Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 862 | 863 | (Page 864) | 865 | 866 | .... | 1897 | newer

  0 0


  0 0


  0 0

   Hatimaye mpiganaji   Goodchance Monyo na Atilia Magelanga wamefunga harusi katika kanisa la Mtakatifu Peter,Oysterbay jijini Dar hapo jana Mei 28 na baadaye tafrija murua kabisa ikafanyika katika ukumbi wa sabasaba
  Pichani ni Bwana harusi Goodchance Monyo akila kiapo cha ndoa mbele ya Mkewe Bi Atilia Magelanga na wageni waalikwa  mbalimbali waliofika kushuhudia tukio hilo adhimu katika maisha ya Mwanadamu,ndani ya kanisa la Mtakatifu Peter,Oysterbay jijini Dar.
   Bibi harusi akimvalisha pete bwana harusi ikiwa pia ni ishara ya upendo na wameishakuwa mwili mmoja 
    Bwana harusi akimvalisha pete bibi harusi kuashiria kuwa wameishakuwa mwili mmoja . 
   Goodchance Monyo na Atilia Magelanga wakiwa katika picha ya pamoja na mpiganaji Goodfrey Monyo mara baada ya ndoa kufungwa.  0 0


   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Siku ya Mazingira Duniani ambayo hudhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka.
    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Siku ya Mazingira Duniani ambayo hudhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mbarak Abdulwakil (kushoto) akifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba alipokuwa akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo hudhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na MazingiraNgosi Mwihava.
  (Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO.
  SERIKALI imeandaa mkakati mpya wa kitaifa wa kupanda na kutunza miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi hatua ambayo itarudisha hali ya mazingira kama yalivyokuwa awali miaka ya nyuma.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba alipokuwa akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Siku ya Mazingira Duniani ambayo hudhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka.

   “Mkakati huu mpya umezingatia kurekebisha changamoto zilizojitokeza katika kampeni za upandaji miti zilizofanyika katika vipindi mbalimbali tangu uhuru wan chi yetu” alisema Waziri Makamba.
  Ili kukabiliana na changamoto hizo, Waziri Makamba amesema kuwa Serikali kupitia Wizara yake imetenga kiasi cha Sh. bilioni 2 ikiwa kianzio kwa lengo la kusimamia mkakati huo katika mwaka wa fedha 2016/2017. 

  Katika kuhakikisha suala la mazingira limepewa kipaumbele, Mfuko wa Taifa wa Mazingira ambao ni mdau mkuu wa mazingira utatengewa vyanzo vya mapato yanayokadiriwa kufikia Sh. bilioni 100 ikiwa ni juhudi za kugharimia mpango huo na mipango mingine ya hifadhi ya mazingira.

  Mkakati huo ni wa miaka mitano ambao unaanza kutekelezwa 2016 hadi 2021 na unakadiriwa kugharimu kiasi cha Sh. bilioni 105.2. 

  Aidha, Waziri Makamba amebainisha kuwa masuala ambayo yatazingatiwa katika kutekeleza mpango huo ni pamoja na uhamasishaji na utoaji motisha kwa watumiaji wa nishati mbadala ili kuondoa matumizi ya kuni na mkaa.

  Ili kuhakikisha mazingira yameboreshwa na yawe rafiki kwa kila kiumbe, utekelezaji na usimamiaji wa mkakati huo, utaanza kutekelezwa kuanzia ngazi ya chini hadi juu ambapo kila kijiji, kitongoji, mtaa, kaya na kila taasisi itapewa lengo la pandaji miti kama msingi wa zoezi hilo.

  “Tutashindanisha shule na vijiji katika upandaji na ukuzaji wa miti na tutatoa zawadi nono na maeneo ya wazi ya Serikali yatapandwa miti” alisema Waziri Makamba.

  Katika kuhakikisha miti iliyopandwa inalindwa na kukua,  Ofisi ya Makamu wa Rais itashirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mkioa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha halmashauri zinatunga sheria ndogo ndogo za kuhimiza upandaji na utunzaji miti nchini.

  Maadhimisho ya mwaka huu Kimataifa yanafanyika nchini Angola ambayo yanalenga kupambana na biashara ya meno ya tembo na pembe za faru yakiongozwa na kaulimbiu “Tunza wanyama porini kwa maisha”
  Siku ya mazingira Duniani imeanza kuadhimishwa  mwaka 1972 ambapo Baraza la Umoja wa Mataifa lilifanya wa mkutano wake wa kwanza unaohusu mazingira uliofanyika Stockholm nchini Sweden na kuundwa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mazingira diniani (UNEP).

