Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 857 | 858 | (Page 859) | 860 | 861 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Mratibu wa Maji, Afya na Usafiri wa Mazingira kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Theresia Kuiwite (kulia). akizungumza  na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya hedhi salama. Wengine ni Mkurugenzi wa Programu za Afya Mashuleni kutoka Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Orsolina Tolage (kushoto) na Msemaji mwakilishi wa Wadau wote wa Mapendeleo waliochangia maadhimisho hayo, Clare Haule.
   Mkurugenzi wa Programu za Afya Mashuleni kutoka Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Orsolina Tolage (katikati), akizungumza  na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya hedhi salama. Kulia ni Msemaji mwakilishi wa Wadau wote wa Mapendeleo waliochangia maadhimisho hayo, Clare Haule na Mratibu wa Maji, Afya na Usafiri wa Mazingira kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Theresia Kuiwite.
   Msemaji mwakilishi wa Wadau wote wa Mapendeleo waliochangia maadhimisho hayo, Clare Haule  akizungumza  na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya hedhi salama. Kushoto ni Mkurugenzi wa Programu za Afya Mashuleni kutoka Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Orsolina Tolage (katikati).

  Na Mwandishi wetu.
  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Hedhi Salama Duniani ambayo hufanyika   Mei 28 kila mwaka.

  Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Kinga , Orsolina Tolage amesema kuwa suala hedhi salama wanaliangalia sana katika kuweza mazingira bora ya afya ya wasichana.

  Amesema kuwa Wizara ya Afya Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imejipanga kwa kushirikiana na wizara ya elimu na Sayansi na Teknolojia juu ya kuangalia watoto wa kike mashuleni wasiweze kukosa kusoma kutokana vifaa vya kumkinga katika hedhi.

  Nae Mratibu wa Maji , Afya na Usafi wa Mazingira Mashuleni wa izara ya elimu na Sayansi na TeknolojiaTheresia Kiuwela amesema kuwa wasichana wanakosa masomo kwa miezi miwili kutokana na hedhi hivyo ni lazima siku hizo zisipotee kwa msichana kukosa kusoma.

  Amesema kuwa wameweka utaratibu wa kupata tauro za kike (Ped) kwa sh.1000 ambapo baadhi ya wasichana hasa katika maeneo ya vijijini wanashindwa kukumdu gharama hizo.

  0 0

  MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi akizindua 
  gari la kubeba wagonjwa (ambulance) 

  Na Fredy Mgunda,Iringa
  MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi kwa kushirikiana na asasi ya kimataifa ya Rafiki Surgical Mission ya Australia ametoa msaada wa gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa iliyopo katika jimbo lake hilo.

  Gari hilo aina ya Toyota Hiace lenye thamani ya Sh Milioni 40 lilikabidhiwa jana kwa uongozi wa halmashauri ya mji wa Mafinga inayosimamia uendeshaji wa hospitali hiyo katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mashujaa, mjini Mafinga.

  Akikabidhi msaada huo Chumi alisema; “napenda ifahamike kwamba gari hilo limenunuliwa na asasi hiyo ambayo mimi ni rafiki yao mkubwa. Uadilifu na uaminifu kwa taasisi hiyo umetufanya tushirikiane vyema katika mambo mengi kwa faida ya wananchi wa jimbo langu la Mafinga.”Alisema gari hilo la wagonjwa ni rafiki kwa wagonjwa na wajawazito kwa kuwa lina vifaa tiba vinavyoweza kutumika kutolea huduma wakati wakipelekwa hospitalini.

  Baada ya kukabidhi gari hilo, Chumi ambaye ni mbunge wa kwanza wa jimbo hilo jipya, mkoani Iringa alikumbusha vipaumbele vyake kwa wapiga kura wake kuwa ni kuhakikisha linapata huduma bora ya maji, elimu, afya na miundombinu ya barabara.Akishukuru kwa msaada huo, Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Dk Innocent Mhagama alisema kabla ya msaada huo, hospitali hiyo ya wilaya ilikuwa na gari moja tu la kubeba wagonjwa.

  “Pamoja na kuhudumia hospitali hiyo ya wilaya, gari hilo moja lilikuwa likihudumia vituo vingine 18 vya kutolea huduma katika wilaya hiyo hivyo,” alisema.Alisema kupatikana kwa gari hilo jipya kutasaidia kuboresha huduma hiyo kwa kuokoa maisha ya wagonjwa na maisha ya mama na mtoto ambayo ni kipaumbele katika utoaji wa huduma za afya.

  Akizungumzia huduma ya mama na mtoto katika hospitali hiyo ya wilaya, Dk Mhagama alisema kwa wastani wajawazito 500 wanajifunga kila mwezi hospitalini hapo.“Kati yao wajawazito zaidi ya 100 huwa wanapata huduma za dharula huku wastani wa wajawazito 10 wakipatiwa huduma za rufaa,” alisema.

