Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

CBE yatoa ufafanuzi tuhuma za upostoshaji.

$
0
0

 Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emmanuel Mjema akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) ripoti ya Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) inayoonesha kuwa chuo hicho kimepata ziada ya bilioni 1.2 kati ya mwaka huu na kufanya chuo kujiendesha kwa faida tofauti na baadhi taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari.

 Mkuu wa Chuo cha Elimu Biashara (CBE) Prof. Emmanuel Mjema akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) ripoti ya Mamlaka ya Udhibiti ya Manunuzi ya Umma (PPRA) ya Mwaka huu inayoonesha chuo hicho ni moja kati ya Taasisi 14 zilizofanya vizuri kwa kushika nafasi ya kwanza kwa kupata alama 95.8 katika kufuatilia sheria ya manunuzi ya umma na kuutaka umma kupuuza taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa wanakiuka sheria hizo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO


Frank Mvungi-Maelezo

Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kimewataka wananchi kupuuza taarifa za upotoshaji zilizoripotiwa na Baadhi ya vyombo vya Habari Hapa nchini kuhusu chuo hicho.

Akizungumza na vyombo vya Habari leo jijini Dar es salaam Mkuu wa chuo hicho Prof. Emmanuel Mjema amesema tuhuma za kuwa chuo hicho kina ubadhirifu wa kutisha si za kweli na zinalenga kuchafua taswira ya chuo hicho.

“Chuo kinafanyiwa ukaguzi wa Hesabu zake na Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za Serikali na kwa kipindi cha miaka minne tumepata hati safi (clean audit report) kuanzia mwaka 2010/2011 hadi 2014/2015 .” alisisitiza Prof. Mjema.

Katika ukaguzi huo ripoti hiyo ilionyesha kuwa Taasisi hiyo imekuwa ikizingatia sheria na kanuni za matumizi ya fedha za umma hali iliyopelekea kupata hati safi kwa kipindi chote.

Pia Chuo hicho kilifanyiwa ukaguzi na Mamlaka ya Udhibiti wa manunuzi Serikalini (PPRA) kwa mwaka unaoishia 2014/2015 na Chuo hicho kupata alama 95.8 hivyo kuwa moja ya Taasisi za Umma zinazofanya vizuri katika kuzingatia sheria na kanuni za manunuzi ya umma.

Prof. Mjema amesema kuwa chuo hicho kimekuwa kikijiendesha bila kupata ruzuku toka Serikalini na pia kuzalisha mapato ya ziada zaidi ya bilioni moja kwa kwa kila mwaka wa fedha kuanzia mwaka 2013 hadi 2015.

Kutokana na Mafanikio hayo chuo hicho kimeweza kuanzisha Kampasi ya Mbeya ambapo chuo hicho kimenunua eneo lenye ukubwa wa ekari 54.9 na pia maboresho katika maktaba ya chuo yamefanyika.

Mafanikio mengine ni kujenga hema kubwa lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 740 na kuboresha karakana ya vipimo na mizani chuoni hapo.

MKUU WA WILAYA IRINGA AWAPA MOYO WAJASILIAMALI

$
0
0
Mkuu wilaya ya Iringa Richard Kasesela alitembelea maduka ya vijana wajasiliamali waliofungua maduka ili kuweza kunyanyua maisha yao. vijana hawa wamepata mikopo na kuweka maduka yao katika hadhi ya kimataifa. Akizungumza nao Kasesela alifurahishwa sana na unadhifu wa maduka hayo yaliyopo mtaa wa msikiti wa miyomboni. Kasesela hutumia jumapili kutembelea wafanya biashara ndogondogo na wale wa sokoni ili kuwahamasisha kukuza biashara zao na kuitangaza. 

Maduka haya yana wiki moja tuu toka yaanzishwe hayana tofauti na yale ambayo ukienda nje ya nchi utayakuta. Wajasilia mali walialamikia wingi wa kodi ndogo ndogo pia mazingira ya baishara bado si rafiki sana. Mkuu wa wilaya aliahaidi kulifanyia kazi. ALITEMBELEA maduka ya fettilicious, M8, Young D na mengineyo.​




AZAM YAZINDUA DUKA LAKE LA VIFAA VYA MICHEZO JIJINI DAR

$
0
0
Na Bakari Issa Madjeshi

Klabu ya Soka ya Azam leo imezindua rasmi duka lake la vifaa vya michezo lililopo Kariakoo,Mtaa wa Swahili na Mkunguni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya uzinduzi wa duka hilo,Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo,Saad Kawemba amesema duka hilo linauza vifaa mbalimbali vya michezo vya timu hiyo na kuuzwa kwa watu mbalimbali.Pia amesema wanatoa nafasi kwa Wanachama wa Klabu hiyo kuwa vifaa hivyo vinapatikana dukani hapo pamoja na kuzingatia familia za Wanachama hao ikiwemo kupatikana Mabegi ya shule kwa watoto wao.

Ameeleza kuwa kwa wale walio nje ya mkoa wa Dar es Salaam watawasiliana na Tovuti(Website) ya Azam pamoja na Mitandao ya kijamii ikiwemo ‘Facebook’.Kawemba amewaomba Wanachama wa Klabu hiyo kujitokeza kununua vifaa hivyo ikiwa ni pamoja na maandalizi ya mechi ya kesho baina ya Azam FC dhidi ya Dar es Salaam Young Africans,mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho utakaopigwa dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Kuhusu maandalizi ya Mchezo wa Kesho wa Fainali baina yao na Yanga,Kawemba amesema wamejiandaa vyakutosha na watahakikisha wananyakua ubingwa wa Kombe hilo ambalo linadhaminiwa na wenyewe Azam.

