Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

WABUNGE WA KAMBI YA UPINZANI WAIBUKA NA MPYA,WAINGIA NA KUTOKA BUNGENI WAKIWA WAMEZIBA MIDOMO YAO KWA PLASTA NA KARATASI

$
0
0

Pichani ni Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia akizungumza jambo mbele ya vyombo vya habari baada ya kutoka nje ya ukumbi wa Bunge Mapema leo asubuhi mjini Dodoma.

Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni leo Wakiongozwa na msemaji wa kambi hiyo Mh.James Mbatia wameingia ndani na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge huku wakiwa wameziba midomo yao kwa karatasi na Plasta Wakidai Naibu Spika anakandamiza demokrasia ndani ya Bunge na kwamba wanaendeleza msimamo wao wa kutokuwa na imani na Naibu Spika Dkt . Tulia Ackson Mwansasu

Hii ni wiki ya pili mfululizo wabunge hao wamekuwa wakitoka bungeni baada ya kutangaza kutohudhuria kikao cha bunge kinachoongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kwa kile wanachodai kutokuwa na imani nane.

Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni wakiwa wameziba midomo yao kwa karatasi na plasta mara baada ya kutoka nje ya ukumbi wa Bunge na kuzungumza na vyombo vya habari mapema leo asubuhi.

Airtel na VETA yapeleka VSOMO DODOMA.

$
0
0

 Meneja huduma kwa Jamii wa Airtel Hawa Bayumi, akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi  Veta Dodoma wakati wa uzinduzi wa programu ya Vsomo inayotolewa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel ambapo wanafunzi wa Chuo cha Veta watapata fursa ya kusoma  kupitia simu ya mkononi kulia ni Meneja mauzo wa Airtel Dodoma Stephen Akyoo na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,Dk Jasmini Tiisekwa.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Dk Jasmini Tiisekwa    akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi  Veta Dodoma wakati wa uzinduzi wa programu ya Vsomo inayotolewa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel ambapo wanafunzi wa Chuo cha Veta watapata fursa ya kusoma  kupitia simu ya mkononi. 
Wanafunzi wa Chuo cha Veta Dodoma wakimsikiliza Meneja huduma za Airtel Tanzania,Hawa Bayuni(hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mpango wa Vsomo ambapo wanafunzi wa Veta watapata fersa ya kusoma kwa kupitia simu ya mkononi.

• Ni mafunzo ya stadi za ufundi kwa njia ya simu za mkononi.
Dodoma 19 Juni 2016, VETA wakishirikiana na Airtel kupitia AIRTEL FURSA inaendelea kufanya mafunzo ya stadi za ufundi kuwa katika njia rahisi na nafuu kwa watanzania. Katika  kuhakikisha kwamba vijana wa kitanzania wanafikiwa popote pale walipo, VETA na Airtel wamewasili katika mkoa wa Dodoma na kutoa fursa ya mafuzo ya stadi za ufundi katika mkoa huo.

kozi zinazotolewa ni pamoja na ufundi pikipiki, ufundi umeme wa majumbani, ufundi wa simu za mkononi , ufundi Alluminium, utaalamu wa masuala ya urembo na ufudi wa kuchomea vyuma. Kozi zinazotolewa katika awamu hii ya kwanza na VETA kupitia kadi ya simu ya Airtel zinatolewa kwa bei ya chini kabisa ya Sh.120,000/=. Muda wa kujisomea kozi ya vitendo katika chuo cha VETA  baada ya kufaulu kozi ya nadharia ni jumla ya masaa 60 . Hii ikimaanisha kuwa mtu atakayeweka msimamo na kusoma kwa bidii ataweza kumaliza ndani ya mwezi mmoja na kuweza kupata cheti chake.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Dk Jasmini Tiisekwa alitoa maoni yake juu ya mafunzo yanayotolewa na VETA kupitia Airtel, alisema, "Nafurahi kwamba VSOMO imekuwa si tu kwa kuwa bei nafuu lakini pia urahisi wanaoupata vijana kwani wanaweza kuendelea na shughuli zao za kila siku kama wameajiriwa na kuboresha ujuzi wao kupitia mtandao pale wanapopata nafasi. Naona wasichana wengi sasa wataweza kupata ujuzi wa kupika kwa kupitia simu  zao za mkononi.

Akitoa maoni yake juu VSOMO, Mkuu wa chuo cha Veta Kipawa Dar Es Salaam, Eng. Lucius Luteganya alisema, "Tunaamini mpango wa VSOMO utabadilisha mtazamo wa vijana wetu na kutumia zaidi teknolojia na kusoma kupitia mitandao.

Amewahimiza vijana wa Dodoma na mikoa ya karibu kutumia VSOMO kama fursa ya kuongeza ujuzi ambao unahitajika katika soko hili gumu la ajira. “Tunafuraha kubwa sana na mpango huu ambao Veta wameweza kuuungana na Airtel kwa kuweza kubadilisha maisha ya vijana wa kitanzania".

Hii ni wiki ya pili toka kuanzishwa kwa VSOMO ambapo vijana wa Dodoma walishiriki katika warsha ya kujiunga na VSOMO mwishoni mwa wiki hii, ambapo vijana wengi walijitokeza na kujiunga na masomo haya ya VSOMO. VSOMO  ni mafunzo ya stadi ya ufundi kwa njia ya mtandao kwa wateja wa Airtel wenye simu za aina ya android, ambapo mteja  anatakiwa kupakua VSOMO kwenye orodha ya menu yake ya simu sehemu ya google play store na kulipa  gharama ya sh 120,000 / = tu.

Taasisi ya Uongozi na Chuo cha Utawala China zatia saini hati ya makubaliano.

