Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 890 | 891 | (Page 892) | 893 | 894 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Mwanasheria msomi, kutoka taasisi huru inayojishughulisha na ushauri wa mambo ya habari, (CZI), David Saile Manoti, (katikati), akiwa na wasomi wenzake, Bi Dotto Nyirenda, (kushoto) na Juma George Chikawe, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Juni 23, 2016. Wanazuoni hao ambao ni wanachama wa CCM, wamesema utafitiunaonyesha Watanzania wengi wanaimani kubwa na Rais Magufuli katika mageuzi yake ya uchumi na nidhamu.
  David Saile Mnoti, Mwanasheria, czi
  Dotto Nyirenda, Mwanadiplomasia, czi

  Juma George Chikawe, Mtaalamu wa Teknohama CZI
  ————————————————————————————
  NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID 

  TAASISI ya ushauri wa mambo ya Habari ijulikanayo kama CZI, imetoa utafiti unaoonyesha kuwa katika kipindi cha miezi 8 ya utawala wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Watanzania wengiwanamkubali Rais na wanayo imani kubwa Tanzania itarudi kwenye “mstari’. 

  Watafiti hao, ambao ni David Saile Manoti ambaye amebobea kwenye masuala ya Sheria, Juma George Chikawe, yeye ni mtaalamu wa Teknohama, na Dotto Nyirenda ambaye amebobea kwenye masuala ya Kidiplomasia, wamesma sambambana utafitihuo pia wameelezea kuwa Rais Magufuli atakapopewa dhamana ya kukiongoza Chama Cha Mapinduzi CCM hapo Julai 27 kwenye mkutano mkuu maalum wa chama hicho tawala, ufanisi wake katika kuongoza nchi utaongezeka. 

  Kwa mujibu wa wanazuoni hao, walisema utafiti wao ulifanyika nchi nzima na walitumia njia ya kuwahoji watu papo kwa hapo, kuwahoji kwa kupitia simu au kuwahoji kimakundi. 

  Akizungumzia utafiti wa miezi 8 ya Rais Magufuli akiwa madarakani, Mwanasheria David Saile Manoti, alsiema, kundi la kwanza walilolihoji ni lile la vijana wenye umri kati ya miaka 14-18 ambao wengi wao ni wanafunzi. “Baada ya kundi hili kuhojiwa lilionyesha imani kubwa ya Rais kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi, atarejesha nidhamu ya masomo mashuleni.” Alsiema Manoti. 

  Kuhusu kundi la vinaja wa miaka 10-30 asilimia 82 ya waliohojiwa wameonyesha imani kuwa Rais John Magufuli ataleta mageuzi kwenye elimu hususan masuala ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu pamoja na kumaliza tatizo la mabweni wka wanafunzi.
  Akizungumzia kundi la miaka 30-60, Manoti alisema, Watumishi wa umma wameonyesha imani kuwa Rais Magufuli atarejesha imani kwa serikali kutokana na jinsi anavyoshughulikia mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. 

  Aidha utafiti unaonyesha kuwa asilimia 89.0 ya kundi hili limeonyesha imani kubwa kwa Rais kumaliza matatizo ya wazee kwa kuanza kuwalipa posho kwa mwezi. 

  Katika utafiti huu, Manoti amebainisha kuwa umoja na mshikamano mongoni mwa Watanzania utaimarika zaidi, vile vile kundi hili limesema Rais Magufulu anazidi kuwa maarufu huku wapinzani wakionekana kupoteza umaarufu klutokana na kushindwa kubuni mbinu mpya ya mapambanoya kisiasa. “Kwa ujumla wake Mh. Rais Magufuli anakubalika kwa asilimia 89% huku akiwapiku Edward Lowassa na Mh. Jakaya Kikwete ambao wao wamegawana zilizobaki, Mh. Kikwete asilimia 7% na Mh. Edward Lowassa akiwa na asilimia 4%. 

  Akizungumzia mkutano mkuu maalum wa CCM, Mwanadiplomasia Dotto Nyirenda yeye amewaasa wana CCM kutambua mambo 10 ambayo Rais Magufuli anatosha kuyasimamia.

  Aliyateja mambo hayo kuwa ni pamoja na rasilimali watu, rasilimali ardhi, majengo na viwanja, wanazuoni wa kila taaluma, wafanyabiashara ndogondogo (machinga), wanayabiashara, wanachama wanaozidi milioni 9, Mashabiki wake wanaozidi milioni 28.9, wakulima, wavuvi, na wafugaji, laini pamoja na “utajiri” huo, CCM haiwezi kujiendesha na inategemea ruzuku kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, pamoja na wafadhili ambao wengine sio wasafi kwenye rekodi zao.

  0 0


  Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (wa kwanza kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Profesa Tolly Mbwete (katikati) hati ya mauzo ya hisa asilimia 35 za Kampuni ya Bharti Airtel Afrika. Serikali imezinunua rasmi hisa za kampuni hiyo ndani ya TTCL ambapo leo wamesaini mkataba wa mauziano wa hisa hizo. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel Afrika, Christian De Faria akishuhudia.
  Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (kushoto waliokaa) akitiliana saini na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel Afrika, Christian De Faria (mwenye tai nyekundu) kwenye hafla ya kusaini mkataba wa mauziano. Serikali leo imezinunua rasmi hisa asilimia 35 za kampuni ya Bharti Airtel Afrika ndani ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Nyuma waliosimama ni viongozi mbalimbali walioshuhudia tukio hilo.

  Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (mwenye tai ya bluu) akionesha hati ya mauziano ya hisa. Serikali leo imezinunua rasmi hisa asilimia 35 za kampuni ya Bharti Airtel Afrika ndani ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), ambapo sasa inakuwa ikiimiliki TTCL kwa asilimia 100. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel Afrika, Christian De Faria (mwenye tai nyekundu) akiwa kwenye hafla ya kusaini mkataba wa mauziano hayo. Nyuma waliosimama ni viongozi mbalimbali wa TTCL na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano walioshuhudia tukio hilo.

  Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (kushoto) akibadilisha hati ya mkataba wa mauziano ya hisa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel Afrika, Christian De Faria. Wanaoshuhudia ni viongozi mbalimbali walioshuhudia tukio hilo.
  Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (mwenye tai ya bluu) akionesha hati ya mauziano ya hisa. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel Afrika, Christian De Faria (mwenye tai nyekundu). Kulia ni Ofisa Mkuu Mdhibiti wa Kampuni ya Bhart Airtel Afrika, Daddy Mukadi akiwa kwenye hafla hiyo.
  Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (katikati) akizungumza katika hafla ya kutiliana saini ya mauziano ya hisa. Serikali leo imezinunua rasmi hisa za Kampuni ya Bharti Airtel Afrika. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Maria Sasabo akiwa katika hafla hiyo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura (wa kwanza kulia).

  Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (kulia) akijadiliana jambo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) kwenye hafla ya kutiliana saini ya mauzo ya hisa za kampuni ya Bharti Airtel Afrika leo Dar es Salaam.
  Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (kushoto) akijadiliana jambo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel Afrika, Christian De Faria kwenye hafla ya kutiliana saini ya mauzo ya hisa asilimia 35 za kampuni ya Bharti Airtel leo Dar es Salaam.

  0 0

  T1 
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akizungumza jambo wakati wa Kikao cha Bodi ya Mradi ya Menejimenti ya Maafa kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 23, 2016.
  T2 
  Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Mradi wa Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa mradi huo Juni 23, 2016.
  T3Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brg. Jen, Mbazi Msuya akizungumza jambo katika kikao cha Bodi ya Mradi wa Menejimenti ya Maafa kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam, tarehe 23 Juni, 2016.
  T4 
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (mwenye suti) akimsikiliza Mtaalam wa Uendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Kimataifa Bw. Godfrey Mulisa wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa mradi huo kilichofanyika  katika Ukumbi Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam, Juni 23, 2016.
  T5 
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kulia) akisalimiana na Mchambuzi wa masuala ya mipango wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Kimataifa Bw. Mads Hove wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa mradi wa Menejimenti wa  Maafa.
  T6 
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Mradi wa Menejimenti ya Maafa mara baada ya kumaliza kikao chao kilichofanyika Ofisini hapo.
  (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

  0 0

   Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.
    Baadhi ya Wasomi wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.
   Sehemu ya walohudhuria wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.
   Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufungua mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.


  0 0

   
  Bw . Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari huku akiwa ameshika gazeti la Dira,wakati alipomuomba Radhi Mh. Dk. Harisson Mwakyembe Waziri wa Sheria na Katiba kutokana na Gazeti la Dira analomiliki kumuandika vibaya.

  MFANYABIASHARA Alex Msama amemuomba radhi Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe kufuatia habari mbili zilizochapishwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania analolimiliki.Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msama alisema amejiridhisha kuwa habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari ‘Utapeli wa Mwakyembe wamwagwa hadharani’ haikufuata misingi ya uandishi wa habari. 

  Habari nyingine ambayo imeonekana kumchafua Dk Mwakyembe ni ile ya Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2 ambazo zimemuumiza kiongozi huyo. Alisema yeye kama mmiliki wa gazeti hilo amesikitishwa na habari hiyo na kwamba hatua ya kwanza anayoichukua ni kumuomba radhi Waziri Mwakyembe. 

  Msama alisema sambamba na kuomba radhi atamfikishia barua Mwakyembe ya kumtaka radhi kwa tukio hilo. “Nimesikitishwa na habari hii kwa kuwa haikuzingatia misingi ya uandishi wa habari, ilihukumu na kuonyesha kuwa lengo lake lilikuwa kumharibia jina Waziri Mwakyembe, ninachukua nafasi hii kumuomba radhi nikiwa mmiliki wa gazeti hilo,” alisema Msama. 

  Aidha Msama alisema hatua nyingine anayochukua ni kumsimamisha kazi mhariri wa gazeti hilo, Mussa Mkama kwa kuwa alishindwa kufanya kazi yake kwa umakini ya kuhakikisha habari anazozipitisha zinafuata misingi ya uandishi wa habari na weledi. Alisema Mkama alipaswa kuhakikisha anafuata weledi lakini alishindwa kufanya hivyo kwa hiyo anamsimamisha kazi na kwamba hatua nyingine kali za kinidhamu zitafuata. 

  “Mimi ni mfanyabiashara sijui mambo ya uandishi, nilimuajiri nikiamini atasimamia yale aliyofundishwa chuoni, kwa kuwa ameshindwa inabidi akae pembeni kwanza,” alisisitiza Msama. Ameahidi kuwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania litakalotoka Juni 27, kwa ukubwa uleule atamuomba radhi Waziri Mwakyembe. 

  Hivi karibuni Waziri Mwakyembe aliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma akilalamikia kuwa habari mbili za gazeti hilo iliyochapishwa na Gazeti la Dira ya Mtanzania la Juni 20 na la Juni 23 mwaka huu zililenga kumchafua na kuahidi kuwa atalishtaki kupitia habari hizo mbili.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile na Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird wakibadilishana Hati ya Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf II, Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile (wa pili kulia) na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird (wa pili kushoto), wakisaini Hati ya Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf II. Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam.
  Waandishi wa habari pamoja na wadau wengine wakifuatilia maelezo ya Hati ya Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird. Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Makubaliano yaliyofanywa kati ya Tanzania na Benki ya Dunia ya ili kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf II. Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akibadilishana mawazo na Mratibu Maendeleo ya Sekta Binafsi na SAGCOT kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kumaliza kusaini Hati ya Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf II. Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam


  Na Benny Mwaipaja, WFM

  Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imesaini hati ya makubaliano na Benki ya Dunia itayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya fedha katika mradi wa Tasaf kiasi cha Shilingi Bilioni 440.

  Hati hiyo ilisainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha, Dar es Salaam, leo, Juni 23, 2016.

  Akiongea wakati wa kusaini hati hiyo Dkt. Likwelile alisema kuwa fedha hizo zitaelekezwa katika mradi wa Tasaf II kwa ajili ya kuziwezesha kaya maskini kukuza kipato chao kupitia ajira za muda zitakazowawezesha kupeleka watoto shule na kuwapatia huduma za afya.

  Aliongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2015/2016 Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imefanya kazi kubwa iliyowezesha miradi kumi kupitishwa ambayo ina thamani ya Shilingi Trilioni 1.9.

