Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 889 | 890 | (Page 891) | 892 | 893 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano toka Wakala wa Serikali Mtandao Bi Suzan Mshakangoto akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wa taasisi yake kutembelea wateja wake ambao ni taasisi za Umma ikiwa ni sehemu ya maadhimishi ya wiki ya Utumishi wa Umma.
  Na Eliphace Marwa - Maelezo

  Wakala wa Serikali Mtandao (eGA) imeandaa utaratibu wa kutembelea wateja wake ambao ni taasisi za umma ili kusikiliza na kutatua changamoto zinazo tokana na huduma wanazotoa,huduma hizo ni pamoja na mfumo wa barua pepe unaorahisisha mawasiliano serikalini.

  Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wataasisi hiyo Bi Suzan Mshakangoto, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mapema hii leo jijini Dar es Salam na kutaja baadhi ya taasisi 34 zitakazoanza kutembelewa kuanzia tarehe 22 Juni hadi Juni 23.

  Alizitaja baadhi ya taasisi hizo kuwa ni pamoja na Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, vijana, Ajira na Walemavu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi, Wizara ya Habari,utamaduni Sanaa na Michezo, Wizara ya kilimo, Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.

  Aidha aliongeza kuwa huduma nyingine zinazotolewa na wakala wa serikali ni pamoja na uhifadhi wa mifumo ya tovuti za serikalini, utoaji huduma za simu za mikononi, Uratibu wa mitandao serikalini, Ugawaji wa masafa ya internet, huduma za ujumbe mfupi wa maandishi (sms) pamoja na utengenezaji wa mifumo ya tovuti na usajili anuani za tovuti.

  Hiyo ni kutimiza Agizo la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Angela Kairuki la kutaka kila Wizara, wakala na Taasisi za Serikali katika kipindi cha Wiki ya Utumishi wa Umma kukutana na wateja wao na kusikiliza kero walizonazo ili kuweza kuzipatia ufumbuzi, aidha kauli mbiu ya mwaka huu ni, “Uongozi wa Umma kwa Ukuaji jumuishi kuelekea katika Afrika tunayoitaka”.

  Kila taasisi itatembelewa na wataalam wawili wa wakala wa serikali watakao sikiliza maoni na kutoa msaada wa kiufundi na ushauri wa kitaalamu katika kutatua changamoto mbali mbali zinazojitokeza juu ya huduma mbali mbali zinazotolewa na wakala.

  0 0
 • 06/22/16--08:29: Article 7
 • Taarifa kwa Umma

  Katika kuadhimisha WIKI YA UTUMISHI WA UMMAyenye kauli mbiu“Uongozi wa Umma kwa ukuaji Jumuishi: kuelekea katika Afrika tunayoitaka”, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini inawajulisha wadau  wote kuwa imetenga siku ya Ijumaa ya tarehe 24 Juni mwaka huu , kuwa siku maalumu ya kukutana  na wananchi ili kutoa elimu na kusikiliza hoja na maoni kuhusiana na  masuala ya Vyama vya Siasa na sheria zake.
  Muda ni kuanzia saa 3.00 Asubuhi hadi saa 9.00 Alasiri katika viwanja vya  Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa

  KARIBUNI WOTE

  Imetolewa na;    Utawala
                          Ofisi ya Msajili ya Msajili wa Vyama vya Siasa
  Juni 22, 2016
      
  0 0


  Na Daudi Manongi,MAELEZO

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi itakabidhi Ripoti ya Uchaguzi mkuu uliofanyika October 2015 kwa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania, Mhe.John Pombe Magufuli kesho tarehe 23 Juni, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw.Ramadhani Kailima kwa waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam.

  Ripoti ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Mwaka 2015 itafanyika kwa mujibu wa Katiba ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ambapo Tume imepewa majukumu ya kuendesha Uchaguzi wa Rais na wabunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uchaguzi wa Madiwani kwa upande wa Tanzania bara.

  Kukamilika kwa Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na kukabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kunakamilisha mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kuashiria kuanza kwa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020.

  0 0

  Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

  22/06/2016

  Katika kuthibiti matumizi ya magari yanayoingia Nchini kwa msamaha wa kodi Serikali imesema kuanzia Julai Mosi magari hayo sasa yatakuwa na namba na rangi maalum.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusu tamko la kuondoa misamaha ya kodi kwenye taasisi za dini kwa kuwa zinatoa huduma za kijamii kama shule na hospitali.

  “Kwa kutambuua mchango mkubwa wa Taasisi mbalimbali za kidini katika utoaji wa huduma za elimu na afya, napendekeza kufuta utaratibu niliotangaza katika hotuba ya bajeti na badala yake Serikali itaimarisha zaidi hatua mbalimbali za uthibiti misamaha ya kodi ikiwemo magari yaliyoingia kwa msamaha wa kodi kuwa na namba na rangi maalum,” alifafanua Mhe.Dkt. Mpango.

  Aliendelea kutaja hatua nyingine kuwa ni taasisi za kidini kuwasilisha vifaa vinavyotarajiwa kununuliwa kutoka nje ya nchi kila mwazo mwa mwaka wa kalenda na kuthibitisha kama vifaa vilivyopewa msamaha mwaka uliopita vilitumika kama sheria inavyotaka.

  Pia, kuwasilisha majina ya watu walioidhinishwa na Shirika au Taasisi kuandika barua ya kuomba msamaha wa kodi, wakiainisha cheo, saini, picha, anwani na namba zao za simu ili kuiwezesha Mamlaka ya Mapato Tanzania kufuatilia bidhaa zilizoombewa na kupewa msamaha kama zimepata kibali cha taasisi hizo.

  Vile vile taasisi hizo zinatakiwa kupata barua kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Serikali ya Mtaa na Mkuu wa Wilaya mahali Taasisi au Mradi unaotekelezwa ulipo. Mhe. Mpango amesema kuwa hatua hizo zimekuja kutokana na bidhaa zinazoombewa msamaha wa kodi kutumika tofauti na kusudi la msamaha huo.

