Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 858 | 859 | (Page 860) | 861 | 862 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Mkandarasi wa Estim Construction anayejenga daraja la Ruvu chini akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa alipokagua ujenzi huo.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Estim Construction kukamilisha ujenzi wa Daraja la Ruvu chini  kwa wakati.
   Muonekana wa nguzo za Daraja la Ruvu chini lenye urefu wa mita 140 ambalo ujenzi wake unaendelea katika barabara ya Msata-Bagamoyo.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikagua vifaa vitakavyofungwa kwenye kingo za Daraja la Ruvu chini ili kukabili mafuriko.
   Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Eng. Manase Ole Kujan (Kushoto), akitoa taarifa ya kikao kazi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (Katikati) katika mafunzo elekezi kwa Watendaji wakuu, Mameneja na Wazalishaji wa wakala huo mkoani Morogoro.

   Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi na Umeme wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Dkt. Wiliam Nshama (Kulia), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (Katikati), katika kikao kazi Mkoani Morogoro. 
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Watendaji wakuu, Mameneja na Wazalishaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), katika kikao kazi Mkoani Morogoro.
   Watendaji Wakuu, Mameneja na Wazalishaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa wakati wa mafunzo elekezi Mkoani Morogoro.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa akikagua ujenzi wa Daraja la Ruvu chini lenye urefu wa mita 140 katika barabara ya Msata –Bagamoyo, Daraja hilo linatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0


  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO 

  Serikali imefanikiwa kuwezesha vikundi 1200 vya wakulima wadogo wadogo nchini ili kupata masoko ya uhakika ya mazao yao wanayozalisha.

  Akizungumza kuhusu mradi wa kuboresha miundombinu ya masoko,uongezaji wa thamani na huduma za kifedha vijijini (MIVARF) Mratibu wa Taifa wa Mradi huo Bw. Walter Swai amesema malengo ya mradi huo ni kuongeza kipato cha wakulima na uhakika wa chakula kwa kutengeneza miundombinu ya upatikanaji wa masoko kwa wakulima kwa kuboresha barabara za kutoka mashambani kuelekea sokoni na kuwapa taarifa sahihi kuhusu masoko na mahitaji yake.

  Bw Walter Swai ameongeza kuwa lengo la mradi ni kufikia vikundi 1,600 kwa nchi nzima katika kutoa elimu ya kuwezesha wakulima kupata masoko ya mazao yao ikiwa ni jitihada za Serikali kuwawezesha wakulima hao kujikwamua kiuchumi.

  “Nia yetu ni kufikia vikundi 1,600 katika mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani na hadi sasa tumefika asilimia 75 ya lengo tulilojiwekea la kuwawezesha wakulima wadogo kupata masoko ya mazao yao” alisema Bw.Swai.
  Naye Mtaalamu wa Masoko ya mazao ya kilimo wa MIVARF Bw. Muhoni Leonard amesema kuwa mradi huo utasaidia kuwapa wakulima taarifa sahihi juu ya masoko na mahitaji yake na kupunguza gharama ambazo zilikuwa zinatumika kwa ajili ya kupata taarifa hizo kutoka kwa madalali.

  “Azma ya mradi huu ni kubadili muundo na utendaji wa wakulima wadogo kuongeza ufanisi katika uzalishaji na upatikanaji wa masoko ya mazao husika” alisistiza Bw Leonard.

  Aidha, mmoja wa wakulima na msindikaji wa mchele kutoka Wilaya ya Chato mkoani Geita Bw.Joseph Nchimani amesema kuwa elimu aliyoipata kutoka MIVARF imemuwezesha kuendesha kilimo cha mpunga kwa njia ya kisasa ambayo imemuwezesha kuongeza thamani ya mchele kwa kuufunga kwenye mifuko iliyo katika hali ya 
  ubora unaokubalika kwenye soko.

  “Kabla ya kuanza kufunga mchele kwenye mifuko nilikuwa nauza jumla ya tani mbili mpaka kumi kwa mwaka ila baada ya MIVARF kuja na kunipa elimu hii nimeweza kuuza mpaka kufikia tani 50 kwa mwaka” alisistiza Bw.Nchimani.

  Program hiyo ya MIVARF inajushughulisha pia na kutoa huduma za kifedha vijijini ambayo ni ya miaka saba inayotekelezwa kwa mikoa 30 ya Tanzania Bara na Visiwani na inasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO

  Tanzania imepiga hatua kubwa sana katika sekta ya mawasiliano  hadi kufikia kuwa kwenye kundi la  nchi zilizoendelea kimawasiliano Duniani.

  Takwimu zinaonyesha kuwa watanzania takribani milioni 39 wana laini za simu za kiganjani pamoja na watumiaji wa intaneti takribani milioni 20 ambapo miaka ya nyuma idadi ya laini za simu za kiganjani zilikuwa 2,963,737.

  Haya ni maendeleo makubwa yanayoifanya Tanzania kuwa nchi bora kwa upande wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James Kilaba alisikika akisema kwamba,"Ukuaji wa kasi wa sekta ya mawasiliano nchini umechangia sio tu katika kuboresha maisha ya wananchi kijamii na kiuchumi bali unachangia sana katika kuinua pato la Taifa".

  Ukuaji huu umetokana na kuwepo kwa sera, sheria, kanuni na mfumo mzuri wa utoaji leseni za huduma za mawasiliano.

  Kama wasemavyo wahenga kuwa ya Kaisari tumpe Kaisari basi sifa zote ziwaendee Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa kazi nzuri wanazozifanya.

  TCRA wana jukumu la kusimamia shughuli  hizo zote wakishirikiana na wadau wa mawasiliano nchini katika kusimamia na kuzitekeleza kwa makini sera,sheria na kanuni hizo ili kuwezesha kupatikana kwa huduma za mawasiliano nchini kote kwa kushawishi uwekezaji ,kusimamia vizuri ushindani pamoja na kutoa fursa sawa kwa watoa huduma.