  "Miongoni mwa miradi iliyopata ufadhili ni pamoja na mradi wa kuboresha mazingira ya biashara uliopata shilingi Bilioni 168, mradi wa kusambaza umeme vijijini (REA), uliopata Shilingi Bilioni 440" Aliongeza Dkt. Likwelile.

  Aidha, alisema kuwa Serikali inaendelea na majadiliano na Benki hiyo kwa ajili ya kuboresha Bandari ya Dar es Salaam, ambapo kiasi cha dola Milioni 600 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.

  Dkt. Likwelile ameishukuru Benki ya Dunia kwa mchango wake mkubwa na kusema kuwa Serikali itahakikisha kuwa inazisimamia taasisi zinazotekeleza miradi hiyo ili ziweze kutumia fedha hizo vizuri na kwa malengo yaliyokusudiwa.

  Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird, amepongeza juhudi za Serikali ya awamu ya tano katika kupambana na rushwa na kuweka mazingira rafiki kwa sekta binafsi.

  Aliongeza kuwa sekta binafsi ndizo zinatoa ajira kwa wingi na kusaidia kuchangia katika kuongeza mapato ya Serikali. Ameahidi kuwa Benki yake itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuiwezesha kufikia malengo yake ya kiuchumi na kijamii kwa faida ya wananchi wake.


   

  0 0

  Katika kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuhakikisha tatizo la madawati nchini linamalizika hadi kufikia Juni, 30 mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa Mashirika ya IPP, Dk. Reginald Mengi ametoa msaada wa milioni 70 kwa wilaya ya Handeni, Tanga na Bagamoyo, Pwani kila moja ikipata milioni 35 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 1,000 ambayo yatasaidia kumaliza tatizo hilo katika wilaya hizo.

  Akizungumza katika halfa ya kukabidhi pesa hizo kwa wakuu wa wilaya wa kampuni hizo, Dk. Mengi alisema ni muhimu kwa watanzania kuungana kwa pamoja na kusaidia kupatikana kwa madawati kwani kwa kufanya hivyo ni kulisaidia taifa.

  Hata hivyo Dk. Mengi alisema kuwa anaamini kama watu matajiri nchini wakiungana kwa pamoja na kujadili jinsi ya kumaliza tatizo la madawati nchini basi jambo hilo litaweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka tofauti na sasa ambapo linakwenda kwa mwendo wa kusuasua.

  "Ukisaidia mtu mmoja katika elimu ni sawa umesaidia jamii na taifa kwa ujumla kama watu matajiri wakisema wakae kwa pamoja na kuangalia jinsi ya kumaliza tatizo hili linaweza kutatuliwa na shida ya madawati kumalizika.


  Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akimkabidhi mfano wa hundi ya milioni 35, Mkuu wa wilaya ya Haneni, Husna Rajab. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mji wa Handeni, Kenneeth Haule, Mwenyekiti wa Mji wa Handeni, Twaha Mgaya na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Handeni, Ramadhani Diliwa.

  Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akimkabidhi mfano wa hundi ya milioni 35 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 500, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Chalinze, Edes Lukoa, Mkurugenzi wa Bagamoyo, Natujwa Melau, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Issa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Said Zikatimu.

  Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akizungumza katika halfa ya kukabidhi milioni 70 kwa wilaya ya Handeni na Bagamoyo ambazo zitawezesha wilaya hizo kununua madawati 1,000 na kila wilaya kupata madawti 500.

  "Matajiri wanatakiwa kutambua kuwa wanatakiwa kurudisha shukrani zao kwa Mungu, taifa na wananchi na hasa kwa walio na hali ya chini kwani hao ndiyo wanaowasaidia kufanya biashara zao kwa amani," alisema Dk. Mengi.

  Aidha amewataka wakuu wa wilaya hizo kuondoa hofu ya kufukuzwa kazi kama watakuwa hawajakamilisha na wanachotakiwa kufanya kwa sasa ni kuongeza juhudi huku akiwashauri kuandaa mikutano katika wilaya zao na kushirikisha wananchi wao ili waweze kuchangia na hatimaye tatizo hilo kumalizika.

  Kwa upande wa mkuu w wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga na mkuu wa wilaya ya Handeni, Husna Rajab wamemshukuru Dk. Mengi kwa msaada ambao amewapatia na kuwataka watanzania wengine kuwa na moyo wa kujitolea kama jinsi amevyofanya Dk. Mengi kwa kuchangia upatikanaji wa elimu bora.

  Awali kabla ya msaada ambao umetolewa na Dk. Mengi, wilaya ya Bagamoyo ilikuwa ikikabiliwa na upungufu wa madawati 2,463 na Handeni ikikabiliwa na tatizo la upungufu wa madawati 4,000.

  Mkuu wa wilaya ya Handeni, Husna Rajab akizungumza katika halfa hiyo.

  Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga akizungumza katika halfa ya kupokea pesa kwa ajili ya madawati 500 yatakayokwenda katika wilaya yake kusaidia kupunguza tatizo la madawati.

  Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akisaini mfano wa hundi kabla ya kuanza kuwakabidhi.

  0 0

  Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Tomoni Farms Limited, Bwana Franklin Bagalla akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani wakati wa utambulisho wa tukio hilo mapema leo Juni 23.2016, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Bwana Willybroad Alphonce.Muonekano wa nje unavyoonekana katika duka hilo la kisasa la bidhaa za shambani.
  Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Tomoni Farms Limited, Bwana Franklin Bagalla akifafanua jambo ndani ya duka hilo la kisasa la bidhaa za shambani
  Baadhi ya bidhaa zinavyoonekana ndani ya duka hilo.
   
  Kampuni ya Tomoni Farms Limited, inayomilikiwa na wazawa, wakijishughulisha na Kilimo cha umwagiliaji cha mazao ya Matunda na Mbogamboga, wamefungua duka na Mgahawa wa Kisasa kwa ajili ya uuzaji wa mazao yao katika hali ya usafi na usalama wa hali ya juu uliopo eneo la jirani na Victoria, Jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa Habari mapema leo Jijini Dar Es Salaam, wakati wa utambulisho wa duka hilo na shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo ya Tomoni Farms Limited, Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni hiyo Bwana Franklin Bagalla ameeleza kuwa, wameamua kuwasogezea watanzania bidhaa bora za kilimo ambazo watazipata moja kwa moja kupitia duka lao hilo na watajiona kama wapo shambani ama bustanini kwa namna ya uwekezaji wao walivyoweza kuuandaa ikiwemo mazingira safi na utunzaji wa kisasa kutoka shambani hadi kumfikia mlaji.

