Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA BENKI KUU YA TANZANIA (1966 – 2016) KUFANYIKA JUNI 22, 2016

0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 50 tangu Benki Kuu ya Tanzania ilipoanzishwa.


Sherehe hizi zitafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam tarehe 22/06/2016 ambapo mgeni rasmi atazindua vitabu viwili na kufuatiwa na kongamano litakaloshirikisha wataalam mbalimbali wa uchumi wakiwemo magavana 20 wa benki kuu kutoka nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.


Mada kuu katika Kongamano hilo itakuwa: “Beyond Aid and Concessional Borrowing: New Ways of Financing Development in Africa and its Implications”, (yaani namna ya kupata fedha za miradi ya maendeleo zaidi ya misaada na mikopo nafuu na athari zake) itakayowasilishwa na Prof. Justin Lin wa Chuo Kikuu cha Peiking, China. Mada hii imechaguliwa kwa kuzingatia changamoto ambazo serikali za Afrika zinakumbana nazo katika kugharamia miradi ya maendeleo wakati ambapo misaada na mikopo nafuu imekuwa ikipungua kwa kiasi kikubwa.


Wachumi waliobobea wa ndani na nje ya nchi, wakiwemo magavana 20 kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC) na wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) watashiriki katika kongamano hilo.


Vitabu vitakavyozinduliwa siku hiyo ni (i) “Tanzania: The Path to Prosperity” kinachoelezea masuala yanayohusu sera za uchumi nchini Tanzania ambacho kimeandikwa na wachumi waliobobea wa ndani na nje ya nchi, na kimechapishwa na Oxford University Press. (ii) Kitabu cha pili ni cha miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania kiitwacho “50th Anniversary of the Bank of Tanzania: Evolution of the Bank of Tanzania’s Role and Functions”, ambacho kinaelezea historia, majukumu, mafanikio na changamoto za Benki Kuu katika kipindi cha miaka 50 na matarajio ya Taasisi hii ya Umma katika maendeleo ya taifa katika kipindi cha miaka 50 ijayo.


Aidha, Tarehe 11/6/16 Mheshimiwa Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa atakuwa Mgeni Rasmi kwenye matembezi ya hisani ya wafanyakazi wa Benki Kuu kutoka makao makuu ya Benki hadi viwanja vya Mnazi Mmoja kuchangia ununuzi wa madawati ya shule za msingi kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki. Wafanyakazi wa Benki Kuu walioko matawini Mtwara, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya, Zanzibar na Chuo cha Benki Mwanza nao pia watafanya matembezi ya hisani kwenye mikoa yao.


Pamoja na matembezi kutakuwa na maonesho yaliyoandaliwa na Benki Kuu katika viwanja vya Mnazi Mmoja yenye lengo la kuwapa wananchi historia ya taasisi hii, ilikotoka, ilipo na inakoelekea katika kutekeleza majukumu yake.


Benki Kuu ingependa kuwakaribisha wananchi kufika kwa wingi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja siku hiyo ya tarehe 11/6/16 kujifunza mengi kuhusu taasisi hii ya umma.


Aidha, tunawaomba wananchi kufuatilia vipindi mbalimbali vya redio na makala kwenye magazeti ambapo mengi kuhusu historia, changamoto, mafanikio na matarajio ya Benki yataelezwa na viongozi mbalimbali wa Benki wa sasa na waliopita.


Benki Kuu ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 1965 na kuanza kutoa huduma rasmi tarehe 14 mwezi Juni mwaka 1966. Katika kipindi cha uhai wake, Benki Kuu ya Tanzania imetimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kulingana na mahitaji ya taifa yalivyojitokeza mwaka hadi mwaka.


Imetolewa na:


Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki

03/06/2016




MAMA JANETH MAGUFULI AWATAKA WATANZANIA KUWAJALI WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI

0
0
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoa wa Lindi Bw. Hemed Said mafuta ya kuzuia mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi leo Ikulu ndogo ya Mkoa wa Lindi.Katikati ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akikabidhi zawadi ya mbuzi na kuku kwa Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoa wa Lindi Bw. Hemed Said walipomtembelea leo asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta ya ngozi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akikabidhi zawadi ya kuku kwa Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoa wa Lindi Bw. Hemed Said walipomtembelea leo asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta ya ngozi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi wakiwa katika picha ya Pamoja na jamii ya watu wenye ulemavu leo asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Chama cha watu wenye Ulemavu wa Ngozi Mkoa wa Lindi walipomtembelea leo asubuhi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta ya kujikinga na mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa wakifurahia jambo na mtoto mwenye ulemavu wa ngozi walipomtembelea leo asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta ya kujikinga na mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi..
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi walipomtembelea leo asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta ya kuzia mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ambapo aliiasa jamii kujali kundi hili na kuacha imani potofu dhidi yao. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi walipomtembelea leo asubuhi Ikulu ndogo Mkoani Lindi kwa ajili ya kupokea msaada wa mafuta ya kuzia mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ambapo aliiasa jamii kujali kundi hili na kuacha imani potofu dhidi yao. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

KIPINDI CHA UNYAYO WANGU: DAVID MANOTI AZUNGUMZIA ADHABU YA WABUNGE WA UPINZANI BUNGENI

0
0
Unyayo wangu ni kipindi kipya kabisa kinachokujia kupita Tone Tv, ambacho kinaletwa kwenu na Mtangazaji wetu Eddie Nyota , kinacholenga shabaha ya watu waliothubutu kufanya jambo fulani katika jamii na wanauelewa na jamii husika. Utajifunza mengina kuburudika pia kupitia kipindi hiki Kinacholenga rika zote.
 

