Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

WANANCHI WAFURIKA BANDA LA BENKI YA NMB KATIKA MAONESHO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI UWANJA WA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI.

0
0
Mgeni Rasmi katika Maonesho ya Wakulima na Wafugaji,Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala manispaa ya Moshi,Wencelaus Lindi akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Benki ya NMB katika maeonesho hayo yanayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Meneja Mwandamizi wa Mahusiano ya biashara na Kilimo wa Benki ya NMB,Oscar Rwechungura (aliyenyoosha kidole) akitoa maelezo kwa mgeni rasmi ,Wencelaus Lindi (aliyekunja mikono) katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji yaliyoandaliwa na Mtandao wa kusaidia wakulima wa AgriProFocus.
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi,Emanuel Kashusho akikabidhi zawadi ya T-shirt ,Kalamu na Key holder kwa mgeni rasmi ,Wencelaus Lindi mara baada ya kutembelea banda la Benki hiyo na kupata maelezo namna inavyoshirikiana na wakulima katika kukuza mitaji yao.
Mgeni rasmi ,Wencelaus Lindi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB pamoja na wananchi wengine waliofika kutembelea banda la NMB.

Meneja Mwandamizi wa Mahusiano ya biashara na Kilimo wa Benki ya NMB,Oscar Rwechungura akitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliotembelea banda hilo.
Afisa Mikoapo wa Benki ya NMB,Gaudencia Mazigo akigawa vipeperushi kwa wananchi waliofika katika banda la Benki hiyo katika maonesho ya wakulima na wafugaji yanaoyofanyika katika uwanja wa Chuo kikuu cha Ushirika Moshi.
Afisa Mikopo wa Benki ya NMB,Josephine Joseph akitoa maelezo kwa wateja waliofika kutembelea banda la NMB wakati wa maoenesho ya Wakulima na Wafugaji yanayofanyika katika uwanja wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi.
Afisa Mikoapo wa Benki ya NMB,Gaudencia Mazigo akigawa vipeperushi kwa wananchi waliofika katika banda la Benki hiyo katika maonesho ya wakulima na wafugaji yanaoyofanyika katika uwanja wa Chuo kikuu cha Ushirika Moshi.  
Meneja Mwandamizi wa Mahusiano ya biashara na Kilimo wa Benki ya NMB,Oscar Rwechungura akitoa maelezo kwa mmoja wa watu waliotembelea banda la NMB.
Meneja wa NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi Emanuel Kashusho akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la NMB wakati wa maoensho ya Wakulima na Wafugaji.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika banda la NMB.

Imeandaliwa na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog kanda ya Kaskazini.

KONGAMANO LA KUKARIBISHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KUFANYIKA KESHO

0
0
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi na rais wa kef mohamed kamilagwa(kushoto) akimuonesha imam qasim ibn ali khan baadhi ya vivutio vilivyopo nchini kupitia jarida
 Imam Qasim Ibn Ali Khan (katikati) akibadilishana mawili matatu kwaajili ya kongamano la kukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani, kulia kwake ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi na rais wa kef mohamed kamilagwa na kushoto kwake ni mjumbe wa kamati hiyo Juma Nchia
 Imam Qasim Ibn Ali Khan pamoja na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano la kuukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani mohamed kamilagwa.

Mke wa imam hasaina m.khan (wakwanza kulia) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwl. j.nyerere akiwa na baadhi ya wanakamati waliojitokeza kumpokea alipowasili nchini tanzania. 
 Imam Qasim Ibn Ali Khankutoka usa akiwa pamoja na baadhi  ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano la nane la kukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani mara baaada ya kuwasili nchini tanzania.

TEA KUENDELEA KUJENGA MABWENI YA WASICHANA

0
0
KUELEKEA maadhimisho ya hedhi salama itakayofanyika Mei 28 , Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imesema itaendelea kujenga mabweni na chemba za kuhifadhi na kuchomea taulo za kike ili kuwafanya wanafunzi wa kike kusoma katika mazingira mazuri.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo iliyoko wilayani Ilala, Meneja Mawasliano na Uhusiano wa TEA, Sylvia Lupembe alisema wanafunzi wa kike wamekuwa na wakati mgumu katika masomo yako kutokana na hedhi.

“ Wanafunzi wa kike wanashindwa kuhudhuria masomo kwa zaidi ya siku 80 kwa mwaka jambo ambalo linarudisha maendeleo ya mazomo yao, kwa kushirikina na wadu wa elimu tumeona tuangalie suala la kuwasaidia, hasa wale alioko kwenye shule ambazo ni vigumu kufikia,” alisema.

Alisema kwa mwaka huu wa fedha, TEA kwa kushirikiana na wadu wa elimu wanakamilisha ujenzi wa mabweni 11 ya wanafunzi wa kike hapa nchini.

Lupembe alitumia fursa hiyo kuishukuru Benki ya CRDB kwa kuwezesha kupatikana na taulo hizo za kike sambamba na mchango wao katika ujenzi wa bweni katika shule ya Sekondari Pangani ambalo limegharimu sh milioni 20.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Yombo Christine Kasyupa, aliwashukuru TEA na benki ya CRDB kwa mchango wao ambao wamekuwa wkaiutoa katika shule hiyo kwani awali walishopokea dawati.

Naye Mwanafunzi Monica Singano anayesomba darasa la Saba A katika shule ya msingi Yombo, alisema msaada huyo umekuja wakati mzuri hasa kutokana na wanafunzi wengi kutoka kwenye familia mabazo hazina uwezo wa kugharamia kununua taulo za kike.