  0 0
 • 05/29/16--08:55: TTCL WAZINDUA NEMBO MPYA.
 • Baadhi ya maofisa waandamizi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakiwa katika picha ya pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (katikati) mara baada ya uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya TTCL pamoja na uzinduzi wa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya maofisa waandamizi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakiwa katika picha ya pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (katikati) mara baada ya uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya TTCL pamoja na uzinduzi wa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam.[/caption] KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imefanya mabadiliko ya nembo yake pamoja na kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE ikiwa ni muendelezo wa mpango wa kufanya mabadiliko ya kibiashara kwa kampuni hiyo. Nembo hiyo mpya ya TTCL na huduma ya 4G LTE vimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa huku akiipongeza kwa hatua hiyo ya kuleta mabadiliko ya kiutendaji na uwajibikaji unaolenga kuonesha tija na ubora. Waziri Mbarawa alisema uzinduzi huo ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli la kufanya kazi kwa bidii, maarifa, uadilifu na kufikia viwango vya juu kabisa vya kutoa huduma kwa umma sambamba na mpango mkakati wa TTCL kibiashara kwa kipindi cha mwaka 2016-2018. "Pamoja na pongezi hizi za dhati, naomba mtambue kuwa uzinduzi huu hautakuwa na maana yoyote pasipo mabadiliko ya kiutendaji utoaji huduma kwa wateja. Watumiaji wa huduma zenu wanahitaji mabadiliko ya dhati ya viwango vya huduma na utendaji ili kuwajengea imani juu ya uwezo wenu wa kuwahudumia," alisema Waziri Mbarawa. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akizinduwa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe akishiriki zoezi hilo. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akizinduwa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe akishiriki zoezi hilo.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akionesha nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) mara baada ya kuizindua. Kushoto ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe akishiriki zoezi hilo. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akionesha nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) mara baada ya kuizindua.
  Kushoto ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe akishiriki zoezi hilo.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akimpongeza, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (kushoto) mara baada ya uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya TTCL pamoja na uzinduzi wa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akimpongeza, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (kushoto) mara baada ya uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya TTCL pamoja na uzinduzi wa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, katika hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam.  Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, katika hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam.Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Edwina Lupembe akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam. Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Edwina Lupembe akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya maofisa wa kampuni ya TTCL pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) wakifuatilia hotuba ya Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (hayupo pichani) katika uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya maofisa wa kampuni ya TTCL pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) wakifuatilia hotuba ya Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (hayupo pichani) katika uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) akijibu maswali ya wanahabari mara baada ya kuzindua nembo mpya ya Kampuni ya TTCL pamoja na uzinduzi wa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (pili kushoto). Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) akijibu maswali ya wanahabari mara baada ya kuzindua nembo mpya ya Kampuni ya TTCL pamoja na uzinduzi wa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (pili kushoto).Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam.  Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam. [/caption] Alisema Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano itafarijika zaidi itakapoona huduma za TTCL kimawasiliano zinaongoza nchini huku zikisaidia kukua kwa sekta nyingine zinazotegemea TEHAMA kufanikisha malengo yao. Aidha aliongeza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na TTCL ili kuhakikisha inafanikiwa katika malengo yake bila kikwazo chochote, kwani hivi sasa sekta ya Habari na Mawasiliano inagusa shughuli nyingi za maisha ya wananchi ya kila siku, kijamii, kiuchumi na kimaendeleo. "Hivi sasa huduma hizi sio tena jambo la ziada katika maisha ya kila siku bali ni huduma za msingi zenye kipaumbele cha juu katika maisha," alisema Waziri Mbarawa.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe (kulia) wakifuatilia hotuba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (hayupo pichani). Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe (kulia) wakifuatilia hotuba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (hayupo pichani)

   Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura alisema uzinduzi wa nembo mpya ya TTCL unaleta muonekano mpya wa kampuni unaoenda sambamba na mageuzi ambayo yanaendelea katika kuboresha miundombinu ya mtandao wa simu na data. Alisema katika safari ya mageuzi TTCL imefanikiwa kuboresha miundombinu ya simu za mezani na mkononi kwa kuleta teknolojia ya 2G GSM, 3G, UMTS na LTE sokoni ili kwenda sambamba na ushindani wa soko la mawasiliano. "...Teknolojia hizi zitaisaidia kuongeza ufanisi, ubunifu katika kutoa huduma ya simu za mezani, simu za mkononi na huduma ya intaneti zenye ubora wa hali ya juu na ya uhakika na gharama nafuu," alisema Dk. Kazaura. Alisema kwa sasa kampuni hiyo inaendelea na juhudi za kuboresha miundombinu ya mawasiliano ya data nchi nzima, hali ambayo itaongeza ubora wa huduma zetu kwa wateja wetu wote ndani na nje ya nchi.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Fidel Castro Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusnini Pemba leo alipofika kuwashukuru wanachama cha Mapinduzi CCM kwa ushindi waliompatia katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 29/05/2016.
  Wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya chakechake Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akizungumza nao leo, wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akizungumza na wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Chakechake Pemba wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) alipokuwa akizungumza na wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Chakechake Pemba wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu
  Kiembe Ramadhan Khamis kutoka Tawi la Mkoroshoni akitoa mchango wake wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Chakechake Pemba kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu
  Balozi Mohamed Kombo Juma (Wawi) akitoa mchango wake wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Chakechake Pemba kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu
  Mwenyekiti wa Wilaya ya Chakechake Pemba akitoa taarifa wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (katikati) wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza WanaCCM kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,(kushoto) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai (kulia),
  Wanachama cha Mapinduzi CCM wialayanya Chakechake akinyanyua mkono juu kuunga mkono maelezo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.]29/05/2016.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(Mb) akitoka katika lango Kuu la Gereza Msalato alipofanya ziara ya kikazi katika Gereza hilo leo Mei 29, 2016 Mkoani Dodoma(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Casmir Minja.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja(wa pili kulia) akiwa ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(wa pili kushoto) walipofanya ziara ya kikazi katika Gereza Msalato lililopo Mkoani Dodoma(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Antonino Kilumbi.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akisaini Kitabu cha Wageni kabla ya kupokea taarifa fupi ya hali ya Ulinzi na Usalama wa Gereza Msalato alipofanya ziara ya kikazi leo Mei 29, 2016.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto) akiongea na Wafungwa wa Gereza Msalato(hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi gerezani hapo(katikati) ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja kwa pamoja wakisikiliza kero mbalimbali za Wafungwa
  Muonekano wa eneo la Gereza Msalato ambalo linajishughulisha na mradi wa upondaji wa kokoto kama inavyoonekana katika picha.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akifanya mahojiano maalum na Waandishi wa Habari mara baada ya kutembelea eneo la mradi wa kuponda kokoto katika Gereza Msalato lililopo Mkoani Dodoma(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akipokea saluti kutoka kwa Mkuu wa Gereza Msalato, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Stevin Mwihambi alipowasili Gerezani hapo kwa ziara ya kikazi.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Mpwawa iliyopo mkoani Dodoma, Mohamed Utaly (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu harambee ya kupata fedha za kununulia madawati itakayofanyika Juni 4 mwaka huu Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Donald Ngwenzi,Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mohamed Maje na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, Samuel Albertus Coy.
  Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mohamed Maje (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
  Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Donald Ngwenzi, akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mohamed Utaly.


