Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Mama Janeth Magufuli awasili mikoa ya Lindi na Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi.

$
0
0
 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipofika mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya kikazi.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi na Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na kinamama waliojitokea kumpokea alipowasili Mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya kikazi. 
 Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi akimshukuru Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli kwa kuamua kufanya ziara ya kikazi mkoani humo.
 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akiongea kwa niaba ya kina mama waliojitokeza kumpokea Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli ambapo alimuahidi kuendelea kumuunga mkono kwenye shughuli zake na kumtaka kwenda mkoni humo mara kwa mara kwa ajili ya ziara za kikazi.Katikati mwenye pochi ya bluu ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa

 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi ya Ungo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipofika mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya kikazi. Katikati ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa

 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi ya Kitenge Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipofika mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya kikazi.

 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi ya Kitenge Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa.

 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akiwakabidhi zawadi ya mbuzi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (kushoto) na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa (katikati).

 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwashukuru kinamama na baadhi ya viongozi waliokuja kumpokea alipofika mkoani Lindi.

 Mtoto Lulu Charles akimpa shada la maua Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipowasili Mkoani Mtwara.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Serikali waliofika kumpokea alipowasili Masasi Mkoani Mtwara. 

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendegu akimueleza Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli utekelezaji wa mambo mbalimbali ya maendeleo katika mkoa wake.


PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO


WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KUSIMAMIA UKUAJI WA UCHUMI KWA MAENDELEO YA NCHI

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameliambia Bunge Mjini Dodoma, Leo, Juni Mosi, 2016 kwamba serikali imejipanga kuchukua hatua madhubuti zinazolenga kujenga Taifa linalojitegemea kwa kukuza uchumi na kupunguza umasikini. 

Amezitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kusimamia na kufuatilia kwa ukamilifu utekekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/17 - 2020/21. Mpango huu unajikita katika kujenga msingi wa uchumi wa viwanda na maendeleo ya watu.

Amesema kuwa ili mpango huu uweze kutekelezwa kwa ufanisi na kupata matokeo tarajiwa, ni dhahiri kuwa zinahitajika rasilimali za kutosha, hususan rasilimali fedha. 

"Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na wadau wengine inalo jukumu la kuimarisha ukusanyaji wa mapato ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa rasilimali fedha" alisisitiza

Dkt. Mpango amesema kuwa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 imeweka bayana majukumu ya Wizara ya Fedha na Mipango ya kuimarisha usimamizi na ukusanyaji wa mapato, kupanua wigo wa vyanzo vipya vya mapato na kusimamia kwa ufanisi matumizi ya fedha za umma kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali.

Amenukuu kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, alipokuwa anawasilisha hotuba yake katika Bunge, Aprili 25 mwaka 2016, aliposema kuwa mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano yenye falsafa ya HAPA KAZI TU, imelenga kufikia kipato cha kati na kufanyika mapinduzi makubwa ya viwanda yanayotegemea sana utulivu wa uchumi. 

"Tutasimamia kikamilifu matumizi ya vifaa na mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato ili kuongeza ufanisi na kudhibiti upotevu wa mapato" Aliongeza Dkt. Mpango

Amesema kuwa serikali itarasimisha sekta isiyo rasmi kuingia katika mfumo wa kodi na hivyo kupanua wigo wa kodi na Kuimarisha ufuatiliaji wa mapato yanayokusanywa na taasisi na mamlaka mbalimbali za Serikali ili kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali. 

Dkt. Mpango amebainisha kuwa watasimamia na kuimarisha ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi na kuboresha usimamizi wake chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania kutokana na uzoefu na mifumo ya ukusanyaji iliyopo nchi nzima

"Tutaendelea kuchukua hatua za kudhibiti na kupunguza misamaha ya kodi isiyo na tija na Kuendelea kuimarisha usimamizi na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara bandarini na maeneo ya mipakani ili kuhakikisha kwamba kodi stahiki zinakusanywa" aliongeza Dkt. Mpango.

Ametaja mikakati hiyo kuwa ni moja ya njia ya kupunguza utegemezi wa misaada kutoka nje ambayo imezidi kupungua kila mwaka.Ametoa mfano wa mwaka wa fedha unaoishia Juni mwaka huu ambapo hadi Machi, wadau wa maendeleo wametoa shilingi bilioni 1,064.89 sawa na asilimia 46 ya fedha zote zilizoahidiwa kutolewa na wadau hao hali iliyoathiri utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyokusudiwa

Ametaja sababu za hali hiyo kuwa ni kupungua kwa misaada toka nje kunatokana na kujiondoa kwa baadhi ya Washirika wa Maendeleo wanaochangia kupitia Misaada na mikopo ya kibajeti na baadhi ya Washirika wa Maendeleo kupunguza ahadi zao. 

"Wafadhili wanaochangia kupitia misaada ya kibajeti walipunguza michango yao kutoka shilingi bilioni 660 mpaka shilingi bilioni 399 katikati ya mwaka wa fedha 2015/16 na wengine kuhusisha utoaji wa fedha na masharti ambayo hayakuwemo katika makubaliano ya awali" Aliongeza Dkt. Mpango

Alisema kuwa katika kushughulikia changamoto hizo, Serikali inaendelea na mazungumzo na Washirika wa Maendeleo ili kuhakikisha kwamba fedha zilizoahidiwa zinatolewa kwa wakati. 

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameliomba Bunge, liidhinishie Wizara yake kupitia mafungu yote tisa ya kibajeti, jumla ya Shilingi Trilioni 8.7 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na shilingi Bilioni 791.99 kwaajili ya miradi ya maendeleo.

Amesema kuwa Kati ya fedha hizo,shilingi bilioni 45.45 ni kwa ajili ya Mishahara na shilingi bilioni 8,671.04 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo.