“ Wengi wa wanafunzi hapa wanatoka familia zisionauwezo wa kununua taulo za kike, wengi wanatumia vitambaa ambavyo haviwezi kuwafanya wanafunzi kukaa shule kuanzia asubuhi hadi mchana, hivyo kulazimika kwenda kubadili huku masomo yakiwa wanaendelea,” alisema
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Yombo, Christina Kasyupa wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa vya kujihifadhi wanawake vilivyotolewa na Benki ya CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo. Kushoto ni Ofisa wa TEA, Happines Tandari, Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia Hassad na Mwalimu Emily Salumu. (Picha na Francis Dande) 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo wakiimbo nyimbo katika hafla hiyo. 
Ofisa wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Happines Tandari akizungumza kaba la makabidhiano ya vifaa hivyo.
Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia Hassad (kushoto), akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Yombo, Christina Kasyupa (katikati) na mwalimu Salumu sehemu ya msaada wa vifaa vya kujihifadhia wanawake ‘taulo za kike’ vilivotolewa na Benki ya CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia Hassad (kushoto), akimkabidhi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo, Monica Singano sehemu ya msaada wa vifaa vya kujihifadhia wanawake ‘taulo za kike’ vilivotolewa na Benki ya CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Christina Kasyupa.
Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia Hassad (kushoto), akimkabidhi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo, Sabina Yona, sehemu ya msaada wa vifaa vya kujihifadhia wanawake ‘taulo za kike’ vilivotolewa na Benki ya CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Christina Kasyupa.
Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia Hassad (kushoto), akimkabidhi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo, Amina Abdalah, sehemu ya msaada wa vifaa vya kujihifadhia wanawake ‘taulo za kike’ vilivotolewa na Benki ya CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwalimu Emily Salumu.
Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia Hassad (kushoto), akimkabidhi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo, Rehema Baina, sehemu ya msaada wa vifaa vya kujihifadhia wanawake ‘taulo za kike’ vilivotolewa na Benki ya CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwalimu Emily Salumu.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo wakiwa wamenyanyua juu maboksi yaliyokuwa na vifaa vya kujihifadhi wanawake 'Taulo za kike'baada ya kukabidhiwa na Benki ya CRDB kupitia TEA.
Wanafunzi wakiwa na furaha.
Maofisa wa TEA wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo.

WASHIND KUMI WA KWANZA WA PROMOSHENI YA MILLIONI 100 NA TUSKER FANYA KWELI UWINI WATANGAZWA

0
0
 Meneja Masoko wa bia ya Tusker Nandi Mwiyombela (kushoto) akitoa maelezo ya promosheni ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini wakati wa droo ya kwanza ya promosheni hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, pembeni yake ni afisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya kubahatisha nchini Humud Semvua.
 Meneja Masoko wa bia ya Tusker Nandi Mwiyombela (kushoto) akiongea kwa njia ya simu na mmoja wa washindi kumi wa kwanza wa promosheni ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini katika droo ya kwanza ya promosheni hiyo, akishuhudiwa na afisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya kubahatisha nchini Humud Semvua (katikati), pamoja na muongozaji wa shoo hiyo Abdallah Mwaipaya ambaye pia ni mtangazaji wa ITV wakati wa droo ya kwanza inarushwa moja kwa moja kupitia ITV.
 Meneja Masoko wa bia ya Tusker Nandi Mwiyombela akiokota kuponi ili kujua mmoja wa washindi kumi wa kwanza.
 Afisa kutoka Bodi ya kusimamia Michezo ya kubahatisha nchini Humud Semvua (katikati) akihakiki namba ya simu ya mmoja wa washindi kumi wa kwanza wakati wa shoo ya sroo ya kwanza ya promosheni ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini jijini Dar es Salaam.
Muendeshaji wa shoo ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini na Mtangazaji wa ITV Abdallah Mwaipaya akitoa maelekezo wakati wa shoo hiyo ambapo washindi kumi wa kwanza walitangazwa.


 Ni wiki mbili tangu promosheni ya TUSKER FANYA KWELI UWINI ilipozinduliwa kiaina yake mikoa miwili tofauti kwa wakati mmoja, Dar es Salaam na Moshi. Leo washindi kumi wamepatikana katika droo ya kwanza na ya kusisimua. Milionea hawa walitangazwa leo katika droo iliyorushwa moja kwa moja na kushuhudiwa na waangalizi kutoka Bodi inayosimamia michezo ya kuigiza Tanzania, wana habari nan a wahusika wakuu wa promosheni hii ambao ni timu nzima ya Tusker lager. 

Washindi kupitia maongezi ya simu walionesha mshangao na furaha kubwa kushinda kitita cha Tsh. 1,000,000 ambapo wamekiri hawakutegemea kupata kiasi hicho cha pesa kwa hivi karibuni. Ukiachilia mbali washindi wa kila wiki wanaopatikana kupitia droo pia wapo watumiaji wa bia ya Tusker wanaojipatia bia kibao za bure kila siku. Promosheni bado ina wiki tisa mbele.

Washindi kumi wa kwanza ni Rehema Matemba, Elias Poto, Deogratius Shayo kutoka Kilimanjaro, Vestina Mainde, Doru B. kutoka Morogoro,  Sebastian Joseph, Michael Mwinuka,  Albert Tarimo na Festo Silvester ambaye ameshinda Millioni 2 wote kutoka Dar es Salaam.


Akiongea kwa njia ya simu mshindi wa kwanza Rehema Matemba ambaye ni mfanyabiashara katika manispaa ya Moshi alishikwa na mshangao kwani hakutegemea na anaona kama ndoto kuwa mshindi wa Milioni 1 kutoka Tusker kwani alishiriki promosheni hii wiki moja iliyopita na kuwa kati ya wale waliobahatika.


Naye mshindi wa pili Albert Tarimo alielezea furaha yake na kuishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuwajali wateja wake kwa kugusa maisha yao ambapo kila mara huja na promosheni za kuvutia kwa wateja wake. “Nilishiriki kujaza vocha ya promosheni hii nilipokua bar nakunywa bia yangu ya Tusker sikutegemea kushinda kwani siku zote huwa sina mazoea ya kushiriki mashindano yeyote yale, nafuraha sana ni mara yangu ya kwanza kushiriki na kuwa moja ya washindi. Milioni 1 niliyoipata itanisaidia kuwalipia wanangu ada za shule kwangu ni faraja sana imekuja kipindi ambacho nauhitaji mkubwa wa pesa.” Alisema Tarimo.


Kwa upande wake Meneja Masoko wa Bia ya Tusker Nandi Mwiyombela alieleza kuwa promosheni hiyo iliypo maalum kwa watumiaji wote ina faida kubwa kwa watumiaji wa bia zao za Tusker kama ilivyoanza kwa wateja kumi wa kwanza leo ambao wameguswa kwa namna tofauti nay a kipekee. “Ikiwa tu hapa ni hatua za mwanzo za promosheni hii kumekuwa na zaidi ya washindi 1000 wa bia za bure na maelfu wameshashiriki. 

Tangu tuzindue Tusker Fanya Kweli Uwini wiki mbili zilizopita tumepata muamko mkubwa kutoka kwa wateja wetu. Leo tumepata washindi wetu kumi wa kwanza ambao watakabidhiwa million 1 kila mmoja na kufanya jumla ya Million 10 kutolewa wiki ya kwanza. “Alisema Nandi.


Aliongeza kuwa “promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini inaendelea na tumebakiwa na wiki tisa, tunapenda kuwakumbusha wateja wetu kuwa bado tuna Million 90 na bia kibao za kushinadaniwa! Kutakua na shughuli mbalimbali za burudani kila wikend yaani Ijumaa na Jumamosi kipindi chote cha kampeni yetu katika bar mbalimbali nchi nzima, hivyo mjitokeze kwa wingi muweze kufanya kweli. 

