Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

MSASA WA SDGS WAENDELEA UDOM, VITIVO VYAKAMILIKA

0
0
Ninajisikia kuelimika na kuelewa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu kiasi ya kwamba ninaweza sasa kuwaelimisha marafiki, vijana wenzangu na familia. Elimu hii hapo awali sikuwa nayo, sikuwa naelewa vyema malengo haya. Ukomo wa mpango huu wa dunia ni mwaka 2030 wakati ambapo mimi nitakuwa na umri wa miaka 40. Nataka kuwa sehemu ya mashuhuda wa mafanikio katika utekelezaji wake na ndio maana nataka kutimiza wajibu wangu kwa kupeleka elimu hii kwa wengine.” anasema Jane, mmoja wa washiriki wa semina.

VIJANA 1000 na wanazuoni 200 wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) wamepatiwa mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu Duniani kwa nia ya kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Dodoma.
Kazi ya kufunza malengo hayo ilifanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo hapa nchini kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi ya Umoja wa Mataifa (UN) kuwezesha uelewa kwa tumaini kuwafanya wananchi hasa vijana kutambua wajibu wao katika kutekeleza malengo hayo.Mafunzo hayo katika Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ni mwendelezo wa mafunzo yaliyozinduliwa Arusha wiki iliyopita na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez.
Mtaalamu wa mawasiliano katika Ofisi ya Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akiendesha mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu Duniani (SDGs) kwa nia ya kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Dodoma kwa wanafunzi wa vitivo mbalimbali na walimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) yaliyomalizika jana chuoni hapo.(Picha na Modewjiblog)

Mafunzo hayo yalifanywa kwa kundi la vijana 50 kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania ili waende kusambaza uelewa wa malengo hayo kwa vijana wenzao nchini kote.

Inatarajiwa kuwa zaidi ya vijana elfu 20 watakuwa wamepatiwa mafunzo katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.Akizungumza katika kampasi ya UDOM Bw. Rodriguez alisema kwamba Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yanahitaji ushirikiano wa watu wote ili kuyafanikisha kama ilivyokusudiwa. Malengo ya Maendeleo Endelevu ukomo wake ni mwaka 2030.

Aliwapongeza wanachuo na wanazuoni kwa kujikita kwao kuelewa Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo ndiyo malengo ya dunia ili kuweza kuyasimamia na kuyatekeleza.Pia alizungumzia umuhimu wa vijana kushiriki katika masuala ya maendeleo hasa kwa kuzingatia kwamba asilimia 60 ya wananchi wa Tanzania ni vijana.

“Mna wajibu mkubwa kwa vijana wenzenu” alisema Bw. Rodriguez na kueleza kwamba amefurahishwa kuona kwamba vijana na wanazuoni 1,200 wameahidi kuwa walimu na mabalozi wa malengo ya maendeleo endelevu majumbani kwao, katika taasisi zao na katika jamii inayowazunguka.
Mmoja wa wanafunzi wa UDOM akipitia makabrasha ya SDGs wakati wa mafunzo hayo.
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Muya Said akitoa maoni wakati wa mafunzo ya siku mbili ya Malengo ya Maendeleo Endelevu Duniani (SDGs) kwa wanafunzi na walimu wa UDOM yenye nia ya kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Dodoma yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini na kumalizika jana chuoni hapo.
Mwanafunzi wa Digrii ya kwanza ya Mifumo ya Biashara katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Janeth Dutu akiuliza swali kwa mkufunzi wa mafunzo hayo (hayupo pichani) wakati wa mafunzo ya siku mbili ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDGs) kwa wanafunzi na walimu wa UDOM yenye nia ya kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Dodoma ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini na kumalizika jana chuoni hapo.
Mkufunzi wa mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDGs), Hoyce Temu akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo wakati zoezi la maswali na majibu.
Mhadhiri Msaidizi wa Maendelelo ya Jamii katika Chuo cha Sayansi za Jamii, Sanaa na Lugha (CHSS) katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Angelo Shimbi akitoa maoni wakati wa mafunzo ya siku mbili ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDGs) kwa wanafunzi na walimu wa UDOM yenye nia ya kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Dodoma yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini na kumalizika jana chuoni hapo.
Pichani juu na chini ni Sehemu ya wanafunzi na walimu wa UDOM wakimsikiliza mkufunzi Hoyce Temu (hayupo pichani) kwa makini wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyomalizika jana chuoni hapo.

Alisema katika hilo Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia kuhakikisha kwamba wake kwa waume na vijana wanatekeleza wajibu wao kwa kushiriki vyema katika mipango ya maendeleo yenye kulenga kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu duniani.
Alisema wajibu wa kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu duniani kunategemea watu wote na hasa vijana.

Akipongeza juhudi za kuelimisha za Umoja wa Mataifa, Profesa Flora Fabian kutoka UDOM, alisema chuo hicho kimefurahishwa kuwa moja ya vituo vya kufunza mabalozi vijana wa kusambaza elimu na wajibu katika kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu.
Alisema malengo hayo ya Dunia ni lazima yajulikane kwa kila mmoja; huku akiwataka wanazuoni kuyazungumza katika kazi zao za kila siku, katika tafiti na ripoti kama ilivyo kwa wanafunzi ambao wanastahili kupikwa kuwa katika nafasi ya kuweza kuchambua malengo hayo kwa kuwa na takwimu na taarifa sahihi.

Alipongeza uamuzi wa utoaji elimu wa Umoja wa Mataifa na kuamini kwamba watasambaza elimu hiyo kwa vyuo vikuu vyote nchini Tanzania.

Septemba 2015, viongozi kutoka nchi 193 duniani walitia saini Malengo ya Maendeleo Endelevu duniani. Malengo hayo mapya yanatarajiwa kufanyiwa kazi katika kipindi cha miaka 15 huku ikiweka pamoja shughuli za maendeleo ya kijamii, kiuchumi yanayojali mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.
Beatrice Mkiramweni kutoka Ofisi ya Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, akipitia makabrasha ya SDGs wakati wa mafunzo ya siku mbili ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDGs) kwa wanafunzi na walimu wa UDOM yenye nia ya kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Dodoma yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini na kumalizika jana chuoni hapo.
Mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDGs) kwa wanafunzi na walimu wa UDOM yakiendelea chuoni hapo.
Kutoka kushoto ni Mhadhiri Msaidizi wa Idara ya Development Studies -UDOM, Edson Baradyana, Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa, Mtaalamu wa Upangaji na Usimamizi wa Miradi -PRO UDOM, Radhia Rajabu, Mhitimu wa kidato cha sita, Aisha Msantu wa Asasi ya Vijana wa Umoja Taifa Tanzania (YUNA) katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Kutoka kushoto ni Mtaalamu wa mawasiliano katika Ofisi ya Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu, Mhitimu wa kidato cha sita, Aisha Msantu wa Asasi ya Vijana wa Umoja Taifa Tanzania (YUNA) pamoja na Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa katika picha ya ukumbusho mara baada ya kuhitimisha mafunzo.
Picha ya pamoja ya baadhi ya wanafunzi wa UDOM walioshiriki kwenye mafunzo ya SDGs yaliyomalizika jana chuoni hapo. (Picha zaidi ingia hapa)