Mtendaji Mkuu wa Klabu ya AZAM FC ,Saad Kawemba akkata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la vifaa vya michezo lililopo Kariakoo,Mtaa wa Swahili na Mkunguni jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi.

Mtendaji Mkuu wa Klabu ya AZAM FC ,Saad Kawemba akioneshwa moja ya mashine ya kisasa iliyomo dukani hapo kwa ajili ya kubandika namba pamoja majina kwenye jezi za washabiki ama wapenzi wa timu hiyo iwapo watapenda kufanya hivyo kwa gharama iliyo nafuu kabisa.
Mtendaji Mkuu wa Klabu ya AZAM FC ,Saad Kawemba akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari waliofika kushuhudia tukio hilo la uzinduzi wa duka la vifaa vya michezo lililopo Kariakoo,Mtaa wa Swahili na Mkunguni jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi

Moja ya jezi "uzi" ukioneshwa mbele ya wana habari hawapo pichani

Mtendaji Mkuu wa Klabu ya AZAM FC ,Saad Kawemba akioneshwa baadhi ya jezi mbalimbali za timu hiyo zinazopatikana dukani humo maalum kwa mashabiki na wapenzi wa soka.

SERIKALI KUZITAMBUA NA KUZIRASIMISHA BANDARI BUBU ZILIZOKIDHI VIGEZO.

$
0
0
Na.Aron Msigwa - MAELEZO
24/5/2016.DODOMA.

Serikali imesema kuwa inaendelea na utaratibu wa kuzitambua na kuzirasimisha bandari Bubu zote zilizokidhi vigezo ambazo zinatumiwa na wafanyabiashara kupitisha bidhaa mbalimbali ili ziweze kuchangia katika Pato la Taifa kulingana na  wingi wa bidhaa zinazopitishwa katika bandari hizo. 

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma leo wakati akijibu maswali ya Wabunge waliotaka kujua mkakati wa Serikali katika kudhibiti bidhaa zinazoingizwa nchini na wafanyabiashara wasio waaminifu kupitia bandari bubu hali inayoikosesha  serikali mapato.

Mhe. Ngonyani amekiri kuwepo kwa ongezeko la wafanyabiashara wasio waaminifu wanaotumia bandari hizo katika maeneo mbalimbali nchini hasa ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi, Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria na maeneo ya mipakani ambayo yanaingia moja kwa moja kwenye makazi ya watu akieleza kuwa wengi wa wafanyabiashara wanakwepa kodi na kutafuta urahisi wa kupitisha mizigo yao.

Amesema maeneo hayo yamekuwa chanzo kikubwa cha upitishaji wa bidhaa zisizokidhi viwango, Silaha na Biashara haramu na kubainisha kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa ndani wasio waaminifu wamekuwa wakishirikiana na raia wa kigeni kuagiza na kuingiza bidhaa hizo kupitia bandari hizo kwa lengo la  kukwepa kodi.

Amesisitiza kuwa  Serikali ya Awamu ya tano inalishughulikia kwa nguvu zote suala hilo kupitia watendaji wake wakiwemo wakuu wa mikoa wa maeneo husika ambao hushirikiana na mamlaka zinazohusika vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama kudhibiti njia na maeneo yote yanayotumiwa na wafanyabiashara hao.

" Kama Serikali tunaendelea kufanya vikao kwa kushirikiana na wakuu wa mikoa na mamlaka zinazohusika kuangalia namna ya kurasimisha bandari bubu zilizobaki ili tuweze kukusanya mapato ya Serikali yaliyokuwa yakipotea kutokana na wingi wa mizigo inayopitishwa" Amesema Mhandisi Ngonyani.

Amefafanua kuwa mwaka katika kipindi cha mwaka 2015 na mwezi Januari,  2016, doria zilizofanyika katika maeneo yanayotumiwa na wafanyabishara hao zilifanikisha kukamatwa kwa wafanyabiashara 98 ambao wote walichukuliwa hatua za kisheria ikiwem mali zao kutaifishwa pamoja na  kuwafikisha mahakamani.

Kuhusu bandari bubu zilizotambuliwa na kuzirasimishwa na Serikali katika  Pwani ya Bahari ya Hindi ni  Mbweni ya jijini Dar es salaam, Mlingotini mkoani Pwani, Kisiju na Nyamisati mkoa wa Pwani na Bandari bubu ya Kilambo mkoani Mtwara.Aidha, amesema Serikali inaendelea na utaratibu wa kurasimisha bandari binafsi umefanyika katika ziwa Victoria mkoani Mwanza na maeneo mengine ambayo serikali inaendelea kuyafanyia kazi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni  amesema kuwa Serikali inaendelea kuvijengengea uwezo vikosi vyake vya ulinzi na usalama kwa kuviongezea vifaa vya kisasa ili viweze kuimarisha doria nchi nzima ili kukabiliana na vitendo vyote vya uvunjaji wa sheria.

Amesema Jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na wananchi kukusanya taarifa za kiharifu ili kuwabaini na kuwakamata wafanyabishara wote wanaojihusisha na uagizaji na uingizaji wa bidhaa kupitia bandari bubu  ambaoumekua ukiisababishia serikali ikose mapato.

" Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinaendelea kukusanya taarifa za kiharifu kutoka kwa wananchi ili kukabiliana na wimbi hili, pia tunaendelea kuviongezea nguvu vikosi vyetu vya ulinzi na usalama ili viweze kutimiza majukumu yao ipasavyo" Amesisitiza Mhe.Masauni.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA KAMPENI YA LONGA NASI LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye uzinduzi wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za vitendo vya Rushwa au maoni ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113. Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 24,2016 katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki kabla ya kuzindua mpango wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za vitendo vya Rushwa au maoni ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113. Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 24,2016 katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia mpango wa utekelezaji wa TAKUKURU kwenye uzinduzi wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za vitendo vya Rushwa au maoni ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113. Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 24,2016 katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam. Kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki, kushoto Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valontino Mlowola.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akivuta kamba kuondoa kitambaa kuzindua mpango wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za vitendo vya Rushwa au maoni ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113. Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 24,2016 katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam. Kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki, kushoto Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valontino Mlowola.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuwia na kupambana na Rushwa Nchini TAKUKURU Valontino Mlowola baada ya kuzindua mpango wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za vitendo vya Rushwa au maoni ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113. Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 24,2016 katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam. (Picha na OMR).

