Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 859 | 860 | (Page 861) | 862 | 863 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Katibu Mkuu kiongozi Dkt. John Kijazi katikati akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani katika hafla fupi ya kupokea msaada wa magodoro 50 kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya pentekoste iliyofanyika katika hospitali ya Mwananyamala wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi na wa kwanza kushoto ni katibu Tawala wa Mkoa Bi. Theresia Mbando.
  Katibu Mkuu kiongozi Dkt. John Kijazi katikati akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi na wa kwanza kulia na wa kwanza kushoto ni katibu Tawala wa Mkoa Bi. Theresia Mbando kuelekea wodini kusalimia wagonjwa wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa magodoro 50 kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya pentekoste iliyofanyika katika hospitali ya Mwananyamala .
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi wa kwanza kushoto akimsikiliza mmoja wa wagonjwa wanaotibiwa katika hospitali ya Mwananyamala akitoa kero zake kuhusu hospitali hiyo wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa magodoro 50 kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya pentekoste iliyofanyika katika hospitalini hapo.
  Wananchi wakitoa malalamiko yao kuhusu huduma zinzotolewa Hospitali ya Mwananyamala mbele ya Katibu Mkuu kiongozi Dkt. John Kijazi na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi hawapo pichani wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa magodoro 50 kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya pentekoste iliyofanyika katika hospitalini hapo.
  Wananchi wakitoa malalamiko yao kuhusu huduma zinzotolewa Hospitali ya Mwananyamala mbele ya Katibu Mkuu kiongozi Dkt. John Kijazi na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi hawapo pichani wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa magodoro 50 kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya pentekoste iliyofanyika katika hospitalini hapo.
  Baadhi ya magodoro yaliyopokelewa hospitalini hapo.


  Na Ally Daud-maelezo

  Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. John Kijazi ameutaka uongozi wa hospitali ya Mwananyamala kuhakikisha kuwa dawati la malalamiko kwa wagonjwa linafanya kazi masaa 24 ili kuboresha huduma katika hospitali hiyo.

  Akizungumza katika hafla ya kupokea msaada wa magodoro Dkt. Kijazi amesema kuwa wagonjwa wanatakiwa kuhudumiwa kwa wakati na kusikilizwa malalamiko yao muda wote wanapopatwa na changamoto hospitalini hapo ili kuweza kuboresha huduma kwa watanzania.

  “Nimepata malalamiko kutoka kwa wananchi ambao walipata matatizo usiku wa kuamkia leo na hakukuwa na mtu wa kuwasikiliza kwa wakati na kushindwa kupata huduma bora walipokuwa na shida hivyo naagiza uongozi kuhakikisha dawati la malalamiko kufanya kazi masaa 24 ili kuondoa kero za Wagonjwa wote”.alisema Dkt Kijazi.

  Aidha Dkt. Kijazi ameushukuru uongozi wa Umoja wa Makanisa ya Pentekoste kwa kutoa msaada wa magodoro 50 yenye thamani ya shilingi milioni 1.631 ili kuendeleza huduma bora kwa wagonjwa wa Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.

  Akipokea msaada huo Dkt. Kijazi alisema kuwa anawaomba viongozi wa Umoja huo na taasisi zingineziendelee na moyo wa kuchangia kwenye shughuli za kijamii kadriwanavyoweza ili kuifikisha Tanzania salama katika kilele cha mafanikio.

  “Nawaomba Umoja wenu, taasisi na wadhamini mbalimbali kuweza kusaidia kuinua na kukuza huduma bora za kijamii ikiwemo mahospitalini ili kusaidia serikali kupiga hatua katika kupambana na changamoto ya vifaa zinazoikabili hospitali ya Mwananyamala” aliongeza Dkt. Kijazi.

  Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi amesema kuwa ana Imani na Serikali ya awamu ya tano katika kutatua kero za wananchi hususani katika Wilaya yake kwani ameshaona mfano wa kupokea msaada huo na kuungwa mkono na Katibu Mkuu Dkt. John Kijazi kwa kushirikiana vizuri kwenye shughuli hiyo.

  “Nafurahi kukutana na kushirikiana kwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi katika shughuli za kijamii hususani katika hili la kuendeleza huduma bora zitolewazo na hospitali ya Mwananyamala ili kuifikisha mbali Tanzania mpya” alisema Bw. Hapi.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), na wadau wa Sekta ya Mawasiliano (hawapo pichani), wakati uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es Salaam.
  Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Edwina Lupembe akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, katika hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dkt. Kamugisha Kazaura akielezea mafanikio ya TTCL kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizindua nembo mpya ya Kampuni ya Simu ya Tanzania (TTCL), jijini Dar es Salam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dkt. Kamugisha Kazaura, wakati wa halfla ya uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), wakifatilia sherehe za uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es Salaam.


  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya (TTCL), kuwa wabunifu ili kuhimili ushindani wa soko katika sekta ya mawasiliano na hivyo kuiwezesha kampuni hiyo kupata faida.

