Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

WAZEE WA KITUO CHA YOMBO, DAR WASAIDIWA NAFANYAKAZI AAR .

0
0

 Ofisa Madai wa Kampuni ya Bima ya Afya ya AAR, Louisa Mwinchumu (katikati) akimkabidhi msaada wa chakula, Hidaya Othuman, mmoja wa wazee wanaohudumiwa na kituo cha wazee cha Yombo Kilakala wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipoenda kutoa msaada kwa wazee hao jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.  Meneja Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya bima ya afya ya AAR Insurance, Hamida Rashid (kulia) akikabidhi zawadi ya nguo, Mzee Filipo Mchopa (katikati) wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipoenda kutoa msaada kwenye kituo cha wazee wa Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki (kushoto) ni Meneja Operesheni wa AAR, Harold Adamson.
 Meneja Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya bima ya afya ya AAR Insurance, Hamida Rashid (kushoto) akimsalimia, Shida Uwesu, mmoja wa wazee wanaohudumiwa na kituo cha wazee cha Yombo Kilakala wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipoenda kutoa msaada kwa wazee hao jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

WAFANYAKAZI wa AAR Insurance Tanzania wametoa msaada wa vyakula, mavazi pamoja na vifaa vya matumizi ya nyumbani kwa kituo cha wazee cha Yombo Kilakala kupitia programu maalum ya kusaidia jamii ijulikanayo kama Jaza Kikapu. Akiongea kwenye makabidhiano ya msaada huo jijini Dar es salaam leo, Meneja Maendeleo ya Biashara wa AAR, Hamida Rashid amesema kwamba kwa muda wa miaka 17 AAR imekuwa na utamaduni wa kuhamasisha wafanyakazi wake kutumia fursa mbalimbali kujitolea kuisaidia jamii hususani makundi ya watu wenye mahitaji maalum kupitia program ya wafanyakazi kujitolea ambapo wafanyakazi hao wamekuwa wakisaidia watu wenye shida mbalimbali. 

 “Sisi AAR Insurance tunataka kuhakikisha tunatoa mchango muhimu kwenye mambo yanayoigusa maisha ya watu ikiwa ni kwa wafanyakazi wetu pamoja na jamii nzima. Tunatazamia kuendelea na uhusiano mzuri na kituo cha wazee cha Yombo Kilakala kwa miaka mingi ijayo.” 

 Rashid alitaja baadhi ya vitu vilivyotolewa msaada kuwa ni pamoja na nguo pamoja na vyombo vinavyotumika kwenye matumizi ya kila siku majumbani ambavyo vilikusanywa kutoka kwa wafanyakazi wa AAR kupitia kampeni yao ya Jaza Kikapu ambapo wafanyakazi walijitolea kutoa vitu mbalimbali kusaidia wenye shida.

 Akizungumzia msaada huu, Meneja Mauzo wa AAR Insurance Tanzania, Bi Tabia Masoud alisema“ni utamaduni wetu kama kampuni kuwajali wateja wetu na jamii iliyotuzunguka kama jinsi tunavyojali familia zetu. Tunafanya hivi ili kuona watu wote katika jamii wakiishi maisha bora.” “Tunaona fahari kuweza kutoa msaada kwa wazee kwani kundi muhimu katika jamii yetu. Wazee hawa wanaishi katika mazingira magumu, hivyo ni matumaini yetu kwamba msaada huu utaleta utofauti katika maisha yao na kuwawezesha kuendelea kufurahia maisha ipasavyo.”

KIKAO KAZI CHA WATENDAJI WAKUU WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, MKOANI DODOMA CHA ONGOZWA NA MASAUNI.

0
0

Watendaji Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakifuatilia kwa makini kikao kazi kilichofanyika chini ya Uenyekiti wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni leo Mei 30, 2016 Mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(Mb) akiongoza kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Kikao hicho kimefanyika leo Mei 30, 2016 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma(kulia) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira.
 Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri w Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Maauni(hayupo pichani). Wa pili kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP, John Casmir Minja(kulia) ni Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, DIGP, Abdulrahmani Kaniki(wa kwanza kushoto) ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Victoria Lembeli(wa pili kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Adengenye.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wafanyika mkoani Mtwara

0
0
Mkuu wa mkoa wa mtwara halima dendego akimbeba mmoja ya watoto waliokabidhiwa chandarua chenye viuwatilifu ikiwa ni sehemu ya hafla ya uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akirusha maputo angani kuashiria uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akimkabidhi chandarua chenye viuwatilifu mmoja ya mama wajamzito ikiwa ni sehemu ya hafla ya uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akimkabidhi chandarua chenye viuwatilifu mmoja ya mama wenye watoto wa chini ya umri wa miezi sita ikiwa ni sehemu ya hafla ya uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Baadhi ya wakazi wa mkoa wa mtwara waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mpango wa kugawa bure vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua.
Baadhi ya watoto wa mkoani mtwara wakishindana kucheza muziki ikiwa ni sehemu ya burudani zilizosindikiza hafla ya uzinduzi wa mpango wa kugawa bure vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua.
Wasanii Joe makini na Niki wa pili kutoka kundi la weusi wakitumbuiza hadhara iliyojitokeza katika uzinduzi wa mpango wa kugawa bure vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua 
Msanii wa nyimbo za taarab isha mashauzi akiimba moja ya kibao chake wakati akitoa burudani kwa wakazi wa mkoa wa mtwara waliohudhuria hafla uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Msanii wa nyimbo za taarab isha mashauzi akitoa burudani kwa wakazi wa mkoa wa mtwara waliohudhuria uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua

Serikali ya Tanzania kwa kushirikana na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya Malaria wameendelea na jitihada za kupambana na ugonjwa huo ili kufikia lengo la serikali la kupunguza vifo hadi kufikia asilimia moja ifikapo mwaka 2020.