KUAHIRISHWA KWA USAILI WA NAFASI ZA KAZI KWA TANGAZO LILILOTOLEWA TAREHE 1 JUNI, 2016

0
0



KatibuwaSekretarietiya AjirakatikaUtumishiwaUmmakwa niabaya Tanzania Metrological Agency (TMA), Tanzania Meat Board (TMB), The Local Government Training Institute (LGTI) na Registration, Insolvency And Trusteeship Agency (RITA) alitoa tangazo katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira la kuita kwenye usaili tarehe 1 Juni, 2016 waombaji wa kazi waliowasilisha maombi na kukidhi vigezo kwa taasisi zilizoanishwa hapo juu.


Kupitia tangazo hili Waombaji kazi wote waliotangaziwa kuitwa kwenye usaili kwa tangazo hilo wanafahamishwa kuwa usaili huo umeahirishwa mpaka watakapotangaziwa tena hapo baadaye.  


Kwa Matangazo ya nafasi za kazi yaliyotolewa mnamo tarehe 6 Mei, 2016, 11 Mei, 2016, 18 Mei, 2016 na tarehe 26 Mei, 2016 nayo waombaji kazi watakaokidhi vigezo watataarifiwa hapo baadae kuhusu mchakato wake unavyoendelea.


Aidha, Kupitia tangazo hili, Sekretarieti ya Ajira kwa niaba ya Serikali inaomba radhi waombaji kazi wote waliowasilisha maombi na wale waliokuwa wamejiandaa kuhudhuria usaili huo kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


Imetolewa na



X.M. DAUDI

KATIBU

Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma.




KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAENDESHA DROO YA PILI YA MILLIONI 100 NA TUSKER FANYA KWELI NA UWINI

0
0
Meneja Masoko wa bia ya Tusker Nandi Mwiyombela (kushoto) akiokota vocha ya ushindi katika droo ya pili ya promosheni ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini iliyofanyika jijini Dar es Salaam, kushoto kwake ni afisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya kubahatisha nchini Humud Semvua akitazama kwa makini mchakato mzima, anayefuata ni muongozaji wa shoo hiyo Abdallah Mwaipaya ambaye pia ni mtangazaji wa ITV
Meneja Masoko wa bia ya Tusker Nandi Mwiyombela (kulia) akimkabidhi vocha ya mshindi afisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya kubahatisha nchini Humud Semvua ili kuhakiki taarifa za mshindi wakati wa droo ya pili ya promosheni ya Millioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa bia ya Tusker Nandi Mwiyombela (kulia) akiongea kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya pili ya promosheni ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini wakati wa droo hiyo, pembeni yake ni afisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya kubahatisha nchini Humud Semvua akifurahia jambo alilosikia kutoka kwa mmoja ya washindi kupitia njia ya simu.

Kundi la pili la washindi wa mamilioni ya Tusker watangazwa.

Wiki iliyopita ilishuhudiwa washindi kumi kutoka mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam na Kilimanjaro wakiondoka na Million moja kila mmoja kupitia promosheni inayoendelea ya Millioni 100 na Tusker Fanya Kweli na Uwiniinayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti. 

Katika droo ya pili iliyochezeshwa leo, washindi wengine kumi walitangazwa. Katika droo hiyo iliyofanyika ITV na kushuhudiwa na maofisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya Kubahatisha walitangazwa washindi kumi ambao ni Rose Mkwizu, Sijali Ally, Anna Lazaro kutoka Dar es Salaam, Elizabert Wiliam kutoka Mlandizi –Pwani, Josephat Lukindo,George Mlay kutoka Kilimanjaro,Geofrey Manangwa kutoka Tanga, Wanzagi na Lucas Fransis kutoka Mwanza na Umoja Nyakwa kutoka Morogoro. 

Mbali na washindi hao ambao walijipatia zawadi ya pesa taslim, pia kuna washindi kibao waliojishindia bia za bure tangu promosheni ilipoanza. Bado kuna wiki nane ambapo zimebaki Millioni 80 kushindaniwa kwa kipindi hicho kilichobaki cha promosheni hiyo.

Naye mmoja wa washindi Elizabert Wiliam alisema kuwa Shoo ya kwanza iliyorushwa kupitia runinga ya ITV ndiyo iliyomsukuma kushiriki promosheni hiyo. “Nilitazama droo ya kwanza wiki iliyopita na siku zote mimi ni mtumiaji mzuri wa bia ya Tusker, baada ya muda punde tu nilienda kunywa huku nikiwa na shauku ya kushinda tu na kuingia kwenye droo” alisema bi Elizabeth. Aliendelea kwa kuipongeza Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuendesha promosheni kama hiyo inayogusa maisha ya wateja wao kwa kubadili sehemu au maisha yote kwa ujumla. Aliongeza kuwa pesa aliyoipata ataitumia katika kukuza biashara zake.

