Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU KUHUDHURIA MKUTANO WA ADB ZAMBIA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo (Jumatatu, Mei 23, 2016) kwenda Lusaka, Zambia kuhudhuria Mkutano wa 51 wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (51st Annual Meeting of the Board of Governors of the African Development Bank – AfDB) utakaofanyika kesho (Jumanne, Mei 24, 2016).

Waziri Mkuu anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli.

Mkutano huo ambao utafunguliwa na Rais wa Zambia, Edgar Lungu utajadili masuala ya Nishati na Mabadiliko ya TabiaNchi. Pia utahudhuriwa na Marais Idriss Deby wa Chad, Paul Kagame wa Rwanda na Uhuru Kenyatta wa Kenya. Nigeria itawakilishwa na Makamu wake wa Rais, Yemi Osinbajo huku Msumbiji ikiwazilishwa na Waziri wake Mkuu, Carlos Agostinho do Rosário.

Watu maarufu waliothibitisha kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Kofi Annan, Ashish Thakkar, John Kufuor, Mary Robinson, Mo Ibrahim, Nancy Lee, Ngozi Okonjo-Iweala na Tony Elumelu.

Mkutano huo utakaofanyika kwenye kituo cha mikutano cha kimataifa cha Mulungushi (Mulungushi International Conference Centre) utahudhuriwa na washiriki zaidi ya 5,000 kutoka nchi 54 ambao ni wanachama wa benki hiyo, washiriki kutoka nchi 26 ambazo si za bara la Afrika (non-regional member countries), wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, wadau wa maendeleo na wawakilishi wa asasi za kiraia. Wengine ni Mawaziri wa fedha, biashara na uchumi na wataalamu kutoka vyuo vikuu.

Waziri Mkuu amefuatana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Asantu Kijaji, wachumi kadhaa pamoja na wataalamu wa sekta ya fedha.

Serikali yawaunganisha watafuta kazi 20,000 na waajiri

$
0
0
Frank Mvungi-Maelezo.

Serikali imefanikiwa kuwaunganisha Watanzania wanaotafuta kazi wapatao 20,000 ikiwa ni moja ya hatua ya kupunguza tatizo la ajira nchini.Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Wakala wa Huduma za Ajira nchini (TaESA) Bi Jamila Mbarouk wakati wa mkutano na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam.

Akizungumzia watafuta kazi waliounganishwa tangu kuanzishwa kwa wakala huyo Jamila alisema kuwa wengi waliounganishwa walikuwa wahasibu, Makatibu muhtasi, wataalamu wa huduma za jamii.“Jukumu letu letu ni kuwaunganisha watafuta kazi na waajiri ndani na nje ya nchi ili waweze kupata huduma hii kwa urahisi kwa kuzingatia sheria na kanuni za Ajira hapa nchini” alisisitiza Jamila.

Katika kupanua huduma ili kuwafikia watanzania walio wengi Jamila amebainisha kuwa (TaESA) imefungua ofisi za Kanda katika Mikoa ya Dodoma,Mwanza, na Arusha .Mafanikio Mengine ni wakala kuendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watafuta kazi 3185 ili kuweza kuhimili ushindani na changamoto za soko la ajira.Mafunzo hayo yametolewa mbalimbali ikiwemo chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Taasisi ya Uhasibu (TIA), Chuo cha Ardhi na Taasisi ya Teknplojia Dar es salaam (DIT).

Akieleza Umuhimu wa mafunzo hayo Jamila amesema kuwa yanalenga kuwajengea uwezo watafuta kazi ili waweze kuandika barua za maombi ya ajira kwa ufasaha, kuandaa wasifu binafsi (CV) na kuwajengea uwezo wa namna ya kufanya mahojiano kwa ufanisi kwa kuzingatia mbinu za kisasa.

Kwa upande wake Afisa Kazi wa TaEsa Bw. Amani Kasale amesema kuwa baadhi ya watafuta kazi wamekuwa na kasumba ya kuchagua maeneo ya kufanyia kazi hasa yale yaliyopo katika miji mikuu hali inayozorotesha juhudi za Serikali kuwaunganisha watafuta kazi na waajiri katika maeneo mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi.Akifafanua Kasale alisema kuwa huduma ya kuwaunganisha watafuta kazi na waajiri inatolewa bure kwa watanzania wote wanaotafuta ajira kwa kuzingatia sheria na Kanuni za ajira hapa nchini.

Pia Kasale alitoa wito kwa vijana wote wanaotafuta ajira kuachana na kasumba ya kuchagua maeneo ya kufanya kazi hasa yale yaliyo katika miji mikuu na kutumia fursa zilizopo maeneo ya pembezoni.Wakala wa huduma za Ajira Tanzania TaESA Ulianzishwa kwa sheria ya wakala Na. 30 ya mwaka 1997 ikiwa na lengo la kuunganisha watafuta kazi na waajiri wenye fursa za ajira ndani na nje ya nchi.

TBC yafanikiwa kufanya upembuzi yakinifu wa kufunga mitambo ya FM eneo la Mbambabay, Wilayani Nyasa.

$
0
0

Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.

SHIRIKA la Utangazaji la Taifa (TBC) limefanya upembuzi yakinifu wa kufunga mitambo ya FM yenye uwezo wa Kilowati moja katika eneo la Mbambabay Wilayani Nyasa Ili kuongeza usikivu wa Redio za TBC.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Dodoma na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbinga Vijijini, Mhe. Martin Msuha aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kuongeza uwezo wa kurusha matangazo ya Kituo cha TBC Songe ili wananchi wa tarafa hizo wapate habari kupitia TBC.

Mhe. Nape ameeleza kuwa Matangazo ya Redio ya Taifa kupitia mtambo wa masafa ya kati yaani ‘’Medium Wave’’ wenye nguvu ya Kilowati 100 yalikuwa yakisikika vizuri katika Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Ruvuma wakati mtambo huo ulipokuwa ukifanya kazi.

‘’Tangu mwezi Julai, 2013 mtambo huo haufanyi kazi kutokana na uchakavu na hivyo kuathiri usikivu wa matangazo ya TBC katika maeneo kadhaa”, alisema Mhe. Nape.Alisema kwamba, kwa kutambua umuhimu wa Wananchi katika kupata matangazzo, TBC ililazimika kuhamisha mitambo yake miwili ya Redio yenye uwezo wa Kilowati moja kwa kila moja iliyokuwa imefungwa eneo la Mshangano, Songea na kuifunga eneo la juu la mlima wa Matogoro-Songea ili usikivu Wake usambae katika eneo kubwa zaidi.

‘’Baada ya kufunga mitambo hiyo, matangazo ya TBC Songea yameboreshwa”, aliongeza Mhe. Nape.Ameongeza kuwa katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 Wizara yake imetenga fedha za maendeleo kwa ajili ya kufunga mtambo eneo la Mbambabay.‘’Kazi hiyo ya uboreshaji wa matangazo katika eneo Hilo itaanza mara tu fedha za kununua na kufunga mitambo hiyo zitakapotolewa”, alisema Mhe. Nape.

