Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 872 | 873 | (Page 874) | 875 | 876 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Mtoto Sharon  Mwakifulefule (kushoto) akisalimiana mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Yatima Trust Fund kilichopo Mbagala Chamanzi jijini Dar es Salaam, wakati alipokwenda kituoni hapo  kwa ajili ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa pamoja na watoto wenzake ambapo alitoa msaada wa vyakula na madaftari.
   Mtoto anayelelewa katika kituo cha Yatima Trust Fund cha Mbagala Chamanzi , Abdul ,akiwa na wenzake wakati Mtoto Sharon Mwakifulefule alipokwenda  kituoni hapo  kwa ajili ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa pamoja na watoto wenzake ambapo alitoa msaada wa vyakula na madaftari.
  Watoto wa kituo cha Yatima Trust Fund  cha Mbagala Chamanzi wakionyeshwa na mlezi wa kituo hicho Yessaya Mwakifulefule jinsi ya kutumia simu wakati alipofika hapo paoja na mwanae Sharon ( 7) (hayupo pichani) kituoni hapo  kwa ajili ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa pamoja na watoto wenzake ambapo alitoa msaada wa vyakula na madaftari.
   Sharon Mwakifulefule (7) akiwaelekeza watoto wanaolelewa katika kituo cha Yatima Trust Fund kilichopo Mbagala Chamzanzi jijini Dar es Salaam, jinsi ya kutumia simu wakati alipofika  kituoni hapo  kwa ajili ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa pamoja na watoto wenzake ambapo alitoa msaada wa vyakula na madaftari. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  Sharon Mwakifulefule (7)wapili kulia akiwa na wazazi wake  pamoja na watoto wa kituo cha kulelea yatima cha Yatima Trust Fund  Mbagala Chamanzi jijini Dar es Salaam,wakati alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa  ambayo aliifanya katika kituo hicho.
   Sharon  akiwagawia juice watoto wanaolelelewa katika kituo cha Yatima Trust Fund cha Mbagala Chamanzi ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa( 7) ambapo alitoa msaada wa vyakula na madaftari.
   Sharon ( kulia) akimlisha keki  Yesaya Linus ambayeni mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Yatima Trust Fund kilichopo Mbagala Chamanzi jijini Dar es Salaam, wakishirikiana kukata keki wakati wa kusherekea siku yake ya kuzaliwa(7) iliyofanyika kituoni hapo.
  Mtoto Yesaya Linus akimlisha keki Sharon Mwakifulefule
   Fatma Ali  ambaye ni mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima Trus Fund kilichopo Mbagala Chamanzi akilishwa keki na Sharon Mwakifulefule wakati wa sherehe yake kuzaliwa (7) iliyofanyika kituoni hapo , ambapo alitoa msaada wa vyakula na madaftari kwa watoto wenzake.
  Sharon Yesaya akimkabidhi msaada wa madaftari Fatma Ali  ambaye ni mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima Trus Fund kilichopo Mbagala Chamanzi jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla yake ya  kuzaliwa (7) iliyofanyika kituoni hapo , ambapo alitoa msaada wa vyakula na madaftari kwa watoto wenzake.
  Watoto wanaolelewa katika kituo cha Yatima Trust Fund kilichopo Mbagala Chamanzi jijini Dar es Salaam,  Mwajuma Idd na Halma juma ,wakikabidhiwa msaada wa unga na Sharon Yesaya, wakati wa hafla ya siku yake ya kuzaliwa (7) ambapo alikwenda kuiadhimisha paoja na watoto wenzake  wa kituo hicho.

  0 0

   Mkurugenzi wa masoko TANAPA,Ibrahim Mussa akizungumza kuhusiana na masuala mazima ya masoko ya utalii hapa nchini katika mkutano wa mwaka wa hifadhi za Taifa Tanzania na wahariri pamoja na wanahabari wandamizi kutoka vyuo mbalimbali vya habari katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha VETA mjini Morogoro leo.
  Mwalimu wa uchumi na utalii wa chuo kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti  wa kamati ya shauri wizara ya maliasili na utalii, Profesa Wineaster Anderson akizungumza katika mkutano wa mwaka wa hifadhi za taifa Tanzania na wahariri na wahabari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na utalii wa ndani pamoja na masoko ya utalii wa ndani hapa nchini.
  Baadhi ya Wahariri pamoja na Wanahabari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mada mbalimbali zilnazojadilia kwenye mkutano huo wa mwaka wa hifadhi za Taifa Tanzania,unaoendelea  hivi sasa katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha VETA mjini Morogoro leo.Picha na Avila Kakingo-Globu ya Jamii

  0 0

  MAMA ni miaka tisa (9) bila wewe katika maisha yetu ya kila siku, tunakukumbuka daima. UPENDO uliotuonyesha katika maisha ya kila siku mama hatuna la kusema, umetuacha tukiwa bado tunahitaji mawazo yako. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa muda wote uliokuwa nasi. 

  Ushauri wako tutaendelea kuufuatilia na mema uliyotufundisha. Daima tutaendelea kukumbuka hekima na busara zako huku tukiwa na tumaini la kuwa siku moja tutaonana nawe pamoja na Maria (IA). 