$
0
0
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja (aliyeketi kulia) na Makamu wa Rais wa Chuo cha Utawala China Bw. Chen Li (aliyeketi kushoto) wakisaini hati za makubaliano ya ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili mapema leo jijini Dar es Salaam. Katika makubaliano hayo, Chuo cha Utawala China kitatoa fursa kwa watumishi wa umma nchini Tanzania kwenda kupokea mafunzo ya kiutawala nchini China, pamoja maandalizi ya makongamano tofauti tofauti na utoaji wa mihadhara kuhusu utawala, maendeleo ya majiji na ‘Kufahamu zaidi China’ yatakayofanyika hapa nchini na China. 
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja (kulia) na Makamu wa Rais wa Chuo cha Utawala China Bw. Chen Li (kushoto) wakibadilishana hati za makubaliano ya ushirikiano baada ya kusaini hati hizo mapema leo jijini Dar es Salaam zenye malengo ya kutoa mafunzo ya kiutawala kwa watumishi wa umma nchini.
 Ujumbe kutoka Chuo cha Utawala China na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Uongozi wakiendelea na mazungumzo wakati wa tafrija fupi ya utiaji saini ya hati za makubaliano kati ya Taasisi hizo mbili zenye malengo ya kuongeza ufanisi serikalini kupitia mafunzo kwa watumishi wa umma.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa akizungumza wakati wa tafrija fupi ya kusaini hati za makubaliano kati ya Taasisi ya Uongozi na Chuo cha Utawala China. 
 Makamu wa Rais wa Chuo cha Utawala China Bw. Chen Li akizungumza wakati wa tafrija fupi ya kusaini hati za makubaliano kati ya taasisi yake ya Chuo cha Utawala China na Taasisi ya Uongozi.

MKURUGENZI WA MANISPAA YA ILEMELA MKOANI MWANZA AKABIDHI MADAWATI KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGI.

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, John Wanga, akizungumza wakati wa kukabidhi madawati katika Manispaa hiyo.


Na BMG

Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, imekabidhi madawati 2,600 kwa shule zote 74 za Msingi za umma zilizopo kwenye manispaa hiyo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dkt.John Pombe Magufuli la kutaka kila wilaya kumaliza tatizo la madawati ifikapo Juni 30 mwaka huu.

Madawati hayo ambayo yametengenezwa kwenye karakana ya shule ya sekondari ya wavulana ya Bwiru, ni sehemu ya mpango wa kutengeneza madawati 9,080 na hivyo kumaliza kabisa tatizo la uhaba wa madawati katika manispaa hiyo.

Akikabidhi madawati hayo hii leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilemela, John Wanga, amesema madawati hayo yametengenezwa kutokana na fedha zitokanazo na makusanyo ya ndani pamoja na michango ya wadau wengine ambapo katika mgawo wa awali, kata zote 19 za manispaa hiyo zimepewa madawati 139 kila moja.

Wanga amesema kila dawati moja lenye uwezo wa kukaliwa na wanafunzi watatu, limegharimu shilingi 98,000 ambapo manispaa ilinunua vifaa ikiwemo mbao, misumari na vyuma na kulipa gharama za ufundi zinazofikia shilingi 15,000 kwa kila dawati na kwamba madawati mengine yaliyobakia kukidhi mahitaji yanaendelea kutengenezwa kwenye karakana hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Manju Msambya, amepiga marufuku matumizi ya madawati hayo kwenye shughuli nyingine ikiwemo mikutano ya kisiasa huku akiwataka wazazi,walezi na jamii nzima kwa ujumla kutambua umuhimu wa kuchangia juhudi za kuboresha elimu.

Renatus Mulunga ambae ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela amesema halmashauri hiyo inafanya kila jitihada kuhakikisha kwamba inatatua tatizo la upungufu wa madawati kwa shule za msingi katika manispaa hiyo, hatua ambayo itasaidia kuboresha ari ya wanafunzi kujisomea.
Utengenezaji wa Madawati ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, ukiendelea katika karakana ya Shule ya Sekondari ya wavulana Bwiru.

Picha Zaidi Bonyeza Hapa

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA KITUO CHA UHAMIAJI HOLILI

$
0
0

Ujumbe ulioongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(), ukishuka kutoka mlimani baada ya ukaguzi wa mpaka uliopo Mlima Nyoka, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yupo mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) .IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati), akikagua mzigo wa John Evarist ambaye ni mfanyabiashara aliyekua akipita kutoka nchini Kenya kupitia mpaka uliopo katika kijiji cha Kamkunji, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yuko mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
Mfanyabiashara John Evarist aliyekua akipita kutoka nchini Kenya kupitia mpaka uliopo katika kijiji cha Kamkunji, mkoani Kilimanjaro, akijibu maswali aliyoulizwa na Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Holili, ACI Kagimbo Hosea(wa kwanza kushoto).Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira aliyepo mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Holili, ACI Kagimbo Hosea ( aliyenyoosha mkono), akimuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto), mwisho wa mpaka unaotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya wakati wa ziara ya Katibu Mkuu kukagua njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.Wa pili kushoto ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, RPC Wilbrod Mutafungwa
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia), akipanda Mlima kwenda kukagua jiwe linalotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya katika Mpaka uliopo eneo la Mlima Nyoka, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yupo mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

