Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu Bunge Walemavu Vijana Kazi na Ajira Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo Bungeni leo kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Serikali dhidi ya waajiri wote wanaoshindwa kuwasilisha michango ya waajiriwa wao katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ambapo tayari Serikali iko kwenye hatua za mwisho kukamilisha mchakato wa kuunda kikosi kazi kitakachoshughulikia swala hilo.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mh. George Masaju leo Bungeni Mjini Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrisom Mwakyembe akijibu moja ya hoja zilizotolewa Bungeni leo na Mbunge wa Nchemba Mhe. Juma Nkamia aliyetaka kujua uhalali wa mtuhumiwa aliyetenda kosa la jinai la kumtukana Rais kuachiwa huru na kwenda kutafuta fedha za kulipa faini ilihali kosa alilotenda limemdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu Bunge Walemavu Vijana Kazi na Ajira, Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Mbunge wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde leo Bungeni Mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akijibu miongozo iliyoombwa na wabunge mapema leo Bungeni mjini Dodoma kabla ya Kuahirisha shughuli za Bunge leo Mjini Dodoma. Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kisasa ya mjini Dodoma wakiwa katika ukumbi wa Bunge kwa lengo la kujifunza majukumu ya Bunge leo Mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt. Susan Kolimba akifafanua kuhusu hatua zinazochukuliwa ili kuimarisha Balozi za Tanzania katika nchi mbalimbali ikiwa ni moja ya hatua za kuimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na mataifa mbalimbali.
Naibu Waziri Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akijibu maswali yaliyoulizwa na Wabunge leo Bungeni juu ya mikakati ya Serikali kuwawezesha wanawake kupitia Benki ya wanawake kwa kufungua madirisha maalum Katika Mikoa mbalimbali hapa Nchini yatakayosaidia kuwasogezea wanawake huduma za Benki hiyo ili waweze kujikwamua kiuchumi. Wanafunzi wa chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Wakiwasili katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Mjini Dodoma leo kwa lengo la kujifunza jinsi Bunge linavyotekeleza majukumu yake.

ULEDI: MICHANGO YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII TUTAPELEKA KWA WAKATI

$
0
0
KATIB1 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Waziri Mkuu,  Bunge na Siasa, Bw. Uledi Mussa akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo kwenye kikao kilichofanyika mjini Dodoma leo mchana (Jumanne, Juni 21,2016).  Picha na Irene Bwire wa Ofisi ya Waziri Mkuu)
KATIB2 
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa OWM  anayeshughulikia masuala ya Waziri   Mkuu,  Bunge na Siasa, Bw. Uledi Mussa  (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo kwenye  kikao kilichofanyika mjini Dodoma leo mchana (Jumanne, Juni 21, 2016). (Picha na Irene Bwire wa Ofisi ya Waziri Mkuu)
KATIB3Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa OWM anayeshughulikia masuala ya Waziri   Mkuu,  Bunge na Siasa, Bw. Uledi Mussa  alipokuwa akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo kwenye kikao kilichofanyika mjini Dodoma leo mchana (Jumanne, Juni 21, 2016). (Picha na Irene Bwire wa Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………

KATIBU MKUU Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Waziri Mkuu, Bunge na Siasa, Uledi Mussa amesema atahakikisha michango ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya watumishi wa Ofisi hiyo inafikishwa kwa wakati.Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, 21 Juni, 2016)  wakati akijibu maswali ya watumishi wa Ofisi hiyo mjini Dodoma katika  maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma inayoanzia Juni 16 hadi 23 ya kila mwaka.

Kila mwaka Tanzania imekuwa ikiungana na mataifa mengine ya Bara la Afrika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika  ambayo kauli mbiu ya mwaka huu ni Uongozi wa Umma kwa Ukuaji Jumuishi:kuelekea katika Afrika tunayoitaka.“Nitafuatilia michango ya watumishi katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuhakikisha inafika kama inavyotakiwa na kwa wakati ili hata wanapomaliza muda wao wa utumishi wasihangaike,” amesema.