  TCRA inaendelea kuhakikisha kuwa rasilimali adimu zikiwemo za masafa na namba za simu zinatumika kwa makini ili kukidhi mahitaji ya Taifa na maendeleo ikiwa ni kutekeleza lengo la Serikali la kuwawezesha wananchi wote kupata habari na kuhakikisha hawaachwi nyuma katika maendeleo ndani ya karne hii ya utandawazi.

  Huduma hizi za mitandao pia zimegawanyika kutokana na kutofautiana kwa mahitaji ya wananchi. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,  huduma za mitandao ni kama ifuatavyo; Intaneti, Benki Mtandao, Elimu Mtandao, Matibabu Mtandao,Biashara Mtandao, Malipo Mtandao pamoja na Mawasiliano Mtandao.

  Huduma hizi zimekuwa zikirahisisha mambo mengi hasa ya kikazi na ya kijamii,ukiangalia kwa sasa ofisi zote za umma na za binafsi wanatumia huduma za mitandao katika kufanya shughuli zao zote za kiofisi kama njia salama ya kuhifadhi data zao.

  Kwa ofisi za  Serikalini wameipa huduma hii jina la Serikali Mtandao (E-Government) ambapo watumishi wa umma wanashauriwa kutumia mtandao huu ili kuhakikisha kazi zote za ofisi zinafanyika katika hali ya usalama na usiri mkubwa.


  Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Nuru Mllao anasisitiza umuhimu wa watumishi wa Umma kupata mafunzo ya huduma za mitandao ili kuepuka matatizo yanayotokana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii wakati wakuteleza majukumu yao.

  “Tumegundua kwamba watumishi wanahitaji muongozo juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, hivyo tunashkuru sana uongozi wa TCRA kukubali kutoa mafunzo kwa watumishi wetu,”alisema Bi.Nuru wakati wa mafunzo ya watumishi kuhusu masuala ya mawasiliano.

  Kwa upande mwingine, jamii inatumia huduma za mitandao kwa ajili ya mawasiliano kupitia intanenti ambapo kama tulivyosema hapo awali jumla ya wananchi milioni 20 wanatumia huduma za intanenti ambazo zinahusisha matumizi ya mitandao ya kijamii kama ya facebook, instagramu,WhatsApp, Forums, Linkedin pamoja na barua pepe katika kuwasiliana kati ya mtu mmoja na mwingine.

  Matumizi hayo ya mitandao ya kijamii pia ni muhimu kwa wananchi kwa kuwa inatumika kama njia rahisi katika kupashana habari kwa haraka na kufanya dunia kuonekana kama kijiji kwani watu hupata habari za masafa ya mbali kwa haraka.

  Kama tunavyojua "Kizuri hakikosi kasoro", japokua matumizi ya huduma za mitandao yana faida nyingi lakini kuna baadhi ya madhara hutokea kama mitandao hiyo ikitumiwa vibaya.

  Meneja Mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy anasema kuwa ongezeko la watumiaji wa huduma za mawasiliano linaenda sambamba na ongezeko la vifaa mbalimbali vinavyowezesha mawasiliano hayo kufanyika.

  "Miongoni mwa vifaa hivyo ni pamoja na simu za kiganjani,vifaa vya mawasiliano ya kiganjani (tablets), kompyuta pamoja na modemu, kadri idadi ya watu na vifaa vya mawasiliano vinavyoongezeka ndivyo matumizi mabaya ya mitandao yanazidi kuibuka,"anasema Mungy.

  Kuna baadhi ya wananchi ambao tunaweza kusema hawana maadili ya kutosha ambao wanatumia vibaya huduma hizi za mitandao kwa ajili ya kujinufaisha kwa njia zisizo za halali pamoja na kuupotosha umma kwa kutuma vitu ambavyo viko  kinyume na maadili ya mtanzania.

  Matumizi mabaya ya mitandao yanapelekea kuwepo kwa madhara kama ya mauaji, wizi, ukiukwaji wa maadili, ugomvi na kutokuelewana katika jamii zetu.

  Ili kuzuia madhara haya ni lazima kila mmoja azingatie matumizi sahihi ya huduma za mitandao. Mamlaka inayosimamia Huduma za Mawasiliano nchini imeelezea baadhi ya mambo muhimu ambayo yatasaidia kuimarisha usalama pindi utumiapo huduma hizo.

  Unatakiwa kutotumia nywila (password) moja kujiunga kwenye mtandao zaidi ya mmoja wala kuweka nywila ambazo mambo yako binafsi ambayo yanajulikana kwa watu wengi ili kuzuia mtu mwingine asipate urahisi wa kubuni kuingia katika mtandao wa mtu mwingine.

  Unashauriwa kubadilisha nywila mara kwa mara pamoja na kutengeneza nywila ambayo ina muunganiko wa namba na herufi ili isiwe rahisi mtu mwingine kuibuni pia nywila ni siri yako hushauriwi kumpa mtu mwingine yoyote.

  Aidha, hutakiwi kuiandika sehemu yoyote kwa ajili ya kumbukumbu wala kukubali au kujibu barua pepe zinazotoka kwa watu usiowajua kwa kuwa wanaweza kutumia kama njia ya kufahamu  nywila yako.

  Mamlaka ya mawasiliano Tanzania inawasisitiza wananchi kujifunza njia bora za kutumia mawasiliano hususani matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii ili iweze kuwanufaisha na kuendelea kukuza uchumi wa nchi kuliko kuitumia vibaya hatimaye ikaleta madhara ambayo yatasababisha matatizo kwa mtu binafsi au Taifa kwa ujumla.

  Watanzania tunatakiwa kubadilika kulingana na hali halisi ya maendeleo ya nchi yetu ambapo kwa sasa teknolojia ya huduma za mitandao inazidi kukua kwa kasi hivyo kurahisisha zaidi huduma muhimu.
  Huduma hizi za mitandao ni kwa ajili ya wananchi wote, hatutakiwi kuziacha  zitupite kushoto.

