Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 865 | 866 | (Page 867) | 868 | 869 | .... | 1898 | newer

  0 0


  0 0

  Na Takdir Ali-Maelezo Zanzibar .
            
  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema haitamvumilia mfanyabiashara yeyote atakayebainika kuuza bidhaa zilizopitwa na wakati.

  Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi  Amina Salum Ali, amesema kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi juu ya tabia ya baadhi ya afanyabiashara kuwauzia vitu vilivyopitwa na wakati.

  Amefahamisha kuwa, udanganyifu huo unaofanywa na wafanyabiashara huwasababishia wananchi kupata maradhi mbalimbali ikiwemo saratani.Akiwa katika ziara ya kukagua maghala mbalimbali ya chakula kisiwani Unguja kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani, Balozi Amina amesema serikali imechoka kuona wananchi wanauziwa vyakula visivyokuwa na kiwango kutokana na kumalizika muda wao wa matumizi.

  Waziri huyo amekemea vitendo vya baadhi ya wafanyabiashara kuuza vyakula vilivyokaa maghalani kwa muda mrefu hata kupindukia  miaka mitano, hali aliyosema ni kuwaathiri na  kuwadhulumu wananchi.“Wazanzibari tumechoka kulishwa michele mibovu. Tunasema sasa imetosha na hatutawafumbia macho wafanyabiashara watakaoendeleza vitendo hivyo,” alisema Waziri Amina.

  Amesema serikali inakusudia kuweka bei elekezi kwa wafanyabiashara wote ili kuzuia  upandaji bei kiholela hali inayowapa usumbufu wananchi hasa wa kipato cha chini.Aidha Balozi Amina amesema kila mwaka ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani, serikali  imekuwa ikipunguza kodi za bidhaa muhimu kwa wafanyabiashara ili kutoa punguzo kwa wananchi.

  Amezitaja bidhaa hizo kuwa ni unga wa ngano, sukari na mchele.
  Hata hivyo, ameeleza kusikitishwa kwake kwamba bei za bidhaa hizo zimebakia palepale au kuongezeka zaidi licha ya nia nzuri ya serikali.Ili kuandaa mazingira ya kuwapa unafuu wananchi, amesema serikali inakusudia kukaa na wafanyabiashara wote ili kujadili na kupanga mipango mizuri kwa itakayowaletea maendeleo wafanyabiashara hao na taifa kwa jumla.

  Kwa upande wao, wafanyabiashara waliotembelewa na Waziri huyo,  wamemuhakikishia kuwa chakula kipo cha kutosha katika kipindi hiki cha kuelelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani.Aidha wamesema chakula hicho kimeagizwa miezi mitatu kabla ya mwezi huo.

  Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mfanyabiashara Abdulghafar Ismail Mohammed wa kampuni ya Evergreen Ltd, ameiomba serikali kukaa pamoja nao pale inapotaka kufanya maamuzi yoyote yanayowahusu ili kuweka uwiano kwa upande wao, serikali na wananchi.

  Ziara ya Balozi Amina ilihusisha maghala ya kampuni za Yassir Provision, Akhtar Enterprises Malindi, Evergreen Ltd Saateni, Sub Sahara Maruhubi, Azam Mtoni, Vigor Turkey Group  na Bopar Enterprises zote za Mombasa mjini Unguja.

  Pamoja na kujua akiba ya chakula iliyopo nchini kupitia ziara hiyo, Waziri Amina pia alitaka  kujua hali ya mfumko wa bei kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza mwanzoni mwa wiki ijayo.


  0 0

  WAZIRI Amina Salum Ali akiangalia vyakula vilivyohifadhiwa katika ghala la kampuni ya Evergreen lililopo Saateni mjini Zanzibar.

  BAADHI ya vyakula vilivyohifadhiwa katika ghala la kampuni ya Evergreen Saaeteni mjini Zanzibar.
  MENEJA Mkuu wa kiwanda cha Zanzibar Miling Corporation Khalid Ali Yussuf, akimpa maelezo Waziri Amina Salum Ali juu ya uzalishaji wa chakula alipotembelea ofisini kwake Mtoni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
  WAZIRI wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali akiwa katika maeneo ya kiwanda cha Zanzibar Miling Corporation Mtoni alipofanya ziara maalum kwa ajili ya kuangalia hali ya chakula nchini wakati huu wa kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhan. 
  WAZIRI wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali akioneshwa ngano na Meneja Mkuu wa kiwanda cha Zanzibar Milling kilichoko Mtoni Zanzibar Khalid Ali Yussuf, katika sehemu ya usagishaji alipotembelea kiwanda hicho.
  MENEJA Mkuu wa kampuni ya Evergreen Abdulghafar Ismail Mohammed akimfahamisha Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali juu ya hali ya chakula nchini alipotembelea katika ghala lake Saateni mjini Zanzibar.
  MENEJA Mkuu wa kampuni ya Bopar Enterprises Said Nassir Said, akizungumza na Waziri Amina Salum Ali wakati Waziri huyo alipomtembelea ofisini kwake Mombasa mjini Zanzibar.PICHA ZOTE NA ABDALLA OMAR – HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0  0 0
 • 06/01/16--04:32: Article 19
 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama, wakati alipokua akiwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani
  Wanachama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama,wakinyoosha mikono juu kuunga mkono hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,wakati alipokua akiwashukuru kuwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani
  Wanachama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,wakati alipokua akiwapongeza na kuwashukuru wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi wa marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani 
  Wanachama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,wakati alipokua akiwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani.
   

