Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

RC SHIGELLA AWATAKA WENYEVITI WA MITAA KUSIMAMIA KWA UMAKINI SHUGHULI ZA MAENDELEO KWENYE MAENEO YAO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh Martini Shigella akizungumza na wenyeviti wa mitaa kuhusu kujadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika Jiji la Tanga,kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Ahmed na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Alhaj Abdulla Lutavi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Ahmed akizungumza katika kikao hicho kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella na kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Tanga,Lucia Mwiru na anayefuata ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Daudi Mayeji 
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Mustapa Selebosi akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa BMK Sahare Jijini Tanga 
Baadhi ya wenyeviti wa Mitaa mbalimbali Jijini Tanga wakiwa ukumbini tayari kumsikiliza RC Shigella 
Kulia ni Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Amiri Mkapanga akifuatilia kwa umakini maelekezo wa RC Shigella kwa wenyeviti wa serikali za mitaa kwenye Jiji la Tanga. 
Picha kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

IDADI YA VIFO KWA WATOTO WACHANGA NA WAKINA MAMA VYAZIDI KUPUNGUA NCHINI.

$
0
0
Balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke kulia akikata utepe kuashilia kuanza rasmi kwa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam na wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando.
Balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke akiongea na waandishi wa habari na Wadau wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando akiongea na waandishi wa habari na Wadau wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Mshauri wa ufundi kutoka Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) Dkt. Baltazar Ngoli wa kwanza kulia akitoa maelekezo ya picha kwa Balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke wa pili kulia pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando wa tatu kulia wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam.
Wadau mbalimbali wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam.Picha zote na Ally Daud-Maelezo


Na Ally Daud- maelezo

Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama vinazidi kupungua kutoka siku hadi siku katika kufikia malengo ya milenia .

Akizungumza hayo katika hafla fupi ya kuzindua maonesho ya picha Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando amesema kuwa Tanzania imepiga hatua katika kufikia malengo ya milenia kwa kupunguza Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama.

“Tumefanikiwa kupunguza Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama ili kufikia malengo ya milenia kwa upande wa afya kupitia mfumo wa kujiunga na bima ya afya kwa jamii” alisema Dkt. Mbando.

Mbali na hayo Dkt Mbando amesema kuwa amewakaribisha wananchi wote hususani wakazi wa Dar es salaam kuudhuria maonesho hayo yaliyofunguliwa leo yenye kauli mbiu ya “Huduma Bora kwa Afya Bora”yatayofikia kilele mpaka Juni 10 mwaka huu ili kupata ujumbe zaidi kupitia picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini.

Aidha ameipongeza Serikali ya Ujerumani kupitia ubalozi wake kwa kushirikiana vizuri na Serikali ya Tanzania na kukubaliana kupata msaada wa Euro milioni 47 kwa muda wa miaka mitatu ijayo katika kuinua sekta ya Afya.

Kwa upande wa balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke amesema kuwa mchango wa Serikali ya ujerumani kwa sekta ya afya Tanzania utaendelea kuwa sehemu ya mpango wa ushirikiano wa nchi mbili ili kuinua sekta hiyo nchini.

SHIRIKA LA NDEGE LA SERBIA LAPIGA HATUA KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZAKE

$
0
0
Ndege kubwa ya kwanza ya shirika la ndege la Serbia, Airbus A330, ikiwa katika uwanja wa ndege wa Nikola Tesla. Ndege hii itakuwa ikifanya safari zake kati ya Belgrade na New York.

Shirika la ndege la Serbia, ambalo ni shirika la ndege la Taifa la Serbia, lilisherehekea hatua nyingine katika mabadiliko kama shirika la ndege linaloongoza katika kanda, kwa kuwasili kwa ndege yake kubwa ya kwanza katika uwanja wa ndege wa Nikola Tesla jana.

Ndege aina ya Airbus A330 itatumika katika ruti za shirika la ndege la Serbia kati ya Belgrade kwenda New York, Ambayo itazinduliwa tarehe 26 Juni 2016, ikiunganisha Serbia na Marekani kwa huduma ya ndege ya moja kwa moja kwa mara ya kwanza katika miaka 24.

Baada ya kutua Belgrade, ndege hiyo ililakiwa kwa salamu za kitamaduni za urushaji wa maji na kukabidhiwa kwa wawakilishi wa ndege hiyo. Waliokuwa katika safari ya kwanza ya ndege hiyo ya kihistoria ni kundi la wadau wakubwa wakiongozwa na Siniša Mali, Mwenyekiti wa shirika la ndege la Serbia na Meya wa Belgrade, na Dane Kondić, Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Serbia.

Ndege hiyo ilikuwa inaongonzwa na Kaptein Davor Mišeljić, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ndege la Serbia, na sasa itasajiliwa na Idara ya Usafirishaji na Uchukuzi ya Serbia (Serbian Civil Aviation Directorate) kabla ya kurejea tena Abu Dhabi kwa ajili ya kukamilisha sehemu za vyumba vya ndege hiyo.


Bwana Mali alisema: “Hii ni hatua kubwa sana kwa shirika la ndege la Serbia na taifa kwa ujumla. Kutazama ndege yetu ya kwanza iliyochorwa picha isemayo Airbus A330 ikitua katika kiwanja chake kipya hapa Belgrade kwa mara yake ya kwanza ilikuwa ni wasaa wa faraja kwetu, kuona kuwa Ndege kubwa inakuja kuwekeza katika hatma ya shirika hili la ndege na taifa la Serbia pia.

