Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

Serikali kuaandaa mashindano ya upandaji miti na ufufuaji wa visiki hai.

$
0
0
Na Daudi Manongi-Dodoma
Waziri wa nchi na Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba amesema kuwa wameandaa mashindano ya upandaji wa miti na ufufuaji visiki hai katika ngazi zote nchini ili kufanikisha mapinduzi ya kijani na kutoa kiasi cha pesa cha shilingi milioni 100 kwa halmshauri itakayofanya vizuri.

Waziri makamba ameyasema hayo alipokuwa akifunga warsha ya siku moja kwa wabunge kuhusu kukabiliana na tishio la jangwa na kuboresha ardhi iliyochakaa ili izalishe zaidi katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Aidha amesema kuwa atashirikiana na Tamisemi na Wizara ya elimu kuhakikisha elimu ya upandaji miti na ufufuaji wa visiki hai inatolewa kuanzia ngazi ya elimu ya Awali ili wanafunzi waanze kupata elimu hii kuanzia katika ngazi ya chini.

Mhe.Mkamba alisema kuwa upandaji wa miti ndio utaleta manufaa makubwa nchini mwetu kwani hakuna sekta isiyotegemea miti toka uumbwaji wa dunia hii kwani Nyanja za Afya,ufugaji,misitu,utalii na maji zote zinategemea uhifadhi wa Mazingira yetu.

Aidha waziri huyo mwenye dhamana ya mazingira alisema kuwa kama jamii yetu haitahifadhi mazingira basi hakuna sekta itakayofaidika na kuongeza kwamba atasimama kidete kutengeneza mikakati ya maendeleo juu ya mazingira.Pia amehaidi Serikali kutenga fedha za kutosha,kutengeneza Sera nzuri,sheria na miongozo yenye tija katika mipango ya maendeleo.

Katika upande mwingine amesema kuwa kwa sasa utaratibu wa kufufua visiki hai ni jambo ambalo litawekwa katika mpango wa maendeleo ya Taifa na kuzitaka wizara zinazohusiana na mazingira kushirikisha watu wote ikiwemo kuwapa elimu kuhusu ufufuaji wa visiki hai.

Aidha Waziri Makamba amesema kuwa serikali ina mkakati mkubwa wa uboreshaji wa Sera za Mazingira uku mkakati wa kupanda na kutunza miti wa mwaka 2016-2021 ukiwa bado katika mipango mahususi ya kuifanya Tanzania kuwa ya Kijani.
Warsha hiyo kwa wabunge imeeandaliwa na shirika la Lead foundation uku ikishirikisha ofisi ya Bunge na wadau kutoka World Vision, Ever Green na World Agroforestry Center ambao walitoa mada mbalimbali kwa wabunge ikiwemo jinsi ya kuhifadhi Uoto wa Asili,Kilimo cha kijani,namna ambavyo ufufuaji wa Visika hai na Ngitili zinavyoweza kuchangia Mpango wa kitaifa wa Upandaji Miti na kuimarisha mshikamano kitaifa wa ustawishaji Miti.

Airtel yafuturu na Bloggers

$
0
0

Mkurugenzi wa rasilimali watu wa Airtel, bwana Patrick Foya akiitambulisha kwa blogger VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania ,kupakua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia simu yake ya Airtel. 
Mmimiliki wa 80/20 blog Shamimu akiuliza swali mara baada ya kupata ufafanuzi juu ya mpango wa VSOMO ushirikiano kati Airtel na VETA kwenye mkutano ulifatiwa na Futari.
Baadhi ya Bloggers wakijaribu kupakua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia simu zao na ipad zao.
Baadhi ya wafanyakazi wa Airtel wakiwa kwenye Futari baada ya mkutano wa VSOMO.

Mzee John kitime (katikati) wakijadili jambo pamoja na shamimu mmiliki wa blog ya 80/20 na Josephat Lukaza mmlimiki wa lukaza blog, wakati wa mkutano wa kuitambulisha VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania ,kupakua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia simu yake ya Airtel


Baadhi ya bloggers wakipata futari

Airtel yafuturu na Bloggers 

Katika mpango wake wa kukutana na kuendelea na mfungo wa mwezi Ramadhani leo Airtel kupitia Airtel FURSA imekutana bloggers na kuzungumzia mambo mbalimbali ikiwemo VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania ,kupakua masomo ya ufundi stadi na kupata cheti kupitia simu yake ya Airtel. 

Akielezea VSOMO Mkurugenzi wa rasilimali watu bwana Patrick Foya alisema, ana anamatumaini kuwa VSOMO masomo ya Ufundi yanayotolewa na VETA kupitia simu za mkononi za Airtel, yatakua suluhisho kwa vijana wengi wenye ujuzi na ari ya kujifunza kufanya shughuli kwa uhakika kwani watakua wamejifunza mbinu zitakazowawezesha kuto bahatisha na kuongeza ufanisi katika kazi zao. 

Nao bloggers walio hudhuria walikua na haya ya kusema, mfumo huu utaleta tija sana kwa vijana wengi ambao wako katika shughuli mbalimbali kupata muda wa kujifunza na kupata taaluma zitakazowawezesha kujiajiri, tunawapongeza Airtel kwa kuanzia mfumo huu wa masomo kupitia simu. 

Aidha waliongeza kwa kusema wao watakuwa mstari wa mbele kushirikiana na Airtel kwa kuwafikia makundi mbalimbali ya vijana katika maeneo yao ya kazi ili kuhakikisha wanaitumia vyema fursa hii katika kujiendeleza kitaaluma.

WASANII PAYUS NA MECRAS WAWASHUKURU MASHABIKI ZAO WA KANDA YA ZIWA.

$
0
0

Msanii Payus kutoka Jijini mwanza.

Na George Binagi-GB Pazzo

Wasanii Payus na Mecras kutoka Jijini Mwanza ambao wanaunda kundi la “Payus & Mecras”, wametoa shukurani zao za dhati kwa wapenzi wote wa muziki ambao wanahakikisha kwamba muziki wao unaziki kuchanja mbuga kitaifa na kimataifa.

Wakiongea na BMG, wasanii hao ambao hivi sasa wameweka kambi mkoani Geita kwa ajili ya mapumziko ya mwezi mtukufu, wa Ramadhan, wamewashukuru wapenzi wa muziki wao hususani kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa ambao wameupokea vyema wimbo wao mpya uitwayo “Chausiku”.

“Baada ya kuachia audio na video ya wimbo wa Chausiku, tumepata conection kubwa sana ambapo mashabiki zetu kutoka mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa wamekuwa wakitupigia simu ili tukapige shows huko waliko jambo ambalo tunalifanyia kazi”. Amesema Mecras.

