pamoja na Taasisi zake mbalimbali. Idara zitakazoshiriki ni Utalii, Wanyamapori, Mambo ya Kale na Misitu na Nyuki.

Kwa upande wa Taasisi ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Chuo cha Taifa cha Utalii, Makumbusho ya Taifa, Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) na Vyuo vya Wanyamapori (Mweka, Pasiansi na Likuyu Semaganga).

Taasisi nyingine ni Vyuo vya Misitu na Nyuki (Olmotonyi, FITI Moshi na Chuo cha Nyuki Tabora), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Wakala wa Mbegu za Miti, Taasisi ya Utafiti wa Misitu na Wadau wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Washiriki wote hao watakuwa kwenye banda moja la MALIASILI, Wizara inawakaribisha wananchi wote kwenye banda hilowaweze kujionea na kuelimika namambombalimbali yanayohusu Utalii, Ufugaji wa Nyuki, Uhifadhi wa Misitu, Malikale na Wanyamapori.

Aidha, Wizara itatoa punguzo kwa watanzania kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumikwa gharama nafuu. Safari ya kwenda na kurudi kwa watoto itakua Tsh. 10,000 na watu wazima Tsh. 20,000. Safari ya kulala itakuwa Tsh. 50,000.

Pia katika maonesho hayo itakuwepo fursa ya kuwaona wanyamapori hai mbalimbali kama vile Chui, Nyoka, Ndege wa aina mbalimbali pamoja na SIMBA.

Kaulimbiu ya Maonesho hayo mwaka huu inasema“Tunaunganisha Uzalishaji wa Masoko” 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Maliasili na Utalii

27 Juni, 2016.

BALOZI WA JAMHURI YA KOREA NCHINI AKUTANA NA RAIS DK.SHEIN

$
0
0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzanzia Mhe,Song Geum-Young alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo '
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzanzia Mhe,Song Geum-Young alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumsalimia Rais
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzanzia Mhe,Song Geum-Young alipofika Ikulu Mjini Zanzibar baada mazungumzo yao. [Picha na Ikulu.]

WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS MAGUFULI MKUTANO MAALUM WA SADC

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo (Jumatatu, Juni 27, 2016) kwenda Gaborone, Botswana kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika wa Double Troika ya Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama (SADC Double Troika Summit) utakaofanyika kesho (Jumanne, Juni 28, 2016).

Mhe. Waziri Mkuu anamuwakilisha Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo utakaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Gaborone (GICC).

Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Botswana Mhe. Lt. Jen. Seretse Khama Ian Khama ambaye ni SADC, utajadili hali ya siasa, ulinzi na usalama nchini Lesotho. Mkutano huu utatanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu ambao utafanyika leo (Jumatatu, 27 Juni, 2016).

Pia mkutano huo utahudhuriwa na Marais wa Afrika Kusini, Mwenyekiti aliyetoka (outgoing chair) wa Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama Mhe. Jacob Zuma , Mhe. Jacinto Filipe Nyusi, Rais wa Jamuhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama.

Wengine ni Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa SADC, Mhe. Robert Mugabe, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe na Mwenyekiti anayeondoka wa SADC.

Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk. Aziz Mlima na Maofisa wengine waandamizi.

Sekta binafsi ishirikishwe katika utekelezaji wa Mpango

$
0
0
 Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa Wachumi na Maafisa Mipango uliofanyika katika ukumbi wa Hazina, Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Wachumi na Maafisa Mipango wakimsikiliza Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (hayumo pichani wakati wa kufunga mkutano wa Wachumi na Maafisa Mipango mwishoni mwa wiki.
(Stori na Picha na Joyce Mkinga)


Na Joyce Mkinga.
SEKTA Binafsi katika ngazi zote ni lazima ishirikishwa katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo 2016/17 – 2020/21 uliozinduliwa hivi karibuni.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri aliyasema hayo alipokuwa akifunga mkutano wa Wachumi na Maafisa Mipango uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Bibi Florence Mwanri amesema sekta binafsi ni wadau muhimu katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo hivyo, wanatakiwa kushirikishwa katika mipango yote ya Serikali.

