Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

TRA YAVUKA LENGO LA MAKUSANYO YA KODI KWA MWEZI MEI 2016

$
0
0
MKamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata akitilia mkazo jambo wakati wa kikao na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya makusanyo ya mapato kwa mwezi Mei 2016,kilichofanyika katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo na kushoto ni Meneja wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Abdul Mapembe.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 1.032 katika mwezi Mei ambayo ni sawa na asilimia 100.7 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 1.025 katika mwezi huo.

Makusanyo ya kipindi cha miezi kumi na moja (Julai 2015 hadi Mei 2016) ni jumla ya shilingi trilioni 11.956 sawa na asilimia 99.2 ya lengo la shilingi trilioni 12.054 katika lengo la kipindi hicho kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi leo kuhusu mwenendo wa makusanyo ya mapato, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata amesema TRA inaendelea na jitihada mbalimbali kuhakikisha inafikia na kuvuka lengo la makusanyo iliyopangiwa na serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na kuendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili Mamlaka katika ukusanyaji wa mapato.

“TRA imejiwekea mikakati thabiti ya kuongeza mapato kwa kipindi cha mwezi mmoja uliobaki ili kuweza kufikia au kuvuka lengo kwa mwaka huu wa fedha, ambapo kwa sehemu kubwa tumeendelea kupambana na magendo hususani katika pwani ya bahari ya Hindi na mipaka yote, kupambana na wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi na wanaokiuka kutumia mashine za kodi za keielektroniki , kuwawajibisha wafanyakazi wasio waadilifu pamoja na kuhakikisha inaboresha zaidi mifumo itakayompa urahisi mlipakodi katika zoezi zima la ulipaji kodi wa hiari, alisema Kamishna Mkuu.

Bw. Kidata ameendelea kusisitiza wananchi na wafanyabiashara kuwa wazalendo kwa nchi yao kwa kutoa na kudai risiti za EFD pindi wanaponunua au kuuza bidhaa pamoja na huduma ili kuongeza mapato ya nchi.

Katika kutekeleza agizo la Mh. Rais na kuhakikisha wafanyabiashara wanatoa ushirikiano katika matumizi ya mashine za EFD Mamlaka imeanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya ugawaji wa mashine za EFD kwa wafanyabiashara wadogo kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

TRA imeanza ugawaji wa mashine za EFD kwa wafanyabiashara wapatao 5,703 wenye mauzo ghafi kati ya Shilingi milioni 14 na milioni ishirini (20) kwa mwaka, wafanyabiashara hao wanatakiwa wafike katika ofisi za Mamlaka ya Mapato za Mikoa wanayolipia kodi ya Ilala, Kinondoni na Temeke ili waweze kuhakiki usajili wao wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) na kupewa kibali cha kupewa Mashine ya EFD zoezi lililoanza Juni Mosi alisisitiza Kamishana Mkuu.

Aidha, Bw. Kidata alifafanua kuwa zoezi hili litaendelea katika Mikoa yote Tanzania kwa awamu kwa utaratibu utakaotangazwa mara kwa mara na hivyo kutoa wito kwa wafanyabiashara wenye mauzo tajwa wote nchini kutoa ushirikiano pindi inapofika zamu yao katika Mikoa yao.

Zoezi hili litasaidia kuongezaka kwa Mapato ya nchi endapo wafanyabiashara na wananchi watakuwa bega kwa bega katika kuhakikisha wanatumia mashine hizo na kutoa taarifa kwa Mamlaka kuhusu wafanyabiashara wote watakao kiuka kutumia mashine hizo za EFD.

Kwa upande wa wananchi, kamshna mkuu amewaasa kuadai risiti kila wanunuwapo bidhaa au kupata huduma na kuhakikisha usahihi wa kiwango walicholipia sambamba na risiti walizopewa .


“Pamoja Tunajenga Taifa Letu"


Imetolewa na:

Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi

WAFANYAKAZI WA SERENGETI WAFANYA USAFI NA KUCHANGIA DAMU HOSPITALI YA TEMEKE

$
0
0
Wafanyakazi wa kiwanda cha Bia Serengeti wakiwa katika picha ya pamoja mapema wiki iliyopita mara baada ya kufanya usafi katika mazingira ya Hospitali ya Temeke 
Meneja wa Usalama na Afya kazin wa SBL Bwana David Mwakalobo akimkabidhi vifaa vya usafi Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Temeke 
Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha bia Serengeti (SBL) akichangia damu ambapo zoezi hilo la kuchangia damu liliambatana na shamrashamra za kilele cha wiki ya usalama na afya kazini zilizoanzia kiwandani kwa matembezi ya hisani kuelekea katika hospitali ya Temeke .
Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) wakifanya usafi katika mazingira ya Hospital ya Temeke mwishoni wa wiki iliyopita katika maadhimisho ya shamrashamra za kilele cha wiki ya usalama na afya kazini zilizoanzia kiwandani kwa matembezi ya hisani kuelekea katika hospitali ya Temeke ambapo wafanyakazi hao walifanya usafi katika mazingira ya hospitali hiyo wakishirikiana na Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Temeke na timu yake 
Usafi ukiendelea katika mazingira ya Hospitali ya Temeke ambapo pia wafanyakazi wa SBL mapema wiki iliyopita ikiwa ni moja ya shughuli za kijamii pia walijitolea kuchangia damu na kupima afya zao katika Hospitali hiyo .

Dar es salaam ,3 Juni ,2016 ;Wafanyakazi wa kiwanda cha bia cha Serengeti (SBL) leo wamechangia damu katika hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam ikiwa ni moja ya mpango ya kampuni kusaidia sekta ya afya nchini.

Uchangiaji wa damu ni moja ya shughuli za kusaidia jamii zinazoendana sambamba na wiki ya afya na usalama kazini kwa kampuni hii,tukio hili linalofanywa kila mwaka likilenga viwanda vya bia na vinywaji vikali kuongeza ufahamu kwa wafanyakazi kuhusu umuhimu wa kuzingatia usalama sehemu za kazi.

