Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

Mkapa awataka watanzania kufanya kazi kwa bidii.

$
0
0
Rais Mstaafu awamu ya tatu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Benjamin William Mkapa akikata utepe kuzindua kitabu cha kitabu cha uchumi wa kisiasa wa madiliko ya Tanzania kijulikanacho kama (political economy of change in Tanzania) ambacho kina lengo la kukuza uchumi na siasa nchini wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa nane wa kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika jijini Dar es salaam kushoto ni Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Prof. Rwekaza Mukandala. 
Mwenyekiti wa Kitaifa wa chama cha ACT wazalendo Bi. Anna Mghwira akichangia hoja wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa nane wa kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika jijini Dar es salaam.
Viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais Mstaafu awamu ya tatu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Benjamin William Mkapa hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa nane wa kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika jijini Dar es salaam.Picha na Ally Daud-Maelezo

Na Ally Daud- Maelezo 

Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamin William Mkapa amewataka watanzania kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano kwa kufanya kazi kwa bidii na kupunguza lawama ili kuonyesha uzalendo aliouacha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 

Rais Huyo Mstaafu ameyasema hayo katika mkutano wa nane wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere ambao umefanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu Cha Dar es salaam na kuongeza kuwa watanzania wengi wamekua na desturi ya kutumia muda mwingi Katika kuilaumu serikali baada ya kufanya kazi kwa maendeleo ya nchi. 

"Watanzania tunatakiwa tufanye kazi kwa bidii ili tuifikishe nchi yetu Kwenye maendeleo na si kutumia muda mwingi Katika kuilaumu serikali " alisema Dkt Mkapa. 

Aidha Dkt. Mkapa amesema kuwa ili uzalendo uwepo tunatakiwa kutumia vizuri uhuru wa kuongea Katika kuleta maendeleo na si kuleta uchochezi Katika nchi na kusababisha uvunjifu wa amani ambayo ameiacha Mwal. J.k nyerere. Mbali na mkutano huo pia kulikua na uzinduzi wa kitabu cha uchumi wa kisiasa wa madiliko ya Tanzania kijulikanacho kama (political economy of change in Tanzania) ambacho kina lengo la kukuza uchumi na siasa nchini. 

Mkutano huo wenye lengo la kudumisha uzalendo na kukuza uchumi nchini umeudhuriwa na wawakilishi Mbali Mbali wa kitaifa na kimataifa wakiwemo baadhi ya mabalozi na wanazuoni kutoka ndan na nje ya nchi. 

Kwa upande wa Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Prof. Rwekaza Mukandala alisema kuwa mkutano huo unalenga kudumisha na kuendeleza aliyoyaacha Baba wa Taifa Hayati Mwl. J.k Nyerere.Mbali na hayo amewataka vijana na watanzania kwa ujumla kumuenzi kwa kufanya kazi kwa bidii ili kujikwamua kiuchumi na kuendeleza ujamaa aliouacha Mwalimu.

ZIARA YA SERIKALI YA JIMBO LA PUNTLAND-SOMALIA NCHINI TANZANIA

$
0
0

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akifafanua jambo wakati wa kikao na ujumbe kutoka Serikali ya Jimbo la Puntland -Somalia walipoitembelea Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo. Kulia kwake ni Waziri wa Kazi, Vijana na Michezo wa Serikali ya Jimbo la Puntland – Somalia, Mhe. Abdirahman A. Abdulle.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akiukaribisha ujumbe kutoka Serikali ya Jimbo la Puntland - Somalia, ulipoitembelea Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo. Kulia kwake ni Waziri wa Kazi, Vijana na Michezo wa Serikali ya Jimbo la Puntland – Somalia, Mhe. Abdirahman A. Abdulle akiwa na Maafisa alioambatana nao.
Waziri wa Kazi, Vijana na Michezo wa Serikali ya Jimbo la Puntland –Somalia, Mhe. Abdirahman A. Abdulle akizungumzia lengo la Serikali yake kuitembelea Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo. Kulia kwake ni Maafisa aliombatana nao.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Henry Mambo akieleza namna Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kitakavyoshirikiana na Serikali ya Jimbo la Puntland – Somalia katika kuijengea uwezo Sekta ya Umma ya Serikali hiyo.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akibadilishana kadi za mawasiliano na baadhi ya Maafisa kutoka Serikali ya Jimbo la Puntland - Somalia mara baada ya hafla fupi ya kuwakaribisha katika Ofisi ya Rais-Utumishi iliyofanyika mapema leo.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Serikali ya Jimbo la Puntland -Somalia walipoitembelea Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.

