Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

TRA yabakiza Tshs. Trilioni 2.363 kufikia lengo lao

$
0
0
 
 Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Kodi Prof. Isaya Jairo akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango wa mafunzo ya kuhitimu kwa wafanyakazi waliopo kwenye fursa za ajira Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katikati Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kushoto ni Bw. Alphayo Kidata  Kaimu Mkurugugenzi Rasilimali Watu na Utawala Bw. Victor Kimaro. .

 Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (katikati) akionesha kitabu cha mtaala mpya wa mafunzo kwa wafanyakazi (TRA) watakaopata fursa za kusoma katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA), kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Prof. Isaya Jairo na kushoto na kushoto ni Kaimu Mkurugugenzi Rasilimali Watu na Utawala Bw. Victor Kimaro.

 Baadhi ya washiriki  waliohudhuria katika uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango wa mafunzo ya kuhitimu kwa wafanyakazi waliopo kwenye fursa za ajira Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliofanyikia jijini Dar es salaam.

Baadhi ya washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni Rasmi  Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata.PICHA ZOTE NA ELIPHACE MARWA -MAELEZO .

Na Ally Daud- Maelezo.
MAMLAKA  ya mapato Tanzania (TRA) imebakiza Tsh. Trilioni 2.363 ili kufikia lengo  waliojiwekea la kukusanya mapato ya trilioni 12.363 katika  mwaka wa fedha 2015/16, ambapo hadi sasa imekusanya kiasi cha Tsh. Trilioni 10.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi  wa awamu ya pili ya mpango wa mafunzo kwa wafanyakazi waliopo kwenye fursa ya ajira za taasisi hiyo  Kamishina Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata alisema taasisi yake imefanikiwa kukusanya kiasi cha  sh trilioni 10 katika muda waliojiwekea na kuahidi kumalizia kiasi cha shilingi trilioni 2.363 kabla ya mwaka mpya wa fedha wa Serikali unaoanza mwezi Julai mwaka huu.

“Tumejiwekea malengo ya kukusanya kiasi cha fedha cha shilingi trilioni 12.363 kwa mwaka huu wa fedha na tumefanikiwa kukusanya shilingi trilioni 10 mpaka mda huu ila tunaendelea na kutimiza lengo letu hadi kufikia July mwaka huu na tutajipanga upya mwaka ujao wa fedha kufikia malengo mapema” alisema Bw. Kidata.

Aidha Bw. Kidata amesema kuwa kwa mpango huo wa mafunzo ulioanzishwa kwa  kushirikiana na Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) ni mafunzo ya mwaka mmoja yanayoendana na usaili mpya kwa wahitimu ili  kufanya Mamlaka hiyo kuwa na wafanyakazi waadilifu na wachapa kazi ili kupaisha uchumi nchi.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo alisema kuwa wameamua kuanzisha mpango huo kwa kushirikiana na Mamlaka ya mapato  ili kufundisha wafanyakazi wa TRA maadili na nyenzo za utendaji kazini  pamoja na kuendesha mafunzo ya dini ili kuwafanya wafanyakazi wawe wacha mungu katika kazi zao.

Aidha Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TRA Bw. Victor Kimaro aliwataka wafanyakazi wote wanatakiwa wafanye kazi kwa maadili hususani upande wa ukusanyaji kodi na Chuo hicho kimewafundisha wafanyakazi hao kufanya kazi kwa ushindani katika maeneo ya kazi ili kuliletea taifa maendeleo yaliyokusudiwa.

IDARA YA MIPANGO MIJI NA VIJIJI ZANZIBAR YABOMOA MILANGO YA MADUKA INAYOJENGWA KATIKA SOKO LA MBOGA MBOGA MOMBASA KWA KUKOSA KIBALI.

$
0
0
WAFANYAKAZI wa Idara ya Miji na Vijiji Zanzibar, wakiwa kazini kubomoa milango ya Maduka inayojengwa bila ya Kibali cha Kamati ya usimamizi na Udhibiti wa Majenzi (DCU). PICHA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
MANDHARI ya Soko la mboga mboga Mombasa Wilaya ya Magharibi Unguja ambalo baadhi ya ujenzi unaendelea kinyume na sheria.

Watanzania Wanaotembelea Uingereza watakiwa kuzingatia taratibu za nchi hiyo katika maombi ya Viza.

$
0
0
Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.

WATANZANIA ambao wanapenda kutembelea nchi ya Uingereza wametakiwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na nchi hiyo katika maombi ya viza ikiwemo kuomba viza mapema, kuwasilisha nyaraka zote muhimu pamoja na taarifa sahihi ili kuepuka usumbufu usio wa lazima.

Ushauri huo umetolewa leo Bungeni Dodoma na Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Ole Nasha ambaye alijibu swali kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga lililotaka kujua ni sababu zipi zinazoifanya Serikali ya Tanzania iridhike na utaratibu unaoleta usumbufu kwa Watanzania wanaotaka kusafiri kwenda Uingereza kutafuta viza kupitia Kenya na Afrika Kusini.

Mhe. Ole Nasha ameeleza kuwa, hapo awali huduma za viza zilikuwa zikitolewa na Ubalozi wa Uingereza nchini, Ubalozi huo ulihamisha shughuli za utoaji wa viza kutoka hapa nchini kwenda nchini Kenya tarehe 1 Desemba, 2008 na kuanzia tarehe 18 Agosti, 2014 huduma hizo zimehamishiwa nchini Afrika Kusini na siyo Kenya tena.

Alifafanua kuwa, kwa mujibu wa Serikali ya Uingereza uamuzi huo ni wa kisera ba umefikiwa ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi wa Idara ya Viza na Masuala ya Uhamiaji ya Uingereza.

“Mchakato wa utoaji viza za Uingereza unafanyika Kikanda, kwa mantiki hiyo maombi yote ya viza kutoka nchi zote za Afrika Mashariki na Kati yanafanyiwa kazi katika Ubalozi wa Uingereza nchini Afrika Kusini”, alisema Ole Nasha.