Spika Mstaafu Mhe. Anna Makinda atembelea Taasisi ya Uongozi

$
0
0
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Prof. Joseph Semboja, akimkaribisha Spika mstaafu wa Bunge Mhe. Anna Makinda pale kiongozi huyo alipotembelea taasisi hiyo kwa mara yake ya kwanza mapema leo. 
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja akimuelezea Spika mstaafu Mhe. Anna Makinda kuhusu mpango wa ujenzi wa ofisi za kudumu za Taasisi hiyo zilizopo katika kijiji cha Kondo, wilayani Bagamoyo.
 Spika mstaafu Mhe. Anna Makinda akiweka saini yake katika kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika ofisi za Taasisi ya Uongozi zilizopo Oyster Bay jijini Dar es Salaam mapema leo.
 Spika mstaafu Mhe. Anna Makinda akimuonesha Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja kitabu cha muongozo na kanuni za Bunge.
Mazungumzo yakiendelea kati ya Spika mstaafu Mhe. Anna Makinda na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja.

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM (BARA) AKUTANA NA WAJUMBE WA TIMU YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI WA UMOJA WA ULAYA (EU)

$
0
0

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe. Philip Mangula akizungumza na Timu ya Wajumbe  Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya waliomtembelea leo ofisini kwake Lumumba jijini Dar es salaam.
Waangalizi wa Uuchaguzi wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) wakimsikiliza kwa makini Makamu Mwenyekiti wa CCM Mhe. Philip Mangula ofisini kwake Lumumba jijini Dar es salaam.
 Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) wakizungumza na  Makamu Mwenyekiti wa CCM Mhe. Philip Mangula ofisini kwake Lumumba jijini Dar es salaam .Kikao hicho pia kilihuzuliwa na Kaimu Mkuu wa Idara Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dkt. Pindi Chana.

Timu hiyo ya Waangalizi wa Umoja wa Nchini za Ulaya ilikuwa na ujumbe wa watu watano ambao ni Mhe. Judith Sargetini, Mbunge na Kiongozi Mkuu wa Waangalizi, Ms Tania Marques Naibu Kiongozi wa Waangalizi, Balozi Roeland Van De Geer (Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya), Ms Luana Reale, (Kansela) na Ms Anna Constatini (Mwambata wa Masuala ya Uchaguzi)


MUHIMBILI YAPOKEA VIFAA VYA KUTOA HUDUMA KWA WATOTO WADOGO

$
0
0
Kushoto ni Mkuu wa Uuguzi na Mazingira ya Ndani, Zuhura Mawona wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akipokea LEO vifaa vya kutoa huduma kwa watoto wadogo kutoka kwa Mratibu wa Global Health Alliance, Sally Dawit.
Vifaa vya kutoa huduma kwa watoto wadogo vikiwa kwenye toroli maalumu la kuhifadhia katika hospitali hiyo.
Kushoto ni Mkuu wa Uuguzi na Mazingira ya Ndani, Zuhura Mawona wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akipokea LEO vifaa vya kutoa huduma kwa watoto wadogo kutoka kwa Mratibu wa Global Health Alliance, Sally Dawit.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Tutangaze vivutio vya kiutamaduni: Prof. Elisante Ole Gabriel

$
0
0

Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw Hassan Bendeyeko akifungua kikao kati ya wadau wa Sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Wizara husika kilichofanyika Mjini Songea Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Afisa Elimu MkoaBw.Gharama KinderuKatibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo akisikiliza maelezo ya baadhi ya vifaa vilivyotumika katika vita ya Majimaji kutoka kwa Afisa Elimu Makumbusho ya Taifa Bi. Blantina Raphael wakati alipotembelea makumbusho hayo mjini Songea, katikati ni Afisa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Gharama Kinderu. picha na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma

Na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel ametoa wito kwa viongozi na wadau wa sekta ya Utamaduni wa Mkoa wa Ruvuma kutangaza Utamaduni na Utalii unaopatikana katika mkoa huo.

Wito huo umetolewa jana mjini Songea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokuwa akizungumza na wadau wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika ofisi za mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

“Mkoa wenu una vivutio vingi vya asili vinavyoonesha tamaduni za wanaruvuma ambavyo vikitumika vizuri ni fursa nzuri ya mapato” alisema Prof Gabriel.Ameongeza kuwa Mkoa wa Ruvuma una vivutio vingi vya Utamaduni vya kuvutia watalii ambavyo ni fursa nzuri ya kutangaza Utamaduni wa Mkoa na Tanzania kwa ujumla.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Hassan Bendeyeko alikiri kuwepo kwa changamoto ya kuvitangaza vivutio hivyo kutokana na ubovu wa miundombinu iliyopo .Hata hivyo alisema kuwa ujenzi wa miundombinu utasaidia vivutio hivyo kufikika kwa urahisi na wanategemea Mkoa huo kuinuka kiuchumi hasa baada ya changamoto hiyo kutatuliwa.

Bw.Bendeyeko alisema kuwa baadhi ya vivutio vya kiutamaduni vinavyo hitaji kutangazwa ili vifahamike ndani na nje ya nchi ni pamoja na Makumbusho ya Majimaji, eneo waliponyongwa wapiganaji wa vita vya majimaji, Ziwa Nyasa pamoja na mbuga mbali mbali.

Aidha alieleza kuwa wanatarajia kuajiri Maafisa Utamaduni wakutosha katika kila Halmashauri ambapo kwa kushirikiana na Maafisa Habari na waandishi wa habari kutangaza vivutio hivyo.

TIMU YA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA YAIADHIBU TIMU MGODI WA BUZWAGI.

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Vita Kawawa aliyekuwa mgeni rasmi katika mchezo huo akikabidhi kombe kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kahama,Anderson Msumba aliyeongozana na nahodha wa timu ya Hospitali ya wilaya ya Kahama. 
 Wachezaji wa timu ya soka ya Hospitali ya wilaya ya Kahama wakifurahia mara baada ya kukabidhiwa kombe ilipoichapa timu ya Mgodi wa Buzwagi mabao 2 kwa 1. 
 Wachezaji wa timu ya Mgodi wa Buzwagi wakisalimiana na viongozi mara baada ya kumalizika kwa mcheoz wa kirafiki ambapo timu ya Hospitali wilaya ya Kahama iliibuka na ushindi wa bao 2 kwa 1 . 
 Baadhii ya wananchi wakifuatilia zoezi la utoaji kombe kwa washindi hao.Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog Kanda ya Kaskazini.