MANISPAA YA KINONDONI YASAINI MKATABA WA KUTENGENEZA MADAWATI NA MAKAMPUNI TISA TOFAUTI

MWENYEKITI WA BODI YA WADHAMINI YA MFUKO WA PENSHENI PPF AKABIDHI VYETI KWA WAFANYAKAZI BORA WA MWAKA 2015/16

$
0
0

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhani Khijjah, akizungumza na baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko huo wakati wa zoezi la kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha Mikutano Dar es Salaam, (DCC). Tukio hilo lilifanyika wakati wa Kikao cha Baraza la wafanyakazi. Picha na Mafoto Blog.
 
************************************

Akizungumza baada ya kukabidhi Vyeti hivyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Ndugu Khijjah, aliwapongeza Wafanyakazi bora wa 2015/16 wa Mfuko huo kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini na kuwataka Wafanyakazi wote wa PPF kufanya kazi kwa bidii bila kurudi nyuma ili kuendelea kutimiza malengo.

Katika Kikao hicho jumla ya Wafanyakazi 22, kutoka Kurugenzi na Idara mbalimbali walikabidhiwa vyeti vya Wafanyakazi Bora na Mwenyekiti huyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa William Erio, akizungumza na kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16, iliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano Dar es Salaam, (DCC) jijini, leo Juni 14, 2016.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Julius Mganga, akizungumza wakati wa Kikao hicho.

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa Mfanyakazi Bora katika Kurugenzi ya Uwekezaji, Agustine Paul, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa Mfanyakazi Bora katika Kurugenzi ya Huduma za Sheria, Enelia Majo, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.

Baadhi ya Wakurugenzi na Wafanyakazi wa Mfuko huo wakimsikiliza mgeni rasmi wakati akihutubia katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kutoa Vyeti kwa wafanyakazi bora wa mwaka 2015/16.


Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa hafla ya utoaji Vyeti kwa Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha Mikutano cha Dar es Salaam (DCC).
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na utoaji Vyeti kwa wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha Mikutano cha Dar es Salaam (DCC).

Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na Vyeti kwa Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha Mikutano cha Dar es Salaam (DCC).
Wafanyakazi bora wakisubiri kupokea Vyeti vyao
Wafanyakazi bora wakisubiri kupokea Vyeti vyao
Wafanyakazi bora wakisubiri kupokea Vyeti vyao
Wafanyakazi bora wakisubiri kupokea Vyeti vyao. Kulia ni Meneja Rasilimali Watu Adolar Duwe
Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti mfanyakazi bora wa Kurugenzi ya Uendeshaji, Mary Myamba, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti kwa Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC). Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti mshindi wa Kanda ya Mashariki na Kati katika Kurugenzi ya Uendeshaji, David Ngamesha, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC). Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa mshindi wa Kanda ya Ziwa katika Kurugenzi ya Uendeshaji, Evarist Ikwalala, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.
Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa mshindi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini katika Kurugenzi ya Uendeshaji, Godwin A. Godwin, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa mshindi wa Kanda ya Kusini katika Kurugenzi ya Uendeshaji, Shida Michael, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa mshindi wa Kanda ya Kaskazini katika Kurugenzi ya Uendeshaji, Emmanuel Tarimo, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa mshindi wa Kanda ya Ilala katika Kurugenzi ya Uendeshaji, Godlisten Gilliard, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.
Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa mshindi wa Kanda ya Kinondoni katika Kurugenzi ya Uendeshaji, Phillipo Kimario, wakati wa Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.
Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa mshindi wa Kanda ya Temeke katika Kurugenzi ya Uendeshaji, Sosthenes Lyimo, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa mshindi wa pili katika Kurugenzi ya Uhasibu, Witness Patrick, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.
Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa Mfanyakazi Bora katika Kurugenzi ya Uhasibu, Agness Ndesingo, wakati wa Kikaoc cha Barazala Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.
Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa Mfanyakazi Bora katika Kurugenzi ya Ukaguzi wa Ndani, Omar Katundu, aliyepokea kwa niaba ya Kalege Enock, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa Mfanyakazi Bora katika Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu, Julie Mtambo, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa mshindi wa pili katika Kurugenzi ya Mifumo ya Habari, Goodluck Msangi, aliyepokea kwa niaba ya Idd Hamis, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa Mfanyakazi Bora katika Kurugenzi ya Mifumo ya Habari, Baraka Mselemu, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa mshindi wa pili katika Kurugenzi ya Rasilimali Watu na Utawala, Anthony Mkinga, wakati wa Kikao cha Barza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio
Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa Mfanyakazi Bora katika Kurugenzi ya Rasilimali Watu na Utawala, Jacob Msigwa, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa Mfanyakazi Bora katika Kurugenzi ya Menejimenti ya Majanga, Diana Kimaro, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni PPF, Ramadhani Khijjah, akimkabidhi Cheti kwa Mfanyakazi Bora wa Mfuko kwa mwaka 2015/16, Omar Katundu, aliyepokea kwa niaba ya Kalege Enock, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi na kukabidhi Vyeti vya Wafanyakazi bora wa Mfuko huo wa mwaka 2015/16 iliyofanyika leo Juni 14, 2016 kwenye Kituo cha mikutano cha Dar es Salaam (DCC) Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.