WABUNGE WAJADILI MAREKEBISHO YA SHERIA MPYA YA UNUNUZI WA UMMA, DODOMA

$
0
0
lik2 
Kamishna wa Sera ya Ununuzi wa Umma, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, DKT. Fredrick Mwakibinga, akiwasilisha mada kwa waheshimiwa wabunge, kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410, iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa, Mjini Dodoma, jana.(Picha zote na WFM)
lik3 
Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Kushoto) na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe, wakifuatilia kwa makini mada kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410, iliyotolewa kwa waheshimiwa wabunge katika ukumbi wa Pius Msekwa, jana Bungeni Mjini Dodoma
lik4 
Baadhi wa Waheshimiwa wabunge wakifuatilia kwa makini mada iliyowasilishwa kwao kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410, iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni Mjini Dodoma Jana.
lik5 
Baadhi wa Waheshimiwa wabunge wakifuatilia kwa makini mada iliyowasilishwa kwao kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410, iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni Mjini Dodoma Jana.
lik6 
Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyaji (Prof. Maji Marefu) akichangia jambo wakati wa mjadala  kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410, wakati wa semina iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni Mjini Dodoma Jana
lik7 
Mbunge wa Nkasi, Ali Kessy, akichangia jambo wakati wa mjadala  kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410, wakati wa semina iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni, Mjini Dodoma, Jana.
lik8Mwenyekiti wa Semina ya Wabunge kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma,Sura 410, Mhe. Hawa Ghasia akiongoza mjadala kuhusu Marekebisho ya Sheria hiyo, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni, mjini Dodoma, jana.
lik9 
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchg. Peter Msigwa, akichangia jambo wakati wa mjadala  kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410, wakati wa semina iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni, Mjini Dodoma, Jana.
lik10 
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe, akifafanua jambo wakati wa semina ya waheshimiwa wabunge kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410, iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni mjini Dodoma jana. Kusoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji na Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Semina hiyo, Mhe. Hawa Ghasia.
lik11 
Kamishna wa Sera ya Ununuzi wa Umma, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Fredrick Mwakibinga, akiwasilisha mada kwa waheshimiwa wabunge, kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410, iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa, Mjini Dodoma, jana.

Tanzania yatajwa katika nchi zinazoongoza kwa unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino

$
0
0

Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Shirika la Kimataifa la Under The Same Sun, Vicky Ntetema na kulia ni Mkuu wa Mawasiliano wa Shirika la Standing Voice, Sam Clarke.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez akielezea jinsi UN waevyojipanga kuwasaidia watu wenye ualbino. Kushoto ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga. Kushoto ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero na kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez.

Tanzania yatajwa katika nchi zinazoongoza kwa unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino Pamoja na juhudi ambazo serikali imekuwa ikizifanya ili kuhakikisha Watanzania wenye ualbino wanakuwa salama na amani lakini bado Tanzania inaendelea kuwa nchi ya hatari kwa watu hao kwa kuwa katika orodha ya nchi ambazo zina kiwango kikubwa cha unyanyasaji.

Akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha kongamano la kikanda kwa ajili ya hatua kuhusu ulemavu wa ngozi Afrika lililofanyika Dar es Salaam, Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero alisema kuwa kwa ripoti ambazo wamekuwa wakizipokea inaonyesha Tanzania ni moja ya nchi ambazo zina unyanyasaji kwa watu wenye ualbino.

"Tangu nimeingia sijawahi kufanya uchunguzi hata katika matokeo ya uchunguzi wa nchi 29 sijaujua sana lakini kwa taarifa ambazo nimekuwa nikipata kutoka kwa taasisi mbalimbali inaonyesha Tanzania ni unyanyasaji wa hali ya juu kwa watu walio na uablino," alisema Ero.

Nae Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanguga alisema katika kongamano hilo wametoka na maazimio ambayo wanaiomba serikali iweze kuyafanya ili kuwezesha watu wenye ualbino kuwa na usalama wa uhakika.

"Tumejadili mambo mengi lakini tunaiomba serikali ihusike moja kwa moja kupinga unyanyasaji, ukatili na ubaguzi nia tunaiona kwahiyo tunaomba waendelee kuwa hivyo na pia waongeze bajeti na zaidi katika matibabu kwa watu wenye ualbino," alisema Nyanduga..

Kwa upande wa Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia Mratibu Mkazi wa mashirika hayo, Alvaro Rodriguez alisema ni wataendelea kuwasaidia watu wenye ualbino ili kuwezesha kupunguza changamoto ambazo zinawakabili.

LEO OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU IMEZINDUA MATOKEO MUHIMU YA UTAFITI WA AFYA YA UZAZI NA MTOTO NA MALARIA TANZANIA WA MWAKA 2015/16.


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA MAKAMPUNI YA POLYTRA INTERNATIONAL NA IMPALA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bw. Jaskaran Chugh ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya Polytra International yenye Makao yake nchini Ubelgiji (katikati) na Bw. Mark Lemki wa Kampuni ya Impala ya Switzerland, Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma Juni 20, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TUSKER FANYA KWELI UWINI YATOA MILLION 20 KWA WASHINDI 20 WIKI HII

$
0
0
Droo hii ya aina yake yawafanya watanzania 20 kuwa milionea leo! Wateja wa tusker hadi leo wamepokea kiasi cha shilingi za kitanzania Milioni 50 kwenye promosheni inayoendeswa na kampuni ya serengeti kupitia bia ya Tusker iitwayo TUSKER FANYA KWELI NA UWINI. 

Tayari washindi 30 walikwishapatikana na wote wamepata zawadi zao za pesa taslimu. Droo ya leo ambayo ilikuwa ya kusisimua ilikuwa tofauti na droo zingine kwani leo washindi ishirini walitangazwa na sio kumi kama ilivyozoeleka.Promosheni hii imeweza kupata washindi kutoka mikoa mbalimbali na washindi wote wamekubali kwamba maisha yao yamebadilika kwa njia moja au nyingine. 