Aidha, alisema kwamba kutokana na uwezo mdogo wa mitambo ya FM inayotumika kwa sasa, mawimbi yake ya sauti hayafiki mbali sana ukilinganisha na yale ya mitambo ya ‘’Medium Wave’’ iliyokuwa ikitumika awali ambayo yanafika eneo kubwa zaidi la Mkoa wa Ruvuma zikiwemo Tarafa za Hagati, Mbuji na Mkumbi.

‘’Kukabiliana na changamoto za usikivu hafifu katika maeneo kadhaa Mkoani Ruvuma, TBC imeshafanya upembuzi yakinifu wa kufunga mitambo ya FM yenye uwezo wa Kilowati moja katika eneo la Mbambabay Wilayani Nyasa Ili kuongeza usikivu wa Redio za TBC,”alisema Mhe. Nape.

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa ameongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Jumanne Maghembe wakielekea Bungeni kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Mhe. Ally Keissy akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Masiliano, Mhe. Eng. Edwin Ngonyani akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Eng. Hamad Masauni (kushoto) akiwa ameongozana na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mhe. Halima Bulembo wakiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Hamis Kingwangalla akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Mhe Najma Murtaza Giga akiwasili Bungeni kuongoza vikao vya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Mbunge wa CCM, Mhe. Mary Mwanjelwa akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wengine wa Majimbo mbalimbali wakiwasili viwanja vya Bunge kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma.(Picha zote na Benedict Liwenga)

Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Balozi Jasem Al-Najem Akabidhi Msaada wa Madawa na Maji kwa Ajili ya Kambi za Kipundupindu Zanzibar.

$
0
0
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Jasem Al-Najem, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar, kulia Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Harusi Said, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi Halima Maulid na kushoto kwa Balozi Daktari Dhamana wa Kanda ya Unguja Dk Fadhil Mohammed na Mkurugenzi Kinga Wizara ya Afya Zanzibar. Dk Mohammed Dahoma. 
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Balozi Jasem Al-Najem, akikabidhi msaada wa Dawa kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar Mhe. Harusi Said, wakishuhudia kulia Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi Halima Maulid na kushoto Daktari Dhamana Kanda ya Unguja Dk Fadhil Mohammed.
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Jasem Al-Najem, akimkabidhi dawa Naibu Waziri Wizara ya Afya Zanzibar, Mhe. Harusi Said, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi Halima Maulid na kushoto kwa Balozi Daktari Dhamana wa Kanda ya Unguja Dk Fadhil Mohammed na Mkurugenzi Kinga Wizara ya Afya Zanzibar. Dk Mohammed Dahoma. 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi Halima Maulid akimkabidhi Madawa Daktari Dhamana wa Kanda ya Unguja Dk Fadhil Mohammed, baada ya kukabidhiwa na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania.
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Balozi Jasem Al-Najem, akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo wa dawa kwa Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Harusi Said. 
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Balozi Jasem Al-Najem, akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo wa dawa kwa Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Harusi Said. 
Daktari Dhamana wa Kanda ya Unguja Dk Fadhil Mohammed akitowa shukrani kwa Balozi wa Kuwait kwa msaada wao kwa Kambi ya Kipundupindu Zanzibar wakati wa hafla ya kukabidhi Madawa na Katuni za Majili kwa matumizi ya Kambi hizo.
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Balozi Jasem Al-Najem, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar nje ya Jengo la Wizara Mnani Mmmoja.Imetayarishwa na Othman Mapara.Zanzinews,Com.
Madawa na Maji vilivyokabidhiwa na Balozi wa Kuwait Nchini TanzaniaBalozi Jasem Al-Najem, kwa Wizara ya Afya kwa ajili ya Kambi za Kipindupindu Zanzibar.
Balozi Jasem Al-Najem, akiwasili katika viwanja vya Wizara ya Afya Zanzibar kwa ajili ya kukabidhi Msaada wa Madawa na Maji.
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Balozi Jasem Al-Najem, akisalimiana na Daktari Dhamana wa Kanda ya Unguja Dk Fadhil Mohammed wakati wa hafla ya kukabidhi Madawa na Maji kwa ajili ya Kambi za Kipindupindu Zanzibar.
Balozi Jasem Al-Najem, akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar kabla ya kuaza kwa hafla ya kukabidhi Madawa na Maji kwa Ajili ya Kambi za Kipindupindu Zanzibar.
Balozi Jasem Al-Najem, akisoma bango lilliloandikwa ujumbe wa hafla hiyo kwa viongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar kabla ya kuaza hafla hiyo ya kukabidhi madawa na maji. kushoto Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Harusi Said na Naibu Katibu Mkuu Halima Maulid. 

WAZIRI NCHEMBA ATUMBUA MAJIPU JIMBONI KWAKE AVUNJA BODI YA MAJI ILIYOFANYA UFISADI WA MAMILIONI YA SHILINGI MRADI WA MAJI

$
0
0
WAZIRI wa Kilimo Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba ajitolea kulipia kiasi cha Tsh milioni 2 kwa kusaidia matengenezo ya mashine ya maji huku akitumbua majipu kwa kuwasimamisha kazi viongozi 15 bodi ya maji ya kijiji cha Mingela jimboni kwake Iramba wilaya ya Iramba mkoani Singida baada ya bodi hiyo kufanya ufisadi wa milioni 9 za mradi wa maji wa kijiji hicho.

Viongozi hao ambao ni pamoja na afisamtendaji wa kijiji cha Mingela ,Mwenyekiti ,katibu ,mhasibu na wajumbe 12 ambao walikuwa wakiunda bodi hiyo ya maji waliwasimamisha baada ya kutafuna pesa hizo za mradi wa maji na kushindwa kulipia milioni 2 kwa ajili ya matengenezo ya mashine iliyoharibika . 

Nchemba ambae ni mbunge wa jimbo la Iramba alifikia uamuzi huo wa kuivunja bodi hiyo ya maji kijijini hapo jana baada ya wananchi wa kijiji hicho kulalamika katika mkutano wake wa hadhara kwa ajili ya kuwashukuru kwa kumchagua na kuanza kutimiza sehemu ya ahadi zake ,kuwa hawana huduma ya maji safi baada kukosa Tsh milioni 2 za kutengeneza mashine ya maji iliyoharibika kwa muda sasa.

Kutokana na kilio hicho cha wananchi Nchemba alilazimika kumwita jukwaani afisa mtendaji wa kijiji hicho Bw Said Mussa na bodi yake ili kueleza mapato na matumizi ya mradi huo wa maji yapo kiasi gani na yapo wapi ,swali lililopelekea viongozi hao kujichanganya kujibu kuwa ni kweli makusanyo ya mradi huo wa maji ni zaidi ya Tsh milioni 9.4 ila benki zipo kiasi cha Tsh 400,000 na pesa nyingine zimetumika kukarabati mashine hiyo iliyokuwa ikihitaji kutengenezwa kwa Tsh milioni 2 .
Waziri wa kilimo , mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akipokelewa na wananchi wa kata ya Tulia jimboni kwake Iramba jana 
Waziri Mwigulu akilakiwa na wapiga kura wake wakati wa mikutano yake ya kuwashukuru 
Waziri Nchemba akiwapungia mikono wananchi wake 
waziri Nchemba akiteta jambo na mmoja kati ya walemavu katika kata ya Tulia jimboni Iramba .
Waziri wa kilimo ,chakula na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akitangaza kuwasimamisha kazi viongozi wa bodi ya maji Mingela Iramba kwa ufisadi wa mamilioni ya maji 
Waziri Nchemba akiwa na mmoja kati ya walemavu wa ngozi katika jimboni kwake 


Na Matukiodaima Blog 
Mganganyiko huu ulimlazimu waziri huyo kuivunja bodi hiyo ya maji na kumwagiza mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Clement Berege kupeleka wakaguzi wa ndani mara moja katika kijiji hicho ili kukagua mapato na matumizi pamoja na kuwachukulia hatua wahusika wote wa ufisadi huo wa pesa za makusanyo ya maji.