Aidha, Waombaji wa viza hapa nchini wanatakiwa kuwasilisha maombi yao pamoja na nyaraka zinazohitajika katika Kituo cha Kuombea Viza (Visa Application Centre) kilichopo Viva Tower, Dar es Salaam.

“Kituo hicho ndicho chenye jukumu la kusafirisha maombi hayo kwenda Afrika Kusini na kurejesha nyaraka husika kwa waombaji nchini, Mwombaji halazimiki kufuata huduma hiyo nchini Afrika Kusini”, alisema Mhe. Ole Nasha.

Amefafanua kuwa, Ubalozi wa Uingereza Nairobi unashughulikia maombi machache ya viza (restricted number of applications) kwa Viongozi wa Serikali na watendaji wengine wenye pasi za Kidiplomasia hasa katika hali ya dharura ambapo maombi hayo yanapaswa kupelekwa moja kwa moja Ubalozi wa Uingereza Nairobi na waombaji wenyewe au kupitia Ubalozi wa Tanzania Nairobi.

“Napenda kuwakumbusha Waheshimiwa Wabunge pamoja na Watanzania wenzangu kwamba. Zoezi la utoaji viza lina utaratibu Wake na moja ya taratibu hizo ni kwamba nchi inayotoa Viza Ina Uluru wa kuamua ni wapi itatolea viza hizo, kwa mantiki hiyo hata Serikali yetu ya Tanzania ku pitia Balozi zake zilizopo nje inazo taratibu zake za kutoa viza kwa wageni wote wanaotembelea Tanzania, ni vema Watanzania ambro wangependa kutembelea nchi ya Uingereza wakazingatia taratibu zilizowekwa na nchi hiyo katika maombi ya viza”, alisisitiza Ole Nasha.

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA KAMISHINA MKUU WA SEKRETARIETI YA MAADILI JAJI KAGANDA.

$
0
0
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila ofisini kwake Mjini Dodoma.

  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisalimiana na  Kamishna Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili, Jaji Salome Kaganda wakati alipofanya mazungumzo  naye ofisini kwake Mjini Dodoma.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

TANZANIA YAPOKEA BILIONI 224 KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

$
0
0
Na Tiganya Vincent_MAELEZO-Dodoma.

Jumla ya shilingi bilioni 224.314 (224,314,313,555.30) zimepokelewa na Serikali toka kwa wafadhili ili kusaidia kupunguza athari na kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri , Ofisi ya Makamu wa Rais ,Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Wawi Mhe. Ahmed Juma Ngwali aliyetaka kujua serikali imeokea kiasi gani toka kwa wafadhili kusaidia kupunguza athari na mabadiliko ya tabianchi tangu 2010 hadi 2015.

Alisema kuwa kati ya fedha hizo shilingi bilioni 7,017(7,017,510,977.40) na shilingi 217.296 (217,296,802,577.90 zilipokelewa moja kwa moja kutoka kwa wadau wengine.Mhe. Mpina alisema kuwa fedha hizo zilipatikana baada ya kuandaa miradi kwa kuzingatia vigezo na viapaumbele vya vyanzo vya fedha husika.

Alisema kuwa kati ya fedha hizo shilingi bilioni 17.2 zilipelekwa Zanzibar kwa ajili miradi ya ujenzi kutwa katika baadhi ya maeneo ya bahari ambayo yameanza kuathirika na upandaji wa mikoko ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.Mhe. Mpina alisema kuwa fedha hizo zimepokelewa kutoka Mifuko iliyo chini ya Mkataba wa Mabadiliko ta Tabianchi na ushirikiano na nchi wafadhili.

MALIASILI NA UTALII KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KUWEKEZA KATIKA UTALII WA KUSINI MWA TANZANIA

$
0
0

Na Tiganya Vincent-MAELEZO_Dodoma.

Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kuwa inatarajia kuboresha utalii wa kusini mwa Tanzania kupitia miradi mbalimbali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo chini ya mradi wa REGROW unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa gharama za shilingi  bilioni 2.1.

Fedha hizo zinafadhiliwa na Benki ya Dunia  sawa na Dola za Kimarekani zisizopungua milioni moja.Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Injinia Ramo Makani wakati akijibu swali Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini Mhe. Hassan Kaunje aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kuendeleza utalii wa ukanda wa kusini.

Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuwekeza katika miundombinu ya utalii kwa ajili ya kuutangaza utalii wa Ukanda wa Kusini mwa Tanzania ili uweze kusaidia ukuaji wa uchumi na ustawi wa Taifa.

Alisema kuwa mpango huo utajumuisha kuimarisha mafunzo ya utalii na kutenga maeneo maaalum ya utalii katika fukwe za bahari na maziwa kwa ajili hoteli za kitalii.

Mhe. Makani alisema kuwa Serikali imepanga kutekeleza mkakati wa kuutangaza maeneo ya utalii ikiwemo vivutio kihistoria na kiutamaduni kama vile mji wa kihistoria wa Mikindani, Kilwa Kivinje, Pori la Akiba Lukwika-Lumese na Pori la Akiba la Seleous.

Aliongeza kuwa ili kukuza utalii wa fukwe katika eneo hilo , Serikalai imejipanga kutenga maeneo maalum hususan kwa ajili ya hoteli za kitalii kando ya Bahari ya Hindi mkoani Mtwara na Lindi.

SERIKALI KUSOGEZA HUDUMA ZA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KWA WANANCHI

$
0
0
Na Benedict Liwenga, Dodoma.

SERIKALI imesema itaendelea kusogeza huduma za Zimamoto na Uokoaji kwa wananchi kwa jinsi hali ya upatikanaji wa fedha itakavyoruhusu.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni wakati akijibu swali la Mbunge wa Tunduma, Mhe. Frank Mwakajoka ambaye alitaka kujua ni lini Serikali itapeleka huduma za Zimamoto katika Mpaka wa Tunduma ili kuokoa mali za wafanyabiashara wanaosubiri kuvuka pindi ajali ya moto inapotokea.