MNUFAIKA WA AIRTEL FURSA AMPATIA ZAWADI MKURUGENZI MKUU WA AIRTEL

$
0
0
Kupitia mradi wa Airtel fursa ambao umekuwa ukitoa msaada mbalimbali kwa vijana nchini kwa kuwawezesha kufanikisha ndoto zao mmoja kati ya kijana anaejihusisha na ubunifu wa sanaa za uchoraji aliyenufaika na mradi huo Bi Theresia Maliatabu leo amemtembelea mkurugenzi mkuu wa Airtel na kumkabidhi picha yake aliyoichora mara tu airtel Fursa kumpatia Kijana huyo vifaa vya kidigital katika semina iliyofanyika miezi miwili iliyopita na kuchagua vijana wawili walioweza kuwezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi katika semina hiyo kwaajili ya kuboresha ubunifu wao.

Akikabidhi zawadi hiyo Theresia alisema” vifaa hivyo vinanisaidia kubuni baadhi ya michoro ambayo ni ya kisasa zaidi, lakini hasa inanisaidia mazoezi katika kuchora na vile vile inanisaida kama sehemu ya kutangaza biashara yangu kupitia social media”.

“Napenda kuwaambia vijana wenzangu kwamba wajiamini na vipaji walivyokuwa nazo wasikate tamaa kwani kila kitu kinawezekana na wasiache kuchangamkia fursa kama hizi zinapojitokeza, aliongeza Theresia

Mpaka sasa Airtel imefanya semina nyingi sana za mafunzo ya biashara ya ujasiriamli hapa nchini katika mikoa mbali mbali na kuweza kufikia vijana wapatao 4000. Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA utaendelea kutoa warsha hizi katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuhakikisha inafikia vijana wengi zaidi. Vijana wanahamasishwa wanaposikia nafasi kama hii popote walipo , kuchangamkia kwa kuhudhuria kwani elimu inayotolewa ni bure kabisa bila gharama yoyote.
Kijana mjasiriamali Theresia Maliatabu (Kulia) akimkabidhi picha aliyoichora kwa ubunifu wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sunil Colaso (Kushoto) kama shukrani yake kwa Airtel baada ya kuwezeshwa kupitia mpango wa Airtel FURSA "Tunakuwezesha" kwa kupatiwa vifaa vya kuboresha biashara yake, akishuhudiwa na Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (katikati). Makabidhiano hayo yalifanyika mbele ya mkutano wa mwezi wa wafanyakazi Airtel uliyofanyika katika ofisi za Airtel Makao makuu morocco jijini Dar es salaam.
Kijana Theresia Maliatabu mmoja kati ya kijana anaejihusisha na ubunifu wa sanaa za uchoraji aliyenufaika na mpango wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” akiongea na wafanyakazi wa Airtel (hawapo pichani ) alipofika kwenye ofisi za Airtel makao makuu kukabidhi picha yake aliyoichora baada ya airtel Fursa kumpatia Kijana huyo vifaa vya kidigital katika semina iliyofanyika miezi miwili iliyopita na kuchagua vijana wawili walioweza kuwezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi katika semina hiyo kwa ajili ya kuboresha kazi zao.

Tanzania – Uganda zajadili upatikanaji ardhi – Bomba la Mafuta

$
0
0
Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, 
Mhandisi Norbert Kahyoza.
Na Rhoda James

Imeelezwa kuwa uelewa juu ya upatikanaji wa ardhi, Ushiriki wa wananchi na ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaohamishwa ili kupisha mradi wa bomba la mafuta litakalo jengwa kutoka kabaale nchini Uganda hadi Tanga Tanzania vitachangia katika kufanikisha zoezi la upatikanaji wa ardhi na kukamilisha shughuli za kimazingira kwa ajili ya ujenzi wa bomba hilo.

Hayo yameelezwa hivi karibuni mjini Dar es Salaam na Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Norbert Kahyoza wakati wa Warsha iliyolenga kujadili upatikanaji wa ardhi na kutathimini athari za Mazingira (EIA) ya ujenzi wa bomba hilo la mafuta kwa serikali ya Tanzania na Uganda.

“Serikali kutoka pande zote mbili lazima tuwe makini kuhusu upatikanaji wa ardhi, lazima wananchi wapate uelewa mzuri na waone uwepo wa umuhimu wa bomba hili la mafuta na faidi zake kwani mradi huu ni muhimu.” alisema mhandisi Kahyoza.

Aidha, Mkurugenzi wa Mkondo wa Chini kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. Wellington Hudson alieleza kuwa warsha hiyo ya upatikanaji wa ardhi pamoja na masuala ya mazingira ni ishara nzuri ya mwanzo katika utekelezaji wa mradi huo wa bomba la mafuta.

Vile vile mwakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini ya Uganda, Francis Elungat alisema kuwa Waganda wamekuwa wakijiuliza ni lini watafaidika na mafuta yao, hivyo amefurahishwa kuona kuwa mradi huo uko mbioni kuanza hivyo wananchi wa Uganda kufaidika na mafuta yao.
Ujumbe kutoka Uganda wakifuatilia Mada zilizowasilishwa katika kikao cha wadau wa mafuta, kutoka kulia ni afisa Mwandamizi wa Mazingira, Jane Byaruhanga, wa pili ni afisa Mwandamizi wa Ardhi, Francis Elungat na afisa mwandamizi wa Ardhi Denis Karamagi.

Mchakato wa upatikanaji wa ardhi na kushugulikia masuala ya mazingira ni hatua za awali za safari ya wananchi wa Uganda kupata faida za mali asilia inchini mwao.

Aliongeza kuwa ujenzi wa bomba la mafuta na kiwanda cha kuchakata mafuta hayo ni muhimu sana kwa wananchi wa Uganda na nchi nyingine za Afrika Mashariki hivyo ni vema pande zote mbili zikubaliana katika hatua zote za utekelezaji wa mradi huo.