  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF), Ellen Mkondya-Senkoro (Kushoto) na Meneja Mwakilishi Mkazi wa Tropical Health Education Trust(THET) Tanzania, Godwin Kabalika (Kulia) wakisaini mkataba kati Taasisi ya Mkapa na Tropical Health Education Trust(THET) kwaajili ya kutoa mafunzo kwa wananchi wa kada ya Afya ya Jamii pamoja na wafanyakazi wa kada ya afya waliopo katika huspitali zilizopo hospitali za rufaa za kanda ya ziwa.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF), Ellen Mkondya-Senkoro (Kushoto) na Meneja Mwakilishi Mkazi wa Tropical Health Education Trust(THET) Tanzania, Godwin Kabalika (Kulia) wakibadilishana mikataba jijini Dar es Salaam leo, Kwaajili ya mradi ambao umaeshirikisha Taasisi pamoja na serikali kwaajili ya kusaidi wataalam pamoja na wanafunzi wa kada ya afya hapa nchini.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF), Ellen Mkondya-Senkoro akizungumza jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Maendeleo ya Mradi wa miaka mitatu ambao utashirikisha vyou vya afya ya jamii pamoja na hospitali za rufaa za kanda ya ziwa pamoja na kusaini mkataba ya makubaliano ya kuendesha mradi wa wataalamu wa afya ya jamii pamoja na watu wa kada ya afya wa mikoa ya kanda ya ziwa. 

  Amesema kuwa mradi huo unashirikisha Taasisi ya Benjamini Mkapa, Tropical Health Education Trust(THET) pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwaajili ya kuwapa mafunzo wafanyakazi pamoja na wafunzi wa vyuo kwaajili ya kuimarisha afya ya jamii hapa nchini.


  Ellen amesema kuwa Mradi wa kada ya afya umeshaanza tangu Machi huu na utagharimu kiasi cha shilingi bilion 3.3 kwaajili ya kuimarisha uwezo wa Afya ya Jamii hapa nchini ambao unalenga katika kuimarisha vyuo vya Afya  kumi na (Teaching Hospital) Mafunzo katika hospitali za kanda ya ziwa.

  Vyuo hivyo vilivyopo mikoa ya kanda ya ziwa vya kada ya afya ni Bukumbi school of Nursing, Ngudu School of Invironmental Health, Tandabui Institute of HST, Geita Nursing & Midwifery School, Bishop Kisula College of HS, Rubya Health Training Institute, Karagwe Institute of Allied Health Sciencies, Murugwanza School of Nursing, Kahama SON, Kolandoto of Nursing na Hospitali za Rufaa za kanda ya ziwa zitakazo fikiwa na mradi huoni Sekou Toure Geita Regional Referral Hospital, Kagera na Shinyanga.
  Kuanalia uhaba wa watumishi wa afya.
  Meneja Mwakilishi Mkazi wa Tropical Health Education Trust(THET) Tanzania, Godwin Kabalika akizungumza jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kusaini Mkataba wa kushirikiana katika kutoa mafunzo ya afya ya jamii ili kupunguza uhaba wa wafanyakazi wa kada ya afya hapa nchini.
  amesema kuwa kupitia mradi huo wataalam wa afya ya jamii wataongezewa ujuzi pamoja na wanafunzi wa vyuo vya kanda ya ziwa watapata ujuzi ambao utakua unastahili. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF), Ellen Mkondya-Senkoro.

  0 0


  Frank Mvungi-Maelezo

  Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) umeanza kufanya utafiti utakaosadia kupunguza kiwango cha Hewa ya Ukaa (green house gases) kinachozalishwa kutokana na shughuli za ujenzi ili kupunguza uharibifu wa mazingira.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Mhandisi Heri Hatibu kutoka wakala huo amesema utafiti utasaidia kupunguza gharama za Ujenzi hapa nchini. Akizungumzia Malengo ya Utafiti huo Hatibu amesema kuwa, utasaidia kupunguza kiwango cha nishati kinachotumiwa kwenye nyumba kwa ajili ya kupooza hewa hivyo kuokoa fedha inayoweza kutumika kufanya mambo mengine.

  “Sekta ya Ujenzi inachangia asilimia 40 ya hewa ya ukaa hivyo lengo la utafiti huu ni kusaidia kuondoa tatizo hili mara baada ya utafiti wetu kukamilika.” Alisisitiza Mhandisi Hatibu. Aidha Hatibu amesema kuwa, utafiti huo utawezesha kusanifu majengo yatakayotumia nishati kidogo kwenye hatua ya ujenzi na hata wakati wa matumizi ya majengo husika. Pia utachochea matumizi ya vifaa vya Ujenzi vinavyopatikana katika maeneo ya karibu na shughuli za ujenzi.

  Pia utafiti huo utasaidi kutoa elimu kwa wadau wa ujenzi kuhusu nishati mbadala katika kutekeleza shughuli za ujenzi, ikiwemo kuacha kukata miti. Vile vile wananchi wataelimishwa kuhusu njia bora za uchomaji wa matofali ili waweze kutumia vifaa vingine badala ya kukata miti kwa ajili ya uchomaji matofali.

  Matokeo ya utafiti huo unaotarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu yatasaidia wadau wa sekta hii kupanga mipango ya ujenzi itakayosaidia kupunguza athari katika mazingira zinazosababishwa na matumizi makubwa katika uzalishaji vifaa vya ujenzi na hata katika ujenzi.Utafiti huo unafanyika katika Mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Morogoro na Tanga.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific  ACP, mkutano  uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano huo.
   Rais Mstaafu wa Nigeria General Olibegan Obasanjo akimpongeza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan baada ya  kuhutubia Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi kwenye mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano huo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandaaji wa Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific  ACP baada ya kuhutubia kwenye mkutano huo uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano huo.
  (Picha na OMR).

  0 0

  Na Daudi Manongi

  Hifadhi ya Taifa ya wanyamapori ya Selous iliyopo kusini mwa Tanzania imepoteza asilimia 90 ya Tembo waliopo katika hifadhi hiyo kutokana na ujangili uliokithiri.