Katika kutekeleza azma hiyo, serikali ya Tanzania na wadau hao wamezindua mpango wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu vya muda mrefu kwa akina wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa.

Akizindua mradi huo kitaifa, mkuu wa mkoa wa Mtwara Bi Halima Dendego amewataka wanawake kuhudhuria kliniki wakati wa ujauzito ili kupata ushauri na kinga dhidi ya malaria ikiwa ni pamoja na kupata chandaru kitakacho mkinga dhidi ya ugonjwa huo.Amesisitiza suala la kusafisha ameneo yote ili kudhibiti mazalia ya mbu waenezao Malaria ikiwa ni njia moja wapo ya kupambana na kuenea kwa ugonjwa huo unaosababisha vifo vya wakina mama wajawazito na watoto wa chini ya miaka 5.

“kwa mujibu wa Takwimu za ugonjwa huo kwa mkoa wa Mtwara, zimeshuka kutoka asilimia 33 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 17 kwa mwaka 2011/2012. Hata hivyo takwimu za kitaifa zinaonesha kushuka kwa ugonjwa huo kutoka asilimia 33 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 9 mwaka 2015”. Alisema Bi Dendego.“Lengo la kitaifa la mapambano dhidi ya Malaria linaonesha kupunguza vifo hivyo hadi kufikia asilimia 5 mwaka huu na asilimia 1 mwaka 2020 hivyo sisi mkoa wa Mtwara tuna jukumu la kuhakikisha takwimu zetu zinaenda sambamba na takwimu za kitaifa”. Amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa kutoka ofisi ya Afya ya shirika la misaada la Marekani USAID Bibi Ana Bodipo -Memba amesema, ushirikiano wa serikila ya Marekani na Tanzania katika mapambano dhidi ya Malaria umeonesha mafanikio makubwa kwani wamefanikiwa kupunguza kwa silimia 50 vifo vitokanavyo na malaria kwa upande wa Tanzania Bara na chini ya asilimia moja kwa upande wa Zanzibar.

“Marekani inafahamu umuhimu wa mapambano dhidi ya Malaria, na hivyo mfuko wa Rais wa Kupambana na Malaria kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo hivyo nah ii ni ishara nzuri katika kufikia malengo ya kuutokomeza kabisa ugonjwa huu.” Alisema Bi Bodipo.

Mwakilishi wa wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Bi Helen Semu amesema, serikali itaendelea na uhamasishaji wa jamii kuendelea kutumia vyandarua vyenye viuwatilifu ili asilimia 85 iliyofikiwa kwa sasa izidi kuongezeka na kufikia lengo la kumaliza kabisa tatizo hilo nchini.“Sisi Serikalini tutahakikisha tunaongeza jitihada za kuhamasisha jamii kuendelea kutumia vyandarua vyenye viuwatilifu ili kila mmoja afahamu umuhimu wa kufanya hivyo na kudhibiti maambukizi na vifo vitokanavyo na ugonjwa huu” alisema bi Helen

Mpango wa utoaji vyandarua vyenye viuwatilifu kwa akina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama CHANDARUA KLINIKI unachukua nafasi ya mpango wa zamani wa HATIPUNGUZO na unasimamiwa na Mradi wa VECTORWORK kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania na unfadhiliwa na mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria chini ya usimamizi wa shirika la misaada la nchi hiyo – USAID.

Vijana nchini watakiwa kuwa huru kutoa maoni yao-jk

0
0
Na: Frank Shija, MAELEZO


Vijana nchini watakiwa kuwa huru kutoa maoni yao na wanapo kosea wawe tayari kukosolewa na kukujirekebisha.


Rai hiyo imetolewa na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne  Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa mahafali ya Pili ya Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika jana katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.


Kikwete alisema kuwa vijana wanapaswa kutoogopa kukosea, kwani watu ujifunza kutokana na makosa hivyo ni vyema wakathubutu kufanya mambo kwa kuzingatia misingi, weledi na kwa uwazi huku wakiepuka migawanyiko.Wakati huo huo Kikwete ameahidi kulisaidia Shirikisho hilo kandana ya Dar es Salaam jumla ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya kusaidia katika kutekeleza mradi wao wa kilimo na ufugaji wa kuku.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (CCM) Bi. Zainabu Abdallah alisema kuwa katika kuenzi na kutambua juhudi za Rais msataafu Jakaya Kikwete katika kusaidia Vijana wataanzisha Tuzo maalumu kwa Vijana zitakazo julikana kama “Jakaya Mrisho Kikwete Youth Awards”.Ambapo lengo lake ni kuhamasisha viongozi waendelee kusthamini michango ya vijana katika kukuza na kuendeleza Taifa letu.


Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (CCM) Seneta ya Dar es Salaam linaundwa na jumla ya matawi 34 ambapo katika mahafali hayo ya pili jumla ya wahitimu 640 walitunukiwa vyeti kutambua mchango wao katika kuimarisha uhai wa Chama chao vyuoni.

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, WCF WAENDELEA NA KAMPENI YA KUELIMISHA MADAKTARI KUHUSU FIDIA KWA WAFANYAKAZI WAPATAPO MADHARA KATIKA KAZI

0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Emmanuel Humba, (kulia), akimkaribisha Naibu Waziri wa Kazi Mhe. Anthony Mavunde alipowasilili kufungua mafunzo kwa Madaktari yanayohusu ajali na maginjwa yanayosababishwa na kazi Jijini Arusha Leo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), umeendelea na kampeni yake ya kutoa mafunzo kwa madaktari ili kujenga uelewa wa kufanya tathmini ya ajali na magonjwa ayapatayo mfanyakazi yanayotokana na kazi safari hii ikihusisha madaktari kutoka mikoa mitano ya ambayo ni Arusha Tanga, Manyara, Kilimanjaro na Singida.

Mafunzo hayo yaliyofunguliwa leo Mei 30, 2016 na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Bw. Anthony Mavunde, huko jijini Arusha, ni muendelezo wa mafunzo mengine kama hayo yaliyotolewa wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam, ambapo madaktari kutoka mikoa ya Dares Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, lindi na mtwara walihudhuria. 

WCF imechukua hatua hiyo ili kujiandaa na UTOAJI WA Mafao kwa mara ya kwanza tangu uanzishwe ifikapo Julai mwaka huu wa 2016.
Mgeni Rasmi Mhe. Anthony Mavunde (MB), Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, akisisitiza jambo wakati alipokuwa akifungua Mafunzo kwa Madaktari kujenga uelewa wa kufanya tathmini ya Ajali na Magonjwa ayapatayomfanyakazi yanayotokana na Kazi Jijini Arusha leo Mei 30, 2016
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba akitoa maelezo ya utangulizi na mipango mbalimbali ambayo Mfuko umejiwekea kwa mujibu wa sheria ili kuhudumia wadau wakuu ambao ni wafanyakazi katika sekta ya umma na binafsi
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakinakili kilichokuwa kikizungumzwa kwenye mafunzo hayo
Mwenyekiti wa Bodiya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, akitoa hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi
Mgeni rasmi Bw. Anthony Mavunde, akizungumza na waandishi wa habari ili kufafanua alichozungumza wakati akifungua mafunzo hayo 

ZIARA YA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA LUHWAVI MKOANI MANYARA LEO

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa CCM,-Bara, Rajab Luhwavi akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Manyara, Luccas Ole Mukusu, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa huo, mjini Babati, leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa huo Ndegesu Ndekobali. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM,-Bara, Rajab Luhwavi akisalimiana na baadhi ya watumishi wa CCM mkoa wa Manyara, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa huo, mjini Babati, leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa huo Ndegesu Ndekobali. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akisaini Kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara, baada ya kuwasili mjini Babati leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM wa mkoa huo, Ndegesu Ndekobali. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akisaini Kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara, baada ya kuwasili mjini Babati leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM wa mkoa huo, Ndegesu Ndekobali. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (kulia) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Manyara Joel Bendera alipoenda ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa, mjini Babati leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Afisa Tawala wa mkoa huo, Eliakim Maswi. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (kulia) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Manyara Joel Bendera alipoenda ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa, mjini Babati leo Mei 30, 2016. 
Katibu wa CCM wa mkoa wa Manyara Ndekobali akishukuru baada ya mazungumzo hayo 
wakiagana baada ya mazungumzo 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akiagana na Afisa Tawala wa mkoa wa Manyara Eliakim Maswi baada ya mazungumzo na mkuu wa mkoa huo Joel Bendera (Katikati), alipoenda ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa, mjini Babati leo Mei 30, 2016.

AKAGUA JENGO LA OFISI YA CCM LILILOUNGUA MWEZI MACHI MWAKA HUU 










Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (kulia) apata maelezo kutoka kwa Katibu wa CCM mkoa wa Manyara, Ndegesu Ndekobali, alipokagua athari za kuungua jengo la CCM mkoa huo, lililopo mjini Babati. Jengo hilo liliungua Machi 7 mwaka huu. 








Luhwavi akimaliza kukagua jengo hilo 






Baadhi ya viongozi wa CCM wakimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajabu Luhwavi kuzungumza nao leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara mjini Babati 






Luhwavi akiingia ukumbini 






Luhwavi akiwa tayari ukumbini 






Katibu wa CCM wa mkoa wa Manyara, Ndekobali akitoa neno la utangulizi 






Baadhi ya watunishi wa CCM kutoka wilaya za mkoa wa Manyara wakimsikiliza Luhwavi 






Masoud Mbengua kutoka Kitengo cha Usalama na Maadili, Makao Makuu ya CCM akizungumza kwenye kikao hicho 






Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Manyara akimkaribisha Luhwavi kuzungumza 






Baadhi ya wafanyakazi wakichukua dondoo, wakati Luhwavi akizungumza nao. (Picha zote na Bashir Nkoromo 



Rais Magufuli ateua Jaji wa Rufani, Mwenyekiti wa NHIF na Mwenyekiti wa DIT

0
0
Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhe. Jaji Shabani Ally Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Kabla ya uteuzi huo Mhe.  Jaji Shabani Lila alikuwa Jaji Kiongozi.

Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.


Wakati huo huo, Rais Dkt. Magufuli amemteua Mhe. Anne Semamba Makinda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).Uteuzi wa Mhe. Anne Semamba Makinda  ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza tarehe 25 Mei, 2016.

Mhe. Anne Semamba Makinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Ali Mchumo.Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Prof. Apollinaria Elikana Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (Dar es salaam Institute of Technology - DIT).

Prof. Apollinaria Elikana Pereka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro.Prof. Pereka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Fredrick Mwanuzi ambaye amemaliza muda wake.

Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.



Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam


30 Mei, 2016

Jela miaka 3 kwa kuomba na kupokea rushwa

0
0
Frank Mvungi

Mahakama ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita imemtia hatiani Mgambo wa Mahakama ya mwanzo Buseresere Bw. Majaliwa Revelian Gwakilala kwa makosa ya kuomba na kupokea Rushwa kinyume na kifungu cha 15 (1 na 2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kesi dhidi ya Mtuhumiwa huyo ilifunguliwa mnamo tarehe 14/1/2016.

Akisoma hukumu mbele ya mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Augustino Mtaki, Hakimu Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo Mh. Mh. Jovith Kato alisema kuwa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mwendesha Mashitaka umethibitisha pasipo shaka yoyote kuwa Mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

Ilisisitiza Sehemu ya Taarifa hiyo kuwa kwa mujibu wa ushahidi Mtuhumiwa aliomba kiasi cha Tshs. 300,000/= na kupokea kiasi cha Tshs. 100,000/- kutoka kwa Bw. Reuben Francis Ndimila ili asimkamate mtuhumiwa aliyeruka dhamana. Taarifa hiyo imeongeza kuwa Mahakama ilimtia hatiani Mtuhumiwa katika makosa hayo mawili ya kuomba na kupokea hongo.

Aidha Mh. Kato akitoa adhabu kwa Mshitakiwa alisema, Mshitakiwa anatakiwa kutumikia kifungo cha miaka Mitatu (3) jela au kulipa faini ya Tshs. 600,000/= kwa kila kosa. Mshitakiwa amepelekwa jela kuanza kutumikia adhabu hizo kama zilivyotolewa. Kesi hiyo ilisajiliwa mahakamani hapo kama kesi ya Jinai Na. 18/2016 na kusikilizwa na Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo. 

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa GEITA Bw. Thobias Ndaro ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Chato kutoa taarifa mbalimbali za vitendo vya Rushwa na ubadhilifu katika miradi mbalimbali ya maendeleo na maeneo mengineyo ili watuhumiwa waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

BASATA, HAANNEEL WAZINDUA MATUKIO YA SIKU YA MSANII KWA MWAKA 2016

0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Haakneel Production Emmanuel Mahendeka ambayo ni waandaaji wa Siku ya Msanii akimwongoza Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel kutia saini kitabu cha wageni wakati alipowasili kuzindua matukio ya Siku ya Msanii (SYM, 2016) kwa mwaka 2016 kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise mwishoni mwa wiki. 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ndilo mbunifu na mmiliki wa maadhimisho ya Siku ya Msanii nchini Godfrey Mngereza (Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bi. Leah Kihimbi (Katikati) na Mkurugenzi wa Kampuni mwendeshaji wa Siku ya Msanii ya Haakneel Production Emmanuel Mahendeka mwishoni mwa wiki kwenye uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016 katika Ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar es Salaam.
Msanii maarufu wa kughani mashairi nchini Mrisho Mpoto akisaini kitabu cha wageni kabla ya kushuhudia hafla ya uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise ulioko jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Sanaa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bi. Vivian Shalua (Kushoto) akifuatilia kwa makini moja ya matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye hafla ya uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016 kwenye Ukumbi wa Alliance Francoise mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Msanii wa Sanaa za Ufundi Gozbetha Rwezaula.
Marais wa Mashirikisho manne ya Sanaa nchini kutoka kushoto Symon Mwakifamba (Filamu), Adrian Nyamangale (Ufundi), William Chitanda maarufu kama MC Chitanda (Sanaa za Maonesho) na Addo November (Muziki) wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali ya uzinduzi wa matukio ya Siku ya Msanii mwaka kwa mwaka 2016
Kikundi cha Sanaa cha Safari kikitoa burudani kwenye hafla ya Uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016 iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar es Salaam
Msanii maarufu wa Sanaa za Uigizaji na Filamu Ahmed Olutu maarufu kama Mzee Chiro akitabasamu na Msanii mwenzie Thecra Mjata wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016 uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio ya hafla ya uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016

MKURUGENZI WA SMART CODES TANZANIA ATAJWA KWENYE ORODHA YA FORBES AFRICA.

0
0
Bwana Edwin Bruno, mjasiriamali wa Kitanzania, mshindi wa tuzo ya kijana mwenye mafanikio 2015, mwanzilishi na mkurugenzi wa kampuni ya Smart Codes (www.smartcodes.co.tz) ametajwa katika jarida la Forbes Africa. Kila mwaka, jarida hilo hutoa orodha ya vijana 30 wenye umri chini ya miaka 30 ambao wana nafasi ya kuwa mabilionea wa baadaye.

