Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MABALOZI MBALIMBALI PAMOJA NA KATIBU MTENDAJI WA SADC IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Ikulu Balozi wa Uturuki hapa nchini Yasemin Aralp aliyefika kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais Dkt. Magufuli.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Denmark hapa nchini Eina Hebogrd Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Denmark hapa nchini Eina Hebogrd mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Picha namba 8. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax Ikulu jijini Dar es Salaam. Dkt. Stergomena alifika Ikulu kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais Dkt. Magufuli 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax pamoja na Maafisa wengine kutoka Ikulu na  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Ndugu Egon Kochanke pamoja na ujumbe wake. Wengine katika picha ni Maafisa mbalimbali kutoka Ikulu. Picha na IKULU
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Balozi wa Ujerumani hapa nchini Ndugu Egon Kochanke Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Balozi wa Ujerumani hapa nchini Ndugu Egon Kochanke wakati wa mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Ujerumani hapa nchini Ndugu Egon Kochanke akimkabidhi Kitabu kinachohusu masuala mbalimbali ya Ujerumani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Ndugu Egon Kochanke mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

MWENYEKITI MJI MDOGO WA HIMO HUSSEIN JAMAL AFANIKISHA UZINDUZI WA KIKUNDI CHA MTAA WAKE WA MIEMBENI

0
0
Mama Kaale akikabidhi Hundi ya kiasi cha shilingi Milioni moja kwa Mwenyekiti wa mji Mdogo wa Himo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM wilaya ya Moshi Grace Mzava akikabidhi fedha kiasi cha shilingi Milioni moja kama mchango wake katika kutunisha mfuko wa kikundi hicho.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM wilaya ya Moshi Grace Mzava akikabidhi pikipiki mbili kwa Mwenyekiti wa kikundi cha Miembeni Uchumi Society,Nelson Gabriel ikiwa ni sehemu ya miradi iliyoanzishwa na kikundi hicho.
Mwenyekiti wa Kikundi hicho Nelson Gabriel akifurahia msaada wa pikipiki uliotolewa kwa kikindi hicho na Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Moshi,Grace Mzava.
Mwenyekiti wa Mji Mdogo wa Himo ,Hussein Jamal akikabidhi kwa Mweka hazina wa kikundi hicho Grace Silayo kiasi cha shilingi Milioni tatu zilizopatikana wakati wa uzinduzi rasmi wa mfuko wa kikundi hicho.
Mwenyekiti wa Mji Mdogo wa Himo ambaye pia ni mwenyekiti wa mtaa wa Miembeni akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfuko wa kikundi cha Miembeni kilijulikanacho kama Miembeni Uchumi Society.
Baadhi ya wananchi ambao ni wakazi wa Mtaa wa Miembeni katika mji mdog wa Himo mkoani Kilimanjaro wanaounda kikundi cha Miembeni Uchumi Society .
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rwaichi Kaale akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mfuko wa Miembeni Uchumi Society.
Baadhi ya wanakikundi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM wilaya ya Moshi Grace Mzava akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kikundi hicho.
Baadhi ya wanakikundi.
Mwenyekiti wa Mji Mdogo wa Himo,Hussein Jamal akitoa pesa kiasi cha Shilingi Milioni moja kama mchango wake wa kutunisha mfuko wa kikundi.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rwaichi Kaale akionesha hundi ya kiasi cha shilingi Milioni moja aliyotoa kwa ajili ya kutunisha mfuko wa kikundi.

Wananchi katika Mtaa wa Miembeni wakiwa wamembeba juu Mwenyekiti wao Hussein Jamal kwa kubuni njia ya kuweza kuwakwamua wakazi wa mtaa huo kiuchumi.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Tanzania and China Mineral Resources Limited kuwekeza katika Mgodi wa Makaa ya Mawe.

0
0

Vijana nchini watakiwa kuwa makini katika kupambana na Ukimwi.

0
0
 Mkurugenzi Idara ya maendeleo ya vijana, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana na Ajira, James Kajugusi akifunga rasmi mkutano wa mkutano wa kitaifa wa mwitikio wa kudhibiti UKIMWI miongoni mwa vijana May, 2016.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho, akitoa neno la hitimisho na kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa kufunga mkutano wa kitaifa wa mwitikio wa kudhibiti UKIMWI miongoni mwa vijana May, 2016.
 Afisa Uraghibishi na Habari wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, akisoma tamko kwa niaba ya vijana, wakati wa kufunga mkutano wa kitaifa wa mwitikio wa kudhibiti UKIMWI miongoni mwa vijana May, 2016.

 Wadau wa shughuli za UKIMWI kwa vijana, wakiwa kwenye mkutano wa kitaifa wa mwitikio wa kudhibiti UKIMWI miongoni mwa vijana May, 2016.

 Baadhi ya waratibu wa afya za UKIMWI nchini, wakifuatilia mada wakati wa kufunga mkutano wa kitaifa wa mwitikio wa kudhibiti UKIMWI miongoni mwa vijana May, 2016.