  DAIMA huachwi kukumbukwa na Mumeo George Mapango, wanao Mariam, Eva (Hawa), Jackson, Rose, Patrick (Said) na Richard, Wadogo zako, Kaka zako, Wakwe zako, Marafiki, Wafanyakazi Wenzako pamoja na Wajukuu zako. 

  INNA LILLAH WAYNA ILAYH RAJ’IUN .


  0 0

  Timu nzima MMG chini yake Ankal Issa Michuzi, inawatakia mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ndugu wote katika Imaan ya Dini ya Kiislam, Duniani kote. Hiki ni kipindi muhimu sana kwa waislam wote katika Ibada ya Toba, hivyo tujitahidi kuhimizana kufanya ibada na kumcha Allah Sub Hannahu Wataala. Amin

  Ramadhan Kareem.

  0 0

  Familia ya mchezaji bora Afrika, Mbwana Samatta wakiwa katika picha ya pamoja katika eneo alilikabidhiwa mchezaji huyo kwa ajili ya kujenga kituo cha michezo katika kijiji cha Mwanzega, MKuranga juzi. wa Kwanza kulia ni kaka yake Mbwana, omari, wa tatu ni baba yake mzani na mama yake mlezi.


  NAHODHA wa  Timu  ya Soka ya Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Ali Samatta ameahidi  kujenga kituo maalum nchini cha kuibua na kukuza vipaji vya wanasoka wachanga ili wafikie viwango vya kimataifa.

  Sambamba na  hilo, ameweka azma  ya kukifanya kituo  chake kuwa na wigo mpana wa kuwawezesha vijana wa  kutoka nje ya  Tanzania kuja  kujifunza  soka katika kituo  hicho na kuwapeleka vijana wawili kila mwaka kwenda kujifunza zaidi mchezo huonchini Ubelgiji.

  Hayo  yamebainishwa  na baba wa mwanasoka  huyo wa kimataifa, Ali Samtta alipozungumza kwa niaba ya  mwanae, katika halfa ya kukabidhiwa  ekari tano  za eneo la ujenzi wa kituo hicho kulikofanywa na Mtandao wa Wasanii na Wanamichezo  nchini, (SHIWATA.).

  Hafla ya makabidhiano  hayo yaliyofanyika juzi katika kijiji  cha wasanii kilichopo Mwenzanga, wilayani Mkuranga.

  Akizungumza  kwa niaba ya mwanae, baba wa  nyota  huyo alisema, azma ya Samatta (Mbwana) ni kujenga kituo kikibwa  cha kimataifa ambacho, moja ya madhumuni ni kuendelea kuwaibua na kuwakuza akina 'Samatta'  wengine wajao.

  Alisema,  Salamu alizoziacha Mbwana kwa wasanii kwanza ni kuishukuru SHIWATA kwa hatua ya kutambua mchango wake kitaifa, hivyo, katika kulipa fadhila ni kujenga uwanja utakaokuwa na hadhi ya kimataifa kwa taifa.

  "Niliongea na Mbwana  amenituma niwakilishe salamu zake kwa kwanza kwa  kuishukuru SHIWATA na kisha kueleza nia yake ya kutaka kuendelea kuibua  vipaji  vya  soka la vijana kupitia kituo kitakachojengwa hapa katika kijiji cha wasanii Mwenzange" alisema Ali Samatta na kuongeza. 

  "Engekuwapo  hapa  leo, lakini alilazimika kusafiri mara tu baada ya kumalizika kwa mechi ya Stars dhidi ya Misri, kurejea  Ubelgiji kwa wito wa  haraka, lakini anatarajia kurejea  tena nchini kwa mapumziko, na mimi amenituma nimwakilishe kwa kauli zake hizi"

  Katika  hatua nyingine, mwakilishi wa mgeni rasmi, Nape Mnauye, Bi Leah Kihindi aliipongeza SHIWATA kwa hatua yake ya kuwawekea misingi wanachama wake ili wawe na makazi ya kudumu kupitia kijiji hicho.

  Sambamba na hilo, alilipongeza shirikisho  hilo kwa kutambua mchango wa Mbwana Samatta katika  soka ambako katika sherehe hizo wanachama 35 walikabidhiwa nyumba na misingi ya kujenga nyumba.


  Mwenyekiti wa SHIWATA< Cassim Taalib akiwatoa taarifa fupi ya kijiji hicho alisema lengo ni kuwasaidia wasanii, wanamichezo na waandishi wa habari kujenga nyumba za kuishi ili kujiandaa kwa ajili ya kuishi maisha ya taabu baada ya kustaafu kazi zao.

  SHIWATA inayomiliki ekari 300 za makazi katika kijiji hicho jumla ya wanachama 185 wamnejenga nyumba kwa njia ya kuchangishana.

  0 0

  Meneja wa Kituo Cha Utabiri Kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Bw. Samwel Mbuya akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu mwelekeo wa Hali ya joto na mvua katika kipindi cha juni hadi Agosti 2016 ambapo inatarajiwa kuwa na hali ya baridi kiasi na vipindi vifupi vya mvua. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Bi Monica Mutoni
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)na vyombo vya Habari Leo Jijini Dar es salaam.(Picha na Maelezo).

