Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live

YANGA YALAANI VITENDO VYA UVUNJIVU WA AMANI NCHINI ANGOLA.

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
UONGOZI wa Yanga umelaani vikali vitendo vya uvunjivu wa amani vilivyotokea katika mchezo wao dhidi ya GD Sagrada Esperanca vilivyofanywa na mwamuzi wa mechi hiyo na vyombo vya usalama.

Katika mchezo huo Yanga wamefanyiwa vurugu ikiwemo na golikipa wa timu hiyo Deogratius Munish 'dida' kupigwa na mawe na Polisi kuingia uwanjani mara kwa mara.

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amesema kuwa Mwamuzi wa mchezo amefanya vitendo vingi ambavyo havipo katika sheria 17 za soka.

"Mwamuzi amefanya vitendo vingi vya uvunjivu wa sheria za mpira wa miguu ikiwemo kuwatoa wachezaji mchezoni kwa kuwapatia kadi huku upande mwingine wakiwa wanafanya makosa pasi kupatiwa onyo lolote,"amesema Muro. Kwa sasa uongozi umeamua kuandika barua kwa shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) kuomba kuondolewa kwa mwamuzi huyo ikiwemo kufungiwa au kutokuchezesha  mechi zao.

Muro amesema kikosi kipo nchini Afrika kusini kikisubiri ndege ya kesho saa 4asubuhi na kuingia mchana ambapo wataingia kambini moja kwa moja kwa ajili ya safari kuelekea Songea kumalizia mchezo wao dhidi ya Majimaji utakaopigwa Jumapili.

WATU WATATU WAUWAWA NA MMOJA KUJERUHIWA JIJINI MWANZA.

$
0
0
                       JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
 JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA.
WATU WATATU WAMEUAWA KWA KUKATWA MAPANGA NA MASHOKA NA MWINGINE MMOJA KUJERUHIWA KICHWANI WAKATI WAKIFANYA IBADA KATIKA MSIKITI WA MASJID RAHMANI ULIOPO ENEO LA IBANDA RELINI  WILAYANI NYAMAGANA.

MNAMO TAREHE 18.05.2016 MAJIRA YA SAA 20:30HRS KATIKA MSIKITI WA MASJID RAHMAN ULIOPO IBANDA RELINI MTAA WA UTEMINI @ MAPANKINI KATA YA MKOLANI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA. WATU WASIOZIDI 15 WAKIWA WAMEVALIA MAVAZI YA KUFICHA USO WAKIWA NA MAPANGA, SHOKA NA BENDERA NYEUSI YENYE MAANDISHI MEUPE WALIINGIA GHAFLA KATIKA MSIKITI TAJWA HAPO JUU WAKATI WAUMINI WA MSIKITI HUO WAKIWA WANASWALI NA KUZIMA TAA NA KUTOA SAUTI WAKISEMA “KWA NINI MNASWALI WAKATI WENZETU WAMEKAMATWA NA WANASHIKILIWA NA POLISI ?” NA HAPO HAPO WAKAANZA KUWAKATA KWA MAPANGA BAADHI YA WAUMINI KATIKA SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO. WALIPATA MAJERAHA MAKUBWA KICHWANI, SHINGONI NA MIKONONI NA WALIPOTEZA MAISHA YAO PAPO HAPO NA MMOJA KUPATA MAJERAHA SEHEMU ZA KICHWANI NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA WILAYA YA NYAMAGANA (BUTIMBA). 
WALIOUAWA, 1. FERUZ ISMAIL ELIAS  MIKA 27, MUHA IMAMU WA MSIKITI HUO NA MKAZI WA IBANDA RELINI, 2. MBWANA RAJAB MIAKA 40, MBONDEI MFANYABIASHARA NA MKAZI WA IBANDA, 3. KHAMISI MPONDA MIAKA 28 DEREVA WA KIWANDA CHA SAMAKI (TFP), MKAZI WA MKOLANI, WOTE WALIJERUHIWA SEHEMU ZA KICHWANI, SHINGONI NA MIKONONI. ALIYEJERUHIWA NI ISMAIL ABEID @ GHATI MIAKA 13, MKURYA MWANAFUNZI WA MADRASA KATIKA  SHULE YA KIISLAMU ITWAYO JABAR HILA ILIYOKO MAENEO YA NYASAKA ALIYEPATA MAJERAHA KICHWANI NA ANAPATA MATIBABU HOSPITALI YA NYAMAGANA.
KUTOKANA NA HALI HIYO, WAUMINI WENGINE WALIFANIKIWA KUKIMBIA HUKU WAKIPIGA MAYOWE YALIYOPELEKEA WAHALIFU HAO KUKIMBIA NA KURUSHA NDANI YA MSIKITI CHUPA MBILI ZA KONYAGI ZILIZOKUWA NA PETROLI NA TAMBI ZA MOTO, CHUPA MOJA ILILIPUKA LAKINI HAIKULETA MADHARA MAKUBWA.
JESHILA LA POLISI  LIMEWAKAMATA WASHUKIWA WATATU KWA AJILI YA KUWAHOJI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, HUKU MSAKO MKALI WA KUWASAKA WATU WENGINE WALIO HUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KWENYE MAUAJI HAYO UKIWA BADO UNAENDELEA. NAPENDA KUWAELEZA  WANANCHI WATULIE WAKATI TUKIENDELEA NA UPELELEZI WA TUKIO HILI, NA NATOA WITO KWA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA ZA WAHALIFU WA MAUAJI HAYO ILI TUWEZE KUWAKAMATA. PIA NASHAURI NA KUSISITIZA KUWEPO NA KAMATI ZA ULINZI NA USALAMA KATIKA NYUMBA ZA IBADA, KUMBI ZA STAREHE PAMOJA NA MITAA YAO. HII ITASAIDIA KWA KIASI KIKUBWA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA KATIKA MAENEO HAYO.