Akiwashukuru wafanyakazi wa SBL kujitokeza kwa wingi kuchangia damu Meneja Uzalishaji wa kiwanda cha Dar es salaam Alice kilembe alisema zoezi hili linaenda sambamba na mipango ya kusaidia jamii na lengo ikiwa ni kusaidia kuboresha afya zao.

“Tunapenda kuwashukuru wafanyakazi wote kujitokeza kuchangia damu .Tunaamini msaada huu wa damu utasaidia kuokoa maisha ya wale wanaohitaji na pia kusaidia kuboresha afya za watu wetu “alisema Kilembe.

Mapema leo Kiwanda cha Serengeti cha Dar es salaam wameshiriki pia katika usafi wa mazingira kuzunguka katika maeneo ya Temeke jambo ambalo meneja uzalishaji wa kiwanda alisema ni “kuitikia wito wa serikali wa kuhakikisha usafi katika maeneo ya wazi”

Kwa mujibu wa Kilembe SBL haijakumbwa na matatizo katika maeneo ya kazi kwa zaidi ya miaka minne ikiwa ni matokeo ya mafunzo ya mara kwa mara kwa wafanyakazi na tahadhari zinazochukuliwa zinazofanya kampuni kukidhi viwango ya kimataifa vya usalama katika mazingira ya kazi.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI TANZANIA NA AKAUNTI YA MALAIKA LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Jukwa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania na Akaunti ya Malaika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam leo Juni 06,2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na watoto waliokua wakiishi katika mazingira magumu wakati uzinduzi wa Jukwa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania na Akaunti ya Malaika vilivyozinduliwa leo Juni 06,2016 katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya CD yenye vipindi mbalimbali kutoka kwa watoto waliokua wakiishi katika mazingira magumu kwenye uzinduzi wa Jukwa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania na Akaunti ya Malaika vilivyozinduliwa leo Juni 06,2016 katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi cheti kwa mwakilishi wa kampuni ya simu za mikononi Zantel kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo kuweza kufanikisha uzinduzi wa Jukwa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania na Akaunti ya Malaika vilivyozinduliwa leo Juni 06, 2016 katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi cheti kwa mwakilishi Mkaazi wa UN Women Bibi Anna Pollins kwa kutambua mchango uliotolewa na Shirika hilo katika kuwezesha kufanikisha uzinduzi wa Jukwa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania na Akaunti ya Malaika vilivyozinduliwa leo Juni 06, 2016 katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akibonyeza Laptop kuzindua Jukwa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania na Akaunti ya Malaika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam leo Juni 06,2016. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Jukwa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania na Akaunti ya Malaika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam leo Juni 06,2016. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na kutoka katika Tasisi mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi wa Jukwa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania na Akaunti ya Mlaika vilivyozinduliwa leo Juni 06,2016 katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam. (Picha na OMR) 

Airtel na mhealth yawawezesha maelfu ya kinamama kupokea taarifa zinazowasaidia kuokoa maisha yao bure

$
0
0
Mratibu wa Kitaifa wa Uzazi Salama, Dr Koheleth Winani ( kulia) na Meneja Huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi (katikati) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Mkazi wa Center for Disease Control (CDC) Tanzania, Dr Maestro Evans wakipongezana baada ya kuzindua namba maalumu itakayowawezesha watoa huduma za afya kuwasajili kina mama wajawazito na wenye watoto kwenye huduma itakayowapa taarifa mbalimbali za afya bure ijulikanayo kama “Wazazi Nipende”. mradi wenye lengo la kupunguza idadi ya vifo vya kina mama wajawazito na watoto.
Mratibu wa Kitaifa wa Uzazi Salama, Dr Koheleth Winani (wa kwanza kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati uzinduzi wa namba maalumu itakayowawezesha watoa huduma za afya kuwasajili kina mama wajawazito na wenye watoto kwenye huduma itakayowapatia taarifa mbalimbali za afya bure ijulikanayo kama “Wazazi Nipende” inayotolewa na Airtel pamoja na mHealth Tanzania chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya. Katikati ni Meneja Huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi akifatiwa Mkurugenzi Msaidi Mkazi wa Center for Disease Control (CDC) Tanzania, Dr Maestro Evans.
Meneja Huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi(katikati) akiongea wakati wa uzinduzi wa namba maalumu itakayowawezesha watoa huduma za afya kuwasajili kina mama wajawazito na wenye watoto kwenye huduma itakayo wapatia taarifa mbalimbali za afya ijulikanayo kama “Wazazi Nipende” inayotolewa na Airtel pamoja na mHealth Tanzania na washirika wengine chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya. Kulia ni Mratibu wa Kitaifa wa Uzazi Salama, Dr Koheleth Winani na kushoto ni Mkurugenzi Msaidi Mkazi wa Center for Disease Control (CDC)Tanzania, Dr Maestro Evans.

Kampuni ya simu za mkononi Airtel imetoa mchango mkubwa katika kuhakikisha inaokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wadogo nchini Tanzania. Airtel imechangia katika kuendesha kampeni ya wazazi Nipendeni (Afya ya wajawazito na Watoto) kwa kutoa elimu kupitia ujumbe mfupi toka mwaka 2012.  Mpaka sasa Airtel imeweza kutuma ujumbe mfupi wa taarifa muhimu za afya zaidi ya milioni 22 kwa wateja zaidi ya 350,000 wenye thamani ya shilingi 1,518, 000,000

Airtel kwa kushirikiana na mHealth Tanzania PPP waendeshaji wa huduma hii inayomilikiwa na wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto inawezesha wateja wake kote nchini kupokea taarifa muhimu za afya ya mama wajawazito na kuwakumbusha kuhudhuria kliniki na kupata chanjo. “Taarifa zinazotolewa kupitia ujumbe mfupi zinahakikisha mtoto ambaye hajazaliwa na mama mjazito wako katika usalama wakati wote” alisema Mratibu na mshauri wa mradi Muttah Saulo kutoka mhealth Tanzania PPP