  Aidha ametoa tahadhari kwa mashirika ya kidini kuanzia sasa, kuhakikisha kuwa yanafuata taratibu zote na Kuzingatia masharti ya msamaha unaotolewa ili kuepuka kufutiwa leseni zao pale zitakapokwenda kinyume na sheria na kanuni zilizowekwa.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akibofya kitufe kuashiria uzi8nduzi rasmi wa maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Dkt Servacius Likwelile alipowasili kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisimama kwa ukakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa akiwa na Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Dkt Servacius Likwelile, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu, na Mkuu wa Mkoa wa Dar e3s salaam Mhe Paul Makonda kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016  0 0

  MSE1
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru LEO amekutana na madaktari bingwa wa hospitali hiyo kwa ajili ya kuwasikiliza na kujibu kero mbalimbali. MSE2 
   Baadhi ya madaktari bingwa wakimsikiliza Profesa Museru baada ya kukutana nao LEO kwenye ukumbi wa CPL katika hospitali hiyo. MSE3Dk Saidia Primos wa hospitali hiyo akiuliza swali kwenye mkutano huo. MSE4Mkurugenzi wa Fedha, Gerald Kimambo (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk John Kimario kwenye mkutano huo LEO.

  Na Neema Mwangomo, Dar es salaam          
                                                                                                                                                                             
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili  (MNH), Profesa  Lawrence Museru leo amekutana na Madaktari  wa MNH  ikiwa ni mkakati wa kukutana na watumishi kwa lengo la kuwasikiliza na kujibu kero zao.
   
  Katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa CPL uliopo ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Museru amewapongeza  madaktari hao kwa kufanya kazi kwa bidii na kuimarisha utoaji huduma kwa wagonjwa na kwamba hali hiyo imechangia MNH kuongeza mapato yake.
   
  Amesema kuongezeka kwa mapato ya Hospitali  na kufikia Shingili Bilioni 4. 5 kwa mwezi kumetokana na kila mmoja kutimiza wajibu wake.Amesema kutokana na mafanikio hayo,  MNH imewaongezea madaktari  wake posho mbalimbali  ili kuongeza tija katika utendaji, lakini pia hospitali  imeamua  kutenga Shilingi Milioni 800 kwa mwaka ili kuwapa mkono wa heri wastaafu wake  jambo ambalo awali halikuwapo.
   
  Hata hivyo amesema mbali na hatua hiyo, pia  MNH imefanikiwa kulipa malimbikizo mbalimbali ya stahiki  za wafanyakazi wake ikiwamo  pesa za likizo kwa madaktari pamoja na watumishi wengine kwa ujumla.“ Awali changamoto kubwa ilikuwa ni ucheleweshaji wa stahiki za wafanyakazi kwa Madaktari na watumishi wengine, lakini katika hilo tumefanikiwa kwani tunaenda nalo vizuri na tumelipa malimbikizo hayo “ amesema Profesa Museru.
   
  Akielezea mipango ya MNH  Profesa Museru amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili ina mipango mbalimbali ya kuendelea kuboresha huduma zake ikiwemo kuongeza vitanda vya Chumba ya wagonjwa Mahututi-ICU-, kuongeza ICU ya watoto pamoja na kina Mama wajawazito.
   
  Kaimu Mkurugenzi huyo Mtendaji wa MNH kesho Juni 23, 2016 atakutana na Wauguzi pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii.

  0 0

  TPA3Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka (kulia), akimkabidhi Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka, vitendea kazi baada ya kuizindua rasmi bodi hiyo.
  TPA1Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka, akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati), wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Katibu MKuu wa WIzara hiyo, Sekta ya Uchukuzi, Dr. Leonard Chamuriho.
  TPA2 
  Wajumbe wa Bodi mpya ya Bandari Nchini (TPA), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo.

  TPA4 
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga alipokagua eneo la kupakulia makontena bandarini hapo.
  TPA5 
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), Eng. Aloyce Matei (wa kwanza kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto), alipokagua miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam.
  TPA6 
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka (kushoto), wakati alipokagua eneo la kuhifadhia  magari katika bandari ya Dar es Salaam.Habari Picha na Benjamini Sawe-Maelezo.

  0 0  Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akipunga mkono kwa Maofisa, wakaguzi, Askari na wageni mbalimbali waliohudhururia sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi .


  Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake wakati wa sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi.
  Maofisa wa Polisi wakisukuma gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova kutoka katika viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi wakati wa sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki.

  Gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova likipita katika ya gwaride ikiwa ni ishara ya kumuaga zilizofanyika katika Chuo cha Polisi Moshi nakuongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki .
  Gwaride Maalumu la Kumuaga Kamishna Mstaafu Suleiman Kova likipita mbele yake kwa mwendo wa haraka wakati wa Sherehe za kumuaga rasmi baada ya kustaafu utumishi.Sherehe hizo zilifanyika katika chuo cha Polisi Moshi (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
  Gwaride Maalumu la Kumuaga Kamishna Mstaafu Suleiman Kova likipita mbele yake kwa mwendo wa haraka wakati wa Sherehe za kumuaga rasmi baada ya kustaafu utumishi.Sherehe hizo zilifanyika katika chuo cha Polisi Moshi (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

  0 0


  Mkurugenzi mtendaji wa WKAC Tanzania Bi THEODOSIA NUHULO akiizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam kuhusu maswala mbalimbali yanayohusu ukandamizwaji wa wanawake hususani wajane nchini Tanzania ikiwemo sheria kandamizi ya mirati ya kimila nchini sheria ambayo imetajwa kuwaumiza wajane wengi .PICHA ZOTE NA EXAUD MTEI MSAKA HABARI

  Na Exaud Mtei

  Serikali ya Tanzania imetakiwa kufanya marekebisho makubwa ya sheria ya mirathi ya kimila sheria ambayo imetajwa kuwa ni kandamizi na inawanyima haki wanawake na wasichana ikiwa ni utekelezaji wa mkataba wa CEDAW ambao nchi imesaini mwaka 1986 ambapo ulikuwa unawaelekeza wanachama kuondoa ubaguzi dhidi ya wanawake katika ngazi za kisiasa,kiuchumi,na kijamii ili kuletwa usawa.

  Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na kikosi kazi cha kamati ya mkataba wa kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake CEDAW ambacho kinaundwa na mashirika tisa yanayotetea haki za wanawake Tanzania kwa namna mbalimbali.

  Akizungumza kwa niaba ya mashirika hayo yote mkurugenzi mtendaji wa kituo cha msaada wa kisheria kwa wanawake WLAC ambao wameyaongoza mashirika hayo katika tamko hilo Bi Theodosia Nuhulo ameeleza kuwa mnamo mwaka 2005 WLAC kwa kushirikana na wadau wengine watetezi wa haki za wanawake walifungua kesi mkakati katika mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam kupinga vipengele kandamizi katika sheria hiyo ya mirathi (Tamko la Mirathi la kimila) la mwaka 1963 lakini mnamo mwaka 2006 ilitupilia mbali kesi hiyo huku ikitamka wazi kuwa vifungu vilivyolalamikiwa ni vya kibaguzi kweli lakini haiwezi kufanya mabadiliko ya kimila katika tamko la kisheria.
  Mkurugenzi wa umOja wa wajane nchi i Tanzania ROSE SARWAT akizngumza na wanahabari wakati Tanzania ikiingia kuadhimisha siku ya wajene nchini ambapo amewataka wajene na watanzania kujitokeza kwa wiingi kesho katika viwanja vya mnazi mmoja kuadhimisha siku hiyo ili kupata Fursa ya kujadili kwa pamoja kuhusu haki zao hususani sjheria hiyo kandamizi kwa wajane.

  Ameeleza kuwa WLAC kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walifanya jitihada zote za kukata Rufaa dhidi ya uamuzi huo lakini mnamo 2010 rufaa hiyo ilitupiliwa mbali tena kwa kigezo kwamba uamuzi na amri iliyotolewa na mahakama kuu ilikuwa na tarehe mbili Tofauti yani tarehe 8/9/2006 na tarehe 7/12/2006.

  Amesema kuwa baada ya jitihada zote hizo kugonga mwamba juu ya sheria hiyo kandamizi ameeleza kuwa serikali ya Tanzania kuzingatia ukubwa wa swala hilo kufanya marekebisho ya haraka kwani ndio chanzo kikubwa cha wanawake wajane nchini Tanzania kushindwa kupata haki zao za msingi zikiwemo za mirathi baada ya vifo vya wenzi wao.
  Mkutano huo ukiendelea

  Bi Theodosia ameendelea kusema kuwa pamoja na jitihada nyingi mbalimbali zinazofanywa na WLAC na wadau mbalimbali watetezi wa haki za wanawake bado serikali haijaonyesha jitihada za maksudi za kutekeleza Taarifa /maamuzi ya kamati ya mkataba wa CEDAW kuhusu sheria ya miradhi ya kimila na hali ya wajane Tanzania ili kuhakikisha kwamba wajane wanapata haki zao.

  Aidha WLAC wameitaka serikali ya Tanzania kuwajengea uwezo majaji na waendesha mastaka na watumishi wa mahakama na wanasheria kuhusu mkataba wa CEDAW na umuhimu kwa kuzingatia haki za binadamu katika maamuzi yao.
  Wanahabari mbalimbali wakisikiliza kwa makini-PICHA ZOTE NA EXAUD MTEI MSAKA HABARI WA HABARI24 BLOG

  Pamoja na hayo WLAC wameitaka serikali kuchapisha taarifa hiyo ya kamati ya CEDAW na kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na mila potofu dhidi ya wanawake na kuwatendea haki badala ya kuwanyanyasa kwa namna mbalimbali.

  Hata hivyo WLAC wameitaka serikali kutoa fidia ya kutosha kwa wajane waliohusika katika kesi mkakati kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki

  0 0


  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Quraan Tukufu, Sheikh Othman Ally Kaporo (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam Juni 23, 2016. Mashindano hayo yatafanyika Jumapili Juni 26, 2016 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Sheikh Mohammed Ally Hassan(kulia) na Sheikh AllySendo
  Abuzar Kholidi kutoka Tajikistan


  NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID

  MASHINDANO ya Kimataifa ya Kusoma na Kuhifadhi Quraan, yanatarajiwa kufanyika Jumapili Juni 26, 2016 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na Waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO leo Juni 23, 2016, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mashindano hayo, Sheikh Othman Ally Kaporo, amesema, mashindano hayo ambayo ni sehemu ya kutekeleza ibadaya funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, yatashirikisha wanazuoni kutoka mataifa mbalimbali Duniani.

  “ Kwa wale watakaojaaliwa, wanaweza kufika kwenye msikiti wa Mtoro ulioko Kariakoo, na kujionea jinsi vijana wadodo wanavyosoma Quraan, kila siku usiku, na Jumapili ndio mashindano yenyewe haswaa.’Alisema.

  Katika mkutano huo na waandishi wa habari, washindani watatu waliwaonyesha waandishi umahiri wao wa kuhifadhi Quraan, miongoni mwao ni wanafunzi wawili wenye umri wa miaka kati ya 8 na 10, Abuzar Kholidi kutoka Tajikistan, na Ahmed Abdallah kutoka Bangladesh. Kijana mwingine aliyeonyesha ufundiwa kuhifadhi Quraan Tukufu ni Gadzhimurad Magomedov, kutoka Russia.
  Ahmed Abdallah kutoka Bangladesh
  Gadzhimurad Magomedov, kutoka Russia  0 0


  0 0

  mao1 
  Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Eva Mbigi akimkaribisha Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (katikati)  ili kuongea na Watumishi wa Ofisi hiyo. aliyekaa kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Muungano kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.
  mao2 
  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbarak Abdulwakil akiongea na kutolea ufafanuzi kero mbalimbali toka kwa  Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.  
  mao3 
  Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Mbarak Abdulwakil alipokua akitoa ufanunuzi wa kero mbalimbali zilizowasilishwa na Wafanyakazi wa Ofisi .