Majina hayo yalikusanywa na kuandaliwa na mhariri wa Forbes Afrika, Ancillar Mangena ambaye naye ana chini ya miaka 30. Katika ujumbe wake, anaandika “Orodha inawakilisha vijana ambao tunaamini wana uwezo wa siku moja kuwa kwenye ukurasa wa mbele wa jarida la FORBES AFRICA, ikimaanisha watakuwa na thamani halisi ya si chini ya dola za kimarekani milioni 200, wameajiri maelfu ya watu na kusaidia kukua bara la Afrika.”

Katika mazungumzo mafupi na Edwin Bruno, anasema “Nimepewa heshima kubwa kuwa kwenye orodha hiyo, hata hivyo hii inatokana na juhudi za timu nzima pale Smart Codes. Ni wao ndio wanaofanya kazi kubwa, ambayo inaonekana ndani nan je ya nchi”

Kuhusu mafanikio yake mengine, Bruno anasema “ Ni kweli, mwaka jana programu yetu ya m-paper, ambayo inakupa nafasi ya kusoma magazeti ya Tanzania…sio vichwa vya habari, ila gazeti lote kutokea ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho kwenye simu yako au kompyuta ilishinda tuzo ya Best Educatinal Innovation Africa, au kwa Kiswahili tuzo ya uvumbuzi bora wa kielimu barani Afrika.”

Bwana Bruno alimalizia kwa kuonesha furaha yake na kuwasihi vijana wengine kufanya kazi kwa kujituma ili waweze kufikia malengo yao au kama yale aliesema mhariri wa Forbes Africa Ancillar, kusaidia kukua kwa bara la Afrika kiuchumi.

YALIYOJILI KATIKA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO LEO MJINI DODOMA

0
0
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson Mwansasu akiongoza kikao cha 32 cha Mkutano wa tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
  Baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati wa 
kikao cha 32 cha Bunge hilo mjini Dodoma
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla akijibu maswali ya wabunge kuhusu sekta ya Afya Bungeni mjini Dodoma.
 Mbunge wa jimbo la Ukonga (CHADEMA) Mhe. Mwita Mwikwabwe akisoma kitabu cha Kanuni za Kudumu za Bunge ndani ya Ukumbi wa Bunge.
  Mbunge wa Nzega Mhe. Hussein Bashe (CCM) akizungumza jambo na Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kulia) nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirishwa kwa kikao cha 32 cha mkutano wa tatu wa Bunge leo mjini Dodoma.
 Wanafunzi wa shule ya Sekondari Barbro Johansson iliyoko jijini Dar es salaam wakiondoka ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Sulemani Jafo akijibu maswali ya wabunge yaliyoelekezwa kwenye wizara yake Bungeni mjini Dodoma.
 Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa wamesimama ndani ya ukumbi wa Bunge kufuatia Naibu Spika wa Bunge hilo Mhe. Tulia Ackson kutangaza kuliahirisha Bunge leo mjini Dodoma.

 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Suzan Kolimba nje ukumbi wa Bunge.
 Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akizungumza jambo na wabunge leo mjini Dodoma.
 Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kushoto) akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
 Mbunge wa Kigoma Mhe. Peter Selukamba akijadiliana jambo na  Mbunge wa Nzega mjini Mhe. Hussein Bashe (kushoto)Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu nje ya Ukumbi wa Bunge mjini.
Kikao cha 32 cha Mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania asubuhi.
 Wabunge wakiondoka ndani ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya Naibu Spika kutangaza kuahirisha shughuli za Bunge leo.
 Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kushoto) akimweleza jambo Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. PICHA/Aron Msigwa na Fatma Salum - DODOMA

WAZIRI MKUU ANATARAJIWA KUFUNGUA MKUTANO WA KULINDA URITHI WA DUNIA.

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix  (katikati)  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha leo ambako May 31, 2016 anatarajiwa kufungua mkutano wa  Kimataifa wa 'Africa  World Heritage' kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha -AICC. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Na Woinde Shizza,Arusha
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa kesho  anatarajiwa kufungua mkutano wa kulinda urithi wa dunia wa Afrika kama nyenzo ya maendeleo endelevu  utakao fanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa AICC jijini Arusha unaotarajiwa kufanyika kwa siku nne .

Akiongea na waandishi wa habari katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi wakati akiongea na waandishi wa habari jijini hapa juu ya maandalizi ya mkutano huo ambao umeandaliwa kwa ushirikiano wa serekali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na shirika la UNESCO  nakituo chake cha urithi wa dunia.

Alisema kuwa madhumuni ya mkutano huo ni kutambua changamoto na mambo ambayo yanatishia  na kuadhiri uhifadhi bora wa maeneo ya urithi wa dunia katika afrika .

Aidha mkutano huo utapendekeza suluisho kwa kupitia upya shughuli zinazotekelezwa katika eneo la urithi wa dunia na kuangalia mchango wa miradi ya jamii za kiafrika na kuandaa muelekeo wa miaka kumi ijayo.
Milanzi alisema kuwa mkutano huo utapendekeza suluhisho kwa kushawishi wanawake kuongeza ushiriki wao katika miradi inayoendana na uhifadhi wa urithi na maendeleo endelevu pamoja kuchunguza jinsi mitafaruku inayotokea kwenye maeneo urithi wa dunia  kutokana na makundi ya kigaidi na kutunza amani utamaduni na uridhi asilia.