Alisema kuwa ni ufisadi mkubwa ambao umefanywa na viongozi hao wa bodi ya maji katika kijiji hicho kwa kutafuna pesa zote pasipo matengemnezo ya mashine ya maradi huo wa maji."Yaani ni ufisadi mtupu ambao sikubaliani nao hata kidogo mashine ya kutengenezwa milioni 2 imetengenezwa kwa milioni 9 na bado haifanyi kazi .....naomba wote mliohusika na ufisadi huu kuanzia leo mkae pembeni na wakabidhiwe ofisi watu wengine ......pia mkurugenzi kuanzia sasa vitabu vyote vya makusanyo ya mapato vithibitiwe ili kuepusha kupoteza ushahidi " 

Hata hivyo aliuagiza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba kutuma wakaguzi wa ndani katika vijiji vyote vya Halmashauri hiyo ili kufanya ukaguzi wa mapato na matumizi kwenye vijiji vyote .Alisema yawezekana viongozi wa vijiji wamekuwa wakitumia vibaya makusanyo ya pesa za wananchi bila kufuata utaratibu wa kusoma mapato na matumizi kwa kila baada ya miezi mitatu kwa mujibu wa taratibu.

Katika hatua nyingine Bw Nchemba aliutaka uongozi wa serikali za vijiji katika wilaya hiyo ya Iramba kuacha kuendelea kuwatoza wananchi ushuru kandamizi wa biashara ndogo ndogo hasa zile zilizopigwa marufuku wakati wa ugonjwa wa kipindupindu kwa kutoza ushuru wa Tsh 10,000 kwa biashara ambayo mwananchi akiuza yote faida yake anaambulia Tsh 5000 hivyo alishauri uongozi wa Halmashauri kushusha ushuru huo ambao ulikuwa maalum kwa mapambano ya ugonjwa wa kipindupindu na kuwatoza ushuru wa Tsh 3500 kwa wananchi wanaojishughulisha kufanyabiashara ndogo ndogo ikiwemo ya upikaji pombe kwa ajili ya kuendesha maisha yao. 

Pia alitaka wananchi kuendelea kudumisha usafi katika biashara zao ili kuondokana na ugonjwa wa kipindupindu ,kwa wananchi ambao walipatwa na maafa wakati wa mvua kubwa zilizonyesha mwaka huu ,alisema kuwa wataalam wa maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu watafika kufanya tathimini ili kuwasaidia wananchi hao.

Akijibu tuhuma hizo mbele ya waziri Nchemba afisa mtendaji wa kijiji cha Mingella Bw Said Mussa alisema kuwa ni kweli walikusanya milioni 9.4 za mradi huo wa maji na fundi kutoka mjini Iramba anahitaji milioni 2 kwa ajili ya kutengeneza mashine hiyo ila kiasi cha pesa kilichopo benki ya Tsh 400,000 pekee hivyo hawana uwezo wa kulipia gharama za fundi.Alisema kuwa kwa upande wake hajui mhusika halisi wa ufisadi huo lakini kwa kuwa waziri amesimamisha kazi wote basi itasaidia kumpata mhusika. 

Samatta sasa kupewa eneo Juni 5

$
0
0
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib (aliyesimama) akizungumza na wanachama (hawapo pichani) maandalizi ya sherehe za kumkabidhi eneo mchezaji bora wa Afrika , Mbwana Samatta katika mkutano uliofanyika Dar es Salaam juzi.

MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umesogeza mbele kwa siku moja sherehe za kumkabidhi eneo mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta hadi Juni 5, 2016 ili kupisha pambano kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na timu ya Taifa ya Misri.

Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassima Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa  maandalizi ya sherehe hizo ambazo awali zilipangwa kufanyika Juni 4, 2016 yamekamilika na Mbwana atakabidhiwa hekari tano za eneo ambazo atalitumia kujenga Kituo cha wanamichezo katika eneo la Mwanzega, Mkuranga mkoa wa Pwani.

Alisema hivi karibuni baba mzazi wa mchezaji huyo, Mzee Ali Samatta alishukuru SHIWATA kutambua mchango wa mwanae katika medani ya soka nchini na kuahidi kusaidia kusimamia juhudi za mwanae katika kuendeleza michezo nchini.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi alithibitisha kufanyika mchezo wa Stars na Misri siku ambayo awali ilipangwa Mbwana kukabidhiwa eneo hilo.

Samatta anayecheza soka ya kulipwa Ulaya atatumia mapumziko ya mechi ya Stars na Misri kukabidhiwa eneo hilo na kadi ya uanachama wa SHIWATA katika kutambua mchango wake kuitangaza Tanzania kuwa mchezaji bora Afrika kati ya wachezaji wanaocheza mpira wa kulipwa ndani ya bara la Afrika.

Katika sherehe hizo wasanii 35 watakabidhiwa nyumba zao kati hiyo, wanachama watatu watakabidhiwa nyumba ndogo, 31 watakabidhiwa misingi na nyumba kubwa moja na kufikia idadi ya nyumba 185 ambazo zimekwisha jengwa kijijini hapo mpaka sasa.

Akizungumza katika mkutano wa wanachama kujiandaa na sherehe hizo walimuomba Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Mnauye awe mgeni rasmi ambapo pia waliomba dua la kumuombea Rais John Pombe Magufuli katika juhudi zake za kupambana na wabadhirifu wa mali ya umma.

MWANAMUZIKI, DIAMOND AWAKABIDHI ZAWADI WASHINDI WA SHINDANO LA SHINDA MILIONI NA RED GOLD JIJINI DAR LEO.

$
0
0
 MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva na Balozi wa Red-Gold  hapa nchini, Abdul Nasibu (Diamond Platnum), Amewakabidhi zawadi za washindi wa shindano shinda  Mamilioni na la Red-Gold la wiki jijini Dar es Salaam leo.

