Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 881 | 882 | (Page 883) | 884 | 885 | .... | 1898 | newer

  0 0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Wadau wa Benki za Wananchi kwenye Ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Juni 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Wziri Mkuu)
  Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Benki za Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua mkutano wao kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Juni 15, 2016.

  Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Benki za Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua mkutano wao kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Juni 15, 2016.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkatano wa Wadau wa Benki za Wananchi kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma juni 15, 2016.


  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezitaka benki nchini zipitie upya riba zake ili Watanzania waweze kukopa na kurejesha kwa urahisi.Amesema riba kubwa zinazotozwa na baadhi ya benki, huduma zisizokidhi mahitaji na uelewa mdogo wa masuala ya kifedha ni miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo wananchi wanapotaka huduma za kifedha.

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Juni 15, 2016) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi (COBAT) mjini Dodoma.

  Mkutano huo ulijumuisha wajumbe kutoka mikoa 10 ya Kigoma, Lindi, Simiyu, Manyara, Katavi, Mbeya, Mwanza, Morogoro, Singida na Dodoma kati ya mikoa 18 ya Tanzania Bara ambayo bado haina Benki za Wananchi ila ipo katika hatua za kuanzisha.Amesema changamoto nyingine ni kutokuwepo kwa taarifa mbalimbali za sheria na taratibu ambazo zinakwamisha ufanisi wa kiutendaji kwa baadhi ya taasisi hasa zile zinazolenga kuwahudumia watu wa kipato cha chini.

  “Tunahitaji kutafuta njia bora ya kutatua changamoto hizi, na Benki za Wananchi ni kiungo muhimu katika kushughulikia changamoto zinazokabili utoaji wa huduma za kifedha,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema ni muhimu kuanzisha Benki za Wananchi katika kila Mkoa ili kuweza kusambaza huduma hizo karibu zaidi na walengwa, hali ambayo itasaidia kupunguza umasikini kupitia ukuaji wa shughuli za kiuchumi.

  Amesema Serikali itaangalia uwezekano wa kuiwezesha mikoa ambayo itaonyesha ari zaidi ya kuanzisha benki zao na akatoa wito waandae mikakati ya kuhamasisha wananchi ili wakusanye mitaji ya kutosha.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa COBAT, Bibi Elizabeth Makwabe amesema Jumuiya yao ilianzishwa mwaka 2006 ikiwa na wanachama saba na sasa hivi wamefikia 10 huku wananchi wanaowahudumiwa na benki hizo ni zaidi ya milioni mbili.

  Amesema Jumuiya za Benki ya Wananchi inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo mfumo hafifu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) pamoja na ufinyu wa mitaji.


  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  JUMATANO, JU
  NI 15, 2016.

  0 0


  Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Ulinzi na Usalama wa Mtoto kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika inayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka. Kushoto ni Afisa Ustawi wa Amana One Stop Centre Bw. Sophian Mndolwa na kulia ni Mratibu wa Timu ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto Manispaa ya Ilala Bw. Waziri Nashiri.

  Mratibu wa Timu ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto Manispaa ya Ilala Bw. Waziri Nashiri (kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mipango ya Manispaa hiyo katika kuwasaidia watoto walio kwenye mazingira hatarishi. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu na katikati ni Afisa Ustawi wa Amana One Stop Centre Bw. Sophian Mndolwa.

  Afisa Ustawi wa Amana One Stop Centre Bw. Sophian Mndolwa akieleza kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu taratibu za kufuata ili kupata huduma katika kituo cha Amana One Stop Centre ambacho kinahusika na kutoa msaada kwa watoto wanaofanyiwa ukatili wa aina mbalimbali. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu.Picha na Fatma Salum (MAELEZO) .


  0 0


  Mkurugenzi wa MCDI,Jasper Makala(Kulia) Akipokea Tuzo ya ya Mwaka 2016 Utunzaji na Uhifadhi wa Misitu toka kwa Dr Gary Knel.Afisa Mtendaji Mkuu Geographic Society jana huko USA.


  Jasper Makala Akikabidhi Tuzo ya Whitley Award Kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi.

  Na Abdulaziz Video,Lindi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kuhifadhi mpingo na maendeleo(MCDI) Mr Makala Jasper(Kulia)Usiku wa jana huko Washington DC-USA Ameibuka Kidedea baada ya kushinda Tuzo ya mwaka 2016 iitwayo National Geographic Society/Buffett Award for Leadership in African Conservation.Tuzo hiyo ina thamani ya Dolla 25,000.

  Jasper Makala Mkurugenzi wa MCDI Yenye makao makuu yake Kilwa Masoko Mkoani Lindi ameiwakilisha vyema Africa na Tanzania Ambapo kwa Kushinda Tuzo hiyo. Ushindi huo ni Baada ya Kuwashinda Wasiriki wengine 30 Toka bara la Africa na Wenye Uwezo mkubwa na kufanya mchuano kuwa mkali sana.


  Iikumbukwe hii ni tuzo ya pili ndani ya miezi miwili ambapo Makala Jasper aliwania tuzo za Whitley huko nchini Uingereza ambapo pia alishinda tuzo hiyo ambayo ilikuwa na thamani ya Paundi £35, 000.Zaidi ya Milioni 100 za Kitanzania.Ushindi huo unatokana na Mawasilisho ya Utunzaji Shirikishi na Uhifadhi wa Misitu

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  JESHI LA POLISI TANZANIA
   
  JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA.
  WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI WILAYANI ILEMELA NA NYAMAGANA.