MADIWANI KILWA NA RUANGWA WAPIGWA MSASA UTEKELEZAJI WA MIFUMO YA UTOAJI HUDUMA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Akitoa Hotuba yake ya Ufunguzi ambapo Pia Aliwataka Madiwani Kuacha Siasa katika Kutekeleza Maendeleo ya Halmashauri zao,Kulia ni Mkurugenzi wa Shughuli za Mikoa Mradi wa Ps,Bw Conrad Mbuya
Madiwani wa Ruangwa Pamoja Na Mwandishi wa Vikao Vya Baraza la Madiwani Ruangwa,Bahati kasabano (Kulia)wakifuatilia mafunzo hayo
Afisa Mshauri wa Masuala ya Utawala Bora PS3, Nazar Sola akitoa Elimu kwa Madiwani juu ya Utekelezaji wa Mifumo ya Utendaji na Utoaji Huduma
Baadhi ya madiwani na watendaji wa halmashauri za Kilwa na Ruangwa Mkoani Lindi wakifuatilia jambo katika semina Elekezi ya Kujenga Uelewa kwa Halmashauri kupitia Mradi kuimarisha Uwezo wa Kutoa Huduma kwa Jamii Chini ya Utekelezaji wa Mradi wa PS3 Unaofadhiliwa na USAID
Lukelo Mhenga Mhasibu Msaidizi(kushoto) pamoja na Fina Maziku wote wa PS 3 wakifuatilia mada katika mafunzoa Hayo ambapo Halmashauri za Wilaya zao za Kilwa na Ruangwa zikiwa ni Halmashauri za Awali kati ya 6 za Mkoa Huo Zilizoanza utekelezaji wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya sekta za umma(PS3) katika sekta za afya, elimu na kilimo.
Bw Joel Shimba,Mshauri wa Utawala Bora PS3(Kushoto )Wakielekezana jambo na bw Victor Msoma,Mshauri wa Fedha PS3(Kulia)Kuhusiana na Mafunzo ya madiwani wa Kilwa na Ruangwa Huku Bi Nseya Kipilyango,Mshauri wa Mifumo ya Tehama wa PS 3(Katikati)Akifuatilia kwa Umakini.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi Akilakiwa na Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini,Suleiman Bungara(BWEGE)Mara Baada ya kuwasili katika Ukumbi wa MM Hotel Mjini Lindi kwa Ajili ya Ufunguzi wa Mafunzo Elekezi kwa Madiwani Wa Halmashauri za Kilwa na Ruangwa ili Kuelewa Jinsi ya Kutekeleza Mfumo ya PS 3.


Na Abdulaziz Video,Lindi

Madiwani wa Halmashauri za Wilaya ya Kilwa na Ruangwa Mkoani Lindi Zimeanza Utekelezaji wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID) kwa Kupatiwa Mafunzo ya Siku 4 na Kuratibiwa na Tamisemi

Kuanza kwa Hatua Hiyo kunafuatia kumalizika kwa Mafunzo kwa Watendaji wa Halmshauri 6 Za Mkoa wa Lindi juu ya Namna ya Kushiriki na Kutekeleza Mradi huo Utakaotekelezwa kwa Kipindi cha Miaka 5 Ijayo

Akifungua Mafunzo hayo,Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi amezitaka Halmashauri Hizo Kufuatilia kwa Umakini Mafunzo yanayotolewa na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa Hombolo ili Kupata Uelewa Juu ya Uendeshaji wa Halmashauri

‘’ Madiwani ni kiungo muhimu baina ya serikali na watendaji wa serikali madiwani Musipokuwa Vizuri Mtaburuzwa na Watendaji hususan katika Utendaji na Utekelezaji wa Miradi hasa Ikiwa Diwani Una Tabia ya Kuomba omba na Kukopa kwa Mkurugenzi au Mkuu wa Idara Lazima Mjipime Nyie Ndio wamiliki wa Halmashauri au hamjijui?’’Alimalizia Zambi

Rais Dkt. Magufuli akabidhiwa Bakaa ya Bilion 12

0
0

NEWZ ALERT: TAARIFA YA KIFO CHA PROF.ESTOMITH NKYA

0
0
Chumba cha Globu ya jamii hivi punde kimepokea taarifa ya kifo cha Mume wa aliyekuwa Waziri wa Serikali ya awamu ya Nne na Mweka Hazina wa CCM Mkoa wa Morogoro Mhe.Dr.Lucy Nkya amefariki dunia,taarifa zinaeleza kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.

Rest in Peace 
Prof.Estomih Nkya

TAARIFA YA MAZISHI ; Msiba wa mzee wetu Prof E J Nkya Baba Mzazi Wa Mnec Wakili Jonas Nkya na Mume Wa aliyekuwa waziri wa Jinsia,Watoto na Afya Dr Lucy Nkya Kwa sasa Upo Nyumbani kwake Morogoro Kilakala, Mazishi yatafanyika Mkoa Wa Kilimanjaro Machame Siku Ya Jumamosi, Kwa Mtakao pata nafasi Karibuni Tukamhifadhi Mzee wetu. Mungu Ailaze Roho Ya Marehemu Mahala Pema, RIP Prof Nkya.

Airtel na VETA WAANZISHA MAFUNZO YA STADI ZA UFUNDI KUPITIA APPLICATION YA SIMU - VSOMO

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Ufundi (VETA), Geoffrey Sabuni wakifanya ishara ya uzinduzi wa mafunzo ya stadi za ufundi kupitia mtandao wa simu ya mkononi yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO, katika hafla iliyofanyika kwenye Chuo cha Veta cha Kipawa jijini Dar es Salaam jana.  Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula na (kulia) ni Mkurugenzi wa VETA, Kanda ya Dar es Salaam, Habib Bukko. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Ufundi (VETA), Geoffrey Sabuni wakifanya ishara ya uzinduzi wa mafunzo ya stadi za ufundi kupitia mtandao wa simu ya mkononi yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO, katika hafla iliyofanyika kwenye Chuo cha Veta cha Kipawa jijini Dar es Salaam jana. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya stadi za ufundi kupitia mtandao wa simu ya mkononi yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO, katika hafla iliyofanyika kwenye Chuo cha Veta cha Kipawa jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kulia) ni Mkuu wa Chuo cha VETA – Kipawa, Mhandisi Lucius Luteganya, Mkurugenzi wa VETA, Kanda ya Dar es Salaam, Habib Bukko, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Ufundi (VETA), Geoffrey Sabuni na Mkurugenzi Mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Ufundi (VETA), Geoffrey Sabuni  akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya stadi za ufundi kupitia mtandao wa simu ya mkononi yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO, katika hafla iliyofanyika kwenye Chuo cha Veta cha Kipawa jijini Dar es Salaam jana
  Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Ufundi (VETA), Geoffrey Sabuni  wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya utambulisho wa program mpya ya VSOMO.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akiteta jambo na wafanyakazi wa Airtel wakati wa utambulisho wa  program mpya ya VSOMO
 mmoja kati ya vijana waliosoma kwa njia ya mtandao chini ya mpango wa VSOMO Saleh Shomari akikabithiwa cheti chake jana wakati wa utambulisho wa mpango huu utakaowawezesha watanzania kusoma masomo ya ufundi yanayotolewa na VETA kupitia simu zao za mkononi
baadhi ya wageni wakifatilia utambulisho wa wa mpango huu utakaowawezesha watanzania kusoma masomo ya ufundi yanayotolewa na VETA kupitia simu zao za mkononi.


