Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

HII NDIO SOKA NA KILA MPENDA SOKA HUWEKA PEMBENI TOFAUTI ZA KISIASA

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa soka nchini, kulia ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanznaia (TFF), Jamal Malinzi, Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Mpira wa Miguu nchini FAT Said El Maamry, upande wa kushoto ni Mwenyekiti wa zamani wa TFF Muhidini Ndolanga na  Rais wa zamani wa TFF Ndugu Leodgar Tenga muda mfupi kabla ya kuanza ka mechi ya Taifa Stars na Misri. 
 Viongozi na wapenzi wa soka wakiimba kwa pamoja wimbo wa Taifa kabala ya mechi kuanza.
 Viongozi na wadau wa michezo wakitoa heshima kwa kusimama wakati wa wimbo wa Taifa.
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze akizungumza na Khamis Mgeja kabla ya mechi haijaanza.
 Timu ya Taifa Stars ikipeleka mashambulizi kwenye goli la timu ya Misri hata hivyo mpaka mchezo umeisha Misri waliibuka na ushindi wa 2-0.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akitazama mechi ya Taifa Stars, wengine pichani ni Rais wa TFF Ndugu Jamal Malinzi na Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Frederick Sumaye.




WANANCHI WA KISIWA PANZA KISIWANI PEMBA WATAKIWA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILILI YA TABIA NCHI

$
0
0

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akipanda mbegu za miti ya mikoko katika eneo la kisiwa cha Panza ikiwa ni siku ya uzinduzi wa upandaji miti hiyo kisiwani Pemba, kushoto ni Afisa Mazingira mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Cretus Shengena.


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb) amewataka wananchi wa kisiwa Panza katika Mkoa wa Kusini Pemba, kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi kwa kutunza mazingira hasa kwa kupanda miti ya mikoko kwa wingi,ili kunusuru kisiwa hicho kumezwa kutokana na kuongezeka kwa kina cha bahari.

Mhe. Mpina ameyasema hay leo kisiwani Pemba alipozingua kampeni maalum ya kupanda miti ya mikoko ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kupanda miti.

Awali Mhe. Mpina alisemakuwa, serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeweza kupata kiasi cha fedha shilingi milioni 165 maalum kwa kuhimili athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi kwa kujenga kuta za fukwe za Ocean Road jijini Dar es Salaam,Pangani Mjini Tanga, Kilimani mjini unguja na kisiwa Panza kisiwani Pemba.

Naibu wa Waziri wa Wizara ya Nishati, Maji na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Juma Makungu Juma (Kushoto), akimueleza jambo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Mpina (katikati) walipokuwa wakielea kupanda miti ya mikoko kisiwa panza kusini Pemba. Kulia ni Muwakilishiwa mkuu wa Wilaya.

Aliongeza kuwa, kiasi hicho cha fedha pia kimeanza kutumika katika kampeni hiyo ya kitaifa ya kupanda miti kwa kupanda miti ya mikoko katika eneo la kisiwa Panza na ambapo miti zaidi ya milioni Moja inatarajiwa kupandwa katika eneo la hekta 238, kisiwani pemba, pamoja na zoezi hilo kuzinduliwa leo kisiwani pemba, miti hiyo aina ya mikoko pia inatarajiwa kupandwa katika maeneo ya kilimani mjini unguja,bwawani,tovuni, micheweni na Rufiji.

Naibu Waziri Mpina aliongeza kwa kusema kuwa suala la mazingira si suala la Muungano lakini serikali hizi mbili zimeona umuhimu wa kushirikiana katika eneo hili ili kuweza kukabiliana kikamilifu na madhara na hasara zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabia nchi ili kunusuru visiwa hivi kumezwa na bahari.

Akitolea mfano wa shule ya msigi na sekondari kisiwapanza ambazo zipo hatarini kumezwa, mhe Mpina aliongeza kuwa wataalam wa masuala ya mazingira watafanya tathmini kikamilifu na kuona namna gani serikali inaweza kuongeza mbinu zaidi za kushughulikia maeneo haya hatarishi, ili maji ya bahari yasiweze kuingia katika maeneo ya makazi.

Naibu Waziri Mpina aliwasisitizia wananchi wa kisiwa panza kutunza mazingira kwa kutokukata miti ovyo na kuchoma misitu na watunze na kuilinda miti ya mikoko iliyopandwa ili kuweza kufikia dhamira ya kukinusuru kisiwa icho kumezwa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mazingira kutoka katika wizara ya Ardhi,Maji,Nishati,na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Juma makungu Juma amesema maeneo mengi ya Zanzibar yaliyopo pembezoni mwa bahari yameharibiwa na shughuli za binadamu, hivyo upandaji wa miti ya mikoko katika maeneo hayo utazuia adhari za mabadiliko ya tabia nchi kwa makazi ya watu na mashamba ambayo yamepelekea watu kuanza kuhama katika makazi yao na haya yote ni matokea ya vitendo vya wananchi.

Wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira na Idara ya Mazingira ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa nadani ya boti kuelekea kiwapanza kisiwani, mkoa wa kusini  Pemba kushiriki zoezi la uzinduzi wa kupanda miti ya mikoko.(Picha na Habari zote na Evelyn Mkokoi).

Zoezi hilo la kupanda miti ya mikoko lililofanyika kisiwani pemba limeenda sambamba na maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambayo hufanyika tarehe tano Juni kila mwaka.

Azania Bank Kids Run 2016 zavutia wengi Dar

$
0
0
 Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka akizungumza katika mbio hizo.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Azania Bank ambao ni wadhamini wakuu wa mbio hizo akizungumza katika mbio hizo.
Mgeni rasmi katika mbio hizo, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo, Dioniz Malinzi akitoa hotuba yake.
  Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT), Dioniz Malinzi  akimpongeza mshindi wa kwanza wa mbio za mita 5 za  Azania Bank Kids Run, Mathayo Sima.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT), Dioniz Malinzi  akimvisha medali mshindi wa kwanza wa mbio za Kilometa 5, Mathayo Sima.
 Mshindi wa kwanza wa mbio za Azania Bank Kids Run 2016 za kilometa 5, Mathayo Sima akipokea zawadi zake kutoka kwa mgeni rasmi.
 Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi (wa tatu kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mbio za Watoto wa Azania Bank Kids Run 2016 akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa mbio za kilometa 5 wavulana. Wengine katika picha ni Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka (wa tatu kulia) pamoja na viongozi wa Benki ya Azania ambao ni wadhamini wakuu wa mbio hizo.