TAKUKURU WAZINDUA KAMPENI YA LONGA NASI JIJINI DAR LEO.

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kamba kuashiria uzinduzi wa gari la matangazo ya Kampeni ya kupambana na Rushwa ya LONGA NASI kwa kupiga namba 113 na kutuma kutuma sms kwenda namba 113 ili kutoa taarifa ya kutoa au kupokea Rushwa kwa TAKUKURU.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye uzinduzi wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za watu wanaotoa rushwa au kupokea rushwa kwaajili ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113 unayoweza kupiga na kutuma sms za kawaida  Uzinduzi huo umefanyika leo  katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Tehama TAKUKURU, Neema  Mwalyelye akitoa maelekezo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipotembelea kwenye  banda la kitengo cha Tehama wakati wa uzinduzi wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za watu wanaotoa rushwa au kupokea rushwa iliyofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam leo.

Naibu Mkurugenzi wa elimu kwa umma TAKUKURU, Stela mpanju akizungumza  kabla ya kuzindua wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za vitendo vya Rushwa au maoni ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113 kupiga au kutuma sms ya kawaida bila gharama yeyote. Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valontino Mlowola akizungumza kabla ya kuzindua wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za vitendo vya Rushwa au maoni ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113 kupiga au kutuma sms ya kawaida bila gharama yeyote. Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Angela Kairuki akizungumza kabla ya kuzindua wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za vitendo vya Rushwa au maoni ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113 kupiga au kutuma sms ya kawaida bila gharama yeyote. Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam.
baadhi ya wananchi na wafanyakazi wa TAKUKURU wakiwa katika uzinduzi wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za vitendo vya Rushwa au maoni ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113 kupiga au kutuma sms ya kawaida bila gharama yeyote. Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam.
Yamoto band wakitumbuiza katika uzinduzi wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za vitendo vya Rushwa au maoni ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113 kupiga au kutuma sms ya kawaida bila gharama yeyote. Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam.
Mwanamziki wa Kizazi kipya, Kala Jelemaya akitumbuiza katika  uzinduzi wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za vitendo vya Rushwa au maoni ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113 kupiga au kutuma sms ya kawaida bila gharama yeyote. Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam.
Wanakikundi cha Msimamo wakitumbiza katika  uzinduzi wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za vitendo vya Rushwa au maoni ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113 kupiga au kutuma sms ya kawaida bila gharama yeyote. Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Angela Kairuki akipata maelekezo alipotembelea katika banda la Tehama la TAKUKURU katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam leo.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Angela Kairuki mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam leo katika uzinduzi wa kampeni ya kupambana na Rushwa kwa kutuma sms a kupiga simu TAKUKURU.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI KATIKA MKUTANO WA ABD LUSAKA.

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Zambia, Edgar Lungu katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika - ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu wa Msumbiji, Carlos Agostino do Rosario katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika - ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016.
 Rais wa Zambia, Edgar Lungu akifungua Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika - ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016.Kushoto kwake ni Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa ambaye alimwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika - ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Nigeria, Prof. Yemi Osinbojo, Rais wa Chad,  Idriss Debyo, Rais wa Zambia, Edgar Lungu na Waziri Mkuu wa Msumbiji,  Carlos Agostino do Rosario.



  Wasanii wa Lusaka wakicheza ngoma ya asili ya Zambia katika mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika - ADB uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi Zambia Mei 24, 2016. Tanzania iliwakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NAPE AFUNGUA MASHINDANO YA KOMBE LA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI ( CDF CUP - 2016) JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihutubia wakati wa kufungua mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup - 2016) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita Meja Jenerali Issa Nassor akihutubia wanamichezo wa kijeshi kwenye sherehe za ufunguzi wa  mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup - 2016) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi Meja jenerali Simoni Mumwi akihutubia wakati wa ufunguzi wa  mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup - 2016) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiangalia picha yake aliopewa na kikundi cha sanaa  wakati wa kufungua mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup - 2016) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipiga penati ikiwa ishara ya kufungua mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup - 2016) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwatakia heri timu ya Tembo kutoka Ruvuma na Kombaini ya Vikosi vya JKT kabla ya kuanza mechi yao kwenye mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup - 2016) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Tembo pamoja na Kombaini ya JKT mara baada ya kufungua mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup - 2016) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na Mwakilishi wa MnadhimuMkuu wa Majeshi Meja Jenerali Simoni Mumwi mara baada ya kufungua mashindano ya tatu ya kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF Cup - 2016) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.



