Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 887 | 888 | (Page 889) | 890 | 891 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa MNH, Aligaesha akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari LEO jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha akizungumza na waandishi wa habari LEO kuhusu hospitali hiyo kuanza kuboresha huduma ya chakula kwa wagonjwa (special diet) wanaolazwa MNH kuanzia Julai Mosi, mwaka huu.
   Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agness Mtawa akifafanua jambo LEO katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu hospitali hiyo kuanza kuboresha huduma ya chakula kwa wagonjwa. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Aminiel Aligaesha akiwa kwenye mkutano huo. 

  ·         Yawaondolea usumbufu ndugu wa wagonjwa kupeleka  chakula mara tatu kwa siku.
  ·         Ndugu watapata muda wa kuendelea na shughuli za uzalishaji
  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeboresha huduma za chakula kwa wagonjwa wote watakaolazwa kuanzia Julai Mosi, mwaka huu ili kuwaondolea ndugu wa wagonjwa usumbufu na gharama za usafiri wakati wa wanapokwenda kuwaona ndugu zao waliolazwa mara tatu kwa siku katika hospitali hiyo.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar Es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw. Aminiel Aligaesha amesema hospitali imeingia ubia na mzabuni ili kutoa huduma hiyo kwa wagonjwa wote wanaolazwa.

  Kwanini Hospitali imechukua hatua hii
  Bw. Aligaesha amesema Hospitali inataka kujikita katika majukumu yake ya msingi ambayo ni kushauri, kuchunguza na kutibu.

  “Aidha Hospitali inataka kuwaondelea adha ndugu wa wagonjwa ambao wamekuwa wakiingia gharama kubwa hususani usafiri wa kuja Hospitalini mara tatu kwa siku, ambapo kwa kukadiria gharama ya usafiri wa ndugu mmoja wa mgonjwa ni kati ya shilingi 6,000/= na 10,000/= kwa siku, kulingana na mahali anapotokea bila kujumuisha gharama za kuandaa chakula cha mgonjwa ambacho mara nyingi ni chakula maalumu. Na kama mgonjwa akilazwa zaidi ya siku tano hadi 10 ndugu mmoja wa mgonjwa gharama atalipia fedha nyingi kwenye usafiri” amesema Bw. Aligaesha


  Ameongeza kuwa adha ya pili wanayopata ndugu ni usumbufu ambapo inabidi kuacha shughuli nyingine za uzalishaji ili kuja kuleta chakula mara tatu kwa siku, hivyo kuingiliana na shughuli zao za kiuchumi na kimandeleo na kushindwa kuzalisha. Hivyo jukumu hili linachukuliwa na Hospitali kuwaondolea adha hii.
  “Pia kuna baadhi ya ndugu wamekuwa wakishindwa kuwaletea chakula wagonjwa wao hivyo hospitali ililazimika kuwapatia chakula ambacho kilikuwa kwa ajili ya wagonjwa wanaotoka mikoani wasio na ndugu hapa Dar Es Salaam” amesisitiza Bw. Aligaesha. 

  Amesema kumekuwepo na ongezeko la msongamano wa watu ndani ya Hospitali toka asubuhi saa 12 mpaka saa 12 jioni, suala linaloingiliana na utoaji huduma hasa saa za mchana kwani muda wa saa 6.00 hadi saa 8.00 mchana ulikuwa unaingiliana na majukumu ya kiutendaji ambapo majopo mbalimbali ya watalaamu yamekuwa yakiendelea na raundi za wagonjwa waliolazwa. Hii wakati mwingine imesababisha mgonjwa kutokupata huduma stahiki kutokana na muingiliano huu.
  ·                      
  “Vile vile msongamano huu ni changamoto kwa ajili ya masuala ya kiusalama ambapo kati ya watu wanaoingia Hospitali kwa kigezo cha kuja kuona wagonjwa kuna wanaoingia kwa lengo la kufanya uhalifu ikiwemo wizi wa mali za Hospitali, magari  pamoja na vifaa vya magari” alisisitiza.
                 
   Amesema kwa kufanya hivyo, Hospitali itapunguza baadhi ya gharama za uagizaji wa vyakula kwa wazabuni, kulinda upotevu na baadhi ya vyakula kuharibika wakati mwingine kwani utunzaji wa vyakula una mahitaji makubwa.

    Bw. Aligaesha amesema Hospitali inakusudia kutoa chakula chenye ubora na viwango vinavyotakiwa kwa wagonjwa ikiwemo kutoa chakula maalumu (special diet) kwa wagonjwa wenye uhitaji huo. 

  Utaratibu wa chakula cha mzabuni kwa wagonjwa
   Kuhusu utaratibu huo Bw. Aligaesha amesema Mzabuni ndiye atakayepika chakula kwa wagonjwa wote waliolazwa na atatayarisha, atakipeleka na kukikabidhi katika wodi husika ambapo jukumu la kumpa mgonjwa kifungua kinywa, chakula cha mchana na jioni linabaki wa Hospitali.
    
     Amesema wagonjwa watapatiwa milo mitatu kwa siku yaani asubuhi, mchana na jioni kazi itakayofanywa na muuguzi wa zamu ambaye atahakikisha wagonjwa wote wamepata chakula kufuatana na mahitaji (diet list) iliyowasilishwa jikoni kutokana na mahitaji yao ya kiafya.

  Muda wa kuona wagonjwa
  Kutokana na uamuzi huu, utaratibu wa ndugu kuleta chakula kwa wagonjwa waliolazwa wakati wa mchana umefutwa na hivyo mchana hatutakuwa na nafasi ya ndugu kuja kutembelea wagonjwa. Muda wa kutembelea wagonjwa utakuwa asubuhi saa 12 hadi saa moja kamili na saa 10:00 jioni hadi saa 12:00jioni ndipo ndugu wataruhusiwa kuingia ndani kuwaona ndugu zao waliolazwa. Katika muda huo ndugu ataruhusiwa kuja na chakula chochote anachofikiri atamuongezea mgonjwa wake kama matunda n.k

  Uchangiaji huduma ya chakula
    Bw. Aligaesha amesema mgonjwa aliyelazwa atachangia kiasi cha shilingi 50,000 atakapolazwa ambapo kati ya hizo, shilingi elfu 10,000 itakuwa ni gharama ya kumuona daktari (Consultation), shilingi elfu 10,000 ikiwa ni gharama ya kulazwa na bei ya chakula itakuwa shilingi elfu 30,000 sawa na shilingi elfu 6,000 kwa siku. Wastani wa mgonjwa kukaa wodini ni siku tano. Gharama hizo zinahusika kwa muda wote atakaokuwa amelazwa.