Naye Meneja Masoko wa Bia ya Tusker Nandi Mwiyombela alieleza kuwa, promosheni ya ‘Tusker Fanya Kweli Uwini’ inaendelea vyema kabisa na washindi wanaendelea kushinda kutoka kila pande za Tannzania ambako sasa mikoa ya kanda ya ziwa imeungana nasi katika promosheni hii wiki iliyopita. Tuna washindi kutoka nchi nzima, Mwanza, Morogoro, Arusha, Moshi na Dar es Salaam. 

Tunapenda kuwathibitishia wateja wetu kuwa promosheni hii si ya watumiaji wa bia ya Tusker waliopo Dar es Salaam tu bali kwa ushahidi huu wa washindi kutoka mikoa mingine unatosha kuthibitisha kuwa ni ya nchi nzima.

Washindi wetu wa wiki iliyopita watapokea zawadi zao za fedha taslim Million 1 katika hafla fupi ya makabidhiano itakayofanyika leo jijini Dar es Salaam na Moshi.

MILIONI 250 ZATUMIKA KUHUDUMIA KAMBI 4 ZA WAZEE NA WALEMAVU NCHINI.

0
0

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI DK. JULIANA PALLANGYO AFANYA ZIARA KATIKA KAMPUNI YA PUMA ENERGY

0
0
 Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo  ya Petroli Nchini  James Andelile,(kulia) akielezea  jambo katika kikao hicho. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati  Dk. Juliana Pallangyo

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati,  Dk. Juliana Pallangyo (kushoto) akiwa ameambatana na  Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali  wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA),Michael Mjinja (kulia) mara alipowasili katika ofisi za Puma  Energy jijini  Dar es Salaam kwa ajili ya kukagua shughuli zake.

 Meneja  Afya, Usalama na Mazingira  kutoka katika kampuni ya  Puma  Energy Blasio Menchi (kulia) akielezea shughuli za kampuni hiyo mbele ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati,  Dk. Juliana Pallangyo pamoja na ujumbe wake.

 Kutoka kushoto Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati  Dk. Juliana Pallangyo, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo  ya Petroli Nchini  James Andelile, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali  wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA),Michael Mjinja,na  Kaimu Kamishna wa Petroli ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya   Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Mwanamani Kidaya wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Meneja  Afya, Usalama na Mazingira  kutoka katika kampuni ya  Puma  Energy Blasio Menchi (hayupo pichani) kwenye ofisi za Puma Energy jijini Dar es Salaam.

 Meneja Uendeshaji  kutoka   Kampuni ya  Puma  Energy Lameck Hiliyai (katikati)  akielekeza  jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati  Dk. Juliana Pallangyo (kushoto) Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo  ya Petroli Nchini  James Andelile (aliyekaa katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali  wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA),Michael Mjinja (kulia) katika kikao hicho kwenye ofisi za Puma Energy jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati  Dk. Juliana Pallangyo (kushoto) na Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo  ya Petroli Nchini  James Andelile (kulia) wakibadilishana mawazo katika  kikao hicho.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dk. Juliana Pallangyo akitoa maelekezo kwa kampuni ya Puma Energy katika kikao hicho


RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI JIJINI DAR LEO

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Gerson John Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Gerson John Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gerson John Mdemu wa pili kutoka kushoto. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga mara baada ya tukio la uapisho kukamilika.


WAZIRI MAKAMBA ASHIRIKI KUPANDA MITI YA MIKOKO NA WAKAZI WA KATA YA MBWENI JIJINI DAR LEO

0
0
    Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akipanda mti aina ya mkoko katika fukwe za bahari ya hindi katika eneo la Mbweni jijini Dar es Salaam. Upandaji huo wa mikoko ni katika kuadhimisha wiki ya mazingira duniani, ambayo kilele chake ni kesho
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba  akishirikiana kupanda miti ya mikoko na wakazi wa kata ya  Mbweni jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha siku ya mazingira hapo tarehe 5 juni.
 . Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akifurahia jambo na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbweni ambao walijumuika pamoja naye kupanda mikoko katika fukwe za Mbweni jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza kupanda mikoko katika fukwe za bahari ya Hindi katika kata ya Mbweni.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akitia saini kitabu cha Wageni alipotembelea Kata ya Mbweni iliyopo Manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya shughuli za upandaji mikoko katika eneo hilo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba Ametoa wito kwa Wananchi  wa Kata ya Mbweni kutunza mazingira na kutoa kipaumbele kwa mazingira. Aliyasema hayo wakati wa zoez la upandaji mikoko lilifanyika katika fukwe za bahari ya Hindi zilizoko Mbweni.

Akiongoza Wananchi wa Kata hiyo kupanda miche 5,000 ya mikoko , Waziri Mkamba alisititiza pia Wanafunzi wa shule waliopo katika eneo hilo kupenda mazingira yao na kuyatunza ili yawafae baadaye.

Wakisoma Risala yao , Wanawake wa Mbweni walimuomba Waziri awasaidie kuwapatia vitendea kazi  kwa ajili ya kuhudumia mikoko pamoja na kumuomba awasaide kuwatatulia changamoto wanazokutana nazo. Ikiwamo ya maafisa wa TRA kukata hovyo mikoko wanapokua wanafanya doria katika fukwe zaMbweni.

Mwisho Waziri aliwahukuru Wananchi wa Mbweni waliojitypkeza kujumuika naye katika zoezi hilo la upandaji mikoko. Shuhuli za upandaji mikoko ni kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira ambayo kilele chake ni tarehe 5 juni kila mwaka. 