“Ndege yetu kubwa kabisa na ndege zetu nyingine kubwa za A319, A320, ndege na A330 ni uwekezaji ulio bora zaidi ambao utaiunganisha Serbia na Marekani katika wiki chache itafungua utalii na biashara kwa ajili ya uchumi.”

Ndege hiyo ina viti 18 katika Daraja la biashara na viti 236 katika daraja la uchumi. Ndege hiyo Aina ya Airbus A330 itafanya safari zake katika safari tano mpya za kila wiki za shirika la ndege la Serbia kati ya Belgrade na New York.

Kuwasili kwa A330 ni hatua mpya kabisa katika hatua za msingi za programu ya kuongeza ndege (re-feeling) ambayo ilianza mwaka 2013 na imekuwa ni kitambulishi cha ndege kumi za kawaida katika miaka kumi tu iliyopita, ikipunguza wastani wa umri wake wa ndege zake kutoka miaka 25 hadi miaka 10.

 Bwana Kondic alisema: Kuwasili kwa ndege aina ya Air bus A330 mchana wa leo lilikuwa ni tukio la kihistoria kwa shirika la ndege la Serbia na ishara ya mafanikio katika siku za usoni.

“Ndege aina ya A330 ni ya kisasa na inatumia mafuta vizuri ambayo inafungua fursa nyingi za kukua kwa shirika la ndege na itaturuhusu kuzindua huduma za muda mrefu kwenda New York, inarahisisha safari kwa kiasi kikubwa huku ikiwezesha muunganiko kati ya Balkans na Marekani.

“Katika wiki zijazo ndege itakuwa tayari ikiwa na madaraja mawili ya Business na Economy ambayo zikiambatana na huduma zetu nzuri tunazotoa, itawapatia wageni wetu uzoefu wa safari usiolinganishwa kupitia Atlantic.”

Dondoo za huduma na bidhaa za ndege ya A330 inajumuisha mfumo wa burudani katika kila kiti inayokuwezesha kuchagua filamu, Muvi na burudani za Kiserbia na Kiingereza, viti vya kulala katika daraja la biashara na Menyu iliyoboreshwa, ikijumuisha huduma ya chakula pale unapohitaji kwa wageni wa daraja la Business.

NECTA SASA KUFUNGA MITIHANI KWA KUTUMIA MASHINE.

$
0
0
Na Fatma Salum-MAELEZO, Dodoma.

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limejipanga kuanza kufunga bahasha zenye karatasi za mitihani kwa kutumia mashine maalum ili kuondokana na hatari ya kuvuja kwa mitihani hiyo na gharama za ufungaji wa mitihani kwa kutumia mikono.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2016/2017, jana Bungeni Mjini Dodoma.

Prof. Ndalichako alisema kuwa katika kuimarisha utendaji kazi wake NECTA itanunua mashine mbili za kufunga mitihani (Auto Poly Wrapping and Packing Machine) ili kuimarisha usalama wa mitihani kwa kupunguza watu wanaoshiriki kwenye maandalizi ya mitihani hiyo.

“Katika mwaka 2016/2017 Baraza litasimika mashine mbili za kufunga bahasha za mitihani hivyo kuondoa hatari zinazoweza kujitokeza kwa kuwa idadi ya watu wanaofanya kazi hiyo itapungua.” alisema Prof. Ndalichako.

Aidha, Prof. Ndalichako aliongeza kuwa Baraza litaboresha mfumo wake wa ukusanyaji na uchakati takwimu na kuweka Mfumo wa Kielektroniki wa kumtambua mwanafunzi kwa namba maalum tangu anapoandikishwa shuleni hadi atakapomaliza mzunguko wa masomo yake.

Alisema kuwa mfumo huo wa utambuzi utaunganishwa nchi nzima ili kuwezesha kufuatilia maendeleo ya mwanafunzi kwenye shule yoyote atakayoenda kusoma ndani ya nchi kwa kuwa namba hiyo atakayopewa na Baraza ataitumia hata kwenye shule nyingine atakazohamia.

“Wizara itaweka Mfumo wa Kielektroniki wa ukusanyaji taarifa za wanafunzi chini ya Baraza la Mitihani ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa hizo wakati wa mitihani na utaratibu huu utapunguza matumizi makubwa ya fedha kupitia mfumo wa TSM9.” alisema Prof. Ndalichako.

Pia alieleza kuwa katika kufanikisha Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), mwaka wa fedha uliopita Mamlaka ya Elimu Tanzania imechapisha vitabu 558,720 vya jinsi ya kujibu mitihani ya Kidato cha Pili na Kidato cha Nne ili kuwawezesha wanafunzi watahiniwa kujibu maswali vizuri katika mitihani yao hatimaye kuongeza ufaulu.

SINA MKATABA NA COASTAL UNION - HUMUD

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KIUNGO wa Coastal Union Abdulhalim Humud (Pichani)amesema yeye ni mchezaji huru na anaweza kukaa mezani na timu yoyote kwa sasa kwani mkataba wake na Coastal Union umekwisha kwa sasa huku timu hiyo ikiwa tayari imeshashuka daraja.

Akizungumza na Michuzi Blog Humud amesema kwa atakayehitaji huduma kutoka kwake basi watakaa mezani na kuingia makubaliano nao na kuweka wazi changamoto alizokutana nazo katika timu ya Coastal Union mpaka kupelekea kushuka daraja na chanzo kikuu kikiwa ni ubovu wa uongozi uliopo pale.