Wiki iliyopita alipatikana mshindi Bw Albert Tarimo ambaye alionyesha kwa furaha ujenzi wake na kusema kwamba atatumia pesa aliyopata kuweza kuongeza matofali, dhahiri kuwa promosheni hiii imemfanya bw. Albert afanye kweli katika harakati zake za ujenzi. 

Kuna ambao wamekiri kutumia pesa hizi kwa kulipa ada na wengine kuongezea mtaji kwenye biashara zao. Droo za Tusker fanya kweli uwini zinafanyika kila ijumaa katika studio za ITV na kushuhudiwa na afisa wa bodi ya bahati nasibu ya taifa na wadau wengine, huku kipindi hiki kikirushwa itv siku hiyo hiyo ya ijumaa jioni. 

Baadhi ya washindi wa droo hii ya nne ni Grace Richard kutoka Dar Es salaam, Kitula kutoka Kahama shinyanga, Martina Japhet kutoka Tabora, J J Malunga kutoka Shinyanga, kutoka mwanza Mr Isaya Stanley Furaha Mushumbuzi kutoka Morogroro, Ibrahim Faiko kutoka Iringa, Victor Mwingo kutoka Pwani . Washindi wote ishirini walipatikana kwenye simu na walionyesha furaha isiyo na kifani. Walipewa maelekezo jinsi ya kupata hela yao na ili kukamilisha ushindi wao. Washindi wote hukabidhiwa pesa yao katika hafla fupi kila ijumaa huku wakiendelea kuburudika na tusker na burudani kemkem.

Bado kuna zaidi ya million hamsini za kushindaniwa kwa wateja wa tusker. Tangu uzinduzi wa kampeni hii wapenzi wa tusker pamoja na kujishindia pesa taslimu pia wameweza kujipatia zawadi nyingi zikiwemo bia za bure za tusker, tshirt na kofia pamoja na kupata burudani maalum. 

Akiongea kwa furaha, meneja wa Masoko Nandi Mwiyombela amesema kwamba kwa sasa promosheni inaendelea vizuri sana na wameweza kufikia malengo. “Pesa taslimu ina nguvu. Kwa kiingereza wanasema ‘Cash is a strong tool’ na kulingana na yale tunayosikia kutoka kwa washindi wetu tumegundua ya kwamba kwa kweli kuwa na zawadi ya fedha taslimu ilikuwa uamuzi mzuri na kwa uhakika wameelezea kuweka au kutumia pesa zao vizuri. Jambo lililotusukuma mpaka kuamua kupata washindi ishirini na sio kumi kwa leo ni kutokana na hamasa tunayopata kutoka kwa washindi wetu. Washindi wanatokea mikoa mbalimbali, hilo ndilo lengo letu kubwa, kupata washiriki na washindi nchi nzima.”, alisema Bi. Nandi.

“Tusker Fanya Kweli Uwini’ inaendelea, pamoja na washindi ishirini tuliowapata leo mpaka kufikia washindi 50. Tumeshatoa pesa taslimu shilingi milioni 50 na sasa imebaki milioni 50. Pia kama, mnanavyojua promosheni hii pia inawazawadia wahudumu wanaohudumia wateja wetu, hadi kufikia leo tumeweza kuwapatia shilingi milioni 22.” kamalizia Bi. Nandi. 

Mteja wa tusker anaruhusiwa kushiriki mara nyingi awezavyo, amepatikana mteja aliyeibuka mshindi kwa mara ya pili katika hii promosheni ambayo haiendeshwi kwa njia ya kompyuta bali kwa kuchanganya kuponi zilizojazwa na watumiaji wa tusker na kuweza kupata majibu sahihi papo hapo. 
Mkaguzi kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Madam Chiku (katikati) akihakiki taarifa za washindi 20 wa droo ya nne,kulia kwake ni Joseph Silumbe - Visibility Manager na kushoto kwake ni Meneja wa bia ya Tusker Jasper Migambile.
SBL Visibility Manager Joseph Silumbe (kulia) akichezesha droo ya nne huku akishuhudiwa na mkaguzi kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Madam Chiku (katikati) pamoja na meneja wa bia ya Tusker Jasper Migambile (kushoto).
SBL Visibility Manager Joseph Silumbe (kulia) akimpa kuponi ya mshindi mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini madam Chiku (katikati) huku akishuhudiwa na Meneja wa bia ya Tusker Jasper Migambile (kushoto).

SERIKALI YAONYA MATUMIZI MABAYA YA VYANDARUA.

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akionyesha kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 kwa wadau wakati wa uzinduzi huo leo jijini Dar es salaam.

Wadau mbalimbali wa takwimu wakifauatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya hayupo pichani wakati wa kuzindua kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 leo jijini Dar es salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akikata utepe kuzindua kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 leo jijini Dar es salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza na wadau mbalimbali wa takwimu hawapo pichani wakati wa kuzindua kitabu cha Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16 leo jijini Dar es salaam. Picha zote na Ally Daud-maelezo.

Na Ally Daud-Maelezo

SERIKALI imetoa wito kwa wananchi kuacha matumizi mabaya ya vyandarua ili kusaidia jitihada za Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Malaria nchini.Akizungumza leo Jijini Dar es salaam katika Uzinduzi wa Utafiti wa Matokeo ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa Mwaka 2015/16, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya wananchi kutumia vyandarua wanavyopewa na Serikali kwa matumizi yasiyo sahihi kama kuvulia samaki, kuwekea wigo mifugo na kuzungushia wigo bustani.