ALIYEKUWA MKURUGENZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM AAGWA

$
0
0
Baadhi ya Mawakili na Wanasheria wakiingiza mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Bwa. Mbonea Wilson Kabwe katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.(PICHA NA BEATRICE LYIMO-MAELEZO).
Familia ya aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Bw. Mbonea Wilson Kabwe wakifuatilia ibada ya kutoa heshima za mwisho ya kuuaga mwili huo.
Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene akiwakisha salamu za rambirambi kutoka Serikalini wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Bw. Mbonea Wilson Kabwe katika viwanja vya Karimjee, leo jijini Dar es salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaa Paul Makonda akiwasilisha salamu za rambirambi kutoka ofisi ya Mkuu mkoa wa Dar es salaam wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Bw. Mbonea Wilson Kabwe katika viwanja vya Karimjee, leo jijini Dar es salaam
Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Bw. Mbonea Wilson Kabwe katika viwanja vya Karimjee kabla ya safari ya kuelekea Mamba, Wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro kwa mazishi.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Bw. Mbonea Wilson Kabwe katika viwanja vya Karimjee kabla ya safari ya kuelekea Mamba, Wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro kwa mazishi.
Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Bw. Mbonea Wilson Kabwe katika viwanja vya Karimjee kabla ya safari ya kuelekea Mamba, Wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro kwa mazishi.
Baadhi ya Ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria ibada ya heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Bw. Mbonea Wilson Kabwe kabla ya safari ya kuelekea Mamba, Wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro kwa mazishi.

SEKTA YA NGOZI KUTENGENEZEWA MAZINGIRA YA VIWANDA

$
0
0
 Katibu wa Wizara ya Viwanda na Uwekezaji-Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda (Mwenye Suti)   akioyeshwa ngozi na zilizoahifadhiwa na katika  Maghala ya Ngozi leo jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Wizara ya Viwanda na Uwekezaji-Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda akiangalia ngozi ambazo zimehifadhiwa katika maghala ya kuhifadhi ngozi leo jijini Dar es Salaam.

Ngozi ambazo zimehifadhiwa katika maghala ya Ngozi  Vingunguti jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Wizara ya Viwanda na Uwekezaji-Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda  (Mwenye suti)akipewa maelekezo na Katibu Mwenezi wa Chama cha Wanunuzi wa Ngozi Tanzania (Wangota) juu hali biashara ya ngozi inavyodorola leo jijini Dar es Salaam. 
(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii)

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SEKTA ya Ngozi imekuwa na Nuksi kutokana na baadhi ya viwanda vya ngozi kufungwa huku wamiliki wa maghala ya ngozi wanalia na biashara hiyo kuwa haitoki hata ikitoka wanauza kwa hasara.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Uwekezaji-Uwekezaji, Profesa, Adolf Mkenda wakati alipotembelea maghala ya ngozi , Profesa Mkenda amesema kuwa serikali itahakikisha inaweka mazingira bora ya wafanyabiasharaya ngozi kuweza ngozi hiyo kuzalisha bidhaa za ngozi kuuzwa ndani na sio kupeleka nje ya nchi.

Mkenda amesema kuwa katika mazingira wanayoweka ni kuhakikisha wawekezaji wa ndani ndio wanamiliki sekta hiyo na sio kutegemea watu wa nje ya nchi ambao wakati wote anakuwa na hati ya kusafiria kurudi kwao baada ya kuona biashara inadorola.

Amesema kuwa kuna kiwanda kimefungwa Shinyanga kutokana na kukosa malighafi ya ngozi huku baadhi ya maghala ya Dar es Salaam yakiwa na ngozi iliyokaa kwa muda wa miaka miwili.

Mmoja wa Wamiliki wa Maghala ya Ngozi, Omary Msangi amesema kuwa viwanda vilivyopo ngozi vinunua ngozi kwa bei ndogo huku gharama za kuhifadhi ngozi ikiwa kubwa.

14 WAKAMATWA MAUAJI YA WATU WATATU MSIKITINI MWANZA

$
0
0
Na Lorietha Laurence-Maelezo

Jeshi la Polisi Nchini linawashikilia watuhumiwa 14 kufuatia tukio la mauaji ya watu watatu lililotokea katika msikiti wa Rahman eneo la Ibanda relini mkaoni Mwanza, Mei 18 mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Advera Bulimba alisema kuwa msako wa kuwakamata watuhumiwa wengine unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

Hivyo amewaomba wananchi kutoa ushirikiano mkubwa kwa jeshi hilo ili kufanikisha kuwakamata wale wote wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hilo.“Nitoe wito kwa wananchi kushirikiana kikamilifu na vyombo vya usalama katika kufichua wahalifu kwa kuwa ni watu tunaoishi nao, hivyo hakuna budi kutoa taarifa zao ili usalama na mali zetu uendelee kuimarika”, aliongeza Kamishna Msaidizi Bulimba.

Hata hivyo, alieleza kuwa hali ya usalama nchini iko shwari na kuwatoa hofu wananchi kwamba jeshi hilo limejipanga kikamilifu katika kuhakikisha hali ya usalama inaendelea kuwepo.“Niwaombe wananchi kuondoa hofu juu ya hali ya usalama na wasiwasi na watoe ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kuhakikisha kwamba wote wanaojihusisha na uhalifu wanakamatwa haraka”, alisema Kamishna Msaidizi Bulimba.

Aliongeza kuwa uchunguzi zaidi wa matukio ya uhalifu nchini unaendelea ikiwemo matukio ya mkoani Tanga, Dar es Salaam na mikoa mingine ili kubaini na kuwakamata wahusika na kufikishwa katika vyombo vya sheria.Hivi karibuni kumeripotia matukio mbalimbali ya uvunjifu wa amani katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo mauaji ya watu watatu waliouawa wakiwa msikitini jijini Mwanza.

WAMILIKI WA SILAHA WATAKIWA KUHAKIKI SILAHA ZAO KABLA YA JUNI 30

$
0
0

Na Lorietha Laurence-Maelezo

Jeshi la Polisi nchini limetoa wito kwa wamiliki wa silahi kujitokeza nakuhakiki silaha zao katika Wilaya wanazoishi kabla ya kumalizika kwa zoezi hilo mnamo Juni 30 mwaka huu.