Kupitia BMG, msanii Payus amewahakikishia mashabiki zao kwamba wategemee kazi nyingine nzuri na bora zaidi kuanzia audio hadi video kama ambavyo wamefanya katika wimbo wao wa Chausiku ambao ni wimbo mpya kutoka Mwanza unaopendwa sana hivi sasa.
Msanii Mecras kutoka Jijini Mwanza

Sikiliza Hapa Wimbo wa Wasanii Hao

MAKAMU WA RAIS ASISITIZA KUSHIRIKISHA WANAUME KATIKA AJENDA YA MTOTO WA KIKE

$
0
0



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye Tamasha Fadhili Mtoto Asome pamoja na Binti Clubs iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Binti Foundation ambapo aliahidi kuwasomesha watoto 100 na aliwasihi Wanawake wanapoweka mipango ya kimaendeleo kuwashirikisha pia wanaume.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa pamoja na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa mara baada ya uzinduzi wa Binti Clubs jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watu waliojitokeza kwenye Tamasha Fadhili Mtoto Asome pamoja na Binti Clubs iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Binti Foundation ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akipitia kitabu cha Binti Foundation wakati wa Tamasha Fadhili Mtoto Asome.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akitazama jambo liliokuwa linaendelea (halionekani pichani) pamoja na Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Binti Foundation Johari Sadiq .
Sehemu ya watoto walioshiriki kuonyesha mitindo mbali mbali ya Mavazi pamoja na Wabunifu wao.

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameyataka Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini (NGOs) yanayoshughulikia masuala ya wanawake na watoto kujenga utamaduni wa kushirikisha wanaume katika kampeni za kumwinua mtoto wa kike kwa lengo la kuleta mabadiliko yanayokusudiwa.

Mheshimiwa Samia ametoa kauli hiyo jana kwenye hafla ya uzinduzi wa Binti club iliyofanyika sambamba na harambee ya fadhili mtoto asome ya kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto 500 wa wilaya ya Kinondoni iliyoandaliwa na Shirika lisislo la Kiserikali la Binti Foundation katika ukumbi wa PSPF jijini Dar es salaam

Alisema wanaume kama wakala wa mabadiliko wanapaswa kushirikishwa na wajue ajenda ili wawe mabalozi wazuri katika kuzungumzia umuhimu wa kumwinua mtoto wa kike kielimu, kiafya na kwenye masuala ya ujasiriamali.

"Tuwaingize wanaume kama wakala wa mabadiliko, tuwashirikishe, wajue ajenda zetu katika mapambano hayo. wanaume wanashikilia sehemu nyingi, watumie nafasi hizo tulete mabadiliko," alisema Makamu wa Rais na kuongeza."Penye mkusanyiko wa watu 100, ukiingiza wanaume 20, na wakajua madhumuni ya mkusanyiko wetu, wataenda kushawishi wenzao 20,000 huko nje."

Aliipongeza Taasisi hiyo ya Binti Foundation kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika suala la elimu kwani safari ya mtoto wa kike ya kupata elimu inakuwa na ugumu zaidi kuliko wanaume kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za mila potofu, hali ya uchumi katika familia na jinsi jamii inavyomwangalia kutokana na ujanajike wake.

"Tuna kazi kubwa ya kumtayarisha mtoto wa kike aweze kupambana na changamoto zinazomzunguka," alidokeza.


Mheshimiwa Samia alitumia fursa hiyo kuelezea hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali katika kukabiliana na changamoto za elimu ikiwa ni pamoja na kuondoa ada katika shule za msingi na sekondari, kuboresha ajira za walimu pamoja na maslahi yao, kujenga mabweni kwa wasichana na kuondoa tatizo la madawati ambapo amewashukuru Watanzania kwa kuchangia madawati.Aliwataka wazazi kuwatunza watoto wao kwani ni zawadi kutoka kwa Mungu na kuhakikisha wanapata elimu zote ya dini na ya dunia ili kuwajenga kimaadili waweze kuwa raia wema.

Mtendaji Mkuu wa Binti Foundation Johari Sadik alimweleza Makamu wa Rais kuwa shirika hilo liliamua kuunga mkono jitihada za serikali ili kuwawezesha watoto kumudu masomo yao na hatimaye kufikia malengo yao."Kwa hiyo ukiwa na fedha taslimu, ama vifaa kama vile kalamu, madaftari, pedi, vyote tunapokea kwa ajili ya kusaidia watoto ambao malengo yao yanaweza yasitimie kutokana na changamoto hizo,"

Kampeni hiyo ya fadhili mtoto asome imeanzia kwa watoto 500 wanaoishi kwenye mazingira magumu wa shule za msingi Mwananyamala, Hananasif, Kumbukumbu na Msasani zilizoko katika wilaya ya Kinondoni, mkoa wa Dar es salaam.Katika hafla hiyo iliyopambwa na onesho la mavazi la watoto Makamu wa Rais ambaye alikubali kuwa mlezi wa Binti Foundation aliahidi kusomesha watoto 100 wakati mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa alitoa ahadi pia ya kusomesha watoto 50.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

KUPANDA MABASI YA MWENDO WA HARAKA JIJINI DAR ES SALAAM SASA NI KWA KADI HUDUMA HIYO KUANZA RASMI KESHO

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Udart), David Mgwasa (kushoto),akionesha kipeperushi chenye maelezo ya matumizi ya kadi zitakazotumika katika mabasi hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Udart Jangwani jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Ofisa Habari UDART, Deus Bugaywa.

Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Mkutano na wanahabar ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

MRADI wa Mabasi Yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (UDART) imeanzisha huduma kwa wateja wao za kutumia kadi maalumu wakati wa kupanda mabasi hayo itakayoanza rasmi leo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, David Mgwasa alisema wameanza kutoa huduma hiyo ya kadi ili kuwarahisishia wateja wao na kuondoa changamoto ya kusubiri tiketi kwa muda mrefu kabla ya kuondoka.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu alisema kwamba kwa kuanzia wametoa kadi 200,000 ambapo kila kadi itauzwa kwa shilingi 5000 ingawa bei halisi kwa kadi moja ni shilingi 500 na sh.4500 inayobaki itakuwa ni malipo ya mteja wao.