  Kwa sasa Hospitali inatoa chakula kwa wagonjwa 650 ambao wamepata rufaa kutoka hospitali za nje ya mkoa wa Dar es Salaam kwa gharama wastani wa shilingi 1.8 bilioni kwa mwaka, sawa na shilingi 150 milioni kwa mwezi kwa vyakula pamoja na  gharama nyingine kama vile za nishati. Takribani wagonjwa kati ya 600 na 700 ambao rufaa zao ni kutoka Hospitali za Dar es Salaam walikuwa hawapati chakula kutoka Hospitalini, na ilibidi ndugu zao wawaletee chakula. Hata hivyo, Hospitali ilikuwa inawapatia chakula tu kama ndugu zao wakishindwa kufanya hivyo.

    Hitimisho.
  “Uongozi wa Hospitali unaamini kwamba mabadiliko haya hayatamuongezea mgonjwa gharama, bali yatampunguzia gharama pamoja na ile adha kama ilivyoainishwa hapo juu. Aidha, uongozi unaamini kwamba uamuzi huu unaendana na azma nzima ya kuboresha utoaji huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuboresha mazingira ya Hospitali. Tunaomba ushirikiano wenu katika kutekeleza jukumu hili ili kusudi wagonjwa waweze kuhudumiwa vizuri zaidi” amesisitiza Bw. Aligaesha.

  0 0

   Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brg. Jen, Mbazi Msuya akisisitiza umuhimu wa Mfumo wa Uchambuzi wa Uhakika wa Chakula na Lishe (MUCHALI) wakati akifungua semina ya uboreshaji mfumo huo mjini Morogoro, tareehe 1 Juni, 2016.
   Baadhi ya washiriki kutoka Wizara, Taasisi na Idara za Serikali wakifuatilia uwasilishaji wa mada za umuhimu wa Mfumo wa Uchambuzi wa Uhakika wa Chakula na Lishe (MUCHALI) wakati akifungua semina ya uboreshaji mfumo huo mjini Morogoro, tareehe 1 Juni, 2016.
   Baadhi ya washiriki kutoka Wizara, Taasisi na Idara za Serikali wakifuatilia uwasilishaji wa mada za umuhimu wa Mfumo wa Uchambuzi wa Uhakika wa Chakula na Lishe (MUCHALI) wakati akifungua semina ya uboreshaji mfumo huo mjini Morogoro, tareehe 1 Juni, 2016.
  Baadhi ya washiriki kutoka Wizara, Taasisi na Idara za Serikali wakifuatilia uwasilishaji wa mada za umuhimu wa Mfumo wa Uchambuzi wa Uhakika wa Chakula na Lishe (MUCHALI) wakati akifungua semina ya uboreshaji mfumo huo mjini Morogoro, tareehe 1 Juni, 2016.
   Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brg. Jen, Mbazi Msuya (mwenye suti) akiwa katika picha ya pamoja na  washiriki kutoka Wizara, Taasisi na Idara za Serikali mara baada ya  kufungua semina ya uboreshaji wa Mfumo wa Uchambuzi wa Uhakika wa Chakula na Lishe (MUCHALI) mjini Morogoro, tareehe 1 Juni, 2016.

  0 0

  Na Mwene Said wa Blogu ya Jamii, Dar es Salaam.

  Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Leonard Kyaruzi amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashtaka mawili ikiwemo kuchepusha na kusambaza taarifa za kumdhalilisha Rais Dk. John Magufuli kwa njia ya mtandao whattsapp.

  Mshtakiwa huyo amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Magreth Bankika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

  Wakili wa Serikali Simon Wankyo alidai kuwa June 2, mwaka huu katika jengo la Tanzanite Tower lililopo barabara ya Sam Nujoma, mshtakiwa alichapisha taarifa ya kumdhalilisha Rais Magufuli.

  Wankyo alinukuu taarifa hiyo kwamba”Hivi huyu Pombe ni kwamba hana washauri? Hashauriki? Au ni zuzu?Bwege sana huyu jamaa, He Doesn’t consider the law in place before opening his mouth! Au nay eye anaumwa ugonjwa wa Mnyika?” .

  Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, mshtakiwa alisambaza taarifa ya kumdhalilisha Rais Magufuli, kupitia mtandao wa Whattsapp kwamba “Hivi huyu Pombe ni kwamba hana washauri? Hashauriki? Au ni zuzu?Bwege sana huyu jamaa, He Doesn’t consider the law in place before opening his mouth! Au nay eye anaumwa ugonjwa wa Mnyika?”.

  Mshtakiwa alikana mashtaka hayo.
  Hakimu Bankika amesema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kuwa na mdhamini mmoja anayetambulika, atakayesaini hati ya dhamana ya Sh. Milioni moja.

  Mshtakiwa alitimiza masharti hayo. Upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Hakimu amesema kesi hiyo itatajwa Julai 18, mwaka huu na mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana.

  0 0


  Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mjini Dodoma kuhusu maadili ya Vyombo vya Habari katika kuhabarisha Umma juu ya miradi ya maendeleo na jinsi vinavyoweza kuwasaidia wananchi kuleta maendeleo na kuepuka kutoa taarifa za upotoshaji.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe na Vyombo vya Habari leo Mjini Dodoma. (Picha Zote na Frank Mvungi – MAELEZO – Dodoma).