Katika hatua nyingine Uledi amewataka Wakuu wa Idara kuandaa  mpango wa mafunzo kwa watumishi na washirikishe kila mtu katika idara husika kabla ya kuuwasilisha kwake.Katibu Mkuu aliyasema hayo wakati akijibu maswali ya baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo, ambapo Anjani Ngulukia (Msaidizi wa Ofisi) alitaka kupatiwa ufanunuzi kuhusu suala la michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo imekuwa haipelekwi kwa wakati.

Pia mtumishi mwingine Ernest Msabalala ambaye ni Mtunza Kumbukumbu Mkuu aliomba ofisi iandae utaratibu wa kuwa na mafunzo kwa watumishi ili kuongeza ufanisi wa kazi.

MACHINGA JIJINI MWANZA WAKUTANA KUAMUA HATIMA YAO.

$
0
0

Mgeni Rasmi, Dkt.Kissui Steven Kissui ambae ni Mwenyekiti wa Shindano la Uwezeshaji Kiuchumi na Ajira Tanzania, akifungua Mkutano wa Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) Jijini Mwanza uliofanyika hii leo.

Na BMG

Mkutano huo ambao uliandaliwa na Shirika la Machinga Mkoa wa Mwanza SHIUMA, ulilenga Machinga kujadiliana na wadau wengine wa Uwekezaji ikiwemo taasisi za kifedha, juu ya Kurasimisha biashara zao na kuwekwa kwenye mifumo rasmi ya Kibiashara na Kijamii.

Machinga wamesema changamoto kubwa zinazowakabiri ni Ukosefu wa Mitaji ya Biashara, Maeneo ya Kufanyia Biashara pamoja na Ukosefu wa Elimu Biashara. Wamesema wanataka nao watambulike na taasisi za kifedha ili wapate fursa ya kukopesheka ili kukuza mitaji yao.

Mgeni Rasmi, Dkt.Kissui Steven Kissui ambae ni Mwenyekiti wa Shindano la Uwezeshaji Kiuchumi na Ajira Tanzania, akifungua Mkutano wa Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) Jijini Mwanza uliofanyika hii leo.

Katibu wa Shirika la Machinga Mkoa wa Mweanza SHIUMA, Venatus Anatory, akizungumza katika Mkutano wa Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) Jijini Mwanza uliofanyika hii leo.

Mmoja wa Machinga akizungumza katika Mkutano wa Machinga Jijini Mwanza uliofanyika hii leo

Mmoja wa Machinga akizungumza katika Mkutano wa Machinga Jijini Mwanza uliofanyika hii leo

Mmoja wa Machinga akizungumza katika Mkutano wa Machinga Jijini Mwanza uliofanyika hii leo

Mwenyekiti wa SHIUMA, Matondo Masanja (katikati), akiwa na wadau wengine katika Mkutano wa Machinga Jijini Mwanza uliofanyika hii leo

Machinga Jijini Mwanza

Machinga Jijini Mwanza

Machinga Jijini Mwanza wakinyoosha mikono juu ikiwa ni ishara ya kukubaliana kwa pamoja na hoja yakurasimisha biashara zao, Kupata maeneo rasmi ya Kufanyia biashara katikati ya Jiji pamoja na Kutambulika katika taasisi za kifedha ili waweze kukopesheka na kupatiwa elimu ya kibiashara.

Tübingen International Africa Festival in Germany opens it doors from the 21 to 24 July 2016

$
0
0
MAKUN1 
The International Afrika Festival Tübingen in Southern Germany The Republic of Burundi is country of honor 2016 From the 21 to 24 July 2016, Tübingen International Africa Festival in Germany opens it doors wide open to arts, culture, dialog tourism, media.. operators under the theme „ not black, not white but colored for a peaceful world“ Exhibitors, festival lovers and cultural tourist in search of plattforms for a short vacation are cordially invited to attend and enjoy. 

Founded since 2007 by Sunjo & Susan TATAH; the International Africa Festival Tübingen in Germany, is a FOUR DAY annual festival with focused on showing casing Africa´s role and contribution to humanity and diversity as well as world peace and stability bringing people of African descent and others from all over the globe, irrespective of their countries of origin, religious background, gender and status together.
MAKUN2
The Festival tells the story of people of Africa descent worldwide, thereby providing a platform to all African interested persons to share and be part of the heritage.As a young, dynamic rapidly growing forward thinking NGO, The International African Festival Tübingen is a platform for mobilization and presentation of cultural activist, Business and developmental activist, , individual donors and philantrophic activist in all sectors. 