Airtel na VETA WAANZISHA MAFUNZO YA STADI ZA UFUNDI KUPITIA APPLICATION YA SIMU - VSOMO

·         Mfumo wa kwanza wa mafunzo ya ufundi kwa njia ya mtandao Tanzania
·         Kuleta ufarahisi na gharama nafuu
·         Mafunzo kupatikana kupitia application maalum

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa kijamii wa Airtel FURSA  imeshirikiana na Mamlaka ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA) kuanzisha application mpya ijulikanayo kama “VSOMO”  yaani VETA SOMO, ili kuwawezesha vijana kupata kozi mbalimbali zinazotolewa katika vituo vya VETA nchini kupitia simu za mkononi . Kuanzishwa kwa VSOMO itasaidia kupanua wigo wa mpango wa Airtel FURSA na kuwafikia vijana wengi zaidi nchini. 

Akiongea  kuhusu uhusiano huo, Mkurugenzi mkuu wa Airtel Sunil Colaso alisema”  tumeona ni muhimu kuwekeza kwenye mpango huu wa VSOMO kwa kuwa tumeona vijana wengi wana kiu na haja ya kutaka kujifunza na kuhitimu mafunzo ili kukuza biashara zao na kupata taaluma zitakazowawezesha kujiajiri. Matumizi ya simu za kisasa yanakuwa kila siku, mpaka sasa takribani wateja milioni 10 wanatumia simu za kisasa na kati yao 70% ni vijana. Hivyo VSOMO itawafikia vijana wengi zaidi nchini kwa urahisi zaidi.Na ndio maana tunauza simu zetu kwa bei ndogo ya hadi Tshs elfu 80,000/=kuhamasisha mafunzi kwa kupitia njia ya simu za mkononi”.

“Tunaamini ushirikiano huu kati ya VETA na Airtel FURSA utawawezesha mamilioni ya vijana wakitanzania kupata mafunzo ya ufundi yanayotolewa na VETA wakati wowote na mahali popote kupitia simu zao za mkononi.   Tunauhakika application hii ya VSOMO itachochea kukua kwa elimu kwa vijana wengi na kuwawezesha kuwa na wafanyabiashara na wafanyakazi bora walio na nyenzo zinazohitajika katika kuleta ufanisi”. Aliongeza Colaso

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Bwana Geoffrey G Sabuni alisema “ nafurahi kuwa sehemu ya utambulisho wa kihistoria wakuanzishwa kwa mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu yenye lengo la kuwapatia watanzania nafasi ya kujiunga kwa wingi katika stadi za ufundi.  Bwana Sabuni aliwapongeza timu nzima iliyoshiriki katika kuanzisha ubunifu huu wa VSOMO na kusema ni jambo litakalowezesha watanzania kwa mara ya kwanza katika historia ya ufundi stadi kuweza kuwa wataalamu watakaopeleka nchi katika uchumi wa kati.  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA alisisitiza VSOMO inaendana na malengo ya VETA ya kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojifunza mafunzo ya ufundi na hivyo kufanya vizuri kwa mafunzo haya kwa hatua hii ya awali kutapelekea kutanua wigo zaidi ili kufikia vijana wengi zaidi

Kwa upande wake Mkuu wa chuo Veta Kipawa, Eng. Lucius Luteganya alithibitisha kuwa Mafunzo kwa njia ya mtandao  yamezoeleka sana duniani lakini kwa Tanzania hii ni mara ya kwanza kuanzishwa kwa mafunzo ya ufundi kwa njia ya mtandao. Kila mwaka VETA inapokea maombi ya kujiunga na kozi mbalimbali toka kwa vijana zaidi ya elfu 15 nchini  na theluthi tatu ya maombi hayo ndo yanayokubaliwa na kupokelewa katika vituo vyetu nchini na kuacha theluthi mbili bila kupata fursa ya mafunzo. VSOMO kwa kiasi kikubwa kitaongeza uwezo wetu wa kufundisha watanzania wengi zaidi hususani vijana  hivyo kuongeza idadi ya watu wenye ujuzi na kuchochea uchumi wa nchi kukua kwa kasi zaidi, alisema Luteganya

” ili kuhakikisha tunasimamia viwango vya elimu vilivyowekwa na VETA, Eng. Luteganya aliongeza kwamba “ wale wote watakaojiunga na VSOMO watatakiwa kufanya mtihani ili kufudhu mafunzo ya vitendo yatakayotolewa na VETA katika vituo vyao nchi nzima. Vyeti vya kuhitimu mafunzo vitatolewa kwa wale watakaofaulu mafunzo katika hatua zote mbili ya nadharia na vitendo. Alithibithisha.

Akiongea kuhusu mpango wa VSOMO, Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya alisema  “mafunzo kwa njia ya mtandao ni rahisi  na yatapatikana kwa wateja wa Airtel wenye simu za aina ya android.  Mteja atatakiwa kupakua ya VSOMO kwenye orodha ya menu yake ya simu sehemu ya google play store na kujiandikisha  bure bila gharama zozote.  Mara baada ya kumaliza masomo yake kwa 40% mwanafunzi atatakiwa kwenda kwenye kituo cha VETA kilichopo karibu nae na kujiandikisha kwaajili ya mafunzo kwa vitendo ambayo yatachukua muda wa wiki 2 kumaliza ikiwa ni sawa na masaa 60  na ndipo atakapokaa kwajili ya mtihani na kutakiwa kufaulu kwa 60% “alisisitiza

Singano alisema” Mwanafunzi atatahiniwa na kisha kuandikishwa na kutakiwa kulipia kiasi cha ada yenye punguzo shilingi 120,000/= kwa kupitia Airtel Money kwa kupiga *150*60#.. Tunatoa wito kwa vijana kutumia fursa hii ya kipekee ili kupata mafunzo ya ufundi kwa urahisi na gharama nafuu kwani gharama ya masomo iko chini zaidi.”


MWAKILISHI WA JIMBO LA MALINDI AKABIDHI MSAADA WA SH. MILIONI MOJA NA LAKI TATU KWA AJILI YA UNUNUZI WA VIFAA VYA MAJI.

0
0
MWAKILISHI wa Jimbo la Malindi Mohamed Ahamada Salum pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Maliasili na Usafirishaji Zanzibar akizungumza na Msaidizi wa Sheha wa Shehiya ya Gulioni Amour Abdalla Amour (kulia) kabla ya kumkabidhi Msaada huo.
MWAKILISHI wa Jimbo la Malindi Mohamed Ahamada Salum akimkabidhi fedha taslimu (sh.1,300,000) Msaidizi wa Sheha wa Shehiya ya Gulioni Amour Abdalla Amour kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya bomba la maji lilopasuka Mtaa Mfenesi Mazizi Shehiya ya Gulioni Mjini Zanzibar.
MSAIDIZI wa Sheha wa Shehiya ya Gulioni Amour Abdalla Amour akimshukuru Mwakilishi wa Jimbo hilo mara baada ya kukabidhiwa msaada huo.
MWAKILISHI wa Jimbo la Malindi Mohamed Ahamada Salum akijionea maji sehemu inayovujisha Hapo Mfenesi Mazizi Shehiya ya Gulioni Mjini Zanzibar.(picha na Abdalla Omar - Habari Maelezo Zanzibar.