  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Charles Makoga alisema halmashauri yake kwa kushirikiana na mbunge huyo itahakikisha inatekeleza ahadi mbalimbali zilizotolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk John Magufuli, mbunge na madiwani ili kuboresha huduma kwa watu wake

  0 0

  Katibu mkuu wizara ya habari,utamduni,sanaa na michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza jambo wakati menejimenti ya wizara hiyo ilipofanya ziara ili kujifunza mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidijitali unavyofanya kazi katika ofisi za wizara ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano leo jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Faustin Kamuzora na Naibu katibu mkuu wizara ya habari,utamaduni,sanaa na michezo Bi.Nuru Khalfan Mrisho.
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Faustin Kamuzora akieleza jambo kwa menejiment kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo walipofika ofisini hapo ili kujifunza mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidijitali.
  Watumishi pamoja na Menejimenti kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Kaimu mkuu wa masijala ya wazi Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Bi.Bupe Munisi(wa kwanza mwenye nguo ya njano) jinsi mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidijiti(DMIS) unavyofanya kazi .
  Menejimenti ya Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakiwa katika ziara mafunzo ya mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidijitali unavyofanya kazi katika ofisi za wizara ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano.
  Na Daudi Manongi.

  Mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidijiti utaongeza kasi serikalini na hivyo kuchochea maendeleo chanya katika kila nyanja.

  Hayo yamesemwa leo na Katibu mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel wakati wa mafunzo yanayotolewa na Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano kwa Menejimenti ya wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakati walipotembelea mfumo wa usimamizi wa nyaraka wa kidijiti.

  Alisema pia kuwa mfumo huu una faida nyingi na ndio ambazo zimeifanya wizara hii kutaka kujifunza ni pamoja na suala la gharama na kwa kuwa serikali ya awamu ya tano iko katika jitihada kubwa za kupunguza matumizi na kwa kuwa bajeti ya shajala ni kubwa katika taasisi nyingi za serikali hivyo mfumo huu wa kidijiti utasaidia kupunguza garama kwani hapatakuwa na haja ya kutumia karatasi na hivyo kupunguza gharama kubwa.

  Prof Elisante pia aliongeza kuwa mfumo huu utaongeza usiri wa nyaraka hizi na kwa sasa zitakuwa zinasomwa na yule tu aliyekusudiwa na kutoa pongezi kwa ofisi ya rais manejimenti ya umma kwa kuhamasisha matumizi ya mfumo huu kwani ukitumiwa vyema utakuwa na manufaa sana.

  Kwa upande wake Katibu mkuu wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Faustin Kamuzora alisema kuwa mfumo huo ulijengwa miaka mitatu iliyopita na unaweza kutumika katika wizara yeyote kwani una ufanisi mkubwa sana kwani kwa sasa utaweza kuangalia mafaili gani yameingia kwa mfumo wa kidijitali na kwa namna hii itapunguza garama na muda kwani hatutakuwa tunatumia karatasi tena.

  Prof.Kamuzora alizitaka Taasisi na Wizara mbalimbali kuwapa elimu ya kutosha watunza kumbukumbu kwani wao ndio wahusika wakuu wa kwanza wa mfumo huu na hivyo kuwataka wahusika kuwapa mafunzo ya kompyuta na kuboresha vifaa kama scanner maofisini mwao.

  Nae mmoja wa watunza kumbukumbu kutoka wizara Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Felomena Swai alisema amenufaika na mafunzo hayo na yatawasaidia katika utunzaji wa kumbukumbu kwani sasa watapeleka barua kwa wakati na kurahisisha utunzaji wa mafaili.

  0 0

  The Contractors Registration Board (CRB) annual general meeting is set to take place this coming Thursday and Friday on 26th and 27th May respectively at Diamond Jubilee hall.

  Sponsored by TIB Corporate bank, the meeting will be the winding up of the Annual General Meeting following the first meeting, which took place in Mwanza at Malaika Beach Hotel on May 5th and 6th. 

  The event will carry the theme 'Deliberate Capacity Building of Contractors for Sustainable Economic Development; Challenges and Way forward'.During the Mwanza consultative meeting, contractors underscored the importance of financial empowerment as a means to enable local contractors to compete in the construction industry particularly in bidding, securing and executing contracts. 

  This was amid reports that at least 65 per cent of projects undertaken by indigenous contractors were shoddy due to poor financial base and lack of professionalism.In its bid to support the performance of local contractors, TIB Corporate Bank introduced hassle-free loans to local contractors of various works aiming to build and strengthen contractors’ financial capacity and create a bigger room for them to play in the construction industry. 

  The loan is extended for meeting working capital needs; purchase of construction equipment; and for providing bank guarantees for the purpose of earnest money deposit or security deposit. 