  MAMLAKA YA HALI YA HEWA (TMA) YATOA MWELEKEO WA HALI YA HEWA KWA KIPINDI CHA JUNI HADI AGOSTI 2016.

  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa mwelekeo wa hali ya hewa kwa kipindi cha Juni hadi Agosti mwaka huu. Akizungumzia kuhusiana na mwelekeo huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri Bw. Samwel Mbuya alisema “Nchi yetu inatarajia kuwa na hali ya baridi kiasi katika kipindi hiki sambamba na vipindi vifupi vya mvua vinavyotarajiwa kujitokeza katika maeneo machache hususanya ukanda wa Ziwa Viktoria na ukanda wa pwani ya Kaskazini (Visiwa vya Unguja na Pemba).

  Katika kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti 2016, maeneo mengi ya nchi yanarajiwa kuwa makavu na yenye hali ya baridi kiasi katika majira haya ya kipupwe. Mifumo ya hali ya hewa inaonesha matarajio ya hali ya joto la wastani hadi chini ya wastani katika maeneo yaliyopo Kusini-magharibi mwa nchi. 

  Hata hivyo,katika msimu wa Kipupwe wa mwaka huu maeneo mengi ya nchi yanatarajiwa kuwa na joto la wastani hadi juu ya wastani. Aidha, izingatiwe kuwa hali ya ubaridi inatarajiwa zaidi nyakati za usiku hadi mapema asubuhi. “Aliendelea kueleza sababu za hali hiyo kuwa ni pamoja na kupungua kwa joto la bahari katika eneo la ukanda wa Tropiki la bahari ya Pasifiki sambamba na Joto la baharí katikaeneo la magharibi wa bahari ya Hindi kuwa la wastani kwa kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti 2016”. 

  Aidha, joto katika bahari ya Atlantiki linatarajiwa kuwa chini ya wastani. Hali hiyo inatarajiwa kusababisha upepo kuvuma kutoka magharibi ukielekea mashariki hususankatika maeneo ya Ukanda wa Ziwa Viktoria. Joto la bahari la juu ya wastani linatarajiwa katika eneo la ncha ya kusini ya bara la Afrika hivyo kuathiri msukumo wa upepo wa kusi.

  Kwa upande mwengine, Afisa Uhusiano wa TMA, Bi. Monica Mutoni alitoa msisitizo kwa wananchi kufuatilia taarifa hususan za tahadhari zinazotolewa na Mamlaka kupitia vyombo mbalimbali vya habari, tovuti ya Mamlaka n.k ili kuokoa maisha na mali. Bi. Monica alisema “Hivi karibuni TMA imekuwa ikitoa tahadhari mbalimbali ikiwa ni pamoja na za kuwepo kwa upepo mkali na mawimbi makubwa kwenye ukanda wa Bahari Hindi, Maziwa na nchi kavu hivyo ni vyema wananchi hasa wale watumiaji wa bahari na maziwa kuchukua hatua stahiki pindi taarifa kama hizo zinapotolewa”.

  Aidha, TMA ilipongeza sekta mbalimbalipamoja na Taasisi, Mamlaka za Serikali na jamii kwa ujumla kwa hatua stahiki zilizochukuliwa katika kipindi chamsimu wa mvua za Masika 2016 kwa kutumia Taarifa, Agalizona Tahadhari za utabiri zilizotolewa na Mamlaka. Ni wazi kuwa kwa hatua hizo madhara ambayo yangeweza kujitokeza yalidhibitiwa na hivyo kuchangia katika kufanikisha mipango na utekelezaji wa shuguli za kiuchumi na kijamii katika kipindi husika.

  Kwa tarifa ya kina kuhusiana na mwelekeo wa hali ya hewa kwa mkoa wako ingia kwenye tovuti ya TMA www.meteo.go.tz au tembelea ofisi zetu

  IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

  0 0

   Wawakilishi wa Jumuiya ya Sadakatasi ya Uturuki wakiwa na wenyeji wao wa Jumuiya ya Muzdalifa ya Zanzibar wakiwasili katika kisiwa cha Tumbatu Jongowe kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali yenye thamani ya shiling milioni kumi na nane. 
   Wananchi wa Tumbatu Jongoe wakishusha vipolo vyenye misaada mbalimbali kwaajili ya mwezi Mtukufu wa Ramazani.   
   Baadhi ya wazee wa Kisiwa cha Tumbatu Jongoe wakiwa kwenye foleni kwaajili ya kupokea misada mbalimbali iliyotolewa na Jumuiya ya Sadakatasi ya Uturuki. 
   atibu Mkuu wa Jumuiya ya Sadakatasi ya Uturuki Emrah Eugin akimkabidhi kipolo chenye Mchele, unga, sukari na mafuta ya kula kwa ajili ya mwezi Mtukufu wa Ramazan mmoja wa wazee wa Tumbatu Jongoe.
   Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Sadakatasi ya Uturuki Emrah Eugin wakatikati na mwenziwe Huseyin Kursun (kushoto) wakiwapa nguo watoto wa Tumbatu Jongoe ikiwa ni miongoni mwatarati iliyojiwekea Jumuiya hiyo. 
  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Sadakatasi ya Uturuki Emrah Eugin akiagana na watoto wa kisiwa cha Tumbatu Jongoe, mara baada ya kumaliza kutoa sadaka ya vitu mbalimbali vyenye thamani ya milioni kumi na nane. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.