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila Akiwakaribisha wananchi walio na kero za migogoro ya Ardhi ofisini kwake ili kuzitatua kero zao ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Moses Kusiluka (katikati mwenye suti na tai) akipokea kero za wananchi zinazohusu migogoro ya Ardhi ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.

  Katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2016, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kupitia watendaji wake wakuu leo tarehe 21/06/2016 amefanya utaratibu maalumu wa kukutana na wananchi wenye kero na migogoro ya ardhi. 
   
  Katika kutekeleza hilo Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Moses Kusiluka wamekutana na wananchi ana kwa ana ili kuwasikiliza na kuzipatia ufumbuzi kero na migogoro yao inayohusu ardhi na nyumba.

  Hatua hii imefuatia baada ya hapo jana tarehe 20/06/2016 viongozi hao kukutana na watumishi wa Wizara hiyo na kutatua kero zao zinazohusu maslahi ya watumishi ambapo kwa mwaka huu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yameamuliwa yafanyike kwa utaratibu huu.

  0 0


  Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Nisha Film Production Salma Jabu (Nisha).
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Nisha Film Production Salma Jabu (Nisha) akizungumza na waandishi wa habari( hawapo pichani) juu ya kufuturisha watoto waishio katika mazingira hatarishi Juni 26 mwaka huu  katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Azania-Upanga, jijini Dar es Salaam kushoto ni  Afisa Uhusiano wa Nisha Film Production, Baraka Nyagenda.
   Meneja wa kampuni ya Nisha Film Production, Myovela Mfwaisa akifafanua jambo kwenye mkuano uliofanyika leo  jijini Dar es Salaam kulia ni Afisa Uhusiano wa Nisha Film Production, Baraka Nyagenda.
  (Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii). 

  0 0

  MSERU1 
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Profesa. Lawrence Mseru akitoa ufafanuzi kuhusu habari iliyoandikwa na Gazeti la Mwananchi kuhusu huduma hospitalini hapo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Bibi. Agness Mtawa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Hospitalini hapo Aminiel Aligaesha.

  Picha na: Frank Shija, MAELEZO.

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru ametoa ufafanuzi kuhusu habari iliyoandikwa katika gazeti la Mwanchi la tarehe 21 Juni 2016 zilizo kuwa zinasema kuwa wagonjwa wa Seli Mundu wanalipishwa ili kupata huduma ya matibabu yao tofauti ilivyokuwa awali.

  Akitoa ufafanuzi huo Profesa Mseru amesema kuwa kwa habari hizo siyo za kweli kwani wagonjwa wa Seli Mundu wanatumia utaratibu wa kawaida ambapo mgonjwa utibiwa katika maeneo wanayotoka na anapaswa kuchangia gharama za matibabu isipokuwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

  Aliongeza kuwa hapo awali kulikuwa na mradi wa utafiti wa Seli Mundu ulioenda sambamba na utoaji wa matibabu kwa wagonjwa waliojumuishwa katika mradi huo uliodumu kwa muda wa miaka 10 hadi ulipofikia ukomo machi 30 mwaka huu.

  Baada ya mradi huo kumalizika wagonjwa wote walirejea katika maeneo yao ambapo huko wanaendelea na matibabu kupitia utaratibu wa kawaida huduma za matibabu.

  0 0

  Mkurugenzi wa Sheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Onorius Njole akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Mpango Maalum wa kutoa huduma ya hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi maarufu kama Informal Sector Scheme ambayo inajumuisha waendesha bodaboda, bajaji na mama lishe. Kulia ni Mkuu wa Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde.
  Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde akiwaeleza waandishi wa habari juhudi za Serikali katika kuboresha na kupanua wigo wa huduma za hifadhi ya jamii hasa kwa wananchi walio kwenye sekta isiyo rasmi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Sheria kutoka SSRA, Bw. Onorius Njole. Mkurugenzi wa Sheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Onorius Njole akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Program maalum ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Waratibu wa Mifuko ya Bima ya Afya ya Jamii nchini kote. Zoezi hilo linaenda sambamba na usajili wa mifuko hiyo. Kulia ni Mkuu wa Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde na kushoto ni Afisa Uhusiano Ally Masaninga.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa SSRA uliofanyika leo jijini Dar es Salaam ambao ulilenga kuufahamisha umma maboresho mbalimbali katika sekta ya hifadhi ya jamii nchini.

  Na Fatma Salum (MAELEZO)

  Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) imejizatiti kupanua wigo na kuboresha huduma za hifadhi ya jamii hasa kwa kundi la watu walio kwenye sekta isiyo rasmi.

  Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Sheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Onorius Njole wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Mpango Maalum wa kutoa huduma ya hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi maarufu kama Informal Sector Scheme ambayo inajumuisha waendesha bodaboda, bajaji na mama lishe.

  Bw. Njole alisema kuwa katika kuhakikisha watanzania wote wananufaika na huduma za hifadhi ya jamii, SSRA inafanya tafiti mbalimbali na kuhamasisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kubuni mafao mbalimbali yanayolenga kuwafikia wananchi wote walio kwenye sekta isiyo rasmi.

  Ili kufanikisha hilo, mwaka 2015 SSRA ilifanya utafiti katika sekta ya usafirishaji na kubaini kuwa asilimia 83 ya waendesha vyombo vya usafiri mijini wakiwemo waendesha bodaboda wako tayari kuchangia kwa hiari katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

  “Kutokana na matokeo hayo mamlaka ilipendekeza kuanzishwa kwa Mpango Maalum ujulikanao kama Informal Sector Scheme ambapo watu waliojiajiri kwenye sekta isiyo rasmi watapata nafasi ya kunufaika na huduma ya hifadhi ya jamii.” Alisema Njole.Njole aliongeza kuwa tayari baadhi ya mifuko imekwishaandaa mafao maalum yanayowalenga waendesha bodaboda, bajaji, daladala na mama lishe ambao watapata fursa ya kuchangia kiasi kidogo kila siku kulingana na kipato chao ili kupata huduma za hifadhi ya jamii kama vile akiba ya uzeeni, matibabu na mikopo.