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KIONGOZI WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA LUO ZHIJUN IKULU JIJINI DAR

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Kiongozi  wa Chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun  kutoka jimbo la Jiangsu nchini China, ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini lu youqing aliyeambatana na Kiongozi huyo wa chama cha Kikomunisti cha China, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Kiongozi  wa Chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun  kutoka jimbo la Jiangsu nchini China.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kiongozi  wa Chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun  kutoka jimbo la Jiangsu nchini China mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa kiongozi huyo wa chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun  pamoja na Balozi wa China hapa nchini lu youqing mara baada ya kumaliza Mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi pamoja na Mkuu wa mkoa wa dar es Salaam Paul Makonda. PICHA NA IKULU

MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI AZINDUA MAONYESHO YA MRADI WA MJI MPYA WA ZANZIBAR

0
0
Katibu Mtendaji Kamisheni ya Ardhi Zanzibar Ahmed Abdulrahman Rashid akitoa maelezo juu ya Mpango Mkuu wa matumizi ya Ardhi wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Mradi wa Mji mpya wa Zanzibar uliofanyika Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge Mjini Zanzibar.
Mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Tanzania Eugen Gies akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho ya Mradi wa Ngambo tuitakayo katika viwanja vya Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi Mjini Zanzibar.
Mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Tanzania Eugen Gies akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho ya Mradi wa Ngambo tuitakayo katika viwanja vya Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud akitoa maelezo namna Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilivyojiandaa katika kuwapatia wananchi nyumba bora za kuishi wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Ngambo Tuitakayo.
Mkurugenzi wa mipango Miji na Vijiji Dkt. Mouhammed Juma akimunyesha Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud namna ya Mji mpya utakavyokuwa mara baada ya kukamilika kwake katika sherehe za uzinduzi zilizofanyika viwanja vya Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi Mjini Zanzibar.
Watoto wakiangalia na kufurahia mji mpya wa Zanzibar utakavyokuwa kupitia Mradi wa Ngambo tuitakayo wakati wa uzinduzi wa maonyesho katika viwanja vya Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi. Picha na Makame Mshenga /Maelezo Zanzibar.

Mama Janeth Magufuli atoa Msaada kwa jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi Mkoani Lindi

0
0

WABUNGE WAPATA SEMINA KUHUSU MALENGO MAPYA 17 YA DUNIA

0
0

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Rodriguez  Alvaro (kulia) akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kulia) mara baada ya kufika Ofisini kwake Bungeni Dodoma leo.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizungumza na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania , Rodriguez  Alvaro (kulia) mara baada ya mwakilishi huyo kufika Ofisini kwake Bungeni Dodoma leo.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Rodriguez  Alvaro (kulia) akimwonesha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kulia) sehemu ya taarifa ya mwaka ya utekelezaji wa programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa nchini mara baada ya kufika Ofisini kwake Bungeni Dodoma leo.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Rodriguez  Alvaro (kulia) akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kulia) taarifa ya mwaka ya utekelezaji wa programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa nchini mara baada ya kufika Ofisini kwake Bungeni Dodoma leo.
Wabunge Mhe. Margaret Sitta (Kushoto) na Mhe. Najma Murtaza Giga, Mwenyekiti wa Bunge wakiwa katika picha ya pamoja kwenye rangi za Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu 17 ya dunia wakati wa Semina ya wabunge kuhusu mchango wao katika utekelezaji wa malengo hayo nchini iliyofanyika Bungeni, Dodoma.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania , Rodriguez  Alvaro (kulia) kwenye rangi za Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu 17 ya dunia wakati wa Semina ya wabunge kuhusu mchango wao katika utekelezaji wa malengo hayo Bungeni Dodoma leo.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa ameshika mabango mawili yenye malengo mapya 2 ya Maendeleo Endelevu kati ya 17 ya Umoja wa Mataifa yanayotakiwa kutekelezwa duniani kote kuanzia mwaka huu hadi 2030.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania , Rodriguez  Alvaro (kulia) wakiwa na mabango yenye Malengo Mapya 2 kati ya 17 ya dunia wakati wa Semina ya wabunge kuhusu mchango wao katika utekelezaji wa malengo hayo Bungeni Dodoma leo.
Mbunge wa Urambo Mhe. Margaret Sitta (Kushoto) na Mhe. Najma Murtaza Giga, Mwenyekiti wa Bunge wakiwa katika picha ya pamoja kwenye rangi za Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu 17 ya dunia wakati wa Semina ya wabunge kuhusu mchango wao katika utekelezaji wa malengo hayo nchini iliyofanyika Bungeni, Dodoma.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Rodriguez  Alvaro akizungumza na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Semina Kuhusu Malengo ya dunia iliyoandaliwa na Umoja huo mjini Dodoma leo.

 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Wabunge wakati wa ufungunzi wa Semina kwa wabunge kuhusu Malengo ya dunia iliyoandaliwa na Umoja huo mjini Dodoma leo.

Mabango yenye Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu 17 ya dunia.

Mtaalam wa Masuala ya Uchumi kutoka Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP), Rodgers Dhliwayo akiwasilisha mada kuhusu namna ya kuyafikia Malengo Mapya 17 ya dunia wakati wa Semina ya Wabunge kuhusu malengo hayo mjini Dodoma.