Aliongeza kwa kusema” akina mama pia wanashauriwa jinsi ya kuwatunza watoto wao kwa usalama baada ya kujifungua, waliojiunga na huduma hii watapata ujumbe mfupi wa idadi isiyopungua nne kwa wiki”

Akiongea kuhusu ushirikiano huo , Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi alisema” Tunayofuraha kuwa sehemu ya mpango huu wa wazazi nipendeni kupitia huduma yetu ya ujumbe mfupi.  Mpango huu unaonyesha uwezo wa teknologia katika jamii na kwamba teknologia ya simu za mkononi inaweza kutoa mchango mkubwa katika kuokoa maisha ya maelfu ya akina mama. 

Maelfu ya wajawazito, wazazi na wasaidizi wamenufaika na huduma hii.  Kwa kutoa huduma hii bure mpaka sasa tumeweza kuwekeza kiasi cha shilingi 1,518, 000,000 na tunaendelea kushirikiana na mhealth Tanzania PP katika kuhakikisha mpango huu unakuwa endelevu na kuwanufaisha watanzania wengi. Airtel tumejipanga kuendelea kuhamasisha usalama katika maisha ya watanzania na kuwawezesha jamii kufatilia na kutia mkazo katika afya zao kwa kuwapatia elimu juu ya afya bure bila gharama zozote.”

Mmoja kati ya watumiaji wa huduma hii , Bi Francis ambaye sasa ni mama mwenye mtoto wa miezi mitatu  alisema”  Tunafurahia huu mpango  kwani unatupatia elimu juu ya afya zetu na watoto na kutusaidia kufatilia siku za kuhudhuria kliniki pamoja na  kuwapeleka watoto kliniki.  Mimi na mume wangu tunafurahi huduma hii ya bure kutoka Airtel inayotuwezesha kuendelea kumlea mtoto wetu katika afya.”

Takwimu kutoka katika ripoti ya mHealth Tanzania PPP Mei 2016 zinaonyesha kila mwezi wateja wa Airtel takribani 7300 wamejiunga na huduma ya bure ya sms ya wazazi nipendeni. Kati yao 43% ni wa kina mama wajawazito na 15% ni wa kina mama wenye watoto wadogo na 44%  ni wasaidizi wa wakinamama wakiwemo waume , ndugu na  wale wanaotafuta taarifa za afya  ya uzazi kwa ujumla.

Raia wa Kigeni 4792 wakamatwa kwa Kukiuka sheria za Uhamiaji.

$
0
0
 
 Kaimu Kamishna Utawala na Fedha kutoka Jeshi la Uhamiaji Bw. Abbas Irovya wa pili kutoka kushoto akiongea na wanahabari hawapo pichani kuhusu ripoti ya operesheni mbalimbali zinazoendelea kufanyika nchini kwa lengo la kudhibiti wahamiaji haramu,wa kwanza kulia ni Mkaguzi wa Uhamiaji Bw. Leslie James Mbotta na wa kwanza kulia ni Mrakibu Msaidizi wa Jeshi hilo Bi. Rosemary Mkandala.(Picha na Benjamin Sawe- Maelezo).

Frank Mvungi-Maelezo.

Takribani raia 4792 wa kigeni wamekamatwa kwa kukiuka sheria, Kanuni na Taratibu za Uhamiaji katika kipindi cha Januari hadi aprili mwaka huu. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salam na Kaimu Kamishna wa Idara ya Uhamiaji Bw. Abass Irovya wakati wa mkutano na Vyombo vya habari uliolenga kutoa taarifa ya Operesheni mbalimbali zinazotekelezwa na Idara hiyo. 

Irovya amesema kuwa Idara hiyo imekuwa ikiendesha Operesheni ondoa uhamiaji haramu tangu mwezi Desemba mwaka jana na imeonyesha mafanikio ambapo raia 1796 wamefukuzwa nchini kwa kukiuka sheria za uhamiaji.“Wananchi walio wengi wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa Idara yetu kutokana na uelewa wao kuongezeka kwa sababu tunayo programu ya kutoa elimu kwa umma na imeonyesha mafanikio makubwa” alisisitiza Irovya

Bw. Irovya aliongeza kuwa waliohukumiwa kifungo ni raia 132 na 383 kesi zao zinaendelea kwenye mahakama katika Mikoa mbalimbali hapa nchini.Raia 388 walilipa faini hali iliyochangia kuongeza mapato ya Serikali kutokana na kukiuka sheria na Kanuni za Uhamiaji hapa nchini.

Kwa upande mwingine kesi 509 zinaendelea katika mahakama mbalimbali hapa nchini na raia 294 waliachiwa huru kutokana na mahakama kutowatia hatiani.Idara ya Uhamiaji ina Vituo takribani 60 katika Mikoa Mbalimbali hapa nchini baadhi vikiwa katika Mikoa ya  anga,Lindi,Mtwara,Ruvuma,Katavi,Kigoma,Simiyu ambapo Idara hiyo imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu athari za raia wa kigeni wanaoingia nchini bila kufuata sheria na taratibu za Uhamiaji.

CASTLE LITE SASA KUPATIKANA KWENYE UJAZO WA MILI LITA 440

$
0
0
Meneja wa Bia ya Castle Light Nicholous John, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, baada ya Uzinduzi wa Chupa mpya yenye Ujazo wa milimita 440 iliyofanyika katika Ukumbi wa Break Point Kinondoni Makaburini.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia TBL, Kushila Thomas, akimpa zawadi mmoja wa wananchi walioshiriki katika uzinduzi huo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya TBL, wakiwa katika hali ya furaha baada ya uzinduzi wa Bia ya Castle Light yenye ujazo wa milimita 440. --- Kampuni ya bia ya TBL imezindua chupa mpya ya bia yake pendwa aina ya Castle LITE yenye ujazo wa mili lita 440 kwenye uzinduzi uliofanyika baa ya Break Point iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam. Kufuatia uzinduzi huu, bia ya Castle LITE yenye ujazo wa mili lita 440 itaanza kupatikana nchi nzima mnamo tarehe 5, mwezi huu. Aidha, ladha ya bia ya Castle LITE itabaki na ladha na sifa zile zile za kipekee kama ilivyo kwenye bia hii yenye ujazo wa mili lita 375, hivyo kuweza kunywewa na kuburudisha wakati wowote.