Baadhi ya wafanyakazi wakipongezana baada ya kupokea Vyeti vyao.
Baadhi ya wafanyakazi wakipongezana baada ya kupokea tuzo hizo.
Viongozi wa Mfuko huo wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi bora wa mwaka 2015/16.

Picha ya pamoja Viongozi, Wakurugenzi na Wafanyakazi bora.

Picha ya pamoja

MANISPAA YA KINONDONI KUTENGENEZA MADAWATI 28000 KWA POSHO ZA WATENDAJI WAKE.

$
0
0

Meya Manispaa ya Kinondoni, Jacob  Boniface akisaini mkataba  wa kutengeneza madawati na  Mkurugenzi wa Kampuni ya Edosama Hardware,  leo jijini Dar es Salaam. 
 Meya Manispaa ya Kinondoni, Jacob akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  wakati wa kusaini mkataba na wazabuni 10 wa kutengeneza mdawati 28000 leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watu waliokuwa wakishuhudia utiaji saini wa mkataba wa kutengeneza madawati wa shule za msingi na Sekondari katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar  es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imekata posho za watendaji wa idara zake kwa muda wa miezi miwili  na kuweza kupata sh.bilioni 1.8 ambazo zitamaliza tatizo la madawati 28000 kwa shule za msingi na sekondari kwa manispaa ya Kinondoni.

Kuondosha kwa posho hizo kulitokana na manispaa  kubaini kuwa hawana uwezo wa kununua madawati 28000  kwa kukosa bajeti hiyo katika mwaka fedha 2015/2016  na kuona posho za watumishi zitumike kununua madawati hayo.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, wakati wa kusaini mkataba  wa kampuni 10 za kutengeneza madawati  28000, Meya wa Manispaa Kinondoni, Jacob Boniface amesema kuwa kwa kuingia mkataba huo kinondoni inachana na tatizo la madawati.

Jacob amesema kuwa Kinondoni wanafunzi kukaa chini ni aibu kutokana na Halmashauri hiyo kuwa na vyanzo mapato vingi.
Amesema kuwa waliongia mikataba kuhakikisha kufikia juni 30 mwaka huu wazabuni wote kuwa wamekamilisha utengenezaji wa madawati.

Jacob amesema kuwa madawati yanayokusanywa na wadau mbalimbali wanayahitaji kwa ajili kuweka akiba ili yakiharibika kuweza kutumika pale penye upungufu.

Ameasema madawati hayo yanatengenezwa kwa bei ndogo kuliko na awamu zote kwani kwa sasa yanatengenezwa kwa sh.85000, wakati kwa manispaa hiyo ilishatengeneza dawati moja kwa sh.400,000.

KANISA LA THE SILOAM LAKABIDHI HUNDI YA SH.MILIONI 19 KWA MKUU WA WILAYA KINONDONI .