  Ripoti ya mfuko wa hifadhi ya wanyapori na mazingira duniani (WWF) imesema kufikia mwaka 2022 kama hakutakuwa na hatua zozote kali zitakazochukuliwa kuwalinda tembo kutokana na ujangili basi watatoweka kabisa.

  Ripoti hiyo imeendelea kusema kuwa kwa miaka ya nyuma mbuga ya Selous ilikuwa mojawapo ya mbuga kubwa kabisa katika bara la afrika yenye tembo wengi ambapo kulikuwa na tembo zaidi ya 110000 lakini kutokana na ujangili uliokithiri katika miaka 40 iliyopita tembo hao wamepungua na kubakia 15000 tu uku mahitaji makubwa ya pembe za ndovu katika nchi ya china yakitajwa na ripoti hiyo kuwa kichocheo kikubwa cha ujangili na mauaji ya idadi kubwa ya tembo hao.

  Aidha ripoti hiyo inaonyesha hathari kubwa kiuchumi itakayotokea kutokana na kwamba Tanzania kupitia Mbuga ya Selous inaingiza dola milioni 6 kwa mwaka ikilinganishwa na Sekta ya Viwanda inayochangia dola bilioni 5 katika pato la Taifa.

  Pamoja na Hayo Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeweka mikakati madhubuti ikiwemo kuunda kitengo chake cha intelijensia na kuunda kanda nane za doria za ushirikiano katika mifumo ya ikolojia ya mbuga ya Selous ambayo imeanza kuwa na mafanikio ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wadau wa uhifadhi kuwezesha upatikanaji wa vitendea kazi na zana kwa ajili ya doria.

  Mwaka 2014 Shirika la Kimataifa la Sayansi,Elimu na Utamaduni la umoja wa mataifa(UNESCO) liliiweka Mbuga ya Selous katika Urithi wa asili ulio hatarini Duniani.

  0 0


  0 0

  TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa kupokea taarifa za vitendo vya mauaji ya kikatili vinavyoendelea kutokea katika maeneo mbalimbali nchini, hususani kanda ya Ziwa, Mkoa wa Pwani, na Dar es Salaam.

  Wimbi hili la matukio ya vitendo vya mauaji na ukatili uliojitokeza kwa kufuatana mwezi Mei 2016 yanavunja haki ya kuishi ambayo ndio msingi wa haki zote za binadamu kwa ujumla wake. 

  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inalaani vikali mauaji haya yote na matendo yote ya kikatili dhidi ya mwanadamu yanapotokea popote nchini. 

  Baadhi ya matukio hayo kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia Tume yametokea usiku wa Mei 11, 2016 katika kitongoji cha Nyigumba, Kijiji cha Sima Wilayani Sengerema, Mwanza, ambako watu watano (5) wa familia moja waliuwawa kwa kukatwa mapanga; Mei 18 watu watatu (3) pia waliuwawa kwa kukatwa mapanga wakiwa katika nyumba ya ibada, Msikiti wa Rahman, eneo la Ibanda relini, mtaa wa Utemini, Kata ya Mkolani,Wilaya ya Nyamagana, Mwanza; Usiku wa Mei 25, mwanamume mmoja na mkewe waliuwawa kwa kukatwa mapanga kijijini Manzavi, Wilayani Butiama, Mara.

  Aidha, mnamo Mei 22, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bulale, Kata ya Buhongwa, Mwanza, Bwana Alphonce Musanyenzi aliuawa. Mauaji mengine yametokea Mei 18, Mkoani Pwani, Askari Polisi, Sajenti Ally Salum Kinyogoli alipouwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika. Mei 23, jijini Dar es Salaam, eneo la Kiwalani, watu wanne (4) waliuawa kwa kuchomwa moto wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao; Mei 26, Bi. Anathe Msuya aliuawa kwa kuchinjwa akiwa nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

  Matukio haya ya ukatili yanakiuka haki ya kuishi iliyoainishwa katika ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sheria za nchi, matamko na mikataba mbalimbali ya haki za binadamu ya kikanda na kimataifa.

  Kufuatia wimbi hili la mauaji linaloonekana kuendelea nchini, Tume inalaani na kukemea vikali vitendo hivyo vya kikatili.

  Mbali ya ukiukaji mkubwa wa haki ya msingi ya kuishi, mauaji haya na matukio haya pia ni kinyume na mafundisho ya imani zetu mbalimbali, hivyo yasifumbiwe macho na kuachwa yaendelee, kwani yanaweza kuleta mazoea mabaya ya kuona suala la kuuwa ni jambo la kawaida na hivyo kuhatarisha amani, maisha ya watu na jamii. 

  Hivyo, Tume inashauri yafuatayo:
  1.Serikali kupitia Jeshi la Polisi ichukue hatua mahsusi kuhakikisha ulinzi wa wananchi dhidi ya mauaji na vitendo hivi, kwani jukumu la kwanza la kuhakikisha usalama wa wananchi ni jukumu la serikali. Jeshi la Polisi lihakikishe watu wote waliohusika kutekeleza mauaji haya wanakamatwa ili sheria ichukue mkondo wake.

  2.Tume inawataka pia wananchi wahakikishe wanashirikiana na vyombo vya dola kufichua maovu na kubaini uvunjifu wowote wa sheria na haki za binadamu ndani ya jamii, na kutoa taarifa kwa mamlaka husika kuzuia matukio kama haya kujirudia, au kusaidia upelelezi wa mauaji haya na matendo mengineyo ya uvunjifu wa sheria.