  ‘This special loan facility for the local contractors is tailor made in order to support and create a favourable operating enviroment, and thus enable them to compete with international contractors and thus contribute to the economy of the country’ said Frank Nyabundege, TIB Corporate Bank Managing Director.

  The meeting in Dar es Salaam will also host an international Construction technology, products and services Exhibition

  0 0

  Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamis Kigwangala.

  Na. Aron Msigwa - Dodoma.

  Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 8 kuboresha miundombinu ya vyuo vya Afya kote nchini katika mwaka wa fedha 2016/2017 ili kuwawezesha wanafunzi wa fani ya Afya kusoma katika mazingira mazuri.

  Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamis Kigwangala ameyasema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Muhambwe Mhe.Atashasta Justus Ntitiye, alieyata kujua mkakati wa Serikali wa kuboresha vyuo vya Afya nchini hususan chuo cha Uuguzi wilayani Kibondo kilicho katika jimboni lake. 

  Dkt.Kigwangala amesema Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 imejipanga kuboresha mazingira ya vyuo vya Afya katika maeneo mbalimbali nchini kikiwemo Chuo cha Uuguzi Kibondo ambacho kimetengewa shilingi milioni 680.Aidha, ameeleza kuwa vyuo vya Afya vimekuwa vikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo madeni ya wazabuni wa vyakula waliokuwa wakiidai Serikali kiasi cha shilingi Bilioni 6.8 kuanzia mwaka 2009 hadi 2015.

  Amebainisha kuwa tayari Serikali imekwishahakiki madeni yote ya wazabuni ili yaweze kulipwa katika mwaka wa fedha 2016/2017 na kuongeza kuwa suala la usambazaji wa vyakula limeachwa chini Sekta binafsi ili zifanye kazi hiyo.

  Katika hatua nyingine Dkt.Kigwangala amesema Serikali inaendelea kuangalia uwezekano wa kuyatumia majengo yaliyoachwa kwenye kambi za wakimbizi zilizofungwa mkoani Kigoma hususan wilayani Kibondo ili yaweze kutumika kama vyuo vya kutolea elimu ya Afya.

  " Niko tayari nikishirikiana na waheshimiwa wabunge kwenda mkoani Kigoma kuzungumza na viongozi wa mkoa huo ili tuweke utaratibu wa namna ya kuyatumia majengo hayo" Amesisitiza Dkt.Kigwangala.

  0 0  Mbunge wa EALA, Shy-Rose Bhanji akichangia mada ndani ya bunge hilo 

  Na Woinde Shizza,Arusha

  Serekali imekuwa ikipoteza kodi nyingi zitokanazo na ushuru wa mazao hasa kutokana na kuwa na mzabuni mmoja ambaye anakusanya kodi za mazao kwa nchi nzima .

  Hayo yamebainishwa na mbunge wa EALA, Shy-Rose Bhanji wakati akiongea na waandishi wa habari ndani ya viwanja vya bunge hil, ambapo alisema kuwa kuna changamoto kubwa ya utekelezaji wa umoja wa forodha hapa nchini Tanzania.

  Alisema kuwa wafanyabiashara wengi pamoja na wakulima ambao wanazalisha mazao pamoja na bidhaa mbalimbali zinazofikia kiwango staili cha asilimia 50 %hadi 100% wanakuwa hawatozwi kodi wakati wanapeleka bidhaa zao katika nchi za jumuiya wanachama .

  Aidha alibainisha kuwa kuna tatizo kubwa kwa upande wa Tanzania, kwani hati ambazo zinatolewa kwa ajili ya kukusanya kodi au kubaini viwango vya kusamehewa kodi zinatolewa na taaasisi moja tu ambayo ni ya TCCIA.Alisema kuwa hili ni tatizo ambalo linatakiwa kutazamwa upya katika nchi yetu na serekali kwa sababu TCCIA haipatikani nchi nzima bali inapatikana katika baadhi ya sehemu ambayo ni mikoa tu huku katika ngazi za wilaya pamoja na vijiji hawapatikani.

  Alisema kuwa hii inapelekea kodi nyingi ya mazao kupotea na pia wananchi wengi pamoja na wafanya biashara wengi kutokujua thamana ya kodi ambayo inaweza kumuwezesha mfanyabiashara kujua unafuu wa kodi.

  “sasa hivi ili kuwapa nafasi wananchi wengi pamoja na wafanyabishara wengi ili waweze kuelewa dhana ya unafuu wa kodi ,ni jukumu la serekali kutoa kutoa hati hizo kwa wadau wengine ili kuleta unafuu wa ulipaji kodi “alisema Bhanji

  Aidha alisema kuwa ili kurahisisha mambo ni vizuri ofisi za biashara za manispaa pamoja na ofisi za biashara za wialaya nawao waweze kupewa ili jukumu na wao waweze kutoa hati ambazo zitawapa nafasi wafanya biashara ambao wanasifa zinazokithi maitaji na wenye sifa kuweza kupata hati hizo .