 Mmoja kati ya washiriki wa mkutano wa kitaifa wa mwitikio wa kudhibiti UKIMWI miongoni mwa vijana akikabidhiwa cheti cha ushiriki na mgeni rasmi James Kajugusi wakati wa kufunga rasmi mkutano huo May, 2016. 

 Mmoja kati ya washiriki wa mkutano wa kitaifa wa mwitikio wa kudhibiti UKIMWI miongoni mwa vijana Jaqueline Maeda akikabidhiwa cheti cha ushiriki na mgeni rasmi James Kajugusi wakati wa kufunga rasmi mkutano huo May, 2016.

Baadhi ya washiriki walio kabidhiwa vyeti vya ushiriki wakati wa mkutano wa kitaifa wa mwitikio wa kudhibiti UKIMWI miongoni mwa vijana, wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi James Kajugusi wakati wa kufunga rasmi mkutano huo. May, 2016.


Picha kwa hisani ya TACAIDS

RAIS DKT SHEIN AKUTANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Uingereza  Mhe,Dkt.Asha Rose Migiro alipofika Ikulu Mjini Zanzibar asubuhi ya leo,[Picha na Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Uingereza Mhe,Dkt.Asha Rose Migiro alipofika Ikulu Mjini Zanzibar asubuhi ya leo

KONGAMANO MAALUM LA WADAU KUJADILI SUALA LA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA) LAFANYIKA LEO JIJINI DAR

0
0
 Naibu Gavana wa BOT Dkt Natu Mwamba akifungua kongamano la wadau kuhusu vitambulisho vya Taifa lililofanyika leo katika ukumbi wa Benki Kuu na kuhudhuriwa na wadau toka sekta mbalimbali nchini

 Mkurugenzi  mtendaji wa Financial Sector Deepening Trust Sosthenes Kewe akichangia mada wakati wa kongamano wa wadau lililohusu mpango wa Usajili vitambulisho vya Taifa

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Dkt. Modestus Kipilimba akionyesha wadau sampuli ya vitambulisho vyenye saini vitakavyoanza kutolewa hivi karibuni, wakati wa kongamano la wadau kuhusu mpango wa vitambulisho vya Taifa

 Mr. Sanjay C. Rughani Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini akiwasilisha mada wakati wa kongamano la wadau katika mpango wa usajili vitambulisho vya Taifa

 Mkurugenzi wa Fedha toka TASAF Bw. Joshua Nyamko akiwasilisha mada katika kongamano la wadau kujadili Vitambulisho vya Taifa

Baadhi wa washiriki wa Kongamano la wadau kuhusu mpango wa Usajili vitambulisho vya Taifa wakisikiliza kwa makini mada ya mkakati wa Usajili kufikia Disemba 31,2016 iliyowasilishwa na NIDA.


Rose Mdami

Wadau kutoka Sekta mbalimbali nchini leo wamekutana katika kongamano maalumu kujadili suala la Vitambulisho vya Taifa na uwezekano wa kukamilika kwa mradi huo ili kuwezesha taifa kuwa na Kanzidata(database) yenye taarifa sahihi zenye kujibu maswali makuu nini ni nani, yuko wapi na anafanya nini. Lengo ni kurahisha utoaji huduma na kuwezesha wananchi kujishughulisha na masuala ya biashara kwa kuwa na mfumo rasmi unaowatambua

Akifungua kongamano hilo, Kaimu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Nato Mwamba amesema mfumo wa Usajili na Utambuzi wa Watu ni mfumo ambao umesubiriwa kwa siku nyingi kwani manufaa yake ni makubwa katika mifumo mbalimbali nchini hususani mfumo wa biashara na taasisi za fedha nchini

Amesema kutokana na kupanuka kwa matumizi ya teknolojia nchini, huduma nyingi zikiwemo huduma za kifedha zinategemea sana kuwepo kwa mfumo wa Vitambulisho vya Taifa ili kuwezesha watu wengi zaidi kunufaika na huduma zitolewazo kwa sasa kwani wengi wanakwama kwa kuwa hakuna mfumo rasmi unaowatambua. 

Mafanikio ya mfumo huu ni kufungua milango kwa wananchi wengi zaidi kunufaika na huduma mbalimbali zinazoendelea kutolewa nchini zikiwemo huduma za kifedha na hivyo kuwataka wadau hao kuwezesha NIDA kufikia malengo ya usajili nchi nzima kufikia Disemba 31, 2016 ili mfumo wa Utambuzi wa Taifa uweze kuunganishwa na mifumo mingine

Akieleza mkakati wa usajili kufikia Disemba 31, 2016, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Dkt. Medestus Kipilimba amesema NIDA imejizatiti kutumia taarifa za zilizokusanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuanza usajili utakaowezesha wananchi waliosajiliwa katika daftari la wapiga kura kuhakikiwa na kupata usajili awamu ya kwanza ambao utahusisha namba ya utambulisho kabla ya kupata kitambulisho cha Taifa. 