  3.Jamii ijenge utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu.
  4.Mamlaka za Serikali za mitaa katika ngazi zote ziwe na mipango madhubuti ya kuhakikisha ulinzi na usalama katika maeneo yao.
  5.Tume inatoa rambirambi kwa ndugu, jamaa na wanafamilia waliopoteza wapendwa wao katika matukio haya na pole kwa majeruhi.
  Jukumu la ulinzi na utetezi wa haki za binadamu ni letu sote!

   Imetolewa na:
  (SIGNED)
  Mhe. Bahame Tom Nyanduga
  Mwenyekiti
  TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
  Mei 31, 2016.

  0 0

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiwa na vikosi vya ulinzi na usalama vinavyotoa ulinzi katika msitu wa Mapangopori ya Amboni mkoani Tanga. Naibu Waziri alifanya ziara ya kutembelea mapango hayo ambayo yalikuwa makazi ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi Maalum kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia Makao Makuu Dar es Salaam, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, William Mwampagale.
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akichungulia pango lililopo katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga.
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitoa maelekezo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo (kulia), mara baada ya kutoka ndani ya pango lililopo katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Katikati ni Mkuu wa Kikosi Maalum kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia Makao Makuu Dar es Salaam, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, William Mwampagale.

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto meza kuu) akizungumza katika Kikao cha Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Mkoa huo, Martine Shigella. Watatu kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Ernest Mangu (wapili kushoto). Viongozi hao wamekutana  mkoani humo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama mkoani Tanga.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella kabla ya kwenda katika msitu wa Mapangopori ya Amboni mkoani Tanga. Naibu Waziri alifanya ziara ya kutembelea mapango hayo ambayo yalikuwa makazi ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI.

  0 0

  Na. Aron Msigwa- DODOMA.
  SERIKALI imesema kuwa itaendelea kuboresha maslahi ya askari wa Jeshi la Polisi na kuwajengea nyumba za kisasa za kuishi ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina wakati akijibu maswali ya wabunge kuhusu mkakati wa Serikali wa kuboresha maslahi ya Askari wa Jeshi hilo kwa niaba ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Bungeni mjini Dodoma leo
  Amesema kuwa Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 itatekeleza Mpango kabambe wa ujenzi wa nyumba za Polisi 4136 ambao utakwenda sambamba na ujenzi wa vituo vya Polisi.

  Amesema Serikali imechukua hatua za haraka kulishughulikia suala la ukosefu wa nyumba za askari hao katika maeneo mbalimbali nchini ili kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yenye ukosefu wa nyumba hizo.

  Amelieleza Bunge kuwa Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha kuwa maslahi ya Askari Polisi yanaimarishwa ikiwemo malipo ya Posho ya pango kwa askari wasio na nyumba ambayo ni asilimia 15 ya mishahara yao ili waweze kulipia gharama hizo.

  Ameongeza kuwa  askari wenye utalaam maalum wakiwemo madereva na madaktari wamekuwa wakilipwa posho ya asilimia 15 ya mishahara yao na kuongeza kuwa askari wanaoajiriwa katika ajira mpya kama madaktari wamekuwa wakilipwa mishahara sawa na madaktari wengine bila kujali vyeo vyao.

  “Serikali tumefanya jitihada kubwa sana kuboresha maslahi ya askari wetu, kama Serikali tumetoa posho za nyumba, posho za utalaam maalum kwa askari wote ambayo ni asilimia 15 ya mshahara wa kila Polisi hii yote ni kuwafanya askari wetu waweze kumudu gharama za maisha” Amesisitiza Mhe. Mpina.
  Ameeleza kuwa kwa askari wanaofanya kazi katika mazingira magumu wakiwemo wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wamekuwa wakipewa posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu (Hardship allowance) kiasi cha shilingi laki moja (100,000) kila mwezi.
  Mhe. Mpina amebainisha kuwa askari wote wanaohitimu mafunzo yao wamekuwa wakikatiwa Bima ya Afya kwa asilimia 100 na Serikali pamoja na udhamini wa mikopo mbalimbali katika taasisi za kifedha ili waweze kupewa mikopo na taasisi hizo.
  Aidha, amesisitiza kuwa serikali imewapandishia kiwango cha Posho ya katikati ya mwezi (Ration Allowance) kutoka shilingi 180,000 za awali hadi 300,000 ambazo wanalipwa kwa sasa nchi nzima.
  Katika hatua nyingine Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imetoa ufafanuzi kuhusu vijana wa kidato cha nne kutochukuliwa kujiunga na  Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi  amesema kuwa hatua ya kuwachukua vijana wote wanaomaliza kidato cha nne kwa sasa haiwezekani kutokana na uwezo mdogo wa kifedha wa Serikali.
  Amesema kuwa uwezo wa JKT kuchukua vijana wa kujitolea kwa sasa ni 5000 hadi 7000 kwa mwaka kulingana na bajeti inayotolewa na kuongeza kuwa mpango wa Serikali ni kuendelea kutenga fedha na kujenga kambi zaidi za mafunzo ili kuwawezesha vijana wengi kujiunga  na mafunzo hayo kulingana na upatikanaji wa fedha.
  Kwa upande wa wahitimu wa kidato cha sita wanaotakiwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa Sheria Mhe. Mwinyi amesema Serikali imewachukua vijana 14,000 na inaendelea kujenga uwezo wa ndani wa kuchukua vijana wengi zaidi.
  Amesema Serikali inakusudia kujenga majengo ndani ya makambi ili kuwezesha vijana wote wanaohitimu kidato cha sita kupitia JKT kabla ya kujiunga na vyuo mbalimbali hapa nchini.
  Aidha, Amefafanua kuwa kwa wale wanaojiunga na JKT kwa kujitolea ambao idadi yao inafikia 5000 sio wote wanaopata nafasi ya kuajiriwa katika vyombo vya Ulinzi na Usalama na kuongeza kuwa ni asilimia 71 ndio hupata ajira kwenye vyombo hivyo huku waliobaki wakilazimika kurudi nyumbani.
  Amebainisha kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inaangalia utaratibu wa kuwawezesha vijana hao ili wanaporudi uraiani waweze kupatiwa mitaji ya kuwawezesha kujiajiri wenyewe.