“Katika mipango yetu katika ngazi zote lazima sekta binafsi ishirikishwe kwa sababu wao ndio watekelezaji wakubwa wa mpango huo” alisema Bibi Mwanri.

Amesema maafisa mipango wanapoibu miradi mbalimbali katika ngazi ya kijiji, wilaya, mkoa ni lazima sekta binafsi ishirikishwe ili kuwapa fursa nzuri ya kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo ambao unalenga katika Kujenga Uchumi wa Viwanda ili Kuchochea Mageuzi ya Kiuchumi na Maendeleo ya watu.

Mkutano huo uliwashirikisha wachumi na maafisa mipango 170 kutoka katika wizara, idara za serikali, sekretarieti na mikoa na wilaya, taasisi za utafiti, na sekta binafsi ulikuwa na kaulimbiu ya Kuelekea kwenye Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo 2016/17 – 2020/21.

Lengo kuu la Mkutano huo ilikuwa ni kujenga uelewa wa pamoja juu ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano na utelekezaji wake.
Mpango huo unatarajia kugharimu Trilioni 107 ambapo Sekta binafsi itachangia  Trilioni 48.

Akiwasilisha maazimio ya mkutano huo Kaimu Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kutoka Klasta ya Uchumi Jumla, Dkt. Lorah Madete amesema Serikali na sekta binafsi wakutane pamoja na kupanga mikakati ya kutekeleza mpango huo wa maendeleo.

Vile vile, Dkt Madete alisema kuwa kuna haja ya Serikali kuingiza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia katika mipango ya Serikali ikiwa ni pamoja na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.
Mkutano huo uliandaliawa Tume ya Mipango kwa ushirikiano na Taasisi ya Uongozi.

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU KUKUTANA NA WADAU PAMOJA NA WANANCHI 28 JUNI, 2016

$
0
0





OfisiyaTaifayaTakwimu

Taarifa kwa UmmaKatika kuazimisha “WIKI YA UTUMISHI WA UMMA” yenye kauli mbiu “Uongozi wa Umma kwa ukuaji Jumuishi: kuelekea katika Afrika tunayoitaka”, Ofisi ya Taifa ya Takwimu inawajulisha wananchi na wadau wote kuwa imetenga siku ya Jumanne tarehe 28 Juni, mwaka huu, kuwa siku maalumu ya kukutana na wananchi ili kutoa elimu na kusikiliza hoja na maoni kuhusu utoaji wa takwimu rasmi nchini.

Muda ni kuanzia saa 3.00 Asubuhi hadi saa 9.00 Alasiri katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Makao Makuu.

KARIBUNI WOTE

ImetolewanaMkurugenzi Mkuu,
OfisiyaTaifayaTakwimu.

NSSF YAOTA ELIMU KUHUSU MAFAO KWA WAFANYAKAZI WA TAZARA

$
0
0
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limetoa Elimu ya Pensheni kwa wâfânyakazi wa TÂZARA.lengo la semina hiyo ni kuwaelimisha wânâchama kuhusu kanuni mpya ya kukokotoa pensheni ya Uzeeni.

Akizungumza na wafanyakazi hao Ofisa Mwandamizi wa Mafao wa NSSF, Christina Kamuzora alisema kuwa kanuni hiyo imekwishaanza kutumika na kuwahakikishia kwamba malipo yao ya pensheni yatatolewa kwa uharaka zaidi kwa kuwa huduma zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa.

Ofisa Mwandamizi wa Mafao wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Christina Kamuzora akizungumza na wafanyakazi wa TAZARA (hawapo pichani), wakati wa utoaji wa elimu kwa wafanyakazi hao.