 Akizungumzia uzinduzi huu, Meneja wa bia ya Castle LITE, Nicholous John amesema; “Castle LITE inaendelea kuja na ubunifu mbalimbali kwenye soko la Tanzania, mfano mzuri ni kampeni yetu ya jinsi ya kutumia nembo yenye rangi ya bluu iliyopo kwenye chupa ya Castle LITE kujua kama bia imepata ubaridi stahiki utakaokupa ladha halisi ya Castle LITE. 

Na sasa tumekuja na Castle LITE yenye ujazo wa mili lita 440 ili kuwapa wateja wetu uwezo wa kuchagua.” Castle LITE hii yenye ujazo wa mili lita 440 itauzwa kwa shilingi 2,500 kwa chupa na shilingi 50,000 kwa kreti na itapatikana kote Tanzania.

 Castle LITE inabaki kuwa bia pekee sokoni yenye nembo ya kipekee inayobadilika rangi na kuwa bluu pale bia inapopata ubaridi stahiki unaomwezesha mnywaji kufurahia ladha ya kipekee ya bia hii. 

 Uzinduzi wa Castle LITE yenye ujazo wa mili lita 440 uliambatana na utambulisho wa basi la kipekee lenye majokofu yanayotoa ubaridi wa hali ya juu ya kutunzia na kuuza bia za Castle LITE zenye ubaridi stahiki unaomwezesha mnywaji kufurahia ladha halisi ya ubaridi wa barafu ya Castle LITE.

Serikali yaondoa tozo ya uhakiki na usajili wa viwanda vidogo vidogo.

$
0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Prof Adolph Mkenda amesema kuwa serikali imeondoa tozo ya uhakiki wa viwango vya ubora na usajili katika kuanzisha viwanda vidogovidogo katika shirika la viwango Tanzania Tanzania(TBS) ambao sasa unafanyika bure.

Prof Mkenda ameyasema hayo alipokuwa akitoa mada katika uzinduzi wa Jukwaa la kuwezesha wanawake na akaunti ya mkopo ya MALAIKA ambayo imeanzishwa katika benki ya Wanawake Tanzania.

Aidha amesema ameagiza kwa wilaya na vijiji kuanzisha viwanda kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya Tano na kuinua uchumi wa nchi yetu.“Bidhaa za kilimo kwa sasa zinapewa dhamana na hivyo basi nawaimiza wanawake waanzE kuanzisha viwanda vidogovidogo kwani uanzishwaji wake ni bure.”Alisema Prof Mkenda.

Pia alisema kuwa kipato cha kati nchini kinaongezeka siku hadi siku na kuwataka wanawake kutolima kwa mazoea na kuwataka wafanye biashara kwa faida kwa kutumia teknolojia sahihi ili kuongeza uzalishaji.

Katika upande mwingine aliwataka wanawake kutokata tamaa katika kujiinua kiuchumi kwani Serikali ya awamu ya tano iko makini na inaweka mazingira mazuri kwa wanawake kama kuondoa tozo zisizokuwa za lazima ili kuvutia wawekezaji wa viwanda vidogo vidogo.

Katika uzinduzi huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Bi Samia Suluhu Hassan alizindua jukwaa hilo na akaunti ya mikopo ya wanawake ya MALAIKA kupitia benki ya wanawake ambayo akaunti hiyo itakuwa na mikopo yenye riba nafuu ya asilimia 5 kwa muda wa miezi sita,mafunzo yanatolewa bure,hamna haja ya kuleta mchanganuo wa mahesabu na hakuna hitaji la dhamana yenye lengo la kuwakwamua wanawake kiuchumi.

WAZIRI MKUU MAJALIWA:MATAIFA YALIYOENDELEA YASHIRIKIANE NA SERIKALI YA TANZANIA KUWAHUDUMIA WAKIMBIZI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameyaomba mashirika ya Kimataifa na Nchi zilizoendelea zishirikiane na Serikali ya Tanzania katika kuwahudumia wakimbizi.

“Kwa sasa tunashirikiana na UN (Umoja wa Mataifa) kuwahudumia wakimbizi, hivyo tunaomba mataifa mengine nayo yatusupport katika jambo hili,” amesema.Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumatatu, Juni 6, 2016) alipofanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji, Mhe. Dibr Reynders ofisini kwake Bungeni, Dodoma.

Amesema Tanzania inahifadhi jumla ya wakimbizi 165,000 kati ya 230,000 walioko katika nchi za Maziwa Makuu, ambapo bajeti ya Serikali haitoshelezi kuwapa huduma wanazostahili.Waziri Mkuu Majaliwa amesema wakimbizi hao wanaishi kwenye kambi mbalimbali nchini zikiwemo za Nyarugusu na Nduta zilizoko wilayani Kasulu na Kibondo ambazo alizitembelea Desemba mwaka jana.

Amesema wakimbizi hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za uhaba wa maji safi, ufinyu wa huduma za afya na elimu na uharibifu wa mazingira .Amesema wengi wa wakimbizi hao ni raia wa Burundi, Kongo na Rwanda, pia amemuomba Mhe. Reynders atakapofika Burundi akahamasishe amani.

