Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 854 | 855 | (Page 856) | 857 | 858 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Majimatitu, Mbagala wakibeba madawati waliyopewa na Benki ya NMB Tawi la Mbagala. Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Majimatitu, Mbagala wakibeba madawati waliyopewa na Benki ya NMB Tawi la Mbagala.Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Majimatitu, Mbagala wakibeba madawati waliyopewa na Benki ya NMB Tawi la Mbagala. Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Majimatitu, Mbagala wakibeba madawati waliyopewa na Benki ya NMB Tawi la Mbagala.
  Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Vicky Bishubo (kulia) akimkabidhi moja ya dawati Mwakilishi wa Afisa Elimu Manispaa ya Temeke, Salum Upunda ikiwa ni miongoni mwa msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na Benki ya NMB Tawi la Mbagala. Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Vicky Bishubo (kulia) akimkabidhi moja ya dawati Mwakilishi wa Afisa Elimu Manispaa ya Temeke, Salum Upunda (kushoto) ikiwa ni miongoni mwa msaada wa madawati 50 kwa Shule ya Msingi Majimatitu yaliyotolewa na Benki ya NMB Tawi la Mbagala.Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mbagala, Muhidin Zaki (kulia) akimkabidhi Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Majimatitu, Abdul Mgomi (kushoto) moja ya dawati kati ya madawati 50 yaliyotolewa kama msaada kwa shule ya msingi Majimatitu. Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mbagala, Muhidin Zaki (kulia) akimkabidhi Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Majimatitu, Abdul Mgomi (kushoto) moja ya dawati kati ya madawati 50 yaliyotolewa kama msaada kwa shule ya msingi Majimatitu.Mwenyekiti wa Mtaa wa Majimatitu 'A', Saidi Haji Mpetta (kulia) akimkabidhi Mkuu Shule ya Msingi Majimatitu, Abdul Mgomi (kushoto) dawati moja kati ya madawati 50 yaliyotolewa na Benki ya NMB Tawi la Mbagala juzi. Mwenyekiti wa Mtaa wa Majimatitu 'A', Saidi Haji Mpetta (kulia) akimkabidhi Mkuu Shule ya Msingi Majimatitu, Abdul Mgomi (kushoto) dawati moja kati ya madawati 50 yaliyotolewa na Benki ya NMB Tawi la Mbagala juzi.Kikundi cha kwaya cha Shule ya Msingi Majimatitu kikiwaburudisha wageni waalikwa katika hafla hiyo ya kukabidhiwa madawati 50 ya msaada kwa shule hiyo. Kikundi cha kwaya cha Shule ya Msingi Majimatitu kikiwaburudisha wageni waalikwa katika hafla hiyo ya kukabidhiwa madawati 50 ya msaada kwa shule hiyo.
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Majimatitu wakisoma risala kwa mgeni rasmi katika hafla hiyo. Wanafunzi wa Shule ya Msingi Majimatitu wakisoma risala kwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Majimatitu akikabidhi risala kwa mgeni rasmi katika hafla hiyo. Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Majimatitu akikabidhi risala kwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Majimatitu, Abdul Mgomi (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhiwa madawati 50 ya msaada kwa shule yake. Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Majimatitu, Abdul Mgomi (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhiwa madawati 50 ya msaada kwa shule yake.Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Vicky Bishubo (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kukabidhi msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na Benki ya NMB Tawi la Mbagala. Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Vicky Bishubo (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kukabidhi msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na Benki ya NMB Tawi la Mbagala. Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Vicky Bishubo (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kukabidhi msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na Benki ya NMB Tawi la Mbagala. Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Vicky Bishubo (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kukabidhi msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na Benki ya NMB Tawi la Mbagala.Mwenyekiti wa Mtaa wa Majimatitu 'A', Saidi Haji Mpetta (kulia) akitoa salamu za shukrani mara baada ya Shule ya Msingi Majimatitu, kukabidhiwa madawati 50 yaliyotolewa na Benki ya NMB Tawi la Mbagala juzi. Mwenyekiti wa Mtaa wa Majimatitu 'A', Saidi Haji Mpetta (kulia) akitoa salamu za shukrani mara baada ya Shule ya Msingi Majimatitu, kukabidhiwa madawati 50 yaliyotolewa na Benki ya NMB Tawi la Mbagala juzi.Mwenyekiti wa Mtaa wa Majimatitu 'A', Saidi Haji Mpetta (kulia) akitoa salamu za shukrani mara baada ya Shule ya Msingi Majimatitu, kukabidhiwa madawati 50 yaliyotolewa na Benki ya NMB Tawi la Mbagala juzi. Mwenyekiti wa Mtaa wa Majimatitu 'A', Saidi Haji Mpetta (kulia) akitoa salamu za shukrani mara baada ya Shule ya Msingi Majimatitu, kukabidhiwa madawati 50 yaliyotolewa na Benki ya NMB Tawi la Mbagala juzi.NMB kulia ikimkabidhi moja ya madawati Mwenyekiti Kamati ya Shule.
  Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Vicky Bishubo (kulia) akimkabidhi dawati Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Shule ya Msingi Majimatitu, Jacob Macha (kushoto) katika hafla hiyo.
  Picha ya pamoja wageni rasmi na bendi ya shule2
  Kikundi cha kwaya cha Shule ya Msingi Majimatitu na bendi ya shule katika picha ya pamoja na wageni rasmi katika hafla hiyo ya kukabidhiwa madawati 50 ya msaada kwa shule hiyo.
  Shule ikikabidhiwa mipira
  Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mbagala, Muhidin Zaki (kushoto) akimkabidhi mmoja wa viongozi wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Majimatitu, kwa ajili ya shule yao. Katika hafla hiyo Benki ya NMB ilitoa pia madawati 50 kama msaada kwa shule ya msingi Majimatitu.
  Shule ikikabidhiwa mipira1Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Vicky Bishubo (kushoto) akimkabidhi mpira mmoja wa viongozi wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Majimatitu, kwa ajili ya shule yao. Katika hafla hiyo Benki ya NMB ilitoa pia madawati 50 kama msaada kwa shule ya msingi Majimatitu.