“Shilingi 4500 zitatumika kama malipo ya nauli kwa siku saba hadi nane kwa kwenda eneo lolote na kuwa kadi hizo zitapatikana katika vituo vya Kimara, Mbezi, Morocco, Gerezani, Posta na kuwa zitakuwa ni endelevu” alisema Rajabu

Aliongeza kuwa katika nchi nyingi zimekuwa zikitumia kadi hizo katika kusafirisha abiria na kuwa kwa hapa nchini ni huduma mpya ambayo itakuwa na changamoto zake kabla ya kuzoeleka.Alisema licha ya kuanzisha huduma ya kadi bado ile ya risiti itaenelea kama kawaida ambapo alisema namna ya kujiunga na hu duma hiyo unatakiwa kupiga *152*22#

IGP Mangu -AKAGUA UJENZI WA KITUO KIPYA CHA KUPOKELEA SIMU ZA DHARURA (CALL CENTRE)

$
0
0
G1 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa kituo kipya cha kupokelea simu za dharura (CallCentre) wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo  ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kitazinduliwa hivi karibuni ikiwa ni hatua mojawapo  ya utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha usalama wa Jamii, unaotekelezwa na Jeshi la Polisi kwakushirikiana na Ofisi ya Rais, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi(PDB) katika mkoa wa Kipolisi Kinondoni ambapo kupitia kituo hicho wananchi wataweza kuripoti matukio na kupokelewa mapema tofauti na ilivyo hivi sasa.
G2 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa kituo kipya cha kupokelea simu za dharura (CallCentre) wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo  ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kitazinduliwa hivi karibuni ikiwa ni hatua mojawapo  ya utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha usalama wa Jamii, unaotekelezwa na Jeshi la Polisi kwakushirikiana na Ofisi ya Rais, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi(PDB) katika mkoa wa Kipolisi Kinondoni ambapo kupitia kituo hicho wananchi wataweza kuripoti matukio na kupokelewa mapema tofauti na ilivyo hivi sasa.
G3 
Askari Polisi wakiwa katika mafunzo maalumu ya kupokea simu katika kituo kipya cha kupokelea simu za dharura (CallCentre) ambacho kitazinduliwa hivi karibuni ikiwa ni hatua mojawapo  ya utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha usalama wa Jamii, unaotekelezwa na Jeshi la Polisi kwakushirikiana na Ofisi ya Rais, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi(PDB) katika mkoa wa Kipolisi Kinondoni  ambapo kupitia kituo hicho wananchi wataweza kuripoti matukio na kupokelewa mapema tofauti na ilivyo hivi sasa.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

THE POOL OF SILOAM CHURCH WAUOMBEA AMANI MKOA WA DAR ES SAALM NA TANZANIA KWA JUMLA, LEO

$
0
0

Wakili wa Mungu wa Kanisa la The Pool of Siloam, Elisha Eliya akiendesha sala maalum ya kuuombea amani mkoa wa Dar es Salaam na Tanzania kwa jumla wakati wa Ibada iliyofanyika leo, katika Kanisa hilo, Mbezi Makonde, jijini Dar es Salaam.

Wakili wa Mungu wa Kanisa la The Pool of Siloam Church, Elisha Eliya akiendesha sala maalum ya kuuombea amani mkoa wa Dar es Salaam na Tanzania kwa jumla wakati wa Ibada iliyofanyika leo, katika Kanisa hilo, Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Bashir Nkoromo

PICHA KEM KEM ZA TUKIO HILO> BOFYA HAPA

WAZIRI NAPE AONGOZA MAMIA KATIKA SIKU YA KIMATAIFA YA YOGA, JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye. akiwa katika mkao wa kusafisha kichwa unaojulikana kwa lugha ya Yoga "KAPALABHATI". Faida za mkao huu ni pamoja na kusafisha njia za kupumulia na kuponya kukohoa, kutibu mafua, pumu na maambukizi kwa njianya kupumua. Hali kadhalika unaufanya mwili kuchangamka na kuipa sura nuru na ujana na pia kustawisha mfumo wa neva na kuboresha mfumo wa kusaga chakula. Wazi Nape, ambaye alifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, aliongoza mamia ya wakazi wa jiji katika kuadhimisha Siku ya YogaDuniani kwenye ufukwe wa Coco Juni 19, 2016. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Mkao wa kusafisha kichwa (Kapalabhati)

Mkao wa kufikiri kwa uzingativu au kama ujulinavyo "Dhyana"
Mkao unaosaidia mwili kuwa imara au kama unavyojulikana "Tadasana". Kutoka kushoto ni Wazir Nape, Balozi wa India nchini Tanzania, Sandeep Arya na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul makonda.
Umbo lapembe tatu au Trikonasana
Mkao wa radi, ujulikanao kwa lugha ya Yoga, Vajrasana, hii inachukuliwa kama mkao wa Tahajudi, wakati mtu anafanya mazoezi kwa ajili ya tahajudi, anatakiwa kufumba macho mwisho wa mazoezi
Yoga ikiendelea, kutoka kulia kwenda kushoto, ni aliyekuwa Balozi wa TanzanianchiniUingereza, Peter Kalaghe, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Balozi wa India nchiniTanzania Sandeep Arya, na Balozi Mbelwa Kairuki

Mkao wa Kapalabhati, mkao wa kusafisha kichwa
Kupoza mwili kwa kudhibiti pumzi, kwa lugha ya Yoga "Sitali Pranayama"

Mkao wa mwili mfu kwa lugha ya Yoga, Savasana, mkao huu unasaidia kupunguza kila aina ya misukosuko na kutuliza mwili na akili.
Mkao wa Nzige, au kwa lugha ya Yoga "Salabhasana" mkao huu unasaidia kwenye matatizo ya viungo na maumivu ya chini ya mgongo, hulainisha misuli ya mapaja, na hips na kwenye maeneo ya figo. Pia hupunguza mafuta kwenye mapaja na makalio, ni mazoezi mazuri katika kupunguza uzito ikiwa ni pamoja na kusaidia viungo vya tumbo kusaga chakula

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki M, Allan Msalilwa (Mbele), akiwa miongoni mwa wananchi waliojitokeza kwenye mazoeziya Yoga Coco Beach. Benki M ndio mfadhili mkuu wa mazoezi hayo


Waziri Nape katika mkao wa "Tadasana", unaosaidia mwili kuwa imara au
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika mkao wa "Tadasana", unaosaidia mwili kuwa imara au
Mkao wa Mti, au kwa jina la Yoga "Vrikshasana" mkao huu unaboresha ufanisi wa misuli na mishipa ya fahamu, pia huimarisha mwili, ustahamilifu na umakini, unaboresha misuli ya miguu na tishu zinazounganisha viungo
Ma MCs katika mkao wa Bhadrasana (Muafaka/Mzuri)

Mkao wa Sungura, kwalugha ya Yoga, "Sasankasana", mkao huu unasaidia kupunguza msongo wa mawazo, hasira na mengineyo, unafungua viungo vya uzazi, unasaidia kupata choo, na kutuliza maumizu ya mgongo
Mkao wa Pumzi Nyuki au kwa lugha ya Yoga, "Bhramari Pranayam", mkao huu una faida ya kupunguza msongo wa mawazo, na unasaidia kutoa wasiwasi, hofu, hasira na kuleta utulivu wa akili. Faida ya kutoa mlio kama wa Nyuki inasaidia kutuliza akili na mfumo wa neva, lakini pia ni mkao mzuri kwa kuleta utulivu kwa ujumla na kuepusha madhara ya msongo wa mawazo