  Na Dotto Mwaibale

  HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpwapwa Dodoma Juni 4 mwaka huu inatarajia kufanya harambe ya kupata fedha za kununulia madawati kwa ajili ya shule za msingi na sekondari wilayani humo ambayo itafanyika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Mkuu wa Wilaya hiyo Mohamed Utaly alisema wamefikia hatua hiyo ili kukabiliana na uhaba wa madawati katika shule hizo ambapo pamekuwa na changamoto kubwa.

  Alisema awali halmashauri hiyo ilikuwa na upungufu wa madawati 16,000 lakini baada ya kuwashirikisha wananchi na kufanya harambee mbalimbali walifanikiwa kupata madawati 6000 na kubaki kiasi cha madawati 10,000 ambayo yanahitaji.

  Utaly alisema halmshauri hiyo katika bajeti yake ya mwaka 2015-2016 ilitenga sh. milioni 180 kwa ajili ya madawati ambapo kunamafanikio makubwa ya kupata madawati hayo yaliyosalia hivyo akatumia fursa hiyo kuwaomba wadau mbalimbali wa ndani wa wilaya hiyo na nje kujitokeza katika harambee hiyo ili waweze kufanikisha jambo hilo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Mohamed Maje alisema changamoto kubwa waliyoibaini ni kutokuwa na kitengo cha kufanya ukarabati wa madawati yaliyo haribika ambacho hivi sasa kimeanzishwa.

  "Kwa muda mrefu hatukuwa na kitengo cha kukarabati madawati yaliyoharibika lakini sasa tumekianzisha na kitasaidia kupunguza changamoto hiyo kwa kitengo hicho kitakuwa kikisaidia na wajasiriamali waliopo kwenye vikundi vya watu 20 ambavyo vipo sita kwa ajili ya kufanya kazi hiyo" alisema Maje.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) akimsalimia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba, wakati alipokuwa anawasili katika ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo katika Jengo la BMTL, jijini Dar es Salaam, jana. Katika hotuba yake, Rwegasira aliwataka watumishi 597 waliositishiwa mikataba yao waondoe hofu kwani hivi karibuni Serikali itaanza kuwalipa fedha zao baada ya taratibu chache za kiutendaji kukamilika.
  Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Ansigar Chilemba akitoa maelezo jinsi taarifa za muombaji wa Kitambulisho cha Taifa zinavyohakikiwa, kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba. Rwegasira alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam jana.
  Afisa Usajili Kitengo cha Ubora wa Kadi, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Jemima Mulokozi (kushoto) akimuonyesha vitambulisho vilivyokamilika vikiwa na ubora unaohitajika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dk. Modestus Kipilimba. Rwegasira alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam jana.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa tano kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba (wa tano kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka hiyo, mara baada ya Katibu Mkuu kumaliza ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam.

  Na Felix Mwagara, MOHA

  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira amesema fedha za kuwalipa watumishi 597 waliositishiwa mikataba yao katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) zipo na watalipwa hivi karibuni.

  Rwegasira alisema kiasi cha shilingi bilioni 2.3 zimetengwa kwa ajili ya malipo ya Watumishi hao waliachishwa kazi Machi 7, 2016 ambapo wanaidai Mamlaka mishahara ya miezi mitatu nyuma, malimbikizo ya fedha katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na makato ya fedha za Bima ya Afya.

  Akuzungumza na watumishi wa Makao Makuu ya NIDA pamoja na Maafisa Wasajili wa Vitambulisho vya Taifa, jijini Dar es Salaam jana, Rwegasira aliwataka watumishi hao waliositishiwa mikataba yao, wasipotoshwe na mtu yeyote kuhusu kutokulipwa haki zao kwani wapo katika hatua ya mwisho ya kukamilisha taratibu ndogo ndogo kabla ya kuanza kuwalipa.

  “Naomba muwaambie waondoe wasiwasi wowote, waache maneno, watulie kwani Serikali ipo makini na fedha tunazo na tutaanza kuwalipa mara tumalizapo taratibu ndogo ndogo zilizobaki.” Alisema Rwegasira.