  Akizungumza wakati akizindua nembo mpya ya kampuni ya TTCL na huduma ya 4G LTE inayowezesha huduma ya mawasiliano ya sauti na data kwa haraka Prof. Mbarawa amesema huu ni wakati wa kubadili mtazamo na kufanya kazi kisasa ili kuvutia wananchi kutumia huduma za TTCL.

  “TTCL lazima mubadilike ili muweze kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia na hivyo kumudu ushindani uliopo sasa katika sekta ya mawasiliano”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Amewataka TTCL kuhakikisha kituo mahiri cha kutunzia taarifa (Data Centre), kinaanza mapema mwezi Juni ili kuwezesha wadau wengi kunufaika na kituo hicho.

  Prof. Mbarawa amesema Serikali inaunga mkono TTCL na imetenga masafa ya 800 MHZ ambayo yataiwezesha TTCL kushindana na makampuni mengine ya watoa huduma ya mawasiliano na kuwaunganisha wateja wengi kutumia huduma za mawasiliano na data.

  “Uzinduzi wa nembo mpya ya TTCL na huduma ya masafa ya 4G LTE uendane na ubunifu kwa wafanyakazi ili muwavutie watumiaji wengi wa simu na hivyo kupata soko kubwa na kuifanya TTCL kuchangia kikamilifu pato la taifa”, amesisitiza Waziri Mbarawa.

  Prof. Mbarawa amesema mawasiliano ni kiungo muhimu cha kufanikisha ukuaji wa sekta za kilimo, taasisi za fedha, uwekezaji, ujasiliamali na utendaji kazi wa Serikali na sekta binafsi hivyo ubunifu katika utendaji utaiwezesha TTCL mpya kufikia malengo yaliyokusudiwa.

  Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amewataka wananchi kuzingatia maelekezo wanayopatiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuhusu namna ya kuzitambua simu na vifaa feki na hatua za kufuata ili ifikapo Juni 16 zoezi la kuzifunga simu feki litakapotekelezwa wasiathirike.

  Kwa upande wake Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Bi. Edwina Lupembe amesisitiza kwamba TTCL imejipanga kuboresha huduma za fedha ili kuwezesha watumiaji wengi wa kampuni hiyo kunufaika na huduma ya kutuma na kupokea fedha.

  “Tumekamilisha mradi mkubwa wa kusimika mitambo ya GSM, UMTS na LTE ambayo itakuwa na uwezo wa kutoa huduma ya mawasiliano 2G, 3G na 4G”, amesema Bi. Lupembe

  Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa mabadiliko ya muonekano wa TTCL yataendana na mtazamo mpya wa wafanyakazi wenye lengo la kuiwezesha kampuni hiyo kuwa ya kisasa hapa nchini.

  Amesema TTCL imejipanga kuboresha simu za mezani, mkononi, na huduma za intaneti ya haraka ili iweze kupata wateja wengi na hivyo kuongeza mapato yake.

  “Teknolojia ya 2G GSM, 3G UMTS na LTE imeongeza nguvu kwa kampuni yetu kuleta ushindani katika soko la mawasiliano na zitaendelea kuongeza ufanisi na ubunifu wa huduma zetu kwa bei nafuu”, amesisitiza Dkt. Kazaura.

  Tayari huduma ya 4G LTE inapatikana katika maeneo mengi ya Ilala, Temeke na Kinondoni jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akitoa agizo la kuhama kwa wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam(Hawapo Pichani) kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha Michezo.Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akisistiza jambo mbele ya wajumbe wa kikao kati ya Serikali na wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadilina kuhusu wananchi hao kuhama eneo hilo kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha Michezo.Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius Mgaya akichangia hoja katika kikao kati ya Serikali na wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadilina kuhusu wananchi hao kuhama eneo hilo kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha Michezo.Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw.Mafuku Rajabu akifafanua jambo katika kikao kati ya Serikali na wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadilina kuhusu wananchi hao kuhama eneo hilo kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha Michezo.Eneo la Changamani kijiji cha Michezo ambalo wananchi wake wanatakiwa kuhama ndani ya miezi miwili kupisha uendelezwaji wa eneo hilo kwa ajili ya michezo mbalimbali.Picha na Raymond Mushumbusi WHUSM


  Na Raymond Mushumbusi WHSUM.

  Serikali imewapa miezi miwili wananchi waishio katika kijiji cha michezo cha Changamani kilichopo Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam kuhama katika eneo hilo kupisha uendelezwaji wa kijiji cha mchezo.

  Agizo hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge alipokutana na wananchi hao katika kikao cha kujadili na kukubaliana muda wa kuhama katika eneo hilo leo Jijini Dar es Salaam.

  “Ndugu zangu tumejadiliana wote na kukubaliana kuwa baada ya miezi miwili mtakuwa mmeshaama katika eneo hilo kupisha uendelezwaji wa kijiji cha michezo kwa ajili ya shughuli za mbalimbali za michezo” alisisitiza Bw. Nkenyenge.

  Naye Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw.Julius Mgaya amesema kuwa mpango wa kuwahamisha wananchi hao unalenga kutekeleza mradi wa kijiji cha michezo kitakachojengwa kwa ajili ya kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo mbalimbali.