Shindano hilo la 'Shinda milioni na Red Gold' lenye kauli mbiu ya Ladha na Mtonyo lililoanza kushindaniwa wiki iliyopita na kupata washindi wawili wa milioni 1 na wawili wa laki 5 na wengine laki moja.
 Mkurugenzi wa  Masoko wa Kampuni inayotengeneza Matunda na mbogamboga M/s Darsh, Darsh Pandit akizungumza jijini Dar es Salaam leo katika hafla fupi ya kuwakabidhi washindi wa wiki wa shindano la Ladha na Mtonyo lililokuwa likijumuisha watumiaji wa bidhaa za Red Gold.
 Mkuu wa Masoko na Biashara, Dominicus Ulikaye akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi washindi wa shindano la Ladha na Mtonyo lililokuwa likishindanisha walaji wa bidhaa za Red- Gold ambapo mshindi anaweza kujishindia shilingi milioni moja mapaka Laki moja kwa kutumia bidhaa hizo.
Kushiriki ni kununua Bidhaa za Red Gold na kutazama kwenye kifuniko namba na kuzituma kutuma kwenda  kwenye kampuni husika.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni M/S Darsh Industries Limited inayotoa bidhaa za Red Gold, Badrish Pandit akizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi zawadi washindi wa shindano la 'Shinda milioni na Red Gold' lililokuwa kikishindanishwa kwa kutumia bidhaa za Red Gold jijini Dar es Salaam.
 Mwanamuziki wa Bongo Fleva na Balozi wa Red-Gold  hapa nchini, Abdul Nasibu (Diamond Platnum) akizungumza kabla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa shindano la'Shinda milioni na Red Gold' jijini Dar es Salaam leo. Shindano hilo lililuwa likishindanishwa kwa kununua bidhaa za Red Gold na kufungua Kizibo kuangalia kama umeshinda kwa kutuma namba zilizo kwenye kizibo hicho.
 Mwanamuziki wa Bongo Fleva na Balozi wa Red-Gold  hapa nchini, Abdul Nasibu (Diamond Platnum) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.












Mwanamuziki wa Bongo Fleva na Balozi wa Red-Gold  hapa nchini, Abdul Nasibu (Diamond Platnum) akiwakabidhi washindi wa shindano la 'Shinda Milioni na Red Gold' jijini Dar es Salaam leo. 
Mwanamuziki wa Bongo Fleva na Balozi wa Red-Gold  hapa nchini, Abdul Nasibu (Diamond Platnum), Viongozi wa Kampuni M/S Darsh Industries Limited wakiwa katika picha ya pamoja jijini Dar es Salaam leo.

SERIKALI YAFAFANUA KUHUSU NDEGE NDOGO ZINAZOENDESHWA NA RUBANI MMOJA.

$
0
0
Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.

SERIKALI imesema kuwa, hakuna kiwango kinachobainisha wazi kuwa ndege yenye uwezo wa kubeba abiria kumi au zaidi ni sharti iendeshwe na marubani wawili.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Eng. Edwin Ngonyani wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Tambwe, Mhe. Khalifa Issa aliyetaka kujua kuhusu Sheria za nchi na za Kimataifa zisemavyo kuhusu ndege za namna hiyo kurushwa na rubani mmoja.

Eng. Ngonyani amesema kwamba, taratibu zinazoongoza fani ya kuendesha ndege nchini huongozwa na miongozo inayokubalika Kimataifa na ambayo imeridhiwa hapa nchini na Bunge.

Amefafanua kuwa, Katika taratibu hizo, kuna matakwa ya kisheria na kiufundi ambayo yakifuatwa yanawezesha kuwa na uwezekano mdogo sana wa kukumbwa na athari ya kiafya na kushindwa kumudu kuendesha ndege.

Ameeleza kuwa, Marubani hupimwa afya zao na madaktari bingwa kila muda maalum kulingana na umri kama ilivyoainishwa katika Kanuni ya 140 mpaka 177 ya The Civil Aviation (Personnel Licensing) Regulations, 2012.

"Serikali inaruhusu ndege kuendeshwa na rubani mmoja kwa kuzingatia taratibu hizo, Aidha, Kanuni 32(5) inasema kwamba ndege iliyoandikishwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuruka kwa shughuli za kibiashara yenye uzito unaozidi kilo 5,700 itakuwa na marubani wasiopungua wawili", alisema Eng. Ngonyani.

Pia amefafanua kuwa, shughuli za Usalama wa Anga nchini zinaongozwa na Sheria Namba 80 "Cvil Aviation Act. 80" na Kanuni zilizotengenezwa chini yake, ambapo urushaji wa ndege yenye abiria tisa au zaidi unaongozwa na Kanuni ziitwazo "The Civil Aviation (Operation of Aircraft) Regulations, 2012" ambapo ndege inayotimiza vigezo vilivyowekwa kwenye vifungu (2), (3) na (4) vya Kanuni ya 32 kuwa na uzito wa chini ya kilo 5,700 inaruhusu kuendeshwa na rubani mmoja.

Ameongeza kuwa, katika viwango vinavyotolewa na Shirika la Kimataiaf la Usafiri wa Anga (ICAO) kwenye kiambatanisho namba 19, chini ya Mkataba wa Kimataifa wa Usafiri wa Anga (Chicago Convention) hakuna kiwango chochote kinachobainisha wazi kuwa ndege yenye uwezo wa kubeba abiria 10 au zaidi ni sharti iendeshwe na marubani wawili.

"Pia hakuna hata mapendekezo ya kiutekelezaji kwenye suala hilo, na hata katika Kiambatanisho cha 6 chenye sehemu tatu kianchohusiana na uendeshaji wa ndege ambacho ndicho kinachozungumzia idadi ya marubani katika uendeshaji wa ndege hakina katazo hilo", alisisitiza Eng. Ngonyani.

Rais Dkt Shein afanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kama ifuatavyo:

1.UTEUZI WA WAKUU WA MIKOA

Uteuzi huo ni kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 61(1) cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

WALIOTEULIWA NI:

I. Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi – Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud.
ii. Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja –Mhe. Vuai Mwinyi Mohammed.

Wakuu wa Mikoa ambao mikoa yao haikutajwa katika taarifa hii wanaendelea na dhamana zao kama kawaida.

2.UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA:

Kwa mujibu wa uwezo aliyopewa chini ya kifungu 61(2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 , Rais amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya kama ifuatavyo:

1. Mkuu wa Wilaya ya Mjini –Mhe. Marina Joel Thomas.
ii. Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” – Mhe. Silima Haji Haji.
iii. Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “A” – Mhe. Hassan Ali Kombo.
iv. Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B”- Mhe. Issa Juma Ali.
v. Mkuu wa Wilaya ya Kati – Mhe. Mashavu Sukwa Said.
vi. Mkuu wa Wilaya ya Kusini-Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa.
vii. Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake- Mhe. Salama Mbarouk Khatib.
Aidha Wakuu wa Wilaya ambao wilaya zao hazikutajwa katika taarifa hii, wanaendelea na dhamana zao kama kawaida.

Uteuzi huo unaanza leo Mei 23, 2016.

Viongozi wote hao waliotajwa wanatakiwa waripoti Ikulu mjini Unguja kesho Mei 24, 2016 saa nane za mchana kwa ajili ya kuapishwa.

Taarifa ya mabadiliko hayo imesainiwa na Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, ambaye ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zanzibar leo 23 Mei, 2016.

SERIKALI YAKAMATA KILO 140 ZA DAWA ZA KULEVYA NCHINI

$
0
0
Na Anitha Jonas – MAELEZO
Dar es Salaam.

Serikali imefanikiwa kukamata takribani kilo 139.69 za dawa za kulevya ikiwemo kilo 53.49 za Heroin, Cocaine kilo 86.2 kuanzia mwaka 2015 mpaka Aprili mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Elimu, Habari na Takwimu wa tume hiyo, Amani Msami, pia tume hiyo imekamata tani 97 za bangi na mirungi.