Hayo yalisemwa na Msemaji wa Jeshi hilo Kamishna Msaidizi Advera Bulimba alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

“Serikali imetoa muda wa miezi mitatu kukamilisha zoezi hili muhimu na tayari miezi miwili imepita hivyo wale ambao bado hawajahakiki silaha zao kuzikakiki sasa kabla ya Juni 30 ili kuepukana na usumbufu” alisema Kamshna Msaidizi Bulimba na kuongeza kuwa:

“Natoa wito kwa watu wote wanaomiliki silaha kinyume na sheria kusalimisha silaha hizo katika vituo vya polisi, ofisi za serikali na kwenye nyumba za ibada na watakaofanya hivyo ndani ya muda ulipangwa hawatachukuliwa hatua zozote za kisheria”.

Aliongeza kuwa baada ya muda ulipangwa na Serikali kupita na wamiliki hawajahakiki silaha zao Jeshi la Polisi nchini litaendesha operesheni kali kuwakamata wale ambao hawakujitokeza katika zoezi la uhakiki na hatua kali zitachukuliwa ikiwemo kufutiwa leseni na silaha zao kutaifishwa na kuwa mali ya Serikali.

Aliwaomba ndugu wa wale walikuwa wakimiliki silaha ambao wamefariki au ni wagonjwa wasalimishe silaha hizo katika vituo vya Polisi kwa niaba ya ndugu zao ndani ya kipindi cha uhakiki wa silaha.Zoezi la uhakiki wa silaha lilianza Machi 21 mwaka huu kufuatana na sheria ya usimamizi wa silaha na risasi ya mwaka 2015, ambapo kifungu cha 66 cha sheria hiyo kinamtaka kila mmiliki kuhakiki kumbukumbu za silaha yake au risasi pale anapoamriwa na mamlaka.

Lengo la kuhakiki kumbukumbu za wamiliki wa silaha ni kupata taarifa sahihi za wamiliki hao zitakazosaidia kubaini wale wote wanaomiliki kinyume na sheria, kuwafahamu wamiliki waliohama na kuhamia makazi mapya, kuwafahamu wamiliki waliofariki ili kuzuia vitendo vya uhalifu na uvunjwaji wa amani nchini.

TAWLA YASISITIZA MABADILIKO YA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUPUNGUZA AJALI NA VIFO

$
0
0

Jonas Kamaleki-Maelezo

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamanda Mohamed Mpinga amesema mabadiliko ya sheria ya usalama barabarani hayaepukiki ili kupunguza vifo na majeruhi vitokanavyo na ajali za barabarani.

Kamanda Mpinga amayesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Usalama Barabarani inayoratibiwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa Usalama Barabarani.

“Sheria zinazohusu masuala ya Usalama barabarani inabidi zifanyiwe marekebisho ili ziweze kusaidia kupunguza vifo na majeruhi kwani zilivyo sasa hazitoi adhabu kali kwa wanaokiuka sheria hizo”alisema Kamanda Mpinga.

Aidha Kamanda huyo alisisitiza kuwa suala la Usalama Barabarani ni la kila mmoja hivyo inabidi litiwe mkazo na watu wote.Kwa upande wake Mkurugenzi wa TAWLA, Bi Tike Mwambipile amesema chama hicho kwa kuzingatia umuhimu wa kushughulikia masuala ya Usalama Barabarani kimeona ni vyema kikafanya kikao hicho ili kupata mawazo ya wadau.

Bi Mwambipile amesema vifo vingi vinavyotokana na ajali za barabarani vinawaacha wanawake wengi wakiwa wajane na watoto yatima wanaongezeka.Ameongeza kuwa fedha nyingi zinatumika kuwahudumia majeruhi badala ya kufanya shughuli nyingine za maendeleo ya jamii.

Naye Mwenyekiti wa TAWLA, Bi Aisha Bade amesema mabadiliko makubwa ya sera na sheria za usalama barabarani ni lazima yafanyike ili kupunguza athari zitokanazo na ajali za barabarani.Bi Bade amesema TAWLA kwa kushirikiana na wadau wengine inafanya juhudi za makusudi ili kuhakikisha sheria hizi zinabadilishwa ili kukabiliana na janga hili.

Visababishi vya ajali kwa hapa nchini vimetajwa na Mratibu wa Mradi Bloomberg wa Usalama Barabarani, Bi Mary Kessy kuwa ni ulevi, kutofunga mkanda, kutoweka vizuizi vya watoto kwenye magari, mwendo kasi na kutovaa kofia ngumu kwa waendesha pikipiki.

KAMPUNI YA VISION INVESTIMENTS YATOA FURSA KWA MAKAMPUNI MENGINE.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vision Investiments Ally Nchahaga (katikati) akifafanua juu ya fursa zitolewazo na Kampuni yao leo Jijini Dar es Salaam, kulia ni Afisa Mahusiano wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Aisha Mohammed na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mauzo cha Kampuni ya Mafuta ya Oil com Aluwy Amar.

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

Kampuni ya Vision Investments imetoa fursa kwa makampuni mengine kushiriki kutoa huduma mbalimbali wakati wa makutano baina ya wanunuzi na wauzaji wa magari yanayoandaliwa na Kampuni hiyo yatakayofanyika Mei 29 mwaka huu.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Ally Nchahaga ambaye amewaomba wauzaji na wanunuzi wa magari pamoja na makampuni mbalimbali kushiriki katika makutano hayo ili kutimiza mahitaji yao ya magari.

“Kama ilivyo ada kila Jumapili ya mwisho wa mwezi Kampuni yetu inawakutanisha wauzaji, wanunuzi wa magari pamoja na makampuni tofauti kutoa huduma shirikishi zinazokwenda sambamba na biashara hii ya magari ya watu binafsi” alisema Nchahaga.Kwa mujibu wa Kampuni ya Vision Investments makutano hayo yatafanyika nchini kwa mara ya sita ambapo mwaka huu yatafanyika katika viwanja vya Coco Mihogo kuanzia sa 4 asubuhi.