Aliongeza kuwa pia  mkutano huo umejikita kwenye sera ya UNESCO  ya mwaka 2015 inayohusu kujumuisha maendeleo endelevu kwenye mkataba wa uridhi wa dunia.

“mkutano huo pamoja na matokeao tegemewa kisayansi, pia uatakuwa na manufaa kwa taifa na sio tu kuitangaza Tanzania kutalii na kisasa bali pia ni fursa muhimu ya kiuchumi kutokana na idadi ya wageniwatakao uthudhuria  mkutano huu pamoja na kuanzisha mitandao wa kitaaluma na kujenga mataji wa kijamii”alisema Malinzi


Aidha pia mara baada ya mkutano huu na kupata muafaka wa yote kutakuwa na tamko lililotokana na majadiliano yaliyokuwa yakifanyika siku zote za mkutano na tamko hili linatarajiwa kutolewa katika hifadhi ya taifa ya Ngorongoro.

KONGAMANO LA KUKARIBISHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI LAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Mmakamu wa Rais mstaafu Dr Mohammed Gharib Bilal akizungumza wakati wa kufungua rasmi kongamano la nane la kukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani liloandaliwa na kalamu education foundation (kef), katika ukumbi wa julius nyerere convention centre jijini dar es salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa benki ya Amana Dr.Muhsin S.Masoud akitoa neno kwa wageni waalikwa, ambapo amana bank ni wadhamini wakuu wa kongamano hilo.
Mke wa imam Qasim - Hasaina M.khan katika kongamano la nane la kukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani lililofanyika jijini dar es salaam, kushoto kwake ni mtwangi. 
Baadhi washiriki wa Kongamano hilo
Makamu wa Rais mstaafu Dr Mohammed Gharib Bilal (wa pili kushoto) akimkabidhi zawadi imam qasim ibn ali khan kutoka marekani (kushoto), wanaoshuhudia ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi na rais wa kef mohamed kamilagwa(kulia) pamoja na mkurugenzi mtendaji wa benki ya amana dr.muhsin s. masoud(wa pili kulia)
Imam Qasim Ibn Ali khan kutoka Marekani akitoa mada wakati wa kongamano la nane la kukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani liloandaliwa na kalamu education foundation (kef), jana jijini dar es salaam.
Baadhi ya Washiriki wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye kongamano hilo

TIMU SITA KUPANDA DARAJA LA PILI TAIFA IFIKAPO JUNI 6.

0
0
MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) msimu wa 2015/2016 inaendelea vizuri katika vituo vinne vya Kagera, Morogoro, Singida na Njombe ambapo itafikia tamati Juni 6 mwaka huu.

Timu sita zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu wa 2016/2017. Timu hizo ni zile zitakazoongoza kila kundi, na washindwa bora (best losers) wawili kutoka makundi mawili tofauti.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeweka waangalizi wake katika kila kituo, na litawachukulia hatua watu wote watakaobainika kutumia michuano hiyo kuchafua viongozi.

Mtwivila City ya Iringa inaongoza kituo cha Njombe ikiwa na pointi sita baada ya kucheza mechi tatu. Katika kituo hicho kesho (Mei 31) kutakuwa na mechi kati ya Jangwani FC ya Rukwa na Nyundo FC ya Katavi kwenye Uwanja wa Amani, kituo cha Morogoro ni Namungo FC ya Lindi yenye pointi saba kwa mechi tatu. Kesho Mei 31 ni mechi kati ya Makumbusho FC na Sifapolitan, zote za Dar es Salaam itakayofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Kitayose ya Kilimanjaro inaongoza kituo cha Singida ikiwa na pointi tisa baada ya kushinda mechi zote tatu ilizocheza na kesho Mei 31 kwenye kituo hicho kutakuwa na mechi kati ya Stand FC ya Tabora na Murusgamba ya Kagera itakayochezwa Uwanja wa Namfua na mpaka sasa vinara wa Kituo cha Kagera ambacho mechi zake zinachezwa Uwanja wa Vijana mjini Muleba ni Mashujaa FC ya Kigoma yenye pointi saba.

MKURUGENZI WA SMART CODES TANZANIA ATAJWA KWENYE ORODHA YA FORBES AFRICA.

0
0
Bwana Edwin Bruno, mjasiriamali wa Kitanzania, mshindi wa tuzo ya kijana mwenye mafanikio 2015, mwanzilishi na mkurugenzi wa kampuni ya Smart Codes (www.smartcodes.co.tz) ametajwa katika jarida la Forbes Africa. Kila mwaka, jarida hilo hutoa orodha ya vijana 30 wenye umri chini ya miaka 30 ambao wana nafasi ya kuwa mabilionea wa baadaye.