  0 0


  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kulia) akioneshwa maeneo mbalimbali ya Gereza la Kilimo Songwe, Mkoani Mbeya alipofanya ziara ya kikazi leo Mei 21, 2016 Gerezani hapo(wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(kushoto) ni Mkuu wa Gereza Songwe, ACP. Laizack Mwaseba.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akiangalia moja ya shamba la alizeti katika Gereza la Kilimo Songwe.Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Rwegasira(kushoto) akiwa na Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja kwa pamoja wakiangalia mazao ya mahindi katika Mashamba mbalimbali ya Gereza la Kilimo Songwe walipotembelea Gereza hilo leo Mei 21, 2016.Mazao ya Mahindi yakiwa tayari yamevunwa katika mashamba mbalimbali ya Gereza la Kilimo Songwe lililopo Mkoani Mbeya kabla ya kupukuchuliwa kwenye mashine maalum.Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa pili kushoto) akiangalia mashine ya kupukuchulia mahindi katika Gereza la Kilimo Songwe lililopo Mkoani Mbeya.Mahindi yakiwa tayari yamepukuchuliwa na mashine maalum katika Gereza la Kilimo Songwe kama yanavyoonekana katika picha. Gereza hilo hivi sasa linauwezo wa kuzalisha chakula cha kulisha Wafungwa wote waliopo katika Magereza yote ya Magereza Mkoa wa Mbeya.Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Asumusio Achacha akimuongoza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira alipotembelea Ofisi za Idara hiyo kabla ya kuelekea Gereza la Kilimo Songwe lililopo Mkoani Mbeya(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Chuo cha Habari Zanzibar wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Tamasha la Michezo ya Vyu Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu) Tr 21 Mey 2016.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akipiga mpira ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Mashindano ya Tamasha la Michezo ya Vyu Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu) Tr 21 Mey 2016.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akipiga mpira ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Mashindano ya Tamasha la Michezo ya Vyu Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu) Tr 21 Mey 2016.

  0 0


  Afisa wa Mfuko wa Hifadhi wa PSPF Ndg Mohammed Salum akitowa maelezo ya manufaa ya Kujiunga na Uchangiaji wa Hiyari kwa Wastaafu wa Jamuhuri ya Muungano na faida zake kupitia Mfuko huo wakati wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo uliodhaminiwa na PSPF.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wastaafu wa Jamuhuri ya Muungano Zanzibar Ndg Khamis Rashid, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmin Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Zanzibar Mhe Nassor Salum Jazira kuufungua mkutano huo Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa Jengo Sanaa Rahaleo Zanzibar. 
  Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe Nassor Salum Jazira akitowa nasaha zake kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wastaafu wa Jamuhuri ya Muungano Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Jengo la Sanaa Rahaleo Zanzibar
   
  Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wasstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg Ramadhani Nzori, akizungumza kabla ya kumkaribisha Afisa wa Mfuko wa Hifadhi wa PSPF kuzungumzia umuhimu wa kujichangia kwa hiari katika Mfuko huo kwa Wastaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
   

  0 0

   Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mungereza (kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 50 kwa  mshindi wa Airtel Music Stars Tanzania 2016, Melisa John, mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo. Melisa amejishindia shilingi milion50 pamoja na kupata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Airtel Trace Music Stars Afrika.
   mshindi wa Airtel Music Stars Tanzania 2016, Melisa John akipongezwa na mama yake baada ya kuibuka mshindi nakupata kitita cha shilingi milioni 50.
   Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Bi Gabriel Kaisi (kulia) akimkabithi Nandi Charles mfano wa hundi ya shilingi milioni 5 mara baada ya kuibuka mshindi wa pili wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania, katika shindano hilo Melisa John aliibuka kuwa mshindi wa kwanza.
  wanavyoimba ili kupata mshindi wa shindano hilo kwa Tanzania
   Mshindi wa tatu wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania Salim Mlindila akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 2 kutoka kwa Meneja wa kampuni ya Tabasamu, Lucy Ngongoseke.
   mshindi wa Airtel Music Stars Tanzania 2016, Melisa John, akiongea mara baada ya kutangazwa mshindi na  kukabithiwa mfano wa hundi ya shilingi miliioni 50. Kulia ni mama yake Melisa John,na kushoto nao MC wa fainali hizo.
   Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Tanzania 2016, Melisa John, akiimba mara baada ya kutangazwa mshindi katika fainali za shindano la Airtel Trace Music Stars  zilizofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam. Melisa amejishindia shilingi milioni 50 pamoja na kupata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Airtel Trace Music Stars Afrika. Mshindi wa pili wa mashindano hayo ni  Nandi Charles na Watatu ni Salim Mlindila

   Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga akitumbuiza wakati wa fainali za shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaama,  wakati wa fainali hizo, Mayunga pia alizindua wimbo wake wa video aliomshirikisha mwimbaji wa Marekani Akon ujulikanao kama “ Please don’t go away”
   Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga akitumbuiza wakati wa fainali za shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaama,  wakati wa fainali hizo, Mayunga pia alizindua wimbo wake wa video aliomshirikisha mwimbaji wa Marekani Akon ujulikanao kama “ Please don’t go away”
   Majaji wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania, Luciano Gadie Tsere(kushoto) na Tony Joett wakifatilia kwa makini washiriki
   Baadhi wa waalikwa waliojitokeza kushuhudia shindano la Airtel Trace music Stars wakiwa katika picha wakati wa koktaili kabla ya shindano hilo kuanza

   Washiriki walioingia katika tano bora ya shindano la Airtel Trace Music Stars wakiimba wimbo wa pamoja wakati wa finali za shindano hilo lililofanyika ukumbi wa JINCC jijini Dar es Saalam. 
   Wageni waalikwa mbalimbali wakifatilia na kuwashangilia washiriki wa shindano la Airtel Trace Music Stars wakiwa Jukwaani  huku wakirekodikumbukumbu mbalimbali kupitia simu zao za mkononi

  Wageni waalikwa mbalimbali wakifatilia na kuwashangilia washiriki wa shindano la Airtel Trace Music Stars wakiwa Jukwaani  huku wakirekodikumbukumbu mbalimbali kupitia simu zao za mkononi.  Mashindano ya Airtel Trace Music Stars ya taifa  yamefikia mwisho ambapo Melisa John alitangazwa kuwa mshindi wakati wa fainalii za shindano hilo lililowashirikisha washiriki watano bora na kufanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Saalam.