$
0
0

Wakili wa Mungu wa Kanisa la The Pool of Siloam Church, Elisha Eliya akimkabidhi mfano wa hundi ya sh.milioni 19 ya kutengeneza madawati kwa shule za msingi na sekondari za manispaa ya kinondoni, leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya, Ally Hapi akizungumza na waumini wa kanisa la The Pool of Siloam Church ambao wamefika katika viwanja vya manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya kumkabidhi hundi ya sh.milioni 19 ya kutengeneza madawati kwa shule za msingi na sekondari za manispaa ya kinondoni, leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Jacob Boniface
Wakili wa Mungu wa Kanisa la The Pool of Siloam Church, Elisha Eliya akitoa neno la shukrani katika hafla ya kumkabidhi hundi ya sh.milioni 19 ya kutengeneza madawati kwa shule za msingi na sekondari za manispaa ya kinondoni, leo jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya waumini wa kanisa la The Pool of Siloam Church waliofika kushuhudia makabidhiani ya mfano wa hundi ya sh.milioni 19 ya kutengeneza madawati kwa shule za msingi na sekondari za manispaa ya kinondoni, leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii).
 
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi amezitaka Taasisi mbali mbali za Dini kujitolea katika kuchangia madawati ili iweze kukabilina na changamoto za madawati katika wilaya hiyo.

Hapi,ameseyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokabidhiwa hundi ya sh.Milioni 19 kutoka kwenye kanisa la The Pool of Siloam Church kwa ajili ya kusaidia kumaliza tatizo la madawati. Ambapo amesema kitendo cha Kanisa hilo kusaidia tatizo la madawati ni jambo jema ambalo litasaidia kumalizana na changamoto ya madawati huku akitaka taasisi zengine kuiga mfano wa kanisa hilo.

Amesema kwa sasa Wilaya yake inakabilia kumaliza changamoto ya ukosekanaji wa madawati ambapo amedai mpaka kufikia mwisho wa mwezi uwenda tatizo la madawati akatika wilaya hiyo litakuwa limekamilika. Hata hivyo,Hapi amewataka watendaji wa manispaa hiyo kuhakikisha wanazipeleka pesa hizo zilizotolewa kunakohusika na sio sehemu nyengine.

Aliongeza kuwa yeye yuko tayari kuwafuata viongozi wa dini ili waweze kumsaidia katika kampeni ya madawati katika kumaliza tatizo hilo katika halmashauri ya Kinondoni kwa wanafunzi kuachana na kukaa chini ya sakafu. Amesema kanisa kujitoa huko atafikisha salamu kwa Rais Dk.John Pombe Magufuli kutokana na mwitikio wa kutambua umuhimu wa elimu na kukubali kuchangia.

Wakili wa Mungu wa Kanisa la The Pool of Siloam Church, Elisha Eliya amesema kuwa mchango wa fedha hizo kwa ajili ya madawati imetokana na mchango wa waumini wa kanisa hilo kwa kuguswa na madawati

Eliya amesema ataendelea kuchangia katika hatua mbalimbali kutokana nafasi ya kanisa katika jamii hasa katika matatizo mbalimbali.

mahakama yatoa hati ya wito kwa mbunge wa singida mashariki tundu lissu

$
0
0
Habari na Mwene Said wa Blogu ya Jamii, Dar es Salaam.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, yatoa hati ya wito kwa Mbunge Singida Mashariki, Tundu Lissu (48) na mwenzake, wa kwenda kujibu mashtaka ya kula njama na kutoa lugha ya uchochezi kwa watu wa Zanzibar.

Mbali na Lissu mshtakiwa mwingine aliyepewa wito huo ni Mhariri wa Gazeti la Mawio, Jabir Idrissa (52) huku Mhariri wa habari Simon Mkina (44) na Mchapishaji Ismail Mehboob (24) wakisomewa mashtaka hayo mapema jana.Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Wakili wa Serikali Paul Kadushi alidai kuwa kati ya Januari 12 na 14, mwaka huu mahali pasipofahamika jijini Dar es Salaam, washtakiwa walikula njama ya kusambaza taarifa ya uchochezi kupitia gazeti la Mawio lililokuwa na kichwa cha habari cha “Machafuko yaja Zanzibar”.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Januari 14, mwaka huu, jijini Dar es Salaam,washtakiwa wote kwa lengo la kushawishi uchochezi kwa Watanzania Visiwani dhidi ya mamlaka za kisheria za serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Ilidaiwa kuwa walichapisha kwenye gazeti la Mawio toleo namba 182 la Januari 14 hadi 20, 2016 ikiwa na habari ya uchochezi yenye kichwa cha habari kisemacho ‘Machafuko yaja Zanzibar”.