Majina hayo yalikusanywa na kuandaliwa na mhariri wa Forbes Afrika, Ancillar Mangena ambaye naye ana chini ya miaka 30. Katika ujumbe wake, anaandika “Orodha inawakilisha vijana ambao tunaamini wana uwezo wa siku moja kuwa kwenye ukurasa wa mbele wa jarida la FORBES AFRICA, ikimaanisha watakuwa na thamani halisi ya si chini ya dola za kimarekani milioni 200, wameajiri maelfu ya watu na kusaidia kukua bara la Afrika.”

Katika mazungumzo mafupi na Edwin Bruno, anasema “Nimepewa heshima kubwa kuwa kwenye orodha hiyo, hata hivyo hii inatokana na juhudi za timu nzima pale Smart Codes. Ni wao ndio wanaofanya kazi kubwa, ambayo inaonekana ndani nan je ya nchi”

Kuhusu mafanikio yake mengine, Bruno anasema “ Ni kweli, mwaka jana programu yetu ya m-paper, ambayo inakupa nafasi ya kusoma magazeti ya Tanzania…sio vichwa vya habari, ila gazeti lote kutokea ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho kwenye simu yako au kompyuta ilishinda tuzo ya Best Educatinal Innovation Africa, au kwa Kiswahili tuzo ya uvumbuzi bora wa kielimu barani Afrika.”

Bwana Bruno alimalizia kwa kuonesha furaha yake na kuwasihi vijana wengine kufanya kazi kwa kujituma ili waweze kufikia malengo yao au kama yale aliesema mhariri wa Forbes Africa Ancillar, kusaidia kukua kwa bara la Afrika kiuchumi.

MFUKO WA PENSHENI WA PPF WAHIMIZA WAKAZI WA TANGA KUJIUNGA NA MFUMO WA WOTE SCHEME

0
0
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles John Mwijage akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Mfuko wa Pensheni wa PFF mara baada ya kufungua maonyesho ya biashara ya kimataifa ya Tanga yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwakidila jijini 
Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mkoa wa Tanga, Jabir Bundile akiwa kwenye banda lao lililopo kwenye maonyesho hayo.
Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mkoa wa Tanga, Jabir Bundile wa pili kulia akitoa elimu kwa mkazi wa Tanga namyanatolewa na mfuko huo.

 WAKAZI wa Mkoa wa Tanga wametakiwa kutumia fursa ya kujiunga na Mfumo wa wote scheme unaotolewa na Mfuko wa Pensheni PPF ili kuwawezesha kukithi mahitaji kwa sababu unalengo kuu la kutambua mchango wa ushiriki kwenye sekta isiyo rasmi katika kuinua uchumi.

Hayo yalisemwa jana na Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mkoa wa Tanga, Jabir Bundile wakati alipozungumza na gazeti hili katika maonyesho ya nne ya biashara ya kimataifa ya Tanga yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwakidila jijini hapa ambapo alisema mfumo huo utasaidia kufikia wananchi wengi.

Alisema kuwa fao hilo likuwa likitoa fursa mbalimbali kwa wafanyakazi waliopo kwenye sekta iliyo rasmi na isiyorasmi ili kuwawezesha kunufaika na mfumo huo kwa ajili ya kukuza shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa mustakabali wa maendeleo yao. 

“Niwaambieni kila mtu au kikundi chenye mlengo wa kiuchumi kilichopo kwenye sekta isiyorasmi kama vile wakulima, wafugaji, wavuvi, mama lishe, waendesha pikipiki, wajasiriamali wadogo wadogo kwa lengo la kuhakikisha wananufaika kupitia mfumo huo “Alisema. 

Aliongeza kuwa pia mfumo huo unawagusa wasanii, wana michezo, wachimbaji madini wadogo wadogo wanaweza kujiunga na mfumo huo kwa lengo la kupata manufaa yanayotokana na mfuko huo. 

Sambamba na hilo pia alisisitiza uwepo wa mafao yanayotolewa na mfuko huo kuwa ni ule wa Afya, Fao la Uzeeni, Mkopo wa elimu ambao unalengo la wanachama kukopa na kujiendeleza kielimu na PPF na mkopo ambao unakuwezesha kutimiza ndoto yako. 

Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

MKUU WA MKOA WA DODOMA, JORDAN RUGIMBANA KUKAGUA MAENDELEO YA UTENGENEZAJI WA MADAWATI WILAYANI CHEMBA NA KONDOA.

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (aliyevaa sweta) akikagua maendeleo ya utengenezaji madawati kwenye karakana zinazotengeneza madawati  ya wilaya za chemba na kondoa Mei 30, 2016.  
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (wa pili kutoka kulia walio kalia dawati) akikagua ubora wa madawati yanayotengenezwa na wilaya ya Chemba kwa lengo la kutekeleza agizo la Mhe. Rais la kumaliza tatizo la uhaba wa madawati Mei 30, 2016.
Mafundi wakiendelea na kazi ya utengenezaji madawati ya Wilaya za Chemba na Kondoa kama walivyokutwa Mei 30, 2016 wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kukagua maendeleo ya utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kumaliza tatizo la uhaba wa madawati.
(Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma)

WATOTO MILIONI 2.7 WAMEDUMAA KUTOKANA KUKOSA LISHE BORA.