"Nimemaliza mkataba wangu na Coastal Union na nipo huru kujiunga na timu yoyote kwa sasa na watakaonihitaji nitakaa nao mezani na kuweka makubaliano kwa kila upande kuridhika na makubaliano hayo,"amesema Humud. Kiungo huyo ameweka wazi matatizo yaliyopo kwenye timu ya Coastal Union na kusema viongozi ndiyo wamefanya mpaka timu hiyo kushuka daraja kwani wameshindwa kuiongoza kipindi chote na hata chama cha mpira wa miguu mkoa nao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana.

Amesema, wamekuwa na kikosi kizuri sana katika ligi ila wakashindwa kujituma sana kwani walikuwa hawapati stahiki zao kama inavyotakiwa na kuishia kucheza mpira wakiwa wameshavunjika moyo na kuona bora liende.

Humud amewahi kukipiga katika timu za Simba na Azam na baadae Sofapaka ya Kenya na amekuwa na msaada mkubwa kwa timu alizopitia katika kipindi chote.

EAC TABLES USD 100 M BUDGET TO EALA

$
0
0
Hon Dr Susan Kolimba, Deputy Minister, Foreign Affairs and East African
Co-operation, Dr Susan Kolimba holds the Budget Speech. She is flanked by the EAC Secretary General, Hon Amb Liberat Mfumukeko.
The deputy Minister of Foreign Affairs and East African Co-operation, Hon
Dr Susan Kolimba presents the Budget Speech to the House. At back is the
EALA Speaker, Rt. Hon Daniel Fred Kidega.
 

The EAC today presented Budget estimates for the Financial Year 2016/2017 totaling $101,374,589 to the East African Legislative Assembly sitting in Arusha. Deputy Minister for Foreign Affairs and East African Co-operation, Hon Dr Susan Kolimba presented the Budget speech to an attentive House on behalf of the substantive Minister and Chair of the EAC Council of
Ministers, Hon Dr. Augustine Mahiga.

The 2016/2017 Budget is adrop down from $110,660,098 Million presented to the House in the previous Financial Year. The Budget prioritizes the full implementation of the EAC Single Customs Territory, enhanced implementation of the EAC Common Market Protocol especially additional commitments and interconnectivity of border immigration systems and procedures acrossn Partner States and enhancement of productivity and value addition in key productive sectors.

The budget also takes cognisance of development of cross-border infrastructure and harmonisation of laws,policies and standards in respective sub-sectors, implementation of a liberalised EAC airspace, enhanced implementation a One Area Network in telecommunications and the implementation of EAC Peace and Security initiatives.

According to the Minister, other key specific priorities are strengthening of the legal and judicial systems, enhancement of Information, Communication and Education to promote popular participation of the citizenry in the EAC integration process and promotion of education, science and technology for creative and productive human resources.

WAZIRI PROFESA MAKAME ATEMBELEA DARAJA LA NYERERE NA KITUO CHA KUPIMIA MAFUTA YAINGIAYO NCHINI KUONA MAENDELEO

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wawakilishi wa kampuni ya Mabey Bridge kutoka Marekani(hawapo pichani) na wadau wengine wa Ujenzi leo kuhusu mpango wa kujenga fly overs takribani tatu katika jiji la Dar es salaamu kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji.
Katibu mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga akifafanua jambo kuhusu mpango wa ujenzi wa kujenga fly overs katika jiji la Dar es salaamu kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo kushoto ni muakilishi kutoka Kampuni ya Kimarekani ya Mabey Bridge Bw. Darren Keep na kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na MawasilianoProfesa Makame Mbarawa.
Msimamizi Mkuu wa Daraja la Nyerere Bw. Gerald Sondo akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu maendeleo ya Daraja pamoja na changamoto wanazozikabili, katika Ziara ya kushtukiza iliyofanya na Waziri huyo leo jijini Dar es salaamu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Fundi mitambo Bw. Simon Dotto kuhusu maendeleo ya ukarabati wa mtambo wa kupima mafuta kutoka kwenye meli kabla ya kuingia kwenye matanki ambao uliharibika hivi karibu kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wahudumu wa kivuko cha Mv Magogoni kuhusu utaratibu wa ukatishaji tiketi katika kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo na changamoto mbalimbali kutoka kwa abiria wanaotumia kivuko cha Mv Magogoni leo jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Beatrice Lyimo).

Kibiti kufanya kongamano la kuipokea Wilaya mpya kwa kushiriki shughuli mbalimbali za Maendeleo.

$
0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO

Viongozi wa umoja na wadau wa maendeleo wilaya mpya ya kibiti (UWAWAMAKI) mkoani Pwani umepanga kufanya kongamano la kuunga mkono tamko la Serikali ya awamu ya Tano ya Mhe.John Pombe Magufuli kwa kuifanya Kibiti kuwa Miongoni mwa Wilaya mpya siku ya jumapili tarehe 29 saa nne asubuhi kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari TEDEO Temeke jijini Dar es Salaam.

Akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Katibu wa umoja huo Bw.Selemani Ndumbogani amesema kuwa wanakibiti wamefarijika sana na kauli ya Serikali ya Kuipatia Kibiti wilaya jambo ambalo lilikuwa kilio cha muda mrefu ikiwa ni takribani zaidi ya miaka arobaini tangu uhuru na kuongezea kuwa walikuwa mbali sana na huduma muhimu za Serikali.

Pia umoja huo umeomba wana jimbo la kibiti hususani Rufiji kujitokeza kwa wingi kwenye kongamano hilo ili liwe lenye mafanikio makubwa.

Miongoni mwa mambo yaliyoandaliwa kufanywa ni pamoja na usafishaji wa mitaa,soko, maeneo ya standi ,eneo litakalojengwa wilaya,na kuendesha dua kwa madhehebu mbalimbali ya dini ili kuiombea kheri wilaya ya kibiti,Pia kuiombea nchi na Rais wetu wa Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli na Mhe.Kassim Majaliwa kuishi kwa amani na usalama katika kusimamia shughuli za Taifa.