  0 0


  TAARIFA KWA UMMA

   Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa imetangaza sifa na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.  Taarifa hizo zinazosambazwa, pamoja na mambo mengine, zinaeleza kuwa sifa zitakazotumika kuwa ni ufaulu wa waombaji katika mitihani yao ya elimu ya sekondari na diploma. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa maelezo rasmi yanapatikana katika tovuti ya Bodi ya Mikopo na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).  Bodi inapenda kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu kuwa taarifa hizo sio za kweli na kuwaomba wawe na subira wakati Bodi inakamilisha taratibu za uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017.  Baada ya kukamilika kwa taratibu hizo, mwongozo wa utoaji mikopo utatolewa rasmi na kutangazwa kwa umma kupitia njia mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari na tovuti ya Bodi ya Mikopo (www.heslb.go.tz).

  IMETOLEWA NA:

  KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI,

  BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,

  JUMANNE, JUNI 7, 2016

  Taarifa hii pia inapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz)

  0 0

  TAARIFA YA JESHI LA POLISI 

  Ndugu zangu waandishi wa habari,

  Katika siku za hivi karibuni, Jeshi la Polisi nchini, limepokea taarifa kutoka kwa baadhi ya vyama vya siasa wakitaka kufanya mikutano na maandamano . hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia vyanzo vyake vya mbalimbali vya habari limebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi (Civil disorder).

  Aidha vyama vingine vya siasa vimeonyesha dhamira ya kupinga kile ambacho kitasemwa na wapinzani wao.

  Vyanzo hivyo vya habari vimebainisha kwamba upo uwezekano mkubwa wa kutokea vurugu baina ya makundi mawili ya kisiasa.

  Kwa hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linapiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia tarehe 07/06/2016 hadi hapo hali ya usalama itakapotengemaa.

  Jeshi la Polisi linawataka wanasiasa kuacha mara moja kuwashinikiza wananchi kutotii sheria za nchi. 

  Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hili.

  Aidha Jeshi la Polisi linawataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi hii na badala yake linawasihi waendelee kushirikiana katika kujenga umoja wa nchi hii.

  Asanteni sana kwa kunisikiliza .

  Imetolewa na:-
  Nsato M. Mssanzya – CP
  Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo
  Makao Makuu ya Polisi. 

  0 0  0 0

  Mkuu wa Idara ya Uhandisi Mazingira (Environmental Engineering) Dr. Fredrick Salukele akiwaelezea wanafunzi matumizi ya vifaa mbalimbali vitumikavyo kwenye shughuli za ufundishaji, utafiti na utoaji ushauri wa kitaalam, mfano wa vifaa hivyo ni Gaschromatograph kinachoonekana kwenye picha.
  Wanafunzi wa Shule ya Mtakatifu Maximilian walipotemblea Maabara ya Sayansi ya Mazingira na Tekinolojia ya Chuo Kikuu Ardhi. Maabara hiyo hutumika kwa ajili ya shughuli za Ufundishaji, Utafiti na Uhauri wa kitaalamu katika fani ya Sayansi ya Mazingira.
  Wanafunzi wakiangalia kwa makini baadhi ya kazi za ubunifu majengo zilizo fanywa na wanafunzi wa Skuli ya Ubunifu Majengo wa Chuo Kikuu Ardhi. Kubuni aina mbalimbali za majengo ni moja kati ya mahitaji kwenye mtaala wa kufundishia program ya Usanifu Majengo ya Chuo Kikuu Ardhi
  Mtaalam kutoka Skuli ya Sayansi ya Jiomatiki wa Chuo Kikuu Ardhi Bw. Pius Lugomela (mwenye shati la bluu), akitoa malezo kuhusu vifaa mbalimbali vya upimaji ramani vilivyoko kwenye maabara ya Skuli iyo.Vifaa kwenye maabara hiyo pia hutumika kwa ajili ya shuguli za ufundishaji, utafiti na ushauri wa kitaalamu kwenye maenneo ya upimaji ardhi na ramani.


  Na. Hadija Maulid - Chuo Kikuu Ardhi. 

  Chuo Kikuu Ardhi kimetoa wito kwa wanafunzi wanaosoma darasa la saba kote nchini kufanya bidii katika masomo ya Sayansi na Hisabati ili waweze kujenga msingi imara na kuandaa mazingira ya kujiunga na fani za Sayansi katika elimu ya Sekondari na vyuo vikuu.

  Wito huo huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na baadhi ya wataalamu wa Chuo hicho mara baada ya kuwapokea wanafuzi 84 wa Shule ya Msingi ya Mtakatifu Maximilian waliotembelea maeneo mbalimbali ya chuo hicho kwa lengo la kujifunza majukumu ya chuo hicho na elimu inayotolewa.

  Wakiwa chuoni hapo wanafunzi hao wamepata fursa ya kuitembelea Skuli ya Sayansi ya Mazingira na Teknolojia (Environmental Science and Technology) Skuli ya Ubunifu Majengo (School of Architecture and Design) na Skuli ya Sayansi ya Jiomatiki na Tekinolojia (School of Geospatial Sciences and Technology).