Mhe. Msauni ameeleza kuwa, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma lina Kituo katika eneo la mtaa wa Kilimanjaro, Wilaya ya Momba katika Mkoa wa Songwe kinachohudumia Wilaya yote ukiwemo Mpaka wa Tunduma.

"Kwa sasa Kituo hiki kina gari moja lililopo matenegenzo Jijini Mbeya, hata hivyo askari wanaendelea kutoa elimu ya Kinga na tahadhari ya Majanga ya Moto na utumiaji wa vifaa vya huduma ya kwanza vya uzimaji moto", alisema Masauni.

Aliongeza kuwa, sambamba na ukaguzi wa majengo ya kutoa ushauri kwa kandarasi au makampuni ya ujenzi kuhusu ujenzi bora wa miundombinu yenye usalama kwa umma.

"Ni azma ya Serikali kupeleka huduma ya Zimamoto katika maeneo yote ya nchi ikiwemo Tunduma, hata hivyo azma hii nzuri inategemea na upatikanaji wa rasilimali fedha, Serikali itaendelea kusogeza huduma za Zimamoto na Uokoaji kwa wananchi kwa jinsi hali ya upatikanaji wa fedha itakavyoruhusu", aliongeza Masauni. 

Wadau wa Mazingira waandaa tamasha la mazingira litakalomhusisha Rais mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

$
0
0
Watanzania  wameombwa kutoa  maoni kuhusu njia zipi  zitumike kutunza mazingira na kukomesha uvuvi haramu wilayani  Temeke katika tamasha  la mazingira litakalofanyika Mei 27, 2016 kwenye fukwe za Sunrise – Kigamboni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika mkutano uliofanyika  jijini Dar es Salaam, Katibu wa CFMA (Collaborative Fisheries Management Area) Godfrey Maduhu alisema  wao wakiwa wadau wa mazingira wameandaa tamasha lenye lengo la kupiga vita uvuvi  haramu na utunzaji wa mazingira.

Maduhu alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano huo, ambao ulishirikisha Mtandao  wa Usimamizi Shirikishi wa Kusimamia Rasimali za Pwani na Bahari,  Balozi wa kujitolea na wadau sekta ya mazingira(WWF).

“Tunapenda kuujulisha umma kuhusiana na tamasha litakalohusisha wadau mbalimbali wa mazingira, litakalokwenda kwa jina la ‘kwa heri Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, karibu Dkt. John Pombe Magufuli,’ lenye lengo la kupiga vita masuala ya uvuvi haramu na kuhamasisha jamii juu ya usimamizi na utunzaji wa mazingira,” alisema Maduhu.

Aidha, Maduhu alisema kwamba lengo la tamasha hilo ni kupanga mikakati juu ya utunzaji na uendelezwaji mzuri wa mazingira na kusikia kauli kutoka viongozi ngazi ya juu hususani kuhusiana na changamoto katika suala la utunzaji wa mazingira.

Maduhu alisema kwamba kama hakutakuwepo na mikakati ya kushughulikia changamoto juu ya uvuvi haramu, Serikali itapoteza mapato mengi kwa kupoteza wateja kutokana na milipuko ya mara kwa mara  katika fukwe za bahari  na kupelekea watalii  kuhofia maisha yao.

Na. Lilian Lundo – Maelezo.

"Maziwa ya Unga si Salama kiafya"- Bodi ya Maziwa Tanzaniaya Unga si Salama kiafya"- Bodi ya Maziwa Tanzania

$
0
0
Bodi ya maziwa Tanzania (TDB) imeeleza kuwa maziwa ya unga ambayo yanatokana na viwandani si salama kiafya kutokana na namna ya utengenezaji na njia inayotumika hadi kumfikia mtumiaji.

Watendaji wakuu wa bodi hiyo ya maziwa wakizungumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa taarifa yao ya utendaji, Majukumu, mafanikio na changamoto, mikakati na mipango yao waliweza kufafanua mambo mbalimbali ikiwemo suala hilo la maziwa ya Unga ambayo si salama kwa afya licha ya kuwepo kwa wingi katika soko la ndani.

Akijibu swali la mwandishi wa mtandao huu kuhusiana na usalama wa maziwa ya unga ambayo yapo hapa nchini, Msajili wa maziwa wa bodi hiyo, Bw. Nelson Kilongozi alifafanua kuwa, Maziwa ya unga kimsingi yanatengenezwa kutoka maziwa yenyewe halisi viwandani na kuwa unga kisha kumfikia mlaji.

Hata hivyo tatizo ya maziwa hayo ya unga ni pale yanapochanganywa viwandani ili kumfikia mlaji kwani yanaongezwa vitu ama yanapunguzwa hivyo kwa wakati mwingine kusababisha matatizo na kuwa si salama kwa mtumiaji hii ni pamoja na kwa watoto wadogo ama mtu aliye mgonjwa.

“Maziwa yakiwa mengi na mafuta yanakuwa kidogo. Na maziwa yakiwa kidogo na mafuta yanakuwa mengi hivyo katika ubora ule wa awali unapungua. Unaweza kukuta low fat baada ya asilia moja unakuta asilimia tatu” alifafanua, Bw Kilongozi
Hata hivyo, Kilongozi aliongeza kuwa, Bodi inaweka sharia na masharti mengi ya kuzuia maziwa hayo ili kulinda soko la ndani la maziwa.

Suala linguine ambalo Bodi hilo iliweza kulifafanua ni maeneo yanayozalisha maziwa kwa wingi ni pamoja na maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo makubwa manne ikiwemo Kaskazini-Manyara Arusha na Kilimanjaro. Pwani-Morogoro Tanga na Dar es Salaam. Nyanda za juukusini-Iringa, Mbeya, Songwe.

Pia kuna maeneo ya Kanda ya Ziwa- Kagera, Mwanza na Shinyanga, hata hivyo mikoa ya Nyanda za Juu kusini ndiyo inazalisha kwa wingi sana kwa asilimia 40 na kufuatia mikoa ya ukanda wa Kaskazini.Bodi hiyo imeeleza kuwa, Tasnia ya Maziwa ni moja ya tasnia muhimu katika sekta yaa mifugo na inachangia takribani theluthi moja ya mapato yanayotokana na sekta hiyo.