The festival is a compact format composed of a varierty of authentic projects- presenting Africa´s know-how – Huge market of Arts, Handworks, Authors, Producers, Designers, Film makers, culinary Arts… as well as full package entertainment such as talents shows with bands playing live music, traditional Ballets, dance performances, Forums, workshops and parties with top Djs / Mcs. 

Each edition bringing together more than 100,000 fun and peace loving visitors. AfrikAktiv invites you to come and visit the International African festival in Germany powered by the African Diaspora and dedicated to the development of its continent and people. Come and have full service funtime. As a family oriented Festival, children and youths are the heartbeat for our festival, we cherish every one of them. 

Our festival offers a special integrated children and youth mini format festival with activities for our young people – special artist with workshops –Acrobatics, clowning, graffitis, dance, creative handworks, special concert just for the young generation under the theme “Empowering the next generation with cultural diversity and humanity values“ For a more visibility on opportunities and potentials available on the African continent and its Diaspora, our festival offers a platform for partnership to all pan-african media and journalist. 

Our festival reaches out to more than million people worldwide particularly on the African continent, here you meet your tailored made target groups. Join and follow us on social media – Facebook, Instagrams, Twitter, youtube..The International African Festival Tübingen, Germany offers opens you the door to enjoy Africa´s authentic Arts and listen to African tell their story the way it is.For more information: Web: www.afrikafestival.net

UZIBUAJI WA MITARO UKIENDELEA JIJINI MWANZA.

$
0
0
Uzibuaji wa Mitaro ukiendelea katika Mitaa mbalimbali ya Katikati ya Jiji la Mwanza. BMG inatoa pongezi za dhati kwa Uongozi wa halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa zoezi hili maana lisipofanyika kwa muda mrefu, mitaro hii huziba, mvua inaponyesha huwa Mitaa ya Jiji haitamaniki tena na inapoteza hadhi ya Jiji la Mwanza.

SEHEMU YA HOTUBA YA MAKAMU WA RAIS KATIKA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA WANAWAKE WAJASIRIAMALI

WAZIRI MBARAWA AFUNGUA MKUTANO WA 19 WA USAFIRI WA ANGA KWA NCHI ZA SADC

$
0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifungua mkutano wa 19 wa Usafiri wa anga kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es Salaam jana leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) Bwana Hamza Johari akifafanua jambo katika mkutano wa 19 wa Usafiri wa anga kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa oganaizesheni ya Usafiri wa Anga kwa nchi za SADC Bwana Geofrey Moshabesh akitoa taarifa ya utekelezaji wa masuala ya usalama wa anga kwa wajumbe wa mkutano wa 19 wa Usafiri wa anga kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es Salaam leo
Wajumbe wa Mkutano wa 19 wa Usafiri wa anga kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa

UHURU FM YATOA MSAADA WA VITU MBALIMBALI VYA SH. MILIONI 3 KWA CHUO CHA UFUNDI STADI KWA WENYE ULEMAVU CHA YOMBO, DAR ES SALAAM

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru FM, Angel Akilimali akijaribu kushona wakati yeye na wafanyakazi wa Radio hiyo, walipowasili kwenye Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kwa wenye ulemavu kilichopo Yombo Kata ya Kiwalani Temeke Dar es Salaam, kutoa msaada wa vitu mbalimbali ambavyo ni pamoja na Mchele, unga, saruji, sabuni kasha la huduma ya kwanza, mifagio, mafuta ya kula, kofia maalum kwa wenye ulemavu wa ngozi, miwani, viti, mafuta maalum kwa wenye ulemavu wa ngozi, vifaa vya michezo ambavyo ni jezi za mpira wa miguu na netiboli, mipira ya kawaida na mipira ya kengere kwa wenye ulemavu wa macho, Kamba ya kuvuta kwa ajili ya walemavu, vyote vyenye thamani za zaidi ya sh. milioni 3. zifuatazo ni picha mbalimbali kuhusiana na tukio hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru FM, Angel Akilimali akimvalisha miwani malum, mwanafunzi wa Chuo hicho mwenye ulemavu wa ngozi.
MKurugenzi Mtendaji wa Uhuru DM Angel Akilimali akimvisha mtandio maalum mwanafuzni wa Chuo hicho mwenye ulemavu wa ngozi. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi kwa wenye ulemavu Yombo, Mariam Chellangwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru FM akikabidhi mpira wenye kengere ndani, kwa ammoja wa wanacfunzi wa Chuo hicho mwenye ulemavu wa macho.
Baadhi ya viongozi wa Uhuru FM, wakiwa na Mwalimu wa Chuo hicho, Aloyce Mkuna (wapili kushoto), baada ya kuwasili kwenye chuo hicho. Kulia ni Mhariri wa Habari Pius Ntiga, Meneja Rasilimali watu na Utawala Narsis Mbise, Sigoli Paul ambaye ni Mwandishi na Mtangazi
Makamu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi kwa wenye ulemavu Yombo, Mariam Chellangwa akiwakaribisha rasmi msafara mzima wa Uhuru FM ulipowasili katika chuo hicho.