  Aidha, Rwegasira aliwataka watumishi wa Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha ifikapo Desemba 31 mwaka huu Watanzania Milioni 23 wanatakiwa watambuliwe na kupata namba kabla ya kuanza kupewa Vitambulisho vya Taifa.

  Hata hivyo, watumishi hao walimuakikishia Katibu Mkuu huyo, kuwa kazi hiyo ya utambuzi itakamilika kama ilivyopangwa na itafanyika kwa umakini mkubwa kama inavyotarajiwa.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modestus Kipilimba alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kuwatembelea na kuwatia hamasa katika kukamilisha kazi pamoja na kufikisha lengo lao la kukamilisha utambuzi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

  “Tunakuahidi Katibu Mkuu kuwa tutatimiza lengo letu na tunakuakikishia tutafanya kazi kadiri ya uwezo wetu tukiongozwa na kauli mbiu ya ‘hapa kazi tu’, alisema Dk. Kipilimba

  Katibu Mkuu Rwegasira alifanya ziara hiyo kwa lengo la kujifunza zaidi shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka, hata hivyo alipata muda wa kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji.

  0 0

  AINA YA NIKON- D 5100
  Wasiliana na mwenye namba hizi 0787 311 222 - 0715 311 222 na 0767 311 222

  0 0

   Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete akihutubia katika mahafali ya 2016 ya Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu wa CCM yaliyofanyika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam leo jioni.
   Vijana vyuo vikuu Dar es Salaam wakiserebuka katika mahafali yao.
   Vijana hao wakiendelea kuserebuka.
   Hapa ni furaha kwa kwenda mbele.
  Ni kama wanasema' Hapa ni ushindi tu 2020 kwani vijana tumejipanga.
  Vijana wakiwa kwenye mahafali hayo.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, January Makamba Akizungumza na Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Parakuyo ambao wengi wao ni wanatoka kwenye familia za Wafugaji. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, January Makamba Akizungumza na Wafugaji kutoka Kijiji cha Parakuyo. 
  Akina mama wa Kijiji cha Parakuyo wakimsikiliza kwa Makini Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, January Makamba wakati alipotembelea Maeneo ya Wafugaji na Kuzungumza nao. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Januari Makamba akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Parakuyo ambao wengi wao ni Wafugaji.Picha na IMANI SELEMANI NSAMILA 

  0 0

  Rais John Pombe Magufuli akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kudhamini mkutano bodi ya makandarasi nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya TIB Corporate, Fank Nyabundege. Anayetazama kati kati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi (CRB) Eng. Consolata Ngimbwa akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. 
  Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya Mikopo wa Benki ya TIB Corporate, Theresia Soka akimweleza mmoja wa makandarasi kuhusu huduma zinazotolewa na benki yake. Anayetazama kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa benki ya TIB Corporate, Bahati Minja.

  Benki ya TIB Corporate imepongezwa na wadau mbalimbali juu ya mpango wake wa kuwawezesha kifedha makandarasi wa ndani ili waweze kutekeleza vema majukumu yao ya kikandarasi.

  Akizungumza wakati wa mkutano wa mashauriano wa mwaka wa bodi ya makandarasi, Kaimu Msajili wa Bodi ya Makandarasi nchini (CRB), Rhoben Nkori alisema anaipongeza benki ya TIB Corporate kwa kukubali kuwapa makandarasi mikopo na udhamini bila gharama zozote kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali.

  ‘Bodi ya Makandarasi (CRB) imeingia makubalinao na benki ya TIB Corporate ili iweze kutoa mikopo baada tu ya kupata barua kutoka bodi ya makandarasi’ alisema bwana Nkori.Mkutano huo wa mashauriano na maonyesho wa bodi ya makandarasi mwaka huu una dhima ya, ‘Mpango wa makusudi wa kuwajengea uwezo wa kiuchumi endelevu wakandarasi wazalendo, Changamoto na mustakabali wake’.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB Corporate, Frank Nyabundege amesema kama benki inayomilikiwa na serikali inaunga mkono moja kwa moja juhudi za serikali za kuwawezesha makandarasi ili waweze kushiriki katika kukuza uchumi.

  ‘Tumeona juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuwawezesha wakandarasi wazalendo, kwa kuanza kuwapa miradi mikubwa, ndio maana tumeanzisha huduma mbalimbali za kibenki kama dhamana ya kibenki bila gharama yoyote pamoja na mkopo wa ununuzi wa vifaa ambazo zitawasaidia wakandarasi wa ndani kufanikisha miradi yao bila usumbufu wowote’ alisema bwana Nyabundege.

  0 0

   Ramani inayoonesha Mpango wa upanuzi wa mfumo wa uondoaji wa majitaka katika jiji la Dar es salaam utakaotekelezwa na Serikali kwa lengo la kuondoa wastani wa uondoaji wa majitaka kutoka asilimia 10 hadi asilimia 30 ifikapo mwaka 2017.

  Mtambo mpya wa kusafishia maji katika chanzo cha maji Ruvu chini mara baada ya kukamilika.Mtambo huo sasa unazalisha maji lita milioni 270 kwa siku.
  Taswira ya Mtambo wa Ruvu Juu mara baada ya upanuzi.


  Na.Aron Msigwa- MAELEZO.

  Serikali imesema kuwa katika mwaka wa fedha 2016/2017 itatekeleza mradi wa ujenzi wa mfumo mpya wa uondoaji na usafishaji wa majitaka yanayozalishwa katika jiji la Dar es salaam ili kuliweka jiji hilo katika hali ya usafi na kuongeza wastani wa huduma hiyo kutoka asilimia 10 ya sasa hadi asilimia 30 ifikapo mwaka 2017.