  0 0


  Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Amis Tambwe akishangilia bao la kuongoza aliloipatia timu yake dhidi ya Azam FC , katika mchezo unaopigwa hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, ikiwa ni Fainali ya Mashindano ya Kombe la Shirikisho (ASFA). hadi Timu ya Globu ya Jamii inaingia mitamboni, Yanga wanaongoza kwa Bao 3-1. Picha na Othman Michuzi.

  Kiungo Mshambuliaji wa timu ya Azam FC, Ramadhan Singano "Messi" akiichambua ngome ya Timu ya Yanga, katika mchezo unaopigwa hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, ikiwa ni Fainali ya Mashindano ya Kombe la Shirikisho (ASFA). hadi Timu ya Globu ya Jamii inaingia mitamboni, Yanga wanaongoza kwa Bao 3-1.
   Mchezaji wa timu ya Yanga Oscar Joshua akimzuia mchezaji wa timu ya Azam FC Himid Mao kwenye mchezo wao wa Fainali ya Mashindano ya Kombe la Shirikisho (ASFA) unaochezwa jioni hii uwanja wa Taifa jijini Dar. hadi Timu ya Globu ya Jamii inaingia mitamboni, Yanga walikuwa wanaongoza Bao 3-1.
  Lango la Azam  FC likiwa hatarini kuvunjwa. 


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (katikatki) akifuatana na Gavana wa Comoro Bw.Hassan Hamadi (kulia) wakati alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Comoro jana akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,katika sherehe za kuapishwa Rais mteule wa Muungano wa Comoro Kanali Azali Assoumani, akiwa na ujumbe aliofuatana nao akiwemo Mama Mwanamwema Shein,(kushoto) Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Visiwa vya Comoro Dr.Ahamada El Badaoui Mohamed.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Gavana wa Comoro Bw.Hassan Hamadi wakati alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Comoro jana akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,katika sherehe za kuapishwa Rais mteule wa Muungano wa Comoro Kanali Azali Assoumani,akiwa na ujumbe aliofuatana nao akiwemo Mama Mwanamwema Shein,
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro Mhe,Chabaka Chilumanga Fereji wakati alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Comoro jana akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,katika sherehe za kuapishwa Rais mteule wa Muungano wa Comoro Kanali Azali Assoumani, akiwa na ujumbe aliofuatana nao akiwemo Mama Mwanamwema Shein.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa Muungano wa Comoro wakati alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Comoro jana akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,katika sherehe za kuapishwa Rais mteule wa Muungano wa Comoro Kanali Azali Assoumani, akiwa na ujumbe aliofuatana nao akiwemo Mama Mwanamwema Shein,[Picha na Ikulu].25/05/2016.]

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne akijibu hoja na michango mbalimbali ya wabunge zilizoelekezwa kwenye wizara hiyo wakati wa Majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 ambayo imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 135.7.
  Baadhi ya wabunge wakimpongeza wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe mara baada ya Bajeti ya Wizara hiyo kupitishwa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 ambayo imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 135.7.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akimweleza jambo Mbunge wa Bunda mjini Mhe. Esther Matiku (CHADEMA) nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kupitishwa kwa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017.

  Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii bungeni mjini Dodoma. 


  Na. Aron Msigwa - Dodoma. 

  Serikali imesimamisha utoaji wa vibali na uuzaji wa wanyama hai kutoka katika hifadhi za Taifa kwenda nje ya Tanzania kwa kipindi cha miaka 3 mpaka hapo itakapotangazwa tena.Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ametoa agizo hilo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu hoja na michango mbalimbali ya wabunge iliyoelekezwa kwenye wizara hiyo wakati wa Majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 ambayo imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 135.7.

  Prof. Maghembe ameiagiza Idara ya Wanyamapori ipange na kuweka utaratibu mpya utakaotumika kusimamia biashara hiyo pindi itakaporejeshwa tena baada ya kumalizika kwa muda wa zuio la Serikali la miaka 3 ikizingatia mazingira ya uhifadhi wa wanyama hao.

  USAFIRISHAJI WA WANYAMA HAI  NJE YA NCHI.

  Amesema kumekuwa na taarifa za baadhi ya watanzania wasio waaminifu ambao wamekua wakijihusisha na vitendo vya kusafirisha wanyama hai waliokatazwa kinyume cha utaratibu jambo ambalo limeisababishia Serikali ipoteze mapato kutokana na wanyama hao.

  Akielezea kuhusu wanyama wanaoruhusiwa kusafirishwa nje ya nchi kama nyani, Kenge,ndege, kobe, wadudu na tumbili amesema wanyama hao wamekuwa wakisafirishwa kinyume na utaratibu na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kwa ajili ya kutumiwa na makampuni ya kimataifa kwenye shughuli za utafiti wa kisayansi wa tiba na chanjo.

  Amesema makampuni hayo yamekuwa yakinufaika binafsi kwa kupata fedha nyingi pindi yanapofanikiwa kupata chanjo au tiba husika huku maeneo waliokotoka yakipata fedha kidogo jambo ambalo serikali ya awamu ya tano imeamua kulifanyia kazi.

  UTALII KUSINI MWA TANZANIA NA MAENEO MENGINE. 

  Amesema Serikali itatekeleza miradi mbalimbali ya uboreshaji wa Utalii wa Kusini ili kuweka mazingira wezeshi na kuondoa vikwazo vilivyokuwa vikisababisha watalii kushindwa kufika katika maeneo ya hifadhi za Taifa eneo la ukanda wa kusini mwa Tanzania.

  Baadhi ya maeneo yatakayoshughulikiwa ni gharama ya usafiri wa ndege kwenda na kurudi katika maeneo hayo kuwa kubwa hadi kufikia Dola za kimarekani 1800 jambo ambalo limekuwa kikwazo kwa watalii hao.