  KWAMBA MNAMO TAREHE 14.06.2016 MAJIRA YA SAA 10:30HRS KATIKA ENEO LA IGOMBE KATA YA BUGOGWA WILAYA YA ILEMELA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA KWENYE DORIA NA MISAKO WALIFANIKIWA KUMKAMATA JONATHAN GABRIEL MIAKA [31] MKAZI WA BUGOGWA AKIWA NA MISOKOTO MIA NNE [400] YA BHANGI KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA ZA NCHI.

  INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ANAFANYA BIASHARA YA KUUZA MADAWA HAYO YA KULEVYA KATIKA MITAA MBALIMBALI YA IGOMBE NA ILEMELA PIA, NA PINDI MTUHUMIWA ANAKAMATWA ALIKUWA AKIFANYA MAWASILIANO NA WATEJA WAKE JINSI YA KUWAPATIA BHANGI HIYO.

  KATIKA TUKIO LINGINE LA TAREHE TAJWA HAPO JUU MAJIRA YA SAA 13:30HRS KATIKA ENEO LA MWANANCHI WILAYANI NYAMAGANA, ASKARI WAKIWA DORIA WALIFANIKIWA KUMKAMATA RAMADHANI HAMAD MIAKA [24] MKAZI WA NYAKATO AKIWA NA BHANGI KILO TATU [03] KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.

  AIDHA INASEMEKANA KUWA MTUHUMIWA AKISHIRIKIANA NA WENZAKE HUFANYA BIASHARA YA KUUZA BHANGI KATIKA MITAA HIYO WANAYOISHI, NDIPO RAIA WEMA WALITOA TAARIFA POLISI NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA AKIWA NA KILO HIZO ZA BHANGI.

  WATUHUMIWA WOTE WAWILI WAPO CHINI YA ULINZI WA JESHI LA POLISI, HUKU MAHOJIANO DHIDI YA UHALIFU WANAOUFANYA WA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA BHANGI UKIENDELEA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU MASHITAKA YANAYO WAKABILI.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI HASWA VIJANA AKIWATAKA KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA ZA MADAWA YA KULEVYA AMBAYO NI HARAMU NA BATILI KATIKA USTAWI WA NCHI YETU, KWANI JESHI LA POLISI LIMEJIPANGA VIZURI KUHAKIKISHA LINAWATAFUTA WALE WOTE WANAOJIHUSISHA KATIKA BIASHARA HIYO NA KUWAKAMATA KISHA KUWAFIKISHA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA KWA AJILI YA KUPEWA ADHABU KALI ILI IWE FUNDISHO KWA WATU WENGINE.
  IMESAINIWA NA:
  SACP: AHMED MSANGI
  KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

  0 0

  TAKDIR ALI NA MIZA OTHMAN HABARI MAELEZO
   
  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itawazuilia leseni wafanyabiashara watakaobainika kuwanyima huduma ama kuwapandishia bei baadhi ya wananchi kutokana na misingi ya kisiasa.

  Akijibu suali la Mwakilishi wa viti maalum Viwe Khamisi Abdallah, katika Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar alietaka kujua iwapo Serikali inafahamu suala la hilo, Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali alisema Serikali inalifahamu suala hilo na tayari linafanyiwa kazi na wakuu wa wilaya.

  Balozi Amina alisema katika kisiwa cha Pemba kumekuwa na uchafuzi wa kisiasa na baadhi ya wanasiasa wanatumia nafasi hiyo kuwapandishia bei wananchi hususan wanachama wa CCM.

  Alisema wamekuwa wakichukua hatua ya kuwafungia kwa muda mfupi wafanyabiashara wenye tabia hiyo lakini hivi sasa watawazuilia leseni kwa muda wa mwaka mmoja kama adhabu na onyo.

  Mapema akijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Fuoni Yussuf Hassan Iddi, Balozi Amina alisema Seriksali inafanya juhudi kubwa za kusimamia bei za bidhaa muhimu ikiwemo,mchele,Unga wa ngano,na sukari ili kuhakikisha hakuna upandaji wa bei kiholela.

  Alikiri kuwa baadhi ya bidhaa hizo zimepanda bei kidogo kutokana na kupanda mara kwa mara kwa thamani ya Dola na kuongezeka kwa gharama nyengine za biashara zikiwemo kuchelewa kushusha mizigo bandarini.

  Alisema Serikali imefanya juhudi kubwa kupunguza tatizo la upandaji wa bidhaa, ikiwemo kufanya mazungumzo na Shirika la Bandari pamoja na Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima (ZNCCIA) ili kutafuta ufumbuzi wa suala hilo. 
   
  Aliongeza kuwa Wizara yake inaendelea na juhudi ya kuhahikisha bidhaa muhimu za chakula kwa ajili ya mwezi mtukufu Ramadhani ikiwemo unga wa ngano,Tende na Sukari vinapatikana kwa bei nafuu ili kuwapunguiza mzigo wananchi ndani ya mwezi huu.

  0 0

  Na Ismail Ngayonga-MAELEZO

  SERIKALI katika mwaka 2016/17 imekusuduia kutoa vifaa vya kujifungulia kwa wanawake wajawazito 500,000 ili kuwasaidia kukabiliana na  matatizo ya uzazi pingamizi ikiwemo ugonjwa wa Fistula.

  Hatua hiyo imekusudiwa kuchochea na kuwahamasisha wanawake wajawazito kujifungulia katika vituo vya huduma ya afya nchini badala ya  kufika kwa wakunga  wa jadi.