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge amesema mradi huo utatekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Korea ya Kusini na Serikali ya Tanzania kwa gharama ya Dola za Kimarekani milioni 89.

  Amesema mradi huo utahusisha upanuzi wa miundombinu ya maji taka kwenye maeneo ya katikati ya jiji, ujenzi wa miundombinu mipya ya kupitishia maji hayo katika maeneo ya Ilala, Magomeni hadi Ubungo pamoja na maeneo ya Sinza, Kinondoni , Mwananyamala, Oysterbay na Masaki.

  Maeneo mengine yatakayoguswa na mradi huo jijini Dar es salaam ni Msasani, Kawe, Mbezi Beach, Kurasini,Keko, Chang'ombe, Temeke, Hananasif, Tandale, Kijitonyama, Makumbusho, Mabibo, Ubungo, Manzese, Sandali, Tandika na Miburani.Mhandisi Lwenge amesema mradi huo wa kipekee utahusisha ujenzi wa mitambo mitatu ya kisasa ya kusafisha majitaka katika maeneo ya Jangwani, Kurasini na Mbezi Beach.

  Aidha, Serikali kwa kushirikiana na Serikali ya Korea ya Kusini na Benki ya Dunia itatekeleza mradi wa huduma ya uondoaji wa majitaka na ujenzi wa miundombinu ya uondoaji wa maji ya mvua katika jiji la Dar es salaam ambayo yamekuwa kero kwenye miundombinu ya jiji hilo.

  "Serikali tumeanza kutekeleza mpango wa kupanua mfumo wa uondoaji na usafishaji wa majitaka yanayozalishwa na watumiaji maji , usanifu wa awali wa miradi mipya ya majitaka umekamilika,kazi inayoendelea ni usanifu wa kina ili kuweza kupata vitabu vya zabuni na michoro itakayotumika kumpata mkandarasi wa ujenzi" Amesisitiza Mhandisi Lwenge.

  Amesema kuwa kupitia mpango huo bomba linalomwaga majitaka baharini litaacha kutumika na badala yake maji hayo yatapelekwa katika mtambo mpya wa kisasa wa kusafisha majitaka utakaojengwa maeneo ya Jangwani ambao pia utasafisha majitaka kutoka maeneo yote ya katikati ya jiji Dar es salaam yaliyo jirani ambapo maji hayo ambayo yatakua yamesafishwa yatauzwa na kutumiwa katika shughuli mbalimbali za upozaji wa mitambo na umwagiliaji.

  Amebainisha kuwa katika kulishughulikia tatizo la majitaka jijini Dar es salaam Serikali itajenga mitambo mingine miwili eneo la Kurasini na Mbezi Beach itakayotumika kuzalisha gesi asilia kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya kusafishia maji hayo hivyo kupunguza matumizi na gharama za umeme.

  Katika hatua nyingine Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge amesema katika mwaka wa fedha 2016/2017, Serikali itafanya ukarabati na upanuzi wa mfumo wa kusambazia maji safi katika jiji la Dar es salaam.

  Ujenzi wa mfumo huo unalenga kuongeza idadi ya wananchi wapya watakaounganishwa na mtandao wa mabomba ya maji safi kutoka Mradi wa Ruvu Juu na ule wa Ruvu Chini ulioigharimu Serikali bilioni 141 ambao sasa maji yake yanaingia katika matanki ya maji yaliyoko Chuo Kikuu Ardhi jijini Dar es salaam.

  Amesema kukamilika kwa mradi wa Ruvu Chini na Ruvu Juu mpaka sasa kumeyawezesha baadhi ya maeneo ya jiji hilo yakiwemo ya Segerea, Kimara, Kibangu na Kinyerezi ambayo yalikua na mabomba ya maji maarufu kama mabomba ya mchina kuanza kupata huduma ya majisafi.

  Aidha, kupitia miradi hiyo mikubwa Serikali inaendelea kuishughulikia kero ya uhaba wa maji katika maeneo ya Bunju,Mabwepande, Boko,Tegeta,Kunduchi, Mbezi Beach, Mbezi Juu, Salasala, Kawe, Makongo, Mikocheni, Msasani, Masaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Sinza, Manzese, Ubungo, Mabibo, Kigogo, Buguruni na maeneo yote ya katikati ya jiji hilo.

  Mhandisi Lwenge amefafanua kuwa Kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 32.93 kimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa mfumo wa kusambaza majisafi katika jiji hilo na kuongeza kuwa wananchi wasiopata huduma ya maji kutoka mtandao wa maji wa DAWASCO wataendelea kuhudumiwa na mradi wa visima vilivyochimbwa.

  " Hadi mwezi Machi, 2016 tumechimba visima 52 na kati ya hivyo visima 32 vinatumika kutoa huduma ya majisafi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam" Amesema Mhandisi Lwenge.

  Wakazi wa jiji la Dar es salaam wapatao milioni 4.5 wamekuwa wakipata huduma ya majisafi kutoka chanzo cha Ruvu Chini ambacho kwa siku kinazalisha mita za ujazo 270,000 kwa siku, Mtambo wa Ruvu Juu unaozalisha mita za ujazo 182,000, Mtambo wa mtoni 9000 na Visima Virefu 27,000 na kufanya jumla ya mita za ujazo zinazozalishwa kwa siku kufikia 502,000 kutoka 300,000 za awali.