Wafanyakazi wa Uhuru FM wakiwa katika picha za pamoja na wanafunzi wa Chuo hicho, mwishoni mwa ziara hiyo. Picha na Emmanuel Ndege. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Article 20

$
0
0
Mamlaka ya viwanja vya ndege tanzania (taa), kesho tarehe 23 juni 2016 siku ya kilele cha wiki ya utumishi wa umma, inawakaribisha wananchi na watumishi wa umma kuja kujua na kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu viwanja vya ndege. 

eneo: makao makuu ya taa, karibu na kiwanja cha zamani cha ndege, barabara ya nyerere. 

muda: huduma zitatolewa kuanzia saa 01:30 asubuhi hadi saa 9:30 jioni. 

kaulimbiu- “uongozi wa umma ukuaji jumuishi kuelekea katika afrika tunayoitaka”
***nyote mnakaribishwa***

imetolewa na kitengo cha sheria na mahusiano taa,
kny: mkurugenzi mkuu
22/06/2016

CCM YAWASILISHA GHARAMA ZA UCHAGUZI KWA MSAJILI WA VYAMA LEO

$
0
0
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa CCM, Stanslaus Mamilo akimkabidhi vielelezo vya CCM vya matumizi ya Uchaguzi mkuu uliopita, kwa Mwangalizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama, Mkuu wa Masijala Galasia Simbachawene, leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo).

Na Bashir Nkoromo

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) leo kimewasilisha kwa Msajili wa Vyama, hati zake za gharama ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana, na kuwa chama cha pili kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria za uchaguzi nchini.

Ujumbe wa CCM uliongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa CCM, Stanslaus Mamilo na Mwanasheria wa CCM Adamson Sinka na kuwasilisha hati na vielelezo vya matumizi hayo kwa Mwangalizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama, Mkuu wa Masijala Galasia Simbachawene.

Akikabidhi hati na vielelezo hivyo Mamililo alisema, CCM imelichukua swala hilo umuhimu mkubwa ndiyo sababu imefanya hivyo ndani ya wakati kwa kuwa mda wa kuwasilisha matumizi ya gharama za uchaguzi kwa wagombea na vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 2015, ni Juni 25, 2016.

"Sisi hatuwezi kuwa kama vyama vingine kwa kuwa ni Tasisi kubwa ambayo  haina budi kufuata kanuni, taratibu na sheria za nchi hasa ikizingatiwa kwamba CCM ndiyo chama tawala hivyo lazima kionyeshe mfanomzuri ili kiendelee kuwa chama cha kuigwa ", alisema Mamilo.Mamililo aliwasilisha hati na vielelezo vya matumizi ya Chama na wagombea wa nafasi mbalimbali  kupitia CCM ikiwemo Urais, Wabunge na Madiwani.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa hati na vielelezo hivyo, Galasia alisema, katika vyama vyote vilivyoshiriki katika uchaguzi mkuu uliopita ni CCM na ACT-Wazalendo ndivyo ambavyo tayari vimekamilisha bila shuruti sheria ya  kuwasilisha gharama zake za uchaguzi.