Katika huu mwanzo mzuri wa promosheni yetu napenda kuwashukuru sana wateja wetukwa kutuunga mkono na walivyoipokea kwa mikono miwili promosheni hii ya Millioni 100 na Tusker Fanya Kweli na Uwini.” Aliongeza Nandi


Droo za promosheni hii zitaendeshwa kila wiki na hiyo italeta msukumo kwa wateja na watumiaji wa bia ya Tusker kushiriki zaidi. Kwa utofauti kabisa hii ni promosheni ya kwanza iliyoangalia na wahudumu wa bar pia ambapo wahudumu watapata Tsh 100,000 endapo aliyemuhudumia akishinda. Hivyo leo washindi kumi wamepata Million 1 kila mmoja na wahudumu kumi pia wamepata 100,000 kila mmoja. 

VIJANA WANAOKUSANYA USHURU WA MAEGESHO YA MAGARI JIJINI MWANZA WALALAMIKIWA.

0
0
Gari la mmoja wa wagonjwa katika kituo cha afya cha Bio Health kilichopo mtaa wa liberty jijini Mwanza likiwa limepigwa cheni.

Na BMG
Vijana wanaokusanya ushuru wa tozo za maegesho ya magari jijini Mwanza, wamelalamikiwa kwa namna wanavyotekeleza majukumu yao kinyume na taratibu.

Vijana hao wamelalamikiwa kutokana na tabia yao ya kuvizia magari yanayoegeshwa katika maeneo mbalimbali jijini Mwanza huku baadhi ya maeneo hayo yakiwa ni halali kwa ajili ya magari kuegeshwa kwa muda.

Katika mtaa wa Liberty jijini Mwanza, vijana hao wamelalamikiwa kutokana na kuvizia magari binafsi yanayowapeleka wagonjwa katika kituo cha afya cha Bio Health kwa ajili ya matibabu.
Picha Zaidi Bonyeza HAPA

WANAMICHEZO WAASWA KUWA WABUNIFU

0
0
Na Anitha Jonas – MAELEZO
Viongozi  wa  Timu ya Michezo Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo wameaswa kuwa wabunifu na kuongeza jitihada za kuunda timu bora za michezo zitakazo jipatia ushindi katika mashindano mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mhazini  kutoka Shirikisho la Michezo,Wizara na Wakala wa Serikali (SHIMIWI) Bw.Brown Nyamtiga mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uchaguzi na washindi kutangazwa. 

“Mkiwa kama Wizara yenye jukumu la kusimamia masuala ya Michezo nchini  ni vyema muwe mfano kwa taasisi zote za serikali kwa kuwa na timu imara zenye uwezo wa kupata ushindi pamoja na hili linawezekana pale mtakapoamuwa kuweka jitihada za dhati katika kusimamia hilo”,alisema Bw.Nyamtiga.

Akiendelea kuzungumza katika uchaguzi huo Bw.Nyamtinga alisema anatambua changamoto ya pesa iliyoko serikalini kwa sasa,hivyo viongozi wanapasawa kuwa wabunifu wa kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha ili kuisaidia serikali suala hilo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Timu aliyeibuka mshindi katika uchaguzi huo Bw.Modest Mfilinge kutoka Utawala alisema katika uongozi wake anatarajia kufanya mageuzi chanya katika sekta ya michezo kwa wafanyakazi wa wizara hiyo ikiwa ni pamoja na kuunda mabonaza yatakayo kuwa yakifanyika kila mwisho wiki.

“Awali ya yote nitafanya jitihada za kutambua wanamichezo katika Wizara na kwa hili naamini ndipo nitakapopata wachezaji mahari watakao unda timu bora ya michezo katika Wizara na kikubwa nitakachohitaji ni ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi wenzangu”,alisema Bw.Mfilinge.

 Pamoja na hayo Bw.Mfilinge alisema mabonanza anayotarajia kuanzisha ni endelevu na anaimani kubwa na viongozi wenzake waliyochaguliwa kuwa watashirikiana vizuri na kufanya kazi nzuri yenye kuleta matokeo chanya katika timu ya wizara. 

Hata hivyo uchaguzi huo wa Wizara umesaidia kupatikana kwa viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Timu Bw.Jackson Manyika kutoka Kitengo cha Uhasibu,Katibu Mkuu Msaidizi Bw.Mfaume Said Mfaume kutoka Utawala,Makamu Mwenyekiti Bw.Francis Songoro,Mweka Hazina Bi. Flora Mwenyembegu, Mjumbe Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa SHIMIWI Bw.Carlos Mlinda pamoja na Wajumbe wa Idara .

CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA BUNGE CHAPATA MWENYEKITI MPYA

0
0
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dodoma Bw. Mchenya John akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge (hawapo pichani) kabla ya Uchaguzi wa Viongozi wa TUGHE tawi la Bunge uliofanyika mapema wiki hii Mkoani Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Ofisi hiyo Bibi. Emma Lyimo.Mwenyekiti aliyemaliza muda wake kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Bunge Bw. Abdallah Hancha (wa kwanza kulia) akitoa neno la shukrani kwa wafanyakazi wenzie wa Ofisi ya Bunge kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa TUGHE uliofanyika mapema wiki hii Mkoani Dodoma. Walioambatana naye ni wajumbe wa Kamati Kuu ya TUGHE tawi la Bunge.Wasaidizi wa kamati ya Uchaguzi wakihesabu kura wakati wa Uchaguzi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Bunge uliofanyika mapema wiki hii kwenye Ofisi za Bunge Mkoani Dodoma.Mwenyekiti mpya wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Bunge Bw. Chacha Nyakega akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa TUGHE uliofanyika mapema wiki hii kwenye Ofisi za Bunge Mkoani Dodoma.

PICHA ZOTE NA FATMA SALUM-MAELEZO

NAIBU WAZIRI LUHAGA MPINA ASHIRIKI USAFI WA MAZINGIRA UDOM

0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina akishirika kufanya usafi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Udom wakati usfi wa mazingira kitaifa iliyofanyika, Dodoma jana
Luaga Mpina akiongozana na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDOM wakati wa siku ya usafi wa Mazingira Kitaifa iliyofanyika eneo la Chuo hicho jana
Luaga Mpina akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDOM wakati siku ya usafi wa Mazingira Kitaifa iliyofanyika eneo la Chuo hicho jana

TAWLA YAWATAKA WANAWAKE KUSHIRIKI SHUGHULI ZA KIUCHUMI ILI KUNDOA UTEGEMEZI

0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Ms. Aisha Zumo Bade akisoma hotuba yake waakati wa wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Chama hicho unaofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam leo.
Mtoa Mada Agustus Emmanuel Fungo akiwasilisha mada ya masuala ya kiuchumi kwa wanasheria wa Chama cha wanasheria wanawake TAWLA wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho unaofanyika Hyyat Regency jijini Dar es salaam leo.