Naye Meneja wa Mradi wa Kampuni ya Total Uganda, Jean Luc Bruggeman, alisema kuwa ni lazima kuwepo na maelewano ya pamoja kwa pande zote mbili juu ya nini kinahitajika na taratibu za upatikanaji wa cheti cha mazingira (EIA) ili kuwezesha kuanza shughuli za ujenzi wa mradi mapema, na kinachotarajiwa kufanyika kulingana na makubaliano ya nchi hizo mbili na kuelewana nani atafanya nini katika mradi huo.
Wajumbe wakifuatilia mada katika kikao cha wadau wa Bomba la mafuta kilichofanyika katika hotel ya New Africa jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo ilihudhuriwa na Ujumbe kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Uganda, Kampuni ya Total E&P Uganda, wajumbe kutoka Halmashauri ya Tanga, Bandari ya Tanga na Dar es Salaam, Shirika la Reli Tanzania, Wizara ya Fedha, Wizara ya Ardhi, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),Chuo cha Ardhi, Tanroads, Ofisi ya Mwanasheria Mkuuna Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania.

MSANII DIAMOND PLATINUMZ AZINDUA LEBO YAKE YA WBC NA KUSAINI NA MKATABA NA MSANII RICH MAVOKO.

$
0
0
 Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Diamond Platnumz (wa pili kushoto) akiwatangaza wasanii wanaosimamiwa na lebo ya ‘WCB Record Label’ ambayo ameizindua leo ndani ya hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza pamoja na mameneja wake Hamis Tale na Mkubwa Fela. Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Msanii Queen Darleen, Raymond na Hamonize. 
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Diamond Platnumz akisaini mkataba wa kufanya kazi na msanii Rich Mavoko huku Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza akishuhudia tukio hilo. Nyuma ni uongozi wa WCB na msanii Diamond.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Diamond Platnumz akibadilishana mkataba na Rich Mavoko mara baada ya kusaini huku Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza akishuhudia tukio hilo.

MSANII wa Muziki wa Kizazi kipya, Diamond Platnumz  amezindua rasmi Lebo ya muziki ‘WCB Record Label’  na kuwatangaza wasanii wanaosimamiwa na lebo hiyo huku msanii Rich Mavoko akisaini mkataba wa kufanya kazi na Lebo hiyo katika Hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam. 

WCB inakuwa ni lebo ya kwanza nchini Tanzania kuanzishwa na kusimamiwa na mwanamuziki, ikilinganishwa na lebo kadhaa ambazo zilikuwa zikisimamiwa na wadau waliokuwa katika tasnia ya sanaa na burudani.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu WCB, Diamond Platinumz alisema lengo la kuanzishwa lebo hiyo ni kusaidia vijana wenye vipaji na kuifanya sanaa ya muziki izalishe pato la taifa.

Msanii Diamond ameomba serikali kuwaunga mkono ili waweze kusonga mbele maana kwa sasa amekuwa na watu kadhaa ambao wamekuwa wakimtegemea katika kufanya sanaa ya muziki.

STAMICO YATAKIWA KUSHIKIRIA UCHUMI -PROFESA NTALIKWA.

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara  ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa ( wa tatu kutoka kushoto waliokaa mbele) Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini  Prof James Mdoe ( wa pili kutoka kushoto waliokaa mbele)  wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya  Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO) mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi  huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa (mbele) akiongoza kikao cha uzinduzi wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Prof James Mdoe, akielezea historia ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SHIRIKA la Madini la Taifa (Stamico) limetakiwa kushirikiria uchumi wa nchi kutokana na  ubia uliopo kati ya Wabia na Serikali.

Hayo ameyasema  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa,  Justin Ntalikwa wakati wa uzinduzi bodi mpya ya Stamico , amesema kuwa mashirika mengi ya serikali yanayosimamia madini ndiyo yamekuwa yakishikiria uchumi wa nchi.

Amesema bodi inawajibu kuhakikisha stamico inabadilika  kutokana na  miradi iliyo chini yake inaendelezwa  na kusimamiwa ipasavyo  ili kuipatia serikali manufaa mbalimbali ikiwemo gawio  katika migodi ya ubia.

Profesa Ntalikwa amesema kuwa bodi katika kufanya kazi zake moja ni kufanya usaili wa wafanyakazi kutokana nafasi nyingi ikiwemo ya mkurugenzi mtendaji  kukaimiwa  na zingine.

Aidha amesema kuwa ina wajibu wa kuboresha mikataba iliyopo kwa kukaa na wabia ili pande zote ziweze kunufaika na manufaa yatokanayo na miradi ya uwekezaji katika sekta ya madini.

Bodi hiyo iliyoteuliwa hivi karibuni na  Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo  inaundwa na wajumbe watano ambao ni pamoja na Abdalah  Mussa, Dkt. Coretha Komba, Felix  Maagi, Dkt. Lightness Mnzava, John  Seka chini ya Mwenyekiti wake  Balozi  Alexander Muganda.

Zaidi ya Bilioni 4 kutumika kuwezesha wajasiriamali Kinondoni

$
0
0
Afisa uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Sebastian Mhowera akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mikakati ya Manispaa hiyo kuwawezesha wanawake na vijana kupitia mfuko maalum ulioanzishwa na Serikali ili kutoa mikopo kwa wajasiriamali hao ili kuwajengea uwezo kushiriki kujenga uchumi.kulia nia Afisa Uhusiano wa Manispaa hiyo Bw.Bornwell Kapinga.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia Mkutano wa Manispaa ya Kinondoni uliofanyika leo Jijini Dar es salaam ukilenga kutoa taarifa kwa wajasiriamali wa manispaa hiyo juu ya namna wanavyoweza kujiunga katika vikundi na hivyo kunufaika na Mikopo inayotolewa kupitia Mfuko wa Kuwawezesha Wanawake na Vijana.( Picha na MAELEZO).


Frank Mvungi-Maelezo

Serikali kutumia zaidi ya bilioni 4 kuwawezesha wajasiriamali wadogo katika Manispaa ya Kinondoni katika Kipindi cha mwaka 2016/2017 ili kuchochea kasi ya ukuachi wa uchumi.Kauli hiyo imetolewa Leo Jijini Dar es salaam na Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Sebvastian Mhowera wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.