Nchahaga alizitaja baadhi ya kampuni zinazotoa huduma shirikishi zikiwemo Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ), Kampuni ya Mafuta ya Oil com, Kampuni ya Coca cola, pamoja na Kampuni ya Simply Elegant ambazo zinatoa huduma za mikopo ya magari, mafuta ya magari, vinywaji pamoja na vilainishi vya magari kwa wateja watakaokuwepo katika makutano hayo.

Aidha, Nchahaga amesisitiza kuwa kampuni yao sio ya maonyesho ya magari wala wao sio madalali bali ni kampuni inayotoa fursa yenye gharama nafuu kwa wanachi kutimiza mahitaji yao ya magari.

Ameongeza kuwa elimu kuhusu magari na vifaa vyake itatolewa bure na mtu yeyote atakayehitaji kuuza gari lake atachangia shilingi elfu 50 ikiwa ni mchango wa kuweka gari lake katika viwanja hivyo pamoja na kufanyiwa matangazo katika mitandao ya kijamii kwa mwezi mzima.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mauzo cha Kampuni ya Mafuta ya Oil com Aluwy Amar amesema kuwa Kampuni yao inatoa huduma mpya ya kulipa kwa kutumia kadi itakayomrahisishia mteja kupatiwa huduma za mahitaji ya mafuta ya magari yao kwa hiyo, watashiriki katika makutano hayo ili kutoa elimu kwa wateja hao kuhusu matumizi ya kadi hizo.

“Huduma hii tumeianza kuitoa kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, huduma za kupatiwa kadi pamoja na kufanya miamala yote ni bure pia mwisho wa mwezi tutatoa huduma ya punguzo la bei kulingana na matumizi ya mteja”,alisema Amar.

Kwa upande wake Afisa Mahusiano wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Aisha Mohammed amesema kuwa wamefurahi kupata fursa hii ya kushiriki katika makutano hayo kwakua anaamini ni njia moja wapo kwa benki hiyo kuwapa mikopo au kuwanunulia magari wateja wao ili kutimiza ndoto zao kwa muda muafaka.

TAASISI YA MBALAWALA YAIPONGEZA NISHATI NA MADINI KUWEZESHA SHUGHULI ZAKE KUFAHAMIKA

$
0
0
Meneja Uendeshaji kutoka Taasisi ya Wanawake ya Mbalawala Women Organization inayojishughulisha na uzalishaji wa briketi za makaa ya mawe wilayani Mbinga mkoani Ruvuma, Hajiri Kapinga (kulia) akielezea mafanikio ya taasisi hiyo mara baada ya taarifa zake kuanza kuchapishwa katika Jarida la Wizara. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasilano Serikalini Wizara ya Nishati na Madini, Asteria Muhozya.

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

Taasisi ya Wanawake ya Mbalawala inayojishughulisha na uzalishaji wa braketi za makaa ya mawe ijulikanayo kama Mbalawala Women Organization yanye makazi yake katika kijiji cha Ruanda wilayani Mbinga mkoani Ruvuma imeipongeza Wizara ya Nishati na Madini kupitia Kitengo cha Mawasiliano Serikali kwa kutangaza shughuli zake hali iliyopelekea wateja wa makaa ya mawe katika taasisi hiyo kuongezeka kadri siku zinazokwenda.

Taasisi hiyo inayofanya shughuli zake karibu na Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka inajishughulisha na utengenezaji wa briketi bora za makaa ya mawe kwa ajili ya kupikia

Pongezi hizo zilitolewa na Meneja Uendeshaji wa Taasisi hiyo Hajiri Kapinga aliyekutana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasilano Serikalini Wizara ya Nishati na Madini, Asteria Muhozya jijini Dar es Salaam na kusema kuwa tangu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kianze kuchapisha habari zinazohusu taasisi hiyo kupitia Jarida lake linalochapishwa kila wiki lijulikanano kama MEM Newsbulletin wameshuhudia idadi kubwa ya wateja ikiongezeka na kuzidi uzalishaji wa taasisi hiyo.

Alisema kabla ya habari zake kuchapishwa na Jarida la Wizara, taasisi hiyo ilikuwa ikiwauzia briketi za makaa ya mawe wateja wake walioko katika vijiji vinavyozunguka mgodi wao wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.

“Mara baada ya taarifa zetu kuanza kuchapishwa na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini tumeshuhudia mabadiliko makubwa kwani tumekuwa tukipokea simu kutoka mikoa mbalimbali hususan Dar es Salaam, Mbeya, Iringa wateja wakihitaji bidhaa, hali inayopelekea mahitaji kuwa makubwa kuliko kiasi tunachozalisha,.” alisema Kapinga.

“Jarida limetufanya tujulikane, hata wahisani wetu wameahidi kuongeza nguvu na misaada katika kuwezesha mradi huu kuendelea vizuri; Jamii inasoma habari zetu na sisi tumesoma masuala mengi kuhusu nishati na madini,” aliongeza.Kapinga aliendelea kusema kuwa ili kukabiliana na mahitaji makubwa ya wateja taasisi hiyo imeweka mkakati wa kununua mtambo mwingine kutoka nje ya nchi ili kuongeza uzalishaji utakaoendana na mahitaji ya wateja.

Alisema mikakati mingine ni pamoja na ujenzi wa ghala la kuhifadhia makaa ya mawe, ununuzi wa magari kwa ajili ya usambazaji wa bidhaa ya briketi za makaa ya mawe katika vituo vya uwakala vitakavyoanzishwa nchini karibu kila mkoa.“Mara baada ya kuanzisha vituo hivyo, wateja wetu watakuwa wanapata bidhaa kutoka kwa mawakala badala ya kukutana na sisi moja kwa moja,” alisema Kapinga.