Mtoa Mada Dr. Elie Waminian Akizungumza wakati akitoa mada wanawake kujiamini katika maisha yao ikiwa ni pamoja na kutokuwa wavivu.

Baadhi ya wanasheria wanawake walioshiriki katika mkutano huo wakifurahia mada zilizokuwa zikitolewa.

Mkurugenzi mtendaji wa Chama cha Wanasheria wanawake Tike Mwambipile akihojiwa na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo

Baadhi ya majaji na wanasheria wakishiriki katika mkutano huo.
Baadhi ya wanasheria wa kutoka TAWLA wakiwa katika mkutano huo.



Na Jonas Kamaleki- MAELEZO

Wanawake wametakiwa kushiriki shughuli za kiuchumi ili kujikomboa na kukandamizwa na mifumo ya kijamii iliyopo sasa nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wanasheria Wanawake nchini (TAWLA), Bi Tike Mwambipile leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa chama hicho.

Bi Mwambipile amesema kuwa wanawake wa Kitanzania wananyanyasisika sana kwani hawana vipato vya kutosha, hivyo inabidi waongeze juhudi katika kuibua na kubuni miradi endelevu ya ujasiriamali ili kukuza vipato vyao.

“Wanawake mnapaswa kujiunga na VICOBA na Saccos ili muweze kupata mikopo yenye riba nafuu kwa ajili ya kufanyia biashara,”alisema Bi Mwambipile akiongeza kuwa kipato kinachopatikana inabidi wanawake wawe na maamuzi ya kukitumia bila kusubiria maelekezo ya waume zao.

Naye Mwenyekiti wa TAWLA, Bi Asia Bade amesema kuwa wakati umefika kwa wanawake kujitambua kuwa ni sehemu muhimu katika jamii hivyo kutumia uwezo wao kujikwamua kiuchumi pasipo kutegemea wanaume.

Bi Bade ameongeza kuwa suala la ushirikishwaji wa wanawake katika shughuli za kiuchumi litawakomboa na utumwa wa kipato ambao umewatesa kwa kipindi kirefu.

Kwa upande wake mjumbe wa Mkutano huo, Dkt. Pindi Chana ameishauri Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuweka sharti la mkakati wa kuwainua wanawake na vijana kwenye mabenki yanayoomba usajili. Ameongeza kuwa bila kuonyesha makakati huo, BOT isitoe kibali kwa benki yoyote.

Dkt. Chana ameonyesha kukerwa na riba za mikopo kuwa juu sana kwa wakopaji na kusema, “Watanzania tunayafanyia mabenki kazi kutokana na riba kubwa wanazotuwekea kwenye mikopo, hii haitunufaishi bali inatutesa katika kurejesha.”

Akionyesha kukerwa na utegemezi wa wanawake, Mjumbe wa Mkutano huo, wakili Mary Kessy amesema ni wakati wa wanawake kuacha kubweteka wakisubiri kupokea kutoka kwa waume zao bali wachangamkie fursa zilizopo ili wawe na kipato cha uhakika.

Bi Kessy amesema kwamba kuna fursa nyingi za kuwainua wanawake kiuchumi ambazo ni pamoja na ushiriki katika shughuli za madini, kilimo, mifugo na uvuvi pia kutumia mabenki ya wanawake.

“Huu sio wakati wa kuchagua kazi, wanawake tujitume, fursa ziko nyingi sana hapaTanzania, kama ni kwenye migodi tuwemo, biashara za kimataifa tufanye na kwenye nafasi za uongozi tujitokeze badala ya kulalamika” amesisitiza Bi Kessy.

Huu ni Mkutano wa 25 ambao unawajumuisha wanawake wanasheria nchini kuweza kubainisha namna ya ushiriki katika shughuli za kiuchumi na kuweka mikakati ya kutoa elimu endelevu ya uzalishaji mali.


KUMBUKUMBU YA MAREHEMU MZEE MAKWAIA

0
0
Ilikuwa siku, miezi na leo hii ni mwaka wa tatu tangu ulipotuacha kwa machungu mengi siku ile ya tarehe 30th May 2013 ukiwa Jaslok Hospital, India. Kimwili haupo nasi bali kiroho tupo nawe, Daima tunamshukuru Mungu kwa muda wote uliokuwa nasi, Sio tu kuwa Baba mwenye upendo bali kwa kuwa ulikuwa mtu wa pekee miongoni mwetu. Uliyebarikiwa kwa mambo mengi, ucheshi wako, hekima na busara zako, na juu ya yote hayo ulikuwa unafanya jambo kwa kusudi maalumu kwa kupenda usawa kwa kila binadamu, na kuwataka watoto wako tuwe na upendo na kutambua umuhimu wa elimu katika familia na jamii.

Tutaendelea kukumbuka na kufuata ushauri wako na mema mengi uliyotufundisha, na daima tutaendelea kukumbuka busara zako Baba na tutaendelea kukuenzi hadi tutakapo kutana tena paradiso.


Daima unakumbukwa sana na mke wako Mama Thecla Makwaia; watoto wako Stella Makwaia, Frank Makwaia, Robert Makwaia na Christopher Makwaia (MK), wajukuu zako Magdalen Christopher Makwaia pamoja na Madeleine Christopher Makwaia, unakumbukwa sana na ndugu zako, marafiki zako, majirani zako wote, wafanyakazi wenzako na Idara mbali mbali ulizowahi kufanyakazi kipindi cha uhai wako.


Tutakukumbuka daima Baba.


PUMZIKA KWA AMANI. AMEN.


*Misa ya kumbukumbu itafanyika tar 29/05/2016 saa 2.30 asubuhi katika kanisa la St. Maximilian Kolbe – Mwenge Afrika Sana.

VIJANA WAHINIZWA KUDUMISHA UZALENDO

0
0
Na Lorietha Laurence

Vijana wamehimizwa kuendeleza upendo na uzalendo katika kutambulisha Taifa la Tanzania ikiwemo kutangaza utamaduni wake kwa mataifa mengine  Barani Afrika na Duniani kwa ujumla. 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Utamaduni wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi, Lilian Beleko jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za kuzindua klabu za Vijana ya Mwalimu Nyerere chini ya usimamizi wa Taasisi ya Ariseamka Afrika ikiwa na lengo la kuwapatia vijana elimu ya msingi kuhusu historia ya ukombozi wa bara la Afrika na masuala mbalimbali ya kijamii.