  Kwa upande wake mmoja ya wawakilishi wa wananchi hao Bw.Atillio Mballa amesema wamekubaliana na muda huo waliopewa na watafikisha ujumbe huo kwa wenzao na kabla ya muda hujafika watakuwa wameshatekeleza agizo hilo.

  Katika mpango wa kukuza na kuendeleza michezo nchini Serikali imejipanga kukuza sekta ya michezo nchini na kuifanya kuwa moja ya rasilimali itakayochangia katika pato la taifa.

  0 0

  Bodi ya Usajili wa Makandarasi imefuta usajili wa jumla ya makandarasi 4572 kwa kushindwa kutimiza matakwa ya Sheria ya Usajili wa Makandarasi ya mwaka 1997.

  Hayo yamebainishwa na Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Bw. Rhoben Nkhori wakati wa Mkutano wa Mashauriano wa CRB uliofanyika jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Bw. Nkhori amesema kuwa katika jukumu la kuratibu mwenendo wa kazi za makandarasi, Bodi ilikagua miradi 2735. Katika miradi hiyo iliyokaguliwa, miradi 1873 sawa na asilimia 68.5 haikuwa na kasoro.

  Ameongeza kuwa miradi mingine ilikuwa na kasoro za kutofanywa na makandarasi waliosajiliwa, kutozingatia usalama wa wafanyakazi, kutokuwa na bango wala uzio na miradi kutosajiliwa. Kwa mujibu wa Bw. Nkhori miradi yote iliyopatikana na upungufu wahusika walichukuliwa hatua mbali mbali kwa mujibu wa sheria.

  Aidha, Bwana Nkhori amesema kuwa kwa mwaka jana, Bodi ilisajili miradi 3,172 yenye thamani ya shilingi trilioni4.23. Katika miradi hii asilimia 44.4 ilifanywa na Makandarasi wazawa na asilimia 55.6 ilifanywa na makandarasi wa kigeni.

  Licha ya mafanikio hayo CRD ilikumbana changamoto kadhaa ikiwemo kuwasilisha nyaraka za kugushi wakati wa usajili hususani kadi za magari na mitambo, vyeti vya wataalam, kutumia majina ya makandarasi kwa udanganyifu kwa kuuza vibao, waendelezaji kutotoa taarifa sahihi za umiliki kwa Bodi na baadhi ya makandarasi kushindwa kuwalipa wafanyakazi na vifaa vya ujenzi.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi, Bi Consolata Ngimbwa amemwomba Mhe. Rais John Pombe Magufuli kuwapa kipaumbele Makandarasi wa humu nchini ili kuwawezesha kiuchumi. “Mhe. Rais tunaomba utupe kipaumbele kwani sisi tukipata hiyo miradi tutawekeza hapa nchi na kuongeza soko la ajira,”alisema Bi Ngimbwa.

  Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema serikali yake itawapa kipaumbele makandarasi wazawa lakini akawataka wajipange na kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili ikiwemo kujiepusha na vitendo vya rushwa.

  Mkutano huu pamoja na mamabo mengine utajadili jinsi ya kuwajengea uwezo makandarasi nchini. Kauli mbiu ya Mkutano huo ni “Juhudi za Makusudi za kukuza uwezo wa makandarasi wazawa, changamoto na mustakhabali.”

  0 0

  Na Rabi Hume, Modewjiblog.

  Katika kusaidia kukamilika kwa Mpango wa Maendeleo Endelevu ambao unataraji kumalizika 2030, Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) imefanya warsha ambayo imekutanisha wadau mbalimbali ili kuona ni jinsi gani wanaweza kubadilishana mawazo ili kufanikisha mpango huo nchini.

  Mgeni rasmi katika warsha hiyo alikuwa ni Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha, Anna Mwasha ambaye wakati akifungua warsha hiyo alisema kuwa mpango huo ni muhiu wa nchi yetu kwa sababu unakwenda kubadili maisha ya kila Mtanzania ili kuondokana na umaskini na kuwa katika maisha bora kama jinsi malengo 17 ya mpango huo yanavyojieleza.

  Mo Dewji Blog ilipata nafasi ya kuhudhuria mkutano huo na kukuandalia habaroi picha jinsi warsha hivyo ilivyofanyika katika ukumbi wa ESRF.
  DSC_2311
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ufunguzi katika warsa iliyoandaliwa na ESRF ili kuzungumzia Mpango wa Mendeleo Endelevu (SDG). (Picha zote na Rabi Hume, Modewjiblog)
  DSC_2330
  Baadhi ya washiriki waliohudhuria warsha hiyo wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii, Dkt. Tausi Kida wakati akifungua warsha hiyo.
  DSC_2341
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo akitoa neno kwa niaba ya UNDP ambao ndiyo wasimamizi wa mpango huo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida na Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha, Anna Mwasha.