  Amesema Serikali itaanzisha vituo vya kuwekea mafuta ya ndege mahali vilipo vivutio vya utalii ili kuziwezesha ndege ndogo kufika kwa urahisi na kupata huduma ya kuongeza mafuta hivyo kupunguza gharama kwa wasafiri wanaotembelea hifadhi za eneo hilo na ndege ambazo hulazimika kurudi jijini. 

  Aidha amesema katika mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali itanunua ndege ndogo abiria ili kuwezeha watalii kufika kwa urahisi katika maeneo ya hifadhiza Taifa.

  UTAMBUZI WA MAENEO MAPYA YA UTALII.

  Serikali kwa kushirikiana na Wakuu wa wilaya, mikoa na Wabunge itaanzisha mpango mpya kuviorodhesha vivutio vyote vya utalii vilivyo katika maeneo yao ili viweze kutangazwa ipasavyo na kuongeza kuwa mara baada ya kukamilika kwa mpango huo itaandaliwa orodha ya vivutio hivyo ili vianzwe kutangazwa rasmi.

  Katika kuimarisha shughuli za utalii nchini serikali itaweka mkazo katika uimarishaji wa utalii wa utamaduni, uimarishaji wa maeneo ya historia na Malikale ili kuwezesha eneo hilo kuchangia zaidi katika pato la taifa.

  ULINZI NA USALAMA WA HIFADHI ZA TAIFA.

  Prof. Maghembe ameeleza kuwa suala la ulinzi na usalama wa hifadhi zote za Taifa liko kwa mujibu wa sheria na kubainisha kuwa serikali imeanzisha Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) litakalochukua mbuga zote zilizokuwa na uongozi ambazo ziko nje ya TANAPA.

  Jeshi hilo litapambana kikamilifu na ujangili, kuimarisha maadili na nidhamu ya askari wa ulinzi wa hifadhi za taifa pamoja na kushughulikia maslahi yao na kuondoa migogoro kati ya askari na wananchi.

  Amesisitiza kuwa mara baada ya Bunge la Bajeti, Wizara itakutana na wahifadhi wakuu wote ili kuweka vigezo vya kuzingatia katika majukumu yao na kusisitiza kuwa wahifadhi wote watakaoshindwa kwenda na kasi ya vigezo vilivyowekwa hawatajumuishwa kwenye jeshi hilo.

  Aidha, amekemea vikali vitendo vinavyofanywa na baadhi ya askari wa hifadhi kupiga raia na kuchoma nyumba za wananchi kuwa havikubaliki na ni kinyume cha majukumu yao.

  " Nimesikiliza kwa makini michango ya wabunge na nimesikia wafanyakazi katika hifadhi zetu wanapiga raia wanaua mifugo na kuchoma nyumba za wananchi jambo ambalo halikubaliki, hatukuwatuma kufanya hivyo" Amesisitiza Prof.Maghembe.

  MIGOGORO YA MIPAKA MAENEO YA HIFADHI.

  Serikali imesema mpaka sasa kuna migogoro ya ardhi 281, kati ya hiyo 35 ambayo ni sawa na asilimia 12.5 ni migogoro ya hifadhi na kuita Mikoa yenye migogoro hiyo kuwa ni pamoja na Mara , Tanga na Kagera inachukua jumla ya asilimia 50.

  Aidha, amesema kuwa mkoa wa Tabora unaongoza kwa kuwa na eneo kubwa la ardhi na unaongoza kwa kuwa na migogoro mingi ya hifadhi kwa asilimia 40.Katika kuishughulikia migogoro hiyo Serikali imeziagiza wizara za Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Maji na Umwagiliaji, TAMISEMI, Nishati na Madini, Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikiana pamoja katika kutatua migogoro yote ya ardhi nchini.

  UBORESHAJI WA MAENEO YA HIFADHI NA MAMLAKA ZA UHIFADHI.

  Amesema katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 kiasi cha shilingi bilioni 1 kimetengwa kushughulikia usafi wa mazingira na ujenzi wa vyoo vya kisasa katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro vitakavyokuwa na uwezo wa kugeuza maji taka kuwa poda ili kuweka mazingira yote ya mlima huo kuwa safi.

  Aidha,amesema kuwa Mamlaka za hifadhi za Taifa zimeendelea kuchangia katika maendeleo ya wananchi katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ujenzi wa madarasa, miundombinu ya barabara, utoaji wa madawati katika halmashauri mbalimbali nchini.