Hadi sasa Tanzania inakadiliwa kuwa na ng’ombe wapatao Milioni 25.8 na kati ya hao, takribani 720,000 ni ng’ombe wa kisasa (pure breed) au chotara wake. Hata hivyo Bodi hiyo inaeleza kuwa uzalishaji wa maziwa hapa nchini umekuwa ukiongezeka kila mwaka na unafikia lita Bilioni 2.06 kwa mwaka 2014/2015 na asilimia 70 ya maziwa hayo uzalishwa na ng’ombe wa asili ambao ufugwa katika mfumo wa asili na asilimia 30 iliyobaki uzalishwa kwa ng’ombe wa kisasa au Chotara.

Fahamu faida za unywaji wa maziwa:
Maziwa ni moja kati ya vyakula vitupatiavyo virutubisho aina mbalimbali katika miili yetu mfano maziwa hutupatia protein, mafuta, vitamini kama A na D madini kama kasiumu na kadhalika. Hutumiwa kama kinywaji baridi au moto kiungo katika vyakula au chakula pekee kwa watoto. Pamoja na umuhimu huu wa maziwa, kuna watu miongoni mwetu hatupendi kunywa maziwa ama tunakunywa lakini ni kwa kiwango kidogo sana.
Anaripoti Andrew Chale, Modewjiblog, Dar es Salaam
Tazama hapa kuona tukio hilo:
DSC_3775Afisa masoko wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Bw. Michael Mkalati akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa mkutano huo juu ya hali ya maziwa hapa nchini. Kulia ni Afisa Habari na Mawasiliano, Bi. Queenter

DSC_3745Mkutano huo wa Bodi ya maziwa ukiendelea
DSC_3750Msajili wa maziwa wa bodi ya Maziwa, Bw. Nelson Kilongozi (wa pili kutoka kushoto) akieleza jambo kwa wanahabari mapema leo juu ya Bodi hiyo na masuala ya maziwa hapa nchini. Wengine ni Afisa masoko wa Bodi ya hiyo, Bw. Michael Mkalati, na Afisa Habari na Mawasiliano, Bi. Queenter na kushoto ni Bi. Kuruthumu Mngoye ambaye ni mkaguzi wa bodi hiyo.
DSC_3737Wanahabari wakifuatilia mkutano huo
DSC_3753DSC_3770Afisa masoko wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Bw. Michael Mkalati (wa pili kutoka kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa mkutano huo juu ya hali ya maziwa hapa nchini uliofanyika Jijini Dar es Salaam. Wengine ni watendaji wa bodi hiyo. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

ILIKUA HALALI AZAM KUPOKWA POINTI 3 KUFUATIA KUMCHEZESHA ERASTO NYONI -TFF

$
0
0
Msemaji wa TFF, Alfred Lucas.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KUFUATIA kunyang'angwa kwa ponti 3 za Azam walipocheza dhidi ya Mbeya City,  Azam kulalamika wakihitaji kupata mrejeo wa adhabu hiyo hatimaye kamati ya masaa 72 imetoa majibu yake baada ya kukutana.

 Azam walituma barua kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) wakilalamikia maamuzi yaliyotolewa na Bodi ya Ligi ya kunyang'anywa alama zao 3 muhimu kufuatia kumchezesha Erasto Nyoni katika mechi yao dhidi ya Mbeya City.

Akitoa ufafanuzi baada ya kukutana kwa kamati hiyo, Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa baada ya kupokea malalamiko hayo wakaamua kukaa chini tena na kuangalia upya ripoti zote za waamuzi na kugundua hakuna uonevu uliofanyika.

"Kamati ya masaa 72 imekaa pamoja  na kupitia ripoti zote za waamuzi wa mechi alizocheza Azam na kugundua kuwa hakuna sehemu wamekosea au kufanya uonevu dhidi ya Azam,"amesema Lucas. Mrejeo huo umekuja baada ya Azam kutuma maombi yao kwa TFF ya kurejea ripoti zote za waamuzi wa michezo yao na baada ya kukaa kamati wamegundua kuwa walikuwa sahihi katika maamuzi ya awali.

"Tumejidhihirisha kabisa kuwa Nyoni amecheza akiwa na kadi  3 za njano alizozipata kwenye mechi tatu tofauti akiwa na timu yake ya Azam,"amesema Lucas.

Kamati imepitia mechi zote za Azam na kugundua katika mchezo wa Ngao ya Jamii Nyoni alipata kadi ya Njano pamoja na mchezo wa Prison na wa Coastal Union ambapo kulingana na kanuni ya  37(4) ya Ligi Kuu Toleo la 2015 inayoelekeza kuwa mchezaji atakayeonywa kwa kadi ya njano katika michezo mitatu hataruhusiwa kucheza mchezo unaofuata wa timu yake hivyo Azam wamekwenda kinyume na Kanuni husika, uzingatia Kanuni ya 14(37) ya Ligi Kuu Toleo la 2015, timu ya Mbeya City imepewa ushindi wa pointi 3 na mabao matatu.

WATUHUMIWA WA UBAKAJI WAFIKISHWA KORTIN NA KUSOMEWA MASHITAKA YAO

$
0
0
Watuhumiwa wa Ubakaji Huko Dakawa,Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wakipelekwa Kortini Mjini humo kusomewa Mashtaka yao mapema leo.

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Morogoro imewapandisha kizimbani washtakiwa sita wakikabiliwa na mashtaka matatu tofauti, wakiwemo washtakiwa wawili wanaokabiliwa na mashtaka na kubaka na kumuingilia kinyume na maumbile bila ridhaa yake binti mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa Wami Dakawa Wilayani Mvomero.