 Watoto wakishiriki mbio za Watoto zilizopewa jina la Azania Bank Kids Run 2016 wakianza mbio za Kilometa moja katika viwanja vya Mnaza Mmoja jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Francis Dande) 
 Askari wa usalama Barabarani akiwa tayari kuongoza mbio hizo.
 Washiriki wakitimu mbio.
Washiriki wa mbio za Kilometa 2 wakianza kutimua mbio.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT), Dioniz Malinzi  akizindua mbioza  Azania Bank Kids Run  zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mbio za mita tano wakianza kutimua mbio.
Washiriki wa mbio za mita tano wakianza kutimua mbio.
Washiriki wa mbio za mita tano wakianza kutimua mbio.
Washiriki wa mbio za mita tano.
Washiriki wa mbio za mita tano.
Mathayo Sima akiwa amewaacha mbali wenzake. 
Mathayo Sima akimaliza mbio za Kilometa 5 na kuibuka mshindi wa kwanza.
 Mshindi wa kwanza wa mbio za Kilometa 5 wavulana, Mathayo Sima akiwa na furaha baada ya kumaliza mbio.
Washiri wa mbio za Kilometa 5 wakimaliza.
  Baadhi ya washiriki wakimalizia mbio za Kilometa 5.

 Watoto wakishiriki mbio za mita 50
Watoto wakionyesha umahiri wa kukimbia mbio fupi.
 Wototo wakichuana.
 Wanariadha wakichuana katika mbio za mita 50.
 Watoto wakiwa na wazazi wao kabla ya kuanza mbio za Mita 100.
Watoto wakikimbia mita 50

Na Mwandishi Wetu

MBIO za Watoto zilizopewa jina la Azania Bank Kids Run 2016, zimefanyika leo jijini Dar es Salaam, ambako Mathayo Sima, aliibuka mshindi katika mbio za kilomita 5 wavulana, akifuatiwa na Antidius Martin.



Katika mbio hizo zilizodhaminiwa na Benki ya Azania, Joshua Paulo alikamata nafasi ya tatu, ambako kwa ushindi huo Mathayo alijishindia medali, fedha taslimu Sh. 200,000, huku Antidius akitwaa medali na Sh. 150,000, wakati mshindi wa tatu Joshua akitwaa medali na sh. 100,000.



Wakali hao pia walijipatia kila mmoja begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo, zawadi ambazo walizipata washindi wa nne hadi wa 10, waliopata pia kifuta jasho cha sh. 15,000.


Washindi wengine na nafasi zao kwenye mabano ni: David Frank (4), Joram Deus (5), Israel Jiro (6), Omary Bawazir (7), Bakari Ali (8), Rahim Seif (9) na Joseph Fabian (10),
Naye George Richard aliibuka kinara wa mbio za kilomita mbili kwa wanaume, akifuatiwa na Florence Lucas, nafasi ya tatu ikichukuliwa na Kassim Khamis. George alijishindia sh. 100,000, huku Florence akijipatia sh. 75,000 na wa tatu ambaye ni Kassim akibeba sh. 50,000.

Hiyo pia ilikuwa ni kategori ambayo pia washindi wa nne hadi wa 10 walijipatia kifuta jasho cha sh. 15,000 na ma begi yenye vifaa vya shule na sare za michezo.

Washindi wa nne hadi wa 10 na nafasi zao kwenye mabano ni: Benjamin Jonathan (4), Edwin Honest (5), Sumeili Letahe (6), Abraham Ali (7), Hamisi Saidi (8), Wilson Daud (9) na Mustapha Hussein (10).

Kwa upande wa wasichana, waliong'ara katika km 2 za Azania Bank Kids Run 2016 ni kinara Regina Deogratius, mshindi wa pili Shadia Ahmad na mshindi wa tatu ni Agness Ernest, ambako Regina alijitwalia medali na fedha kiasi cha shilingi 75,000, Shadia akajishindia medali na pesa sh. 50,000, huku Agness akitwaa medali na sh. 40,000.

Washindi wa mbio za kilomita moja wavulana na nafasi zao kwenye mabano ni: Emmanuel Daud (1), Mecko Hussein (2), Manyama Ephata (3), Awadh Abdulaziz (4) na Ezra Damas (5).

Wengine waliofanya vema kwenye kategori hiyo ni pamoja na Erick Yohana (6), Sebo Hussein (7), Mohamed Ismail (8), Hans Jacob (9) na Deus Pendael (10).
Upande wa wasichana, kilomita moja mshindi alikuwa ni Angela Edwin, mshindi wa pili ni Mariam Jabir, huku mshindi wa tatu akiwa ni Mency Adam.

wengine na nafasi zao kwenye mabano ni: Angel Elman (4), Veronica Adam (5), Feada Manyama (6), Merin Frank (7), Truresha Omary (8), Maria Lohan (9) na Neema Jonas (10).

BENKI YA POSTA YAWASAIDIA VIJANA BIHARAMULO

$
0
0
Meneja Mahusiano Mwandamizi wa Benki ya Posta Tanzania Noves Moses(katikati) akionyesha fedha kissing cha shilingi milioni 8 zilizotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya kuwasaidia vijana waendesha bodaboda wa Wilaya ya Biharamulo. Wa kwanza kushoto Ni Mbunge wa jimbo la biharamulo Oscar Mukasa, Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Darry Rwegasira na kulia Ni Diwani wa kata ya Biharamulo mjini David Mwenenkundwa na Meneja wa TPB tawi la Bukoba Juvestina Tarimo.