  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Be.Sabasaba Moshingi,(kushoto), akijibu baadhi ya hoja za wajumbe wa Mkutano wa mwaka wa wanahisa wa Benki hiyo jijini Dar end Salaam Leo Mei 25, 2016. Wajumbe walipokea taarifa ya uendeshaji Benki hiyo kwa mwaka 2015 ikiwa ni pamoja na mipango ya uendeshaji wa Benki kwa mwaka huu wa 2016. Pamoja na mambo mengine, Bw.Moshingi alisema benki inampango wa kuingia kwenye soko la his a(Dar es salaam stock exchange), sambamba na kuongeza Huduma za ATM kwenye matawi yake mbalimbali kote nchini. Katikati no Mwenyekiti wa Bodi, Profesa Lettice Rutashobya, na kulia in Katibu wa Bodi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria wa Benki hiyo, Bi.Mystica Mapunda Ngongi.Wakichangia hoja mbalimbali baada ya kupokea taarifa ya mahesabu ya fedha iliyosomwa na Meneja wa kampuni ya ukaguzi wa mahesabu ya Nexia SJ Tanzania, Bw.Fulgensio Mgaya, ambaye alisema mahesabu ya Benki hiyo hayakukutwa na dosari, wajumbe wa mkutano huo, Bi.Theresia A Chitumbi na Bw. James Sando, wameupongeza uongozi wa Benki hiyo kwa usimamizi thabiti na uendeshaji mzuri wa Benki. (PICHA NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said). 
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Benki ya Posta Tanzania, TPB, Profesa Lettice Rutashobya, (wapili kulia), akiendesha mkutano wa mwaka wa wanahisa wa benki hiyo, jijini Dar es Salaam Mei 25, 2016. Kikao hicho kimejadili utendaji kazi wa benki katika mwaka wa 2015/2016 ambapo wajumbe walijadili mapato ya benki, upanuzi wa huduma za kibenki nchini ikiwa ni pamoja na mabporesho ya huduma kwa wateja. Wengine pichani kutoka kulia, ni Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence Mafuru, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar, Bw. Hamisi Mussa Omar.
  Mwenyekiti akiendesha kikao cha wanahisa wa TPB.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Benki ya Posta Tanzania, TPB, Profesa Lettice Rutashobya, (wapili kulia), akiendesha mkutano wa mwaka wa wanahisa wa benki hiyo, jijini Dar es Salaam Mei 25, 2016. Kikao hicho kimejadili utendaji kazi wa benki katika mwaka wa 2015/2016 ambapo wajumbe walijadili mapato ya benki, upanuzi wa huduma za kibenki nchini ikiwa ni pamoja na mabporesho ya huduma kwa wateja. Wengine pichani kutoka kulia, ni Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence Mafuru akizungumza kwenye mkutano huo
  Wakurugenzi wa idara mbalimbali za TPB, wakibadilishana mawazo wakati wa mapumziko
  Katibu Mkuu wizara ya fedha serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw.Hamisi Mussa Omar(kulia), na Mkurugenzi wa sheria na Katibu wa Bodi ya TPB, Bi.Mystica Mapunda Ngongi.
  Picha ya pamoja ya uongozi wa TPB, na wanahisa waliohudhuria mkutano huo
  Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Bw. Sa asaba Moshingi, akipitia makabrasha
  Katibu Mkuu wizara ya fedha, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw.Hamisi Mussa Omar. (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Bw.James Sando wa TPC.
  Msajili wa Hazina kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Lawrence Mafuru, (kushoto), akiteta jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Bw. Sabasaba Moshingi
  Mwenyekiti wa Bodi ya TPB, Profesa Lettice Rutashobya, (kulia), akifurahia jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Bw. Sabasaba Moshingi

  0 0


  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema vita inayoendeshwa na Serikali ya awamu ya tano dhidi ya wala rushwa na wale wanaofanya ufisadi siyo nguvu ya soda kama wengi wanavyofikiri.

  “Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kupambana na wala rushwa na mafisadi. Wala hatutanii. Hawa tutacheza nao na wala wasidhani vita hii ni nguvu ya soda. Tutaendelea kuwasaka hadi tufike mwisho,” alisema Waziri Mkuu wakati akizungumza na Watanzania waishio Zambia katika mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Lusaka, Zambia juzi jioni (Jumanne, Mei 24, 2016).

  “Hatutaki tabia iliyokuwepo ya mwananchi anakuja ofisini kutaka huduma lakini hasikilizwi hadi atoe chochote, sisi hiyo tabia hatutaki kuisikia kabisa. Tumedhamiria kurudisha heshima kwenye utumishi wa umma na nimeanza kupata faraja kwani sasa hivi (nimeambiwa) katika baadhi ya taasisi unasikia mtu akiulizwa una shida gani, nenda pale, jambo ambalo zamani halikuwepo,” alisema.

  Alisema Serikali imeamua kupigia debe dhana ya utumishi wenye uadilifu kwa sababu huo ni utamaduni mpya. “Ni kipindi kigumu kidogo cha mabadiliko lakini tumesimamia mabadiliko haya na ndiyo maana watumishi wote tumewasisitizia kuwa suala la uaminifu, uadilifu na uwajibikaji ni muhimu,” alisema na kuongeza:

  “Hatutamvumilia mtumishi yeyote ambaye hatakuwa tayari kuwatumikia Watanzania au atakayeendekeza uzembe lakini pia hatutamuonea mtu yeyote. Hapa tunasisitiza usawa na hatutaki kutengeneza gap kati ya mwananchi mtumishi na wa mwananchi wa kawaida, tunataka kila mwananchi aione Tanzania ni nchi yake na kila kinachozalishwa ni sehemu yake. Tukifika hapo, tunaamini kila mmoja ataweza kuisemea nchi yake.”

  Akizungumzia kuhusu ubadhirifu wa fedha za umma, Waziri Mkuu alionya kwamba Serikali imelipa kipaumbele suala la uaminifu na uadilifu kwenye fedha za Serikali na kwamba haitakuwa tayari kuona fedha hizo zikifujwa.

  “Hivi sasa Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo na fedha hizo zitaenda vijijini. Tunataka zikafanye kazi iliyokusudiwa, na wale wadokozi wajue kuwa wamekalia kaa la moto,” alisema huku akishangiliwa.

  Alisema watumishi wa umma wana wajibu wa kusimamia kazi zilizopangwa na kuhakikisha miradi iliyolengwa inakamilika. “Kama fedha zimeletwa kujenga zahanati simamia zahanati ijengwe na ni lazima zahanati hiyo ionekane,” alisema.

  Alisema bajeti ya mwaka huu imeongezeka kutoka sh. trilioni 21 hadi trilioni 29 lengo kuu likiwa ni kuleta maendeleo kwa wananchi. “Ndiyo maana tumepandisha bajeti ya maendeleo kutoka asilimia 27 hadi asilimia 40. Ole wake atakayepokea fedha hizi halafu zisifanye kazi yake, ukiipoteza wewe utafute njia ya kwenda,” alisema huku akishangiliwa.