  “Baada ya kuwekeza kwa miaka mine katika kilimo cha Matunda na Mboga mboga kwa kutumia teknolojia ya umwagiliaji, huku tukiwa na uhakika wa kutoa mazao Mwaka mzima, sasa tumewekeza katika miundo mbinu ya kuhakikisha mazao yetu yanawafikia walaji yakiwa katika hali ya usafi na usalama. Hivyo kupitia katika duka letu hili la kisasa hapa Dar es Salaam linatoa fursa kwa wananchi kujipatia bidhaa za kila aina na watazipata kwa hali ile ile kama zipo shambani na tunawakaribisha sana” alieleza Bwana Bagalla.

  Aliongeza kuwa, Mazao yote yanavunwa na kusafirishwa katika magari maalumu kutegemea na uhitaji wa mazao hayo, na hupokelewa, kuchambuliwa na hatimaye kuhifadhiwa katika jokofu kubwa la baridi kuhakikisha kwamba ubora wa bidhaa unabakia kama ule wa shambani na baada ya hapo bidhaa hizo huuzwa kupitia duka hilo la kisasa na zingine hutumika katika mgahawa wao ambao pia unatengeneza aina mbali mbali za Juice nzito na nyepesi ambazo mara nyingi wataalam wa Afya wanashauri watu kutumia.

  Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo ya Tomoni Farms Limited, Bwana Willybroad Alphonce amesema kuwa katika kufikia malengo na uendeshaji wameweza kutumia kiasi kikubwa cha fedha cha Zaidi ya Bilioni moja.

  Na kuongeza kuwa, wakiwa miongoni mwa Watanzania wazawa, wamewaomba watanzania kuwaunga mkono kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamemsaidia mkulima aliyoko kijijini ambaye bidhaa zake zinaharibika huku mijini zikihitajika kwa wingi, kwani licha ya wao kuendesha shughuli za kilimo pia wamekuwa wakinunua baadhi ya mazai kutoka kwa wakulima wengine ikiwa tu na lengo la kusaidia soko hasa la ndani.

  “ Wateja watakao fika dukani kwetu watajipatia vitu mbalimbali. Ni wakati muafaka sasa kuchangamkia fursa hii ya bidhaa za mashambani ambazo zinatoka kwenye ardhi yetu ya nyumbani yenye rutuba za kutosha na uhifadhi wa hali ya usafi na usalama kwa mlaji.

  Tunawakaribisha wote wanaotambua umuhimu wa kupata lishe bora kupitia matunda na mboga mboga huku tukiwasisitiza wale wote wenye watoto kuhakikisha wanawaleta pale Farm Fresh Bar waanze kuzoea toka mapema kuchangamana katika Bar zenye manufaa Kiafya” alimalizia

  Tomoni Farms Limited inaendesha duka hilo la kisasa la mazao ya shambani, pia ina mgahawa na Bar maalum ambayo inahudumia bidhaa za matunda pekee ikiwemo juice za kila aina pamoja na masuala yote ya vyakula vya mboga mboga ambavyo ni vya asili.
  Baadhi ya mbogamboga za aina mbalimbali zikiwa zimehifadhiwa katika vifaa maalum

  Sehemu ya asili hasili inayotengenezwa na kampui hiyo  Sehemu ya mchele na bidhaa zingine za nafaka zinazopatikana katika duka hilo.

  sehemu ya matunda

  Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha moja ya bidhaa za matunda yanayopatikana dukani hapo.

  Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha moja ya maboga bidhaa zinazopatikana dukani hapo.  Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha mboga mboga za aina mbalimbali zinazopatikana dukani hapo.

  Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha bidhaa maharage ya aina tofauti dukani hapo.

  Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha moja ya bidhaa za asali dukani hapo.

  Mfanyakazi wa kampuni ya Tomoni Farms Limited, Dada Jacqueline Mafubo akionyesha moja ya bidhaa za kalanga dukani hapo.

  baadhi ya bidhaa zikiwa kwenye jokofu maalum zinapoifadhiwa.

  Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Tomoni Farms Limited, Bwana Franklin Bagalla akionyesha wanahabari (Hawapo pichani) bidhaa mahala zinapohifadhiwa katika jokofu maalum la matunda na mboga mboga.

  Baadhi ya wanahabari na wadau wakijadiliana jambo nje ya kamouni hiyo ta Tomoni Farms Limited.

  Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Tomoni Farms Limited, Bwana Franklin Bagalla akiwa nje ya Bar maalum ya masuala ya matunda halisi pamoja na mbogamboga

  Nje ya duka hilo la kisasa linavyoonekana lililopo katika jengo la Green House, eneo la jirani na Victoria, Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Umoja Switch Bw Danford Mbilinyi Akizungumza na Vyombo vya Habari leo wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya UMOJASWITCH.

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Umoja Switch Bw Danford Mbilinyi Amezindua Amezindua Rasmi Maadhimisho ya Miaka 10 ya Umojaswitch..Katika Hotuba yake aliyoitoa kwa Vyombo vya Habari Amesema Miaka 10 iliyopita Benki ndogo zilikuwana Changamoto Kubwa ya kuweza Kupatia Huduma za ATM wateja wao kwani Mitaji na Gharama za uwekezaji,Uendeshaji wa ATM na Wigo wao wa utoaji wa Huduma hii Uliwapa Changamoto kubwa.Kutokana na ChangamotoHizo Mabenki Sita Yaliamua Kuanzisha Umoja wao ili Yaweze Kuweka ATM na Kuwezesha Benkihizo Kushirikiana katika Utoaji wa Huduma a ATMKWA Wateja wao,Umoja huo Ndio uliozaa UMOJASWITCH.

  Akielezea Zaidi Bw Danford Mbilinyi Amesema kwa Sasa Umoja Switch Ina Jumla ya Mabenki 27 Yanayoshirikana katika Utoaji wa Huduma za Kibenki Kupitia ATMzaidi ya 250 Nchi nzima.Kupitia Umojaswitch Mteja wa Benki Yenye Tawi Moja Inamwezesha Mteja wake Kupata Huduma Sehemu Yoyote Tanzania.
  Mafanikio ya Umojaswitch ni Mafanikio ya Ushirikiano na Mabenki Pamoja na Mzingira Wezeshi yaliowekwa na Serikali Kuptia Benki Kuu.Wakti Umoja Huo Ulioanzishwa na Kuanza kutoa Huduma zake Jumla ya Benki sita tu ndio walikuwa wanachama wa Umoja Swich Pamoja na ATM 27 tu.
   