  0 0

  Baadhi ya Wafanyakazi wa  MultiChoice-Tanzania wakiwa katika vazi la kiafrika siku ya kuazimisha Africa day.

  Jinsi Chaneli za TV za Barani Afrika zilivyofanikiwa kuelezea habari za Afrika katika mtazamo wa Kiafrika. 

  Haukasiriki unapoangalia onyesho katika televisheni au filamu ya kutoka Afrika au kumhusu muafrika na kisha ukatahamaki, “ Hii haina chochote kinachofanana na Afrika ninayoijua?”. Kwa miongo kadhaa, tasnia ya burudani ya filamu na televisheni imetawaliwa na simulizi zenye maudhui ya nchi za Magharibi- hata pale zinapokuwa za kutoka Afrika na kwa ajili ya Waafrika. Kwa bahati nzuri, ndani ya miaka kadhaa iliyopita, tumeona mabadiliko japo ya taratibu lakini ya uhakika, ya simulizi zenye uhalisia kuhusu Waafrika zikisimuliwa kuhusu bara letu.

  MultiChoice tunajisikia fahari kutokana na ushiriki wetu katika mabadiliko na maendeleo haya tangu kuanzishwa kwetu barani Afrika miaka 20 iliyopita. Mojawapo ya malengo yetu ya msingi ni pamoja na kuhakikisha kwamba huduma zetu zinawaendeleza wateja wetu kwa kuwaletea maudhui ambayo wanaweza kuyahusisha nayo na maisha yao ya kila siku. 

  Lengo hili linatukumbusha dhamira yetu ya kuendelea kuunga mkono na kuendelea kuwekeza katika tasnia ya burudani barani Afrika na kuonyesha vipaji vya waafrika kupitia chaneli za hapa barani Afrika za MNet. Kutoka Nollywood mpaka Riverwood, tunaamini katika kusimulia na kuelezea habari au simulizi za Ki-Afrika ambazo watazamaji wetu wanaweza kuzihusisha nazo na maisha yao ya kila siku. Siku ya Afrika inapokaribia tarehe 25 May mwezi huu, tunasheherekea wasimulizi mbalimbali kutoka Afrika ambao wanachangia katika ukuaji wa tasnia ya filamu na televisheni ya Afrika.

  Watazamaji wetu wametuamini kuwa waangalizi na wahifadhi wa simulizi za kiafrika na kuhakikisha panakuwa na simulizi zenye uwiano kuhusu Afrika. Kimsingi hakuna simulizi moja ambayo inafafanua au kuelezea kila kitu kuhusu bara letu na ndio maana chaneli zetu za zinazolenga bara la Afrika ambazo zinajumuisha Africa Magic, Maisha Magic Bongo, Maisha Magic East (E36) na Zambezi Magic, Mzansi Music na Mzansi Bioskop- zimeahidi na kujizatiti katika kuelezea simulizi za Afrika kama zilivyo. Chaneli hizi zinaleta mtazamo tofauti kuhusu maisha ya Afrika ambayo watazamaji wake wanaweza kuyahusisha na maisha yao ya kila siku.


  0 0

  · Music Superstar AliKiba and well-known food personality Marion Elias joined Jamie Oliver’s Food Revolution with a live cooking demonstration on Facebook on Friday 20th May

  · 9 per cent of boys and 12 per cent of girls under the age of 20 in Tanzania are classed as overweight and obese in 2013*

  Tanzania saw the launch of Food Revolution Day on Friday, 20th May 2016 amidst a fanfare of celebrities, live cooking events, a flurry of social media activity and, of course, the British celebrity chef and campaigner Jamie Oliver, who launched the campaign. Jamie and his army of revolutionaries staged a series of live events on Facebook to encourage governments at the World Health Assembly meeting in Geneva on 23rd May to tackle the child nutrition crisis.

  Now in its fifth year, highlights included chefs and celebrities streaming live on Facebook on 20th May during a seven-hour cooking marathon, calling for people around the world to sign up to the Food Revolution. In India the campaign’s Global Champions - music superstar AliKiba and well-known food personality Marion Elias - were the hosts of the live event on Facebook which took place in Mbuyuni Primary School, Oysterbay.  
  Food Revolution Day, which is saw Jamie joined by a host of well known chefs and personalities, all of whom carried out Facebook Live broadcasts from the around the world to help make history. Some of the notable names included: Jacqueline Fernandez and Chef Kunal Kapur (Mumbai, India); Chef Gennaro, Chef Clodagh McKenna, Charlotte Crosby, Alfie Deyes, Tanya Burr and Jim Chapman (London); Kris Jenner, Wolfgang Puck and Cody Simpson (L.A. USA); Chef Donna Hay (Sydney, Australia); Chef Ali and Juliani (Nairobi, Kenya); Chef Tim Malzer, Chef Steffen Henssler and Janina Uhse (Hamburg, Germany); Chef Ana Luiza Trajano and Chef David Hertz with guests Marina Person and Felipe Solari (Sao Paulo, Brazil); cookery personality Marion Elias and AliKiba (Dar-es-Salaam, Tanzania); Chef Eros and Waje (Lagos, Nigeria); Chef Lynn Crawford (Toronto, Canada); and Bart Van Olphen and Miljuschka Witzenhausen (Netherlands).
  Food Revolution Day was also supported on social media by Coldplay, James Corden, Kate Hudson, Nicole Scherzinger, Rio Ferdinand, Paloma Faith, Niall, Zoella, Jim, Tanya, Louis, Pixi Woos, Haste Kicthen, Olly Murs, Ronan Keating, Marlon Roudette, Cascada, Cornelia Pletto, Palina Rojinski, Holger Stromberg, Chris Mears, Naomie Harris, Jake Paul, Emmanuelle Chriqui and Keltie Knight.