‘‘Watu wengi wamekuwa wakitumia vyandarua vinavyotolewa na Serikali kwa matumizi yasiyo sahihi badala ya kujikinga na Mbu waenezao malaria. Hii ni kutokana na utafiti huu kuonyesha kuwa asilimia 14 ya watoto wa chini ya miaka 5 ambao walipimwa Malaria kwa kutumia kipimo cha kutoa matokeo kwa haraka yaani Rapid Diagnostic Tests (RDT) walikuwa na Malaria,” amesema Dkt. Ulisubisya.

Aidha amesema kuwa kiwango cha maambukizi ya Malaria bado ni kikubwa ikilinganishwa na kiwango kilichopatikana wakati wa Utafiti wa UKIMWI na Malaria wa Mwaka 2011-12 hivyo ni vyema jamii ikaendelea kupambana na ugonjwa huu kwani bado ni tishio kwa watoto na Wananchi kwa ujumla.Dkt.

Ulisubisya amesema kuzinduliwa kwa Matokeo haya kutasaidia Serikali kuboresha huduma za afya kwa kuyafanyia marekebisho mapungufu yaliyopo katika utoaji wa huduma za malaria nchini.Akizungmzia huduma za afya kwa akinamama wajawazito, Dkt. Ulisubisya amesema utafiti umeonyesha kuwa kiwango cha akina mama wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma ya afya, kutoka asilimia 51 mwaka 2010 kufikia asilimia 60 mwaka 2015 na kuongezeka kwa kiwango cha akina mama wanaosaidiwa na wataalam waliosomea wakati wa kujifungua kutoka asilimia 50 kufikia asilimia 60 mwaka 20015/16.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Kitakwimu, Mr. Irenius Ruyobya amesema kuwa utafiti huu ni wa muhimu sana katika kuboresha huduma za afya hasa katika kupambana na Malaria.

Amesema ili Serikali iweze kuboresha huduma za afya na kupambana na Malaria, takwimu hizi ambazo zimezinduliwa leo zitasaidia Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa afya katika kupanga, kutekeleza na kupima utekelezaji wa miradi mbalimbali ya afya nchini.Mr. Ruyobya amesema utafiti huu ni wa sita kufanyika nchini ambapo kwa mara ya kwanza ulifanyika mwaka 1991 na kufuatiwa na utafiti wa mwaka 1996, 1999, 2004/5 na 2010.

UFAFANUZI KUHUSU KUJITOA KWENYE MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

Mangula azindua Kitabu cha “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua leo jijini Dar es salaam

$
0
0

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula(mwenye shati jeupe) akizindua Kitabu chenye jina la “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) Bi. Deborah Charles, Agusto Matefu, Mwenyekiti wa Kamati ya Mijadala na Kongamano ambaye pia ni Mwandishi wa kitabu hicho Amos Siyantemi na wa mwisho kushoto ni Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw. Daniel Zenda. Kampeni hiyo inalengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula(mwenye shati jeupe) akionyesha Kitabu chenye jina la “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua mara baada ya kukizindua leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) ambaye pia ni Mwandishi wa kitabu hicho Amos Siyantemi na kushoto ni Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw. Daniel Zenda. Kampeni hiyo ina lengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) Amosi Siyantemi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha Majipu ya Nchi yetu “ Tushirikiane kuyatumbua leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula na kushoto Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw. Daniel Zenda. Waandishi wa habari wakifuatilia uzinduzi wa Kitabu cha Majipu ya Nchi Yetu “Tushirikiane kuyatumbua” leo jijini jijini Dar es Salaam. Kitabu hiko kimezinduliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula (hayupo pichani).Uzinduzi wa Kitabu hicho umeenda sambamba na utambulisho wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM). Kampeni hiyo ina lengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.

Picha zote na: Frank Shija, MAELEZO

SERIKALI YAASWA KUPIGA VITA DHIDI YA UKATILI NA UNYANYAPAA DHIDI YA WATU WENYE UALBINO.

$
0
0
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za watu wenye ualbino, Ikpowose Ero, akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana juu ya maazimio yaliyofikiwa katika mkutano wa watu wenye ualbino Afrika uliofanyika nchini hivi karibuni, Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa UN, Alvaro Rodrigers na Mkurugenzi mkazi wa Under the same  Sun.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SERIKALI imeaswa kupiga vita dhidi ya  ukatili, unyanyapaa pamoja na  mauaji Watu Wenye Ualbino ili kuweza  kila mtu kuishi kwa amani katika nchi yake.  

Katika kupiga vita dhidi ukatili na unyanyapaa ya watu wenye Ualbino ni kuweka mkakati wa kuandaa mashitaka kwa ubora zaidi dhidi ya uhalifu wa Ualbino ,kuandaa kanuni za kusimamia waganga wa jadi pamoja na kuimarisha kampeni maalum na endelevu za ufahamu kwa miaka miwili mfululizo ili kupunguza vifo vitavyotokea mara kwa mara.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar  es Salaam uliohusisha  nchi  29  Kanda ya Afrika,Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa, Ikponwosa Ero, amesema mauaji ya watu wenye Ualbino  yanaendelea kutokea Barani Afrika na kufanya jamii hiyo kukosa haki ya kuishi  kutokana mauaji dhidi yao.
  
Amesema  kuna matukio mengi dhidi ya watu wenye ualbino  lakini yamekuwa hayaripotiwi kwa sababu ya usiri katika masuala ya ushirikiana,ushiriki wa familia na ushiriki wa matajiri na watu wenye nguvu ya kifedha.

Naye, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga amesema serikali inatakiwa kuongeza bajeti yake ili watu wenye Ualbino wapate haki sawa katika masuala ya matibabu.