  Aidha, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde alieleza kuwa mamlaka hiyo inaendelea na zoezi la kutambua na kusajili Mifuko yote ya Bima ya Afya ya Jamii (CHFs) kwa lengo la kuboresha huduma na kuimarisha mfumo wa utoaji huduma za afya kwa wananchi.

  Pia Bi. Sarah alisema kuwa SSRA imeandaa program maalum kwa ajili ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa Wakurugenzi wa Halmashauri na Waratibu wa Mifuko ya Bima ya Afya ya Jamii nchini kote na zoezi hilo linaenda sambamba na usajili wa mifuko hiyo kwa mujibu wa Sheria ya SSRA, Sura ya 135.

  “Program hii imeanzia Kanda ya Kati ambako ilihusisha Wilaya 27 na jumla ya CHF 5 zilisajiliwa na nyingine 22 zinakamilisha taratibu za usajili. Zoezi hili linatarajiwa kuendelea Juni 22 kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambako jumla ya CHF 25 zinatarajiwa kusajiliwa.”

  Sambamba na program hiyo Serikali kupitia Wizara ya Afya na Wizara yenye dhamana ya masuala ya hifadhi ya jamii na SSRA inafanya mapitio ya mfumo wa usimamizi wa Mifuko ya Bima ya Afya ya Jamii (CHF) ili kupata mfumo utakaoweza kutoa huduma ya afya kwa watanzania wote.

  0 0  0 0


  Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa umma wa Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni muendelezo wa ziara zake katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.
  Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na Menejimenti ya Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 Mkoani Kilimanjaro. Mhe. Kairuki amesisitiza Maafisa Rasilimaliwatu wafanye kazi kwa weledi na watakaoshindwa hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao.
  Baadhi ya Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 Mkoani Kilimanjaro.

  0 0

  Rais wa kikundi cha Upendo Women's Group ambaye pia ndiye mwenyekiti cha kikundi hicho Mh:Theresia Greca,ametoa shukrani za dhati kabisa kwa Rais mstaafu wa Tanzania Mh: Benjamin William Mkapa kwa kuwachangia kikundi chao,Shukrani za pekee kwa Kaimu Balozi wa Tanzania Mrs Agnes Kayola na Ubalozi mzima kwa mchango wao mkubwa wa kufanikisha zoezi zima la ufanikishaji wa fedha za kuisaidia hospital ya Mwananyamala nchini Tanzania.{picha na maelezo toka Maganga One Blog} 
  Pichani wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali waliohudhuria sherehe za uchangishaji wa fedha kwa ajili ya hospitali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam.Shukrani zinatolewa na wana Upendo Women's Group kwa ufanikishaji wa zoezi zima 
  Baadhi ya Viongozi na wanachama wa Upendo Women's Group,kina mama wenye makazi yao nchini Ubegiji wametoa shukrani zao za dhati kabisaa kwa kila mmoja alishiriki vyema katika kufanikisha shughuli yao ya uchangishaji wa fedha kwa ajili ya kuisadia hospitali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.Wana Upendo wanapeleka shukrani zao kwa Rais Mstaafu Mh:Benjamin William Mkapa kwa kujitolea mchango wake,Bila kusahau shukrani zao kwa Kaimu Balozi wa Tanzania Mrs Agnes Kayola na Ubalozi mzima wa Tanzania nchini Ubelgiji.Wanatoa shukrani kwa vikundi mbalimbali vya maonyesho na kila mmoja aliyefanikisha zoezi zima. 
  Katika kuchangisha fedha ili kusaidia hospitali ya Mwananyamala nchini Tanzania, Upendo Women's Group waliaanda maonyesho mbalimbali ikiwemo na maonyesho ya mavazi.
  Afisa Ubalozi Mr.Shayo {kushoto} pia nae alishiriki katika sherehe hizi fupi za uchangishaji wa pesa wa kuisaidia hospital ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam.Wana Upendo Group wanatoa shukrani zao za dhati kwa ushiriki na mchango wao mkubwa waliojitolea wa maafisa ubalozi wa Tanzania katika kufanikisha zoezi zima. 
  Mmoja wa wageni ambaye siku hiyo alinunua bidhaa nyingi kutoka Tanzania ikiwa ni moja ya kuchangia wakina wa Upendo Women's Group ambao walifanya sherehe ya mfuko wa uchangishiaji hospital ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania,kina mama wa Upendo wanatoa shukrani zao za dhati kwa kila mmoja aliyewezesha ufanikishaji wa Harambee hiyo.
  Mmoja wa wageni waalikwa ambaye alichangia Harambee siku hiyo kwa kununua Kahawa halisi kutoka Tanzania.Wana Upendo wanatoa shukrani zao za dhati kwa ushiriki wa wageni hao.
  Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mrs Agnes Kayola akielezea ushiriki wa serikali katika kuisaidia jamii na wananchi wake katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya.Kaimu huyo alikisifia kikundi cha kinamama wa Upendo Women's Group cha nchini Ubelgiji kwa jitihada wanazofanya kuisaidia hosptali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam. Wana Upendo Women's Group wanatoa shukrani zao za dhati kwa msaada waliopata kutoka kwa kaimu Balozi Mrs Agnes Kayola na Ubalozi mzima kwa ushiriki wao,shukrani zingine kwa Rais mstaafu Mh:Benjamin William Mkapa kwa mchango wake wa kukisaidia kikundi. 