  Baada ya kuimba kwa umahiri mkubwa wimbo wa mwanamuziki wakimarekani Mica Paris ujulikanao kama “My One Temptation” Melisa aliweza kuwaaminisha majaji kwamba hakika yeye anastahili kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars msimu wa 2.

  Melisa amejishindia shilingi milion 50 huku mshindi wa pili Nandi Charles akijishindia shilingi milioni 5 na mshindi wa tatu Salim Mlindila akiondoka na shilingi milioni 2.

  Kufatia ushindi huo Melisa sasa amepata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars Afrika yatakayoshirikisha washiriki kutoka nchi 9 zikiwemo Niger, DR Congo, Gabon, Kenya, Madagascar, Malawi, Nigeria, Ghana and Zambia yanayotegemea kufanyaka tarehe 11 Juni 2016 , Lagos nchini Nigeria.

  Mshindi wa  Airtel Trace Music Afrika atapata nafasi ya kupata mafunzo ya muziki  na kurekodi video na mwanamuziki nguli na mtunzi wa nyimbo Keri Hilson , Atlanta nchini Marekani.

  “Nimefurahi sana kuibuka mshindi leo, pamoja na ushindi huu mashindano yalikuwa ni ya ushindani kwani kila mshiriki alikuwa na uwezo wa kuimba na mzuri kwa namna tofauti. Nashukuru Mungu kwa kunifikisha hapa na nawashukuru Airtel kwa kutuandalia jukwaa hili ambapo leo limenifanya niweze kuishi ndoto zangu. Napenda sana kuimba na napenda sana mziki naamini huu ni mwanzo mzuri wa safari yangu ya kuwa mwanamuziki nyota” alisema Mshindi wa Airtel Trace Music Stars 2016 Melisa John.

  Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde alisema “ Airtel inajivunia kuwa sehemu ya kuinua maisha ya vijana wengi, tunaamini kupitia program zetu za kuwawezesha vijana tutagusa maisha ya vijana wengi na kuwawezesha kuzifikia ndoto zao. Tumefurahia mashindano ya mwaka huu yamekuwa na mvuto zaidi na tunampongeza Melisa kwakuibuka kuwa mshindi. Tunamtakia afanye vyema katika michuano ya Afrika nchini Nigeria.”

  Katika fainali hizo Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga alitoa burdani ya nyimbo yake ya “ Nice Couple”na kuweza kuzindua kibao chake na video yake ijulikanayo kama “ Please don’t go away” e inayomshirikisha mwanamuziki nguli kutoka marekani, Akon

  0 0

  Msanii kutoka nchini Marekani Neyo akishambulia jukwaa na kuwapagawisha wakazi wa jiji la Mwanza .
  Neyo akiwa pamoja na Diamond Platnumz jukwaani wakiambulisha wimbo wao mpya mbele ya mashabiki na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya.
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ruby akiimba kwenye tamasha la Jembe Festival kwenye uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
  Rapa Stamina akiupagawisha umma na mistari iliyo simama kwenye tamasha la Jembe mjini Mwanza.
  Mr. Blu akirap nyimbo zake zilizompa umaarufu kwenye tamasha la Jembe lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
  Diamond Platnumz na vijana wake wakishambulia jukwaa kwenye tamasha la Jembe lililofanyika kwenye viwanja vya CCM Kirumba mjini Mwanza.
  Mgeni rasmi wa tamasha la muziki la Jembe , Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM Dk. Sebastian Ndege kwenye chumba maalum nyuma ya jukwaa ,CCM Kirumba .


  0 0


  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Bruce Zhang akisoma hotuba yake kwa wageni waalikwa wakati wa halfla ya uzinduzi wa programu ya elimu inayoitwa “Seeds for the Future” nchini Tanzania. Programu hiyo ambayo inatoa nafasi 10 kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini kwenda kujifunza na kufanya kazi na Kampuni ya Huawei iliyopo Shenzhen, China ilizinduliwa rasmi mjini Dodoma mwishoni mwa juma.
   Meneja Uhusiano wa Huawei Tanzania Bw. Jimmy Liguo akifafanua jambo kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) kuhusiana na programu ya “Seeds for the future” wakati wa uzinduzi rasmi wa programu hiyo uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa juma. Kupitia programu hiyo Huawei imejitolea kudhamini mafunzo ya TEHAMA kwa wanafunzi 10 wa vyuo vikuu hapa nchini kila mwaka kwa kipindi cha miaka 10.
    Mgeni rasmi na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Tanzania Prof. Simon Msanjila kushoto) akisikiliza hotuba mbalimbali za wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa programu ya Huawei “Seeds for the future” ambayo inatoa nafasi 10 kila mwaka kwa muda wa miaka 10 kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini kwenda kujifunza na kufanya kazi na Kampuni ya Huawei yenye makao makuu yake Shenzhen, China ambapo wataweza kujipatia ujuzi. Uzinduzi rasmi wa programu hiyo ulifanyika mjini Dodoma mwishoni mwa juma. (Katikati) ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Zanzibar Mhe. Abdullah Mzee na (Kulia) ni Mkuu wa Idara ya TEHAMA katika Chuo kikuu cha Dar es salaam Dk. Musa Kisaka.
   Mgeni rasmi na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Tanzania Prof. Simon Msanjila (katikati) akipeana mkono na mwakilishi wa Ubalozi wa China hapa nchini Lv. YouQing mara baada ya kuzindua rasmi programu ya Huawei”Seeds for the future” ambayo inatoa nafasi 10 kila mwaka kwa muda wa miaka 10 kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini kwenda kujifunza na kufanya kazi na Kampuni ya Huawei yenye makao makuu yake Shenzhen, China. Uzinduzi rasmi wa programu hiyo ulifanyika mjini Dodoma mwishoni mwa juma. (Kulia) ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Zanzibar Mhe. Abdullah Mzee.

  Wageni wa Meza kuu na baadhi ya wafanyakazi wa Huawei wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi 10 wa vyuo vikuu nchini ambao kupitia programu ya “Seeds for the Future” inayodhaminiwa na Huawei walichaguliwa kwenda China kujifunza na kufanya kazi na kampuni hiyo yenye makao makuu yake Shenzhen, China. Uzinduzi rasmi wa programu hiyo ulifanyika mjini Dodoma mwishoni mwa juma.