Mtaalam wa Masuala ya Uchumi kutoka Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP), Rodgers Dhliwayo akiwasilisha mada kuhusu namna ya kuyafikia Malengo Mapya 17 ya dunia wakati wa Semina ya Wabunge kuhusu malengo hayo mjini Dodoma.PICHA/Aron Msigwa-MAELEZO.

Na Fatma Salum-MAELEZO, Dodoma.



Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametakiwa  kusimamia vyema utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo kwa kuhakikisha kuwa Serikali inatekeleza mipango iliyojiwekea kwa wakati ili kuimarisha ustawi wa wananchi wanaowawakilisha na taifa kwa ujumla.


Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Dodoma na Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson  wakati akifungua semina fupi ya Wabunge kuhusu Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Dunia iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa kufanya kazi pamoja  (Delivery as One).

Dkt. Tulia amesema kuwa Wabunge wana  jukumu la kuzingatia malengo hayo na kuhakikisha yanatekelezwa kwa kuwa mipango yote na mikakati ya maendeleo hupitia Bungeni hivyo hawana budi kusimamia malengo hayo ipasavyo kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu.
Akizungumza wakati wa semina hiyo Mwakilishi Mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli  inafanya kazi nzuri katika utekelezaji wa Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Dunia na kuwataka Wabunge kuwa mabalozi wazuri katika utekelezaji wa malengo hayo.
Bw. Rodriguez ameongeza kuwa ni muhimu sana kwa Wabunge kuweza kuyaelewa malengo hayo ya Dunia ili waweze kufanikisha utekelezaji na ufuatiliaji wake katika ngazi zote za Taifa.
Mwaka 2015 nchi 193 ikiwemo Tanzania zilikubaliana kwa pamoja kutekeleza mkakati wa kumaliza umaskini, kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na kupigania haki na usawa. Katika kufanikisha hilo nchi hizo zilikubaliana kupitisha Malengo Endelevu 17 ambayo ni Kutokomeza Umaskini, Kukomesha Njaa, Afya Njema na Ustawi, Elimu Bora, Usawa wa Jinsia, Maji Salama na Usafi, Nishati Mbadala kwa Gharama Nafuu, Kazi zenye Staha na Ukuzaji Uchumi, Viwanda, Ubunifu na Miundombinu, Kupunguza Tofauti.
Malengo mengine yaliyoafikiwa na nchi hizo ni Matumizi na Uzalishaji wenye Uwajibikaji, Miji na Jamii Endelevu, Kuchukua Hatua dhidi ya Mabadiliko ya Tabia Nchi, Kuendeleza Uhai katika Maji, Kulinda Uhai katika Ardhi, Amani, Haki na Taasisi Madhubuti na Ushirikiano ili Kufanikisha Malengo.
Naye Naibu Katibu Mtendaji Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Maduka Paul Kessy amesema kuwa Tanzania imejipanga kutekeleza malengo hayo kwa ufanisi ili kufikia azma ya kuiondoa nchi yetu miongoni mwa nchi maskini na kuiwezesha kuwa nchi ya uchumi wa kati na maendeleo ya viwanda.
“Utekelezaji wa malengo haya utakwenda sanjari na utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao msingi wake ni kuchochea mabadiliko ya uchumi na maendeleo ya watu.” Alisema Kessy.
 


DK. SHEIN AZIPAMBA TIMU ZA UMISSETA

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Omar King kwa niaba ya Rais wa Zanzibar akimkabidhi vifaa vya michezo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Elimu Khadija Bakari Juma kwa ajili ya wanafunzi watakaoshiriki mashindano ya UMISETA kuanzia tarehe 13 mwezi huu Mkoani Mwanza. Picha na Makame Mshenga /Maelezo Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Omar Hassan (King) akizungumza na wanamichezo watakaoshiriki mashindao ya UMISETA wa Kanda ya Unguja na Pemba katika Uwanja wa Amani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar wakati alipowakabidhi vifaa vya michezo timu zitakazoshiriki mashindano hayo Mjini Mwanza kuanzia tarehe 13 mwezi huu.
\
Na Kijakazi Abdalla-Maelezo

WANAMICHEZO wamekumbushwa kuzingatia nidhamu na uvumilivu wanapokuwa viwanjani.

Wito huo umetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu za skuli za Zanzibar zitakazoshiriki mashindano ya UMISSETA inayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza baadae mwezi huu.
Akiwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Omar Hassan ‘King’ katika uwanja wa Amaan leo, Dk. Shein amesema mambo hayo ndio msingi wa mafanikio kwa wanamichezo wakiwa kwenye mashindano au nje ya viwanja.

Aliwataka wanamichezo hao Mwanza, kushirikiana na kuunganisha nguvu wakiwa jijini Mwanza ili waweze kurudi na ushindi utakaoinua jina la Zanzibar katika medani ya michezo nchini Tanzania.

Hata hivyo, Mhe. Rais hakuacha kueleza jinsi anavyosikitishwa na kudorora kwa michezo humu visiwani, ambako alisema kunasababishwa na utitiri wa timu nyingi.“Jambo hili la kuwepo utitiri wa timu ndilo linalodumaza michezo hapa Zanzibar na kuifanya baadhi yao isipewe kipaumbele,” alisema.Lakini amewasisitiza wanamichezo hao kuelewa kwamba wana wajibu wa kushindana kadiri ya uwezo wao kwani serikali inajitahidi kuwanjengea mazingira mazuri kwa kuwa inatarajia kupata ushindi hasa katika michezo inayopendwa na mashabiki wengi ikiwemo mpira wa miguu.