  Tofauti na Ssas umoja huo una Wanachama 27 unaotoa Huduma kwa zaidi ya wateja Milionoi 2 kupitia Zaidi ya ATM 250.Mafanikio ya Umoja Huo yanachangiwa na Ubunifu na Huduma zitolewazo na Umojaswitch kama Kuhamisha Fedha Kutoka Benki moja kwenda Nyingine zilizopo ndani ya Umoja huo Kupitia ATM Pamoja na Huduma za Kununua Luku Mpesa pamoja na Kulipia Huduma Mbalimbali Kupitia Hudama za Mobile Banking na zile za Uwakala.

  Katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Umojaswitch ni Kutoa Elimu kwa Wananchi Kuhusu Umuhimu wa Mtandao huu na Technolojia kwa Ujumla Katika Kukuza na Kuendeleza Sekta ya Kibenki na Mchango wake katika maendeleoa ya Maisha ya Kila siku, Pia katika Maadhimisho haya Wanategemea Kufanya Shuguli Mbalimbali ikiwemo kuchagiza Matumizi ya Technolojia na Ubunifu Kwenye Vyuo vikuu hapa Nchini kwajili ya kuwa Kichocheo muhimu Katika Maendeleo ya Sekta ya Kibenki h

  0 0


  Mkurugenzi wa Mradi wa PS3 Dk. Emmanuel Malangalila akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili yaliyo wakutanisha pamoja wataalam mbalimbali wanaohusika na usimamizi wa rasilimali watu kutoka katika mikoa na tasisi za serikali ili kupata kitini cha kutolea mafunzo kwa watumishi wapya wanaoajiriwa serikalini. Mafunzo hayo yanafanyika mjini Bagamoyo mkoani Pwani. 

  Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) nchini ambao unatekelezwa katika mikoa 13 na kuzinufaisha halmashauri 97.
  Baadhi ya maofisa kutoka Ofisi ya Rais, tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Serikali za Mitaa, Miriam Mmbaga akifuatiwa na Beatice Kimoleta

  Washiriki wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wasimamizi wa rasilimali watu katika taasisi na Halamashauri mbalimbali nchini. Mafunzo hayo yanalenga kuwaweza waajiri hao kutafuta mbinu ikiwepo mafunzo na motisha mbalimbali kwaajili ya kuwafanya watumishi wapya wanapoajiriwa kuendelea kufanya kazi katika mazingira yeyote.
  Mkuu wa Kitengo cha Mifumo ya Rasilimali wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Josephine Kimaro akitoa mafunzo kwa viongozi wa sekta ya Afya waliojitokeza kushiriki semina hiyo mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
  Washiriki wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wasimamizi wa rasilimali watu katika taasisi na Halamashauri mbalimbali nchini. Mafunzo hayo yanalenga kuwaweza waajiri hao kutafuta mbinu ikiwepo mafunzo na motisha mbalimbali kwaajili ya kuwafanya watumishi wapya wanapoajiriwa kuendelea kufanya kazi katika mazingira yeyote.
  Mkurugenzi wa Mradi wa PS3 Dk. Emmanuel Malangalila (kushoto) akiwa na washiriki wengine wakifuatilia mada katika mafunzo hayo.
  Mshauri wa masuala ya Rasilimali watu kutoka PS3, Sheillah Matinhure akiwasilisha mada juu ya mafunzo ya awali na kuwaingiza kazini watumishi wappya pamoja na kupokea changamoto kutoka kwa viongozi wa Serikali za Mitaa.
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Miriam Mmbaga akiwasilisha mada.
  Washiriki na wawezeshaji wakifuatilia mada

  Washiriki wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wasimamizi wa rasilimali watu katika taasisi na Halamashauri mbalimbali nchini. Mafunzo hayo yanalenga kuwaweza waajiri hao kutafuta mbinu ikiwepo mafunzo na motisha mbalimbali kwaajili ya kuwafanya watumishi wapya wanapoajiriwa kuendelea kufanya kazi katika mazingira yeyote.

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Edwin Ngonyani (kushoto)na Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (kulia) baada ya mazungumzo kati ya wizara hiyo na Viongozi wa kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel, Sunil Colaso ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji (wapili kushoto) na Beartice Singano.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Frank Mvungi – MAELEZO - Dodoma

  Watumishi wa Umma waaswa kuzingatia maadili katika kutekeleza majukumu yao hasa wanapowahudumia wananchi ili kuongeza tija.

  Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.Akifafanua Mhe.
   
   Majaliwa amesema kuwa ni dhamira ya Serikali kuhakikisha kuwa watumishi wote wa Umma wanazingatia uadilifu, uchapakazi, sheria, taratibu na kanuni zinazosimamia Utumishi wa Umma.“Serikali itawachukulia hatua kali wale wote watakaotumia madaraka yao vibaya bila kujali vyeo vyao” alisisitiza Mhe. Majaiwa.

  Katika hatua nyingine Mhe. Majaliwa amesema kuwa Serikali hivi karibuni itawasilisha Bungeni muswaada wa Sheria utakaosaidia kuanzishwa Kwa Divisheni ya kushughulikia Mafisadi katika Mahakama Kuu.Lengo la Serikali ni Kuhakikisha kuwa wananchi wanahudumiwa vizuri pale wanapohitaji huduma mbalimbali ndio sababu tunaendelea kuimarisha vyombo vyetu kama Taasissi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili zitekeleze majukumu yake vizuri.

  Katika kuimarisha maadili Mhe. Majaliwa amesema kuwa Serikali inaangalia uwezekano wa kuanza kujumuisha masomo ya maadili katika mitaala ya Elimu hapa nchini ili kuongeza kasi ya kukuza na kujenga maadili miongoni mwa jamii.

  0 0


  Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Victor Gideon (kulia) akihudumia mteja katika Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma leo.
  Afisa Malalamiko wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. James Katubuka (kulia) akihudumia mteja katika Siku ya kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 iliyofanyika Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma leo.