Na Angela Sebastian, Biharamulo.

WAENDESHA pikipiki zinazofanya biashara ya kubeba abiria katika Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wameshauriwa kujiunga katika vikundi rasmi na vya uzalishaji mali ili waweze kunufaika na fursa za huduma za kibanki ambazo hutolewa na banki ya posta Tanzani .

Ushauri huo ilitolewa jana na mkuu wa Wilaya hiyo Darry Rwegasila wakati akifungua mafunzo ya waendesha pikipiki zaidi ya 100 waliopata mafunzo ya udereva na kupewa leseni kwa udhamini wa banki ya posta hiyo.

sema kuwa umoja ni nguvu kwahiyo wakiunda umoja wanakuwa na sauti moja pia hata viongozi wataweza kupata mawazo yao kwa urahisi kupiti umoja huo ili kuwatafutia fursa mbambali au kutatua changamoto zao zinazowakabili na kupandisha uchumi wao wa kipatao.

Alisema kuwa makondi hayo yatasaidia kuingia katika mfumo rasmi ambao utawawezesha kupata huduma zinazotolewa na taasisi mbalimbali kama vile banki ya posta ambazo zinalenga kuwakwamua vijana katika lindi la uamskini unaowakabili pia unaonekana kuwa kero kubwa katika maisha yao ya kila siku.

“Mkitaka kuingia katika soko hulia lazima muwe na umoja ili muweze kufikia raslimalia zinazopatikana kama vile kupata misaada,mikopo na mafunzo kama haya waliowaletea watu wa banki ya posta kutokan ana faida wanayoipata na kugawana na wahitaji” alisema Dc.

Pia aliwashauri kuacha kufanya matumizi yasiyo ya maana ,bali watumie kidogo wanachokipata kujiwekea akiba banki ili waweze kukuza mitaji yao kwani wao ni vijana bado wanamahitaji mengi.

Kwa upande wa meneja mahusiano mwandamizi wa banki ya posta Tanzania Noves Moses alisema kuwa banki hiyo inajali wananchi ,pia vijana ni kundi kubwa lenye mchango mkubwa katika suala zima la uchangiaji wa uchumi wa Taifa.

Alisema banki hiyo walipata maombi toka kwa mbunge wa jimbo la Biharamulo Oscara Mukasa akiomba kuwawezesha vijana hao kupata mafunzo na kupewa leseni ili kuondoka ana adha ya kukimbizana na polisi kila kukicha na kupoteza muda mwisngi ambapo hushindwa kujiingizia kipatao.

Alisema banki hiyo ilikubali ombi hilo ambapo ametoa kiasi cha shilingi milioni 8 kwa ajili ya mafunzo hayo ya kupata leseniya uendeshaji wa vyombo hivyo vya moto kwa vijana 100 kwa Wilaya ya hiyo.Alisema kuwa banki hiyo imejiwekea mikakati mikubwa ya kuleta na kuimalisha ustawi wa ndani ya jamii ambapo misaada mingi wanayoitoa huelekezwa katika eneo hilo ambayo hulenga masuala ya afya na elimu.

Naye mbunge wa jimbo la Biharamulo aliyeomba msada huo kwa ajili ya vijana wake Oscar Mukasa alisema kuwa ni wajibu wake kuboresha maisha ya vijana waliko jimboni mwake ili waondokane na mambo yanayoweza kuwapelekea kujiingiza katika vitendo viovu ikiwemo uvunjifu wa amani na maandamano yasiyofaa.

Mukasa alisema lengo la kuomba banki hiyo itoe msaada huo ni kuhakikisha vijana wanaepukana na maisha ya misukosuko ya kukosa leseni ambayo walikuwa wakikumba na nayo.

Katibu Mkuu Mambo ya Ndani aitaka mikataba ya miradi ya nyumba polisi

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kulia) na wasaidizi wake wakitoka katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi la Oysterbay jijini Dar es salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira ameliagiza Jeshi la Polisi kuwasilisha Mkataba wa Miradi ya ujenzi wa nyumba za kuishi askari eneo la Kunduchi, Mikocheni pamoja na Kituo cha polisi cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, mradi unaohusisha pia majengo mbalimbali ya Mwekezaji ambaye Jeshi la Polisi limeingia nae Mkataba.

Katibu Mkuu amesema mradi huo ni mkubwa sana na wa muda mrefu na hivyo ameliagiza jeshi hilo kuuwasilisha Mkataba huo ambao utekelezaji wake unaendelea ili aweze kuufahamu vizuri mkataba huo unaolihusisha Jeshi la Polisi na Mwekezaji wa Kampuni ya Mara World Tanzania limited.

Jenerali Rwegasira ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki muda mfupi baada ya kukagua miradi hiyo katika maeneo ya Kunduchi na Mikocheni ambako zinajengwa nyumba za kuishi askari wa jeshi hilo na kwamba ujenzi wake bado unaendelea. Jenerali Rwegasira ametembelea pia mradi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi eneo la Oysterbay ili kuona maendeleo ya ujenzi huo sambamba na kufahamu hatua iliyofikiwa hadi sasa katika maeneo hayo ya jeshi.

Aidha mwekezaji huyo ambaye ni Kampuni ya Mara World Tanzania limited katika eneo la Polisi Oysterbay atajenga kituo cha polisi cha kisasa, ofisi za kukodisha, hospitali, maduka makubwa na hoteli.Kwa upande mwingine, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara yake ya Uhamiaji imewahamisha jumla ya Maofisa na askari wa Idara ya Uhamiaji hamsini na tisa (59) kutoka Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam na wilaya zake walikokuwa wakifanya kazi na kupelekwa sehemu mbalimbali nchini.