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI ATEMBELEA KITUO CHA UHAMIAJI CHA HOROHORO

$
0
0

Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga,DCI Andrew Kalengo, akimuelekeza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira,mara baada ya kutembelea daraja la Mwakijembe, linalotumiwa na wakazi wa nchi za Tanzania na Kenya. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (aliyevaa kiraia), akifafanua jambo kwa viongozi wa Idara ya Uhamiaji Wilayani Nkinga, mara baada ya kutembelea jiwe linaloonyesha mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika kijiji cha Jasini kilichopo Kaunti ya Kwale. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto), akionyeshwa namba za jiwe la mpaka unaotenganisha nchi za Kenya na Tanzania mara baada ya kutembelea kituo cha Uhamiaji Horohoro. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akiweka saini katika kitabu cha wageni, mara baada ya kuwasili katika kituo cha Uhamiaji Horohoro, wilayani Mkinga mpakani mwa Kenya na Tanzania, barabara kuu ya Mombasa-Tanga.Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Horohoro, DCI Deogratius Magoma, akimuelekeza jamboKatibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira mara baada ya ukaguzi wa ofisi za jengo la kituo hicho zinazotumika katika utoaji huduma za uingiaji na utokaji wa raia wa kigeni na raia wa Tanzania wanaopitia mpaka wa horohoro , wilayani Mkinga, jijini Tanga. Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi.  



Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto), akisalimiana na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama, mara baada ya kuwasili katika kituo cha Uhamiaji Horohoro,wilayani Mkinga mpakani mwa Kenya na Tanzania, barabara kuu ya Mombasa-Tanga.Katibu Mkuu yuko jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
 
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

World Sickle Day June 19, 2016

$
0
0
Happy World Sickle Cell Day... Let's join our efforts in awareness and educating the society about SCD. Let's pray for those in hospitals and those who have passed away due to this unbearable condition. Let's pray more for the families and friends for their beloved ones having SCD.




Sickle Cell remains a burden in Tanzania, which is 5th in the World with the number of individuals with Sickle Cell Disease.

Understanding the disease would help for instance in seeking professional medical help early on and greatly reduce morbidity and mortality caused by the disease.


SICKLE CELL FACTS
❖ Sickle Cell Disease is an inherited disease from BOTH the father AND mother
❖ BOTH parents must at least have the Sickle Cell Trait for them to have a child with Sickle Cell Disease
❖ It is a lifetime disease that currently has no cure
❖ With proper professional medical care, an individual with the disease can live a long and happy life with a career and family


‪#‎KuwaMjanjaElewaSikoSeli‬

Watanzania waaswa kujifunza mchezo wa YOGA.

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza katika Siku ya Kimataifa ya Yoga iliyofanyika katika viwanja vya Coco kushiriki Siku ya kimataifa ya Yoga leo June 19, 2016 katikati ni Balozi wa  nchini Mhe. Sandip Aryan na kulia ni Mkuu wa Mkoa  wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda. Picha na raymond Mushumbusi WHUSM

Na Raymond Mushumbusi WHUSM

Watanzania wameaswa kujifunza mchezo wa Yoga ili kuimarisha miili yao na kujikinga dhidi ya matatizo mengi yanayosababishwa na mfumo wa maisha.

Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye mara baada ya kushiriki katika mahadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Yoga yaliyofanyika katika viwanja vya Coco.

Mhe. Nape Nnauye alisema kuwa mchezo huo unatoa fursa kwa watu wa kabila, dini na mataifa mbalimbali kujumuika pamoja na kujifunza utamaduni na michezo mbalimbali. “ Yoga sio kwa jamii ya kihindi peke yake ila ni kwa ajili ya watu wote Duniani na nawashauri watanzania wenzangu tujifunze mchezo huu kwa manufaa ya afya zetu na maendeleo ya michezo nchini”.Alisema Mhe. Nnauye.

Kwa upande wake Balozi wa India nchini Mhe. Sandip Arya ameshukuru Serikali kupitia Wizara ya abariHhhhhhahahahahwjvuajdsdhA

ISDUHDWWFUFWEGUA Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kutoa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha Siku ya kimataifa ya Yoga na kuahidi kuendelea kushirikiana zaidi katika kuendeleza michezo nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la Mchezo wa Kabaddi ambao ni wasimamizi wa mchezo wa Yoga nchini Bw. Abdallah Nyoni amesema Siku ya kimataifa ya Yoga ni fursa kwa watanzania kujifunza mchezo huo hasa vijana ili kujenga uwezo kwa watanzania kushiriki katika michezo mbalimbali ikiwa ni juhudi za kuendeleza michezo na na kuongeza ajira nchini.

Yoga ni mazoezi ya kiroho na kimwili yenye asili katika falsafa ya Uhindi, hujumuisha umoja wa roho na mwili, mawazo na matendo na uelewa kati ya mwanadamu na mazingira yanayomzunguka pamoja na mtazamo wa kuijumla wa afya ya binadamu.

Desemba 11,2014,Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha mapendekezo na kukubali azimio ambalo lilitambua Juni 21 kila mwaka iwe siku ya Kimataifa ya Yoga kwa kusambaza taarifa zaidi kuhusu faidi za Yoga duniani.

Mhagama; Tumieni nguvu katika kuwalazimisha wananchi kulima kukabiliana na njaa

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (katikati) akiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mohamed Utaly kukagua shamba la mihogo la mkulima wa kijiji cha Nga’mbi wilayani humo Bahati Mtonyi (kushoto), aliyepata mbegu za muhogo kutoka ofisi ya waziri mkuu idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akipata maelezo kutoka kwa mkulima wa muhogo kijijini Nga’mbi wilayani Mpwapwa, Bahati Mtonyi, aliyepata mbegu za muhogo kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa (kulia kwake) Mbunge wa jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje, (kushoto) Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mohamed Utaly na Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu , Brig.Jen, Mbazi Msuya, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (katikati) akiongozwa na Mbunge wa jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje kukagua mashamba ya muhogo kijijini Nga’mbi wilayani Mpwapwa baada ya wakulima kupewa mbegu za muhogo kutoka ofisi ya waziri mkuu idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Gereza la Mpwapwa, John Tembo, jinsi gereza hilo lilivyo panda mbegu za muhogo kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa upandaji wa mbegu hizo wilayani Mpwapwa, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (katikati) akifurahia mihogo iliyovunwa katika mashamba ya wakulima kijijini Mazae wilayani Mpwapwa baada ya wakulima kupewa mbegu za muhogo kutoka ofisi ya waziri mkuu idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa, mara baada ya kukagua utekelezaji wa upandaji wa mbegu hizo, tarehe 19 Juni 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akinawishwa mikono na Mkuu wa Gereza la Mpwapwa, John Tembo, mara baada ya kuonja chakula cha wafungwa wa gereza hilo, wakati alipotembelea gereza hilo kukagua shamba la mbegu mbegu za muhogo walizopata kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa tarehe 19 Juni 2016, (Katikati) Mkurugenzi idara ya uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akishiriki kuonja chakula cha wafungwa wa Gereza la Mpwapwa wakati alipotembelea gereza hilo kukagua shamba la mbegu za muhogo walizopata kutoka ofisi hiyo idara ya uratibu maafa kwa ajili ya kukabili maafa ya njaa tarehe 19 Juni 2016, (Kulia kwake), Mbunge wa jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje na (kushoto) Mkurugenzi idara ya uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MUU)