  0 0

  Diwani wa Kata ya Mabatini Jijini Mwanza, Deus Mbehe (Chadema) akikata utepe kama ishara ya Uzinduzi wa Kikundi cha Kusaidiana cha USHIRIKIANO PEOPLE'S kinachoundwa na Wanachama zaidi wa 100 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kata ya Mabatini.

  Na BMG

  Kikundi hicho kiliundwa baada ya kuibuka stofahamu ya wananchi kusaidiana katika masuala mbalimbali ikiwemo misiba, baada ya baadhi ya wanachama wa chadema kutengwa katika shughuli za misiba katika Kata ya Mabatini.

  Uzinduzi wa Kikundi hicho ulifanyika katika Ukumbi wa Kilimanjaro uliopo Mabatini Stand huku ukiambatana na harambee kwa ajili ya kukiimarisha kikundi ambapo diwani wa Kata ya Mabatini ambae alimwakilisha diwani wa Kata ya Butimba, akichangia shilingi Laki Tano huku wageni wengine waalikwa wakifanikisha harambee hiyo kufikisha shilingi Milioni Moja, laki moja na elfu sabini.

  Wanachama nao waliahidi kila mmoja kuchangia shilingi elfu kumi, pesa ambazo kwa ujumla zitasaidia kukabiliana na mapungufu yanayokikabili kikundi hicho. Mapungufu hayo ni pamoja na viti 120, sufuria nne, turubai mbili pamoja na sahani 200 lengo likiwa ni kujiimarisha katika mahitaji mbalimbali yanayohitajika katika shughuli mbalimbali.

  Mwenyekiti wa Kikundi hicho chenye wanachama 103 hadi sasa, Salma Ibrahim, amewasihi wananchi wengine kujiunga na kikundi ili kuongeza nguvu ya kusaidiana katika masuala mbalimbali ikiwemo sherehe, misiba na kuinuana kiuchumi bila kujali itikadi zao za kisiasa.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Ntibenda (kushoto) akipokea madawati kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa Itifaki na Uhusiano wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Catherine Kilinda. AICC imechangia madawati 100 kuunga mkono juhudi za serikali kuhakikisha shule zinakuwa na madati ya kutosha. 
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Ntibenda (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea msaada wa madawati 100 kutoka Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). Katikati ni Afisa Mwandamizi wa Itifaki na Uhusianoi wa AICC, Catherine Kilinda.

  Kituo cha Mikutano cha KimataifaArusha (AICC)kimemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Ntibenda madawati 100 yenye thamani shilingi milioni nane ili kupunguza tatizo la upungufu wa madawati katika mkoa huo.

  Akipokea madawati hayo jijini Arusha jana, Ntibenda amesema kwamba msaada huo ni sehemu ya juhudi za serikali mkoani Arusha kuwashirikisha wadau wa maendeleo ili kuhakikisha shule zote za mkoa huo zinakuwa na madawati ya kutosha.

  “Napenda niishukuru sana AICC kupitia kwa Mkurugenzi Mwendeshaji Elishilia Kaaya kwa kuitikia vema wito wa serikali ya mkoa wa kuomba wadau wasaidie kuondoa tatizo la upungufu wa madawati katika mkoa wetu”, alisema Mkuu wa Mkoa. 

  Alitoa wito kwa wadau mbalimbali mkoani Arusha wakiwemo wafanyakazi wa ofisi ya Mkoa wa Arusha nao kujitokeza ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha kila mwanafunzi ana kaa katika dawati.

  Akizungumza baada ya kukabidhi madawati hayo, Afisa Mwandamizi waItifakina Uhusiano wa AICC, Catherine Kilinda amesema kwamba AICC kama shirika la umma linawajibu wakuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu hapa nchini.

  “Sisi kama shirika la umma linalojiendesha kibiashara tunaona fahari kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia wa kuhakikisha watoto wetu wa shule hawakai chini na ndio maana leo hii tumekabidhi msaada huu ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais katika kuinua sekta ya elimu”, alieleza Catherine.

  AICC ambayo inajihusisha na kutoa huduma za Mikutano, upangishaji w ofisi na nyumba pamoja na kutoa huduma za afya, imekuwa ikitumia sehemu ya faida katika kusaidia jamii hasa katika sekta ya elimu.

  0 0


  Wakazi wa kijiji cha Rondo Mnara wakimsikilza Mbunge wa jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye .
  Mbunge wa jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauyeakicheza ngoma ya asili ya Wamwela pamoja
  Wakazi wa Chihodya kata ya Chiponda wakishangilia jambo wakati Mbunge wa jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauyealipokuwa akihutubia.


  Mbunge wa jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na viongozi wa kijiji cha Rondo Mnaramara baada ya kuwasili tayari kuwahutubia wakazi hao waliojitokeza kwa wingi.
  Sehemu ya wakazi wa kijiji cha Rondo Mnara wakiwa tayari kumsikiliza Mbunge wa jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye
  Mbunge wa jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipitia moja ya jambo la msingi pamoja na diwani wa kata ya Rondo Mama Halima Mwambe muda mfupi kabla ya kuanza kuhutubia wakazi wa Rondo Mnara.