  Wateja wakihudumiwa katika Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiwa ni Siku ya kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damiani Lubuva wakiwa wameinua juu vitabu vya Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015 wakati mwenyekiti huyo alipomkabidhi Rais taarifa hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam leo

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva akimkabidhi Rais Dkt John Pombe Magufuli Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwa uliofanyika Novemba 25, 2015 Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na hadhira baada ya kukimkabidhiwa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Novemba 25, 2015 Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  .

  Baadhi ya waalikwa wa hafla ya hafla ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kukabidhiwa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwa uliofanyika Novemba 25, 2015.

  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Davis Mwamunyange (kulia) akizungumza jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu wakati wakisubiri Rais Dkt. John Pombe Magufuli kukabidhiwa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Novemba 25, 2015 na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo

  Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria hafla ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumkabidhi Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Novemba 25, 2015 , Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  Mwanasheria Mkuu Mstaafu Jaji Mstaafu Mark Boman akiteta jambo na Mkurugenzi wa Uchaguzi Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Rajab Kiravu kwenye hafla ya tume hiyo kumkabidhi Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Novemba 25, 2015 na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya Mabalozi waliohudhuria hafla ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumkabidhi Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Novemba 25, 2015, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Davis Mwamunyange (kulia) akiwa na Wakuu wa Vikosi vya Majeshi, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu, na Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Rashid Othman, Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna Mstaafu Valentino Mlowola na Kamishna wa Uhamiaji (Sheria) Said Kamugisha wakiwa kwenye hafla ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kukabidhiwa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Novemba 25, 2015 na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

  .
  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Philip Mangula akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP) Said Soud Said ambaye ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati walipohudhuria hafla ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumkabidhi Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Novemba 25, 2015 na iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akifurahia jambo na Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Rashid Othman.Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John William Kijazi.
  Baadhi ya viongozi wa vyama vya Siasa waliohudhuria hafla ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumkabidhi Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Novemba 25, 2015, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu, wakati akiwasili kwenye ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam kuhudhuria hafla ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kukabidhiwa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Novemba 25, 2015 na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliyofanyika leo.Kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Davis Mwamunyange na kushoto kwa IGP ni Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Rashid Othman, Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)Kamishna Mstaafu Valentino Mlowola na Kamishna wa Uhamiaji (Sheria) Said Kamugisha.
  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Davis Mwamunyange akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda walipohudhuria hafla ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kukabidhiwa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Novemba 25, 2015 na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.Katikati ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu.
  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kabla ya hafla ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kukabidhiwa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Novemba 25, 2015 na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva.
  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akialimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Ikulu kukabidhiwa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Novemba 25, 2015 na Tume ye Taifa ya Uchaguzi (NEC) huku Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi(aliyevaa kanzu) akishuhudia.Wanaofuata kulia ni Mawaziri Wakuu Wastaafu Dkt. Salim Ahmed Salim na Jaji Mstaafu Joseph Warioba na Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ramadhani Kailima akiwasilisha kwa ufupi kilichomo kenye Taarifa ya Uchaguzi Mkuu 2015.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli (wa pili kulia) akiwaongoza viongozi wenzake kuimba wimbo wa Taifa baada ya kukimkabidhiwa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Novemba 25, 2015 Ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya kukabidhiwa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mabalozi Wanaoziwakilsisha Nchi zao hapa nchini na wawakilisha wa Taasisi za Kimataifa.Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji Mkuu Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid.Picha zote na Hussein Makame-MAKAME

  0 0


  Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Ummy Mwalimu akiongea na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam kuhusu mlipuko wa ugonjwa unaosababishwa na sumukavu uliotokea hivi karibuni mkoani Dodoma. Picha na Ally Daud-Maelezo.

  Na Ally Daud-Maelezo

  Ugonjwa unaosababishwa na Sumukavu kwenye Mahindi ya chakula umegundilika katika Wilaya za Chemba na Kondoa Mkoani Dodoma baada ya kupeleka jopo la Wataalam waliofanya utafiti na kugundua kuwepo kwa ugonjwa huo.

  Akizungumza hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Ummy Mwalimu amesema kwamba matokeo ya awali ya watafiti hao imeonyesha kwamba ugonjwa huo umesababishwa na ulaji wa chakula kilichokuwa na sumukavu na kuleta madhara.

  “Hayo ni matokeo ya awali ya watafiti wa wizara yangu hivyo basi nasubiri matokeo ya vipimo vya damu na haja ndogo vilivyopelekwa kwa uchunguzi zaidi katika Maabara ya CDC, Atlanta iliyopo nchini Marekani na matarajio yetu ni kupata majibu hayo katika kipindi kisichozidi wiki moja” aliongeza Bi Mwalimu.

  Aidha Bi. Mwalimu amesema kwamba mpaka kufikia tarehe 24 Juni 2016, idadi ya wagonjwa imefikia 32, na idadi ya vifo imebakia 7. Hii ni baada ya kuongezeka kwa wagonjwa 11 katika kipindi cha wiki moja.

  “Hadi jana kulikuwa na jumla ya wagonjwa 9 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Dodoma, na 14 wako katika Hospitali ya Wilaya ya Kondoa. Wagonjwa watatu waliolazwa Hospitali ya Mkoa Dodoma, na wawili waliolazwa Kondoa, bado hali zao ni tete” aliongeza Bi. Mwalimu.

  Pamoja na hayo Bi. Mwalimu alisema kwamba Serikali itaendelea kuimarisha mikakati ya kitaifa ya kupunguza uchafuzi wa sumukuvu katika vyakula, ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo wa kupima vimelea hivyo katika damu na mkojo miongoni mwa taasisi za ndani ya nchi.

  “ Tutaendelea kutoa matibabu kwa wananchi walioathirika na Ugonjwa huo, kwenye Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali ya Wilaya ya Kondoa ili kudhibiti na kurudisha afya za wananchi katika kiwango kinachohitajika” aliongeza Bi. Mwalimu

  Aidha Bi. Mwalimu ametoa rai kwa wananchi na wakazi wa Dodoma kwamba wanapaswa kuchambua nafaka zilizoharibika (zilizooza, kuvunjika, zilizobadilika rangi), kukoboa mahindi kabla ya kusaga au kuacha kutumia nafaka zitakazoonekana kuharibika sana ili kuepukana na kiasi kilichozidi sumukavu kwenye nafaka.