Alisema kuwa pia wamejipanga kutoa elimu ya matumizi ya briketi za matumizi ya makaa ya mawe na utafutaji wa masoko kwa kushirikiana na wadau wa utengenezaji wa majiko sanifu yanayotumia briketi za makaa ya mawe kwa matumizi ya majumbani.

Akielezea uanzishwaji wa taasisi hiyo, Kapinga alisema kuwa taasisi hiyo ilianzishwa chini ya ufadhili wa Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka (Tancoal Energy Limited) unaomilikiwa na kampuni ya Intra Energy ya Australia kwa asilimia 70 na Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwa asilimia 30 ambao wanafurahishwa na hatua iliyofikiwa na taasisi hii katika uzalishaji ya briketi za makaa ya mawe.

Aliongeza sambamba na uzalishaji wa briketi za makaa ya mawe, taasisi hiyo imekuwa ikitoa mafunzo juu ya utumiaji wa briketi ya makaa ya mawe katika vijiji na miji jirani na mgodi wake pamoja na ushiriki katika maonesho mbalimbali ndani ya mkoa wa Ruvuma.“Lengo letu ni kuhakikisha briketi za makaa ya mawe zinazoendelea kuzalishwa katika mgodi wetu zinatumika majumbani, shuleni , vyuoni na taasisi mbalimbali na kupunguza uharibifu wa mazingira kwa kutumia kuni” alisema Kapinga

Aliendelea kusema kuwa lengo la uanzishwaji wa taasisi hiyo lilikuwa ni kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala kupitia briketi za makaa ya mawe na kuachana na matumizi ya kuni ambayo ni chanzo cha uharibifu wa mazingira.Naye Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Asteria Muhozya alisema kuwa lengo la Jarida la Wizara ni kutangaza shughuli za nishati na madini ikiwa ni pamoja na taasisi zake

Muhozya aliongeza kuwa jarida la Wizara lipo tayari kutangaza shughuli za wadau wa Madini na Nishati ili kuhakikisha kuwa sekta hizo zinakuwa na kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi

SERIKALI YAOMBWA KUSAIDIA UINGIZWAJI WA MAFUTA YA WATU WENYE UALBINO

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO

Taasisi ya Josephat Torner Foundation inayojishughulisha na watu walemavu wameiomba Serikali kusaidia uingizaji wa mafuta ya ngozi kwa watu wenye albino nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Josephat Torner alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ambapo alibainisha changamoto mbalimbali zinazo wakabili watu wenye ualbino.

“Watu wengi wenye ualbino wanaishi chini ya miaka 40 kutokana na kukosa mafuta ya kulinda ngozi dhidi ya miale ya jua, mafuta hayo huwasaidia kutoathilika na magonjwa ikiwemo kansa ya ngozi,” alisema Torner.

Torner alisema kuwa mafuta ya ngozi kwa watu wenye ualbino yanauzwa kati ya shilingi 30,000 na 40,000 kwa chupa ambapo mtu mwenye ualbino mmoja anatumia wastani wa chupa tano kwa mwaka.Mkurugenzi huyo alisema kuwa gharama ya mafuta hayo ni kubwa kwa watu wenye ualbino ambao wengi wao wanaishi maisha ya chini na hasa wale wanaoishi vijijini ambao hawawezi kumudu kuyapata na kununua mafuta hayo.

Aidha, aliongeza kuwa kama Serikali itasaidia uingizwaji wa mafuta hayo na kupunguza ushuru ili yaingie nchini kama madawa kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) tofauti na hali ilivyo sasa ambapo yanatozwa kodi kama vipodozi, hatua hiyo itasaidia kupunguza kwa kiasi kubwa kushuka bei mafuta hayo na kuwafikia walengwa.

Kwa upande wake, Mratibu wa taasisi ya Afrikan Albino Foundation kutoka Netherland nchini Tanzania Bas Kreukniet amesema kuwa ikiwa Serikali itashiriki katika uingizaji wa mafuta hayo kuna uwezekano wa mafuta hayo kuuzwa shilingi 4,000 kwa chupa.

Aliongezea kuwa ikiwa bei ya mafuta hayo itapungua itawasaidia watu wengi wenye ualbino hasa wa kipato cha chini na wale waishio vijijini kutumia mafuta hayo na kuwasaidia kujikinga na miale ya jua.

Hadi sasa taasisi ya Afrikan Albino Foundation imeweza kuwasaidia watu wenye ualbino wapatao 13,000 tangu waanze kuleta mafuta hayo nchini mwaka 2004 ambapo kila mwezi jumla ya chupa 5,200 huingizwa nchini kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye ualbino.

SHERIA MPYA YA USHIRIKA YAWANUFAISHA WAKULIMA WA TUMBAKU

$
0
0
Na Fatma Salum- MAELEZO, Dodoma.

Serikali imebainisha kuwa Sheria Mpya ya Ushirika (Sheria namba 6 ya mwaka 2013) imesaidia kupunguza changamoto za wanachama wa Vyama vya Ushirika pamoja na wakulima wa Tumbaku nchini.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Tate William Ole-Nasha aliyasema hayo leo bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu maswali ya wabunge kwenye kipindi cha maswali na majibu.

Mhe. Ole-Nasha alisema kuwa baadhi ya marekebisho ya Sheria hiyo yanayowanufaisha wanachama wa Vyama vya Ushirika wakiwemo wakulima wa tumbaku ni pamoja na kuwachukulia hatua viongozi wabadhirifu wa vyama hivyo.

“ Katika maeneo yanayolima tumbaku viongozi wabadhirifu wa Vyama vya Ushirika 26 Mkoani Ruvuma wakiwemo Maafisa Ushirika wawili wamesimamishwa kazi na kufikishwa mahakamani.” alisema Ole-Nasha.