  Akifafanua zaidi, Waziri Mkuu alisema vita inayoendeshwa imelenga kuifanya Tanzania ibadilike na itoke kwenye uchumi wa chini na kuingia uchumi wa kati. “Swali la msingi ni je tunafikaje hapo? Jibu ni kupitia uzalishaji wa bidhaa viwandani,” alisema.

  “Nyote ni  mashahidi wa jinsi ambavyo shilingi yetu imekuwa ikishuka thamani kulinganisha na dola ya Marekani. Tulitoka sh. 1,600/-, tukapanda hadi sh. 1,900/- na sasa tumefikia sh. 2,180/-. Hii ni kwa sababu tunaagiza zaidi bidhaa kutoka nje ya nchi badala ya kuzalisha, hatuwezi kuendelea hivi na ndiyo maana tumeamua kuwa nchi ya viwanda. Leteni mitaji nyumbani muwekeze,” alisisitiza.

  Akijibu swali kuhusu Serikali kutafuta njia ya kutoa mikopo kwa Watanzania waishio nje ya nchi, Waziri Mkuu alisema mkopo ni mkataba kati ya taasisi ya kifedha na mkopaji kwa hiyo Serikali haiwezi kubeba dhamana hiyo. “Benki wanataka ijue taarifa zako mkopaji, wanataka wajua dhamana zako ni zipi, wajiridhishe na shughuli unazofanya. Je panakopesheka hapo?,” alihoji.

  Hata hivyo, aliwaeleza kwamba wakitaka kuwekeza nyumbani wanaweza kupata mikopo kutoka benki ya maendeleo ya kilimo (TADB), Benki ya Rasilmali (TIB Corporate na TIB Development). “Hizi benki ni za wakulima na wajasiriamali, na zina masharti yake, kwa hiyo ni lazima wakakague eneo lako au mahali unapofanyia biashara au wakague leseni yako na ukweli wa maombi uliyopelekea. Sasa ukiwa Zambia watawezaje kukukopesha? Kwa hiyo ukitaka fedha uwe nyumbani,” alisema.

  Akijibu swali ni vipi Serikali itawasaidia wanadiaspora kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wakiwa nje ya nchi, Waziri Mkuu alisema Serikali haijawahi kujaribu jambo hilo licha ya kuwa ilikwishapokea mapendekezo kadhaa kutoka nchi mbalimbali lakini kwa vile wameliuliza, yeye analibeba na kwenda kulifanyia kazi.
    
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  ALHAMISI, MEI 26, 2016.

  0 0


  0 0

  Naomba tuipigie kura Short filamu ya MIKONO SALAMA, Inayowakilisha Tanzania kwenye Shindano la Galway African Film Festival, Ipigie kura kushinda tuzo ya Filamu Bora. 

  Kura yako Moja ni muhimu kwa ushindi, Hii ni kwa ajili ya Uzalendo na Ushindi Kwa Nchi
  Vote, Repost, share kisha Sambaza kwa wingi iwezekanavyo.

  BOFYA LINK HIYO KUIPIGIA KURA FILAMU HIYO.

  Kwa njia Rahisi ya kupiga kura angalia hapo chini.

  IANGALIE FILAMU HIYO HAPA

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wakandarasi  nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) ambapo aliwataka makandarasi wazawa kuwa wazalendo na nchi yao ikiwemo kuepuka vitendo vya rushwa katika maeneo ya Kazi. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wageni na watendaji wa serikali wakati akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
   Kaimu Msajili kutoka Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) Rhoben Nkori akiongea wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB)na kuahidi kuendelea kuwapa kipaumbele makandarasi wazawa na kukabiliana na changamoto zinazowakabil.

   Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) Mhandisi Consolata Ngimbwa akiongea na wakandarasi(hawapo pichani) ambapo aliwataka makandarasi wazawa kufanya kazi kwa weledi na kusisitiza kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa makandarasi wenye nia ya kuwakwamisha.

   Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na wakandarasi  nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) ambapo aliwaahidi makandarasi nchini kuwasimamia kikamilifu na kuwapa fursa na kazi mbalimbali za ujenzi nchini.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi ya mabanda wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi ya mabanda wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi ya mabanda wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo kwa wawakilishi wa makampuni mbalimbali waliowezesha kufanyika kwa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
  PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo kwa wawakilishi wa makampuni mbalimbali waliowezesha kufanyika kwa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
  Baadhi ya Makandarasi nchini wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wakandarasi  nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akielezea majukumu ya ofisi hiyo kwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini Bi. Bella Bird (kulia kwake) alipotembelea leo, Makao Makuu ya Ofisi hiyo iliyopo Barabara ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akielezea majukumu ya ofisi hiyo kwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini Bi. Bella Bird (kulia kwake), Menejimenti ya NBS na wageni walioambatana na Mkurugenzi Mkazi huyo alipotembelea leo, Makao Makuu ya Ofisi hiyo iliyopo Barabara ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam. ( PICHA NA EMMANUEL GHULA)Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Abina Chuwa akimkaribisha Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird (kushoto) alipotembelea leo Makao Makuu ya Ofisi hiyo iliyopo Barabara ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam.

  Na Veronica Kazimoto

  BENKI ya Dunia imeahidi kuendelea kuisaidia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kifedha ili iweze kutekeleza majukumu yake ya utoaji wa Takwimu Rasmi nchini.

  Akizungumza leo alipotembelea Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini Ms. Bella Bird amesema kutokana na umuhimu wa takwimu katika kupanga na kupima matokeo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo, Benki ya Dunia itaendelea kuisaidia NBS ili iendelee kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kutoa takwimu kwa wakati.

  “Ili Ofisi ya Taifa ya Takwimu iweze kutoa takwimu kwa wakati, inahitaji kuwekeza katika matumizi ya technolojia ya kisasa ya ukusanyaji wa takwimu, hivyo Benki ya Dunia itaendelea kutoa msaada wa kiufundi na kifedha ili kufikia malengo yaliyoainishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya utoaji wa takwimu rasmi nchini”, amesema Ms. Bella Bird.