Kadushi alidai katika shtaka la tatu, Januari 13, mwaka huu Jengo la Jamana lililopo Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Mehboob, kwa lengo la kushawishi Watanzania wa Visiwani, dhidi ya mamlaka za kisheria za serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Upande wa huo wa Jamhuri ulidai katika shtaka la nne, Januari 13, mwaka huu katika Jengo la Jamana mshtakiwa Mehboob alichapisha gazeti la Mawio toleo namba 182 bila kuwa na kiapo kutoka kwa msajili wa magazeti.

Shtaka la tano, Januari 14, mwaka huu jijini Dar es Salaam, kwa makusudi na bila kuwa na mamlaka ya kisheria waliwatishia watanzania wa Visiwani, wasijitokeze kwenye Uchaguzi Mkuu wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu.

Ilidaiwa kuwa washtakiwa waliwatishia kwamba uchaguzi huo utasababisha kutokea kwa vita na machafuko utakaosababisha umwagaji wa damu kupitia makala iliyochapishwa na gazeti la Mawio yenye kichwa cha habari “Machafuko yaja Zanzibar”.

Hakimu Simba aliwataka washtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotoka katika taasisi zinazotambulika watakaosaini hati ya dhamana yenye thamani ya Sh. Milioni 10 kila mmoja walitimiza masharti hayo.

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alidai kuwa mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya washtakiwa hayana mashiko ya kisheria mahakama iyafute na kuwaachia huru.Alidai kuwa sheria za magazeti za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bara haziingiliani na Tanzania Visiwani hivyo kesi hiyo haina mashiko ya kisheria.

Wakili Kadushi aliomba muda wa siku saba kwa ajili ya kujibu hoja za utetezi.Hakimu alisema kesi hiyo itasikilizwa majibu ya hoja za Jamhuri Juni 28, mwaka huu na washtakiwa Lissu na Idrissa wafike mahakamani kusikilizwa mashtaka yao.

Article 24


TAZAMA VIJUSO VYA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO

DKT SALIM ATUNUKIWA NISHANI YA KUDUMISHA MAHUSIANO YA KIDIPLOMASIA KATI YA TANZANIA NA CUBA

$
0
0

Balozi wa Cuba Jorge Luis Lopez Tormo (kulia), akimvisha nishani Waziri Mkuu mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim kutokana na kutambua mchango wake katika kudumisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Cuba, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam . (Picha na Francis Dande)
Balozi wa Cuba Jorge Luis Lopez Tormo (kulia), akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu, Salim Ahmed Salim hapo jana kabla ya kuvishwa nishani ya kuutambua mchango wake katika kudumisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Cuba, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.

TAARIFA YA MKUTANO WA KUSIKILIZA MAONI YA WADAU JUU YA MUSWADA WA FEDHA WA MWAKA 2016

$
0
0
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwa mujibu wa Kanuni ya 118 ya Kanuni za Kudumu za Bunge,  Toleo la mwaka 2016, Nyongeza ya Nane, Sehemu ya Tatu  Kifungu cha 9, imepewa jukumu la kusikiliza maoni na mapendekezo ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha kila mwaka. 

Katika kutekeleza jukumu hilo, Kamati ya Bajeti imepanga kufanya Mkutano wa Wadau wote wa masuala ya kodi (Public Hearing) kwa ajili ya kusikiliza maoni yao na mapendekezo kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2016. 

Mkutano huo umepangwa kufanyika siku ya Alhamisi Tarehe 16 Juni 2016 kuanzia Saa Tano asubuhi katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Mkoani Dodoma.
Kwa kuzingatia umuhimu wa Muswada huo, Kamati inawaalika wadau wote kufika na kuwasilisha maoni yao kabla haujapelekwa katika hatua nyingine. Maoni ya wadau yanaweza pia kuwasilishwa kwa njia ya Posta au Barua pepe kwa anuani ifuatayo: 
 
Katibu wa Bunge, Ofisi ya Bunge, S.L.P 941, DODOMA Barua pepe: cna@bunge.go.tz 
Imetolewa na,
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano. Ofisi