Akifafanua Mhowera amesema fedha hizo zitatolewa kupitia Mfuko wa wanawake na Vijana unaolenga kuwawezesha kishiriki katika shughuli za uzalishaji hali itakayachangia kukuza uchumi.Kwa Sasa manispaa ya Kinondoni inajumla ya Vikundi 546 vya wanawake na vijana vyenye jumla ya wajasiriamali 2729 ikilinganishwa na vikundi 40 na wanufaika 200 waliokuwepo mwaka 2013.

Wajasiriamali wanaonufaika na fedha za mfuko huo ni wale wanajishughuisha na shughuli za Kiuchumi kiwemo kilimo,Biasharandogondogo,Ushonaji,Ufugaji,Uvuvi,Mafundi seremala,wasusi.Pia Mhowera alitoa wito kwa wajasiriamali wa Wilaya ya Kinondoni kujitokeza kuchangamkia fursa zinazotokana na mfuko wa wanawake na vijana.

Kuanzishwa kwa mfuko huu katika manispaa ya Kinondoni ni utekelezaji wa agizo la Serikali Kuu lililoagiza Halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya mfuko wa kuwawezesha wanawake na vijana.Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inaandaa maonesho kwa ajili ya wajasiriamali wadowadogo wanaonufaika na Mikopo ya Mfuko wa wanawake na vijana inayotolewa na Manispaa hiyo ambapo maonesho hayo yatafanyika mwishoni mwa wiki ijayo.

NSSF yashauriwa kusaidia wasanii.

$
0
0
Meneja wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Ruvuma Bw. Felix Wisso.

Na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii( NSSF) Mkoa wa Ruvuma limeshauriwa kuinua maisha ya wasanii kwa kuwaunganisha na mfuko huo ili kuhakikisha maisha ya wasanii yanaboreshwa.

Akizungumza katika kikao kati ya wadau wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Wizara, Katibu Mkuu wa Wizara Wizara hiyo Prof Elisante Ole Gabriel amesema kuwa mfuko huo uangalie namna ya kukusanya wasanii na kuwaweka pamoja ili waweze kujiunga.

“kwa upande wa wasanii wao ni jeshi kubwa tutafute namana ya kuwasajili kama wanachama rasmi wa NSSF ili waweza kutambulika katika ajira rasmi” alisema Prof Gabriel.

Prof Gabriel alisema kuwa wasanii wanachangamoto nyingi zinazo wakabili ambazo zinarudisha nyuma kada yao moja wapo ikiwa ni hiyo ya kutokuwa wanachama wa mifuko ya Jamii.

Kwa upande wake Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma Bw. Felix Wisso amesema lengo la mfuko huo ni kudumisha maisha ya watanzania walio katika sekta zote hivyo basi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkoa wanaangalia namna ya kuwainua wasanii hao kupitia mikopo itolewayo na mfuko huo.

Ameongeza kuwa shirika lake limejipanga kikamilifu kuendana na kasi ya utendaji wa Serikali ya awamu ya tano hivyo basi elimu ya kujiunga na mfuko huo itaendelea kutolewa kwa wananchi .

“Wasanii wanaweza kuitangaza nchi yetu vizuri sana kama tu jamii itaamua kuwatambua na sanaa ikawa ni ajira kamili kama ajira nyingine.”Alisema Bw. WissoAidha aliwasisitiza viongozi wa wasanii pamoja na Maafisa Utamaduni kuwahamasisha wadau wao kuingia katika mfuko huo wa jamii kwani ni dhamana ya maisha yao.

Taarifa kuhusu Usimamizi wa Miradi ya TEHAMA Serikalini

eGA yataka Taasisi Mbalimbali kutekeleza Miradi ya TEHAMA.

$
0
0
Meneja habari, elimu na Mawasiliano wa Wakala wa Serikali Mtandao(eGA) Bibi. Suzan Mshakangoto akiongea na waandishi wa habari na wafanyakazi wa taasisi hiyo hawapo pichani kuhusu ushiriki wa Taasisi za kiserikali katika kupanga na kutekeleza miradi ya TEHAMA Serikalini uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Meneja habari, elimu na Mawasiliano wa Wakala wa Serikali Mtandao(eGA) Bibi. Suzan Mshakangoto katikati akiongea na waandishi wa habari na wafanyakazi wa taasisi hiyo kuhusu ushiriki wa Taasisi za kiserikali katika kupanga na kutekeleza miradi ya TEHAMA Serikalini uliofanyika leo jijini Dar es salaam.Picha zote na Ally Daud-Maelezo

Na: Frank Shija, MAELEZO

02/06/2016

Ofisi naTaasisi za umma zashauriwa kushirikiana naWakala wa Serikali Mtandao (eGA) katika kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya Tehama.Ushauri huo umetolewa na Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Bibi. Suzan Mshakangoto wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Bi. Mshakangoto amebainisha kuwa kumekuwapo na changamoto ya Taasisi za umma kuanzisha miradi ya TEHAMA inayofanana huku zikiwa na taarifa zinazokinzana na kuisababishia gharama zisizo za lazima Serikali.Aidha alisema kuwa ili kujiridhisha na miradi ya TEHAMA Wakala hiyo imeweka vigezo katika Orodha hakiki ya miradi ya TEHAMA Serikalini, inayopatikana katika tovuti ya Wakala ili uweze kuhakikiwa na kuthibitishwa. 

“Kutokana na utaratibu huo kuleta changamoto mbalimbali,taasisi yeyote ya umma inatakiwa kuwasilisha mradi wake kwaWakalaya Serikali Mtandao ukiwa unaendana na vigezo vilivyowekwa katika orodha ya miradi ya TEHAMA Serikalini inayopatikana katika tovuti ya wakala ambayo ni www.ega.go.tz” AlisemaBi. Suzan.

Changamoto zinazojitokeza kutokana na utaratibu huo ni pamoja na kutofautiana kwa taarifa ya aina moja kutoka taasisi tofauti akitolea mfano wa Rita wanaweza kuwa na Jina la Juma Hassan na mtu yulelyule ukienda Bima ya Afya anaitwa Juma Kassim Hassan.Kutokana na mkanganyiko huo na Wakala inashauri na kuzitaka taasisi zote za Serikali kuwasilisha andiko la miradi yao ya Tehama kwa Wakala ya Serikali Mtandao ili kuhakikiwa kama zinakidhi vigezo, malengo na dira ya maendeleo ya Serikali ya mwaka 2025 na kama mradi huo niendelevu. 