  Mkurugenzi huyo Mkazi amefafanua kuwa Benki ya Dunia inatambua umuhimu wa takwimu katika maendeleo ya nchi zote duniani ikiwemo Tanzania katika kupanga sera na kutekeleza miradi mbalimbali ya nchi husika.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa ameishukuru Benki ya Dunia kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikiisaidia Ofisi ya Taifa ya Takwimu ambayo imeongeza tija katika ukusanyaji na utoaji wa takwimu rasmi nchini.

  “Napenda kuchukua fursa hii kuishukuru Benki ya Dunia kupitia ujio wako kuitembelea Ofisi ya Taifa ya Takwimu na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi hii ikiwa ni pamoja na ukusanyaji na utoaji wa takwimu rasmi hapa nchini,” amesema Dkt. Chuwa.

  Dkt. Chuwa amesema Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeendelea kupanua wigo wa uzalishaji wa takwimu nchini ikilinganishwa na karne zilizopita.

  Benki ya Dunia inaisaidia Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kutoa ushauri wa kitalaam pamoja na fedha kupitia Mpango Kabambe wa Kitaifa wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu nchini ambapo awamu ya kwanza itakamilika mwezi Juni, 2018.

  0 0


  Picha ya Mwanahabari Makongoro Oging' enzi za uwai wake.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers alikokuwa akifanyia kazi Makongoro Oging', Eric Shigongo akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye lenye mwili wa marehemu Oging' wakati wa kuagwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ilala ya Amana Dar es Salaam mchana wa leo.
  Mmiliki wa Blog ya Michuzi, Issa Michuzi akitoa heshima za kwa mwili wa marehemu.
  Mhariri wa Habari wa Gazeti la Champion, Salehe Ali akitoa heshima za mwisho kwa marehemu.

  Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Makongoro kulipeleka kwenye gari kabla ya kuanza kwa safari ya kwenda mkoani Mara. 

  0 0


  Kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikiendelea leo mjini Dodoma.
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson akifuatilia kwa makini michango ya wabunge wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu ndani ya Bunge mjini Dodoma.

  Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.

  Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akijadiliana jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde bungeni mjini Dodoma.

  Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi , Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kwa mwaka 20016/2017 mjini Dodoma. Wizara hiyo katika mwaka wa fedha 2016/2017 imeomba kupitishiwa shilingi Trilioni 1.39 .

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angella Kairuki akifuatilia jambo ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo. Picha/Aron Msigwa-MAELEZO.

  0 0

   Mkurugenzi wa M- bet Dhiresh Kaba (kushoto) akipongezana na Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando (kulia) mara baada ya kuzindua ushirikiano utakaowawezesha wateja watakaobashiri michezo mbalimbali na kisha Mr. Money kuwawezesha  kulipia kwa kutumia huduma ya Airtel Money. akishuhudia ( nyuma kushoto) ni Meneja wa Airtel Money , Asupya Naligingwa.

   Meneja wa Airtel Money, Asupya Naligingwa (kushoto) akiongea wakati wa kuzindua ushirikiano kati ya kampuni ya Airtel na M-bet utakaowawezesha wapenzi wa kubashiri michezo mbalimbali kubaashiri na kisha Mr. Money kuwawezesha kulipia kupitia huduma ya Airtel Money. pichani ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando  katikati) akifatiwa na Mkurugenzi wa M- bet Dhiresh Kaba.

   KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imeshirikiana na kampuni ya M- bet na kuwawezesha wateja wa M-bet kubashiri michezo wa mpira wa miguu ikiwemo ligi E Premier League, Laliga, Bundesliga, Serie A  kisha  kufanya malipo kwa urahisi na usalama kwa kupitia huduma ya Airtel Money

  M- Bet ni kampuni inayowawezesha wateja wake kubashiri mshindi katika michezo mbalimbali ya soka duniani kote.


  Akiongea wakati wa kutangaza ushirikiano huo Mkurugenzi wa M-Bet Mr. Dhiresh Kaba alisema “Mr Money wa Airtel Money ametupatia suluhisho la kupokea malipo na kulipa wateja wetu ushindi wao kwa usalama zaidi, hili limekuja wakati sahihi kwa kwa kuwa sasa tunaelekea msimu mpya wa ligi za mpira wa miguu hasa ligi ya Uingereza ambapo  wanaobashiri wataweza kubashiriri wakiwa popote na kufanya malipo bila ya kuwa na haja ya kutembelea ofisi za M-Bet kwa urahisi na usalama”

  Ili kuweza kufurahia huduma hii unachotakiwa kufanya  tembelea tovuti ya m-bet www.m-bet.co.tz,   pakua  program ya m-bet App.net. Tabiri na ushinde na m-bet.  Mshindi anaweza kushinda hadi shilingi mil 10.  Ili uweze kukamilisha malipo yako huhitaji kubeba pesa tasilimu tena badala yake fanya malipo kwa njia salama ya Airtel Money kwa kupiga  *150*60# kisha chagua namba 5 malipo au(lipia bill) alafu chagua namba 3 weka namba ya kampuni 300300 na kuweka kumbukumbu namba yake. Aliongeza Mr. Dhiresh Kaba wa M-Bet

  Kwa upande wake Meneja wa Airtel Money Mr. Asupya B. Nalingigwa alisema”Mr, Money anaendelea kudhihirisha kauli yake ya kwamba yeye ni nafuu na uhakika pale unapotaka kufanya malipo, leo uzinduzi huu wa kulipia tozo za kubashiri/kubet kwa Airtel Money itasaidia kuwaepusha wateja wanaoshiriki mchezo huo wa kubet/kubashiri  majanga ya kutembea na burungutu la pesa taslim kwa kuwa ni salama zaidi.  