 “Serikali ihakikishe kuwa vifaa vya kuimarisha uwezo wa kuona vinapatikana kwa ajili ya mtu m wenye ualbino  anapokuwa darasani na kutoa vizuia jua nafuu kama tiba muhimu ili kuziua saratani ya ngozi, ambayo inaendelea kuondoa maisha ya watu hao”amesema Nyanduga.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa The Under Sun (TUS), Vick Mtetema amesema kwa pamoja wataendelea kupambana na unyanyapaa na mauaji dhidi ya watu wenye ualbino.

Amesema polisi wa kimataifa na watu wa Uhamiaji washirikiane kwa pamoja ili kulinda watu wanaopitisha watu wenye Ualbino.

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA MADAWATI 50 SHULE YA MSINGI MAKOLE DODOMA

$
0
0

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi,Vijana na Ajira, Antony  Mavunde (kushoto), akipokea msaada wa madawati 50 yenye thamani ya zaidi ya sh milioni 6 kutoka kwa Mkurungenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamisi yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya Shule ya Msingi Makole iliyopo Manispaa ya Dodoma,mwishoni mwa wiki
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde (wa pili kushoto), akifurahi pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Makole iliypo manispaa ya Dododma mara baada ya makabidhiano ya msaada wa madawati 50 uliotolewa na wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, wengine katika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Dk. Jasmin Tsekwa (wa pilikulia) na kulia ni Mkurungenzi Benki ya CRDB tawi la  Dodoma, Rehema Hamisi. 
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma wakiwa wamekaa kwenye madawati ambayo waliikabidhi shule ya msingi makole iliyomjini Dodonma jana ,msaada huo unathamani ya zaidi ya sh milioni 6.
Mkurungenzi Benki ya CRDB tawi la Dodoma Rehema Hamisi (kulia) akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Makole iliyopo mjini Dodoma, baada ya kuwakabidhi msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na wafanyakazi wa wa benki hiyo ili kuunga mkono juhudi za Serikali kupunguza tatizo la madawati mashuleni.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, tawi la Dodoma, Rehema Hamisi akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo kwa ajili ya Shule ya Msingi ya Makole Manispaa ya Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi,Vijana na Ajira, Antony  Mavunde akioa hotuba yake wakati wa hafla ya kupokea madawati 50 yaliyotolewa kama msaada na wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma kwa ajili ya Shule ya Msingi Makole. 
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Makole Dodoma.
Wanafunzi wakitumbuiza kwa kuimba kwaya.

Milioni 200 kupanua mfumo wa maji safi Kasulu

$
0
0
Na: Lilian Lundo – Maelezo – Dodoma


Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji imetenga jumla ya shilingi milioni 200 katika bajeti ya Mwaka 2016/2017 ili kupanua mfumo wa maji safi katika Mji wa Kasulu.

Hayo yamesemwa leo, Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Kasulu Mhe. Daniel Nswanzugwako juu ya ukabarati wa vyanzo vya maji vilivyopo Mjini Kasulu ili maji yafike katika mitaa ya kata za Mrusi, Mwilavya na Kidyama.

“Serikali inatambua changamoto ya mtandao wa maji inayoukabili Mji wa Kasulu, katika mwaka wa fedha 2016/17 imetenga Milioni 200 kwa ajili ya kupanua mfumo wa maji safi katika mji huo,” alisema Mhe. Kamwelwe

Aidha, Mhe. Kamwelwe aliendelea kwa kusema kuwa, fedha hizo zitatumika katika kuboresha hali ya huduma ya maji ikiwemo kuongeza mtandao wa maji Mjini Kasulu ambapo pia kata za Mrusi, Mwilavya na Kidyama zitapata huduma ya maji safi na salama.

Pia Mhe. Naibu Waziri huyo amesema kuwa Serikali imekamilisha usanifu na uandaaji wa makabrasha ya zaburi kwa ajili ya mradi wa majisafi wa kujenga chujio katika Mji wa Kasulu ili kuondokana na tatizo la maji kuwa machafu.

Wizara hiyo pia imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1 katika bajeti ya mwaka 2016/17 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya upanuzi wa miundombinu ya usambazaji maji Masasi – Nachingwea kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Masasi – Nachingwea.

Mradi huo unaohudumia wakazi wapatao 188,250 wa Miji ya Masasi na Nachingwea pamoja na baadhi ya Halmashauri za Wilaya ya Masasi, Nachingwea na Ruangwa. Aidha wizara hiyo itaendelea kutenga fedha zaidi katika bajeti zijazo ili kupanua huduma ya upatikanaji wa maji nchi nzima.

Bilioni 2.5 kuanza kujenga hospitali ya Wilaya ya Morogoro

$
0
0
Na: Lilian Lundo – Maelezo – Dodoma

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetenga jumla ya shilingi Bilioni 2.5 katika bajeti ya mwaka 2016/017 ili kujenga hospitali ya Wilaya ya Morogoro.

Hayo yamesemwa leo,Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Selemani Jaffo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Morogoro Mjini Mhe. Azizi Abood juu ya msongamano mkubwa wodi za akina mama hospitali ya Rufaa Morogoro.

“Msongamano wa wagonjwa katika wodi ya wazazi Hospitali ya Mkoa unatokana na kukosekana kwa hospitali ya Wilaya ya Morogoro.Ili kukabiliana na tatizo hilo, Serikali immepanga kuanza ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Morogoro katika bajeti ya mwaka 2016/17,” alisema Mhe. Jaffo

Mhe. Jaffo aliendelea  kusema kuwa, fedha hizo zilizotengwa zitaanza kwa ujenzi wa jengo la utawala na jengo la wagonjwa wa nje.(OPD).