MKUTANO MKUU WA MTANDAO WA MASHIRIKA YA WAZEE TANZANIA WAZINDULIWA

0
0

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu (Mb.) amezitaka Halmashauri zote nchini kutoa vitambulisho kwa wazee waliopo katika Halmashauri zao. Haya ameyasema leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mtandao wa Mashirika ya Wazee, uliofanyika Mkoani Dodoma katika Ukumbi wa Maktaba Kuu ya Mkoa.
Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb.) Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mtandao wa Mashirika ya Wazee Tanzania.
Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb.) Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akihutubia wazee walioshiriki katika Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Mashirika ya Wazee Tanzania

Akihutubia katika uzinduzi wa Mkutano huo Mheshimiwa Waziri Ummy alizitaka Halmashauri kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao wa kutoa vitambulisho kwa wazee ili kuwezesha utambuzi wa wazee waliopo katika Halmashauri zao hususan katika utoaji huduma na mahitaji mbalimbali.

Mfano wa kitambulisho kinachotolewa kwa wazee wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasuru.

Waziri Ummy alisisitiza kuwa Halmashauri zinatakiwa kutekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya “Mzee Kwanza” hususan katika utoaji wa huduma za afya ambapo kila kituo cha Afya cha Umma kinatakiwa kiwe na chumba na watumishi maalum wa kuhudumia wazee. Pia ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanakuwa na regista ya Wazee kwa kuainisha pia ujuzi wa wazee hao.

Mheshimiwa Waziri Ummy alieleza kuwa Serikali inatarajia kuwasilisha muswada wa sheria ya Wazee Bungeni Mwezi Septemba mwaka huu. Pia, aliwahakikishia wazee kuwa tatizo la upatikanaji wa dawa kwa wazee litapatiwa ufumbuzi kwa kiasi kikubwa kuanzia mwezi Julai 2016.

LEAT YAWATAKA WANANCHI KUHIFADHI MAZINGIRA NA MALIASILI

0
0
Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Asumpta Mshama akihutubia wananchi wakati wa sherehe za siku ya mazingira duniani, katika kijiji cha Lugodalutali, wilaya ya Mufindi.
kikundi cha sanaa kutoka kijiji cha mapogoro kikihamasisha utunzaji wa mazingira na maliasili ktk sherehe za siku ya mazingira zilizo fanyika tarehe 3 June 2016 kijijini Lugodalutali. Kikundi hiki kinalelewa na Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT).
LEAT yagawa vitabu na vipeperushi vinavyotoa elimu ya mazingira na maliasili.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) imewaasa wananchi kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa mazingira na maliasili na kuzitaka mamlaka za usimamizi wa mazingira na maliasili kutimiza wajibu wao kwakuwa serikali imewaamini na kuwapa jukumu hilo.

Akizungumza na wananchi wa wilaya ya Mufindi katika maadhimisho ya siku ya mazingira iliyofanyika katika kijiji cha Lugoda Lutali wilayani Mufindi mkoani Iringa Afisa Mawasiliano wa LEAT Miriam Mshana ,alisema kuwa uharibifu wa mazingira umechangiwa kwa sehemu kubwa na shughuli za binadamu ikiwa ni pamoja na ukataji miti ovyo bila kupata vibali na uvunaji haramu wa wanyamapori, usio rafiki kiuchumi na kimazingira.

Mshana alisema, uvunaji wa kasi hasa wa misitu umeathiri na kuchangia mabadiliko ya tabia nchi, kuiweka nchi katika hatari ya kuwa jangwa. Uvunaji haramu wa wanyamapori hususan tembo umeipa hasara taifa.Kwa mujibu wa ripoti ya Mtaalam Mashuhuri wa tafiti za tembo duniani, Ian Douglas Hamilton, kwa mara ya kwanza mwaka 1976 alifanya utafiti wa angani, Tanzania kwa ujumla ilikuwa na tembo 316,000, ambayo ilikuwa idadi kubwa sana ikilinganishwa na maeneo mengine duniani’’’’’alisema mshana .Kwakufanya hivyo tutakuwa tunaitikia wito wa kaulimbiu ya mwaka 2016 ya siku ya mazingira duniani-‘Shiriki kufanya dunia mahali pazuri’. 

Jowika Ksunga ni mkuu wa wilaya ya Mufindi nae alisema, Mwaka 1976, mbuga ya Selou pamoja na maeneo jirani ilikuwa na idadi ya tembo109,000,Utafiti uliofanywa mwaka 2013, ulibaini kuwa mbuga ya Selou ilikuwa na tembo 13,084 pekee.Kasunga alisema takwimu hizo zinaashiria hatari ya kutoweka kabisa kwa tembo katika nchi yetu na itaathiri biashara ya utalii ambayo ilikuwa ikitoa mchango mkubwa katika pato la taifa.


"Maeneo mengi ya mijini yamechafuliwa kwa utupaji taka ovyo, hivyo kuharibu mandhari ya miji yetu na kuchangia katika magonjwa ya milipuko ikiwemo kuhara na kipindupindu, alisema Kasuga.Alisema, utupaji taka ngumu na zenye sumu karibu na makazi ya watu au vyanzo vya maji, umeleta athari kubwa kiafya kwakuwa kemikali hizo hupenya ardhini na kudhuru ardhi na vyanzo vya maji, hasa kwa wananchi wanoishi karibu na viwanda na sehemu za uchimbaji madini.

“Inasikitisha kuwa wamiliki wa viwanda vingi na machimbo ya madini wanakiuka sheria ya mazingira lakini pia wameshindwa kuwajibika kwa jamii zinazo wazunguka ambazo ndio wadau wakubwa wa biashara zao, kwa kaidi kuchukua hatua za kuzuia uharibifu wa mazingira hata baada ya athari kutokea”, alisema Jowika

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Asumpta Mshama alisema kuwa shirika la LEAT limekuwa mstari wa mbele kwa zaidi ya miaka 20, katika kusimamia mazingira nchini katika sekta ya madini, viwanda, machinjio na mazingira kwa ujumla.Asumpta alisema taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyotolewa mwezi Aprili, 2016 inaonesha takribani watu milioni 2 hufa kila mwaka duniani na zaidi ya watu bilioni moja hupatwa na magonjwa yanayo sababishwa na uchafuzi wa mazingira.

"Iwapo serikali, wananchi na wamiliki wa viwanda na machimbo ya madini, kila mmoja akitimiza wajibu wa kutunza mazingira tutakuwa natekeleza haki ya kuishi, haki ya afya bora na ustawi, kama ambavyo serikali ilivyo ridhia katika mikataba mbalimbali ya kimataifa ikiwemo mkataba wa Stockholm nchini Sweden na Rio De janeiro nchini Brazil"alisema Asumpta.

MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA(TCAA) WATOA MSAADA WA KOMPYUTA KWA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU WA AKILI WA SHULE YA MSINGI MTAMBANI BOKO DAR ES SALAAM

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa AngaTanzania.(TCAA), Hamza Johari(kushoto), akikabidhi msaada wa Kompyuta kwa wanafunzi wenye mahitaji maluum wenye ulemavu wa akili wa shule ya Msingi Mtambani, iliyopo Boko jijiniI Dar es salaam. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mwalimu Mkuu msaidizi wa Shule hiyo Mariana Saso na Mkuu wa Kitengo Maalumu cha Wanafunzi wenye Ulemavu wa akili wa shule hiyo Asaph Maerere.Hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya TCAA Ukonga, Banana.
Mkuu wa Kitengo Maalumu cha Wanafunzi wenye Ulemavu wa akili wa shule ya msingi Mtambani iliyopo Boko jijini Dar es Salaam, Asaph Maerere. akiwa na wanafunzi wake wakiwa wamebeba kompyuta mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa AngaTanzania.(TCAA), Hamza Johar(hayupo pichani) .
Wanafunzi wenye mahitaji maluum ya ulemavu wa akili wa shule ya Msingi Mtambani, iliyopo Boko jijini Dar es salaam,wakifurahia komputa mara baada ya kukabidhiwa msaada na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa AngaTanzania.(TCAA), Hamza Johar(hayupo pichani)hafla hiyo Hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya TCAA Ukonga, Banana.