  KAMPUNI ya Huawei inayoongoza kwenye utoaji wa huduma ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ulimwenguni, leo imezindua programu ya elimu inayoitwa Seeds for the Future hapa nchini Tanzania.
   
  Programu ya ‘Seeds for the Future’ inatoa nafasi 10 kwa wanafunzi wa hapa nchini kutoka vyuo vikuu kwenda kujifunza na kufanya kazi na Kampuni ya Huawei yenye makao makuu yake Shenzhen, China.
   
  Mradi huo umelenga kuwa kusaidia kile kinachofundishwa shuleni kukidhi mahitaji halisi ya soko la ajira kwa vijana hapa nchini ikiwa ni pamoja na kupanua uelewa wa TEHAMA na kuhamasisha ushiriki katika sekta hii ili kuendana na  jamii ya sasa teknolojia ya habari na mawasilino.
   
  Akizunguma wakati wa sherehe ya kuwaaga wanafunzi waliochaguliwa kusoma China, Mkurugeni Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Technologies Tanzania, Bruce Zhang alisema ni wazi kwamba wanafunzi hawa watapewa kipaumbele kwenye fursa za kujifunza kupitia kujumuika na wafanyakazi wa Huawei na kutembelea maabara ya kampuni hiyo ambako wataweza kuona na kufanya majaribio ya teknolojia ya hali ya juu ya mawasiliano.
   
  Alisema vijana hao watapa ujuzi wa kisasa unaowawezesha kushindana katika sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano, huku wakijufunza kukabiliana na ushindani katika soko la ajira.
   
   “Uzinduzi wa mpango huu inathibitisha kuwa tutaendelea kusaidia sekta ya TEHAMA hapa nchini,” alisema mkurugenzi huyo.
   
  “Kupitia ushirikiano huu na Huawei, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), Ninaamini wanafunzi hawa watakuwa na fursa ya kipekee kufanya kazi na kusoma makao makuu ya Huawei, huku wakijifunza utamaduni wa China na kutembelea maeneo muhimu ya vivutio vya utalii,” alisema Bruce
   
  Alisema, mradi huu unafanyika kwenye nchi mbalimbali ulimwenguni ambako Kampuni ya Huawei inafanya shughuli zake na hapa nchini mpango umeshaandaliwa kwa wanafunzi 10 ambao watashiriki programu hii China na watasafiri tarehe 20 Mei mpaka  3 Juni ambapo watashiriki mafunzo hayo muhimu.
   
   
  Alisema, ‘Seeds for the Future’ ni jambo linalodhihirisha kwamba Huawei imeweka mkazo katika maendeleo ya elimu ya TEHAMA vyuo vikuu kama jinsi ilivyojidhihirisha wakati wa kuzindua mradi huu wa elimu.”
   
  Naye Mgeni rasmi wa shughuli hiyo ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Profesa Simon Msanjila alisema kuanzishwa kwa programu hii ni ushahidi kwamba Kampuni ya Huawei imedhamiria kusaidia maendeleo ya TEHAMA katika vyuo vikuu nchini pamoja na kuifanya Tanzania kung’ara katika teknolojia ya habari na mawasiliano.
   
   “Hii itawawezesha wanafunzi wetu kujifunza kwa kuelewa na kuwaandaa kuwa wafanyakazi mahiri kwenye masuala ya IT na sekta ya mawasilino,” alisema Profesa Msanjila.
   
  .
  Naibu Katibu huyo wa Elimu aliongeza kwamba; “Programu ya Seeds for the Future itawasaidia wanafunzi kutoka vyuo hivyo viwili kujifunza mambo mengi ili kuendana na mahitaji ya soko la dunia kwenye TEHAMA.

  0 0


   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari akihutubia mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB katika ukumbi wa AICC Arusha. 
   Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambo akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Wanahisa.
   Mwenyekiti Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akijibu maswali ya wanahisa.

  Wanahisa wakiwa katika mkuano.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Hapa ni katika Msikiti wa Masjid Latif Ahmadiyya Muslim Jamaat Nsalala uliopo kijiji cha Nsalala ,kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga ambapo leo Jumapili Mei 22,2016 Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Mkoa wa Shinyanga(Ahmadiyya Muslim Jamaat Shinyanga) imefanya mkutano wa Mwaka wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Shinyanga ukiwa na kauli mbiu ya " Love For All Hatred For None (Mapenzi Kwa Wote Bila Chuki Kwa Yeyote".

  Mgeni rasmi alikuwa katibu tawala msaidizi idara ya uchumi na uzalishaji aliyemwakilisha kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga John Mongella huku waumini wa dini hiyo kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga wakihudhuria mkutano huo.

  Mkutano huo uliolenga kuhamasisha amani katika jamii kwa kuwakumbusha waumini kumjua mwenyezi mungu hali itakayosaidia kupunguza hata kumaliza kabisa vitendo vya kihalifu ikiwemo mauaji ya watu wasio na hatia kama vile vikongwe na albino, umehudhuriwa pia na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry (pichani juu).

  Akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry alieleza kusikitishwa na kitendo cha mauaji ya watu watu msikitini na kuongeza kuwa dini ya kiislam hairuhusu vitendo kama hivyo huku akiviomba vyombo vya dola kufanya uchunguzi ili kubaini wahusika wa kitendo hicho haramu.

  Kupitia mkutano huo jamii imeelimishwa juu ya dhana potofu dhidi ya uislamu ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakihusisha dini hiyo pamoja na vikundi vya kigaidi mfano wa Boko haram, Isis, Al-shabaab na vingine vingi ambavyo vimekuwa vikidhuru binadamu.