   Baadhi ya Mawaziri na Wabunge wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha 34 mjini Dodoma.
   Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Moga iliyoko jijini Dar es salaam wakifuatilia shughuli za kikao cha 34 cha Bunge mjini Dodoma. Wanafunzi 90 wa shule hiyo wamelitembelea Bunge hilio kujifunza namna linavyoendeshwa.
   Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha 34 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ndani ya Ukumbi wa Bunge kabla ya kuanza kwa kikao cha 34 cha Mkutano wa 3 wa Bunge mjini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Malisili na Utalii Mhe. Ramo Makani akijibu maswali ya Wabunge yaliyoelekezwa kwenye wizara hiyo wakati wa kipindi cha Maswali na majibu leo, Dodoma.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Muhagama akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa Serikali ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
   Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 leo mjini Dodoma. Wizara hiyo inaliomba Bunge lipitishe kiasi cha shilingi Trilioni 8.7 kwa ajiri ya matumizi ya kawaida na matumizi mengine.
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto) na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji wakiandika maoni ya Wabunge waliokuwa wakichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara Fedha na Mipango kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 leo mjini Dodoma.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(kulia) akimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina nje ya Ukumbi wa Bunge leo.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto nje ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma.
   Baadhi ya Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Moga iliyoko jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge kufuatilia shughuli za kikao cha 34.
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto) akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kulia) kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma. 

  0 0


  Kaimu Afisa Mtendaji wa Legal Services Facility (LSF), Bi Scholastica Jullu akizungumza na waandishi wa habari jinsi wasaidizi wa kisheria wanavyosaidia kubadilisha maisha ya watanzania 
  Jopo la viongozi wa LSF wakionyesha ripoti jinsi wasaidizi wa sheria walivyotatua matatizo ya wananchi nchini, kutoka kushoto ni Meneja Mawasiliano, Renatus Sona, Afisa Mradi na Haki za wanawake, Bi Fortunata Kitokevya, Kaimu Afisa Mtendaji, Bi Scholastica Jullu, wa pili kulia Meneja Ufuatiliaji na Matokeo, Juma Mwenga na mwisho kulia ni Bw. Masele

  MFUKO wa msaada wa kisheria (LSF) umetoa ruzuku kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 18 kwa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojishughulisha utoaji wa msaada wa kisheria kwa ajili ya mafunzo kwa wasaidizi wa sheria 4,000 nchi nzima.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Afisa Mtendaji, Bi Scholastica Jullu amesema kwamba ruzuku imetolewa kuanzia 2012 kwa mashirika hayo ili kuweza kutoa mafunzo kwa wasaidizi wa sheria katika kutatua matatizo yanayowakabili wananchi hasa wa vijijini.

  “Dhumuni la uanzishwaji wa mfuko huu ni kulinda haki za binadamu kupitia ujengaji uwezo wa kisheria na kuongeza upatikanaji wa huduma za kisheria kwa watu masikini na wanajamii wengine walio katika hatari ya kukosa haki zao hususani wanawake nchini,” aliongeza Bi Jullu Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011, LSF imechangia katika kukuza na kulinda haki za binadamu huku ikiweka msisitizo katika ulinzi w haki za wanawake na makundi maalum.

  Amesema kwamba kutokana na mafunzo waliopata wasaidizi wa kisheria nchini imewezesha upatikanaji wa huduma za usaidizi wa sharia kwa watanzania takribani milioni thelathini na tano (35 milioni).Alifafanua kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013 mpaka mwaka 2015 takribani watu 90,000 walipata huduma za msaada wa kisheria na watu 300,000 walifikiwa na elimu ya sheria nchini nzima.

  Mambo ambayo wasaidizi wengi wa sheria wanayokutana nayo ni matatizo ya ardhi, ndoa, mirathi, watoto na jinsi ambao asilimia 80 yalishughulikiwa na asilimia 9 tu yalipelekwa kwenye vyombo vingine vya utoaji haki kama vile mahakama, mabaraza ya usuluhishi, serikali za mitaa na polisi.
  Bi Jullu alisisitiza mchakato umeanza kwa wadau wa sheria, mashirika yasiyo ya kiserikali na serikali ili kuja na sheria itakayowatambua wasaidizi wa kisheria kwenye mifumo ya serikali.

  Kwa upande wake, msaidizi wa kisheria kutoka wilaya ya ilala, Bi Beatrice Bange amesema kwamba changamoto kubwa ni uelewa mdogo wa watanzania wengi kuhusu huduma za wasaidizi wa kisheria na msaada wa kisheria.Aliongeza kwamba matatizo mengi anayokutana nayo katika wilaya ya ilala ni ndoa, mirathi na matatizo ya ajira kwa wafanyakazi wa kada ya chini.Utafiti uliofanywa na shirika hilo mwaka jana ulionyesha kuwa zaidi ya asilimia 70 ya watanzania hawana uelewa kuhusu msaada wa kisheria na uwepo wa wasaidizi wa sheria.

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiongoza kikao kilichoshirikisha watendaji kutoka kampuni zinazojishughulisha na utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi za Statoil na ExxonMobil pamoja na Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC).
  Meneja Mkazi wa Kampuni inayojishughulisha na shughuli za utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta ya Statoil Tanzania, Øystein Michelsen, (kushoto) akielezea shughuli zakampuni hiyo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia).
  Meneja Mkazi wa Kampuni inayojishughulisha na shughuli za utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta ya Statoil Tanzania, Øystein Michelsen akisisitiza jambo katika kikao hicho.
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha watendaji kutoka kampuni zinazojishughulisha na utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi za British  Gas (BG), Ophir, Pavilion pamoja na Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC)

  Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa ili Tanzania iweze kuwa nchi ya viwanda, nishati ya uhakika inahitajika na kutaka makampuni kuwekeza katika uzalishaji wa umeme unaotokana na gesi.