  Baadhi ya wageni waliohudhuria sherehe za umoja wa kikundi cha kina mama wenye makazi nchini Ubelgiji kijulikanacho kwa jina la Upendo Women's Group.Kina mama wa Upendo wanatoa shukrani kwa kina mmoja aliyeshiriki katika hafla yao ya uchangishaji wa fedha za kuisadia hospitali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania,sherehe hizi zilifanyika nchini Ubelgiji. 
  Dr.Pendo Maro ambaye ndiye alikuwa mshehereshaji wa hafla ya uchangishaji wa fedha kwa kikundi cha kina mama cha Upendo Women's Group nchini Ublgiji akifungua uchangishaji wa sherehe hizo

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa kufungua Mafunzo ya siku tatu ya Wanawake Wajasiriamali yalioandaliwa na Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani, Dar es Salaam.(PICHA NA OMR).
  Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mhe. Mama Anna Mkapa akihutubia kwenye ufunguzi wa mafunzo kwa wanawake wajasiriamali ambapo mgeni Rasmi wa ufunguzi huo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 

  Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Ndugu Steven Martin akielezea kwa ufupi mafanikio ya mafunzo ambayo yametimiza miaka 19. 

  Sehemu ya wakina ama waliohudhuria ufunguzi wa Mafunzo ya Wanawake Wajasiriamali kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani,Dar Es Salaam. 

  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Esther Mkwizu akizungumza na wajumbe walihudhuria mara baada ya unfunguzi rasmi wa mafunzo kufanyika kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani jijini Dar es Salaam. 

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janetth Magufuli ,Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema wakifurahia jambo wakati wa shughuli za ufunguzi wa mafunzo ya wajasiriamali wanawake ,kushoto ni Mwenyekiti wa wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote, Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mama Anna Mkapa. 

  Baadhi ya wakina Mama waliohudhuria wakifuatilia kwa makini hotuba za ufunguzi wa mafunzo ya wanawake wajasiriamali. 

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi.Jacline Maleko akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan pamoja na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa mara baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa Wanawake Wajasiriamali yaliofanyika kwenye Bwalo la JKT Mgulani jijini Dar es Salaam.

  0 0  0 0

  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Songea Benson Mpesya akiongea na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na wale wa Ofisi yake leo ikiwa ni utekelezaji wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambapo viongozi na watumishi wanakutana kujadili na kutatua kero mbalimbali.
  Sehemu wa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa kwenye kikao kazi cha kujadili kero na changamoto za utendaji wao ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya utumishi wa umma.Kikao kimefanyika katika ukumbi wa Maliasili uliopo ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo.
  Afisa Utumishi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma Happy Msanga akitoa maelezo kwa mgeni rasmi kuhusu namna ambavyo Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yalivyotelezwa.Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Benson Mpesya na kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa Joel Mbewa.
   
  Serikali imewataka watumishi wa umma mkoani Ruvuma kutimiza kikamilifu wajibu wao ndipo wadai haki wanazostahili

  Rai hiyo imetolewa leo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya wakati alipozungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na wilaya ya Songea kwenye ukumbi wa Maliasili mjini Songea .Ameyasema haya ikiwa ni utekelezaji wa maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma ambapo viongozi na watendaji wakuu wa taasisi za umma wanakutana na watumishi wao kusikiliza kero na changamoto zinazokwamisha utendaji kazi

  Mpesya amewataka watumishi wa serikali kutafakari kwa makini majukumu yao na huduma yao kwa umma kama inakidhi viwango vinavyotakiwa na wananchi na hivyo kustahili malipo.Aliongeza kusema watumishi wanao wajibu kwa umma wa kuwahudumia kwa weledi,wakati na bila ubaguzi wa dini au kabila au eneo analotoka mtu

  Amekemea tabia ya baadhi ya watumishi wa serikali kudai haki na marupurupu bila kutimiza wajibu wao.Kila mtumishi anatakiwa kujua wajibu wake ndani ya ofisi anayoifanyia na ndipo haki zake zitafuata kwa mujibu wa sheria ,kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

  “Mnatakiwa kutambua kuwa ninyi watumishi wa serikali ni watoa huduma mlioajiliwa na wananchi wa Tanzania hivyo muwaheshimu na kuwathamni” alisema Mpesya.Amewonya watumishi wa umma kutokufanya kazi kama wanaharakati na walalamikaji badala yake watumie taaluma zao kutekeleza kazi zao

  “Taifa letu linakwenda pabaya kwani tumekuwa na watumishi wa umma wanaofanya kazi ya kuorodhesha kero na changamoto badala ya kusaidia kutatua na kuwahudumia wananchi kuyafikia maendeleo wanayoyahitaji” alisema Mpesya.Hivyo amesisitiza watumishi wote kutumia weledi wa taaluma zao na kujiamini wakati wote wanapotekelza kazi zao huku wakiacha tabia ya kuwasumbua wananchi kwa kuwaeleza njoo kesho 

  Pamoja na changamoto wanazokutana nazo watumishi wa umma Mpesya amewetakawa kuwa wakweli na kuepuka lugha ya njoo kesho ambazo ni lugha za kisiasa.
   

  0 0


  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bw. Aminiel Aligaesha akizungumza na waandishi wa habari LEO kuhusu hospitali hiyo kuanza kuboresha huduma ya chakula kwa wagonjwa (special diet) wanaolazwa MNH kuanzia Julai Mosi, mwaka huu.Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agness Mtawa akifafanua jambo LEO katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu hospitali hiyo kuanza kuboresha huduma ya chakula kwa wagonjwa. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Aminiel Aligaesha akiwa kwenye mkutano huo.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa MNH, Aligaesha akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari LEO jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo hicho LEO katika hospitali hiyo.


  Yawaondolea usumbufu ndugu wa wagonjwa kupeleka chakula mara tatu kwa siku .

  · Ndugu watapata muda wa kuendelea na shughuli za uzalishaji
  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeboresha huduma za chakula kwa wagonjwa wote watakaolazwa kuanzia Julai Mosi, mwaka huu ili kuwaondolea ndugu wa wagonjwa usumbufu na gharama za usafiri wakati wa wanapokwenda kuwaona ndugu zao waliolazwa mara tatu kwa siku katika hospitali hiyo.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar Es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw. Aminiel Aligaesha amesema hospitali imeingia ubia na mzabuni ili kutoa huduma hiyo kwa wagonjwa wote wanaolazwa.

  Bw. Aligaesha amesema Hospitali inataka kujikita katika majukumu yake ya msingi ambayo ni kushauri, kuchunguza na kutibu.