Alisema, uwasilishaji wa gharama hizo ni muhimu sana kwa kuwa ni suala la kisheria, kwa kuwa vyama au wagombea wanaoshindwa kutimiza sheria hiyo watachukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa makahamani ambako wakipatikana kwa upande wa Chama kitafungiwa kushiriki uchaguzi wowote utakaofuatia na kwa upande wa wagombea mhusika atatozwa faini ya sh. milioni 2, au kifungo cha mwaka mmoja jela au vyote pamoja.

Kulingana na Sheria ya Uchaguzi, chama kinatakiwa kisitumie ghara inayozidi sh. bilioni 17, na kikilazimika kuzidi kiwango hicho kisididi zaidi ya asilimia 15 ya kiwango kinachotakiwa, huku kwa upande wa wagombea kiasi kinachotakiwa ni sh. bilioni saba na kwa wabunge sh. milioni 33 hadi 88 kulingana na mazingira ya jimbo.

Article 18

$
0
0

Ofisi ya mwanasheria Mkuu wa Serikali inatoa taarifa kuwa itakutana na  wadau wake wote siku ya  ALHAMISI  TAREHE 23 JUNI  21016, ili kupokea  na kujibu malalamiko, kero, hoja na maoni mbalimbali kuhusu Utendaji kazi wa Ofisi ikiwa ni maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2016.
Mkutano huo utafanyika kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Ndogo ya Bunge, Dar es Salaam.

Wadau wote wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanaombwa kuhudhuria katika Mkutano huo muhimu.

Imetolewa na:                 

 Gerson Mdemu
                        NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

Kijana aliyewezeshwa na Airtel FURSA aweza kutoa ajira kwa vijana wengine 15

$
0
0

Kijana Innocent Kipondya aliyewezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa kuwawezesha vijana hapa nchini ujulikanao kama Airtel FURSA Tunakuwezesha akimuonyesha Meneja Masoko wa Airtel Kanda ya ziwa Emmanuel Raphael mazao aliyepota baada ya kuwezeshwa, alipotembelewa shambani kwake hapo jana.
Kijana Innocent Kipondya aliyewezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa kuwawezesha vijana hapa nchini ujulikanao kama Airtel FURSA Tunakuwezesha akibeba mazao aliyofuna baada ya kuwezeshwa miezi 11 iliyopita.

Kijana Innocent Kipondya (juu ya Toyo) aliyewezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa kuwawezesha vijana hapa nchini ujulikanao kama Airtel FURSA Tunakuwezesha akiwa anaelekea sokoni baada ya kuvuna mazao yako na kupata faida na kuweza kuajiri vijana wengine 15.
 
 Mwanza, Mafanikio ya Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kuhakikisha Kijana mkulima mdogo aliyewezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA Tunakuwezesha ameweza kuongeza ukubwa wa shamba, mazao na kuajiri wengine yameanza kuonekana baada ya mkulima mdogo Innocent Kipondya wa kijiji cha Mwalogwabagole wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kuajiri vijana wenzake 15 shambani kwake.

Kupata mafanikio kwa Innocent kunafuatia miezi 11 iliyopita Airtel FURSA kumwezesha pampu ya kuvuta maji na mpira wake, ikiwa ni pamoja na bajaji kwa ajili ya kusafirisha mazao sokoni.

Innocent amesema ilikuwa inampa wakati mgumu kulima wakati wa kiangazi lakini sasa anaweza kulima wakati wote kwa kumwagilia kutokana na pampu ya kuvuja maji aliyowezeshwa na Airtel FURSA.

“ Kabla sijashikwa mkono na Airtel Fursa nilikuwa napata changamoto ya mazao kukauka kutokana na maji kuwa mbali, lakini sasa licha ya kupanua kilimo, nina uhakika wa kulima mwaka mzima” amesema Innocent

Innocent amemwambia mwandishi wa habari hii kuwa, soko la nyanya ni la uhakika na sasa ameamua kulima mbogamboga na kupanua kilimo cha mpunga, japo kuwa wadudu waharibifu ni kikwazo kwake kupata mazao mengi zaidi. Ameipongeza Airtel kwa kuwajali vijana hapa nchini, na sasa amefanikiwa kusimamisha jengo na baadaye ana mpango wa kununua wanyama kazi kwa ajili ya kulima.