  0 0

  Na.Aron Msigwa- Dar es salaam.

  Wito umetolewa kwa Taasisi,mashirika, makampuni na watu binafsi kuanzia  ngazi ya familia kuendelea kuitumia Siku ya jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kufanya usafi wa mazingira, kupanda miti na kutunza vyanzo vya maji kwa hiari bila kusubiri kushurutishwa na sheria kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wakiwemo wafanyabiashara na wafanyakazi wa taasisi na mashirika mbalimbali waliokuwa wakitekeleza wakifanya usafi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam leo wamesema kuwa hatua ya Serikali kuirasimisha Siku ya jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kuwa siku ya usafi wa mazingira kitaifa inaweka msisitizo kuhusu jukumu la kila mwananchi kuwa mlinzi na mwangalizi wa mazingira katika sehemu anayoishi.

  Wamesema Suala la usafi wa mazingira linawahusu watu wote, hivyo kila mwananchi anao wajibu wa kushiriki kikamilifu kufanya Usafi wa Mazingira kwenye Makazi yake, Maeneo ya Biashara, maeneo ya Taasisi za Umma na maeneo yenye mikusanyiko ya watu mbalimbali kama masoko na minada.

  Bi. Zaituni Musa mkazi wa Mwananyamala, Kinondoni jijini Dar es salaam aliyekuwa akisafisha mifereji eneo la mtaa anaoishi akishirikiana na wananchi wenzake amesema kuwa suala la usafi wa mazingira ni jukumu la kila mwananchi bila kuangalia cheo au nafasi yake katika jamii kwa kuwa kuishi katika mazingira machafu kuna athari kubwa kiafya hususan kuchangia milipuko ya magonjwa ikiwemo Kipindupindu.

  " Suala la usafi wa mazingira linatuhusu sote, ni wakati wa kuchukua hatua na kuacha kuishi kwa mazoea,nawaomba watanzania wenzangu tufanye usafi bila kulazimishwa na Serikali kila mmoja atimize wajibu wake" Amesisitiza Bi.Zaituni.


  Baadhi ya Wafanyakazi wa DAWASA waliokutwa wakifanya usafi wa mazingira kutii agizo la Kufanya Usafi kwa kila Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi ili kuyaweka maeneo ya Ofisi za Malamka hiyo katika hali ya usafi.

  Baadhi ya Wakazi wa Mwananyamala wakipakia Taka walizozoa katika mitaa yao katika gari la kuzoa Taka la Manispaa ya Kinondoni.

  Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kufanya usafi wa Mazingira katika maeneo mbalimbali, Mwananyamala jijini Dar es salaam.

  Baadhi ya Wafanyakazi wa DAWASA waliokutwa wakifanya usafi wa mazingira kutii agizo la Kufanya Usafi kwa kila Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi ili kuyaweka maeneo ya Ofisi za Malamka hiyo katika hali ya usafi.


  0 0

  Na Ally Daud-Maelezo

  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , imesitisha tamko la utoaji wa vyakula kwa wagonjwa watakaolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kupisha utafiti wa kina kuhusu huduma hiyo ili kuweza kutoa kilicho bora kwa watanzania.

  Akizungumza hayo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Ummy Mwalimu amesema kwamba wameamua kusitisha mpango mpaka watapotangaza tena ili kufanya utafiti kujua kama kuna faida au hasara kwa wananchi.

  “Natoa tamko kwamba huduma hii iliyotarajiwa kuanza hivi karibuni isitishwe mara moja ili kupisha watafiti waweze kufanya uchunguzi kujua inawasaidia kwa kiasi gani wananchi” alisisitiza Bi. Mwalimu.

  Aidha Bi. Mwalimu amesema kwamba huduma hiyo itatolewa kwa wagonjwa watakaolazwa hapo kwa kulipia shilingi elfu 50 ikiwemo shilingi elfu kumi ya kumuona daktari , elfu kumi ya kitanda na elfu 30 iliyobaki ni kwa malipo ya chakula kwa wiki.

  “Huduma hii inalenga kuwasaidia wananchi katika kuwaandalia chakula stahiki kwa wagonjwa na kupunguza usumbufu kwa waangalizi wa wagonjwa wao kuleta vyakula hospitalini ili kuimalisha afya zao kwa ujumla” aliongeza Bi.Mwalimu.


  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir wakati wakielekea kufuturu Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam  Alhadi Mussa Salum. 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir mara baada ya kufuturu na makundi ya watu mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam. 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir , Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum pamoja Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wakiwa wamesimama wakati wa dua mara baada ya kufuturu. 

  Baadhi ya wananchi wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mtoto mwenye ulemavu wa ngozi aliyetambulika kwa jina moja la Yusuph mara baada ya kuwafuturisha Ikulu jijini Dar es Salaam. 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya makundi ya akina mama waliojumuika katika futari hiyo. 
  PICHA NA IKULU


  0 0


  MBUNGE wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikabidhi gari la wagonjwa (ambulance)jana, kwa mganga mkuu wa halmashauri ya Mji wa Chalinze,dkt Hangai ,mbunge huyo alikabidhi magari ya wagonjwa mawili ikiwa ni pamoja na kituo cha afya Miono.
  MBUNGE wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiwasha gari la wagonjwa (ambulance) mara baada ya kulikabidhi katika kituo cha afya cha Chalinze, mbunge huyo alikabidhi magari ya wagonjwa mawili ikiwa ni pamoja na kituo cha afya Miono.(Picha na Mwamvua Mwinyi)


  Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze

  MBUNGE wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani,Ridhiwani Kikwete amekabidhi magari ya kubebea wagonjwa (ambulance)katika kituo cha afya cha Chalinze na Miono yote yakiwa yamegharimu zaidi ya sh.mil 200.

  Ridhiwani ametoa magari hayo kwa lengo la kupunguza adha ya usafiri kwa wagonjwa hususan wanaotakiwa kwenda kupata matibabu zaidi katika hospital ya rufaa ya Tumbi na Muhimbili.

  Akikabidhi magari hayo jana ,kwa mganga mkuu wa halmashauri ya Mji wa Chalinze, dkt Rahim Hangai, mbunge huyo alisema wakati huu sio wa longolongo bali ni wakati wa kutumikia wananchi na kutekeleza yale viongozi waliyoyaahidi ndani ya jamii.