  Hayo yamebainishwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati akijibu Swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mgeni Jadi Kadika.

  Mbunge huyo alitaka kufahamu mikakati ya Serikali ya kutokomeza tatizo la ugonjwa wa fistula nchini.Waziri Ummy alisema ugonjwa wa fistula umekuwa ukiwapata wanawake wa hadhi ya chini hususani wale wa vijijini ambapo kuna uhaba wa miundombinu ya vituo vya afya, uhaba wa wataalam  na msongamano wa wa kupata huduma.

  Waziri Ummy alisema ugonjwa wa fistula hausababishwi na kurogwa, laana au kutembea na wanaume wengi, kama ambavyo baadhi ya wanajamii wanavyoelewa, hivyo ili kukabiliana na uginjwa huo Serikali imekuweka mikakati mbalimbali ikiwemo kuhamasisha wanawake kujifungulia katika vituo vya afya.

  “Tutawahamisha wanawake wote wajawazito hususani wa kiuanzia miezi 2 na kuendelea wanaanza kliniki mapema ili kuwasadia na uzazi pingamizi,”  alisema Ummy.

  Aidha Waziri Ummy alisema Serikali pia imekusudia kuhakikisha kuwa hospitali za rufaa za mikoa nchini zinakuwa na huduma ya upasuaji kwa wagonjwa wa fistula ili kuwawezesha wanawake wenye tatizo hilo wanapata huduma za matibabu kwa ufanisi.

  Alisema ugonjwa wa fistula umekuwa na madhara ya kijamii, kiafya na kiuchumi ikiwemo wajawazito wengi kupoteza watoto, wanawake kuachwa na waume zao pamoja na akina mama hao kushindwa kujihusisha shughuli za maendeleo.

  0 0


  Na Ismail Ngayonga-MAELEZO,Dodoma

  SERIKALI imekusudia kutunga sheria ya kupiga marufuku ajira za wasichana wa kazi wenye umri chini ya miaka 18 kabla ya mwisho wa mwaka 2016.

  Hatua hiyo inaelezwa inakusudia kuinua hadhi ya kazi na ajira za wasichana wa kazi nchini, kwani muda wa kurasimisha ajira hizo umefikia wakati wake.

  Hayo yamebainishwa leo mjini hapa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizungumzia na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika inayoadhimishwa tarehe 16 Juni kila mwaka.

  alisema hatua inachuliiwa na Serikali kutokana na wasichana wengi wa ndani kutumikishwa kazi hiyo katika umri mdogo na kulipwa ujira mdogo.

  “Tumepanga kutunga kanuni na sheria ya kupiga marufuku ajira za wasichana wa kazi wenye umri chini ya miaka 18, na ndio maana tunawachukua katika umri mdogo sana na kuwalipa ujira mdogo, hivyo ukimchukua binti wa miaka 18 utaweza kuinua hadhi ya kazi ya kazi yenyewe” alisema Waziri Ummy.

  Akizungumzia kuhusu maadhimisho hayo, Waziri Ummy aliitaka jamii kukataa kurubuniwa kwa pesa na katika kuwavichua watu wanaofanya vitendo vya ukatili kwa watoto ikiwemo kulawiti na kuwabaka na badala yake watoe taarifa katika vyombo vya dola ili adhabu kali zichuliwe dhidi yao.

  Aidha Waziri Ummy aliwata wazazi nchini kujenga tabia ya kukagua maumbile ya watoto wao hususani watoto wa kike ikiwemo kuwaogesha angalau mara moja kwa mwezi, kwani kwa kufanya hivyo kutamwezesha mzazi kufahamu afya ya kimwili ya motto wake.

  Kwa mujibu wa Waziri huyo alisema vitendo vya ulawiti havifanywi kwa watoto wa kike pekee bali na watoto wa kiume pia wamekuwa wahanga wa vitendo hivyo, ambapo ameitaka jamii kutowaamini ndugu au jamaa zao kulala kitanda chumba kimoja na watoto wao.

  “Kwa mujibu wa taarifa za jeshi la Polisi, vitendo hivi vimekuwa vikifanyika zaidi majumbani kwa asilimia 49, asilimia 23 wakati wa kurudi na kwenda shule na asilimia 15 wakiwa shuleni, hivyo kwa takwimu hizi unaweza kuona ukubwa wa tatizo ulivyo” alisema Waziri Ummy.

  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akihutubia wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi kutoka mikoa yote nchini (hawapo pichani), katika ukumbi wa Mikutano wa Kambarage ulioko katika Jengo la Hazina Mjini Dodoma Wadau wa sekta ya Benki za Wananchi kutoka mkoani Mwanza, wakisikiliza kwa makini mada zilizotolewa kuhusu uanzishwaji wa benki hizo nchini, katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage ulioko katika Jengo la Hazina mjini Dodoma

  Wakiri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Benki za wananchi nchini, Bi. Elizabeth Makwabe, baada ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano huo uliowashirikisha viongozi wa mikoa mbalimbali nchini katika ukumbi wa Kambarage, Jengo la Hazina mjini Dodoma.

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (Kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa mkoa wa Singida, Mhandisi Mathew Mtigumwe, mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa siku moja wa wadau wa Jumuiya ya Benki za wananchi, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kambarage, ulioko katika jengo la Hazina Mjini Dodoma.Picha zote na Benny Mwaipaja, WFP


  Na Benny Mwaipaja-WFP

  WAZIRI MKUU, Mhe. Kassim Majaliwa, amezishauri taasisi za fedha nchini zipunguze viwango vya riba zinazotoza kwenye mikopo ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi hususan waishio vijijini kujikwamua kiuchumi

  Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Juni 15, 2016, wakati akifungua mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi (COBAT), ulioshirikisha viongozi wa mikoa 28 nchini, uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Mjini Dodoma.

  Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa amesema kuwa riba kubwa inayotozwa na taasisi hizo za fedha ni kubwa na kuwafanya wananchi wengi washindwe kunufaika na fursa za mikopo inayotolewa, hali inayowafanya waendelee kuwa masikini.

  “Kama Benki zitatoa mikopo yenye riba nafuu, kila mwananchi atamudu kupata mtaji na kufanya biashara yake akijua kuwa riba si kubwa na tayari Serikali imeanza kufanya mazungumzo na taasisi za fedha kuhusu jambo hili ili ziweze kufanya mapitio ya riba zake”Aliongeza Mhe. Kassim Majaliwa

  Ameipa mikoa ambayo haijaanzisha benki za wananchi-COBAT, muda wa miezi mitatu kuanzisha mchakato huo ili kufikisha huduma rasmi za kifedha kupitia benki hizo ili kuchochea na kuamsha uzalishaji mali wenye tija katika jamii.

  Amesema lengo muhimu la kuwainua wananchi kimaisha litatimia kwa kuhamasisha wananchi mijini na vijijini, wenye kipato cha chini kabisa katika kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba na kuwekeza katika hisa ili kukuza mitaji itakayosaidia shughuli za maendeleo kwenye maeneo yao yote.

  Ameahidi kuwa Serikali itaangalia uwezekano wa kuiwezesha mikoa itakayoonesha ari zaidi ya kuanzisha benki zao za wananchi kwa kuzishirikisha Halmashauri za wilaya, Manispaa, Miji na Majiji.

  “Inawezekana kabisa kuanzisha benki hizo kwa kukusanya hisa kutoka kwa wananchi na Halmashauri zikachangia ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kufikiwa na huduma za kibenki katika maeneo yao”Alisisitiza Waziri Mkuu.

  Amesema ni matumani ya serikali ya awamu ya tano kwamba uanzishwaji wa benki hizo una umuhimu mkubwa kwa kuwa zitakuwa kiunganishi mahsusi ambacho kikiwa imara kitaleta mabadiliko chanya katika kuwawezesha wananchi kujikwamua na kujiletea maendeleo ya haraka.

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, ameeleza kuwa hadi kufikia mwaka 2016, mikoa 8 tu ya Tanzania bara ndiyo imeanzisha benki za wananchi-COBAT kati ya mikoa 26 iliyopo.

  Amezitaja benki hizo zilizoko chini ya Jumuiya ya Benki za Wananchi Tanzania-COBAT kuwa ni Mucoba (Mufundi), Mbinga (Mbinga), Mwanga (Mwanga), Uchumi (Moshi), Tandahimba (Mtwara), Meru (Arusha), Njombe (Njombe) na Efatha (Dar es salaam)

  Dkt. Mpango amesema kuwa Benki hizo zinawateja wanaokadiriwa kufikia 600,000 zikiwa na jumla ya mali iliyofikia shilingi Bilioni 86.3 na amana za wateja shilingi Bilioni 69.2 na kutoa mikopo kwa wateja wake inayofikia shilingi Bilioni 56.2

  “Mpango wa kuhakikisha huduma za fedha zinawafikia wananchi wengi zaidi ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya taifa inayolenga kuipeleka Tanzania katika nchi ya kipato cha kati na yenye uchumi imara ifikapo mwaka 2015” Amesisitiza Dkt. Mpango

  Amesema hadi kufikia Desemba mwaka 2015, Taasisi za benki za wananchi za mikoa, vyama vya ushirika vya akiba na mikopo, zimeongezeka hadi kufikia 4,093, zikiwa na wanachama 733,876 na kuwekeza kiasi cha shilingi Bilioni 377.6

  “Aidha, Asasi za Fedha za Kijamii (Vicoba, Vsla, Rosca), zinakadiriwa kufikia 100,000 na zina wanachama milioni 2.2 na mtaji wa shilingi Trilioni 1.2” aliongeza Dkt Mpango

  Amesema kuwa utafiti uliofanyika hivi karibuni na shirika la Finscope umebaini kuwa asilimia 57.4 ya watanzania wanapata huduma rasmi za kifedha, ambapo kati ya hao, asilimia 13.9 wanapata huduma za kibenki huku asilimia 43.5 wanapata huduma za kifedha zisizo za kibenki.

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, amezitaja changamoto zinazoikabili sekta ya Fedha nchini kuwa ni upungufu wa mitaji, ukusanyaji mdogo wa amana, kiwango cha riba kuwa juu, ushindani kutoka benki za biashara na taasisi zingine za Fedha, kukosekana kwa wataalamu wa kuziendesha na kukosekana kwa sheria na kanuni mahsusi kwa benki za wananchi na Ushirika.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Benki za Wananchi Tanzania-COBAT, Elizabeth Makwabe, amesema kuwa katika kipindi cha miaka 20 sasa, benki za wananchi zimeendelea kupanua huduma zake ambapo hadi sasa, mali, amana na mikopo vimeongezeka kutoka shilingi Bilioni 71.2 mwaka 2014 hadi kufikia shilingi Bilioni 86.3 mwaka 2015

  Ameiomba serikali kuwekeza fedha za kutosha kwenye benki za wananchi katika mfumo wa fedha za kuzungusha (Revolving Fund) ili kusisimua uchumi katika maeneo ya vijijini pamoja na kuzitaka Halmashauri za wilaya kuwekeza mitaji kwenye benki hizo katika maeneo yao.