Alisema mbali na kukamata kilo hizo, takwimu zinaonesha kuwa watumiaji wa Heroin nchini wanakadiriwa kuwa kati ya 200,000 hadi 425,000 ambapo kati ya hao 30,000 hutumia dawa hizo kwa njia ya kujidunga sindano.

“Serikali imefanikiwa kukamata takribani kilo 53.49 Heroin, Cocaine kilo 86.2 kuanzia mwaka 2015 mpaka Aprili mwaka huu” alisema Msami na kuongeza kuwa:

“Watumiaji wa Heroin nchini wanakadiriwa kuwa kati ya 200,000 hadi 425,000 ambapo kati ya hao 30,000 hutumia dawa hiyo kwa njia ya kujidunga”.Msami alifafanua kuwa mbali na kukamata dawa hizo, tume hiyo ilikamata tani 81.3 za bangi na Mirungi tani 15.7.

Aliongeza kuwa mbali na hayo idadi ya watuhumiwa waliyokamatwa wakijihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya zikiwemo Bangi,Mirungi, Heroin na Cocaine walikuwa 14,503.Hata hivyo, alisema takwimu hizo zinaonyesha jitihada za serikali katika kukabiliana na biashara ya dawa za kulevya nchini na si ukubwa wa usafirishaji wa Heroin na Cocaine nchini.

“Moja ya jitihada za Serikali katika kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya ni kutungwa kwa Sheria ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Na.5 ya mwaka 2015.” Alisema Msami.

Alifafanua kuwa sheria hiyo imeweka adhabu kali kwa makosa ya kujihusisha na matumizi na biashara ya dawa ya kulevya ikiwemo kifungo cha maisha kwa yeyote atakayesafirisha dawa za kulevya.

Atakeyehusisha watoto na dawa za kulevya jela miaka 30

$
0
0
Anitha Jonas – MAELEZO

SERIKALI imesema kuwa mtu yeyote atakayekamatwa kwa kosa la husisha au kushawishi mtoto kujiingiza katika matumizi au biashara ya dawa za kulevya atahukumiwa kifungo cha miaka isiyopungua 30. 

Hayo yamesema na Mkuu wa Kitengo cha Elimu, Habari na Takwimu wa Tume ya kuratibu na kudhibiti wa Dawa za Kulevya, Amani Msami kupitia Taarifa ya tume hiyo kwa vyombo vya habari.

Msami alisema adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Sheria ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Na.5 ya mwaka 2015 tofauti na Sheria ya Kuzuian Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya Na. 9 ya mwaka 1995 iliyokuwa na mapungufu.Alisema mbali na adhabu hiyo, sheria hiyo mpya imeweka adhabu ya kifungo cha maisha na faini ya shilingi Milioni 200 kwa kumiliki mitambo ya kutengeneza dawa za kulevya.

Msami aliongeza kuwa Sheria hiyo pia imeweka adhabu kali ya kifungo cha maisha pamoja na faini isiyopungua Shilingi Bilioni moja kwa watu wanaofadhili biashara ya Dawa za Kulevya.“Aidha, sheria hii imeweka adhabu kali ya kifungo cha maisha pamoja na faini isiyopungua Shilingi Bilioni moja kwa watu wanaofadhili biashara ya Dawa za Kulevya ambao mara nyingi ni watu wenye uwezo,”alisema Msami.

Mkuu huyo wa Kitengo, alisema Serikali kupitia vyombo vya Dola iliwabaini, kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya wafanyabiashara wadogo na wakubwa wa dawa za kulevya.Aliwataja baadhi ya watuhumiwa wakubwa wa dawa hizo waliokamatwa na kuchukuliwa hatua kuwa ni Ali Khatibu haji (maarufu kwa jina la Shkuba, Mohammed Mwarami (maarufu kwa jina la Chonji na Mwanaidi Mfundo (maarufu kwa jina la Mama Leila).

Msami alisisitiza wito wa Serikali kwa wananchi kutoa ushirikiano wa dhati kwa ajili ya kutoa taarifa kuhusu watu wanaojihusisha na biashara ya dawa ya kulevya ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Rais Magufuli ateua Naibu AG na Mshauri wake wa Uchumi

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi akisoma taarifa ya Uteuzi wa viongozi mbalimbali uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Gerson J. Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Gerson J. Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri (Cabinet Clerk).

Bw. Mdemu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Tulia Ackson ambaye amechuguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mshauri wa Rais, masuala ya uchumi.


Kabla ya uteuzi huo Profesa Longinus Rutasitara alikuwa Mhadhiri wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi leo tarehe 23 Mei, 2016 imeeleza kuwa uteuzi huu unaanza mara moja.

  
Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

23 Mei, 2016 

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI MKUU NA JAJI MKUU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo na Rais Dkt. Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU. 

MATUKIO KATIKA PICHA LEO KUTOKA BUNGENI, DODOMA

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira ambaye pia ni Mbunge Jimbo la Kisesa, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (kushoto) akiwa ameongozana na Mbunge wa CHADEMA Jimbo la Iringa Mjini, Mhe. Mchungaji Peter Simon Msigwa wakielekea Bungeni kwa ajili ya vikao vya asubuhi ndani ya bunge hilo leo 24 Mei, 2016.
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Sospeter Mwijarubi Muhongo akiwasili Bungeni kwa jili ya kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 24 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Mbunge wa CHADEMA Jimbo la Mikumi, Mhe. Joseph Leonard Haule akiwasili Bungeni kwa jili ya kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 24 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mb), Mhe. Eng. Edwin Amandus Ngonyani (kushoto) akiwa ameongozana na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Eng. Hamad Yusuf Masauni wakielekea ndani ya Bunge kwa ajili ya vikao vya asubuhi vya bunge hilo leo 24 Mei, 2016.
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew John Chenge (kulia) akiwa ameongozana na Mbunge mwenzie wakielkea ndani ya Bunge kwa ajili ya vikao vya asubuhi ndani ya bunge hilo leo 24 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge Jimbo la Ngorngoro, Mhe. William Tate Ole-Nasha akiwasili Bungeni kwa jili ya kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 24 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mhe. Mary Machuche Mwanjelwa akiwasili Bungeni kwa jili ya kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 24 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako akiwasili Bungeni kwa jili ya kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 24 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambaye pia ni Mbunge wa CCM Muleba Kaskazini, Mhe. Charles John Mwijage akiwasili Bungeni kwa jili ya kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 24 Mei, 2016 mjini Dodoma.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO, DODOMA.

DC KIHATO: NI AIBU MWANAMKE KUTOKA ALFAJIRI KUTAFUTA KUNI, MUME AMELALA!

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Luteni mstaafu Abdallah Kihato, akipanda mti katika Ofisi ya Kijiji cha Magoza kama sehemu ya utunzaji wa mazingira pamoja na uzinduzi wa mradi wa Majiko Banifu uliofadhiliwa na Green Voices. 

“NI aibu mwanamke anatoka alfajiri kwenda kutafuta kuni wakati mume amelala, tena ni mateso makubwa kwa wanawake,” ndivyo anavyoanza kueleza Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Luteni mstaafu Abdallah Kihato, wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Magoza.