  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Kikosi cha kwanza cha timu ya Soka ya Tanzania -Taifa Stars kilichoanza dhidi ya Harambee Stars ya Kenya hapo jana Jumapili.
  Mshambuliaji wa Taifa Stars, Elias Maguli (Kulia) akichuana na David Odhiambo wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliofanyika Uwanja wa Moi Kasarani, Nairobi Kenya hapo jana. timu hizo zilitosahana nguvu kwa kutoka sare ya 1-1.
  Winga wa Taifa Stars, Shiza Ramadhani akichuana na beki Joakins Atudo wa Harambee Stars katika mchezo huo.

  0 0

  Dakitari wa macho akiwa katika jukumu la kumpima macho mwanafunzi wa shule ya msingi msasani

  Rais wa klabu ya Rotary ya Oyster bay jijini Dar es Salaam, Bwana Mohammed Versi akizungumza na wanahabari

  Baadhi ya madakitari wakiwa katika majukumu yao ya kuhakikisha kila mwanafunzi anapata matibabu

  Dar es Salaam, 29 Mei 2016
  Klabu ya Rotary ya Oyster Bay ya jijini Dar es Salaam imeandaa kambi ya matibabu na kutoa huduma za afya kwa wanafunzi wa shule mbili za Msasani, Msasani A na Msasani B na kufanikiwa kutoa huduma kwa wanafunzi zaidi ya 950. Kambi hiyo ya siku moja ilitoa vipimo vya afya, ushauri, matibabu na huduma mbalimbali za meno, macho, malaria, usafi wa mwili, minyoo, masikio, pua na koo (ENT), pamoja na magonjwa ya ngozi. Kampeni ya Damu Salama pia ilifanyika wakati wa kambi hiyo ili kuwawezesha uchangiaji wa damu katika benki ya damu salama.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Rais wa klabu ya Rotary ya Oyster bay jijini Dar es Salaam, Bwana Mohamed Versi alisema waliguswa kufadhili upimaji huo kwa sababu suala la afya ni jambo la msingi kwa mwanadamu
  "Rotary tumekuwa na utaratibu wa kusaidia jamii, na hii si mara ya kwanza kusaidia shule hii, tayari tumeshajenga maktaba mbili, tumeweka maji safi na salama, tumepanda miti, tumejenga ukuta ili kuimarisha ulinzi na awamu hii tumeona ni vyema tutoe huduma ya afya"

  Uongozi wa shule ya msingi Msasani umesema umefurahishwa na kitendo cha klabu ya Rotary ya Oyster Bay kwa kutambua kuwa afya njema ni silaha bora kwa mtoto katika mafaniko ya kielimu.
  "Nawashukuru mno Rotary maana wamekuwa washirika waaminifu wa vitendo na si maneno pekee.

  Bado tunaomba wadau wengine waige mfano huu katika kutusaidia, bado tuna changamoto mbalimbali zinazotukabili" alisema mwalimu mkuu wa shule hiyo, Egidius Mjumangoma
  Kambi hiyo ya matibabu ni muendelezo wa huduma mbalimbali za kijamii zinazotolewa na klabu hiyo katika shule za Msasani A na B. Miradi katika shule hiyo ilianza katika eneo la maji na usafi ambapo shule hizo zilipatiwa maji safi na salama ya kunywa pamoja na ya matumizi mengine.

  Klabu hiyo pia ilifanya ukarabati wa majengo na kuweka vitabu katika maktaba mbili kwenye shule hizo. Maktaba hizo zina vitabu vipya na vinavyovutia kwa matumizi ya watoto, makabati yenye vitabu vipya vipatavyo elfu nne (4,000) vingi vikiwa katika lugha ya Kiswahili, ili kutoa hamasa ya kusoma kwa watoto wadogo.

  Klabu hiyo ya Rotary Oyster Bay, kwa sasa iko katika ujenzi wa ukuta kuzunguka shule hizo ili kuweka usalama wa mali za shule pamoja na wanafunzi. Ujenzi huo umewezeshwa na fedha zilizopatikana kutoka kwenye mojawapo ya shughuli za ukusanyaji fedha zinazofanywa na klabu hiyo. Mojawapo ya kazi zilizofanyika wakati wa kambi ya matibabu ilikuwa ni ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukuta huo ambapo wanaklabu na wageni waalikwa walishiriki katika ziara hiyo.

  Kambi hiyo ya matibabu imefanyika kwa udhamini wa Diamond Trust Bank, Whitedent, Knight Support, Vital Supplies, Mansoor Daya, Cello na Sayona kwa ushirikiano na Hindu Mandal Hospital, TDA, Damu Salama na wanafunzi kutoka Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) na Hubert Kairuki Memorial University (HKMU).

  Maktaba hizi mbili zilifadhiliwa chini ya mpango uitwao “Rotary Global Grant”, ambapo katika tafsiri za Rotary, ni pale ambapo Rotary International na ofisi ya Rotary katika kanda husika hutoa msaada wa kifedha kwa klabu yoyote ya Rotary ndani ya kanda. Klabu inayopewa ufadhili huo inatakiwa kushirikiana na klabu yoyote kutoka kanda nyingine ili kuendesha mradi wa jamii ulio endelevu na ambao matokeo yake yanaweza kupimika.