Mapema, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Khadija Bakari Juma, akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo, alitoa shukurani zake kwa Rais wa Zanzibar kutokana na msaada huo wa vifaa.Alieleza matumaini yake kwamba vifaa hivyo vitawapa hamasa zaidi washiriki wa mashindano hayo ili wapate ushindi na kuweza kutembea kifua mbele.

Vifaa vilivyotolewa ni vya mpira wa miguu, mpira wa wavu (volleyball) na mikono (handball), riadha pamoja na mpira wa meza (table tennis).Michuano ya UMISSETA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi jijini Mwanza Juni 13 na kufikia tamati Juni 25, mwaka huu.

Katika mashindano hayo, Zanzibar itawakiliishwa na timu mbili ambazo ni kanda ya Unguja na ile ya Pemba.

VISIMA VINGI DAR VIMECHIMBWA BILA KUFUATA UTARATIBU.

0
0
Na Fatma Salum- MAELEZO, Dodoma.

Serikali imesema kuwa visima vingi Jijini Dar es Salaam vimechimbwa bila ya kufuata kanuni na taratibu za uchimbaji hivyo maji yake si salama kwa matumizi ya binadamu.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge aliyasema hayo wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake Bungeni mjini Dodoma.

Mhe. Lwenge alibainisha kuwa katika kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu uliotokea mwezi Agosti 2015 Jijini Dar es Salaam na kuenea nchini, Serikali ilifanya uchunguzi wa sampuli za maji ya visima 108 vya jijini humo na matokeo ya uchunguzi huo yalionesha kuwa visima 66 maji yake si salama.

“Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na wadau wengine ilifanya ukaguzi na kupima uwepo wa vimelea vya vijidudu vya ugonjwa huo katika visima vya maji vinavyotumika jijini Dar es Salaam na sampuli za maji ya visima 108 zilichukuliwa, kati ya hivyo visima 20 vifupi na visima 46 virefu maji yake yaligundulika kuwa si salama. Kwa ujumla visima vingi vilivyopo kwenye maeneo ya watu vimechimbwa bila ya kufuata kanuni na taratibu.” Alisema Mhe. Lwenge.

Aidha, Waziri Lwenge alisema kuwa Serikali pia ilifanya ukaguzi wa ubora wa maji kwenye vyanzo vya maji katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Mara, Manyara, Kagera, Kigoma, Morogoro na Dodoma ambapo vyanzo vya maji vipatavyo 600 vilikaguliwa na kubaini kuwa maji yaliyo salama ni chini ya asilimia 40.

Mhe. Lwenge alieleza kuwa Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) imekamilisha uandaaji wa miongozo ya utekelezaji wa Mpango wa Usalama wa Maji (Water Safety Plan) kwa Vyombo vya Watumiaji wa Maji na Mamlaka za Maji.

“Miongozo hiyo inakusudia kuboresha huduma za upatikanaji wa maji safi na salama kwa Mamlaka za Maji na Vyombo vya Watumiaji wa Maji Vijijini (COWSOs) kuanzia kwenye chanzo cha maji hadi kwa mtumiaji.” Alifafanua Mhe. Lwenge.

Kutekelezwa kwa mpango huo kutaboresha usimamizi wa usalama wa maji katika vyombo hivyo na kuwaepusha wananchi kutumia maji yasiyo salama pamoja na kupunguza upotevu wa maji katika mifumo ya kusambaza maji kote nchini.

WIzara ya habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo yakabidhi Bendera ya Taifa kwa Mshindi wa Airtel Trace Music Stars

0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi (kulia), akikabidhi Bendera ya Taifa kwa Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Star 2016, Melisa John, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kuiwakilisha nchi katika fainali za mashindano ya Afrika zitakazofanyika Lagos nchini Nigeria Juni 11 mwaka huu. Wanaoshuhudi ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa pili kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Ngereza.


· Mshindi anaenda kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Afrika nchini Nigeria

Wizara ya habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imekabidhi bendera ya taifa kwa mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars ambaye ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Afrika inayotegemea kufanyika Lagos Nigeria

Melisa John mwenye umri wa miaka 22 anayetokea mkoa wa Dar es Saalam aliibuka mshindi katika fainali zilizoshirikisha washiriki tano bora walioingia kwenye kinyanganyiro hicho. Melisa ataondoka nchini tarehe 4 Juni 2016 kwaajili ya mandalizi ya awali na mazoezi ya muziki yatakayoshirikisha washiriki wengine 8 kutoka nchi za Afrika ambazo Airtel inayoendesha biashara zake kisha kushiriki kwenye fainali zitakazofanyika 11 Juni 2016

Akiongea wakati wa kukabidhi bendera, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi Leah Kihimbi alisema Sanaa ni Kazi ,ajira na ni bidhaa yenye thamani kubwa. Muziki kama tanzu mojawapo ya Sanaa ina nafasi kubwa katika kubadili maisha ya mtu na nchi kiuchumi endapo itatumika vizuri. ile dhana kuwa kazi ya Muziki ni kuburudisha imepitwa na wakati.Wanamuziki sasa tuingie kazini.