WAZIRI LUKUVI AZINDUA BARAZA LA ARDHI WILAYA YA LUSHOTO MKOANI TANGA

0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akikata utepe kuashiria kuzindua Ofisi ya Baraza la Ardhi la Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga ambako wakazi wa wilaya hiyo walikuwa wakilazimika kusafiri umbali mrefu kwenda wilayani Korogwe kuitafuta haki yao pindi wanapokumbwa na utata katika ardhi.
Waziri Lukuvi akikagua Ofisi mpya ya Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi wilayani Lushoto mkoani Tanga baada ya kuizindua jana asubuhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akiwahutubia wananchi wa wilayani Lushoto mara baada ya kuzindua ofisi mpya za Baraza la Ardhi wilayani Lushoto jana.
Jengo lililo na Ofisi mpya za Baraza la Ardhi Wilayani Lushoto mkoani Tanga linavyoonekana katika picha.
Samani zilizopo kwenye ofisi za Baraza la Ardhi wilayani Lushoto Mkoani Tanga linavyoonekana pichani.
Samani zilizomo ndani ya jengo hilo la Baraza la Ardhi wilayani Lushoto zinavyoonekana.
Waziri Lukuvi akihutubia wananchi wa Lukuvi mara baada ya kuzindua ofisi hizo mpya za Baraza la Ardhi wilayani Lushoto.
Akipokea mchango wa wadau wa Usambara Investment waliojitolea rima 10 za karatasi kwaajili ya matumizi ya ofisi hizo.

Akisikiliza malalamiko ya mmoja wa wakazi wa Wilaya ya Lushoto mara baada ya kuzindua ofisi mpya za Baraza

Ongezeko la ajali lapelekea Polisi kukamata makosa kumi kila siku

0
0
Jeshi la Polisi limesema kuwa ongezeko la makosa ya watumiaji wa barabara limechangia jeshi hilo kuagiza askari wake kukamata watumiaji kumi kila siku wanaovunja sheria za barabarani.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi, Kikosi cha usalama barabarani Mohammed R. Mpinga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo, jijini Dar es Salaam.

Kamanda Mpinga amesema kuwa kumekuwa na ongezekezo kubwa la uvunjifu wa sheria za barabarani kwa kipindi cha Januari hadi Mei mwaka huu ambapo katika kipindi hicho makosa 290,161 zaidi yaliyokamatwa tofauti na mwaka jana.

Alisema kwa kipindi cha Januari hadi Mei 2015 jumla ya makosa 484,034 yalikamatwa nchi nzima wakati kwa kipindi cha Januari mpaka Mei 2016 jumla ya makosa 774,195 yalikamatwa Tanzania bara.

“Kwa mfano kwa kipindi cha Januari hadi Mei mwaka 2015 jumla ya makosa ya usalama barabarani 484,034 yalikamatwa katika mikoa yote Tanzania Bara na kwa kipindi kama hicho cha Januari hadi Mei mwaka 2016 jumla ya makosa 774,195 yalikamatwa pia katika mikoa yote Tanzania Bara” alisema Kamanda Mpinga.

Akizungumzai hoja ya kuweka kiwango cha ukamataji wa makosa kwa askari wa jeshi hilo, Kamanda Mpinga alisema kuwa Polisi haiwezi kuweka idadi ya makosa ya kukamata wakati madereva wanaendelea kufanya makosa barabarani na ajali zinaendelea kutokea.

“Askari wameelekezwa wakamate makosa mengi iwezekanavyo kutokana na kuendelea kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba madereva wengi Barabarani hawazingatii sheria za Usalama Barabarani hivyo kusababisha ajali,” alisema Kamanda Mpinga.Aidha Kamanda Mpinga amewatahadharisha madereva wote kuacha kufanya makosa Barabarani kwani Jeshi la Polisi halitawavumilia, litawakamata na kuwachukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria.

Makosa yanayofanywa na madereva wengi ni pamoja na kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari (Overtaking), kupita taa nyekundu, kuendesha kwa mwendo kasi, kuendesha wakiwa wamelewa, madereva bodaboda kutovaa kofia ngumu, kubeba mishikaki, kutokuwa na leseni na pikipiki kutokuwa na Bima.

Serikali yatenga bilioni 11,820 kwa miradi ya Maendeleo 2016/17 Jonas Kamaleki

0
0
 Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Phillip Mpango mara baada ya kuwasilisha hotuba ya taaarifa ya hali ya uchumi 2015 na mpango wa maendeleo wa taifa 2016/17 mjini Dodoma .

Serikali imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 11,820.503 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa mwaka wa Fedha 2016/17.Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Philip Mpango wakati akitoa hotuba kuhusu taarifa ya hali ya uchumi nchini na mpango wa maendeleo wa taifa 2016/17.

Waziri Mpango amesema kuwa kiwango hicho ni sawa na asilimia 40 ya bajeti yote ya serikali na kuongeza kuwa fedha za ndani ni shilingi bilioni 8,702.697 ambazo ni sawa na asiliia 74 ya bajeti ya maendeleo na fedha za nje ni shilingi bilioni 3,117.805 sawa na aslimia 26 ya maendeleo.Aidha, Mpango amesema kuwa sekta binafsi inatarajiwa kuwekeza kiwango kikubwa cha fedha ili kuanzisha na kuendeleza viwanda ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango huo.

“ Kwa ujumla fedha za maendeleo zimeelekezwa zaidi katika miradi inayolenga kuendeleza viwanda kama vile uchukuzi,ujenzi, nishati, kilimo, maji, elimu na afya,”amesema Waziri Mpango.

Ameongeza kuwa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2016/17 umeainisha miradi mikubwa ya kielelezo ambayo itapewa msisitizo katika utekelezaji wake.

Waziri Mpango ameitaja miradi hiyo kuwa ni mradi wa makaa ya mawe ya Mchuchuma, mradi wa chuma Liganga, ujenzi wa reli mpya kati ya Dar – Kigoma na Tabora- Mwanza na matawi yake Isaka- Kigali/Keza- Msongati na Kaliua- Mpanda kwa kiwango cha standard gauge.

Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2016/17 utategemea zaidi ushiriki wa sekta binafsi.