  Akitoa neno la Shukrani kwaniaba ya wakuu wa mikoa waliohudhuria mkutano huo, mkuu wa mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera, ameahidi kuwa mikoa yote 18 ambayo haijaanzisha benki za wananchi itahamasisha na kuanzisha benki hizo kwa faida ya wananchi wao.

  0 0


  Katibu wa TAHLISO Siraji Madebe akizungumza leo

  Siku chache baada ya Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima kuwashutumu viongozi wa CCM kwamba wanamipango ya kutomkadhi chama Rais Dk. John Magufuli, Shirikiho la Wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), limemshukia na kulaani vikali kauli hiyo kwamba ni yauchochezi.

  Akizungumza leo latika Ofisi za Shirikisho hilo, jijini Dar es Salaam, Katibu wa TAHLISO Siraji Madebe, amesema, Gwajima kama kiongozi wa dini ajitokeze hadharani kutaja viongozi anaodai walimpigia simu kuelezea mkakati huo wa kutomkabidhi Chama Dk. Magufuli.

  SOMA TAARIFA KAMILI KAMA ILIYOTOLEWA NA TAHLISO

  Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania limeshitushwa na taarifa za uchochezi zilizotolewa na kiongozi wa dini wa kanisa la Ufufuo na Uzima hivi karibuni likituhumu viongozi wa Chama cha Mapinduzi kuwa na mipango ya kutokumkabidhi Chama Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mh. John Joseph Pombe Magufuli.

  Sisi kama Vyuo Vikuu tunalaani vikali sana kauli yenye dalili za uchochezi zinazotaka kupandikiza chuki miongoni mwa viongozi wetu wa Serikali na Chama kwa ujumla. Lakini kama kiongozi wa dini mwenye hofu ya Mungu tunamtaka ajitokeze kuwataja hadharani wale waliompigia simu kumuomba awasaidie bila kuwasahau na wale wanaozunguka mikoani kwa ajili ya kuhamasisha zoezi hilo kama alivyoeleza.

  Ndugu waandishi wa habari, pamoja na mambo mengine kwa faida ya watanzania kiongozi huyu angetaka ufafanuzi juu ya jambo hili angewasiliana na katibu wetu wa Chama cha Mapinduzi Comrade Abdulrahman Kinana au Naibu Katibu Mkuu wetu wa Chama Cha Mapinduzi Comrade Rajab Luhavi badala ya kwenda kuaminisha waumini na watanzania jambo lisilokuwa na uhakika.

  Lakini ndugu zangu katika maelezo yake alidhihirisha wazi kwamba hakiungi mkono Chama Cha Mapinduzi na pia hakumuunga mkono mhe. Rais katika kipindi cha kampeni, hivyo asichukue nafasi hiyo ya kutaka kugombanisha na kukisambaratisha Chama Chetu.

  Tunatoa rai kwa viongozi na Taasisi za kidini zote nchini kutojihusisha na masuala ya kisiasa na badala yake kutekeleza majukumu yaliyokusudiwa kwa uwepo wao. Kuhusisha siasa na dini ni kuchochea uhasama na kupandikiza mbegu za chuki, vurugu, uchochezi na kuhatarisha uvunjifu wa amani baina ya wananchi, viongozi na Taifa kwa ujumla. Hivyo hatuko tayari kuwavumilia watu wote wenye nia ya kutuvurugia amani tuliyo nayo na kutuingiza kwenye migongano ya kidini.

  Tanzania ni moja na watanzania ni wamoja bila kujali tofauti za kisiasa, kidini na kikabila.

  Mwisho tunapenda kuiomba serikali kupitia vyombo vya dola kushughulikia kwa kina jambo hili na kulichukulia hatua ili kukomesha vitendo vya uchochezi baina ya watanzania na baina ya viongozi.

  0 0


  0 0


  FUT4 
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea machache baada ya futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini aliyoandaa Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Juni 14, 2016

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasihi Watanzania wote kuungana na Waislamu walio katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kuiombea Tanzania iendelee kuwa nchi ya Amani, Utulivu, Umoja na Mshikamano ili iweze kutimiza malengo yake ya kimaendeleo na kuimarisha ustawi wa jamii.

  Rais Magufuli ametoa kauli hiyo mbele ya Masheikh, Maimamu na viongozi wa dini ya Kiislamu na baadhi ya viongozi na waumini wa madhehebu mengine mbalimbali ya dini aliowaalika katika futari jana jioni tarehe 14 Juni, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.

  "Kwa niaba ya serikali na mimi mwenyewe na watanzania kwa ujumla, napenda kutumia fursa hii adhimu kuwatakia waislamu wote nchini Tanzania mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, uwe mfungo wa amani na wenye baraka, lakini pia ninamuomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema azikubali funga zenu na kuwalipa malipo stahiki."Niwaombe ndugu zangu waislamu msisahau kuliombea taifa hili amani, palipo na amani ndipo palipo na maendeleo ya kweli, palipo na amani ndipo biashara itaenda vizuri, palipo na amani hata mahubiri mazuri kwa watu yatasikika vizuri, tulisimamie hili kwa manufaa ya Tanzania" Amesema Rais Magufuli.