Meneja Masoko wa Airtel Kanda ya ziwa Emmanuel Raphael ,mbali na kumpogeza Innocent kwa bidii aliyoionyesha alipomtembelea, amesema dhana ya kampuni yake ni kuendelea kuinua vijana na wajasiliamali wadogo hapa nchini ili kuweza kubadilisha maisha yao.

“Miezi 11 nilikuja hapa, shamba la nyanya lilikuwa moja tu,lakini sasa naona mashamba manne,bustani ya mbogamboga,kilimo cha mpunga hata vitungu,nampongeza sana Innocent” aliongeza Emmanuel

Airtel Fursa ni mradi wa kijamii wenye lengo la kuhamasisha vijana, kuwapa fursa ya kujiendeleza kibiashara na kuwapa ujuzi utakoawawezesha kuimarisha biashara zao katika mikoa yote nchini .

SAGCOT WASAINI MAKUBALIANO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAKAMPUNI ZILIZOOMBA UFADHILI WA FEDHA KWAAJILI YA UIMALISHAJI WA VIWANDA PAMOJA NA UKUZAJI WA KILIMO.

$
0
0
MFUKO wa kichocheo wa SAGCOT wasaini makubaliano ya utekelezaji wa Mradi na kampuni zilizoomba ufadhali wa Fedha kwaajili ya uimarishaji wa Viwanda pamoja na ukuzaji wa Kilimo hapa nchini jijini Dar es Salaam leo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, Ami Mpungwe akizungumza katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo amesema kuwa Mfuko wa SAGCOT wamesaini mikataba kwaajili ya kibiashara kwanzia mtaji kati ya Dola Za Kimarekani milioni 50 hadi 100 zitakuwa zikitolewa  kwa miradi kupitia madirisha ya Matching Grant Fund(MGF) ambao utakuwa ukitatua changamoto za wakulima na masoko yao.

Pia amesema kuwa dirisha jingine ni la Social Venture Capital(SVC) dirisha hili litalenga kuwzesha kujengwa kwa viwanda vikubwa ba vya kati ili kutoa masoko kwa wakulima hasa wa maeneo amayo yana mazao mengi lakini hakuna kiu ya sekta binafsi ya kuwekeza katika maeneo hayo.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joel Malongo akizungumza na vongozi wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, wawakilishi wa vyama vya wakulima na wawakilishi wa wabia wa Maendeleo jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye kinyang'anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, Ami Mpungwe akizungumza na wawakilishi wa vyama vya wakulima na wawakilishi wa wabia wa Maendeleo  hapa nchini jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye kinyang'anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko.
 Katibu Mkuu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, John Kyaruzi akizungumza na wawakilishi wa vyama vya wakulima na wawakilishi wa wabia wa Maendeleo  hapa nchini jijini Dar es Salaam leo pamoja na kuwakaribisha wawakilishi wa wakulima kwenda kuelezea kazi zao mbele ya Mgeni rasmi kutoka wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji.
Mwenyekiti kampuni ya Cane Care Limited, Dr. George Mlingwa akifafanua jambo mbele ya Mgeni Rasmi na mwakilizshi wa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Joel Malongo kuhusiana na kampuni yake ya Kilimo cha Miwa pamoja na  hatua za uandaaji wa utengenezaji wa Sukari hapa nchini katika kiwanda chake Kidogo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joel Malongo (Mwenye tai nyekundu waliosimama) akisuhudia  wawakilishi wa vyama vya wakulima wakisaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye kinyang'anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko huo jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joel Malongo katikati kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, Ami Mpungwe na  Katibu Mkuu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, John Kyaruzi wakiwa katika mkutano huo wa wakati wa kusaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye kinyang'anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano wa kusaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye kinyang'anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

WAZIRI WA AFYA , MAENDELEO YA JAMII , JINSIA, WAZEE NA WATOTO ATEMBELEA VIJIJI VILIVYOKUMBWA NA MLIPUKO WA UGONJWA USIOJULIKANA WILAYANI KONDOA.

$
0
0
Mbunge wa Kondoa,Juma Nkamia akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kutembelea vijiji vilivyokumbwa na mlipuko wa ugonjwa usiojulikana  katika kijiji cha mwaisabe, Wilayani Kondoa.
Katika ziara hilyo ameambatana na wataalam mbalimbali ambao wameweka kambi kwenye vijiji hivyo ili kufuatilia wagonjwa majumbani.vile vile ametembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya kondoa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Kondoa Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kutembelea vijiji vilivyokumbwa na mlipuko wa ugonjwa usiojulikana  katika kijiji cha mwaisabe,Wilayani Kondoa.