IMESAINIWA NA:
……………………….
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

UTT-PID yaiwezesha Manispaa ya Lindi kuvuna Bilioni 2 katika mradi wa viwanja

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya UTT-PID, Bi. Elpina Mlaki akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Godfrey Zambi wakati wa mkutano huo ambao jumla ya Bilioni 2, za mradi wa viwanja kwa Manispaa ya Lindi ziliweza kupatikana katika mradi wa upimaji viwanja.Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (katikati) akizungumza na wajumbe wa mkutano huo uliojumuisha uongozi wa Mkoa wa Lindi pamoja na Bodi ya UTT-PID ikiambatana na Menejimenti yake.Mwenyekiti wa Bodi ya UTT-PID, Bi. Elpina Mlaki akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Godfrey Zambi wakati wa mkutano huo ambao jumla ya Bilioni 2, za mradi wa viwanja kwa Manispaa ya Lindi ziliweza kupatikana katika mradi wa upimaji viwanja.

LINDI: Manispaa ya Lindi imepata Gawio la Zaidi ya Sh 1.9 Bilioni kutokana na uwekezaji wa pamoja na Upimaji wa viwanja kwa kushirikiana na taasisi ya Uwekezaji Tanzania (UTT-PID).

Akielezza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ya Lindi, Bw. Jomaary Satura wakati wa kikao cha kuangalia mafanikio kilichofanyika jana, ambapo alibainisha kuwa, fedha hizo ni mafanikio ya upimaji wa viwanja 2,500 kati ya 10,000 walivyokusudia kupima awamu ya kwanza.

“Fedha hizi zimetumika kujenga miradi mbalimbali kwenye Manispaa yetu. Ikiwemo kujenga Maabara na vifaa vyake, Ujenzi wa Zahanati, Nyumba ya Mganga na Boti ya kisasa.” Alieleza Mkurugenzi huyo.

Aidha aliongeza kuwa, mapato ya ndani ya ndani kwa sasa yameongezeka kwa kupanda kutoka Sh 700 Milioni mwaka 2013 hadi Sh 2.4 Bilioni.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya UTT-PID, Bi. Janet Mmari amesema mradi huo umegharimu Sh.1.9 Bilioni hivyo umeonyesha mafaniko kwa jamii.“Mradi huu ulikuwa ni wa gawio la asilimia 50 kwa 50. 
 
Tunawapongeza Manispaa kwa kufanya kazi vizuri” alisema Bi. Janet Mmari.Naye Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alisema kuwa, awamu ya pili watashirikisha makundi yote ikiwemo wanasiasa ilikuondoa mivutano inayosababisha kuchelewa kwa maendeleo.

“Maendeleo yanapatikana mawazo yanapogangana. Nyingine ni changamoto za kawaida na uelewa, Wanasiasa kuingilia kunatokana na masilahi binafsi” alieleza Mkuu wa Mkoa huyo.

SARUJI YA WAASHI TEMBO FUNDI YAZINDULIWA LEO.

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Ilse Boshoff na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa kapuni hiyo Allan Chonjo (kulia) wakizindua chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Fundi” ambayo ni mahususi kwa ajili ya uashi leo kwenye kiwanda cha Saruji cha Tembo Cement jijini Mbeya (Picha: Mpiga Picha Wetu).
Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan Chonjo (kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Ilse Boshoff (katikati) na Emily Sindato (kulia), Mkuu wa Ufundi wa kiwanda hicho wakizindua chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Fundi” ambayo ni mahususi kwa ajili ya uashi leo kwenye kiwanda cha Saruji cha Tembo Cement jijini Mbeya.
  (Picha: Mpiga Picha Wetu)

Kampuni ya Saruji Lafarge Tanzania imezindua saruji ya kwanza maalumu kwa matumizi ya uashi. Saruji hii inayojulikana kama Tembo Fundi itawapa wajenzi chaguo bora kwa ajili ya kazi za uashi ikiwa ni pamoja na kupiga plasta ukuta, kusakafia, kujengea tofali na kupangilia marumaru. Saruji hiyo iliyotengenezwa maalum kwa kazi ya uashi wa kuta za nje na ndani ina ubora katika kufanya kazi, nguvu kwenye ugundishaji inashika vizuri na ina umaliziaji bora wenye kuleta matokeo yaliyo bora zaidi kwenye kujenga tofali, uzio, marumaru na sakafu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Ilse Boshoff, alisema wakati wa uzinduzi leo kwamba Tembo Fundi imeundwa mahususi kwa ajili ya kazi za uashi na kuwapa wajenzi utendaji bora wa kazi na thamani ya fedha.
“Ikiwa imetengenezwa kutokana na uzoefu na utaalamu wa Lafarge kimataifa katika kuzalisha saruji, Tembo Fundi ni rahisi kutumia katika kupiga plasta, tofauti na saruji ya matumizi ya jumla ambayo itamchukua muashi muda mrefu katika kusawazisha ukuta.

Alisema faida nyingine muhimu katika matumizi ya Tembo Fundi ni unafuu katika gharama kutokana na mfuko mmoja wa Tembo Fundi kutumika eneo pana zaidi ukilinganisha na mfuko wa saruji ya matumizi ya jumla. Kutokana ya kwamba inafanya kazi vizuri na uimara wake kudumu kwa muda mrefu Tembo Fundi itawasaidia wajenzi kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge, Allan Chonjo alisema daima Lafarge imekuwa ikiwasikiliza wateja wake. Tembo Fundi ndio suluhisho la mahitaji ya saruji yenye ubora kwani inatumia maji kidogo, inadumu, haipati nyufa na ina uwezo wa kujenga eneo pana zaidi na kuufanya ukuta wako ung’ae zaidi.

“Tembo Fundi inapatikana katika ujazo wa kilogramu 50 na ni ubunifu wetu katika kurahisisha kazi za uashi. Lafarge imewekeza sana katika utafiti uliopelekea uvumbuzi wa saruji kama hii ambayo inapendwa na wajenzi katika masoko mbalimbali kimataifa. Hii ni moja ya dhima zetu za kuhakikisha tunawapa wajenzi sulhisho maalumu katika kazi zao. Tembo Fundi itasambazwa katika maduka yetu yote ya jumla na rejareja pamoja na kwenye kontena zetu za usambazaji.