Na Mwandishi maalum

WAZIRI wa ofisi ya waziri mkuu Sera, Bunge vijana ajira kazi na watu wenye ulemavu Jenista Mhagama, amemwagiza mkuu wa wilaya ya Mpwapwa kuhakikisha anatumia nguvu katika kuwalazimisha wananchi kulima ili kukabiliana na tatizo la njaa ambalo limekuwa likiukabili mkoa wa Dodoma.

Mhagama aliyasema hayo jana wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea wakulima wa zao la mhogo ambao walihamasishwa kulima zao hilo linalostahimili ukame ili kukabiliana na njaa.Alisema kuwa katika kuhakikisha tatizo la njaa linakwisha mkuu wa wilaya huyo anatakiwa kuweka mikakati mipya ambayo itakuwa na tija katika kuhakisha njaa inakwisha wilayani hapo.

Aidha alisema kuwa uongozi wa wilaya hiyo unatakiwa kubuni mikakati mipya tofauti na ile ya zamani ili kutumia nguvu kazi iliyopo katika kushiriki kilimo na kusaidia kuondokana na tatizo la njaa.“Kama mtaendelea na mikakati yenu ya kila siku tatizo la njaa halitakwisha mnatakiwa hivi sasa kutumia nguvu lazimisheni wananchi walime mazao yanayostahimilimi ukame kama mihogo na mtama”alisema Mhagama.

Alisema kuwa ofisi ya waziri mkuu kupitia kitengo cha maafa ilitoa sh. Milioni 35 kwajili ya kununua mbegu za mihogo na mtama kwajili ya wananchi ya wilaya hiyo waliokuwa wanakabiliwa na baa la njaa.Aliongeza kuwa kwa namna alivyo jionea maendeleo ya baadhi ya wakulima waliolima mihogo wameweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na baa la njaa kwa kipindi kirefu.

“Kwa hali hii basi sisi kama ofisi wa waziri mkuu hatuna haja ya kuendelea kuleta chakula cha msaada tena huku kwakuwa zao la mihogo ambalo sisi tulileta mbegu imeweza kuwasaidia wakulima kuondokana na njaa lakini pia wengine wamejenga nyumba na kuezeka kwa bati”alisema Mhagama.
Aidha Mhagama alisema kuwa kutokana na wakulima hao kuonyesha mafanikio uongozi wa wilaya hiyo uongeze bidii katika kuhamasisha kilimo cha zao hilo.

“Inabidi muwe na hata sheria ambazo zitawalazimisha wananchi kila mmoja wao kulima heka mbili za muhogo na mbili zingine za mtama na katika hili msimbembeleze mtu tumieni nguvu ili kuweza kuondokana na na tatizo la njaa mkoani hapa”alisema.Hatahivyo alimwagiza ofisa kilimo wa wilaya Yustina Munishi , kuhakisha idadi ya wakulima inaongezeka tofauti na iliyopo hivi sasa.

“Hadi mwakani tarehe kama ya leo nataka kuja kukaguma mashamba zaidi ya 300 na kama sitayakuta kwa idadi hiyo utakuwa huna kazi afisa kilimo”alisema.Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mohamed Utaly alisema kuwa watakipanga kuhamasisha kilimo cha zao hilo la muhogo ambalo limeonekana kuwa mkombozi wa njaa.

“Katika kipindi kijacho cha kilimo kupitia mikakati yetu tutahakikisha kila kaya inalima heka mbili za mhogo na heka mbili za mtama ili kuondokana na baa la njaa ambalo limekuwa likiikabili wilaya hiyo kila mwaka”alisema Utaly.Naye mmoja wakulima hao Bahati Mtonyi,alisema kuwa kupitia zao hilo la muhogo ameweza kujenga nyumba na kujilipia ada kila mwaka kiasi cha sh. 600.000.

MAKAMU WA RAIS AHIMIZA WATOTO KUPEWA ELIMU KATIKA MASHINDANO YA KUHIFADHI QURAN

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwasili kwenye ukmbi wa Diamond Jubilee ambapo kulikuwa na mashindano ya kuhifadhi Quran yalioandaliwa na Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Aisha Sururu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akizungumza na Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Aisha Sururu Bi. Aisha Sururu (kushoto) na Katibu wa Taasisi hiyo Bi. Joha Lemky wakati wa mashishindano ya kuhifadhi Quran yaliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Sehemu ya Viongozi waliohidhuria mashindano hayo ya kuhifadhi Quran
Majaji wa Mashindano ya kuhifadhi Quran yalioandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Aisha Sururu kwenye ukumbi wa Diamond.
Sheikh Muharami Mziwanda akitoa elimu juu ya umuhimu wa kuijua Quran kwenye mashindano ya Kuhifadhi Quran yaliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Kijana mwenye ulemavu wa macho Ali Hamisi Mpemba akisoma Juzuu 30 wakati wa mashindano hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa nasaha zake mara baada ya shindano la kuhifadhi Quran lililoandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Aisha Sururu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidi mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake na mshindi wa jumla wa kuhifadhi quran juzuu 30 ,Ashura Amani (16) mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Benjamini Mkapa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa kike walioshiriki mashindano ya kuhifadhi quran kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi nchini kuhakikisha wanawapa watoto wao elimu tangu wakiwa wadogo ili iwajengee misingi bora katika maisha yao.

Mheshimiwa Samia ameeleza hayo wakati akizungumza kwenye mashindano ya Qur'an yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es salaam.Alisema wazazi wanapaswa kutambua kuwa hakuna zawadi kubwa kwa mtoto kama elimu kwa sababu itamjengea misingi ya kujua afanye nini katika kuendesha maisha yake kwa mafanikio.

"Vile vile, niwaombe wazazi tuwatengenezee watoto wetu fursa wapate muda wa kupata elimu. Ukimpa utajiri mtoto na kwa kuwa hana elimu anaweza asiutumie vizuri; lakini ukimpa elimu itamfaa katika kuendesha maisha yake," alisema Makamu wa Rais.

Aidha, aliwataka washindi wote wa kuhifadhi Qur'an wasisite kutafuta elimu zaidi ya dini na ya dunia kama maandiko ya kitabu kitakatifu cha Qur'an yanavyousia ili iweze kuwasaidia ulimwenguni na huko akhera kwenye maisha ya milele.