  “Aidha Hospitali inataka kuwaondelea adha ndugu wa wagonjwa ambao wamekuwa wakiingia gharama kubwa hususani usafiri wa kuja Hospitalini mara tatu kwa siku, ambapo kwa kukadiria gharama ya usafiri wa ndugu mmoja wa mgonjwa ni kati ya shilingi 6,000/= na 10,000/= kwa siku, kulingana na mahali anapotokea bila kujumuisha gharama za kuandaa chakula cha mgonjwa ambacho mara nyingi ni chakula maalumu. Na kama mgonjwa akilazwa zaidi ya siku tano hadi 10 ndugu mmoja wa mgonjwa gharama atalipia fedha nyingi kwenye usafiri” amesema Bw. Aligaesha

  Ameongeza kuwa adha ya pili wanayopata ndugu ni usumbufu ambapo inabidi kuacha shughuli nyingine za uzalishaji ili kuja kuleta chakula mara tatu kwa siku, hivyo kuingiliana na shughuli zao za kiuchumi na kimandeleo na kushindwa kuzalisha. Hivyo jukumu hili linachukuliwa na Hospitali kuwaondolea adha hii.
  ·
  “Pia kuna baadhi ya ndugu wamekuwa wakishindwa kuwaletea chakula wagonjwa wao hivyo hospitali ililazimika kuwapatia chakula ambacho kilikuwa kwa ajili ya wagonjwa wanaotoka mikoani wasio na ndugu hapa Dar Es Salaam” amesisitiza Bw. Aligaesha.

  Amesema kumekuwepo na ongezeko la msongamano wa watu ndani ya Hospitali toka asubuhi saa 12 mpaka saa 12 jioni, suala linaloingiliana na utoaji huduma hasa saa za mchana kwani muda wa saa 6.00 hadi saa 8.00 mchana ulikuwa unaingiliana na majukumu ya kiutendaji ambapo majopo mbalimbali ya watalaamu yamekuwa yakiendelea na raundi za wagonjwa waliolazwa. Hii wakati mwingine imesababisha mgonjwa kutokupata huduma stahiki kutokana na muingiliano huu.
  ·
  “Vile vile msongamano huu ni changamoto kwa ajili ya masuala ya kiusalama ambapo kati ya watu wanaoingia Hospitali kwa kigezo cha kuja kuona wagonjwa kuna wanaoingia kwa lengo la kufanya uhalifu ikiwemo wizi wa mali za Hospitali, magari pamoja na vifaa vya magari” alisisitiza.

  Amesema kwa kufanya hivyo, Hospitali itapunguza baadhi ya gharama za uagizaji wa vyakula kwa wazabuni, kulinda upotevu na baadhi ya vyakula kuharibika wakati mwingine kwani utunzaji wa vyakula una mahitaji makubwa. Bw. Aligaesha amesema Hospitali inakusudia kutoa chakula chenye ubora na viwango vinavyotakiwa kwa wagonjwa ikiwemo kutoa chakula maalumu (special diet) kwa wagonjwa wenye uhitaji huo.  Kuhusu utaratibu huo Bw. Aligaesha amesema Mzabuni ndiye atakayepika chakula kwa wagonjwa wote waliolazwa na atatayarisha, atakipeleka na kukikabidhi katika wodi husika ambapo jukumu la kumpa mgonjwa kifungua kinywa, chakula cha mchana na jioni linabaki wa Hospitali.

  Amesema wagonjwa watapatiwa milo mitatu kwa siku yaani asubuhi, mchana na jioni kazi itakayofanywa na muuguzi wa zamu ambaye atahakikisha wagonjwa wote wamepata chakula kufuatana na mahitaji (diet list) iliyowasilishwa jikoni kutokana na mahitaji yao ya kiafya.

  Kutokana na uamuzi huu, utaratibu wa ndugu kuleta chakula kwa wagonjwa waliolazwa wakati wa mchana umefutwa na hivyo mchana hatutakuwa na nafasi ya ndugu kuja kutembelea wagonjwa. Muda wa kutembelea wagonjwa utakuwa asubuhi saa 12 hadi saa moja kamili na saa 10:00 jioni hadi saa 12:00jioni ndipo ndugu wataruhusiwa kuingia ndani kuwaona ndugu zao waliolazwa. Katika muda huo ndugu ataruhusiwa kuja na chakula chochote anachofikiri atamuongezea mgonjwa wake kama matunda n.k

  Bw. Aligaesha amesema mgonjwa aliyelazwa atachangia kiasi cha shilingi 50,000 atakapolazwa ambapo kati ya hizo, shilingi elfu 10,000 itakuwa ni gharama ya kumuona daktari (Consultation), shilingi elfu 10,000 ikiwa ni gharama ya kulazwa na bei ya chakula itakuwa shilingi elfu 30,000 sawa na shilingi elfu 6,000 kwa siku. Wastani wa mgonjwa kukaa wodini ni siku tano. Gharama hizo zinahusika kwa muda wote atakaokuwa amelazwa.

  Kwa sasa Hospitali inatoa chakula kwa wagonjwa 650 ambao wamepata rufaa kutoka hospitali za nje ya mkoa wa Dar es Salaam kwa gharama wastani wa shilingi 1.8 bilioni kwa mwaka, sawa na shilingi 150 milioni kwa mwezi kwa vyakula pamoja na gharama nyingine kama vile za nishati. Takribani wagonjwa kati ya 600 na 700 ambao rufaa zao ni kutoka Hospitali za Dar es Salaam walikuwa hawapati chakula kutoka Hospitalini, na ilibidi ndugu zao wawaletee chakula. Hata hivyo, Hospitali ilikuwa inawapatia chakula tu kama ndugu zao wakishindwa kufanya hivyo.