  Aidha, Wanafunzi hao walipata fursa ya kuuliza maswali mbali mbali kwa wataalamu.

  Ziara hiyo imelenga kuwahamasisha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo ya Sayansi ili waweze kupata alama za juu zitakazowawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita na kisha kujiunga na Chuo kikuu Ardhi ili baadaye wawe wataalamu katika fani mbalimbali za Ardhi na Mazingira.

  0 0

  SERIKALI kupitia Bodi ya Utalii Nchini (TTB) na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), katika mwaka 2016/17 imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 2.7 kwa ajili ya kuitangaza sekta ya utalii ndani na nje ya nchi.

  Akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum (CCM), Maria Kangoye, leo Bungeni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani alisema bajeti hiyo ni ongezeko la asilimia 14.7 za fedha za Serikali zilizotengwa katika bajeti ya mwaka ya 2015/16.

  Makani alisema Serikali itaendelea kuboresha sekta ya utalii kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo na vyanzo vingine vya mapato kama ilivyoanishwa katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano 2016/17- 2020/21.

  Alisema Serikali pia imepanga kuimarisha Chuo cha Utalii katika kampasi za Bustani iliyopo Dar es Salaam, Temeke na Arusha ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi na umahiri wa wakufunzi, kuboresha upatikanaji wa vifaa vya kufindishia na kuboresha miundombinu ya kampasi hizo.

  “Kuhusu uimarishaji wa miundombinu, Wizara yangu imetenga jumla ya Tsh. Milioni 500 katika bajeti ya mwaka 2016/17 ili kukamilisha ujenzi wa jengo la Utalii katika Bustani ya Chuo cha Utalii Tanzania” alisema Mhandisi Makani

  Aidha Mhandisi Makani alisema kuwa Chuo cha Utalii Tanzania kwa kushrikiana na Chuo cha Vancouver University cha Canada kupitia mradi wa ISTEP uliopo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Ufundi kitaanzisha mafunzo ya Uongozi katika shahada kuanzia mwezi septemba 2018.

  Aidha Mhandisi Makani alisema Serikali inaendelea kuelekeza nguvu katika vyuo vilivyopo kwa kuongeza idadi ya wahitimu wa ngazi ya kati na baadaye wa ngazi ya shahada, ambapo kwa sasa Chuo cha Utalii Tanzania kitaanza kuboresha utoaji wa mafunzo katika tansia za ukarimu na Utalii katika ngazi ya shahada.

  0 0

  Na Ismail Ngayonga-MAELEZO

  SERIKALI imesema kisiwa cha shungimbili kilichopo Wilayani Mafia mkoani Pwani hakijauzwa kwa kampuni ya Zululand ya Afrika Kusini na badala yake kimeingizwa katika uwekezaji kupitia kampuni ya Thanda Tanzania Ltd inayojenga hoteli ya kitalii.

  Akijibu swali la Mbunge wa Mwanakwerekwe (CCM), Ali Said Khamis, leo Bungeni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani alisema Alisema uwekezaji huo umepitia taratibu zote za Serikali na pindi utakapokamilika mwekezaji atatekeleza wajibu wake ikiwemo kulipia tozo zote kwa mamlaka zinazohusika kwa mujibu wa sheria.

  Makani alisema alisema kisiwa cha shungimbili ni miongoni mwa visiwa 15 ambayo ni maeneo tengefu yanayosimamiwa na Taasisi ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu nchini (MPRU).

  Mhandisi Makani alisema MPRU iliianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge na.29 ya mwaka 1994 ambapo miongoni mwa majukumu yake ni kusimamia maeneo yote yaliyotangazwa kuwa hifadhi za Bahari na maeneo tengefu ya bahari.

  Aliongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ndiyo yenye dhamana ya kuingia mikataba  yote ya kimataifa yenye maslahi kwa Taifa.

  Aidha akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Singida, Martha Mlatta, Makani alisema Serikali inaendelea kuvijengea uwezo vyuo vya utalii vilivyopo nchini ili kuhakikisha kuwa wahitimu wake wanakuwa mahiri katika soko la ajira nchini.

  “Mfanyabiashara akitafuta mwajiriwa ni lazima ahakikishe kuwa anaye mwajiri anakuwa na sifa zote za kumletea faida, hivyo na sisi pia tunataka wahitimu wetu katika vyuo vya utalii wanakuwa wanapata umahiri wa kutosha ili waweze kuajiriwa katika nafasi za juu kabisa katika kampuni yoyote”   alisema Makani.

  Mbunge Mlatta alitaka swali lake la nyongeza alitaka kufahamu Serikali ina mikakati ipi katika kuhakikisha kuwa wahitimu wa Tanzania wanapewa nafasi za juu za kazi katika hoteli za kimataifa.

  0 0

  Vanessa Mdee Mdee (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi  Mwendeshaji wa TTB Bi Devota Mdachi (katikati), Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa TTB (kushoto), Afisa Uhusiano Mkuu wa TTB Bw. Geofrey Tengeneza na Meneja Masoko wa TTB  Bw. Geofrey Meena.
   Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Bi Devota Mdachi (kulia) akijadliana jambo na Vanessa Mdee  leo walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania.