0
0

 Baadhi ya Vyakula Lishe ambavyo vinatakiwa kwa kila mlo ambavyo vinatakiwa kila mtu anapokula.
 Mchungaji wa makanisa ya Kipentekoste, Sixtus Mallya akichangia mada hasa kwenye imani za dini kukataza baadhi ya vyakula na kusema kuwa vyakula hivyo vimekatazwa na Biblia amesema kuwa lishe ni kitu cha mhimu kwa ukuaji wa mwili.
Mkurugenzi wa Jukwaa la Lishe Tanzania (Panita), Tumaini Mikindo akizungumza na viongozi wa dini jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Lishe nchini.


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WATOTO milioni 2.7  sawa na asilimia 35   wana udumavu kutokana na kukosa lishe hali inayofanya  serikali kupoteza pato la taifa  katika kuhudumia watoto hao.



Utadumavu huo umepungua kutoka asilimia 42  mwaka 2010 hadi kufikia asilimia 35  mwaka 2015.

Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa dini katika suala lishe, Mkurugenzi wa Jukwaa la Lishe Tanzania (Panita), Tumaini Mikindo amesema viongozi wa dini wana umuhimu kuwa mabalozi wa kuhamasisha lishe katika ngazi ya familia katika nyumba za ibada.



Amesema kuwa  kiwango cha watoto waliodumaa hawawezi kurekebishika kutokana na kuadhiri maumbile ya mtoto pamoja na kinga yake kuwa  duni kwa ugonjwa wa utapiamlo.



Mikindo amesema kuwa suala la lishe haliangaliwi huku likiwa linaadhiri maendeleo ya familia kutokana na malezi ya mtoto aliyedumaa ni tofauti na mtoto asiyedumaa.



Nae Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Pazi Mwinyumvua amesema kuwa wanawake wanashindwa kunyonyesha watoto kwa sababu kulinda maumbile kwani mwanamke akinyonyesha kuwa maziwa yanaanguka.



Mwinyimvua amesema wanashindwa kula chakula na mbogamboga kwa madai kula mboga mboga ni suala la watu wenye kipato cha chini.



kusababisha ukuaji wao.

SEKTA YA MAWASILIANO WANAOANDAA MKAKATI WA KITAIFA WA USALAMA KWENYE MTANDAO.

0
0

Mtaalamu Mwelekezi wa Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya madola Dkt. Martin Koyabe akitoa mada kuhusu uandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mitandao. 
 Wadau wa Sekta ya Mawasiliano wanaoandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mtandao wakiwa katika picha ya pamoja.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Injinia Clarence Ichwekeleza akifungua Semina ya wadau na wataalamu kutoka Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya Madola (hawapo pichani) kuhusu Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mtandao nchini.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

SERIKALI YAANZA KUTUMIA TEHAMA KUENDESHA MCHAKATO WA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA.

0
0
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira Bi. Riziki Abraham (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari Leo jijini Dar es salaam kuhusu utaratibu mpya wa kutumia teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kutangaza nafasi za kazi,kupokea maombi,kuwaita kwenye usaili waombaji wa kazi na kuwapa taarifa za kazi na kuwawezesha waombaji kupata ajira kwa kutumia mfumo huo (TEHAMA).Kulia ni Kaimu Naibu Katibu wa Sekretarieti hiyo anayeshughulikia TEHAMA Bi. Mtage Ugullum.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira uliofanyika leo jijini Dar es salaam Ukilenga kutoa taarifa kuhusu matumizi ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kuendesha mchakato wa ajira katika utumishi wa umma.(Picha na Idara ya Habari Maelezo)

Frank Mvungi-Maelezo.

Serikali imeanza kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ( TEHAMA) katika kutangaza nafasi za kazi,kupokea maombi,kuwaita waombaji kazi kwenye usaili na kuwawezesha kutumia teknolojia hiyo kupata ajira.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira Bi Riziki Abraham wakati wa mkutano na Vyombo vya Habari uliolenga kueleza mikakati ya Serikali kuboresha mfumo wa kupokea maombi ya ajira na kuyashughulikia.

“Sekretarieti ya Ajira inatoa rai kwa waombaji fursa za Ajira kujisajili katika mfumo wa Ajira unaopatikana kupitia anuani ya tovuti ya www.ajira.go.tz na mfumo wa” job alert system” au kupitia simu za kiganjani kwa kupiga *152*00# ili kuomba fursa za ajira zinazopatikana” Alisisitiza Riziki.

Akifafanua kuhusu faida za kutumia TEHAMA kuendesha mchakato wa ajira, Riziki amesema kuwa mfumo huo unasaidia kupunguza idadi ya siku za kuendesha mchakato wa ajira kutoka siku 90 hadi 52 kwa sasa.Aliongeza faida nyingine kuwa ni Serikali inapanua wigo wa utoaji taarifa za uwepo wa fursa za Ajira hasa kwa waombaji wa ajira waishio vijijini.

Alisema mfumo huu unalenga kupunguza changamoto kadhaa zikiwemo malalamiko ya baadhi ya waombaji fursa za ajira kuhusu upotevu wa maombi yao ya kazi.Hadi kufikia Mei, 2016 jumla ya waombaji wa fursa za Ajira waliokuwa wamejiandikisha kwenye mfumo wa utumaji maombi ya kazi walikuwa (97,765).

Aidha jumla ya waombaji wa fursa za Ajira 89,484 wamejiunga kwenye mfumo wa kupata taarifa za uwepo wa fursa za Ajira kupitia simu za kiganjani.
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images