Wafanyakazi wa TAZARA wakimsikiliza Ofisa Mwandamizi wa Mafao wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Christina Kamuzora (hayupo pichani)

KITUO CHA HUDUMA NA MTOTO EAGT LUMALA MPYA CHA JIJINI MWANZA CHAKABIDHI MSAADA KWA WATOTO WENYE UHITAJI

$
0
0

Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma na Mtoto EAGT Lumala Mpya, Jorum Samwel (kulia mwenye suti), akitoa ufafanuzi juu ya msaada wa vitanda, magodoro na vyakula uliotolewa na Kituo hicho ambacho kiko chini ya Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.

Na BMG

Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba katika Manispaa ya Ilemela mkaoni Mwanza, limekabidhi misaada ya vitu mbalimbali ikiwemo vitanda, magodoro na vyakula kwa watoto wanaotoka katika familia duni ambao wanaolelewa na kanisa hilo.

Akikabidhi msaada huo hii leo, Askofu wa kanisa hilo Dkt.Daniel Moses Kulola, amesema watoto 18 waliokabidhiwa msaada huo ni sehemu ya watoto 264 wanaolelewa na kanisa hilo kupitia Kituo cha Huduma ya Mtoto iliyoanzishwa kanisani hapo tangu mwaka 2010.

Askofu Dkt.Kulola amesema hiyo si mara ya kwanza kwa kanisa hilo kutoa msaada wa vitu hivyo na kueleza kuwa limekuwa likifanya hivyo mara kwa mara ikiwemo kuwalea watoto hao kwenye maadili na afya njema na kuwaandaa kuwa watumishi wema katika jamii kwa baadae.

Nae Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma na Mtoto EAGT Lumala Mpya, Jorum Samwel, amesema msaada huo umetolewa baada ya uongozi wa Kanisa kuzitembelea familia hizo na kujionea hali duni za maisha wanayoishi ambapo baadhi yao hulazimika kulala chini baada ya nyumba zao kuathiriwa na mafuriko ya mvua yaliyotokea mwishoni mwa mwaka jana.

Wazazi, walezi na watoto walionufanika na msaada huo, wameushukuru uongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya kupitia Kituo cha Huduma ya Mtoto, ambapo wametanabaisha kwamba msaada huo utawasaidia kuondokana adha ya kulala chini iliyokuwa ikiwakabiri.

Msaada huo wa vitanda, magodoro, mashuka, mahindi na mchele umegharimu zaidi ya shilingi milioni tisa ambazo zilitolewa na wahisani kutoka nje ya nchi ambapo wazazi na walezi wametakiwa kutambua kwamba jukumu la kuwalea watoto katika maadili mema ni la jamii nzima badala ya kuwaachia viongozi wa dini na taasisi za kijamii pekee.
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola, akitoa ufafanuzi juu ya msaada wa vitanda, magodoro na vyakula uliotolewa na Kituo cha Huduma ya Mtoto ambacho kiko chini ya Kanisa hilo.
Mmoja wa watoto walionufaika na msaada huo akitoa shukurani kwa niaba ya watoto wengine
Mmoja wa wazazi/walezi walionufaika na msaada huo akitoa shukurani kwa niaba ya wazazi/walezi wengine
Mmoja wa wazazi/walezi walionufaika na msaada huo akitoa shukurani kwa niaba ya wazazi/walezi wengine
Watoto baada ya kukabidhiwa msaada wa vitanda, magodoro na mashuka
Watoto baada ya kukabidhiwa msaada wa vitanda, magodoro na mashuka
Mtoto katika ubora wake
Msaada wa vyakula kwa watoto wanaolelewa na Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza

Kila mmoja katika jamii anao wajibu wa kuhakikisha mtoto anapata malezi bora

MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI AKANUSHA TAARIFA YA WANYAMA KUCHINJWA MAISARA-ZANZIBAR

$
0
0

Na Miza Othman/Khadija Khamis - Maelezo Zanzibar .

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahamoud amekanusha uvumi wa baadhi ya wananchi kuwa wanyama walioshindwa kugombolewa ndani ya muda uliowekwa, kuchinjwa na kuuzwa kwa beinafuu Maisara.