“Klabu ni jambo jema na zuri kwa vijana wa sasa ukizingatia wengi wao hawakuwepo wakati ukombozi wa bara la Afrika hivyo kupitia klabu hizi mtajifunza mengi” alisema Bi.Beleko.

Aidha aliongeza kuwa viongozi wa Afrika walijitolea kwa moyo mmoja kuonyesha uzalendo kwa kuwaunganisha waafrika katika kupigania uhuru wa bara la hilo ili kuwakomboa kutoka mikononi mwa wakoloni na kuweza kujitegemee kwa kuwa na viongozi wake.

Naye Mwanzilishi wa Taasisi ya Ariseamka Afrika Bi Kulthum Maabad ameleza kuwa ili vijana waweze kujikomboa kutoka katika umaskini ni muhimu kwanza kujikomboa kifikra kwa kupata elimu muhimu ikiwemo ya uzalendo wa kuitumikia nchi zao kwa uaminifu.

Kwa upande wake Msaidizi Maalum wa mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere nchini ameeleza kuwa kuna umuhimu wa kujifunza na kuujua mchango mkubwa uliofanywa na Mwalimu Nyerere katika ukombozi wa bara la Afrika kwa kusoma vitabu vyake na kupitia nukuu zake

Uzinduzi wa klabu za Vijana ya Mwalimu Nyerere umeenda sanjari na kilele cha maadhimisho ya wiki ya ukombozi wa afrika ambapo hukumbukwa kwa kuwaenzi waasisi wa upigania uhuru kwa kuwepo kwa maonyesho mbalimbali ya Sanaa,Lugha na Utamaduni.

MAONESHO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YALIYOANDALIWA NA AGRIPROFOCUS YAFANYIKA UWANJA WA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI.

0
0
Mgeni Rasmi katika maonesho ya Wakulima na Wagaji ,Mkuu wa idara ya Utumishi na Utawala Manispaa ya Moshi,Wencelaus Lindi akisoma hotuba ya ufunguzi wa maonesho hayo yaliyoandaliwa na Mtandao wa kusaidia Wakulima wa AgriProFocus yanayofanyika katika uwanja wa Chuo kikuu cha Ushirika mjini Moshi. 

Baadhi ya vijana walionesha kuvutiwa na kuingia katika shughuli za kilimo wakijaribu kuangalia aina ya mbegu zinazotolewa na East West Seed walipotembelea banda hilo.
Baadhi ya vijana walivutika zaidi katika ufugaji wa kuku wa kisasa mara baada ya kutembelea banda la Brac.

Baadhi ya wananchi wakiwemo wakulima na wafugaji waliohudhuria ufunguzi wa maonesho hayo ya siku Mbili.
Afisa Msaidizi wa  Mtandao wa wadau mbalimbali wanaosaidia wakulima wenye ndoto wa AgriProFocus ,Hildagard Okoth akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Wenceslaus Lindi wakati akitembelea mabanda katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji yanayoendelea katika uwanja wa Chuo kikuu cha Ushirika Moshi.
Afisa Ugavi wa SEVIA,Lewis Mlekwa akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi alipotembelea banda la taasisi hiyo katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji yanayoendelea katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara mjini Moshi.
Bwana Shamba wa kampuni ya Agrichem Africatz Ltd ,Mrisho Yusuph akimuonesha mgeni rasmi baadhi ya mbegu zinazotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya wakulima.
Mgeni rasmi akiwa katika banda la East West Seed akipewa maelezo juu ya aina mbalimbali ya mbegu zinazotolewa na kikundi hicho.
Meneja Mradi mkazi wa Farm Radio International ,Joseph Sarakikya akiomuonesha mgeni rasmi namna radio zinavyoweza kutumika katika kusaidia wakulima .
Afisa mahusiano wa taasisi ya fedha ya Vision Fund ,Elias Mlaki akitoa maelezo kwa mgeni rasmi mara baada ya kutembelea banda la taasisi hiyo.
Baadhi ya wananchi wakiwa wametembelea mabanda mbalimbali kujionea maoensho hayo ya wakulima na wafugaji.
Ndani ya Banda la Brac wanaonesha namna ufugaji wa kuku wa kisasa unavyoweza kumnufaisha mfugaji.
Mabanda mbalimbali yaliyoko katika maonesho hayo.
Mmoja wa wafanyakazi katika banda la East west seed akimvisha kofia mmoja wakulima waliofika kutembelea banda hilo.
Afisa Msaidizi wa Mtandao wa wadau mbalimbali wanaosaidia wakulima wenye ndoto wa AgriProFocus akizungumza na wanahabari mara baada ya uzinduzi wa maonesho hayo.

Imeandaliwa na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog kanda ya kaskazini.

TPRI YATOA ONYO KWA WANANCHI

0
0

NA WOINDE SHIZZA, ARUSHA.


Taasisi ya ukaguzi na uthibiti wa viwatilifu tpri imetoa onyo kwa wananchi, kuwa makini na matumizi ya vyandarua vilivyo ingia nchini kutoka nje ya nchi,  huku vikiwa na alama ya uwepo wa dawa ya kuua mbu lakini havina maelezo ya kulinda afya za watumiaji  na havimo kwenye orodha ya msajili wa viuatilifu.


Msajili wa viuatilifu  dk elikana lekei ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kufuatilia shehena ya vyandarua hivyo kuingizwa nchini, huku vikiwa havina maelezo ya tpri huku akionesha baadhi ya vyandarua  hivyo.


kwa upande wao wazalishaji wa vyandarua wamesema hali hiyo inatokana na vyandarua vya nje kuingizwa nchini bila ushuru na kwamba imeathiri viwanda vya ndani na kulazimika kupunguza zaidi ya wafanyakazi elfu mbili.


BALOZI WA TANZANIA NCHINI KENYA AITEMBELEA TIMU YA TAIFA MAZOEZINI

0
0
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. John Haule akipiga picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa timu ya soka ya Tanzania baada ya kuzungumza nao na kuwatoa hofu ya maisha na usalama wakiwa Nairobi, Kenya. Taifa Stars ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani.
Kipa wa timu ya soka ya Tanzania-Taifa Stars, Deogratius Munishi maarufu kwa jina la Dida, akifanya mazoezi ya kuzuia penalti kwenye Uwanja wa Camp Toyoyo uliopo Jericho, nje kidogo ya jiji la Nairobi. Taifa Stars ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani.
Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania-Taifa Stars, kikifanya dua kwenye Uwanja wa Camp Toyoyo uliopo Jericho, nje kidogo ya jiji la Nairobi. Taifa Stars ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani.
Mshambuliaji Elius Maguri na Kiungo Hassan Kabunda wakipumzika katika mazoezi hayo.
Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania-Taifa Stars, kikikifanya dua kwenye Uwanja wa Camp Toyoyo uliopo Jericho, nje kidogo ya jiji la Nairobi. Taifa Stars ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani. (Picha na Alfred Lucas wa TFF).