  Mada mbalimbali zimetolewa na viongozi wa jumuiya hiyo ikiwemo nafasi ya dini katika maisha ya binadamu,malezi ya watoto na majukumu ya wazazi sawa na mafundisho ya dini ya kiislamu,umuhimu wa kuwa kiongozi (Khalifa) wa kiroho na barakaza ukhalifa pamoja na masharti ya kujiunga na jumuiya hiyo(masharti 10 ya Baiat na wajibu wa waumini.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa mkutano huo,ametusogezea picha 55 kilichojiri.
  Mgeni rasmi katika mkutano huo Mohammed Idd Nchira akiwahutubia waumini wa dini ya kiislamu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya ambapo alisema suala amani katika jamii ni watu wote hivyo kuwataka watanzania kudumisha amani ya nchi kwa kuepuka kutenda uhalifu .
  Aliyesimama ni Afisa wa polisi kutoka ofisi ya mkuu wa upepelezi na makosa ya jinai mkoa wa Shinyanga Issa Ramadhan akitoa neno ambapo alisema jamii yenye malezi mema haiwezi kuwa na vitendo vya kihalifu na kuwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kuwafichua watu wote wanaofanya vitendo vya uhalifu

  Wanawake wa Kiislam wakiwa katika Msikiti wa Masjid Latif Ahmadiyya Muslim Jamaat Nsalala uliopo kijiji cha Nsalala ,kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika mkutano huo wa mwaka,ambapo kwa mara ya pili sasa mkutano kama huo unafanyika mkoani Shinyanga,mkutano mwingine ulifanyika mwaka 2014

  Waumini wakifutilia kilichokuwa kinaendelea kwenye mkutano huo.   0 0

   Stephen Gimase (Kulia) ambaye ni miongoni wa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” akiangalia vifaa alivyokabidhiwa na Airtel FURSA kwa ajili ya kuboresha biashara yake ya kutengeneza mashine za kutengenezea vifaranga vya kuku, Kushoto ni Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi 
  Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (2 Kushoto) akimkabidhi Theresia Maliatabu (Kulia) ambaye ni miongoni wa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” vifaa vyakuboresha biashara yake ya uchoraji ikiwemo meza ya kuchorea na kompyuta ya kisasa. Kijana huyu Aliyechaguliwa kutoka kwenye mafunzo ya biashara ya ujasiriamali  ya Airtel FURSA yaliyofanyika Dar es Salaam wiki chache zilizopita. Akishuhudiwa na mama yake mzazi Judith Benedicto (Katikati) na mama mkubwa Salome Benedicto (Kulia) pamoja na Afisa mauzo wa Airtel katika hafla iliyofanyika Mbagala kuu, jijini Dar es Salaam.


  • Wawezeshwa vitendea kazi vyenye dhamani ya shilingi milioni tano.

  Dar Es Salaam Mei 21, 2016, Airtel Tanzania inaendeleza dhamira yake ya kuendelea kuwashika mkono vijana hapa nchini  ambapo mwishoni mwa wiki hii kupitia mpango wake wa kutoa semina ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana ujulikanao kama Airtel FURSA Tunakuwezesha, uliweza kuchagua vijana wawili walioweza kuelezea na kuwakilisha changamoto wanazozipata katika biashara wanazozifanya mbele ya jopo la washauri ambao leo hii wamekabidhiwa  vitendea kazi vyenye dhamani ya shilling milioni 5  ili kuweza kukabiliana na changamoto hizo.

  Akizungumza wakati wa sherehe ya makabidhiano hayo, Meneja wa Airtel huduma kwa Jamii Hawa Bayumi alisema "baada ya kufanya mafunzo ya biashara ya ujasiriamali wiki chache zilizopita na kuweza kufikia vijana zaidi ya 300 jijini Dar Es Salaam  waliojitokeza na kuzifahamu vyema FURSA zinazowazunguka ili kujitengenezea ajira na na uwezo wa kujenga fursa nyingine. Leo hii tupo hapa kuwawezesha hawa walioonyesha bidi zaidi”

  “Na siku hiyo ilikuwa ni siku ya faraja kwani vijana waliweza kujifunza mambo mengi sana na mwisho wa siku waliweza kuelezea na kuwasilisha biashara zao mbele ya jopo la washauri na ulikuwa uamuzi mgumu sana lakini mwisho wa siku tuliweza kupata vijana wawili bora walioweza kushinda nyoyo za jopo la washauri hao, ambao leo  hii tupo hapa kwajili ya kuwakabidhi vifaa vyao ili waweze kwenda  kukabiliana na changamoto walizonazo katika biashara zao. "

   Mpaka sasa Airtel imefanya semina nyingi sana za mafunzo ya biashara ya ujasiriamli hapa nchini katika mikoa mbali mbali na kuweza kufikia vijana wapatao 4000. Lakini hii ni mara ya kwanza kwa  Airtel kufanya semina hiyo na hapo hapo kuchagua vijana wawili walioweza kuwezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi katika semina hiyo. 

  Huu ni mfumo mpya ambao Airtel Fursa umeuanzisha kwani zaidi ya kuwapa elimu ya mafunzo ya biashara ya ujasiriamali vile vile watawezeshwa kuongezewa nguvu mali na kuimarisha biashara wanazozifanya. Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA itaendelea kutoa warsha hizi katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuhakikisha inafikia vijana wengi zaidi.

  Hivyo tunawahamasisha  vijana wanaposikia nafasi kama hii popote walipo , kuchangamkia kwa kuhudhuria kwani  elimu inayotolewa  ni bure kabisa bila gharama yoyote. "aliongeza Bayumi.

  Nae kwa upande wake  kijana Stephen Gimase, mmoja wa vijana aliyeshinda kwa kuweza    kuelezea na kuwakilisha changamoto anazozipata katika biashara waliyonayo mbele ya jopo la washauri wiki chache zilizopita katika mafunzo hayo, anayejishughulisha na shughuli za kutotoa vifaranga vya kuku,  alisema ,”naishukuru sana Airtel kwa kunipatia vifaa vya kisasa kwa ajili ya biashara yangu. Naahidii  kuwa nitafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha nakuza biashara yangu na kujenga ajira kwa vijana wengine hapa nchini. Hii ni atua ya kwanza ya mafanikio ya maisha yangu nawashukuru Airtel kwa kuwa sehemu ya maisha safari yangu ya mafanikio "alisema Stephen.

  Kijana mwingine aliyeweza kupata bahati ya kuwezeshwa na Airtel FURSA katika mafunzo hayo  ni msanii wa kuchora picha, Theresia Maliatabu ambaye amewezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi kwa ajili ya kuendeleza biashara yake kwa kupatiwa kompyuta na ubao wa kisasa wa kuchorea picha zake . Wakati wa sherehe ya makabidhiano hayo , Theresia aliwashukuru Airtel kwa kuweza kumshika mkono , na kuahidi kwamba ataifanya kazi yake kwa ubora zaidi na kuweza kufikia ndoto yake ya kuwa mchoraji bora na maarufu hapa nchini na hata nje tya nchi.