Pia Waziri Mkuu Majaliwa amesema Tanzania inakkaribisha wawekezaji kutoka nchini Ubelgiji na mataifa mengine kuja kuwekeza katika Sekta za Viwanda, Nishati na Miundombinu.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amesema hali ya siasa visiwani Zanzibar ni ya utulivu na Rais Dk. Ali Mohamed Shein anafanya kazi vizuri kwa kushirikiana na vyama vya upinzani.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mhe. Reynders aliyetaka kujua hali ya kisiasa inavyoendelea visiwani huko.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
06 Juni, 2016 .

RAIS DKT MAGUFULI ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA RAIS WA SAHARAWI, AKUTANA NA NAIBU WAZIRI MKUU WA UBELGIJI, BALOZI WA MAREKANI NA KUAGANA NA BALOZI WA ITALY

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa pole kwa Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya kidemokrasia ya Saharawi nchini Mhe. Brahim Buseif alipokwenda ubalozini hapo kutoa pole na kusaini Kitabu cha Maombolezo ya kifo cha Rais wa Saharawi Mhe. Mohamed Abdelaziz Mikocheni jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akifanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa mambo ya Nje wa Ubelgiji Mhe. Didier Reynders aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italy nchini Mhe. Luigi Scotto aliyemtembelea na kumuaga baada ya kumaliza muda wale wa kazi Ikulu Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Mark Childress aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

CCM YAVUNJA UKIMYA

UFAFANUZI WA MASHTAKA YA NAIBU SPIKA

Hafla ya ugawaji maeneo iliyofanyika katika Kijiji cha Wasanii Wilayani Mkuranga.

$
0
0
(Video na Benedict Liwenga, Sauti na Hussein Makame)

Wizara ya Maji na Umwagiliaji yapewa mafunzo ya mitambo ya kusafishia maji

$
0
0
 Mkurugenzi Msaidizi wa Ubora wa Maji Wizara ya Maji na Umwagiliaji  Philip Chacha akiishukuru Kampuni ya TRUNZ kutoka Uswisi kwa mafunzo waliyoyatoa kuhusu matumizi ya mitambo inayochuja chumvi na baadhi ya madini yasiyotakiwa katika maji, mafunzo hayo yamefanyika Juni 6,2016 Jijini Dar es Salaam, kulia ni Kaimu MkurugenzI Uratibu wa Programu Muhandisi Dorisia Mlashani.

 Mtaalamu wa Teknolojia ya mitambo inayochuja chumvi na baadhi ya madini yasiyotakiwa kwenye maji Ronny Graul kutoka Kampuni ya TRUNZ ya Uswisi akikinga maji yaliyokwisha chujwa kutoka katika moja ya mitambo ya kisasa inayotumika kusafishia maji, wanaomtazama ni baadhi ya  wataalamu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji waliohudhuria mafunzo ya matumizi ya mtambo huo yaliyofanyika Juni 6,2016 Jijini Dar es Salaam.

Mtaalamu wa Teknolojia ya mitambo inayochuja chumvi na baadhi ya madini yasiyotakiwa kwenye maji Ronny Graul kutoka Kampuni ya TRUNZ ya Uswisi akionyesha jinsi mtambo huo unavyofanya kazi, wanaomtazama ni baadhi ya wataalamu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji waliohudhuria mafunzo ya matumizi ya mtambo huo yaliyofanyika Juni 6,2016 Jijini Dar es Salaam.




Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO

Wizara ya Maji na Umwagiliaji imepewa mafunzo na Kampuni ya TRUNZ kutoka Uswisi juu ya mitambo inayosafisha maji yenye chumvi na madini yasiyotakiwa katika maji ili kusaidia ongezeko la upatikanaji wa maji safi na salama nchini.

Mafunzo hayo yametolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mtaalamu wa Teknolojia kutoka katika Kampuni hiyo, Ronny Graul ambaye ameelezea na kuonyesha jinsi mitambo hiyo inavyosafisha maji yenye chumvi au madini yasiyotakiwa hadi kuwa safi na salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu.

“Mitambo hii inatumia nguvu ya jua na umeme kidogo sana lakini inafanya kazi kubwa ya kusafisha maji yenye chumvi na madini ambayo hayahitajiki katika maji yakiwemo madini ya floride, chuma,zinki, shaba pamoja na naitreti na kuyaacha maji yakiwa safi na salama katika viwango vinavyohitajika na Shirika la Afya Duniani (WHO)”,alisema Graul.

Mtaalamu huyo ameongeza kuwa mitambo hiyo inapatikana kiurahisi na ina uwezo mkubwa wa kusafisha maji hasa kwa maeneo yenye visima vya maji yenye chumvi pamoja na madini yasiyotakiwa ambapo kwa Tanzania maeneo yaliyokithiri kwa kuwa na maji yenye chumvi nyingi ni Mtwara,Singida, Dar es Salaam na Pwani.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Maji Mjini wa wizara hiyo, Muhandisi Mary Mbowe alisema kuwa lengo la Wizara kuomba mafunzo hayo ni kufahamu namna gani mitambo hiyo inavyofanya kazi ili kama itakidhi vigezo iweze kununuliwa na kupelekwa katika maeneo sugu yenye maji ya chumvi hivyo, kusaidia Watanzania wengi kupata maji safi na salama.

Kwa upande wa Mkurugenzi Msaidizi wa Ubora wa Maji Philip Chacha pamoja na wataalamu wengine wa ubora wa maji kutoka wizarani hapo wamesema kuwa wamejidhihirisha kwa ubora wa mitambo hiyo na jinsi ilivyo na uwezo mkubwa wa kusafisha maji kwa kwa muda mfupi hivyo, itaweza kuokoa maisha ya Watanzania hasa waishio vijijini kwani wataepuka magonjwa yanayosababishwa na maji yasiyo safi na salama.

Mitambo hiyo imeundwa na mitambo miwili inayofanya kazi kwa pamoja ambapo mtambo wa kwanza unajulikana kwa jina la AQUIFIER 200 unaotumika kuondoa chumvi na madini yasiyotakiwa katika maji na mtambo wa pili unaitwa SURVIVOR 300 ambao unachuja maji na kuyaacha yakiwa safi na salama kwa kunywa bila kuchemsha wala kutia dawa ya kusafishia.