  As part of Food Revolution Day, Jamie also took an International Omelette Challenge global to get people, young and old, experiencing first-hand how super-quick, easy and delicious healthy grub can be wherever you are, and encourage more noise on social media for the Food Revolution. 
   

  0 0  0 0


  0 0

  Ipo kauli isemayo "Mfupa Uliomshinda Fisi" ikiashiria jambo gumu mithiri ya mfupa mgumu ambao umemshinda fisi ambae ni mnyaba bingwa wa kutafuna mifupa ya kila aina.

  Ndivyo unaweza kusema ukiitazama picha hizi, kwani suala la kuzagaa ovyo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kwa jina la Machinga jijini Mwanza, ni mfano halisi wa mfupa ulioshindikana kutafunwa na halmashauri ya jiji la Mwanza.

  Mara kadhaa juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika ili kuwaweka wafanyabiashara hao katika mpangilio mzuri kwa ajili ya wao kufanya biashara katika maeneo rasmi yaliyotengwa lakini utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua kwani mafanikio yake yakishindwa kuwa ya kudumu licha ya nguvu kubwa kutumika.

  Kabla ya kipindi cha kampeni za Uchaguzi mkuu mwaka jana, halmashauri ya jiji la Mwanza ilifanikiwa kuwaondoa machinga katika maeneo yasiyo rasmi lakini baada ya kampeni kuanza, machinga walirejea mitaani kwa kasi ya ajabu na hakuna aliewagusa tena ambapo hivi sasa kila kona ya jiji la mwanza machinga wamezagaa ovyo.

  Baadhi ya Machinga jijini Mwanza wanaomba sekta hiyo kuboreshwa ili kuondokana na changamoto zinazowakabiri ikiwemo kukosa maeneo maalumu kwa ajili ya wao kufanyia biashara hatua ambayo itasaidia kuondokana na kadhia mbalimbali ikiwemo kukabiliana na mgambo wa jiji wanaokuwa wakiwaondoa katika maeneo yasiyo rasmi kufanyia biashara.

  Bonyeza HAPA Kwa Picha Zaidi.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia ambako walihudhuria mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB, Mei 24, 2016, Majaliwa alimwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  · Ni katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi

  WAKUU wa nchi za Afrika wametaka kuwepo na juhudi za pamoja katika kukabiliana na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabiachi yanayolikumba bara hilo.

  Kauli hiyo ilitolewa jana mchana (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati wa majadiliano baina ya viongozi kutoka Zambia, Chad, Nigeria, Msumbiji na Tanzania mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 51 wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano cha kimataifa wa Mulungushi, jijini Lusaka, Zambia.

  Wakishiriki kwenye mjadala wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliohusu Nishati na Mabadiliko ya Tabianchi, viongozi hao walisema bara la Afrika linahitaji kupata maendeleo zaidi licha ya tatizo la nishati linalolikumba bara hilo hivi sasa.

  Akichangia mjadala huo, Rais wa Zambia, Bw. Edgar Lungu alisema nchi yake imepania kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme vijijini lakini imekuwa ikikabiliwa na tatizo la uhaba wa mvua kwa zaidi ya miaka miwili hali ambayo alisema imechangia kukosekana kwa umeme katika maeneo mengi nchini humo.

  “Uhaba wa mvua umepunguza kiwango cha maji katika bwawa la Kariba ambalo hutumika kuzalisha umeme nchini mwetu. Na hapa kwetu, karibu asilimia 80 ya umeme wetu, unategemea uzalishaji wa umeme kutokana na vyanzo vya maji,” alisema.

  Rais wa Chad, Bw. Idriss Deby Itno aliitaka benki ya AfDB ichukue nafasi ya mdau mkuu kwenye uwekezaji wa sekta ya nishati na kuzisadia nchi za bara hili kupata mitaji ya uwekezaji na ushauri wa kitaalamu.