Amesema hatua ya kufanya usajili wa awali na kutoa namba ya utambulisho itawezesha wananchi kuanza kufaidi utambulisho wao kwa kuwawezesha kupata huduma mbalimbali. Hata hivyo ili mwananchi kupata utambulisho kamili lazima kukamilisha hatua za usajili kwa kuhakikisha anawasilisha nyaraka muhimu za utambuzi ili kuendelea kupata huduma nyingine

Kwa mara ya kwanza NIDA itaanza kuzalisha vitambulisho vyenye saini ya mwombaji ambayo itawekwa kwenye uso wa mbele wa kitambulisho na nyumba ya kitambulisho kutakuwa na saini ya mtoaji. Amesema hatua zote katika kukamilisha mpango huo zimekamilika

Kongamano hilo limehudhuriwa na wadau toka Taasisi za fedha nchini, TASAF, Wamiliki wa makampuni ya simu nchini, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Benki ya Dunia (World Bank), SSRA, BIMA, Melinda and Bill Gates Foundation, Tanzania Bankers Association( TBA) na wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Serikali.


Mtanzania achaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mashauriano ya masuala ya Kisheria katika Nchi za Asia na Afrika (AALCO)

0
0




Profesa Kennedy Gastorn, Katibu Mkuu mpya AALCO 

Mkurugenzi wa masuala ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Kennedy Gastorn amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria katika nchi za Asia na Afrika-‘Asian-African Legal Consultative Organisation-AALCO’.

Profesa Gastorn alichaguliwa kwa kauli moja wakati wa Mkutano wa 55 wa Jumuiya hiyo yenye jumla ya nchi wanachama 47 uliofanyika Mjini New Delhi, India tarehe 17 Mei, 2016 na kuhudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Baraka Luvanda. 

Aidha, Profesa Gastorn ambaye alikuwa ni mgombea pekee wa nafasi hiyo baada ya kupendekezwa na Tanzania na kupitishwa na Umoja wa Afrika, anachukua nafasi ya Katibu Mkuu anayemaliza muda wake Profesa Rahmat Mohamad wa Malaysia ambaye muda wake unamalizika rasmi ifikapo mwezi Agosti, 2016 na Profesa Gastorn anatarajia kukabidhiwa madaraka hayo mwanzoni mwa mwezi Agosti, 2016.

Mkutano wa Jumuiya ya AALCO ulifanyika kuanzia tarehe 16 Mei na kumalizika tarehe 20 Mei, 2016.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 20 Mei, 2016.

SERIKALI KUMLINDA MKULIMA KWA KUANZISHA VITUO VYA UNUNUZI WA MAZAO

0
0
Na Tiganya Vincent, Dodoma.

Wakala wa Vipimo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali za Mitaa inakusudia kuanzisha  vituo maalum vya ununuzi wa mazao ya wakulima (buying centres) katika vitongoji nchi nzima ili kuondoa unyonyaji na ukandamizaji unaofanwa na wachuuzi wa mazao ya wakulima.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo Mhe. Rashid Shangazi aliyetaka kujua ni lini Serikali itasimamia sheria kuondoa unyonyaji unaofanywa na wachuuzi wakati wa kununua mazao ya wakulima.

Alisema kuwa katika kutekeza hayo hakuna mfanyabiashara atakayeruhusiwa kusafirisha mazao ambayo yamefungashwa kinyume kinyume cha Sheria ya vipimo na kuongeza kuwa katika kusimamia jambo hilo vitaanzishwa vituo maalum vya ukaguzi bila kusabaisha usumbufu katika ufanyaji biashara.

Mhe. Mwijage amewaagiza Maafisa Ugani walioko vijijini watumike kusimamia matumizi ya vipimo rasmi katika vituo hivyo na kutoa taarifa zote muhimu kwa Wakala wa Vipimo.

Aidha ,alisema kuwa Serikali imeamua kufanyia mapitio Sheria ya Vipimo sura 340 ili kuondokana na unyonyaji na ukandamizaji unaofanywa na wachuuzi wa mazao ya wakulima.

Alisema kuwa Serikali imeamua kufanyia mapitio ya Sheria hiyo ili kuweka mazingira mazuri kwa lengo la kumlinda muuzaji kwa kuwadhibiti manunuzi wanaotumia njia za udandanyifu wakati wanaponunua mazao ya wakulima.Mhe. Mwijage alisema kuwa katika kipindi kifupi kijacho Serikali itawalisha mabadiliko hayo bungeni ili ifanyiwe marekebisho yanayostahili.

Aidha , Waziri huyo alisema kuwa pamoja na marekebisho ya Sheria ya Vipimo yanatarajia kufanywa , Wakala wa Vipimo imewasilisha Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mapendekezo ya kutungwa kwa sheria ndogo(by laws)  ili ziweze kuwaongoza wakulima na wafanyabiashara kufungasha mazao. 