  0 0

  WAKALA wa Majengo Tanzania imesema tayari imekusanya zaidi ya asilimia 40 ya madeni waliyokuwa wakiwadai watumishi wa Umma waliopanga katika nyumba za serikali.

  Akizungumza na waaandishi wa habari leo wakati wafanyakazi wa TBA wakifanya usafi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam zilizopo nyumba hizo , wakati wa maadhimisho ya kilele cha Wiki ya utumishi wa Umma, Elius Mwakalinga alisema, kabla ya kulipwa kwa fedha hizo  TBA ulikuwa ukidai zaidi ya bilioni sita ambapo baada ya kutolewa kwa notisi ya kulipa tayari wamekusanya bilioni 2.6.

  Amesema, bado shughuli ya kuwatoa wapangaji wengine linaendelea katika mikoa mbalimbali na katika Mkoa wa Dodoma wamefanikiwa kuwaondoa  wapangaji katika nyumba 27 huku Mkoa wa Mwanza shughuli hiyo kukwama baada ya kuibuka fujo kati ya mpangaji na mfanyakazi  wa Kampuni ya udalali ya Yono ambao ndio wasimamizi wa shughuli hiyo.

  “Kazi yetu sisi sio kuleta vita tunataka fedha irudi ili tuendelee na ujenzi wa nyumba nyingine, tumesikitishwa na kitendo cha mpangaji wetu Mwanza ambaye aliamua kuleta fujo na kumshambulia mfanyakazi  wa kampuni ya udalali wa Yono wakati akiondolewa tunaomba tu wawe wastaarabu wanapotakiwa kuondoka au wakubali kulipa,” alisema Mwakalinga.

  Aidha amesema ili kuondoa tatizo la ucheleweshwaji wa ulipaji kodi katika nyumba hizo kuanzia mwezi Julai wapangaji binafsi wataanza kulipa kodi kwa miezi sita huku watumishi wa umma wakiendelea kulipa kwa miezi mitatu mitatu.

  Pia amesema TBA inatarajia wa kupeleka  mapendekezo serikalini ili kuona namna ya kuwasaidia watumishi wa umma ambao hawakuwa na uwezo wa kununua nyumba za serikali na walikuwa ni wapangaji ili waweze kuendelea kuishi katika nyumba hizo hata baada ya kustaafu.
   Mkurugenzi mtendaji wa Wakala wa Majengo nchini(TBA), Elius Mwakalinga akishiriki shughul ya kufanya usafi pamoja na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya kilele cha Wiki ya utumishi wa Umma leo  jijini Dar es salaam.
   wafanyakazi wa TBA wakifanya usafi wakati wa maadhimisho ya kilele cha Wiki ya utumishi wa Umma leo jijini Dar es salaam. 
  Usafi ukiendelea leo jijini Dar es Salaam.
  (Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii).

  0 0  MTOTO LUQMAN ALLY AMEPOTEA NA ANATAFUTWA NA WAZAZI WAKE.
  Luqman Ally (14)(Pichani) anatafutwa na wazazi wake, amepotea tar 13 Juni mwaka huu, anasoma shule ya Msingi Mbagala Islamic Darasa la Sita iliyopo Mbagala jijini Dar es Salaam.

  Mara ya kwanza alitoroka wiki mbili zilizopita na akapatikana katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira Magumu cha Chad kilichopo Mazese.

  Taarifa imetolewa katika kituo cha Polisi cha Majimajitu Mbagala jijini Dar es Salaam kwa RB .NO MAT/RB/618/16. 

  Yeyote ambaye atamwona mtoto huyo apige 

  NAMBAYA YA SIMU. 0655891200. MAMA YAKE MZAZI WA LUQMAN.

  0 0

   Ofisa Mawasiliano Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Theresa Chilambo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka (katikati), kuzungumza na wanahabari kuhusu maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa yatakayoanza rasmi Juni 28, 2016 hadi Julai 8, 2016 katika viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji wa Biashara, Anna Bulondo.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka (katikati), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonesho hayo. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka akizungumza na wanahabari kuhusu maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa yatakayoanza rasmi Juni 28, 2016 hadi Julai 8, 2016 katika viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji wa Biashara, Anna Bulondo. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

   Rais Paul Kagame wa Rwanda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayotarajiwa kuanza Juni 28,2016 hadi Julai 8,2016 ambayo yatafunguliwa rasmi Julai 1,2016 na Rais huyo akiambatana na mwenyeji wake Rais Dk.John Magufuli. 

   Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Edwin Rutageruka alisema maonesho hayo yatatoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi pamoja na taasisi mbalimbali kutangaza biashara na huduma wanazotoa, kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani kujifunza mambo ya biashara na uzalishaji bora wa bidhaa kulingana na soko la kimataifa, kutengeneza jukwaa la kibishara ambap hutoa fursa kwa wafanyabiashara kutengeneza mitandao ya mawasiliano baina yao inayowasaidia kukuza biashara na kufikia malengo waliyojiwekea na kutoa fursa kwa wafanyabiashara kuuza bidhaa zao. Rutageruka alisema nchi 30 zitashiriki maonesho hayo huku makampuni yakiwa 650.

   Alitaja viingilio katika maonesho hayo kuwa kwa watoto itakuwa ni sh.1000 na wakubwa sh.3000 hiyo ni kuanzia Juni 28n hadi Julai 8,2016 lakini katika siku ya Julai 7, 2016 kwa wakubwa itakuwa ni sh. 4000. Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi na wafanyabiashara kutumia fursa hiyo kutembelea kwenye maonesho hayo ili kujifunza mambo ya biashara.