  “Tunahitaji kutumia fursa ambazo benki yetu inazo katika kukabilianana changamato za ukosefu wa nishati. Tukiweza kutekeleza jambo hilo, tutafanikiwa kuwa na miradi ambayo ni makini na kwa maana hiyo tutaweza kuliangaza bara letu la Afrika kwa kupata mwanga wa uhakika,” alisema.

  Kwa upande wake, Makamiu wa Rais wa Nigeria, Prof, Yemi Osinbajo alisema bara la Afrika halina budi budi kuweka kipaumbele kwenye masuala ya maendeleo yake wakati likitafuta suluhisho la kukabiliana na athari za mazingira.

  “Tunapaswa kutafuta njia za kubalance mahitaji makubwa ya umeme ambayo bara letu linakabiliwa nayo dhidi ya athari za kimazingira ambazo zinapigiwa kelele na mataifa makuna na zinahatarisha kutunyima fursa ya kuendelea haraka kama ilivyokuwa kwao,” alisema na kuongeza:

  “Kama nchi zilizoendelea zinataka sana kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi, zinatakiwa zitupatie fedha, teknolojia na wataalamu ambao watasaidia kuendesha mitambo ili tupate nishati safi kutokana na mafuta ya petroli na dizeli sababu ni rasilmali ambazo tunazo.”  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema ili kuondokana na tatizo la nishati, kuna haja ya kuwa na viongozi wenye utashi wa kisiasa ambao watakuwa tayari kuruhusu uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya nishati na kuongeza kuwa Tanzania inapitia upya sheria zake ili kuruhusu miradi mikubwa ya uwekezaji kwenye sekta hiyo.  Aliwaambia washiriki wa mkutano huo kwamba milango ya uwekezaji Tanzania iko wazi kwa ajili ya wawekezaji walio tayari kuwekeza kwenye sekta hiyo na kutaja fursa ambazo Tanzania inazo kwenye sekta ya nishati ikiwemo gesi asilia, makaa ya mawe, madini ya urani, maji, upepo na nishati ya joto kutoka ardhini (geothermal energy).

  Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário alisema kuna haja ya kuwa na taasisi ya uzalishaji na ugawaji umeme ya pamoja (electricity pool) ambayo itaruhusu wazalishaji wa umeme wawauzie wanunuzi wakubwa.

  Waziri Mkuu ambaye Lusaka kuhudhuria mkutano huo wa ADB kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli, amerejea nchini leo (Jumatano, Mei 25, 2016).


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATANO, MEI 25, 2016.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Halfan Mshiro pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia Mjema wakiokota baadhi ya uchafu katika kaburi la nguli mpigania Uhuru wa Tanganyika Hayati Kaluta Amri Abeid Kaluta walipozuru kaburi hilo katika kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni mtoto wa tano wa hayati sheikh Kaluta Bw. Amiri Kaluta Amri Abedi na kulia ni Naibu Meya Bw. Salum Faisal.
  Mtoto wa tano wa hayati sheikh Kaluta Bw. Amiri Kaluta Amri Abedi (watatu kulia) akiongoza dua ya kumuombea baba yake hayati sheikh Kaluta Amri Abeid wakati ujembe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ulipozuru katika kaburi la nguli huyo kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sofia Mjema (kushoto mbele) akizungumza wakati ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ulipozuru katika kaburi la nguli mpigania Uhuru wa Tanganyika Hayati Kaluta Amri Abeid Kaluta kuadhimisha siku ya Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Bibi. Nuru Halfan Mshiro.
   


  0 0

   Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, akisalimiana na Meneja Rasilimali watu wa zamani wa Uhuru Publications Ltd, Lucas Kisasa, baada ya kumkuta nje wakati akienda ofisi za kampuni hiyo leo kujitambulisha kwa viongozi wa Kampuni hiyo ambayo ni wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani na viongozi wa Peoples Media Ltd ya Uhuru FM, leo. Kulia ni mpigapicha wa Magazeti ya Uhuru, Emmanuel Ndege na Wapili ni dereva wa UPL Chamlungu.
  Kaimu Katibu wa NEC, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Pindi Chana ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akizungumza na viongozi hao.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO. 
   
   Kaimu Mkurugenzi wa Peoples Media Angel Akilimali akijitambulisha 
   Kaimu Meneja Rasilimali watu na Utumishi Paul Mg'ong'o akijitambulisha  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Nigeria, Prof. Yemi Osinbojo, Rais wa Chad, Idriss Debyo, Rais wa Zambia, Edgar Lungu na Waziri Mkuu wa Msumbiji, Carlos Agostino do Rosario (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hadi sasa Serikali imekwishapokea maombi 52 kutoka makampuni mbalimbali ambayo yanataka kuwekeza kwenye sekta ya umeme nchini Tanzania.Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati akizungumza na Watanzania waishio Zambia katika mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Lusaka, Zambia.