TCRA YAWANOA WADAU WA MAWASILIANO KANDA YA ZIWA KABLA YA KUZIMA SIMU BANDIA

0
0
Wadau wa Mawasiliano Kanda ya Ziwa, wakiwa katika picha ya pamoja katika Semina juu ya utoaji wa elimu juu ya simu bandia (fake) na halali (orginal) ulioandaliwa na TCRA, kabla ya kusitisha matumizi ya simu bandia mwezi ujao.

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), imeendelea kuwakumbusha watumiaji wa simu za mkononi kuhakiki simu zao kabla mamlaka hiyo haijazima simu bandia ifikapo Juni 16 mwaka huu.

Soma Zaidi HAPA

Wadaiwa 21,721 wajitokeza HESLB kurejesha mikopo

0
0


Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Robert Kibona akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utekelezaji wa agizo la siku 60 kwa wadaiwa wa Bodi hiyo na waajiri, ambapo takribani asilimia 72 ya wadaiwa wote wameshawasilisha taarifa zao. Kulia ni Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi hiyo
Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Cosmas Mwaisobwa (kushoto) akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utaratibu wa urejeshaji wa mikopo kwa wadaiwa ambao mikopo yao imeshaiva. Kulia ni Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Robert Kibona.PICHA NA FATMA SALUM-MAELEZO

Na FATMA SALUM -MAELEZO

Jumla ya wadaiwa wapya 21,721 wa mikopo ya elimu ya juu wamejitokeza ili kuanza kulipa madeni yao kufuatia agizo la siku 60 lililotolewa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) mnamo Machi 14 mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Robert Kibona wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu tathmini ya agizo lililotolewa na bodi hiyo kwa wanufaika wa mikopo na waajiri ili kutimiza wajibu wao kisheria.

Bw. Kibona alifafanua kuwa jumla ya Shilingi bilioni 151.5 zinatarajiwa kurejeshwa na wadaiwa hao ambao walikopeshwa ili kuwawezesha kupata elimu yao ya juu katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi kuanzia mwaka 1994.“Lengo la agizo lilikuwa ni kuhahakisha madeni yote yaliyoiva yanakusanywa ili kuongeza uwezo wa kukopesha watanzania wengi zaidi na agizo hili limeisha Mei 13 mwaka huu.” alisema Bw. Kibona

Kwa mujibu wa Bw. Kibona, kati ya wadaiwa waliopatikana, wadaiwa 19,528 walipatikana baada ya Bodi kuchambua taarifa za waajiriwa zilizowasilishwa na waajiiri na wadaiwa wengine wapatao 2,007 walijitokeza kwa hiari.“Waajiri wana wajibu wa kisheria wa kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao, baadhi yao walifanya hivyo katika siku hizo sitini na tukawabaini wadaiwa hao, tunawapongeza waajiri kwa ushirikiano walioutoa na wanufaika wote waliojitokeza kwa hiari” alisema Bw. Kibona.

Aidha Bw. Kibona aliongeza kuwa Bodi imeongeza siku 30 za ziada kuanzia Mei 20, 2016 kwa wadaiwa waliobaki kujitokeza na uamuzi huo umetokana na tathmini iliyoonyesha kuwa kuna idadi kubwa ya waajiri na wanufaika wanaoendelea kujitokeza. Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo Bw. Cosmas Mwaisobwa alisema kuwa kiwango cha ukusanyaji wa madeni kwa mwezi kinatarajiwa kuongezeka kutoka shilingi bilioni 2.7 zinazokusanywa hivi sasa na kufikia shilingi bilioni 8 ifikapo mwezi Juni 2016.

Katika kipindi cha mwaka 1994/1995 hadi sasa, kiasi cha shilingi trilioni 2.44 kimetolewa kwa wanufaika 378,504 wakiwemo wanafunzi wanaoendelea na masomo yao hivi sasa ambao kwa sasa hawana wajibu wa kulipa hadi pale watakapomaliza au kusitisha masomo yao.

MWANAFUNZI MBARONI KWA KUMTUKANA RAIS WA ZANZIBAR DKT.SHEIN PAMOJA NA MKUU WA MAJESHI.

0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo.

Na Woinde Shizza,Arusha
Jeshi la polisi mkoani hapa linamshikilia mwanafunzi wa Mwaka wa tatu wa chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru aliyejulikana kwa jina la Harold Mmbando (23) mkazi wa Arusha kwa kosa la kutoa taarifa za uchochezi dhidi ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Mkuu wa majeshi Davis Mwamunyange pamoja na kusambaza ujumbe wa maneno makali juu ya viongozi hao.

Akiongelea tukio kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa tukio hilo lilitokea May 17 mwaka huu majira ya saa 09:00 asubui .