  DSC_2354
  Mgeni rasmi katika warsha hiyo, Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha, Anna Mwasha akifungua warsha hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF).
  DSC_2367
  DSC_2384
  Washiriki wakiendelea kufatilia kinachoendelea katika warsha hiyo.
  DSC_2478
  Stephen Chacha kutoka Shirika la Beyond 2015 for Africa akizungumza jinsi Mpango wa SDG unaweza kufanyika nchini.
  DSC_2481
  DSC_2521
  Mmoja wa washiriki, Dkt. Kitila Mkumbo akichangia mada zilizokuwa zikijadiliwa.
  DSC_2457
  Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando (kushoto), akitoa taarifa fupi kabla ya kumribisha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi (katikati), wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kinondoni ya Mwananyamala Dar es Salaam leo mchana. Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Michael John, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Salum Ali Hapi.
  Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Makani ya Pentekosti (MMPT), Askofu Saldonie Sinde (katikati), akimkabidhi Katibu Mkuu magodoro 50 yaliyotolewa na Umoja wa Makanisa hayo kwa ajili ya kusaidia hispitali hiyo.
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Kijazi (katikati), akienda kutembelea hospitali hiyo. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe.
  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi (kulia), akiwajulia hali wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kinondoni ya Mwananyamala alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika hospitali hiyo.
  Katibu Mkuu Kiongozi akizungumza na viongozi mbalimbali katika ziara hiyo.
  Hapa Katibu Mkuu Kiongozi akisikiliza malalamiko kutoka kwa wananchi waliofika katika hospitali hiyo kupata huduma (hawapo pichani)

  Viongozi mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Kijazi.
  Mkutano ukiendelea.

  0 0  0 0   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wakandarasi, Wahandisi na wadau mbalimbali wa sekta ya Ujenzi kabla ya kufungua rasmi Mkutano  wa Siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini CRB uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipewa maelezo kuhusu katapila linalotumika katika kazi mbalimbali za ujenzi mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi jijini Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Diamond Jubilee kwa ajili ya Ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini CRB.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati akikagua baadhi ya mitambo na magari mbalimbali katika maonesho ya vifaa hivyo vinavyotumika katika sekta ya ujenzi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vifaa vya ujenzi katika moja ya mabanda mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi jijini Dar es Salaam.
   Wadau mbalimbali wa Sekta ya Ujenzi wakiwemo Wahandisi na Wakandarasi wakipiga makofi wakati wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano huo wa Mashauriano wa CRB jijini Dar es Salaam. 
  PICHA NA IKULU.

  RAIS Magufuli akemea vitendo vya ruswa kwa wakandarasi
  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amewataka wakandarasi nchini kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kulisaidia Taifa kupiga hatua ya kimaendeleo.

  Mhe. Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akifungua Mkutano wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini (CRB) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

  “Mnaweka viwango vikubwa vya fedha kwenye miradi ili muweze kupata fedha ya kutoa rushwa, kwa nini mnafanya hivyo?”amewauliza Mhe. Rais Magufuli na kuwambia kuwa kama wapo watumishi wa serikali wanaowaomba rushwa ili wapate kazi waitaarifu Takukuru mara moja ili wachukuliwe hatua.

  Mhe. Rais amewataka wakandarasi wazawa wajipange kufanya kazi na kuwaonya wasiwe wanaweka viwango vikubwa ambavyo vinachangia kuwakosesha zabuni. 

   Akitoa mfano, Mhe. Magufuli alisema katika ujenzi wa mahakama za mwanzo hapa nchini, jengo moja lilikadiriwa kukamilika kwa milioni 200 lakini wakandarasi wa Tanzania walioomba zabuni hiyo walitoa kiwango cha kati ya shilimgi milioni  670 na bilioni 1.4. Amesema kwa jinsi hii hata mtu awe na huruma ya namna gani hawezi kuwapa kazi.

  Amesema serikali yake itawajali kwanza wakandarasi wa hapa nchini lakini akawataka wajipange na pengine waungane ili kufanya kazi kwa pamoja.

  Aidha, Mhe. Rais amesema ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Tanzania unakaribia kuanza lakini akauliza wakandarasi wa hapa nchini wamejipangaje katika kushiriki ujenzi huo. 

  Kuhusu ulipaji wa madeni ya wakandarasi, Mhe Rais amesema, serikali yake imekuwa ikilipa madeni hayo na itaendelea kufanya hivyo hadi deni litakapoisha. Amesema kwa kuanza serikali imelipa bilioni 650 na baadaye ikatumia bilioni 462 kutoka Mfuko wa Barabara kuwalipa wakandarasi.

  Amesema wakandarasi ni watu wa muhimu sana katika maendeleo ya Taifa na ni injini ya maendeleo kwani wako kila sekta ya maendelo. Amesema kwa mfano  wako katika ujenzi wa mioundombinu, kwenye zana za kilimo,kwenye  uvuvi, na pia usafirishaji wakandarasi hawakosekani.

  0 0


  Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa wakifuatilia mada ya Menejimenti ya Maafa kutoka kwa Mratibu wa Maafa wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.John Kiriwai uliofanyika Ukumbi wa Empire mkoani Shinyanga tarehe 26 Mei, 2016.
  Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa wakifuatilia Majukumu ya Kamati za Maafa wakati wa mkutano huo katika Ukumbi wa Empire mkoani Shinyanga tarehe 26 Mei, 2016.
  Mkurugenzi wa Utafiti na Mipango Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Naima Mrisho akiwailisha mada ya kukabiliana na maafa wakati wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa katika Ukumbi wa Empire mkoani Shinyanga tarehe 26 Mei, 2016.
  Mkurugenzi wa Utafiti na Mipango Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Naima Mrisho (wa pili kulia walio kaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo Mkoani Shinyanga tarehe 26 Mei, 2016.