  “Uongozi wa Hospitali unaamini kwamba mabadiliko haya hayatamuongezea mgonjwa gharama, bali yatampunguzia gharama pamoja na ile adha kama ilivyoainishwa hapo juu. Aidha, uongozi unaamini kwamba uamuzi huu unaendana na azma nzima ya kuboresha utoaji huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuboresha mazingira ya Hospitali. Tunaomba ushirikiano wenu katika kutekeleza jukumu hili ili kusudi wagonjwa waweze kuhudumiwa vizuri zaidi” amesisitiza Bw. Aligaesha.

  0 0

  Waziri Mwakyembe.
   
  Na: Frank Mvungi – MAELEZO- Dodoma

  Vyombo vya Habari nchini Vimetakiwa kuzingatia weledi katika kutimiza majukumu yake ili kusaidia Taifa kufikia maendelo ya kweli na endelevu.

  Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa mkutano na vyombo vya habari. Akifafanua Mhe. Mwakyembe amesema ili Taifa liwe na Maendeleo ni lazima kuwa na Vyombo vya Habari vinavyozingatia weledi wa taaluma ya uandishi wa habari pamoja na Sheria na Kanuni zinazosimamia tasnia hiyo.

  “Navipongeza Vyombo vingi vya Habari hapa nchini ambavyo vinafanya kazi nzuri ya kuelemisha Umma na kuchochea maendeleo ya nchi yetu ila kuna wachache ambao kwa makusudi wameamua kupotosha Umma” alisisistiza Dkt. Mwakyembe

  Hivi Karibuni gazeti moja lilitoa taarifa zinapotosha Umma kwa kumhusisha Waziri huyo na maswala ya Ufisadi ambapo alitumia fursa hiyo kuviasa vyombo vya habari kuepuka kuandika au kusambaza habari ambazo ni za upotoshaji na hazina maslahi kwa Taifa na hazijafanyiwa uchunguzi wa kina.

  Akitolea mfano chombo hicho cha habari Mwakyembe amesema kuwa, kimekuwa kikiripoti taarifa zinazogusa masuaa ya Ulinzi na Usalama pasipo kuangalia maslahi ya Taifa kwanza hali inayoonyesha kukosekana kwa uzalendo. Mwakyembe aliongeza kuwa tasnia ya habari imekuwa na ni vema sasa waandishi wote kuzingatia maadili ya taaluma hiyo ili kuepuka kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa kukiuka sheria na kanuni za uandishi wa habari.

  Tasnia ya Habari ni muhimili muhimu katika kuchochea Maendelo ya Taifa lolote lile kwa kuelimisha kuhamasisha na kuamsha ari ya wananchi kujiletea maendeleo.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

  Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) chini ya mkakati wa kukuza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya ujenzi Tanzania (CoST -Tanzania) limepanga kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika sekta hiyo ili kuondokana rushwa na kuhakikisha wananchi wanaelewa thamani halisi ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya umma.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho wakati wa ufunguzi wa mkutano uliowashirikisha wadau wa ujenzi kutoka nchi mbalimbali Duniani kujadili changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

  Dkt. Leonard Chamuriho amesema kuwa kikao hicho kina lengo la kuweka uwazi katika miradi yote inayotekelezwa kwa fedha za wananchi ili kuondokana na rushwa zinazojitokeza katika kufanikisha miradi hiyo.

  “Rushwa inazungumziwa sana katika suala la ujenzi ila naomba tuzidishe uwazi katika sekta hii na kuwafanya wananchi waelewe kinachoendelea katika miradi yao hii itatutasaidia sana kupambana na rushwa, na taswira ya kuwa na rushwa katika miradi ya ujenzi haitakuwepo”,alisema Dkt. Chamuriho.

  Dkt. Chamuriho ameongeza kuwa msimamo wa Serikali ni kuhakikisha thamani ya fedha inazingatiwa katika miradi ya ujenzi na kuwepo kwa uwazi na uwajibikaji Kutasaidia kuondokana kabisa na suala la rushwa.

  Aidha, Dkt. Chamuriho amewashukuru wadau wa maendeleo wakiwemo Idara ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID), Benki ya Dunia (WB) pamoja na Serikali ya Uholanzi wanaoendelea kusaidia miradi ya ujenzi iliyo chini ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) na kutoa rai kwa wadau wengine wa maendeleo kuendelea kusaidia katika miradi mingine ya maendeleo.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa CoST -Tanzania, Kazungu Magili amesema kuwa changamoto kubwa iliyokuwepo ni kuifanya CoST-Tanzania kujitegemea kwa kutosimamiwa na taasisi yoyote na kupitia mazungumzo yaliyofanywa kati ya CoST na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ana imani kuwa yataweza kufikia muafaka na kuifanya kuwa sekta inayojitegemea kabla ya mwezi Julai mwaka 2016.

  0 0


   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia), akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Nchini (TEMESA) Eng. Le- Kujan Manase wakati alipokagua mradi wa ukarabati wa ujenzi wa vivuko vitatu jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng. Le- Kujan Manase akitoa maelezo ya moja ya kifaa kinachotumika kwenye kivuko cha MV Magogoni kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kulia Profesa Makame Mbarawa  wakati alipokagua mradi huo.
  Muonekano wa Kivuko cha MV. Magogoni kikiwa kwenye hatua za mwisho za matengezo yanayofanywa na kampuni ya M/S Songoro Marine Transport Courtyard ya Mwanza na TEMESA Jijini Dar es salaam.
  Picha zote na Benjamin Sawe- Maelezo

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amekagua ukarabati na Ujenzi wa Vivuko vya MV. Magogoni na MV. Pangani na kuwataka wajenzi wa vivuko hivyo kuhakikisha vinakamilika kwa wakati.


  Akizungumza mara baada ya kuvikagua Vivuko vya Old MV- Magogoni na Ujenzi wa vivuko vipya vya Pangani na New Magogoni, Prof. Mbarawa ameelezea kuridhishwa kwake na hatua za ujenzi zilizofikiwa na kusisitiza kuwa upo umuhimu wa kazi hizo kufanywa hapa hapa nchini badala ya kupelekwa nje ya nchi.