  Nalingigwa alisisitiza kuwa Mr. Money wiki iliyopita alitangaza huduma pekee zinazotolewa na Airtel Money ikiwemo mikopo ya Timiza, nyongeza ya Uniti ukinunua LUKU kwa Airtel Money, nyongeza ya muda wa maongezi au vifurushi kwa Airtel Money bado Mr Money anaendeleza kuweka suluhisho kwa kila mahitaji, bidhaa na huduma mbalimbali”.  

  “ni uhakika kuwa Mr Money sasa atapokea malipo ya wewe unaebashiri na kisha atakulipa pesa ya ushindi wako wakati wowote mara baada ya kuthibitiishwa kuwa wewe ni mshindi na utaitoa kwa WAKALA  yoyote wa Airtel alisisitiza Bw, Nalingigwa.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

  Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imepiga marufuku vikundi vya mazoezi vinavyofanya mazoezi kwenye barabara kuu ya uwanja wa Taifa ili kuzuia foleni na ajali za barabarani.

  Tamko hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa Halmashauri hiyo, Joyce Msumba alipokua akitoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya wananchi kuhusu foleni ya magari inayosababishwa na wachezaji wanaotumia barabara kuu ya Temeke kuelekea uwanja wa Taifa.

  “Halmashauri yetu imepiga marufuku wachezaji wote wanaokimbia kuelekea uwanja wa Taifa kupitia barabara kuu na badala yake wanatakiwa kutumia njia za waendao kwa miguu (service road) zilizopo pembezoni mwa barabara kuu”,alisema Joyce.

  Joyce aliongeza kuwa kila kundi la wachezaji wana viongozi wao ambao walishapewa maelekezo na Halmashauri juu ya suala hilo kwahiyo,viongozi hao wana wajibu wa kuwasimamia wanamichezo wao.Kwa upande wake Afisa Utamaduni wa Halmashauri hiyo, Emmanuel Ndumukwa amewaomba wanamichezo hao kuzingatia sheria za barabarani ili kuepusha ajali.

  “Mara nyingi tunawaeleza wanamichezo wazingatie sana sheria za barabarani pamoja na kutumia bendera nyekundu kama alama ya kuashiria uwepo wao katika barabara ili kuzuia ajali”,alisema Ndumukwa.

  0 0


  Wadau na wateja mbalimbali wanaotumia mtandao wa mawasiliano unaoongoza nchini Vodacom Tanzania,Wanakumbushwa kwamba kununua simu zinazoendana na viwango vya mamlaka ya mawasiliano nchini na kuachana na simu zisizo na viwango vilivyobainishwa na Mamlaka hiyo ili wasiachwe nje ya mtandao tarehe 15 Juni ambayo imetangazwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuwa zoezi hilo la kuzima simu zisizo na viwango litafanyika.

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia amesema kuwa Vodacom ikiwa kampuni inayoongoza kwa kuwa na mtandao mkubwa na watumiaji wengi wa mtandao wake inaamini kuwa kuna baadhi ya wateja wake wako hatarini kuachwa nje ya mtandao kutokana na kutokuwa na simu zenye viwango vilivyobainishwa na Mamlaka ya Mawasiliano.

  “Natoa wito kwa wateja wetu ambao hadi kufikia sasa hawajaangalia kama simu zao zinakidhi viwango ama wameangalia lakini hawajachukua hatua ya kununua simu zenye viwango vinavyotakiwa wafanye hivyo kwa kuwa umebaki muda wa siku chache kabla ya simu zao kuzimwa na kuwaacha nje ya mtandao” alisema Mworia.

  Katika kuhakikisha wateja wake hawaachwi nje ya mtandao alisema kuwa Vodacom kwa kushirikiana na wadau wanaotengeneza simu tayari imeingiza simu zenye kiwango cha ubora na gharama nafuu nchini ambazo zinapatikana katika maduka yake yaliyopo sehemu mbalimbali nchini.

  “Tusingependa wateja wetu waachwe nje ya mfumo wa mawasiliano na kukosa huduma za mawasiliano hivyo tutaendelea kufanya kazi na serikali na taasisi nyingine za mawasiliano kuhakikisha watanzania wanaendelea kupata huduma bora za mawasiliano. Simu zenye viwango na zenye gharama nafuu kuanzia shilingi 18,000/= na kuendelea zinapatikana kwenye Maduka yetu yalioyosambaa kote nchini ” alisema.


  0 0

   
   .  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akisalimiana na Mhe. Jaji Lameck Mlacha alipowasili Mwanza tayari kwa kuanza ziara ya kukagua shughuli za Mahakamakatika kanda ya Mwanza.
    Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
   Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akizungumza na Jaji Mfawidhi wa Mwanza Mhe. Robert Makaramba alipowasili jijini Mwanza tayari kuanza ukaguzi wa shughuli za Mahakama katika Kanda ya Mwanza.

  0 0

  Miss Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara akigawa penseli, vikiwemo vitabu, mabegi ya kubebea vitabu na vitu vingine mahitaji ya shule hiyo ya vidudu ya Highland Nursery school iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam. Vitu hivyo vilitolewa msaada na wadau kutoka Washington, DC.
  Miss Tanzania USA Pageant, Aeesha Kamara akigawa mabegi ya kubebea vitabu kwa watoto wa Highland Nursery School ya Tabata jijini Dar es Salaam.
  Miss Tanzania USA Pageant akiongea na watoto hao wa shule ya Highland Nursery School ya Tabata jijini Dar es Salaam.
  Miss Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara akiwa katika picha ya pamoja na watoto wa Highalnd Nursery school wakiwemo walimu wao.
  Watoto wakimsikiliza Miss Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara (hayupo pichani) alipokua akiongea nao.
  Watoto wakitega sikio kwa makini kumsikiliza Miss Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara (hatyupo pichani) alipokua akiongea nao,

older | 1 | .... | 858 | 859 | (Page 860) | 861 | 862 | .... | 1897 | newer