Mkuu huyo alisema taarifa hizo hazina ukweli ukweli ni kwamba wanyama hao wataendelea kutunzwa na Serikali kwa kipindi kinachokubalika na kwa wale ambao watakaoshindwa kuwakombowa wanyama wao watataifishwa na kuwa mali ya Serikali.

Ameyaeleza hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Afisini kwake Vuga Mjini Zanzibari wakati akitowa taarifa maalumu kwa wananchi wa Mkoa Mjini Magharibi kuhusu Uthibiti wa wanyama kwenye maeneo yasio ruhusiwa.

Hata hivyo amewataka wafugaji kutokubali kutowa fedha kwa wahusika na ukamataji wa wanyama bila ya kupitia taasisi husika (Manispaa), kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kuwataka wananchi kutoa taarifa kwa Masheha, Polisi au Manisipaa iwapo kutajitokeza hali hio ili kuzuia vitendo vya rushwa.

Aidha ameeleza katika utekelezaji wa zoezihilo kumejitokeza changamoto zikiwemo malalamiko kwa baadhi ya waumini wa dini ambao wanyama wao wanawatumia kwa ajili ya shughuli za ibada wamekamatwa.

Vilevile kumejitokeza kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaohusisha zoezi hilo na mambo ya kisiasa kwa kuwashajihisha wananchi kuvunja sheria kwa kupingana na utekelezaji wa zoezi hilo.

Alisisitiza kuwa zoezi hilo ni endelevu na Serikali ya Mkoa wa Mjini Magharibi haitokuwa na muhali katika utekelezaji wa kazi zao na atakaekwenda kinyume na agizo hilo hatuwa za kisheria zitachukuliwa zidi yake.

Alifahamisha Utekelezaji wa sheria hizo umekuja kutokana na kukithiri kwa uvunjifu wa nidhamu kwa baadhi ya wafugaji katika maeneo mengi ya Mkoa wa Mjini Magharibi jambao ambalo linasababisha uchafunzi wa mazingira, ongezeko la ajali, kukuthiri kwa wizi, kuanza kwa migogoro baina ya wafugaji na wakulima, uharibifu wa miiundombinu pamoja na uhalifu wa kutumia mapanga. 

Mahamoud aliwataja wanyama wasioruhusiwa kufungwa ni Ng’ombe, Punda, Mbuzi na Kondoo na maeneo yaliyopigwa marufuku ni shehia zote za Wilaya ya Mjini , baadhi ya shehia za Wilaya ya Magharibi “B” ambazo Mbweni, Kiiembesmaki, Michungani, Mombasa,Kwamchina, Tomondo, Uzi, Sokoni meli,Melinne, Tavet,a Mwanakwerekwe, Mikarafuuni, Pangawe Mnarani, Majogoo na Magogoni. 

Katika utekelezaji wa zoezi hilo alisema hadi sasa wamefanikiwa kuwakamata jumla ya wanyama 114 kati ya hao Ng’ombe 72, Punda 14 na Mbuzi 28.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

WAZIRI NAPE NNAUYE AZINDUA STUDIO YA REDIO YA JAMII KATIKA CHUO KIKUU HURIA TANZANIA OUT), JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akikata utepe wakati wa Uzinduzi wa Redio ya Jamii ya ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akijadiliana jambo na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa toka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues wakati wa Uzinduzi wa ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa ndani ya Studio ya ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ akijibu baadhi ya maswali toka kwa Waandishi wa Habari mara baada ya kuizindua rasmi 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiongea na Viongozi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Wageni waalikwa, baadhi ya Wanafunzi wa chuo hicho pamoja na Waandishi wa Habari wakati wa Uzinduzi wa Redio ya Jamii ya ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda akiongea na Viongozi wa Chuo hicho, wageni waalikwa, baadhi ya Wanafunzi wa chuo hicho pamoja na Waandishi wa Habari wakati wa Uzinduzi wa Redio ya Jamii ya ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa toka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akiongea na Viongozi wa Chuo hicho, wageni waalikwa, baadhi ya Wanafunzi wa chuo hicho pamoja na Waandishi wa Habari wakati wa Uzinduzi wa Redio ya Jamii ya ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam
.