  Pamoja na kuwaalika watanzania wote kuliombea taifa, Rais Magufuli pia amewahakikishia watanzania wote kuwa serikali yake ipo imara kuhakikisha inailinda na kuidumisha amani iliyopo.Aidha, Dkt. John Pombe Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na umoja na ushirikiano wa viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini wanaounda Kamati za amani za mikoa.Pia amewataka wafanyabiashara wa vyakula waache kupandisha bei za vyakula hasa vinavyotumika wakati wa mfungo huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuwawezesha waliofunga kumudu kununua vyakula hivyo.

  Katika futari hiyo Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wameungana na viongozi mbalimbali wa dini wakiwemo Kaimu Mufti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Alhaji Hamid Masoud Jongo, Askofu Mkuu wa Anglikani wa Mkoa wa Dar es salaam Baba Askofu Valentino Mokiwa, na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na Mwenyekiti wa Wanawake Waislamu Tanzania Hajjat Shamim Khan.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  15 Juni, 2016 .

  0 0


  Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Mary Mashingo akimkabidhi meneja uzalishaji wa kampuni ya Asas Dairies Ltd Bw Lipita Mtimila tuzo baada ya kampuni yake kushinda tuzo ya ubora katika maonyesho ya wiki ya Maziwa Nchini
  Tuzo ya Ushindi ya mwaka 2016
  KAMPUNI ya Asas Dairies Ltd ya mkoani Iringa kwa mara ya nne mfululizo imeendelea kushika nafasi ya kwanza kitaifa uzalishaji wa maziwa nchini . Kampuni hiyo imeshinda tuzo ya wazalishaji wakubwa wa bidhaa bora za maziwa katika mashindano wiki ya maziwa yaliyofanyika juzi kwenye viwanja vya shule ya sekondari Mpechi mkoani Njombe .

  Kampuni hiyo imeibuka mshindi wa kwanza baada ya kuongoza katika nafasi zote tatu za ubora wa bidhaa zilizoshindanishwa katika mashindano hayo .Akikabidhi tuzo hizo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Mary Mashingo pamoja na kupongeza makampuni yaliyoshiriki katika zoezi hilo bado alipongeza kampuni ya Asas Dairies Ltd kwa kufanya vizuri katika mashindano hayo ya ubora wa maziwa nchini

  Alisema kuwa jitihada zilizoonyeshwa na kampuni hiyo ni kubwa na zinapaswa kuigwa na makampuni mengine hapa nchini.Kwani alisema kuwa kuongoza katika nafasi zote zilizoshindaniwa si jambo dogo ni jitihada kubwa zimefanyika na ni hatua ya kujivunia kwa kampuni hiyo.

  Pia aliipongeza bodi ya maziwa Tanzania kwa kuandaa mashindano kama hayo kwani ni sehemu ya kipimo kwa wamiliki wa viwanda vya maziwa nchini na sehemu ya kujitathimini . Kwa upande wake meneja uzalishaji wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Lipita Mtimila alisema kuwa mbali ya kampuni hiyo kuongoza kwa mwaka huu bado ilipata kuongoza katika mashinadano kama haya miaka mitatu nyuma na hii ni mara ya nne kuongoza .

  Katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na bodi ya maziwa Tanzania( TDB) kampuni ya Asas Dairies iliweza kuibuka na ushindi wa jumla baada ya kushinda tuzo zote tatu dhidi ya makapuni mengine ya uzalishaji maziwa yaliyoshiriki katika mashindano hayo .Bw Mtimila aliwataka watanzania kuendelea kuzipenda bidhaa za Asas Dairies Ltd na kuwa lengo la kampuni hiyo ni kuendelea kuzalishaji bidhaa zenye ubora zaidi .Pia alipongeza watanzania na watumiaji wa bidhaa za Asas Dairies Ltd kutokana na ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa kuendelea kutumia maziwa yanayozalishwa na kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Iringa
   Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Mary Mashingo akitembelea banda la kampuni ya Asas dairies Ltd

  Viongozi wakitazama bidhaa za kampuni ya Asas
  Wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja katika maonyesho ya wiki ya Maziwa
  Meneja uzalishaji wa kampuni ya Asas Dairies Ltd Bw Lipita Mtimila akionyesha cheti cha ushindi wa jumla ambacho kampuni hiyo ilikabidhiwa
  Bw Mtimila akionyesha vyeti vya ushindi wa uzalishaji wa bidhaa bora
  Vyeti vya ushindi  Na Matukiodaima Blog

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  BEKI mahiri wa kulia wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Shomari Kapombe, amechaguliwa na mashabiki kuwa Mchezaji Bora wa timu hiyo msimu uliopita ambalo zoezi hilo la kumtafuta mchezaji wa kutwaa tuzo hiyo lilianza rasmi Juni 8 mwaka huu kwa hatua ya awali kabla ya Ijumaa iliyopita kuingia hatua ya fainali iliyohusisha wachezaji sita waliopigiwa kura nyingi zaidi na mashabiki katika akaunti ya Azam FC kwenye mtandao wa kijamii wa facebook.

  Hadi zoezi hilo linafikia tamati Kapombe ameweza kuwabwaga wapinzani wenzake watano kwenye kinyang’anyiro hicho ambao ni Nahodha Msaidizi Himid Mao ‘Ninja’, beki kisiki Pascal Wawa, kipa Aishi Manula na mawinga Farid Mussa na Ramadhan Singano ‘Messi’. Beki huyo ametwaa tuzo hiyo baada ya kujizolea kura 203 kati ya zote 560 zilizokubaliwa, Aishi amemfuatia akiwa nazo 125, Farid (95), Singano (48), Himid (45) na Wawa (44).