Katika kesi hiyo iliyovuta hisia ya mamia ya wananchi wa mkoa wa Morogoro, washtakiwa Iddi Adam Mabena (21) mkazi wa Njombe na Zuberi Thabit (30) mkazi wa Mbarali Mbeya wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi  wa Mahakama ya mkoa wa Morogoro Mary Moyo, wakikabiliwa na shtaka la kubaka na kulawiti, wanalodaiwa kutenda aprili 27 mwaka huu majira ya usiku katika nyumba ya kulala wageni ya Titii iliyopo Wami Dakawa wilayani Mvomero.

Upande wa Serikali katika shtaka hilo lililofanyika faragha kwa mujibu wa sheria, umewakilishwa na waendesha mashtaka Gloria Rwakibalila, Edgar Bantulaki na Calistus Kapinga. Washtakiwa wote wawili wamekana mashtaka na kesi hiyo imepangwa kufikishwa tena Juni Mosi mwaka huu  kwa ajili ya kutajwa.

Upande wa mashtaka umewasilisha kiapo cha pingamizi la dhamana kwa ajili ya usalama wa washtakiwa kwa vile shauri hilo limegusa hisia ya jamii na kwa  vile upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, hivyo washtakiwa wanaweza kuharibu upelelezi.

Katika shtaka jingine lililofikishwa mbele ya Hakimu Ivan Msaki wa Mahakama hiyo, washtakiwa sita wakiwemo Iddi Mabena, Zuberi Thabiti na wengine wanne Rajab Salehe, Ramadhani Ally Makunja anayetetewa na wakili Ignas Punge, Muhsin Ngai na John Petter maarufu kama Paroko, wakazi wa Wami Dakawa wilayani Mvomero wanadaiwa kusambaza picha chafu na za ngono kwa njia ya mtandao kinyume na sheria ya makosa ya mtandao no 14 ya mwaka 2015.

Washtakiwa wote sita wamekana mashtaka ambapo upande wa mashtaka ukiongozwa na mawakili watatu wa serikali uliomba washtakiwa wanyimwe dhamana kwa usalama wao na kutoharibu upelelezi kwa vile bado haujakamilika, huku ule wa mshtakiwa namba nne ukiomba kuwasilisha kiapo cha kupinga mshtakiwa kunyimwa dhamana, ambapo suala hilo la dhamana katika shauri hilo litafikishwa tena juni mosi kwaajili ya kujadiliwa na washtakiwa wote wamerudishwa rumande.

CAG AGIZA VYANZO VYA MAPATO VYA SERIKALI VIANGALIWE UPYA.

$
0
0
 Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali, CAG Profesa Mussa Assad akizungumza na waandishi wafanyakazi ofisi hiyo wakati mkutano baraza jpya la wafanyakazi la wafanyakazi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu  Katibu Mkuu Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora , Susan Mlay akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa ofisi ya CAG leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu  Katibu Mkuu Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora , Susan Mlay akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa ofisi ya CAG leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
OFISI ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za serikali imeitaka serikali kuangalia upya vyanzo vyake vya mapato na matumizi ya fedha  kwa sasa sio nzuri.

Akizungumza katika mkutano wa kwanza wa Baraza jipya la wafanyakazi wa ofisi hiyo, Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali, CAG Profesa Mussa Assad hiyo ni changamoto ambayo inapaswa kuangaliwa na kutafutiwa ufumbuzi na changamoto zinazoikabili ofisi yake, amesema kuchelewa kupokea mgao wa fedha za miradi ya maendeleo kwa wakati inasababisha ofisi hiyo kushindwa kutekeleza mipango na kukamilisha miradi husika kwa wakati.

Profesa Assaad amesema  idadi ya watumishi iliyokuwepo katika ofisi yake ilikuwa 81 ikaongezeka hadi kufika 150 lakini bado wanahitaji watumishi wengine 129 wenye fani ya ukaguzi.

Aidha amesema  kuwa kulingana na weledi wa wakaguzi hao Tanzania imeteuliwa kukaimu nafasi ya uenyekiti wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na China iliyomaliza muda wake mwaka 2014.

Nae Naibu  Katibu Mkuu Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora , Susan mlay amesema watumishi wanatakiwa kuwa na weledi katika kufanya kazi ili kuleta tija kwa taifa ikiwa pamoja na kuangalia masilahi yetu kutokana na kazi wanazozifanya.

TFDA YAWA MWENYEJI WA MAFUNZO YA WADAU KUHUSU USALAMA WA CHAKULA BARANI AFRIKA

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, akitoa maelezo ya awali katika ufunguzi wa mafunzo kwa washiriki wa Kongamano kuhusu Usalama wa Chakula kwa wadau kutoka nchi 11 za Bara la Afrika. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya (aliyekaa katikati), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya siku tano kuhusu Usalama wa Chakula kwa wadau kutoka nchi 11 za Afrika. Wengine waliokaa ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, Mkurugenzi wa Huduma za Maabara wa TFDA, Bi. Charys Ugullum, Mwakilishi wa FAO na Mwakilishi wa IAEA, Bw. Alex Mulori. 
 

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekuwa mwenyeji wa mafunzo ya siku tano, tarehe 16 – 20 Mei, 2016, kwa wadau wa udhibiti katika mnyororo wa Usalama wa Chakula hususan upimaji katika maabara Barani Afrika.
Akifungua mafunzo hayo yaliyowashirikisha wadau wapatao 50 kutoka nchi 15 za Afrika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya, alisema kuwa Lengo kuu la mafunzo na mkutano ni kujadili majukumu, wajibu na mchango wa kila mdau katika suala zima la kuhakikisha chakula ni salama kwa walaji.

Dr. Mpoki alisema, “ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yataongeza uelewa wa namna bora ya usimamizi wa mifumo ya udhibiti wa Chakula Salama kwa kubadilishana uzoefu miongoni mwa wadau mliopo hapa’ .

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, wakati wa kutoa maelezo ya awali kuhusu mafunzo hayo yanayodhaminiwa na Taasisi ya Kimataifa ya Nguvu za mionzi (IAEA), alieleza kuwa kufanyika kwa mafunzo haya nchini Tanzania ni heshima kubwa na ishara ya mwendelezo wa TFDA kufikia Dira yake ya kuwa taasisi inayoongoza barani Afrika katika kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa Tiba.