Akizungumzia uhamisho huo, Meja Jenerali Projest Rwegasira amesema uhamisho huo umefanyika ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika Idara ya Uhamiaji, ambapo amesisitiza kuwa zoezi hilo la kuwahamisha Maofisa wa Idara ya Uhamiaji linaendelea kufanyika nchi nzima ikiwa ni hatua za kuboresha utendaji kazi na hivyo kuongeza ufanisi zaidi wa kiutendaji.

Jenerali Rwegasira ameeleza kuwa watumishi wote waliopewa uhamisho wanatakiwa kuripoti kwenye vituo vyao vipya mara moja na kutoa angalizo kuwa mtumishi yeyote atakayeshindwa kuripoti kwa visingizio mbalimbali atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwemo kuachishwa kazi.

MTOTO DANIEL AIBIWA, MSAADA KWA ATAKAYE MUONA ATOE TAARIFA POLISI

$
0
0
Kijana Daniel anayetafutwa na wazazi wake.

Kijana Daniel ambae anatafutwa na wazazi wake amepotea tangia jana huku juhudi kubwa ya kumtafuta inayofanywa na wazazi, ndugu zake zikiwa bado hazijafanikiwa. Maa ya mwisho kijana Daniel alionekana na kijana anayekisiwa kuwa na Umri wa Miaka 7 Eneo la Africana akiwa amechoka huku akimvuta kuelekea njia ya Tegeta.

Tunaomba Watu, Mtu yeyote atakayeweza kumuona basi anaweza kumfikisha Kituo Cha Polisi kilicho karibu nae.Kwa bahati mbaya aiyetuma ujumbe huu katika makundi mbalimbali ya Whatsapp hakuweza kuweka namba zake za simu. 

Lakini Endapo mtu atamuona basi anaweza kutoa taarifa Polisi au hata Pia Kutoa taarifa kupitia makundi mbalimbali ya Whatsapp ambayo tunaamini pia taarifa itawafikia haraka wazazi au hata ndugu kama ambavyo taarifa ya kupotea kwake ilivyoweza kutufikia sisi na kuamua kutoa msaada wa kutangaza kupitia hapa.

Tunajua ni jinsi gani Maumivu wanayoyapata wazazi wake lakini Tunamuombea kwa Mungu amlinde huko aliko na Malaika wake wamrudishe kijana wetu Daniel Salama Salimini kwenye himaya ya wazazi wake.

Lukaza Blog inatoa pole kwa Wazazi kwa kupotelewa na Mtoto wao Kipenzi lakini tunapenda kuwaambia kuwa Wamwamini Mungu kwa maana Kila hatua wazikabidhizo kwake na kuamini basi Mungu atawatendea.

Waziri JANUARY MAKAMBA ashiriki Kilele cha Siku ya Mazingira

$
0
0
Waziri wa Mazingira January Makamba akionesha Ufundi wa Kuzima Moto, ikiwa ni shamrashamra za Kilele cha Siku ya Mazingira katika Viwanja vya Mwembe yanga Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mazingira January Makamba akihutubia Wananchi waliojitokeza katika kilele cha Siku ya Mazingira katika Viwanja vya Mwembe yanga Jijini Dar es Salamm. 
Wananchi Wakipita Mbele ya Mgeni Rasmi kuonesha zana za Kufanyia Usafi....
Waziri wa Mazingira January Makamba akifurahia jambo na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida mara baada ya kuwasili viwanja vya Mwembe yanga.

RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA IBADA KANISA LA MAOMBEZI LA MCHUNGAJI ANTONY LUSEKELO ‘MZEE WA UPAKO’ UBUNGO KIBANGU

$
0
0


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo wakati akiagana na Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ katika kanisa lake la Maombezi lililopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. Rais Dkt. Magufuli alihudhuria ibada hiyo pamoja na kukagua barabara inayotoka Ubungo Kibangu hadi Barabara ya Mandela eneo la Riverside.
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi Mchungaji Anthony Lusekelo ‘mzee wa upako akiagana na mke wa Rais Mama Janeth Magufuli mara baada ya kuhudhuria  ibada katika Kanisa la Maombezi Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais Dkt. Magufuli akiwashukuru waumini (hawapo pichani ) wa kanisa hilo la Maombezi la Mzee wa Upako.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakati wakitoka kwenye kanisa la Maombezi la Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

OLE SENDEKA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYANI KILWA MKOANI LINDI, AFURAHI KUONANA NA ALIYEKUWA MGOMBEA MWENZA WA MREMA MWAKA 1995

$
0
0
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa akizungumza wakati wa kuagana na Msemaji wa CCM, Chrisopher Ole Sendeka, mwishoni mwa ziara ya Msemaji huyo wa Chama, katika wilaya ya Kilwa mkoani humo.
 Katibu wa CCM mkoa wa Lindi Adelina Geffi, akimshukuru Msemaji wa CCM, leo wakati wa kuagana mwishoni mwa ziara ya msemaji huyo wilayani Kilwa mkoani Lindi.
 Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akizungumza na viongozi wa  CCM mkoa wa Lindi na Wilaya ya Kilwa, mwishonimwa ziara yake katika wilya hiyo leo.

 Msemaji wa CCM, Ole Sendeka akitembezwa na Sultani Ahmed Sultani, Sultani alipomtembeza katika eneo la kitegauchumi cha hoteli yake katika mji mdogo wa Kilwa mkoani Lindi kabla ya kuondoka kurejea Dar es Salaam, leo
Sultani Ahmed Sultani akimuonyesha mradi wa kutengeneza madawati Msemaji wa CCM, Ole Sendeka, Sendeka alipotembelea mradi huo leo kabla ya kurejea Dar es Salaam, baada ya ziara yake wilaya Kilwa mkoani Lindi.