SHINDANO LA MAISHA PLUS MSIMU WA 5 LAZINDULIWA RASMI, KUONYESHWA MOJA KWA MOJA NA AZAM TV

0
0
Mkurugenzi wa Azam Media Tido Mhando (Kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maisha Plus East Africa Mkurugenzi wa Maisha Plus East Africa msimu wa 5 ambapo shindano linatarajiwa kuanza hivi karibuni itakapotangazwa ratiba ya kutafuta washiriki wa shindano hili mikoani na nchi zingine za Afrika Mashariki, kulia ni mmoja wa waandaji wa shindano hilo Bw. Masoud Kipanya, Masoud Kipanya ni miongoni mwa waanzilishi wa Maisha Plus na mtangazaji wa kipindi hicho ambacho huandaliwa na kampuni ya DMB Company Limited na mwaka huu inandaa kwa udhamini mkubwa wa Azam Media, Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika jana katika studio za Uhai Productions – Azam, Tabata jijini Dar es salaam.
Joyce Fisoo Katibu Mtendaji wa bodi ya filamu Tanzania akizungumza mawili matatu wakati wa uzinduzi huo kama mgeni mwalikwa lakini pia kama mdau muhimu wa shindano hilo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo
Mmoja wa waandaji wa shindano hilo Bw. David Seburi akizungumza na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya waandaji wa shindano la Maisha Plus kulia Francis Bonga na David Sevuri wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana.Jikho Man na Vitalis Maembe wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana.
Mwandaaji wa shindano hilo Bw. Masoud Kipanya akizungumza na baadhi ya washiriki waliowahi kushiriki katika shindano hilo kulia ni Abdul aliyekuwa mshindi.Aliyewahi kuwa mshindi wa shindano hilo Abdul akizungumza na wageni waalikwa katika uzinduzi huo uliofanyika jana.
Baadhi ya wafanyakazi wa Azam Media wakiwa katika hafla hiyo.
Mwanahabari na Bloger John Bukuku akihojiwa na mtangazaji wa Azam Tv Benerick ambaye pia alikuwa ni mmoja wa washiriki wa msimu uliopita wa Maisha Plus.

SERIKALI YAAHIDI KUVIPATIA MAJI VIJIJI VINAVYOZUNGUKA BOMBA KUU LA MAJI LA ZIWA VICTORIA NA MAENEO YA PEMBEZONI MWA TANZANIA.

0
0
Serikali imesema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 itatekeleza mradi wa maji katika vijiji 100 vilivyo pembezoni mwa bomba kuu la maji linalotoka ziwa Victoria hadi Kahama na Shinyanga ili kuwawezesha wanachi wanaoishi katika vijiji hivyo kupata huduma ya maji safi na salama.

Akizungumza Bungeni mjini Dodoma leo, Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge amesema kuwa mradi wa kuvipatia maji vijiji hivyo utakwenda sambamba na uboreshaji wa huduma ya maji kwenye vijiji 40 vilivyotambulika katika Halmashauri za Misungwi, Kwimba, Shinyanga na Msalala.

Amesema kazi ya kupima na kufanya usanifu wa miradi katika katika vijiji hivyo vya Halmashauri ya Msalala na Shinyanga imeanza na gharama yake imekadiriwa kufikia shilingi bilioni 2.59 huku akiongeza kuwa hadi machi, 2016 ujenzi wa miradi ya maji umekamilika katika vijiji 11 vya Halmashauri hiyo.

Mhe.Lwenge amesema katika mwaka wa bajeti 2016/2017 Wizara yake itakamilisha ujenzi a miradi ya maji katika Halmashauri za wilaya za msalala na Shinyanga na kuanza Usanifu wa miradi hiyo kwenye Halmashauri za Kwimba na Misungwi ambapo kiasi cha shilingi milioni 760.67 kimetengwa kwa kazi hiyo.

Amevitaja baadhi ya vijiji ambavyo sasa wananchi wake wanapata maji safi na salama kufuatia kukamilika kwa miradi hiyo kuwa ni Nyashimbi, Magobeko, Kakulu, Butegwa, Ngihomango, Jimodoli, Kadoto,Lyabusalu ,Mwajiji Ichongo na Bukamna.

Katika hatua nyingine Mhe.Lwenge amesema Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 kwa kushirikiana na Serikali ya Ubelgiji itatekeleza mradi mkubwa wa maji utakakaowawezesha wananchi Laki mbili (200,000) wa Halmashauri zote za mkoa wa Kigoma kupata maji safi na salama.

Amesema mradi huo unatarajia kugharamia kiasi cha Euro milioni 8.8 ambapo kati ya fedha hizo Euro milioni 8 zitatolewa na Serikali ya Ubelgiji na fedha iliyobaki itatolewa na Serikali ya Tanzania.

Ameongeza kuwa vijiji 26 vya kipaumbele vya mkoa wa Kigoma vimeainishwa kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi na kuongeza kuwa wizara yake tayari imeshatenga kiasi cha shilingi bilioni 5.28 zote zikiwa ni fedha za nje kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Pia amesema Serikali katika mwaka wa 2016/2017 wa fedha imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1 kufanyia ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya maji ili kuzipatia maji kata saba za wilaya ya Masasi zenye idadi ya watu 84,082.

Aidha, amesema katika mwaka huo wa fedha serikali itatekeleza mradi wa kutoa maji mto Ruvuma kuyapeleka Mtwara –Mikindani pamoja na vijiji 26 vitakavyopatikana kilometa 12 kutoka eneo la bomba kuu.

Mradi huo utatekelezwa kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya China kwa gharama ya dola za Kimarekani milioni 189.9 ambapo kazi ya ujenzi wa chanzo kutoka mto Ruvuma , Chujio la kutibu maji , nyumba ya kusukuma maji , matanki 26, tanki kuu la ujazo wa lita milioni 30 litakalojengwa eneo la maghamba.

Aidha, vituo vya kuchotea maji 234 na ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji umbali kilometa 63 yatajengwa ili kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 9 hadi lita milioni 120 kwa siku ili kutosheleza mahitaji ya watu na viwanda mbalimbali vinavyojengwa vikiwemo vya Saruji na Gesi.

SERIKALI YAWATOA HOFU WATANZANIA KUHUSU UPATIKANAJI MAFUTA YA NDEGE.