  Tunaamini kwamba kupitia mpango huu wa mafunzo ya biashara ya ujasiriamali yanayotolewa na Airtel Fursa tunaamini vijana wengi watatoka na kukimbilia mafunzo haya kwani watakuwa wameweza kunufaika na kupata mafunzo haya katika nyanja mbali mbali za kuwawezesha kuanzisha na wengine kuweza kuendeleza biashara zao kwa njia ya ufanisi zaidi.


  0 0

  makongoro
  Makongoro Oging' enzi za uhai wake.
  Makongoro (2)
  Makongoro Oging’ enzi za uhai wake akimkabidhi msaada wa fedha Kundi Luhende (kushoto) katika Hospitali kuu ya magonjwa ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar.

  WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, watayarishaji wa magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi, wamepata pigo kwa kuondokewa na mfanyakazi mwenzao, aliyekuwa Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Makongoro Oging' aliyefariki jana jioni (Jumamosi) Mei 21, 2016 baada ya kuugua kwa muda mfupi. Marehemu alikuwa akiendelea kwa matibabu akiwa nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam ambapo mauti yalimfika.Makongoro (1)
  Makongoro Oging' enzi za uhai wake akiwa na wakili Mabere Nyaucho Marando (kushoto).

  Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana kusubiri taratibu za mazishi na msiba upo nyumbani kwake Tabata- Magengeni jijini Dar es Salaam. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda kijijini kwao Wilaya ya Rorya mkoani Mara kwa ajili ya maziko. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Mungu ailaze roho ya marehemu Makongoro mahali pema peponi-Amina.Makongoro (3)
  Makongoro Oging’ akiongea na baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Ualimu Chang' ombe, jijini Dar es Salaam walikuwa katika mgomo.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na viongozi wengine wakiwa katika chanzo cha maji cha Nsere .
  Chanzo cha Maji cha Nsere ambacho kiwango cha maji kinatajwa kushuka kutoka lita za ujazo Milioni 12 hadi Milioni 9.5.
  Mkuu wa mkoa Saidi Mecky Sadick akitembelea maeneo ya chanzo hicho.
  Mkuu wa Mkoa Said Mecky Sadick na viongozi wengine wakiwa katika chanzo cha maji cha Shiri 

  Mkuu wa Mko wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidick akiwa ameongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) John Ndetico (mwenye tai) alipofanya ziara katika mamlaka hiyo .
  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) John Ndetico akitoa taarifa ya Mamlaka hiyo kwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick alipotembelea ofisi za MUWSA.
  Baadhi ya Viongozi wa Serikali pamoja na Wakuu idara katika Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakisikiliza kwa makini taarifa iliyokuwa ikitolewa.
  Meneja ufundi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi(MUWSA) Mhandisi Patrick Kibasa akitoa maelezo ya chanz hicho kwa Mkuu wa mkoa Said Mecky Sadick na ujumbe wake.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadick na ujumbe wake wakitembelea maeneo mbalimbali ya chanzo hicho.
  Mkuu wa mkoa Said Mecky Sadick akitia saini katika kitabu cha wageni alipotembelea chanzo cha maji cha Shiri.
  Mkuu wa Mko wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick akitembelea kisima cha maji cha Mawenzi.
  Kisima cha Maji cha Mawenzi.
  Tani la Maji lililopo katika eneo la Kisima cha Mawenzi.
  Mkuu wa Mkoa akiwa katika jengo la kuendeshea mitambo ya visima viwili vipya vya mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) vilivyopo eneo la KCMC.
  Ujumbe wa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ukiwa katika moja ya visima vya zamani ambacho kinataraji kufanyiwa ukarabati.
  Meneja Ufundi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) akitoa maelezo katika tanki la maji la Longuo ambalo litatumika kwa ajili ya kuhidhi maji yatakayotumika kwa wakazi wa Kiborironi na vijiji vya Korini na Kikarara.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  . Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga,Miraji Msile akiwaelekeza jambo waratibu wa CHF wakati wa semina ya waratibu wa CHF mkoa mzima wa Tanga ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo.
  MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akisisitiza jambo wakati wa semina ya waratibu wa CHF mkoa mzima wa Tanga ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo.
  Mratibu wa GIZ Mkoa wa Tanga,Apolinary Primus Rutakuburwa ambao wanasapoti huduma za afya na matibabu kulia akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo kushoto ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akifuatilia kwa umakini.
   Maafisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga wakiongozwa na Dr.Sana kulia wakifuatilia semina hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo. 
  Mratibu wa CHF Mkoa wa Tanga,Apolinary Primus Rutakuburwa kulia akisisitiza jambo kwa waratibu wa CHF mkoa wa Tangawakati wa semina iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo. 
  Waratibu wa CHF Mkoa wa Tanga wakinakili maelezo kutoka kwa Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga (NHIF) Ally Mwakababu wakati wa semina iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo waratibu wa mkoa mzima.

  Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkakati wa uboreshaji wa mtandao unaofanywa na kampuni yake. Anayetazama kulia ni Mkuu wa Zantel upande wa Zanzibar, Mohamed Mussa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkakati wa uboreshaji wa mtandao unaofanywa na kampuni yake. Anayetazama kulia ni Mkuu wa Zantel upande wa Zanzibar, Mohamed Mussa, na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel upande wa Zanzibar, Ibrahim Attas.
  Mkuu wa Zantel upande wa Zanzibar, Mohamed Mussa akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkakati wa uboreshaji wa mtandao unaofanywa na kampuni yake. Anayetazama kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin.

  Kampuni ya simu inayoongoza visiwani Zanzibar, Zantel, imewekeza jumla ya dola milioni 10 za kimarekani ili kuimarisha huduma zake za mawasiliano nchini.Mpango huo unajumuisha kubadilisha mfumo mzima wa mawasiliano kwa kubadilisha vifaa vilivyokuwepo na kuweka mitambo mipya kwa madhumuni ya kuimarisha mawasiliano ya simu na kuongeza kasi ya mtandao.