 Msemaji wa CCM Christpher Ole Sendeka, akipozi na Sultani Ahmed Sultani ambaye aliwahi kuwa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya NCCR Mageuzi, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 ambapo Mgombea Urais wa Chama hicho alikuwa Augustine Mrema. Sendeka amekutana na Sultani baada ya kuagana na viogozi wa CCM mwishoni mwa ziara yake wilayani Kilwa mkoani Lindi leo asubuhi. Hafla hiyo ya kuagana ilifanyika kwenye Hoteli ya Sultani, Kilwa Masoko.
 Msemaji wa CCM Christpher Ole Sendeka, akifurahia jambo na Sultani Ahmed Sultani ambaye aliwahi kuwa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya NCCR Mageuzi, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 ambapo Mgombea Urais wa Chama hicho alikuwa Augustine Mrema. Sendeka amekutana na Sultani baada ya kuagana na viogozi wa CCM mwishoni mwa ziara yake wilayani Kilwa mkoani Lindi leo asubuhi. Hafla hiyo ya kuagana ilifanyika kwenye Hoteli ya Sultani, Kilwa Masoko.
 Msemaji wa CCM Christpher Ole Sendeka, akimpongeza Sultani Ahmed Sultani ambaye aliwahi kuwa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya NCCR Mageuzi, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 ambapo Mgombea Urais wa Chama hicho alikuwa Augustine Mrema. Sendeka amekutana na Sultani baada ya kuagana na viogozi wa CCM mwishoni mwa ziara yake wilayani Kilwa mkoani Lindi leo asubuhi. Hafla hiyo ya kuagana ilifanyika kwenye Hoteli ya Sultani, Kilwa Masoko.
 Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa na Katibu wa CCM wa mkoa huo, Adelina Geffi kabla ya kuondola Wilayani Kilwa mwishoni mwa ziara yake wilayani humo mkoani Lindi leo. Kulia ni Mmiliki wa hoteli walipokuwa, Sultani Ahmed Sultani
 Msemaji wa Chama Ole sendeka akiwa katika picha ya pamoja
 Msemaji wa CCM, Ole Sendeka akielekezwa jambo, na Sultani Ahmed Sultani, Ali alipomtembeza katika eneo la kitegauchumi cha hoteli yake katika mji mdogo wa Kilwa mkoani Lindi kabla ya kuondoka kurejea Dar es Salaam, leo
 Sultani Ahmed Sultani akiwa amemfungulia mlango wa gari, Msemaji wa CCM, Ole Sendeka alipotaka kuondoka katika eneo la hoteli yake, katika mji mdogo wa Kilwa mkoani Lindi leo
 Msemaji wa CCM, Ole Sendeka akiagana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa  

 Msemaji wa CCM Ole Sendeka akiingia katika gari tayari kwa safari ya kurudi Dar es Salaam
Msemaji wa CCM, Ole Sendeka akianza safari yake ya kurudi Dar es Salaam, baada ya ziara yake ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama katika wilaya ya Kilwamkoani Lindi leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

Kampuni ya Auto Xpress yazinduwa Tawi lake Dar es Salaam

$
0
0
Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joseph Malongo (wa pili kulia) akikata utepe kuzinduwa Kampuni ya Auto Xpress tawi la Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Makapuni ya Auto Xpress, Sandeep Shah pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Auto Xpress Tanzania, Leonard Mususa (wa kwanza kulia).Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joseph Malongo (wa pili kulia) akikata utepe kuzinduwa Kampuni ya Auto Xpress tawi la Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Makapuni ya Auto Xpress, Sandeep Shah pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Auto Xpress Tanzania, Leonard Mususa (wa kwanza kulia).Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joseph Malongo (wa pili kulia) akikata utepe kuzinduwa Kampuni ya Auto Xpress tawi la Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Makapuni ya Auto Xpress, Sandeep Shah pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Auto Xpress Tanzania, Leonard Mususa (wa kwanza kulia).Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joseph Malongo (wa pili kulia) akikata utepe kuzinduwa Kampuni ya Auto Xpress tawi la Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Makapuni ya Auto Xpress, Sandeep Shah pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Auto Xpress Tanzania, Leonard Mususa (wa kwanza kulia).Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joseph Malongo (wa pili kulia) akizungumza katika uzinduzi wa Kampuni ya Auto Xpress tawi la Dar es Salaam.Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joseph Malongo (wa pili kulia) akizungumza katika uzinduzi wa Kampuni ya Auto Xpress tawi la Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Makapuni ya Auto Xpress, Sandeep Shah akizungumza kabla ya uzinduzi wa kampuni hiyo kwa tawi la Dar es Salaam. Kampuni ya Auto Xpress tawi la Tanzania inafanya kazi ya ukaguzi wa magari kiufundi (service) kwa mfumo wa kisasa kwa kutumia kompyuta pamoja na uuzaji wa vifaa madhubuti kwenye magari. Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Makapuni ya Auto Xpress, Sandeep Shah akizungumza kabla ya uzinduzi wa kampuni hiyo kwa tawi la Dar es Salaam. Kampuni ya Auto Xpress tawi la Tanzania inafanya kazi ya ukaguzi wa magari kiufundi (service) kwa mfumo wa kisasa kwa kutumia kompyuta pamoja na uuzaji wa vifaa madhubuti kwenye magari.

HAWA NDIO MABALOZI WA BIDHAA YA SANSAN

$
0
0
 MKURUGENZI WA SANSAN MR. MEJA MMASI AKINA BRAND  AMBASSORDOR WA BIDHAA HIZO RAHMA AWADHI NA WAREMBO WENGINE
 MSHINDI WA PILI WA MISS ARUSHA 2016 RAHMA AWADHI AKIWA NA   WAREMBO WENGINE WAKIONYESHA ISHARA YA NGUMI KAMA UIMARA WA BIDHAA  HIZO
 MSHINDI WA PILI WA MISS ARUSHA 2016 RAHMA AWADHI NDIE  BRAND AMBASSADOR WA BIDHAA ZA SANSAN AMBAO NDIO WALIOKUWA WADHAMINI WA  MSHINDI WA PILI
RAHMA BRAND AMBASSADOR WA BIDHAA ZA SANSAN  AKIWA NA   WAREMBO WENGINE NA BAADHI YA BIDHAA HIZO

MBWANA SAMATTA PAMOJA NA WASANII WA SHIWATA WAKABIDHIWA MAENEO YAO KATIKA KIJIJI CHA WASANII WILAYANI MKURANGA.