DC Kihato alisema hayo hivi karibuni alipokuwa anazindua mradi wa Majiko Banifu wa kikundi cha ‘Moto Moto’ unaotekelezwa na wanawake wa kijiji hicho kupitia mradi wa Green Voices.

Mkuu huyo wa Wilaya alisema kwamba, kitendo cha mwanamke kuamka alfajiri kwenda vichakani kutafuta kuni kinaitia doa hata ndoa yenyewe kwa maana kinaongeza mateso kwa upande mmoja hasa mama anapokosa usingizi wa alfajiri.

Alisema mradi huo wa majiko banifu ni wa msingi hasa katika kipindi hiki ambapo mazingira yameharibiwa kutokana na ukataji ovyo wa miti kwa ajili ya mkaa na kuni, hali ambayo inawawia vigumu hata wanawake kupata kuni za kupikia.

Majiko hayo banifu yanajengwa kwa kutumia udongo wa kawaida wa kwenye vichuguu na gharama pekee ni sukari na vibao vya kufyatulia matofali.“Misitu yote imekatwa, tena wanaume ndio wanaoongoza kwa ukataji wa miti huku wanawake wakiwa ndio waathirika wakubwa.

“Kila siku ukisimama barabarani utaona malori na baiskeli zimebeba mkaa na kuni kupeleka mjini (Dar es Salaam), wanaume wanaona fahari kukata kuni na mkaa kwenda kuuza lakini hawako tayari kutafuta kuni za kupikia nyumbani, ni aibu kubwa,” alisema DC Kihato.

Aidha, alisema kuni bora zinapelekwa kuuzwa mjini Dar es Salaam wakati wanawake wanabaki kuokoteza kuni ndogo ndogo ambazo zinakwisha baada ya muda mfupi, hivyo kulazimika tena kurudi vichakani.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Luteni mstaafu Abdallah Kihato, akiwasili katika Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang’anda kuzindua mradi wa Majiko Banifu uliofadhiliwa na Green Voices ambao unalenga wanawake kupaza sauti zao katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi. 

Majiko Banifu yaliyotengenezwa na kikundi cha akinamama cha ‘Moto Moto’ katika Kijiji cha Magoza. Majiko hayo ni rafiki wa mazingira kwani yanatumia kuni chache na hivyo kusaidia kupambana na  mabadiliko ya tabianchi. Mradi huo umefadhiliwa na Green Voices.
DC Abdallah Kihato akisikiliza maelezo ya namna ya utengenezaji wa majiko hayo.
Mratibu wa Mradi wa Majiko Banifu, Bi. Regina Kamuli, akionyesha mojawapo ya majiko yaliyotengenezwa na akinamama wa Kijiji cha Magoza.



Mkuu huyo wa wilaya alisisitiza kwamba ni vyema wanawake wa kikundi hicho cha ‘Moto Moto’ wakawa waalimu kwa wenzao ili kusambaza teknolojia hiyo ya majiko banifu ambayo ni rafiki wa mazingira kwani yanatumia kuni kidogo.

Hata hivyo, alihimiza kikundi hicho kisajiliwe rasmi ili kitambulike katika Halmashauri ya Wilaya na kipate fursa mbalimbali za mitaji kutoka halmashauri pamoja na taasisi za fedha.

“Jisajilini rasmi ili Idara ya Maendeleo ya Jamii iwatambue ili fedha  zinapokuja kwa ajili ya akinamama na vijana muweze kunufaika, kila mwaka kuna fedha zinazokuja wilayani kwa ajili ya wanawake na vijana, lakini wanaonufaika ni wachache kutokana na wananchi kushindwa kuunda vikundi na kuvisajili,” alisema.

Aidha, alisema kwamba, pindi watakapojisajili wanaweza kuanzisha hata karakana ya kutengeneza majiko hayo na kuyauza katika vijijini vingi wilayani humo ili kukuza kipato pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Elimu mliyoipata ni mtaji, badala ya kutengeneza majiko yenu wenyewe, mnaweza kutengeneza mengi na kuyasambaza katika vijiji vingine, lakini ninyi pia ni walimu tayari mnaweza kuitwa mahali popote kuwafundisha wanawake wenzenu na mkapata fedha,” alisema.

DC Kihato akikaribishwa na baadhi ya viongozi na wananchi wa Kijiji cha Magoza tayari kuzindua mradi wa Majiko Banifu yaliyotengenezwa na kikundi cha akinamama wa kikundi cha ‘Moto Moto’ kijijini hapo. Mradi huo umefadhiliwa na Green Voices.

Bi. Regina Kamuli akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Luteni mstaafu Abdallah Kihato (hayuko pichani) wakati wa uzinduzi huo. Wengine pichani ni akinamama wanaounda kikundi cha ‘Moto Moto’ ambao ndio wametengeneza majiko banifu kwa lengo ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Mradi huo umefadhiliwa na Green Voices.


Katika kuunga mkono jitihada hizo, DC Kihato alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya kuwaweka katika orodha wanawake hao ili wakaonyeshe bidhaa hiyo ya majiko wakati wa mkesha wa Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Mwalusembe jana Mei 23.

Wanawake hao wameshawezeshwa na uongozi wa Halmashauri na wamehudhuria na kuonesha majiko yao katika sherehe za Mwenge kijijini hapo.

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Mkuranga, Bw. Nambunga, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya kwenye uzinduzi huo, alisema atatoa ushirikiano wa kutosha kwa akinamama hao kuhakikisha wanasajili kikundi chao pamoja na kuzitumia fursa mbalimbali zilizopo.

“Mimi ndiye ninayeshughulikia maendeleo ya jamii, hivyo nawaahidi kwamba nitakuwa nanyi bega kwa bega ili hata fedha hizo zinazokuja wilayani kwa ajili ya vikundi vya kijamii ziweze kuwafikia,” alisema.  

Mratibu wa mradi huo wa majiko banifu, Regina Kamuli, amesema licha ya kuwafunza akinamama hao kutengeneza majiko, lakini pia wameazimia kupanda miti kwa ajili ya kukabiliana na Tatio la uhaba wa kuni katika kijiji hapo.

DC Kihato aliunga mkono jitihada za upandaji miti na yeye mwenyewe alipanda miti mitatu kama sehemu ya uzinduzi wa upandaji miti kijijini hapo huku akiagiza kila kaya ipande miti 10.

“Kila kaya ikipanda miti walau kumi tu tutabadilisha hata mazingira, naomba ninyi akinamama wa kikundi hiki ndio muwe mfano wa upandaji miti na wanakijiji wote lazima wachukue hatua,” alisema mkuu wa wilaya.

DC Abdallah Kihato akiwahutubia wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabianchi  na kuzindua rasmi mradi wa Majiko Banifu kijijini Magoza. Wa pili kutoka kushoto ni Mratibu wa Mradi wa Green Voices nchini Tanzania, Bi. Secelela Balisidya.

DC Kihato katika picha ya pamoja.

DC Kihato akifanya mazungumzo na baadhi ya akinamama wanaotekeleza mradi wa Green Voices nchini Tanzania  walipomtembelea ofisini kwake kabla ya kwenda kuzindua mradi wa Majiko Banifu.