Alisema kuwa mwanafunzi huyo alitoa taarifa za uchochezi kuhusu mkuu wa majeshi ambapo alimtaka mkuu huyo wa majeshi kupindua nchi na kusema kuwa haiwezekani viongozi wote wawe nje ya nchi huku akuna kiongozi aliyepewa mamlaka ya kukikaimu kiti.


“mtuhumiwa huyo aliandika maneno haya ,Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote wawe nje halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti,hayo ndio maneno aliyoyasema mtumiwa huyo “alisema Mkumbo.

Aidha aliongeza kuwa mbali na maneno hayo piamtumiwa huyo alisambaza ujumbe mwingine wenye maneno yafuatayo,”Dr Shein akiuawa kama Karume sitashangaa wala kustuka naomba mungu mauaji ya kisiasa yaliyotokea Zanzibar yawe kwaviongozi wa kisasa hasa watawala na sio wananchi wa kawaida”hayo ndio maneno aliyoyaandika mtuhumiwa huyo kupitia mitandao ya kijamii kama faccebook.

Mkumbo alisema kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi tu upelelezi utakapo kamilika,huku akitoa rai kwa watu wote wanaotumia mitandao ya kijamii kutumia mitandao hiyo ya kijamii pasipo kukiuka sheria na taratiu za kisheria .

Alitumia muda huo pia kutoa onyo kali kwa yoyote atakaye bainika anatumia mitandao vibaya na kusema kuwa atachukuliwa hatuakali za kisheria dhidi yake.

Wakati hayo yakiendelea mshtakiwa wa kesi ya kumtukana Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli Isaac Emily (40),  mkazi wa Olasiti jiji hapa inatarajiwa kuanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Juni 5 mwaka huu katika mahakama ya hakiku mkazi Arusha.

Wanaobadilisha taka kuwa bidhaa watambuliwe

0
0
Na: Lilian Lundo – Maelezo

Balozi wa kujitolea wa mazingira, Omary Kombe ameiomba Serikali kuwatambua watu wanaobadilisha taka kuwa bidhaa kwa kuendeleza taaluma hiyo ili kuinua uchumi na kuondokana na tatizo la uchafu nchini.
 
Akiongea na waandishi wa habari  Mei 18, 2016 jijini Dar es Salaam, Kombe alisema kwamba kwa kuwatambua watu hao, tatizo la taka litakwisha kwa kiwango kikubwa nchini hasa katika jiji la Dar es Salaam.

“Wapo watu ambao mara nyingi tunawaona kwenye maonyesho mbalimbali kama vile sabasaba ambao wanauwezo wa kubadili taka kuwa bidhaa za majumbani kwa mfano, mkaa, mapambo na bidhaa nyingine, ni vizuri Serikali ikawatumia  watu hao kuondokana na tatizo la taka nchini,” alisema Kombe.

Aliongeza kwamba mazingira bado ni machafu licha ya serikali ya awamu ya tano kuweka  mkazo katika suala zima la usafi kuanzia ngazi ya familia mpaka Taifa ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.

Kombe alisema kwamba, tatizo hilo la uchafu litatatuliwa kama watu wenye uwezo wa kubadilisha taka kuwa bidhaa watatambuliwa na kufanya kazi hiyo kuwa rasmi.

Aidha alisema kuwa, kwa kubadilisha taka kuwa bidhaa kutapunguza kiwango cha taka nchini, kuongeza ajira pamoja na  kuipunguzia Serikali mzigo wa kutenga maeneo kwa ajili ya kuhifadhia taka kila mara.

Usafi ni kauli mbiu ambayo imeshika kasi awamu hii ya tano ambapo katika sherehe za Uhuru (Tisa Desemba) Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliwataka watanzania wote kushiriki usafi maeneo yanayowazunguka na vituo vya jamii kama hospitali, zahanati na vituo vya afya.

MWANAFUNZI MBARONI KWA KUMTUKANA RAIS WA ZANZIBAR DKT.SHEIN PAMOJA NA MKUU WA MAJESHI MWAMUNYAGE

0
0

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo

Na Woinde Shizza,Arusha

Jeshi la polisi mkoani hapa linamshikilia mwanafunzi wa  Mwaka wa tatu  wa chuo cha maendeleo  ya jamii .Tengeru  aliyejulikana kwa jina la  Harold Mmbando (23)  mkazi wa Arusha kwa kosa la kutoa taarifa za uchochezi dhidi ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Mkuu wa majeshi Davis  Mwamunyange  pamoja na kusambaza ujumbe wa maneno makali juu ya viongozi hao.

Akiongelea  tukio kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo  alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 17 mwaka huu majira ya saa 09:00  asubuhi .

Alisema kuwa mwanafunzi huyo alitoa taarifa za uchochezi kuhusu mkuu wa majeshi  ambapo alimtaka mkuu huyo wa majeshi kupindua nchi na kusema kuwa haiwezekani viongozi wote wawe  nje ya nchi huku hakuna kiongozi aliyepewa mamlaka ya kukikaimu kiti.