$
0
0

 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (katikati) akimkabidhi cheti cha umiliki wa eneo la ukubwa wa ekari tano baba yake Mbwana Samatta kwa niaba ya mwanae Mbwana Samatta wakati wa hafla ya uwagawaji maeneo kwa ajili ya wasanii na Mwanasoka huyo bora wa ndani ya Afrika Juni, 2016 Wilayani Mkuranga. 

 Baadhi ya nyumba katika kijiji cha Wasaanii kama zinavyoonekana katika picha Wilayani Mkuranga. 

 
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Leah Kihimbi (wa pili kulia) akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasaanii Tanzania (SHIWATA) Bw. Casim Taalib (kulia) pamoja na Afisa Utamaduni Wilayani Mkuranga kukagua nyumba za Wasanii 5 Juni, 2016 Wilayani Mkuranga.


JIJI LA ARUSHA LAKABILIWA NA TATIZO LA UHABA WA VIWANJA VYA MICHEZO

$
0
0
Picha maktaba uwanja wa sheik Amri Abeid


Na Woinde Shizza, Arusha

JIJI la Arusha linakabiliwa na uhaba mkubwa wa viwanja vya michezo
hali inayochangia timu nyingi kushindwa kufanya vizuri kutokana na
kutokuwa na eneo maalumu la kufanyia mazoezi.

Hayo yalisemwa jana na Mratibu wa ligi ya kombe la vijana la Sakina
,Musa Giriba wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa ligi hiyo
inayoshirikisha timu 14 zinazocheza ambapo fainali watapatikana
mshindi wa kwanza hadi wa tatu michezo inayofanyika katika viwanja
vya shule ya msingi Ngarenaro.

Alisema kuwa,jiji la Arusha kuna timu nyingi zenye mwamko na
zinazopenda michezo ila changamoto inakuja kwenye viwanja vya kufanyia
mazoezi hali inayowafanya vijana wengi kukata tamaa.

Giriba alisema kuwa, kombe hilo la vijana la Sakina linalenga
kuwasaidia vijana kuona umuhimu wa kupenda masomo na kutumia muda wao
mwingi kwenye mazoezi na kuondokana na makundi yasiyofaa ikiwemo ya
uvutaji wa madawa ya kulevya.

Alisema kuwa, pamoja na kujitahidi kuwaweka vijana pamoja na kuunda
timu hizo bado wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa vifaa
vya michezo ikiwemo jezi,mipira na nyavu,hivyo aliomba wadau
mbalimbali kujitokeza kusaidia timu hizo .

‘kwa kweli timu nyingi zinafanya vizuri sana na zinapenda kuendelea
mbele zaidi ila tuna changamoto ya wafadhili wa timu zetu ,kwani mpaka
sasa hivi hatuna wafadhili na tunajiendesha wenyewe kwa kusuasua
,hivyo tunaomba wadau watusaidie ili tufanye vizuri zaidi’alisema
Giriba.

Alitaja timu hizo zinazocheza kuwa ni Town Centre FC,Chinga
City,Sakina youth , Kali Star, Gaza Fc,Kivalovumba,Esso Star,Baston
Fc,Kim Power,Weekend , Morris ,Kilombero Star ,Pentagon na Mchichi Fc.

Naye Afisa michezo wa jiji la Arusha , Benson Maneno alisema kuwa
kutokana na changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ya viwanja vya
mipira wamejipanga kutengeneza uwanja wa shule ya sekondari Arusha
ambapo tayari wametenga bajeti shs 70 milioni.

Maneno alisema kuwa,fedha hizo ni kwa ajili ya kutengeneza uwanja huo
ili timu zote ziweze kushiriki na kufanya mazoezi muda wote na
hatimaye kukuza na kuinua vipaji vya wanamichezo jiji la Arusha .

Alisema kuwa,wanasubiri bajeti hiyo ipitishwe mwaka wa fedha mwezi wa
7, ambapo aliahidi kuipatia timu hiyo nyavu za magoli na mipira minne
wakifika nusu fainali.

TAARIFA YA UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKALA WA UAGIZAJI WA MAFUTA KWA PAMOJA (PBPA)

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

                                                                                                                          
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter M. Muhongo (Mb), amemteua Dk. Steve Mdachi kuwa Mwenyekiti waBodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), kuanzia tarehe 03 Juni, 2016.

Kufuatia uteuzi huo, amewateua pia wafuatao kuwa Wajumbewa Bodi ya Wakurugenzi ya PBPA kuanzia tarehe 03 Juni, 2016.

1.  Dkt. Daniel Sabai

2.  Dkt. Henry  Chalu

3.  Dkt. Siasa Mzenzi

4.  Mr. Salum Mnuna


 Imetolewa na;
KATIBU MKUU

6 Juni, 2016



WAZIRI MAGHEMBE AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA NA WAHARIRI KUTOKA VYOMBO MBALIMBALI MKOANI MOROGORO LEO

$
0
0
Waziri wa Maliasili na utalii Mh.Jumanne Maghembe akifungua mkutano wa mwaka wa hifadhi za Taifa Tanzania na wahariri na waandishi waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha VETA mjini Morogoro leo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Kebwe Steven Kebwe. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro leo, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa hifadhi za Taifa Tanzania na wahariri pamoja na waandishi wa andamizi nchini.
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi wakimsikiliza waziri wa Maliasili na utalii,Jumanne Magembe Mjini Morogoro leo.
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi wakimsikiliza waziri wa Maliasili na utalii,Jumanne Magembe Mjini Morogoro leo,alipokuwa akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa hifadhi za Taifa Tanzania na wahariri pamoja na waandishi wa andamizi nchini.
Baadhi ya Wahariri na waandishi waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakijadiliana jambo kabla ya mkutano huo kuanza,mjini morogoro leo

Washindi wa promosheni ya milioni 100 na tusker fanya kweli uwini Watajwa.