  Profesa Muhongo aliyasema hayo jijini Dar es Salaam katika nyakati tofauti alipokutana na watendaji wa kampuni zinazojishughulisha na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Nishati  na Madini na Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) lengo likiwa ni kupokea taarifa ya maendeleo ya miradi mbalimbali ya makampuni hayo.

  Kampuni hizo zinazofanya kazi kwa kushirikiana na Shirika la TPDC ni pamoja na British Gas (BG),  Ophir, ExxonMobil na Statoil.Profesa Muhongo alisema kuwa hakuna nchi yoyote duniani iliyopiga hatua kimaendeleo bila kuwa na nishati ya uhakika ya umeme na kuwataka wawekezaji kuchangamkia fursa kupitia gesi nyingi iliyogunduliwa.

  Alitaja maeneo yanayohitaji uwekezaji katika kuzalisha umeme kwa kutumia gesi kuwa ni pamoja na Mtwara, Lindi, Somanga Fungu, na Mkuranga.Aliongeza kuwa viwanda 37 pamoja na vya sementi vinahitaji gesi na kusisitiza kuwa iwapo sekta ya gesi itatumiwa ipasavyo inaweza kuchangia nchi kupiga hatua na kuingia katika kundi la nchi zenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama Dira ya Maendeleo ya Taifa inavyosema.

  Wakati huo huo Profesa Muhongo, aliwataka watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake kufanya kazi kwa kasi ili kuendana na kasi ya uwekezaji katika shughuli za utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta.“Sekta ya gesi na mafuta ambayo ni mpya inahitaji umakini na kasi ili kuvutia wawekezaji zaidi,” alisisitiza Profesa Muhongo.

  Akizungumzia mikakati ya serikali katika kuzalisha wataalam katika masuala ya mafuta na gesi Profesa Muhongo alisema kuwa serikali imekuwa ikitoa ufadhili kwa wanafunzi katika ngazi za shahada za uzamili na uzamivu katika vyuo vilivyopo nje ya nchi vyenye uzoefu katika fani hiyo, pamoja na uanzishwaji wa programu hizo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo cha Madini.

  Alisema kuwa mpaka sasa kuna idadi ya takribani wanafunzi 98 waliohitimu masomo hayo na kuziomba kampuni hizo kuajiri wataalam hao ili wawe na mchango mkubwa kwenye sekta ya gesi.“ Nia ya Serikali ni kuwa na wataalam wazawa ambao watanufaika kupitia uchumi wa gesi kwa kufanya kazi katika viwanda vya kuchakata gesi na kuzalisha umeme unaotokana na gesi,” alisema Profesa Muhongo.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Dk. James Mataragio alisema kuwa shirika hilo limekuwa likishirikiana na kampuni hizo katika hatua zote muhimu hususan katika kiwanda cha kuchakata gesi asilia kimiminika (Liquefied Natural Gas) na kuongeza kuwa mpaka sasa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda limeshapatikana.

  Alisema kuwa, Tanzania inatarajia kuwa kitovu kikuu cha gesi barani Afrika kwani gesi nyingi itakayozalishwa itauzwa katika nchi nyingine.Aliongeza kuwa nchi kama Uganda, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na Zambia zimeonesha nia ya  kuhitaji gesi kwa ajili ya kuzalisha nishati ya uhakika kwa kuwa nchi hizo zinatumia maji kuzalisha umeme ambapo uzalishaji wake hupungua hususan wakati wa kiangazi kutokana na kupungua kwa kina cha maji.

  Naye Meneja Mkazi wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Øystein Michelsen, alisema kuwa kampuni yake ipo tayari kushirikiana na Serikali kuhakikisha kuwa miradi yake inakamilika kwa wakati.Alisema tangu kampuni hiyo kuanza shughuli zake nchini, imekuwa ikishirikiana na Serikali kwa kutoa ufadhili wa masomo katika masuala ya gesi na mafuta nje ya nchi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri.

  Aliongeza kuwa kampuni ya Statoil imekuwa ikitoa elimu ya ujasiriliamali kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara ili waweze kushiriki katika uchumi wa gesi kupitia utoaji wa huduma zake kwa Kampuni hiyo.

  0 0

  Na Immaculate Makilika – MAELEZO

  Serikali ya Tanzania yasifika kwa kuwa na uongozi unaozingatiaSheria na Utawala Bora.

  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angella Kairuki alipokuwa akifungua Mkutano wa siku mbili wa Kimataifa kuhusu Utawala wa Sheria na Utawala bora.

  Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kujadili masuala ya Afrika katika kukuza utawala wa sheria katika utekelezaji wa agenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 na agenda ya Umoja wa Afrika ya 2063.

  “Mkutano huu wa kistoria nchini Tanzania utasaidia kuleta mageuzi katika Taasisi zinazosimamia masuala ya Sera na Sheria ambayo yatachochea maendeleo mazuri katika nchi za Afrika”, alisema Waziri Kairuki.

  Akiendelea kuzungumza Waziri Kairuki alisema uwepo wa Marais wastaafu kama Mhe.Benjamin Mkapa na Dkt. Jakaya Kikwete, katika mkutano huo ni ushahidi tosha wakuwepo na mafanikio ya utawala wa sheria na utawala bora nchini Tanzania.