SERIKALI YAIMARISHA UDHIBITI WA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI NA BIASHARA YA MADINI

$
0
0
w1 
Kaimu Mtendaji Mkuu kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Bw. Gilay Shamika akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwenye wakala hiyo ikiwemo kuongezeka kwa makusanyo ya mirabaha kwenye shughuli za uzalishaji na uuzaji wa madini nchini. Kulia ni Msemaji wa Wakala hiyo Bw. Yisambi Shiwa.
w2 
Msemaji wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Bw. Yisambi Shiwa akiwaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam namna walivyoimarisha udhibiti wa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini kwa kuongeza wakaguzi migodini na vituo vya ukaguzi kwenye maeneo mbalimbali na kuhakikisha shughuli hizo zinafanyika kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira. Kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa TMAA, Bw. Gilay Shamika na kulia ni Mwanasheria Bw. Gimonge Ngutunyi.
PICHA NA FATMA SALUM (MAELEZO).

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS NA MCHUMI MKUU WA BENKI YA DUNIA MSTAAFU

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na aliyekuwa Makamu wa Rais na Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia Profesa Justin Yifu Lin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katima mazungumzo na aliyekuwa Makamu wa Rais na Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia Profesa Justin Yifu Lin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016. Kushoto ni Balozi wa China nchini Dkt. Dkt. LU Younqing,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Balozo wa China nchini Dkt Lu Younqing baada ya kuwa na mazungumzo na aliyekuwa Makamu wa Rais na Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia Profesa Justin Yifu Lin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 22, 2016. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizarta ya Viwanda na Biashara Dkt. Adelhem James Meru na Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Asia katika Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Mbelwa kairuki.PICHA NA IKULU

kikao cha Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

$
0
0



Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi (kushoto) akizungumza na watumishi wa Sekretarieti hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasimimali watu Bibi Victroria Fovo.

Baadhi ya wakuu wa Idara wakinukuu hoja na maoni ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira wakati wa kikao kati ya Katibu wa Sekretarieti hiyo na Watumishi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

Baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira wakisikiliza ufafanuzi kutoka kwa Katibu wa Sekretarieti hiyo Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani) baada ya kuwasilisha maoni na ushauri kuhusiana na utendaji kazi wa taasisi hiyo.

Serikali yapokea msaada wa madawati 300 toka Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania.

$
0
0

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem (katikati) akikabidhi msaada wa madawati kwa Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga, kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima mapemahii leo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem (katikati) pamoja na Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga (kulia) wakiwa wamekalia madawati ambayo yametolewa msaada kwa serikali ya Tanzania, kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga (Katikati aliyekaa) kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem na kulia ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi na Wakurugenzi toka wizara hiyo mara baada ya kupokea msaada wa madawati toka ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam. 




Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akikabdhi msaada wa madawati kwa Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga akitoa neno la shukrani kwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem wakati akipokea msaada wa madawati toka kwa balozi huyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo

———————————————————————–

Na Eliphace Marwa- Maelezo

Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa madawati 300 toka Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya kutatua tatizo la uhaba wa madawati katika shule za msingi hapa nchini.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga kwa niaba ya serikali alisema kuwa amesema kuwa kupokea madawati hayo ni sehemu ya kutekeleza wito wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

“Waziri Mkuu alitutaka sisi katika nafasi zetu tuwashirikishe wadau mbalimbali ili kuweza kutekeleza adhma ya serikali ya kutatua tatizo la wanafunzi kukaa chini ili waweze kupata mazingira bora ya kupata elimu, alisema Balozi Maige.

Balozi Maigaaliongeza kuwa Kuwait iko tayari kuisaidia nchi ya Tanzania kwa kuwajengea uwezo wataalam toka Tanzania kwa kuwapa elimu ya mafuta na gesi kwani Kuwait ina uzoefu mkubwa katika sekta ya mafuta na gesi.

Naye Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem alisema kuwa Serikali ya Kuwait itaendelea kutoa misaada kwa serikali ya Tanzania kadri itakavyowezekana pindi pale itakapohitajika.