$
0
0
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Serengeti Breweries (SBL) mkoa wa  Arusha ,Orest Mmbaga akikabidhi mfano wa Hundi ya Sh Milioni moja kwa Eliasi Polo mkazi wa Moshi akiwa ni miongoni mwa washindi 10 wa kwanza wa Promosheni ya Tusker Fanya kweli.Makabidhiano ya Hundi yamefanyika katika baa ya Kinondoni iliyopo eneo la Kiusa,Moshi mjini.
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Serengeti Breweries (SBL) mkoa wa Kilimanjaro,Godwin Seleli akikabidhi mfano wa Hundi ya Sh Milioni moja kwa Deogratius Shayo  wa Moshi akiwa ni miongoni mwa washindi 10 wa kwanza wa Promosheni ya Tusker Fanya kweli .Makabidhainao ya Hundi yamefanyika katika baa ya Kinondoni iliyopo eneo la Kiusa,Moshi mjini.
  Meneja Masoko wa Bia ya Tusker Nandi Mwiyombela (kushoto) akimkabidhi mfano wa Hundi mmoja wa washindi 10 wa kwanza wa Promosheni ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini Michael Mwinuka mkazi wa Tabata Dar es Salaam katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
 Meneja Masoko wa Bia ya Tusker Nandi Mwiyombela (kushoto) akimkabidhi mfano wa Hundi mmoja wa washindi 10 wa kwanza wa Promosheni ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini Sebastian Joseph mkazi wa Bunju Dar es Salaam katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
 Meneja Masoko wa Bia ya Tusker Nandi Mwiyombela akieleza jambo kwa wageni waalikwa wakati wa hafla ya kukabidhi hundi kwa washindi wanne kutoka Dar es Salaam ambao ni kati ya  washindi kumi wa kwanza wa promosheni ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli 
Mmoja ya washindi kumi wa kwanza wa promosheni ya Tusker Fanya Kweli na Uwini Festo Silvester ambaye ameshinda mara mbili na kupata jumla ya pesa taslim Million 2, akitoa shukrani kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti mara baada ya kukabidhiwa pesa zake.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,PROF JUMANNE MAGHEMBE AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TANAPA NA WAHARIRI NA WAANDISHI WA HABARI WAANDAMIZI.

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa kufungua Mkutano wa mwaka wa Hifadhi za Taifa (TANZANIA) na Wahariri,Wanahabari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari ,mkutano unaofanyika katika ukumbi wa VETA mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Kebwe Stephen Kebwe akizungumza wakati  ufunguzi mkutano wa mwaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania na Wahariri,Wanahabari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari .
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati wa mkutano  wa mwaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania ,Wahariri,Wanahabari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari 
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akitoa maelezo ya awali kuhusu mkutano wa mwaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania ,Wahariri,Wanahabari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari ,Mkutanoo unaofanyika mkoani Morogoro.
Baadhi ya Wahariri na Wanahabr waandamizi wakiwa katika mkutan huo.
Baadhi ya Wahariri na Wanahabari waandamizi wakiwa katika mkutano huo unaofanyika ukumbi wa Veta mjini Morogoro.
Baadhi ya wawasilishaji wa mada katika mkutano wa mwaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Wahariri,Wanahabari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari .

Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wakifanya utamburisho .
Mhariri Mtendaji wa Kaampuni ya New Habari (2006) Ltd ,Absalom Kibanda akitoa neno la shukrani mara baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano huo kufanywa na Waziri wa Maliasili na Utalii ,Prof Jumanne Maghembe.
Washiriki wa mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Malialisili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe pamoja na viongozi wengine wa serikali na TANAPA.N a Dixon Busagaga wa Michuzi Blog .

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, (WCF), WAPONGEZWA NA SSRA KWA KUWAFIKIA WADAU MUHIMU

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku tano kwa madaktari wanaotoka mikoa ya kanda ya ziwa kuhusu ajali na magonjwa yanayotokana na kazi Jijini Mwanza. Bi. Isaka alisisitiza umuhimu wa WCF na madaktari kufanya kazi pamoja ili waweze kulipa fidia stahiki kwa wafanyakazi wote kutoka sekta Binafsi na Umma. Wengine pichani kutoka kushoto ni Afisa Utumishi Mkuu, Mkoa wa Mwanza, Bw. Salvatory KyaKyarwenda, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko huo, Bw. Emmanuel Humba.
Mwenyeketi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Emmanuel Humba akitoa hotuba yake.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akizungumza mwanzoni mwa mafunzo hayo.
Baadhi ya Madaktari, wakufunzi kutoka ILO wakifuatilia maelezo ya utangulizi
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo
Mkurugenzi Mkuu, Bw. Masha Mshomba, akifafanua baadhi ya mambo kwa waandishi wa habari
Picha ya pamoja
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Irene Isaka (kulia), akisalimiana na mtaalamu wa ajali na magonjwa yanayosababishwa na kazi kutoka Shirika la Kazi Duniani, (ILO), Dkt. Jacque Palletier.

NA K-VIS MEDIA, MWANZA

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi Irene Isaka ameipongeza Bodi ya Wadhamini na Mkuurgenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa kuweza kuwafikia wadau wake muhimu kwanza kabla ya kuanza kutoa Fidia kwa Wafanyakazi. 

Bi Isaka aliyasema hayo leo Juni 6, 2016 wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa madaktari 124 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa kwenye ukumbi wa jengo la PPF Plaza jijini Mwanza.Aidha, amesema kuwa sasa hivi wafanyakazi wasifanye kazi kwa wasiwasi kwani kuna chombo maalumu ambacho ndiyo kinga na msaada wao endapo watapatwa na majanga katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Pia Bi. Isaka ametoa wito kwa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), na madaktari kote nchini kufanya kazi pamoja ili waweze kulipa fidia stahiki kwa wafanyakazi wote kutoka sekta Binafsi na Umma.

Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, ni taasisi ya Serikali iliyoko Ofisi ya Waziri Mkuu, na ulianzishwa kwa sheria ya Fidia Kwa Wafanyakazi namba 20 ya mwaka 2008. Lengo la kuanzishwa kwake ni kuhakikisha Mfanyakazi anapata fidia stahiki kutokana na kuumia kazini au magonjwa yatokanayo na kazi na kwa wanafamilia kupokea fidia kwa niaba ya mwenza wao aliyefariki akiwa kazini.

Mafao yatolewayo na Mfuko huo ambayo kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba ni pamoja na Fao la matibabu, fidia ya ulemavu wa muda, fidia ya ulemavu wa kudumu, Fidia ya huduma ya marekebisho (Rehabilitation services), Fedha za uangalizi wa mara zote, (Constant attendance care grant), Fedha za mazishi, na fidia kwa wategemezi wa mfanyakazi aliyefariki akiwa kazini au kutokana na maradhi yaliyosababishwa na kazi aliyokuwa akifanya. “Mfuko utaanza kutoa mafao ya kwanza kabisa tangu uanzishwe kuanzia mwaka wa fedha unaoanza Julai, 2016/2017.” Alisema Mkurugenzi Mkuu, Bw. Masha Mshomba.Mafunzo hayo yanatolewa kwa ushirikiano wa WCF na Shirika la Kazi Duniani, ILO. 

MSANII DIAMOND ATOA MSAADA WA MADAWATI 600 KWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MHE. MAKONDA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akimpongeza Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' mara baada ya kumtembelea ofisini kwake na kutoa mchango wake wa madawati yapatayo 600 kwa ajili ya kuchangia maendelea ya mkoa. Akiongea katika makabidhiano hayo msanii huyo alisema ni jambo jema kwao kuweza kujitolea mchango huo ili kuweza kumuunga mkono Mhe. Makonda katika kukabilana na changamoto za elimu.
Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' akiongea mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati yapatayo 600 kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ili kuweza kupunguza tatizo la wanafunzi kukaa chini. Makabidhiano hayo yalifanyika leo Juni 6, 2016 ofisini kwa mkuu wa mkoa jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akitoa shukrani zake za pekee kwa Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' kwa kuweza kutoa madawati 600 ikiwa ni mchango wake katika elimu ya kuweza kufanya wanafunzi kukaa sehemu salama. Mhe. Makonda alisema kuwa wakati umefika kwa wasanii wakaweza kujitoa katika jamii ambayo imekuwa ikiwapa wao sapoti na msanii Diamond amekuwa wa kwanza kuonyesha moyo wa pekee kwa kurudisha fadhila.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa WCB mara baada ya kumtembelea ofisini kwake.

TANI 70,000 ZA SUKARI ZAAGIZWA ILI KUMALIZA KERO YA UHABA WA SUKARI - WAZIRI MWGULU

$
0
0
Waziri wa Kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba katikati akizungumza na mpiga kura wake Gaile Elias ambae alipata kumgonga na Baiskeli mwaka 1999 wakati akiwa masomoni na jana wakati wa ziara yake alikutana nae ,kushoto ni katibu wake Bw Daud Ntukuna akishuhudia 

Na matukiodaimaBlog 
WAZIRI wa Kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba amewaomba radhi watanzania kwa usumbufu mkubwa walioupata baada ya kuadimika kwa sukari kwa siku miezi michache iliyopita na kuwa serikali inaendelea kutafuta ufumbuzi wa kudumu kwa kuagiza sukari tani 70,000 kutoka nje ya Tanzania.

Mwigulu ambae ni mbunge wa jimbo la Iramba aliyasema haya jana wakati wa ziara yake ya kuwashukuru wananchi wake kwa kumchagua kuendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana pasipo kufanya kampeni .

Akijibu kero za wananchi wa kijiji hicho cha Kilampanda alisema kuwa kero hiyo ya sukari si kwa kijiji hicho pekee kwani kuna baadhi ya maeneo wananchi walikuwa wakikosa kabisa sukari hata ile inayouzwa kwa bei kubwa japo kwa sasa hali ya upatikanaji wa sukari imeanza kurejea katika hali ya kawaida baada ya serikali kuagiza sukari kutoka nje .

Alisema kuwa kuwa tani zaidi ya 20,000 zimeingia nchini wiki moja iliyopita na hivi sasa tani 15,000 zipo njiani kuingia nchini hivyo bei ya sukari itashuka zaidi ya bei ya sasa baada ya sukari kuingia kwa wingi.

“ Mimi niwahakikishie muda si mrefu hali ya Sukari itarejea katika bei ya kawaida japo wapo baadhi ya watu wananunua akiba ya sukari kwa wingi kwa bei ya sasa ila nawaondoa hofu kuwa sukari itapatikana kwa wingi mbeleni kwani uzalishaji utaanza hivi punde”

Alisema kuwa imekuwa ni kawaida bei kupanda juu zaidi pindi bidhaa zinapoadimika japo ushukaji wake huwa wa kusuasua na katika kukabiliana na uhaba wa sukari na mfumko wa bei serikali imelazimika kuagiza sukari kwa wingi na itaendelea kufanya hivyo ili kuwa na sukari ya ziada ili kutopata adha tena ya sukari.

Hata hivyo alisema kwa kuwa sukari hiyo tano 20,000 zimekwisha ingia na tani 15,000 zipo njiani kuingia suara ya usambazaji linaendelea kufanyika ili kuwafikia wananchi kote nchini ,sukari itakayouzwa kwa bei ilekezi ya serikali.

Awali wananchi wa kijiji hicho cha Kilampanda walimlalamikia waziri huyo kupanda kwa bei ya sukari hadi kufikia kiasi cha Tsh 3000 kwa kilo na kabla ya serikali kutoa bei elekezi sukari kila mfanyabiashara alikuwa akiuza kwa bei yake wengine wakiuza hadi Tsh 4000 kwa kilo jambo ambalo lilikuwa likiwatesa wananchi wenye kipato cha chini.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images