Tanzania kupata milioni 800 kutoka Marekani, Rais Magufuli ahakikishiwa na Balozi wa Marekani

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu: 255-22-2114512, 2116898

E-mail: press@ikulu.go.tz

Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,

      IKULU,

 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  

11400 DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

Marekani itatoa dola milioni 800 kwa Tanzania kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.


Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress aliyekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kutolewa kwa fedha hizo ni uthibitisho kuwa kutotolewa kwa fedha za awamu ya pili ya mradi wa changamoto za milenia (MCC-2) hakujaondoa uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Marekani ikiwemo utoaji wa misaada ya maendeleo.


"Tumezungumza mambo kadhaa, na wiki hii Tanzania na Marekani kupitia shirika letu la misaada la USAID tunatarajia kutiliana saini mkataba wa zaidi ya dola milioni 400 kwa ajili ya mwaka ujao, pia tumezungumza kuwa kutakuwa na dola milioni 800 zitakazotolewa na Marekani kwa ajili ya miradi mbalimbali na hii haihusiani na MCC.


"Ukweli ni kwamba tunayo mengi ya kufanya pamoja katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu na kilimo na tutafanya kila juhudi kuhakikisha haya yanafanikiwa"Amesema Balozi Mark Childress muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo na Rais Magufuli.

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali yake ya awamu ya tano itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na Marekani na kwamba fedha za msaada kutoka Marekani ni muhimu kwa maendeleo ya Tanzania.


"Amekuja kutuhakikishia kwamba watatoa hela kwa ajili ya Tanzania na anasema sasa hivi watatoa zaidi ya dola milioni 800, na mkataba mwingine tunaweza tukasaini hata kesho wa dola milioni 410, anasema kutotoa hela za MCC hakuna maana kupotea kwa urafiki wa Tanzania na Marekani, urafiki wa Tanzania na marekani upo pale pale na sasa wanaongeza hela nyingi zaidi katika kuonesha kwamba juhudi za HAPA KAZI TU zinaendelea" amesema Rais Magufuli.


Wakati huo huo Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji Mhe. Didier Reynders Ikulu Jijini Dar es salaam, ambapo viongozi hao wamezungumzia kuendeleza na kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili hususani katika maendeleo.


Pamoja na kuzungumzia miradi ya ushirikiano inayotekelezwa kati Tanzania na Ubelgiji katika mkoa wa Kigoma, viongozi hao pia wamekubaliana kuongeza ushirikiano katika biashara na uwekezaji ambapo Mhe. Didier Reynders ameahidi kushawishi kampuni nyingi za Ubelgiji kuja kuwekeza hapa nchini.


Katika hatua nyingine Rais Magufuli ameagana na Balozi wa Italia hapa nchini Mheshimiwa Luigi Scotto ambaye amemaliza muda wake wa miaka mitatu.Balozi Luigi Scotto amesema katika kipindi chake amewezesha kuongezeka kwa biashara kati ya Italy na Tanzania kwa asilimia 35 na ameielezea Tanzania kuwa ni nchi nzuri aliyoipenda na kwamba ataendelea kutangaza fursa zilizopo Tanzania huko Italia na kwingineko.

Mapema leo asubuhi, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametia saini kitabu cha maombelezo katika Ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Nchi za Kiarabu ya Saharawi iliyopo Mikocheni Jijini Dar es salaam, kufuatia kifo cha Rais wa nchi hiyo Mohamed Abdelaziz aliyefariki dunia Jumanne iliyopita tarehe 31 Mei, 2016.


Rais Magufuli ambaye amepokelewa na Balozi wa Saharawi hapa nchini Mhe. Brahim Salem Buseif amesema Marehemu Mohamed Abdelaziz ambaye pia alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Polisalio Front, atakumbwa kwa juhudi zake za kupigania ukombozi na uhuru wa Saharawi.

"Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Tanzania napenda kutoa salamu zangu za pole kwa Serikali na wananchi wa Saharawi kwa kumpoteza kiongozi ambaye alijitoa kwa ajili ya kupigania ukombozi na uhuru wa Jamhuri ya Saharawi.


"Namuombea kwa Mwenyezi Mungu, aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina"Amesema Dkt. Magufuli katika salamu hizo.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam


06 Juni, 2016

Usaili wa Maisha Plus Mtwara, funga kazi

$
0
0
Muhitimu wa shahada ya kilimo William Mbaga alibanwa kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ikiwemo faida za kilimo cha 'greenhouse' pamoja na namna ambavyo maziwa ya mtindi yanapatikana. William alijieleza kwa ujasiri.
William Mbaga akiondoka baada ya kufanya usaili.Washiriki wenye fani na ujuzi mbalimbali walijitokeza wakiwemo madereva bodaboda, mafundi, waigizaji, waimbaji, wasusi n.k
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
Waigizaji pia walikuwemo katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.


Ni asubuhi tulivu katika fukwe za bahari ya hindi kusini mwa Tanzania ambapo vijana wengi wamejitokeza kufanya usaili wa mashindano ya Maisha Plus East Africa 2016. Wapo wanaoonekana kujiamini na wengine wamejawa uoga. "Ni siku niliyoisubiri kwa hamu sana" anasema Faustine Komba miongoni mwa washiriki kutoka Mtwara.
Safari ya msimu wa tano wa mashindano ya Maisha Plus imeanza rasmi kwa kuanza na usaili uliofanyika katika hotel ya NAF Beach iliyoko Mtwara. Washiriki kutoka mikoa ya jirani nao pia walijitokeza. "Maisha Plus kwangu ni ndoto ya muda mrefu sana, niliposikia mnakuja Mtwara nikasema piga ua lazima nishiriki" Anasema Ismail Likando aliyesafiri kutoka Lindi.
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
 
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.