Nchi zinazoshiriki katika mafunzo haya ni pamoja na Algeria, Benin, Botswana, Cameroon, Egypt, Ethiopia, Mauritius, Mali, Chadi, Namibia, Sudan, Tunisia, Uganda, Zimbabwe na Tanzania.
Matokeo ya mafunzo haya yatakuwa ni dira ya utekelezaji wa mradi wa udhibiti wa mnyororo wa Usalama wa Chakula kabla ya kufikia mwisho wa mwezi Disemba 2016.

Wadau wa mnyororo wa udhibiti wa Usalama wa Chakula walioshiriki katika mafunzo haya wanatoka kwenye maeneo ya maabara, ukaguzi, uzalishaji wa vyakula na walaji.

WAKAZI WA ARUSHA WAPATA MAFUNZO YA HIFADHI YA JAMII NA NSSF.

$
0
0
SHIRIKA la  Taifa la  Hifadhi ya Jamii (NSSF) yazidi kutoa elimu juu ya hifahdi ya jamii kwa wananchi mbalimbali ikiwa ni  mpango maalamu wa kuwafikia wanachama  wengi zaidi.

Katika mkoa wa Arusha NSSF imetoa elimu kwa wafanyabiashara wadogowadogo katika soko la Kilombero. Zoezi hilo litaendelea kesho tarehe 19/05 katika eneo la soko la Kilombero.
Wananchi wakiwa katika foleni ya kujiandikisha uanchama wa NSSF wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi iliyofanyika katika Soko la Kilombero jijini Arusha.


Afisa Masoko na Uhusiano  wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Amani Marcel (kushoto), akimkabidhi mwanachama mpya fulana wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi iliyofanyika katika Soko la Kilombero Jijini Arusha. 
Afisa wa NSSF Bi. Irene Mshanga akimwandikisha mwanachama Mpya wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi inayoendelea katika soko la Kilombero jijini Arusha.

 Afisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano wa NSSF, Amina Mbaga Akitoa ufafanuzi kwa Mwanchama mpya wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi inayoendelea katika Soko la Kilombero Jijini Arusha leo.
Afisa Masoko na Uhusiano wa NSSF, Anna Nguzo Akitoa ufafanuzi kwa Mwanchama mpya wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi inayoendelea katika Soko la Kilombero Jijini Arusha leo.

JESHI LA POLISI MWANZA LATOA BARAKA ZOTE ZA USALAMA KWA TAMASHA LA JEMBEKA 2016

$
0
0
Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr Sebastian Ndege (kulia) akisalimiana na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi alipomtembelea ofisini kwake mapema leo kwa lengo la kumkaribisha kuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika tamasha kubwa la Burudani JEMBEKA FESTIVAL 2016. 

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi Amewahakikishia Ulinzi na Usalama wakazi wa jiji la Mwanza na Vitongoji vyake pamoja na wageni wote watakao hudhuria tamasha la Jembeka festival 2016 linalotarajiwa kufanyika Jumamosi hii ya tarehe 21 Mei 2016 katika kiwanja Cha CCM Kirumba kilichopo jijini Mwanza.

Kamanda Msangi ameyasema hayo leo ofisini kwake alipokutana na kuzungumza na Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr Sebastian Ndege (Jembejembe) Alipomtembelea kwa lengo la kumkaribisha kuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika tamasha hilo la kipekee nchini Tanzania.

“Napenda kutoa wito kwa wakazi wa jiji la Mwanza,wageni kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania na nje ya Tanzania hili ni tamasha la kipekee hapa mkoani kwetu hivyo napenda kuwaasa wananchi wote kufurahi na kuhudhulia tamasha hilo kwa furaha pia napenda kutoa rai kwa wananchi kujiepusha na vitendo vya uvunjaji wa amani”,Alisema Kamanda Msangi.

Kwa upande wake Dr. Sebastian Ndege amemshukuru Kamanda Msangi kwa ushirikiano aliouonesha tangu awali na hili la sasa kuhakikisha anaimarisha ulinzi na usalama siku hiyo ya tamasha na kuahidi kutumia vyombo vyake vya habari katika kulisaidia jeshi hilo kutoa elimu ya ulinzi shirikishi.

“Nashukuru sana kwa ushirikiano tunaoupata kutoka kwa Jeshi la polisi ngazi zote kwani wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Mwanza inakuwa salama hivyo mimi pamoja na timu yangu tunaahidi kusimama bega kwa bega na jeshi letu kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake stahiki linapokuja suala la ulinzi, usalama wa mtu mmoja mmoja na hata utoaji wa elimu kwa umma kuhusu namna ya kuzuia uhalifu, ili Mwanza yetu iwe mahali salama"

Aidha Kamanda Msangi ameahidi kuimarisha Ulinzi wa ndani na nje kwa maeneo yote ya wilaya ya Ilemela ambako uwanja wa CCM Kirumba ndiko unakopatikana na amewatoa hofu Wananchi wote pamoja na wageni watakaohudhuria tamasha hilo kwa kuhofia usalama. "Atakaye kuja kwa hila tutamdhibiti"

Tamasha la Jembeka festival 2016 mwaka huu litatumbuizwa na msanii kutoka nchi ya Marekani Neyo anayetarajiwa kutua nchini kesho usiku.Wakali wengine kutoka hapa nchini Tanzania akiwemo Diamond, Juma Nature, Ney wa Mitego, Maua Sama, Ruby, Fid q, Mo Music, Baraka da prince, na wengine kibao, wanatarajiwa kumwaga mvua ya burudani siku hiyo.

JEMBEKA FESTIVAL linaloandaliwa na Jembe ni Jembe Entertainment kupitia Jembe FM, hufanyika kila Mwaka mkoani Mwanza na tamasha hilo kuhudhuriwa na watu zaidi ya Elfu sabini toka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr Sebastian Ndege (kulia) akisalimiana na Katibu wa Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu alipomtembelea ofisini kwake mapema leo kwa lengo la kumkaribisha kuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika tamasha hilo la kipekee nchini Tanzania. 
Aksante sana Gazeti la Mwananchi toka Mwananchi Communication kwa kutusaidia kufikisha taarifa mlango kwa mlango PAMOJA SANA. 