Mwaka huu mwezi Februari Rais wa awamu ya tano Dr.John Pombe magufuli alitangaza kuipandisha adhi wilaya hiyo mpya ya kibiti ambapo kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imempa mamlaka rais ya kugawa nchi kwa kadri ambavyo atakavyoona inafaa.



Serikali yanunua vifaa vya kupima Ubora wa Majengo bila kuyaharibu

$
0
0
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bw. Elius Mwakalinga akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu kutekelezwa kwa mpango wa Serikali wa kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanapata makazi bora ambapo wakala huo unajenga nyumba 10,000 ili kutimiza azma hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Milki  Bw. Baltazar Kimangano na kushoto ni Mkurugenzi wa Ushauri Bw. Edwin Nnunduma.

Mhandisi  Ujenzi kitengo cha Upimaji  na Ukaguzi Majengo  toka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)  wakwanza kulia Bi Khadija Salum  akionesha kwa waandishi wa Habari sehemu ya vifaa vilivyonunuliwa na wakala huo kwa ajili ya kupima ubora wa majengo yaliyokwisha jengwa na yale yanayoendelea kujengwa ili kuhakikisha kuwa Serikali inakuwa na majengo yenye ubora kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa.


( Picha   na Habari na Frank Mvungi ).



Frank Mvungi-Maelezo


Serikali kupitia wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imenunua vifaa vya kupima Ubora wa Majengo bila kuyaharibu (Non destructive Testing equipments) .


Hayo yamesemwa Leo Jijini Dar es salaam na Mtendaji Mkuu waTBA  Bw. Elius Mwakalinga wakati wa mkutano na vyombo vya Habari uliolenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa  miradi mbalimbali  ya ujenzi inayotekelezwa na wakala huo.Akifafanua Mwakalinga amesema kuwa wakala huo umenunua vifaa vya kisasa ili kuwezesha ukaguzi wa ubora wa Majengo ya Serikali ili kuwa na majengo yenye Ubora unaotakiwa.

“Lengo la kununua vifaa hivi ni kuhakikisha kuwa majengo yote ya Serikali yanakuwa na ubora kwa kuwa tutayapima yaliyopo na yale yanayojengwa ili tuweze kuchukua hatua pale inapodi” alisisitiza Mwakalinga.Akieleza umuhimu wa vifaa hivyo Mwakalinga amesema kuwa  hakutakuwa na wasiwasi tena kuhusu uwezekano wa wakandarasi kudanganya wakati wa ujenzi.

Aidha vifaa hivyo vitawezesha Wakala kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika majengo ya Serikali ili kubaini hali ya ubora wa majengo hayo ambapo gharama ndogo za ada ya ushauri zitatozwa kwa Taasisi husika.Vifaa hivi ni kama Rebund hammer inayotumika kupima uimara wa zege iliyokauka, cover meter kwa ajili ya kupima ukubwa wa nondo na umbali uliowekwa.

Akitaja vifaa vingine Mwakalinga amesema kuwa ni “Utrasonic system/testing device” kwa ajili ya kupima muonekano wa ndani ya zege iliyokauka.Mbali ya jukumu la kuhakiki ubora wa majengo ya Serikali, Wakala umeendelea na mpango wa ujenzi wa nyumba zinazouzwa kwa gharama nafuu kwa watumishi wa umma ambapo mpango wa wakala huo ni kujenga nyumba elfu kumi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

RC KILIMANJARO AITAKA NHIF KUWA WABUNIFU ILI KUONGEZA WANACHAMA

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Saidi Meck Sadik ametoa rai kwa watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kubuni mbinu mpya za kuwahudumia wanachama wao ili kuhamasisha watanzania wengi kujiunga na mfuko huo.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya wa Siha Dkt. Charles Mlingwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa mfuko huo uliofanyika Mkoani humo.

Mhe. Meck Sadik amesema kuwa Baraza la wafanyakazi ndiyo chombo sahihi cha uwakilishi wa sauti za watumishi katika kupanga malengo ya Taasisi pia ni chombo cha kutatua migogoro ya kikazi na hivyo kumaliza mapema tofauti zinazojitokeza katika sehemu za kazi kabla hazijaathiri utendaji.

“Kutokana na umuhimu wa huduma zenu kwa umma, Baraza la Wafanyakazi la Mfuko wenu linatakiwa lichukue sura mpya na kuwa ni mahali pa ubunifu na kisima cha kuibua mbinu mpya za kuwahudumia vizuri wanachama wenu na kujua namna gani mtaendelea kuwavutia Watanzania wengi zaidi kujiunga na Mfuko”,alisema Meck Sadik. 

Mhe. Meck Sadik ameongeza kuwa anawapongeza kwa ubunifu wao wa kubuni mipango mbalimbali ya uchangiaji inayolenga kuwafikia watanzania wa makundi mbalimbali kulingana na hali zao za vipato na uwezo wao wa kuchangia.

“Hali halisi ya uchumi wa watanzania mnaifahamu, siyo watu wengi wenye uwezo wa kugharamia matibabu kwa fedha taslimu hivyo, huduma za matibabu kupitia Mfuko huu ni ukombozi mkubwa kwa kundi kubwa la watanzania”, alisema Meck Sadik.