  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0
 • 05/26/16--23:05: TASAF KUWANUSURU WAHADZABE
 • Mfuko wa Maendeleo ya jamii –TASAF-umeanza mkakati maalumu utakaowezesha jamii ya Wahadzabe walioko katika mikoa ya Arusha,Manyara na Singida kuandikishwa katika Mpango wa Kunusuru Kaya maskini unaotekelezwa na mfuko huo nchini kote.

  Wakizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini unavyotekelezwa katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha,viongozi wa TASAF walioambatana na wadau wa maendeleo walioongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchi za Tanzania Bi.Bella Bird,na baadhi ya maafisa wa benki hiyo kutoka Marekani ,baadhi ya wahadzabe waliomba kuorodheshwa katika Mpango huo ili waweze kunufaika na huduma zitolewazo kupitia utaratibu wa kuhawilisha fedha.

  “ baadhi ya wananchi wenzetu wameandikishwa kwenye mpango huku wengi wetu hatujapata fursa hiyo na tumeanza kuona namna wanavyonufaika na huduma za mpango huo’’ alisisitiza mmoja wa wahadzabe katika kijiji cha Endamaghan umbali wa kilometa 70 kutoka makao makuu ya wilaya ya Karatu mkoani Arusha.

  Akizungumza baada ya kutembelea makazi ya wahadzabe Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird amepongeza jitihada zinazochukuliwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- kwa kuweza kuwafikia wananchi ambao wanakabiliwa na umaskini nchini kote.

  ‘’Benki ya Dunia inatambua na kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania katika kukabili tatizo la umaskini miongoni mwa wananchi wake,umuhimu mkubwa pia unapaswa kuwekwa katika kunusuru jamii za watu walioko katika mazingira magumu wakiwemo wahadzabe” alisisitiza Bi. Bird.

  Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF-Bwana Ladsilaus Mwamanga alisema zoezi la kutambua na kuziandikisha kaya maskini katika jamii ya Wahadzabe lilifanyika. Hata hivyo alisema zoezi hilo liliathiriwa kwa kiwango kikubwa na mfumo wa maisha ya jamii hiyo wa kuhamahama kutafuta chakula kwa kuwinda wanyama na kuokota matunda na asali.

  “Hatukuweza kuwaandikisha wote ingawa kimsingi wanastahili kuingizwa kwenye Mpango,hii ilitokana na kuhamahama kwa wananchi hao kujitafutia chakula hususani matunda, asali na mizizi” alisisitiza Bwana mwamanga.

  Hata Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF ameahidi kuwa kazi ya kuziandikisha kaya za walengwa katika jamii hiyo ya wahadzabe na nyingine zenye maisha ya kuhamahama itafanyika upya na kwa haraka ili waweze kuziingiza kwenye Mpango wa Kunusuru na Kaya Maskini unaotia mkazo katika kuboresha maisha ya walengwa hususani kupitia sekta za elimu, afya,lishe na kukuza kipato kwa kaya za walengwa.

  Zifuatazo ni picha za ziara ya viongozi wa TASAF na Wadau wa Maendeleo katika maeneo ya wahadzabe,wilayani Karatu Mkoani Arusha.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga (aliyevaa Kaunda suti) akiwasikiliza baadhi ya wananwake wa jamii ya Wahadzabe katika kijiji cha Endaghan wilayani Karatu mkoani Arusha wakati wa ziara ya wadau wa maendeleo na TASAF kuona utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini .
  Baadhi ya Wananchi kutoka jamii ya Wahadzabe wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird ( hayupo pichani) alipotembelea kijiji cha Endamaghan kuona utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia TASAF.
  Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird akiwahutubia wakazi wa Endamaghan katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha juu ya utekelezaji wa Mpango 
  Mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Endamaghan kutoka jamii ya Wahadzabe akipokea fedha za ruzuku kupitia mpango huo.
  Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika kijiji cha Endamaghan wakiwemo jamii ya Wahadzabe wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird (hayupo pichani) juu ya utekelezaji wa Mpango huo.
   