Hivi sasa kwenye soko la saruji hakuna saruji iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya uashi jambo ambalo linawalazimisha watumiaji kutumia saruji ya matumizi ya jumla kwa ajili ya kazi za uashi na kupelekea ongezeko la gharama za ujenzi na kukosa matokeo mazuri katika ujenzi.

BENO AIPANIA TIMU TAIFA.

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
GOLIKIPA wa timu ya Prisons, Beno Kakolanya amefurahi kuweza kuitwa katika kikosi cha timu ya Taifa na amesema atahakikisha Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Charles Boniface Mkwasa hajutii maamuzi yake ya kumuita ndani ya kikosi chake. 

Hii ni mara ya kwanza kwa golikipa huyo wa kutumainiwa ndani ya kikosi cha Prisons kuitwa ndani ya kikosi cha timu ya Taifa lakini Msimu uliopita Beno hakupata nafasi ndani ya kikosi chake huku akifanikiwa kudaka mechi tatu na toka alipoanza kucheza mpira malengo yake makubwa yalikuwa ni kujituma ili siku moja ndoto zake zije kutimia.

Amesema, kwa sasa amepata nafasi hiyo atahakikisha anaitumia vema hasa katika maandalizi ili kupata nafasi ya kudaka katika mechi mbili zilizo mbele yao. "Nitahakikisha Mwalimu Mkwasa hajutii maamuzi yake ya kunijumuisha ndani ya kikosi chake na nitajitahi kufanya vizuri katika mandalizi ya michezo yetu miwili ule wa kirafiki dhidi ya Harambee Stars ya Kenya pamoja na ule wa AFCON dhidi ya Misri", amesema Beno. 

Beno ameanza kupata nafasi ndani ya Prisons msimu wa Ligi wa 2013/14 baada ya aliyekuwa golikipa namba moja wa timu hiyo kuvunjika kidole huku golikipa namba mbili akipumzishwa baada ya kufungwa mechi mbili mfululizo. Msimu wa Ligi wa 2014/15 golikipa huyo alicheza mechi tatu huku msimu huu akizikosa mechi takribani 10 za awali kutokana na maumivu ya bega yaliyomuweka nje kwa miezi miwili.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA DKT.ASHA ROSE MIGIRO OFISINI KWAKE LEO.

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika Picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dkt Asha Rose Migiro leo Ikulu Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dkt. Asha Rose Migiro kabla ya Mazungumzo yao Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mazungumzo na Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dkt. Asha_Rose Migiro alipotembelea Ofisini kwake leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

MeTL Group yatoa msaada wa Mil. 30.7 kwa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili

$
0
0
Mkuu wa Shule ya Tiba katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS), Prof. Slyvia Kaaya (wa nne kulia) akizungumza machache kabla ya kukabidhiwa rasmi viti 200 na uongozi wa kampuni ya MeTL. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni ya MeTL, Murtaza Dewji.

Kwa kutambua umuhimu wa elimu, kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) imetoa msaada wa Milioni 30.7 kwa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) ili kusaidia ununuzi wa viti 200 ambavyo vitatumiwa na wanafunzi wa udaktari wa watoto.

Akizungumza na Modewjiblog kuhusu msaada huo, Mkuu wa Shule ya Tiba katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS), Prof. Slyvia Kaaya, amesema kabla ya kupata msaada huo walikuwa wakitumia chumba kidogo ambacho kilikuwa hakiwatoshi wanafunzi wanaosomea udaktari wa watoto hivyo msaada huo umekuwa muhimu kwao ili kupunguza changamoto ambazo zinawakabili.

“Msaada huu utatusaidia sana na hata sasa hivi tuna matarajio tutakuwa na matokeo mazuri kwa kuongezeka kwa watahiniwa, wanafunzi kuhudhuria vipindi na hata kwa walimu uadilifu wa kufundisha utaongezeka,” alisema Prof. Kaaya.

Aidha Prof. Kaaya alisema pamoja na msaada huo lakini bado wanachangamoto ambazo zinawakabili ambazo zinahitaji kutafutiwa ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kufunga viyoyozi na kuweka mitambo ya kuzuia mwangwi ili kuwawezesha wanafunzi kusoma bila kuwa na matatizo.

Nae Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer alisema kampuni yao imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kwa jamii ili kusaidiana na serikali kumaliza baadhi ya changamoto zilizopo na wamejipanga kuendelea kuwa wakitoa misaada kwa wahitaji.

“Tunaamini elimu ni muhimu kwa maendeleo ya baadae tunatoa msaada ili wasome na wawasaidie wengine kupitia elimu wanayoipata chuoni,” alisema Fatema Dewji-Jaffer.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni ya MeTL, Murtaza Dewji (kushoto) akitoa salamu za kampuni ya MeTL kabla ya kukabidhi viti 200 kwa uongozi wa MUHAS. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji-Jaffer.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), Fatema Dewji -Jaffer (wa tatu kulia) akimkabidhi moja kati ya viti 200 Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS), Prof. Aporinal Kamuhangwa (wa pili kushoto) vilivyotolewa na kampuni ya MeTL Group. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Tiba katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS), Prof. Slyvia Kaaya. Wengine wanaoshuhudia tukio hilo kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni ya MeTL Group, Murtaza Dewji na Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez (kulia). Mstari wa nyumba ni watumishi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba (MUHAS).
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano yaliyofanyika katika jengo la Watoto lililopo Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS), Prof. Aporinal Kamuhangwa akitoa shukrani kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni ya MeTL Group, Murtaza Dewji baada ya kukabidhiwa viti hivyo.
Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez (kulia) akizungumza neno baada ya hafla fupi ya kukabidhi viti hivyo.
Uongozi wa MeTL na MUHAS wakiwa wamekaa kwenye viti hivyo.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), Fatema Dewji -Jaffer (katikati) akifurahi jambo na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni ya MeTL Group, Murtaza Dewji. Kushoto ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS), Karim Manji.
Viti 200 vya MUHAS vilivyotolewa na Kampuni MeTL.