  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali mara baada ya kupokea Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Damian Lubuva Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Damian Lubuva Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha UDP mzee John Momose Cheyo mara baada ya kumaliza kuzungumza na wageni mbalimbali katika tukio la upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha UPDP Fahmi Dovutwa mara baada ya kuhutubia katika tukio la upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo pamoja na Mwanachama wa Chama cha UDP Goodluck Ole Medeye , Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo pamoja na Jaji Mark Bomani Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu Salim Ahmed Salim mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya Uchaguzi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya taifa ya Uchaguzi(NEC)
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wa Serikali,Marais Wastaafu, Mawaziri Wakuu Wastaafu, Tume ya Uchaguzi na Mabalozi wa nchi mbalimbali mara baada ya kupokea Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo mara baada ya kupokea Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mwanasiasa mkongwe John Shibuda huku Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein naye akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mzee John Momose Cheyo mara baada ya kukamilika kwa tukio la upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
  Baadhi ya Wageni na Mabalozi kutoka nchi mbalimbali wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupokea taarifa hiyo ya Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). PICHA NA IKULU.

  0 0

  Na. Immaculate Makilika -MAELEZO

  Ni ukweli usiopingika kwamba dunia imeingia katika maendeleo ya teknolojia yanayopelekea matumizi ya vifaa vya kisasa na vyenye utaalamu wa hali ya juu katika kufanya shughuli mbalimbali, ambazo hapo awali zilifanywa kwa kutumia nguvu kubwa na idadi kubwa ya watu na kwa muda mrefu.

  Maendeleo hayo ya teknolojia yamejidhihirisha katika nyanja nyingi mojawapo ni hii ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano umerahisisha mawasiliano na unatoa fursa kwa jamii kwa ujumla kuwa huru zaidi katika kutekeleza majukumu yake.

  Serikali inatoa fursa kwa wananchi kutoa hoja na kero zao popote pale walipo kwa kuanzisha tovuti katika wizara, taasisi na ofisi zake ambazo zinawezesha wananchi kupata tarifa muhimu na kwa urahisi kuhusu wizara, ofisi ama taasisi husika na serikali kwa ujumla.

  Katika kuzingatia maendeleo hayo ya teknolojia ya habari na mawasiliano, mwaka 2006 Rais wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, aliitaka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati huo chini ya Idara ya Habari -MAELEZO kuanzisha, kuratibu na kusimamia Tovuti ya Wananchi.

  Dhamira kubwa ya kuanzishwa kwa tovuti hii ni kutokana na matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Ibara ya 18 toleo la mwaka 2005, maagizo ya Sera ya Habari na Utangazaji ya mwaka 2003; na dhana ya Serikali inayozingatia Haki za Binadamu na Utawala Bora kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 19 ya Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu na Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

  Aidha, tovuti hii inatoa fursa kwa wananchi kuwasiliana moja kwa moja na Serikali yao, kuwawezesha watanzania popote walipo duniani kuweza kuwasilisha hoja zao, maoni na malalamiko serikalini kwa kutumia mtandao wa intaneti .

  Vile vile, Tovuti ya Wananchi inarahishisha upelekaji wa hoja za wananchi kwenda kwa maafisa husika wa serikali ili zifanyiwe kazi na kujibiwa na kuiwezesha serikali kurudisha majibu na kutoa maelezo ya kina kuhusu hoja zinazopokelewa kutoka kwa wananchi kupitia njia za intaneti na ujumbe mfupi (SMS)

  Malengo hasa ya kuanzishwa kwa tovuti ya wananchi ni: 

  Kuimarisha na kupanua dhana ya uwazi na uwajibikaji Serikalini dhana ambayo ni nguzo muhimu ya utawala bora. Kusaidia mapambano dhidi ya rushwa, uonevu, unyanyasaji na maovu mengine katika jamii kwa kusaidia mawasiliano ya haraka na vyombo husika vya dola. 

  Malengo mengine ni pamoja na kuiwezesha Serikali kupata maoni ya wananchi juu ya vipaumbele vyao vya maendeleo na kuhusu ubora wa huduma mbalimbli wanazopatiwa na watumishi wa umma kwa lengo la kuziboresha pamoja na kuiwezesha Serikali kupata hoja na takwimu zitakazoiwezesha kubuni mbinu mikakati mipya ya mageuzi ya kiuchumi na kijamii ili nchi yetu ipige hatua kubwa zaidi ya maendeleo na kuifanya ifikie uchumi wa kati ifikapo 2020.

  Katika hotuba ya bajeti ya mwaka 2016/2017 iliyowasilisha Bungeni na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye, alisema kuwa Wizara imeratibu utoaji wa ufafanuzi kuhusu hoja na kero mbalimbali za wananchi kwa serikali zilizowasilishwa kupitia Tovuti ya Wananchi. katika kipindi cha mwezi Julai, 2015 hadi Machi, 2016. Jumla ya hoja 93 zilipokelewa. kati ya hizo, hoja 70 zimepatiwa ufafanuzi na hoja 23 zimeendelea kufanyiwa kazi.

  Lakini pia Tovuti ya Wananchi imepokea jumla ya hoja 117,336 tangu ilipoanza kazi mwaka 2007 hadi kufikia Machi mwaka 2016, kati ya hizo hoja 78,328 zimeshughulikiwa, huku wananchi 48 walitembelea Idara ya Habari- MAELEZO na kuwasilisha hoja zao. Hoja hizo zimeshughulikiwa.

  Wananchi hao ni pamoja na wananchi wa mtaa wa Zavara katika kata ya Chanika ambao eneo lao lilivamiwa. Hoja yao iliwasilishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala na kushughulikiwa. Mtoto mwenye saratani aliwasilisha hoja yake na kupelekwa Wizara ya Afya na kufanikiwa kupata matibabu nchini India.

  Aidha, wananchi wengi waliowasilisha hoja zao zilizohusu kucheleweshwa kwa kusikilizwa kwa kesi zao mahakamani, hoja zao zilishughulikiwa na kesi zao zilisikilizwa na kutolewa maamuzi. 