  Ridhiwani alisema hatotaka kuona gari hilo haliwatendei haki wananchi hivyo aliomba litumike kwa ajili ya wagonjwa na sio vinginevyo.
  Alisema awali kituo cha afya cha Miono kilikuwa na gari la kubebea wagonjwa lakini kwasasa limeharibika hivyo kuamua kupeleka gari jingine lililokuwepo kituo cha afya cha Chalinze.
   
  “Hadi sasa tumeshakabidhi magari ya wagonjwa katika hospitali ya wilaya iliyopo Msoga ambapo tumeikabidhi gari la wagonjwa tulilokabidhiwa na mh Rais John Magufuli ,nyingine ndio hizi mbili tulizokabidhi leo”alisema Ridhiwani. 
   
  Alieleza kuwa tatizo la ukosefu wa magari hayo lipo kwenye maeneo mengi ya jimbo hilo hivyo amejipanga kushirikiana na wadau na wafadhili mbalimbali kutatua changamoto hiyo hatua kwa hatua. Aidha Ridhiwani alisema amepokea malalamiko juu ya kulipishwa gharama za mafuta kutoka kwa wagonjwa ambao walikuwa wakilipishwa sh.30,000 hadi 80,000 kwa wale wanaotoka Miono lakini kuanzia mwezi Julai mwaka huu hakuna mgonjwa atakaetozwagharama hizo. 
   
  Nae mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Chalinze, Saidi Zikatimu alimshukuru Ridhiwani kwa niaba ya wanaChalinze na kuahidi kushirikiana nae ili kuinua maendeleo ya jimbo hilo.Zikatimu alisema ni jumla magari matatu ambayo yametolewa hadi sasa kutokana na juhudi za mbunge huyo iwe kwa kuomba wafadhili na jitihada zake mwenyewe. 
   
  Diwani wa kata ya Bwilingu ,Lucas Rufunga pamoja na diwani wa kata ya Miono Juma Mpwimbwi walimshukuru mbunge huyo na kumuomba asichoke kushirikiana nao kuzipatia ufumbuzi changamoto nyingine zinazowakabili kwenye sekta ya afya. Kwa upande wake mganga mkuu wa halmashauri ya Mji wa Chalinze, dkt Rahim Hangai alishukuru kupokea msaada huo na kusema atahakikisha linatumika kwa matumizi lengwa.

  Alielezea kuwa wanampongeza mbunge huyo kwa kujitoa kwake kuwatumikia wanaChalinze. “Umekuwa ukionyesha kwa vitendo na sio maneno, tunaamini hukutoa kwasababu ni tajiri ama una magarii mengi bali ulitoa kwa ajili ya moyo wako wa huruma na upendo wa kusaidia “alisema dkt Hangai.

  Dkt Hangai alisema wanaamini ameguswa na changamoto iliyokuwa ikiwakabili ya kupunguza tatizo la usafiri. Hata hivyo alisema magari hayo itaboresha huduma za wagonjwa na hasa mama wajawazito na watoto katika rufaa.

  Dkt Hangai alielezea kuwa licha ya kutatuliwa changamoto hiyo lakini bado wanakabiliwa na changamoto ya ufunguzi wa huduma za upasuaji katika jengo kutokana na ukosefu wa vifaa ili kupunguza rufaa za wajawazito, upasuaji kwenda Tumbi.

  Nyingine ni uzio wa kituo, mashine ya kufulia nguo za wagonjwa, uchakavu wa jengo la (OPD) wagonjwa wa nje, jengo la huduma ya mama na mtoto, chumba cha maiti na majeruhi. Dkt Hangai alimuomba Ridhiwani kubeba changamoto hizo ili aweze kuzitatua.

  Kuhusiana na changamoto hizo Ridhiwani alisema ameyachukua yote na kuahidi kuyafanyiakazi kadri itakavyokuwa.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho(wa pili kutoka kulia) akipiga picha ya pamoja na viongozi wa juu wa wafanyakazi wa TAZARA. Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho (Katikati) akipiga picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza jipya la Wafanyakazi wa TAZARA. (Picha zote na Andrew ).


  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa. Makame Mbarawa (MB) amezindua rasmi Baraza Kuu la kwanza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) tukio lililofanyika mapema leo Juni  25.2016, Jijini Dar es Salaam.

  Akisoma hutuba ya ufunguzi wa Baraza hilo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho kwa niaba ya Waziri Profesa Mbarawa, Amelitaka Baraza hilo kufanya kazi kwa moyo mmoja katika hali ya kuifufua TAZARA kiutendaji na ufanisi kama ilivyokuwa zamani.

  Akisoma hutuba hiyo, aliwapongeza viongizi wa wanaounda Mamlaka hiyo akiwemo Mhandisi Bruno Ching’andu kwa kuteuliwa kwake kuongoza Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia na viongozi wengine pamoja na wafanyakazi wote.

  Ambapo alisema kuwa, ni dhahiri hatua ya leo imefikiwa baada ya jitihada kubwa na hasa tukitilia maanani hali ya kifedha ambayo TAZARA inapitia katika kipindi hiki. Hivyi kuwapongeza kwa uamuzi huo kwani Mabaraza yana umuhimu mkubwa katika maeneo ya kazi na yameonyesha mafanikio makubwa kila yalipoanzishwa kwani yameweza kuongeza uhusiano mwema kati ya Manejimenti, Vyama vya Wafanyakazi na wafanyakazi kwa upande mwingine.

  “Mabaraza haya ni dhana ya ushirikishwaji ikiwa na maana kuwapatia wafanyakazi fursa ya kushauri juu ya masuala ya utendaji kazi, sera za taasisi, ufanisi wa kazi, mazingira ya kazi, ustawi wa wafanyakazi katika elimu, nidhamu, vyeo, pamoja na motisha kwa wafanyakazi. Pia dhana hii ya  ushirikishwaji ni kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003 kifungu cha 108.

  Pia ni kwa mujibu wa Sheria ya majadiliano katika Utumishi wa Umma Na. 19 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2005. Pia Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2007 kifungu Na. 73 (1 - 3).

older | 1 | .... | 890 | 891 | (Page 892) | 893 | 894 | .... | 1897 | newer