“mtuhumiwa huyo aliandika maneno haya ,Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote wawe nje halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti,hayo ndio maneno aliyoyasema mtumiwa huyo “alisema Mkumbo.

Aidha aliongeza kuwa mbali na maneno hayo pia mtuhumiwa huyo  alisambaza ujumbe  mwingine wenye maneno yafuatayo,”Dr Shein akiuawa kama Karume sitashangaa wala kustuka naomba mungu mauaji ya kisiasa yaliyotokea Zanzibar yawe kwa viongozi wa kisasa hasa watawala na sio wananchi wa kawaida”hayo ndio maneno aliyoyaandika mtuhumiwa huyo kupitia  mitandao ya kijamii kama faccebook.

Mkumbo  alisema kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi tu upelelezi utakapo kamilika,huku akitoa  rai kwa watu wote wanaotumia mitandao ya kijamii kutumia mitandao hiyo  ya kijamii pasipo kukiuka sheria  na taratiu za kisheria .Alitumia muda huo pia kutoa onyo kali kwa yoyote atakaye bainika  anatumia mitandao vibaya na kusema kuwa  atachukuliwa hatuakali za kisheria  dhidi yake.

Wakati hayo yakiendelea mshtakiwa  wa kesi ya kumtukana Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania  John Pombe Magufuli Isaac Emily (40),  mkazi wa Olasiti jiji  hapa  inatarajiwa kuanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Juni 5 mwaka huu katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha.

TAPELI WA MADINI BANDIA JIJINI DAR ES SALAAM ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI.

0
0
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina (CP),Simon Sirro akizungumza na waandishi habari juu ya matukio ya kialifu katika jiji la Dar es Salaam ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina (CP),Simon Sirro akionyesha baadhi ya vitu walivyokamata kwa Wenceslaus Mtui anayedaiwa kuwa ni tapeli ya madini bandia leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waandishi wakimsikiliza Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina (CP),Simon Sirro leo jijini Dar es Salaam picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linashikilia mkazi wa Makongo, Wencelaus Mtui anayedaiwa kuhujihusisha na utapeli wa madini kwa kumtapeli mtu na kisha madini bandia yenye thamani ya Sh.Milioni 90,000.

Akizungumza na waandishi habari leo Ofisini Kwake, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina (CP),Simon Sirro amesema kuwa mtu aliyetambeliwa kiasi cha fedha hizo alilipa kupitia benki ya CRDB kwa madini bandia ya dhahabu Kilogram 20 zenye thamani ya Dola za Kimarekani 40,000.

Amesema baada ya mtu huyo kulipa fedha hizo alikabidhiwa vipande vitatu vya madini venye uzito wa Kilogram 212 na kugundua kuwa ni madini bandia.

Jeshi la polisi lilipompekuwa ofisini kwake na nyumbani kwake walimkuta ,Chuma cha kuchomea madini,Mashine ya kupima madini ,vifaa vya kubania (Seal 53) pamoja na taarifa mbalimbali za malipo ambayo ameweka benki na kutoa.

Mtui ambaye anadaiwa kuwa ni tapeli wa madini pandia anamiliki kampuni ya Crown Logistics and Cargo Handling Limiited.

Wakati huo huo jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam linamskilia Waziri Jamal (39) mkazi wa Mbezi Msakuzi ambaye wamemkamata na silaha moja aina ya Bastola Browning 6.35 Calbre yenye namba za usajili A.08416/ Car 90522 na baada ya kumhoji wameweza kubaini mtandao wao wa watu nane.

Aidha jeshi la polisi limesema kuwa askari aliyeuawa jana kwa kupigwa risasi ni wa mkoa wa pwani na kuahidi lazima watakamatwa wote waliohusika.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA RIPOTI YATOLEO LA NANE LA UCHUMI TANZANIA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye uzinduzi wa ripoti ya Toleo la nane 8 kuhusu hali ya Uchumi Tanzania uliofanyika leo tarehe 20/5/2016 katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es salaam. 
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Makamu wa Rais picha hayupo wakati wa uznduzi wa ripoti ya toleo la nane 8 kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania uliofanyika leo tarehe 20/05/2016 .kwenye hotel ya Hyatt Begency jijini Dar es salaam.[Picha na OMR]
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya uungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia Madame Bella Bird baada ya uzinduzi wa ripoti yatoleo la nane 8kuhusu hali ya uchumi Tanzania.

Serikali imesisitiza azma yake ya kuweka mazingira mazuri ya biashara ili kuiwezesha sekta binafsi kuchangia kikamilifu katila maendeleo ya Taifa.Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo kwenye uzinduzi wa ripoti ya toleo la nane la hali ya uchumi Tanzania uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es salaam.