Aidha, aliendelea kujibu maswali ya yaliyoelekezwa katika wizara hiyo kwa kusema kuwa, Serikali katika bajeti ya mwaka 2016/17 imetenga shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha kuhifadhi maiti (mortuary) Wilaya ya Chunya.

Chumba hicho cha kuhifadhi maiti kinatarajiwa kugharimu shilingi milioni 230 ambapo ujenzi wa jengo utagharimu shilingi milioni 60 na Majokofu yatagharimu shilingi milioni 160.

Kwa sasa Wilaya hiyo ina chumba maalum ambacho kimetengwa kwa ajili ya kuhifadhi mati mbili tu ambacho hakitoshelezi huduma hiyo hali ambayo huwalazimu wahitaji kufuata huduma ya kuhifadhi maiti Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.

Mkutano wa Magavana unaosimamiwa na Taasisi ya Usimamizi wa Fedha na Uchumi kutoka (MEFMI).

$
0
0
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Serikali imesema itaendelea kufanya biashara na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kupitia fursa zilizopo nchini ikiwemo uwekezaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Beno Ndulu alipokuwa akifungua mkutano wa Magavana na Manaibu Gavana kutoka nchi 14 za Mashariki na Kusini mwa Afrika unaosimamiwa na Taasisi ya Usimamizi wa Fedha na Uchumi kutoka (MEFMI).

“Tanzania imeanza miaka 2 hadi 3 kujiwekea akiba ya sarafu ya Yuan ya nchini China kutokana biashara mbalimbali ambapo hadi sasa nchi ina akiba ya asilimia 5 za fedha ya China Yuan” alisema Profesa Ndulu.

Hatua hiyo ya Tanzania inafuatia Sarafu ya China ijulikanayo kama Yuan kuingizwa kuwa miongoni mwa sarafu sita zinazotumika Duniani.

Mkutano huo unafuatia majumu ya Benki Kuu hizo za nchi wanachama kuwa na jukumu la kuwa walinzi wa akiba ya fedha za kigeni na wawezeshaji wa masuala ya biashara za kimataifa.

Maweneo ambayo Tanzania inayatumia kama njia moja wapo ya kujiongezea sarafu ya China ni pamoja na uwekezaji katika hati fungani inafaida zaidi ikilinganishwa na nchi za Ulaya na nchi nyingine duniani.

Profesa Ndulu alizitaja sarafu nyingine ambazo zinatumika duniani zinazotambuliwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ni pamoja na Dola ya Marekani, Euro inayotumiwa na nchi za Ulaya, Swiss Frank ya Uswiss, Paund ya Uingereza, Yen ya Japani pamoja na Yuan ambayo itaanza kutumika kimataifa kuanzia mwezi Septemba 2016.

Mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na China ni ya kihistoria yanayohusisha Serikali za nchi hizo mbili ambao ulijengwa kwa msingi imara wa Waasisi wa mataifa hayo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Muasisi wa Taifa la China Mwenyekiti Mao Tse Tung.

Mkutano wa huo wa MEFMI unatoa fursa ya kipekee kubadilishana mawazo kwa viongozi hao juu ya ushirikishwaji wa Yuan Kichina ndani ya kikapu cha hifadhi ya sarafu ya IMF / Benki ya Dunia katika nchi wanachama wa MEFMI.

Kufanyika kwa mkutano huo ni moja matukio ya kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yanayotarajiwa kutahudhuriwa na Wachumi waliobobea wa ndani na nje ya nchi, wakiwemo magavana 20 kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

WAZIRI MKUU NA MATUKIO BUNGENI LEO.

$
0
0

bue3 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano  na Mazingira   Luhaga  Jaelson  Mpina  kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Juni 20, 2016.
bue4 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano  na Mazingira   Luhaga  Jaelson  Mpina  kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Juni 20, 2016.
bue1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, bungeni mjini Dodoma Juni 20, 2016.
bue2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Bernadeta Mushashu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 20, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Wananchi wa Chasimba kuweni wavumilivu mtakula mbivu

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho-MAELEZO

Baada ya mtafaruku mkubwa kutokea katika Kijiji cha Chasimba kilichopo katika Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam na kuwaacha wakazi wa eneo hilo katika hali ya sintofahamu juu ya maisha yao ya siku zijazo, wakazi wa eneo hilo wamepata ahueni baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Willium Lukuvi kuingilia kati na kutoa suluhu ya mtafaruku huo.

Mgogoro huu baina ya wananchi wa Kijiji cha Chasimba na mwekezaji wa Kiwanda cha Saruji cha Twiga, Bw. Alfonso Rodriguez kilichopo Wazo Hill ambao ulianza takribani miaka 15 iliyopita baada ya Mkurugenzi huyo kugundua kuwa wananchi wamevamia eneo lake na kujenga makazi yao.

Hayo yalitokea baada ya kiwanda hicho kushindwa kuilinda mipaka yake kwa muda mrefu na kusababisha wananchi kujenga maeneo hayo na kukaa kwa muda mrefu sana hali iliyowapelekea kujiona kama wana haki na eneo hilo na kukataa kuhama.

Mkurugenzi Msaidizi Usanifu wa Miji na Uendelezaji Upya Maeneo wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Immaculata Senje alisema kuwa eneo hilo ni mali ya mwekezaji wa Kiwanda hicho."Ni ukweli usiofichika kuwa eneo hili la Chasimba ni mali ya mwekezaji na ana hati ya mwaka 1957 aliyopewa na Wizara yetu inayoonyesha ukubwa na mipaka ya eneo lake kwahiyo wananchi ndio wavamizi wa eneo hilo".anakiri Bi. Senje.