Maswali mengi yalilenga kupima uelewa wa vijana kuhusu mambo mbalimbali ya kijamii ikiwemo mtazamo wao juu ya mwenendo wa kiuchumi. Mengine yalilenga kuwachanganya tu.





A video posted by Maisha Plus (@maishaplus2016) on Jun 5, 2016 at 10:39pm PDT


Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.

Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.


Mshiriki Grace Pemba anaelezea changamoto mbalimbali alizokutana nazo kutokana na kuolewa akiwa na umri mdogo, anasema hadi sasa ana watoto wawili ambao wanaishi na baba yao. Alipoulizwa maswali zaidi Grace alijawa na simanzi na kujikuta akitoa machozi, "Nimelia kwa sababu mmenikumbusha nyuma nilikotokea" anasema Grace mfanyakazi wa Saloon kutoka mkoani Mtwara.




Mshiriki Grace Pemba akijifuta machozi.


Wakati usaili ukiendelea hali ya kujaa kwa maji baharini ilitokea na kulazimisha timu ya Maisha Plus kubadili utaratibu wa awali wa upigaji picha.

Waandaaji wa mashindano ya Maisha Plus wakibadili utaratibu wa awali wa kupiga picha baada ya maji kujaa.
 

Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.

Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.

Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.

Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.

Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.

Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.

Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.





Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.


Mashindano ya Maisha Plus kwa mwaka huu yanatarajia kuchukua washiriki 30 kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Kenya, Tanzania na Uganda ambapo mshindi atajishindia ufadhili wa wazo la biashara lenye thamani ya Tzshs. Milioni 30.


"Mwaka huu washiriki wajipange sana. Maandalizi yaliyofanywa kufanikisha msimu huu hayajawahi kutokea katika historia ya Maisha Plus. Ni kama tunaanza moja" Alisema Masoud Kipanya, miongoni mwa majaji na waanzilishi wa mashindano haya.




"Tumewekeza katika teknolojia ya kisasa ili kupata picha za matukio yenye uhalisia zaidi. Watazamaji wategemee burudani safi isiyomithirika kupitia Azam Two." Alisema David Sevuri, miongoni mwa waanzilishi wa Maisha Plus.


Taarifa mbalimbali kuhusu mashindano haya zinapatikana kupitia tovuti rasmi ya www.maishaplus.tv

TPA YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

$
0
0
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari (TPA) yaadhimisha siku ya mazingira duniani kutokana na kutambua umuhimu wake kwa kuwa na mitambo mbalimbali ambayo inazalisha hewa ambayo inaweza kuharibu mazingira.

Hayo ameyasema Afisa Mwandamizi Mkuu wa Mazingira wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Thobias Mwasobwa amesema kuwa shughuli za bandari zianaenda na mitambo hivyo suala mazingira hawawezi wakaliacha likiharibu mazingira.

Amesema kuwa tangu kuanza kwa maadhimisho hayo wametoa elimu kwa watu 60 ambao watakuwa mabalozi katika utunzaji wa mazingira katika sehemu zao kazi kutokana na shughuli nyingi ambazo kwa namna moja au nyingine zinaweza zikaharibu mazingira. Aidha amesema wataendelea kutoa elimu zaidi juu mazingira na mabadiliko ya nchi kama mamlaka inalitambua na wanadhibiti jinsi ya kuweza kuhifadhi mazingira 
 
Baadhi ya wafanyakazi wa mamraka ya Bandari TPA wakifanya usafia katika eneo la Chuo Cha Bandari Dar es Salaam jana kwa ajili ya maadhimisho ya Usafi wa mazingira duniani.

Mwarobaini wa kukatika kwa umeme Arusha wapatikana Ni baada ya kukamilika kwa kituo cha kupoza umeme cha KIA, Wateja zaidi ya 89,000 waunganishwa

$
0
0
Na  Greyson Mwase, Arusha

 Imeelezwa kuwa kukamilika kwa kituo cha  kupoza umeme  cha KIA kilichopo karibu na  Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kilimanjaro  International Airport) kumepelekea tatizo  la kukatika kwa umeme kuisha katika mkoa wa Arusha na baadhi ya maeneo  ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro na kuongeza kipato   kwa wakazi wa mkoa huo.

Kauli hiyo ilitolewa na Meneja wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mkoa wa Arusha Mhandisi Gaspa Msigwa,  kwenye ziara ya waandishi wa habari kutoka  vyombo mbalimbali  vya habari nchini katika miradi ya  TEDAP na mradi wa usafirishaji umeme kutoka Iringa  hadi Shinyanga katika msongo wa kilovolti 400 (BITP) inayofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB).
Sehemu ya kituo cha kupoza umeme cha KIA 132/33kV kilichopo mkoani Kilimanjaro kama kinavyoonekana pichani.

Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kuona hatua za utekelezaji, mafanikio na changamoto za miradi hiyo pamoja na kupata maoni ya wanufaika wa miradi hiyo.

Akielezea mradi huo Mhandisi  Msigwa alisema ujenzi wa kituo hicho uliogharimu Dola za Marekani Milioni 7, ulianza mwaka  2011 na kukamilika mapema   Desemba mwaka  2013.

Alisema   kabla ya ujenzi wa kituo hicho, umeme ulikuwa unasafirishwa kutoka katika kituo cha Kiyungi kilichopo mkoani Kilimanjaro hadi jijini Arusha umeme ambao  ulikuwa hautoshelezi katika matumizi ya  majumbani na katika  viwanda vidogo.
Meneja Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mhandisi Emmanuel Manirabona (wa pili kutoka kulia) akielezea mafanikio ya kituo cha kupoza umeme cha KIA 132/33kV kilichopo mkoani Kilimanjaro.

Aliongeza kuwa  pia kulikuwepo na tatizo la kupotea kwa  umeme mwingi kutokana na  kusafirishwa katika umbali mrefu.