  “Hakikisheni mnaongeza nguvu na wataalam ili kazi zote za vivuko na ujenzi wa boti za kuongozea Meli (Tag), zifanyike hapa hapa nchini na hivyo  kuokoa fedha nyingi zinazotumika kila mwaka kwa Tug zote saba kukarabatiwa nje ya nchi ”, Amesema Prof. Mbarawa.


  Ameitaka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kutenga na kujenga eneo maalum litakalotumika kufanyia ukarabati wa vivuko, matishali na boti za kuongozea Meli ili kuboresha huduma ya ufundi katika vyombo vya majini.

  “lazima kuwe na mkakati wa kuokoa takribani dola Milioni mbili nukta tano zinazotumika kwaajili ya ukarabati wa Tag zetu kila mwaka”, Amesisitiza Prof. Mbarawa.


  Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Nchini (TEMESA), Eng. Le- Kujan Manase amemweleza Prof. Mbarawa kuwa kazi zote za ukarabati wa vyuma na umeme zinafanywa na Mkandarasi kampuni ya M/S Songoro Marine Transport Courtyard ya Mwanza na matengenezo ya Injini na mitambo ya kuendeshea Kivuko yanafanywa na mafundi wa TEMESA na kazi zote zinatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwezi wa nane.


  Kukamilika kwa kivuko cha Old Magogoni na Vivuko vipya viwili vya Pangani na New Magogoni kutaiwezesha TEMESA kuwa na vivuko 30 vinavyotoa huduma hapa nchini na hivyo kuboresha huduma hiyo katika maeneo mengi.


  Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amewataka wenye malori yanayoengeshwa pembeni ya barabara ya kuiingilia Bandarini kutafuta mahali pengine pa kuegesha magari hayo ili kuondoa usumbufu kwa wasafirishaji wanaoingia na kutoka bandarini.


  Kivuko kipaya cha Pangani kinatarajiwa kukamilika mwezi septemba na kile kipya cha Magogoni mwezi Oktoba mwaka huu.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. 

  0 0

  Meneja wa bank ya CRDB tawi la Usa River wilayani Arumeru mkoani arusha akimlisha keki moja ya mtoto alieshiriki katika maadhimisho ya siku ya mtoto Africa iliyoandaliwa na bank hiyo katika viwanja vya Usa River Academy.
  Watoto wakishandana kukimbia katika siku ya mtoto wa Africa iliyoandaliwa na bank ya CRDB tawi la Usa River wilaya ya Arumeru mkoania Arusha katika viwanja vya usa river academy.
  Watoto wakishandana kukimbiza kuku katika michezo iliyoandaliwa na bank ya CRDB tawi la Usa River wilayani Arumeru mkoani Arusha hivi karbuni katika michezo ya kuazimisha siku ya mtoto wa Africa iliyofanyika katika viwanja vya shule ya Usa River Academy.
  Watoto wakishandana kukimbia na magunia katika siku ya mtoto wa Africa iliyoandaliwa na bank ya CRDB tawi la Usa River wilaya ya Arumeru mkoania Arusha katika viwanja vya usa river academy.
   
  Na Woinde Shizza,Arusha

  Benki ya CRDB tawi la Usariver imewahimiza wazazi na walezi kujenga tabia ya kuwaendeleza watoto katika michezo na vipaji walivyonavyo ili viweze kuwaimarisha kiakili na kimwili na kuwanufaisha baadae.

  Meneja wa Tawi hilo Jenipher Tondi ameyasema hayo katika michezo ya watoto iliyoandaliwa na benki hiyo katika viwanja vya USARIVER ACADEMY ambapo watoto walipata fursa ya kucheza michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,netiboli,kukimbiza kuku na mbio za kukimbiza magunia..

  Amesema kuwa wazazi hawana budi kuendeleza vipaji vya watoto kwani vinaweza kuwa na faida kwa familia,jamii na taifa. “wazazi wawape watoto nafasi ya kushiriki katika michezo ili kuweza kuvumbua vipaji vyao vilivyojificha sababu vipaji ni ajira tosha”

  Pia amewakumbusha wazazi kuwawekea watoto akiba ya fedha kwa ajili ya kumsaidia mtoto katika kulipa fedha za ada kwa kufungulia account zisiszo kuwa na riba.
  Kwa upande wao watoto walioshiriki katika michezo hiyo Oscar Damian na Angela John wameishukuru benki hiyo kwa kuwajali na kuwapa nafasi ya kukutana na watoto wenzao ambapo wameweza kuburudika na michezo iliyoandaliwa.

  Jane Nassari amewataka wazazi kujenga utamaduni wa kuwaruhusu watoto wao kushiriki kwenye michezo kwasababu michezo huleta afya ya akili,furaha na mashirikiano.

  Mzazi aliyefika katika siku hiyo Angelina Joseph amesema kuwa mazingira bora ya michezo yanapaswa kujengwa ili watoto wapende michezo na kunufaika nayo kwa kuitumia kama njia ya kujiimarisha kiafya na kiakili.

  0 0


  Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Leah Kihimbi (kushoto) akizungumza na wadau wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho kuhusu mikakati ya kuboresha sekta ya sanaa za Maonesho leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha Bibi. Shani Kitogo na kulia ni Afisa Uchumi kutoka Wizara hiyo Bw. Richard Kundi.Na Anitha Jonas – WHUSM Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Bw. William Chitanda akieleza changamoto za shirikisho kwa watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hawapo pichani) wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya kuboresha sekta ya sanaa za Maonesho leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Bw. Efraim Zakaria kutoka kikundi cha Watoto Arts Organization (WAAO).
  Katibu wa Kikundi cha Binti Leo Bi. Agness Lukanga (katikati) akieleza utendaji wa kikundi chao kwa watendaji wa masuala ya Sanaa na Utamaduni wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya kuboresha sekta ya sanaa za Maonesho leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Sanaa za Maonesho Tanzania Bw. Nkwama Ballanga. 


  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 887 | 888 | (Page 889) | 890 | 891 | .... | 1898 | newer