  Mashabiki wengi waliompigia kura Kapombe hawakusita kufanya hivyo wakidai alikuwa ni nguzo muhimu kwa Azam FC msimu uliopita baada ya kucheza kwa bidii na kufunga mabao muhimu kwa timu hiyo na hata alipokosekana pengo lake lilionekana huku pia wengine wakimpongeza Aishi Manula aliyeshika nafasi ya pili wakisema naye alifanya kazi kubwa.

  Mbali na tuzo hiyo ya mashabiki, Kapombe pia alifanikiwa kuwa mchezaji pekee wa Azam FC aliyepata Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi inayotolewa na mdhamini wa Ligi Kuu, Kampuni ya Vodacom, akitwaa ya mwezi Januari mwaka huu na moja ya rekodi zake za msimu uliopita, ni kuwa beki pekee wa ligi hiyo aliyefunga mabao mengi kuliko mwingine yoyote akitupiwa wavuni mabao nane huku katika mechi zote ilizocheza Azam FC akicheka na nyavu mara 12 na kutoa pasi za mwisho saba na akicheza jumla ya dakika 3188.

  0 0


  Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza mwendeshaji wa mafunzo hayo, Andrew Christian ambaye yupo Geneva, Switzerland aliyekuwa akitoa elimu kuhusu ukaguzi kwa wafanyakazi
   
  Wakiwa kama wakaguzi wa huduma za afya na usalama kwa wafanyakazi katika maeneo ya kazi, Wakala wa Afya na Usalama sehemu za Kazi (OSHA) wameeleza kuwa wataboresha ukaguzi wao hasa kwa wafanyakazi walio na UKIMWI jinsi wanavyohudumiwa na waajiri wawapo kazini.

  Akizungumza na Mo Blog katika mafunzo ya jinsi ya kufanya kaguzi sehemu za kazi kwa watu walio na UKIMWI, Kaimu meneja usajili na takwimu za afya na Usalama OSHA, Dk. Abdalssalaam Omary, alisema kupitia mafunzo hayo wanataraji kuboresha ukaguzi zao ambazo zifanywa katika maeneo ya kazi ambazo zinakuwa zinawahusu watu walio na UKIMWI.

  “Tunaamini kuwa baada ya mafunzo tutakuwa na maboresho katika kaguzi zetu sababu tumepata nafasi ya kukutana na wenzetu kutoka sehemu nyingine na kubadilishana uelewa kwahiyo tutakuwa tofauti na awali,” alisema Dk. Omary.

  Alisema pamoja na kujipanga kuboresha kaguzi zao alisema kuwa bado wamekuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo kwa muda mwingine zinaweza kuwa zinawafanya wakwame na kueleza changamoto hizo ni pamoja na fedha na madaktari kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzi wafanyakazi.

  Kwa upande wa serikali kupitia Kaimu Kamishna wa Kazi Msaidizi, Rehema Moyo alisema kuna sheria ambazo zimewekwa ambazo zinakataza waajiri kufanya vitendo vya ubaguzi kwa wafanyakazi na hivyo kama kuna waajiri wanawafanyia vitendo ambavyo havikubaliki kisheria basi watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakani kujibu mashitaka yanayowakabili.

  “Sera zipo utekelezaji ndiyo mgumu kuna vitendo vya ubaguzi lakini kujua ndiyo inakuwa changamoto maana ni mpaka muhusika aseme na sheria zipo kama mwajiriwa akikutwa na hatia anaweza hata kufungwa gerezani au kupigwa faini,” alisema Bi. Moyo.

  Nae Mratibu wa maswala yanayohusiana na UKIMWI maeneo ya kazi kutoka Shirika la Kazi (ILO), Getrude Sima, alisema kupitia mafunzo hayo wanaamini washiriki wataweza kupata kitu kipya ambacho kitawasaidia katika kaguzi wanazozifanya ili waweze kutambua zaidi matatizo yanayowakuta wagonjwa wa UKIMWI wawapo kazini na jinsi ya kuwasaidia.
  .
  Mwendeshaji wa mafunzo, Andrew Christian akiwa Geneva, Switzerland ambaye alikuwa akitoa elimu kuhusu ukaguzi kwa wafanyakazi.

  Wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0


  Mkuu wa Hazina wa Benki ya Exim Tanzania,Bw George Sumbusho (kulia) pamoja na Mkuu wa kitengo Huduma za Reja reja wabenki hiyo Bw Rahul Singh (wa pili kulia) wakichangia damu sambamba na wafanyakazi wenzao waliojitokeza makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu duniani .Anaewahudumia ni Ofisa wa Mpango wa taifa wa damu salama (NBTS) Bw. Allen Ligonga.
  Meneja Msaidizi Huduma kwa wateja wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Ally Mandai (kulia) akichangia damu sambamba na wafanyakazi wenzake waliojitokeza makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu duniani .Anaewahudumia ni Ofisa wa Mpango wa taifa wa damu salama (NBTS) Bw. Allen Ligonga.
  Baadhi ya wafanyakazi na wateja wa Benki ya Exim Tanzania waliojitokeza makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu duniani .Anaewahudumia ni Ofisa wa Mpango wa taifa wa damu salama (NBTS) Bw. Allen Ligonga.

  Wafanyakazi wa benki ya Exim, wateja pamoja na watu wengine Tanzania jana walijotokeza kwa wingi kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya uchangiaji damu duniani.