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akizugumza na wadau mbalimbali wa sanaa katika hafla ya uzinduzi wa siku ya msanii, leo jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu ameiagiza BASATA kuangalie namna bora na kuhakikisha maazimisho ya siku ya Msanii yanaadhimishwa nchi nzima na kwa mafanikio makubwa, pia amesema Makampuni na mashirika mengi yamekuwa yakiwatumia wasanii kwenye kazi zao mbalimbali ni vyema wajitokeze pia kwenye kudhamini maazimisho ya siku ya Msanii na kuzienzi kazi zao.
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza akimkaribusha mgeni rasimi katika uzinduzi huo wa siku ya msanii leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya wadau mbalimbali wa sanaa waliofika katika uzinduzi wa siku ya msanii katika ukumbi wa Alliance Francoise leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Sehemu ya Watendaji wakuu wa Kampuni ya MultiChoiche Tanzania wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wao, Francis Senguji (wa pili kushoto) wakiwa katika tafrija ya kuadhimisha siku ya Afrika, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya New Afrika, Jijini Dar es salaam.
   Meneja Masoko wa Kampuni ya MultiChoiche Tanzania, Furaha Samalu akizungumza machache katika tafrija hiyo ya kuadhimisha siku ya Afrika, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya New Afrika, Jijini Dar es salaam.
   Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya MultiChoiche Tanzania, Francis Senguji akizungumza machache katika tafrija hiyo ya kuadhimisha siku ya Afrika, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya New Afrika, Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Furaha Samalu.
   Burudani ya Ngoma za Kiafrika ikitolewa.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani Boinakheri akisalimiana na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi Comoro mara baada ya kuapishwa leo kwa kushinda uchaguzi mkuu wa April 10 na uchaguzi wa Marudio wa Mei 11 mwaka huu hafla ilifanyika leo uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro
  Vikosi vya majeshi ya Ulinzi vya Comoro vikitoa heshama kwa Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani Boinakheri aliyeapishwa leo na jaji Mkuu wa Mahakama ya Katiba Mhe,Loutfi Soulaimane katika sherehe zilizofanyila uwanja wa mpira Mjini Ngazija nchini Comoro,
  Makamo wa Rais wa Muungano wa Comoro Mhe,Jafar Ahmada Sais wa kisiwa cha Ngazija akiapishwa leo na Jaji wa mahakama ya katiba ya Nchi hiyo Mhe,Loutfi Soulaimane (hayupo pichani ) wakati wa sherehe za kuapishwa Rais kanali Azali na makamo wake 3 iliyofanyika leo baada ya ushindi wa uchaguzi Mkuu uliofanyika Aprili 10 na marudio ya uchaguzi huo uliofanyika mwezi mei 11 mwaka huu,hafla ilifanyika uwanja wa mpira mjini Ngazija leo,Mei 26 2016.[Picha na Ikulu.]
  Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani Boinakheri akitoa hutuba yake katika sherehe za kuapishwa zilizofanyika leo kufuatia kushinda Uchaguzi Mkuu uliofanyika April Kumi (10) na uchaguzi wa marudio uliofanyika mey 11 mwaka huu,hafla ya sherehe ilifanyika uwanja wa mpira Mjini Ngazija nchini Comoro,
  Rais Mstaafu wa Muungano wa Comoro Mhe,Dkt.Ikililou Dhoinine (kulia) akiwa na Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani Boinakheri (wa pili kulia) mara baada ya kuapishwa akiwa na Makamo wake wawili Mhe,Abdullah Said Sharman (kushoto) wa Kisiwa cha Mwali na Mhe,Mustarigan Aboud wa Kisiwa cha Anjouan (wa pili kushoto) katika uwanja wa mpira mjini Ngazija nchini Comoro leo,
  Rais Mstaafu wa Muungano wa Comoro Mhe,Dkt.Ikililou Dhoinine (kulia) akiwa katikapicha na Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani Boinakheri mara baada ya kuapishwa leo baada ya kushinda uchaguzi Mkuu wa April kumi(10) na uchaguzi wa marudio wa mei kumi na moja mwaka huu hafla ilifanyika leo uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro,
  Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani Boinakheri akitoa salamu kwa kikosi cha Bendera mara baada ya kuapishwa leo akiwa mshindi katika kushinda uchaguzi Mkuu wa April kumi(10) na uchaguzi wa marudio wa mei kumi na moja mwaka huu hafla ilifanyika leo uwanja wa Mpira Mjini Ngazija nchini Comoro

  [Picha na Ikulu.]

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete wakifurahia jambo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU


  0 0

  AutoSueco (VOLVO) Commercial Manager, Mr. Alen Nkya (right) gestures with President of Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli (left) and other delegates regarding construction equipment and trucks during Contractors International Conference in Dar es Salaam recently Photo By NICOMEDIATZ.com.

  0 0

  Kijana Mmoja (picha) Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu.

  Na BMG

  Tukio hilo limetokea hii leo na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia mnarani hadi majira ya saa sita mchana.

  Mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa akiyatumia.

  Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza, mmoja wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, amsetoa rai kwa makampuni yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili kuondoa hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema.

  Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu "rukaa, ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume" hali ambayo ilikuwa ikimuongezea morari kijana huyo na hivyo kujirusha kweli kutoka katikati ya mnara huo.

  Baada ya kijana huyo kujirusha kutoka katikati ya mnara hadi chini, alipoteza fahamu na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure kwa ajili ya huduma ya kwanza.