WALIMBWENDE MISS ARUSHA WAJINOA VIKALI,WAAHIDI KULITETE TAJI LA MISS TANZANIA 2016

$
0
0
 .
Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la kumsaka mlibwende wa mkoa wa Arusha wakiwa katika pozi
warembo hao wakiwa wanacheza hii ikiwa ni moja ya mazoezi yao wanayoyafanya ndani ya ukumbi wa hoteli Naura Spring Arusha ambapo wameweka kambi
 Na Woinde Shizza,Arusha.
 
Kusimamishwa kwa shindano la umrembo Tanzania (Miss Tanzania ) kwa mwaka mmoja imekuwa ni changamoto kubwa kwa waandaaji wa shindano hilo, kwani warembo wengi wamesahau mambo kibao ndani ya mashindano hayo pia kueleza kuwa shindano hilo limepoteza umaarufu wake.

Hayo yamebainishwa na muaandaaji wa shindano la kumsaka mrembo wa mkoa wa Arusha kutoka katika kampuni ya Tour Visual Entertainment, Penda Simwita wakati akiongea na mwaandishi wa habari jana katika kambi ya kumuandaa Miss Arusha.

Alisema kuwa kwa upande wake shindano hilo limekuwa gumu kidogo, kwani warembo wengi walibweteka na kujisahau kuwa kuna shindano kama hili kwa mwaka huu, hivyo ilimlazimu kutembelea katika vyuo mbalimbali vya hapa mkoani Arusha kwa ajili ya kuwasaka warembo watakaoshiriki shindano hili.

"Pamoja na kuwatafuta,tumefaniwa kuwapata warembo wazuri wenye sifa na naamini wataweza kutetea taji la Miss Tanzania,kwani wana uwezo na kizuri zaidi najiamini naweza kuwaandaa maana hata mrembo ambaye anashikilia taji sasa hivi alitoka mkoa wa Arusha" alisema Mwandaaji huyo.

Mmoja wa warembo wanaoshiriki shindano hilo ,Maurine Ayubu alieleza hisia zake za kufurahi kushiriki shindano hilo,alisema kuwa ana uwezo wa kufanya vizuri,na kwamba ana uhakika wa kufanya vyema kwa sababu sifa zote za kuwa mrembo wa Mkoa wa Arusha anazo na kwamba anaamini atatetea taji la Miss Tanzania libaki Arusha kama linavyoshikiliwa kwa sasa na mrembo wa Tanzania Lilian kamazima

Jumla ya warembo 17 kutoka katika mitaa mbalimbali na wilaya mkoani hapa wanatarajiwa kupanda jukwaani mapema May 28 mwaka huu katika ukumbi wa Hotel ya Naura Spring kwa ajili ya kumsaka mlibwende wa mkoa wa Arusha ambaye atawakilisha mkoa katika kinyang'anyiro cha kumsaka mrembo wa Tanzania na tukumbuke mpaka hivi sasa taji hilo la mrembo wa Tanzania linashikiliwa na mrembo kutoka mkoa wa Arusha Lilian Kamazima

WAKONGWE WA TASNIA YA HABARI WAKUTANA NA KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI,UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (kushoto) akisikiliza kwa makini historia ya sekta ya habari nchini kutoka kwa mwandishi mkongwe mzee Charles Simpungwe (kulia) leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mtendaji wa Mfuko wa Hugo Van Lawick ambaye pia ni mstaafu wa Idara ya Habari -Maelezo, Willie Mbunga.Mfuko wa huo unajihusisha na utoaji wa Tuzo kwa wapiga Picha mahiri.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (kushoto) akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu sekta ya habari kutoka kwa Mratibu wa Mfuko wa Hugo Van Lawick Van Lawick Ali Chimbyangu ambaye pia ni mwandishi mkongwe aliye fanya kazi katika vyombo yva RTD, Daily News na African Juornal, Charles Simpungwe (wapili kulia) wakati wa kikao baina yake na wahabari hao leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni  Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari George Msonde, mwandishi mkongwe Charles Simpungwe na Katibu Mtendaji wa Mfuko wa Hugo Van Lawick ambaye pia ni mstaafu wa Idara ya Habari -Maelezo, Willie Mbunga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akielezea jambo wakati wa kikao baina yake na wahabari wakongwe kilichoofanyika katika ukumbi wa wizara leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mratibu wa Mfuko wa Hugo Van Lawick Ali Chimbyangu ambaye pia ni mwandishi mkongwe aliye fanya kazi katika vyombo yva RTD, Daily News na African Juornal, Charles Simpungwe na Katibu Mtendaji wa Mfuko wa Hugo Van Lawick ambaye pia ni mstaafu wa Idara ya Habari -Maelezo, Willie Mbunga.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (kushoto) akisikiliza kwa makini historia kuhusu sekta ya habari nchini kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Mfuko wa Hugo Van Lawick ambaye pia ni mstaafu wa Idara ya Habari -Maelezo, Willie Mbunga (katikati) wakati wa kikao baina yake na wahabari hao leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni  mwandishi mkongwe Charles Simpungwe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (wapili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari wakongwe mara baada ya kikao baina yao leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mratibu wa Mfuko wa Hugo Van Lawick Ali Chimbyangu ambaye pia ni mwandishi mkongwe aliye fanya kazi katika vyombo yva RTD, Daily News na African Juornal, , Katibu Mtendaji wa Mfuko wa Hugo Van Lawick ambaye pia ni mstaafu wa Idara ya Habari -Maelezo, Willie Mbunga na mwisho kushoto ni Charles Simpungwe
Picha na Frank Shija; WHUSM.