Hali ya uchumi Tanzania ni ripoti inayochapishwa na Benki ya Dunia mara mbili kwa mwaka kwa lengo la kukuza mjadala wa sera unaojengeka baina ya wadau na watunga sera na kuchochea mdahalo kwenye masuala muhimu ya uchumi nchini.Makamu wa Rais alisema Serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa za kuendeleza nchi lakini katika baadhi ya miradi na hasa ile mikubwa mambo hayakuwa yanaenda vizuri kutokana na ukosefu wa fedha.

"Dunia ilivyo sasa, tutapata fedha, tena nyingi kutoka sekta binafsi. Sasa kuna haja ya kurekebisha sheria zetu, sera na matamko mbalimbali ili kuiingiza sekta binafsi," alisema Mheshimiwa Samia.Alisema Serikali imeona kushirikiana na sekta binafsi kupitia mpango wa ubia baina ya sekta za umma na binafsi (PPPs) ndiyo njia pekee ya kuiwezesha Tanzania kupiga hatua ya maendeleo.

Alibainisha kwamba katika uzinduzi huo wajumbe wametafakari pia umuhimu wa kuwaingiza wazalishaji na hasa wakulima wadogo na wakubwa kama sehemu ya ubia wa maendeleo ya Tanzania.
Makamu wa Rais alitumia fursa hiyo kuelezea jitihada za serikali katika kukusanya kodi, kupunguza rushwa na kuimarisha nidhamu katika matumizi ya serikali na kusema hatua hizo zimezaa matunda huku makusanyo ya mapato ya kodi kwa kila mwezi yakivuka lengo tangu Disemba, mwaka jana.

Mapema, akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird alisifia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa kiwango cha asilimia 7 kwa mwaka 2014 na 2015 ukilinganisha na wa Afrika kwa ujumla ambao umeshuka toka asilimia 4.8 mwaka 2014 hadi asilimia 3.2 mwaka 2015.

Aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Magufuli kwa kupambana na rushwa, ufisadi na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa kodi ambao umeiongezea heshima serikali ndani na nje ya nchi.Bella alisema wakati Tanzania inaelekea kwenye uchumi wa kati serikali inapaswa kufanya kazi kwa karibu na sekta binafsi (PPPs) kwa ajili ya uwekezaji.
 
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
20/5/2016.

TRA YAWAPA ELIMU YA MLIPAKODI WAFANYABIASHARA RAIA WA CHINA WAISHIO NCHINI TANZANIA.

0
0

2 3
Baadhi ya wafanyabiashara raia wa China wanaoishi nchini Tanzania na kufanya biashara wakiwa katika semina ya mlipa kodi iliyofanyika leo kwenye mgahawa wa Tang Ren Chinese jijini Dar es salaam1
Meneja wa Elimu kwa mlipa kodi kutoka TRA Bi. Diana Masalla akitoa elimu ya mlipa kodi na sheria za kodi kwa wafanyabiashara raia wa China wanaoishi hapa nchini na kufanya biashara katika semina ya mlipa kodi iliyofanyika leo kwenye mgahawa wa Tang Ren Chinese jijini Dar es salaam, ambapo kabla semina hiyo imefunguliwa na Bw. Sun Chengfeng Mwakilishi wa masuala ya Kiuchumi na Kibiashara kutoka serikali ya Watu wa China nchini Tanzania, Semina hiyo inalenga kuwapa wafanyabiashara hao elimu na uelewa wa masuala mbalimbali ya kisheria katika kodi na umuhimu wa kulipa kodi.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE)
4
Bw. Sun Chengfeng Mwakilishi wa masuala ya Kiuchumi na Kibashara kutoka Serikali ya Watu wa China nchini Tanzania akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina hiyo iliyofanyika kwenye mgahawa wa Tang Ren Chinese jijini Dar es salaam.

YANGA YAWASILI NCHINI,YAPOKELEWA KWA KISHINDO NA MASHABIKI WAKE

0
0
Golikipa wa timu ya Yanga Deogratius Munish Dida akizungumza na waandishi wa habari baada y kuwasili kutoka Angola.
 Kocha Mkuu wa Yanga Hans Van De Pluijm akiwasabahi mashabiki wa timu ya Yanga waliofika kuwalaki uwanja hapo mapema leo mchana

 Wachezaji wa Yanga wakitoka  nje ya uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakitokea nchini Angola
 Wachezaji wa Yanga wakitoka  nje ya uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakitokea nchini Angola
 Kocha Mkuu wa Yanga Hans Van De Pluijm akiwasabahi mashabiki wa timu ya Yanga
  Wachezaji wa Yanga wakitoka  nje ya uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakitokea nchini Angola.

MAAFISA WA JESHI LA MAGEREZA 327 WA CHUO CHA MAGEREZA KIWIRA, MKOANI MBEYA WATUNUKIWA VYEO.