Ninawapongeza Airtel wamelielewa hili na kuamua kuunga mkono Serikali kwakuwa na mpango kabambe wa kuibua vipaji vya Vijana kupitia Sanaa ya Muziki uitwao Airtel Trace Music Stars wenye lengo la kuwawezesha Vijana,wanamuziki chipukizi kushiriki na kufikia ndoto zao, ikiwa pia ni utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Utamaduni inayosisitiza Mashirika na Taasisi kushiriki kikamilifu katika kukuza na kuendeleza Sanaa na Wasanii.

“napenda kumpongeza Melisa kwa ushindi huo na kumuhasa kuonyesha nidhamu na kuwa na mwelekeo wa kufikia lengo lake wake wote wa mashindano kwani mashindano haya yanatoa fursa pana zaidi ya ushindi hivyo hii ni nafasi ya pekee sana kwako kuitumia fursa hii ipasavyo na kuhakikisha unajenga mahusiano mazuri ya kudumu, kuongeza wigo mpana wa marafiki na mashabiki na pia kuonyesha uwezo/ talanta yako katika mziki” aliongeza Kihimbi

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “tunajivunia kuanzisha mpango huu kabambe ambao si tu unawawesha vijana kubadili maisha yao bali unawapa nafasi ya kufanya muziki na kuonyesha vipaji vyao nje ya mipaka ya nchi. Tunafurahi kuwawezesha vijana wanamuziki chipukizi kupata nafasi hadimu za kufanya kazi na magwiji wa muziki duniani kama Akon na Keri Hilston hivyo tunaomba watanzania watumie fursa hizi kupitia programu zetu za kijamii chini ya mpango wetu wa Airtel Fursa kujikwamua kimaisha wao pamoja na jamii inayowazunguka.”

Kwa upande wake Melisa John amewashukuru Airtel na Serikali kwa ushirikiano katika kukuza tasnia ya muziki na kuchochea ajira kwa vijana wengi, “nimejipanga vyema kukabiliana na changamoto iliyoko mbele yangu na ninawaahidi kuipeperusha vyema bendera ya nchi yangu. 

Napenda kuwaomba mashabiki zangu na watanzania kwa ujumla kunipigia kura kwa kutuma ujumbe mfupi wenye neno MEL kwenda namba 15594 kura yako ni muhimu na itachangia kunipa ushindi”

OLE SENDEKA ATIKISA KILWA MASOKO, MKOANI LINDI, MAMIAWAHUDHURIA MKUTANO WAKE WA HADHARA LEO

0
0
 Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akihutubia mkutano wa hadhara uliofayika leo jioni katika Viwanja vya Mkapa Garden, Kilwa Masoko mkoani Lindi. Sendeka amesema, Wapinzania wanadai kwamba Rais Dk. John Magufuli uongozi wake ni wa Kidikteta, wameamua kujaribu hoja hiyo kwa kuwa wameishiwa hoja na hata hivyo hoja yao hiyo haiwezi kuwa na mashiko kwa Watanzania ambao wanaamini Rais Dk. Magufuli anavyofanya sasa kupasua majipu na kupambana na vitendo vya ufiadi, kufuja rasilimali za nchi, uzembe na umangimeza ni sahihi. 
 Wananchi wakimshangilia Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka alipoingia kwenye mkutano wa hadhara uliofayika leo jioni katika Viwanja vya Mkapa Garden, Kilwa Masoko mkoani Lindi leo jioni
 Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akihutubia mkutano wa hadhara uliofayika leo jioni katika Viwanja vya Mkapa Garden, Kilwa Masoko mkoani Lindi. Sendeka amesema, Wapinzania wanadai kwamba Rais Dk. John Magufuli uongozi wake ni wa Kidikteta, wameamua kujaribu hoja hiyo kwa kuwa wameishiwa hoja na hata hivyo hoja yao hiyo haiwezi kuwa na mashiko kwa Watanzania ambao wanaamini Rais Dk. Magufuli anavyofanya sasa kupasua majipu na kupambana na vitendo vya ufiadi, kufuja rasilimali za nchi, uzembe na umangimeza ni sahihi.  
Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akiwaaga wananchi baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara uliofayika leo jioni katika Viwanja vya Mkapa Garden, Kilwa Masoko mkoani Lindi. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO


 Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akiingia kwenye mkutano wa hadhara uliofayika leo jioni katika Viwanja vya Mkapa Garden, Kilwa Masoko mkoani Lindi . Pamoja naye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa huo, Ali Mtopa
 Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akislimia Wazee Maarufu ambao ni Waasisi wa TANU na baadaye CCM, alipowasili kwenye mkutano wa hadhara uliofayika leo jioni katika Viwanja vya Mkapa Garden, Kilwa Masoko mkoani Lindi
 Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akwafurahia wananchi wlaliokuwa wakimshangilia alipoingia kwenye mkutano wa hadhara uliofayika leo jioni katika Viwanja vya Mkapa Garden, Kilwa Masoko mkoani Lindi
 Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa, wakiwafurahia wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara uliofayika leo jioni katika Viwanja vya Mkapa Garden, Kilwa Masoko mkoani Lindi, leo jioni
 Vijana wa bodaboda wakiingia kwa mbwembwe za aina yake kwenye mkutano huo
 Vijana waendesha bajaji wakiingia kwa mbwembwe za aina yake kunogesha mkutano huo
 Vijana Chipukizi wa CCM wacheza sarakasi wakiingia kwa gari lao kwa mbwembwe za aina yake kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye Vianja vya Mkapa Garden, wilayani Kilwa Masoko mkoani Lindi leo
 Kijana wa kikundi cha Sarakasi cha Umoja wa Vijana wa CCM akionyesha umahir wake, vijana hao walipocheza sarakasi kabla ya mkutano huo kuhutubiwa na Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka leo jioni katika Viwanja vya Mkapa Garden, Kilwa Masoko mkoani Lindi
 Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akiwafurahia vijana hao wakati wakicheza sarakasi kwenye mkutano wa hadhara uliofayika leo jioni katika Viwanja vya Mkapa Garden, Kilwa Masoko mkoani Lindi
 Vijana wa Brass Band ya Umoja wa Vijana wa CCM wakiingia kwenye mkutano huo
 Wananchi wakishangilia kwenye mkutano huo
 Menyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM wilaya ya Kilwa mkoani Lindi akihamasisha wananchi kwenye mkutano huo