  Akizungumza na waandishi wa habari wakati zoezi hilo likiendelea, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu kutoka benki hiyo Bw. Frederick Kanga alisema hatua hiyo ni muendelezo tu kwa kuwa kuwa wamekuwa wakifanya hivyo tangu mwaka 2010 na lengo kuu kukabiliana na tatizo upungufu wa damu salama kwenye vituo vya afya hapa nchini.

  “Mara zote tumekuwa tukijisikia kuwa na furaha ya ajabu inapofika siku kama hii ya leo kwa kuwa tunaamini kwamba tunapata fursa ya kutimiza wajibu wetu kama sehemu ya jamii lakini pia kwa kufanya hivyo tunakuwa tumeshiriki kuokoa maisha ya wenzetu wanaopoteza maisha kwa kukosa damu salama pale wanapoihitaji,’’ alisema.

  Kauli hiyo ya Bw. Kanga inakwenda sambamba na kauli mbiu ya uchangiaji damu ya mwaka huu inayosema: “Sote tunaunganishwa na damu’’. Kauli mbiu hiyo inalenga kuonyesha namna gani maisha ya watu wenye uhitaji wa damu huokolewa na wenzao wanaojitokeza kuchangia damu.

  Akizungumza wakati akisimamia zoezi hilo Afisa Uhamasishaji na elimu kwa umma kutoka Mpango wa taifa wa damu salama (NBTS) Bi. Fatma Mujungu alisema uhaba wa damu hapa nchini umekuwa ukichangiwa kwa kiasi kikubwa na mtazamo wa Wananchi walio wengi kwamba wapo tayari kuchangia damu pale tu inapohitajiwa na mmoja wa wanandugu wa familia husika.

  “Hivyo basi natoa wito kwa Wananchi mmoja mmoja pamoja na taasisi nyingine kuiga mfano wa benki ya Exim Tanzania ambayo imekuwa na utamaduni wa kuchangia damu kila mwaka ili kuokoa maisha ya watanzania wote,’’ alisema.

  Kwa upande mwingine baadhi ya wafanyakazi na wachangiaji hao walisema wamekuwa wakiguswa na hitaji hilo muhimu la kuchangia damu kila mwaka kwa kuwa wao ni sehemu ya jamii na wanahitaji kuleta mabadiliko ndani ya jamii kwa kuokoa maisha ya wenzao wenye uhitaji wa huduma hiyo muhimu.

  0 0


  0 0

  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni amewataka walipa kodi na ushuru katika Manispaa hiyo kudai stakabadhi za kielektroniki baada ya kufanya malipo ili kuziba mianya ya upotevu wa mapato.

  Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Aron Kagurumjuli alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii juu ya njia wanazozitumia katika ukusanyaji wa ushuru wa Manispaa hiyo.

  “Napenda kuwasisitiza wananchi kuwa unapofanya malipo yoyote ya Manispaa lazima uhakikishe unapewa stakabadhi ya kielekroniki na iwapo hutopewa, unaruhusiwa kutoa taarifa kwa kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi kwenda 0767643460 na utapatiwa maelekezo ya nini cha kufanya”,alisema Kagurumjuli.

  Kagurumjuli ameongeza kuwa Ofisa yeyote atakayekaidi kutoa stakabadhi hizo atachukuliwa hatua kali za kisheria kwani kukwepa kulipa mapato ni kurudisha nyuma uchumi wa nchi.

  Aidha, Mkurugenzi huyo ameyataja maeneo ambayo mwananchi anaweza kulipia kodi au ushuru na kupata stakabadhi za kielekroniki ni Ofisi za Manispaa, Ofisi za Kata, Benki ya CRDB pamoja na watumishi wa Manispaa waliopo katika shughuli maalumu za ufuatiliaji wa kodi na ushuru.

  Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilianza kutumia mfumo wa kulipa kodi na ushuru kwa njia ya kielekroniki mnamo mwaka 2013 , na mwaka 2015 ilipata tuzo ya ukusanyaji bora wa mapato kwa njia hiyo kwa Tanzania na Afrika nzima.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kuzima simu feki  leo  Juni 16 mwaka huu.
  Meneja wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

  Na Chalila kibuda, Globu ya Jamii.
  SIMU ziliingizwa nchini zikiwa hazina kiwango kuzimwa rasmi leo,  katika kuhakikisha kila mtu anatumia simu yenye  kiwango kwa usalama  wa afyanyake na ulinzi wa nchi.

  Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba amesema kuwa katika uzimaji wa simu wameshatoa elimu juu ya simu hizo.
  Kilaba amesema kuwa simu ambazo watu walibadilisha (Flash) nazo zitazimwa kwani  kufanya hivyo ni kosa la kisheria na mtu anayefanya hivyo kifungo chake ni miaka 10 jela.

  Amesema hakuna kitu chochote kinachofanya simu zisiweze kuzimwa hivyo watu wajiandae zoezi hilo na simu zitazozimwa wametakiwa kuzihifadhi katika mazingira salama.

  Aidha amesema katika elimu wametoa hivyo kesho kutakuwa na mkutano wa wadau mbalimbali wa makampuni ya simu, na wamiliki wa maduka ya simu pamoja na mafundi katika kubadilishana mawazo wakati wa kuzima simu feki.

  ‘’Simu feki kesho kuzimwa. Hatutakuwa na mabadiliko ya kuongeza muda au vinginevyo kutokana na elimu iliyotolewa juu simu ya  feki ambazo baada soko kushindikana mjini walipeleka vijijini’’amesema Kilaba  .

  0 0
 • 06/16/16--03:30: Article 17


older | 1 | .... | 881 | 882 | (Page 883) | 884 | 885 | .... | 1898 | newer