VIWANDA VIPYA KUJENGWA ILI KUKABILIANA UPUNGUFU WA SUKARI.

$
0
0
Na Tiganya Vincent, Dodoma.

Serikali inaendelea na mazungumzo na wawekezaji wanaokusudia kuwekeza katika viwanda vya sukari ili kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa bidhaa hiyo nchiniKauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati akijibu maswali ya papo kwa papo ya kila Alhamis.

Alisema kuwa lengo la mazungumzo ya kutaka viwanda viweze kuongeza uzalishaji wa sukari ili uweze kufikia tani 420,000 katika kipindi miaka minne ijayo na hivyo kupunguza uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.Mhe. Majaliwa alisema kuwa maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vipya ya Sukari ni pamoja na Kigoma, Morogoro na Bonde la Rubada lilipo katika mto Rufiji.

Kuhusu kutojengwa kiwanda cha Sukari katika eneo la Bagamoyo , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali ilikataa kuruhusu ujenzi wa kiwanda cha Sukari katika eneo hilo baada ya Kamati ya Bunge kushauri kuwa kisijengwe kwa sababu kingehatarisha uhai wa wanyama waliomo katika Mbuga ya Saadan kwa kuwa kingetumia maji mengi kutoka Mto Wami.

Mhe. Majaliwa alisema kuwa hali hiyo ingesababisha upungufu wa maji ambayo ni tegemeo kwa wanyama wa Mbuga ya Saadan yambao ni muhimu kwa sekta ya utalii nchini.Kwa upande wa upungufu wa sukari nchini , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali imeagiza tani 70,000 kutoka nje ya nchi.

Alisema kuwa mahitaji ya sukari ni tani 420,000 lakini zilizopo ni tani 320,000 na kuwepo kwa upungufu wa tani 100,000.Mhe. Majaliwa alisema kuwa Bodi ya Sukari nchini ili kukabiliana upungufu huo imeweka utaratibu wa uagizaji huo ili kuhakikisha Waagizaji wa Sukari nje wasije wakaingiza sukari nyingi kinyume cha inayohitajika na hivyo kuathiri viwanda vya hapa nchini.

Aliongeza kuwa Bodi hiyo kwa kushirikiana Mamlaka ya Mapato nchini (TRA ) itasimamia kuhakikisha kuwa sukari inayoingiza nchini ndio inayohitajika.Kuhusu bei elekezi ya sukari , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali inaweka kiwango ili kumlinda mwananchi wa kawaida.

Kwa upande wa upungufu wa sukari nchini, Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali imeagiza tani 70,000 kutoka nje ya nchi.Alisema kuwa mahitaji ya sukari ni tani 420,000 lakini zilizopo ni tani 320,000 na kuwepo kwa upungufu wa tani 100,000.

Mhe. Majaliwa alisema kuwa Bodi ya Sukari nchini ili kukabiliana upungufu huo imeweka utaratibu wa uagizaji huo ili kuhakikisha Waagizaji wa Sukari nje wasije wakaingiza sukari nyingi kinyume cha inayohitajika na hivyo kuathiri viwanda vya hapa nchini.Aliongeza kuwa Bodi hiyo kwa kushirikiana Mamlaka ya Mapato nchini (TRA ) itasimamia kuhakikisha kuwa sukari inayoingiza nchini ndio inayohitajika.

Kuhusu bei elekezi ya sukari , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali inaweka kiwango ili kumlinda mwananchi wa kawaida.Alisema kuwa bei hiyo zinazingatia gharama zote ikiwemo usafirishaji kuto ka zinapoagizwa na kumfikia mlaji.

DK. PINDI CHANA AKUTANA NA MAOFISA KATIKA IDARA YAKE CCM LEO

$
0
0
Kaimu Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Pindi Chana akizungumza wa maofisa katika idara hiyo, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Pindi Chana akizungumza wa maofisa katika idara hiyo, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Pindi Chana akizungumza wa maofisa katika idara hiyo, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Pindi Chana akiwa katika picha ya pamoja na maofisa katika idara hiyo, baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam. Walioketi, kushoto ni Salehe Mhando na kulia ni Amos Siayantemi na waliosimama kutoka kushoto ni Lightness Shauri Habib Twahir, Margaret Mtui na Rajab Fondogoro. 
Kaimu Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Pindi Chana akifurahia jambo na Ofisa katika Idara hiyo, Amos Siyantemi, baada ya kuzungumza wa maofisa katika idara hiyo, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO 

Mkapa kuongoza timu ya usuluhishi wa mgogoro wa Burundi

$
0
0
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO 19 Mei, 2016
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Benjamin Mkapa, ameteuliwa kuongoza mazungumzo kuhusu mgogoro wa Burundi ikiwa ni jitihada za viongozi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika kuleta  amani ya kudumu nchini humo.
Mheshimiwa Mkapa, aliyeteuliwa na Mkutano wa 17 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki atakuwa kiongozi wa timu ya usuluhishi wa mgogoro wa Burundi katika kikao kitakachofanyika kuanzia mei 21 hadi 24 mwaka huu, katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa ulipo jijini Arusha (AICC), ambapo inatazamiwa wadau wa pande zote za mgogoro watashiriki.
Aidha, Mkutano huo wa 17 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ulifafanua  kuwa Rais wa Uganda, Mheshimiwa Yoweri Museveni, ataendelea kuwa msuluhishi wa kudumu kutoka jumuiya hiyo.

Serikali ya Burundi ilikubali kufanyika usuluhishi na iko tayari kushiriki katika mazungumzo ya amani yanayofanywa na viongozi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki yakihusisha wadau wote wa siasa nchini Burundi ikiwa ni jitihada za kuumaliza mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo.

DOLA ZA KIMAREKANI BILIONI 3 KUTUMIKA KUANZISHA MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA.