Aidha, Mhe. Meck Sadik amewakumbusha wajumbe wa Baraza hilo kuwa wao ni kiungo muhimu kati ya wafanyakazi na uongozi wa Mfuko kwa hiyo, wana wajibu wa kuyaelewa malengo ya Taisisi yao kiutendaji na kuyawasilisha kwa wafanyazi wenzao wakiwa kama wamiliki wa kile walichokubaliana na uongozi kuwa ndiyo dira na mwelekeo wa taasisi.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernald Konga amesema kuwa mfuko huo utaendelea kushirikiana na Serikali, kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ili kupunguza au kumaliza kabisa tatizo la upungufu wa dawa nchini.

“Tunajua kuwa upungufu wa dawa katika vituo vya matibabu umekuwa ni mojawapo ya kero kubwa katika sekta ya afya. Ili kuondokana na kero hiyo, Mfuko umeanza kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na upungufu huo kwa kuanzisha mpango maalumu wa kutoa mikopo ya dawa kwa watoa huduma waliosajiliwa ili kuhakikisha kuwa wanachama wetu na watanzania kwa ujumla wanapata dawa kila wanapokwenda kupata huduma za matibabu”,alisema Konga.

Chimbuko la Mabaraza ya Wafanyakazi linatokana na Agizo la Rais Na. 1 la mwaka 1970 lililoagiza kuwa mahali popote penye wafanyakazi wa kudumu kumi na kuendelea panatakiwa pawe na chombo cha kuwawakilisha.

Sekta ya wanyamapori inufaishe zaidi jamii inayoishi pembezoni mwa hifadhi za wanyama

$
0
0
Manufaa yanayotokana na hifadhi za taifa na vivutio vya utalii hayatoshi tu kutumika kama nyenzo ya kupunguza vitendo vya ujangili na uvamizi katika maeneo yaliyotengwa na serikali ikiwa hakutakuwa na ushirikishwaji wa kutosha na wa moja kwa moja kwa wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka rasilimali hizo.

Pamoja na mchango mkubwa wa utalii katika uchumi taifa na kuwepo kwa manufaa kwa vijiji vinavyozunguka hifadhi za taifa na vitutio vingine vya utalii, jamii bado imeshindwa kuzitambua faida hizo ili kushiriki kikamilifu katika kupambana na ujangili na uvamizi holela wa maeneo hayo.

Je, jitihada zinazofanywa na serikali na wadau kutoa elimu kwa jamii na kuibua fursa muhimu katika sekta hii zinatosha?

Ili kujibu swali hilo Jukwaa linalohusu masuala ya Usimamizi Shirikishi wa jamii wa maliasili mnamo Mei 26, 2016 limewakutanisha wadau wa mazingira, maliasili na utalii kujadili mambo muhimu yanayoweza kuchangia katika kufungua milango ya fursa katika sekta ya wanayamapori.
Mratibu wa Jumuiko la Maliasi Tanzania (TNRM), Faustine Ninga akifafanua jambo wakati wa Jukwaa la Masuala ya Usimamizi Shirikishi wa Jamii wa Maliasili lililofanyika Mei 26, 2016 jijini Dar es Salaam.
Demetrius Kweka kutoka Engility, (wasimamizi na waendeshaji wa mradi wa PROTECT), akizungumzia hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo
Wadau wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano huo
Afisa Utalii Mwandamizi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Wilfred Msemo akiwasilisha mada
Meneja Msaidizi wa Hifadhi ya Taifa ya Selous, akiwasilisha mada wakati wa Jukwaa la Masuala ya Usimamizi Shirikishi wa Jamii wa Maliasili lililofanyika Mei 26, 2016 jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS SAFARINI PAPUA NEW GUINEA

$
0
0
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anaondoka nchini leo kwenda Papua New Guinea ambako atamwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (ACP) ambao utafanyika kuanzia Mei 30 hadi Juni 01, mwaka huu.

Mkutano wa Papua New Guinea ambao utatanguliwa na mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za ACP utafanyika chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mhe. Peter O'Neil.Kauli mbiu ya mkutano huo wa mwaka huu ni "Umuhimu wa nchi za ACP kujipanga kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za maendeleo endelevu."

Maeneo ya mjadala ni pamoja na kukuza usawa na maendeleo endelevu kwa ajili ya wananchi wa nchi wanachama, kuimarisha majukumu ya nchi za ACP katika utawala bora na maendeleo na pia masuala ya amani, usalama and utulivu wa kisiasa kama ni sharti mojawapo kwa maendeleo.
Kwa sasa umoja huo wa ACP una nchi wanachama 79 ambapo kati ya hizo nchi 48 ni za kutoka kusini mwa jangwa la Sahara, 16 kutoka Caribbean na 15 kutoka Pacific.

Umoja wa nchi za ACP ulianzishwa baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa Georgetown mwaka 1975 kwa msaada wa iliyokuwa Tume ya Uchumi ya Ulaya kwa madhumuni ya kuratibu ushirikiano baina ya nchi wanachama na Umoja wa Ulaya ukizingatia kwamba nyingi ya nchi hizo ni makoloni ya nchi za ulaya.

Katika msafara huo Makamu wa Rais amefuatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dk. Servacius Likwelile na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Celestine Mushi.
Makamu wa Rais na ujumbe wake anatarajia kurudi nchini Juni 3,mwaka huu.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
27/5/2016

AZAM MEDIA YASAINI MKATABA WA BILION MBILI KURUSHA LIGI YA WANAWAKE NA U20.