 Kada wa CCM, Mohammed Albadawi ambaye amewahi kuwa kiongozi wa CUF katika ngazi mbalimbali na pia kuwania Ubunge katika jimbo la Mafia katika Uchaguzi Mkuu uliopita, akikichambua chama hicho alipohutubia kwenye mkutano huo leo.
 Vijana wakichangamsha mkutano huo
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa akimkaribisha Ole Sendeka kuhutibia mkutano huo
 Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Lindi Ali Mtopa akiserebuka kidogo jukwaani kabla ya kuwachia Uwanja Ole Sendeka

MABALOZI KENYA WAADHIMISHA SIKU YA AFRIKA

0
0
 Na sasa ni wakati wa kuserebuka! Balozi Haule (wa tatu kulia), Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Fastjet, Bw. Jimmy Kibati (wa pili kulia) na mshereheshaji, wanajimwaga uwanjani baada ya Balozi kukabidhi washindi wawili (kushoto) tiketi za kwenda Dar es Salaam na kurudi kwa ndege ya Fastjet.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa wa Kenya, Balozi Amina Mohamed (wa pili kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule, alipotembelea banda la Tanzania kwenye maonyesho ya kusherehekea Siku ya Afrika. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Monica Juma na kushoto ni mke wa Balozi Haule, Bibi Maria.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya, Balozi Monica Juma, akitizama bidhaa za kutoka Tanzania kwenye maonyesho hayo.
Wageni kwenye banda la Tanzania.

 Balozi wa Uganda nchini Kenya, Mhe. Angelina Wapakhabulo (kushoto) akionja mvinyo aina ya Presidential unaotengenezwa Dodoma alipotembelea  banda la Tanzania. Wa pili kushoto ni Balozi wa Tanzania, Mhe. Haule

Mabalozi wa nchi za Afrika waliopo Kenya, jana waliadhimisha sherehe za Siku ya Afrika (AU Day), ambazo ziliahirishwa mwezi uliopita kupisha Mkutano wa Kimataifa wa Mazingira kuhusu Afrika, uliofanyika Nairobi. Siku ya Afrika huadhimishwa Mei 25 kila mwaka.

Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa wa Kenya, Balozi Amina Mohamed, alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo zilizofanyika viwanja vya Ubalozi wa Malawi jijini Nairobi. Katika hotuba yake, Waziri huyo alisema nchi za Afrika simepiga hatua katika kujenga amani na utengamano chini ya Agenda 2063, inayolenga kuliinua bara hili kiuchumi.

Chini ya mpango huo, Afrika imekusudia kumaliza kabisa mizozo ya kivita na mifarakano mingine kati ya nchi wanachama ifikapo mwaka 2020. Malengo mengine makubwa ni kupunguza utegemezi nje wa bajeti ya mipango ya maendeleo ya Afrika, na kuondoa vikwazo vya miingiliano ya watu, bidhaa na huduma baina ya nchi za bara hilo.

Waziri Mohamed alisema Wakuu wa Nchi na Serikali pamoja na mawaziri wa Mambo ya Nje watapatiwa pasi za kusafiria za Afrika mwezi Oktoba mwaka huu chini wa mpango wa kuondoa vikwazo vya usafiri barani Afrika. Sherehe hizo ziliandaliwa na Mabalozi wa Kundi la Afrika (African Diplomatic Community) nchini Kenya, akiwemo Balozi wa Tanzania, Mhe. John Haule.

MLIMBWENDE WA TAJI LA MISS ILEMELA 2016 APATIKANA.

0
0

Mlimbwende Maria Frances (katikati) ametwaa taji la MISS ILEMELA 2016. Shindano la kumsaka mlimbwende huyo lilifanyika usiku wa jana June 04,2016 katika viunga vya Rock City Mall Jijini Mwanza.Katika shindano hilo, nafasi ya pili imenyakuliwa na Mwanaisha Hija (kulia) huku nafasi ya tatu ikinyakuliwa na Happness Contantine (kushoto).

Washiriki wa Miss Ilemela waliobahatika kuingia nafasi tano bora. Kulikuwa na washiriki 22
Washiriki wa Miss Ilemela 2016 wakipita jukwaani kwa madaha kabisa
Msanii Nay Wa Mitego akitoa burudani katika shindano la Miss Ilemela 2016.


YA LEO LEO

0
0

Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images