RAIS MAGUFULI AANDAA FUTARI YA PAMOJA YA VIONGOZI MBALIMBALI WA DINI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika foleni na wageni wake kwenda kuchukua chakula wakati wa kufuturu katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndg. Ramadhani Madabida akifuatiwa na Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ na wagemi wengine wakipakua chakula katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea machache baada ya futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea machache baada ya futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016 .Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipongezwa na kaimu Mufti Sheikh Hamid Masoud Jongo baada ya kuongea machache katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Kadhi Mkuu wa Tanzania Sheikh Abdallah Mnyasi katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wageni mbalimbali katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama Shamim Khan katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016. Kushoto ni Mke wa rais Mama Janeth Magufuli akifuatiwa na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Fr. Stephano Kaombwe katika futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisaliminia na wageni waliohudhuria futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini iliyoandaliwa na Rais Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisaliminia na wageni waliohudhuria futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini iliyoandaliwa na Rais Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisaliminia na wageni waliohudhuria futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini iliyoandaliwa na Rais Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akikatika picha ya pamoja na wageni waliohudhuria futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini iliyoandaliwa na Rais Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA WADAU WA KOROSHO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa zao la korosho kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma juni 14, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TTB YJIKITA ZAIDI KUITANGAZA NCHI KUPITIA MITANDAO

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw. Philip Chitaunga akifafanua jambo mbele ye wandishi wa habari (hawapo pichani) katika ofisi za Bodi hiyo leo jijini Dar es salaam.

Na: Geofrey Tengeneza

Bodi ya Utalii Tanzania imeanzisha touvuti maalumu iitwayo Destination Tourism Portal pamoja na Nyenzo (App) kwa watumiaji wa simu za mikononi na hivyo kuendelea kujikita zaidi katika matumizi ya tovuti na mitandao ya Kijamii (e-marketing) katika kutekeleza majukumu yake ya utangazaji wa vivutio vya Utalii vya Tanzania duniani kwa lengo la kuvutia watalii wengi zaidi.

“Tovuti hii inalenga zaidi katika kuwasaidia wajasiriamali wadogo na wa kati katika sekta ya utalii kufanya biashara zao kwa urahisi na kukuza mapato yao na faida zaidi” alisema Bw. Chitaunga. Ameongeza kuwa Tovuti hii inatumia anuani ya www.tanzaniatourism.com ina taarifa nyingi sana za vivutio vya utalii vinavyopatikana hapa nchini lakini pia taarifa kuhusu malazi (accommodation) na huduma nyinginezo na kwamba inamwezesha mtalii kufanya malipo online. 

Mkurugenzi huyo wa Masoko amesema kuwa sambamba na uanzishaji wa tovuti hiyo, tumeanzisha pia nyenzo rasmi ya Utalii iitwayo Tanzania Tourism App ambayo kama ilivyo kwa portal ina taarifa nyingi za utalii ikiwa ni pamoja na vivutio vya utalii, malazi na namna ya kupanga safari kwa mtalii anayetaka kutembelea Tanzania, na kufanya malipo online. Amesema kuwa Nyenzo (App) hii inapatikana katika Google play store kwa watumiaji wa simu za Android duniani kote na muda si mrefu itapatikana pia katika AppStore kwa watumiaji wa simu za Iphone.

Amedokea kuwa zipo nyenzo (Apps) kadhaa zilizoanzishwa na makapuni au watu binafsi kama vile Tanzania Safari Guide; Tanzania Travel Safari; Destination Tanzania: Tanzania Travel and Tourism n.k lakini hii ya kwetu ndiyo hasa rasmi ya Serikali.

KUTOKA CCM LUMUMBA LEO

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa Korea Song Geum-Yung, Ofsni kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba ijini Dar es Salaam, leo Juni 15, 2016. (Picha na Bashir Nkoromo). Mweneyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akisalimiana na Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya shughuli zake za kiofisi, leo Juni 15, 2016. (Picha na Bashir Nkoromo).

WATENDAJI WABADHIRIFU WA BODI YA MIKOPO KUSHUGHULIKIWA -PROFESA NDALICHAKO.

$
0
0
WAZIRI wa Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Profesa  Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana  kuwachukulia hatua watendaji wote waliosimamishwa kati katika wizara ya elimu pamoja na  kuwafikisha vyombo vya dola. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu- Elimu wa Wizara ya Elimu,  Sayansi na Teknolojia, Dk. Leunard Akwilapo.
Kutoka Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia, Tarish Kibenga Katikati Naibu Katibu Mkuu- Sayansi na Ubunifu, Simon Masanjila na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya  Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia, Anna Mhere.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Profesa  Joyce Ndalichako ametangaza kiama kwa watendaji wote wa  Bodi ya Mikopo waliofanya ubadhirifu wa fedha za wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa kuwapa watu wasiohusika.