0
0
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege baada ya kugundulika baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege baada ya kugundulika baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongozana na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaamWaziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongozana na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam eneo yalipo matanki ya mafuta ya kampuni ya GAPCO ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege baada ya kugundulika baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni wa Kampuni ya Oryx Energies Godifrey Fernandes akimuonesha Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo baadhi ya maeneo yanapohifadhiwa mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (wa pili mtasari wa kwanza kulia) akiongozana na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta eneo la “Deport” ya PUMA wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta katika leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya madereva wanaosafirisha mafuta ndani na nje ya nchi leo jijini Dar es salaam.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Serikali imewatoa hofu na kuwahakikishia Watanzania na abiria wanaotumia usafiri wa anga nchini kwamba mafuta ya ndege yapo ya kutosheleza matumizi kwa muda wa siku 14 wakati shehena nyingine za mafuta hayo zinaendelea kuingia nchini.

Hayo yamesememwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo alipofanya ziara leo jijini Dar es salaam kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege nchini baada ya kugundua baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.

“Mafuta ya ndege yapo na ndege zitaendelea kufanya safari kama ratiba zao zilivyopangwa na Watanzania msiwe na wasiwasi, tumejiridhisha, mafuta yanatosheleza kwa muda wa siku 14 wakati hatua ya shehena nyingine kuingia nchini zinaendelea” alisema Prof. Muhongo.Ziara hiyo ya Waziri Prof. Muhongo inafuatia kugundulika kwa mafuta ya ndege yaliyoingizwa nchini mapema mwezi Mei mwaka huu, ambayo hayafai kwa matumizi yaliyokusudiwa kutokana na kuchanganywa na mafuta ya petroli.

Aidha, Prof. Muhongo ameitaka kampuni ya Sahara Energy Resources yenye makao yake makuu nchini Nigeria ambayo ndio ilioingiza mafuta hayo nchini, kusimamisha shughuli zake mara moja hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.Imeonekana si mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kuingiza mafuta machafu nchini, hatua iliyomfanya Waziri huyo kuchukua msimamo huo wa Serikali hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.

Akizungumzia hatua hiyo na hali ya mafuta nchini, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Uingizaji Mafuta kwa Pamoja nchini, Michael Mjinja amesema kuwa mafuta ya ndege yapo na yanatosheleza kwa wiki mbili kuanzia sasa.Mjinja aliongeza kuwa wanakuhakikisha uhaba wa mafuta hayo hautokei tena nchini ambapo wanaendelea kushirikiana na kampuni ya Total na SP Rwanda ambazo hadi sasa ndio zenye mafuta safi yanayokubalika kwa matumizi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TIPER iliyoko eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam, Stephane Gay amesema kuwa kampuni yake ina nafasi ya kutosha ya kuyahifadhi mafuta yote ambayo hayastahili kutumika ili matanki na mitambo ya kampuni zote zilizopata mafuta hayo yafanyiwe usafi upya tayari kwa kuweka mafuta safi yanayoingia nchini.

Ziara ya Waziri Prof. Muhongo imehusisha kutembelea matanki ya kampuni tano za mafuta ikiwemo Puma, GAPCO, Oil Com, TIPER pamoja na Kampuni ya Oryx Energies.

NAPE AENDELEA KUKUTANA NA WANANCHI WA VIJIJI VILIVYOPO NDANI YA JIMBO LAKE AAHIDI KUMALIZA AHADI ZAKE MAPEMA MNO

0
0



Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Kilimanjaro kilichopo kata ya Mtumbya ikiwa muendelezo wa mikutano yake ya kila kijiji katika jimbo lake ambapo alizungumzia utekelezaji wa ahadi alizoahidi na kuwahakikishia wananchi hao kuwa ahadi zake zitakamilika mapema mno.

Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiongozana na wakazi wa kijiji cha Kilimanjaro kilichopo kata ya Mtumbya kwenda kujionea maendeleo ya ujenzi wa zahanati.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiangalia maendeleo ya ujenzi wa zahanati ya wanakijiji cha Kilimanjaro kilichopo jimbo la Mtama , wilaya ya Lindi Vijijini.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwasomea wakazi wa kijiji cha Mtumbya vijiji vitakavyopata umeme wa mradi wa umeme vijijini ( REA) awamu ya tatu katika jimbo la Mtama.
Mkazi wa kijiji cha Mtumbya Bw. Subiri Hashimu Saidia akiuliza swali wakati wa mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye na wananchi hao.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na wakazi wakijiji cha Mpenda, Mtama .
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Mpenda ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa barabara ya kutoka Mtama, kupitia Mpenda , Mtumbya kwenda Kilimanjaro mkandarasi ameshapatikana na ataanza kazi hiyo mara moja na kuwahakikishia kuwa pamoja na kuwepo miradi mikubwa ya maji lakini Mpenda na Kilimanjaro watapata visima mapema.

MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA AWATAKA VIJANA KUWA MFANO KATIKA NCHI ZAO

0
0
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro Rodriguez akizungumza katika mkutano wa Baraza Kivuli la Umoja wa Mataifa kuhusu Vijana kutoka nchi nane Afrika uliofungwa jana kwenye makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha .
Mratibu wa Kongamano hilo Marx Chocha akizungumza jambo kwenye mkutano huo.
Vijana wakisikiliza kwa makini mada mijadala iliyokua inatolewa.
Ushiriki wa vijana wa kike ulipewa umuhimu wa kipekee katika mkutano huo na walionesha uwezo wao katika kujadili masuala mbalimbali yakiwemo ajira ,usalama na amani na mabadiliko ya tabia nchi.
Mshiriki kutoka Zanzibar,Asma Omar akipokea zawadi yake baada ya kuibuka mshindi katika kusambaza habari za mkutano kwa njia ya mitandao
Mshiriki kutoka jijini Dar es Salaam,Lilian Kimani akipokea cheti chake baada ya kutambuliwa kufanya vizuri kama mkuu wa Itifaki kwenye mkutano huo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro Rodriguez akimkabidhi mmoja wa vijana cheti cha kutambua mchango wake .
Mshiriki kutoka Zanzibar,Asma Omar akifatilia kwa makini.
Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UN)Hoyce Temu
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro Rodriguez akimkabidhi mmoja wa vijana cheti cha kutambua mchango wake .
Vijana wakiwa wamechangamka kwenye mkutano wa Baraza Kivuli la Umoja wa Mataifa.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro Rodriguez(katikati)akiwa na washindi waliofanya vizuri katika matumizi ya mitandao.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro odriguez(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na vijana kutoka nje ya nchi waliohudhuria mkutano huo.
Spika wa Bunge la Muungano mstaafu,Mzee Pius Msekwa na mke wake,Mama Anna Abdallah .