  Akizungumza na waandishi wa habari visiwani humu, Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Bwana Benoit Janin alisema kuimarisha huko katika huduma za simu na mtandao kwa upande wa Zanzibar ndio kilikuwa kipaumbele cha kwanza cha kampuni ya Zantel.‘Kampuni ya Zantel imeanza safari mpya kabisa yenye lengo la kuimarisha na kurudisha nafasi ya mtandao wa Zantel katika ubunifu na kutoa huduma bora visiwani hapa’ alisema bwana Janin.Bwana Janin pia alisema uboreshaji wa huduma za Zantel ni mpango endelevu na katika kipindi kifupi kijacho, Zantel itaendelea kufunga vifaa vipya hali ambayo itawafanya wateja waweze kuwasiliana kwa bei nafuu na bila ya bughudha.

  ‘Maboresho haya yamelenga kuhakikisha tunakuza na kuimarisha teknolojia ya mawasiliano ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za kipekee na kutekeleza ahadi yetu ya kuendelea kuongoza katika kutoa huduma bora kwa wateja wetu’ alisema Bwana Benoit.Janin pia alielezea mpango wa kampuni ya Zantel kuboresha huduma ya EzyPesa kwa kurekebisha mfumo mzima ili uweze kuhimili mawakala wengi na kuongeza huduma za ndani ya mfumo huo. Katika kipindi kifupi pia kampuni ya Zantel pia imefanikiwa kuondoa mtandao wa 2G na kuweka mtandao wa 3G, sambamba na kuzindua rasmi mtandao wa kasi wa intaneti wa 4G mjini Unguja. 

  ‘Nina furaha kubwa jinsi utekelezaji wa mikakati yetu unavyoendelea wa kuboresha huduma zetu ambao utawapa wateja wetu nafasi ya kufurahia huduma zetu na pia kuwapunguzia gharama za mawasliano huku tukukidhi mahitaji ya wateja wetu kwa wakati huu na siku zijazo’ alisema Janin. Bwana Janin pia alisema tayari matatizo ya mawasiliano ya huduma za 3G yameshatatuliwa kwa kutumia mkonga wa fiber katika ya maeneo ya Unguja na Pemba.

  ‘Tumefanikiwa kuyatatua matatizo madogo madogo katika mji mkongwe kwa kuweka vifaa ambavyo vimesaidia sana kuondoa msongamano wa mawasiliano majumbani na katika sehemu za wazi’ alisema Janin. Kampuni ya Zantel ambayo ilizindua huduma ya mtandao wa 4G katika mji wa Unguja mwezi uliopita pia imefanikiwa kufikisha mawasiliano kwa asilimia 80% ya watanzania kutoka asilimia 40% waliyokua wanawafikia awali.

  0 0

  HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA


  KUSHIKILIWA NA KIKOSI KAZI MAALUM CHA KUPAMBANA NA UJANGILI KWA MHIFADHI MWANDAMIZI GENES SHAYO.


  Mhifadhi Mwandamizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Genes Shayo (60) anashikiliwa na Kikosi Kazi Maalum cha kupambana na ujangili nchini kufuatia taarifa za kuhusishwa kwake na upatikanaji wa jino la tembo wilayani Arumeru mkoani Arusha.

  Shirika la Hifadhi za Taifa kupitia taratibu za utendaji kazi lilipokea taarifa za kintelijensia tarehe 14.05.2016 zikimhusisha mwananchi mmoja mkazi wa Ngarenanyuki, Arumeru Emmanuel Nassari (46) ambaye ni Mchungaji wa Kanisa TAG kumiliki jino la tembo na kuwa alihitaji kupata mtu wa kufanya naye biashara. Baaada ya kupata taarifa hizi shirika liliwasiliana na Kikosi Kazi Maalum cha Kitaifa kinachohusika na masuala ya ujangili ili kushirikiana kwa ajili ya ufuatiliaji.

  Kikosi Kazi hiki mara baada ya kupata taarifa hizi kiliendelea na taratibu zake za kiuchunguzi na baada ya ufuatiliaji walifanikiwa kumkamata Emmanuel Nassari tarehe 15.05.2016 akiwa na jino moja la tembo ambapo katika mahojiano yaliyofanyika alimhusisha Mhifadhi Mwandamizi wa TANAPA Genes Shayo kuwa anazo taarifa za yeye kuwa na jino hilo na hivyo kukamatwa tarehe 16.05.2016 kwa ajili ya mahojiano zaidi. 

  Shirika la Hifadhi za Taifa linaendelea kutoa wito kwa raia wema wa nchi hii kuendelea kutoa taarifa za kufichua vitendo vya ujangili na kwamba halitasita kuchukua hatua stahiki kwa yeyote anayehusika na vitendo hivi ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wake watakaobainika kisheria kuhusika na vitendo hivi.

  Imetolewa na Idara ya Mawasiliano

  Hifadhi za Taifa Tanzania

  S.L.P 3134

  ARUSHA

  Simu: +255 027 254 4082

  Baruapepe: dg@tanzaniapaks.go.tz

  Wavuti: www.tanzaniaparks.go.tz

  0 0

  Mkufunzi mkuu wa maswala ya ujasiliamali, Tobias Swai akiwapongeza washindi 50 wa shindano la Ajira Yangu Business Plan Compitition jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la uwezeshaji wa wananchi kiuchumi (NEEC), Bang'i  Issa akizungumza wakati wa kufungua masomo ya vijana walioshinda kurishiriki shindano la Ajira yangu Business plan Competition jjini Dar es Salaam leo.


  Mwakirishi  kutoka shirika la kazi (ILO), Geras Shirove akizungumza na washindi wa shindano la Ajira yangu jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya washiriki wa shindano la Ajira yangu waliohudhulia katika shindano hilo wakiwa kwenye mkutano leo jijini Dar es Salaam.

  Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
  WASHIRIKI wa shindano la kibiashara  la Ajira yangu Business  plan Competition  wameaswa kutumia  vyema fursa waliyoipata ya kupata mafunzo kwani yanaweza kubadili mitazamo yao ya kimaisha hususani katika masuala ya kujiajiri badala ya kuwa na fikra za kuajiliwa. 