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (kushoto) akiongea na Waandishi wa Habari (hawako pichani) kuhusu kuanza kwa mradi wa Mgodi wa kuchimba chuma na makaa ya mawe Liganga na Mchuchuma leo mjini Dodoma 19 Mei, 2016. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayosimamia viwanda, biashara na uwekezaji, Mhe. Dkt. Dalaly Kafumu pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji toka Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Bwana Mlingi Mkucha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayosimamia viwanda, biashara na uwekezaji, Mhe. Dkt. Dalaly Kafumu (kulia) akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawako pichani) kuhusu kuanza kwa mradi wa Mgodi wa kuchimba chuma na makaa ya mawe Liganga na Mchuchuma leo mjini Dodoma 19 Mei, 2016. Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia taarifa toka kwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage leo mjini Dodoma. (Picha zote na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma)

Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.

JUMLA ya dola Bilioni 3 za Kimarekani zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa Mgodi wa Makaa ya Mawe na Chuma wa Liganga na Mchuchuma.Kauli hiyo imetolewa Leo mini Dodoma na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage wakati akiongea na Waandishi wa habari mini Dodoma.

Amesema mradi huo unaojengwa kwa ubia kati ya Tanzania Kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Kampuni ya China ya Sichuan Hongda Group unatarajia kuanza mwaka huu.Mhe. Mwijage amesema kuwa fedha za kuwalipa fidia wananchi wanaozunguka maeneo ya mradi huo ziko tayari ambapo zinatarajiwa kutumika zaidi ya bilioni 13 kwa ajili ya fidia na makazi.

Alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutasadia kuzalisha umeme Megawati 600 ambapo 250 zitatumika katika Kiwanda cha Chuma na nyingine 350 zitapelekwa kwenye Gridi ya Taifa kwa ajili ya kuongeza nguvu katika nishati ya umeme.

‘’Pamoja na kuchimba chuma, Mradi wa Mchuchuma na Liganga utahusisha ujenzi wa Kinu cha Umeme chenye uwezo wa Megawati 600”, alisema Mhe. Mwijage.Ameongeza kuwa, Tanzania kwa sasa itakuwa na umeme wa gesi, maji na umeme wa makaa ya mawe ambapo umeme wa makaa ya mawe utakuwa msaada mkubwa kwa nchi kwani hautegemei tabianchi kama ilivyo vyanzo vingine vya umeme.

Mhe. Mwijage amesema kuwa katika mradi huo, Tanzania itakuwa na hisa asilimia 20 na Mwekezaji kutoka China atakuwa na asilimia 80, lakini hisa za Tanzania zinaweza kuongezeka hadi kufikia 45.Chini ya mradi huo, Mwekezaji huyo anatakiwa kutoa elimu kwa Vijana katika ngazi zote za teknolojia zitakazohusika kutengeneza mgodi huo.

‘’Tutafundisha vijana wetu kwa ngazi tofauti kwani kampuni hii ni ya ubia kati ya Tanzania na China, tuna mamlaka sawa, tuna Wakurugenzi wetu wa Tanzania ndani ya hiyo kampuni, kwahiyo tutashiriki na hatutakuwa watazamaji”, alisema Mhe. Mwijage.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayosimamia Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambaye pia ni Mtaalam katika masuala ya madini, Mhe. Dkt. Dalaly Kafumu amesema kuwa, lengo la kuwajengea makazi wakazi wa maeneo ya mradi huo ni kuwawezesha wakazi hao kuwa na uhusiano mzuri na mgodi unaotarajiwa kujengwa.

‘’Serikali imeamua kuwajengea makazi wananchi ambao wanazunguka mradi Ili kuepusha wakazi hao kutumia pesa watakayolipwa kama fidia kwa matumizi mengine na kukosa makazi baadaye kuja kuilaumu Serikali kwamba imewadhulumu kwa kutowapa pesa za kutosha za kujenga nyumba”, alisema Dkt. Kafumu.

KASTICO: ASIKITISHWA NA VIFO VYA WATOTO WAWILI TOMONDO UZI ZANZIBAR.

$
0
0
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imewataka Wazazi, Walezi na Wazee kuwalinda watoto wao dhidi ya Mazingira hatari yanayowazunguka ili kuwaepusha na athari za vifo pamoja na ulemavu.

Wito huo ulitolewa na Waziri wa Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Zanzibar, Mauldine Castiko wakati akiwafariji wahanga wa tukio la vifo vya watoto wawili waliotumbukia katika Kisima cha Maji na kupoteza maisha huko katika mitaa ya Tomondo Uzi, Unguja.

Alisema wazazi na jamii kwa ujumla wanatakiwa kuwa waangalifu katika mazingira wanayoishi kwa kuyaweka katika hali ya usalama ili kuwaepusha na madhara watoto wadogo yanayoweza kuwasababishia vifo na hatari zingine zinazoepukika.Castiko alitoa mkono wa pole kwa familia hiyo na kuwaomba waendelee kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa watoto hao wasiokuwa na hatia.

Aliisihi familia hiyo kuendelea kuvumilia katika kipindi kigumu cha msiba huku watu waliohusika na uzembe wa kusababisha vifo vya watoto hao wachukue juhudi za haraka kwa kufunika Kisima hicho ili kisiendelee kuhatarisha maisha ya watoto wengine mtaani.Alisema serikali imesikitishwa na tukio hilo la vifo vya watoto wasiokuwa na hatia na kuahidi kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa familia hiyo.

Alizitaka mamlaka zinazohusika na masuala ya ulinzi wa Raia na Mali zao kuendelea kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo ili watu watakaobainika kuhusika kwa uzembe na tukio wachukuliwe hatua za kisheria.“Familia, Ndugu na Jamaa wa marehemu nakupeni pole na kukuombeni muendelee kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Lakini pia nachukua fursa hii kuwaomba wazazi na walezi kuwa makini na watoto wenu hasa awa wadogo kwani mazingira wanayokuwa wakicheza mengi hayana usalama juu ya maisha yao.”, alisisitiza Waziri huyo na kuongeza kuwa serikali haitowavumilia watu wanaohatarisha maisha ya watoto kwa makusudi na hatakayebainika akifanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.