HOTUBA YA HALI YA UCHUMI MWAKA 2015 NA MPANGO WA MAENDELEO 2016/2017 ILIYOSOMWA BUNGENI DODOMA NA WAZIRI WA FEDHA

0
0

RC KAGERA MEJA JENERALI MSTAAFU SALUM KIJUU AFANYA ZIARA KIWANDA CHA KAGERA SUGAR

0
0
 Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akikagua stoo ya sukari katika kiwanda cha kagera sugar kuona akiba ya sukari iliyobakia sambamba na kujionea hali halisi ya uzalishaji wa sukari kiwandani hapo.
 Mkuu wa mkoa wa kagera  Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akisikiliza taarifa ya kiwanda cha kagera sugar kutoka kwa meneja mkuu wa kiwanda hicho(hayupo pichani)katika ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho.Lengo la ziara hiyo ikiwa ni kuona akiba ya sukari iliyobakia sambamba na kujionea hali halisi ya uzalishaji wa sukari kiwandani hapo.Picha na Editha Karlo,Globu ya Jamii-Kigoma
 Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu (mwenye suti)akiwa na viongozi wa kiwanda cha kagera sugar wakati alipofanya ziara yake kiwandani hapo
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja jenerali staafu Salum Kijuu na ujumbe wake wakiangalia sehemu ya maji yaliyojaa kwenye shamba la miwa la kiwanda cha kagera sugar,hali hiyo ilipelekea kiwanda kusimamisha uzalishaji
 Baadhi ya mifuko ya sukari iliyohifadhiwa katika stoo ya kiwanda cha kagera sugar
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akipanda moja ya trekita linalofanya kazi katika mashamba ya miwa ya kagera sugar

WAZIRI WA AFYA AZINDUA BARAZA LA USHAURI LA AFYA YA JAMII NA MAZINGIRA

0
0
Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akisoma baadhi ya vifungu vya sheria ya Baraza la Ushauri la Afya ya Jamii na Mazingira kabla ya kulizindua Baraza hilo katika hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi sheria Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Afya ya Jamii na Mazingira Dk. Omar Juma Khatib mara baada ya kulizindua.
Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Afya ya Jamii na Mazingira Dk. Omar Juma Khatib akizungumza na wajumbe wa Baraza hilo wakati wa uzinduzi, kushoto yake Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo.
Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Afya ya Jamii na Mazingira Dk. Omar Juma Khatib akizungumza na wajumbe wa Baraza hilo wakati wa uzinduzi, kushoto yake Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo.
Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akimtakia Kheri Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Afya ya Jamii na Mazingira Dk. Omar Juma Khatib katika utendaji wa kazi zake. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.


Na KhadijaKhamis –Maelezo Zanzibar 8/06/2016.

Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo amelizindua rasmi Baraza la Ushauri la Afya ya Jamii na Mazingira lenye wajumbe nane kutoka sekta za Serikali na sekta binafsi .

Akizindua Baraza hilo katika Wizara ya Afya Mnazimmoja, alisema lengo la kuundwa Baraza hilo ni kudhibiti hali ya afya na mazingira ili kuisaidia jamii kujiepusha na maradhi ya mripuko na maradhi ya kuambukiza.

Alisema Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Muhammed Shein alimteuwa Mwenyekiuti wa Baraza hilo mwaka 2013 lakini kutoakana na kutokuwepo wajumbe ambao huteuliwa na Waziri anaehusika na Afya lilishindwa kufanyakazi kwa muda wote.

Aliwataka wajumbe hao kuwa wabunifu katika kutafuta fedha za kusaidia kuendesha kazi bila kutegemea Bajeti ya Wizara kwani fedha wanazopata ni kidogo na haziwezi kuendesha Baraza kwa ufanisi.Ameeleza matumaini yake kwa wajumbe hao, kutokana na umahiri wao wa masuala ya Afya na Mazingira, watafanyakazi kwa mashirikiano na kuleta ufanisi mkubwa kwa jamii ambayo imetuzunguka .

Nae Mwenyekiti wa Baraza hilo Omar Juma Khatib alimshukuru Waziri wa Afya kwa kuona umuhimu wa kuwepo Baraza hilo na kuharakisha kuteuwa wajumbe kuanza kazi rasmi.Ameahidi kuwa atashirikiana na wajumbe kuhakikisha kuwa wanapunguza vifo vinavyotokana na mazingira machafu na kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa taratibu na sheria zilizowekwa .

“Wajumbe kazi iliyopo mbele yetu ni muhimu sana kwani inagusa maisha ya watu wetu, hivyo tunapaswa kutoa michango na mapendekezo yetu katika kufanikisha kazi hii, ”alisisitiza Mwenyekiti.Wajumbe wa Baraza hilo wamemshukuru Waziri kutokana na muda mfupi tokea achukue nafasi hiyo kuona kunaumuhimu wa kuundwa rasmi Baraza kwa kufanya uteuzi wa wajumbe.

Wameahidi kuwa watatoa ushirikiano wa karibu kwa Mwenyekiti wao ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa na Serikali ya kuundwa Baraza la Ushauri wa Afya na Mazingira yanafikiwa .

IDARAYA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

RAIS MAGUFULI AFUTA HATI YA MASHAMBA YA MKONGE YALIYOTELEKEZWA MKOANI TANGA

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli amefuta hati ya mashamba ya Mkonge, yenye hekta zaidi ya 5,000 yaliyokuwa yametelekezwa na kuwa mapori ambayo hayaendelezwi kufuatia malalamiko ya wakazi wa zaidi ya 2,000 wa kijiji cha Kibaranga kuhangaikia maeneo ya kilimo na kusababisha migogoro ya mara kwa mara baina yao.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibaranga katika mkutano wa hadhara, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi amesema hili ni shamba la tano kufutwa na Mheshimiwa Rais katika mkoa wa Tanga kufuatia wawekezaji waliopewa hati ya kuyaendeleza kushindwa kutekeleza makubalino.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella amesema Serikali mkoa wa Tanga imepewa jukumu la kugawa ardhi hiyo watahakikisha kuwa wanaweka utaratibu utakaowezesha kuwa kila mwananchi apate shamba na hati ili yaweze kuwaendeleza wananchi.

Kufuatia hatua hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia ulinzi na usalama Mheshimiwa Adadi Rajab amesema watahakikisha wawekezaji matapeli hawaruhusiwi kujimegea ardhi kwa manufaa yao na badala yake mashamba hayo yaendelezwe na wananchi waliokabidhiwa ili yaweze kuwapa manufaa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza muda mfupi baada ya kuwasili wilayani humo akitokea Lushoto, Tanga kabla ya kuelekea Kijiji cha Kibaranga kufuta hati ya Shamba lililokuwa limetelekezwa na mwekezaji.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza wanakijiji wa Kibaranga kuwaelezea uamuzi wa Rais Dk John Pombe Magufuli kufuta hati ya Shamba lililokuwa limetelekezwa na mwekezaji, kwenye kijiji cha Kibaranga kilichopo wilayani Muheza mkoani Tanga jana jioni.
Mbunge wa Jimbo la Muheza mkoani Tanga kilipo kijiji cha Kibaranga, Adadi Rajabu akizungumza baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kuwaelezea wanakijiji hao uamuzi wa Rais Dk John Pombe Magufuli kufuta hati ya Shamba lililokuwa limetelekezwa na mwekezaji, kwenye kijiji cha Kibaranga kilichopo wilayani Muheza mkoani Tanga jana jioni.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza wanakijiji wa Kibaranga kuwaelezea uamuzi wa Rais Dk John Pombe Magufuli kufuta hati ya Shamba lililokuwa limetelekezwa na mwekezaji, kwenye kijiji cha Kibaranga kilichopo wilayani Muheza mkoani Tanga jana jioni.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza wanakijiji wa Kibaranga kuwaelezea uamuzi wa Rais Dk John Pombe Magufuli kufuta hati ya Shamba lililokuwa limetelekezwa na mwekezaji, kwenye kijiji cha Kibaranga kilichopo wilayani Muheza mkoani Tanga jana jioni.
Mbunge wa Jimbo la Muheza mkoani Tanga kilipo kijiji cha Kibaranga, Adadi Rajabu akizungumza baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kuwaelezea wanakijiji hao uamuzi wa Rais Dk John Pombe Magufuli kufuta hati ya Shamba lililokuwa limetelekezwa na mwekezaji, kwenye kijiji cha Kibaranga kilichopo wilayani Muheza mkoani Tanga jana jioni.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza muda mfupi baada ya kuwasili wilayani humo akitokea Lushoto, Tanga kabla ya kuelekea Kijiji cha Kibaranga kufuta hati ya Shamba lililokuwa limetelekezwa na mwekezaji.