  Kwa upande wa Rais Mstaafu Mhe.Benjamin Mkapa, amesema ili Bara la Afrika liendelee Kiuchumi ni lazima watu wake wapate elimu ya uraia ili waweze kushiriki zaidi katika masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo yao pamoja na kuwepo na uongozi utakaoleta mabadiliko “transformative leadership”.

  Naye, Waziri wa Haki Sudani ya Kusini Mhe. Pwanauwilla Unango amesema pamoja na kuwa Bara la Afrika lina matatizo mengi kama vita, njaa, magonjwa na ndoa za utotoni, dunia isiitazame Afrika kwa mtazamo huo pekee, bali inahitaji msaada kutoka Jumuiya za Kimataifa.

  Mkutano huo wenye kauli mbiu “Kufikia agenda ya 2030 na agenda ya 2063:Utawala wa Sheria kwa Maendeleo Endelevu ya Afrika”, (Achieving the 2030 agenda and agenda 2063:The rule of law as a driver of Africa’s suistainable development) , umeandaliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Sheria (IDLO) la nchini Italia, kwa Ushirikiano wa Serikali ya Tanzania umehusisha wadau mbalimbali wakiwemo Mawaziri, kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Mabalozi kutoka ndani na nje ya Afrika pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya kutetea Haki za Binadamu.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa Fedha 2016/2017, Bungeni Mjini Dodoma leo
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, (Kulia) akifurahia jambo na Mbunge wa Viti Maalumu kutoka Zanzibar, Tauhida Cassian Galoss Nyimbo, mara baada ya kuwasilishwa kwa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 mjini Dodoma leo.
  Waziri wa Fedha na MIpango, Dkt. Philip Mpango (kushoto) na Naibu Waziri wake Dkt. Ashatu Kijaji, wakiwa makini kuandika hoja mbalimbali za wabunge wakati wakichangia Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni Mjini Dodoma leo.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi waandamizi wa Wizara hiyo ambapo kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Dorothy Mwanyika na kushoto kwake ni naibu Katibu Mkuu Amina Hamis Shaban.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza jambo na Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma mara baara ya kuwasilishwa kwa Bajeti ya Wizara hiyo.

  0 0

  Na Fatma Salum- MAELEZO.

  Dodoma

  Serikali imeagiza kuwa kuanzia Mwezi Julai mwaka huu ni lazima mfumo wa kielektroniki utumike katika utoaji wa risiti kwa tozo, faini, ada na malipo mengine yote ya Serikali Kuu, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wakala wote wa Serikali ili kudhibiti upotevu wa mapato.

  Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.

  Dkt. Mpango alisema kuwa agizo hilo pia linahusisha malipo ya faini za mahakamani, faini za usalama barabarani, viingilio kwenye mbuga za wanyama na vibali vya kuvuna maliasili.

  “Naziagiza ofisi zote za Serikali kutoa risiti za kielektroniki kwa malipo yote yatakayofanyika kwani matumizi ya vifaa na mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato yataongeza ufanisi na kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali.” Alisema Dkt. Mpango.

  Katika kufanikisha hilo Dkt. Mpango aliongeza kuwa Maafisa Masuuli wote wanaelekezwa kusimamia ipasavyo utekelezaji wa agizo hilo.

  Katika hatua nyingine, Dkt. Mpango alisema kuwa Serikali imeamua kufanya uthamini wa majengo kwa mkupuo ili kuongeza mapato yatokanayo na kodi ya majengo na usimamizi wake utakuwa chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.

  Katika hotuba hiyo Dkt. Mpango amefafanua mkakati wa Wizara yake kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano kuanzia 2016/17 hadi 2020/21 ambao umejikita katika kujenga msingi wa uchumi wa viwanda na maendeleo ya watu.


  0 0

  Na Fatma Salum- MAELEZO,Dodoma.

  Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imetenga shilingi bilioni 10 katika mwaka wa fedha 2016/2017 kwa ajili ya ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Mtwara.

  Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani leo Bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtwara Vijijini Mhe. Hawa Ghasia lililohoji kuhusu ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Mtwara.

  Mhe. Ngonyani alisema kuwa Serikali imeendelea kufanya matengenezo ya mara kwa mara katika uwanja huo na TAA inafanya tathmini ya uchakavu wa matabaka ya lami (Pavement Evaluation) ya njia ya kuruka na kutua ndege ili kubaini ukarabati stahiki unaotakiwa na matumizi ya fedha zinazohitajika na kazi hiyo ya tathmini inatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 2016.

  Aidha, Mhe. Ngonyani alieleza kuwa katika mpango wa muda mrefu, Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege inaandaa Mpango Kabambe (Master Plan & Concept Design) kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa uwanja huo kutoka daraja 3C la sasa kwenda daraja la 4E ili kuweza kuhudumia ndege kubwa zaidi hivyo kuwa kitovu cha usafiri wa anga kwa Ukanda wa Kusini.

  “Ukarabati na upanuzi wa uwanja utahusisha miundombinu yote ya kiwanja ikiwemo taa na mitambo ya kuongozea ndege pamoja na majengo. Kazi hiyo ya uandaaji wa Mpango Kabambe na Usanifu wa Awali inatarajiwa kukamilika Julai 2016.” Alisema Ngonyani.

  Ikiwa ni mpango wa muda mfupi, Mhe. Ngonyani aliongeza kuwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege imeingia makubaliano na Kampuni ya British Gas (BG) kwa ajili ya kutumia taa zake ambazo ni za kuhamisha kwa ajili ya kuongozea ndege pale ambapo ndege itatakiwa kutua usiku katika uwanja huo.

  0 0

   Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha 34 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ndani ya Ukumbi wa Bunge kabla ya kuanza kwa kikao cha 34 cha Mkutano wa 3 wa Bunge mjini Dodoma.

   Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Moga iliyoko jijini Dar es salaam wakifuatilia shughuli za kikao cha 34 cha Bunge mjini Dodoma. Wanafunzi 90 wa shule hiyo wamelitembelea Bunge hilio kujifunza namna linavyoendeshwa.
   Baadhi ya Mawaziri na Wabunge wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha 34 mjini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Malisili na Utalii Mhe. Ramo Makani akijibu maswali ya Wabunge yaliyoelekezwa kwenye wizara hiyo wakati wa kipindi cha Maswali na majibu leo, Dodoma.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Muhagama akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa Serikali ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
   Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 leo mjini Dodoma. Wizara hiyo inaliomba Bunge lipitishe kiasi cha shilingi Trilioni 8.7 kwa ajiri ya matumizi ya kawaida na matumizi mengine.
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto) na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji wakiandika maoni ya Wabunge waliokuwa wakichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara Fedha na Mipango kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 leo mjini Dodoma.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(kulia) akimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina nje ya Ukumbi wa Bunge leo.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto nje ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma.
   Baadhi ya Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Moga iliyoko jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge kufuatilia shughuli za kikao cha 34.
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto) akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kulia) kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma. 

  Na. Aron Msigwa- DODOMA.

  Serikali imesema kuwa itaendelea kuboresha maslahi ya askari wa Jeshi la Polisi na kuwajengea nyumba za kisasa za kuishi ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina wakati akijibu maswali ya wabunge kuhusu mkakati wa Serikali wa kuboresha maslahi ya Askari wa Jeshi hilo kwa niaba ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Bungeni mjini Dodoma leo
  Amesema kuwa Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 itatekeleza Mpango kabambe wa ujenzi wa nyumba za Polisi 4136 ambao utakwenda sambamba na ujenzi wa vituo vya Polisi.

  Amesema Serikali imechukua hatua za haraka kulishughulikia suala la ukosefu wa nyumba za askari hao katika maeneo mbalimbali nchini ili kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yenye ukosefu wa nyumba hizo.

  Amelieleza Bunge kuwa Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha kuwa maslahi ya Askari Polisi yanaimarishwa ikiwemo malipo ya Posho ya pango kwa askari wasio na nyumba ambayo ni asilimia 15 ya mishahara yao ili waweze kulipia gharama hizo.

  Ameongeza kuwa  askari wenye utalaam maalum wakiwemo madereva na madaktari wamekuwa wakilipwa posho ya asilimia 15 ya mishahara yao na kuongeza kuwa askari wanaoajiriwa katika ajira mpya kama madaktari wamekuwa wakilipwa mishahara sawa na madaktari wengine bila kujali vyeo vyao.

  “Serikali tumefanya jitihada kubwa sana kuboresha maslahi ya askari wetu, kama Serikali tumetoa posho za nyumba, posho za utalaam maalum kwa askari wote ambayo ni asilimia 15 ya mshahara wa kila Polisi hii yote ni kuwafanya askari wetu waweze kumudu gharama za maisha” Amesisitiza Mhe. Mpina.
  Ameeleza kuwa kwa askari wanaofanya kazi katika mazingira magumu wakiwemo wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wamekuwa wakipewa posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu (Hardship allowance) kiasi cha shilingi laki moja (100,000) kila mwezi.
  Mhe. Mpina amebainisha kuwa askari wote wanaohitimu mafunzo yao wamekuwa wakikatiwa Bima ya Afya kwa asilimia 100 na Serikali pamoja na udhamini wa mikopo mbalimbali katika taasisi za kifedha ili waweze kupewa mikopo na taasisi hizo.
  Aidha, amesisitiza kuwa serikali imewapandishia kiwango cha Posho ya katikati ya mwezi (Ration Allowance) kutoka shilingi 180,000 za awali hadi 300,000 ambazo wanalipwa kwa sasa nchi nzima.
  Katika hatua nyingine Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imetoa ufafanuzi kuhusu vijana wa kidato cha nne kutochukuliwa kujiunga na  Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi  amesema kuwa hatua ya kuwachukua vijana wote wanaomaliza kidato cha nne kwa sasa haiwezekani kutokana na uwezo mdogo wa kifedha wa Serikali.
  Amesema kuwa uwezo wa JKT kuchukua vijana wa kujitolea kwa sasa ni 5000 hadi 7000 kwa mwaka kulingana na bajeti inayotolewa na kuongeza kuwa mpango wa Serikali ni kuendelea kutenga fedha na kujenga kambi zaidi za mafunzo ili kuwawezesha vijana wengi kujiunga  na mafunzo hayo kulingana na upatikanaji wa fedha.
  Kwa upande wa wahitimu wa kidato cha sita wanaotakiwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa Sheria Mhe. Mwinyi amesema Serikali imewachukua vijana 14,000 na inaendelea kujenga uwezo wa ndani wa kuchukua vijana wengi zaidi.
  Amesema Serikali inakusudia kujenga majengo ndani ya makambi ili kuwezesha vijana wote wanaohitimu kidato cha sita kupitia JKT kabla ya kujiunga na vyuo mbalimbali hapa nchini.
  Aidha, Amefafanua kuwa kwa wale wanaojiunga na JKT kwa kujitolea ambao idadi yao inafikia 5000 sio wote wanaopata nafasi ya kuajiriwa katika vyombo vya Ulinzi na Usalama na kuongeza kuwa ni asilimia 71 ndio hupata ajira kwenye vyombo hivyo huku waliobaki wakilazimika kurudi nyumbani.
  Amebainisha kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inaangalia utaratibu wa kuwawezesha vijana hao ili wanaporudi uraiani waweze kupatiwa mitaji ya kuwawezesha kujiajiri wenyewe.


older | 1 | .... | 865 | 866 | (Page 867) | 868 | 869 | .... | 1898 | newer