$
0
0

 Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu nchini(TFF), Jamal Malinzi,(Kushoto) akizungumza kabla ya kusaini mkataba kati ya TFF na Azam Media kwaajili ya kurusha matangazo ya mpira wa Miguu, Ligi ya Wanawake Taifa na Ligi ya Vijana wa chini ya miaka 20. Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Ryhs Torrington.
Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu nchini(TFF), Jamal Malinzi,(Kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Ryhs Torrington wakibadilishana mikataba jijini Dar es Salaam leo.
 Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu nchini(TFF), Jamal Malinzi,(Kushoto) na  Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Ryhs Torrington wakisaini Mkataba wenye thamani ya shilingi bilioni mbili kwaajili ya kurusha matango ya Mojakwa moja ya Ligi ya wanawake na vijana wa chini ya miaka 20.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHIRIKISHO la mpira wa miguu Nchini (TFF) limeingia mkataba na kampuni ya Azam Media wenye thamani ya Bilioni 2 kwa muda wa miaka mitano ikiwa ni kwa ajili ya kurusha matangazo ya ligi kuu ya wanawake pamoja na ligi ya vijana U-20 itakayoanza mwezi August mwaka huu.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Raisi wa TFF, Jamal Malinzi amesema kuwa mkataba huo ni wa miaka mitano ambapo ligi kuu ya vilabu vya wanawake itaanza kwa kushirikisha klabu 10 huku ligi ya U20 ikishirikisha timu zote zitakazokuwa ligi kuu na sheria itatungwa kama kuna timu yoyote itashindwa kuingiza wachezaji uwanjani itakatwa pointi tatu.

"Kama klabu itashindwa kuingiza timu ya vijana uwanjani itakatwa alama tatu na kanuni hiyo itatungwa rasmi kuanzia msimu ujao pia naamini huu utakuwa ni mwanzo mzuri wa vijana kupata nafasi za kuibua vipaji vyao, na nazitaka timu za wanawake wawe wavumilivu kwani tutaanza na timu 10 kisha tutaendelea kuziongeza kadri siku zinavyokwenda,"amesema Malinzi. Azam media imekuwa ikishirikiana naTFF katika kukuza na kuboresha tasnia ya michezo hususani mpira wa miguu nchini kwa kuingia mikataba kama hii ya urushaji wa matangazo ya moja kwa moja.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wanawake,Amina Kaluma amewashukuru sana kampuni y Azam Media kwa hatua ya kununua haki za matangazo na kuziwezesha timu za wanawake kuanzisha ligi yao itakayokuwa na tija kwa kusaidia kuinua soka la wanawake.

"Nawashukuru sana Azam Media kwa hatua mliyofikia ya kununua haki za matangazo na kuziwezesha timu za vijana na wanawake pia mmekuwa na mchango mkubwa sana kwenye kuinua mpira wa miguu nchini,"amesema Kaluma. Changamoto kubwa ni kutokuwa na waamuzi,makocha,makamisaa wanawake kwahiyo kwa heshima zaidi nawaomba mjitokeze kwenye kozi mbalimbali kwani kama tukiwa mbele zaidi tunaweza kuisimamia ligi yetu wenyewe.

Naye Mkurugenzi wa Azam Media, Rhys Torrington amesema kuwa wanatarajia kupanga ratiba itakayoenda sawa na ligi kuu kwani watakachokiangalia ni kuweza kupanga ratiba ya ligi ya vijana iende sawa na mechi za ligu kuu na hilo anawaomba TFF kuweza kuliangalia hilo.

Mkataba huo utawezesha timu la ligi kuu zilizokuwa zinalalamika kuhusiana na kusafiri na timu za U20 kuanza kwenda nazo kokote kutokana na kulalamika kutakuwa na fedha za kutosha.

Hotuba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Wakandarasi, 26 mei 2016

Wasanii wa Kundi la Weusi na Isha Mashauzi kuzindua kampeni ya Chandarua Kliniki leo mkoani Mtwara

$
0
0
Kundi la Wasanii wa Hip Hop Weusi.
Na Mwandishi wetu Mtwara

Wasanii Aisha Ramadhani maarufu Isha Mashauzi na kundi la muziki wa Hip hop la Weusi wanatarajiwa kushiriki katika kuhamasisha mapambano dhidi ya ugonjwa malaria katika mradi unaojulikana kama KLINIKI CHANDARUA.

Mradi huo unaotarajiwa kutoa vyandarua bure kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa unazinduliwa jumamosi wiki hii Mkoani Mtwara.

Mkurugenzi wa matekelezo kutoka mradi wa Victor Works Bi, Noela Kisoka amesema wasanii hao watashiriki katika kuhamasisha kampeni hiyo kwa kupitia muziki na wao watashiriki katika uzinduzi wa mradi huo.
Isha Mashauzi

" Tunatarajia kuwa na wasanii kutoka katika kundi la Weusi ambao wanaimba muziki wa kizazi kipya lakini pia tutakuwa na mwanamuziki wa Taarab Isha Mashauzi ikiwa ni hatua ya kuufanya muziki kuwa sehemu ya hamasa ya utekelezaji wa mradi huu" alisema Kisoka.

" Wananchi wa Mtwara wajitokeze kwa wingi kutazama burudani ya muziki wa wasanii hao lakini pia kupata taarifa kuhusiana na Mradi wetu wa KLINIKI CHANDARUA ambao siku hiyo (leo) ndio tutauzindua" alisisitiza Kisoka.

Wasanii hao wamewasili jana jioni mkoani mtwara,tayari kuwasha moto katika uzinduzi wa mradi huo unaotarajiwa kufanyika katika viwanja vya mashujaa mkoani hapa.

Mradi wa KLINIKI CHANDARUA utazinduliwa mkoani mtwara na mkuu wa mkoa huo Halima Dendego na unatekelezwa kwa pamoja kati ya serikali ya Tanzania, shirika la Victor Works na kudhaminiwa na shirika la misaada la marekani USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria.