Waziri huyo alifafanua kwamba Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 pamoja na Mikataba mbali mbali ya Kimataifa inayohusika na Haki za Binadamu iliyoridhiwa na serikali ya Tanzania inatambua na kutetea haki za Watoto kuhakikisha wanapata ulinzi wa kuishi na huduma mbali mbali za msingi kama walivyo watu wengine.

Alisema Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuweka mazingira rafiki ya kuhakikisha maisha ya watoto yanakuwa salama wakati wote wakiwa ndani na nje ya familia zao huku ikiimarisha sheria na miongozo ya kusimamia haki zao Kikatiba.Alitoa agizo kwa wananchi wote wa Zanzibar wanaomiliki visima vya maji ama kuchimba mashimo mbali mbali yanayoweza kuhatarisha maisha ya watoto, kufukia ama kuvifunika visihatarishe maisha ya watoto wengine.

Aidha alisema jamii inatakiwa kuwa makini na watoto wadogo hasa kwa kipindi hiki cha maradhi ya miripuko ya Kipindupindu kwa kuwaepusha watoto wasile wala kunywa maji machafu na vyakula visivyokuwa salama kwa afya zao.“ Kuna baadhi ya familia hawafutilii mwenendo wa watoto wao pindi wanapokuwa nje ya majumba yao kujua wanakula nini wala wanacheza katika mazingira gani hali ambayo inaweza kuwaweka katika mazingira hatarishi watoto wetu.”, alisema Waziri huyo.

Naye Mama mzazi wa watoto hao, Mariam Hassan alishukuru ujio wa kiongozi huyo na kueleza kwamba vifo vya watoto hao ni pigo kubwa kwa familia yake.Alisema kwamba watoto hao walikuwa mazingira ya mtaani wakicheza ambapo yeye alikuwa akiendelea na harakati za kuandaa chakula cha mchana ghafla majira ya saa 7:30 mchana akaambiwa kwamba watoto wake wamedondoka katika kisima cha jirani yao hapo mtaani.

Baada ya kupata taarifa hiyo alifika katika kisima hicho ambapo alikuwa watu mbali mbali wakiendelea na juhudi za kuokoa maisha ya watoto hao lakini walipotolewa walikutwa washafariki kwani haikujulikana wameingia wakati gani.Aliwataja watoto hao kuwa ni Yussuf Faki Juma mwenye umri wa miaka miwili(2) na Muhamadi Ali Abdallah umri wa mwaka 1 na miezi nane wote wakiwa watoto wa familia moja.

Jamii yatakiwa kudumisha na kuenzi utamaduni .

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Utamaduni Bi. Lily Beleko  kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya siku ya Uanuwai wa Utamaduni yanayotarajia kufanyika  Mei 21 mwaka huu ,kulia ni Afisa Habari  wa Wizara hiyo Bw.Benjamini Sawe.
 Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Utamaduni Bi. Lily Beleko  kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo akisikiliza swali kutoka kwa mwandishi wa habari  (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu maadhimisho ya siku ya Uanuwai wa Utamaduni yanayotarajia kufanyika  Mei 21 mwaka huu.

Na Shamimu Nyaki WHUSM

 Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Uanuwai wa  Utamaduni Duniani Serikali imeitaka jamii kuhifadhi kulinda na kuheshimu utamaduni wa nchi kwa vile ndio kitambulisho cha Taifa letu ili kuweza kutambulika ndani na nje ya nchi.

Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,utamadunu,Sanaa na Michezo  Bi.Lily Beleko wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu cha maadhimisho ya siku ya Uanuwai wa  Utamaduni Duniani ambapo kauli mbiu ya madhimisho ya mwaka huu ni” Utamaduni wa Uadilifu na Nidhamu ya Kazi Huleta Maendeleo”, “Sasa Kazi  Tu”
.
Kaimu Mkurugenzi wa Utamaduni Bi.Lily Beleko amesema kuwa ni wajibu kwa kila  mtanzania kuheshimu  Utamaduni wetu na kushiriki kikamilifu katika  kuutambua, kuujenga, kuuendeleza  na kuurithisha kwa vizazi vingine.“Siku hii ni maalumu kwa kila mtanzaniana na kila mmoja hana budi kukubaliana na harakati hizi za kulinda, kuhifadhi na kuendeleza Utamaduni wetu kwa ajili ya vizazi vijavyo”Alisema Bi Lily. 

Bi.Lily Beleko ameongeza kuwa  nchi haiwezi kutambulika na kuheshimika  kama Taifa huru bila kuwa na Utamaduni wake hivyo kuwepo kwa maadhimisho haya kunaipatia jamii fursa ya kuendelea kukumbushana ,kuhamasishana na kuhimizana katika kuuenzi utamaduni wa nchi.

Siku ya Uanuwai wa Utamaduni Duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 21 Mei, ambapo siku hiyo imeteuliwa na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuona umuhimu wa kuhifadhi na kuendeleza Utamaduni na hivyo kupitisha Azimio Na 57/249 mnamo mwaka 2002.