Aidha wito umetolewa kwa wafanyabiashara wanaojihusisha na miradi au utengenezaji wa mifumo ya Tehama Serikalini kujiridhisha kama miradi waliyokusudi kuitekeleza inakidhi vigezo vya kuanzisha miradi ya TEHAMA kama vilivyoainishwa katika orodha ya miradi ya Tehama Serikalini.

Wakala wa Serikali Mtandao (eGA) ni taasisi ya Serikali kwa mamlaka iliyonayo kisheria inawajibika kusimamia na kuratibu masuala yote yanayohusu Serikali Mtandao hivyo ni wajibu wake inapoona mambo yanaenda kinyume na taratibu na miongozo ya usimamizi wa miradi ya Tehama Serikalini.

Walioficha sukari ardhi iwakatae-Dkt. Charles Gadi

$
0
0

Na: Lilian Lundo – MAELEZO

Askofu wa Kanisa la Good News for All Ministry Dkt. Charles Gadi amewapa siku tatu walioficha sukari kuitoa na ikiwa watakaidi agizo hilo basi ardhi iwakatae.

Askofu Gadi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya uhaba wa sukari nchini na maandalizi ya mkutano wa kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakaofanyika jiji la Arusha.

“Tanzania haina tatizo la sukari bali sukari ziko kwenye maghala, wafanyabiashara wamezificha ili waje kuuza kwa bei ya juu. Tunamuomba Mungu ili watu hao ardhi iwakatae ikiwa hawatatoa sukari ndani ya siku ya tatu,”alisema Askofu huyo.

Pia, Askofu Gadi ametoa wito kwa wafanyabiashara kuacha tabia ya kuficha sukari na wakumbuke kuwa waislam wapo katika maandalizi ya kutimiza nguzo muhimu ya imani ya dini yao ambapo wataanza mwezi wa Ramadhani na watahitaji sukari kwa ajili ya kuandaa futari.

Vile vile Askofu huyo ameiomba Serikali kuagiza sukari kwa wingi ili waumini wa dini ya Kiislam waweze kutimiza kwa urahisi nguzo ya mwezi wa Ramadhani.Aidha, akizungumzia juu ya mkutano wa maombi utakaofanyika jiji la Arusha, Askofu Gadi amesema kuwa mkutano huo ni maalum kwa ajili ya kumuombe Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili aweze kufanikiwa katika nia yake ya kujenga upya uchumi, uadilifu na ustawi wa Tanzania.

Mkutano huo unategemewa kufanyika siku ya Jumatano Juni 08, 2016 kuanzia 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni viwanja vya relini, ambao umeandaliwa na Kanisa la Good News for All Ministry kwa kushirikiana na Umoja wa Makanisa ya Arusha.

YALIYOJIRI NDANI NA NJE YA UKUMBI WA BUNGE LEO MJINI DODOMA JUNI 3, 2016.

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akichangia jambo wakati wa kikao cha 35 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.
Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni akijibu maswali ya wabunge wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni Dodoma.
Baadhi ya Wabunge na Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha 35 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson (kulia) akisalimiana na Meneja wa VETA mkoa wa Iringa Bw. Maganga nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.Katikati ni Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson (kulia) akizungumza jambo na Meneja wa VETA mkoa wa Iringa Bw. Maganga (kushoto) na Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Mchezaji wa kulipwa wa mpira wa kikapu nchini Marekani kutoka Tanzania Hasheem Thabeet (kushoto) akifurahia jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju (wa pili kutoka kushoto) na baadhi ya Wabunge nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Haki , Maadili na Madaraka ya Bunge na Mbunge wa Newala Mhe. George Mkuchika (katikati) akizungumza jambo na Mbunge wa Iringa Mjini Mhe. Peter Msigwa nje ya Ukumbi wa Bunge Dodoma.Kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsisitiza jambo Meneja wa VETA mkoa wa Iringa Bw. Maganga nje ya Ukumbi wa Bunge Dodoma.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzania Bungeni Mhe. Freeman Mbowe akifurahia jambo na Mbunge wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde nje ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma.
Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Venance Mwamoto (wa pili kutoka kulia), , Mhe. Livingstone Lusinde (wa tatu kutoka kulia) na Mhe. Joseph Kasheku Msukuma ( pili kutoka kushoto)wakifurahia jambo na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe nje ya Ukumbi wa Bunge leo.
Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto (wa pili kutoka kulia), Mbunge wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde (wa tatu kutoka kulia) na Mbunge wa Geita vijijini Mhe. Joseph Kasheku Msukuma ( pili kutoka kushoto)wakimweleza jambo Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe nje ya Ukumbi wa Bunge leo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Kulia) akizungumza jambo na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni leo mjini Dodoma.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto), Mhe. Margaret Sitta Mbunge wa Urambo (katikati) na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakielekea ndani ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma leo.
Baadhi ya Waheshimiwa wabunge wakiingia ndani ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Waheshimiwa wabunge wakiingia ndani ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson akiendesha kikao cha 35 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
Mchezaji wa kulipwa wa mpira wa kikapu nchini Marekani kutoka Tanzania Hasheem Thabeet (kulia) akiwa na baadhi ya wageni mbalimbali waliolitembelea Bunge leo.Picha na Aron Msigwa na Fatma Salum–MAELEZO, DODOMA.

MAMA MAGUFULI AMSHUKURU NABII TB JOSHUA

TAMKO LA MH. WAZIRI JANUARY MAKAMBA KUHUSU SHUGHULI ZINAZOHITAJI KUFANYIWA TATHMINI YA ATHARI KWA MAZINGIRA (TAM)

$
0
0
TAMKO LA MHE. JANUARY Y. MAKAMBA (MB), WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA) KUHUSU SHUGHULI ZINAZOTAKIWA KUFANYIWA TATHMINI YA ATHARI KWA MAZINGIRA (ENVIRONMENTAL IMPACT ASSESSMENT)
TAREHE 2 JUNI, 2016


Ndugu Wananchi;

Katika ulimwengu wa sasa si rahisi kutenganisha mazingira na maendeleo. Ni wazi kuwa ufumbuzi wa matatizo ya uharibifu wa mazingira huwa mgumu kwa sababu chanzo chake kimo katika mifumo ya uendeshaji wa shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii yenye manufaa kwa uhai na ustawi wa binadamu. Shughuli zinazosababisha uharibifu wa mazingira ndizo hizo zinazomwezesha mwanadamu kuishi na kujiendeleza. 