Akinamama wanaotekeleza mradi wa Green Voices nchini Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na DC Abdallah Kihato. Kutoka kushoto ni Siddy Abubakar Mgumia, Tukuswiga Mwaisumbe, Secelela Balisidya, Judica Losai, Farida Hamisi na Regina Kamuli.



Idara ya Misitu ilitoa jumla ya miti 500 ya kuanzia ambapo iliahidi kuendelea kushirikiana na kikundi hicho katika kampeni ya upandaji miti.

Regina ni mmoja kati ya akinamama 15 wanaotekeleza mradi wa Green Voices waliopatiwa mafunzi nchini Hispania mapema mwaka huu kwa nia ya kuwawezesha akinamama kupaza sauti zao kuhusu mabadiliko ya tabianchi kwa kufanya miradi ambayo itahamasisha mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira.

Akizungumzia mradi wa Green Voices, mratibu wa mradi huo unaotekelezwa nchini Tanzania, Secelela Balisidya, alisema mradi wa majiko banifu ni sehemu ya miradi 10 inayotekelezwa chini ya Green Voices ambapo Tanzania ndiyo pekee iliyopendekezwa kutekeleza mradi huo unaofadhiliwa na taasisi ya Foundation for Women of Africa.

Taasisi hiyo inaongozwa na Makamu wa Rais wa zamani wa Hispania, María Teresa Fernández de la Vega.

Mradi wa Green Voices unatekelezwa katika mikoa sita ya Tanzania Bara ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Mwanza, Kigoma, Morogoro na Kilimanjaro.

“Miradi hiyo ni kilimo cha miti ya matunda mkoani Kigoma, kilimo cha viazi lishe visiwani Ukerewe mkoani Mwanza, Ufugaji Nyuki mkoani Morogoro na Pwani, ukaushaji wa mbogamboga kwa kutumia nishati ya jua mkoani Morogoro, usindikaji wa vyakula mbalimbali kutokana na muhogo mkoani Pwani, kilimo hai cha mbogamboga, kilimo cha uyoga mkoani Dar es Salaam, mradi huu wa majiko banifu mkoani Pwani na mradi wa utafiti wa jiko linalotumia nishati ya jua mkoani Kilimanajro,” alifafanua Secelela.

Alisema, lengo kubwa la mradi wa Green Voices ni kupaza sauti za akinamama kueneza ujuzi wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi ili jamii nzima ya Kitanzania iweze kujifunza zaidi na kuzitumia mbinu hizo katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Mradi huo unatarajiwa kutelekezwa kwa mwaka mmoja ili kutoa fursa kwa akinamama kutumia ujuzi wao kupambana na mabadiliko ya tabianchi na sauti zao kusikika, kwa sababu kazi wanazozifanya kila siku za utunzaji wa familia zinahusiana moja kwa moja na mazingira.

Serikali kupitia taasisi na idara zake zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Wizara ya Maendeleo ya Jamii imekuwa ikiendesha program mbalimbali za mafunzo ya ufundi ikiwemo utengenezaji wa majiko banifu na sanifu kama inayoendelea katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa.

Hata hivyo, bajeti ndogo imekuwa changamoto kubwa kwa wananchi wengi kushindwa kufikiwa na elimu ya aina hiyo.




UBOVU WA BARABARA ZA MITAA KATIKA MANISPAA YA ILEMELA MKOANI MWANZA

$
0
0
Hii ni barabara ya Sabatho-Kirumba iliyopo katika Mtaa wa Ngara, Kata ya Kirumba, Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. Barabara hii ni imeharibika kutoka na mvua zilizonyesha Mkoani Mwanza kwa zaidi ya miezi minne iliyopita.

Wakazi wa mtaa huu wanasema, viongozi wa Serikali ya Mtaa, Kata pamoja na Manispaa, unafahamu adha wanayoipata na mara kadhaa wamekuwa wakifika kujionea barabara hiyo jinsi ilivyoharibika hivyo wanaamini itarekebishwa japo wanasikitishwa kwa namna marekebisho yake yanavyochelewa.

Ni barabara ambayo ipo mita chache kutoka Kituo cha Polisi Kirumba, ikiunganisha makazi ya wananchi kutoka jengo la chama cha waalimu mkoani Mwanza hadi kanisa la SDA Kirumba.
Chombo chochote cha usafiri hakina uthubutu wa kupita katika barabara hii. Hakika inasikitisha na ni hatari kwa maisha ya wakazi wa Kirumba.
Hii ni moja kati ya barabara mbovu zilizopo katika Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza kwa ujumla hivyo tutaendelea kupachika picha zake hapa kama sehemu ya kuwakumbusha wahusika kuwahisha utekelezaji wa ukarabati barabara wa barabara hizo.Picha na BMG.

VIJANA WATAKIWA KUACHANA NA UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA

$
0
0

Kiongozi wa Intersport Club akipokea kombe baada ya ushindi.

Na Woinde Shizza,Arusha

Timu ya Intersport club yaibuka kidedea katika Tamasha la vijana mara baada ya kuifunga Club ya mairiva bao 3 kwa 1 katika fainali iliyofanyika katika uwanja wa Shekhe Amir Abeid uliopo Jijini Arusha.

Tamsha hilo ambalo lilianza mapema mwanzoni mwa mwezi huu limeweza kufikia tamati huku vijana wakiwatoa wito kwa wadau mbalimbali wa michezo kujitokeza kuanzisha mashindano kama haya kwani yanawasiadia kwa kiasi kikubwa 

Akizungumza wakati wa fainali za mashindano hayo muuandaaji wa mashindano hayo ambaye ni mwenyekiti wa CCM kata ya Sakina Neema Mollel alisema kuwa lengo la kuanzisha tamasha hili la vijana ni kuwaleta pamoja vijana na kuwapa elimu ya jinsi ya kupiga vita utumiaji wa madawa ya kulevya kwa vijana 

Alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wanajishirikisha na utumiaaji wa madawa ya kulevya ivyo aliona ni bora akatumia muda huu kuwaleta pamoja ili kuwapa elimu pamoja na kuwashirikisha katika tamasha hili la michezo ambalo limeweza kuwafundisha vijana wengi huku wengine wakiwa wameamua kuaachana kabisa na kutumia madawa haya ya kulevya badala yake wameamua kushiriki katika mazoezi pamoja na michezo.

"nia alisi ya kuandaa mashindano haya ni kuwaleta kwa pamoja vijana pamoja na kupiga vita madawa ya kulevya kwa vijana,kuwaleta vijana pamoja,kuwaondoa vijana wasiendelee kukaa mitaani bila kazi kwani michezo ni ajira"Alisema Neema Mollel

Aidha aliwataka wazazi na jamii kwa ujumla kuwajengea vijana misingi Imara ilikuwajengea mtizamo mzuri wa maisha ya mbeleni badala ya kuwatupia lawama ambazo baadae zinajenga uadui kati yao na wazazi na jamii.

Akikabidhi kombe kwa washindi ambao ni Interspot club ,mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha Wilfred Soilel amesema kuwa Michezo hujenga hujenga urafiki kati ya vijana ,wanafahamiana pia afya ya mwili inaimarika, pia itamfanya kijana ufahamu wake kuchangamka.
Sambamba ugawaji wa zawadi katika fainali hizo mshindi wa kwanza Intersport club kutoka kata ya Ungalimited, amekabidhiwa Kombe pamoja na Tsh 100,000 ,Mshindi wa pili Mairiva club Tsh 75,000 na mshindi wa tatu ni Black Eagle Tsh 50,000. 