0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Rwegasira akiwa katika Jukwaa akipokea Salaam ya heshima kutoka kwa Gwaride Maalum lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili katika sherehe za kufunga Mafunzo hayo ya Maofisa wa Jeshi la Magereza, Chuo cha Magereza Kiwira kilichopo, Rungwe Mbeya(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Rwegasira akikagua moja ya Gadi ya Wanaume inayoundwa Gwaride rasmi la sherehe hizo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Rwegasira akimvisha cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza mmoja wa Wanafunzi Wahitimu kwa niaba ya Wahitimu wote wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili. Mwanafunzi huyo amefanya vizuri katika Mafunzo hayo.
Onesho Maalum la kujihami kutoka kwa Askari wa Jeshi la Magereza katika namna ya kupambana na adui yeyote wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao. 

Na Lucas Mboje, Rungwe.
JUMLA ya Askari 327 wa Jeshi la Magereza, kati yao wanaume 257 na wanawake 81 wametunukiwa cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza baada ya kuhitimu mafunzo ya Uongozi daraja la Pili kozi namba 1 katika Chuo cha Magereza Kiwira, Wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya.

Cheo hicho wametunukiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira katika Sherehe za ufungaji wa mafunzo hayo zilizofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho leo Mei 20, 2016.

Akizungumza katika sherehe hizo Meja Jenerali Rwegasira amesema Askari na Maafisa wa Jeshi la Magereza nchini wanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia Haki za Binadamu na Utawala Bora kila wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kazi.

Jenerali Rwegasira amesema Maafisa hao wahitimu wakazingatie elimu waliyopewa wakati wa mafunzo ili wakawe mfano kipindi cha utendaji kazi wao ikiwa ni pamoja na kuhamasisha na kuwaongoza wenzao ambao hawakupatiwa elimu kama yao.

Aidha, amewaasa kutowatesa Wafungwa walioko magerezani bali kuwahudumia kwa kuzingatia kanuni na taratibu za uendeshaji wa magereza kwani Wafungwa ni Binadamu kama watu wengine ispokuwa tu wameikosea jamii.

"Tuzingatie falsafa ya kwamba mfungwa yupo gerezani kwa ajili ya kutumikia adhabu na si kwa kuongezewa adhani. Kwa kufanya hivyo, Serikali yetu itakuwa inazingatia Utawala wa Sheria na hivyo kuwa Taifa linalozingatia na kuheshimu Haki za Binadamu na Utawala Bora". Alisisitiza Jenerali Rwegasira.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja amesema kuwa changamoto nyingi ambazo kwa kiasi fulani zimeathili utekelezaji wa majukumu ya Jeshi hilo ni pamoja na ufinyu wa bajeti, makazi duni ya maafisa na askari, uhaba wa vitendea kazi na uchakavu wa vyombo vya usafiri.

Kamishna Jenerali Minja ameongeza kuwa tayari Jeshi hilo limechukua hatua mbalimbali za kufanya maboresho kwa lengo la kufanya Jeshi la Magereza kuwa la kisasa katika kutekeleza majukumu yake kisayansi na kwa ufanisi unaotarajiwa.

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kushoto) akifurahia jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi(katikati). Kulia ni Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, SACP. Stanford Ntirundura.
Askari Wanafunzi ambao wanaendelea na Mafunzo yao ya Awali wakifuatilia sherehe hizo za kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili.
Maafisa Wandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza wakiteta jambo mara baada ya kufungwa rasmi kwa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili(kulia) ni ACP. Solomon Urio(katikati) ni ACP. Lazaro nyanga(kushoto) ni ACP. Ismail Mlawa.


(Picha zote na Lucas Mboje).

MATUKIO YA BUNGENI LEO.

0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akibadilishana mawazo na na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwa(kulia) jana mjini Dodoma wakati wa mapumziko ya mchana ya kikao cha Bunge.
  Afisa Habari wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Patson Sobha(aliyenyosha mkono) akitoa maelezo kwa wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma walitembelea Bunge kama sehemu ya mafunzo jana mjini Dodoma.
 Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Dkt. Dalaly Kafumu(kushoto) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Simanjirio Mhe. James Ole Milya(wa pili kushoto), Mbunge wa Tarime Vijijini Mhe.John Heche(wa pili kulia) na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwa(kulia) jana mjini Dodoma wakati wa mapumziko ya mchana ya kikao cha Bunge.

 Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe Venance Mwamoto(kushoto) jana mjini Dodoma wakati wa mapumziko ya mchana ya kikao cha Bunge.
Picha na Tiganya Vincent, Dodoma.

RC. MAKONDA ATOA MSAADA WA MAGODORO SHULE YA SEKONDARI YA TAQWA JIJINI DAR LEO

0
0



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananachi wa msikiti wa Taqwa alipotembelea kwa ajili ya kuangalia athari za moto katika shule ya sekondari ya Taqwa iliyoungua juzi leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikabidhi msaada wa magodoro kwa Imamu wa Msikiti wa Taqwa Abdul Wakil kwa ajili shule ya sekondari ya Taqwa iliyopo Ilala jiji Dar es Salaam iliyoungua na Moto juzi.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images