Hali ya mazingira inahusika sana na kuboresha “mazingira” ya vitega uchumi na kuinua kiwango cha maisha ya wananchi. Na kwa kweli, maliasili ya mazingira ndio msingi wa maisha na maendeleo ya Watanzania. Kwa mantiki hii, inabidi kutazama mambo mengi yanayochangia katika uharibifu wa mazingira; kutambua matatizo ya mazingira katika undani wa shughuli mbalimbali za maendeleo; kutambua sababu na kupima athari zake, na kubuni mbinu au kuchukua tahadhari za kudhibiti au kuzuia uharibifu huo bila kusimamisha wala kupunguza kasi ya shughuli za maendeleo. 

Ni kwa sababu hii serikali imepitisha sera na sheria za sekta mbalimbali zinazogusa mazingira na imebuni programu na miradi mingi ya utekelezaji, katika kuhakikisha haya yanafanyika. 

Ndugu Wananchi;

Kama mnavyofahamu, Ofisi ya Makamu wa Rais inasimamia utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (SURA YA 191), pamoja na Kanuni zake. Sheria hii ndiyo Sheria mama ya masuala yote yanayohusu mazingira kwani Sheria hii inatekelezwa kwa kuzingatia sheria mbalimbali za kisekta ikizingatiwa kwamba suala la mazingira ni suala mtambuka. 

Sehemu ya Sita ya Sheria hii yenye kifungu cha 81 hadi cha 103 inaelekeza kila shughuli ya maendeleo ifanyiwe Tathimini ya Athari kwa Mazingira na inatoa ufafanuzi wa hatua za kufuata.

Kifungu cha 81(1) kimeweka wajibu wa kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na kubainisha katika Jedwali la Tatu la Sheria.

Ndugu Wananchi;

Kimsingi mambo hayo yaliyotajwa  katika Jedwali la Tatu la Sheria ni ya jumla. Melezo ya kina yametolewa katika Kanuni za Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Ukaguzi za mwaka 2005. Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi  limebainisha orodha ya  miradi ambayo inatakiwa kufanyiwa tathmini kabla ya kuanza utekelezaji wake. Orodha hii imegawanyika katika makundi mawili (2). Kundi la kwanza, yaani (A), ni la miradi ambayo  lazima ifanyiwe Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwani ni miradi ambayo inaonekana kuwa utekelezaji wake unaweza kuwa na athari kubwa kwa mazingira, hivyo utafiti wa kina unahitajika ili kubaini ukubwa wa athari na kupendekeza hatua mahsusi za kuepusha athari hizo.


Kundi la pili, yaani (B), ni miradi ambayo inaonyesha kuwa utekelezaji wake unaweza kuwa na athari kwa mazingira ingawa athari zake zinaweza kuwa ni ndogo ukilinganisha na miradi iliyotajwa katika Kundi A. Miradi hii inatakiwa kufanyiwa Tathmini ya Awali ya Mazingira (Preliminary Environmental Assessment) ili kuweza kuamua kama miradi hii inaweza kuendelea bila kufanyiwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (full Environmental Impact Assessment). Hivyo kulingana na matokeo yatakayopatikana katika Tathmini hiyo ya awali miradi iliyoko katika kundi hili inaweza kuendelea bila kufanyiwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira au kufanyiwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira.


Shughuli au miradi inayohusika katika Kundi A, ambayo ni lazima ifanyiwe Tathmini ya Athari kwa Mazingira, ni kama ifuatavyo:-

·        Shughuli za kilimo: kilimo cha mashamba makubwa, miradi ya kilimo inayohitaji kuhamisha makazi ya wanavijiji, uanzishwaji wa matumizi ya mbegu mpya za mazao, uingizaji wa viumbe ambavyo vinasaba vyake vimefanyiwa mabadiliko ya kijenetiki n.k;

·        Usimamizi wa mifugo na maeneo ya malisho: uswagaji wa mifugo mingi, kuingizwa kwa spishi mpya au za kigeni;

·        Shughuli za misitu: ukataji wa mbao na utayarishaji, ujenzi wa barabara ndani ya misitu ya hifadhi, biashara ya mkaa, kuni na shughuli nyinginezo za uvunaji wa misitu, na kuanzisha biashara ya magogo au kubadilisha matumizi ya ardhi ya misitu kwa matumizi mengine kwenye vyanzo vya maji;

·        Shughuli za uvuvi: uvuvi wa kati na mkubwa, ufugaji mkubwa wa samaki pamoja na ufugaji wa kamba, uzalishaji na hifadhi ya minofu ya samaki viwandani;

·        Shughuli zinazohusiana na  wanyamapori: ukamataji wa wanyamapori na biashara ya wanyamapori, kuanzishwa kwa maeneo ya uwindaji yanayohusisha uhamishaji wa makazi ya vijiji,  ranchi ya wanyamapori na ufugaji na bustani na hifadhi za wanyapori;

·        Shughuli za utalii na burudani: ujenzi wa maeneo ya kutembelea au hoteli pembezoni mwa fukwe za maziwa na bahari, kingo za mito na visiwani; huduma za utalii na burudani katika maeneo yanayolindwa na maeneo yanayozunguka (mbuga za wanyama, bustani za majini, hifadhi za misitu) kwenye visiwa na maeneo yanayozunguka maji, ujenzi mkubwa kwa ajili ya michezo na burudani;

·        Shughuli za madini: uzalishaji na usambazaji wa umeme, gesi, utunzaji wa gesi asili, umeme wa maji, ujenzi wa miradi mikubwa ya nishati jadidifu na isiyo jadidifu;