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la uwezeshaji wa wananchi kiuchumi (NEEC), Bang'i Issa wakati akizungumza na washirikibwa shindano la Ajira yangu Business plan Competition jiji Daf es Salaam leo. Amesema kuwa watumie fursa hiyo kwani wao ni washindi wa awamu ya kwanza na kuwa kwenye 50 bora kati ya 831. Ni ushindi mmojawapo. 

  Bang'i amesema kuwa wazingatie mafunzo watakayoyapata ili wachaguliwe kwe 20 bora na 10 bora.
   Pia amewaasa washiriki wa shindando hilo  kuwatumia vizuri wakufunzi pamoja na mkufunzi mkufunzi mkuu vizuri ili baadae wafanye  umakini vizuri katika kuboresha màandiko yao na kuyawasilisha kwaajili ya mchunjo.


   Nae  mwakilishi  kutoka ILO, Geras Shirove amesema kuwa  amewapongeza washiriki 50 wa kiendelea kushindania shindano hilo kwani washiriki wa shindano hilo walikua 831.

  0 0

  MWENYEKITI wa Mtaa wa Bulale wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Alphonce  Nyinzi  (48) ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika wakati akielekea nyumbani kwake.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Ahmed Msangi amesema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 22 mwaka  huu majira ya  saa 2 usiku.

  Msangi amesema kuwa marehemu aliekuwa akifahamika  kwa jina maarufu "msukuma" mfanyabiashara na mkazi wa bulale aliuawa kwa kupigwa risasi kifuani na kutokea chini ya kwapa upande wa kulia na watu wawili wasio fahamika pamoja na risasi hiyo kumjeruhi  Neema Marangula (23) Mkazi wa Bulale katika Kiganja cha mkono wa kulia.

   Amesema kuwa wakati Mwenyekiti huyo akitoka  kwenye kikao alichofanya na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mtaa wa Bulale akiongozana na wajumbe wawili alikutana na Neema Marangula akiwa na mume wake ambao walikua wanawafuata marehemu na Balozi kwa ajili ya kuzungumzia mzozo wa ndani ya ndoa yao kwa hiyo walikua wanahitaji kusuluhishwa.

  Mwenyekiti  huyo (marehemu) na wajumbe wake wawili wakiwa pamoja na Neema pamoja na mumewe wakiwa wanajadili tatizo hilo hapo barabarani mara ghafla wakatokea watu wawili ambao walikua wakipita barabarani na kuwaambia mko chini ya ulinzi na mmoja wao akatoa bunduki na kumpiga risasi mwenyekiti huyo  ambaye alianguka chini huku wenzake wakikimbia kujiokoa kutoka eneo hilo lakini pia wale wahalifu  wakakimbia na kutokomea gizani vichakani.

  Amesema wananchi wa eneo hilo  ambapo mwenyekiti aliuawa walijitokeza kwa msaada wa kumsaidia walimchukua na kumkimbiza hospitali kwa matibabu lakini alifariki dunia wakiwa njiani. majeruhi Neema Marangula amelazwa Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure kwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

  Mwili wa marehemu  umehifadhiwa katika  Hospitali Mkoa wa Mwanza Sekou Toure kwa ajili ya uchunguzi wa daktari, chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika pamoja na  uchunguzi tukio hilo bado unaendelea.

  Msangi  amewaomba  wananchi wenye taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo zitakazo saidia kufanikisha kukamata wahusika wazitoe  polisi lakini pia kutoa ushirikiano kwa viongozi wao na kuhakikisha wanatengeneza makazi salama huko wanapoishi na maeneo ya shughuli zao na  msako mkali unafanyika na kuhakikisha wahusika wa tukio hilo wanakamatwa.

  0 0

  Na Fatma Salum- MAELEZO, Dodoma.

  Serikali kupitia jeshi la Magereza imesaini Mkataba na Kampuni ya Poly Technologies ya China kujenga nyumba 9,500 kwenye vituo vyote vya Magereza nchini.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Yusuf Masauni wakati akijibu swali kuhusu kuboresha makazi ya askari lililoulizwa na Mhe. Devota Minja (Mb) leo bungeni mjini Dodoma. 

  Mhe. Masauni alibainisha kuwa  kupitia mkataba huo Serikali itapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto iliyopo ya uhaba wa nyumba kwa ajili ya askari wa jeshi hilo ambapo mahitaji kwa sasa ni nyumba 14,500 wakati zilizopo ni nyumba 4,221 hivyo kupelekea upungufu wa nyumba 10,279. 

  “Serikali inafahamu kuwa lipo tatizo la baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza na Polisi kuishi katika nyumba chakavu zisizokuwa na hadhi, hivyo katika kukabiliana na tatizo hili Serikali imeendelea kuzifanyia ukarabati mkubwa baadhi ya nyumba na pia kujenga nyumba mpya”. Alisema Masauni.

  Mhe. Masauni alifafanua  kuwa mgawanyo wa ujenzi wa nyumba hizo mpya ni Makao Makuu ya Magereza nyumba 472, Arusha nyumba 377, Dar es Salaam nyumba 952, Dodoma 356, Kagera 364, Kigoma 272, Kilimanjaro 390, Lindi 233, Manyara 206, Mara 378, Mbeya 622, Iringa 336, Morogoro 669, Mtwara 215, Mwanza 398, Pwani 384, Rukwa 358, Ruvuma 320, Shinyanga 337, Singida 299, Tabora 408, Tanga 382, KMKGM Dar es Salaam 219, Chuo cha Ukonga 115, Chuo cha Kiwira 183, Chuo cha Ruanda 62, Chuo KPF 27, Bohari Kuu 82 na Bwawani nyumba 84. 

  Aidha, Mhe. Masauni aliongeza kuwa kwa upande wa Jeshi la Polisi, Serikali inakusudia kujenga nyumba 4,136 katika mikoa 17 ya Tanzania Bara na Zanzibar zitakazosaidia kupunguza tatizo la makazi kwa askari wa jeshi hilo. 

  Mhe. Masauni alilieleza bunge kuwa Serikali itaendelea kutatua changamoto ya uhaba wa nyumba kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo mikopo yenye riba nafuu, Miradi Shirikishi (PPP) na kwa kutumia fedha za bajeti ya Serikali kadri hali ya uchumi itakavyokuwa inaimarika.

older | 1 | .... | 854 | 855 | (Page 856) | 857 | 858 | .... | 1896 | newer