  Baada ya shule hizo kuchukuliwa chini ya uangalizi wa Klabu ya Rotary ya Oyster Bay, miradi mingine inapangwa kufanyika katika shule hizo mbili ambapo mafunzo kwa walimu yameandaliwa kufanyika ndani ya mwaka huu. Walimu wa shule hizo watapewa mafunzo ya namna ya kufundisha watoto, yani namna na kutumia maktaba hizo mpya kwa lengo la kukuza kiwango cha uelewa kwa watoto wadogo kwenye jamii zetu.

  0 0

  Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (Kulia) akizungumza na vyombo vya habari wakati wa hafla ya makabidhiano ya kompyuta 30 kwa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya kisasa, akishuhudiwa na Meneja Msaidizi wa chuo Oscar Mwambene (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Mafunzo Eunice Nderingo Ulomi (kushoto), hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo Temeke, Dar es Salaam.

    Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) akikabidhi kompyuta 30 kwa Meneja Msaidizi wa chuo cha Taifa cha Utalii (NCT)  Oscar Mwambene (katikati)   kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya kisasa, akishuhudiwa na Mkurugenzi wa Mafunzo Eunice Nderingo Ulomi (kushoto) katika hafla iliyofanyika chuoni hapo Temeke, Dar es Salaam.
   Mkuu wa idara ya Utalii katika Chuo cha Taifa cha Utalii Elina Makanja (Kushoto) akimwelekeza mwanafunzi Agape Gerald (Kulia) mara baada ya kukabidhiwa kompyuta 30 kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya kisasa, akishuhudiwa na Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (Katikati).
  Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) wakitumia kompyuta zilizokabidhiwa na Airtel kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili kuwawezesha kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya kisasa.


  Katika kuendeleza dhamira  yake ya kusaidia Jamii kwa kujenga ubora wa ya elimu ya ICT hapa nchini, Airtel imekabidhi kompyuta 30 kwa Chuo cha utalii cha Taifa (NCT) ambapo ni sehemu mojawapo ya  mipango yake ya kusaidia vijana wajasiriamali hapa nchini ujulikanao kama Airtel FURSA  wa kutoa huduma kwa jamii  katika kuboresha upatikanaji wa teknolojia ya kisasa na ubora wa elimu nchini Tanzania.

  Kama kampuni yenye kutoa huduma bora za simu za mkononi, Airtel itaendelea kusaidia sekta ya ICT hapa nchini kwa kuwawezesha  vijana kupata elimu iliyobora  na kuwa vijana wenye mafanikio katika Jamii yao.

  Akizungumza wakati wa sherehe za makabidhiano hayo  yaliyofanyika katika Chuo cha utalii cha Taifa (NCT) kilichopo Temeke, meneja huduma kwa jamii wa Airtel,  Hawa Bayumi alisema kuwa Airtel itaendeleza dhamira yake ya kuunga mkono juhudi ya kuboresha kiwango cha elimu hapa nchini.

  “ Leo hii tumekabidhi kompyuta hizi tukiamini  kwamba tunachangia nchi yetu kuwa na elimu bora, ni jambo la muhimu kwa wanafunzi na walimu kuwa na vifaa bora mashuleni. Ndio maana Airtel imeweka mkazo katika swala la kusaidia Jamii kwa upande wa elimu  kwa kutoa vitendea kazi vitakavyoweza kusaidia kujifunzia na kupata elimu ya ujasiriamali na hatimaye kuchangia vyema na kupata matokeo bora. Kutokana na msaada huu kwa NCT tunaamini kabisa kwamba kiwango cha elimu kwa Wanafunzi kitaongezeka na hata urahisi wa walimu katika ufundishaji utaongezeka kwa kiwago kikubwa, na vile vile tunawawezesha kizazi kijacho kujikita zaidi katika teknolojia na kujua mambo mengi zaidi yanayoendelea dunia nzima kutokana na technolojia inayokuwa kila siku, "alisema Bayumi

  Akizungumza kwa niaba ya chuo, mkurugenzi wa Mafunzo wa NCT, Eunice Nderingo Ulomi, aliwashukuru Airtel kwa kwa msaada huo wa kompyuta , na kubainisha kuwa kompyuta hizo zitachangia kuongeza kiwango cha elimu kwa mwanafunzi kitaaluma. "Mara nyingi kompyuta huwa inatazamwa kama si kitu cha muhimu katika Jamii yetu, ila ni kifaa muhimu sana kinachomuwezesha mwanafunzi kupata habari nyingi sana za masomo na hata kujua mambo mbalimbali yanayoendelea dunia nzima hasa katika karne hii ya 21," alisema Ulomi.

  "Lengo letu ni kuhakikisha tunatoa elimu iliyobora katika  sekta ya utalii . Kupokea kompyuta hizi kutaboresha hali ngumu  tuliyakuwanayo ya upungufu wa vifaa hivi hapa chuoni na tunaamini tutatoa elimu iliyobora ambayo itasidia kupunguza changamoto tulizakuwanazo, ambazo zimekuwa zikitufanya tukwame katika mambo mengi sana, hivyo zitatusaidia  kukuza ujuzi wa kila mtu hapa chuoni, vile vile zitasaidia kuongeza mapato ya serikali, kukuza nchi yetu  katika ushindani wa kitalii na kuongeza uingizaji wa watalii ambapo itasaidia kuongeza sekta nyingine za kiuchumi katika upande wa maonyesho ", aliongeza Ulomi

older | 1 | .... | 862 | 863 | (Page 864) | 865 | 866 | .... | 1897 | newer