  0 0

   Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza cha maswali na majibu na uchangiaji wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi leo mjini Dodoma.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Peter Mavunde ambaye akiwasalimia kwa furaha wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Dodoma leo kwenye viwanja vya Bunge.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Peter Mavunde akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi -VETA mkoa wa Dodoma nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
   Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju (katikati) akizungumza na viongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) waliolitembelea Bunge mjini Dodoma.
   akiwasisitiza jambo viongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) alipokutana nao nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
   Waziri wa Elimu,Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako (kushoto) akimweleza jambo Rais wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) Bw. Frank Nkya (kulia) nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma
   Waziri wa Elimu,Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako (kulia)akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angella Kairuki (kushoto) nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
  Waziri wa Elimu,Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja nawanafunzi wa Chuo cha Ufundi -VETA mkoa wa Dodoma nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.PICHA/Aron Msigwa-MAELEZO.

  0 0

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunzi Amina Abdallah wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Ukombozi jijini Dar es salaam ambaye amepanda basi la Mwendo Kasi Ajentina na kushuka Manzese, Waziri Mkuu Majaliwa ametumia usafiri wa DART leo kutoka Feri kwenda Kimara Mwisho wakati alipokagua miundombinu ya usafiri huo ili kujionea mafanikio na changamoto mbalimbali zinazojitokeza mara baada ya mradi huo kuanza mwezi mmoja sasa ili ziweze kurekebishwa na kuuboresha zaidi. 

  Usafiri DART umekuwa mkombozi kwa wasafiri wengi wa jiji la Dar es salaam wakati wanapotoka majumbani mwao na kuelekea kazini na kurejea majumbani mwao,Katikati ni Bw. David Mwaibula aliyekuwa Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) zamani aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM).
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia jambo wakati Mkurugenzi wa DART Bw. David Mgwasa akisamimiana na Bw. David Mwaibula aliyekuwa Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) zamani aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.
  Baadhi ya abiria wakisafiri pamoja na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kwenye basi la DART.
  Moja ya Basi likiwa katika ruti yake kutoka Kimara kuelekea Posta.

  *Ataka watu walipe tiketi rasmi, wafuate taratibu

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua utendaji kazi kwenye mabasi ya mwendokasi yanayotoa huduma katika Jiji la Dar es Salaam na kubaini changamoto kadhaa ambazo amesema zitarekebishwa kadri mradi unavyoendelea.

  Waziri Mkuu ambaye alilipa nauli na kupanda basi namba 23 lenye usajili namba T125 DGW kuanzia kituo cha Ferry, Kivukoni, ametumia muda wa dakika 50 kufika Kimara mwisho kwa kutumia usafiri huo.

  Waziri Mkuu alipanda basi hilo saa 3:30 asubuhi na lilianza safari saa 3:33 baada ya kusubiri wengine wapande. Kwa wastani ililtumia kati ya dakika mbili hadi tatu kutoka kituo kimoja hadi kingine. Basi hilo liliwasili Kimara Mwisho saa 4:23 asubuhi.

  Akizungumza na waandishi wa habari akiwa Kimara mwisho mara baada ya kumaliza ziara hiyo fupi ya ukaguzi leo (Ijumaa, Mei 27, 2016), Waziri Mkuu alisema aliamua kufanya ziara hiyo ya ghafla ili kuangalia matumizi ya njia za mabasi yakoje na pia kuona abiria wanaelewa vizuri namna ya kuitumia huduma hiyo.

  Amesema ameridhishwa na mradi unavyofanya kazi ila ameelezwa kuna usumbufu kwenye mageti wakati abiria wanapotaka kuthibitisha tiketi zao hasa wakati wa asubuhi kunapokuwa na msongamano wa abiria. Pia alielezwa kwamba kuna baadhi ya abiria wanakuja na tiketi za jana yake jambo ambalo linaleta usumbufu kwa sababu hazitambuliki kwenye mfumo wao.

  “Nimeridhishwa na uharaka wa njia kwa sababu na mimi mwenyewe nimetumia dakika 50 kufika hapa ingawa kuna maeneo nimeona kuna haja ya kuwa na taa maalum za kuzuia magari (special sensors) wakati mabasi yakipita ili kuepusha ajali,” alisema.

  Aliyataja maeneo hayo kuwa ni kwenye makutano ya barabara ya Morogoro na mtaa wa Samora, Morogoro na Jamhuri na makutano ya Morogoro na Kisutu.

  Waziri Mkuu aliwataka Watanzania waende na tiketi rasmi badala ya kutumia tiketi za jana kwa sababu kufanya hivyo ni makosa na  mtu anakuwa amedhamiria. “Hawa watachukuliwa hatua za kinidhamu. Mtu akija na tiketi ya jana akamatwe na kupelekwa polisi, huyu atakuwa amedhamiria,” alisema Waziri Mkuu wakati akiongea na mhudumu mmoja katika kituo cha Kimara Mwisho.

  “Ninawasihi wananchi wanaotumia usafiri huu wajifunze kufuata utaratibu na kuwasisitizia kuwa kila abiria aje na tiketi ambayo ni rasmi,” alisema na kuongeza: “Haya mabasi nimebaini yako vizuri. Ninatoa msukumo kwa watumishi wa umma wapande mabasi haya ili kupunguza msongamnao wa magari barabarani.”

  Katika kupiunguza baadhi ya changamoto, Waziri Mkuu alisema Serikali itasimamia uboreshaji wa ukataji tiketi ili kuondoa usumbufu kwa abiria. Pia alivionya vyombo vya moto viache kutumia njia maalum ya mabasi hayo.