Joyce ameyasema leo wakati akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam leo. amesema kuwa bodi ya mikopo baada ya kufanya ukaguzi maalum katika hoja 17 ni hoja moja imepata majibu na kuzaliwa dosari zingine ambazo kutokuwa na mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu kwa watu ambao wanarejesha mikopo.


Amesema kuwa kutokana na matatizo ya bodi ya mikopo ameigiza bodi kuhakikisha wanachukua hatua kwa watendaji wote waliosimamishwa ikiwemo kuwafikisha vyombo vya dola.


Joyce amesema kuwa katika dosari nyingine wanafunzi zaidi 2,000 wamepewa mikopo katika vyuo viwili lakini wanafunzi hao hawapo katika vyuo vilivyotajwa.


Amesema kuwa kuna wanafunzi wanalipwa sehemu mbili  ya mikopo ya bodi kwa Tanzania Bara na Zanzibar kwa wakati mmoja huku kuna wanafunzi hawapati  mikopo kabisa na watoto wa masikini.


Aidha amesema bodi hiyo inatakiwa kufanyia kazi dosari zote pamoja na hatua ambazo wamezichukua kwa baadhi ya watendaji ambao wamefuja fedha za walipa kodi.


Joyce amesema kuwa matatizo mengine ni Baraza la Usajili wa vyuo vya  Elimu na ufundi (NACTE) kufanya kazi kazi ambazo wao wenyewe hawana uwezo nazo ikiwemo kukagua baadhi ya vyuo ambavyo vingine vinatoa digrii ya pili.


Amesema yote wanaangalia kwa kupitia sheria na kuona jinsi ya kuboresha utendaji kazi kwa NACTE kufanya kazi kwa uwezo unaostahili.

DAWASCO kuongeza uzalishaji toka lita milioni 70 mpaka 106 kwa siku

$
0
0

Na Daudi Manongi-MAELEZO

Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) Bi. Everlasting Lyaro amesema kuwa uzimaji wa mtambo wa Ruvu Juu kwa wakazi wa Dar es Salaam na Mji wa Kibaha mkoani Pwani siku tatu kuanzia ijumaa ya tarehe 17 mpaka tarehe 19 Jumapili umelenga kuongeza uzalishaji kutoka lita milioni 70 mpaka lita milioni 106 kwa siku.

Bi Lyaro alisema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na Idara ya Habari Maelezo akitoa ufafanuzi kuhusu taarifa za uzimaji wa mtambo wa Ruvu Juu.

Alisema kuwa sababu kubwa za kuzima mtambo huo ni kumruhusu mkandarasi (WABAG) kuunganisha mtambo mpya wa Maji na ule wa zamani ili kufanikisha kampeni ya kumtua mama wa Dar es Salaam ndoo kichwani kwa kumfikishia maji nyumbani kwake.

Kuzimwa kwa mtambo huo wa Ruvu Juu kutapelekea maeneo ya Mlandizi,Kibaha,Ubungo,Kimara,Kibamba,Kibangu,Makuburi,Tabata,Segerea na Kinyerezi kukosa maji kwa kipindi hicho cha masaa 72.

Aidha wananchi wa maeneo husika wanashauriwa kuhifadhi maji ya kutosha kwa siku hizo tatu na DAWASCO inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kwani jitihada hizi ni maboresho ya kuwasogezea maji karibu.

COCA-COLA KUENDELEA KUDHAMINI MASHINDANO YA UMISSETA NCHINI TANZANIA.

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla akikagua wachezaji wakati wa Uzinduzi wa mashindano ya UMISETA ambayo mwaka huu yamedhaminiwa na kampuni ya Coca Cola. Uzinduzi huo ulifanyika May 10, 2016 katika uwanja wa Sokoine ambapo kulifanyika michezo na burudani mbali mbali. .