Aidha Balozi Maiga alitumia muda huo kutoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu ujio wa Rais wa Rwanda Paul Kagame hapa nchini siku ya Julai Mosi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi.

“Rais wa Rwanda atawasili hapa nchini Julai Mosi na ataweka saini makubaliano mbalimbali waliyofikia kati ya Tanzania na Rwanda baada ya hapo Rais Kagame ataambatana na mwenyeji wake Rais Magufuli mpaka katika viwanja vya maonesho vya Sabasaba ambapo Rais Kagame atayazindua rasmi maonesho hayo ya arobaini”, alisema Balozi Maiga.

Aidha Balozi Maiga aliongeza kuwa Rais Kagame jioni atakaribishwa Ikulu na mwenyeji wake Rais Magufuli kwa ajili ya dhifa ya kitaifa.

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene (wapili kulia) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama watatu kulia) bungeni mjini Dodoma Juni 22, 2016. Wengine kutoka kushoto ni Mbunge wa Babati Vijijini Jitu Vrajlal Son, , Mbunge wa Bukoba Vijijini Jasson Rweikiza,Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde, Mbunge wa Korogwe Stephen Ngonya na Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wananchi kutoka jimbo la Ukongwa waliotembeklea bunge kwa mwaliko wa Mbunge (wapili kulia) Juni 22, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Utumishi, na Utawala Bora , George Simbachawene (kulia) na Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay (kushoto) kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Juni 22, 2016. Wapili kushoto ni Mosses Kirway na wapili kulia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu yaTaifa ya CCM, Thomas Lulu, wote wakiwa ni wageni waliotembelea Bunge wakitoka Mbulu.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wizara ya Ardhi kubaini taasisi zinazodaiwa fidia na wananchi

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 itabaini taasisi zote na watu binafsi wanaodaiwa fidia na wananchi ili waweze kulipa fidia hizo.

Akiongea leo Bungeni, mjini Dodoma Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Angelina Mabula amesema kuwa ni kweli tatizo hilo lipo na tayari Serikali imechukua hatua kwa kuzielekeza Halmashauri zote na taasisi nyingine kulipa fidia stahiki kwa wananchi pale wanapotaka kutwaa maeneo yao.

Mhe. Mabula amesema kuwa taasisi nyingi zimekuwa zikichukua mashamba ya wananchi na kushindwa kuwalipa fidia hivyo kulimbikiza madeni hayo kwa muda mrefu hali inayokwamisha shughuli za maendeleo.

“Halmashauri za Wilaya, Taasisi na Maafisa Ardhi hawaruhusiwi kuchukua mashamba ya wananchi kabla hawajakamilisha utaratibu wa malipo ya fidia kwa wananchi hao, ili kuondokana na malimbikizo ya madeni ya fidia ambayo malipo yake huchukua muda mrefu na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi,” alisema Mhe. Mabula.

Aidha Mhe. Mabula amewataka wananchi wanaodai fidia kuwa wavumilivu wakati Wizara yake inaendelea kufanya upembuzi wa taasisi hizo ili ziweze kulipa fidia zote zinazodaiwa na wananchi.

Vilevile Wizara hiyo imetoa ramani za mitaa kwa wenyeviti wa mitaa wa Jiji la Dar es Salaam ili wenyeviti hao waweze kutambua matumizi ya maeneo yao, kwa mfano maeneo ya wazi, na nini kijengwe katika maeneo yao kama vile nyumba fupi au ndefu, hoteli au chuo ili kuondokana na migogoro ya kubolewa nyumba kwa kujenga eneo lisiloruhusiwa.

“Tumeanza kwa mkoa wa Dar es Salaam lakini zoezi litaendelea kila Mkoa na kila Wilaya Nchi nzima, ili Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji waweze kutambua matumizi ya maeneo yao, hivyo kuchukua hatua kwa haraka pindi ambapo maeneo hayo yanatumika tofauti na matumizi yaliyoko” alifafanua Mhe. Mabula.

Aidha Mhe. Mabula amezitaka Halmashauri kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba, na Maendeleo ya Makazi kuwapa uwezo wenyeviti hao ili waweze kufanya kazi hiyo kiufanisi.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images