  Pia aliwataka polisi wanaofanya doria za usiku kupita kwenye fly-overs na kuwaondoa watu wanaolala kwenye maeneo kwani wanahatarisha usalama wa watu wanaotumia njia hizo. “Zile siyo sehemu za kulala, wanaofanya hivyo wanahatarisha usalama wa watumiaji wa njia hizo, kwa hiyo polisi wakiwakuta watu wa aina hiyo wawakamate mara moja,” alisema.

  Kwa upande wake, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohammed Mpinga ambaye alifuatana na Waziri Mkuu kaktika ziara hiyo, alisema amepiga marufuku magari na pikipiki kutumia njia hiyo hata kama ni magari ya Serikali.

  “Tulishapiga marufuku magari na pikipiki kutumia njia hiyo hata kama ni magari ya Serikali, ninawasihi madereva watambue hili na watii,” alisema.

  Machi 22, mwaka huu Waziri Mkuu alitembelea soko la Feri kwa lengo la kuangalia mfumo wa majiko ya gesi sokoni hapo (kuzuia moshi) na kukagua ujenzi wa ukuta unaotenganisha soko hilo na mabasi yaendayo kasi.

  Aprili 15, mwaka huu, Waziri Mkuu alifanya kikao na kuwaagiza wakuu wa taasisi zinazohusika na utekelezaji wa mradi huo kuhakikisha wanatoa elimu kwa umma ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza pindi majaribio yakianza.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM,
  IJUMAA, MEI 27, 2016.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikagua kituo cha Kimara Mwisho mara baada ya kuwasili kituoni hapo
  Moja ya basi la Mwendo kasi likipakia abiria katika kituo cha Kimara Mwisho leo.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunziambaye jina lake halikufahamika mara moja wakati alipofika kwenye kituo cha mabasi ya Mwendo kasi Kimara Mwisho leo.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiuliza swali kwa mmoja wa wafanyakazi wanaokatisha tiketi katika vituo hivyo wakati alipokagua miundombinu ya DART leo.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiangalia utendaji kazi unavyoendelea ikiwa ni pamoja na kubaini changamoto zinazojitokeza.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikaua kituo cha Kimara Mwisho.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Mkurugenzi wa DART Bw. David Mgwasa katikati ni Mzee David Mwaibula.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua miundombinu hiyo leo kulia ni Mzee David Mwaibula na katikati ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga.

  0 0

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
  BAADA ya kuiongoza timu yake kutetea ubingwa wa ligi kuu, fainali ya kombe la FA na kuingia hatua ya makundi nahodha wa timu ya Yanga, Nadir Haroub 'canavaro' (Pichani)amesema kuwa watahakikisha wanapiga kufa na kupona kuweza kuisaidia timu yao kuingia hatua ya nusu fainali kwani kama watafanya vizuri michezo mitatu ya mwanzo basi watakuwa wameweza kuvuka makundi.

  Canavaro amesema mwaka huu wamekuwa na kikosi bora ambacho kimekuwa kinaleta ushindani wa hali ya juu katika kila mechi watakayokuwa wanacheza na hicho kinakuwa ndiyo msingi mkubwa kwao wa kufanya vizuri zaidi.

  "Tumeingia hatua ya makundi na tunajua ni moja ya hatua ngumu sana tuliopo ila michezo mitatu ya mwanzo tukipata alama basi tutaingia nusu fainali na hatimaye fainali kabisa na ikiwezekana tutaleta kombe nchini,"amesema Canavaro. 

  Na katika kujiandaa zaidi kocha mkuu Hans Van De Pluijm anajua ni wapi atapeleka kikosi kwa ajili ya maandalizi zaidi kwani Juni 17 tunaanza kucheza na Mo bejala nchini Algeria na siku 10 baadae kutakuwa na mechi nyingine dhidi ya TP Mazembe Jijini Dar es salaam.

  Amesema, kwa sasa wachezaji wote wanatakiwa kujiweka sawa na kuwazia mashindano yaliyokuwa mbele yao katika kipindi hiki kwani kufanya vizuri kwao kutalitambulisha taifa zaidi.

  Wakati huohuo,
  Timu ya Taifa imeondoka Alfajiri ya leo huku nahodha huyo wa zamani Canavaro akiwa hajajumuika na kikosi hicho kinachonolewa na Charles Boniface Mkwasa na kuendelea kuweka msimamo wake wa kutokuchezea timu ya taifa kwani ameshaamua na tayari barua ipo TFF.

  "Nimeshaweka msimamo wangu kuwa sitachezea tena timu yaTaifa na ndio maana sijajiunga nao kuelekea Kenya kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Harambee Stars,"amesema Canavaro.

  Toka kujiengua kwa Canavaro,Mkwasa anamuita kwa mara ya kwanza baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mechi alizocheza akitoka katika majeraha yaliyomuweka nje kwa takribani miezi mitatu bila kucheza.

older | 1 | .... | 859 | 860 | (Page 861) | 862 | 863 | .... | 1896 | newer