Jumamosi hii, May 21,2016 itakuwa ni Jembeka Festival Msimu wa Pili. Utamu wa Jembeka Festival unaanzia kwa Mkali Neyo kutoka nchini Marekani pamoja na Mkali Diamond Platnumz kutoka Tanzania. Pia watakuwepo wasanii wengine kibao. 

Kumbuka ni katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kwa kiingilio cha Shilingi 10,000, 50,000 na 100,000 so huu ni muda wa kununua tiketi mwana wa kwetu.Imedhaminiwa na Vodacom Tanzania! Vodacom Kazi ni Kwako. Special Thanks FastJet, EF Outdoor, Mwananchi Communications,Samsung, Ndege Insurance, Syscorp Corporation, KK Security, JembeFm-JembeniJembe, Gsengo Blog, Binagi Blog, Michuzi Blog, Dj Choka, Lakairo Hotel na wadau wengine.

WATAKA UWANJA WA NDEGE MWANZA UJENGWE KISASA ILI KUINUA SEKTA YA UTALII.

$
0
0
Na Tiganya Vincent-MAELEZO_Dodoma 

Baadhi ya Wabunge wanaotoka Kanda ya Ziwa wameomba Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano kujenga Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa kiwango cha Kimataifa ili kuimarisha sekta ya Utalii na usafiri wa anga katika kanda ya Ziwa.

Walisema kuwa hatua itasaidia watalii wanaokuja nchini kushuka moja kwa moja mkoani Mwanza na kisha kuelekea katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na maeneo mengine ya vivutio vya hapa nchini bila kupitia nchi jirani.

Kauli hiyo imetolewa jana na Wabunge Dkt.Raphael Chegeni  na Mhe. Ezekeil Maige wakati wakichangia hotuba kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi  na Mawasiliano kwa mwaka ujao wa fedha.

Mhe. Dkt.Chegeni alisema kuwa Uwanja wa Ndege wa Mwanza ni muhimu ukajengwa kwa viwango vya Kimataifa ili uweze kuruhusu ndege mbalimbali kubwa na ndogo kuweza kutua bila tatizo.

Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuunganisha Mkoa wa Mwanza na nchi jirani za Rwanda, Uganda na Burundi na hivyo kuruhusu ndege nyingi kutoka Nchi hizo kutua bila kwenda katika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere .

Mhe. Dkt. Chegeni  aliongeza kuwa uwanja huo endapo utajengwa kwa kiwango cha Kimataifa utasaidia kuwa kiungo muhimu kwa mikoa 10 ya kanda ya ziwanana kati.

Naye Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Maige alisema kuwa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza sio tu utasaidia kuunganisha mkoa huo na mikoa mingine bali utasaidia kuchochea uchumi wa eneo la Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla kwani watalii na wasafiri wengine watakuwa na fursa ya kuingia Mwanza bila kupitia nchi jirani.

Aliongeza kuwa endapo zoezi hilo litafanyika kwa kiwango cha kimataifa litatoa fursa kwa ndege nyingi za ukumbwa tofauti tofauti kutua katika Uwanja huo na hivyo kupunguzia wananchi ughali wa bei unaotozwa na baadhi ya Kampuni za Ndege ambazo zinatoa huduma za usafiri mkoani humo.

Tume ya maendeleo ya ushirika yakusudia kuvifuta vyama 1,862 vilivyokiuka matakwa ya Sheria.

$
0
0
 Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) Kuhusu makusudio ya Tume hiyo kuvifuta vyama 1862 katika daftari la vyama vya Ushirika vyama ambavyo vimekiuka matakwa ya sheria ya vyama vya ushirika No.6 ya mwaka 2013. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
 Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) Kuhusu makusudio ya Tume hiyo kuvifuta vyama 1862 katika daftari la vyama vya Ushirika vyama ambavyo vimekiuka matakwa ya sheria ya vyama vya ushirika No.6 ya mwaka 2013. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa na kushoto Afisa Uhusiano wa Tume hiyo Bw. Bunyanzu Ntambi.



Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo.PICHA NA HASSAN SILAYO- MAELEZO

Airtel Money Yazindua kampeni ya Mr Money kwa Wateja wake

$
0
0


Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colasso akiongea wakati wa kutambulisha Mr Money anayehakikishia wateja na watumiaji wa huduma za Airtel Money uhakika na gharama nafuu katika huduma za kifedha.

Airtel Tanzania imemtambulisha “Mr. Money” rafiki na mtoa habari njema atakayewasaidia wateja kutatua changamoto zao na kuwaelimisha kuhusu faida mbalimbali zinazotolewa kupitia huduma ya Airtel Money

Mr. Money ametengenezwa kuonyesha utofauti katika huduma za kifedha na kuondoa matabaka katika huduma tunazozitoa sokoni na kuzifanya ziwe zinafanana.

Mr. Money ataweza kuongea na watu katika umri tofauti vijana kwa wazee na kuleta uhai na thamani pindi wateja watakapotumia huduma zetu za kifedha. Kupitia mkakati huu mpya tunategemea huduma ya Airtel Money itakuwa zaidi

Akiongea wakati wa uzinduzi, Bwana Sunil Colaso, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania alisema “Mr. Money atakuwa msaidizi ambaye atakusaidia kufanya mambo mengi zaidi kupitia huduma ya Airtel Money. atashughulikia changamoto zote na kutoa ufafanuzi juu ya faida mbalimbali zinazopatikana kupitia huduma ya Airtel Money na atasimamia mambo makuu mawili Uhakika na gharama nafuu katika huduma ya Airtel Money”.