WAHITIMU WA USCF - TAASISI YA UHASIBU TANZANIA WATAKIWA KUWA WAADILIFU MAKAZINI

0
0
Wanafunzi wametakiwa kuwa waadilifu pindi wanapomaliza chuo na kwenda kuingia makazini. Kauli hiyo ameitoa Mwenyekiti wa bodi ya Ushauri TAREA, Godwin Msigwa (pichani) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya umoja wa wanafunzi wa kikiristo wa vyuo vikuu Tanzania katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika weekend iliyopita. 

Msingwa alisema ni vyema vijana wakatambua kuwa maisha mazuri ni yake ya kufanya kazi kwa uadilifu na kuacha ujanja ujanja katika kazi. "Leo mnaenda mtaani mtapata kazi ninawaomba mkafanye kazi kwa uadilifu, mfano wewe ukipata kazi ya kusimamia manunuzi ya dawa muendele ukanunue dawa zenye ubora maana usipofaya hivyo utasababisha vifo vya watu na hiyo dhambi si ndogo, Muogopeni Mungu,' Alisema Msigwa. 

Aliongeza kuwa wakati umefika kwa watanzania wakaonyesha uzalendo kwa mambo yao wenyewe, wasingoje mpaka wasukumwe katika kufanya kazi kwa bidii. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG. 
Mchungaji wa KKKT akitoa neno wakati wa mahafali ya umoja wa wanafunzi wa kikiristo wa vyuo vikuu Tanzania katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika weekend iliyopita. 
Mchungani akiwaombea wanafunzi wakafanye vyema katika mitihani yao wakati wa mahafali ya umoja wa wanafunzi wa kikristo wa vyuo vikuu Tanzania katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika weekend iliyopita.


Wahitimu wakifuatilia neno kutoka kwa mchungaji wakati wa mahafali ya umoja wa wanafunzi wa kikiristo wa vyuo vikuu Tanzania katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika weekend iliyopita. 


Katika neno alililolitoa mchungaji huyu aliwaasa wahitimu kuwa na hofu ya Mungu pindi wanapopewa majukumu ya kazi. 


Mgeni rasmi mwenyekiti wa bodi ya Ushauri TAREA, Godwin Msigwa (wa tatu toka kushoto) akiserebuka na mchungaji wa KKKT pamoja na wageni waalikwa. 


Wahitimu wakijimwaga. 

VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA VYAPIGWA MSASA NA TGNP

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi Lilian Liundi akifungua semina  kwa Wanaharakati pamoja na viongozi wa vituo vya taarifa na Maarifa waliofika katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa TGNP Mtandao leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Geofrey Adroph)
Mkuu wa Program ya Taarifa na Utafiti kutoka TGNP, Gloria Shechambo akitoa elimu kwa wanaharakati kuhusu utendakazi wao wa kila siku wakati wa semini iliyofanyika katika ukumbi wa TGNP Mtandao.
 Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kata ya Kibuko, Bw. Valentino Lukoo akitoa ufafanuiz kuhusu maendelea yaliyofikia katika kata yao baada ya kuonekana kwa changamoto nyingi katika kata hiyo
 Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kata ya Igale, Bi Lidya Sankemwa Mwakalinga akizungumzia mipango ya kata yao kuhusu utoaji wa taarifa husika katika kata yao.
 Mwanaharakati kutoka Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kata ya Nsalal  Bi. Felister Kais akizungumzia changamoto wanazozipata katika utoaji wa taarifa.
Mwanaharakati kutoka  Mabibo, Bw. Furaha Mbakile akichangia mada
 Afisa program Utafiti na Uchambuzi kutoka TGNP, Bw. Alphonce Stima akiongea jambo wakati wa utoaji wa Semina kwa Wanaharakati pamoja na viongozi wa vituo vya taarifa na Maarifa waliofika katika semina hiyo

Wanaharakati pamoja na iongozi wa vituo vya taarifa na Maarifa wakitazama hotuba ya  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango anasoma na kuwasilisha Hali ya Uchumi kwa mwaka 2015 na Mpango wa Maendeleo Bungeni 
 Afisa program Utafiti na Uchambuzi kutoka TGNP, Bw. Alphonce Stima akiongea jambo mara baada ya kumalizika kwa Hotuba  ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango anasoma ama kuwasilisha Hali ya Uchumi kwa mwaka 2015 na Mpango wa Maendeleo Bungeni Dodoma
Afisa Programu mwandamizi wa Ushawishi na utetezi kutoka TGNP Mtandao, Bi. Anna Sangai akitoa elimu wanaharakati pamoja na viongozi wa Taarifa na Maarifa katika ukumbi wa TGNP jijini Dar es Salaam leo
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake katika Jitihada za Maendeleo (WAJIKI), Janeth Mawinza akichangia mada
 Afisa Program uchambuzi na Machapisho kutoka TGNP Mtandao, Bw. Deogratius Temba akiwaeleza wanaharakati pamoja na viongozi wa Taarifa na Maarifa jinsi ya ufanyakazi wa TGNP Mtandao

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi Lilian Liundi(kulia) akifuatilia Bunge kupitia njia ya Television katika ofisi ya TGNP  Mtandao



 Baadhi ya Wafanyakazi wa TGNP Mtandao, Wanaharakati, viongozi wa Taarifa na Maarifa pamoja na wananchi wakifuatilia Bunge kwa njia ya Televisioni ndani ya Ukumbi wa TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam

HII HAPA HOTUBA YA BAJETI KUU YA SERIKALI 2016/2017 ILIYOSOMWA BUNGENI LEO.

0
0

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAANZISHA SAFARI JIJI LA PERTH NCHINI AUSTRALIA KWA NDEGE YA BOEING 787-9 DREAMLINER.

0
0
Ndege ya uzinduzi ya Shirika la Ndege la Etihad ikipokelewa na magari ya zimamoto yaliyomwaga maji kuashiria uzinduzi rasmi wa Safari za ndege kati ya jiji la Perth Australia na Abudhabi. 

Ndege ya Shirika la Usafiri wa Anga la Etihad Boeing 787 Dreamliner imetua kwa mara ya kwanza katika Jiji la Perth nchini Australia baada ya kuzinduliwa kwa safari zake rasmi ikitokea Abu Dhabi.

Ndege ya Etihad EY486 iliondoka Abu Dhabi siku ya tarehe 02 Juni muda wa saa nne na nusu usiku na kuwasili Perth mji mkubwa uliopo magharibi mwa Australia saa saba na nusu mchana ambapo ilipokelewa rasmi kwa tamaduni za uzinduzi wa ndege mpya.