 Mashindano kwa ajili ya fainali za kitaifa za Copa-UMISSETA ambayo yanadhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola, na ambayo yalipangwa kuanza kufanyika siku ya leo hadi hapo tarehe 24 Juni 2016 yametangazwa kuahirishwa. Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya serikali iliyotolewa hapo jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), George Simbachawene, serikali imechukua uamuzi huo ili kupisha utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli la upatikanaji wa madawati, ambao kikomo chake ni mwisho wa mwezi huu. Mashindano haya ya fainali za Copa-UMISSETA yalilenga kuzikutanisha timu za mikoa mbalimbali nchini kwa pamoja Jijini Mwanza, zikiwa zimeundwa na wachezaji mbalimbali kutoka shule za sekondari ili wachuane kwenye michezo na sanaa.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke - Dar es Salaam, Sophia Mjema (kushoto), akisalimiana na wachezaji wa timu ya Makongo Sekondari katika Mashindano ya UMISETA ambapo kampuni ya Coca Cola ndiyo walikuwa ni wadhamini wakubwa wa michuano hiyo kwa mwaka 2016. - “Thamira yetu katika kudhamini mashindano haya na kushirikiana TAMISEMI iko pale pale, tukiwa tumejidhatiti kuendelea kuunga mkono jitihada za kutambua na kuinua vipaji vya vijana ambao watakuja kuifikisha Nyanja ya michezo nchini katika kiwango cha juu zaidi. Tutaendelea kuunga mkono na kusaidia kukua kwa sekta ya michezo nchini, hususani mashindano ya mpira wa miguu pamoja na mpira wa kikapu kwa vijana,” alisema David Karamagi, Mwakilishi Mkazi wa Coca-Cola Tanzania. Karamagi aliongeza kuwa kampuni ya Coca-Cola Tanzania inayo imani ya dhati na ikiamini ya kwamba mashindano ya michezo yanayoanzia ngazi ya chini kabisa ndiyo namna thabiti nay a kipekee katika kuibua vipaji vya wachezaji nchini. Pia Karamagi alisema kuwa, wakati wadau wakisubiri kwa hamu kutangazwa kwa tarehe mpya za kurejewa kwa fainali za mashindano haya nchini, Coca-Cola Tanzania ilishajipanga kudhihirisha ya kwamba michezo ni zaidi ya ushindani, kwa kuweza kuambatanisha mashindano haya na kujenga mshikamano wa timu shindani, urafiki na hata nidhamu kwa wachezaji na timu za mikoa inayoshiriki. Hivyo basi, kwa udhamini ulioingiwa mwaka huu, Coca-Cola Tanzania itaweza kupanua wigo wa ushirikishwaji wa michezo murua zaidi mbali ya mpira wa miguu, hasa kwa kuweza kujumuisha mpira wa kikapu. “Kampuni ya Coca-Cola nchini tutaendelea na dhamira yetu ya kuunga mkono jitihada ya vijana mbalimbali nchini kote katika kuwasaidia kudhihirisha vipaji vyao kupitia mashindano mbali mbali ya michezo, ikiwa ni pamoja na UMISSETA na Copa Coca-Cola’” alimalizia Karamagi.

SIMU FEKI KUZIMWA KESHO.

$
0
0

Meneja wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kuzima simu feki ifikapo kesho Juni 16 mwaka huu.

Na Chalila kibuda, Globu ya Jamii.
SIMU ziliingizwa nchini zikiwa hazina kiwango kuzimwa rasmi kesho, katika kuhakikisha kila mtu anatumia simu kiwango kwa usalama  na ulinzi wa nchi.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba amesema kuwa katika uzimaji wa simu wameshatoa elimu juu ya simu hizo.

Kilaba amesema kuwa simu ambazo watu walibadilisha (Flash) nazo zitazimwa kutokana na kufanya hivyo ni kosa la kisheria na mtu anayefanya hivyo kifungo chake ni miaka 10.

Amesema hakuna kitu chochote kinachofanya simu zisiweze kuzimwa hivyo watu wajiandae zoezi hilo na simu zitazozimwa wametakiwa kuzihifadhi katika mazingira salama.

Aidha amesema katika elimu wametoa hivyo kesho kutakuwa na mkutano wa wadau mbalimbali wa makampuni ya simu, na wamiliki wa maduka ya simu pamoja na mafundi katika kubadilishana mawazo wakati wa kuzima simu feki.

‘’Simu feki kesho kuzimwa hatutakuwa na mabadiliko ya kuongeza muda au vinginevyo kutokana na elimu iliyotolewa juu simu ya  feki ambazo baada soko kushindikana mjini walipeleka vijijini’’amesema Kilaba  .

TAARIFA KUTOKA CHAMA CHA CUF

Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images