Alama za Jumuiya ya Afrika Mashariki zaanza kutumika rasmi

$
0
0
Na Immaculate Makilika- MAELEZO 19 Mei, 2016

Serikali imetangaza rasmi alama za Jumuiya ya Afrika Mashariki zitakazotumika kwenye Ofisi za Serikali na katika shughuli zote rasmi za kiserikali.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Bi. Mindi Kasiga amezitaja alama hizo kuwa ni bendera ya Taifa,bendera ya Jumuia ya Afrika Mashariki, wimbo wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na wimbo wa Taifa.
Kasiga amewambia waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuwa, kuanzia sasa bendera ya Jumuiya hiyo  itapepea sambamba na Bendera ya Taifa kwenye Ofisi zote za Serikali huku wimbo wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ukiimbwa sambamba na wimbo wa Taifa katika shughuli rasmi za serikali kuanzia ngazi za Halmashauri hadi Taifa, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa Mkataba wa uanzishwaji wa jumuiya hiyo kifungu cha 7(a).
“Mkataba huu unasisitiza jumuiya hii kuwa jumuiya ya watu, hivyo watanzania watahusishwa katika hatua zote za mtangamano huo, pamoja na kushirikishwa kikamilifu katika hatua mbalimbali za jumuiya ili kujua madhumuni ya kunufaika na fursa mbalimbali zitakazaopatikana ndani ya Jumuiya hiyo”, alisema Bi. Kasiga
Aidha, matumizi ya alama hizi ni njia mojawapop ya kujenga uzalendo na kumfanya Mwananchi ajisikie kuwa sehemu ya ushirikiano huu, aliongeza Bi. Kisiga
Vilevile, taasisi binafsi  zinaweza kutumia alama hizi, huku shule na vyuo vikisisitizwa kutumia alama hzi kama sehemu ya kuelimisha na kuhamasisha vijana kuhusu Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.Wizara ya Mambo ya Nje, na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inaratibu upatikanaji wa sampuli ya alama hizo kwa gharama za taasis, wizara au Ofisi husika.

BARAZA LA BIASHARA LA TAIFA LAZINDUA BODI YAKE WILAYANI BUHIGWE

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mary Tesha akizungumza na wajumbe wa baraza la biashara wa Wilaya ya Buhigwe wakati akizindua baraza hilo.
 Baadhi ya wajumbe wa baraza ka biashara wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma, wakisikiliza mada kutoka kwa Meneja biashara wa Baraza la Taifa la biashara Willy Magehema(Hayupo pichani)wakati wa uzinduzi wa baraza hilo Wilayani Buhigwe
Meneja biashara wa Baraza la Taifa la biashara(TNBC) Willy Magehema akitoa mada juu ya uendeshwaji wa mabaraza ya biashara.

BASI LA MWENDO KASI LAUA MWANAFUNZI

$
0
0
Pichani chini ni baadhi ya wananchi wakiweka masalia ya Kichwa cha Mtoto, Nasra Mkinze mwanafunzi wa Darasa la Pili, ambapo haikufahamika mara moja jina la shule hiyo, baada ya kugongwa na Gari la Mwendokasi T 953 DGV kwa kile kinacho daiwa chanzo ni Mwendesha Bodaboda MC 351 AWX kutaka kuwahi mataa ya Shekilango Dar es Salaam mchana huu  na ndipo Dereva huyo wa mwendokasi kuruhusiwa na kumgonga akiwa amembeba Shemeji yake na mtoto (akimwita baba mdogo) dereva wa Bodaboda walipokua wakienda mkoani Morogoro kwenye arobaini  . (PICHA NA KHAMISI MUSSA )
  Msamaria Mwema akiweka ndani ya Gari la Polisi mwili wa mtoto  Nasra Mkinze mwanafunzi wa Darasa la Pili,
 Wananchi wakiwa wamelizingira Gari la Mwendokasi.
  Askari wa Usalama Barabarani akizungumza na wananchi eneo la tukio na Pikipiki iliyosababisha ajali hiyo ikiwa imezungukwa

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA WAWEKEZAJI WA MCHUCHUMA NA LIGANGA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wawekezaji wanaokusudia kuanza uwekezaji katika mgodi wa Mchuchuma na Liganga pamoja na viongozi wa NDC ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma Mei 19, 2016. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa NDC, Dkt. Chrisant Mzindakaya.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WATAKIWA KUACHA KUBEZA MAFANIKIO YA SERIKALI

$
0
0

Frank Mvungi –Maelezo.

Wanaharakati na wanasiasa wanaobeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano, wametakiwa kuacha kuupotosha umma juu ya mafanikio yaliyofikiwa na Serikali hiyo chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam leo na Afisa Habari wa CZI- information And Media Consults Co. Ltd, Augustino Matefu wakati wa mkutano na vyombo vya Habari uliolenga kueleza mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano.Alisema Serikali ya awamu ya tano imeonesha mafanikio makubwa katika sekta ya ukusanyaji mapato, elimu, miundombinu, afya na kujenga uwajibikaji miongoni mwa watumishi wa umma.

Hivyo alitoa wito kwa Watanzania wote kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano na kuwapuuza wanaharakati na wanasiasa hao wanaunga mkono wale wasioitakia mema Tanzania na Serikali ya awamu ya tano kwa ujumla.Alisema katika sekta ya mapato, Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miezi saba iliyopita imefanikiwa kuongeza mapato kutoka shilingi bilioni 900 kwa mwezi kabla ya utawala wake hadi shilingi trilioni 1.5 kwa sasa.

“Rais wa awamu ya tano ameondoa michango yote ya shule za msingi na Sekondari ambayo ilikuwa kero kwa wazazi na wananchi kwa ujumla” alisisitiza Matefu Katika mpango wa elimu bure Matefu alibainisha kuwa umesaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa kujiunga na elimu ya msingi na ile ya Sekondari.

Aliongeza kuwa Rais Magufuli amejenga Barabara ya Mwenge hadi Moroko kwa Fedha za ndani hali inayoonyesha kuwa Serikali inayo dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.Alisema hata Hosipitali ya Taifa Muhimbili Kupatiwa vitanda vya kutosha na hivyo kuondoa tatizo la msongamano katika wodi ya wazazi na kwa sasa wagonjwa wanalala kwenye vitanda.

“Mambo mengine yaliyofanywa na Serikali katika kipindi hiki yanalenga kuinua maisha ya wananchi wa chini ikiwemo kujenga mazingira mazuri yatakayowezesha shughuli za uzalishaji kuongezeka ili kuinua hali ya maisha ya wananchi” alisema Matefu.Kujengwa kwa utamaduni wa uwajibikaji miongoni mwa watumishi wa umma ni moja ya mambo yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano ambapo sekta ya utumishi wa umma imeonesha mabadiliko makubwa katika uwajibikaji.
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live




Latest Images