Pia Mhe. Ole-Nasha alifafanua kuwa sheria ya sasa inakataza vyama kukopa zaidi ya asilimia 30 ya mali zake (Own Capital) ili kuzuia vyama hivyo kuingia kwenye madeni makubwa yasiyolipika na hatimaye kusababisha migogoro ndani ya vyama.

Akizungumzia mafanikio upande wa tozo, Ole-Nasha lisema kuwa kuanzia sasa Mkutano Mkuu utakuwa chini ya uenyekiti huru utakaochaguliwa na wajumbe wa mkutano huo kinyume na awali ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu. 
“Lengo ni kulinda maslahi ya wakulima ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa tozo zote zinazoidhinishwa na Mkutano Mkuu zinakuwa na maslahi kwa wakulima wa Tumbaku.” Aliongeza Ole-Nasha.

Kwa mujibu wa Ole-Nasha Serikali inatambua uwepo wa kodi nyingi na tozo kwenye mazao mbalimbali ya chakula na biashara hivyo kwa kushirikiana na wadau imedhamiria kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara katika sekta ya kilimo kwa kupitia upya taratibu, vibali, tozo, kodi, ushuru na ada nyingine zinazotozwa ili kutoa nafuu kwa wakulima.

TANZANIA KUIUZIA UMEME ZAMBIA - MAJALIWA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ina mpango wa kujenga njia ya umeme kutoka Mbeya hadi Zambia kupitia Tunduma ili kupunguza tatizo la umeme linaloikabili nchi hiyo.

“Serikali ya Tanzania inajenga njia ya umeme ya msongo wa KV 400 kutoka Iringa - Dodoma – Singida – Shinyanga ambayo ni sehemu ya mradi mkubwa wa umeme unaolenga kuunganisha Zambia, Tanzania na Kenya,” amesema.

Amesema  upembuzi yakinifu kwa ajili KV400 kutoka Iringa hadi Mbeya umekwishakamilika tangu mwaka 2012, na hivi sasa Serikali inatafuta fedha kwa ajili kuunganisha kipande cha kutoka Mbeya na gridi ya Taifa ya Zambia.

Waziri Mkuu ambaye anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli, ametoa ufafanuzi huo leo mchana (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati akichangia hoja kwenye mjadala wa wakuu wa nchi na Serikali uliohusuNishati na Mabadiliko ya TabiaNchi kwenye ukumbi wa mikutano cha kimataifa wa Mulungushi.

Amesema ili kukabiliana na changamoto ya nishati barani Afrika, nchi za bara hili zinahitaji kuwa na fedha ama mitaji, teknolojia ya kisasa na wataalamu wenye ujuzi wa kutosha jambo ambalo amesema ni gumu kulikamilisha kila nchi peke yake.

Amesema ili kukaribisha wawekezaji kwenye sekta ya umeme, Tanzania inafanyia marekebisho sheria zake ili kuruhusu uwekezaji kwenye sekta hiyo.

Akizungumzia kuhusu hali ya nishati Tanzania, Waziri Mkuu alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na gesi asilia yenye ujazo wa futi trilioni 57.25 (tcf), makaa ya mawe yenye uhjazo wa tani bilioni 1.9 (asilimia 25 imevumbuliwa), umeme wa nguvu ya maji wa gigawati 4.7 ambazo ni asilimia 12 tu ndiyo inatumika. Pia alisema Tanzania ina deposits za urani yenye ujazo wa ratili milioni 200 (200 million pounds), joto la ardhini (geothermal) linaloweza kuzalisha umeme wa megawati zaidi ya 5,000. “Hivyo ni mbali na vyanzo vya umeme utokanao ua upepo na jua,” alisema.

Akizungumzia kuhusu usambazaji wa umeme vijijini, Waziri Mkuu alisema Tanzania kupitia REA imefanikiwa kusambaza umeme kwenye asilimia 52 ya vijiji vyote na inatarajia kufikia asilimia 90 ifikapo mwaka 2025.

Akishiriki mjadala huo, Makamu wa Rais wa Nigeria, Bw. Yemi Osinbajo alisema bara la Afrika linahitaji kuwa na vyanzo vikubwa vya umeme kama kweli linataka kufanikiwa kukamilisha kuwa na viwanda vya kutosha.

“Hatuwezi kuwaza kuwa na viwanda vingi wakati tukitegemea umeme wa nguvu ya jua peke yake… huu unahitaji uwekezaji mkubwa na eneo kubwa la kuweka mitambo,” alisema.

Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário
                                                                                                     
Akishiriki mjadala huo, Makamu wa Rais wa Nigeria, Bw. Yemi Osinbajo alisema bara la Afrika linahitaji kuwa na vyanzo vikubwa vya umeme kama kweli linataka kufanikiwa kukamilisha kuwa na viwanda vya kutosha.

“Hatuwezi kuwaza kuwa na viwanda vingi wakati tukitegemea umeme wa nguvu ya jua peke yake… huu unahitaji uwekezaji mkubwa na eneo kubwa la kuweka mitambo,” alisema.

Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário alisema masuala ya nishati yanahitaji uwekezaji mkubwa kwa hiyo akashauri makampuni kuungana kwenye uwekezaji na kuibua miradi ambayo ina tija (feasible and viable).

Waziri Mkuu amefuatana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Asantu Kijaji, wachumi kadhaa pamoja na wataalamu wa sekta ya fedha.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, MEI 24, 2016.

Ratiba ya Kuaga Mwili wa Makongoro Oging' Mei 26

MAJALIWA AKUTANA NA KAGAME LUSAKA

$
0
0
Waziri Mkuu, Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia ambako walihudhuria mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB, Mei 24, 2016, Majaliwa alimwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images