Ndege ya kurudi, EY487 iliondoka Perth saa 11 jioni na kuwasili Abu Dhabi saa sita na dakika 25 usiku wa tarehe 3 Juni.

Ndege hiyo ya B787-9 Dreamliner ya Etihad ni bora na kisasa kwa abiria kwa madaraja yote. Ina jumla ya viti 299 na ina uwezo zaidi ya asilimia 14 ukilinganisha na ndege ya Airbus A330-200. Kwa abiria wa daraja la juu, ni zaidi ya asilimia 27 kwa ubora wa viti vyake.

Makamu wa Rais wa Masoko wa Shirika la Ndege Etihad, Shane O’Hare alisema uamuzi wa kuleta ndege bora zaidi unaendana na umuhimu kibiashara baina ya Austaria Magharibi na shirika hilo.
 “Tangu tumezindua usafiri wa ndege kati ya Perth na Abu Dhabi miaka miwili iliyopita, tumefurahia kuhudumia watu wa madaraja tofauti kwa mafanikio.”

“Dreamliner imeongeza nafasi 518 kwa wiki katika safari za anga, jambo hili linatupa nafasi zaidi kuendana na mahitaji halisi ya wateja wetu.”

“Imewezesha pia wageni wetu kusafiri kwa raha mustarehe, huduma bora na ukarimu kutoka kwa wahudumu wetu wa Etihad.”

 “Ndege hiyo ya kisasa imeundwa kuendana na mahitaji mbalimbali ya weteja wetu, ikiwamo sehemu kubwa ambayo watapata viburudisho, pia ikiwa ni ndege bora zaidi kwa safari za mbali na karibu, huku huduma mbalimbali za burudani zikiwemo ndani ya ndege pamoja na huduma za kiwango cha juu.”

 “Bwana O’Hare aliongeza kuwa, “Kuanzishwa kwa huduma ya ndege ya Dreamliner kutawezesha kukuza utalii Magharibi mwa Australia.”

 “Kwa kuongeza safari za ndege kwa wiki Perth, Shirika letu la Etihad litakuwa chachu ya kuongeza ukuaji katika sekta ya utalii ambapo itawezesha watu mbalimbali kutoka ulimwenguni kote kutembelea hata wakati wa mapumziko.”

 “Kwa pamoja na washirika wetu wa masuala ya usafiri, tunatoa huduma za usafiri Ulaya, Mashariki ya Kati na ukanda wa kaskazini Marekani na hii sasa inatoa huduma bora kati ya Perth na Abu Dhabi.”

Ndege ya Etihad b787-9 iliyo katika kiwango cha juu ni matarajio itawahudumia watu wengi hapo baadaye ikiwa na vyumba maalumu  vilivyosheheni kila huduma kwenye daraja la kwanza 28 na viti 271 kwenye daraja la kati.

Katika daraja la kwanza kuna vyumba maalumu vyenye huduma zote muhimu vikiwa na nafasi ya kutosha pamoja na huduma ya kitanda. Pia, daraja la kwanza kuna mifumo mizuri ya ambayo itamwezesha abiria kusogeza kiti chake kadiri anavyopenda huku akiburudika na runinga ya kisasa pamoja na vifaa vya kuvaa masikioni vinavyomwezesha kupunguza kelele.
Aidha daraja la kati lenye viti 271 inampa mteja nafasi ya kupumzika kupitia kwenye kiti chake kwa namna kilivyotengenezwa ikiwa ni pamoja na kupata ya huduma ya runinga yake binafsi kwenye kiti chake.

Abiria akiwa kwenye Dreamliner atapata burudani ya muziki iliyounganishwa kwenye ndege hiyo. Huduma hiyo inapatikana kwa masaa yote uwapo kwenye ndege. Pia, kuna chaneli zinazorusha matangazo yake ya live huku zikiwa ni screen ambazo zina kiwango cha ubora wa hali ya juu huku zikimfanya abiria kujisikia vizuri.
Pia, hudma ya simu na wi-fe pamoja na sehemu za kuchomeka USB zinapatikana kwenye kila kiti.

Etihad limekuwa shirika linaloongoza kwa huduma bora zinazotolewa ndani ya ndege ikiwa na watoa huduma wenye uzoefu. Watoa huduma hao wana mafunzo ya kutosha kutoka kwenye vyuo vinavyotambulika kimataifa ambao watamsaidia abiria kila anapohitaji msaada hususani wale wanaosafiri na watoto.

Vyakula bora na salama vinavyopikwa na wataalamu kutoka hoteli maalumu, vinatolewa kwenye daraja la kwanza na wengine wanaweza kupata huduma hiyo kulingana na mahitaji ya abiria.

Shirika la Etihad ndilo shirika pekee linalotoa huduma ya usafiri kutoka magharibi mwa Australia na USA ikiunganisha na uwanja wa Ndege wa Abu Dhabi. Ipo huduma inayomwezesha mgeni kukamilisha masuala ya uhamiaji na ukaguzi wa kiusalama kwa USA wanaposafiri kwenda Abu Dhabi ili kupunguza usumbufu wanapowasili uwanja wa ndege wa Marekani.

Shirika la Etihad lilizindua safari za Airbus A330-200 Perth Julai 2014.

Tofauti na Perth, Shirika la Etihad pia linaunganisha zaidi ya miji 8 magharibi mwa Australia. Etihad imefanikiwa kuunganisha watu na miji ya Broome, Geraldton, Kalgoorlie-Boulder, Kununurra, Karratha, Paraburdoo, Port Hedland na Newman.

Vilevile Shirika la Etihad linatoa huduma katika mji wa Sydney ikiwa na safari mara mbili kwa siku ikiunganisha na Virgin Australia, pia mara mbili kwa siku Melbourne na mara mbili kwa siku mji wa Brisbane.

Perth ndiyo mji wa pili kwa ukubwa Australia unaohudumiwa na ndege ya kisasa ya Shirika la Etihad B787-9 Dreamliner na kwa mji wa Brisbane ilianza safari zake kwa mara ya kwanza Juni 2015.
Pia, ndege hiyo inatoa huduma Singapole, Washington DC, Zurich na Dusseldorf.

Vilevile Shirika linatarajia kuanzisha huduma hiyo Istabul, Johnnesburg na Shangai kwa kipindi hiki kilichobaki kwa mwaka huu.

Aidha ndege za Boing 787 Dreamliner inategemewa kuwa ndizo ndege zikazotoa huduma kwa miaka michache ijayo katika shirika hilo kutokana na ubora wake na teknolojia yake ya kisasa.

Wanaotumia ndege ya Dreamliner watafurahia usafiri huo kutokana na kuwa na madirisha makubwa, hewa nzuri ya ndani ya ndege, mandhari mazuri pamoja na vifaa vilivyopo ndani vyenye kutumia teknolojia ya kisasa.

Safari za  Abu Dhabi-Perth:

Namba ya Ndege
Inakotoka
Kuondoka
Mahali/kwenda
Kuwasili
Siku
Ndege
EY486
Abu Dhabi
(AUH)
4:30 usiku
Perth
(PER)
7:50 mchana next day
Daily
B787-9
EY487
Perth
(PER)
11:00 jioni
Abu Dhabi (AUH)
6:25 mchana
next day
Daily
B787-9

Muhimu: Muda wa kuondoka na kuwasili umewekwa kwa masaa ya eneo husika.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images