Waziri wa Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amezindua studio ya redio ya jamii ya ‘Community Media Network of Tanzania’ (COMNET) katika Chuo kuku Huria( OUT ) itakayotumika kusambaza habari maeneo yenye uhaba wa redio.

Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam,ambapo Mhe. Waziri amesema kuwa studio hiyo itasaidia idadi kubwa ya wanachi wanaoishi vijijini kupata habari kutoka Serikalini na kutoa mrejesho wa kile watakachosikia kwa urahisi.“Ni Studio muhimu kwa ajili ya kusambaza demokrasia kwa watu hasa wale waliopo vijijini kwa vile redio nyingi bado hazijawafikia”Alisema Mhe.Nape.

Aidha amewataka wanafunzi wa taaluma ya uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma katika chuo hicho kutumia studio hiyo kujifunza zaidi kwa vitendo na kuzingatia maadili ya uandishi wa habari kwa kuandika habari zenye ukweli kutoka vyanzo sahihi ili kutoa ujumbe wenye manufaa mazuri kwa jamii.

Kwa upande wake Makamu mkuu wa Chuo hicho Prof. Elifas Bisanda amesema studio hiyo imeanzishwa kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni(UNESCO) kwa lengo kutoa elimu kwa jamii ambayo imekuwa haipati habari kwa urahisi.



Amewataka wanahabari na wananchi kwa ujumla kufikisha habari katika studio hizo kwa kuwa inatumia njia ya haraka na rahisi katika kufikisha ujumbe kwa kushirikiana na redio mbalimbali za jamii.

Naye mwakilishi kutoka Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi,na Utamaduni(UNESCO) Bi. Zulimira Rodrigues amesema studio ya redio ya ‘Community’ ipo kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu maendeleo ya wanawake na vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.

Mpaka sasa Shirika hilo limefanikiwa kuanzisha redio za jamii katika baadhi ya mikoa ya Tanzania bara ambayo ni Mwanza,Arusha na Tanga na katika baadhi ya maeneo ya Unguja na Pemba.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa ndani ya Studio ya ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari mara baada ya kuizindua rasmi 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa ameongozana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda kwenda kuzindua Studio ndani ya Chuo hicho 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.


ZOEZI LA UHAKIKI WA VYAMA VYA SIASA LAANZA LEO

$
0
0

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Uhakiki wa vyama vya Siasa , Bw. Sisty Nyahoza (kulia) akihakiki daftari lenye orodha ya wanachama wa Chama cha National League for Democratic (NLD) wakati wa zoezi la kuhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa chama hicho Oscar Emmanuel Makaidi na Katibu Mkuu wa NLD Tozzy Ephraim Matwanga.
Bw. Ibrahim Mkwawa, Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Uperembe “Monitoring” (katikati) akikagua nyaraka mbalimbali za Chama cha Sauti ya Umma (SAU) wakati wa uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa lililoanza leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mhasibu Bi. Severa Assey kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Bw.Willy Brown Nyantiga, Mhasibu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini akihoji taarifa za fedha wakati wa zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa kwa chama cha NLD Jijini Dar es Salaam leo . Katikati ni Mwenyekiti wa chama , Bw. Oscar Emmanuel Makaidi na Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Tozzy Ephraim Matwanga ( kulia).
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU) wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Msajili Msaidizi wa Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Uperembe Bw. Ibrahim Mkwawa ( hayupo pichani) wakati wa uhakiki wa utekelezaji masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa lililoanza leo jinini Dar es Salaam.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Uhakiki wa Vyama vya Siasa Bw. Sisty Nyahoza (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama cha National League for Democratic (NLD) wakati wa zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam leo.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa uperembe Ibrahim Mkwawa (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU) wakati wa zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam leo.

Picha na: MAELEZO
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images