  Mwanamuziki maarufu wa Bongo fleva nchini Tanzania Vanessa Mdee amesema yuko tayari kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) katika kuvitangaza vivutio vya Utalii vya Tanzania ndani nab nje ya nchi.
  Mdee ametoa ahadi hiyo alipotembelea ofisi za Bodi ya Utalii leo jijini Dar es salaam na kufanya mazungumzo na uongozi wa Bodi hiyo kuhusu namna TTB inavyoweza kushirikiana nae katika kutangaza na utalii wa Tanzania.

  Ujio huo wa mwanamziki huyo ambaye pia ni nguli wa miondoko ya R&B, Hip Hop, na Afro Pop ulifuatia mwaliko wa uongozi wa TTB kuomba kukutana na kuzungumza na mwanamuziki huyo katika azma na mkakati wa TTB kuwatumia wasanii na watu wengine maarufu nchini katika kutangaza Utalii wa Tanzania.

  Katika mazungumzo hayo Vanessa Mdee amesema yuko tayari kufanya kazi na TTB kwa lengo la kutangaza vivutio vya Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwa balozi wa hiari wa Utalii “ Tutaendelea kujadiliana kuona ni namna gani nzuri tunaweza kushirikiana, na mimi niko tayari kuifanya kazi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa Balozi wa hiari wa Utalii” alisema Mdee.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Bi Devota Mdachi alielezea kufurahishwa kweke na utayari wa Vanessa Mdee katika kuunga mkono juhudi za TTB katika kuutangaza na kuundeleza Utalii wa ndani sambamba na ule wa Kimataifa, na kuahidi kukamilisha haraka mchakato mazungumzo hayo na hatimaye kusainiwa kwa makubaliano baina ya pande hizo mbili.

  Katika kutekeleza jukumu lake la kuitangaza vivutio vya Utalii Tanzania ndani na nje ya nchi Bodi ya Utalii Tanzania imekuwa ikibuni na kutekeleza mbinu na mikakati mbalimbali kama vile kuweka matangazo katika televisheni za kimataifa, kutumia mitandao ya kijamii viwanja vya mipira ya miguu, kuandaa safari za waandishi wa habari, kutumia watu maarufu na njia nyinginezo nyingi.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano 2016/2017-2020/2021 unalenga kuboresha maisha ya Watanzania wengi kwa kuhakikisha Sekta zinazoajiri watu wengi na walio masikini zinakuwa kwa kasi.

  Akizindua Mpango huo leo (Jumanne, Juni 7, 2016) katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali itahakikisha Sekta za Kilimo, Viwanda, Uvuvi na Mifugo zinakua kwa kasi ya kuridhisha ili kuongeza fursa za ajira na kupunguza umasikini.

  Amesema utekelezaji wa Mpango huo ambao umefungamanisha maendeleo ya viwanda na maendeleo ya watu na unatazamiwa kujibu changamoto ya umasikini Tanzania.

  Waziri Mkuu amesema katika Mpango huo kuna maeneo mbalimbali ya  vipaumbele yaliyoainishwa katika Mpango huo ni miradi mikubwa kama ya chuma cha Liganga, kufufua shirika la Ndege, Makaa ya Mawe Mchuchuma, ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha standard Gauge ambayo matokeo yake yanatarajiwa kuwa kichocheo cha utekelezaji wa miradi mingine.

  “Tunatarajia ifikapo mwaka 2025 tuwe tumejenga nchi ambayo ina maisha bora, yenye amani, umoja na utawala bora, jamii inayojifunza na iliyoelimika, yenye uwezo wa kuzalisha na kuwa na ukuaji wa uchumi endelevu na wenye ushindani,” amesema.

  Waziri Mkuu Majaliwa amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha ukuaji huo wa uchumi unakuwa shirikishi zaidi katika utekelezaji wa Mpango huu na kwamba uendelezaji wa viwanda ndio utakaoleta mafanikio makubwa karika mwelekeo huo.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa amesema jumla ya viwanda 39 kati ya 106 vilivyobinafsishwa kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ambavyo vilikuwa vya vinazalisha bidhaa za chuma, ngozi, korosho zana za kilimo, sabuni na mafuta ya kupikia wamevifunga na kutoviendeleza.

  Kufuatia hatua hiyo Waziri Mkuu Majaliwa amesema Wizara ya Fedha na Mipango kupitia kwa Msajili wa Hazina itaendelea na zoezi la kuvirejesha viwanda hivyo Serikalini ili waangalie utaratibu mwingine ulio bora wa kuviendeleza kwa kupitia Mpango huo wa Maendeleo.

  Amesema Mpango huo ambao utajikita zaidi katika kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuendeleza viwanda vikubwa, vya kati na vidogo na vile vilivyobinafsishwa ili kuongeza fursa za ajira na kipato kwa wananchi wengi.

  Akizungumzia kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano ambao utahitimishwa Juni 30, 2016 Serikali ilifanikiwa kutekeleza miradi ya maendeleo kama ujenzi wa barabara za lami na madaraja ya Kigamboni, Maligisu Nagoo, Mbutu na Ruhekei.