  “Haya maombi yamekwishapokelewa na wenye makampuni wamekwishahojiwa kuangalia uwezo walionao katika suala zima la uwekezaji wanaotaka kuufanya, na tukiwapata wenye uwezo na wenye nia ya dhati watapatiwa miradi ya kuiendesha,” alisema.Aliwataka Watanzania hao waishio Zambia watumie fursa ya uwepo wao huko kutafuta marafiki ambao wanaweza kuja kuwekeza kwenye miradi mbalimbali nchini kwani Serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu wakati wananchi wanahitaji kupatiwa huduma muhimu.

  “Serikali peke yake haiwezi kufanya kazi ya uwekezaji kwa hiyo tunahitaji kushirikiana na sekta binafsi, taasisi za kifedha na washirika wa maendeleo na ndiyo maana kule kwenye mkutano nimewaeleza washiriki kwamba milango ya uwekezaji Tanzania iko wazi.Alisema kupatikana kwa umeme wa uhakika kutawezesha wananchi wengi zaidi kujiingiza katika shughuli za kiuchumi na hivyo kuinua uchumi wa nchi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

  Alisema malengo ya Serikali ya awamu ya tano ni kuona kuwa nchi inakuwa na mitambo mingi ya kuzalisha umeme na umeme wote unaozalishwa na mitambo hiyo inaunganishwa na gridi ya Taifa ili kuondokana na tatizo la mgao wa umeme nchini.Alisema Tanzania ina vyanzo vingi vya nishati vikiwemo gesi asilia, makaa ya mawe, madini ya urani, maji, upepo, nishati ya joto kutoka ardhini (geothermal energy) na nishati inayotokana na vinyesi vya mifugo (biomass) ambayo alisema vinatumika kwa watu wachache (siyo kitaifa).

  Alisema kupatikana kwa gesi asilia nchini kumeleta neema ambapo mabomba ya gesi yamekwishajengwa kutoka Mtwara hadi Kinyerezi na kutoka Kilwa-Songosongo hadi Dar es Salaam. “Sasa hivi kuna utafiti unaendelea juu ya uwezekano wa kusambaza gesi ya kupikia majumbani. Tumeanza pale Mikocheni (DSM) na sasa hivi wanafanya utafiti mwingine kule Mtwara ili wananchi waweze kutumia gesi hii kupikia badala ya mkaa,” alisema.

  Akielezea kuhusu uwekezaji kwenye makaa ya mawe, Waziri Mkuu alisema Serikali imelenga kutumia makaa ya mawe ili kuendeshea mitambo ya kwenye viwanda vikubwa badala ya kutumia umeme au mafuta ya dizeli kama inavyofanyika sasa. “Baadhi ya wenye viwanda wanabadilisha mifumo ya kuendeshea mashine zao ili iweze kuendana na teknolojia ya makaa ya mawe pindi tu uchimbaji ukishika kasi,” alisema.

  Akifafanua kuhusu juhudi za Serikali katika kusambaza nishati ya umeme, Waziri Mkuu alisema tangu kuanzishwa kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), vijiji zaidi ya 3,000 katika ya vijiji 12,000 vilivyopo nchini vimefikiwa na nishati ya umeme.

  “Tulianza na REA awamu ya kwanza, awamu ya pili na sasa tunaenda awamu ya tatu. Hata mkipiga simu kwa ndugu zenu vijijini, mtakuta katika kila kata kuna vijiji kati ya vinne hadi vitano ambavyo vimefikiwa na nishati ya umeme kupitia mradi wa REA,” alisema.

  Waziri Mkuu amerejea nchini leo (Jumatano, Mei 25, 2016).

  0 0


  0 0
 • 05/25/16--06:25: MATUKIO YA BUNGE LEO.
 •  Mbunge wa jimbo la Nkasi Kaskazini (CCM) Mhe. Allya Kessy akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la Kawe (CHADEMA) Mhe. Halima Mdee nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
   Mwekekezaji na Msambazaji wa nguzo za umeme nchini kutoka Kampuni ya New Forest iliyoko mkoani Iringa akiwaonesha jambo Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mhe. Ally Kessy (kushoto) na Mbunge wa jimbo laKilolo Mhe. Venance Mwamoto kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
   Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jummanne Maghembe (kushoto) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mhandisi Ramo Makani waifuatilia hoja mbalimbali za wabunge wakati wakichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo Bungeni Dodoma.
    Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jummanne Maghembe (kushoto) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mhandisi Ramo Makani waifuatilia michango mbalimbali ya wabunge wakati wakichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo Bungeni Dodoma.
   Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Hussein Mwinyi akifuatilia kwa makini mjadala wa Waheshimiwa Wabunge wakati wa kipindi cha maswali na Majibu.
   Mbunge wa Bunda Mjini Mhe. Esther Bulaya akichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo
   Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi Mhe. Andrew Chenge akiongoza kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.
  Baadhi ya Wananchi kutoka jamii ya Wafugaji waliohudhuria kikao cha Bunge leo mjini Dodoma kushuhudia Michango ya Wabunge wakati wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii mjini Dodoma leo.
  Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamis Kigwangala akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Bunge Bw. Owen Mwandumbya (kulia) na Mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Elisha Eliya leo mjini Dodoma.Picha/Aron Msigwa - MAELEZO.