SERIKALI YATANGAZA KUISAFISHA SEKTA YA ELIMU NA WATUMISHI WA UMMA WENYE VYETI BANDIA.

0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof.Joyce Ndalichako akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Na.Aron Msigwa - DODOMA.


Serikali imetangaza rasmi kuanza kwa kampeni ya kuwashughulikia na kuwaondoa katika utumishi wa umma watumishi wote walioajiriwa katika sekta hiyo wakitumia vyeti bandia .Aidha, imewataka watumishi hao waanze kujitathmini na kuanza kujiondoa wenyewe kabla ya kufikiwa na mabadiliko makubwa ya kusafisha sekta ya elimu na utumishi wa umma yanayokuja nchini. 

Kauli hiyo imetolewa Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof.Joyce Ndalichako wakati wa majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Amesema Serikali ya awamu ya tano imejipanga kufanya mabadiliko makubwa katika Sekta ya Elimu nchini ili kuhakikisha kuwa Elimu inayotolewa katika shule, vyuo na taasisi mbalimbali inazalisha wahitimu wenye sifa na ubora kwa maslahi ya Taifa .Amesema katika kulitimiza hilo Serikali itawachukulia hatua kali za kinidhamu na kisheria watendaji wote walioshiriki na wale wanaoendelea kushiriki kwa namna moja au nyingine kukwamisha maendeleo ya elimu nchini ikiwa ni pamoja na wale waliohusika katika udahili wa wanafunzi wasio na sifa katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Songea.

"Serikali ya awamu ya tano imedhamilia kwa dhati kabisa kuboresha kiwango cha elimu yetu kwa kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa elimu, naomba niwahakikishie kwamba pale panapohitajika kufanyika mabadiliko tutayafanya bila woga" Amesisitiza. 

Amesema katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali za elimu hapa nchini, serikali imejipanga kubadilisha mfumo wa elimu ambao umekuwa ukilalamikiwa kwa muda mrefu na kwamba mabadiliko hayo yatafanyika kwa kuwashirikisha wadau wote wa sekta hiyo.

" Tunapotaka kufanya mabadiliko kwenye mfumo wetu wa elimu tumekubali tumekubali kwamba tuna changamoto, katika changamoto hizi lazima tuwe na mahali pa kuanzia hivyo tunapochukua hatua tunaomba Watanzania mtuunge mkono" Amesisitiza Prof.Ndalichako.Prof.Ndalichako Amesema lengo la Serikali kupitia Wizara yake ni kuhakikisha sekta ya elimu inaboreshwa hapa nchini kwa kuendelea kutoa wahitimu bora wanaokidhi vigezo na viwango katika soko la ajira.

Amesisitiza kuwa mkakati wa Serikali ni kuanza kuwafuatilia wahitimu wote wasio na viwango ambao wako katika maeneo mbalimbali ya ajira huku akisisitiza kwamba elimu ya Tanzania ni sawa na kiwanda kinahitaji malighafi nzuri ili kitoe bidhaa bora.Ameeleza kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kuvikagua vyuo vyote vinavyotoa elimu ya juu kuona kama vinakidhi sifa na vigezo vya kiutendaji ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wale wote wanaowadanganya wananchi na kuwapotezea muda vijana wanaowadahili bila kuzingatia sifa.

"Wizara yangu tunaendelea kufanya mawasiliano na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili tuchukue hatua kwa wote walioichezea sekta hii muhimu, tulichofanya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph kinaendelea kwa vyuo vingine".Akizungumzia suala la Ada elekezi amefafanua kuwa suala hilo linaendelea kutazamwa kwa umakini mkubwa kwa kuwashirikisha wadau husika wa sekta hiyo kwa kulifanyia utafiti kwa kuzingatia changamoto zinazojitokeza.

Ili kukidhi matarajio ya wananchi kuhusu suala la ada elekezi amesema serikali inaendelea kuchukua hatua kwa kulifanyia utafiti kuliangalia na madaraja ya shule binafsi na kuongeza kuwa serikali itaendelea kutumia taratibu zilizowekwa na Ofisi ya Kamishna wa Elimu nchini.Amesema Serikali kupitia Ofisi ya Kamishna wa Elimu inaendelea kulifuatilia kwa karibu suala la ada na michango mingine kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuona kama michango na ada zinazotozwa zinazingatia maslahi ya Taifa.

Prof. Ndalichako amebainisha kuwa ukaguzi utakaofanywa katika shule hizo utajielekeza katika kuangalia uhalali wa michango inayotozwa kwa wanafunzi ikiwemo mchango ya kila muhula ya majengo, ulinzi na mingineyo ambayo imekuwa kero kwa wananchi. Kama Serikali hatuwezi kukubali wananchi kuendelea kutozwa michango ya majengo wakati kigezo kimojawapo cha mtu kuruhusiwa kutoa elimu ni kuwa na majengo, hili halikubaliki na hatutalifumbia macho" Amesisitiza Prof.Ndalichako.

Amewataka wananchi kuelewa kwamba serikali kutotoa ada elekezi haina maana kwamba imejitoa kabisa katika kufuatilia masuala ya elimu hapa nchini bali itaendelea kujenga mazingira mazuri ya kuwawezesha watanzania kupata elimu bora kwa gharama nafuu.Kuhusu ujenzi wa maabara amesema kuwa Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 12 kwa ajili ya kununulia vifaa vya maabara kwa shule zote 1536 ambazo zimekamilisha ujenzi wa majengo ya maabara kote nchini.

Katika hatua nyingine amesema kuwa Serikali katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 itafanya ukaguzi wa vyuo vyote vya Maendeleo ya Jamii kote nchini ili majengo ya vyuo hivyo yaweze kutumika kuanzishia vyuo vya Ufundi Stadi VETA katika wilaya na mikoa ili kuwapatia stadi za kazi vijana waweze kujitegemea kwa kujiajiri wenyewe.

Kwa upande wao baadhi ya Wabunge waliopata nafasi ya kuchangia wakati wa Kupitisha Bajeti ya wizara hiyo wameiomba Serikali kuweka mkazo katika usimamizi wa Sekta ya Elimu nchini ili shule, Taasisi na vyuo vya Tanzania vitoe wahitimu wenye ubora kwa maslahi ya Taifa.

Aidha, wameiomba Serikali kupitia Bajeti hiyo itenge fedha za kutosha kwa ajili ya kuimarisha shughuli za ukaguzi wa shule, kuboresha maslahi na kulipa madai ya walimu pamoja na kuziimarisha Mamlaka za Udhibiti wa Elimu ili ziweze kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images