Muandaaji wa tamasha la michezo kwa vijana wa mkoa wa Arusha Neema Mollel ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Sakina pamoja na mlezi wa Timu za mpira kata ya Sakina Jijini Arusha akiongea katika fainali za Tamasha la vijana lililofanyika katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini hapa.
Martini Shimweta( Mdau) ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Olmatejoo A.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha Mjini Wilfred Soilel.
Diwani wa kata ya Ungalimited akiwa anawaasa vijana kuachana na madawa ya kulevya katika fainali hizo

Twanga Pepeta kuzindua Albamu ya 13 Mwanza Jumamosi, kuchangia madawati

$
0
0
Mkurugenzi wa bendi ya African Stars, Asha Baraka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  kuhusiana na uzindua albamu yake ya 13 ijulikanayo kwa jina la Husiyaogope Maisha mkoani Mwanza kwenye ukumbi wa Villa Park Jumamosi Mei 28. Kulia ni mwimbaji wa bendi hiyo, Haji Ramadhani.

Bendi ya muziki ya African Stars “Twanga Pepeta” itazindua albamu yake ya 13 ijulikanayo kwa jina la Usiyaogope Maisha mkoani Mwanza kwenye ukumbi wa Villa Park Jumamosi.

Akuzungumza jijini jana, Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka alisema kuwa maandalizi ya uzinduzi huo yamekwisha kamilika na wanamuziki wake wapo kwenye maandalizi ya mwisho kwa ajili ya uzinduzi huo.

Mbali ya wimbo wa Husiyaogope Maisha uliotungwa na Ali Choki, nyimbo nyingine zinazounda albamu hiyo ni Ndoa (Luizer Mbutu), Uso Chini, (Choki), Michepuko (Msafiri Diouf), Mapenzi Yanaumiza (Haji Ramadhani) na Ganda la Mua uliotungwa na Saleh Kupaza ambaye kwa sasa hayupo kwenye bendi hiyo.

Asha alisema kuwa wamekwisha rekodi nyimbo zote na mauzo ya CD 1000 ya kwanza, yatatumika kuchangia ununuzi wa madawati mkoani humo. Alisema kila CD itauzwa Sh3, 000 na Sh 1,000 watatumia kununua madawati.

“Hii ni heshima kwa wapenzi wa muziki wa Mwanza, bendi inafanya uzinduzi wa albamu hii kwa mara ya kwanza mkoani, albamu zote 12 zilizinduliwa hapa Dar es Salaam, hii ni mara ya kwanza katika historia ya bendi yetu,”

“Tunataka tuwe tofauti, mpango wa kununua madawati pia utafanyika katika uzinduzi wa albamu hiyo kwa mkoa wa Dar es Salaam katika siku itakayopangwa, tumepiga hesabu na kujua dawati moja ni Sh50,000 (kama utatengeneza mwenyewe), “ alisema Asha.

Alisema kuwa albamu hii ni ya aina yake kwani wanamuziki wake wametunga nyimbo ambazo mbali ya kuburudisha, pia zinatoa mafundisho mbalimbali.Albamu za nyuma ya bendi hiyo ni Kisa Cha Mpemba, Jirani, Fainali Uzeeni, Chuki Binfasi, Ukubwa Jiwe, Mtu Pesa, Safari 2005, Password, Mtaa wa Kwanza, Mwana Dar es Salaam, Dunia Daraja na Nyumbani ni Nyumbani.

DC MONDULI AENDESHA ZOEZI LA UKAMATAJI WATOTO MINADANI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Francis Miti.


Na Woinde Shizza,Monduli

Imeelezwa kuwa Asilimia 10 ya watoto wilayani Monduli wanatajwa kutokwenda shule kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro,pamoja na kufanya biashara katika baadhi ya minada wilayani humo jambo ambalo limeamsha hisia za viongozi wa wilaya na kuamua kufanya operesheni ya kuwakamata na kuwapeleka shule kwa lazima Zaidi ya watoto 21.

Hayo yameelezwa leo naAfisa elimu msingi Theresia Kyala kutoka wilaya ya Monduli mara baada ya ya zoezi la ukamataji wa watoto watoro amnao wanafanya biashara eneo la minada ambapo zoezi hilo lilifanyika mnada wa katika eneo la losirwa iliyoko kata ya mto wa mbu iko ambapo ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa wilaya ya Monduli bw,Francis Miti ambapo eneo hilo lina wakazi laki tatu kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 huku Zaidi wakiwa ni wakazi wa jamii ya kifugaji.

Ambapo zoezi hilo limeendeshwa chininya usisamizi wa mkuu huyo na uongozi wa idara ya elimu imetembelea eneo la mnada wa Kigongoni na kuona watoto namna ambavyo wanaendelea kufanya biashara ndani ya mnada huo wakati wenzao wakiwa madarasani ambapo nikazungumza na baadhi ya watoto hao ambao wanaelezea baadhi ya sababu zilizowapelekea kutokwenda shule ikiwemo ugumu wa maisha huku wengine wakishindwa kujielezea.

Theresia Kyara ni afisa elimu msingi wilayani Monduli alisema kuwazoezi la operesheni hiyo wameianza rasmi katika soko la Alhamisi la eneo la monduli mjini na kufanikiwa kukamata watoto 16 na leo hii wamekamata watoto 21 hii kati ya hao watoto sita wamepelekwa bweni shule ya Manyara inaongeza idadi ya watoto ambao hawajaenda shule katika wilaya hiyo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo ya Monduli Francis Miti amesema kuwa ameamua kutoa agizo hilo na kutekelezwa kwa lengo la kuwawezesha kwa kila mtoto mwenye sifa ya kwenda shule aweze kupata elimu hiyo ya kuanzaia msingi bure kwa lengo la kumuunga mkono mh,Rais katika utoaji wa elimu bure ili kuweza kuweza kushinda katika sekta ya elimu.

Pia amewataka wazazi wote wenye watoto kuhakikisha wanapeleka shule watoto wao na kuwaandikisha na endapo mzazi ama mlezi atakae mhusisha na kumkataza mtoto wake hatua za kisheria zitachukuliwa.Mkuu wa wilaya ya Monduli ameongeza kuwa zoezi hili la ukamatwaji wa watoto hao ambao kati yao wapo waliotoka kwaajili ya kuchunga katika minada huku wengine wakiwa hawajasoma kabisaa.

Nae mmoja wa mzazi bi,Moses ole laizer amesema kuwa zoezi hilo la kukamata watoto hao litaleta tija katika jamii kutokana na kuwa hakuna sababu inayofanya watoto hao wasiende shule kutokana na elimu kuwa bure na wazazi kuwaachia baadhi yao kuenda kufanya biashara minadani.Aliongeza kuwa baadhi ya Jamii za kifugaji hususani wamasai wamekuwa na muamko mdogo wa kupeleka watoto wao kupata elimu jambo ambalo linawanyima haki ya msingi kwa kila mtoto mwenye sifa kwenda shule
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images