Makamu wa Rais alielezea kufarijika kwake kuona kuwa idadi ya washindani inaongezeka kila mwaka bila ya kubagua jinsia zao na washiriki wa mashindano hayo wakiwa na umri mdogo."Hii inaonyesha kwamba vijana wanayo fursa nzuri ya kuhifadhi Qur'an Tukufu tena juzuu nzima wakiwa wadogo endapo sisi kama wazazi tutalifanyia kazi na kuwahimiza vijana wetu," alidokeza.

Mapema Katibu wa Taasisi ya Aisha Sururu Foundation iliyoandaa mashindano hayo Bi Jokha Lemky alimweleza Makamu wa Rais kuwa kwa mwaka huu mashindano hayo yameshirikisha mikoa 24 ya Tanzania Bara na Visiwani yakiwa na washiriki 653 ambapo 66 ndiyo wameingia fainali.

Alisema pamoja na mafanikio hayo lakini Taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto za kukosekana kwa kompyuta, photocopy, usafiri, scholarship na zawadi kwa washindi jambo ambalo Makamu wa Rais alisema atajitahidi kufanya kazi bega kwa bega na Taasisi hiyo katika kutatua changamoto hizo.

Katika mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'an Makamu wa Rais alikabidhi zawadi kwa washindi waliohifadhi juzuu tatu hadi 30 ambapo aliyehifadhi juzuu 30 alipata shilingi milioni tano.Mashindano hayo yalihudhuriwa na waumini mbalimbali wa dini ya kiislam wakiwemo Balozi wa Algeria nchini na wawakilishi wa mabalozi wa Misri, Sudan na Iran.

TANZANIA KUSHIRIKI MIAKA 65 YA JUNDOKAN KARATE 2018, NAHA CITY, OKINAWA, JAPAN.

$
0
0

Mwalimu wa Karate wa kimataifa Sensei Rumadha

Magwiji wa karate duniani wakiwa katika picha ya pamoja katika kongamano la Karate European Jundokan Gasshuku.

………………………………………………………………………………….
Sensei Rumadha Fundi mwalimu wa karate mtanzania anatambuliwa na baraza la OKINAWABODOKAN & KARATE FEDERATION” lenya makao Okinawa,Japan,juzi katika alikuwa ni mwakilishi pekee kutoka Afrika katika kongamano la walimu magwiji wa karate lilifanyika Lisabon,Ureno.

Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu ni chimbuko la dojo iliyo
jengwa na Master Eiichi Miyazato miaka 63 iliyo pita huko mjini Naha,
Okinawa baada ya kifo cha mwanzilishi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu ,
Master Chijun Miyagi , ambayo hivi sasa inaendeshwa na mtoto wake
Yoshihiro Kancho Miyazato.

Sensei Rumadha Fundi, amepokea na kukubali mwaliko kama
mwakilishi wa “JUNDOKAN SO HONBU” Tanzania ikiwa natumaini la usajiri wa
chama hicho hapa Tanzania ambao kwa sasa bado unalegalega.
Sensei Rumadha yupo nchi Ureno hivi sasa akishiriki katika kongamano la Karate ” European Jundokan Gasshuku 2016″.

Na wakati huohuo, kitengo kinachisimamia ubora na uthabiti wa
sanaa asili ya mitindo ya karate toka Okinawa kiitwacho ” OKINAWA
BODOKAN & KARATE FEDERATION” imefanya mabadiliko hivi karibuni
yatakayo tofautisha karate asilia na ile ya kimichezo itayo kuwa
katika michezo ya Olympics.

Kutokana na mabadiliko ya kimbinu na ufasaha yanayo onekana
katika michezo, shirikisho hilo limeamua kutofautisha kabisa jinsi
karate asilia izidi kuimarika na kutochujwa na kuwa sanaa nyepesi.
Pia, kuhakikisha kwa kiundani zaidi kwamba mbinu halisi,
zinazingatiwa na ma- Sensei wote wa mitindo ya karate toka visiwani
Okinawa duniania kote.

Hivyo ime teuwa timu ya Karate ya Okinawa ( Masters) toka
mitindo mbalimbali inayo tambulika na ” BUDOKAN” kusambaza uadilifu wa
mitindo hiyo kama jinsi ilivyokuwa inafundisha na waasisi wake asilia.
Semina hii inayoendelea nchini Ureno inawawezesha walimu (
Sensei) kuwa na mabadiliko au kuendana sambamba na jinsi sanaa inavyo
jadiliwa katika chimbuko lake chini ya shirikisho hilo huko
Okinawa,Japan.

Tunatumaini kwamba chama cha “JUNDOKAN SO HONBU” kitapata
usajili wake nchini Tanzania pasipo fika mwaka 2018, chini ya Sensei
Rumadha Fundi mwakilishi wa “JUNDOKAN SO HONBU” Afrika mashariki na Kati. Endapo usajili utaleta kulegalega na kuvuta muda zaidi, basi chama
hicho hakitakuwa na budi, bali kitajisajili visiwa vya Zanzibar kwanza.
Alimalizia hivyo; sensei Rumadha

MTUMISHI WA MUNGU MASANJA MKANDAMIZAJI ARINDIMA KATIKA MKUTANO WA OYES 2016 JIJINI MWANZA.

$
0
0

Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akihudumu katika Mkutano Mkubwa wa Injili wa Open Your Eyes and See OYES 2016 wenye lengo la kuwafungua watu wote kiroho na hivyo kuondokana na vifungo mbalimbali vinavyowakabiri, uliofanyika katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.

Mkutano huo ulianza June 12,2016 na kufikia tamati jana June 19,2016 katika viwanja vya Kanisa hilo. Wahubiri na waimbaji mbalimbali walihudumu katika mkutano huo akiwemo Mchungaji wa Kimataifa kutoka nchini Canada Mama Domitila Nabibone ambae amewahi kufariki na kufufuka siku ya nne, Mwimbaji na Mhubiri Joseph Rwiza pamoja na Mwimbaji Chamwenyewe Jembe ambapo watu wengi walifunguliwa kiroho na kuokoka katika mkutano huo. Na George Binagi-GB Pazzo
Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akihudumu katika Mkutano Mkubwa wa Injili wa Open Your Eyes and See OYES 2016, uliofanyika katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.

Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akiimba katika Mkutano wa OYES 2016

Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akiimba katika Mkutano wa OYES 2016

Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola (Kushoto), akiwa na Mama Mchungaji, Mercy Kulola (Kulia) katika Mkutano wa OYES 2016

Mama Mchungaji, Mercy Kulola (kushoto) akiwa katika Mkutano wa OYES 2016

Mwimbaji Chamwenyewe Jembe (Kushoto) pamoja na Mhubiri na Mwimbaji Joseph Rwiza (Kulia) wote kutoka mkoani Morogoro wakiwa katika Mkutano wa Injili wa OYES 2016

Wazee wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakiwa katika Mkutano wa OYES 2016

Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakiwa katika Mkutano wa OYES 2016

Ni katika Mkutano wa OYES 2016 ambao umewafungua watu wengi kiroho



Wakazi wa Jiji la Mwanza pamoja na Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakiwa katika Mkutano wa OYES 2016

Wakazi wa Jiji la Mwanza pamoja na Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakiwa katika Mkutano wa OYES 2016.

Prof Jay: Beef na Team zinawafanya wasanii wasifike kimataifa

Article 22

RASIMU YA MWISHO YA MICHORO YA MPANGO MJI KABAMBE WA ARUSHA 2035 KUIDHINISHWA NA WADAU

$
0
0

 
Wawakilishi toka Serikali za mitaa, Serikali ya mkoa na Serikali kuu, sekta binafsi na taasisi za kijamii za kiraia zinakutana leo tarehe 20 Juni mjini Arusha ikiwa ni mkutano wa tatu wa wadau wa mpango mji  wa Arusha 2035.
 
Timu yenye wataalamu kutoka jiji la Arusha,Mkuu wa wilaya wa Arusha na Meru Arusha, tume ya undeshaji ya Mkoa  na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi watazindua  Rasimu ya Mwisho ya Mpango Mji Kabambe wa Arusha 2035 , wakisaidiwa na mshauri mtaalam aliyeteuliwa toka Singapore, Surbana International Consultants   

Maeneo ndani ya mpango mji itachukua kilometa za mraba 278 za mji wa Arusha na kilometa za mraba 330 zilizochaguliwa za wilaya ya Arusha na Arumeru zikifanya jumla ya kilometa za mraba 608.

Rasimu hii ya Mwisho ya mchoro pendekezi itaonyesha matumizi ya siku zijazo ya ardhi ndani ya eneo linalopangwa . Pamoja na haya utaonyesha mpango mzima wa usafirishaji na barabara, mpango wa aina mbali mbali za barabara,  miundombinu na usafirishaji wa mizigo utaelezwa kwa kina.

Hali kadhalika mchoro pendekezi unaoonyesha mpango mzima wa miundombinu utaelezewa kwa kina, hii ni pamoja na mpango kazi na mtandao wa maji safi na maji taka, maji ya mvua, taka ngumu, mfumo wa umeme na mtandao wa mawasiliano ya teknolojia. Maendeleo ya uchumi wa pamoja na ulinzi wa mazingira itakuwa ni sehemu kubwa ya mada. Michoro ya usanifu wa kina utawasilishwa kuonyesha uwezo wa kijamii na kiuchumi wa siku zijazo “Mji Mkuu Kijani wa Afrika Mashariki”.

Uwasilishwaji wa Rasimu na wataalamu utakamilishwa na maelezo ya kina ya “Mpango wa Utekelezaji”. Mpango pendekezi unalenga kuwa wa maono lakini pia uoneshe uhalisia kwa hivyo umuhimu wa uundaji wa hati maalum yakusaidia utelekelezaji wa mpango huu. 
 
“Rasimu ya mwisho ya michoro ni hatua muhimu kwa mkoa wetu. Mahitaji ya baadaye kwa ajili ya mji wetu unaokua, unatuhitaji kuwa na mipango ya nyumba zaidi, miundombinu bora, mipango ya maendeleo bora kwa ajili ya viwanda, makazi na maeneo ya kijani kwa njia inayojali mazingira. Hii rasimu ya mwisho inatupa fursa ya kuweza kutengeneza mji wa kijani, kitovu cha kanda, na kuonyesha mfano wa ufanisi katika upangaji wa mji” alisema Juma Idd Mkurugenzi wa Jiji la Arusha.

Mkutano wa kwanza wa wadau ulifanyika Mei mwaka 2015, ulizungumzia mchanganuo wa  muktadha wa kanda kwa wadau na pia kupendekeza mtazamo na mpangilio wa siku zijazo wa mamlaka ya jiji la Arusha. Mtazamo wa jumla wa matokeo ya waatalaam ya mkutano wa wadau uliopita utajadiliwa mbele ya wadau watakaokuwepo.

Huu ilifuatiwa na mkutano wa pili wa wadau Novemba 2015, na mkutano wa wataalam Dar es Salaam , Disemba 2015.

Lengo la mkutano huu wa mwisho wa wadau kama ilivyoagizwa na Sheria ya Mipango ya mwaka 2007 ni kuidhinisha hii Rasimu ya mwisho. Hatimaye Rasimu ya Mwisho ya Michoro itatumwa kwa madiwani, kwa Katibu Tawala wa Mkoa  na kwa Mkurugenzi wa Mipango Miji kwenye Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Baada ya kuipitia, jamii itapata fursa ya kushiriki kikamilifu, kukusanya maoni na mapendekezo, kabla ya idhini ya mwisho kutoka kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Hatua hii shirikishi inalenga kupokea mchango muhimu wa kuboresha mpango mji wa Arusha kutoka kwa wadau wote.

Wananchi wote watajulishwa mara kwa mara kuhusu hatua za maendeleo za mpango mji kupitia vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni machapisho, na mitandao ya kijamii. Watu wote wanakaribishwa kutoa maoni yao juu ya mpango mji.

Kupitia Facebook: Arusha 2035, Instagram: Arusha2035 na Twitter: Arusha_2035, kwa kutoa maoni yao kwenye sanduku la maoni katika wilaya na ofisi za kata au baruapepe: arusha2035@gmail.com.



KUHUSU SURBANA

Surbana Consultans Pte. Ltd. Ni kampuni iliyosajiliwa Singapore mwaka 2003 kama kampuni inayofanya biashara ya ushauri wa kitaalam ikitoa huduma kamili za ujenzi, ikiwemo usanifu wa majengo, uhandisi, ukadiriaji majenzi, na usimamizi wa miradi ya ujenzi, coastal engineering and miundombinu, mipango miji, tekinologia ya ujenzi na usimamizi wa miji mikubwa.

Kuanzia hapo, Surbana imefanikiwa kutanua huduma zake za kibiashara katika nchi 30 wakati ikibakia kuongoza katika soko la ujenzi wa nyumba za makazi Singapore. Kwa mchango wake mkubwa katika mazingira yaliyojengwa, Surbana imepokea tuzo mbalimbali ikwepo World Habitat Award na tuzo ya FIABCI Prix D’excellence . Surbana imepewa hadhi ya kuwa moja ya kampuni kumi bora za usanifu wa majengo na ujenzi Singapore na Building and Construction Interchange Asia (BCI Asia).