  Tovuti hii inamwezesha Mtanzania yeyote aliyeko mahali popote duniani penye mtandao wa intaneti au mwenye simu ya mkononi kuwasiliana na Maafisa Wakuu wa Wizara yoyote ili kutoa maoni, ushauri, pongezi au malalamiko au kuiuliza swali serikali moja kwa moja.

  Hoja huwasilishwa Serikalini kwa kutumia intaneti kwa kufungua anwani ya tovuti – www.wananchi.go.tz – bonyeza sehemu iliyoandikwa weka hoja. Njia nyingine ya kuwasilisha hoja ni kwa kuandika ujumbe mfupi kwa kutumia simu ya mkononi. Hii itatumika mara baada ya namba ya kutuma na kupokea ujumbe huo itakapokuwa tayari, kwa kuandika barua kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO S.L.P 8031 au tembelea ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO zilizopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam karibu na Makao Makuu ya Shirika la Bima la Taifa (NIC).

  Hoja zinapotumwa huingia moja kwa moja katika Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala wa Serikali. Iwapo mtumaji hana uhakika na sehemu ambapo anataka hoja yake aielekeze, hoja hiyo huingia moja kwa moja makao makuu ya Tovuti ya Wananchi, Idara ya Habari – MAELEZO, waratibu wa Tovuti huiwasilisha hoja hiyo Wizara au taasisi inayohusika. 

  Hoja hizo hutafutiwa majibu na Maafisa wa Wizara husika ambao nao huyatuma majibu hayo kwa mtuma hoja ndani ya siku tano za kazi, kwa kupitia njia aliyoitumia mtuma hoja.
  Baadhi ya Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wameweza kuwasilisha kero zao kupitia na Tovuti hii ya Wananchi, ambapo walipatiwa majibu ya hoja zao, kama vile Bibi Valeria Luzebigo aliweza kupata majibu ya vipimo kutoka kwa mkemia Mkuu wa Serikali kufuatia kifo cha baba yake mzazi.

  Aidha Bwana Saidi Bundela, mkazi wa Dar es Salaam mwenye ulemavu wa miguu alipatiwa msaada wa magongo ya kutembelea na Rais Msaaafu Dkt. Jakaya Kikwete. Naye BwanaGeofrey Bwananali, mkazi wa Dar es Salaam ameendelea kupatiwa msaada wa matibabu ya ngozi baada ya kuwasilisha matatizo yake kupitia tovuti hii.

  Ni wakati sasa kwa watanzania walioko ndani na nje ya nchi kutumia fursa hii ya maendeleo ya teknolojia hasa matumizi ya Tovuti ya Wananchi katika kuwasilisha hoja na kero mbalimbali, ambazo zinalenga kuboresha hali ya wananchi pamoja na utendaji wa Serikali kwa maendeleo ya Taifa.

  Tovuti ya Wananchi imekuwa msaada mkubwa kwa watumiaji. Ni wito kwa kila Mtanzania kutumia haki yake ya kikatiba ya kutoa maoni yake kwa uhuru kupitia Tovuti hii. Ikumbukwe kwamba mawasiliano hai katika maisha ni kama mishipa ya damu mwilini.

  0 0


  Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema wakati akifungua mkutano wa wadau mbalimbali wa kujadili program mpya mbili za masomo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili katika Biashara ya Kimataifa na Ugavi, Usimamizi mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na chuo hicho.
  Mmoja wa washiriki wa Mkutano huo akichangia wakati wa Mkutano huo.
  Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini majadiliano kuhusu program mpya mbili za masomo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili katika Biashara ya Kimataifa na Ugavi, Usimamizi wa mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na CBE.
  Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliohudhuria katika chuo hicho kujadili program mpya mbili za masomo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili katika Biashara ya Kimataifa na Ugavi, Usimamizi mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na chuo hicho.

  Na. Aron Msigwa – Dar es salasam.

  Tanzania bado inahitaji wataalam waliobobea katika Biashara ya Kimataifa na wale wanaosimamia mfumo wa uzalishaji, usambazaji na utunzaji wa bidhaa mbalimbali hususan mazao ya chakula ili kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo gharama kubwa ya uagizaji, utunzaji, usambazaji na hasara ya kuharibika kwa mazao inayowakumba wafanyabiashara walio wengi kabla ya kufikisha bidhaa zao kwa walaji.

  Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema wakati akifungua mkutano wa wadau mbalimbali wa kujadili program mpya mbili za masomo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili (Masters)katika Biashara ya Kimataifa na Ugavi, Usimamizi wa mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na chuo hicho.

  Amesema ili kukabiliana na changamoto hizo zinazowakumba wakulima na wafanyabiashara walio wengi hasa wale wa matunda ambao hupoteza karibu asilimia 40 ya mazao yao, lazima hatua madhubuti zichukuliwe kwa kuwajengea uwezo wa kitaalamu vijana wa Kitanzania ambao wataweza kukabiliana na changamoto ya wakulima kupata hasara kwa kuhakikisha mazao yanayotoka kwenye maeneo ya uzalishaji yanafika yakiwa salama.

  ‘Leo tuna mkutano wa wadau kwa sababu CBE tuko katika hatua za mwisho za mchakato wa kuanzisha Programu mpya za Shahada za uzamili katika katika masuala ya Ugavi (Procurement and Supply Chain Management) pia Shahada ya Uzamili katika Biashara ya Kimataifa (International Business Management) ili tuweze kutoa mafunzo yatakayowasaidia watanzania’’

  Amebainisha kuwa mazao kama matunda mara nyingi yamekuwa yakiharibika katika hatua ya kuvunwa, kusafirishwa na kuhifadhiwa jambo linalowasababishia hasara wakulima pamoja na wasafirishaji kwa kuwa hawana ujuzi na utalaam wa usimamizi wa bidhaa na mazao yao.