Jukwaa Langu June 6 2016: Haki, Wajibu na Nafasi ya DIASPORA kwa Tanzania

$
0
0
Photo Credits: WikiProject African Diaspora
Katika kipindi cha JUKWAA LANGU wiki hii, tumejadili kuhusu DIASPORA.
Ni ipi nafasi, wajibu na haki yetu katika nchi yetu (Tanzania)?
Ni kweli kuwa tuna watu ama mahala muafaka kutuwakilisha nchini kwetu?
Na je! Tuna vyanzo halisi vya habari na taarifa kutoka Tanzania?
Tu,eumgama ma waTanzania wa Uingereza na Marekani kujadili hili

Mahojiano na Chef Issa Kapande toka Sweden

$
0
0
Chef Issa ma ma-Chef  wa timu ya Stockholm, Sweden, waliposhiriki na kushika nafasi ya kwanza katika kipengele cha timu za kanda kwenye mashindano ya Kombe la Dunia la Mapishi  2014 yajulikanayo kama  Villeroy & Boch Culinary World Cup 2014  yaliyofanyika nchini Luxemborg.
Chef Issa Kapande ni mpishi maarufu na mmiliki wa mgahawa mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania nchini Sweden, unaojulikana kama Tanzania Restaurant.

Alikuwa mkarimu sana kujiunga na Mubelwa Bandio kuzungumzia safari yake katika fani ya upishi na mpaka alipofikia.
Karibu ujiunge nasi kusikiliza



UN yawapiga msasa wanafunzi wa UDOM kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)

$
0
0
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendesha semina fupi kuhusu Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) (hawapo pichani) inayoendelea mjini Dodoma chuoni hapa.

Katika kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo yanatakiwa kumfikia mtu mmoja mmoja, ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini (UN) imetoa mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), mafunzo ambayo yataweza kuwajengea uwezo kuhusu mpango huo na jinsi unavyoweza kubadili maisha yao.

Akizungumza na MO blog kuhusu mafunzo hayo, Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu alisema kuwa mafunzo hayo kwa wanafunzi wa UDOM ni sehemu wa mafunzo ambayo yanatolewa na ofisi ya UN nchini ili kuwawezesha Watanzania kuufahamu mpango huo ambao una malengo ya kubadili maisha ya kila mwananchi, mpango ambao utamalizika mwaka 2030.

Alisema katika mafunzo hayo wametoa elimu kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa wanafunzi zaidi ya 200 na hayo siyo mafunzo ya kwanza kwani wameshatoa mafunzo kama hayo kwa wabunge wa Tanzania lakini pia wameshafanya mafunzo kama hayo jijini Arusha ambapo yalihudhuriwa na vijana zaidi ya 200.

“Tunataka kila Mtanzania ajue kuhusu Malengo ya Maendeleo Eendelevu (SDGs) tumeshatoa elimu sehemu nyingine hii siyo ya kwanza na tutaendelea kwenda maeneo mengine kutoa elimu zaidi na katika hilo ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini ipo imejipanga kufanya hivyo,” alisema Bi. Temu.

Nae Mkuu wa Kitovu cha Mitaala katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Willy Komba alisema mafunzo hayo yamewajenga na kupata elimu ambayo walikuwa hawajaipata awali inayohusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na pia kueleza kutokana na umuhimu wake watakaa kuangalia ni jinsi gani wataweka katika mtaala wa masomo ili wanafunzi wajifunze kuhusu SDGs.

“Sababu na mimi ndiyo Mkuu wa kitengo cha mitaala nitakaa na wenzangu tuone jinsi gani tunaweza kuweka katika mitaala yetu ili hata wanafunzi wajifunze kama masomo, tunawashukuru kwa mafunzo yenu mmetupa changamoto mpya ambayo hatukuwa nayo,” alisema Komba.
Sehemu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakisiliza kwa makini wakati semina fupi kuhusu Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDGs) iliyoendeshwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, ambaye pia ni mmoja wa wakufunzi wa masuala ya SDGs, Hoyce Temu akifafanua jambo wakati wa semina fupi ilihusisha wanafunzi wa UDOM inayoendelea mjini Dodoma.



Mwanafunzi wa mwaka wa tatu UDOM wa Didgrii ya kwanza ya Mifumo ya habari na Mawasiliano, Lobezi Kulilo akihoji kuhusiana elimu ya SDGs kuwafikia watu walio vijijini.




Mwanafunzi wa Digrii ya kwanza ya Sayansi ya Kompyuta UDOM, Traygod Lyimo akiuliza swali kwa wakufunzi kuhusiana na SDGs.




Pichani juu na chini ni Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakipitia vipeperushi mbalimbali vyenye taarifa za kina kuhusu Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDGs) wakati wa semina fupi iliyoandaliwa na Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini.














Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wanafunzi wa UDOM wakati wa semina fupi kuhusu Malengo ya dunia iliyoandaliwa na Umoja huo mjini Dodoma jana.




Mkuu wa Kitovu cha Mitaala katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Willy Komba akitoa neno la shukrani kwa Umoja wa Mataifa kwa kuwapatia mafunzo ya SDGs mara baada ya kumalizika semina fupi kwa wanafunzi wa UDOM.




Kutoka kushoto ni Waziri wa Habari wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), James Msofe, Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, ambaye pia ni mmoja wa wakufunzi wa masuala ya SDGs, Hoyce Temu na Mwanafunzi wa mwaka wa tatu UDOM wa Didgrii ya kwanza ya Mifumo ya Upashanaji Habari, Lobezi Kulilo katika picha kumbukumbu wakilishilia mabango ya SDGs.




Baadhi ya wanafunzi wa UDOM walioshiriki semina fupi kuhusu SDGs iliyoandaliwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa chuoni hapo katika picha ya pamoja na vibao vyenye Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu.




Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa UDOM mara baada ya kumalizika kwa semina kuhusu Malengo ya Dunia iliyoandaliwa na Ofisi ya Umoja Mataifa mjini Dodoma jana.
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images