  Pia ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam (km 542), ujenzi wa mitambo ya kuchakata gesi katika maeneo ya Madimba na Songosongo, ujenzi wa vituo vya kupokelea gesi vya Somanga-Fungu na Kinyerezi.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  07 Juni, 2016                   

  0 0


  Na Daudi Manongi-MAELEZO


  Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Yamungu kayandabila amesema kuwa serikali iko mbioni kuunda chombo cha kudhibiti upandaji wa kodi za nyumba za kupanga.Dkt Kayandabila ameyasema hayo leo hii jijini Dare s Salaam alipokuwa akizungumza katika kipindi cha asubuhi cha Power Breakfast kinachorushwa na Clouds Fm.

  “Sisi kama serikali tumesikia kilio cha wapangaji na tuko mbioni kumaliza tatizo hili kwa kuunda chombo kitakachodhibiti upandaji wa kodi hizi za nyumba kiholela,tumeshapokea kesi nyingi sana kutoka kwa wananchi na hivyo tumejipanga kulitatua kabisa tatizo hili”Alisema Dkt Yamungu.


  Aidha katibu mkuu huyo amewaasa wapangaji wa nyumba za kupanga kuhakikisha wanakuwa na mikataba ya kisheria yenye makubaliano ya pande zote mbili kupunguza migongano isiyokuwa ya kilazima na kushauri kama watashindwa kumudu gharama za mwanasheria wanaweza kuwatumia wenyeviti wa serikali za mitaa kama mashaidi katika kusaini mikataba yao.


  Awali ya yote Dkt Yamungu alizungumzia kukamilika kwa Sera ya nyumba ambayo iko mbioni kukamilika ikizungumzia masuala haya yote na kwa kiasi kikubwa sera hii itapunguza migogoro mingi ya masuala ya nyumba kwa ujumla.


  Mwaka huu mwezi wa nne Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi aliweka wazi Bungeni nia ya serikali kutungwa kwa sheria itakayounda chombo cha kudhibiti upandaji wa kodi za nyumba za kupanga. 

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea mfano wa hundi ya Bilioni 12 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Mkurugenzi wa uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani Kobwey ikiwa ni bakaa ya tume hiyo zilizopangwa kutumika na Tume ya Uchaguzi katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka 2015.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea mfano wa hundi ya Bilioni 12 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Mkurugenzi wa uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani Kobwey ikiwa ni bakaa ya tume hiyo zilizopangwa kutumika na Tume ya Uchaguzi katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka 2015.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakimsiliza Mkurugenzi wa uchaguzi Bw. Ramadhani Kailima Kobwey wakati akitoa taarifa ya namna Tume ya Uchaguzi ilivyookoa kiasi cha shilingi Bilioni 12 zilizopangwa kutumika katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka 2015.
  0 0

  Jonas Kamaleki-MAELEZO

  Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 inatarajia kuajiri walimu 35,411 katika shule za msingi na sekondari ili kuongeza tija katika sekta ya elimu nchini.

  Hatua hiyo ni mkakati wa Serikali wa kukabiliana na upungufu wa walimu 22,460 wa masomo ya Sayansi na Hisabati katika shule za sekondari, hatua inayoelezwa kuwafanya wanafunzi kutofanya vizuri katika masomo hayo.

  Hayo yamesemwa jana Bungeni na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Buyugu Kasuku Samson Bilago aliyetaka kujua idadi ya walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati wanaohitajika ili kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014.

  Profesa Ndalichako ameongeza kuwa idadi ya walimu wa sekondari waliopo kwa sasa ni 88, 999 kati ya hao walimu 18, 545 ni wa masomo ya Sayansi na Hisabati ambapo 70, 454 ni wa masomo ya Lugha, Sanaa na Biashara.

  Kuhusu uboreshaji wa miundombinu mashuleni Profesa Ndalichako amesema Serikali kupitia Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji imeendelea kutenga fedha katika bajeti ya kila mwaka kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu mashuleni, ujenzi wa nyumba za walimu, vyoo vya walimu na wanafunzi na ujenzi wa madarasa.

  Aidha, Profesa Ndalichako amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2015/2016 serikali ilitenga bilioni 67.83 ambazo zimeshapokelewa katika Halmashauri mbali mbali na zimetumika kwa ajili ya ukarabati, ujenzi na umaliziaji wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa vyoo na uwekaji wa umeme katika shule za sekondari 528 nchini.