Mgogoro huo ulileta tafrani kubwa baada ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kutoa agizo kuwa wananchi waliojenga katika eneo hilo wahame mara moja na kwenda eneo ambalo wamepangiwa na Wizara ambapo takribani wakazi 30 waligoma kuondoka katika eneo hilo na kuamua kwenda mahakamani kudai haki yao, hatua ambayo haiukupata suluhu ya mgogoro.

Ili kuwasaidia wakazi wa Chasimba, Waziri Lukuvi aliamua kuingilia kati kwa kufanya mazungumzo ya amani na muwekezaji wa kiwanda hicho ambapo alimuomba Mkurugenzi huyo kuwaachia wakazi wa Chasimba sehemu hiyo kwa makubaliano maalumu watakayoafikiana.

Hatimaye mazungumzo baina ya wawili hao yalileta picha mpya kwa wakazi wa Chasimba baada ya Muwekezaji kukubali kuachia sehemu ya eneo lake kwa ajili ya makazi ya wananchi hao.

Mnamo Mei 13 mwaka 2015 ulifanyika Mkutano wa hadhara wa kutangaza kurudisha eneo hilo kwa wananchi, mkutano huo uliokutanisha uongozi wa wizara, uongozi wa kiwanda cha saruji, uongozi wa Manispaa ya Kinondoni, Shirika la Umeme Tanzania, Idara ya Maji, Polisi, Mbunge wa Kawe Halima Mdee ambao walipewa maagizo mbele ya wakazi wa Chasimba ya kupanga eneo hilo kuwa la makazi.

"Sasa natamka rasmi kuwa ardhi hii imerudishwa kwa wananchi na imeshabadilishwa kutoka kuwa ardhi ya biashara na kuwa ardhi ya makazi kwahiyo nimeongozana na wahusika ambao watalipanga eneo hili kwa kuzingatia dhana ya mpango shirikishi ambapo kamati ya wananchi itashirikiana na wataalamu wa wizara yetu katika upangaji wa eneo hilo ili kuwezesha uwekaji wa huduma za jamii",alisema Lukuvi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Bw. Rodriguez anakiri kuwa mgogoro huo ulikuwa ni wa mda mrefu na umekuwa ukiwanyima usingizi kwahiyo, alimpongeza Waziri Lukuvi kwa kumaliza mgogoro huo na kuwaahidi wakazi hao kushiriki katika ujenzi wa miundombinu.

Hatimaye eneo la Chasimba sasa limekuwa rasmi la wakazi wa Chasimba, eneo hilo lina takribani Kaya 4,096, wastani wa watu watano kila kaya na jumla ya takribani watu 20,480.Akizungumzia hatua hiyo, Mkazi mmoja wa Chasimba Juma Athumani alieleza kufurahi baada ya mgogoro huo kuisha.

"Nimeishi hapa kwa miaka 30, sasa nina watoto 11 na wajukuu kadhaa katia eneo hili, hapo awali mwekezaji aliposema tutoke kuwa eneo hili ni lake nilikua sielewi kabisa lakini nimefurahi sana kwa hatua hii iliyofikiwa". Alisema Athumani.

Tangu kuisha kwa mgogoro huu Mwezi Mei mwaka 2015, wizara inajitahidi kuendana na kasi ya "hapa kazi tu" iliyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuanza kupima viwanja kwa ajili ya wananchi hao ambapo hadi kufikia Mei 31 mwaka 2016 jumla ya viwanja 491 vimeshapimwa kati ya viwanja 2180 vinavyotarajiwa kupimwa katika eneo hilo.

Wizara ina malengo ya kumaliza kupima viwanja hivyo ifikapo mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu na baada ya hapo wananchi hao wataletewa huduma za kijamii zikiwemo za Afya, shule,sehemu za kuabudu,viwanja vya michezo,miundombinu ya umeme, maji pamoja na barabara.

Wizara inawataka wananchi kuwa wavumilivu na kuacha kulalamika kwa kuwa wizara inaendelea na kazi katika eneo hilo na kila kitu kinaenda kwa wakati kwamba baada ya upimaji wa maeneo kuisha ndipo huduma za kijamii zitafuata.

Mkurugenzi Immaculata alisema "wakazi wa Chasimba mnatakiwa kuelewa kuwa kila kitu kinatakiwa kufanywa kwa kufuata sheria kwahiyo lazima twende taratibu ili kuepuka migogoro mingine kutokea, tunawasihi wakazi wa kijiji hicho kusubiri upimaji uishe ndipo huduma za kijamii zifuate".

Kila Mtanzania anahitaji kuishi kwa amani na utulivu katika sehemu aliyoichagua na kuiridhia lakini kutokana na nchi kuongozwa na sheria katika kila jambo basi hakuna budi kufuata sheria za ardhi zilizowekwa ili kuepuka usumbufu pamoja na migogoro inayopelekea kuwa na ugomvi na mauaji yanayosababisha amani kutoweka na kurudi nyuma kwa maendeleo ya mtu mmoja au Taifa zima.

Wahenga wanasema,"heshimu wenzio ili nawe uheshimiwe", shukrani kwa wakazi wa Chasimba kuwa wavumilivu wakati Serikali inakamilisha taratibu za kuendeleza eneo hilo kwa kupima viwanja halali na baadae kuwekewa miundombinu ya kijamii .

Lakini pia ni vyema wakazi hao wakafuata sheria ili kuhakikisha kwamba hakuna mtu au mamlaka yoyote itakayowasumbua kwenye eneo lao ambalo watakuwa wakilimiki kihalali.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images