DC WA KINONDONI,MH ALLY ASHIRIKI ZOEZI LA USAFI KIMARA

$
0
0
Mh DC Ally Salum Hapi Hapi wa Kinondoni Mapema Leo amefanya usafi na Wananchi wa Kimara pamoja na Vikundi mbali mbali Vikiongozwa na HIDAYA FOUNDATION ambao walikutana Pamoja hospitali ya Kimara na kufanya usafi Hapo.

DC alifika nakufanya usafi kwa pamoja na wananchi na Vikundi Hivyo zaidi ya 5 ambavyo walishirikiana na Wananchi kufanya usafi.Kisha baada ya usafi Palikuwa na Matembezi toka Hospitali mpaka Kituo cha Suka ambapo ndiko palisomwa Lisala na Hotuba ya Mgeni Rasmi.

Mh DC Amewaomba Wananchi hao kuwa Waendelee kujitolea kuhudumia na kusaidia Jamii."Kwani usafi ni Jambo muhimu sana na Jambo hili si la serikali kwani ukiumwa kipindupindu Ni wewe na Sio Serikali, hiyvo tujitahidi kutunza maeneo tunayoishi. Lakini pia tujitahidi kusaidia kwa Hali na Mali Jamii yetu kwa kutoa Misaada mbali mbali ya Kijamii ili kuisaidia Serikali",Alisema Mh DC Hapi.

Changamoto kubwa wameomba Kituo cha Police kwani Mitaa ya Kimara kuna wizi na Ujambazi umekuwa ukifanyika kwa kiasi kikubnwa katiaka maeneo hayo.Aidha Dc amewahidi Wananchi hao kuishughulikia changamoto hiyo.
 DC Mh Ally Salum Hapi akisalimiana watu mbalimbali wakiwemo na wana kikundi cha HIDAYA FOUNDATION,Kabla ya kuanza zoezi la usafi mapema leo asubuhi Kimara,jijini Dar
  DC wa Kinondoni,Mh Ally Salum Hapi pichani kati akiwa sambamba na baadhi ya Wananchi wakishiriki usafi
 DC wa Kinondoni,Mh Ally Salum Hapi akizungumza na baadhi ya Wananchi mbalimbali mapema leo kabla ya kuanza kufanya usafi na Wananchi wa Kimara pamoja na Vikundi mbali mbali Vikiongozwa na HIDAYA FOUNDATION ambao walikutana Pamoja hospitali ya Kimara na kufanya usafi hapo.

SHIRIKISHO LA RIADHA TANZANIA LAMSHUKURU RAIS WA TFF,JAMAL MALINZI KWA MCHANGO WA TIMU YA TAIFA YA RIADHA INAYOJIANDAA NA OLYIMPIC.

CCM Z’BAR YAWATAKA VIONGOZI WAKE KUPAMBANA NA UPOTOSHAJI.

$
0
0

Na Is-haka Omar, Zanzibar.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewaagiza viongozi wake kuzisoma vizuri Katiba ya CCM, Kanuni za maadili na Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, ili wawe na uwezo wa kujibu hoja za baadhi ya watu wanaosambaza fitna na uzushi wa kukichafua chama hicho.

Kimesema kiongozi yeyote mwenye uwezo na uelewa mzuri juu ya miongozo hiyo hawezi kuyumbishwa na kauli na maneno ya mitaani badala yake atakuwa na msimamo imara wa kusimamia maslahi ya chama kupitia vikao halali.Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai wakati akizungumza na viongozi mbali mbali wa Chama kuanzia ngazi za matawi hadi wilaya huko katika Wilaya ya Amani Kichama, Unguja.

Aliwasihi viongozi hao kutumia vikao halali vinavyokubalika kikanuni kujadili changamoto na kasoro zinazojitokeza ndani ya chama kwa lengo la kuepuka maneno ya mitaani yanayoweza kusababisha migogoro isiyokuwa ya lazima ndani ya CCM.Alisema baada ya chama hicho kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa Marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu kwa asilimia 91, kilichobaki kwa sasa ni viongozi na wanachama kushirikiana vizuri na Rais, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani kusimamia vizuri Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho yam waka 2015/2020.

“ Sisi viongozi tukiendelea kuwa wamoja na wenye kushirikiana kwa lengo la kusimamia maslahi ya CCM kwa vitendo basi, naamini kwamba chama chetu nacho kitaendelea kuwa imara na kushinda kwa kila uchaguzi.

Pia tujue kwamba ushindi wa uchaguzi mkuu wa marudio ndio mwanzo wa kujipanga kimikakati kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020, kwani hakuna muda tena wa kusubiri ni lazima tuwe karibu zaidi na wanachama wetu ambao ndiyo wapiga kura wetu.”, alisisitiza Vuai huku akiwasihi vuiongozi hao kusoma alama za nyakati kwa kutathimini changamoto na kasoro zilizotokea katika uchaguzi mkuu uliopita ili zisizokee tena katika uchaguzi ujao.

Naibu Katibu Mkuu huyo, aliendelea kufafanua kwamba CCM ni chama chenye asili ya amani na utulivu na kinachoamini kwamba umoja na msikamano ndiyo fursa ya kuifikisha katika kilele cha Zanzibar na maendeleo endelevu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.Akizungumzia suala la ajira, Vuai aliwashauri vijana kutokata tamaa kwani CCM inaendelea kuikumbusha serikali kutafuta njia mbadala za kuhakikisha vijana wenye sifa, vipaji,uwezo na maarifa ya ujuzi mbali mbali wa chama hicho wananufaika na matunda ya ajira kutoka serikalini ama sekta binafsi.

Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo, alilaani vikali kitendo cha Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad katika ziara yake ya Pemba cha kuwakataza wananchi hasa wafuasi wake wasilipe kodi na kuwapandikiza mbegu za chuki zinazolenga kuingiza nchi katika migogoro inayoweza kuathiri uchumi wa nchi.Alisema kitendo hicho hakikubaliki kwani kinavunja sheria za nchi na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kwa makusudi jambo linalotakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria na vyombo vya dola kabla nchi haijangia katika machafuko.

“Sio kwamba serikali inamuogopa Maalim Seif bali inafanya kila jambo kwa kufuata sheria na Katiba ya nchi, lakini pia ni lazima tukumbuke kwamba hakuna mtu aliyekuwa juu ya sheria.”, alisema Vuai na kuwasihi wananchi hasa wafuasi wa CCM wasiwe na jazba na watulie huku wakisubiri mamlaka husika zichukue hatua kwa watu wanaovunja sheria za nchi.Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Amani Kichama, Abdallah Mwinyi alimuahidi Naibu Katibu Mkuu huyo kuyafanyia kazi mambo yote yaliyotolewa kama nasaha na ushauri kwa lengo la kuongeza ufanisi wa kiutendaji ndani ya chama hicho.

Nao baadhi ya viongozi wa ngazi mbali mbali waliohudhuria kikao hicho, wameelezea kuridhishwa kwao na mikakati mizuri iliyopo ndani ya chama itakayosaidia kufanikisha ushindi wa dola katika uchaguzi mkuu 2020.Pamoja na hayo wameahidi kuendelea kuwa wamoja katika kulinda maslahi ya CCM kwani ndiyo chama pekee kinachojali na kuthamini utu wa wananchi kupitia kauli njema za kuhimiza amani na utulivu wa nchi.

MAHAKAMA ZA GEITA ZATAKIWA KUMALIZA KESI KWA WAKATI

$
0
0
Na Lydia Churi – Geita

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman amezitaka Mahakama za mkoa wa Geita kuhakikisha zinamaliza kesi kwa wakati ili kutekeleza lengo lililowekwa na Mahakama ya Tanzania.

Akizungumza na watumishi wa Mahakama jana mkoani Geita, Jaji Mkuu alisema Mahakama ya Tanzania ilijiwekea malengo ya kumaliza kesi katika mahakama zake kwa wakati kulingana na aina ya mahakama.

Alisema kwa mahakama za Hakimu Mkazi, mahakama za Wilaya pamoja na Mahakama za Mwanzo lengo lilikuwa ni kumaliza kesi zote ndani ya mwaka mmoja ili kuwafanya wananchi kuendelea kuwa na imani na mahakama zao kwa kuwa ni zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wanahudumiwa na mahakama hizo. 

Jaji Mkuu alisema kwa mahakama za Mwanzo ambazo ziko 970 nchini kote lengo lilikuwa ni kuhakikisha hazikai na kesi kwa zaidi ya miezi sita kwa kuwa ndizo mahakama zinazohudumia wananchi wengi zaidi. 

Alisema ili kuziwezesha Mahakama kutekeleza lengo walilojiwekea, tayari Mahakama ya Tanzania imeajiri Mahakimu wapya 107 ambao watasambazwa kwenye Mahakama zote za Mwanzo nchini kwa ajili yakwendakutoa huduma ya msingi ya mahakama ya kutenda haki kwa wananchi wa Tanzania.

Akizungumzia suala la utoaji wa nakala za hukumu, Jaji Mkuu amezitaka Mahakama za mkoa wa Geita kutoa nakala hizo mapema iwezekanavyo ili kutoa haki ya kukata rufaa kwa wananchi ambao hawakuridhishwa na hukumu walizopewa katika kesi zao.

Alisema Mahakama ya Tanzania itaongeza idadi ya Makatibu Mahususi na kuongeza vifaa katika Mahakama zake ili kuongeza kasi ya uchapaji wa nakala za hukumu. Alisema asilimia 80 ya bajeti inayotolewa kwa muhimili huo imetengwa kwa ajili ya kuendesha kesi katika mahakama za Mwanzo, Wilaya na zile za Hakimu Mkazi.

Jaji Mkuu anaendelea na zaira yake katika Mahakama Kuu kanda ya Mwanza ambapo anatembelea mikoa Mwanza, Geita na Mara ili kukagua shughuli za kimahakama katika kanda hiyo.

TANCDA YAPIMA AFYA ZA WABUNGE DODOMA

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalum, Bupe Mwakang'ata (CCM) Mkoa wa Rukwa, akipimwa mapigo ya moyo wakati wa programu maalumu ya wabunge kupimwa afya zao. Programu hiyo ilifanywa bure na Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza katika Zahanati ya Bunge, Dodoma leo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Leonidas Gama akipimwa afya na Muuguzi Asha Shao bungeni Dodoma
Mbunge wa Viti Maalum, Joyce Sokombi akipimwa afaya na Muuguzi kutoka Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Asha Shao. Katikati ni muuguzi mwingine Christina Chamwela
Mhudumu wa Afya wa Hospitali ya Dodoma akimpima kimo Mbunge
Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, Costantine Kanyasu akipimwa mapigo ya moyo
Mbunge Kanyasu akipimwa kimo
Mbunge wa Jimbo la Nachingwe, Hassan Masala akipimwa kimo
Mbunge wa Jimbo la Makambaku, Deo Sanga akipimwa afya
Baadhi ya wabunge wakipata ushauri nasaha
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images