  0 0

  Mgeni rasmi Kaimu RAS Mkoa wa Rukwa Bw. Abubakary Kunenge, akitoa hotuba wakati wa ufungizi wa semina ya elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa wakulima wa MVIWATA Rukwa, Kulia ni Mwenyekiti wa MVIWATA Rukwa Bi. Lydia Ruhilo na kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Mohamed Nyasama.
  Sehemu ya Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Sumbawanga wakisikiliza kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa kutoka SSRA wakati wa Semina ya elimu ya Hifadhi ya Jamii Mkoani Rukwa hivi karibuni.
  Afisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Samuel Nzunda akiwasilisha mada wakati wa semina ya elimu ya Hiafadhi ya Jamii mkoani Rukwa.
  Wawakilishi kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), wakiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi wa Chuo cha VETA-Kigoma mara baada ya semina ya elimu ya Hifadhi ya Jamii iliyoendeshwa na SSRA mkoani humo hivi karibuni.
  Bi Carina Wangwe, kutoka SSRA akifafanua jambo wakati wa semina ya elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa wadau mkoani Kigoma.
  Afisa kutoka SSRA, Bw. Ally Masaninga akiwasilisha mada wakati wa semina ya elimu ya Hifadhi ya Jamii mkoani Kigoma hivi karibuni.
  Wanafunzi wa Chuo cha UfundiStadi – VETA Kigoma wakisikiliza kwa makini mada kutoka kwa maofisa wa SSRA. 
  Wawakilishi wa SSRA wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Newma-Kigoma mara baada ya semina ya elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa wanafunzi wa Chuo hicho.
  Bw. Onorius Njole, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kutoka SSRA akifafanua jambo wakati wa semina kwa wadau wa Chuo cha Ualimu Mpanda.
  Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi – VETA Mpanda wakisikiliza kwa makini mada kutoka SSRA.
  Afisa kutoka SSRA Bi. Beatrice Ngong’ho akigawa vifaa kwa wanafunzi wa Chuo Cha Ualimu Mpanda wakati wa semina ya elimu ya Hifadhi ya Jamii mkoani Katavi.
  Sehemu ya wafanyakazi na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA mkoani Mpanda wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka SSRA wakati wa semina za elimu kwa Umma mkoani humo.

  0 0


  Tarehe 8 Juni ni siku ya Bahari Duniani. Nipe Fagio itaadhimisha siku hii kupitia shughuli mbalimbali za kuelimisha na uhamashishaji ikiwemo kampeni katika mitandao ya kijamii pamoja na michezo ya kuigiza kwenye jukwaa la wazi, katika jitihada za kutafuta ushirikiano wa umma katika swala la kuweka bahari zetu safi, hivyo basi zenye afya. Taka katika bahari inazidi kuwa miongoni mwa vitisho vikubwa kwa dunia yetu. 

  Watafiti waliobobea katika tafiti za bahari wametoa ripoti kuwa asilimia 40 ya sakafu ya bahari yetu imefunikwa kwa vipande vidogo vidogo vya plastiki vinavyoelea pamoja na taka nyingine. Hii inaleta madhara makubwa sio tu kwa viumbe vya bahari bali pia kwa afya zetu wenyewe, mienendo na usalama wa maisha yetu. Kwa masikitiko, maji ya bahari jijini Dar es Salaam pia yana hadithi yake. 

  Shughuli za kawaida kama kuogolea katika bahari au kula samaki, ambazo hapo awali zilichukuliwa kama vigezo vya mwenendo wa maisha yenye afya sasa hivi vimegubikwa na utata. Kutokana na ongezeko la ukuaji wa miji pamoja na hali duni iliyopo ya usafi na ukosefu wa huduma ya uzoaji taka, sehemu kubwa ya taka kutoka mijini inaibuka katika hali ya uchafuzi wa mazingira kwenye maeneo yasiyo rasmi kinyume cha sheria kama mito na mifereji ambayo huelekea moja kwa moja baharini. 

  Bila shaka, jambo hili linaleta madhara makubwa sana kwa afya ya umma na mazingira yetu. Plastiki haswa,ndiyo inayochukuwa mamia ya miaka kuoza, na inazidi kuwa mojawapo ya taka zenye utata katika mikondo yetu ya maji. Wanyama wa baharini huishia kula plastiki hizi wakifikiri ni chakula. Hii inaleta madhara makubwa kwa usalama wa viumbe vya baharini, lakini watafiti pia wanahofia afya za binadamu wanaotegemea samaki kama chanzo kikuu cha mlo wao. 

  Nipe Fagio, shirikisho la kijamii linalojikita katika kuboresha usafi, afya na usalama wa jiji, lilikusanya kilo 2,515 za taka katika siku moja tu ya usafi, maeneo ya Coco Beach Septemba iliyopita. Taka iliyokusanywa kwa wingi zaidi ni vizibo vya chupa, mifuko ya kufungia chakula, viatu na mifuko ya plastiki. 

  Nipe Fagio kwa mara nyingine inaomba ushirikiano wa umma katika kampeni ya Siku ya Bahari Duniani ambayo itakuwa na shughuli zifuatazo: Mchezo wa kuigiza katika jukwaa la wazi Coco Beach, siku ya Jumapili tarehe 12 Juni, saa kumi hadi kumi na moja jioni. Kiingilio ni bure Better Bag Challenge (Nani Mwenye Mfuko Bora), itahamasisha kukataa kutumia mifuko ya plastiki na badala yake kutumia mifuko ambayo itaweza kutumika tena na tena. #SelfiefortheSea (# Pichakwaajiliyabahari), Umma unahamsishwa kutuma picha zao zikiambatanishwa na ujumbe wenye ahadi yake kusaidia juhudi za kuweka bahari yetu safi na yenye afya.

older | 1 | .... | 872 | 873 | (Page 874) | 875 | 876 | .... | 1897 | newer