  Aidha, ameongeza kuwa asilimia 40 ya gharama hizo hutumika katika masuala ya usafirishaji na ufuatiliaji wa bidhaa husika kuifikisha kwa mlaji na kusisitiza kwamba gharama hizo husababishwa na mfumo mzima unaopaswa kupitiwa kabla ya kuifikisha bidhaa husika sokoni jambo ambalo lingerekebishwa kwa kuwa na wataalam wa kutosha kusimamia sekta hiyo.

  "Tanzania tunahitaji wataalam waliobobea katika eneo hili, tumekuwa na changamoto nyingi, mfano mfanyabiashara akinunua mahindi kutoka wilaya ya Mpanda au Namanyele anayapata kwa bei ya chini kwa kuwa eneo lile lina wazalishaji wengi, akiyasafirisha kuyaleta jijini Dar es salaa gharama yake inapanda karibu mara tano gharama hii ni ile inayoletwa na mfumo wa usambazaji wa bidhaa husika" Amesisitiza Prof. Mjema.

  Amesema uanzishwaji wa Programu hizo utayaangalia masuala mbalimbali yakiwemo ya ufungaji wa bidhaa husika, maghala ya kuhifadhia bidhaa hizo, suala la usafirishaji na usimamizi wa bidhaa husika yakiwemo mazao ya kilimo kuhakikisha kuwa hayaharibiki kabla ya kuwafikia walaji.

  Kuhusu uanzishwaji wa programu ya Biashara ya Kimataifa amesema kuwa kutokana na uchumi wa Tanzania kukua kwa kasi, watanzania wengi sasa wanafanya biashara ya Kimataifa na wengi wao wanakosa weledi katika kufikia matarajio ya biashara zao.

  Amesisitiza CBE imeliona eneo hilo kuwa linapaswa kutazamwa na kufanyiwa kazi ili Watanzania wanaofanya Biashara ya kimataifa waweze kupata mafanikio katika biashara za Kimataifa, kuelewa changamoto za biashara hiyo na vitu vinavyotakiwa kuzingatiwa ili kupata matokeo yaliyokusudiwa.

  "Uchumi wa Tanzania unakuwa kwa kasi, tunaanzisha programu hizi ili kuwawezesha watanzania kujua kwamba katika biashara za Kimataifa kuna changamoto gani, lazima tuwaandae watanzania kuingia katika uchumi wa dunia wakiwa na utaalam na uelewa wa kutosha kuhusu mikataba ya kimataifa na biashara ya kimataifa ili kukidhi haja ya nchi na mahitaji ya kimataifa" Amesisitiza Prof. Mjema.

  Amesema kuwa uanzishwaji wa programu ya Suppy Chain Management unatumia mtaala wa Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC) ambao pia unakubalika na Shirika la Kimataifa la Biashara (WTO) kwa kuwa unatumika kufundishia duniani kote na kuongeza kuwa mtaala huo wameushusha katika ngazi ya Taifa kwa kuangalia hali halisi ya mazingira na changamoto zinazoikabili Tanzania katika masuala ya Ugavi.

  "Wahitimu wa fani ya Usimamizi wa Mfumo wa Usambazaji wa bidhaa mbalimbali (Supply Chain Management) watakaopata vyeti vyetu vya kuhitimu wataweza kufanya mtihani wa ITC utakaowawezesha kukidhi viwango vya kimataifa na kuwawezesha wahitimu hao kukubalika duniani kote katika fani hiyo" Amesisitiza Prof. Mjema.

  Naye Mshauri Msimamizi kutoka SCM na Mwakilishi wa Shirika la Biashara la Kimataifa (WTO) Tanzania, Bw. Pamphill Kiluwa akizungumza wakati wa mkutano huo amesema kuwa uanzishwaji wa program ya Biashara ya Kimataifa na ile inayohusika na Ugavi na Usimamizi wa mfumo wa Uzalishaji, Usambazaji na Utunzaji wa bidhaa kutoka kwa mzalishaji kwenda kwa mlaji unalenga kuzalisha wataalam wenye weledi wa kutosha .

  Amesema kuwa uzalishaji wa wataalam hao utaweza kukidhi haja ya wateja kulingana na mahitaji yao ndani na nje ya nchi kwa kukidhi mahitaji yaliyopo katika masuala ya Ununuzi, usafirishaji ,uhifadhi wa bidhaa na vifaa mbalimbali katika ngazi ya Taifa na Kimataifa.

  Naye Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa chuo hicho Dkt. Michael Haule akizungumzia programu hizo amesema kuwa zitakuwa mkombozi kwa Watanzania huku akisisitiza kuwa kumekuwa na mapungufu katika masuala ya Ugavi na Manunuzi hasa upande wa kununua,kupakia na kusafirisha bidhaa mbalimbali kutoka eneo la uzalishaji hadi kumfikia mlaji wa mwisho na kusisitiza kuwa uanzishwaji wa programu hizo

  Amesema Shahada ya Biashara ya Kimataifa itawaezesha wahitimu kufanya kazi katika mashirikia na taasisi za kimataifa za ndani na nje ya nchi na kueleza kuwa ufundishaji wa kozi hizo utachukua miezi 18.

  Dkt. Haule amebainisha kuwa ufundishaji wa kozi hizo chuoni hapo utatumia mbinu na Teknolojia ya kisasa kuwawezesha wanafunzi kusoma kwa njia ya mtandao huku akibainisha kuwa chuo hicho sasa kiko katika hatua za mwisho za majadiliano yanayohusisha wadau mbalimbali kupata ushauri wa kitaalam ili kiweze kuufanyia kazi kuboresha mitaala hiyo kabla ya kuwasilisha Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa ajili ya usajili ili ianze kutumika ikiwa ni hatua ya mwisho.

  Aidha, amesema kuwa katika kufanikisha hatua mbalimbali za mchakato wa kuanzishwa kwa program hizo mpya, wataalam wa CBE walitembelea mikoa 17 wakihoji waajiri, wanafunzi , wananchi na wadau mbalimbali maeneo ya uzalishaji ili kupata uhakika wa mahitaji halisi ya soko la kozi hizo nchini Tanzania.