Moja kati ya huduma za uhakika nafuu na zakibunifu zinazotolewa na Airtel Money ni pamoja na Mkopo ya Airtel Timiza, huduma hii ni mikopo isiyo na dhamana kwa wateja na mawakala wa Airtel Money ikifatiwa na Airtel Money Tap Tap pia ni huduma nyingine ya kibunifu inayotoa nafasi kwa wateja kufanya malipo kupitia kadi maalumu

Mr. Money ameshaanza kupasha habari njema kwa wateja wake kwa kuwawezesha wateja wake kupata Luku uniti za ziada pale wanaponunua LUKU kupitia Airtel Money, Mr. Money anaendelea na dhamira yake ya kutoa nyongeza ya ziada ya uniti za LUKU, na nyongeza za ziada za muda wa maongezi mteja atakapoongeza muda wa maongezi kupitia huduma ya Airtel Money, pamoja na kupata muda wa maongezi wa bure pale atakapotumia Airtel money kufanya malipo, kutuma pesa kwa wapendwa wao bure bila gharama yoyote na kuwawezesha wateja wake kufaidika kwa kiasi kikubwa na hivyo kuleta kutoa huduma zenye gharama nafuu zaidi sokoni

Usikose kupata habari njema kutoka kwa Mr Money kuanzia sasa kwani tunaamini kwa namna moja au nyingine zitabadili maisha yako.
kufurahia huduma mbalimbali zinazotolewa na Mr Money piga *150*60#

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI, DODOMA.

$
0
0
Waziri wa Nishati na Mdini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi mara walipokutana Bungeni mjini Dodoma wakati wa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madinileo 19 Me, 2016 bungeni hapo. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Profesa Jumanne Maghembe akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya asubuhi katika Bunge hilo leo 19 Mei, 2016. 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (kushoto) akiwa ameongozana na Mbunge mwenzie wakiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya asubuhi katika Bunge hilo leo 19 Mei, 2016. 
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya asubuhi katika Bunge hilo leo 19 Mei, 2016. 
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha (kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa CHADEMA, Mhe. Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay wakati walipowasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya Vikao vya asubuhi vya bunge hilo leo 19 Mei, 2016. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (kushoto) akiwa na Mbunge mwenzie wakiingia ndani ya bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao vya asubuhi vya bunge hilo leo 19 Mei, 2016. 
Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya asubuhi katika Bunge hilo leo 19 Mei, 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akijibu maswali ya papo kwa papo leo Bungeni mjini Dodoma 19 Mei, 2016.
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Andrew Chenge (kushoto) akiwa ameongozana na Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Mhe. Cecilia Paresso wakielekea ndani ya Bunge kwa ajili ya Vikao vya asubuhi vya bunge hilo 19 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wa Majimbo mbalimbali wakiwasili katika viwanja vya bunge kuhudhiria vikao vya asubuhi ndani ya bunge hilo mjini Dodoma leo 19 Mei, 2016. 
Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (mwene gauni la kitenge) akiwa na baadhi ya Wabunge wakielekea ndani ya bunge kwa ajili ya vikao vya asubuhi vya bunge hilo 19 Mei, 2016 mjini Dodoma. 
aziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akielekea ndani ya bunge kwa ajili ya vikao vya asubuhi vya bunge hilo 19 Mei, 2016 mjini Dodoma. (Picha zote na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma).

KAMPUNI YA WIA GROUP YAKABIDHI PIKIPIKI TATU KWA SERIKALI YA MTAA WA OYSTERBAY JIJINI DAR LEO.

$
0
0
KAMPUNI ya WIA GROUP yakabidhi msaada wa Pikipiki Tatu kwa Serikali ya Mtaa wa Oystebay jijini Dar es Salaam leo, ilikuhakikisha Ulinzi na usalama wa mtaa huo unakua imara zaidi.
 Meneja mahusiano wa Kampuni ya Wia Group inayojishughulisha na masuala ya mawasiliano, Abraham Mwapongo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay, Zefrini Lubuva, Ofisa Operesheni wa Wilaya ya Kinondoni, Inspeta Msaidizi Samwel Mkama na  Vijana wa Ulinzi na Usalama wa Mtaa wa Oysterbay wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kampuni ya Wia Group kukaidhi pikipiki tatu kwaajili ya ulinzi na usalama wa mataa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam leo.





 Meneja mahusiano wa Kampuni ya Wia Group inayojishughulisha na masuala ya mawasiliano, Abraham Mwapongo(Katikati) akikabidhi vyeti vya manunuzi ya Pikipiki, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay, Zefrini Lubuva(Kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Ofisa Operesheni wa Wilaya ya Kinondoni, Inspeta Msaidizi Samwel Mkama. 

Meneja mahusiano wa Kampuni ya Wia Group inayojishughulisha na masuala ya mawasiliano, Abraham Mwapongo akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa Pikipiki tatu kwa Serikali za mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam. Mwapongo amewaomba wadau mbalimbali washirikiane katika kuimarisha ulinzi na usalama wa mtaa wa Oysterbay kwa kutoa michango na ushirikiano kwa viongozi wa mtaa huo ili kuepusha madhara yatakayojitokeza hasa ya wizi katika jamii yao.
 Meneja mahusiano wa Kampuni ya Wia Group inayojishughulisha na masuala ya mawasiliano, Abraham Mwapongo (Kulia)akipongezwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay, Zefrini Lubuva jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kukabidhiwa Pikipiki Tatu na Kampuni ya Wia Group kwaajili ya kuimarisha ulizi na usalama wa mtaa wa Oysterbay.
Vijana wa ulinzi shirikishi wa mtaa wa Oysterbay wakiwa kwenye pikipiki mara baada ya kupewa pikipiki hizo ili zisaidie kurahisisha kufanya Doria malimvali katika mtaa huo. 
Ofisa Operesheni wa Wilaya ya Kinondoni, Inspeta Msaidizi, Samwel Mkama akiishukuru kampuni ya Wia Group kwa kutoa ushirikiano wa ulinzi shirikishi kwa wanamtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam leo.
Amesema kuwa Kampuni hiyo iigwe mfano kwani imesaidia sana jeshi la Polisi kwani Jeshi hilo ndilo yenye jukumu la kulinda usalama wa raia pamo na mali zao.
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images