Kampuni ina uzoefu mkubwa barani Afrika, kuanzia 2005. Miradi yao ni pamoja na mradi uliowapatia tuzo ya mpangomji na kiwango cha kanda cha mipango mji, mji wa Kigali, Rwanda. Surbana kwa sasa inatoa ushauri kwa Serikali ya Tanzania , pia kwa Mpango Mji Kabambe wa Mwanza.
 Kwa kuongezea, mipango miji ya  Cazenga/Sambizanga nchini Angola, Oyo-Oliombo nchini DRC na Royal Bafokeng, Afrika Kusini.

Biashara zote za ushauri na maendeleo ya miji sasa inaajiri zaidi ya watu 2,200 katika miji 17 katika bara la Asia, na mashariki ya kati. Surbana inamilikiwa wa Temasek Holdings (60%) na CapitLand (40%).

Kwa Maelezo Zaidi au Maswali:
Mkurugenzi wa Jiji

MHASHAMU ASKOFU, JOSEPHAT LOUIS LEBULU ATOA SAKRAMENTI YA KIPAIMARA WA WATOTO 26 WA PAROKIA YA BIKIRA MARIA MAMA WA HURUMA BEACH BICHI JIMBO KUU LA DAR ES SALAAM.

$
0
0
ASKOFU wa  Mkuu wa Jimbo katoliki la Arusha, Mhashamu Askofu, Josephat Louis Lebulu  ametoa Sakramenti ya Kipaimara kwa watoto 26 wa Parokia ya Bikira Maria mama wa Huruma- Mbezi Beach  jimbo kuu la Dar es Salaam jana Juni 19,2016.
Askofu wa  Mkuu wa Jimbo katoliki la Arusha, Mhashamu Askofu, Josephat Louis Lebulu(Mwenye Kofia ya Kichungaji) akiwa katika picha ya pamoja na watoto 26 waliopata Kipaimara jana  pamoja na viongozi mbalimbali wa Parokia ya Bikira maria Mama wa Huruma Mbezi Beach jimbo kuu la Dar es Salaam.
 Baadhi ya watoto wakiandamana kuelekea ndani ya kanisa kwaajili ya Kupata Sakramenti ya Kipaimara.
 Watoto wakiwa kanisani katika Parokia ya Bikira Maria mama wa Huruma- Mbezibichi  jimbo kuu la Dar es Salaam jana Juni 19, 2016.

Watoto wakienda kumpongeza Askofu wa  Mkuu wa Jimbo katoriki la Arusha, Mhashamu Askofu, Josephat Louis Lebulu(Mwenye Kofia ya Katikati kwa kufika katika Parokia ya Bikira Maria mama wa Huruma- Mbezi beach  jimbo kuu la Dar es Salaam jana Juni 19, 2016. 

 Baadhi ya Waumini wailiohudhuria ibada ya Askofu wa  Mkuu wa Jimbo katoliki la Arusha, Mhashamu Askofu, Josephat Louis Lebulu, katika Parokia ya Bikira Maria mama wa Huruma- Mbezi beach   jimbo kuu la Dar es Salaam jana Juni 19, 2016. 
 Watoto waliopata Sakramenti ya Kipaimara wakiwa  katika picha ya pamoja na Parokia ya Bikira Maria mama wa Huruma- Mbezi beach   jimbo kuu la Dar es Salaam jana Juni 19, 2016 mara baada ya kupata Sakramenti hiyo.
Mtoto aliyepata Sakramenti ya Kipaimara, Samwel Stephano Kakingo, akiwa katika picha na Msimamizi wake mara baada ya Kupata Sakrament hiyo na Askofu wa  Mkuu wa Jimbo katoliki la Arusha, Mhashamu Askofu, Josephat Louis Lebulu alipofika na kuwapa Sakramenti ya Kipaimara katika parokia hiyo.
 Mtoto aliyepata Sakramenti ya Kipaimara, Samwel, Stephano Kakingo.
 Mtoto aliyepata Sakramenti ya Kipaimara, Samwel, Stephano Kakingo mwenye mataji akiwa katika picha ya Pamoja na wazai wake.
 Mtoto aliyepata Sakramenti ya Kipaimara, Samwel Stephano Kakingo akiwa katika picha ya pamoja na Shangazi zake.
  Mtoto aliyepata Sakramenti ya Kipaimara, Samwel Stephano Kakingo akiwa katika picha ya pamoja na baba yake mdogo Kushoto na mama zake wadogo.
  Mtoto aliyepata Sakramenti ya Kipaimara, Samwel Stephano Kakingo (mwenye mataji) akiwa katika picha ya pamoja na ndugu na jamaa waliofika kumpongeza mara baada ya kupata Sakramenti ya Kipaimara.
 Mtoto aliyepata Sakramenti ya Kipaimara, Samwel Stephano Kakingo (mwenye mataji) akiwa katika picha ya pamoja na majirani.
Mtoto aliyepata Sakramenti ya Kipaimara, Samwel Stephano Kakingo (mwenye mataji)akiwa katika picha ya pamoja na wadogo zake.
 Mtoto aliyepata Sakramenti ya Kipaimara, Samwel Stephano Kakingo (mwenye mataji) akiwa katika picha ya pamoja na mama yake mdogo (kulia) mdogo wake Jakson Kakingo na Shangazi yake Neema Mbwilo wa kwanza kushoto.

 Keki ya Pongezi kwa Samwel Stephano Kakingo.
 Mtoto aliyepata Sakramenti ya Kipaimara, Samwel Stephano Kakingo kulia akiwa na mpambe wake.
 Mtoto aliyepata Sakramenti ya Kipaimara, Samwel Stephano Kakingo (Kulia) akikata keki.
 Shangazi wa Samwel Stephano Kakingo, Lulu Kakingo akimsaidia Samwel kukatakata keki kwaajili ya kujipongeza.
 Mtoto aliyepata Sakramenti ya Kipaimara, Samwel Stephano Kakingo akilishwa keki na Mpame wake jana mara baada ya upata Sakramenti ya Kipaimara na Askofu wa  Mkuu wa Jimbo katoliki la Arusha, Mhashamu Askofu, Josephat Louis Lebulu.
 Mpambe wa Samwel akilishwa keki.
 Samwel akimlisha keki Baba yake.
  Samwel akimlisha keki Mama yake.
  Samwel akimlisha keki Babu yake, Mzee Peter Kakingo.
  Samwel akimlisha keki Bibi yake, Mama Kakingo.
















Askofu wa  Mkuu wa Jimbo katoliki la Arusha, Mhashamu Askofu, Josephat Louis Lebulu (Aliyevaa  Msalaba) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waumini wa Parokia ya Bikira maria Mama wa Huruma Mbezi beach  jimbo kuu la Dar es Salaam mara baada ya kutoa Sakramenti ya Kipaimara kwa watoto 26 wa Parokia hiyo.

VIJUSO VYA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNI 20

Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images