  0 0


  0 0

   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi , Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania( TCAA) Mbwana J. Mbwana(wapili kushoto) akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari.(kushoto)  wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga Tanzania, wa kupitia na kujadili maombi ya kampuni zinazoomba leseni za kuendesha biashara ya kutoa huduma za usafiri wa anga hapa nchini,uliofanyika leo makao makuu ya TCAA Banana Ukonga jijini Dar es Salaam. Jumla ya kampuni 27 zimewasilisha maombi ya kutoa huduma zake katika sehemu mbali mbali nchini ikiwa ni pamoja na Pemba, Dar es Salaam, Mara na  Kilimanjaro,Wengine kutokkulia ni wajumbe wa Bodi  Hanif M. Malik na Jaffari K. Mpili. 
   Badhi ya wadau wa usafiri wa anga Tanzania wakiwa kwenye  mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga Tanzania, wa kupitia na kujadili maombi ya kampuni zinazoomba leseni za kuendesha biashara ya kutoa huduma za usafiri wa anga hapa nchini,uliofanyika leo makao makuu ya TCAA Banana Ukonga jijini Dar es Salaam. Jumla ya kampuni 27 zimewasilisha maombi ya kutoa huduma zake katika sehemu mbali mbali nchini ikiwa ni pamoja na Pemba, Dar es Salaam, Mara na  Kilimanjaro.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari akiongea  na wadau mbalimbaliwakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga Tanzania, wa kupitia na kujadili maombi ya kampuni zinazoomba leseni za kuendesha biashara ya kutoa huduma za usafiri wa anga hapa nchini,uliofanyika leo makao makuu ya TCAA Banana Ukonga jijini Dar es Salaam. Jumla ya kampuni 27 zimewasilisha maombi ya kutoa huduma zake katika sehemu mbali mbali nchini ikiwa ni pamoja na Pemba, Dar es Salaam, Mara na  Kilimanjaro.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA)  Mbwana J. Mbwana(wapili kushto) akiongoza kikao hicho .


  Wadau wa Usafiri wa Anga Tanzania, leo wamekutana kupitia na kujadili maombi ya kampuni zinazoomba leseni za kuendesha biashara ya kutoa huduma za usafiri wa anga hapa nchini.

  Katika mkutano huo uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania- TCAA, Banana- Ukonga, jumla kampuni 27 zimewasilisha maombi ya kutoa huduma zake katika sehemu mbali mbali nchini ikiwa ni pamoja na Pemba, Dar es Salaam, Mara na Kilimanjaro.Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TCAA, Bwana Mbwana J. Mbwana na wajumbe wengine wa bodi hiyo, Prof. Arnold J. Temu, Hanif M. Malik. Yussuf M. Ali, Jaffari K. Mpili na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza S. Johari .

  TCAA yenye jukumu la kisheria la kusimamia na kudhibiti masuala ya ki- usalama, kiuchumi katika sekta ya usafiri wa anga pamoja na kutoa huduma za uongozaji ndege, hutoa leseni kwa kampuni zinazoomba kutoa huduma za usafiri wa anga hapa nchini baada ya kampuni hizo kukidhi vigezo na kanuni zinazosimamia sekta.

  Mikutano hiyo ya kupitia maombi ya leseni za usafiri wa anga hufanyika kila mwaka ambapo maombi ya kampuni mpya na zile ambazo tayari zinafanya shughuli zake hupitiwa na wadau na kujadiliwa , kabla ya bodi ya wakurugenzi wa bodi kuridhia na kutoa leseni kwa kamapuni husika.

  0 0

  The Clerk to the Assembly administers the oath to the EAC Secretary General, Amb Liberat Mfumukeko 
  The EAC Secretary General, Hon Amb Liberat Mfumukeko signs the oath of Allegiance to the House
  CONGRATULATIONS: The EALA Speaker, Rt. Hon Daniel Kidega offers his congratulations to the EAC Secretary General, Hon Amb Liberat Mfumukeko moments after taking the Oath 
  The EAC Secretary General, Hon Amb Liberat Mfumukeko is led in to the House to take the Oath of Allegiance by the Clerk to the Assembly, Kenneth Madete. At back is Hon Hafsa Mossi and Hon Isabelle Ndahayo (photo by Woinde shizza,Arusha ).

older | 1 | .... | 857 | 858 | (Page 859) | 860 | 861 | .... | 1897 | newer