  0 0

  Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika wa Taasisi ya Marekani ya Kudhibiti Magonjwa – (Centre for Disease Control and Prevention – CDC) Dkt. Michelle Roland akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi magari tisa yenye thamani ya Shillingi Millioni mia nane na kumi kwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016.

  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa pamoja na mwakilishi wa katibu Mkuu wa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Claud Kumalija wakionyesha ufunguo wa gari mbele ya waandishi wa habari na wageni waalikwa kuashiria kupokea magari tisa yaliyotolewa na Shirika la ICAP Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016. Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akiwasha gari kama ishara ya kupokea magari tisa yenye thamani ya Shillingi Millioni mia nane na kumi kutoka Shirika la ICAP Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016. Hafla ya makabidhiano ya magari hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (wa kwanza kulia) pamoja na wageni waliohudhuria katika hafla ya kukabidhiana magari wakiangalia baadhi ya magari yaliyotolewa na Shirika la ICAP Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016. Hafla ya makabidhiano ya magari hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
   
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhiana magari tisa yenye thamani ya Shillingi Millioni mia nane na kumi kutoka Shirika la ICAP Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016. Kushoto kwake ni Claud Kumalija mwakilishi wa katibu Mkuu wa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Dkt. Fatuma Mrisho akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhiana magari tisa yenye thamani ya Shillingi Millioni mia nane na kumi kati ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Shirika la ICAP Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016. Kushoto kwake ni Claud Kumalija mwakilishi wa katibu Mkuu wa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kulia kwake ni Dkt. Michelle Roland Mkurugenzi Mkaazi wa Taasisi ya Marekani ya Kudhibiti Magonjwa – (Centre for Disease Control and Prevention – CDC).(PICHA ZOTE NA IMMANUEL GHULA)


  Na: Veronica Kazimoto Dar es Salaam

  OFISI ya Taifa ya Takwimu imekabidhiwa magari tisa aina ya Land cruiser yenye thamani ya Dola za kimarekani laki nne na elfu tano ($ 405,000) sawa na Shillingi za kitanzania Milioni mia nane na kumi (810,000,000/=) kutoka Shirika lisilo la kiserikali la ICAP linaloendeshwa na Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika mwezi Septemba, 2016.

  Akizungumza katika hafla ya kukabidhiana magari hayo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amelishukuru Shirika la ICAP kwa msaada huo ambao utasaidia kupunguza gharama za kukodi magari kwa ajili ya kufanyia utafiti.

  “Napenda kuchukua fursa hii kulishukuru Shirika la ICAP kwa kutupatia msaada huu wa magari tisa yenye thamani ya Shillingi milioni mia nane na kumi. Huu sio msaada mdogo kwani fedha ambazo zingetumika kukodisha magari ya utafiti, sasa zitatumika katika shughuli nyingine za kimaendeleo,” amesema Dkt. Chuwa.

  Amesema katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), takwimu rasmi zinahitajika ili kupima utekelezaji wake na hivyo utafiti huu utakapokamilika utasaidia kutoa takwimu zitakazotumika kupima utekelezaji wa malengo hayo.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la ICAP Tanzania, Dkt. Fernando Morales amesema utafiti huu unalenga kupima Viashiria na Matokeo ya UKIMWI nchini ili kujua ni kwa kiwango gani Tanzania imepiga hatua katika kupambana na ugonjwa huo.

  Dkt. Morales amesema msaada huu wa magari utasaidia kurahisisha usafiri wa kutoka eneo moja la utafiti hadi lingine na kuweza kusaidia katika upatikanaji wa taarifa muhimu za utafiti huu.

  Nae Mkurugenzi Mkaazi wa Taasisi ya Marekani ya Kudhibiti Magonjwa – (Centre for Disease Control and Prevention – CDC) Dkt. Michelle Roland amesema kutokana na utafiti huu kufanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya ukusanyaji wa takwimu, kutasaidia kupunguza gharama ambazo zingetumika kama utafiti huu ungefanyika kwa njia ya kutumia madodoso ya karatasi.

  Ameongeza kuwa utafiti huu utafanyika kwa kutumia sampuli wakilishi ya kaya zipatazo 15,800 Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, na kuwafikia walengwa wapatao elfu arobaini (40,000) wakiwemo watoto wasiopungua elfu nane (8,000).

  Matokeo yanayotarajiwa kupatikana katika utafiti huo ni pamoja na taarifa sahihi kuhusu hali ya maambukizi mapya ya VVU, upatikanaji wa huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU hapa nchini na kutambua ni kwa kiwango gani huduma hizi zimesaidia katika kuudhibiti ugonjwa wa UKIMWI.

  Utafiti huu wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utafanywa kwa pamoja na Shirika la ICAP Tanzania, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Tanzania Bara, Wizara ya Afya kwa Tanzania Zanzibar, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar (OCGS), Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) na Tume ya UKIMWI Zanzibar (ZAC).

  0 0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

  Taarifa iliyotolewa leo tarehe 23 Juni, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inasema uteuzi huu umeanza tarehe 21 Juni, 2016.Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Cuthbert Mhilu ambaye amemaliza muda wake.Prof. Maboko ni Mhadhiri wa Jiolojia  katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).

  Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Omari Ali Amir kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu.

  Kabla ya uteuzi huo Dkt. Omari Ali Amir alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inasema uteuzi wa Dkt. Omari Ali Amir umeanza tarehe 21 Juni, 2016.

  Utaratibu wa kujaza nafasi ya Mkurugenzi Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa bahari kuu ni wa kubadilishana kila baada ya miaka mitatu kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, ambapo Mkurugenzi Mkuu akitoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi Naibu Mkurugenzi Mkuu hutoka upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kinyume chake.


  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  23 Juni, 2016

older | 1 | .... | 889 | 890 | (Page 891) | 892 | 893 | .... | 1898 | newer