·        Bidhaa za petroli: Utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi, ujenzi wa mitambo ya kuzalisha mafuta na gesi, ujenzi au upanuzi wa ghala la kuhifadhia petroli, gesi, diseli, lami ndani ya maeneo ya biashara, viwanda na makazi ya watu, usafirishaji wa bidhaa za petroli;

·        Usafiri na mindombinu: ujenzi, upanuzi au ukarabati wa barabara, viwanja vya ndege, reli na eneo la kutengeneza meli au miundombinu ya bandari

·        Shughuli za chakula  na vinywaji: utengenezaji wa mafuta yatokanayo na mimea na wanyama, machinjio, usindikaji wa tumbaku;

·        Viwanda vya nguo, ngozi, mbao, kemikali;

·        Shughuli za usafishaji na utupaji taka: ujenzi wa mitambo ya uteketezaji taka, mtambo wa kuhudumia maji taka;

·        Shughuli za usambazaji maji: na

·        Shughuli za mipangoya maendeleo ya ardhi, nyumba na makazi: kuanzisha makazi mapya ya watu na wanyama, miradi mikubwa ya mijini (ujenzi wa magorofa, vituo vya magari, masoko n,k), ujazaji wa ardhi ikiwa ni pamoja na ardhi chini ya maji.


Aidha shughuli zilizotajwa katika Kundi (B), ambazo ni lazima kufanyiwa Tathmini ya Awali ya Mazingira (Preliminary Environmental Assessment) ni hizi zifutazo:-

·        Ufugaji wa samaki;

·        Ufugaji wa mifugo midogo wa mjini;

·        Ukulima wa mboga na maua;

·        Uzalishaji wa mkaa;

·        Utegaji wa ndege na biashara ya ndege pori;

·        Bustani za wanyama pori na ndege;

·        Kilimo cha mjini; na

·        Utengenezaji wa vigae.


Ndugu Wananchi;

Shughuli au miradi iliyoelezwa hapo juu imetajwa kwa ufupi kwa kuwa ni vigumu kuandika vipengele vyote vilivyotajwa kwenye Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 pamoja na Kanuni zake kwa kuwa ni vingi mno. Hivyo, natoa wito kwa watu wote wanaotaka kuwekeza katika shughuli yoyote kuitafuta, kuisoma na kuielewa Sheria hii pamoja na Kanuni zake ili kuweza kuitekeleza kwa ukamilifu.


Ndugu Wananchi;

Mtakumbuka tarehe 29 Mei, 2016 wakati nikitoa Tamko kuhusu  maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani kwa mwaka huu nilieleza wazi kuwa Serikali imetoa miezi miwili, hadi ifikapo tarehe 1 Agosti 2016 kwa wale wote ambao hawana Vyeti vya Tathmini ya Athari kwa Mazingira katika shughuli zao  waende Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanyiwa Ukaguzi wa Mazingira (Environmental Audit).


Napenda kutoa wito kwa mara nyingine kwa wale wote wanaofanya shughuli zilizoorodheshwa katika Kundi A na B katika Jedwali la Tatu la Sheria ya Mazingira kuhakikisha kuwa wanatembelea Ofisi za NEMC mara moja ili kuweza kupata utaratibu kamili wa kuwezesha shughuli zao kufanyiwa Ukaguzi wa Mazingira. Niseme tu wazi kuwa baada ya muda uliotajwa hapo juu kuisha hatutakuwa na uvumilivu kwa mtu yeyote ambaye atashindwa kutekeleza agizo hili. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa, ikiwemo kuzifungia shughuli hizo, kwa wale wote watakaoshindwa kutii na kutekeleza agizo hili. Hatutakubali kisingizio cha kutoijua Sheria au kutojua mahitaji ya kufanyiwa Tathmini ya Athari ya Mazingira.


Wakati huo huo, Serikali inapanga utaratibu wa kurahisisha mchakato wa upatikanaji wa Vyeti vya Tathmini ya Athari kwa Mazingira ili upatikanaji wa vyeti hivyo usicheleweshe uwekezaji wa kibiashara au shughuli za maendeleo.



January Makamba (MB)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais

Muungano na Mazingira


2 Juni 2016

Maafisa Maendeleo ya Jamii Kuchochea ukuaji wa Uchumi

$
0
0
Frank Mvungi-Maelezo

Maafisa Maendeleo ya jamii walioajiriwa katika Halmashauri hapa nchini wameongezeka kutoka 1,855 mwaka 2005 hadi kufikia 2,675 ikiwa ni ongezeko la asilimia 44 hali inayosaidia kuboreshwa kwa huduma za jamii.

Kauli hiyo imetolewa Leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia vyuo vya Maendeleo ya Jamii Bi. Neema Ndoboka toka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake Wazee na Watoto wakati wa Mkutano na Vyombo vya Habari uliolenga kueleza mafanikio yaliyofikiwa na Wizara hiyo katika kukuza Sekta ya Maendeleo ya Jamii hapa nchini.

Akifafanua Ndomboka amesema kuwa chuo cha Maendeleo ya jamii Tengeru kimepandishwa hadhi kuwa Taasisi ya Elimu ya Juu inayotegemea kiutendaji hali itakayosaidia kuongeza kiwango wa Maafisa Maendeleo ya Jamii wanaohitimu katika chuo hicho.

Pia Ndomboka amesema kuwa vyuo vinavyosimamiwa na Wizara hiyo vinatoa wahitimu wanaokidhi mahitaji ya soko la ajira kutokana na umahiri na uzoefu wanaojengewa wakiwa vyuoni.

Aidha wahitimu wa Kidato cha nne na kidato cha sita wenye utashi katika fani ya maendeleo ya jamii wanakaribishwa kutuma maombi yao kwenye “Central Admission System” (CAS),kupitia www.nacte.go.tz.

Taaluma ya Maendeleo ya Jamii inatolewa kwa kuzingatia taratibu na Kanuni zinazotolewa na kusimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).hivyo NACTE inasimamia uandaaji wa mitaala inayotumika katika utoaji wa mafunzo,muda wa masomo,mitihani na Vigezo vyake,pamoja na ubora wav yeti wanavyotunukiwa wahitimu kwa kila ngazi.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images